Title wakatoliki wana

Wakatoliki wanaabudu sanamu?

Kulingana na Biblia, Wakatoliki ni kweli wanaabudu sanamu…

Biblia inasema, katika

Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”,

Sasa tatizo sio kutengeneza sanamu, wala kuning’iniza picha manyumbani mwetu za watakatifu au za wanafamilia wetu, bali tatizo ni “kuzisujudia” na “kuzitumikia”…Hivyo vitu viwili ndio tatizo.

Sasa Kanisa katoliki linafundisha watu kusujudia sanamu pamoja na kutumikia sanamu. Na kumbuka sanamu haimaanishi tu lisanamu likubwa kama lile la Nebkadneza, bali sanamu  hata ndogo tu kama punje ya harage pia ni sanamu…mbele za Mungu zote ni sawa!

Sasa Waumini wa kanisa katoliki wanafundishwa kuzipa hizi sanamu heshima fulani kana kwamba zimebeba kitu cha kiungu ndani yake..Kitendo tu cha kuzipa heshima fulani, kama kwamba ni kitu cha Kiungu hiyo tayari ni Ibada ndani ya moyo wa Mtu, na ndio kitu kinachomchukiza Mungu..

Kadhalika, kutumikia maana yake ni kukiwekea hicho kitu utaratibu fulani ambao ni kama sheria fulani inayokufanya wewe kuwa mtumwa wa hicho kitu…Kwamfano kusali rozari kila siku asubuhi, mchana na jioni na kuogopa hata kuikanyaga kwa bahati mbaya  hiyo ni kuitumikia rozari….ambapo kwako inakufanya kuwa mtumwa..Jambo hilo ni machukizo mbele za Mungu.

Sasa si wakatoliki wote wanajua hilo, na si wakatoliki wote wana nia mbaya katika kwenda kuabudu katika kanisa hilo, wengi wana nia ya kweli ya kwenda kumtafuta Mungu, isipokuwa Mfumo wa Udini umewafunga hata hawawezi kuiona kweli tena!..Lakini wale Bwana aliowachagua wakati ukifika wanapokutana na Ukweli wanafunguka macho na kurekebisha njia zao, kwa kutoka katika mifumo ya kanisa hilo na kugeukia kumwabudu Mungu katika roho na Kweli.


Mada Nyinginezo:

JE BIKIRA MARIAMU ALIKUFA?

JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?

JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?

JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

WANA WA MAJOKA.

Kwanini Bwana aliwaaita waandishi na mafarisayo wana wa majoka?, Na hao wana wa majoka kwasasa wanawawakilisha watu wa namna gani?.

Najua ulishawahi kuyasoma haya maandiko, lakini naomba usome tena kwa utulivu lipo jambo nataka ulione la tofauti naamini litakufungua macho yako na kukuponya katika uelekeo ambao pengine ulidhani upo sawa kumbe haupo sawa.

Mathayo 23:29 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,

30 na kusema, KAMA SISI TUNGALIKUWAKO ZAMANI ZA “BABA ZETU”, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.

31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.

32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.

33 ENYI NYOKA, WANA WA MAJOKA, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.

36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”

Amen.

Jaribu kufikiria hawa watu kauli waliyokuwa wanaitumia siku zote za maisha yao… KAMA SISI TUNGALIKUWAKO ZAMANI ZA “BABA ZETU”, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii…

Hiyo ni uthibitisho tosha, kutuonyesha kuwa wao walikuwa sio wana wa manabii, sio uzao wa watu waliomcha Bwana, walikuwa na baba zao tofauti na wale tunaowasoma habari zao kwenye biblia, walikuwa tofauti na wakina Musa, tofauti na wakina Samweli, tofauti na wakina Eliya, tofauti na akina Daudi, tofuati na makuhani wote wa kweli wa Mungu..Tunasoma wanaafikiana kabisa  na kuthibitisha kuwa kweli BABA zao walikuwa na huduma moja tu duniani nayo ni hiyo, kama sio kuwapiga watu wa Mungu, na kuwafukuza miji kwa miji basi waliwasulibisha na kuwaua hadharani.

Maneno hayo yakiwa yanatoka katika vinywa vyao kwa ujasiri, tunamwona Bwana Yesu akiwashangaa na kuwauliza,..mwajishuhudia kabisa mkisema kama “sisi tungalikuwako zamani za BABA ZETU!!!….ati nini? …BABA ZETU!!

kumbe wale ni BABA zenu??, Baba zenu nyie sio mitume na manabii waliouliwa na wale wauaji, lakini wale ndio mnaowaona kuwa ni baba zenu..Mnajishughudia kabisa kuwa nyie ni watoto wa wauaji,!! Mnajishuhudia kabisa nyie ni wana wa majoka, mnasubiri kukua mkomae kama baba zenu ili nanyi mfanye kazi zile zile walizokuwa wanazitenda baba zenu za kuwapiga manabii wa Mungu na kuwaua na kuwasulibisha… Kwasababu WANAJISHUHUDIA WENYEWE.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba hata leo hii, katika kanisa la Mungu jambo hili hili linajirudia..Leo hii ndugu nataka nikuambie kabla haujapinga neno lolote hapa, au kutoa maneno ya kejeli naomba nikuulize swali BABA ZAKO NI WAKINA NANI?..Unajishuhudia kwa mababa wapi?..Usije ukajikuta na wewe upo miongoni wa watoto wa MAJOKA yaliyowaua mababa wa Kweli wa Mungu, ukijidanganya kuwa wewe nawe ni miongoni mwa wana wa mitume…Jitathimini.

Kabla hujafikiria kusema mimi ni mshirika wa dini Fulani, au dhehebu Fulani embu fanya utafiti kwanza, hao mababa zako au waanzilishi wao walikuwa na historia gani huko nyuma? Chimbuko lao ni lipi?.

Cha kuhuzunisha sana KANISA la kirumi ( KATOLIKI) ambalo leo hii ndio kanisa lenye washirika wengi ulimwenguni, na washirika wake na wengi wa washirika wake wanajivunia kuitwa Wakatoliki, lakini tukilitazama chimbuko lake ni la kushtusha sana, nasema tena sio kidogo, bali ni sanaa!!..Hivi karibuni viongozi wa kanisa hilo likiongozwa na PAPA kiongozi wao mkuu wanaomba msamaha kwa mauaji ya wakristo na watakatifu wengi wa Mungu zaidi ya MILIONI 68 yaliyofanywa tangu kipindi cha kanisa la kwanza hadi wakati wa matengenezo. ..

Wanakiri kuwa ni kweli “BABA” zao walifanya hivyo, na ndio maana wanawaombea msamaha, ..Ingekuwa sio baba zao wasingejisumbua kuwaombea msamaha, lakini sasa wanakiri kuwa Baba zao, ndio waliohusika na mauaji yale mabaya na ya kikatili hawakuwa mitume watakatifu wa Mungu ambao hatujawahi kuona hata siku moja katika maandiko mtume mmoja kamnyooshea mtume mwanzake kidole, sembuse kuua na kusulibisha watakatifu zaidi ya milioni 68, kama sio MAJOKA haya ni NINI tena??. Tuwe wawazi.

Na kibaya zaidi ndugu zetu wengine wasiojua historia ya kanisa vizuri, wanaungana nao na kujiita wao ni watoto wa Kanisa hilo la damu. Hawajui kuwa na wao mbele za Mungu wanaingizwa katika hatia moja na baba zao wanakuwa wana wa majoka.. Ndugu usidhani haya mambo hayafanyiki hata sasa, mimi nakueleza kitu nilichokishuhudia na kukionja mwenyewe, siongelei kidini au kishabiki, au kwa chuki, nami pia nilikuwa huko kwa neema za Bwana nikatoka..Kwa ujasiri wote nataka nikuambie Hasira ya Mungu ipo juu ya kanisa hili la uongo KATOLIKI. Ndugu tenga muda usome historia ya kanisa, usikubali tu! Kurithishwa kitu pasipo kujua asili yake..

Na ndio maana Bwana Yesu bila unafiki aliwaambia..

32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.

33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.

36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”

Usipotaka kutoka huko, katika kanisa la damu, ujue hukumu ipo juu yako, na wewe pia utakuwa umeshiriki katika kuwaangamiza watakatifu wa Mungu bila hata ya wewe kujua, wakati huo kama sio sasa, utadhani unamtolea Mungu Ibada kwa watu wa Mungu kufa, kumbe umeshakomaa katika viwango vya juu vya baba zako kwa uuaji. Usidhani utagundua, hutagundua hilo mpaka siku ile ya hukumu ndio utajua ni jinsi gani umeshiriki katika damu za watakatifu wengi.

Bwana Yesu aliwaonya mitume wake mapema akawaambia..

Yohana16 :1 ‘Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.

2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. 

Lakini hilo halitadumu siku zote, wakati wao umeshawekwa tayari, wote watakuja kuangamizwa katika ile siku ya Bwana, kwa yale mapigo makuu ya mwisho yatakayoachiliwa juu ya dunia nzima.(Ufunuo 16) watapewa kwanza wainywe damu ya watakatifu waliyoimwaga tangu Habili mpaka mtakatifu wa mwisho atakayeuliwa na wao, na baadaye watauliwa na kunyokea katika lile ziwa la moto.

Na ndio maana injili tuliyonayo sasa, si tu ya kuwaambia watu watoke dhambini, bali pia ni ya kuwahubiriwa watu kutoka katika DINI ZA UONGO. Watu wasije wakafa kwa kukosa kuzijua hila za shetani.

Mwisho kabisa, sauti ya Mungu kwetu ni hii:

Ufunuo 18: 4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.15 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake’’.

Hivyo kama wewe ni mtu wa Mungu, na sio wana wa majoka yaliyohusika kuua watu wa Mungu wasio na hatia watakatifu zaidi ya milioni 68, na bado wanaendelea sasa kwa siri, na watazidi sana katika kile kipindi cha dhiki kuu,..leo hii unaisikia sauti yake ikisema na wewe na kukumwambia mwanangu TOKA HUKO!!!

Usifanye moyo wako mgumu. Ondoka! Kwa furaha zote, uipishe ghadhabu ya Mungu.

Ukiulizwa wewe ni nani, sema mimi ni Mkristo hiyo inatosha..kwasababu ndio watakatifu wa kwanza, maBABA zetu wa imani mitume na manabii walivyoitwa, na hakukuwahi kuonekana dosari yoyote ya mauaji, au ya fitina ndani yao…Hao ndio mababa wetu. Tuwafuate wao.. BIBLIA TAKATIFU NENO LA MUNGU. Haleluya!!

Lakini Hawa mababa wengine hatujui watokako, asili yao ni upande mwingine wa adui…ni maadui wa msalaba, katika mavazi ya kondoo.

Ubarikiwe.

Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba..

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

UZAO WA NYOKA.

MPINGA-KRISTO

NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU?

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.


Rudi Nyumbani

Print this post

JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?

Historia fupi ya Rozari kama inavyosomwa na kanisa katoliki.(kulingana na wakatoliki inajulikana kama Rozari takatifu)

Rozari asili yake ni neno la kiingereza “rosary” lenye maana ya “bustani ya maua ya waridi”…Maua ya Rose kwa kiingereza ndio yanaitwa “waridi”..Kwahiyo bustani yake ndio inayoitwa rosary.

Katika sehemu za Ulaya kuna utaratibu wa kupelekeana maua hayo ya waridi ni kama ishara ya kuonyeshana upendo (Ingawa upendo halisi hauwakilishwi kwa maua)…

Hivyo yapo maua hayo ya waridi yaliyo ya rangi ya nyekundu na Nyeupe. Hivyo wakatoliki wanaamini kuwa Maria ni mama mtakatifu kwao, hivyo anastahili kupelekewa mfano wa ua hilo la waridi..na Hivyo sala ya rozari ndio kama ishara ya kumpelekea mama huyo ua hilo jeupe la Waridi kama ishara ya upendo wao kwake.

Sasa Historia ya hiyo sala ya rozari takatifu kwa wakatoliki ilianzia wapi?

Ilianzia karne ya 3 ambapo kulikuwa na watu wanaojulikana kama wahermiti kulingana na Wakatoliki. Watu hawa waliamua kuwa wanasoma kitabu cha Zaburi kila siku SURA ZOTE 150. Lakini baadaye wakazipunguza na kukusudia kusoma sura zote 150 kwa muda wa wiki moja.

Kwa kuwa walikuwa ni watu wasio na elimu, walitumia mbegu ndogo za mimea kuwakilisha kila zaburi moja wanayoisoma..Hivyo wakawa na mbegu 150, kwa idadi ya zaburi zote 150, hivyo kila walipokuwa wanamaliza kusoma zaburi moja waliweka mbegu moja katika kapu ili iweze kuwasaidia kujua wapo zaburi ya ngapi..n.k

Baadaye kulingana na kanisa katoliki, wanasema watu hao majirani zao walivutiwa na sala hiyo ya zaburi, na wao pia wakaanza sala kama hiyo lakini wakawa wanasali sala ya “Baba yetu uliye mbinguni” mara 150, badala hiyo ya Zaburi.

Baadaye tena wakabadilika na kuanza kutumia shanga 150 zilizopitishwa kwenye kamba badala ya vimbegu vidogo  vya mimea walivyokuwa wanavitumia hapo kabla.

Ilipofika karne ya 11 kadinali wa kikatoliki Mt. Peter Damiani, aliibadilisha sala hiyo kutoka katika kusali “Baba yetu uliye mbinguni” mara 150…Na kuwa “salamu Maria” mara 150.

Baadaye tena akatokea kiongozi mwingine wa kikatoliki akazigawanya hizo sala katika makundi 15..na kila baada ya salamu Maria 10 aliiweka Baba yetu uliye mbinguni…ikiwa vile vile kamba yenye vishanga 150.

Baada ya kipindi fulani tena wakavipunguza vile vishanga na kubakia vishanga 50 tu. Hivyo ndio mpaka leo wanasali rozari yenye vishanga hivyo 50.

Lakini Je jambo hilo ni  la kimaandiko?

Jibu ni la! Si la kimaandiko kwasababu hakuna sehemu yoyote katika maandiko tumeagizwa tusali sala ya “Salamu Maria”. Kwasababu Maria si mtu anayetuombea..yeye alishakufa, wafu wote hawana habari na mambo ya maisha yetu haya…..Anayetuombea ni mmoja tu biblia imemtaja ambaye ni ROHO MTAKATIFU.

Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa”.

Umeona? ni Roho Mtakatifu na si Bikira Maria. Na Roho Mtakatifu hatumuombi atuombee na kusema “Salamu Roho Mtakatifu tunaomba utuombee”..hapana Roho Mtakatifu anatuombea pale na sisi tunapoomba..aidha kwa kunena kwa lugha au kwa maneno dhahiri..Yeye ni kama Mkalimani wetu mbele za Mungu. Mkalimani hawezi kuzungumza kama wewe huzungumzi.n.k

Hivyo sala yoyote inayohusisha kumwomba Mtakatifu fulani aliyekufa atuombee ni sala ya upotofu..inayowafumba watu macho na kuwafanya wawe wavivu wa kuomba wenyewe na kutamani  kila wakati kuombewa tu! Na mtu anayesali sala hiyo anamwabudu shetani bila yeye kujijua.

Hali kadhalika sala halisi inatoka ndani ya Moyo, na si desturi au utaratibu fulani au fomula fulani ya kufuata. Unapotumia mfumo fulani wa kuhesabu shanga na kutimiza idadi fulani ya maneno..hapo utakuwa husali chochote zaidi ya kutimiza wajibu tu..Na hatuendi kumwomba Mungu ili kutimiza wajibu..Mungu anataka ibada halisi inayotoka ndani ya moyo wa mtu hata kama itamchukua mtu maneno machache lakini maadamu imetoka katika moyo uliomiminika mbele zake..hiyo inathamani kubwa sana mbele za Mungu kuliko maneno elfu yasiyo na maana.

Ukitumia mfumo fulani bila kuomba kwa Roho ni sawa na umemwekea Mungu baba, nyimbo zilizorekodiwa katika kaseti azisikilize afurahi..Umeona? ukifanya hivyo ni kumdharau Mungu..anachotaka kutoka kwetu ni nyimbo zinazotoka ndani ya vinywa vyetu zinazotoka moyoni..na sio nyimbo zilizorekodiwa…Kadhalika na sala anataka zinazotoka mioyoni mwetu na si zinazojirudia rudia kama kaseti.

Hivyo kwa hitimisho..sala ya Rozari  si sala ya kimaandiko..Imebuniwa na Shetani, na lengo lake ni kuwaharibu watu kiroho. Hivyo kama upo huko ndugu..toka haraka sana!..Anza kumwabudu Mungu leo katika Roho na Kweli..Tupa hiyo rozari usiisali tena…umeshaujua ukweli, na pia washirikishe wengine wasiojua ukweli huu..

Hizi ni nyakati za mwisho shetani anatumia kila namna  kuwazuia watu wasiijue kweli. Na anawatumia watumishi wake ambao kwa nje wanaonekana ni watakatifu, wanaonekana ni watumishi wa Mungu kumbe ndani ni Mmbwa mwitu wakali.

Bwana akubariki sana.

Ikiwa bado hujaokoka na unatamani kuokoka basi hujachelewa..kumbuka kuokoka sio dini mpya..bali ni kitendo cha kumpokea Yesu maishani mwako na kufanyika kiumbe kipya..kumkiri kwamba yeye pekee ndiye njia ya kweli na mpatanishiwa wa Mungu na wanadamu. Ukimkiri namna hiyo na kudhamiria kuacha dhambi kwa vitendo na kujikana nafsi yako na kumfuata yeye…ataingia moyoni mwako na kukubadilisha na kukufanya kuwa kiumbe kipya. Hivyo tubu na baada ya kutubu nenda katafute ubatizo sahihi wa kimaandiko wa kuzamishwa katika maji tele (Yohana 3:23) na kwa Jina la Yesu Kristo.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

UPAKO NI NINI?

SAKRAMENTI NI NINI, NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?

LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?

JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?

Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

Rudi Nyumbani:

Print this post

UJAZO WA BIBLIA KATIKA MGAWANYO WAKE.

> Kuna vitabu vingapi katika Agano Jipya na Agano la Kale?,

> Kuna sura/milango mingapi katika kila mgawanyo?

> Na watu gani waliotajwa sana katika biblia zaidi ya wengine wote?

KUJUA HAYO YOTE, TAZAMA MAJEDWALI YAFUATAYO 

(Slide kushoto kusoma zaidi taarifa katika jedwali).

N/AMGAWANYOIDADI YA VITABUIDADI YA SURA (MILANGO)IDADI YA MISTARI
1.AGANO LA KALE3926023,145
2.AGANO JIPYA279297,957
JUMLA661,18931,102
JINANAFASI (KATIKA BIBLIA)IDADI ALIZOTAJWA (Mara ngapi)NAFASI
YOABUJemedari wa Mfalme Daudi12916
ISAKAMwana wa Ibrahimu12915
SAMWELINabii (Mwana wa Elkana)14214
YEREMIANabii (Mwana wa Hilkia)14513
PETROMtume (Mwana wa Yona)19312
YOSHUAJemedari wa Israeli21911
PAULOMtume (Mwenyeji wa Tarso)22810
YUSUFUMwana wa Yakobo2469
SULEMANIMfalme (Mwana wa Daudi)2728
ABRAHAMUBaba wa Imani2947
HARUNIKuhani Mkuu3426
SAULIMfalme (Mwana wa Kishi)3625
YAKOBOIsraeli (Mwana wa Isaka)3634
MUSANabii (Mwana wa Amramu)8033
DAUDIMfalme (Mwana wa Yese)9712
YESU KRISTOMFALME wa Wafalme, Bwana wa mabwana, Mwana wa Mungu, Mwokozi, Simba wa kabila Yuda, Mesia, Mwokozi na Mchungaji Mkuu.1,2811

Kwanini YESU KRISTO ndiye anayeonekana kutajwa sana katika Biblia??.. Ni kwasababu yeye ndiye kitovu cha UZIMA, na Biblia yote inamhusu yeye, na kutuelekeza kwake.

YESU KRISTO, ndiye Njia, KWELI na UZIMA.. Mtu hawezi kumwona MUNGU nje ya YESU KRISTO (Yohana 1:18 na 14:6)

Tafadhali shea na wengine;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

TAKWIMU ZA KIBIBLIA

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Rudi nyumbani

Print this post

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

AGANO LA KALE

Vitabu vya Agano la Kale vimegawanyika katika makundi makuu manne (4)

      1. VITABU VYA SHERIA. (Tazama jedwali chini).

JINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGO/SURAMAJIRA YA UANDISHI
1.MWANZOMUSA50Jangwani
2.KUTOKAMUSA40Jangwani
3.MAMBO YA WALAWIMUSA27Jangwani
4.HESABUMUSA36Jangwani
5.KUMBUKUMBU LA TORATIMUSA34Jangwani

     2. VITABU VYA HISTORIA (Tazama Jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.YOSHUAYoshua24Kaanani
2.WAAMUZINabii Samweli21Israeli
3.RUTHUNabii Samweli4Israeli
4.1SAMWELINabii Samweli31Israeli
5.2SAMWELIEzra (Mwandishi)24Israeli
6.1WAFALMEYeremia (Nabii)22Israeli
7.2WAFALMEYeremia (Nabii)25Israeli
8.1NYAKATIEzra (Mwandishi)29Uajemi
9.2NYAKATIEzra (Mwandishi)36Uajemi
10.EZRAEzra (Mwandishi)10Israeli
11.NEHEMIANehemia13Israeli
12.ESTAMordekari10Shushani Ngomeni(Uajemi)

     3. VITABU VYA MASHAIRI (Tazama Jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.AYUBUMusa42Jangawani
2.ZABURI Daudi, Sulemani, Wana wa Asafu,Ethani, Hemani, Musa, wana wa Kora na wengine wasiotambulika.150Israeli
3.MITHALISulemani31Yerusalemu (Israeli)
4.MHUBIRISulemani12Yerusalemu (Israeli)
5.WIMBO ULIO BORASulemani8Yerusalemu (Israeli)

    4. VITABU VYA MANABII WAKUBWA (Tazama Jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.ISAYAIsaya (Nabii)66Israeli
2.YEREMIAYeremia (Nabii)52Israelil (Yerusalemu)
3.MAOMBOLEZOYeremia (Nabii)5Misri
4.EZEKIELIEzekieli (Nabii)48Babeli
5.DANIELIDanieli (Nabii)12Babeli

     5. VITABU VYA MANABII WADOGO (Tazama jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.HOSEAHosea (Nabii)14israeli
2.YOELIYoeli (Nabii)3israeli
3.AMOSIAmosi (Nabii)9israeli
4.OBADIAObadia (Nabii)1israeli
5.YONA Yona (Nabii)4israeli
6.MIKAMika (Nabii)7israeli
7.NAHUMUNahumu (Nabii)3israeli
8.HABAKUKIHabakuki (Nabii)3israeli
9.SEFANIASefania (Nabii)3israeli
10.HAGAIHagai (Nabii)2israeli
11.ZEKARIAZekaria (Nabii)14israeli
12.MALAKIMalaki (Nabii)4israeli

         AGANO JIPYA

Vitabu vya Agano jipya vimegawanyika katika makundi makuu matano (5)

    1. VITABU VYA INJILI (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.MATHAYOMathayo (Mtume)28Antiokia (Siria)
2.MARKOMarko (Mwanafunzi)16Rumi au Siria
3.LUKA Luka (Mwanafunzi na, Tabibu)24Antiokia (Siria)
4.YOHANAYohana(Mtume, mwana wa Zebedayo)21Efeso (Uturuki)

   2. KITABU CHA HISTORIA (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.Matendo ya MitumeLuka (Mwanafunzi na Tabibu)28Rumi

   3. VITABU VYA NYARAKA ZA PAULO MTUME (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA SURAMAHALI KILIPOANDIKWA
1.WARUMIPaulo (Mtume)16Korintho (Ugiriki)
2.1WAKORINTHOPaulo (Mtume)16Efeso (Uturuki)
3.2WAKORINTHOPaulo (Mtume)13Makedonia (Ugiriki)
4.WAGALATIAPaulo (Mtume)6Efeso (Uturuki)
5.WAEFESOPaulo (Mtume)6Gereza
6.WAFILIPIPaulo (Mtume)4Gereza
7.WAKOLOSAIPaulo (Mtume)4Gereza
8.1WATHESALONIKEPaulo (Mtume)5Korintho (Ugiriki)
9.2WATHESALONIKEPaulo (Mtume)3Korintho (Ugiriki)
10.1TIMOTHEOPaulo (Mtume)6Makedonia (Ugiriki)
11.2TIMOTHEOPaulo (Mtume)4Rumi (Kifungoni)
12.TITOPaulo (Mtume)3Ugiriki
13.FILEMONIPaulo (Mtume)1Rumi (kufungoni)
14.WAEBRANIAinaaminika kuwa ni Paulo (Mtume)13Rumi

   4. VITABU VYA NYARAKA KWA WATU WOTE (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKWA
1.YAKOBOYakobo (Ndugu yake Bwana YESU)5Haijulikani
2.1PETROPetro (Mtume)5Babeli
3.2PETROPetro (Mtume)3Haijulikani
4.1YOHANAYohana (Mtume)5Inaaminika Efeso
5.2YOHANAYohana (Mtume)1Efeso
6.3YOHANAYohana (Mtume)1Haijulikani lakini inasadikika Efeso
7.YUDAYuda (Ndugu yake Bwana YESU)1Haijulikani

   5. KITABU CHA UNABII (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.UFUNUO WA YOHANAYohana (Mtume, mwana wa Zebedayo)22Patmo (kisiwani)

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAJINA YA MANABII WANAWAKE

MANABII WA BIBLIA (Wanaume)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).

MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni sawa kuomba novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia?

Mtakatifu Rita, ambaye kwa kanisa katoliki anajulikana pia kama ‘mwombezi wa mambo yasiyowezekana’, na ‘mfanya miujiza’.

Ni mama aliyezaliwa mwaka 1381, katika mji unaitwa Kashia, taifa la Italy. Aliolewa akiwa na umri mdogo lakini baada ya mume wake na watoto wake wawili  kufa aliamua kujiunga na utawa, ijapokuwa alipitia changamoto, kujiunga na jamii hiyo kwasababu tayari alikuwa ameshaolewa(sio bikira), lakini mwishoni alifanikiwa.

kulingana na kanisa katoliki maombi ya Rita yaliwaletea wengi majibu, lakini pia alitambulika kwa jeraha dogo kwenye kipaji cha uso wake, wakiamini kuwa ni alama ya ukristo, kufuatana na mateso ya Yesu msalabani, mahali alipowekewa taji ya miiba. Alikufa kati ya umri wa miaka  75-76.

Na ilipofika tarehe 24 May 1900, papa Leo XIII, Alimtangaza kuwa mtakatifu. Yaani ukitangazwa kuwa mtakatifu, unakidhi vigezo vya kuwa mwombezi wa walio hai.

Tangu huo wakati wakatoliki wengi dunia wamekuwa wakimfanyia novena, na litania. Na wengi wakishuhudia kuwa matatizo yao sugu, yakitatuliwa, hivyo imemfanya kuwa maarufu sana.

Lakini Je! Jambo hili ni kweli? Ni vema kufahamu kuwa katika maandiko matakatifu (BIBLIA), Hakuna mahali popote, tunafundishwa kuwa watakatifu waliokufa zamani au sasa wanaweza kutuombea. Zaidi sana wanakuwa hawaelewi neno lolote linaloendelea duniani, biblia inasema hivyo katika;

Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Umeona? Kwahiyo desturi hii, ya kupeleka maombi yetu kwa watakatifu watuombee, ni ya kipagani, Ni ibada za sanamu,  ambayo asili yake ilianzia kwenye dini zinazoamini mizimu inaweza kuwasiliana nasi. Kusema hivi haimaanishi tunawapinga wakatoliki, au tunatangaza chuki hapana, bali tunasemezana ukweli ili tupone, kwasababu safari yetu ni moja sote tuurithi uzima wa milele, sisi tunasema ni wakristo.

Haijalishi utakuwa ulifanya novena ya Rita ikakuletea majibu kiasi gani, bado ni ibada ya sanamu, kumbuka pia shetani analeta majibu, si ajabu mambo hayo kutendeka, ili watu wapumbazike katika hayo.

2Wakorintho 11:14  Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Mwombezi wetu ni mmoja tu naye ndiye YESU KRISTO (1Yohana 2:1). Lakini sio pamoja na Petro, au Paulo, au Eliya, au Mariamu, au Yusufu. Hao wote ni watakatifu ambao walihitaji ukombozi tu kama sisi, na wenyewe walituelekeza kumtazama Yesu Kristo, na sio wao.

Mtume Paulo alisema maneno haya;

1Wakorintho 1:13  Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Hivyo hakuna haja ya kupeleka maombi yako kwa mtakatifu yoyote, na vilevile wale walio kule hawawezi kutuombea sisi pia. Halikadhalika wewe huwezi kumwombea mwenye dhambi aliyekufa, kwamba Bwana amtoe matesoni. Imani hiyo haipo pia katika biblia. Soma (Waebrania 9:27). Mafundisho ya watu kupitia toharani hayapo katika biblia.

Tujifunze kusoma biblia tutafunguka kwa mengi, mapokeo ya kidini sio Neno la Mungu. Hao wanaoabudu miti na mawe twaweza kuwacheka, lakini tukawa kama wale tu isipokuwa katika mfumo mwingine, tusipopenda kusoma biblia. Tukikataa kuwa wafuasi tu wa kidini tukapenda Neno la Mungu, Roho Mtakatifu atatusaidia kufunguka kwa mengi.

Hivyo ikiwa wewe ulikuwa ni mmojawapo wa wanaopeleka maombi kwa Rita wa kashia, au  kwa mtakatifu mwingine yoyote acha sasa kufanya hivyo. Tubu dhambi ukabatizwe, upokee Roho Mtatakatifu ambaye atakuongoza na kukutia katika kweli yake yote(Yohana 16:13).

Ikiwa upo tayari leo kuokoka, basi waweza fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Novena ni nini? Na je ipo kibiblia?

Roho Mtakatifu ni nani?.

LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

Kuomba katika roho ni kupi? na je nifanye nini ili niweze kuomba hivyo?

SISI TU MANUKATO YA KRISTO.

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

Rudi nyumbani

Print this post

Novena ni nini? Na je ipo kibiblia?

Jibu: Neno “Novena” limetokana na neno la kilatini “Novem”… lenye maana ya “Tisa”(9). Madhehebu baadhi ikiwemo Katoliki na Orthodox yamelitohoa neno hili na kulitumia katika aina Fulani ya mfululizo wa sala kwa kipindi cha siku 9.

Sala hizo zinahusisha kuomba kwaajili ya  jambo fulani au kushukuru, na zinahusisha ibada za kuomba Rozari kwa wakatoliki (jambo ambalo si sahihi kibiblia). Na kwanini kusali Rozari sio agizo la biblia?, fungua hapa kwa maelezo Zaidi >>>JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?

Sasa msukumo wa kuomba Novena, (yaani siku 9) mfululizo umetokana na matukio maalumu yanayotokea baada ya siku 9, au miezi 9 kumalizika. Kwamfano utaona kabla ya Pentekoste kutimia, walikusanyika Mitume na watu wengine baadhi mahali pamoja kuomba, na wakaomba kwa muda wa siku 9, baada ya Bwana Yesu kupaa na siku ya 10 ikawa ni Pentekoste.

Hivyo ushawishi huu wa kupokea Roho Mtakatifu baada ya maombi ya siku 9, ukaaminika na madhehebu hayo kuwa ni lazima uendelee ili kupokea kitu kingine mfano wa hicho kutoka kwa Mungu, vile vile mwanamke anajifungua mtoto baada ya miezi 9, hili nalo likawafanya viongozi wa madhehebu haya kuamini kuna kitu katika 9, (novena).

Sasa swali ni je! Biblia imetuagiza kutumia mfumo wa Novena, katika maombi ili kupokea jambo maalumu kutoka kwa Mungu? Kwamba tuwe na maombi maalumu ya kurudia rudia kwa muda wa siku 9 ili tupokee jambo kutoka kwa Mungu?.

Jibu ni la!.

Biblia haijaagiza mahali popote tusali “Novena” kwamba tuwe na kipindi Fulani maalumu cha siku 9 mara wa mara ili Mungu aachilie kitu juu yetu. Utaratibu huu umetengenezwa na wanadamu, kufuatia ushawishi wa siku ya Pentekoste. Hivyo kama umetengenezwa na wanadamu, hauwezi kuwa Sharti, au Agizo la lazima kwa wakristo, kwamba usipofanya hivyo ni kosa kibiblia!.

Agizo hili linaweza kuwa la binafsi, kama tu vile mfungo usivyokuwa sharti, ni jinsi mtu atakavyosukumwa na kuongozwa kufunga!.

Lakini mbali na hilo hata kama Novena ingekuwa ni agizo la biblia, bado inavyofanyika na madhehebu baadhi ikiwemo Katoliki, bado haifanyiki sawasawa na maandiko.. Kwasababu katika biblia tunaona kabla ya Pentekoste walikuwa wamekusanyika mahali pamoja wakisali, wakimwomba Mungu na Mariamu mama yake Yesu alikuwemo miongoni mwao, naye pia akimwomba Mungu, na hawakuwa na sanamu ya mtakatifu Fulani aliyetangulia kufa!, bali walikuwa wakimwomba Mungu aliye juu, (Matendo 1:12-14)

Lakini leo hii katika sala hizo za Novena ni kinyume chake!, wanaoombwa ni watakatifu waliokufa ikiwemo Maria mwenyewe, jambo ambalo ni kinyume kabisa na maandiko!, hivyo badala ziwe sala za Baraka, zinageuka na kuwa ibada za sanamu! (Bwana Yesu atusaidie sana!!).

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Novena haipo kibiblia,..kama mtu atajiwekea utaratibu wake binafsi wa kusali Novena, na sala hiyo ikawa ni kulingana Neno la Mungu, isiyohusisha sanamu wala desturi za kipagani basi hafanyi dhambi!, huenda ikawa bora kwake.

Lakini inapogeuka na kuwa sharti, na tena ikahusisha ibada za sanamu basi inakuwa ni machukizo makubwa mbele za Bwana kulingana na maandiko.

Bwana atusaidie!.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

SALA YA BWANA. (Namna ya kuiomba)

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

SALA YA UPONYAJI/MAOMBI YA UPONYAJI.

Kuna tofauti gani kati ya SALA na DUA?

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

Rudi nyumbani

Print this post

NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?

Shalom. Jina la kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Karibu katika mwendelezo wetu unaoangazia matendo ya baadhi ya watu walioishindania imani hadi kufa bila kuiacha..Tulishawaona baadhi nyuma na Leo tutamwangazia mwingine anayeitwa Mtakatifu Denis wa Ufaransa.

Mtu huyu, alitokea karne ya tatu, Ni maarufu sana katika historia ya nchi Ufaransa, na hata katika vitabu vinavyoelezea historia ya mauaji ya wakristo, Huyu alikuwa kama mmishionari aliyezaliwa Italy, na kusafiri yeye pamoja na wenzake wawili nchini Ufaransa kwa lengo la kupeleka habari njema za Yesu Kristo,..Alipofika kule, Mungu alikuwa pamoja naye kwani alikuwa na bidii kubwa sana ya kuwageuza watu kwa Kristo, na hata wale makuhani wa dini za kipagani walipoona wanapotezewa waumini wao wengi, wanageuzwa na kuwa wakristo, wakaamua kuwaaundia visa watu hawa. Kama tu vile wakati mtume Paulo alipofika Efeso na kuwageuza watu wengi, na wale wenyeji wa mji walipoona wanapata hasara ya watu kutonunua bidhaa za miungu yao wakawaletea visa, ili Paulo na wenzake waletewe dhiki. Na ndivyo ilivyotokea kwa hawa.

Na sasa serikali ya Rumi iliposikia habari yao, ikawakamata na kuwafunga, ikumbukwe kuwa Rumi wakati huo ilikuwa katika vita vikali dhidi ya watu wote waliokuwa wanaonekana kueneza imani ya kikristo duniani. Lilikuwa ni taifa la kipagani asilimia 100. Hivyo Waliwafunga wakawaacha magerezani kwa muda mrefu, na mwisho wa siku wakawatoa magerezani na kuwachukua mpaka katika kilele cha mlima mmoja ili kuwaua kwa kuwakata vichwa, waliwakata wote lakini walipofika kwa mtakatifu Denis, na kukiondoa kichwa chake, walishaangaa kuona anakiokota tena kichwa chake, na kuanza kutembea maili kadhaa, akihubiri injili kila alipopita.

Tendo hili liliwaogopesha watu wengi sana waliokuwa wanashuhudia maajabu yale, na mahali alipoacha kuhubiri na kuanguka chini Mahali palepale ndipo ulipogeuzwa mji ule na kuitwa kwa jina lake ambao hadi sasa upo huko ufaransa,. Na juu ya kaburi lake wakatoliki baadaye walijenga kanisa lijulikanalo kama Basilica of Saint-Denis. (lakini kumbuka huyu Mt. Denis mwenyewe hakuwa mkatoliki wala mafundisho yake hayakuwa ya kikatoliki bali ya kanisa la kwanza la mitume wa Yesu Kristo, yaani Neno la Mungu lisiloghoshiwa).

Hadi leo sanamu lake limewekwa huko katika makumbusho za kitaifa huko Paris. Hizi ni historia ambazo zimethibitishwa. Hatuna mengi ya kuzungumza Lakini Tukiwatazama watu kama hawa tunapata ujumbe gani?

Biblia inasema..

Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu”.

Ikiwa tunazungukwa na watu waolikuwa tayari kufungwa, hadi kuuawa kwa kukatwa vichwa kama hawa na bado walikuwa hawana hata mpango wa kumwacha Mungu, hadi Mungu anawapa nafasi ya kuendelea kuhubiri angali vichwa vyao havipo, sisi je tunapaswa tuweje?..Ikiwa hatujafikia hatua ya kumwaga damu kwa ajili ya ushuhuda kwa Kristo, lakini ni rahisi kurudishwa nyuma na mambo madogo, madogo tu yasiyokuwa na maana, tujiulize siku ile tutawezaje kusimama pamoja na watu kama hawa mbele ya Kristo? Tutawezaje kupata thawabu moja na wao watu ambao wamepiga mbio bila kuishiwa pumzi, wameishindania imani ipasavyo, kama biblia inavyotuambia katika sura iliyotangulia waebrania sura ya 11

“36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;

37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;

38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.

39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;

40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.

Umeona mstari wa 40 unavyosema, hawakukamilishwa, hawakuipokea ahadi au thawabu yao, kwa ajili yetu sisi, mpaka sisi nasi tutakapomaliza mbio, ili kwa pamoja tupokee tuzo bora..Lakini kama sisi tutaendelea kuwa vuguvugu, na walegevu, tutaendelea kuuchezea wokovu, tutaendelea kuishi kama vile sio watu waliomaanisha kweli kuenda mbinguni, Siku ile biblia inatuambia tutatupwa katika giza la nje,.

Hakuna tukio lingine lolote tunalolisubiria mbele yetu isipokuwa tukio la unyakuo tu, dalili zote zimeshatimia, siku yoyote parapanda inalia na wafu waliolala katika Kristo, watafufuka, kisha wataungana na watakatifu walioko duniani, na kwa pamoja tutakwenda mbinguni kwenye karamu ya mwana kondoo.

Utajisikiaje siku hiyo kujiona umebaki hapa chini, na kibaya zaidi ukikumbuka umehubiriwa injili mara nyingi lakini ulishupaza shingo yako. Utakuwa katika hali gani..Hao ambao unawafurahisha siku ile wote kwa pamoja mtakuwa katika majonzi na majuto ya milele.

Huu ni wakati wa kumaanisha kumfuata Kristo kwa moyo wote, bila kujali, ndugu watakuonaje, marafiki watakuonaje, kazini watakuonaje, shuleni watakuonaje..ni wakati wa kupiga mbio kwa kutua mizigo yote ya dhambi, kisha kumtazama yeye aliyetuita,..Kumbuka toba ya kweli inatoka moyoni na sio kinywani, unaweza ukaongozwa sala ya toba hata mara 100 kama toba yako haikutoka moyoni ni sawa na kazi bure..yule mwanamke kahaba aliyemfauta Yesu akamlilia, akammwagia machozi yake mengi, miguu pake hakuwa anafanya jambo la kuigiza tu, kama linavyofanywa na wengi leo hii, bali alikuwa anaonyesha ni jinsi gani amemaanisha kutubu dhambi zake, na ukahaba wake, hadi akashindwa kuzungumza mbele zake,.na Yesu kuona vile tu bila hata ya kuisikia sauti yake au maneno yake, alisema amesamehewa dhambi zake..Unaona hakuongozwa sala yoyote pale, lakini alipoona moyo wake umetubu na kugeuka, japokuwa dhambi zake zilikuwa nyingi, alisamehewa zote..

Vivyo hivyo na wewe ukidhamiria kuacha dhambi zako kwa moyo wako wote, na kwa nguvu zako zote, ukageuka na kusema kuanzia leo mimi na ulimwengu basi nimeamua kumfuata Yesu bila kugeuka tena nyuma..Ujue kuwa hapo ndipo Mungu atakapokusamehe dhambi zako, kinachobakia kwako ni kuukamalisha wokovu wako kwa kwenda kubatizwa na kumwishia Kristo maisha yako yote yaliyobakia hapa duniani..

Hivyo kwa kumalizia unapokutana na hili Neno WINGU LA MASHAHIDI, kichwani kwako usiusahau ujumbe huo, kuwa lipo wingu kubwa la mashahidi wa Kristo linalotuzunguka, ndilo linalotuhimiza na sisi tupige mbio kama wao, katika mashindano tuliyowekewa mbele yetu kushinda tulivyokuwa tunapiga hapo mwanzo, na mbio hizo tunapiga kwa kutua kila mizigo ya dhambi inayotusonga kwa kadiri tuwezavyo ili tuwe wepesi Zaidi na zaidi..Ili na sisi tukapokee tuzo iliyobora kama wao, hata zaidi ya wao siku ile.

Ubarikiwe sana.

Mada Nyinginezo:

ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

 

HERI NINYI MLIAO SASA, KWA SABABU MTACHEKA.

TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?

DANIELI: Mlango wa 9

UFUNUO: Mlango wa 11

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE VIBWENGO NI KWELI VIPO?

Je Vibwengo ni kweli vipo au ni hadithi za kutunga?.. Je namna ya kuvidhibiti vibwengo, mapepo na mashetani ni ipi? Na roho hizo za vibwengo zifanyaje kazi?

Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa kuna roho za malaika na roho za mashetani…Malaika walioasi ndio wanaojulikana kama mashetani leo…Na malaika hawa wanafanya kazi katika mamlaka ya giza…Yaani kazi yao ni kwenda kinyume na kila kazi ya Mungu…

Kadhalika malaika hao walioasi (yaani mashetani au kwa jina lingine Mapepo)..wapo wa aina nyingi na wenye tabia tofauti tofauti…Kama vile malaika walivyo wengi  na wenye tabia tofauti tofauti…kadhalika na mapepo nao ni hivyo hivyo…Katika biblia tunasoma kuna malaika wa maji..(Ufu.16:5)..kadhalika kuna malaika wanaohusika na nchi, bahari, pia wapo malaika wa kuleta habari kama Gabrieli, ..wapo malaika wa sifa kama maserafi na makerubi, wapo wa vita kama Mikaeli na wengine wengi.

Na katika upande wa pili wa malaika walioasi ni hivyo hivyo wana vipawa tofauti tofauti..yapo mapepo yanayohusika tu na maji, mengine moto, mengine yanahusika kusababisha majanga kama ajali,.. mengine kuleta magonjwa, mengine kuharibu nchi n.k..Lakini yote lengo lao kuu ni kupambana dhidi ya ufalme wa Nuru..

Sasa Vibwengo ni aina ya mashetani/mapepo yanayoangukia katika moja wapo ya hilo kundi…Vibwengo vina kazi ya kuwasumbua wale watu ambao hawajaokoka au hawajasimama vizuri kiimani..Na kwasababu ni roho za mapepo zile zile ambazo zinatenda kazi katika ufalme wa giza..hivyo lengo lao ni kuleta mauti ndani ya Mtu.

Na mtu anaweza kuishi na jamii hiyo ya mapepo aidha kwa kujua au kwa kutokujua…wakati mwingine mapepo hayo (vibwengo) vinaweza kujidhihirisha dhahiri kwa mtu..na mtu kuvishuhudia kabisa kwa macho…

Mara nyingi vinajidhihirisha kwa umbo la mtu mfupi sana aliyejaa..au aina fulani ya wanyama ambao wanaonekana kama watu..mfano wa maumbo yanayoonekana mara nyingi na vibwengo ni maumbo ya mfano wa nyani..Anaonekana mtu kama nyani lakini si nyani n.k…Na mapepo hayo yasipopatiwa  ufumbuzi mapema yanaweza kusababisha hata kifo cha kiroho na cha kimwili kwa mtu..au yanaweza kusababisha tatizo fulani lenye madhara makubwa…Hivyo si busara kuzipuuzia roho hizo chafu.

Mambo gani yanayokaribisha uwepo wa vibwengo?

Jambo la kwanza ni dhambi ndani ya maisha ya mtu..Mtu yeyote ambaye anaishi katika maisha ya dhambi anafungua mlango mpana sana  wa kusumbuliwa au kuingiliwa na roho zozote za mapepo..Mtu anayetenda dhambi ni kama mtu aliyewasha WIFI data kwenye simu yake ya mkononi.. kiasi kwamba simu yoyote iliyokaribu na yake inaweza kukamata mawimbi yatokayo katika hiyo simu yake…Kadhalika mapepo ni hivyo hivyo, mtu anayefanya dhambi ni kama amewasha WIFI katika ulimwengu wa roho,..kwamba hata mapepo yaliyokuwa yanatembea tembea huko na huko ni rahisi kupata habari za huyo mtu.. na kumwingia au kumletea madhara fulani.

Dhambi zifuatazo ndizo zinazoongoza kukaribisha uwepo wa vibwengo kwa mtu..na si tu vibwengo bali hata jamii nyingine zote za mapepo.

1) IBADA ZA SANAMU : Hii inahusisha aina zote za aubuduji sanamu, aidha za watu au za wanyama…unapoisujudia sanamu ya aina yoyote ile ni mlango mpana sana wa kuingiliwa na mapepo..au kuishi na vibwengo pamoja nawe…

2) UASHERATI : Dhambi hii inashika nafasi ya pili katika kukaribisha uwepo wa mapepo ndani ya mtu na hata kuvutia uwepo wa vibwengo..Asilimia kubwa ya watu wanaoona roho hizo za vibwengo lazima kwa namna moja au nyingine ni waasherati. wa kimwili.

3) USHIRIKINA/UCHAWI : Ushirikina ni hali ya kujihusisha husisha na masuala ya nguvu za giza,… kama kwenda kwa waganga au kwa watabiri wa nyota, au utambuzi…Mtu anayehudhuria kwa waganga huyo ni mshirikina hata kama sio mchawi kabisa…lakini kitendo tu cha kwenda kwa waganga kutafuta suluhisho fulani..huo tayari ni ushirikina..na ni mlango mpana sana unaoshika namba tatu kukusogeza karibu na uwepo wa roho za mapepo hususani vibwengo.

4) KUJIPAMBA:

Ikiwemo uvaaji wa wigi, kujitoboa mwilini na kujiweka vito kama hereni, mabangili, mikufu…pia upakaji wa wanja, upuliziaji wa marashi makali yasiyojulikana hata yametengenezewa wapi,..uchoraji wa hina na uchoraji tattoo..Mambo hayo  yanahusika sana katika kuvuta uwepo wa roho za vibwengo na jamii nyingine za mapepo…Ndio maana hata vibwengo vyenyewe vinakuwa kama vimepaka chokaa usoni, au vinatoa harufu ya marashi fulani yasiyojulikana..hiyo yote ni kuonesha vimekutana na mahali ambapo panastahili wao kuwepo..

5) UVAAJI MBAYA:

Mavazi yote yasiyopasa…kama suruali kwa wanawake, magauni kwa wanaume, mavazi ya nusu uchi kama vimini, vitop, nguo za kubana n.k…ni WIFI kwa mapepo….Hata roho hizo za vibwengo viwatokeapo watu zinakuwa kama zimevaa mavazi yasiyoeleweka, kiasi kwamba huwezi kukitambua kama ni jinsia ya kiume au ya kike…Sasa vinakuwa vinatafuta mahali panapowastahili…kwa watu wa jamii zao.

6) ULEVI, UVUTAJI SIGARA na ANASA: Disko ni makao ya mapepo, mtu anayeingia disko tayari anatoka na pepo pasipo hata yeye kujijua…Mapepo ndio makao yao huko, sehemu ambazo watu wapo akili nusu kutokana na ulevi…sehemu ambazo watu wanacheza cheza madansi na kucheka cheka na kuwa na mizaha…Ndio maana hata vibwengo vyenyewe viwatokeapo watu ni lazima viwe nusu-nusu kama vimelewa hivi…vinakuwa nusu vinaakili timamu nusu vitahira…vinachekacheka, mara vinacheza cheza, vinakuwa na mizaha mizaha…yote hiyo ni kwasababu ndiyo asili yao..Hivyo vinatafuta watu wenye asili kama yakwao vikae nao..na hao wapo bar, disko au kwenye vikundi vya kamari.

7) UTAZAMAJI WA PORNOGRAPHY: Pornograph ni picha za ngono..ambazo siku hizi zinatazamwa hata kupitia simu za mkononi…Ufahamu uliojaa zinaa ni lango kubwa la roho hizo…

Namna ya kuvidhibiti vibwengo na roho nyingine zozote za mapepo.

Suluhisho pekee la kuepukana na roho hizo za vibwengo ni kuokoka!…Kuokoka maana yake ni kutubu kwa kudhamiria na kumaanisha kabisa kuacha dhambi…unaacha dhambi zote ulizokuwa unazifanya hizo zilizoorodheshwa hapo juu na nyingine zote ambazo hazijaorodheshwa…Unatubu na kumwambia Bwana Yesu unahitaji wokovu na unamhtaji yeye..si tu kwaajili ya kuepukana na vibwengo, bali kwasababu unahitaji kufanyika kuwa kiumbe kipya na kuwa mkamilifu kama Mungu alivyo.

Ukisha tubu hatua inayofuata ni kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kama ulikuwa hujabatizwa,.. na baada ya hapo Roho Mtakatifu aliyeingia ndani yako atafanya mengine yote yaliyosalia.

Ukishaokoka namna hiyo! na kudhamiria kuacha dhambi…basi wewe mlango wa mapepo hautakuwepo ndani yako…Haiwezekani funza kuwepo ndani yako au kwenye mazingira yanayokuzunguka kama umefanya usafi kweli kweli…Dawa ya kuondoa funza ndani kwako ni kuwa msafi sio kuwaambia funza ondokeni kwangu…kadhalika dawa ya kuondoa mapepo na vibwengo karibu na wewe ni kuwa msafi.. (yaani kujiweka katika hali ya utakatifu), ambayo hiyo inakuja kwa kutubu dhambi na kuziacha..(yaani kuokoka) na sio kwenda kutafuta maombezi huku na huko…

Ikiwa umeshawahi kusumbuliwa na roho hizo za vibwengo..basi hiyo ndio dawa pekee tuliyopewa katika biblia takatifu.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali share na wengine


Mada Nyinginezo:

Wakatoliki wanaabudu sanamu?

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?

PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.

Rudi Nyumbani:

Print this post