Title Devis

AGANO LA MOYO LENYE NGUVU

Amri za kwanza Mungu aliziandika juu ya mawe aliyoyachonga yeye mwenyewe, lakini mawe yale ambayo juu yake amri 10 yalivunjwa vunjwa na Musa wakati ule ule aliposhuka kutoka mlimani…

Kutoka 31: 18 “Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu”

Baadaye Mungu akamwambia Musa achonge, mbao nyingine mbili za mawe mfano wa zile za kwanza zilizochongwa na Mungu mwenyewe..Na Musa alipochonga aliwapa wana wa Israeli…

Kutoka 34:1 “Kisha Bwana akamwambia Musa, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; nami nitaandika juu ya mbao hizo maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, hizo ulizozivunja”.

Mbao hizi za pili nazo hazikudumu muda mrefu, kwamaana alipokuja Mfalme Nebukadreza alivunja sanduku na kuzipoteza kabisa,.na kukawa hakuna tena sanduku la ushuhuda ambalo ndani yake mna mbao hizo za mawe zilizobeba Amri za Mungu.

Lakini baada ya miaka Mingi kupita Bwana Mungu akarudia tena kuziandika amri hizo kwa mara nyingine ya mwisho, lakini safari hii si katika mwamba aliouchonga yeye kwa vidole vyake, wala si katika mwamba uliochongwa na Musa, BALI KATIKA MOYO WA MTU.

Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; NAMI NITAKUWA MUNGU WAO, NAO WATAKUWA WATU WANGU. 

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.

Umeona? Kumbe agano jipya linahusu Moyo!.. Maana yake hatuhitaji tena kwenda Yerusalemu kuzisikia amri, wala sharia wala maagizo ya Mungu, bali tunapomwamini Yesu zile sharia zinaandikwa ndani yetu na kidole cha Mungu mwenyewe.

Na matokeo ya sharia, na amri za Mungu kuandikwa ndani ya mioyo yetu, maana yake muda wote zitakuwa zinabubujika na hivyo hakuna haja ya mtu kukufundisha kuzishika amri, zenyewe tu zitakuwa zinabubujika ndani yako.. kama maandiko yanavyosema hapo katika mstari wa 34…. “Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana”.

Hiyo ndio sababu kwanini watu waliompokea Yesu kikweli kweli na kujazwa na Roho wake Mtakatifu, haihitaji kuwaambia wala kuwakazania kuwa ulevi ni dhambi, au uvaaji mbaya ni dhambi.. Tayari sheria ipo ndani yao, hata pasipo kuambiwa na mchungaji,… ndani ya mioyo tayari kuna mahubiri yaliyoandikwa na kidole cha Mungu mwenyewe yanayowaambia kuwa si sawa kufanya baadhi ya mambo. Hayo mahubiri haihitaji wasafiri mbali kwenda kuyatafuta, tayari yanakuwa yameandikwa ndani yao, haihitaji kuwakumbusha kusali, tayari hayo mahubiri yapo ndani yao, haihitaji kuwakumbusha kwenda ibadani, tayari hayo maagizo Bwana kayaandika ndani yao, hivyo daima yanabubujika.

Kumbukumbu 30:11 “Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali.

 12 Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya? 

13 Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya? 

14 Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na MOYO WAKO, upate kulifanya”

Lakini maandiko hayo hayawezi kuandikwa ndani ya moyo wa mtu, kama mtu huyo hajafungua moyo wake kwa kumwamini Yesu na kumkiri kwa kinywa, vile vile kwa kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, pamoja na kubatizwa, kwa maana maandiko yanasema hivyo..

Warumi 10:6  “Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini),

7  au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.)

8  Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.

9  Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

10  Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”.

Je sheria za Mungu zimeandikwa ndani yako??

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

JE! UNAMPENDA BWANA?

Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?

Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

Mti wa Mshita ni mti wa namna gani?

Rudi nyumbani

Print this post

Mawaa ni nini? Kama tunavyosoma katika biblia?

Mawaa ni nini? Mawaa ni dosari au kasoro iliyo katika kitu, ambayo inapelekea kukifanya kitu hicho kisifae tena, au kikose vigezo.

Kwamfano mtu ambaye ana sifa ya kuwa na uso mzuri halafu, kukatokea jipu shavuni. hapo ni sawa na kusema ana-mawaa. Jipu lile limeuharibu uzuri wake.

Au ukinunua bati la kuwekeza kwenye nyumba yako, halafu ukaona tobo katikati ya bati hilo, tayari lina mawaa, halifai kwa ujenzi. Au shati jeupe halafu likawa na doa dogo jeusi, huo ni mfano wa mawaa, halifai kwa kuvalika.

Vilevile rohoni na sisi pia hatupaswi kuonekana na mawaa ya aina yoyote,  Kwamfano katika vifungu hivi; Mungu anatarajia kanisa lake alilolikomboa kutoka katika dhambi lisionekane na mawaa (dosari yoyote) ndani yake

Wakolosai 1:21  “Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22  katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama”

Hivyo wewe kama mkristo uliyeokoka, ni lazima ujue kuwa una wajibu wa kuishi maisha ya utakatifu na ukamilifu, usiseme nimeokolewa kwa neema Yesu alishayamaliza yote, Hivyo unaenda kama utakakavyo, anaitenda kazi ya Mungu huku unaishi na mke/mume ambaye si wako. Wewe una mawaa, na hivyo mbingu huwezi kuiona.

Au unatoa zaka, unaimba kwaya, ni kiongozi wa vijana, na huku unatazama picha za ngono mtandaoni, hapo una-mawaa, Unafunga na kusali, unadumu hekaluni usiku na mchana na huku unakula rushwa kazini kwako. Hapo ndugu una-mawaa.

Hivyo hatuna budi kuwa kanisa la Kristo kwelikweli Bwana analolitazamia lisilo na mawaa wala lawama, wala kunyanzi. Ndivyo tutakavyopokewa kuingia katika uzima wa milele.

Neno hilo utalipata katika vifungu hivi

1Timotheo 6:13  “Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14  kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.

Yohana 1:27  “Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa”.

Soma pia

Waebrania 9:14, 2Petro 2:13

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka, kama la! Ni nini unachosubiria mpaka sasa, una habari kuwa  parapanda inakaribia kulia, Yesu anarudi? Dalili zote zimeshatimia? Fikiri akikukuta katika hali hiyo utamweleza nini? Angali ukweli umeshaujua? Embu tubu leo dhambi zako, mgeukie Kristo, azioshe, akupe uzima wa milele bure.

Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo akupe uzima wa milele bure, basi fungua hapa ili uweze kupata mwongozo wa sala hiyo. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).

TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

Mtakatifu ni Nani?

ISHARA YA KANISA LA LAODIKIA

USIPOWATAMBUA YANE NA YAMBRE, KATIKA KANISA LA KRISTO, UJUE UMEPOTEA.

Rudi nyumbani

Print this post

JE YESU ALINENA KWA LUGHA?

Katika maandiko hakuna vifungu vya Moja Kwa Moja vinavyorekodi tukio la Bwana Yesu kunena Kwa lugha.

Lakini Kwa ufahamu wa Rohoni tuliopewa twajua kuwa ni wazi Yesu alinena Kwa lugha. Kutokurekodiwa Kwa tukio hilo hakumaanishi kuwa hakuwahi kunena Kwa lugha, kwasababu maandiko yanasema yapo mambo mengi aliyoyafanya Yesu kama yangeandikwa hata vitabu vyote duniani visingeweza kutosha, Kwa wingi wa habari zake.(Yohana 21:25)

Hivyo si Kila tukio la Bwana Yesu limeandikwa  kwenye biblia.

Halikadhalika Ifahamike kuwa taaarifa za kunena Kwa lugha aliyezieleza kwa mara ya kwanza Kwa mitume ni Bwana Yesu.(Hawakufunuliwa baadaye)   Hivyo hawezi kuwaambia watu jambo ambalo yeye mwenyewe halipo ndani yake, au hajawahi kulifanya.

Marko 16:17-18

[17]Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

[18]watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Vilevile Yesu ndiye mwanadamu pekee aliyetiwa mafuta mengi na Roho kuliko mtu yeyote aliyewahi kutokea duniani, (Waebrania 1:9). Zile karama zote za Roho zilikuwepo ndani yake, alikuwa ni nabii, mwalimu, mwinjilisti, mchungaji, mtume, n.k. na karama za uponyaji, miujiza, upambanuzi alikuwa nazo, hivyo hatuwezi kushangaa pia na hii kunena Kwa lugha kuwemo ndani yake.

Kwa kuhitimisha ni wazi kuwa Bwana Yesu alinena Kwa lugha. Hivyo akampendeza kukimwaga  kipawa hicho na kwetu pia.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?

WANAWAKE WAOMBOLEZAJI

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

IJUE FAIDA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA!

YEYE ATAWABATIZA KWA ROHO MTAKATIFU NA KWA MOTO.

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.

Rudi nyumbani

Print this post

MAPAMBO YA WANAWAKE WALIOUKIRI UCHAJI WA MUNGU.

Masomo maalumu kwa wanawake.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo taa na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).

Je wewe ni mwanamke? Na unapenda upate kibali mbele za watu?..au je wewe ni binti na unatamani upate ndoa, tena iliyo bora na ya Baraka?, au je wewe ni mwanamke uliyeolewa na unatamani ndoa yako Bwana aibariki na pia upate kibali na heshima Zaidi katika ndoa yako?. Kama ndio basi hakikisha unazingatia mapambo!!..

Katika biblia kuna wanawake waliofanya utafiti wa mapambo yaliyo bora na mazuri na yenye mvuto mkubwa, ili kwamba wawe na mvuto wa heshima mbele za watu, wengine ili wapate ndoa nzuri na kibali kwa wenzi wao..na walipoyatumia hayo mapambo wakafanyika kuwa wanawake bora kuliko wote, na wenye kukubalika kuliko wote.

Wanawake hawa hawakutumia mapambo ya kiulimwengu kama kupaka wanja machoni au kupaka rangi mdomoni ili waolewe au waheshimiwe na waume zao, vile vile hawakuvaa nusu uchi ili wavutie mbele ya wanaowatafuta kuoa, wala hawakusuka nywele ili waonekane warembo, wala hawakupaka rangi katika kucha zao, ili wavutie mbele za watu na kupata ndoa, lakini walitumia mapambo ya aina nyingine na hayo hakawapa ndoa wanazozitafuta, yakawapa heshima wanayoitafuta, yakawapa kibali wanachokitaka n.k.

Na mapambo hayo ni yapi…..?

1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, ROHO YA UPOLE NA UTULIVU, ILIYO YA THAMANI KUU MBELE ZA MUNGU.

5 MAANA HIVYO NDIVYO WALIVYOJIPAMBA WANAWAKE WATAKATIFU WA ZAMANI, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote”.

Nataka tuuangalie huo mstari wa 5 unaosema “MAANA HIVYO NDIVYO WALIVYOJIPAMBA WANAWAKE WATAKATIFU WA ZAMANI”..

Kwahiyo kumbe zamani kulikuwa na wanawake “watakatifu” na “wasio watakatifu”. Na kila kundi lilikuwa na aina yake ya mapambo ili lipate kibali na kuvutia.

Na hapa biblia inatufundisha wanawake wa zamani waliokuwa watakatifu ijapokuwa katika masomo yao kulikuwa na vipodozi vingi, kulikuwa na rangi nyingi za kucha, na za uso na za mdomoni, lakini wao kwa ufunuo waliokuwa nao hawakuchagua mojawapo wa  hayo mapambo, badala yake waliona yana kasoro, hivyo wakachagua mapambo ya ndani ambayo ni UPOLE, HESHIMA, UTII NA UTULIVU.

Wakaona hayo ndio yatakayowafanya waolewe, ndio yatakayowafanya wapendwe na waume zao, ndio yatakayowafanya wapate kibali katika ndoa zao na jamii zao, ndiyo yatakayowafanya waonekane wa thamani, na si kupaka wanja, au kupaka rangi mdomoni, au kujichubua, au kuvaa nusu tupu.

Ndio maana sasa utaona biblia inasema kama vile Sara alivyokuwa mtii kwa Ibrahimu mumewe hata kufikia hatua ya kumwita Ibrahimu “bwana”, Roho hiyo ya unyenyekevu na utii, na utulivu, ndio iliyomfanya Sara awe “mama wa mataifa” na si “wigi kichwani” wala rangi mdomoni, wala hereni sikioni. Kulikuwa na wanawake wengi katika ile nchi, ambao walikuwa wanajiremba na pengine hata kukaribia kufanana na malaika, lakini Ibrahimu hakuwachagua hata mmoja wao!.

Ibrahimu alimchagua Sara kwasababu alikuwa ni mtii, na mtulivu..(alikuwa na mapambo ya ndani)

“5 MAANA HIVYO NDIVYO WALIVYOJIPAMBA WANAWAKE WATAKATIFU WA ZAMANI, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana…”

Vile vile roho ya upole na ya kujisitiri iliyokuwa juu ya Rebeka, ndio iliyomfanya apate kibali kwa Isaka, kiasi kwamba alipofikishwa kwa Isaka, alifunika kichwa chake kwa shela (Mwanzo 24:62-67), ndio iliyomfanya awe mama wa Taifa kuu la Israeli (Yakobo), na si mavazi ya vimini, au ya mgongo wazi,…Na vivyo hivyo wanawake wengine wote watakatifu walitumia mapambo hayo ili kujipatia kibali.

Lakini wale wengine wa kidunia, walitumia mapambo ya nje, yaani.. vipodozi vyote walivyovitaka, waliweka pini katika pua zao, waliweka rangi kwenye kucha na kwenye kope, na midomoni, walipaka wanja machoni, na kupaka hina mwilini na kuweka nywele bandia n.k lakini wengi wa hao waliishia kutamaniwa tu na si kupendwa kama walivyotafuta,

Na wengine waliishia kuonekana kama makahaba, kama Yezebeli, (maana biblia inaonyesha Yezebeli alikuwa ni mwanamke mwenye kupaka uwanja machoni na kupamba kichwa, maana yake kusokota rasta, na kuweka nywele bandia, na ndio maana biblia ikamtaja kama mwanamke kahaba na mchawi soma 2Wafalme 9:22,30, Ufunuo 2:20-22).

Na siku zote mapambo haya mawili hayawezi kwenda pamoja!, ukitumia moja lazima lingine utalikosa…

Ukiwa unapaka uso rangi, unajichubua, unatoboa pua  huwezi kuwa na unyenyekevu, utii, utulivu, au mapambo mengine yote ya ndani huwezi kuwa nayo… ni lazima tu utakuwa na kiburi, tamaa, wivu,.  

Na vile vile huwezi kuwa mtii, mnyenyekevu, mpole (mapambo yote ya ndani) halafu ukavaa nusu uchi, vimini au nguo za kubana…

Ingekuwa mapambo haya mawili yanaweza kwenda pamoja (yaani ya ndani na ya nje) basi biblia isingesema wanawake wasijipambe kwa “mapambo ya nje”, badala yake ingesema “wasijipambe  kwa mavazi ya nje tu pake yake bali pia wajipambe kwa mapambo ya ndani”. Lakini utaona imekosoa moja na kulihakiki lingine, ikiwa na maana kuwa mapambo haya hayawezi kwenda pamoja.

Mama, dada, binti unayetaka kwenda mbinguni?, na unayetaka kupendeza na kupata kibali.. basi zingatia kujipamba kwa mapambo ya ndani na nje jiweke katika hali yako ya asili, uone kama hutapata kazi unayoitafuta, au ndoa, au kibali popote pale uendapo kama ilivyokuwa kwa akina Sara, na wanawake wengine wa kwenye biblia, na Zaidi ya yote pia utaenda mbinguni kwasababu miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na si midoli ya matangazo ya nguo masokoni.

1Timotheo 2:9  “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

10  bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)

LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA.

Rudi nyumbani

Print this post

je! Paulo aliwalaani Wagalatia na Wakorintho?

SWALI: Maandiko yanasema tusilaani, je! Paulo aliwalaani wagalatia na wakorintho?

Wagalatia 1:8  Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9  Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.

1Wakorintho 16:22  Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.

Mtume Paulo alipokwenda katika Galatia na kuwakuta baadhi ya watakatifu wa pale wamegeukia injili nyingine, iliyoletwa na wayahudi, inayosema  ili mtu ahesabiwe haki ni lazima amwamini Kristo pamoja na sheria ya Musa, zaidi ya vile mtume alivyofundisha kwamba kinachoweza kumwokoa mtu ni Imani tu katika Kristo!. Sasa alipoona wamefikia hatua hiyo mbaya ndipo aliposukumwa kusema  maneno hayo makali  kwa wagalatia , kwamba  “mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo waliyoipokea kwake, na alaaniwe”.

Lakini ni vema kufahamu kuwa kauli hii na ile ya 1Wakorintho 16:22 imetumiwa vibaya na baadhi ya wakristo kwa vizazi vingi, kwamba kwa ajili ya injili tunaruhusiwa kuweka laana kwa watu.  Lakini je! Paulo aliwaalaani watu wale?

Jibu la! Kwasababu kama angekuwa ameruhusiwa kuwalaani maadui na wanaokwenda kinyume na , yeye basi asingesema tena maneno haya ya kubariki katika Warumi 12:14

Warumi 12:14  Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

Na isitoshe mtume Paulo alikuwa anawaombea sana rehema ndugu zake  Wayahudi waliopotoka, mbali na neema (Warumi 10:1)

Kama hakuwalaana Je! Katika vifungu hivyo alimaanisha nini?

Hilo Neno kulaani, tukisoma katika tafsiri ya awali ya biblia ya kigiriki  linasomeka kama “Anathema”

Ambalo linamaanisha “mtu aliye chini ya laana/Hukumu ya Mungu”

Hivyo katika vifungu hivyo, Mtume Paulo aliposema “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe” Alimaanisha Hivi;

Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na awe kama mtu aliye chini ya laana ya Mungu”

Na ndio maana mtume Paulo katika hiyo nyaraka yake mbeleni alieleza kwa mapana zaidi, jinsi gani watu waliokuwa wanategemea sheria ili kuwaokoa walivyokuwa chini ya laana ya hukumu. Soma;

Wagalatia 3:10  Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

Kwa hitimisho ni kuwa, mtume Paulo hakuwalaani wakorintho au wagalatia. Bali aliwaeleza uhalisi, madhara ya kuipotosha injili ya Kristo. sisi kama wakristo hatupaswi kuwalaani watu ambao wanatupinga/ au wanahubiri injili inayopotosha, bali ni kuwaombea rehema, wageuzwe, lakini bila kuwaficha matokea ya kutenda kwao huko, Kwamba wapo chini ya laana ya Mungu na hivyo waogope! Kwasababu hukumu ipo.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?

Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasichukue chochote isipokuwa fimbo tu?

MWAGA DAMU YAKO KWA AJILI YA BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post

Ipi tofauti kati ya matoleo na sadaka?

Jibu: Jina la Bwana Yesu Kristo lisifiwe daima.

Matoleo ni Neno la ujumla linalomaanisha aidha sadaka, au michango.

Neno Matoleo linatokana na neno “Kutoa” Hivyo chochote kile mtu anachokitoa kwa Mungu wake kinaitwa Matoleo.

Lakini sadaka ni toleo rasmi ambalo linalenga moja kwa moja madhabahu, na matoleo ya sadaka tofauti na matoleo mengine kama michango ni kwamba sadaka inakuwa ni siri lakini michango mengine inaweza isiwe Siri,

Kwamfano yale matoleo Anania na Safira mkewe waliyoyatoa ya kuuza viwanja na kuleta thamani yake chini ya miguu ya mitume, hayakuwa siri, bali lilikuwa ni jambo linalowekwa wazi kwa wote.

Lakini sadaka haipaswi kuwa kitu cha kuonyesha mbele za watu, bali kinapaswa kiwe siri ya mtu na Mungu wake…kama Bwana wetu Yesu alivyotufundisha.

Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”.

3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;

4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.

Na Matoleo yote (iwe changizo au sadaka). Yana thawabu kubwa mbele za Mungu kama yakitolewa kwa nia njema na dhamiri njema na kulingana na Neno la Mungu,na Mungu anayaangalia sana.

Ukiahidi au ukipanga kumtolea Mungu kitu, basi hakiksha unatimiza kama ulivyoahidi au ulivyopanga pasipo kupunguza hata kidogo, ili isiwe kwako dhambi kama ilivyokuwa kwa Anania na Safira mkewe, ambao waimdanganya Roho Mtakatifu kwa matoleo yao.(Matendo 5:1-11).

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +25569303661

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;

Rudi nyumbani

Print this post

UUNGU NI NINI? (1Petro 1:3-4)

2 Petro 1:3  Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe

4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

Uungu ni Ile Hali ya kuwa kama Mungu.

Kwamfano mtu anayefanya vitendo viovu kama vya  uuaji, utoaji mimba, uchawi, ushoga tunasema anafanya “Ushetani”.. Kwasababu anatenda kazi za shetani. 

Vivyo hivyo tunaposema “Uungu”. Tunamaanisha kuwa kama Mungu, au kufanya kazi kama za Mungu, au kuwa na sifa za Mungu ndani yako.

Na Tabia ya Mungu ndani ya Mtu. Si Kila mtu anazo. Bali ni wale tu waliozaliwa na yeye. Yaani waliokoka

Hizi ni baadhi ya Tabia za kiungu.

1. Uzima wa milele:

Kitu ambacho Mungu anawakiria watu wake waliompokea ni uzima wa milele. Ambao upo ndani yake. Mwanadamu wa Tabia ya asili Hana uzima wa milele ndani yake. Akifa Hana Tumaini la kuishi. Lakini aliyezaliwa mara ya pili. Huishi milele. Kwasababu uungu upo ndani yake.

Yohana 10:34  “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?”

Ukiwa kama mwana wa Mungu sifa hii ni lazima itaonekana ndani yako. Hakikisho la uzima wa milele, mwovu hana uzima wa milele.

2. Matunda ya Roho

Pili mtu mwenye uungu ndani yake, anatoa tabia za Mungu ndani yake, ndio zile tabia za Roho tunazozisoma katika Wagalatia 5:22, kama vile Upendo, , fadhili, uaminifu, utakatifu n.k.

Wagalatia 5:22-25

[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, [23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. [24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. [25]Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

Mambo ambayo huwezi kuyaona kwa mtu mwenye tabia ya asili. Yeye huwa kinyume chake, au akijaribu kufanya basi ni kwa unafki, kwasababu havipo moyoni mwake.

3. KUSHINDA DHAMBI:

Na pia mtu mwenye tabia ya uungu unakuwa na uwezo wa kuushinda ulimwengu(yaani dhambi) kama vile Kristo alivyoushinda ulimwengu..

1 Yohana 3:9

[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

Maana yake,dhambi inakuwa haina nguvu ndani yake. Maandiko yanasema hata wao wenyewe wakishangaa tunawezaje kuishi  maisha ya mbali na dhambi (1Petro 4:4). Hawajui  Ni kwasababu sisi tuna tabia za uungu ndani yetu.

Maandiko mengine yanayoeleza Neno uungu. Ni haya  (Matendo 17:29, Warumi 1:20).

Bwana akubariki.

Je! Na wewe utatamani uwe na tabia za Ki-Mungu ndani yako?. Ni wazi kuwa hii ni kiu ya kila mmoja wetu. Kama ni hivyo basi, hauwezi kwa akili yako au nguvu zako, bali kwa Roho wa Mungu. Kwasababu biblia inasema wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika wana wa Mungu (Yohana 1:12). Hivyo huu ni uwezo utokao kwa Mungu mwenyewe, na sio kwa mwanadamu. Na tunaupata kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kwa kumkiri Yesu, na kumfanya kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu. kisha kumpa nafasi ya kuyatawala maisha yetu.

Hivyo basi ikiwa upo tayari siku ya leo kutubu dhambi zako, ili Bwana akufanye kiumbe kipya. Basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa Sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

Uzima wa milele ni nini?

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

DANIELI: Mlango wa 12.

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

Ni kosa gani alilolifanya Eli, ilihali aliwaonya watoto wake?

Rudi nyumbani

Print this post

SILAHA MADHUBUTI YA MALAIKA. (Itumie itakusaidia)

Ni lazima tujue namna mbalimbali za kupambana na adui yetu (Ibilisi). Tunajua yeye ni mpinzani wetu, na  mpinzani sikuzote huwa si rahisi kukubali kushindwa kirahisi, ni lazima ataleta ukinzani. Na ndio hapo suala la Kukemea linakuja wala  hatumbembelezi wala hatumsihi-sihi, bali tunamkemea.

Kukemea maana yake ni kukipinga/ kukifukuza kitu kwa nguvu, kwa mamlaka uliyonayo.

Tunaona sehemu nyingi Yesu akimkemea ibilisi Pamoja na mapepo yake, ambayo yalikuwa yanawatesa watu.

Mathayo 17:18  “Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile”.

Marko 8:33  Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu

Hivyo na sisi tumepewa mamlaka hiyo, ya kumkemea ibilisi na mapepo yake, na uovu, na magonjwa, na vitu vya asili  kwa jina la Yesu na vikatii. 

Lakini pia tuna majira si lazima tufanye hivyo, Tutatumia nguvu nyingi sana!  Leo tutaona silaha nyingine za Malaika ambayo wanatumia kumshughulikia shetani.. Maandiko yanatuambia wanao uwezo mkuu kuliko sisi lakini hawatumii uwezo wao wakati wote, kufanya hivyo kila wanapokutana na adui yao shetani.

Kwamfano, Wakati Fulani Malaika Mikaeli alipokutana na shetani, wakiushindania mwili wa Musa, maandiko yanasema, hakutumia uwezo wake kumlaumu, bali alisema Bwana na akukemee!.

Yuda 1:9  “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee”.

Utajiuliza ni kwanini afanye vile? Sio kwasababu alishindwa, lakini alitambua SILAHA kubwa Zaidi itamfutilia mbali adui yake. Kwa namna nyingine Mikaeli alikuwa anamchonganisha shetani kwa Mungu. Na ukikemewa na Mungu unatarajia nini? Kama sio kupotelea mbali kabisa moja kwa moja.

Hivyo shetani anaiogopa vita ya Mungu Zaidi ya ile ya malaika au wanadamu.  

Utaona tena jambo kama hili hili alilitenda Malaika mwingine, wakati ule wa Yoshua kuhani mkuu alipokuwa amesimama mbele za Bwana kuomba, na shetani naye amesimama kumpinga. Yule Malaika alimwambia shetani “Bwana na akukemee”.

Zekaria 3:1 “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.  2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?”

Umeona? Hivyo si kila wakati unapopishana na adui yako uso kwa uso, ufikirie kurusha makombora, kuvunja, kuharibu na kubomoa ngome, ndio yapo majira utasimama kuomba hivyo lakini pia tulia kwasababu maandiko yanasema VITA NI VYA BWANA. Mkabidhi Bwana yote. Kwamfano shetani amekuletea majaribu ya magonjwa sugu. Mwambie Bwana yaone mateso yangu, UMKEMEE SHETANI. Arudi nyuma yangu.

Sasa Maombi kama haya, usiyaombe juu juu tu,Fahamu kanuni,  Ni maombi ya kumwita Mungu aingilie tatizo hilo, amwone mtesi wako, Ili pale anapopatumia kama mlango wa kukusumbua AMKEMEE atoke. Tatizo  Lililokutesa kwa muda mrefu Bwana alifutilie mbali, kwa kulikemea. 

Ni maombi aliyoyafanya Esta. Alipoona adui yake Hamani, amepanga vita dhidi yake na uzao wake na ndugu zake wauawe. Hakuhangaika, kushindana na Hamani adui yake. Aliona mambo yatakuwa mengi na kuumizana kichwa. Bali alikwenda moja kwa moja kwa mfalme. Akajinyenyekeza mbele zake, akamfanyia karamu kubwa sana, tena akamwomba katika karamu hiyo aje na yule adui yake, washiriki pamoja.  ndipo mfalme akamuuliza haja yako ni nini, Lakini tunaona Esta bado hakumwambia tatizo lake kwa haraka,, akamfanyia tena na mara ya pili mfalme na adui yake karamu iliyo kubwa kama ile ya kwanza, akawaalika.. Ndipo Mfalme akamuuliza tena Esta haja yako ni nini?. Ndipo Esta sasa akaeleza akasema, ni HUYU ADUI YANGU HAMANI, amepanga kuniua mimi. 

Akamwachia mfalme hukumu yote. Saa ileile Hamani akaenda kutundikwa msalabani, yeye na nyumba yake yote ikauliwa. Na Habari yake ikawa imeisha pale  hadi hivi leo.  Wala Esta hakuita kikosi, wala hakuchukua upanga, wala hakumwambia mfame muue, mvunje shingo, mchome moto Hamani. Hakusema hayo alichomwomba mfalme ni uhai wake tu (Esta 5).

Na ndivyo Mungu atakavyofanya kwa adui yetu Ibilisi na mapepo yake, pale ambapo tutataka Bwana ashughulike na matatizo yetu, zaidi ya sisi kushughulika nayo kuyakemea. Lakini ni sharti sisi tumkaribie yeye, kwa moyo wa upendo, tumfanyie karamu, ya Kupendeza ndipo  tuzikabidhi changamoto zetu kwake.

Hivyo silaha hii ukiitumia vema itakusaidia sana. Jenga ukaribu wako na Mungu, Fanya ibada nyingi, mtolee Bwana sadaka, mwimbie sifa, mtukuze sana, ruka-ruka uweponi mwake, mpendeze moyo wake..( fanya hivi Zaidi ya kurusha makombora, na maombi ya vita) kisha mwishoni ndio mwambie Bwana amkemee adui yako. . Matokeo utayaona makubwa sana, haijalishi tatizo ulilonalo limekusumbua kwa muda mrefu kiasi gani, umepambana nalo kwa muda mrefu kiasi gani, limekuja na kujirudia rudia mara nyingi kiasi gani. Ugonjwa huo hautibiki kwa namna ipi, utakwenda tu.. Safari hii halitarudi kwako tena milele.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

ESTA: Mlango wa 1 & 2

ESTA: Mlango wa 5, 6 & 7

Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?

VITA DHIDI YA MAADUI

HUDUMA YA MALAIKA WAWILI.

USIRUHUSU INZI WATUE JUU YA ROHO YAKO.

Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).

Rudi nyumbani

Print this post

Dinari ni nini na Rupia ni nini (Mathayo 20:2,Ufunuo 6:6)

Dinari ilikuwa ni sarafu ya kirumi yenye thamani ya (utumishi wa kibarua wa siku nzima)..Kwamfano leo hii tuseme kibaru atalipwa kwa siku shilingi elfu 20, na ukawa ndio utaratibu wa nchi nzima, kuwalipa vibarua kiasi hiko kwa siku kama mshahara, basi kiasi hiko cha fedha kingekuwa na thamani sawa na Dinari kwa wakati huo.

Tutalithibitisha hilo Zaidi katika ule mfano Bwana alioutoa wakulima walioajiriwa katika shamba la mizabibu..

Mathayo 20:1  “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu

2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima KUWAPA KUTWA DINARI, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu”.

Kwahiyo “ malipo ya utumishi wa kutwa nzima wa kibarua” ndiyo yaliyokuwa na uthamani wa “Dinari”  na uzito wa sarafu ya Dirani ulikuwa ni “gramu 3.85”,

Kwa urefu kuhusiana na vipimo hivyo fungua hapa  >>>VIPIMO VYA KIBIBLIA

Lakini tukirudi katika “Rupia”.. tunaisoma sehemu moja tu katika kitabu cha Ufunuo 6:6

Ufunuo 6:5  “Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.

6  Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa NUSU RUPIA, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu RUPIA, wala usiyadhuru mafuta wala divai”.

“Rupia” ni sarafu nyingine yenye thamani sawa na “Dinari”.. ambayo ilikuwa inatumiwa zaidi namataifa mengine tofauti na Rumi (uthamani wake ulikuwa ni sawa na mshahara wa kibarua wa kutwa)… Na mpaka sasa bado baadhi ya mataifa yanatumia Rupia!.

Lakini ni somo gani tunalolipata kutoka katika thamani hii ya fedha (Dinari na Rupia)?

Somo kubwa tunalolipata si lingine Zaidi ya lile tunalolisoma katika Mathayo 20:1-16, kuwa thawabu za Mungu hazichunguziki.

Kwa urefu unaweza kusoma hapa >>KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

AINA TATU ZA WAKRISTO.

GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?

Rudi nyumbani

Print this post

Kuba ni nini (Ayubu 22:14)?

Jibu: Tusome,

Ayubu 22:12 “Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!

13 Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?

14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU. 

15 Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?”

Kuba ni mzunguko wa Anga, Ukitazama juu utaona ncha za mbingu ni kama duara, ndio maana jua wakati wa asuhuhi ni kama “linachomoza kutoka chini upande wa mashariki” na wakati wa mchana linaonekana lipo juu kabisa (utosini) lakini inapofika  jioni “linazama tena chini upande wa magharibi”..

Sasa huo mduara wa anga ndio unaoitwa “KUBA” na maandiko yanasema Bwana anatembea juu ya mduara huo, kuonyesha utukufu wake.

Ayubu 22:14 “Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU”. 

Hivyo andiko hili linaonyesha utukufu na ukuu wa Mungu, kuwa yuko juu sana na mwingi wa uweza.

Je umemrudia yeye aliyezifanya Nyota na Mwezi, na anga na viumbe vyote?..

Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.

 2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

MKUU WA ANGA.

NYOTA ZIPOTEAZO.

Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?

Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.

Mbinguni ni sehemu gani?

Rudi nyumbani

Print this post