Title kuota unapewa pesa

KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

Awali ya yote ili upate ufasaha wa ndoto yako, na kuepuka kudanganywa na kila aina ya tafsiri mtu yeyote anayoweza kukuletea, awali ya yote unapaswa ufahamu ndoto yako inaangukia katika kundi lipi,

Yapo makundi makuu matatu (3) ya ndoto:

  1. Kundi la kwanza: ni zile ndoto zinazotokana na Mungu,
  2. kundi la pili: ni zile zinazotokana na adui(Shetani)
  3. kundi la tatu: ni zile zinazotokana na mtu mwenyewe,

Ndoto zinazoangukia katika kundi hili la tatu ndizo zinazootwa na watu mara kwa mara kila siku na kama mtu asipoweza kuzitambua atajikuta anahangaika nazo, na huku hazina maana yoyote ya kumsaidia, kwasababu ni ndoto zinazokuja kutokana na shughuli anazozifanya kila siku au mazingira yanayomzungumka muda wote hivyo hizi huwa hazibebi  ujumbe wowote..

Kwahiyo ni rahisi ubongo wake kuchukua yale matukio anayoyofanya kila siku na kuyatengenezea matukio yanayofanana na hayo katika ndoto usiku na kuota, ukijiona unaota hivyo basi puuzia ndoto hizo

Ikiwa unahitaji kufahamu kwa undani juu ya makundi haya basi pitia somo hili kwanza >>>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?   kisha ndio tuendelee,

 Kwamfano ndoto za namna hii za kujiona unapewa pesa, utakuta mtu mmoja kazi yake kila siku ipo kwenye pesa kama vile benki au mfanyabiashara ambaye muda wote analipa na kulipwa pesa, hivyo kuota anapewa pesa linaweza kuwa ni jambo la kawaida kwake kutokea katika ndoto zake za kila siku, kwasababu ubongo ulishajiengenezea ulimwengu kama huo.

Lakini ikitokea umeota ndoto katika mazingira, ambayo hayaendani na wewe kupewa pesa, au umeota ndoto hiyo na ukaiona si ndoto ya kawaida, au ulikuwa katika maombi ya kumwomba Mungu kitu Fulani na imekuja na uzito Fulani hivi, au amani Fulani hivi, basi fahamu kuwa upo ujumbe unapaswa kujifunza ndani yake.

Kumbuka kibiblia Fedha inawakilisha chombo cha kuletea jawabu.

Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote”.

Hivyo Mungu kukuonyesha katika ndoto, unapewa fedha, ni ishara kuwa amekupa jawabu la ombi lako, na hivi karibuni utapata haja yako..Ila tilia maanani kitu kimoja hapo biblia inaposema, fedha huleta jawabu la mambo yote haimaanishi  kuwa inaleta majibu mpaka kwenye mambo ya rohoni hapana, fedha haiwezi kuleta uzima ndani ya mtu wala haiwezi kununua upendo..lakini kama ukichunguza hapo utaona mistari hiyo inalenga mambo ya ki mwilini..kama vile shughuli za karamu, nguo, chakula, nyumba, gari, biashara, ambavyo hivi kimsingi vinahudumiwa na fedha..

Pia tazama..

1  Kuota ajali.
2 Kuota upo nchi nyingine.
3 Kuota unajifungua
4 Kuota upo makaburini
5 Kuota unacheza mpira
6 Kuota unaanguka
7 Kuota upo kanisani
8 Kuota umeachwa na gari
9 Kuota unang’oka meno
10 Kuota unaanguka

Lakini tukirudi kwenye hiyo ndoto ya pesa vile vile usitegemee sana kuwa atatumia njia hiyo hiyo uliyoiona kwamba kweli kuna mtu atakujana  kukupa wewe fedha hapana, inaweza ikawa hivyo au isiwe hivyo, anaweza  kutumia njia pengine ya kuirutubisha kazi yako unayoifanya sasa hivi ,au ukapata kibali mahali Fulani pengine kazini kwako, ambapo boss wako atakulipa vizuri zaidi kuliko sasa hivi, au ukapata mkopo wa kufanya biashara yako n.k.Na kama ukijiangalia ndio utagundua vitu vya aina hiyo hiyo ndio ulivyokuwa unamwomba Mungu…

Hivyo ametumia ndoto ya fedha kama ishara ya kukuonyesha kuwa maombi yako ameyasikia,..Lakini usitazamie kuwa mtu anayemwomba Mungu mambo ya rohoni kama vile uzima wa milele, au Roho Mtakatifu, au nguvu za Mungu, ataonyeshwa ndoto za namna hiyo kama jibu la maombi yake hapana.. Mungu atamwonyesha Maono ya rohoni, pengine usishangae mtu kama huyo kuona maono ya mbinguni, au kukutana na malaika ndotoni, au kuisikia sauti ya Mungu ikisema naye, au kuota anahubiri au anafundishwa biblia n.k…

Hivyo kaa katika matarajio huku ukiulinda ukamilifu na utakatifu  katika kazi yako, ndipo Mungu ataitimiza ahadi yake juu yako. Lakini kama wewe upo nje ya Kristo ukaota ndoto kama hiyo, fahamu kuwa ni ishara mbaya nayo ni ishara ya upotevu zaidi..utakwenda kufanikiwa lakini ni ili upotee..

Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”.

Usisibirie udanganyifu wa mali au mafanikio vikuangamize..Mrudi Muumba wako mapema, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa Jina la YESU KRISTO ikiwa bado hukubatizwa kisha anza kumwangalia Mungu ili yeye atembee pamoja na wewe katika njia zako zote.

Ubarikiwe.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mithali 1:32

kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.

Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?

USHUHUDA WA RICKY:

MTETEZI WAKO NI NANI?

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

NOTI YA UFALME WA MBINGUNI.

LULU YA THAMANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je kuwashwa mkono ni ishara ya kupata pesa?

Swali: Je ni kweli kwamba kiganja cha mkono wa kushoto au wa kulia kikiwasha basi ni ishara ya kupata pesa?


Jibu ni LA!.. hakuna uhusiano wowote  kiganja kuwasha na fedha kumjia mtu. Labda kama mtu huyo ana pepo la utambuzi ndani yake..

Kama mtu ana pepo la utambuzi basi anaweza kuhisi kitu Fulani kikimjia, ikiwemo pesa kutoka katika chanzo kisicho cha kiMungu, au akahisi hatari kutoka katika upande wa maadui zake (maana yake upande wa Mungu), na ishara hizo anaweza kuzihisi kwa njia kama hizo za kuwashwa mkono, au kuwashwa sehemu nyingine ya mwili.

Lakini mtu mwenye Roho wa Mungu hisia zake zipo katika Neno la Mungu..Anaposoma Neno la Mungu na kudumu katika uwepo huo basi anaweza kuhisi Baraka zijazo, au hatari ijayo.

Kwamfano Neno hili katika biblia linaweza kukupa hisia za Baraka zijazo…

Mithali 13:11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.

Mtu akilisoma hili Neno la kulishika, tayari atakuwa anajua ni nini kitafuta katika shughuli anayoifanya.. lakini si kukisikilizia kiganja kinasema nini!.. Na maneno mengine yote ya Mungu ni hivyo hivyo..

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba,  Elimu ya kusoma viungo vya mwili na kutabiri mambo yajayo ni elimu ya adui na ya kupotosha..

Lakini pia kumbuka si kila anayewashwa mkono basi ana pepo la utambuzi!.. La!, mkono unaweza kuwasha kwa sababu nyingine yoyote ya kibaolojia, na mtu asiwe na pepo!.. (Hata hivyo asilimia kubwa ya wanaowashwa mikono hawana mapepo). Hivyo kilicho kikubwa na cha msingi ni kudumu katika Neno la Mungu.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)

Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).

MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA.

Biblia inaposema Yesu ameketi mkono wa kuume inamaana gani?

Rudi nyumbani

Print this post

KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?

Ndoto za ajali zinaweza kuja katika maumbile mengi tofauti tofauti, wengine wanaota ajali za pikipiki, wengine za magari, wengi ndege, wengine meli, wengine treni, katika namna tofauti tofauti. Wengine wanaota mtu kagongwa na gari, au magari yanagonga gongana n.k… kwa vyovyote vile, ndoto hizo zinabeba maudhui moja nayo ni “AJALI”

Sasa ili kupata tafsiri sahihi ya ndoto hiyo ni vizuri ukajitambua wewe upo katika kundi gani.

1.) Kundi la kwanza ni waliookoka.

2) Kundi la pili ni wenye dhambi.

Tukianzana na kundi la kwanza: Ikiwa wewe, umeokoka (yaani unao uhakika umesimama ndani ya Kristo).  Basi fahamu kuwa ni Mungu anakutahadharisha tukio lililopo mbele yako, aidha kuna ajali utakutana nayo, au itatokea kwa mtu mwingine, au mahali fulani. Hivyo  unachopaswa kufanya, ni kuingia katika maomba ya kuvunja hiyo mipango ya adui. Ambayo pengine imepangwa kwako au kwa mtu mwingine..kemea kwa bidii kwa mamlaka uliyopewa katika jina la Yesu. Na Mungu ataisambaratisha hiyo mipango yote.

Ikiwa ndoto hiyo imekuja kwa uzito usiipuuzie, kwasababu Mungu kukuonyesha hivyo, ni ili usimame kama askari wa Mungu kushindana na hizo nyakati mbaya kabla hazijafika.( Soma Ayubu 33:14-15)

Kundi la Pili: Mwenye dhambi.

Ikiwa wewe ni mwenye dhambi(yaani hujaokoka, Kristo hayupo ndani yako). Ujue ndoto hiyo ni ishara ya tahadhari kubwa sana kwako. Kwamba kipindi si kirefu Mungu atakuadhibu, na kuadhibu kwake, kunaweza kukawa ni kifo cha ghafla, au kunaswa katika dhambi zako unazozifanya, na ukashindwa kutoka huko milele.

Soma hii Habari kwa makini;

Ezekieli 7: 6 “Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.

7 AJALI YAKO IMEKUJIA, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.

8 BASI HIVI KARIBU NITAMWAGA GHADHABU YANGU JUU YAKO, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.

9 Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga.

10 ANGALIA, SIKU HIYO; ANGALIA, INAKUJA; AJALI YAKO IMETOKEA; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka”.

Umeona? Hayo maandiko yenyewe yanajieleza, ikiwa wewe ni mzinzi, fahamu kubwa ajali ya Ukimwi ipo mbele yako, wewe ni fisadi ajali ya vifungo ipo mbele yako, wewe ni mwizi ajali ya kifo ipo mbele yako, wewe ni mshirikina ajali ya jehanum ipo mbele yako.

Kwa ujumla kama wewe ni mwenye dhambi ujue mwisho wako upo karibuni sana. Na ukifa ni motoni. Ndio tafsiri ya ndoto hiyo.

Unasubiri nini mpaka hayo yote yakukute, ikiwa upo tayari leo kutubu dhambi, basi, Bwana Yesu atakusamehe, na kukuepusha na madhara hayo yote aliyokuonyesha mbele yako. Angeweza kukaa kimya tu, hayo mambo yakukute kwa ghafla, lakini kwasababu hataki uangamie ndio maana amekutahadharisha mapema.. Hivyo leo hii fungua moyo wako, kubali kugeuka, na uache dhambi zako zote, ili Kristo ayatengeneze tena Maisha yako.

Ikiwa upo tayari kutubu leo, basi fungua hapa, kwa ajili ya mwongozo wa SALA YA TOBA. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Angalia pia Kuota Unajenga nyumba

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

KUOTA UNA MIMBA.

Usipokuwa na uelewa wa kutosha  juu ya ndoto, unaweza ukajikuta unatoka nje ya kusudi la Mungu ambalo amekukusudia wewe uishi kwalo hapa duniani..

Na hiyo imewafanya watu wengi wazunguke huko na huko, kutafuta tafsiri ya ndoto zao..Lakini jambo la kwanza na la msingi sana kufahamu ni kuwa, tunapaswa kujua kuwa ndoto yoyote ni lazima iwepo katika mojawapo ya  makundi haya matatu:

> Kundi la kwanza ni ndoto zinazotokana na Mungu,

> Kundi la Pili ni ndoto zinazotokana na shetani,

> na kundi la tatu ni ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe.

Sasa ndoto hizi zinazotokana na mtu mwenyewe huwa zinaathiriwa sana na mambo mbalimbali aidha kutokana na mazingira ya mtu yanayomzunguka au shughuli anazozifanya mara kwa mara,  au mambo anayoyawaza kila wakati..Na aina hii ya ndoto ndiyo inayochukua asilimia kubwa sana ya ndoto watu tunazoziota kila siku, naweza kusema hata asilimia 95 ya ndoto tunazoziota kila siku na hizi huwa hazina maana sana, lakini watu kwa kukosa ufahamu imefanya wahangaike kutwa kuchwa kutafuta tafsiri ya kila ndoto yanazoziota mpaka inawafanya kuwa watumwa wa ndoto…Kumbe kiuhalisia sio kila ndoto ina ujumbe wa kutufaa..

Hivyo mtu akishakuwa na uelewa wa namna ya kuzigawanya ndoto hizi katika makundi haya hatapata shida kuitafsiri ndoto yake..Hivyo nakuashuri pitia kwanza somo hili kisha ndio tuendelee.  >> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI? 

Sasa ukiota una mimba: Ikiwa ndoto hiyo haitokani na shughuli zako mwenyewe au mazingira yanayokuzunguka, au mawazo unayoyawaza kila mara, kwasababu kumbuka ndoto kama hizi huwa zinawatokea mara nyingi wanawake, kwahiyo uwezekano wa kuangukia katika  kundi hilo la tatu la ndoto ni mkubwa kwasababu wanawake maisha yao tangu wakiwa watoto wanawaza siku moja ni kuwa na mtoto kwahiyo kuota wamebeba mimba si jambo la kushangaza, au utakuta mwingine maisha yake yote anatamani sana kuwa na mtoto, hana watoto, moja kwa moja mtu kama huyo ni rahisi kuota ni mjamzito au mwingine utakuta anaishi na mwanamke mjamzito  karibu na mazingira yake au jana amemwona mwanamke mmoja barabarani akipita akiwa mjamzito akajikuta usiku anaota kabeba mimba akadhani kuwa ndoto hiyo inamaana sana kwake..,

Ikiwa ni hivyo, basi zipuuzie tu, ni ndoto zinazokuja kutokana na mawazo yako. Hizo hazibebi ujumbe wowote kwako.

Lakini hapa tunadhania kuwa ndoto hiyo haijatoka katika vyanzo vya namna hiyo, 

Sasa fahamu kuwa tendo lolote kuchukua mimba liwe ni jema au liwe ni baya, liwe limekuja kwa  njia ya uzinzi au kwa njia ya haki ni lazima tu kiumbe kipya kije duniani mwisho wa siku hakuna namna!..Na kabla hakijaja lazima dalili Fulani zionekane…Hivyo kama ndoto yako  imekuwa ni ya kujirudia rudia basi itilie maanani zaidi kwasababu inaweza kuwa imebeba ujumbe kutoka kwa Mungu,..

Utakumbuka Farao alipoota ndoto ile ihusuyo miaka saba na njaa na miaka saba ya neema, ilikuja mara mbili, hata kama ilichukua taswira nyingine lakini ujumbe ulikuwa ni mmoja..ndipo akawa na uhakika wa kuwa ndoto ile ni ya kuizingatia..Vivyo hivyo na wewe ikiwa unaota mara kwa mara una mimba, ni mjamzito izingatie sana ndoto hiyo.

Kwahiyo jambo unalopaswa kufanya hapo kwa kuwa wewe ndiye unayeyafahamu maisha yako zaidi kuliko mtu mwingine yeyote , kaa chini kwa utulivu mwingi utafakari maisha yako na njia yako unayoiendea sasa hivi..iwe ni katika huduma yako, iwe ni katika familia yako, iwe ni katika shughuli yako unayoifanya sasa, kuna uamuzi uliuchua, au kuna jambo ulilifanya  ambalo hivi karibuni utakwenda kuona matokeo yake..

Hivyo kama ulimwomba Mungu juu ya kitu Fulani, kwa muda mrefu akupatie basi kaa katika matarijio ya kukipata, au kama ulijitaabisha katika kitu ambacho kwasasa faida yake haionekana kaa katika matarajio ya kukipata muda si mrefu..

Sara alikuwa katika matarajio ya kupata mtoto kwa muda mrefu, lakini wakati ulipofika malaika alimjia na kumwambia panapo wakati kama huu mwakani utalea mtoto..VIvyo hivyo na wewe kama upo katika mstari ulionyooka na Mungu wako basi tarajia Mungu kukupa kile ulichokuwa unakitafuta. Kwasababu mimba sikuzote ni matokeo ya ile mbegu iliyoingia ndani yako..Kama ni mbegu njema uliipanda basi utavuna kilicho chema.

Vile vile kama ulikuwa ni mwovu unafanya mambo yasiyompendeza Mungu nawe pia kaa katika matarajio ya kukipata hicho ulichokuwa unakifanya, ikiwa ulikuwa mchawi jiandae kuvuna matunda ya uchawi wako, ikiwa ulikuwa ni tapeli au mla rushwa jiandae kukumbana na ulichokihangaikia, kama ulikuwa ni mrushi vile vile jiandae kukutana na malipo yake hivi karibuni…

Usishangae kukutana na mabaya, kwasababu biblia inasema dhambi nayo huwa inapitia hatua hizo hizo mpaka kufikia mauti.

Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”

Zaburi 8:14 “Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.”

Isaya 59:3 “Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya.

4 Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.”

Hivyo kama unatenda maovu sasa, acha mara moja, Tubu dhambi zako, umegukie muumba wako YESU KRISTO kabla huo wakati wa mabaya haujafika, lakini kama unajijua upo katika njia iliyonyooka na umekuwa katika dua ya kumwomba Mungu kwa ajili ya kitu Fulani chema..Basi kuwa katika matarajio ya kukipata siku za hivi karibuni.

Ubarikiwe.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?

FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.

USHUHUDA WA RICKY:

MTETEZI WAKO NI NANI?

KUOTA UNAPEWA PESA.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).

Jibu: Tusome,

Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.

Kulingana na huu mstari je ni kweli fedha ni jawabu la kila kitu?.

Jibu ni La! Fedha haitoi jawabu la mambo yote, kama ndio basi fedha ingeweza kununua uzima wa milele, hivyo kusingekuwa na haja ya Bwana Yesu kutoa uhai wake kwaajili ya uzima wa roho zetu.

Lakini biblia inatufundisha kuwa tumekombolewa kwa damu ya Yesu na si kwa fedha.

1 Petro 1:18 “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo”.

Vile vile fedha haiwezi kutibu kifo, wala kununua amani, kwasababu wapo watu wenye pesa nyingi lakini hawana amani n.k.

Lakini kama hivyo ndivyo kwamba fedha si jawabu la mambo yote, kwanini biblia iseme ni jawabu la mambo yote?.

Ili kupata jibu la swali hili ni vizuri tukausoma mstari huo kwa kutafakari kwa kina sehemu za kwanza za mstari huo na zile za mwisho.

Mstari huo unaanza kwa kusema.. “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko” na unaendelea kwa kusema… “Na divai huyafurahisha maisha”…na unamalizika kwa kusema “NA FEDHA HULETA JAWABU LA MAMBO YOTE”.

Sasa swali ni mambo gani hayo ambayo fedha inaleta majibu yake?.

Jibu: Ni mambo hayo yanayotajwa hapo juu, maana yake yahusuyo karamu hizo ziletazo kicheko zenye ulevi…. na si mambo mengine tofauti na hayo.

Na kweli mambo ya kidunia karibia yote jawabu lake ni fedha, maana yake ukiwa na fedha utaweza kuyafanya au kuyapata, na ukizikosa fedha pia unaweza kuyakosa.

Anasa zote za kidunia zinahitaji pesa, na wanaotaka anasa wanazitafuta pesa kwasababu hilo ndio jibu lake.

Lakini wana wa Mungu, hawaishi kwa fedha wala fedha si jawabu la mambo yao yote…bali Damu ya Yesu ndio jawabu la mambo yao yote.

Wana wa Mungu hata pasipo pesa wanaweza kuishi vizuri kabisa, na pia hawana tabia ya kupenda fedha, bali fedha yao ni Damu ya Yesu katika Roho Mtakatifu.

Je upo ndani ya agano la damu ya Yesu au Mungu wako ni fedha?.

Waebrania 13:5 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)

KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)

MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.

KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.

Rudi nyumbani

Print this post

Yesu alifundisha kwa mifano. Je hiyo mifano maana yake nini?

Biblia inasema Bwana Yesu alifundisha kwa mifano. Naomba kuelewa hiyo mifano ni nini? Na dhumuni lake lilikuwa ni lipi?

Mifano, ni hadithi zinazoambatanishwa na habari husika, ili kueleza uhalisia zaidi wa ukweli huo.

Bwana Yesu alitumia mfumo huu, wa hadithi za kidunia ili kueleza uhalisia wa mambo ya ufalme wa mbinguni. Na takribani mafundisho yake yote yalitegemea mifano.

Mathayo 13:34 “Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;

35 ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali”.

Mpaka ikafikia wakati Fulani wanafunzi wake wanamuuliza kwanini unapenda kutumia mifano kufundisha watu?(Mathayo 13:10)

Kwamfano alipotaka kueleza habari ya madhara ya kutokusamehe, alitumia hadithi ya yule mtu aliyedaiwa talanta elfu kumi, ambaye alikuwa karibuni na kuuzwa kwa kukosa cha kulipa, lakini bwana wake akamuhurumia akamsemehe deni lote, lakini yeye alipokutana na mtumwa wake aliyemdai dinari 100 tu hakutaka kumsamehe, matokeo yake bwana wake aliposikia tabia yake hiyo akamkamata na kumtupa gerezani, mpaka na yeye atakapolipa yote(Mathayo 18:21-35).

Hivyo mtu unaposikia hadithi hiyo, inakupelekea kuelewa zaidi jinsi Mungu naye anavyojisikia pale tunaposhindwa kuwasamehe watu makosa yao .

Katika Biblia ni mifano zaidi ya 30 Bwana Yesu aliisema, lakini ni mingi zaidi ya hiyo aliifundisha, ambayo haijaandikwa kwenye biblia, (Yohana 21:25)

Madhumuni na mifano hiyo yalikuwa ni mawili:

  1. 1) Kufafanua zaidi ukweli wa habari husika
  2. 2) Kuficha ukweli wa habari husika

Bwana Yesu alipoizungumza kwa waliokuwa na kiu ya kusikia, aliieleza kwa uwazi wote bila maficho yoyote.

Lakini alipokutana na kundi la watu ambao hawakuwa na nia ya kujifunza, watu wenye wivu,  mafarisayo na waandishi ambao walimkufuru Roho Mtakatifu pamoja na maherodi, alikuwa anatumia mifano ya mafumbo, ili wasielewe chochote. Na alipokuwa peke yake alihakikisha anawafunulia mafumbo hayo wale ambao walikuwa na kiu ya kuujua ukweli.

Mathayo 13:13 “Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.

14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.

15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya”.

Hivyo mfumo huu hata sasa Bwana anautumia rohoni.. ukiwa kweli na nia ya kumjua Mungu, atakufundisha sana, na kutumia hata mifano halisi ya kimaisha ili mradi tu ahakikishe unayaelewa mapenzi yake, vema na kwa ufasaha wote. Lakini ikiwa mwovu, na unajifanya unamjua Mungu, ukweli ni kwamba hutamwelewa, atakuja kwako kwa mafumbo mengi tu.. Utakuwa kila siku ni mtu wa kutomwelewa Mungu, na kumtumikia kidini tu.

Bwana Yesu atusaidie tuwe na kiu ya kweli kwake. Kwasababu hii biblia haijakusudiwa kila mtu aielewe bali wale wenye nia tu ya dhati kwa Bwana..walio maskini wa roho.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KWA WALE WALIO NJE “YOTE” HUFANYWA KWA MIFANO

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.

MAKABURI YAKAFUNUKA; IKAINUKA MIILI MINGI YA WATAKATIFU WALIOLALA;

Ni kwanini Yesu alisema “Na wakisikia wasikie, wasielewe Wasije wakaongoka?”

Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.

KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?

Rudi nyumbani

Print this post