Yearly Archive 2020

KUMTUMIKIA MUNGU, KUNAWEZA KUWE KINYUME NA MATARIJIO YAKO.

Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, Biblia inatuambia Neno lake ni kama fedha iliyosafishwa motoni mara saba,(Zab 12:6) ikiwa na maana kuwa Neno lile lile moja linaweza kuwa na mafunuo saba. Hivyo hatuchoki wala hatuachi kujifunza Neno lake kila inapoitwa leo. Na ndio maana biblia ni kitabu pekee kilichobaki duniani ambacho hakijawahi kupitwa na wakati.

Kuna jambo la muhimu sana, naamini tunaweza kujifunza kwa wale watu watatu waliopewa talanta na Bwana wao kwenda kuzizalisha. Tukisoma pale tunaona yule wa kwanza alipewa talanta 5, na kuwa uaminifu akafanikiwa kuzalisha nyingine tano, na yule wa pili alipewa talanta 2 na kwa uaminifu naye pia akaweza kuzalisha talanta nyingine mbili, Lakini yule wa tatu, ambaye hakuzalisha chochote,  kuna maneno aliyazungumza, ambayo yalifichua siri ya Bwana wake, jinsi alivyokuwa na hiyo ndio ikawa sababu kubwa ya yeye kutokwenda kuzalisha chochote.

Embu tusoma habari yake, kwa ufupi, na mbeleni kuna jambo geni ambalo Mungu atatufundisha leo.

Mathayo 25:24 “Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, BWANA, NALITAMBUA YA KUWA WEWE U MTU MGUMU, WAVUNA USIPOPANDA, WAKUSANYA USIPOTAWANYA;

25 BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO KATIKA ARDHI; TAZAMA, UNAYO ILIYO YAKO.

26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.

Sasa turudie tena huo mstari wa 24 anasema, nalitambua ya kuwa wewe ni mtu Mgumu.. Jiulize swali unadhani alikuwa anamsingizia Bwana wake kumwita mtu Mgumu? Hakuwa anamsingizia hata kidogo,alikuwa anazungumza kwa alichokiona kwa Bwana wake, ambaye alikuwa anamtumikia tangu siku nyingi…Tena akazidi kuendelea kumwambia, wewe huwa unavuna usipopanda, na unakusanya usipotawanya..Jiulize unadhani pia hapa alikuwa anamsingizia? Jibu ni la, nataka tusisimamie upande mmoja, embu tuangalie hoja za huyu mtumwa zilikuwa ni nini.

Kwa kauli zake ni kwamba alimwona huyu Bwana wake, ni mtu ambaye si mwepesi kuelewa,  hususani pale wanapokuwa kazini na mambo hayakuenda sawa siku hiyo, hata aelezejwe, ni mgumu sana kuelewa, akiambiwa kulikuwa na shida hii, ndio maana fedha haijapatikana ya kutosha, ni ngumu kuelewa, na ndio maana anasema Ninajua kuwa wewe ni mtu Mgumu.

Vilevile kulingana na maelezo yake, huyu Bwana wake ni mtu ambaye, anatarajia kupata vingi kutoka kwa wafanyakazi wake, licha ya kwamba, hawekezi vya kutosha, ni bwana ambaye hatimizi sana wajibu wake, kama tajiri, bali kazi yote anawaachia wafanyakazi wake,watumike na mwisho wa siku anataka mapato mengi kutoka kwao. Na ndio maaana akawa na ujasiri wa kumwambia Unavuna usipopanda..Yaani unatarajia upate mengi, mahali ambapo hujawekeza kwa vingi.

Sasa Kwa kauli zake hizi mbili, pengine ndio ikampelekea asikitendee kazi kile alichopewa na badala yake akakifukia chini

Lakini wakati yeye anafikiria hivyo, wakati yeye anaona Bwana wake hawajali wafanyakazi, huku nyuma wenzake wanaona hakuna haja ya kumfikiria Bwana wao vibaya, wakaenda kuvifanyia kazi vile walivyopewa. Hata kama kazi ilikuwa ni ngumu isiyo na vitendea kazi vingi lakini wao waliendelea kufanya hivyo hivyo tu.

Lakini huyu mmoja akasema mimi nitamuhifadhia fedha yake akirudi nimpe, nisipate lawama, kwasababu huyu boss wangu ninamjua , naweza kumzalishia kimoja tu, hapa, akaja kunikaripia ni kwanini sikumletea vingi, hivyo wacha nimwekee kilicho chake.akirudi akikute, niepukane na lawama.

Lakini kama tunavyosoma Bwana wake alipokuja na kumkuta hana faida yoyote alimwita mtumwa mbaya na mlegevu.. Kwanini asingeichukua na kuiweka kwa watoa riba, mahali ambapo hapana hatari ya kupata hasara, mpaka akaamua kwenda kuichimbia chini iozee huko.. ?

Mnyang’anyeni kile alichopewa wapewe wale wengine. Na akatupwe katika giza la nje. Ndiko kutakakokuwa na kilio na kusaga meno

Ndugu, mfano huu unatuhusu sisi, yaani mimi na wewe. Kazi ya Mungu leo hii tunaweza kuiona ni ngumu ya kuchosha, kinyume na matarajio yetu, mpaka inawapelekea  wengine kusema mpaka Mungu anipatie kwanza gari na nyumba ndio nitakwenda kumtumikia, mwingine anasema mpaka Mungu anipe fedha za kutosha ya kujenga kanisa ndio nitaanza kumtumikia kwasababu kazi ni yake na si yangu.

Ndugu yangu kama tunavisubiria tuvipate kwanza hivyo ndio tuanze ndo tumfanyie Mungu kitu tutasubiri sana, Kama tunangojea tuwezeshwe kwa vitu fulani vingi ndio tuseme leo tunajitoa kwa Mungu, hapo tusijidanganye, huo wakati hautafika. Kile ulichopewa na Mungu anzana nacho, na mbele ya safari Mungu atakufanikisha.

Wengine wanasema ngoja nipate pesa kidogo ya kuweza kumudu maisha yangu ndio nitaanza kumtolea Mungu, sadaka zangu. Kama mawazo yako yapo hivyo, ujue hicho kipindi kamwe hakitakaa kikufikie, utasubiri, utangoja, utamlilia Mungu akupe, kamwe hatakupa..Utoaji unaanzana na kile kimoja ulicho nacho, unakwenda kumtolea Mungu, Kama Mungu kakubariki kwa elfu mbili unamtolea elfu moja, hivyo hivyo, lakini ukisubiria upate vingi ndio upeleke kwa Mungu, sahau hilo jambo.

Ndivyo Kristo anavyofanya kazi hivyo, unaweza kumwona ni Bwana mgumu kweli, ambaye hawekezi vya kutosha kwanza kwa wafanya kazi wake, anawaacha wafanye kazi katika umaskini ..lakini hiyo ndio tabia yake. Unapaswa uielewe tu usonge mbele.

Leo hii utaona kama umetelekezwa lakini faida yake siku moja utaiona,  utatateseka, lakini thawabu yake ni kubwa kulinganisha na mateso yako ya leo. Embu tafakari wale aliowapa talanta tano aliwalipa nini baadaye, utaona aliwaambia wakatawale miji mitano, na wale wa mbili akawaambia wakatawale miji miwili. Unaona, faida kidogo tu inampelekea Bwana kukupa miji. Hivyo Mungu anayosababu kwanini atake umtumikie au umtolee katika hali hiyo uliyopo. Zipo thawabu nono zinatusubiria huko mbinguni

Hivyo na sisi tusianze kusema kazi ya Mungu ni ngumu, au kumtolea Mungu ni kugumu. Tufanye tu. Tusiwe watumwa walegevu na wabaya wenye sababu nyingi zisizojenga.

Bali tuwe kama wale wawili wa kwanza. Ili Kristo atakapouona uaminifu wetu, ndio atuongeze, na kutupa vingi zaidi kwa majira yake.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

THAWABU ZA SIRI, ZA WATAKATIFU MBINGUNI.

USIISHI BILA KUIFANYA KAZI YA MUNGU KABISA..

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Nini maana ya..“wakiwazuia watu wasioe” (1Timotheo 4:1)

KIFO CHA MTAKATIFU POLIKAPI (Policarp).

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya..“wakiwazuia watu wasioe” (1Timotheo 4:1)

Swali: Mtume Paulo anasema katika 1Timotheo 4:3, kwamba “wakiwazuia watu wasioe”. Alikuwa ana maana gani hasa?.

Jibu: Tusome

1Timotheo 4:1  “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2  kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”.

Ni kweli nyakati za Mwisho biblia imetabiri watu watajitenga na imani na “kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani”.. Na pia “watawazuia watu wasioe”

 Ukisoma hapo kwa makini utaona ni anasema “watawazuia watu wasioe” na sio “watawakataza”.. Kuwakataza ni tofauti na kuwazuia. Sasa Bwana Yesu alisema maneno haya..

Luka 11:52 “Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.”

Maana yake ni kwamba mtu anayegeuza maarifa ya Ufalme wa mbinguni, au anayeyapotosha, na kwenda kuwapotosha wengine, ni sawa na amewazuia watu hao kuingia katika ufalme wa mbinguni, kwasababu ameuondoa mlango wa maarifa.

Kwamfano mtu anayepotosha maarifa ya jinsi ya kuoa kibiblia na kumfanya yule mtu asioe kabisa au aoe kimakosa, hapo amemzuia mtu huyo kuoa.

Sasa Utauliza hilo jambo lipo leo?.. Mbona leo tunaona makanisani watu wanahubiriwa waje wapokee wachumba?..hatusikii watu wakizuiliwa kuoa?

Ndio jambo hilo lipo kwa sana, na limeenea duniani kote. Watu wengi sana wamezuiliwa kuoa/kuolewa pasipo wao wenyewe kujijua ingawa wapo katika mahusiano, au kile kinachoitwa ndoa. Kwasababu roho hii inatenda kazi kwa siri sana.

Kwamfano makanisa yanayofungisha ndoa za jinsia moja, na kuzibariki, na kusema ni ndoa takatifu. Watu wa namna hiyo, wanawazuia watu kuoa, kwasababu hiyo ndoa ya jinsia moja waliyoifungisha sio ndoa, bali ni kitu kingine. Hivyo mtu ataendelea kubaki katika hiyo ndoa ya kishetani akijua tayari kaoa, au kaolewa, kwasababu tu mchungaji wake kaidhinisha.. kumbe yupo katika laana, kwa kuzuiliwa kuoa/kuolewa inavyopaswa..

Pia leo hii kuna kundi kubwa la wanaume ambao hawajaoa (maana yake hawajafunga ndoa ya kikristo) lakini wanaishi na wanawake na kuzaa nao watoto na bado wanajiita wakristo, na wanahudhuria kanisani, wala hawaambiwi chochote katika kusanyiko walilopo, zaidi wanawekewa mikono na kubarikiwa ndoa yao hiyo batili, hawaambiwi chochote pengine kwasababu ni wachangiaji wakubwa hapo katika hilo kusanyiko. Hawa nao wamezuiliwa kuoa (yaani wamefungiwa mlango wa maarifa na viongozi wao wa dini). Kwasababu viongozi wao hao wanajua kabisa waasherati hawataurithi uzima wa milele lakini bado hawawafundishi au kuwakumbusha watu wanaowaongoza. Ambapo wangepaswa wawaambie na kuwakemea watubu, na wakafunge ndoa watoke katika hayo maisha ya uasherati wanayoishi.

Katika kanisa la kwanza, watu wa namna hiyo (wanaoishi pamoja huku hawajaoana) walikuwa wanatengwa kabisa, mpaka watakapotubu (na hiyo ni kwa faida ya roho zao)..lakini leo hii wanabarikiwa, jambo ambalo linahuzunisha sana.

Kadhalika yapo makanisa yanayofungisha ndoa za watu walioachana..Utakuta mwanamke kaachana na mumewe bila sababu yeyote, na kaenda kutafuta mwingine na anampeleka kanisani, kufungisha ndoa nyingine ya pili, na viongozi wengi pasipo kumhoji wala kufuatilia historia ya yule mtu kabla ya kuifungisha hiyo ndoa, wanafungisha hivyo hivyo tu, (ili pengine wasije wakamkwaza yule mshirika kipofu, kwasababu pengine ndiye mchangiaji mkubwa pale) bila kujua wamemzuia kuoa inavyopaswa kimaandiko yule mtu anayeoa, (wamemfungia mlango wa maarifa), na kumfanya aishi maisha ya uzinzi maisha yake yote.

Kwasababu huyo anayekwenda kumuuoa tayari ni mke wa mtu, hivyo anakwenda kufanya uzinzi..lakini kwasababu anaona hata mchungaji kakubaliana na hilo, na yeye dhamira yake inampa kibali kuoa kitu kilichoachwa, kwasababu mchungaji wake kakubali.. (Huyu naye kazuiliwa kuoa pasipo yeye kujijua)..Bwana Yesu alisema maneno yafuatayo.

Luka 16:18  “Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini”.

Pia yapo makusanyiko yanayofundisha na kufungisha ndoa za mitara (yaani za wake wengi). Utakuta kijana amefikia umri wa kuoa, na kwa dhamira njema anatafuta mtu wa kuoa, lakini anambiwa na kiongozi kwamba ni ruksa kuoa hata wake wawili, hivyo anakwenda kuoa wanawake wawili, na bila kujua kuwa alichofungishwa sio ndoa bali ni kitu kingine, na bila kujua kuwa tayari kashazuiliwa kuoa, kama maandiko yanavyosema.

Na pia watu wote wanaoishi na magirlfriend au maboyfriend na wanafanya uasherati, na wanahudhuria kusanyiko au kanisa ambalo viongozi wao hawawaambii ukweli, au basi wamezuiliwa kuoa, na pia kama wanaujua ukweli lakini hawataki kuoana lakini wanaendelea kudumu katika uasherati wao, hawa wamejizuia wenyewe kuoa/kuolewa, hivyo wasipotubu watahukumiwa, (Biblia inasema hivyo)

Waebrania 13:4  “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.

Hivyo hii roho inafanya kazi kwa nguvu sana nyakati hizi za Mwisho, na inawachukua wengi. Ni kwanamna gani mtu anaweza kujihadhari nayo?..Ni kwa kufanya mambo yafuatayo.

 1. Kwanza kwa kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, nguvu zako zote na akili zako zote.

Ukimpenda Mungu kwa viwango hivyo, itakufanya umtafute Mungu kwa bidii sana, itakufanya usiku na mchana utafute kulijua Neno lake kwa kulisoma na kulitafakari hiyo itakusaidia kujaa maarifa ya kutosha kumhusu Mungu, na hivyo kukufanya usiwe rahisi kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho ya uongo, mfano wa hayo ya ndoa za mitara, au za jinsia moja au za kuachana. Kwasababu utakuwa unalijua neno vizuri, hivyo hata mtu akija kukuambia Sulemani alioa wake wengi hivyo na wewe unaweza kuoa wake wengi, uwe unajua andiko la kuweza kuiangusha hiyo roho. Lakini kama Neno la Mungu halipo kwa wingi ndani yako, utahubiriwa mafundisho ya uongo nawe utaamini na kupotea. Na kujikuta upo kwenye mahusiano kumbe mbele za Mungu unazini na umeshazuiliwa kuoa kitambo sana.

2. Kwa kusali na kuomba kwa bidii.

Hizo ni silaha mbili kuu ambazo katika hizo ni ngumu kuchukuliwa na adui kwa vyovyote vile.

Bwana atubariki sote na kutusaidia.

Kama hujampokea Yesu, kumbuka siku zinaenda, na ile siku inazidi kukaribia, jiulize akirudi leo utakuwa wapi?

Marana atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Uchaji ni nini kama tunavyosoma katika 1Timotheo 2:10?

JE NI LAZIMA KUBADILISHA JINA BAADA YA KUOKOKA?

KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.

MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

Rudi nyumbani

Print this post

Ukoma wa nyumba ulifunua nini zamani?

Ukoma enzi za biblia ni ugonjwa uliojulikana kama pigo kuu kutoka kwa Mungu, kutokana na dhambi ambazo mtu alizozitenda.

Mtu aliyegundulika  kuwa ana ukoma ilikuwa anatengwa na jamii nzima ya Israeli. Anapelekwa mahali ambapo wakoma wenzake walipo, mbali kidogo na makazi ya kawaida ya watu na haruhusiwi kuja kujichanganya na watu wengine asije akawaambukiza wale wasio na ugonjwa huo. Hata familia yake mwenyewe hakuruhusiwa kuisogelea, aliendelea kukaa huko huko, mbali kwa kipindi chote ambacho Mungu atamponya, na kama ikitokea hata ponywa basi maisha yake yote atakuwa ametengwa. Walawi 13.

Lakini ukoma haukuwa tu katika mwili bali ulikuwa pia katika nyumba. Utajiuliza nyumba nazo zilipigwa na ukoma na Mungu? Jibu ni ndio biblia inatuambia hivyo;

Wana wa Israeli walipokuwa jangwani Mungu aliwaagiza, akawaambia watakapoifikia hiyo nchi ya ahadi, na kukutana na nyumba ambayo Mungu kaipiga kwa ukoma, wasiikae, wasubiri  kwanza kwa muda wa siku saba, kisha kuhani atakwenda kuingalia, na akiona ukoma ule, umeisha ndipo watakaporuhusiwa kukaa, lakini kama bado upo itakarabatiwa pale palipoathirika, na hapo watasubiri tena, kuangalia, ikiwa umeisha basi watu wataruhusiwa kuingia, lakini kama bado, kinyume chake ugonjwa ndio umezidi tu kutapakaa nyumba nzima..Basi nyumba hiyo yote ilikuwa inabomolewa na kila kitu chake kilikwenda kutupwa nje ya mji.

Walawi 14:33 “Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

34 Hapo mtakapoingia nchi ya Kanaani, ambayo nawapa kuwa ni milki yenu, nami nitakapolitia pigo la ukoma katika nyumba ya nchi hiyo ya milki yenu;

35 ndipo mwenye nyumba hiyo atakwenda na kumwambia kuhani, akisema, Naona mimi ya kwamba pana kama pigo katika nyumba yangu;

36 ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, mbele ya kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili kwamba vyote vilivyomo nyumbani visiwekwe kuwa unajisi; kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aitazame;

37 naye ataliangalia hilo pigo, na tazama, likiwa pigo limo ndani ya kuta za nyumba, nalo lina mashimo-mashimo, rangi ya majani, au mekundu, na kuonekana kuingia ndani kuliko huo ukuta;

38 ndipo kuhani atatoka katika nyumba hiyo mpaka mlangoni pa nyumba, na kuifunga hiyo nyumba muda wa siku saba;

39 siku ya saba kuhani atakwenda tena, naye ataangalia; na tazama, likiwa pigo limeenea katika kuta za nyumba;

40 ndipo kuhani atawaambia wayatoe hayo mawe, yaliyo na pigo, na kuyatupa mahali penye uchafu nje ya mji;

41 naye atafanya kwamba hiyo nyumba ikwanguwe ndani pande zote, na chokaa watakayokwangua wataimwaga nje ya mji mahali palipo na uchafu;

42 kisha watatwaa mawe mengine, na kuyatia mahali pa mawe hayo; naye atatwaa chokaa nyingine, na kuipaka chokaa hiyo nyumba.

43 Na kama hilo pigo likirudi tena, na kutokea ndani ya nyumba, baada ya yeye kuyatoa hayo mawe, na baada ya kuikwangua nyumba, na baada ya kupakwa chokaa,

44 ndipo kuhani ataingia ndani na kuangalia, na tazama, likiwa pigo limeenea ndani ya hiyo nyumba, ni ukoma unaokula hiyo nyumba; ni katika unajisi.

45 Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hata mahali palipo na uchafu.

Ukoma wa nyumba ulifunua nini zamani?

Sasa ni kwanini Mungu aitazame mpaka nyumba na kuipiga kwa ukoma? Kwa wakati ule zipo nyumba ambazo zilijengwa katika damu, nyingine katika dhuluma, nyingine rushwa, wizi, nyingine uzinzi n.k. Sasa nyumba kama hizi, Mungu hakuruhusu watoto wake, wazikae na ndio maana akazipiga kwa ukoma.

Hiyo inatufundisha nini sisi wa agano jipya?

Biblia inatuambia miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, ni nyumba za Mungu. Sasa pale anapotaka kushuka halafu anakutana na vimelea vya ukoma wa kiroho, tunachokisubiria ni nini kama sio kuharibiwa? Anakuja na kukutana na ulevi, uzinzi, uvutaji sigara, ni nini mtu huyo anatarajia kama sio kuuliwa na Mungu.

Anapokuja na kukutana na ushirikina, fitina, utazamaji wa picha za ngono, anakutana na uvaaji wa suruali kwa mwanamke, na nguo za kikahaba, na uchubuaji ngozi, ni nini anakingojea hapo kama sio kuharibiwa?

Kuna watu wanasema Mungu haangalii mwili bali roho, nataka nikuambie mwili wako unathamani kubwa kwa kama tu vile roho yako ilivyo, na usipoangalia na kuutunza utapigwa tu na Mungu, Kama aliweza kuzipiga nyumba ambazo hazina uhai wowote zamani, atashindwaje kuupiga mwili wako ulio na uhai ndani yake.

1Wakorintho 3:17 “Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Kama vile nyumba inavyopewa siku saba za kuangaliwa maendeleo yake, kama ukoma utaondoka au utaendelea, vivyo hivyo, na wewe ambaye unaliharibu hekalu la Mungu, usipumbazike kuona mbona hakuna hatua yoyote Mungu anayoichukua juu yangu. Upo wakati Mungu atasema sasa inatosha, mtu huyu hana faida yoyote kwangu, nimwondoe, tu… Anaweza asikuue kimwili, lakini rohoni ukawa mfu aliyeoza anayesubiria tu kufa kwenda kuzimu.

Mungu anatazamia tumzalie matunda katika miili yetu, vinginevyo atatung’oa  mara moja, kwasababu kukaa bila kumzalia matunda anatuona kama TUNAMUHARIBIA TU NCHI YAKE.

Luka 13:7 “Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?”

Hivyo, tubu mrudie Mungu, hizi ni nyakati za kumalizia, Kristo yupo mlangoni kurudi. Ulimwengu haujawahi kukutimizia furaha ya roho yako. Ni Kristo tu peke yake ndiye anayeweza kukupumzisha na kukuponya.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

DANIELI: Mlango wa 12.

“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?

Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?

Rudi nyumbani:

Print this post

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

Zamani  enzi za biblia  Njia kuu ya mfalme, ilikuwa ni njia iliyotengenezwa mahususi kuunganisha mataifa mengi na miji mingi, na lengo lilikuwa ni kurahisisha shughuli za kibiashara na usafirishaji katikati ya mataifa hayo wana chama., njia hiyo ilitoka Misri, na  kupita Yordani, na moja kwa moja mpaka Nchi ya Syria, ..Ilikuwa ni maarufu kwa mataifa mengi sana zamani zile,

Hivyo Safari katika barabara hii ilikuwa ni uhakika kwasababu vizuizi vyote vya  barabarani vilidhibitiwa, palipokuwa na mito paliwekwa madaraja, palipokuwa na mabonde palisawazishwa, hivyo mtu yeyote aliyesafiri kwa njia hii safari yake ilikuwa ni ya uhakika na ya kuchukua muda mfupi sana kulinganisha na mtu aliyesafiri kupitia njia nyingine.

Kama tu vile leo hii tunavyoiona ile  “barabara kuu ya kaskazini”  almaarufu kama (The great north Road) ambayo inatoka Cape town kule Afrika ya kusini na kwenda moja kwa moja mpaka  Cairo Misri Afrika ya kaskazini.  Barabara hii imekatiza pia katika nchi ya Tanzania Dodoma-babati  na nchi ya  Kenya.  Na lengo la kuwekwa barabara hii ni sababu zilezile za kibiashara na kimaendeleo. Hivyo mtu akitaka kusafiri kutoka Kaskazini mwa Afrika kwenda Kusini, kwa miguu au kwa gari akipitia barabarani hii, basi safari  ni ya uhakika, na salama bila kukutana na kipingamizi chochote njiani.

Sasa Tukirudi katika biblia wakati wana wa Israeli walipokuwa jangwani wakiendelea katika safari yao kuelekea nchi ya ahadi, tunaona walipita katika na mji wa Edomu,(kwa sasa ni kusini mwa Yordani) walipofika katika taifa lile wakawaomba wapite katikati yao kuifauata sasa hii njia kuu ya mfalme.. Lakini kama tunavyosoma Waedomi, waliwakatalia, wakawatishia kupigana nao, hivyo ikawabidi wana wa Israeli wapitie njia nyingine ndefu zaidi ili kuwazunguka waendelee na safari yao.

Hesabu 20:17 “tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; TUTAIFUATA NJIA KUU YA MFALME, tusigeuke kwenda upande wa kuume, wala upande wa kushoto, hata tutakapopita mpaka wako.

18 Edomu akamwambia, Hutapita katika nchi yangu, nisije nikakutokea kupigana nawe kwa upanga.

19 Wana wa Israeli wakamwambia, Tutakwea kwa njia kuu; tena kama tukinywa maji yako, mimi na wanyama wangu wa mifugo, ndipo nitakulipa thamani yake; nipe ruhusa nipite kwa miguu yangu wala sitaki neno lingine lo lote.

20 Akamwambia, Hutapita katika nchi yangu. Kisha Edomu akamtokea ili kupigana naye, na watu wengi, na kwa mkono wa nguvu.

21 Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hivyo Israeli akageuka na kumwacha.

22 Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima, wakafikilia mlima wa Hori”.

Tunaona tena walipofika mbele tena kidogo, walikutana na watu wa taifa lingine walioitwa Waamori, na wao pia wakawaomba wapite  kuifuata hiyo  njia kuu ya mfalme, wakiahidi kuwa hawatachukua chochote au kuleta dhara lolote katika nchi yao,. Lakini mfalme wa Waamori akawakatalia na zaidi ya yote akapanga vita kupigana nao, lakini walipigwa na kutekwa nyara mji wao wote.

Hesabu 21:22 “Nipe ruhusa nipite katika nchi yako; hatutageuka kando kwenda mashambani, wala kuingia katika mashamba ya mizabibu hatutakunywa maji ya visimani; TUTAKWENDA KWA NJIA KUU YA MFALME, hata tutakapokuwa tumepita mpaka wako.

23 Lakini Sihoni hakukubali kumwacha Israeli kupita katika mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, akatoka aende kupigana na Israeli jangwani, akafika mpaka Yahasa; akapigana na Israeli.

24 Israeli wakampiga kwa makali ya upanga, na kuimiliki nchi yake, tangu mto wa Arnoni hata mto wa Yaboki, mpaka nchi ya wana wa Amoni; kwa kuwa mpaka wa wana wa Amoni ulikuwa una nguvu”.

Unaona? Unaweza ukajiuliza swali moja, pamoja na kwamba walikuwa wanafukuzwa lakini hawakuchoka kuitafuta njia kuu ya mfalme? Hiyo yote Ni kwasababu walijua urahisi na wepesi uliopo kwa kuifuata njia ile, hajalishi kuwa maadui wengi kiasi gani walisimama katikati yao kuwazuia. Waliitafuta kwa bidii hii njia kuu ya mfalme.

Tunapata fundisho gani?

Kumbuka Agano la kale ni kivuli cha mambo yanayoendelea katika agano jipya.

Hata sasa ipo njia kuu ya mfalme mmoja ambayo inaunganisha dunia na mbingu. Kaisi kwamba mtu akiifuata njia hiyo, uhakika kwa kufika mbinguni upo bila vizuizi vyovyote hapa katikati kwani, tayari imeshatengenezwa, na hukakikishwa. Na njia yenyewe ni YESU KRISTO.

Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, MIMI NDIMI NJIA, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.

Hakuna njia nyingine yoyote ya kando kando itakayokufikisha mbinguni ikiwa utaikataa hii ya Yesu Kristo, mtu yeyote anayejiita mtume hawezi kukufikisha mbinguni, dini yoyote haiwezi kukufikisha mbinguni, wala raisi, au kiongozi yoyote ya kiimani, anayeweza kukufikisha mbinguni. Ni Yesu tu peke yake, Ukimwamini yeye, ukamtii na ukamfuata, uhakika wa kumuona Mungu ni asilimia zote. Hivyo mkaribishe leo maishani mwako uanze kupita juu ya njia hii kuu moja ya uhakika. Nyingine zote zitakupoteza ndugu yangu.

Utatumia gharama kubwa, utatoa jasho jingi, lakini mwisho wa siku utapotea. Kwasababu safari hii ya hapa duniani ni ndefu, yenye mabonde mengi, na milima mingi, yenye utelezi mwingi, na miiba mingi njiani, hivyo utahitaji NJJIA moja tu ya uhakika ya iliyounganika bila kukatika katika ili kukufikisha kule ng’ambo na hiyo ni Yesu tu peke yake.

HUO NDIO UKWELI PEKEE ULIODUMU DUNIANI KWA WAKATI WOTE.

Hivyo Ikiwa utapenda kumpa Yesu leo maisha yako, basi fungua hapa kwa maelekezo ya sala ya Toba >>> SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?

MAMA UNALILIA NINI?

JIFUNZE KUTOA KATIKA HAZINA YAKO VITU VIPYA NA VYA KALE.

Rudi nyumbani

Print this post

Mbari ni nini kibiblia?

Neno hili linatwa mara nyingi sana katika biblia, sana sana mahali ambavyo vinatajwa vizazi vya wana wa Israeli.

Mbari, kwa jina lingine ni UKOO. Kwamfano unaweza kukutana na  sehemu fulani inasema, “hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao”. Hapo inamaanisha kuwa “hao ndio wakuu wa ukoo wa baba zao”,

Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo;

1Wafalme 8:1 “Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni”.

1Nyakati 7:4 “Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi”.

1Nyakati 8:28 “Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu”.

1Nyakati 9:33 “Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku”.

1Nyakati 26:13 “Nao wakatupiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo sawasawa na wakubwa, kwa kadiri ya mbari za baba zao”.

Luka 1:26 “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,

27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, WA MBARI YA DAUDI; na jina lake bikira huyo ni Mariamu”.

Soma pia Nehemia 10:34, 11:13

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?

Rudi nyumbani:

Print this post

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndio cha kweli cha roho zetu.

Kawaida ya Mungu ni huwa hatoi agizo juu ya agizo. Yaani kwa mfano leo akikupa agizo fulani ulitelekeze, haundi agizo lingine juu yake kulibatilisha hilo la kwanza, Atafanya hivyo endapo tu lile la kwanza litakuwa limeisha muda wake.

Mara nyingi tunakuwa tukiacha yale maagizo ya kwanza ya Mungu, na hiyo inatupelekea aidha kukutana na hukumu yake, au kushindwa kutekeleza mipango yetu  kwa wakati.

Kwamfano utakutana na nabii mmoja katika biblia enzi za wafalme, ambaye alipewa maagizo na Mungu ya kwenda kumtolea unabii Mfalme mwasi Yeroboamu, akaambiwa akishamaliza kazi yake asile wala asinywe chochote katika mji huo, wala asilale au kupumzika na njia atakayoipita asiirudie tena hiyo hiyo. Lakini huyu nabii alipomaliza kweli kazi ya huduma alianza safari ya kuondoka. Lakini akiwa njiani alikutana na nabii mwingine mzee, akamshurutisha, aende kulala nyumbani kwake. Lakini yeye akamwambia Bwana amenionya nisikae mahali popote kwenye mji huu.

Sasa yule nabii mzee alipoona kuwa kijana huyu hataki, akamtungia habari za uongo na kumwambia, Bwana ameniambia ameghahiri, mpango wake, hivyo anataka uje ule upumzike nyumbani kwangu. Na yule kijana pasipo kufikiria ni kwanini Mungu awe kigeugeu, saa hiyo hiyo akamwamini, kwasababu  tu ni nabii mwenzake tena mzee, anauzoefu wa mambo ya kinabii, akaenda kukaa kwake.  Kitu kilichomtokea hatuna haja ya kueleza, sote tunajua alikuja kuliwa na simba, kwa kuyaasi maagizo ya Mungu (Soma 1Wafalme 13)

Tunamwona Mtu mwingine anaitwa, Balaamu, naye pia mwanzoni Mungu alimuonya asiende kuwalaani Israeli, lakini baadaye akawa analazimisha mawazo yake kwa Mungu, kilichofuata ilikuwa ni Mungu kumwambia haya nenda nitakuwa pamoja nawe..kumbe hakujua tayari njia Mungu alikuwa ameshamuandalia malaika wake amuue, na kama sio yule punda kumsaidia habari yake tusingeisoma leo hii kwenye biblia (Soma Hesabu 22).

Hiyo yote ni kutozingatia agizo la kwanza Mungu alilokupa, Siku zote agizo linalokuja juu ya agizo lile la mwanzo huwa halitokani na Mungu.

Tukisoma tena habari nyingine maarufu katika biblia ile ya Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka  Babeli utumwani, baada ya kukaa kule miaka 70. Biblia inatuambia Mungu alimuamsha moyo mfalme Koreshi wa uajemi, ili atoe amri kuwa watu wote waondoke kwenye makoloni yake, waende Yerusalemu kumjengea Mungu nyumba, kufuatana na unabii uliotolewa na Yeremia zamani.

Tunaona baada ya hapo Mfalme aliwapa zawadi nyingi sana, Hivyo waliondoka kwa moyo mkunjufu  wakijua kabisa Mungu kaitimiza ahadi yake ya kwenda kumjengea nyumba Yerusalemu. Lakini walipofika kule na kuanza kutia msingi wa nyumba ya Mungu, maadui zao wakaanza kunyanyuka hilo likawadhoofisha, na kama hiyo haitoshi wakaandika waraka wa uchongezi wakampelekea mfalme mwingine wa uajemi ambaye alikuja kutawala baada ya Koreshi, aliyeitwa Dario,  mfalme alipousoma, akatoa amri nyingine, kuwa usiendelee ujenzi wowote Yerusalemu, wa nyumba ya Bwana. Na mtu yeyote atakayefanya vile ilikuwa ni kifo.

Wayahudi waliposikia, juu waraka huo mpya, wote wakavunjika moyo, wakaacha kuijenga nyumba ya Mungu ambayo ilikuwa tayari katika hatua nzuri, Hivyo ikapelekea nyumba hiyo kubakia hivyo hivyo kwa muda wa miaka mingi sana..Kila mtu akarudi kuendelea na shughuli zake kila siku.

Wakasau kuwa ni Mungu ndiye aliyewapa maagizo kuwa wakamjengee nyumba yeye, hawakujiuliza sasa haya maagizo mengine yanatoka wapi?

Mpaka baadaye sana, tunaona manabii wawili yaani Hagai na Zekaria wanatokea, wanawatabiria na kuwauliza kwanini mnaacha kujenga nyumba ya Mungu, wakidai kuwa huu sio wakati wa kumjengea Mungu? Kwa muda wako soma kitabu chote cha Hagai utaona mambo hayo.

Unaona, walisikiliza sauti ya pili, wakaicha ile ya kwanza, na hiyo ikawapelekea kucheleweshwa kwa huduma yao waliyokuwa wameshaianza,.. Siku zote sauti ya pili ni ya shetani, na sio ya Mungu.

Vilevile katika agano jipya kuna agizo ambalo tayari Mungu alishatupa.

Marko 16:15-16 Inasema..

“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Hili ni agizo ambalo Kristo alishatoa kibali, kufanya.. Lakini dunia ya sasa shetani ameshaiingilia, kiasi kwamba, sehemu nyingine watu hawaruhusiwi kuhubiri kabisa, sheria za nchi zao zimekataza..Sasa wewe kama mkristo ukiogopa sheria ya wanadamu, ukasema pengine huu sio wakati wa kufanya hivyo, ujue kuwa utafanana na wana wa Israeli walipokuwa wanalijenga hekalu la pili, utasubiria wee, na kamwe hiyo siku ambayo unayoina itafaa haitafika, Mungu atakachofanya ni kukumbusha tu, uliacha agizo la kwanza.

Sio hilo tu yapo maagizo mengine madogo madogo, yanakubana kiasi kwamba yanakufanya ushindwe hata kuiendeleza kazi ya Mungu, mpaka uwe na hiki au kile, au ukamilishe hiki au kile..Hayo yote hatupaswi kuyazingatia sana, mengine yana agenda ya shetani nyuma yake kukumwisha tu, bali tuzingatie lile agizo kuu la mwanzo ambalo Kristo ametupa enendeni ulimwenguni kote.

Mwingine atasema familia yangu iko hvi au vile..hupaswi kuangalia hayo yote

Safari ya imani, si mteremko muda wote, kuna wakati itasumbuliwa na mambo mengi, lakini hatupaswi kuyaogopa kwasababu Mungu ameshaahidi atakuwa na sisi katika hayo yote. Kama tu vile alivyokuwa kwa mababa zetu katika mapito yao.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:

Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?

BWANA AYAGANGE NA MACHO YETU PIA.

Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?

KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?

SWALI: Biblia inamaanisha nini inaposema “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?(Yuda 1:23)


JIBU: Maneno hayo utayasoma katika vifungu hivi;

 Yuda 1:22 “Wahurumieni wengine walio na shaka,

23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, MKILICHUKIA HATA VAZI LILILOTIWA UCHAFU NA MWILI.

24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu”;

Kama tunavyosoma vifungu hivyo, vinaeleza wajibu wa kila aliyeokoka katika kuwavuta wengine katika Imani. Mtume Yuda anaeleza yapo makundi mbalimbali ya watu waonaopaswa kuokolewa, lipo kundi la watu  ambalo linapaswa lihurumiwe kwa hofu, yaani lichukuliwe katika uchanga, na utulivu, livutwe kwa upendo wa Mungu tokea mbali, kundi hili ni la watu wote ambao hawamjui Mungu, wanaoishi duniani leo hii. Walevi, wezi, wazinzi, waoabudu sanamu, n.k.

Lakini lipo kundi lingine linalopaswa kuokolewa kwa kunyakuliwa katika moto. Unajua mpaka mtu awe  ndani ya moto, huhitaji kumbembeleza bembeleza, ili kumtoa, unachopaswa kufanya ni kumnyakua  tu atoke kule kwa gharama zozote zile, kwasababu akiendelea kubaki kule muda si mrefu atakufa. wapo watu ambao unaona kabisa wanakwenda kuangamia kwa mienendo yao ya dhambi, wapo wengine unaona kabisa wapo katika dakika za mwisho wamalizie mwendo wao hapa duniani, na bado hawajaokoka, wapo watu ambao wameshakata tamaa kiasi cha kwamba kilichobakia kwao ni kujiua tu siku yoyote, wapo watu ambao wamefungwa katika minyororo na mateso ya ibilisi, wao wenyewe hawawezi tena kufanya chochote juu ya maisha yao , n.k. Sasa watu kama hawa wanapaswa waokolewe kwa nguvu ya ziada. Kwa kuwafungua na kuwaombea sana, na kuwafuatialia kwa ukaribu sana, na wengine kwa kuwahubiria injili ya Jehanamu ili wajue huko wanapoelekea ni wapi, waogope wageuke kabla kifo hakijawakuta..

Sasa katika kazi hiyo yote ya uokoaji, mwandishi anasema.. “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”. Yaani kujilinda nafsi zenu, na nyinyi msije mkachukuliwa katika dhambi zao. Na ndio maana hapo anatumia mfano wa vazi lililotiwa unajisi kwa uchafu. Katika agano la kale vazi lililotiwa unajisi ni vazi lililovaliwa na mtu mwenye ukoma. Ambalo lilikuwa ni rahisi kumuambikaza mtu mwingine ukoma huo endapo atalishika au kulivaa.  Yaani kwa ufupi Nguo zote zilizokuwa zinatiwa unajisi wa aina yoyote ile, uwe ni ule unaotoka mwilini au vyovyote vile uliweza kumtia unajisi hata mtu mwingine asiyestahili endapo tu atazigusa au kuzivaa. (Walawi 21:11, Hesabu 6:6).

Yapo matendo ambayo, ni rahisi kutiwa na watu wengine unajisi kwayo, unapokwenda kumubuhiria mzinzi, hakikisha na wewe huna uzinzi ndani yako, unapokwenda kumuhubiria mlevi hakikisha na wewe vimelea vya ulevi havipo ndani yako, vivyo hivyo na kila mtu unayekwenda kumshuhudia.  Unapaswa ujichunge wewe mwenyewe kwanza. Kwasababu shetani naye anatenda kazi.

Wagalatia 6:1” Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, UKIJIANGALIA NAFSI YAKO USIJE UKAJARIBIWA WEWE MWENYEWE”.

Hiyo ndio maana ya kulichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?

MAMA UNALILIA NINI?

Je mtu anayeua anabeba dhambi zote za yule aliyemuua?

Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?

Rudi nyumbani

Print this post

Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?

Jibu: Tusome.

Danieli 9:21 “naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni”.

Kurushwa upesi kunakozungumziwa hapo ni “kuruka kwa haraka” au kwa lugha rahisi zaidi ni “kuruka/kupaa kwa spidi”. Ndege wa angani huruka kwa upesi..Kwa mfano ni rahisi kumsogelea ndege kama njiwa, na akikuona tu, mara ghafla utamwona kapiga mbawa na kupotelea kwenye ukingo wa anga. Hiyo ndiyo maana ya kuruka kwa upesi.

Na Biblia inasema hapo Danieli alimwona Malaika Gabrieli akirushwa kwa upesi na Mungu..  Maana yake alikuwa anamwona katika maono, akija kwa kasi, na akiondoka kwa kasi.

Kumbuka wapo malaika wenye mbawa na wasio na mbawa (maana yake wasioruka)..Gabrieli ni miongoni mwa malaika wenye mbawa, na wa kupeleka ujumbe kwa watu.

Ni kawaida kile kitu kinachopeleka ujumbe kwa haraka sana ni bora kuliko kile kinachopeleka kwa taratibu. Hivyo Gabrieli ni malaika mwenye sifa ya kupeleka ujumbe kwa haraka sana

Malaika Gabrieli ameonekana katika agano la kale na vile vile katika agano jipya. Katika agano la kale, ndio hichi kipindi cha Nabii Danieli alipotumwa ampe ujumbe juu ya mambo yanayokuja.

Na katika Agano jipya alionekana kipindi cha Kuhani Zakaria, Baba yake Yohana Mbatizaji, alipotumwa na Mungu ampe ujumbe kuhusu kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji ambaye atatangulia kumtengenezea Bwana njia (Soma Luka 1:19). Na pia kipindi kifupi baadaya akaja kuonekana tena kwa Bikira Mariamu kumpa ujumbe wa kubeba mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Unaweza kusoma Luka 1:26).

Na hata leo Malaika Gabrieli anatumwa kwa watu wengi duniani walio waaminifu kwa Mungu kuwapa jumbe mbalimbali.

Kama utapenda kujua zaidi kuhusu Malaika unaweza kufungua hapa >> Malaika

Je umempokea Kristo?. Yesu anarudi.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Je! Kuna malaika wangapi mbinguni?

MALAIKA WAPELELEZI WA HUKUMU WANAPITA SASA.

Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?

Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?

Rudi nyumbani

Print this post

MAMA UNALILIA NINI?

Leo tutajifunza jinsi gani matatizo yetu yanavyoweza kuweza kutupofusha hata tusiione miujiza yetu.

Kuna wakati Mungu, anakuwa ameshakwisha anza tayari kututendea miujiza, lakini kutokana na kuwa tunayapa sana matatizo yetu uzito mkubwa kuliko yanavyostahili, inatupelekea hata miujiza yenyewe tuiione kama si kitu pale inapoanza kuja.

Embu fikiria wakati Kristo alipokufa na kulazwa pale makaburini, tunaona kuna mambo mengi yalikuwa yanaendelea pale, lakini kikubwa ambacho tunaweza kujifunza leo ni lile tukio la Mariamu Magdalene. Yeye alipofika pale alianza kulia kwa uchungu, akifikiria miujiza yote aliyotendewa na Yesu tangu akiwa duniani, akifikiria jinsi alivyoishi maisha ya haki na upendo usiokuwa na unafiki, wala hakufanya kosa lolote, na leo hii, anaona wamemuua, tena afadhali ingekuwa wamemuua na kumsulubisha tu, na kumwacha, lakini safari  hii wameuiba  mpaka na mwili wake pia, hilo ndio lililomfanya alie sana kwa uchungu, kiasi cha kumfanya ashindwe kuondoka pale aendelee tu kulia,

 Lakini biblia inatuambia muda si muda, akiwa amesimama pale anachungulia ndani ya kaburi ghafla aliwaona malaika wawili, wamekaa, mmoja kichwani pa mahali walipomlazia Yesu na mwingine, miguuni..Lakini wale malaika wawili wakamuuliza swali, Mama unalilia nini?

Yohana  20:11 “Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.

13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka”.

Fikiria, ule uchungu wa mawazo ulimfanya hata asahau kuwa wale ni malaika wa Mungu, Uchungu wa kuibiwa kwa Bwana kulimfanya hata asifikirie wale watu wawili wenye mavazi yaliyong’aa meupe wametokea wapi muda ule, na wanafanya nini pale..Yeye moja kwa moja anaanza kuzungumza nao kama vile, ni watu wa kawaida anaokutana nao barabarani siku zote.

Kama hilo halitoshi, wakati anaendelea kulia pal, nje, akamwona Tena mtu mwingine anatembea tembea karibu yake,(hakujua kama ndiye Yesu) ndipo Yesu akamuuliza swali lile lile aliloulizwa na wale malaika..Mama unalilia nini?..

Yohana 20:15 “Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.

16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu)”.

Unaona, Yesu alipogeuka na kumshtua MARIAMU!!!..Ndipo akabutuka na kugundua kuwa Yule ni Yesu aliyesimama mbele yake.  Kama asingeshtuliwa, bado angeendelea kukaa katika majonzi yake tu, analia lia ovyo wakati Yesu anazungumza na yeye.

Wakati mwingine matamanio yetu yanakuwa makubwa kupitiliza,  mpaka yanatupofusha tunashindwa  hata kuona miujiza ya Mungu, kama sio kumwona Mungu mwenyewe.

Jambo kama hili utaliona kwa Balaamu pia, wakati ule anataka kwenda kuwalaani Israeli,  alipokuwa njiani, punda wake alifunguliwa kinywa na Mungu, na kuanza kuongea naye.. Sasa yeye kwasababu moyo wake wote tayari ulikuwa kule anapoelekea, kuwalaani Israeli, hata kuzungumza na Punda hakuona kama ni muujiza ule, badala yake akaanza kuzungumza naye kama anavyozungumza na mwanadamu mwenzake tu..Kama alivyofanya Mariamu.

Hesabu 22:28 “Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?

29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.

30 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!

31 Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi”.

Umeona? Pengine na wewe umekuwa ukizitazama sana shida zako, kuliko kuutazama uweza wa Mungu. Pengine ipo miujiza mikubwa Mungu ameshaanza kukufanyia lakini huwezi kuiona kwasababu wakati wote ukienda kwa Mungu unatazama tu ukubwa wa shida zako, na sio uweza wa Mungu.

Unasahau kuwa ni Malaika wa Bwana wamesimama pale pale unapopalilia, unasahau kuwa ni Yesu mwenyewe mkuu wa Uzima, amesimama pembeni yako kuzungumza na wewe na wewe juu ya hilo tatizo lako, lakini wewe unalia tu.. Leo nakuambia tuliza  moyo wako, usilie mahali ambapo tayari Mungu ameshakusikia, bali, mshukuru yeye, zungumza  na yeye, utaona miujiza mingi ambayo tayari ameshaanza kukufanyia katika maisha yako.

Mungu akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

YESU MPONYAJI.

NAWE UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.

Rudi nyumbani

Print this post

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Shalom,

Kuna kipindi mitume walimpelekea Bwana hitaji hili;

Luka 17:5 “… Tuongezee imani”.

Kwao pengine hili lilikuwa ni hitaji jepesi sana , lakini kwa upande wa Bwana halikuwa ombi la kuwajibu kwa sentensi mbili, au kwa kuwawekea  mikono tu na kupokea, hapana, na ndio maana baada ya ulizo hilo, hakukuwa na jibu la moja kwa moja kutoka kwa Bwana.

Sehemu nyingine alipoona upungufu wa Imani yao Bwana Yesu aliwaambia , namna hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa “kufunga na kuomba”(Mathayo 17:21)  Na sehemu nyingine biblia inasema, Imani huja kwa kukisikia Neno la Mungu(Warumi 10:17).. Ikiwa na maana kuwa kwa jinsi unavyosoma Neno la Mungu, na kuona uweza wa Mungu alioufanya, tangu enzi na enzi, sasa kwa jinsi unavyosoma sana na kusikia Neno lake, ndivyo imani yako inavyojengeka kwake, na hatimaye unakuwa na imani timilifu, hata ya kuweza kuamishi milima kwa jina lake.

Lakini katika yote hayo utagundua kuna kitu kimoja kinachoitwa BIDII ndani yake..Ikiwa na maana imani haiwezi kuja hivi hivi tu kwa kukaa, kama hutakuwa na bidii ya kuitafuta, haitakaa ije kwako kamwe, haiji kwa kuwekewa mikono, wala haiji kwa kuombewa,..

Sasa Imani ni nguzo mojawapo ya Ukristo, zipo nguzo nyingine mbili za Ukristo nazo ni Upendo na Tumaini. Lakini leo hatutazungumzia juu ya Tumaini, bali tutazungumzia juu ya Upendo, ambao ndio mkuu kuliko hata Imani au tumaini.

Upendo ni kilele cha Ukristo, Kwasababu biblia inasema Mungu mwenyewe ni Upendo.

Na Mkristo aliyekuwa sana kiroho, atatambulika kwa kiwango chake cha Upendo. Lakini wengi wetu tunadhani upendo ni kuonyesha tabasamu zuri kwa mtu, au kumsaidia mtu sana. Hivyo ni kweli ni vimelea vizuri vya Upendo, Lakini Upendo wa ki-Mungu unavuka hapo, na kwenda zaidi.

Embu tuvipitie baadhi ya vipengele vikuu,na mwishoni kabisa tutajifunza jinsi gani tutaupata huu Upendo mkamilifu.

1 Wakorintho 13

13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.

Ukianzia kusoma ule mstari wa 4, utaona misingi inayoubeba upendo ikanza kuzungumziwa,  anasema huvumilia. Jiulize  je ndani yako ulishawahi kuvumilia mabaya mangapi pale ulipotendewa, je pale alipokuaibisha uliweza kutunza siri yake?, je, ulimsamehe pale alipokuaibisha, je ulivumilia yote hayo yote bila kuweka kinyongo, au kukomoa?

Anasema tena, Upendo hufadhili; Neno fadhili ni pana sana, ni zaidi ya kumfanyia mwenzako wema, ambao hauna malipo yoyote kwako. Anasema tena, hautakabari, haujivuni, huatafuti mambo yake mwenyewe, je maisha na namna hiyo yapo ndani yako? Wewe kama mkristo uliyeokoka?

Anasema Upendo haukosi kuwa na adabu, Je! Wewe wakati wote unayo adabu kwa watu wote?, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, yaani inafikia hatua hauoni mabaya bali mema tu mtu anayokufanyia, Je ulishawahi kuwa mtu wa namna hii?  Ulishawahi kuwa mtu wa kustahimili mambo yote, au kuvumilia mambo yote, au ni baadhi tu ya mambo umeyaweza? Kama ni baadhi tu basi Upendo wa ki Mungu bado haujakamilika ndani yako. Haijalishi utajiona ni mwema kiasi gani.

Hivyo utoshe tu kusema kwa namna ya kibinadamu  Pendo hili la Ki-Mungu, si rahisi kulipata kwa maneno tu, au kwa kuombewa au kwa kuwekewa mikono, , hauwezi kustahimili yote, yapo mengine ambayo yatakuudhi, upo wakati ambao utawahusudu wengine, upo wakati ambao, utahesabu mabaya tu n.k. Huo ndio ukweli.

Lakini sasa tufanyeje ili tuyashinde hayo yote?

Kanuni ni ile ile, kama ya IMANI, unapaswa uonyeshe bidii, katika kutekeleza hivyo vitu.

1Petro 4:8 “Zaidi ya yote IWENI NA JUHUDI NYINGI KATIKA KUPENDANA; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”.

Inahitaji juhudi, mpaka ujijenge na kuwa tabia ndani yako, unapoona mwenzako amekutendea mabaya, unapaswa ujitahidi kwa nguvu zote, kuyaachilia yale mabaya anayokufanyia, na kujifunza kuyatafakari yale mazuri yake.. Ndio siku za mwanzoni mwanzoni, itakuwa ni ngumu lakini unavyojijengea utaratibu huo kwa nguvu, baadaye inageuka na kuwa ni tabia yako. Mpaka mwisho wa siku, hata jambo liwe ni gumu kiasi gani, utaona linatapita tu mbele yako kama upepo, bila kikusumbua hata kidogo .

Kumbuka tena vimelea hivyo vya upendo haviji hivi hivi tu, kwa kuombewa, au kusubiria, bali vinakuja kwa kuonyesha bidii, yaani kuvitendea kazi, mpaka ufikie hatua ya kutoona uchungu, au kutohusudu, kunahitaji kukataa usengenyaji kuanzia sasa, kukataa kusikiliza maneno ya watu mabarazani, pale wanapomzungumzia mtu mwingine kwa ubaya. Kunahitaji kujitoa kwa wengine, bila kujali unapata faida gani kwao..N.k.

Warumi 12:10 “Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;”

Upendo ni kitu cha kujazilishwa, yaani kila siku unakiongezea nyama mpya, kimoja huzaa kingine, na kingine huzaa kingine, mpaka tunafikia vile viwango vya Upendo wa ki-Mungu

2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,

6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,

7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.

8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo”.

Hivyo mimi na wewe kuanzia leo tuanze kuyatendea kazi haya, tujazilishe upendo wetu, siku baada ya siku tuongeze kimelea kipya cha upendo, Kwasababu tujue kuwa kitu cha kwanza ambacho kitatusogeza kwa Mungu kwa urahisi na haraka si Imani au tumaini bali ni Upendo, kwasababu yeye mwenyewe ni Upendo, na ndio maana Paulo anasema, hata nijapokuwa na Imani timilifu ya kuamisha milima kama sina Upendo mimi si kitu. Maana yake ni kuwa, huwezi kumwona au kumjua Mungu ukiukosa huo,

1Yohana 4:8 “Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo”.

Hivyo jambo hili, na kuwa nalo siriazi, ni kulitendea kazi kwa bidii zote, kila wakati kila muda mpaka lijengeke na kuwa tabia yetu.

1Petro 1:22 “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo”.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UPENDO WA MUNGU.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?

TUSIWE WATU WA KUPUNGUKIWA AKILI.

Rudi nyumbani

Print this post