Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;
Waefeso 6:18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote
Yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu
Watu wengi wanaamini kuomba katika Roho ni kuomba kwa “kunena kwa lugha tu”. Nje ya hapo sio kuomba kwa Roho. Lakini tukiwa na mtazamo huo basi tutakuwa na uelewa finyu kuhusu Roho Mtakatifu.
Ukweli ni kwamba hiyo ni namna mojawapo kati ya nyingi ambazo Roho wa Mungu anamjalia mtu kuomba.
Maana ya ‘kuomba katika Roho’ Ni kuomba ‘ndani ya Roho ya Mtakatifu/ ndani ya utaratibu/ uwepo wa Roho Mtakatifu’. Na hiyo ni zaidi ya kunena kwa lugha, Hii ikiwa na maana Mtu anaweza kuomba lakini asiwe katika uwepo huo. Na matokeo ya hivyo ni maombi kuwa makavu sana, yasiyo na nguvu.
Sasa mstari mama unaotufundisha juu ya uombaji wa Roho Mtakatifu ni huu;
Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA”
Hapo anasema “kuugua kusikoweza kutamkwa” . Maana ya kuugua hapo ni kuweka uzito, au presha, au shauku ya kuomba ndani ya mtu isiyokuwa ya kawaida. Tofauti na angejitahidi kwa nguvu zake yeye mwenyewe. Sasa mtu akifikia hatua hiyo, basi tayari kuanzia huo wakati anaomba katika Roho hata kama maneno yake ni ya kawaida anayoyatumia. Maombi hayo yana nguvu na yanasikika sana mbele za Mungu.
Kwamfano, ndio hapo utakuta mtu anaomba, lakini mara anasikia kububujika machozi ndani yake, mwingine anazidi kuona kiu ya kuendelea kuombea jambo lile lile kwa muda mrefu tofauti na sikuzote. Mfano wakati ule Bwana Yesu alipokuwa Gethsamane anaomba.
mwingine anajisikia wepesi usio wa kawaida, uchovu wote umeondoka ijapokuwa alikuwa amechoka sana, anaanza furahia maombi, anafurahia kuendelea kubaki palepale muda mwingi kuendelea kuomba,
Sasa hali kama hizi ukizifikia, ujue tayari umeshazama katika Roho, umeshawezeshwa na Roho, maombi yako yanakuwa na nguvu sana,
Mwingine anasikia raha Fulani moyoni, akiwa anaomba, mwingine ndio anazama katika kunena kwa lugha (kwa kusukumwa na Roho), na sio kwa akili. Mwingine anasindikizwa na kuusikia uwepo wa Mungu umemfunika, nguvu za Mungu zinashuka mwilini mwake, n.k. na unajikuta unafurahia sana maombi..
Kusudi la sisi kuomba sio kwenda kujitesa au kujiumiza, hapana bali ni mahusiano, tena ya kama mtu anazungumza na Baba yake. Kiasi kwamba ukitoka kwenye maombi unaona umetoka kweli kuwasiliana na mtu, sio umetoka kuusemesha ukuta, usiokuwa na mrejesho wowote, umeomba hewani hewani tu
Sasa ni mapenzi ya Mungu kwamba sisi watoto wake kila tuombapo tuombe katika Roho Mtakatifu. Tuzame, tuyafurahie maombi yetu. Sasa tunawezaje kufikia hatua hiyo?
Kabla ya kuona namna ya kufikia hicho kilele. Tuone kwanza vikwazo vinavyomzuia mtu asiombe kwa Roho.
VIKWAVYO VINAVYOPINGANA NA MTU KUOMBA KATIKA ROHO.
Hawa ndio maadui wawili wakubwa wa mtu kuzama. Ndio maana wewe kama mwombaji ni lazima uwafahamu, na ujue kabisa huna budi kushindana nao na ni lazima ukutane nao. Vinginevyo usipowatilia maanani kila siku maombi yako yatakuwa ni ya “kawaida sana” na kila utakapofikiria kitu kinachoitwa maombi utaona kama vile unapelekwa gerezani.
Ndugu Mungu hajakusudia tujihisi hivyo sisi watoto wake tunapomkaribia yeye, tuwe kama tunaliomba sanamu lisilonena, amekusudia kutupa mrejesho, na ndio hiyo zawadi ya Roho kuugua ndani yetu. Lazima atupe mrejesho wake kwamba yupo nasi.
Sasa uanzapo, hakikisha unaunyima mwili wako, raha zote, zinazokinzana na wewe kuomba. Kwamfano, ukijiona mwili unasinzia au unapoa wakati wa kuomba usipende kukakaa kwenye kiti, ni heri upige magoti, ukishindwa tembea-tembea. Tena ni vizuri ukanyoosha na mikono yako juu, huku umefunika macho. Kisha anza kuomba.
Usiogope adhabu hizo za mwanzoni hazitadumu muda mrefu sana utaingia katika Roho, ni mwili tu unakuambia wacha, kunitesa, wewe ulazimishe tu, ukikuambia leo siku nzima umefanya kazi legea-legea, pinga hayo mawazo. Hivyo ukiwa Sasa katika hali hiyo. Anza kuomba lakini pia tumia ahadi za Mungu zilizopo kwenye biblia ni muhimu sana, kulingana na jambo unaloliombea, mkumbushe Bwana, ulisema hivi, na hivi kwenye Neno lako,, Ulisema ni nani aliye Baba, mtoto wake akimwomba mkate atampa jiwe, mkumbushe mwambie ulisema, kama ungetazama dhambi zetu ni nani angesimama,..mwambie ulisema niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua n.k..Tumia njia hiyo, kujimimina kwa Bwana
Omba huku umetilia umakini(concentrate), mawazo yako ukiyalazimisha yasiende nje ya Mungu. Tengeneza picha halisi Mungu amesimama mbele yako kukusikia, fumba macho. Usiruhusu kufikia mambo ya nje, kwasababu akili yako itakuwa shapu kukutoa, ukitoka rudi, endelea kuomba. Ndio ni kipindi kifupi utataabika , lakini hatimaye utazama tu.. Sasa ukiendelea kudumu kwa kung’ang’ania huko kwenye maombi hayo kwa kipindi fulani. Hayo mazingira rafiki ya Roho Mtakatifu kuyaingilia maombi yako. Utashangaa tu, wepesi usio wa kawaida umezuka ndani yako. Tangu huo wakati endelea kuomba kwa jinsi usikiavyo rohoni, kwani hayo maneno unayoyaomba mengine hutaelewa unayatolea wapi, huyo ni Roho Mtakatifu anaomba na wewe.
Ndio maana akasema msifikiri-fikiri, kwasababu Roho mwenyewe atawajalia. Wengine kabla ya kuomba wanasema sijui nitaomba nini? Ndio hujui kwasababu bado hujazama, ukishazama utaweza tu kuomba kwasababu ni yeye ndio anayekujalia. Wengine wanasukumwa kunena kwa lugha n.k.
Adui wa pili ni shetani. Huyu anapaswa apingwe kwa kukemewa. Kabla ya kuanza maombi, hakikisha unayateka mazingira yako ya kimaombi. Ukimwomba Mungu, afukuze uwepo wote wa mapepo, hapo ulipo. Dalili ya shetani, ni pale unashangaa ukiwa unataka kuomba kichwa kinauma au tumbo, au hali Fulani isiyo ya kawaida inakuvaa katika mwili wako. Huyo ni shetani, mpinge kwa kukemea kisha endelea na maombi. Au mwingine anaona mazingira ya kusumbuliwa, mara kelele Fulani za nje, au simu zinaingia, ambazo si kawaida sikuzote kuwepo. Ndio maana ni vizuri katika kuomba kwako uzime simu. Ukae mbali na mazingira yenye mwingiliano, hiyo itakufanya umpe adui wakati mgumu kukusumbua.
Zingatia tu: Shetani haogopi sana maombi ilimradi maombi, anaogopa sana maombi yaliyo katika Roho, Hata kama ni ya muda mfupi, hayapendi, na ndio atakayoyapiga vita sana. Hivyo usiwe mwepesi mwepesi kupenda kuomba juu juu.
Kwahiyo ukizingatia mambo hayo mawili kutakufanya uzame rohoni katika maombi yako yote. Na utayafurahia na utaona matokeo pia.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika sanduku la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA.
SALA YA BWANA. (Namna ya kuiomba)
JE! TUNAPASWA TUOMBE MARA NGAPI KWA SIKU?
Wakili kibiblia ni mtu aliyepewa usimamizi wa nyumba (Au kaya) ya mtu mwingine. Na usimamizi huo unajumuisha kuanzia kwenye ngazi ya kifamilia, mpaka mali alizonazo bwana wake.
Uwakili tunaona tangu enzi za agano la kale, kwamfano, Eliezeri alikuwa ni wakili wa Ibrahimu. Na tunaona yeye ndio alikuwa mwangalizi wa mali zake, lakini pia ndiye aliyehusika kwenda kumtafutia Isaka, mke katika ukoo wa baba zake Ibrahimu (Mwanzo 15:2, Mwanzo 24).
Lakini pia tunamwona Yusufu, naye alikuwa ni wakili katika nyumba ya Potifa, aliachiwa vyote avisimamie, (Mwanzo 39:5-7).
Vilevile tukirudi kwenye agano jipya tunaona, Bwana Yesu alitumia mifano ya mawakili, kuwawakilisha watumishi wake wanaofanya kazi ya kuhudumu/kulichunga kundi lake, kwamba kwa mifano ya wao na sisi tujifunze utumishi uliosahihi kwake.
Kwamfano Luka 12:40-48 Inasema;
“Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
41 Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia?
42 Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye WAKILI mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
43 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.
44 Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
45 Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;
46 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.
47 Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”
Ikiwa wewe umepewa dhamana ya kulichunga/kulisimamia kundi, basi tambua kuwa Bwana anataka aone uaminifu wako wa kuwahudumia na kuwalinda watu wake aliokupa. Yesu alipomuuliza Petro Je! Wanipenda akasema ndio nakupenda!, Hapo hapo akamwambia chunga kondoo zangu, lisha kondoo wangu. Kuonyesha kuwa ikiwa wewe ni mtumishi na unasema unampenda Bwana, basi ujue upendo wako ni kuwachunga na kuwalisha kondoo wa Bwana.
Lakini pia uwakili sio tu kwa waliowatumishi wa Mungu, bali pia kwa kila mwaminio, aliyeokoka, amepewa uwakili wa kuifanyia kazi kwa ile talanta aliyopewa.
Bwana Yesu alitumia mfano wa Yule mtu aliyesafiri, akawaita watumwa wake, akawawekea mali yake yote wafanyie biashara, Hivyo mmoja akapewa talanta 5, mwingine 2, mwingine 1. Kama tunavyoijua habari wale wawili wa kwanza wakafanikiwa kuzalisha, lakini Yule mmoja wa mwisho hakuifanyia chochote talanta yake, akaiacha mpaka aliporudi bwana wake. Matokeo yake ikawa ni kunyang’anywa na kutupwa katika giza la nje (Mathayo 25:14-30).
Hiyo ni kutufundisha kuwa hakuna hata mmoja wetu, ambaye hajapewa karama na Mungu, hivyo unapaswa ujiulize, je! Talanta yangu ninaitumiaje, Uwakili wangu ninautumiaje Je! Ni katika kuujenga ufalme wa Mungu, au katika mambo yangu mwenyewe.
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa waliokoka wote ni mawakili wa Kristo. Na hivyo Bwana anataka aone wakihudumu katika nyumba yake kwa uaminifu wote. Na ndivyo mitume wa Bwana walivyojiona mbele za Mungu.
1Wakorintho 4:1 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.
2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
Vifungu vingine ambavyo utakutana na neno hili ni hivi; Luka 16:1-13, 1Wakorintho 9:17, Waefeso 3:2, Wakolosai 1:25.
Bwana akubariki.
Swali ni je! Umeokoka? Kama sio unasubiri nini? Mpokee sasa Bwana Yesu ili akupe uzima wa milele bure. Kumbuka hizi ni siku za mwisho, Yesu yu mlangoni kurudi , akikukuta hujaitendea kazi talanta yako utamjibu nini, Na umeshaisikia injili?
Ikiwa upo tayari leo kumpokea Bwana, akusamehe dhambi zako, basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)
Tirshatha ni nini? (Ezra 2:63)
Beelzebuli ni nani? (Mathayo 12:24).
Swali: Je waliokufa kabla ya Bwana Yesu kuja (yaani watu wa agano la kale)wataokolewaje?.. kwamaana tunajua kupitia damu ya Yesu tu! ndio tunapata ukombozi wa hakika wa dhambi, sasa waliokuwa wanaishi katika agano la kale wataokolewaje na ilihali Kristo alikuwa hajafa bado, na damu iondoayo dhambi haijamwagika?.
Jibu: Ni kweli ukombozi unapatikana kupita damu ya Yesu tu!
Lakini ni vizuri kufahamu kuwa Agano jipya halikuja kulifanya agano la kale liwe uongo, badala yake limekuja kulikamilisha agano la kale, kama Bwana wetu Yesu alivyosema mwenyewe katika Mathayo 5:17..
Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza”
Sasa Ili tuelewe vizuri hebu tutafakari mfano ufuatao.
Taasisi moja imedahili wanafunzi wake walioingia kupitia mfumo wa makaratasi, kwamba mwanafunzi ili akubalike kujiunga na chuo hana budi kuwasilisha fomu zake katika ofisi ya taasisi hiyo…. Lakini mwaka mmoja baadaye ikabadili mfumo na kuanza kudahili wanafunzi wapya kupitia mfumo wa kieletroniki kwamba ili mwanafunzi akubalike kujiunga na taasisi hiyo hana budi kutumia mfumo wa kielekroniki hata akiwa nyumbani kupitia internet. Na kwamba hakuna mwanafunzi yeyote atakayeweza kupokelewa bila kutumia mfumo huo, kwani ni mrahisi na mwepesi katika kutunza kumbukumbu.
Sasa swali ni je! mfumo huo mpya ulioanza utawafanya wale wanafunzi wa zamani ambao walitumia mfumo wa zamani kuwa si wanafunzi halali tena wa taasisi hiyo?.. au itawafanya wale waliokwisha kuhitimu zamani, waliotumia mfumo wa zamani vyeti vyao kuwa batili?.
Jibu ni la!.. Wataendelea kuwa wanafunzi, isipokuwa watakaojiunga upya hawana budi kutumia mfumo mpya..kwasababu mfumo wa zamani utakuwa umeshabatilika!.
Kadhalika na Agano la kale ni hivyo hivyo…Ulikuwa ni mfumo wa zamani wa kuwasogeza watu karibu na Mungu, lakini ulikuwa na mapungufu mengi!.. Lakini muda ulipofika, ulikuja mfumo bora Zaidi na mwepesi na wa haraka ambao utamwingiza mtu katika ufalme wa Mungu kirahisi na kihakika zaidi, na huo ndio mfumo wa Agano jipya kupitia agano la damu ya Yesu Kristo, na si tena damu ya mafahali na kondoo..kama maandiko yanavyosema katika Waebrania 10:4.
Waebrania 10:4 “Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.”
Na hivyo kulifanya Agano la kwanza liwe chakavu na agano la pili liwe jipya sawasawa na Waebrania 8:13.
Waebrani 8:13 “Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”
Neno “kuukuu” maana yake ni “kuchakaa”… kwahiyo lilipokuja agano jipya, basi agano la kwanza likafanyika kuwa la kale, lisilotumika tena… hivyo kwasasa halifanyi kazi tena.
Kwahiyo waliokuwepo ndani ya Agano la kwanza kabla ya Bwana Yesu hao watahesabika kuwa watakatifu sawasawa tu waliopo sasa katika agano jipya leo, ndio maana akina Musa, Eliya, Henoko, Ibrahimu, Daudi, Danieli na wengineo wanatajwa kuwa miongoni mwa watakatifu, tena mashujaa wa Imani… ijapokuwa hawakubatizwa! Wala kumwona Masihi..
Lakini baada ya Bwana Yesu kuja na damu yake kumwagika basi wote watakaozaliwa baada ya hapo, hawana budi kulitumia agano jipya, na kuachana na lile la kale…na yeyote atakayejitumainisha kwa agano la kale basi hataweza kuokoka kabisa.
Hiyo ndio sababu kwanini tunapaswa tulijue sana Agano jipya na misingi yake, kwasababu tukianza kuwatanzama watu wa Agano la kale, pasipo kujua misingi ya agano jipya, tutajikuta tunachukua vitu visivyofaa kwa watati wa sasa….kwamfano tukimtazama Daudi na maisha yake na kanuni alizokuwa anatembelea si zote zitatufaa sisi watu wa agano jipya, kwamfano utasoma ijapokuwa Daudi aliupendeza Moyo wa Mungu sana lakini alikuwa na wake wengi na alikuwa na visasi na maadui zake.
Sasa tutachukua na kujifunza Imani ya Daudi, unyenyekevu wa Daudi na mengine mazuri, lakini hilo la kuoa wake wengi, Agano jipya inalikataza, hilo la kulipiza kisasi agano jipya limetuzuia..…hatuna budi kumsikiliza aliye mkuu Zaidi ya Daudi, na Sulemani, na Musa, na Eliya ambaye ni Yesu, anayetajwa kama Mjume wa Agano jipya (katika Waebrania 9:15 na Waebrania 12:24), ambaye anasema kila amwachaye mkewe na kuoa mwingine azini, na ndoa ni mke mmoja, mume mmoja..si Zaidi ya hapo!(Mathayo 19:4), ambaye amesema “tusilipe kisasi” (Mathayo 5:38-39). n.k
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
LITURJIA NI NINI? NA JE IPO KIMAANDIKO?.
Biblia ilimaanisha nini iliposema “Mwanamke atamlinda mwanamume” Yeremia 31:22?
Nini maana ya “Bwana Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa waliokufa?”(Ufunuo 1:5)
Jibu: Tusome,
Mwanzo 33:17 “Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi”.
Tafsiri ya neno “Sukothi” ni “Mahema”.. Hii ni lugha ya kiebrania.
Mahali hapa ni pale ambapo Yakobo alipiga kambi baada ya kutoka Padan-aramu, mji aliokuwepo Labani.(Mwanzo 28:1-2), na alikaa huko Padan-aramu kwa muda wa miaka 21, baada ya kulaghaiwa na Labani kwa muda wote huo.
Akiwa njiani baada ya kutoka kwa Labani alifika mahali ambapo ilimgharimu kutulia kidogo kisha andelee na safari, hivyo badala ya kujenga makazi ya kudumu, yeye akajenga mahema machache tu, kwasababu ya muda kwani bado alikuwa katika safari ya kuelekea Shekemu (Mwanzo 33:18). Hivyo Yakobo akaliita eneo hilo Sukothi kutokana na mahema hayo, na eneo hilo likaendelea kuitwa hivyo kwa vizazi vingi baadaye.
Na eneo la Sukothi kijeografia lipo maeneo ya nchi ya Yordani mpakani na Israeli.
Waamuzi 8:4 “Basi Gideoni akafika Yordani, akauvuka, yeye na hao watu mia tatu waliokuwa pamoja naye, walikuwa wamepungukiwa na nguvu, lakini wawafuatia vivyo.
5 Naye akawaambia watu wa Sukothi, Tafadhali wapeni mikate hao watu waniandamao; kwa maana wanapungukiwa na nguvu, nami ni katika kuwafuatia Zeba na Salmuna, wafalme wa Midiani”.
Kujua ni somo gani lingine tunalipata kuhusu Sukothi?…Fungua hapa >>TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Raheli aliwalilia vipi watoto wake?
Kwanini Labani aseme Yakobo ni Mfupa wake na nyama yake?(Mwanzo 29:14)
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
SWALI: Bwana Yesu asifiwe naomba kufahamu maana ya hili andiko;
1Wakorintho 14:20 “Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima”
JIBU: Kwa kawaida mtoto mchanga anakuwa kama mjinga, haelewi mambo mengi, anachofahamu ni kile tu kilichopo nyumbani, mambo mengine ya nje, hayajui, na ndicho kinachomfanya asijisumbue na hayo mengine, ambayo watu wazima wanayasumbukia,. Vivyo hivyo na Mungu anataka katika suala la uovu, tuwe hivyo. Kama wajinga, hatujui kinachoendelea, hatuna maarifa nayo, hatuwezi kuyaelewa. Na hiyo itatufanya tuwe salama.
Kwamfano ukiulizwa habari za nyimbo Fulani mpya za kidunia zilizotoka, huna taarifa nazo, Ukiulizwa habari za ligi za mipira, ni kama taarifa usizozielewa, ukisemeshwa na mambo ya kubeti, ni kama mtu anazungumza na wewe kwa lugha za mafumbo.
Ndio maana andiko hili linasema hivyo;
1Wakorintho 16:19b “…lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya”
Kutokujua kila kitu katika huu ulimwengu sio dhambi, na wala hilo halitakuzuia uishi vema. Hivyo tunapaswa tuchuje, ni nini kinatufaa na kipi kisichotufaa, Vile visivyotufaa tuviweke kando, tuwe watoto katika hivyo, lakini vile vitujengavyo, ambalo ni NENO LA MUNGU, basi tuwe watu wazima. Tulijue sana hilo kwasababu ndio uzima wetu ulipo.
Bwana akubariki
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia?
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13)
Nini maana ya msiwe waalimu wengi (Yakobo 1:3)?
Je biblia inatufundisha tuwe wapole kiasi? (Wagalatia 5:22-23)
Je biblia inatufundisha tuwe wapole kiasi? (Wagalatia 5:22-23)
SWALI: Nimesikia hili neni Rhema, likitajwa sana Kwa watumishi na sehemu mbalimbali, naomba nifahamishwe maana yake Nini, mbona silioni kwenye biblia?
JIBU: Ni vema kutambua kuwa Biblia, katika eneo la agano jipya sehemu kubwa imeandikwa kwa lugha ya kiyunani. Hivyo Kuna baadhi ya maandishi ambayo tukiyasoma katika lugha nyingine mfano kwenye yetu hii ya kiswahili, tunaweza kuona yalimaanisha jambo lile lile moja lakini tukirudi kwenye lugha ya asili ya kiyunani yalimaanisha maana zaidi ya Moja.
Kwamfano, tunapokutana na hili Neno “NENO”. kwenye tafsiri yetu ya kiswahili, Mahali pote limeandikwa hivyo hivyo tu “Neno” likimaanisha Neno la Mungu.
Lakini tukirudi kwenye lugha ya asili ya kiyunani zipo sehemu limelitajwa kama “Logos”na sehemu nyingine kama “Rhema”
Logos ikiwa na maana Neno la Mungu la Daima/ wazo la Mungu/mpango wa Mungu ulioandikwa na pia kama Yesu Kristo mwenyewe, ambaye ndio Neno lililofanyika mwili.
Lakini ‘Rhema’: maana yake ni “Neno lililosemwa na Mungu” . Ni neno la wakati husika, sio la daima.
Mfano wa maandiko yanayolitaja Neno kama Logos ni haya: Yohana 1:1-18, Yakobo 1:22, Waebrania 4:12. N.k
Na mfano wa maandiko yanayolitaja Neno la Mungu kama Rhema ni haya;
Mathayo 4:3-4
[3]Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. [4]Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Hapo Bwana aliposema, “ila Kwa Kila Neno litokalo katika kinywa Cha Bwana”..alimaanisha Neno lisemwalo na Bwana.. mfano wa Eliya alipomwambia yule mwanamke mjane, Bwana asema hivi; “lile pipa la unga halitapinguka, Wala Ile chupa ya mafuta haitaisha”. (1Wafalme 17:14). Halikuwa Neno ambalo lilitumika Kwa wakati wote, ambalo hata sasa tunaweza litumia sisi, Bali la wakati ule ule tu, amefunuliwa, akalisema na ikiwa hivyo.
Lakini ‘Rhema’ ni yaliyonenwa Kwa wakati huo tu..tofauti ya Yale yaliyokuwa Daima.
Neno lingine ambalo linasomeka kama Rhema katika biblia,. Ni wakati ule mitume wamehangaika usiku kucha kutafuta samaki, lakini kulipokucha Yesu akawaambia watweke.mpaka vilindini wakavue. Petro akasema maneno haya;
Luka 5:5
[5]Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
Aliliamini Neno lililosemwa na Bwana (na ikiwa vile).
Ili kuelewa vizuri tunaweza kusema “logos” ni BIBLIA TAKATIFU, na Rhema’ ni Neno mtu analofunuliwa Kwa kipindi Fulani.
JE! MUNGU ANASEMA NA SISI HATA SASA KAMA RHEMA?
Ni kweli Mungu ameshatupa njia yake kuu ya kusema na sisi, ambayo ni Kwa kupitia Biblia. Lakini pia bado Mungu anasema nasi, na kutushushia Neno lake Kwa wakati husikia litufae.
Tuwapo katika kanisa. Mungu hutumia karama mbalimbali, kusema nasi, au kutupa ujumbe wake. Anasema kutumia unabii au fundisho, au Neno la hekima, au maono, au ndoto, kutuwasilishia Neno lake.
Lakini pia ni lazima tujue kuwa Neno hilo lililofunuliwa ni sharti lisikinzane na Neno lake lililoandikwa. Vyote viwili vikichanganyikana huleta matokeo makamilifu na kutufanya tumwone Mungu katika uhalisia wake zaidi katika maisha yetu, kwasababu yeye Yu hai.
Lakini ipo hatari kubwa sana. Kwani katika siku hizi za mwisho wapo baadhi ya watu wanalichukua Neno liliokuwa kama Rhema, na kulifanya logos yao. Ndio hapo wanaposoma Bwana Yesu alitema mate chini akachanganya na udongo, akampaka mtu machoni akaona, hivyo na wenyewe wanafanya hivyo Kwa kisingizio kuwa andiko limeruhusu. Au wanapomsoma mtume Paulo anatoa leso yake, Kisha watu wanapona kupitia Ile, na wenyewe wanafanya hivyo hivyo, wakisema andiko limeruhusu. Hawajui kuwa ulikuwa ni ufunuo wa wakati ule ambao si agizo kuu, ni Rhema’.
Na madhara ya jambo hili ndio linageuka kuwa ibada ya sanamu. Tunayo mifano kadhaa katika biblia ya watu ambao waligeuza Rhema kuwa Logos, ikawapelekea kuingia katika laana. Kipindi Wana wa Israeli wakiwa jangwani, walipomkosea Mungu alimwagiza Musa aunde nyoka wa shaba, ili Kila amtazamaye apone. Na kweli ilikuwa vile. Lakini baada ya pale haikuwa sheria mama kama vile torati, kana kwamba waendelee kufanya vile. lakini tunaona baadhi ya watu walikuja kuifanya kama ndio sehemu Yao ya ibada ya uponyaji Kwa Mungu,.mpaka Mungu akachukizwa ikawapelekea kupelekwa tena utumwani Babeli, ikiwa kama mojawapo ya sababu.(2Wafalme 18:4)
Agizo letu la wakati wote ni JINA LA YESU TU! ndio logos yetu Bwana aliyotuagiza tutumie, wakati wote. Ikiwa hujafunuliwa kutumia kisaidizi/kiambatanishi kingine basi usifanye kwani huyo sio Mungu nyuma yake. Tegemea Biblia zaidi.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Shekina ni nini? Na Je! Utukufu wa shekina unamaana gani?
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
Miimo ni nini na kizingiti ni nini?
Maziara ni nini? Je! Na Tunaruhusiwa kuyajenga kwenye makaburi yetu?
Katika maandiko hakuna vifungu vya Moja Kwa Moja vinavyorekodi tukio la Bwana Yesu kunena Kwa lugha.
Lakini Kwa ufahamu wa Rohoni tuliopewa twajua kuwa ni wazi Yesu alinena Kwa lugha. Kutokurekodiwa Kwa tukio hilo hakumaanishi kuwa hakuwahi kunena Kwa lugha, kwasababu maandiko yanasema yapo mambo mengi aliyoyafanya Yesu kama yangeandikwa hata vitabu vyote duniani visingeweza kutosha, Kwa wingi wa habari zake.(Yohana 21:25)
Hivyo si Kila tukio la Bwana Yesu limeandikwa kwenye biblia.
Halikadhalika Ifahamike kuwa taaarifa za kunena Kwa lugha aliyezieleza kwa mara ya kwanza Kwa mitume ni Bwana Yesu.(Hawakufunuliwa baadaye) Hivyo hawezi kuwaambia watu jambo ambalo yeye mwenyewe halipo ndani yake, au hajawahi kulifanya.
Marko 16:17-18
[17]Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
[18]watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Vilevile Yesu ndiye mwanadamu pekee aliyetiwa mafuta mengi na Roho kuliko mtu yeyote aliyewahi kutokea duniani, (Waebrania 1:9). Zile karama zote za Roho zilikuwepo ndani yake, alikuwa ni nabii, mwalimu, mwinjilisti, mchungaji, mtume, n.k. na karama za uponyaji, miujiza, upambanuzi alikuwa nazo, hivyo hatuwezi kushangaa pia na hii kunena Kwa lugha kuwemo ndani yake.
Kwa kuhitimisha ni wazi kuwa Bwana Yesu alinena Kwa lugha. Hivyo akampendeza kukimwaga kipawa hicho na kwetu pia.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
IJUE FAIDA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA!
YEYE ATAWABATIZA KWA ROHO MTAKATIFU NA KWA MOTO.
Jibu: Jina la Bwana Yesu Kristo lisifiwe daima.
Matoleo ni Neno la ujumla linalomaanisha aidha sadaka, au michango.
Neno Matoleo linatokana na neno “Kutoa” Hivyo chochote kile mtu anachokitoa kwa Mungu wake kinaitwa Matoleo.
Lakini sadaka ni toleo rasmi ambalo linalenga moja kwa moja madhabahu, na matoleo ya sadaka tofauti na matoleo mengine kama michango ni kwamba sadaka inakuwa ni siri lakini michango mengine inaweza isiwe Siri,
Kwamfano yale matoleo Anania na Safira mkewe waliyoyatoa ya kuuza viwanja na kuleta thamani yake chini ya miguu ya mitume, hayakuwa siri, bali lilikuwa ni jambo linalowekwa wazi kwa wote.
Lakini sadaka haipaswi kuwa kitu cha kuonyesha mbele za watu, bali kinapaswa kiwe siri ya mtu na Mungu wake…kama Bwana wetu Yesu alivyotufundisha.
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Na Matoleo yote (iwe changizo au sadaka). Yana thawabu kubwa mbele za Mungu kama yakitolewa kwa nia njema na dhamiri njema na kulingana na Neno la Mungu,na Mungu anayaangalia sana.
Ukiahidi au ukipanga kumtolea Mungu kitu, basi hakiksha unatimiza kama ulivyoahidi au ulivyopanga pasipo kupunguza hata kidogo, ili isiwe kwako dhambi kama ilivyokuwa kwa Anania na Safira mkewe, ambao waimdanganya Roho Mtakatifu kwa matoleo yao.(Matendo 5:1-11).
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +25569303661
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
2 Petro 1:3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe
4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Uungu ni Ile Hali ya kuwa kama Mungu.
Kwamfano mtu anayefanya vitendo viovu kama vya uuaji, utoaji mimba, uchawi, ushoga tunasema anafanya “Ushetani”.. Kwasababu anatenda kazi za shetani.
Vivyo hivyo tunaposema “Uungu”. Tunamaanisha kuwa kama Mungu, au kufanya kazi kama za Mungu, au kuwa na sifa za Mungu ndani yako.
Na Tabia ya Mungu ndani ya Mtu. Si Kila mtu anazo. Bali ni wale tu waliozaliwa na yeye. Yaani waliokoka
Hizi ni baadhi ya Tabia za kiungu.
Kitu ambacho Mungu anawakiria watu wake waliompokea ni uzima wa milele. Ambao upo ndani yake. Mwanadamu wa Tabia ya asili Hana uzima wa milele ndani yake. Akifa Hana Tumaini la kuishi. Lakini aliyezaliwa mara ya pili. Huishi milele. Kwasababu uungu upo ndani yake.
Yohana 10:34 “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?”
Ukiwa kama mwana wa Mungu sifa hii ni lazima itaonekana ndani yako. Hakikisho la uzima wa milele, mwovu hana uzima wa milele.
Pili mtu mwenye uungu ndani yake, anatoa tabia za Mungu ndani yake, ndio zile tabia za Roho tunazozisoma katika Wagalatia 5:22, kama vile Upendo, , fadhili, uaminifu, utakatifu n.k.
Wagalatia 5:22-25
[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, [23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. [24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. [25]Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Mambo ambayo huwezi kuyaona kwa mtu mwenye tabia ya asili. Yeye huwa kinyume chake, au akijaribu kufanya basi ni kwa unafki, kwasababu havipo moyoni mwake.
Na pia mtu mwenye tabia ya uungu unakuwa na uwezo wa kuushinda ulimwengu(yaani dhambi) kama vile Kristo alivyoushinda ulimwengu..
1 Yohana 3:9
[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Maana yake,dhambi inakuwa haina nguvu ndani yake. Maandiko yanasema hata wao wenyewe wakishangaa tunawezaje kuishi maisha ya mbali na dhambi (1Petro 4:4). Hawajui Ni kwasababu sisi tuna tabia za uungu ndani yetu.
Maandiko mengine yanayoeleza Neno uungu. Ni haya (Matendo 17:29, Warumi 1:20).
Bwana akubariki.
Je! Na wewe utatamani uwe na tabia za Ki-Mungu ndani yako?. Ni wazi kuwa hii ni kiu ya kila mmoja wetu. Kama ni hivyo basi, hauwezi kwa akili yako au nguvu zako, bali kwa Roho wa Mungu. Kwasababu biblia inasema wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika wana wa Mungu (Yohana 1:12). Hivyo huu ni uwezo utokao kwa Mungu mwenyewe, na sio kwa mwanadamu. Na tunaupata kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kwa kumkiri Yesu, na kumfanya kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu. kisha kumpa nafasi ya kuyatawala maisha yetu.
Hivyo basi ikiwa upo tayari siku ya leo kutubu dhambi zako, ili Bwana akufanye kiumbe kipya. Basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa Sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Ni kosa gani alilolifanya Eli, ilihali aliwaonya watoto wake?
Dinari ilikuwa ni sarafu ya kirumi yenye thamani ya (utumishi wa kibarua wa siku nzima)..Kwamfano leo hii tuseme kibaru atalipwa kwa siku shilingi elfu 20, na ukawa ndio utaratibu wa nchi nzima, kuwalipa vibarua kiasi hiko kwa siku kama mshahara, basi kiasi hiko cha fedha kingekuwa na thamani sawa na Dinari kwa wakati huo.
Tutalithibitisha hilo Zaidi katika ule mfano Bwana alioutoa wakulima walioajiriwa katika shamba la mizabibu..
Mathayo 20:1 “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu
2 Naye alipokwisha kupatana na wakulima KUWAPA KUTWA DINARI, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu”.
Kwahiyo “ malipo ya utumishi wa kutwa nzima wa kibarua” ndiyo yaliyokuwa na uthamani wa “Dinari” na uzito wa sarafu ya Dirani ulikuwa ni “gramu 3.85”,
Kwa urefu kuhusiana na vipimo hivyo fungua hapa >>>VIPIMO VYA KIBIBLIA
Lakini tukirudi katika “Rupia”.. tunaisoma sehemu moja tu katika kitabu cha Ufunuo 6:6
Ufunuo 6:5 “Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
6 Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa NUSU RUPIA, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu RUPIA, wala usiyadhuru mafuta wala divai”.
“Rupia” ni sarafu nyingine yenye thamani sawa na “Dinari”.. ambayo ilikuwa inatumiwa zaidi namataifa mengine tofauti na Rumi (uthamani wake ulikuwa ni sawa na mshahara wa kibarua wa kutwa)… Na mpaka sasa bado baadhi ya mataifa yanatumia Rupia!.
Lakini ni somo gani tunalolipata kutoka katika thamani hii ya fedha (Dinari na Rupia)?
Somo kubwa tunalolipata si lingine Zaidi ya lile tunalolisoma katika Mathayo 20:1-16, kuwa thawabu za Mungu hazichunguziki.
Kwa urefu unaweza kusoma hapa >>KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?