SWALI: Naomba kufahamu biblia inaposema wenye kuhadaa roho zisizo imara ina maana gani? (2Petro 14)
JIBU: Tusome;
2Petro 2:14 “wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, WENYE KUHADAA ROHO ZISIZO IMARA, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;
15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;
16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.
17 Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa”.
Katika siku za mwisho biblia inatabiri kuwa litatokea kundi Fulani la watu mahususi, lenye kazi ya “kuhadaa roho za watu watu”.
Kuhadaa ni kudanganya, Lakini biblia bado haisemi kundi hili litahadaa kila mtu tu, hapana bali inasema, litahadaa watu “wenye roho zisizo imara”.
Kwa kawaida kitu kisicho imara ni kitu kisichoweza kudumu kwa muda mrefu, kisichoweza kustahimili mazingira ya mtikisiko, au mazingira magumu kwa muda mrefu kwasababu kimeundwa chini ya ubora. Kwamfano, ukinunua kiatu cha ngozi, na mwingine akanunua kile cha plastiki, mkavitembelea wote kwa pamoja, utaona baada ya muda mfupi kile cha plastiki, kinachakaa na kuisha kabisa, lakini kile cha ngozi kinaendelea kudumu, Kwasababu gani? Ni kwasababu kiatu kile cha plastiki sio imara.
Vivyo hivyo katika roho siku hizi za mwisho, Kuna wakristo walio imara, na wengine ambao sio imara, kuna wenye nguvu ya kudumu katika wokovu haijalishi ni mitikisiko mingapi inawakumba kwasababu hapo mwanzo walimaanisha kweli kweli kumfuata Kristo.. Hawa wana heri sana, ibilisi hawezi kuwahadaa.
Lakini kundi lililo hatarini ni hili ambalo leo linaokoka kwa Bwana, kesho linarudi nyuma, leo ni moto kesho ni vuguvugu, leo linahudhuria mikesha, kesho linasahau, leo linaeleweka, kesho halieleweki, leo lipo ibadani wiki ijayo halifiki kabisa, likiwa na wapendwa linazungumza habari za Mungu, lakini likikaa na watu wa kidunia, linabadilika rangi, linafanana na wao. Lipo hapo katikati, Kudondoka kiwepesi katika dhambi ni jambo la kawaida kwao, ukiliuliza mbona umefanya hivi litakuambia nimepitiwa tu na shetani.
Sasa watu kama hawa ni lazima shetani atawahadaa tu,kwa hila zake, Na watakapodanganywa hawawezi kufahamu kwasababu wao ni roho zisizo imara. Kama Balaamu alipowahadaa wana wa Israeli, kwa kuwashawishi wazini, na mwisho wa siku Mungu akawapiga kule jangwani, Pale Edeni Hawa alipodanganywa na nyoka hakujua chochote, kwasababu moyo wake haukuwa imara kwa Mungu.
Ndugu kama na wewe ni mmojawapo tubu dhambi mgeukie Bwana, kisha maanisha kabisa kumfuata Yesu kwa gharama zozote, Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho. Watu waliovuguvugu Bwana ameahidi kuwatapika, na wewe angalia usitapikwe. Au kudanganywa na ibilisi. Simama imara kwa Bwana. Kataa ukristo feki, au wa juu juu usioingia gharama.
1Wakorintho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari”.
1Wathesalonike 3:12 “Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote”.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?
Ni mlima gani Yule Mwanamke Msamaria aliokuwa anaumaanisha? (Yohana 4:19)
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
Nini maana ya siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja? (2Petro 3:8)
SWALI: Nini maana ya huu mstari? Hapo anaposema yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
Mhubiri 10:8
[8]Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
JIBU: Mistari hiyo inawazumgumzia watu ambao wanasababisha matatizo kwa wenzao. Au watu wanaowakosesha wengine waliokuwa tayari katika njia sahihi.
Na ndio maana hapo anaanza kwa kusema mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake..Akiwa na maana kuwa dhara lile unalolipanga kwa mwingine limpate ndilo hilo hilo litakupata wewe.
Mfano wa watu kama hawa katika biblia ni Hamani, ambaye alikua adui wa Mordekai na wayahudi wote, mpaka akafikia hatua ya kumtengenezea msalaba Mordekai, lakini kinyume chake msalaba ule ndio ukamtundika yeye mwenyewe.
Lakini kwenye hicho kipengele cha pili anasema Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.. Maana yake ni kuwa maboma sikuzote hujengwa kwa lengo la kudhibiti maadui, tukiachilia mbali wanadamu, lakini pia wanyama wakali kama fisi, mbweha na nyoka wasivamie mifugo.
Hivyo anaposema abomoaye boma..anamaanisha aondoaye ulinzi wa mwenzake ili maadui kama nyoka wapite, wawadhuru, kinyume chake atadhurika yeye.
Hii ikifunua nini?
Wapo watu leo hii, wanaoondoa maboma ya watu wengine kwa hila zao. Na maboma yanayomaanishwa hapo si mengine zaidi ya YESU KRISTO. Yeye ndio boma letu, Biblia inasema hivyo..
Zaburi 18:2
[2]BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Hivyo watu watu wanawakosesha kwa kuwalaghai ili ibilisi awameze, wanawazuia wasimwabudu Mungu sawasawa na mapenzi yake, wanawazuia wasimwombe Mungu wao, ili wapoe..lakini kinyume chake wao ndio watamezwa. Na Bwana atawaponya watu wake.
Mfano wa watu kama hawa,ni wale maliwali wa Umedi waliompangia visa Danieli, ili asimwombe Mungu wake, kutwa mara tatu. Wakidhani kuwa ndio atapotelea mbali kwenye tundu la simba. Lakini kinyume chake wao ndio walimezwa na ibilisi.
Hivyo kamwe usijaribu kumkosesha mtu wa Mungu, wala usijaribu kumwondolea boma lake (Yesu Kristo), ukadhani ndio tayari atarudi nyuma. Wewe ndio utarudishwa nyuma na shetani.
Tusiwe watu wa kusababisha mabaya/madhara kwa wengine. Ndio kiini cha mistari hiyo.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Wale Nyoka wa Moto jangwani, walikuwa ni wa namna gani?
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
Mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili
SWALI: Kuota nasubiriwa mahali Fulani, nihutubie halafu mimi nachelewa, au natingwa na mambo mengine ina maana gani?
JIBU: Ndoto ya namna hii, mara nyingi huwa inaotwa na makundi ya watu ambao wanawajibika katika kuwahudumia wengine, aidha ni viongozi, au wahubiri.
Na huwa zinakuja katika sura tofauti tofauti, wengine wanaota wanasubiriwa kwenye mikutano wahutubie, lakini wanajikuta, wakicheleweshwa na mambo madogo madogo, pengine foleni, au watu, au vishughuli visivyokuwa na msingi. Wengine wanaota wanapaswa wapande madhabahuni wawahubirie wengine, lakini mara wanajiona wapo uchi, wanatafuta suti zao wavae, hawazioni, muda unazidi kwenda, mpaka mwishoni watu wanaondoka, wote na yeye bado hajatokea madhabahuni. N.k.
Hivyo ukiota ndoto ya namna hii tafsiri yake ni kuwa, wewe kama kiongozi kiwango chako cha utayari katika nafasi hiyo Mungu aliyokuweka bado kipo chini. Na ndio maana unashindwa kufika pale, yapo mambo ambayo yanatia vikwazo kwako. Bwana anasema..
2Timotheo 4:2 “lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”
Hivyo unachopaswa kufanya ni kuondoa visababu, au hivyo vizuizi vidogo vidogo, mbele yako, ambavyo pengine vinakusababishia uone huo sio wakati ufaao, kwa kumtumikia Mungu, kisha kuwa tayari, kusimama na Bwana kwa ukamilifu wote, kama askari ambaye amevitwa utayari miguuni kwa ajili ya vita.
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu UTAYARI tupatao kwa Injili ya amani”
Kwa kuzingatia hayo, utakuwa umelitatua hilo tatizo, katika wito wako.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KUOTA UNALIA/UKIOTA UNALIA KWA UCHUNGU.
KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu.
Neno la Mungu linasema…
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”
Andiko hilo ni muunganiko wa maneno mawili, Neno la kwanza ni “TUTAFUTE KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE”, na neno la pili, ni “TUTAFUTE KWA BIDII KUWA WATAKATIFU”.
Ni sawa na mtu aseme “katafute shati na kiatu chumbani”…tukiichambua sentensi hiyo tunapata maneno mawili, 1) Tukatafute shati na pia 2) Tukatafute kiatu.
Vivyo hivyo hapo biblia iliposema “Tutafute kwa bidii kuwa na amani na watu wote” na “huo utakatifu”..imemaanisha “tutafute amani” na pia “tuutafute kwa bidii utakatifu”.
Ikimaanisha kuwa utakatifu, ni wa kutafutwa, Tena kwa bidii sanaa!!..
Na ni kwanini tumeambiwa tuutafute kwa bidii???…Ni kwasababu hapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao.
Unaweza usiwe na Imani kama ile ya Eliya lakini bado ukamwona Mungu, unaweza usiwe mhubiri wa madhabahu lakini bado ukamwona Mungu.(Kwa kumtumikia Mungu kwa njia nyingine).
Lakini ukikosekana utakatifu, kumwona Mungu haiwezekani.
Na utakatifu maana yake ni kukaa mbali na kila aina ya dhambi.
Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho alizidi kilisisitiza hilo katika kitabu cha Wagalatia 5:19-20.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.
Hapa mwisho anamalizia kwa kusema “watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”. Hii inaogopesha sana..
Sasa Utakatifu, tunautafutaje?..
Dhambi yoyote kabla haijaleta madhara huwa inaanza kama mbegu ndogo..biblia inasema chanzo cha dhambi ni tamaa.
Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Unapokuwa na uwezo wa kuzitawala tamaa zako, basi dhambi kwako itakuwa mbali, na hivyo siku zote utajiweka katika hali ya utakatifu..lakini kila kitu kinachokuja mbele yako wewe unakitamani, kila mtindo wa uvaaji, ulaji au mtindo wa kimaisha unaokuja mbele zako unautamani, basi fahamu kuwa upo hatarini kuupoteza ukamilifu wako.
2. KWA KUKAA MBALI NA VICHOCHEO VYOTE VYA DHAMBI.
Dhambi inayo vichocheo, kama vile hasira ilivyo na vichocheo, kwa mfano vichocheo vya dhambi ya uasherati ni utazamaji wa pornography, mazungumzo mabaya na ya mizaha, makundi mabaya ya watu, uvaaji mbaya, filamu za kidunia ambazo asilimia kubwa maudhui zake ni kuchochea tamaa ya zinaa, vile vile magroup na kurasa mbalimbali katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, whatsapp, instagram na mengineyo.
Mtu anayekesha muda wote kwenye facebook au kwenye mitandao mingine ya kijamii, mtu huyo kamwe asitegemee atakuwa salama..
Biblia inasema “Tutafute kwa bidii!!”…Sio kwa ulegevu..Maana yake “ukamilifu” hatuwezi kuupata tukiwa walegevu.
3. KWA KUOMBA NA KUJIFUNZA NENO.
Tunapokuwa waombaji, katika ulimwengu wa roho shetani na mapepo yake yananakaa mbali nasi..Hivyo na viwango vyetu vya utakatifu vinapanda..Vile vile tunapokuwa watu wa kujifunza Neno la Mungu, tunakuwa tunatakasika kwasababu Neno la Mungu lina maonyo ndani yake, na linatufunza na kutukumbusha kudumu katika Imani na utakatifu. Dalili ya kwanza ya mtu anayerudi nyuma kiimani, ni kupungukiwa na nguvu ya kujifunza Neno. Hivyo ili na sisi viwango vyetu vya utakatifu vipande hatuna budi tuwe wasomaji wa Neno la Mungu (yaani biblia) .
Bwana atusaidie, tuupate utakatifu!
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana libarikiwe… Karibu tuyatafakari maandiko pamoja.
Katika dunia hii ya siku za mwisho, ni watu wengi sana wanaomjua Yesu, na maisha yake yote, jinsi alivyokuwa kwamba alizaliwa wapi, mama yake katika mwili alikuwa ni nani, baba yake alikuwa ni nani, wanafunzi wake walikuwa ni wangapi, na sasahivi yupo wapi, na kwamba atarudi tena.. n.k N.k. Ni watu wengi sana wanamjua Bwana Yesu wanaamini kuwa katoka kwa Mungu. Ndio maana leo hii ukimwuliza mtu kama anamjua Bwana Yesu, atakuambia Ndio, ukizidi kumwuliza kama anamwamini Bwana Yesu atakuambia tena Ndio!. Ni wachache sana wanaosema kuwa hawamjua kabisa wala hawamwamini. Hiyo ndio hali ya siku hizi za mwisho.
Lakini leo napenda nikuambie au nikukumbushe kuwa “kumjua tu Yesu peke yake, hakukufanyi wewe kuupata uzima wa milele”. Tusome maandiko yafuatayo..
Yohana 3:2 “Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.
Umeona?..Nikodemo pamoja na wenzake walimjua Yesu, na waliamini kuwa katoka kwa Mungu.. na hata wanakwenda mbele zake kumwambia Imani yao hiyo kwake. Lakini tunaona jibu la Bwana Yesu lilikuwa ni tofauti..
Kikawaida nilitegemea kuwa Bwana Yesu angemsifia Nikodemo na kumwambia “heri wewe Nikodemo kwa kuyajua hayo”.. lakini kinyume chake Bwana anamjibu Nikodemu na kumwambia…”Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.
Akiwa na maana kuwa haijalishi mtu amfahamu kiasi gani, au amwamini kiasi gani, kama mtu huyo hatazaliwa mara ya pili, imani yake hiyo ni bure..
Haijalishi Nikodemo na wenzake wanamjua Yesu kwa viwango gani, au wanamwamini kwa viwango gani, kama hawatakubali kuzaliwa mara ya pili, hawataurithi uzima wa milele.
Sasa swali linakuja katika vichwa vyetu, Nini maana ya kuzaliwa mara ya pili?
Swali hili hata Nikodeo alimwuliza Bwana, na Bwana Yesu alitoa maana yake, katika mistari inayofuata…
Yohana 3:4 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu”.
Umeona hapo?.. Kumbe tafsiri ya kuzaliwa mara ya pili, ni KUZALIWA KWA MAJI na KWA ROHO.
Sasa swali lingine, tunazaliwaje kwa Maji, na kwa Roho.
Tunazaliwa kwa Maji kwa njia ya Ubatizo, pale tunapobatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo, sawasawa na Matendo 2:38, hapo ndipo tunapozaliwa kwa Maji. Watu wengi sana wanaupuuzia Ubatizo, na kusema si wa lazima!.. na kusema ukishaamini inatosha, si lazima ubatizwe.. Kumbuka hapo!, hata Nikodemo alimwamini Bwana Yesu, na alijua ndio kashakamilika, lakini Bwana Yesu anamwambia..Usipozaliwa kwa Maji, huna uzima.. Vivyo hivyo, na mtu yeyote ambaye hatabatizwa katika ubatizo sahihi, baada ya kuujua ukweli hana Uzima wa milele, hiyo ni kulingana na mananeo ya Bwana YESU.
Na tunazaliwaje pia kwa Roho?.
Tunazaliwa kwa Roho, kwa njia ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndio muhuri wa Mungu katika maisha yetu..
Waefeso 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye MLITIWA MUHURI HATA SIKU YA UKOMBOZI”.
Kwahiyo mtu yeyote atakayemkataa Roho Mtakatifu, baada ya kuamini, huyo sio wa Mungu, haijalishi anamjua Bwana Yesu kwa kiwango gani!.
Warumi 8:9 “..Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.
Hivyo mtu anapobatizwa sahihi na kupokea Roho Mtakatifu wa kweli, hapo anakuwa kazaliwa mara ya pili, anakuwa ni kiumbe kipya, lakini si kilichokomaa bali ni kichanga, kilichozaliwa katika dunia mpya kisichojua chochote!.
Kwahiyo baada ya kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu, sio mwisho wa safari, bali ndio mwanzo wa safari, kama vile mtoto aliyezaliwa anavyopitia hatua za kukua mpaka kufikia utu uzima na kukomaa, vivyo hivyo na mtu aliyezaliwa mara ya pili, ni lazima apitia hatua za kukaa chini, kuukulia wokovu, kwa bidii zote, ili awe imara.. Lakini akiacha kuukulia wokovu, basi mtu huyo atakufa kiroho, na kazi yake itakuwa ni bure.Lakini zipo faida nyingi sana za kuzaliwa mara ya pili..Ni nyingi sana, hata katika maisha ya hapa hapa duniani, lakini faida iliyo kubwa kuliko zote ni hiyo Bwana Yesu aliyoitaja kwamba UTAUINGIA UFALME WA MUNGU.
Je umezaliwa mara ya pili?
Kama bado unangoja nini baada ya kuyajua haya yote?.. Tafuta ubatizo sahihi…wa maji mengi na kwa Jina la Bwana Yesu, na Ujazo wa Roho Mtakatifu.
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Shalom, jina la Bwana libarikiwe.
Ni vema tukajifunza tabia kadha wa kadha za Mungu, ili na sisi tuziige hizo tuwe wakamilifu kama yeye. Leo tutajifunza tabia mojawapo ya Mungu, ambayo pengine unaweza ukastaajabu Mungu anawezaje kuonyesha angali yeye ni Mungu. Hivyo kwa kupitia hiyo tutajifunza na sisi mienendo yetu.
Kwamfano ukisoma kitabu cha Mwanzo, baada ya Mungu kumaliza uumbaji wake wote, baadaye utaona tena anasema “si vema”(Mwanzo 2:18). Sasa utajiuliza iweje aone tena si vema, kwani kazi yake hapo mwanzo ilikuwa haijakamilika? Inahitaji marekebisho.. Mpaka aanze tena uumbaji mwingine wa kumpa Adamu msaidizi?..
Jibu ni kwamba Sio kwamba hakulijua hilo? Hapana alishalijua na tayari alikuwa ameshamuumba Hawa katika akili yake tangu zamani (Soma Mwanzo 1:27). Lakini alijifanya kana kwamba amesahau, ili kutufundisha sisi pia, tuwe watu wa kupenda marekebisho. Marekebisho sio dhambi, ni karama ya Mungu..Kwani kwa kupitia hiyo tutafikia ukamilifu, ukiwa mtu wa kuridhika na maisha yaleyale, mienendo ile ile, huna maboresho yoyote, ujue tabia hii ya Ki-Mungu haipo ndani yako.
Vivyo hivyo kuna tabia nyingine, ya kushangaza aliionyesha Mungu, na leo tutajifunza. Utakumbuka wakati ule, anakwenda kuiteketeza Sodoma na Gomora, alikutana kwanza na Ibrahimu, na alipomaliza kuzungumza naye akabidi pia amweleze Ibrahimu mpango wake, akamwambia maneno haya;
Mwanzo 18:20 “Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
21 BASI, NITASHUKA SASA NIONE KAMA WANAYOTENDA NI KIASI CHA KILIO KILICHONIJIA; NA KAMA SIVYO, NITAJUA.
22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana”
Tafakari kwa ukaribu hayo maneno..“nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua”.. Ni nini unajifunza hapo, kwamba huyu ni mtu asiyechukua maamuzi ya haraka kwanza bila kwenda kuthibitisha kwa undani ukweli wa tukio lenyewe.
Sio kwamba Mungu alikuwa hana uhakika wa kilichokuwa kinaendelea..Lakini alijifanya kana kwamba hajui, akaacha shughuli zake mbinguni, akateremka chini, aingie sodoma, atembee kwenye miji yake, ili apate uhakika wa taarifa zilizomfikia. Alijipa nafasi kati ya kile anachokisikia na maamuzi anayoyatoa.
Na kweli alikuta vilevile kama vilio vyao vilivyomfikia, lakini faida yake ni kuwa ndani yake alimwona mwenye haki mmoja, naye ni Lutu na familia yake, ndipo akamwokoa na ghadhabu ile. Lakini kama Bwana angetoa hukumu yake moja kwa moja kutoka kule mbinguni, pindi tu alipopokea taarifa na kusema ‘haya nyie malaika kapigeni kiberiti miji ile’.. Lutu angeonekania wapi?.
Tumeyabomoa maisha yetu sana, tumewaharibu wakina Lutu wetu, kwa kuchukua maamuzi ya haraka kwa kila tukio/Taarifa tunayoisikia, masikioni mwetu, au kwa kila jambo linalotokea ghafla mbele yetu.
Kwamfano Umesikia ndugu yako amekusengenya, usiwe na haraka wa kurudisha majibu ya chuki. Jifanye kama hilo ulilolisikia ni la uongo hata kama umelithibitisha.. Hiyo itakupa nafasi ya wewe, kutafakari kujua chanzo cha tatizo ni nini, na hatimaye utajikuta huwenda wewe ndio ulikuwa sababu ya yeye kuwa vile, na hapo utamsamehe, au kumwombea, au kujiombea wewe rehema. Lakini ukarudisha majibu ya kumchukia, au kumsema na wewe. Utajibomoa zaidi kuliko kujijenga.
Waweza sikia taarifa mbaya, au hujapendezwa na jambo Fulani au tukio fulani kwenye kanisa, kabla hujazira na kuondoka, pata nafasi ya kuomba, na kumshirikisha Mungu, kupitia viongozi wako wa kiroho, kama vile Mungu alivyomshirikisha rafiki yake Ibrahimu. Hiyo itakusaidia kuchukua maamuzi yaliyo ya busara zaidi.
Hata katika mambo ya maisha, kwenye familia, ukoo, pengine hata kazini kwako, ofisini, n.k, zipo taarifa nyingi zinaweza kukufikia za wafanyakazi wenzako, hupaswi kuzimeza moja kwa moja na kuzitolea maamuzi hata kama umezithibitisha kuwa ni za kweli.. Tuliza moyo wako, tafakari, omba, ndipo baadaye Mungu akuongoze cha kutenda. Utafanya vizuri zaidi.
Ni muhimu sana, kuweka “NAFASI” Katika mioyo yetu. Kile kinachoingia, kisirudishe majibu hapo hapo. Ni heri viingie mia, kikatoka kimoja chenye majibu ya busara, kuliko kuingia 100, vikatoka vyote 100, vyenye kisasi, na maumivu, na mapigo. Ilimgharimu Bwana asiziamini taarifa zake, iweje wewe uamini za kwako, au za wanadamu wengine?
Bwana atusaidie.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
UUMBAJI BORA WA MUNGU, UPO NDANI YA MWANADAMU.
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)
Ni miaka mingapi ya njaa Daudi aliyoambiwa achague? Ni miaka 7 au miaka 3?
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WANAWAKE.
Kuwa mwombolezaji:
Yeremia 9:20 “Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia”.
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu, mkuu wa uzima, karibu katika kujifunza maneno ya uzima. Huu ni mwendelezo wa mafundisho maalumu yawahusuyo wanawake.
Leo nataka tuone jambo ya kitofauti lililokuwa linawatokea wanawake wengi wa-Kimungu katika biblia. Na kwa kupitia hilo naamini lipo la kujifunza wewe kama mwanamke, uliyeokoka.
Na jambo yenyewe ni “kufungwa Tumbo la uzazi”. Ukisoma kuanzia mwanzo, wanawake wengi hodari walioitwa wacha Mungu, walifungwa matumbo yao wasiweze kuzaa, tukianzia kwa Sara, mpaka Rebeka, tukiendelea hadi kwa Raheli, na Ana-Mama yake Samweli, na Mke wa Manoa aliyemzaa Samsoni, na Elizabeti mama yake Yohana. Wote hawa walikuwa ni matasa. Unajua ni kwanini?
Wengi wanachukulia katika jicho la laana na mikosi, lakini ukitafakari vizuri, hakukuwa na laana yoyote juu ya watu hawa, kwasababu maandiko yanatuambia ni Mungu mwenyewe ndio aliyewafunga matumbo yao, Tengeneza picha Sara ambaye wafalme waliojaribu kumuiba wamfanye mke wao, Bwana aliwaadhibu vikali, mtu kama huyo iweje awe amebeba laana?
Hivyo lipo funzo kubwa sana nyuma yake, linalowahusu wanawake wote. Na funzo lenyewe ni kwamba Mungu anataka mwanamke yeyote, awe mwombolezaji, ili kusudi lake litimie, aulekeze moyo wake kwake kwa machozi mengi na dua, maombi, kwasababu kwa kupitia yeye, Mungu atalifanikisha kusudi lake kubwa duniani. Na ndio maana ilimgharimu Mungu awafunge matumbo wale wanawake wote, ambao alijua kabisa kwa kupitia wazao wao, Mungu atatukuzwa.
Ndio hapo utamwona mwanamke kama Ana, mke wa Elkana analia kama mlevi kule hekaluni, juu ya uzazi wake, yeye akidhani kwamba Mungu anasikiliza dua za tumbo lake, kumbe Mungu alikuwa anasikiliza maombi ya kuletwa mwamuzi Samweli duniani… Kwasababu ili shujaa aje ilihitaji maombolezo mengi sana.
Lakini kama moyo wake ungelitambua hilo tangu mwanzo, kuomba kwa bidii juu ya mwamuzi Israeli, kulikuwa hakuna sababu ya yeye kufungwa tumbo. Yanini?
Ndivyo ilivyokuwa kwa Raheli na Elizabeti, na wanawake wengine.
Binti, dada, Mama, bibi.. Tambua kuwa wewe umewekwa, kama mzalisha Nuru ulimwenguni. Maombi yako, machozi yako, sala zako, maombolezo yako, ni changizo kubwa sana la Mungu kuleta mapinduzi katika kanisa, familia, na hata taifa kwa ujumla.
Usisubiri Mungu akufunge tumbo lako, ndipo uanze kulia, na kuomboleza,. Bali jitambue sasa, Kumbuka Tumbo, linaweza kuwa pia kazi yako, au afya yako n.k ukiona hicho ndicho kinachokukosesha raha sasa, na umekiombea kwa muda mrefu bila mafanikio, basi tambua umefungwa hivyo na Mungu makusudi, ili uuelekeze moyo wako kwake.
Sasa hapo usiombe Mungu akupe mtoto au akupe kazi au akuponye huo ugonjwa, au akukombe kiuchumi, hapana omba Mungu, alete geuko kwa kanisa, kwa familia yako, kwa taifa, kwa kupitia wewe, ombea sana rehema na toba. Na hayo yaliyosalia Mungu alishakujibu siku nyingi yeye mwenyewe alishayatimiza. Kutokukujibu kwake haraka sio kwamba akutese hapana, machozi yako kwake hayajatosha, na umeyaelekeza pasipostahili.
Mwanamke usipokuwa mwombolezaji, fahamu kuwa unalididimiza kanisa, usipokuwa mwombaji, unalidhoofisha kanisa la Kristo kwelikweli. Tambua huduma hii, ili Kanisa liweze kusimama vema, wachungaji waweze kuhubiri, vipawa na karama vinyanyuke kwenye kanisa hadi kwenye familia, wewe ndio unayeweza kufungua milango hiyo.
Bwana atusaidie kujua hilo;
Yeremia 9:17 “Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; 18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.
20 Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.
21 Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu”.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA-KONDOO.
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)
Nini maana ya kupiga Kite! Katika biblia.
Luka 23:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura”
Je umeshawahi kumwombea msamaha mtu aliyekufanyia ubaya?.
Wengi wetu huwa tunaweza kusamehe tu, lakini tukaishia kusema “namwachia Mungu”. Tukiwa na maana kuwa Mungu ndiye atakayeshughulika na huyo mtu au hao watu na sio sisi.
Ni kweli, si vibaya kuwa mtu wa kusamehe na kumwachia Mungu, ashughulike na yaliyosalia, lakini msamaha wa namna hiyo hauumfanyi mtu kuwa mkamilifu.
Msamaha mkamilifu ni ule wa wewe kusamehe, na pia kumwombea msamaha kwa Baba yule aliyekukosea.
Bwana Yesu aliwasamehe wale wote waliomsulubisha, wale wote waliomtemea mate na kumpiga mijeledi, lakini pamoja na kwamba aliwasamehe yeye binafsi, pia alijua msamaha wake yeye binafsi hautoshi, kuwacha wale salama..alijua bado ghadhabu ya Mungu ilikuwa juu yao, hivyo akamwomba pia Baba asiwaadhibu, na Baba akawasamehe. (Huo ndio msamaha mkamilifu).
Ndugu Ukiteswa na kudhalilishwa, kwanza samehe wewe mwenyewe na kisha mwombee msamaha kwa Baba yule anayekufanyia huo ubaya.,
Ukidhulumiwa msamehe yule aliyekudhulumu kisha mwombee msamaha pia kwa Mungu, usiishie kumsamehe tu.(Kwasababu hajakuudhi tu wewe, amemuudhi pia na Mungu, hivyo mwombee msamaha kwa Mungu pia).
Ukipigwa msamehe yule aliyekufanyia huo ubaya na kisha mwambie pia Bwana amsamehe.
Tukiwa watu wa aina hiyo, basi tutakuwa wakamilifu kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyokuwa mkamilifu, na kwasababu hiyo ndio tutaitwa waKristo.
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,…………
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
NENO LA MUNGU NI UFUNUO MKAMILIFU.
TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!
Je wale waliomsulubisha Bwana, wataenda mbinguni, kwakuwa walisamehewa?
Ayubu 23:12 “
[12]Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu”,
Huyu ni Ayubu, …si ajabu kwanini Mungu alimwona ni mtu mkamilifu aliyemcha Mungu, kuliko watu wote waliokuwa ulimwenguni wakati ule.
Kitendo cha kuyatunza maneno ya Mungu zaidi ya riziki..si jambo dogo, ni kumaanisha kwa hali ya juu sana.
Ni kawaida mtu akiamka asubuhi jambo la kwanza atakalowaza ni ale nini, anywe nini..haiwekezani mtu apitishe siku nzima bila kukumbuka kuna kitu kinapaswa kiwekwe tumboni, Au asifikirie miradi yake, au kazi zake zinakwendaje siku hiyo,. Labda awe na hitilafu katika neva za ubongo wake.
Lakini Ayubu, ilikuwa ni kinyume, chakula/rizki ilikuwa ni “B” …”A” alipoamka asubuhi alikuwa anatafakari atayatimiza vipi maagizo ya Mungu, alikuwa anawaza siku itapitaje pitaje bila kupiga hatua mpya ya ukamilifu.
Hicho ndicho kilichokuwa chakula chake, alionyesha tabia iliyokuwa kwa mkuu wake YESU KRISTO. Ambaye tunasoma wakati fulani alipofuatwa na wanafunzi wake kuletewa chakula, aliwaambia maneno haya:
Yohana 4:30-34
[30]Basi wakatoka mjini, wakamwendea.
[31]Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule.
[32]Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.
[33]Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?
[34]Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.
Ayubu alipoamka asubuhi aliwaza toba,kwa ajili ya wengine.., (Soma Ayubu 1:5)
Alihakikisha Neno la Mungu halidondoki, alifanya agano na macho yake, asiwatazame wanawake akawatamani, (Ayubu 31:1). Aliwaza kuwafundisha wengine hekima na busara na kuwasaidia waliokuwa katika dhiki na uhitaji, (Ayubu 31:16-18), mtu wa namna hii Mungu hawezi acha kumwangalia na ndio maana tunasoma Habari zake mpaka leo.
Je na sisi tunaweza kufanana na watu kama hawa ambao walikuwa na tabia sawa na sisi. Kumbuka Ayubu hakuwa myahudi, wala nabii, wala kuhani..biblia inamwita MTU tu, fulani aliyetokea katika nchi moja iliyoitwa USI.
Na sisi, hivi hivi tulivyo tuna wajibu wa kumaanisha kuyatunza maneno ya Mungu, katika wokovu wetu, tuhakikishe tunayafanya maneno yake ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, ili tusiwe wasahaulifu.
Bwana Yesu alitupa amri tupendane..ni lazima tujifunze tabia hii, kila siku, alisema pia tusamehe, tusiposamehe Baba yetu naye hataweza kutusamehe makosa yetu.
Haijalishi umekosewa mara ngapi, umeibiwa mara ngapi, umedhulumiwa mali nyingi kiasi gani, kamwe usiyasahau maneno ya Bwana Yesu.. ‘samehe mara saba sabini…’
Bwana Yesu alisema, kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni..ukilisahau hili neno ukawa ni mvivu wa kuomba walau saa moja kwa siku kama alivyosema, wewe sio mkamilifu.Ifikie hatua kama vile tukumbukavyo muda wa kula ndivyo tukumbuke muda wa maombi na ibada. Huko ndiko kuyatunza maneno yake zaidi ya riziki zetu.
Na kwa bidii hiyo Bwana atatuona na kujidhihirisha kwetu,kwasababu sikuzote anazunguka ulimwenguni kote kutafuta watu wenye kumaanisha huku kama Ayubu ajifunue kwao.
2 Mambo ya Nyakati 16:9
[9]Kwa maana macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake…”
Bwana atutie nguvu.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
JE UNA MATUMAINI YA KUPATA TENA KILE ULICHOPOTEZA?
Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?
Bwana alimaanisha nini kusema“maana mtenda kazi astahili posho lake”
JIBU: ‘Bila kazi ya mikono’ maana yake ni kuwa pasipo kisaidizi chochote cha kibinadamu, kwamfano neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;
Danieli 2:34 “Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande”.
Huu ni utabiri unaomwelezea Yesu Kristo, jinsi atakavyokuja kuangusha ngome zote za ufalme wa huu ulimwengu, yeye ndio hilo jiwe dogo linalozungumziwa hapo, Na biblia inasema, lilichongwa bila kazi ya mikono maana yake ni kuwa lilijichonga lenyewe kutoka mwambani, lilijimegua lenyewe, likaenda na kuipigia ile sanamu, kufunua kuwa Kristo, hakuletwa na mwanadamu hapa duniani, alizaliwa pasipo baba, halikadhalika atakapokuja kuangusha hizi falme sugu za ulimwengu, hatosaidiwa na mtu, wala hata tegemea msaada wa mtu yeyote yeye mwenyewe ataupiga kwa uweza wake, na wote utaanguka kisha atauweka utawala wake usio na mwisho, ambao utaifunika dunia nzima,
Kufahamu jinsi atakavyojua kuzipiga hizi falme za dunia Soma Ufunuo 19:11-16
“11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.
15 NA UPANGA MKALI HUTOKA KINYWANI MWAKE ILI AWAPIGE MATAIFA KWA HUO. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA”.
Lakini pia Neno hili, utalisoma katika vifungu vingine, ambavyo vinamwelezea mtawala katili aliyetokea zamani katika ufalme wa Uyunani, aliyeitwa Antiokia Epifane, mtawala huyu alikuwa ni kivuli cha mpinga-Kristo anayekuja, kwani, alikuwa na nguvu nyingi, na kwasababu hiyo akawaua wayahudi wengi, na kama hiyo haitoshi akalitia unajisi hekalu la Mungu, ambalo hata wafalme wengine walikuwa wanaogopa kufanya matendo kama hayo, yeye hakujali hiyo alikuwa anamtukana Mungu wa Israeli hadharani, na kuchukua nguruwe na kuwaingiza hekaluni, lakini biblia inasema alivunjika, bila kazi ya mikono.
Danieli 8:25 “Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono”.
Maana yake ni kuwa, Mungu hatotumia jeshi, au wanadamu, au kitu chochote kijulikanacho kumuua, bali yeye mwenyewe atampiga na kufa ghafla, na ndivyo ilivyokuwa katika historia alipatwa na ugonjwa wa ajabu na ghafla, akafa. Kama alivyokuwa Herode wakati ule alivyoliwa na chango, baada ya kujitukuza kama Mungu. (Matendo 12:23).
Kazi zote za huu ulimwengu ni mbovu, kama Yesu mwenyewe alivyosema katika Yohana 7:7, na ndio maana atakuja kuziondosha zote. Falme zote zitaanguka, ustaarabu wote utaondolewa, Yesu atakuja kuweka ustaarabu wake mpya wa amani hapa duniani.
Sasa jiulize, mambo unayoyasumbukia leo hii, kana kwamba ndio uzima wako yatakufaidia nini huko mbeleni? Ishi ndani ya Kristo kama mpitaji na msafiri, ukijua kuwa huna makazi ya kudumu hapa, tumia nguvu zako, kuwekeza katika ufalme ujao udumuo, hata kwa hicho unachokisumbukia.
Kumbuka mambo haya yapo karibuni kutokea, huwenda hata ndani ya kizazi chetu, tukayashuhudia haya yote.
Maran Atha.
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?
Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?
Je mama mjamzito anaruhusiwa kufunga?
UTAKAPOKUWA MZEE, UTAINYOSHA MIKONO YAKO. NA MWINGINE ATAKUFUNGA
Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.