Wagalatia 6:7 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.
Hapo inasema “chochote” ikiwa na maana kuwa hata vitu visivyokuwa na maana vikipandwa vinaleta majibu.
Na chochote kinachopandwa huwa kinapandwa kama mbegu…na kinapovunwa kinavunwa kama tunda…embe linapandwa kama mbegu, lakini linavunwa kama tunda..
Mtu akipanda mbegu ya dhambi yoyote moyoni mwake leo, akaipalilia hiyo tabia moyoni mwake, baada ya muda fulani, atavuna matunda ya dhambi hiyo..Na matunda yake ni ya aina mbili…MAUTI YA MWILI, na MAUTI YA ROHO…
Mauti ya Mwili, inaweza kuja kutokana aidha Ugonjwa unaotokana dhambi hiyo au janga fulani kwamfano dhambi ya uasherati mauti yake ya kimwili inaweza kutokana na ugonjwa fulani kama HIV, GONOREA au kaswende au inaweza kuja kupitia chanel nyingine yeyote tofauti na hiyo..Wengi hawajui kuwa vifo vingi vya ghafla vinatokana na matokeo ya dhambi…hususani dhambi ya uasherati…
Aina ya pili ya tunda la dhambi ni Mauti ya kiroho. Hii ni ile hali mtu anakufa katika kuisikia Injili na kuiamini, upo usemi unaosema “sikio la kufa halisikii dawa” kadhalika, roho iliyokufa haiwezi kuisikia Injili tena, na mwisho wake ni ziwa la moto.
Jiepushe na uasherati kwasababu apandacho mtu ndicho atakachovuna, jiepushe na ushirikina, ulevi, anasa, ushoga, ulawiti, usagaji, utazamaji wa picha na video chafu, ulaji rushwa n.k kwasababu mambo hayo yote matunda yake ni kifo.
Kwasababu biblia inasema Mshahara wa dhambi ni Mauti.
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
JE! KUNENA KWA LUGHA MPYA KUKOJE?
JE! KUOMBA KWA BIDII KAMA ELIYA NI KUOMBA KWA NAMNA GANI?
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
Ufunuo 12:17 “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.”
Timotheo 1:4 “Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha;
5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.”
2Yohana 1:4 “Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.
5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
Mithali 14:1 “Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.”
Mada Nyinginezo:
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.
Awali ya yote ili upate ufasaha wa ndoto yako, na kuepuka kudanganywa na kila aina ya tafsiri mtu yeyote anayoweza kukuletea, awali ya yote unapaswa ufahamu ndoto yako inaangukia katika kundi lipi,
Yapo makundi makuu matatu (3) ya ndoto:
Ndoto zinazoangukia katika kundi hili la tatu ndizo zinazootwa na watu mara kwa mara kila siku na kama mtu asipoweza kuzitambua atajikuta anahangaika nazo, na huku hazina maana yoyote ya kumsaidia, kwasababu ni ndoto zinazokuja kutokana na shughuli anazozifanya kila siku au mazingira yanayomzungumka muda wote hivyo hizi huwa hazibebi ujumbe wowote..
Kwahiyo ni rahisi ubongo wake kuchukua yale matukio anayoyofanya kila siku na kuyatengenezea matukio yanayofanana na hayo katika ndoto usiku na kuota, ukijiona unaota hivyo basi puuzia ndoto hizo
Ikiwa unahitaji kufahamu kwa undani juu ya makundi haya basi pitia somo hili kwanza >>>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI? kisha ndio tuendelee,
Kwamfano ndoto za namna hii za kujiona unapewa pesa, utakuta mtu mmoja kazi yake kila siku ipo kwenye pesa kama vile benki au mfanyabiashara ambaye muda wote analipa na kulipwa pesa, hivyo kuota anapewa pesa linaweza kuwa ni jambo la kawaida kwake kutokea katika ndoto zake za kila siku, kwasababu ubongo ulishajiengenezea ulimwengu kama huo.
Lakini ikitokea umeota ndoto katika mazingira, ambayo hayaendani na wewe kupewa pesa, au umeota ndoto hiyo na ukaiona si ndoto ya kawaida, au ulikuwa katika maombi ya kumwomba Mungu kitu Fulani na imekuja na uzito Fulani hivi, au amani Fulani hivi, basi fahamu kuwa upo ujumbe unapaswa kujifunza ndani yake.
Kumbuka kibiblia Fedha inawakilisha chombo cha kuletea jawabu.
Mhubiri 10:19 “Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote”.
Hivyo Mungu kukuonyesha katika ndoto, unapewa fedha, ni ishara kuwa amekupa jawabu la ombi lako, na hivi karibuni utapata haja yako..Ila tilia maanani kitu kimoja hapo biblia inaposema, fedha huleta jawabu la mambo yote haimaanishi kuwa inaleta majibu mpaka kwenye mambo ya rohoni hapana, fedha haiwezi kuleta uzima ndani ya mtu wala haiwezi kununua upendo..lakini kama ukichunguza hapo utaona mistari hiyo inalenga mambo ya ki mwilini..kama vile shughuli za karamu, nguo, chakula, nyumba, gari, biashara, ambavyo hivi kimsingi vinahudumiwa na fedha..
Pia tazama..
Lakini tukirudi kwenye hiyo ndoto ya pesa vile vile usitegemee sana kuwa atatumia njia hiyo hiyo uliyoiona kwamba kweli kuna mtu atakujana kukupa wewe fedha hapana, inaweza ikawa hivyo au isiwe hivyo, anaweza kutumia njia pengine ya kuirutubisha kazi yako unayoifanya sasa hivi ,au ukapata kibali mahali Fulani pengine kazini kwako, ambapo boss wako atakulipa vizuri zaidi kuliko sasa hivi, au ukapata mkopo wa kufanya biashara yako n.k.Na kama ukijiangalia ndio utagundua vitu vya aina hiyo hiyo ndio ulivyokuwa unamwomba Mungu…
Hivyo ametumia ndoto ya fedha kama ishara ya kukuonyesha kuwa maombi yako ameyasikia,..Lakini usitazamie kuwa mtu anayemwomba Mungu mambo ya rohoni kama vile uzima wa milele, au Roho Mtakatifu, au nguvu za Mungu, ataonyeshwa ndoto za namna hiyo kama jibu la maombi yake hapana.. Mungu atamwonyesha Maono ya rohoni, pengine usishangae mtu kama huyo kuona maono ya mbinguni, au kukutana na malaika ndotoni, au kuisikia sauti ya Mungu ikisema naye, au kuota anahubiri au anafundishwa biblia n.k…
Hivyo kaa katika matarajio huku ukiulinda ukamilifu na utakatifu katika kazi yako, ndipo Mungu ataitimiza ahadi yake juu yako. Lakini kama wewe upo nje ya Kristo ukaota ndoto kama hiyo, fahamu kuwa ni ishara mbaya nayo ni ishara ya upotevu zaidi..utakwenda kufanikiwa lakini ni ili upotee..
Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”.
Usisibirie udanganyifu wa mali au mafanikio vikuangamize..Mrudi Muumba wako mapema, tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa Jina la YESU KRISTO ikiwa bado hukubatizwa kisha anza kumwangalia Mungu ili yeye atembee pamoja na wewe katika njia zako zote.
Ubarikiwe.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mithali 1:32
kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
Mahusiano yoyote yale yanayohusisha watu wa jinsia moja ni machukizo mbele za Mungu..Biblia imeweka wazi katika kitabu cha Mambo ya Walawi
Walawi 18:22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”.
Walawi 20:13 “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao”
Kutokana na anguko Ipo asili ya dhambi ambayo mtu anazaliwa nayo… inafanya kazi ndani ya mtu, tangu akiwa tumboni mwa mama yake…hiyo inamfanya mtu anazaliwa na tabia fulani fulani ambazo asili yake ni dhambi…mfano wa tabia hizo ni kama hasira zisizokuwa na sababu, kiburi, uchungu usiokuwa na sababu, ukorofu, utundu, tamaa ya uasherati n.k vyote hivyo vinatokana na ile asili ya dhambi mtu anayozaliwa nayo.
Lakini pamoja na hayo, kuna dhambi ambazo Mungu aliziweka mbali sana na mwanadamu kuzifikia, na hizo hazimo miongoni mwa dhambi za asili..Ni dhambi lakini mtu anakuwa hazaliwi nazo… Mtu mwenyewe kwa mapenzi yake anapokuwa mtu mzima anaweza kuzipachika ndani yake na kuzifanya.
Na moja ya dhambi hizo ni dhambi za kumtamani mtu wa jinsia moja na ya kwako. Hiyo tamaa ya namna hiyo haipo ndani ya mtu tangu anazaliwa. Mwanamke kumtamani mwanamke mwenzake au mwanamume kumtamani mwanamume mwenzake…
Dhambi hii ni moja ya dhambi mbaya sana kuliko nyingi kwasababu ipo kinyume na UHAI na UZIMA.
Hebu tafakari endapo Adamu angekuwa na Adamu mwenzake sisi tungetokea wapi? Au wakina Hawa wangeumbwa wawili, sisi tungetokea wapi leo?.. Neno la Bwana linalosema zaeni mkaongezeke lingekuwa wapi?…Hebu fikiri Wanyama wangekuwa wote wa jinsia moja..hii mifugo tuliyonayo leo ingekuwa wapi?…Maziwa tunayokunywa yangetokea wapi? Nyama tunazokula nazo zingetokea wapi, asali tunayoifurahia ingetoka wapi? Endapo nyuki wote wangekuwa wakike au wakiume?
Hata chakula tusingekuwa nacho, kwasababu hata mimea ina sehemu ya kike na ya kiume…sasa kama mimea yote ingekuwa na sehemu ya kiume tu, au ya kike tu…hiyo ngano tunayokula kila siku ingetokea wapi? Mboga tunazokula zingetokea wapi?..Kwahiyo dunia isingekuwa dunia wala Maisha yasingekuwepo endapo kungekuwa na jinsia moja tu duniani.
Kwahiyo dhambi ya mahusiano ya jinsia moja ni dhambi ya KIFO, Kwasababu ipo kinyume na UHAI…Chochote ambacho kipo kinyume na Uhai ni Kifo. Na yeyote afanyaye dhambi ya kifo atakufa.
Kaa mbali na ushoga ni dhambi, kaa mbali na usagaji, wapo wengi wanafanya dhambi hizi kwa siri, pasipo kujua madhara ya dhambi hiyo, Ni dhambi zinazoivuta ghadhabu ya Mungu kwa haraka sana….Dhambi zilizoifanya sodoma na ghomora ziteketezwe ni dhambi hizo za mahusiano ya jinsia moja. Na dhambi hizi hazina cha kujitetea kwasababu ni dhambi za makusudi..Mtu anazipandikiza ndani yake akiwa na akili timamu kabisa, hazina ushawishi wowote..hakuna mazingira yoyote yanayomshawishi mtu kumtamani mtu wa jinsia moja na yeye, ni mtu mwenyewe anazitengeneza ndani yake kwa msaada wa roho za mapepo.
Warumi 1:26 “Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”
Tubu, kama wewe ni mmojawapo, kisha uanze uanze kutafuta kuyafanya mapenzi wa Bwana. Naye atakuangazia neema zake.
Shalom.
Mada Nyinginezo:
NINI TOFAUTI KATI YA DHAMBI, UOVU NA KOSA KIBIBLIA?
LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.
Isaya 41:21 “Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo”.
Mathayo 6:6 “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.11 Utupe leo riziki yetu.12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina”.
Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”
Ufunuo 7:11 “Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina”.
Mada Nyinginezo:
NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU.
UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.
Ayubu 19:23 “Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa! Laiti yangeandikwa kitabuni!
24 Yakachorwa katika mwamba milele, Kwa kalamu ya chuma na risasi.25 Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.
26 Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;”
Yeremia 17:1 “Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu;”
2Nyakati 36: 14 Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu.
15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake”
Mada Nyinginezo:
MUNGU KUSEMA NA WEWE PEKEE, HAITOSHI KUKUPA USHINDI.
NABII ELISHA ALIKUWA ANA MAANA GANI KULIA NA KUSEMA”GARI LA ISRAELI NA WAPANDA FARASI WAKE”?
Kama unamcha Mungu kweli, na unakwenda katika njia zake, yeye ni mwaminifu hawezi kukusahau. Kabla maisha yako hayajaisha hapa duniani, atakuridhisha, atakufikisha mahali ambapo ni zaidi hata ya ulivyokuwa unafikiri.
Kama hakumsahau Yusufu, ambaye aliuzwa Kama Mtumwa Taifa la mbali kabisa, hawezi kukusahau wewe kama unakwenda katika njia zake.
Kama hakumsahau Musa ambaye aliacha hazina zote za Misri na kwenda majangwani, hawezi kukusahau wewe uliyeacha kila kitu na kumfuata Mungu..
Waebrania 11:26 “akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana”
Kama hakumsahau Hana aliyekuwa Tasa na kumpatia watoto wengi..Hawezi kukusahau wewe unayemcha leo, hajabadilika ni yeye yule vizazi na vizazi,
Isaya 49:14 “Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.
15 Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
16 Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima”.
Mche tu yeye! Jitenge na uovu, kuwa mtumishi wake..Utauona wokovu wake, hatakusahau kamwe! hawezi kusema uongo.
Isaya 44:21 “Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi”
Kinachowakosesha wengi ni dhambi katika maisha ya watu,vitu kama uasherati, usengenyaji, wizi, ulaji rushwa, utukanaji, ibada za sanamu, wivu, biashara haramu, uvaaji mbaya, kutokusamehe n.k hivyo ndivyo vitu vinavyoharibu mpango wa Mungu juu ya maisha yetu…Lakini mtu akijitenga na hivyo Kamwe Mungu hawezi kumsahau, haijalishi itapita miaka mingapi lakini atakuja kuuona utukufu wa Mungu maishani mwake.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?
Moja kwa moja ndoto kama hii inatoka kwa Yule mwovu, kukimbizwa kwa namna yoyote ile maadamu ni kukimbizwa basi ni kutoka kwa yule mwovu, iwe ni kuota unakimbizwa na watu au kuota unakimbizwa na nyoka au kuota unakimbizwa na ng’ombe, au kuota unakimbizwa na simba, au kuota unakimbizwa na tembo au kuota unakimbizwa na nyuki, au kuota unakimbizwa na kichaa, ni ndoto kutoka kwa mwovu…Sikuzote kitu kinachokimbizwa ni kitu kilicho dhaifu, cha kuwindwa ili kiliwe, swala anakimbizwa na simba, ni kwasababu yeye ni dhaifu, lakini kitu chenye ujasiri kamwe hakikimbizwi.
Ukijiona unakimbizwa fahamu kabisa moja kwa moja kuwa wewe ni dhaifu rohoni, na hiyo ni kutokana na kuwa upo nje ya Kristo au kama upo basi hauijatambua mamlaka uliyonayo ndani ya Kristo kwa uchanga wako wa kiroho au kwa uzembe wako wa kutokujishughulisha na mambo ya Mungu..
Mithali 28:1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
Hivyo mrudie Mungu wako kama bado haujaokoka, Tubu ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na uwe kwa Jina la Yesu Kristo, ili upate ondoleo la dhambi zake. Au kama tayari ulikuwa ndani ya Kristo na ulikuwa unayumba yumba huu ni wakati wako sasa kusimama imara.
Kisha anza kujifunza biblia kwa bidii, na pia tafuta kanisa la kiroho la kwenda kujifunzia Neno la Mungu, ili likae kwa wingi ndani yako, upate kujua nafasi uliyonayo katika Kristo. Mpaka siku moja na wewe uote unamkimbiza shetani.
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”
Usipuuzie ndoto hizo, kwasababu shetani kweli anakuwinda akumeze…Fanya uamuzi wa busara kumgeukia Mungu.
Ubarikiwe.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
Hii ni moja ya ndoto ambayo inaotwa na watu wengi sana, na hii huwa inachukua maumbile tofauti tofauti, wengine utakuta wanaota wanafanya mitihani na hawajajiandaa, wanachoshtukia tu ni wakati wa mtihani umefika, na hakuna chochote walichofanya wanajiuliza siku zote alikuwa wapi…wengine wanaota wanafanya mtihani mgumu sana lakini wenzao wanaonekana wanafahamu cha kujaza yeye hajui,
wengine wanaota kama walikatisha masomo wakaondoka, baadaye waliporudi muda umeshapita mitihani ya mwisho imekaribia, wengine wanaota wamerudia madarasa ya nyuma ambayo tayari wameshayavuka siku nyingi na ni lazima wayavuke ili waendelee na madarasa ya mbele, wengine wanaota wapo wanafundishwa, wengine wanapewa adhabu, wengine wapo tu n.k.…Kwa ufupi ndoto unazoota upo katika mazingira ya shule, zote zina maudhui moja.
Na ndoto hizi huwa zinatesa sana, zinaweza kujirudia hata kila baada ya wiki au mwezi, au miezi kadhaa, inategemea na mtu na mtu, lakini ni ndoto ambazo haziachi kuja.
Biblia inasema..
Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”
Mungu siku zote huwa anapenda kutumia vitu vinavyotuzunguka kutufikishia sisi ujumbe fulani , na ndio maana utaona Bwana Yesu alipokuwa anafundisha mifano yake yote alikuwa anatumia mambo ya kawaida tu yanatozunguka sikuzote ili kutufikishia sisi ujumbe na tuulewe utaona wakati mwingine alitumia mifano ya ndege, wafanyabiashara, wafalme, harusi n.k…
Hivyo na Mungu ili kukufikisha ujumbe wake wa wokovu huwa anapenda kutumia mfano wa kitu ambacho kimetukuka sana mbele yako, kitu chenye maana sana kwako ambacho ukikikosa anajua kabisa umekosa maisha na hicho si kingine zaidi ya ELIMU.
Kufunua kuwa Ipo elimu iliyokuu ambayo inayo ufunguo sio tu wa maisha ya hapa bali pia wa maisha ya ulimwengu unaokuja, na hiyo si nyingine zaidi ya Elimu ya Ufalme wa Mbinguni..Mungu anakuonyesha hali yako ya kiroho ilivyo kupitia maisha yako ya shuleni, kama unavyojiona upo shuleni hujajiandaa, au mtihani ni mgumu basi katika roho ndivyo hivyo ulivyo.. kuwa upo nyuma, na unapaswa ushinde, yapo madarasa haujayavuka bado, upo pale pale kiroho umekwama, unatamani uendelee mbele unashindwa au unaona ni ngumu kwasababu bado hujayamaliza madarasa ya nyuma Mungu aliyokupa.
Hivyo unapaswa uongeze bidii yako kwa Mungu, ili ufike pale Mungu anapotaka kufika, ongeza kiwango chako cha maombi, jifunze Neno la Mungu sana, ishi maisha yanayompendeza Mungu, punguza muda wa kuihangaikia dunia, na ongeza muda wako wa kumtafuta Mungu, kwasababu yeye ndio ufunguo wa kweli wa maisha yako ndugu. Ukimpata Mungu umepata vyote.
Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”
Hivyo ukiwa na bidii na Mungu akaridhika na wewe basi atakuvusha na kukupeleka katika kiwango kingine cha kiroho na kiufahamu. Kumbuka Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha ndoto kama hizo, Hivyo usipuuzie ungeza bidii yako kwake.
Ubarikiwe.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.
MTEGEMEE MUNGU, NA SI MWANADAMU.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu YESU KRISTO, Suala la upambanuzi wa ndoto ni moja ya mambo ambayo yanawasumbua wengi, lakini kwa bahati mbaya watu wengi wamekosa kujua tafsiri ya ndoto zao, kulingana na maandiko…
Hivyo kabla ya mtu hukimbilia kupewa au kutafuta tafsiri ya ndoto yake ni vizuri kwanza akafahamu kuwa ndoto zimegawanyika katika makundi makuu matatu, kundi la kwanza ni zile ndoto zinazotokana na Mungu, kundi la pili ni zile zinazotokana na shetani na kundi la tatu ni ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe, na hizi ndizo zinazochukua sehemu kubwa ya ndoto tunazoziota karibu kila siku, na aina hii ya tatu huwa inakuja kutokana na shughuli zetu tunazozifanya kila siku au mazingira yanayotuzunguka kila siku..
Ndoto za namna hii huwa hazibebi ujumbe wowote, hivyo hazihitaji kutafsiriwa, mara nyingi zinapaswa zipuuziwe..ikiwa hujafahamu vizuri namna ya kuitambua ndoto yako kulingana na makundi haya basi bofya somo hii ulipitie kisha ukishamaliza tuendelee…>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?
Watu wengi wamekuwa wakiniuliza tafsiri ya ndoto hii ya kuota nyoka, sasa ikiwa ni ndoto ambayo inajirudia rudia, basi izingatie sana..kumbuka Nyoka katika maandiko tangu mwanzo anasimama kama ishara mbaya,
Na nyoka amebeba tabia kuu tatu, ya kwanza ni kudanganya kama tunavyomsoma pale Edeni alivyomdanganya Hawa (Mwanzo 3:1-5), tabia ya Pili ni kuuma kama biblia inavyotuambia atakugonga kisigino (Mwanzo 3:15), na ya tatu ni kumeza, kama tunavyosoma katika kitabu cha Ufunuo 12:4), pale alipotaka kummeza mtoto yule alipotaka kuzaliwa,..Na tabia hizi zote Shetani anazo na ndio maana kila mahali alifananishwa na joka, na sio kiumbe kingine chochote kama vile kondoo au njiwa.
Hivyo ndoto za namna hii nyingi zinatoka kwa shetani, na chache sana zinakuja kutoka kwa Mungu, lakini tukianza kuchambua upande mmoja mmoja hatutamaliza, wengine wanaota wanakimbizwa na nyoka, wengine wanaota wanaumwa na nyoka, wengine wanaota wameviringishwa na nyoka, wengine wanaota wapo karibu na ziwa au bahari na lijoka likubwa linatoka huko, wengine wanaota wanamezwa na joka, wengine wanaongea nayo n.k. n.k. vyovyote vile chamsingi ambacho mtu anapaswa kufahamu hapo ni kuwa ziwe zinatoka upande wa Mungu au upande wa shetani,..Ni kwamba ADUI YUPO MBELE YAKO.
Hapo Shetani yupo karibu na wewe kutimiza kazi hizo tatu au aidha mojawapo,
Jambo la kwanza ni kukudanganya au tayari ameshakudanganya: Sasa Ikiwa upo nje ya Kristo yaani hujaokoka basi fahamu kuwa upo chini ya udanganyifu wa shetani tayari, hivyo hapo unaonyeshwa hali yako ilivyo rohoni, Jambo unalopaswa kufanya ni kurudi kwa Kristo haraka sana kabla udanganyifu haujawa mkubwa zaidi ukakuzalia matunda ya mauti, hapo ulipo tayari umepofushwa macho pasipo hata wewe kujijua. Hivyo tubu umgeukie Mungu haraka sana, maadamu muda bado upo.
Au kwa namna nyingine shetani anakaribia kukushawishi kuingia katika kosa au dhambi ambayo itakugharimu sana, hata maisha yako, hivyo angalia njia zako, uchukue tahadhari, funga milango yote ambayo unaona itakupeleka mbali na Kristo, acha kufanya vitu ambavyo sasa hivi unavifanya unaona kabisa havimpendezi Mungu, acha haraka sana, upo mtego wa shetani nyuma yake.
Pili shetani anakutegea mtego au anataka kukuletea madhara aidha katika huduma yako, au afya yako,au familia yako au shughuli yako, anataka kukugonga kisigino chako usisonge mbele, hapo unapaswa uongeze kiwango chako cha maombi kama Bwana Yesu alivyosema ombeni msije mkaingia majaribuni..Hivyo ili kumshinda silaha uliyonayo ni kuomba sana.
Tatu shetani anataka kukimeza kile ambacho Mungu amekipanda ndani yako:
Na jambo la kwanza huwa anakimbilia ni NENO LA MUNGU hilo ndilo huwa anafanya bidii sana kupambana nalo kwasababu anajua likishakuwa ndani ya mtu litakwenda kuleta madhara makubwa sana katika ufalme wake hivyo anasimama hapo karibu na wewe ili akimeze kile ulichokisikia.. inafananishwa na zile mbegu ambazo zilingukia njiani ndege wakaja kuzila,
Mathayo 13:18 “Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.
13.19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”
Hivyo kwa ufupi ikiwa upo nje ya Kristo fanya hima uingie ndani, na ikiwa upo ndani ya Kristo chukua tahadhari uimarishe uhusiano wako na Kristo kwasababu shetani yupo karibu na wewe kushindana nawe kwa kila hali..
Ubarikiwe.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.
JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.