Title kwanini wakristo

Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?

SWALI: Kwanini wakristo wa kwanza waliposikia kuwa Petro kafunguliwa hawakuamini badala yake walitumia neno “Ni malaika wake”..kwanini wawaze vile au waseme vile?


JIBU: Tusome.

Matendo ya Mitume 12:11-17

[11]Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.

[12]Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba.

[13]Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza.

[14]Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango.

[15]Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. WAKANENA,  NI MALAIKA WAKE.

[16]Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu.

[17]Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.

Wayahudi tangu zamani hadi sasa wanaamini kuwa kila mtu anaye malaika mlinzi..Na malaika hawa wanaweza kuja katika maumbile tofauti tofauti..wanaweza kuja kwa sura ya mtu mwingine au kwa sura au sauti  ya yule mtu anayemlinda.

Vilevile tunaweza kulithibitisha hilo pia katika maneno ya Bwana aliyoyasema katika (Mathayo 18:10) Kwamba wapo malaika wanaosimama kwa ajili ya watu tangu wakiwa wadogo.

Sasa kulingana na hiyo habari ni kuwa Roda aliposikia sauti ya Petro, .hakuhangaika kuhakikisha kwamba yeye anayegonga ni Petro au la! bali aliamini moja kwa moja na kwenda kutoa taarifa ..Lakini alipowapelekea habari wale waliokuwa ndani haikuwa rahisi kwao kuamini moja kwa moja kama yule angeweza kuwa Petro. Kwasababu kutokana na mazingira Petro aliyofungiwa, ni ngumu kutoka kwani alikamatwa kwa amri ya mfalme, na vilevile alikuwa chini askari 16.

Hivyo jambo ambalo wangeweza kudhani ni kuwa malaika wake ndio amekuja kwa maumbile ya Petro au pengine kwa umbile lingine isipokuwa katumia sauti ya Petro labda kuwafariji au kuwapa taarifa juu ya kifo  chake.

Lakini  walipoona Petro anazidi kugonga mlango wakaenda kumfungulia, wakathibitisha kuwa kumbe alikuwa ni Petro na sio malaika wake.

Ni nini tunaweza kujifunza katika habari hiyo?

Ni karama ya Mungu kuwatuma malaika zake kutuhudumia.Lakini malaika hawa hawamuhudumii kila mtu tu ilimradi hapana bali ni watakatifu tu..ikiwa na maana kama wewe ni mwovu ujue kinachokulinda ni rehema za Mungu tu ili uendelee kuishi, lakini hakuna huduma yoyote unayoweza kupokea kutoka kwa malaika zake. Kinyume chake ni kuwa mapepo ndio walinzi wako.

Na ndio maana huwezi kuishi maisha ya raha au ya amani hata kama unazopesa zote ulimwenguni..ni kwasababu ufalme wa Mungu haupo wala hautembei pamoja na wewe. Ni heri ukatubu leo ukamkabidhi Yesu maisha yako. Naye atakuokoa na kuuleta ufalme wake wa mbinguni kutembea pamoja na wewe. Hapo ndipo utakapoona tofauti yako ya jana ambayo hukuokoka na leo ambayo umeokoka.

Na wokovu unakuja kwanza kwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha na pili ni kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu.

Hivyo kama utapenda kumpokea Kristo leo basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi kwa msaada huo wa kiroho bure. Kumbuka saa ya wokovu ni sasa na wakati uliokubalika ni leo.

+255693036618/ +255789001312

Bwana akubariki

Mada Nyinginezo 

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.

TUSIRUHUSU MAMBO YA KUSUBIRISHA, YAVURUGE MUDA WETU NA MUNGU.

Mafundisho

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ulokole ni nini? Na kwanini wakristo waliookoka wanaitwa walokole?

Ulokole/ Walokole wametoka wapi?


JIBU: Kabla ya kwenda kujua maana ya ulokole, ni muhimu kujua kwanza maana ya neno ‘kanisa’..Tafsiri ya kwanza ya kanisa sio “jengo” bali ni “mkusanyiko wa watu waliomwamini Yesu”..Kwahiyo popote palipo na mkusanyiko wa watu waliomwamini Yesu, tayari hilo ni kanisa hata kama hakuna jengo. Soma mistari ifuatayo itakusaidia Matendo 2:47,1Wakorintho 1:2,14:5,14:23,15:9,16:19 n.k

Na kanisa la Kristo ni moja tu duniani kote ambalo linajulikana kama Bibi-arusi wa Kristo…Hilo ndio linajumuisha wakristo wote waliomwamini Yesu na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake (kumbuka hapa hatuzungumzii madhehebu), bali kanisa la Kristo moja ambalo pia sio jengo, bali watu wote duniani waliomwamini Yesu. Na watu hawa ambao ndio kanisa la Kristo, ndio watakaokuja kunyakuliwa siku ya parapanda katika tukio lijulikanalo kama UNYAKUO WA KANISA. Unaitwa unyakuo wa kanisa na si makanisa…kwasababu kanisa la Kristo ni moja tu.

Lakini sasa Kanisa la Kristo ni kweli ni moja lakini lina washirika wengi, na haliwezi lote kukusanyika pamoja na kwa wakati mmoja kufanya ibada, au kumwabudu Mungu, kama ni hivyo basi halina budi kuwepo na makusanyiko tofauti madogo madogo katika kila eneo ili kukamilisha kusudi lile lile la kukusanyika pamoja…Ndio hapo wakristo waliopo Mkoa wa kilimanjaro watakusanyika kivyao, na waliopo Morogoro watakusanyika kivyao huko waliko, n.k..

Lakini kumbuka Imani ni moja, na Kristo ni yule yule anayeabudiwa kote, utendaji kazi unaweza ukawa unatofautiana kulingana na kanisa na kanisa, lakini Imani ni sharti iwe ile ile moja, Bwana mmoja, Roho Mmoja, Ubatizo mmoja sawasawa na (Waefeso 4:3-7), tofauti na hapo hilo ni jambo lingine.

Sasa katika mkoa huo huo wa Morogoro pia sio wakristo wote wapo Morogoro mjini, kuna wengine wapo vijiji vya ndani huko…hao nao hawana budi wakusanyike huko walipo, hakuna sababu ya kusafiri mpaka mjini….na huko vijijini pia kuna uwezekano wa watu wasiwe karibu karibu…hivyo tena yatazaliwa makundi mengine madogo madogo mengi kulingana na mahali, hata inaweza kufikia kanisa likawa na watu watano..lakini yote yenye imani moja. Umbali ndio unaosababisha yajigawanye hivyo.

Sasa haya makanisa mengi madogo madogo ambayo yanakuwa katika eneo husika kwa kiingereza yanajulikana kama LOCAL CHURCHES, (Yaani kanisa la eneo husika aidha mtaa, au kijiji).

Na makanisa haya zamani, kutokana na uchache wa watu yaliyonayo na maeneo yalipo mengi yaliishia kudharaulika… na asilimia kubwa ya washirika wake ni maskini…kwasababu wengi wanaoishi vijijini au katika miji midogo midogo si matajiri kulinganishwa na wale wanaoishi mijini. Hivyo walidharaulika lakini kama biblia inavyosema kuwa..

Yakobo 2:5 “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao”

Hivyo hao waliodharaulika na kujulikana kama “Local churches”… ndio waliokuwa wa kiroho zaidi..Ishara nyingi na miujiza mingi ilifuatana na haya makanisa madogo madogo, kuliko hayo makubwa, …ndio watu waliokuwa na bidii zaidi ya kumtafuta Mungu, na ndio waliokuwa wanamheshimu zaidi Mungu.

Sasa kutokana na makanisa hayo madogo madogo kufahamika kama local churches…na washirika wao ndio wakajulikana kama “local people”..na kwa lugha yetu hii wakatafsiriwa kama (wa-locally) au WALOKOLE.

Hivyo kama mtu utaitwa mshamba kwa sababu unamwamini Yesu na kuzishika amri zake basi hiyo ni THAWABU. Kuliko kama utaitwa mwenye Elimu na wa-kisasa na huku umemwacha Kristo.

Ufunuo 3:17 “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona”

Usijisifie ukubwa wa kanisa unaloabudu, wala wingi wa watu wa kanisani kwenu…Jisifie Yesu uliye naye maishani mwako hata kama upo kanisa la watu watano..jitathmini je! unazishika amri zake hapo ulipo?, je! unaishi kulingana na neno lake? Kiasi kwamba hata parapanda ikilia utakwenda naye!..Je hapa nilipo nanufaika roho yangu kiasi gani?..kama sinufaiki rohoni ni heri nikatafute wenzangu wenye Imani ya kweli hata kama ni wachache, ninusuru roho yangu..kuliko kuendelea kwenye umati wa watu wengi na kuipoteza nafsi yangu…

Ni heri nijulikane mlokole lakini naenda mbinguni kuliko kukubalika na kila mtu, mwisho wa siku naishia kwenda jehanamu. Na kama pia hapo ulipo penye watu wachache huoni dalili ya kuurithi uzima wa milele ni heri ukaenda kutafuta penye watu wengi ambao wanakwenda mbinguni..Lakini siku zote kumbuka mlango ni mwembamba na njia ile imesonga na ni wachache wanayoiona…na mlango ni mpana wa njia iendayo upotevuni na wengi wanauendea.

Bwana akubariki na Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?

MIHURI SABA

Wafilisti ni watu gani.

YEREMIA

MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini wakristo wengi ni maskini?.

Mtu anayeuliza swali hili ninaamini kabisa anauliza kutoka katika dhana hii “Kama Mungu ni tajiri, kwanini basi na watu wake wasiwe matajiri kama yeye”…Na ndio maana swali kama hili la kwanini wakristo wengi ni maskini linajengeneza kichwani mwake…Lakini laiti kama angejiuliza kwa kulinganisha wakristo na watu wengine, au kuulinganisha ukristo na dini nyingine basi swali hili ninauhakika lingeshajijibu lenyewe kichwani mwake..

Kwani bila shaka hakuna asiyejua idadi ya matajari na maskini duniani haiwezi kuwa sawa na wala haitakaa ikaribiane daima, karibu katika kila Nyanja na kila eneo na kila sekta, utakuta maskini au watu wenye uchumi wa kati ni wengi kuliko matajiri, hata ukienda katika mataifa yanayojiona kuwa ni matajiri, hata ukirudi mataifa maskini, hata ukienda katika dini zote, sio tu katika ukristo, ukienda pia kwa waislamu utakuta waislamu wengi ni maskini kuliko matajiri, ukienda kwa wahindu utakuta hivyo hivyo, ukienda kwa wasio na Mungu jambo ni lile lile kwahiyo ukitazama kwa jicho hilo utagundua kuwa  hilo sio jambo la kushangaza sana.

Lakini kwasababu tunataka kuwalinganisha sawasawa na Mungu wao wanayemtumikia, naomba ubofye somo hili ulipitie taratibu naamini utapata majibu yote yaliyojibiwa kulingana na maandiko..…>>>  JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

Mada Nyinginezo:

BIBLIA INAPOSEMA “HERI WALIO MASKINI WA ROHO MAANA UFALME WA MBINGUNI NI WAO”JE HATUNA RUHUSA YA KUWA MATAJIRI KATIKA ROHO?.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWANINI LEO HII KUNA KUNDI KUBWA LA WAKRISTO WALIORUDI NYUMA?

Shalom. Karibu tujifunze Neno la Mungu, maadamu ule mwisho unakaribia..

Kila siku tunapaswa tukumbuke kuwa wokovu ni tunu ya thamani ambayo tunapaswa tuishikilie kwa gharama zozote, wokovu kuupata ni rahisi sana, lakini kuushikilia mpaka mwisho si kitu kirahisi, kwasababu kuna ufalme mwingine (wa giza) hapa duniani ambao upo mahususi kwa kazi hiyo moja tu ya kuhakikisha watu wanaupoteza wokovu hata kama walikuwa wameshaupata.

Na ndio hapa wahubiri tunapaswa tusisitize kwa watu, Kwasababu ndivyo walivyofanya hata na mitume (baba zetu wa imani), ukiangalia utaona mafundisho yao yote yalikuwa ni ya kutilia msisitizo  suala la kuishindiania imani, wakatuambia TUISHINDANIE imani ambayo tumekabidhiwa sisi watakatifu mara moja tu.

Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”.

Sio kwamba walikuwa hawaoni fursa za kibiashara zilizokuwa zimewazunguka mitaani mwao, walikuwa wanaziona, pengine hata zaidi ya sisi, lakini hawakuona sababu ya kutuandikia kwenye hichi kitabu kinachoitwa biblia, kwasababu walijua  vita hasaa vipo wapi, mapambano hasa ya mwanadamu duniani yapo wapi..

Tukumbuke kuwa tukibadilishwa maisha yetu, na kufanywa kuwa viumbe vipya, mambo hayatabakia kuwa vilevile kama yalivyokuwa mwanzoni.. Shetani ni lazima aamke na kuanza kuuwinda wokovu wako kwa gharama zozote zile.. atakuchukia kwa ukomo wa chuzi pale tu atakapokuona unaanza kupiga hatua katika wokovu wako, na sio katika mafanikio ya biashara yako, shida yake kubwa ni Imani yako.

Na katika kipindi ambacho unapaswa ujiandae kukutana naye uso kwa uso basi ni wakati ambapo umeanza maisha mapya ya wokovu.

Lakini kama usipoliweka hilo akilini, ukaambiwa ukiokoka basi, wewe ni wa mbinguni moja kwa moja, njoo sasa tukufundishe mambo mengine ya kidunia..Nataka nikuambie maisha yako ya rohoni yapo hatarini sana kugeuka.(Ndio maana kuna kundi kubwa la wakristo waliorudi nyuma leo hii).

Kwasababu shetani ni lazima atahakikisha analeta mambo mawili kwako, la kwanza ni DHIKI, na la pili ni UDHIA.

Mathayo 13:20 “Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha;

21 lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa”.

Dhiki, ni mateso unayoyapata kutokana na kile ulichokiamini; Na udhia ni maudhi utakayoyapata kutoka kwa watu, kwa kile unachokiamini, huu ndio wakati ambapo pengine hata ndugu/familia hawatakuelewa au watakutenga, ni wakati ambapo pengine utajikuta unapingwa na viongozi wako wa dini, au wanakupiga na kukufunga kisa tu umemfuata Yesu, au umekuwa na msimamo Fulani wa Neno la Mungu, ni wakati ambapo mambo yako yanaweza yasiende sawa, utapitia kuvunjwa moyo mara kadhaa, lakini Mungu atakuwa pamoja na wewe,  kumbuka yote hayo yanasababishwa na shetani, ili tu kukutikisha urudi ulipotoka. Yanatokea kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Mungu.

Lakini ni ya muda tu, hayawezi kudumu milele, Mungu hawezi kuruhusu yadumu milele. Kuna kipindi kitafika yataisha. Lakini ni wachache sana wanaoweza kuvumilia hata hicho kipindi kiishe..

Na hapa ndipo watu wengi wanaporudi nyuma. Na kuuacha wokovu. Kwasababu hawakujiandaa kwa huo wakati.

Kumbuka kuwa tutaufikia mwisho mzuri wa imani, kwa kuishindania kwa gharama zozote na  kwa kuvumilia..hilo tu.

Luka 8:15 “Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia”.

Bwana atusaidie tuweze kuyashinda hayo yote.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?

MUNGU HANA MBARAKA MMOJA TU!..MWAMINI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka?

(Maswali yahusuyo pasaka)

Swali: Je kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka, kwamfano mwaka 2023 pasaka ilikuwa ni Aprili 13, lakini mwaka huu 2024 ni Marchi 31, na inategemewa kubadilika tena katika mwaka ujao na miaka yote inayokuja, kwanini iwe hivyo, wakati Krismasi ni tarehe ile ile 25 miaka yote?


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa pasaka ni moja ya sikukuu 7 za wayahudi, na inasheherekewa na wayahudi katika kila terehe 14 ya mwezi wao wa Kwanza, ambapo mwezi wao wa kwanza unaangukia katikati ya mwezi Machi na Aprili kwa kalenda tunayoitumia sisi.

Lakini kuhusiana na kwanini tarehe za pasaka zinabadilika kila mwaka kwa upande wa wakristo, ni kutokana na MWONEKANO WA MWEZI.

Mwezi unapozuka mzima (yaani angavu/full moon) basi jumapili inayofuata ndiyo inayosherekewa na wakristo wengi kama jumapili ya pasaka.

Kuna miaka ambapo “mwezi mwangavu” unawahi kuchomoza na kuna miaka unachelewa. Ikiwa na maana kuwa kama mwezi mwangavu  utaonekana jumatano basi jumapili inayofuata itakuwa jumapili ya pasaka, ambayo itakuwa ni baada ya siku nne,  Kwamfano kwa mwaka 2023 mwezi mwangavu ulionekana jumatano ya Tarehe 5 Aprili, hivyo jumapili iliyofuata ya tarehe 9 ndio ikawa jumapili ya pasaka.

Lakini kwa mwaka 2024, Mwezi mwangavu umewahi kuonekana, kwani umeonekana Jumatatu ya tarehe 25 Machi, hivyo jumapili inayofuata ya tarehe 31 Machi, ndio itakayokuwa jumapili ya pasaka.

Lakini pia kwa mwaka 2025, Mwezi mwangavu unatarajiwa kuonekana jumapili ya tarehe 13 Aprili, hivyo jumapili itakayofuata ya tarehe 20 Aprili ndio itakayokuwa jumapili ya pasaka.

Kwahiyo hiyo ndio sababu kwanini tarehe hizo zinabadilika badilika kila mwaka, (ni kutokana na mwonekano wa mwezi).

Sasa kujua pasaka ni nini na kama wakristo ni halali kuiadhimisha fungua hapa >>PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

KWARESMA IPO KIMAANDIKO?

Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

Rudi nyumbani

Print this post

KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI

Hizi ni sababu kuu nne (4), ambazo zinampa sababu mwaminio yoyote kuihubiri injili kwa nia yote kutoka moyoni.

1) Kwasababu ni agizo kuu la Bwana.

Marko 16:15  “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16  Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”

Bwana wetu alituagiza, na kutupa jukumu la kufanya sisi kama wakristo. Sio tu kusema sisi tumeokoka halafu basi, hapana bali ni pamoja na kuwafanya wengine kuwa kama sisi, kuwafanya kuwa wanafunzi wa Kristo.

2) Kwasababu ya ushuhuda wako mwenyewe.

Mitume walikuwa na ujasiri wa kumuhubiri Kristo, kwasababu ya ushuhuda wao wenyewe kwa mambo waliyoyaona kwa  Bwana Yesu akiwatendea.

Matendo 4:18  Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.

19  Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;

20  maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.

Ukisoma pia 1Yohana 1:1-3  Mtume Yohana anasema..

1Yohana 1:1  Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;

2  (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

3  HILO TULILOLIONA NA KULISIKIA, TWAWAHUBIRI NA NINYI; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.

Hii ikiwa na maana, kuwa kila mkristo aliyekombolewa, anaoushuhuda wa mambo makuu aliyotendewa na Yesu tangu siku alipookoka, Tofauti kubwa aliyoipata katika maisha yake mpya ukilinganisha na yale ya zamani, jinsi mizigo yake ilivyotuliwa, hofu kuondolewa, magonjwa yake kuponywa, kufunguliwa, kupokea furaha ya wokovu isiyo na kiasi, amani, utulivu. N.k.

Yote haya kwa mkristo anayethamini wema wa Mungu hataona aibu kutamani na wengine wauonje uzuri huo ulio katika Kristo Yesu. Na hivyo atatoka nje! na kwenda kuwahubiria wengine Injili ya Yesu Kristo,kama mitume walivyofanya.

3) Kwasababu watu wanaouhitaji wa kusikia habari za Injili.

Hili lilimkuta mtume Paulo, Hapo mwanzoni alidhani yeye ndio anayekwenda kuwashawishi watu kuhusu Yesu, lakini siku moja aliona maono, watu wa mbali Makedonia wakiwa na uhitaji mkubwa sana wa kumjua Mungu. Hivyo akalitii ono lile akaenda.

Matendo 16:9  Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.

10  Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.

Hata sasa, wapo watu wengi wana kiu ya kuijua njia ya kweli, mioyoni mwao wakiwa na shauku ya kuifahamu hiyo NJIA. Lakini sisi tukikaa na kusema hakuna mwenye haja, twajidanganya. Hatupaswi kuona watu kwa nje wanatuchekea, wanafurahi, wana raha, tukadhani hali zao rohoni ndio hivyo zilivyo, tukapuuzia kuwahubiria injili. Wengi wapo kwenye vifungo na wanatamani wapate msaada wa kutoka huko, hawasemi tu. Na anayeweza kuwatoa hapo ni Kristo tu peke yake. Siku ukizungumza nao ndio utajua kweli walikuwa na haja na Kristo. Hivyo usichague wa kumshuhudia. Fahamu tu watu wana haja na kuujua ukweli. Hubiri injili ya Kristo.

4) Kwasababu roho za watu zinakwenda kuzimu.

Tunajua mtu akifa nje ya Kristo, hakuta tumaini, ni moja kwa moja jehanamu. Tengeneza picha ndugu zako uwapendao, rafiki zako, wazazi wako, na wanadamu wenzako wanakwenda kwenye moto wa milele. Wewe una raha gani leo hii usiwashuhudie habari za Yesu Kristo?.Embu tengeneza picha habari ya Yule tajiri na Lazaro, (Luka 16:19-30) alitamani, mtu atoke kuzimu akawahubirie watu injili ili wasifike mahali pale pa mateso, lakini akaambiwa wapo Musa na manabii huko duniani (ambao ndio sisi), tuwahubirie.

Hivyo kwa sababu hizo kuu nne (4), wewe kama mwaminio uliyeokoka, huna budi kuwashuhudia wengine habari za Kristo. Utasema mimi sina uzoefu, Kumbuka Yesu haitaji uzoefu wako, kuwaokoa watu, kwasababu hata wewe hukuupokea kwa uzoefu wowote, anahitaji kuwaambia Yesu anasemehe dhambi, anaokoa wanadamu, anatoa uzima wa milele bure, anatuepusha na hukumu ya milele, anatua mizigo ya watu, anafariji, anaponya roho, anatupa nguvu ya kuushinda ulimwengu na dhambi. Njoo kwake, akufanye kiumbe kipya upokee uzima wa milele. Hivyo tu. Na hayo mengine mwachie yeye, usifikiri fikiri atakuongoza kwa jinsi utakavyokuwa unasema.

Mathayo 10:20 “ Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.

Anza sasa.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NI INJILI GANI UNAHUBIRI?

INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

Rudi nyumbani

Print this post

Ubani ni nini?.. Na je wakristo tunaruhusiwa kuchoma ubani?

Swali: Je kuna ubani katika biblia?.. Na kazi ya Ubani ni nini?


Jibu: Ubani ni moja ya viungo vilivyotumika zamani kutengenezea manukato matakatifu yaliyoitwa “Uvumba”..

Viungo hivi (ubani) vinatokana na utomvu unaozalishwa na mmea ujulikanao kama “Boswelia” (Tazama picha juu). Mti wa Boswelia unaanza kutoa utomvu kati ya miaka 8 mpaka 10 baada ya kupandwa kwake, miti hii pia inastawi Zaidi sehemu zenye ukame.

Katika biblia “ubani” ulichanganywa pamoja na viungo vingine vitatu (3) ambavyo ni NATAFI, SHEKELETHI na KELBENA, kutengeneza Manukato matakatifu yaliyoitwa Uvumba ambapo Kuhani mkuu aliyachoma pamoja na kisha kuvukiza moshi ndani ya ile Hema kabla ya kufanya shughuli za upatanisho.

ubani katika biblia

Na uvumba wa aina hiyo, haukuruhusiwa kutengenezwa mfano wa huo kwa matumizi yoyote yale tofauti na hayo ya nyumba ya Mungu.. (maana yake haikuruhusiwa mtu kutengeneza kwa fomula hiyo na kufanya kama marashi nyumbani kwake, au ibada nyumbani kwake, ilikuwa ni kosa).

Kutoka 30:34 “Bwana akamwambia Musa, Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja;

35 nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu;

36 nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.

37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili ya Bwana.

38 Mtu ye yote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake”

Sasa kuelewa kwa upana Zaidi kuhusu “Uvumba” na maana yake kiroho basi fungua hapa >>KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

Lakini swali ni je! Sisi wakristo tunaruhusiwa kuchoma Ubani katika ibada au manyumbani mwetu?

Jibu ni La!.. Wakristo hatujapewa maagizo yoyote ya kuchoma ubani wala kujishughulisha nao. Manukato ya Ubani yalitumika katika agano la kale katika hema ya kukutania, na baada ya agano jipya kuanza, mambo hayo yakawa ni ya KIROHO na si ya kimwili tena, hivyo hakuna Uvumba, wala ubani wala hivyo viungo vingine unaopaswa kuhusishwa na ibada yoyote katika agano hili jipya.

Kwanini Ibada hizo za Kuvukiza uvumba na ubani hazipo tena sasa?

Ni kwasababu ile ile za kuondoka ibada za kafara za wanyama.. Hatuwezi sasa kutumia Ng’ombe au kondoo kwaajili ya utakaso wa dhambi zetu, na wakati kuna damu ya YESU, ambayo inatusafisha sasa katika ulimwengu wa roho.

Vile vile hatuwezi kuchoma ubani, na kuvukiza uvumba kama njia ya kuvuta uwepo wa Mungu na wakati tunaweza kufanya hivyo kwa njia ya sala na maombi.

Zaburi 141:2 “Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni”

Sasa Kafara za wanyama (Ng’ombe, mbuzi, kondoo na njiwa) na kuchoma ubani zimebaki kuwa ibada za miungu!… Wote wanaofanya hizo, wanavuta uwepo wa mapepo na si wa Mungu! Hivyo ni muhimu kuwa makini.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

SISI TU MANUKATO YA KRISTO.

MADHABAHU NI NINI?

Chetezo ni nini katika biblia? (Walawi 10:1)

NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini Bwana achukizwe na mtumwa yule aliyeficha talanta yake ardhini? (Mathayo 25:26-30)

Swali: Kwani kulikuwa na ubaya gani, wa bwana yule kurudisha talanta ile moja?, kwani hakupoteza kitu wala hajaleta hasara yoyote?..je kulikuwa na sababu gani ya yeye kuhukumiwa vile?.


Jibu: Ili tuweze kuelewa vizuri sababu ya mtumwa yule kuhukumiwa vile, tuisome habari yenyewe kwa uchache..

Mathayo 25:14  “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita WATUMWA WAKE, akaweka kwao MALI ZAKE.

15  Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri”.

Nataka tuzingatie hayo maneno mawili “Watumwa wake” na “Mali zake”.

Kwa haraka tukiisoma habari hii tunaweza kutafakari kuwa huyu mtu aliwekeza mali zake kwa “rafiki zake” au “ndugu zake”..

Ingekuwa heri kama ingekuwa ni “rafiki zake” au “ndugu zake” kwani hata wasingeleta faida yoyote angeweza kuwaelewa  lakini aliwekeza mali zake kwa “watumwa wake” ambao ni watu anaowalipa mshahara huenda kila siku au kil amwisho wa mwezi.

Sasa ili tuelewe vizuri, tengeneza picha una biashara yako (labda duka) halafu umeajiri mfanya kazi pale na kukubaliana naye mshahara, na ukaondoka na kurudi jioni na kukuta hajafanya kazi yoyote na Zaidi anakuambia fedha zako za mtaji zipo pale pale hajazigusa.

Bila shaka utachukizwa naye..kwanini?..cha kwanza ulitegemea kupata faida ndio maana wewe ukamweka pale, pili mshahara wake unatokana na faida katika hiyo kazi, kwa utendaji wake..

Kwahiyo kama hatafanya kazi yoyote na mwisho wa mwisho wa siku au mwezi atataka mshahara je utamlipa nini?…maana utakapofika mwisho wa mwezi atakudai mshahara, na wewe umeshaingia naye mkataba wa kumlipa..

Kwahiyo ni wazi kuwa ni lazima utakasirika, kwasababu kutokufanya kwake kazi ni hasara kwako, kwasababu mwisho wa siku ni lazima utamlipa, hivyo anakurudisha nyuma hata kama hajagusa mtaji wako, lakini mwisho wa siku utaathirika wewe katika wakati wa kumlipa mshahara..Hivyo ni hasara!!!

Ndicho kilichowatokea yule mtumwa aliyeficha talanta aliyopewa na bwana wake, maana yake ni kweli kairudisha ile talanta kama ilivyo, lakini mwisho wa mwezi atataka mshara (kwasababu yeye ni mwajiriwa na si ndugu/rafiki).. sasa bosi wake atatolea wapi fedha ya kumlipa ikiwa hajazalisha chochote?..

Ndio maana bwana wake akamwambia ni heri hata angeipeleka kwa watoa riba kuliko kuificha ardhini.

Hili ni fundisho kamili kwa wakristo kwamba vipawa na karama na uwezo tuliojaliwa na Bwana basi tutumie katika kumtumikia Mungu pasipo udhuru, kwasababu sisi ni watumwa wake!, ametuweka kwa faida yake…

Bwana atusaidie tusifiche talanta zetu ardhini bali tuzitendee kazi au tuzipeleke kwa watoa riba.

Mathayo 25:27  “basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28  Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

29  Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

30  Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”

Kufahamu kwa mapana maana ya “kupeleka fedha kwa watoa riba”, basi fungua hapa >>>Watoao riba ni akina nani? (Mathayo 25:27)

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

JINSI YA KUISHINDA HALI YA MSONGO WA MAWAZO.

BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”

Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini maombi kwa Marehemu si sahihi kibiblia?

Jibu: Katika biblia hakuna mahali popote panapoonyesha marehemu waliombewa..isipokuwa katika sehemu moja tu inaonyesha Marehemu mmoja aliyekuwepo katika mateso ya kuzimu aliomba ndugu zake walio hai wakahubiriwe injili ili wasifike katika dhambi na kwenda kule aliko, lakini tunaona maombi yake hayo hayakuwa na matokeo yoyote.
Hebu tuisome hiyo habari..

Luka 16:27 “Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishiwa hata na mtu akifufuka katika wafu”

Umeona?..Huyu Tajiri alijaribu kuwaombea watu walio hai wasifike alipo lakini maombi yake yalizuiliwa, halikadhalika Sisi tulio hai hatuwezi kuwaombea watu waliokufa kwamba watolewe katika mateso ya kuzimu.

Kama kuna maombi ya kuwaombea wafu watoke katika mateso ya kuzimu na kuingia paradiso, basi vile vile yatakuwepo pia maombi au sala za kuwatoa watu peponi na kuwapeleka kuzimu.. Lakini kama hakuna maombi ya mtu kumtoa mtu peponi(yaani paradiso) na kumpeleka kuzimu…vile vile hakuna maombi yoyote ya kuweza kumtoa mtu kuzimu na kumpeleka peponi.

Utasema tunazidi kulithibitisha vipi hilo kimaandiko?

Hebu tuzidi kuisoma hiyo habari ya Tajiri na Lazaro…Tuangalie maombi mengine aliyoomba kuhusiana na yeye kutolewa kule.

Luka 16:23 “Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ILI WALE WATAKAO KUTOKA HUKU KWENDA KWENU WASIWEZE; WALA WATU WA KWENU WASIVUKE KUJA KWETU”.

Hapo mwisho anasema..kati Yao (hao walio kuzimu na walio peponi)..KUMEWEKWA SHIMO KUBWA kama mpaka, ili walio kuzimu wasiweze kuvuka kuingia peponi na walio peponi wasivuke kwenda kuzimu..Ikiwa na maana kuwa hakuna mwingiliano wowote wa walio kuzimu na walio peponi..Hilo shimo katikati yao lipo mpaka sasa.

Hivyo kwa hitimisho, maombi ya kuwaombea heri Marehemu au kuwaombea wapunguziwe adhabu ni maombi yasiyo ya kimaandiko na hayana matokeo yoyote… Vile vile sala za kuwaomba watakatifu waliofariki watuombee halipo kimaandiko.

Ni vizuri kutengeneza maisha yetu hapa duniani kabla ya kufa, kwa kumwamini Bwana Yesu na kutubu dhambi, kwasababu tukishakufa hakutakuwa na nafasi nyingine ya pili.

Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”.
Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je sisi wakristo tunaruhusiwa kufanya 40 za marehemu?

MATESO YA KUZIMU.

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

USIRUHUSU INZI WATUE JUU YA ROHO YAKO.

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

Rudi nyumbani

Print this post

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Wakati ambapo Israeli inapitia manyanyaso makali kutoka kwa wakaanani kwa miaka 20, mpaka yakawafanya wamlilie Mungu kwa nguvu ili awaokoe..Tunasoma kwenye biblia Mungu alisikia kilio chao akawanyanyulia mwamuzi Debora pamoja na baraka..

Hivyo Mungu akawaagiza wana wa Israeli wapange majeshi, ili wakapigane na adui zao, na hakika Bwana atawashindia..makabila mengi yalikubali kupeleka majeshi yao, lakini yapo makabila mengine hayakutaka kujishughulisha na jambo hilo..na hayo si mengine zaidi ya  Dani, Asheri, na nusu ya kabila la Manase na Gadi. Haya yote yalikuwa mbali kidogo na eneo la vita, Yaliona kama vile vita haviwahusu wao, hivyo yakawa bize kuendelea na mambo yao..

Waamuzi 5:17

[17]Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani, 

Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? 

Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, 

Alikaa katika hori zake.

Kwamfano kama hapo maandiko yanasema Dani alikaa katika merikebu, maana yake ni kuwa alikuwa ni mfanya biashara, aliona kuacha biashara zake za melini, za uchukuzi, na kwenda kujishughulisha na vita, ni upotezaji wa muda, kupigania taifa la Mungu ni kazi kichaa, wacha niendelee na biashara zangu..Na ndivyo hata hayo mataifa mengine yalivyokuwa, yalichowaza ni biashara, na mahangaiko ya hii dunia mpaka Agizo la Mungu likawa halina maana tena kwao, hata utumwa wa taifa lao hawakuuona, mateso na dhihaka taifa lao lilipokuwa linapitia hawakuona kama ni kitu zaidi ya biashara.

Ndipo Debora akaongozwa na Roho kutunga wimbo huo wa kuwashutumu ambao mpaka sasa tunausoma..

Hata sasa, tabia za makabila haya kama Dani zipo miongoni mwa wakristo wengi, ni mara ngapi utamwambia mkristo twende tukashuhudie, kwasababu tumeamuriwa kufanya hivyo na Kristo..lakini atakuambia sina muda, nipo buzy, sina mtu wa kumuacha kwenye biashara yangu…

Anaona biashara yake ni bora kuliko kuokoa roho za watu wanaopotea, huyu ni Dani anayekaa merikebuni..kipaumbele chake ni shughuli za huu ulimwengu, kazi, pesa, ndizo anazozitaabikia kutoka Januari mpaka Disemba, mwaka kwa mwaka, hana rekodi ya kufanya chochote kizuri  kwa ajili ya ufalme wa Mungu, lakini yupo tayari kujenga majumba, na mahoteli, na ma-meli ili kutanua wigo wake wa kibiashara..

Ni kweli Mungu anaweza kuokoa watu wake pasipo wewe, lakini vilevile kumbuka Mungu anaweza kubaki na mbingu yake pasipo wewe..usipokwenda mbinguni hakumpunguzii yeye kitu.

Hatushangai hata ni kwanini hili kabila la Dani halionekani miongoni mwa makabila ya Israeli yatakayookolewa siku za mwisho (Ufunuo 7:1-8). Sababu mojawapo ni hii..Na sisi tujichunguze tutambue kipaumbele chetu kwa kwanza ni kipi. Je siku ile tutakuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya Kristo?

Bwana atupe kuliona hili.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.

Hori ni nini kibiblia (Waamuzi 5:17, Luka 2:7)?

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?.

NYOTA ZIPOTEAZO.

Kuna tofauti gani kati ya ‘Mungu’ na ‘Mola’?

NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?

Rudi nyumbani

Print this post