Mithali 23:26 “Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. 27 Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba. 28 Naam, huotea kama mnyang’anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu”.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Kwa neema zake karibu tujifunze maneno ya uzima.
Hapo anaanza kwa kusema ‘mwanangu nipe moyo wako’..Halafu baada ya moyo anasema na “macho yako pia yapendezwe na njia zangu”…..Ni kwanini aseme hivyo? Ni kwasababu hapo ndipo kiini cha tatizo sugu la uzinzi kilipo.
Nataka tuone kwa jicho la ndani kwamba kahaba au Malaya anayezungumziwa hapa sio Yule unayekutana naye barabarani,akijiuza, bali ni Yule ambaye amesimama katika macho yako. .. Bwana Yesu alimjua kahaba huyu ndio maana akasema
Mathayo 5:28 “lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”
Umeona, huyu anapitia machoni, kisha akishafunguliwa mlango anaingia moyoni mwako kuzini na wewe. Haonekani kwa macho ya kibinadamu, huyu hana gharama yoyote, hatoboi siri, wala hakuzungushi zungushi, wakati wowote ukimuhitaji yupo hapo mlangoni kwenye macho yako anataka kuingia.
Sasa akishapewa nafasi ya kutosha ndio hapo anapochukua umbile la mtu ili kujidhihirisha kwa nje tu. Ataonekana aidha kwa kumfuata wewe, au yeye kukufuata wewe..sio makahaba wote watakufuata.
Daudi hakufuatwa na mke wa Uria, bali ni yeye ndiye aliyemfuata, mwisho wa siku akatumbukia katika shimbo refu, akajitia unajisi mwenyewe(akajiongezea hila). Ni kwasababu gani? Ni kwasababu alimpa nafasi Yule aliyesimama mbele ya macho yake, alipomwona mwanamke anaoga, badala ayafiche macho yake akimbie mbali, aikatae hiyo hali isiingie moyoni mwake akairuhusu, ndipo kahaba huyo aliyechukua umbile la mke wa mtu akajidhihirisha kwa nje, akamfuata na kwenda kuzini naye.
Samsoni, hakufuatwa na Delila, isipokuwa alivutiwa katika macho yake, alipoona wanawake wa kifilisti ni warembo zaidi ya wakiyahudi,wana maumbile mazuri, wanavaa vizuri, akayatii macho yake..Na ndio hayo hayo yalikuja kupofuliwa baadaye, akatumbukia katika rima jembamba, akafa bado ni kijana.
Sulemani, hakujazuia macho yake, wala moyo wake, Ndio maana akajikusanyia wanawake wengi kwa jinsi alivyopenda, yeye mwenyewe kama alivyoandika katika kitabu cha mhubiri;
Mhubiri 2:10 “Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
Matokeo yake ikawa ni wao kumgeuza moyo. Na kumkosea Mungu, akaabudu miungu mingine, akawa ni miongoni mwa wenye hila(dosari), katika wanadamu.
Lakini Yusufu, hakuruhusu moyo wake na macho yake yashawishwe na huyu kahaba sugu, hata alipojaribiwa kwa nguvu alikimbia kabisa. Akajiepusha na anguko hilo.
Bwana Yesu alipokitazama kizazi kile, alikiona kama ni kizazi cha Uzinzi (Marko 8:38), sio kwasababu kila mtu alikuwa anazini tu ovyo ovyo huko barabarani, hapana, lakini aliwaona hawa makahaba wa siri wakizini nao mioyoni mwao,
Tusemeje sasahivi.?
Picha na video za ngono ambazo zimewaharibu watoto na vijana, vipindi vya tv, na tamthimilia na muvi ambazo zinabeba maudhui ya kizinzi ndani yake, vinaongoza matendo haya rohoni.
Kujichua, na mazungumzo mabaya maofisini, mashuleni, na vijiweni yanaongeza kwa kasi uasherati rohoni. Ni lazima tufahamu Ile kukutana na mvulana/msichana ni matokeo tu ya nje, ambayo hupaswi kujutiwa sana zaidi ya chanzo husika ambacho kinaanzia kwenye macho kisha baadaye moyoni.
Awali ya yote ni kwa kudhamiria kabisa kutubu dhambi zetu na kuuacha ulimwengu, kwa kumkaribisha Yesu mioyoni mwetu. Pili ni kwa kufanya agano na macho yetu, kama alivyofanya mtumishi wa Mungu Ayubu.
Ayubu 31:1 “Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana”?
Usifungue macho yako kushawishwa na kimelea chochote ambacho kinaweza kukusababishia tamaa moyoni mwako, pambana sana hapo, Ikiwa upo katika ndoa fungua tu kwa mkeo/mumeo..Ikiwa upo nje, usiruhusu kabisa.. weka mipaka na marafiki wa jinsia tofauti, acha kutazama muvi, au picha picha mitandaoni, acha mazungumzo mabaya, ukipishana na mwanamke amevaa kizinzi macho yako yasigeuke nyuma endelea mbele. Kwa kufanya hivyo utafanikiwa kumuua huyu kahaba atokeaye mbele ya macho yako.Na hawa wa nje watakufa wenyewe. Utaishi maisha ya ushindi sikuzote.
Bwana atuponye, Bwana atusaidie.
Mathayo 23:26 “Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi”
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA.
1Timotheo 5:22 “Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi”.
Hapa tunaona mtume Paulo, anampa Timotheo maagizo ya namna ya kuwa kiongozi bora (Askofu bora) wa makanisa la Mungu. Utaona anampa maagizo ya utaratibu wa kuwaandika wajane, kwamba ahakikishe wanaoandikwa ni wale walio wajane kweli kweli. (soma 1Timotheo 5:9-16).
Pia utaona anampa vigezo vya uongozi kwa viongozi wapya wa makanisa mapya, kwamba wanapaswa wawe wameshuhudiwa kuwa na sifa njema…ndipo awawekee Mikono!, lakini asiwe mwepesi wa kuwawekea mikono kwa haraka.
Na pia viongozi wa makanisa (yaani wachungaji, maaskofu na wote wanaosimama kama viongozi wa kanisa) basi wanapaswa wapewe heshima maradufu, maana yake Wakumbukwe katika riziki na mahitaji yao mara dufu zaidi ya wengine, kwasababu wanakesha kwaajili ya roho za watu, kuwaombea na kuwachunga na kufundisha.
1Timotheo 5:17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.
18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake”
Na zaidi sana asikubali Mashitaka ya Wazee kwa haraka, (Juu ya wachungaji, au mashemasi)..isipokuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.. kwamaana ibilisi anapenda kuwatumia watu kuzusha jambo Fulani la uongo juu ya kiongozi wa kanisa, lengo lake likiwa ni kuliharibu kundi hilo..
Kwahiyo hapa Mtume kwa uongozo wa Roho anamwonya Timotheo asiwe mwepesi kusikiliza au kuamini maneno yazungumzwayo au mashitaka yaletwayo dhidi ya viongozi wa makanisa.. Bali alichunguze jambo kwa makini mpaka atakapopata uthibitisho kamilifu kwa vinywa vya mashahidi wengi.
Lakini la mwisho kabisa Paulo anamwambia Timotheo kuwa ASIZISHIRIKI DHAMBI ZA WENGINE!.
1Timotheo 5:22 “Usimwekee mtu mikono kwa haraka, WALA USIZISHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE. UJILINDE NAFSI YAKO UWE SAFI”.
SASA NINI MAANA YA KUZISHIRIKI DHAMBI ZA WENGINE?
Kwanza ni muhimu kufahamu hao “wengine” wanaotajwa hapo ni akina nani?.. Wengine wanaotajwa hapo sio watu wa mataifa (yaani ambao hawajaokoka), la! Bali wengine wanaotajwa hapo ni “watu walio ndani ya Kanisa”. Watenda dhambi hawapo tu Bar!, au kwenye madanguro..bali wapo wengi pia kanisani.
Sasa Mtu wa kanisani anapofanya dhambi na wewe ukaiona na kuifanya kama hiyo hiyo? Maana yake na “wewe umeishiriki ile dhambi”, Kwamfano unapomwona mtu kaingia kanisani kavaa Nusu tupu, au kavaa nguzo zinazobana au zisizo na maadili, na wewe ukaona na ukamwiga, siku inayofuata na wewe ukavaa kama yeye..basi hapo kibiblia umeshiriki dhambi za huyo mwingine, hata kama kanisa zima linafanya mambo yasiyofaa sisi tunapaswa kushiriki dhambi zao, Kwasababu kuna madhara makubwa sana ya kushiriki dhambi za wengine.
Vile vile inawezekana wewe ni Mwimbaji ndani ya kanisa, lakini kuna waimbaji wenzako matendo yao ni ya giza, maandiko yanatuonya tusishiriki dhambi zao, maana yake tusiwe kama wao..
Vile vile wewe kama ni kiongozi (Mchungaji, askofu, shemasi)..halafu ukamwona kiongozi mwingine anafanya mambo yaliyo kinyume na maandiko, aidha ni mla rushwa, au ni mwizi, au mzinzi, au mlevi na anafanya mambo mengine mabaya na wewe ukaiga ule ubaya au ukaufumbia macho..kibiblia umeshiriki dhambi zake huyo kiongozi.
Na hapa Mtume Paulo anamwonya Timotheo kuwa ajihadhari asije akashiriki dhambi za wengine, ajilinde nafsi yake awe safi.
SASA MADHARA YA KUSHIRIKI DHAMBI ZA WATU WENGINE NI NINI?
Unaposhiriki dhambi za mwingine, maana yake MAPIGO nayo mnashiriki sawasawa, na LAANA pia mtashiriki sawasawa, maana yake kama Mungu amemkusudia kumwangamiza kabisa mtu huyo kutokana na tabia yake ya wizi anaoufanya kila siku ndani ya Nyumba ya Mungu, na wewe ukamwiga kwakufanya mara moja moja tu.. basi mtashiriki kiwango cha adhabu sawa.. Wewe unayeiba mara moja moja na Yule anayeiba kila siku wote kiwango chenu cha adhabu kitafanana, kwahiyo utajikuta wewe unayefanya kidogo mnapata adhabu sawa na Yule anayefanya sana.
Ndio maana Paulo anamwonya Timotheo asizishiriki dhambi za wengine, bali ajilinde nafsi yake awe safi.. Na sisi hatuna budi kuzilinda nafsi zetu ziwe safi.. Na tujiepushe na dhambi za wengine.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.
Bwana alimaanisha nini kusema “Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake”?
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).
Lipo la kujifunza juu ya Yule mtu aliyepooza kwa miaka 38, na jinsi alivyopokea uponyaji wake katika siku moja.
Maandiko yanasema mtu huyu pamoja na wenzake walikuwa wakingojea muujiza katika birikia (au bwawa) moja lililoitwa bwawa/birika la Bethzatha, kwamaana kuna wakati malaika alishuka na kuyatibua maji ya bwawa hilo, na alipoyatibua yalikuwa yanaonekana mfano wa kuchemka.. (Siku zote Maji yaliyotibuliwa kimwonekano ni kama yanayochemka).
Kwahiyo wote walimtegemea huyu malaika ashuke, labda pengine alishuka kila baada ya miaka 2 au mitatu… Na cha ajabu ni kwamba pindi anaposhuka na kuyatibua maji, anayeponywa ni mtu mmoja tu!, (Yule aliyeingia wa kwanza) wengine mtasubiri mzunguko mwingine ambao haujulikani tena utakuwa ni lini.
Kwahiyo hawa wagonjwa walikuwa wanaishi kwa mashindano, kila mmoja akipambana kuingia wa kwanza.
Lakini siku moja Bwana Yesu alipita maeneo yale, na kuona hilo jopo la wagonjwa! Likisubiri Maji yachemke, likisubiri MAJI HAYO YA UPAKO, yavuviwe.. Na hapa anakutana na mmoja wa wagonjwa ambaye angalau alikuwa na imani ya kuponywa. Na swali la kwanza alilomwuliza “ni kama anataka kupona”..kama hataki maana yake asingemlazimisha..(siku zote Bwana huwa hatulazimishi kupona, ndio maana alisema tuombe!, maana yake tusipoomba hawezi kutulazimisha kupata)..
Tusome…
Yohana 5:1 “Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [WAKINGOJA MAJI YACHEMKE.
4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane
6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, ALIMWAMBIA, WATAKA KUWA MZIMA?
7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo”.
Ni somo gani tunajifunza hapo?
1.MAJI YA UPAKO HAYANA MATUMAINI YOYOTE.
Hebu tafakari huyu mtu ametumaini juu ya maji hayo ya upako kwa miaka 38, na hajaambulia chochote..Na ndicho kinachoendelea sasa, Idadi kubwa ya watu wamemwacha Yesu na kujitumainisha na Maji ya upako, chumvi za upako, na mafuta ya upako.. Pasipo kujua kuwa Mungu hajawahi kuvitukuza vitu hivyo… Mungu kamtuza tu Mwanae kupitia jina lake (jina la Yesu).
Ni mara chache chache sana Bwana Mungu anaruhusu watu wapokee uponyaji kupitia maji, au mafuta au leso kama Paulo. (Matendo 19:11-12)., lakini hiyo ni mara moja sana tena baada ya miaka mingi.. sio jambo la desturi kama linavyohubiriwa leo na manabii wengi wa uongo, ndio maana huoni mahali popote Paulo akiitumia hiyo kama staili ya kuombea watu wapone.
Hakuna mahali Petro katuma katengeneza mafuta yenye lebo yake na kuyapeleka Makedonia na Antiokia ili watu wafunguliwe.
Sasa kwanini Mitume pamoja na wakristo wote wa kanisa la kwanza hawakufanya hiyo aina ya uganga?? Ni kwasababu waliielewa hiyo habari ya huyo mtu aliyeponywa na Bwana pale kwenye birika la Bethzatha.
Jambo la Pili tunaloweza kujifunza ni kuwa Bwana Yesu baada ya kumponya huyo mgonjwa, hakumwambia jitiwike godoro lako ubaki hapo birikani, badala yake alimwambia aondoke hapo birikani… Hiyo ikifunua kuwa Kristo hakuwa anapendezwa na watu kudumu birikani, vile vile Leo hii Kristo ni Yule Yule hajabadilika.. hata leo hapendezwi na watu wanaodanganywa katika visima vijulikanavyo kama visima vya upako.
2. BWANA ALIKUWA ANAPITA KATIKATI YA WAGONJWA.
Jambo lingine tunaloweza kujifunza ni ziara ya Bwana kando kando ya lile birika..Utaona Bwana Yesu aliye mponyaji mkuu hakuwemo kwenye lile birika, wala hakuyagusa yale maji..bali alikuwa nje anapita pita akitafuta mtu wa kumponya, na huenda aliwajaribu wengi lakini walimdharau na kuendelea kujitumainisha katika kisima cha upako!.
Na Kristo ni Yule Yule, hata leo hayupo ndani ya kisima chochote kile kijulikanacho kama kisima cha upako, haijalishi hicho kisima kina sifa au historia ya kutendeka miujiza mikubwa kiasi gani, bado Kristo hayupo hapo!!!, hata kisima cha Bethzatha kilikuwa na historia ya miujiza mikubwa lakini KRISTO hakuyagusa hata maji yake..
Ndugu acha kujitumainisha katika maji, chumvi, mafuta, udongo au visima vijulikanavyo kama vya upako.. HUKO KRISTO HAYUPO!!! Na unadanganywa kuwa utapokea uponyaji, huo uponyaji utaungoja karne na karne hutaupata kwasababu Mungu Baba hajatukuza visima, wala michikichi, wala alizeti, wala mapeasi ya upako wala mchanga..Mungu Baba kamtukuza Mwanae mmoja tu!!!… ambaye ni YESU KRISTO!!!.. Ukijaribu kutafuta faida nje ya huyo Mmoja YESU, unapoteza muda, na unaelekea njia ya kuchanganyikiwa kama usipofunguka macho mapema…
Wafilipi 2:9 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
3. BWANA AMTOA YULE MTU PALE BIRIKANI.
Jambo la tatu na la mwisho tunaloweza kujifunza ni kuwa Bwana Yesu baada ya kumponya huyo mgonjwa, hakumwambia jitiwike godoro lako ubaki hapo birikani, badala yake alimwambia aondoke pale birikani… Hiyo ikifunua kuwa Kristo hakuwa anapendezwa na watu kudumu birikani, vile vile Leo hii Kristo ni Yule Yule hajabadilika.. hata leo hapendezwi na watu wanaodanganywa katika visima vijulikanavyo kama visima vya upako.
Yesu Kristo, kupitia jina lake ndiye chemchemi ya upako, ndiye kisima cha upako, yeye ndiye mafuta ya upako, yeye ndiye udongo wa upako, tukimpata huyo na kuyashika maneno yake, basi hakuna kifungo chochote kitakachodumu katika maisha yetu.. Yule mgonjwa alimpata Yesu akafunguliwa magonjwa yake ambayo kisima cha upako kilishindwa kumfungua, sasa tunahitaji fundisho gani tena tuelewe, na ilihali biblia imeshatupa hili funzo la huyu mgonjwa?
Je umemwamini Yesu?, je umefungwa na nguvu za giza?.. usikimbilie maji, wala mafuta bali kimbilia toba!, omba rehema na toba mbele zake kwa kumaanisha kabisa na atakusamehe na kukupa Roho wake mtakatifu na zaidi sana kukuponya tena bure!
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
OLE WAKO KORAZINI NA BETHSAIDA.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
Jibu: Neno “kaniki” limeonekana mara mbili tu katika biblia..(Yeremia 8:21 na Yeremia 14:2).
Na sehemu zote mbili linamaanisha “vazi jeusi lililovaliwa na watu wanaoomboleza” aidha kutokana na janga fulani au msiba.
Tamaduni za kuvaa kaniki katika misiba, zipo mpaka leo katika baadhi ya jamii za watu, ndio maana katika baadhi ya misiba utaona watu wanavaa mavazi meusi.
Desturi hiyo ilikuwepo tangu enzi na enzi…
Na katika biblia tunaona Yeremia aluvaa vazi hili wakati anaomboleza kutokana na msiba mkubwa uliowapata watu wake (yaani wana wa Israeli) baada ya kuuawa na Nebukadreza na baadhi yao kuchukuliwa mateka mpaka Babeli.
Yeremia 8:21 “Kwa sababu ya maumivu ya binti ya watu wangu nimeumia mimi; nimevaa kaniki; ushangao umenishika”.
Na wana wa Yuda wote waliomboleza kutokana na msiba huo.
Yeremia 14:2 “Yuda huomboleza, Na malango yake yamelegea Wameketi chini wamevaa kaniki; Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu”.
Je na sisi leo tunapoomboleza ni sharti kuvaa “Kaniki” (vazi jeusi)? Jibu ni La! Sio Sharti wala Amri..
Zaidi sana maombolezo ya misiba ya kidunia hayatufaidii chochote katika maisha yetu ya kiroho…lakini maombolezo ya dhambi zetu yanafaa sana..
Tunapoomboleza kwaajili ya dhambi zetu na za wengine, kwaajili ya makosa yetu na ya wengine, maaombolezo hayo yanafaa zaidi na yana matunda makubwa.
Yakobo 4:8 “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9 HUZUNIKENI NA KUOMBOLEZA NA KULIA. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa KUOMBOLEZA, na furaha yenu kuwa hamu.
10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
Nuru yetu inapaswa iangaze au isiangaze kulingana na Mathayo 5:16 na Mathayo 6:1?
Swali: Katika Ufunuo 22:16, tunasoma ile nyota inamwakilisha Bwana Yesu, lakini tukirudi katika Isaya 14:12, tunasoma ile nyota inamwakilisha shetani, hapa imekaaje?
Jibu: Tusome..
Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi”.
Tusome tena..
Isaya 14:12 “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa”
Kwa haraka ni rahisi kufikiri au kutafsiri kuwa hiyo ni nyota ile ile moja inayozungumziwa hapo, lakini ki uhalisia sio nyota moja bali ni nyota mbili tofauti, isipokuwa zote ni nyota za asubuhi.
Sasa tofauti ya nyota hizi mbili ni ipi?.
1.MAJIRA
Nyota inayotajwa katika Ufunuo 22:16 ambayo inamwakilisha Bwana Yesu inatajwa kama Nyota ya asubuhi, lakini ile ya Isaya 14:22 ambayo inamwakilisha shetani inatajwa kama ni nyota ya alfajiri. SASA ALFAJIRI na ASUBUHI, ni majira mawili tofauti.
Alfajiri ni mapema zaidi kuliko asubuhi, alfajiri inaanza saa 10 usiku mpaka saa 12 na asubuhi inaanza saa 12 mpaka saa Tano na dakika 59.
Sasa hapo biblia inaposema shetani ni nyota ya alfajiri maana yake ni kuwa nyota hiyo inaonekana alfajiri tu wakati wa giza na kukisha pambazuka inapotea lakini hiyo nyingine ambayo inamwakilisha Bwana Yesu ni Nyota ya asubuhi maana yake ni kuwa wakati kunapopambazuka na ile nyota ya alfajiri inapopotea kutokana na mwanga wa jua, hii nyota ya asubuhi bado itakuwa inaendelea kuangaza..
Sasa kama wewe ni mtu wa kupenda kuchunguza anga, utakuwa umegundua kuwa kunakuwepo na nyota moja asubuhi ambayo wakati nyota nyingine zimeshapotea yenyewe bado inaangaza.. Sasa nyota hiyo ndiyo inayomwakilisha Bwana Yesu, na ndio nyota ya asubuhi.
Na sifa nyingine ya hii nyota ya asubuhi, huwa pia ndio ile ile ya jioni, wakati ambapo nyota nyingine bado hazijatokeza kutokana na mwanga wa jua, hii ya asubuhi ndio inakuwa ya kwanza kutokeza..hiyo ikifunua tabia nyingine ya Bwana Yesu kuwa yeye ndiye MWANZO na MWISHO. (Alfa na Omega, Ufunuo 22:13).
Sasa kwa mapana na marefu kuhusu hii nyota ya asubuhi, na tabia zake kwa undani unaweza kufungua hapa >>> NYOTA YA ASUBUHI
Sababu hii ya majira itatupeleka moja kwa moja kuelewa tofauti nyingine inayofuata ya nyota hizi mbili.
2. MNG’AO
Nyota inayotajwa katika Ufunuo 22:16, ambayo inamwakilisha Bwana Yesu Kristo inatajwa kama ni nyota yenye KUNG’AA Lakini inayozungumziwa katika Isaya 14:12 haitajwi kama inang’aa, ni kama nyota nyingine tu ambazo zinaangaza usiku…lakini ya asubuhi haing’ai..maana yake kukisha pambazuka basi yenyewe inaisha nguvu, lakini nyota ya Bwana Yesu inang’aa katika giza na vile vile katika Nuru. Na hata mchana kwasababu ya ukamilifu wa Mkuu wa uzima Yesu.
Mithali 4:18 “Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.
Je umemtumainia Yesu aliye Nuru ya kweli, ambayo wakati wa mchana atakuwa nawe na wakati wa usiku utamwona?.
Shetani ni nyota inayoangaza kwa nuru ya uongo ndio maana haitajwi kama ni nyota ing’aayo (Soma 2Wakorintho 11:14), na inayopotosha, na inayoangusha wengi kama maandiko yanavyosema hapo katika Isaya 14:12.
Hivyo Kama bado hujampokea Yesu mpokee leo, na unampokea kwa kuamini kuwa yeye ni Bwana na alikuja kufa kwaajili ya dhambi zako na kukiri kwa kinywa chako, na kuungama dhambi zako zote kwa kumaanisha kutorudia tena kuzifanya.
Na baada ya hapo kutafuta ubatizo sahihi ambao ni kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa maji mengi (Matendo 2:38),
Na baada ya hapo Roho Mtakatifu atakuongoza na kukutia katika kweli yote ya maandiko.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 24:26 “Aibusu midomo atoaye jawabu la haki”
JIBU: Kwa namna nyingine inasomeka hivi “ Atoaye jawabu la haki, ni sawa na mtu abusuye mdomo wa rafiki yake”
Kwa tamaduni za kale za kiyahudi, ishara ya kuonyesha upendo wa dhati kwa mtu ilikuwa ni kubusiana midomo, sio kama sasa inavyotumika kama ishara ya mahusiano ya kimwili.
Na ndio maana katika maandiko utaona mitume wanaagiza watakatifu wasalimiane kwa busu takatifu (Warumi 16:16), halikadhalika utaona Yuda alipomsaliti Bwana alimbusu.
Lakini kwa tamaduni zetu, sasa ishara ya upendo ni kupeana mikono, na mahali pengine kukumbatiana, lakini sio kubusiana.
Tukirudi katika mstari, anaposema, ‘atoaye jawabu la haki’ Yaani mtu ‘anapoamua kwa haki’ au ‘anapozungumza ukweli kwa mwenzake, au kwa jirani yake, bila unafiki au upendeleo, , rohoni anatafsirika kama ni mtu ambusuye rafiki yake, mtu ampendaye rafiki yake sana, kwa kumkumbatia au kumpa mkono.
Tofauti na inavyoeleweka. Na wengi, kwamba ukimweleza mwenzako ukweli, ni kuunda uadui. Lakini Bwana wetu hakulijali hilo, ndio maana japokuwa alichukiwa na viongozi wengi wakidini kwa kuwa kwake muwazi (Yohana 8:40-45), lakini leo hii tunauona upendo wa dhati aliokuwa nao kwetu kwa kufanya hivyo.
Nasi pia Bwana atusaidie tuwe na ‘jawabu la haki’ vinywani mwetu. Tudhihirishe upendo wa kweli.
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Ni nani aliyesema “Nitume mimi”? katika
MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU.
Biblia Inatufundisha kuomba pale tunapokuwa katika majaribu, au tunapokuwa katika hali ya kuhitaji jambo Fulani.
Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”.
Lakini pia haitufundishi tu kuomba bali pia inatufundisha KUIMBA NYIMBO WAKATI WA FURAHA!. (Hili ni jambo la muhimu kulijua).
Biblia inasema..
Yakobo 5:13 “Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? NA AOMBE. Ana moyo wa kuchangamka? NA AIMBE ZABURI”
Hapo anasema mtu wa kwenu akiwa amepatikana na mabaya basi aombe, labda kapatwa na maradhi, au kakumbana na majaribu mazito..katika hali hii, biblia imesema tuombe!! Na Mungu atatusikia na kutuokoa au kutuponya na misiba yetu..
Zaburi 107:
4 “Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa.
5 Waliona njaa, waliona na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao
6 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao”
Lakini pia biblia inasema ikiwa mtu ANA MOYO WA KUCHANGAMKA..Na AIMBE ZABURI..ambaye ana Maana yake kama mtu moyoni mwake anayo furaha, au kapata furaha…pengine kaona mkono wa Bwana ukimtetea, au Bwana kampa afya na kumwokoa na mabaya, Bwana kampa amani, kampa utulivu n.k… mtu wa namna hii biblia imeshauri kuwa na “Aimbe zaburi” asikae tu kama alivyo!..
Sasa Zaburi ni nini?
Zaburi ni nyimbo maalumu za KUMTUKUZA MUNGU, KUMSIFU na KUMSHUKURU baada ya Bwana kututendea mema.. (Nyimbo hizi zinakuwa katika mfumo wa mashairi mazuri) mfano wa hizi ni zile Daudi alizokuwa anaziimba, kila baada ya kuuona wema wa Bwana!.
1Nyakati 16:7 “Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze.
8 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake.
9 Mwimbieni, MWIMBIENI KWA ZABURI; Zitafakarini ajabu zake zote.
10 Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana”
Kila tunapomshukuru Bwana au tunapomsifu kwa Nyimbo hizi za Zaburi, tunajipandishia thamani zetu mbele za Mungu, na tunaithibitisha mioyo yetu mbele za Mungu.
Unajua ni kwanini Daudi alipata kibali sana Mbele za Mungu?.. Sababu mojawapo ni desturi yake hiyo ya kumwimbia Mungu Zaburi..(na ndio maana hata kitabu chake kikaitwa kitabu cha Zaburi).
Zaburi 57:7 “Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti. NITAIMBA, NITAIMBA ZABURI,
8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.
9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, NITAKUIMBIA ZABURI KATI YA MATAIFA.
10 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni.
11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako”
Kwahiyo ni muhimu kufahamu kuwa KUOMBA ni muhimu lakini pia KUIMBA ni muhimu sana (Hususani Zaburi)..Mambo haya mawili yanakwenda pamoja!.. haijalishi sauti yako ikoje, wewe mwimbie Mungu, kwasababu Mungu katuumba ili tumtukuze yeye na kumsifu, pasipo kujalisha sauti zetu.
1Wakorintho 14:15 “Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; MTAIMBA kwa roho, TENA NITAIMBA kwa akili pia”
Lakini pia ni muhimu kujua kuwa Nyimbo za Zaburi lengo lake ni kumtukuza Mungu na kumshukuru, na kumwimbia na sio mipasho. Siku hizi za mwisho utaona mtu baada ya kufanyiwa wema na Mungu, ndio wakati wa yeye kuimba nyimbo ambazo anakuwa hana tofauti na watu wa kidunia ambao wanasemana kwa nyimbo!, huo ni udunia!. Na mtu wa namna hii asitegemee atapokea chochote kutoka kwa Bwana, haijalishi ananukuu zaburi kutoka kwenye biblia.
Siku zote ni lazima Nia zetu za kumwimbia Bwana ziwe takatifu mbele zake, na tusifanane na watu wa kidunia.. Hakuna mahali popote Daudi alimwimbia Sauli zaburi za kujionyesha kama yeye kakubaliwa mbele za Mungu zaidi ya Sauli, lakini kinyume chake utaona siku zote Daudi alimwombea rehema Sauli na zaidi sana alimheshimu hata kufikia hatua ya kumwita Sauli Masihi wa Bwana (yaani mpakwa mafuta wa Bwana), mtu ambaye usiku na mchana alikuwa anaitafuta roho yake.
Na sisi ni lazima tufanane na Daudi, tunamwimbia Mungu wetu Zaburi, huku fahamu zetu na akili zetu zikiwa zinamwelekea yeye(Bwana), na si zinawaelekea wale wanaotutesa, au kutuudhi, au kushindana nasi..huku tukiwaombea wote wanaopingana nasi kama Bwana Yesu, Mwalimu mkuu alivyotuelekeza katika…Mathayo 5:43
Mathayo 5:43 “ Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki?”
Bwana Yesu azidi kutubariki sote na kutusaidia.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Je ni kweli kila nafsi itaonja mauti kulingana na (Zaburi 89:48)?
JIBU: Neno Kristo limetoka katika lugha ya kigiriki (Khristos) ambalo likitafsiriwa katika Kiswahili linatamkika kama KRISTO.
Lakini Neno hili hili, kwa lugha ya kilatini (Christus), likitafsiriwa katika Kiswahili linatamkika kama KRISTU.
Swali ni Je! Ipi ni tafsiri sahihi?
Tufahamu kuwa biblia yetu (husasani sehemu kubwa ya agano jipya) haikuandikwa katika lugha ya kilatini, au kiingereza, au kichina, au kifaransa.. Hapana bali iliandikwa katika lugha ya Kigiriki ya kale. Hivyo tafsiri ya biblia yetu ya Kiswahili tunaitolea moja kwa moja kutoka katika lugha hiyo ya kigiriki, na sio kiingereza au kilatino.
Hivyo ni vizuri tukitumia lahaja ya lugha ya asili, iliyotumika kwenye biblia(Kigiriki) kuliko nyingine.
Japo wapo wanaotumia lahaja ya kilatino (Kristu), pia hawafanyi makosa, maadamu ni Kristo Yule Yule analengwa na sio mwingine. Ni sawa na anayesema ‘Sulemani’ au ‘Solomoni’. Ni Yule Yule mlengwa isipokuwa katika lahaja mbili tofauti.
Maana ya Kristo ni “Mtiwa-Mafuta” Ambapo kwa lugha ya kiyahudi anaitwa “MASIHI”. Hivyo tunaposema Yesu Kristo, tunamaanisha Yesu mtiwa mafuta. Yaani Yesu aliyeteuliwa na Mungu mahususi kwa kazi ya kuwakomboa wanadamu. Ni yeye tu ndiye mwokozi wa ulimwengu wala hapana mwingine.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Akida ni nani kibiblia, na kazi yake ni ipi? (Mathayo 8:5)
Babewatoto ni nani katika biblia?(Isaya 34:14).
Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 11: 26 “Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake”.
JIBU: Kuna wakati sukari ilikuwa adimu sana katika taifa letu, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa walipoona janga hilo limetokea, wakanunua sukari nyingi, tani kwa matani, wakazificha, hivyo ikaifanya sukari (hata hiyo kidogo iliyokuwepo) kuwa adimu zaidi.. Lengo lao ni sukari izidi kupanda bei ili waiuze kwa bei ya juu sana wapate faida kubwa.
Lakini jambo hili liliwaathiri watu wengi, hususani wafanyabishara wadogo wanaotegemea sukari kuzalisha bidhaa zao, pamoja na watu wa hali ya chini wasioweza kununua sukari kwa bei ya juu. Matokeo yake ikawa ni watu kulaumu na kuwakasirikia sana wanaofanya vitendo hivyo.
Au wakati ambapo maji ni adimu, baadhi ya watu hupadisha bei, kwa lengo la kujipatia faida kubwa zaidi, watakaa na maji yao kwenye visima mpaka atakapotekea mwenye bei kubwa. Watu wa namna hii ukichunguza utaona wanaishia kulaaniwa sana na watu wanaowazunguka.
Ndio maana ya huo mstari “Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake”..
watu watampenda na kumbariki Yule ambaye atawauzia huduma yake kama ilivyo desturi ya sikuzote.
1Yohana 3:17 “Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?”
Na rohoni pia ni vivyo hivyo,..Wakati tuliopo sasa maandiko yalitabiri ni wakati wa njaa kubwa sana ya kiroho, watu wakizunguka huko na kule kutafuta Neno la kweli la Mungu (Amosi 8:11-12). Lakini inasikitisha kuona baadhi ya watu wakificha maarifa, au huduma, kisa tu, hawalipwi vizuri..kumuona mtume/nabii ni sh. Laki moja. Kununua kitabu cha mhubiri Fulani ni sh.elfu themanini. Badala tuuze kwa bei nafuu, tunauza kibiashara, kisa tunafahamu ni lazima tu vitanunuliwa kwasababu sisi ni maarufu.
Bwana atusaidie. Tutoe nafaka tusiizuie
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kusemethi ni nini katika biblia?
Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?
KWA KUWA WASEMA MIMI NI TAJIRI.
Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)
Gengeni ni wapi, wale nguruwe walipoteremkia? (Marko 5:13)
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu lililo mwanga wa njia yetu na taa iongozayo miguu yetu.
Kuna mambo ambayo mbele ya macho yetu ni madogo, na huenda yakaonekana hayana maana sana au umuhimu sana, lakini kwa Mungu ni ya maana sana, kiasi kwamba usipoyafanya baada ya kuyajua yanaweza kukuweka mbali na Mungu maili nyingi sana sana pasipo hata kutegemea.
Na kuna mambo ambayo mbele ya macho yetu tunayaona ni ya muhimu sana lakini mbele za Mungu yakawa ni madogo sana. Sasa ni muhimu sana kujua yale ya muhimu na yale ambayo si ya muhimu. Na kawaida ya shetani ni kuyafanya yale ambayo si ya muhimu sana kuwa ya Muhimu na yale ya Muhimu sana kuwa ya kawaida.
Kwamfano kuna mahali Bwana Yesu aliwaambia Mafarisayo kuwa wameacha mambo ya msingi na muhimu kama Adili, rehema na imani na badala yake wanakesha kuzitukuza zaka wanazozitoa..Wakidhani kuwa Mungu anapendezwa na Zaka zao zaidi ya wao kuwa na rehema, kwasababu yeye mwenyewe alisema kuwa anataka rehema na si sadaka! (Mathayo 9:13). Maana yake cha msingi kwanza ni rehema na ndipo sadaka zifuate..
Mathayo 23:23 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia”.
Vile vile kuna maagizo mengine manne (4) ambayo ni ya Muhimu lakini shetani kayafanya yaonekane kama sio ya muhimu machoni pa watu.
1.Ubatizo.
Ubatizo ni agizo la muhimu sana kwa kila mtu baada tu ya kuamini, na ubatizo ulio sahihi na wa kimaandiko ni ule wa kuzama katika maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Soma Yohana 3:23, Matendo 2:38, na Matendo 19:5), shetani ameurahisisha ubatizo machoni pa watu wengi kwasababu anaujua umuhimu wake, na kaelekeza nguvu kubwa sana hapo kuzuia watu wasibatizwe kwasababu anaelewa uthamani wa ubatizo.
Ndio maana leo hii utaona mtu yupo tayari kwenda kuogelea katika fukwe za bahari, au katika mabwawa maalumu (swimming pools) hata masaa 6 na asichoke, lakini kitendo cha kutii tu agizo la kuzamishwa kwenye maji mara moja na kuibuka kwa jina la Yesu hataki, hapo ndio utaona jinsi shetani alivyowekeza nguvu zake nyingi, kuzuia jambo hilo.
2. Wanawake kufunika vichwa (wawapo ibadani).
Biblia imeagiza wanawake wafunike vichwa wawapo ibadani kwasababu ya malaika (1Wakorintho 11:10). Sasa ukitaka kujua malaika wana umuhimu gani kasome safari ya wana wa Israeli, ujue waliwekwa chini ya nani.
Kutoka 23:20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake”.
Mwanamke asiyefunika kichwa chake awapo ibadani baada ya kuujua ukweli, anaharibu uwepo wa Mungu na kujipunguzia Baraka za rohoni (haya ni mambo madogo machoni petu lakini mbele za Mungu ni makubwa na ya muhimu).
3. Kushiriki meza ya Bwana.
Bwana Yesu alisema tushiriki meza yake mara kwa mara, kwaajili ya ukumbusho wake.. Bwana Yesu kaitukuza meza yake hiyo zaidi hata ya siku yake ya kuzaliwa.. Hakuna mahali popote kaagiza tufanye ukumbusho wa siku yake ya kuzaliwa, lakini hapa kaagiza tushiriki meza yake kama ukumbusho wa siku yake ya kufa
1Wakorintho 11:24 “naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU.
25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, KWA UKUMBUSHO WANGU.
26 Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo”.
Sasa sisi tukilipuuzia agizo hili la kushiriki meza ya Bwana na kuona kama ni dogo tu!, na lisilo na maana.. Basi tufahamu kuwa tumekaidi Agizo kuu la muhimu kwa faida yetu wenyewe.. Kama upo mahali ambapo hupati nafasi ya kushiriki meza ya Bwana basi harakisha sana kutafuta kufanya hivyo.
4. Kutawadhana miguu.
Moja ya Agizo ambalo shetani kalifanya lionekane halina maana kabisa ni hili la kuoshana miguu, lakini ni agizo kuu sana, na la Muhimu sana.. Hebu turejee biblia tuone kama agizo hili lina umuhimu wowote.
Yohana 13:5 “Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. YESU AKAMWAMBIA, KAMA NISIPOKUTAWADHA, HUNA SHIRIKA NAMI.
9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.
10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote”
Hebu rudia kuusoma huo mstari wa 8, majibu Bwana Yesu aliyompa Petro.. alimwambia “KAMA NISIPOKUTAWADHA, HUNA SHIRIKA NAMI”. Kumbe kitendo cha kudharau au kukataa kuoshana miguu kinaweza kusababisha sisi kupoteza ushirika na Mungu moja kwa moja!!… ni jambo la kuogopesha sana!, na la kulitafakari sana..
Hebu tuendelee kusoma mistari inayofuata, tuone kama agizo hilo lilikuwa ni lazima kwetu..
1Wakorintho 13:12 “Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?
13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.
17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda”
Hapo Bwana Yesu kasema wazi kabisa wala hatuhitaji ufunuo wowote kuelewa… Ni lazima kuoshana miguu sisi wakristo kwa wakristo..na ndio ulikuwa utaratibu wa kanisa la kwanza (soma 1Timotheo 5:9-10). Kwahiyo na sisi ni lazima tutii agizo hilo vinginevyo tutapoteza ushirika na Bwana.
Shetani atakuhubiria leo kupitia watumishi wake kuwa “agizo hilo si la msingi” ndugu usidanganyike!..hata Petro alidhani hivyo, lakini saa alipoujua ukweli, alitamani hata Bwana Yesu amwoshe mwili mzima!..
Bwana Yesu atusaidie.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.
Ni maneno gani Bwana Yesu aliyokuwa anayaandika ardhini? (Yohana 8:7).
TENDA AGIZO LA YESU, HILO NDIO LITAKALOKULINDA.
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)