Swali: Biblia inatufundisha katika Wagalatia 5:23 kuwa “tuwe wapole kiasi”, sasa napenda kujua mtu utakuwaje mpole kiasi.
Jibu: Tusome,
Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 UPOLE, KIASI; juu ya mambo kama hayo hakuna sharia”.
Hapa biblia haisemi kuwa tunda la Roho Mtakitifu kuwa ni “Upole kiasi” kana kwamba “upole unapaswa uwe na kiasi”…. La! Bali inasema tunda la Roho ni “Upole”, halafu “Kiasi”… hayo ni maneno mawili yaliyotengenishwa na alama ya mkato.
Maana yake “Upole” ni kitu kingine na “Kiasi” ni kitu kingine. Ikiwa na maana kuwa Tunda la Roho “Upole ulio wote” na sio upole kiasi.
Biblia inatufundisha tuwe watu wapole kama Hua (Njiwa).
Mathayo 10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua”
Hua ni ndege mpole sana ndio maana Roho Mtakatifu alitumia umbile la Hua kushuka juu ya Bwana Yesu wakati ule alipobatizwa (Mathayo 3:16)... Na maandiko yanazidi kutufundisha kuwa Bwana Yesu ni Mpole..
Mathayo 21:5 “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.
Soma pia, Mathayo 11:29, utaona sifa hiyo ya Bwana ya upole ikitajwa..
Na sisi pia ni lazima tuwe na sifa hiyo ya “Upole” kama ishara mojawapo ya kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu… shetani kaligeuze Neno hili la Upole na kuweka “Upole kiasi” ili kuchochea ubaya ndani ya watu.. Kwamba ni vizuri kuwa wapole lakini tusiwe wapole sana, tuwe wapole tu kiasi!. Huo ni uongo wa adui!.
Na kumbuka kuna tofauti ya “upole” na “unyonge”. Biblia haitufundishi kuwa wanyonge, bali kuwa wapole, Mtu mpole ni yule ambaye ana uwezo wote wa kutumia ukali lakini hautumii!, kama alivyokuwa Bwana Yesu… Lakini mnyonge ni yule anayekuwa analazimika kuwa hivyo mpole kutokana tu na mazingira..na akitoka katika hayo mazingira basi tabia yake ya ubaya na ukali usio na maana na vurugu inajidhihirisha.
Bwana atusaidie .
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.
Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).
Jibu: Tusome kuanzia mstari wa 5..
Zaburi 91:5 “Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri”.
“Uele” ni janga linaloleta mauti linaloweza kumpata mtu.. ajali ya gari ni mfano wa Uele, Ajali ya kuzama kwenye maji ni mfano wa “Uele”, janga la kuungua moto mpaka kufa ni mfano wa “Uele”.
Maandiko yanatufundisha kuwa wote wamtumainio Bwana, na kumkimbilia na kumfanya kuwa ngome na msaada, hawatakuwa na hofu na majanga hayo, kwani Mungu ni ngome ya wote wanaomcha, naye ndiye awaokoaye na majanga.
Zaburi 121:4 “Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele”.
Je una hofu na UELE?..Mpokee Yesu kwa kutubu dhambi na kujazwa Roho Mtakatifu, naye atakupa furaha nawe utaishi maisha ya raha na ya utulivu.
Zaburi 127:2 “……Yeye humpa mpenzi wake usingizi”
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?
Je! Mungu anasababisha ajali au Majanga?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).
Jibu: Tusome,
“Ganjo” ni mahali palipoharibika.. Jengo lililoharibika linaitwa “Ganjo” yakiwa mengi yanaitwa “maganjo”, mji ulioharibiwa aidha kwa vita au kwa janga fulani pia unaitwa “Ganjo”.
Katika biblia neno hili limeonekana mara kadhaa..
Walawi 26:30 “Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.
31 Nami nitaifanya MIJI YENU IWE MAGANJO, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo.
32 Nami nitaitia hiyo nchi ukiwa; na adui zenu watakaokaa huko wataistaajabia”
Tusome pia…
Ezekieli 29:12 “Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, ITAKUWA MAGANJO muda wa miaka arobaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.”
Neno hili pia unaweza kulisoma katika mistari ifuatayo likiwa na maana hiyo hiyo..Walawi 26:33, 2Nyakati 34:6, Ayubu 3:14, Isaya 6:11, 7:19, Yeremia 4:7, Ezekieli 6:14, 36:38, na Amosi 9:14.
Vile vile hii dunia siku moja itafanyika kuwa “GANJO”, kutokana na dhambi!.. Bwana ataiharibu kwa moto kama alivyoiharibu nyakati za Nuhu, kwa maji.
2Petro 3:6 “kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu”.
Je umeokoka? Kama bado, saa ya wokovu ni sasa, tupo mwisho wa nyakati.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?
Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa?
Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?.
Fahamu Maana ya Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”.
Mara nyingi Sulemani kwa hekima ya Roho aliongozwa kuona uhusiano uliopo kati ya uvivu na umaskini. Kama tu kinyume chake, sehemu nyingine alivyoweka uhusiano kati ya bidii na utajiri(Mithali 10:4). Vivyo hivyo uvivu na umaskini havipishani.
Na kama anavyosema hapo, uvivu humpeleka mtu katika usingizi, lakini sio usingizi tu bali ule mzito, Kwasababu gani? Ni kwasababu mwili haupo katika hali ya kujishughulisha, na hivyo utalala tu, na Bado utaendelea kulala siku baada ya siku.. Na matokeo yake kutokuzalisha chochote kinachoonekana, hatimaye, umaskini unaingia.
Hivyo mstari huo unalenga Nyanja mbili. Ya kwanza ni ule uvivu wa mwilini, na ya pili ni ule uvivu wa rohoni.
Mungu katuumbia kufanya kazi, watu wote (ikiwemo watakatifu). Maana yake ni kuwa ikiwa huna huduma yoyote ya madhabahuni Bwana amekuitia, ambayo inakufanya utumike muda wote hapo. Ni sharti ufanye kazi. Mtume Paulo alilionya kanisa juu ya watu ambao hawafanyi kazi kwamba ni sharti wajishughulishe ili wapate na kitu cha kuwagawia na wengine (2Wathesalonike 3:10)
Lakini pia Uvuvi wa rohoni. Mtakatifu anapokuwa mvivu, kusoma Neno, yaani muda wa Neno anakwenda kutazama filamu, anakwenda kijiweni kucheza drafti,.Anakuwa mvivu kuomba, Unapofika huo muda tu anaona usingizi ni bora kuliko kuomba,.Au Mtakatifu hataki kushuhudia habari za Kristo kwa wengine, anasema jua kali. Sasa mtu huyo anajiandaa kuwa maskini kiroho. Yaani atakuwa katika wokovu usiokuwa na matunda, ukuaji wake wa kiroho utakuwa hafifu, Neema ya Mungu haitatenda kazi kwa wingi juu yake, na hivyo atakosa mema mengi ya Mungu katika safari yake wa wokovu hapa duniani.
Uvuvi wowote, una hasara, kwahiyo tuuweke katika orodha ya maadui zetu wa imani.
Bwana atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Fahamu Maana ya;
Mithali 19:11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Mstari huo unatufundisha mtu aliyejaa “Busara” moyoni ni mtu wa namna gani..
Anaeleza ni Yule ambaye anaouwezo wa kughahiri hasira yake, na pia kupenda kusemehe makosa. Ambayo ndio sifa ya Mungu, Aliyonayo, soma;
Kutoka 34:6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
Hivyo na sisi hatuna budi kutokuwa watu wa kukasirika haraka, mpaka ikaleta athari nje, kwamfano umeumizwa na mke/mume wako, tunapaswa tujifunze kuachilia mara moja, lakini pia kusamehe, sio kuweka kinyongo, au uchungu moyoni. Au mtu amefanya kosa la kukuudhi ambalo anastahili adhabu, si vema kuwa wepesi wa kuadhibu bali kuahirisha hasira hizo kwasababu Mungu naye anatusamehe makosa yetu, hatuadhibu kila kosa.
Bwana alisema kusamehe kwetu hakupaswi kuwe na ukomo, alitumia lugha ya hata ‘saba mara sabini’ kwa siku(Mathayo 18:22). Kuonyesha kuwa kusamehe kwetu kunapaswa kuwe endelevu. Ili tufikie hatua ya Kuona ‘fahari’ katika uwezo wa kusamehe, zaidi ya kuona fahari katika uwezo wa ‘kupata vitu’. Yaani tuhesabu ni watu wangapi tumewasamehe, hapo ndio iwe furaha yetu. Na kwamba tuipime busara yetu kwa kiwango cha kuiharisha hasira zaidi ya uwezo wa ‘kuwa na maneno mengi ya hekima’.
Bwana atusaidie.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
NIFANYE NINI NIWEZE KUDHIBITI HASIRA?
Mungu anatufundisha kusamehe mara saba sabini, ila Kwanini yeye hakumsamehe Adamu alipoasi?
TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.
BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.
KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?
SWALI: Nini maana ya Mithali 24:11 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe.
JIBU: Mstari huu una maana mbili,
Mana ya kwanza ni uhai kama ‘uhai’ alionao mwanadamu yoyote,
Maana yake ni kuwa uonapo, mtu asiyekuwa na hatia, amepangiwa njama za kuuliwa, au ndio anakaribia kufa, na wewe unaowezo wa kumsaidia huna budi kufanya hivyo wala usijifanye kama hiyo sio biashara yako.
Ni mfano wa Yule mtu aliyevamiwa na wanyang’anyi ambaye Bwana Yesu alimtolea mfano, akasema mlawi alimpomwona akapita kando, kuhani naye alipomwona akapita kando, lakini Yule msamaria akamuhurumia, akamtibu, akaokoa uhai wake. Na Yesu akasema huo ndio Upendo.(Luka 10:25-37)
Ni sawa na wakati ule Paulo amepangiwa njama na wayahudi wamvizie auawe, lakini mjomba wake alipogundua alikwenda kumjuza akida wa kikosi (Matendo 23:12-22). Huyo amemwopoa aliyekaribu na kuchinjwa.
Ni sawa na Mordekai alichofanya kwa Mfalme, Ahusuero, wale watu walipopanga njama ya kumuua akaenda kuwasemelea (Esta 6:1-12),. Ni sawa na Yonathani, alivyomtunza Daudi dhidi ya upanga wa baba yake Sauli ili asiuliwe. Hivyo hawa wote, walilitambua andiko hili, na wala hawakuogopa kutoa siri, za wale waliokusudia mabaya juu ya maisha ya wengine.
Hata leo, vifo vingi vya kikatili, vingeweza kuzuilika kwa sehemu kubwa, endapo baadhi ya wanaojua matukio hayo wangetoa taarifa mapema. Kwamfano utaona mtu anawekewa sumu kwenye chakula, wewe unayejua, ni wajibu wako kutoboa siri hiyo, ili uutunze uhai wa mtu. Utaona mwizi anapigwa, huna budi kuripoti polisi mapema maadamu jambo hilo lipo ndani ya uwezo wako, ili askari waje kumkamata wampe wao adhabu stahiki, lakini ukipita ukasema hainihusu, atachomwa moto. Lakini kumbuka uhai unathamani, hata wa mtu aliye mbaya, unathamani nyingi.
Lakini ukisema hainuhusu, Utakuwa unajipunguzia pia rehema nyingi kwa Mungu, ndio maana mstari unaofuata unasema;
Mithali 24:11 “Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. 12 Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?”
Hivyo penda uhai, pia tunza uhai wa watu, popote pale uonapo unahatarishwa. Usiwe mzito kusaidia.
Lakini maana ya pili ya mstari huu ni ule Uhai wa rohoni.
Wapo watu ambao ibilisi, anakaribia kuwameza, na ukiwaacha ndani ya kipindi kifupi hakika wataangamia kabisa kiroho. Wengine wanakaribia kufa kwasababu ya huzuni mioyoni mwao, kukata tamaa, kwasababu ya dhiki na magonjwa, wengine wanakaribia kuzama katika ushirikina, wengine kwenye imani potofu ambazo zinakwenda kuwaua roho zao n.k. Hivyo makundi kama haya, unapoyaona, mwelekeo wao wewe kama mkristo uliyesimama huna budi kuwasaidia ili waokoke, wasipotelee katika mauti ya roho zao, na kwenye minaso ya adui mfano wa Yuda. Wala usisime hiyo sio shughuli yangu.
Yuda 1:22 “Wahurumieni wengine walio na shaka, 23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Hivyo tutunze Uhai, wa mwili na Roho za watu wa Mungu, naye Bwana atatunza na wetu.
Bwana akubariki
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?
Biblia inamaanisha nini inaposema “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake”?
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?
Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu libarikiwe.
Karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu.
Kuna mambo makuu mawili ambayo yanaweza KUMUUNGANISHA MTU MOJA KWA MOJA NA USHIRIKA WA MAPEPO.
Na mambo hayo ni SADAKA NA UASHERATI. Haya mambo mawili yanaenda pamoja, ndio maana wanaoenda kwa waganga utaona wanaambiwa watoe sadaka, au wafanye zinaa, lengo la zile sadaka si kuimairisha maisha ya wale wanaozitaka (waganga), wala lengo la ile zinaa si kuwafurahisha hao waganga bali ni kumuunganisha yule mtu na madhabahu ile!.
Sasa nataka tuangalie mfano mmoja wa kwenye biblia wa watu waliojiunganisha na madhabahu za mashetani kwa njia hizo mbili; (MATOLEO PAMOJA NA UASHETANI). Na hao si wengine Zaidi ya Wana wa Israeli walipokuwa katika safari yao ya kwenda Kaanani.
Tusome,
Hesabu 25:1 ”Basi Israeli akakaa Shitimu, KISHA WATU WAKAANZA KUZINI PAMOJA NA WANAWAKE WA MOABU;
2 kwa kuwa waliwaalika hao watu WAENDE SADAKANI, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.
3 IKAWA ISRAELI KUJIUNGAMANISHA NA BAAL-PEORI; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.
4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli.
5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baalpeori”
Mstari wa 3 hapo unasema hao watu kajiunganisha na “Baali-peori” ambaye ni mungu wa wamoabi, na njia waliojiunganisha nayo ni UASHERATI na SADAKA!
Na adui njama aliyoitumia ni KUALIKA!.. walioalikwa tu! Lakini kumbe walikuwa wameshaandaliwa “wanawake wa kuzini nao” na kwa tamaa zao wakaingia kwa wanawake hao na kuzini, pasipo kujua kuwa kwa kitendo hiko tayari walikuwa wameshajiungamanisha na miungu yao, na hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli na Mungu akapigo kwa pigo kuu.
Ndugu, (kaka, dada,mama, baba) jihadhari na uasherati, jihadhari na Mialiko isiyo rasmi inayohusisha jinsia mbili tofauti.. Mtego wa shetani si wewe ufanye tu dhambi ya uzinzi, bali lengo lake ni wewe kukuunganisha na miungu na madhabahu ya huyo unayekwenda kuzini naye.
Na madhara ya kuunganishwa na mtu huyo ni kwamba zile “laana” na “hukumu” anazozibeba na wewe unazibeba..Ndicho kilichowatokea wana wa Israeli walipozini na wanawake wa Moabu, Taifa la Moabu lililaaniwa na wote waliozini na wale wanawake walibeba zile laana.
Ndivyo maandiko yanavyosema katika 1Wakorintho 6:15…
1Wakorintho 6:15 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja”.
Sasa inawezekana ulifanya hayo pasipo kujua, na hivyo ulijiungamanisha na madhabahu za kuzimu. Suluhisho la kwanza si kwenda kuombewa!… bali ni wewe kutubu! Kwa kumaanisha kutofanya machukizo hayo tena. Na baada ya kutubu, hatua inayofuata ni ubatizo sahihi na kisha kudumu katika Imani huku ukijitenga na uovu na vichocheo vyake vyote.
1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).
Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tena tujifunze maneno ya uzima.
Kulikuwa na aina nne za wito ambao Bwana aliwaitwa mitume wake.
Matendo 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi
Sasa nini maana ya kuwa SHAHIDI? Kuwa shahidi maana yake ni kuwa tayari kupitia mateso au kumwaga damu yako kwa ajili ya kumtetea Yule anayekutuma. Hivyo mtu yoyote aliyemwaga damu yake, kwa ajili ya Yesu huyo ni SHAHIDI. Hivyo mitume walijua kabisa hatma yetu ni kumwaga damu tu, huko mbeleni. Na watu kama hawa wanakuwa na nafasi ya juu sana, mbele ya Kristo siku ile watakapofika mbinguni, kwasababu wanakuwa wamepitia sehemu ya mapito yaleyale aliyoyapitia Bwana wao hapa duniani.
Leo tutatazama aina nne(4), za mashahidi wa Kristo. Na wewe pia utajipima upo wapi kati ya hawa na kama haupo popote basi, ufanye bidii uwe katika wingu hili la Mashahidi wa Yesu.
2Wakorintho 11:23 “Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. 24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. 25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini”.
Hata sasa, wapo watu wanateswa kwa namna mbalimbali, wengine wanamwaga damu kwa mapigo, watu kama hawa ni mashahidi wa Bwana. Sawa tu wale mitume wake.
Hili ni kundi la pili ambalo linamwaga damu pia. Ijapokuwa haitaonekana kwa nje lakini rohoni Mungu anawaona kama wamemwaga damu kwa ajili ya ushuhuda wake. Kwamfano tukiangazia kile kisa cha Daudi ambapo wakati Fulani alitamani kunywa maji ya kisima kilichokuwa katikati ya maadui zake wafilisti. Lakini tunaona mashujaa wake watatu waliposikia, waliondoka kisirisiri, wakahatarisha maisha yao, kwenda katika marago ya wafilisti, na kuyachukua yale maji na kumletea Daudi, lakini Daudi hakuyanywa alisema ile ni damu yao na sio maji tena.
2Samweli 23:14 Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu. 15 Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! 16 Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana. 17 Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
Umeona? Maji yamekuwa damu kwasababu ya hatari waliyoingia watu wale. Vivyo hivyo na wewe ujitoapo sadaka kwa ajili ya Bwana, unapohatarisha hata kazi yako, muda wako, ujana wako, ili tu umfanyie Mungu jambo. Ndugu hilo linakuwa sio jambo la kawaida bali ni damu yako unayoimwaga kwake.
Kulikuwa na Yule mwanamke alikwenda kumtolea Bwana sadaka ya senti mbili, lakini maandiko yanasema ndio iliyokuwa riziki yake yote, hajui kama kesho ataiona, pengine hata jana yake hakula. Si ajabu kwanini Bwana aliona ametoa zaidi ya wengine wote. Kwasababu kilichokuwa anakitoa ni uhai wake, na sio sadaka ya kawaida.
Jiulize nguvu zako unazozisumbukia daima unazimalizia kwa nani, je! Ni kwenye kujenga tu, ni kuwekeza, ni kuvaa ni kula? Au ni nini? Vipi kwa Mungu wako, unampa sehemu ndogo tu, ni kweli utapata thawabu? Lakini je! Ulishawahi kufikiria kutenda jambo linalokugharimu wewe kwa Bwana wako? Damu yako unaimwaga wapi?. Watakatifu wa kanisa la kwanza, waliweza kuuza mali zao za thamani na kumtolea Bwana, na sisi tunafanya nini kwa Bwana?.
Hili nalo ni kundi lingine la wanaomwaga damu. Ukisoma Marko 9:43-49, kuna maneno Bwana Yesu alisema, kuhusiana na viungo vyetu. Akasema ikiwa kimojawapo kinakukosesha kikate, ili usikose uzima wa milele. Unajua sikuzote kiungo kikatwapo, ni lazima damu imwagike. Ukiuondoa mguu wako, yapo maumivu, lakini pia ipo damu itakayokutoka.
Viungo vinaweza vikawa ni wazazi, marafiki, ndugu, kazi, mazingira n.k. Ikiwa mzazi anakukosha usisimame vema na Mungu, anakukataza usimwabudu Bwana,au usihubiri huna budi kutomtii kwasababu hiyo, ni kweli utakutana na maumivu, damu itatoka, lakini umemtii Kristo.
Ndicho alichokifanya mfalme mmoja aliyeitwa ASA, yeye alimcha Mungu, na alipoona mama yake anamletea habari za ibada za masanamu, akamwondoa kwenye kiti cha umalkia, japokuwa ni fedheha kubwa alionyesha lakini aliona ni heri kumtii Kristo zaidi ya mwanadamu (1Wafalme 15:11-13)
Hata leo, watu ambao, wameachwa, na viongo vyao vya karibu, au wameviondoa, kwasababu ya Kristo, visiwaghasi, labda ni kazi, ndugu, rohoni wanaonekana kama wamemwaga damu zao kwa ajili ya ushuhuda wa Kristo, na hivyo ni mashahidi wa Bwana. Ndugu usiopoge maumivu, mpende Bwana zaidi ya chochote.
Yesu alipokuwa anaomba, kwa maomboleza na dhiki nyingi kwa ajili yetu muda mfupi kabla ya kusulibiwa, maandiko yanasema jasho lake, likageuka kuwa matone ya damu.
Luka 22:41 “Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, 42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. 44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Hivyo na wote, waombolezao kwa ajili ya haki, machozi yao si bure, wanaokesha kuliombea kanisa, na kazi ya Mungu, wanaowaombea wengine kwa machozi na huzuni, wanadumu madhabahuni kwa Bwana muda mwingi mfano wa Ana (Luka 2:36). Rohoni wanamwaga damu, japo wanaweza wasilijue hilo. Na hivyo ni mashahidi wa Kristo duniani. Thawabu yao mbinguni ni sawasawa na wale waliokatwa vichwa kwa ajili ya Bwana.
Swali ni je! Mimi na wewe tunasimama wapi? Paulo anasema ninakufa kila siku, je! Na sisi tunafanya hivyo kwa Bwana wetu? Bwana atusaidie tuwe maaskari wake kwelikweli, ili siku ile ajivunie sisi mbele za Mungu na malaika zake.
Fanyika shahidi mwaminifu wa Bwana.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
KIFO CHA MTAKATIFU PERPETUA NA FELISTA.
VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
MAMBO YA KUJIFUNZA KWA KLOPA NA MKE WAKE!
Maana Ya Maneno Katika Biblia.
Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tuyatafakari maneno ya neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Sisi kama wakristo hatuna budi kutambua kuwa yapo majira mbalimbali tutapishana nayo angali tukiwa hapa duniani katika safari yetu ya imani. Leo tutaona mojawapo ya majira ambayo, huna budi kupishana nayo sehemu Fulani katika maisha yako. Na watakatifu wengi wanapofikia hatua hii, huwa wanavunjika moyo, na wengine kudhani Mungu amewaacha. Lakini la! Ni moja ya mapito ambayo Bwana anayaruhusu kwasababu zake maalumu.
Na majira hayo ni ya kuondolewa msaada, au usaidizi, au ukaribu, au faraja ya ndugu, ya marafiki, au ya wapendwa. Yategemea na pito la mtu mwenyewe. Na sio kwamba ni wabaya, hapana, ni Mungu tu peke yake kaamua kufunga milango hiyo. Ili abaki yeye na Mungu wake tu, katika chumba cha siri cha rohoni.
Tujifunze kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ambaye, alikuwa mashuhuri sana, na kila mahali alipokwenda alizingirwa na makutano mengi, wakati mwingine alijificha ili watu wasimwone, kwasababu walikuwa wanamsonga sana, hata nafasi ya kula ilikosekana, maelfu ya watu walitamfuata popote alipokwenda.
Lakini kuna majira, hata wale waliokuwa karibu naye (yaani mitume) walimkimbia akabaki yeye peke yake, na hilo aliliona mapema akawaambia wanafunzi wake, ili wasije wakajisikia vibaya.
Yohana 16:32 Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Na ilikuja kutokea hivyo (Soma Marko 14:27-51). Kwasababu ilikuwa ni sehemu ya pito la mwana wa Mungu.
Halikadhalika yupo mtume Paulo, kama tunavyojua yeye ndio alikuwa kama askofu-kiongozi wa makanisa ya mataifa. Alikuwa na marafiki wengi, alikuwa na wapendwa wengi waliomsapoti na kumfariji, katika utumishi wake. Lakini upo wakati alijikuta peke yake. Mpaka akaandika sehemu ya waraka huo na kumtumia Timotheo. Jambo ambalo huwezi dhani linawezekana kwa askofu wa makanisa.
2Timotheo 4:16 “Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. 18 Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina”
Hivyo, hii sio bahati mbaya, ijapokuwa tunazungukwa na wapendwa, na familia, na watoto, na marafiki, lakini kuna wakati Bwana atataka ubaki peke yako na yeye. Na hivyo katika kipindi hicho utakachojikuta, upo mbali nao, au huoni msaada wowote kutoka kwao kama ilivyokuwa kule mwanzo, au hawakuulizii tena, huna mtu wa kucheka naye, kuimba naye. Usijione mpweke, bali mtazame Kristo, elekeza mawazo yako kwake, kwasababu kuna jambo anataka kukufundisha.
Na wakati huo ukiisha, utaona tena anakurejeshea, faraja yako, wapendwa wako, rafiki zako, ndugu zako, na safari inaendelea. Kama alivyofanya kwa Ayubu.
Ayubu 42:10 “Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza. 11 Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja”.
Hivyo weka akiba ya wakati huo, kwasababu hutaukwepa ikiwa wewe ni mwana wa Kristo.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZEA.
HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?
Fahamu mambo ambayo ni wajibu wako kufanya, na yale ambayo unapaswa umsubiri kwanza Roho Mtakatifu akuongoze.
Kama mkristo ni vizuri kuweza kutofautisha mambo ambayo ni wajibu wako kuyafanya, na mambo ambayo utahitaji kwanza uongozwe na Roho Mtakatifu kuyafanya. Ukishindwa kutambua yaliyo wajibu wako, kisha ukasubiri Roho akuongoze, utapotea, halikadhalika ukishindwa kutambua yale ambayo utapaswa usubiri Roho akuongozwe ukayafanya kwa matakwa yako,vilevile utajikuta unapata hasara.
Hivyo haya ni baadhi ya mambo ambayo Mungu anaona ni wajibu wako, na unapaswa uyafanye, na haya usitazamie Bwana atakufunulia uyafanye. Ni mfano tu wa baadhi ya mambo ya mwilini, kwa mfano hakuna mtu anayeweza kusubiri afuatwe na Mungu na kuambiwa ale chakula ndio ale, au anywe maji ndipo anywe, hapana, ni wewe tu mwenyewe utaona unahisi njaa, na hivyo utatafuta kila namna ya kupata chakula na utakula, wala hutamlaumu Mungu kwanini hakumfunulia juu ya chakula . Vivyo hivyo na baadhi ya mambo ya kiroho.
Haya ni mambo ya kuzingatia kuyafanya pindi tu uokokapo kwa maendeleo yako bora ya kiroho.
Kuomba: Maombi hayaepukiki kwa mwamini yoyote, wapo watu wanasema siwezi kuomba bila kuongozwa na Mungu. Ndugu Maombi hayahitaji kuongozwa, yanahitaji kujiongoza kwanza. Kuomba ni lazima iwe desturi yako kila siku, na kiwango cha chini Bwana alichotoa kwa kila mwaminio ni SAA 1.
Mathayo 26:40 Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Hivyo tangu sasa zingatia kujiwekea utaratibu huu, vinginevyo maisha yako ya wokovu yatakuwa ni mazito sana kuyaishi.
1) Kusoma Neno: Neno ndio chakula chetu cha rohoni, kwasababu Bwana alisema, mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa Neno lake. Kama hutajiwekea ustaarabu ya kutenga muda wako kila siku wa kuyatafakari maandiko, ukasubiri ipo siku Bwana ataanza kukufunulia uanze kusoma kitabu gani, na gani..Utapotea ndugu yangu. Hii njaa ya kiroho tuliyonayo siku hizi za mwisho, tutasubiri kweli, tuletewe chakula mdomoni?. Ni sisi wenyewe kuchangamka kusoma biblia daima, haijalishi wewe ni mchungaji umesoma biblia yote mara saba, au umeokoka leo,wote tunapaswa tuwe watu wa kusoma na kujifunza Biblia.
2) Mifungo ya mara kwa mara: Tunaposema mifungo ya mara kwa mara tunamaanisha ile mifungo ambayo, kila mmoja anaweza kuistahimili, ya saa 24, au siku mbili, au tatu, bila kula. Mifungo inakurahisishia wigo wako wa kimaombi, na kuivuta roho yako juu, ili iweze kukutana na uso wa Mungu kirahisi. Kwahiyo usingoje, kusikia sauti Fulani ikuambie anza kufunga. Anza kujijengea utaratibu huo wewe mwenyewe, walau kila mwezi uhesabu kuna siku kadhaa umefunga.
3) Ibada: Halikadhalika ukikoka, usisubiri Bwana akuambie nenda kanisani ukaniabudu. Au anza kuniimbia sifa. Ni wajibu wako, ‘kumvukizia’ Mungu wako uvumba wa shukrani, sifa, matoleo, nyimbo, ushirika wa meza yake n.k. mara nyingi kwa jinsi uwezavyo. Wengine watasema ipo changamoto ya makanisa, ndio hiyo isiwe sababu ya kutulia tu nyumbani, nenda kwingine, pakiwa pabaya tafuta kwingine, hatimaye Mungu ataiona nia yako, na kukupa mahali sahihi pa kutuliza moyo wako. Maana kila atafutaye huona.
4) Kushuhudia habari za Yesu kwa wengine: Kuwaeleza wengine Habari za Yesu, ni wajibu wetu sote, aidha umeokoka leo, au umekomaa kiroho. Kushuhudia haihitaji ujuzi mwingi wa kimaandiko kama wengi wanavyodhani, hata kueleza uzuri wa Kristo na ushuhuda wako kwa mwingine tayari ni injili hiyo.. Paulo alipookoka, tu baada ya kubatizwa hapo hapo akaanza kuwaeleza wengine habari za Yesu na uchanga wake wote.
Matendo 9:18 “ Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.21 Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani?”
HAYA NI MAMBO AMBAYO UNAPASWA USUBIRI, UONGOZWE NA ROHO
1) Kuanza huduma: Huduma ni kama kituo rasmi cha kuwasaidia watu kiroho, kwa ule wito uliowekewa na Mungu ndani yako. Na hapa, ni kuwa makini sana, kwasababu mtu akishaona amekoka, au anayo-karama Fulani, anachowaza ni kwenda kuanza kanisa, au akishajiona anao-ushawishi Fulani wa kuwakusanya watu anakwenda kuanza huduma. Ndugu hiyo ni hatari. Chukua mfano rahisi, leo hii wapo watu ambao wanaujuzi Fulani, labda tuseme wajenzi, lakini kama hawana elimu ya shuleni iliyothibitishwa hawawezi kupewa usimamizi wa majengo makubwa wayasimamie, kwasababu wanajua hata kama watakuwa wanaelewa aina nyingi za michanga na matofali, lakini bado kuna mambo watayakosa tu, ya ndani yahusuyo ujenzi, ambayo yanapatikana darasani tu, na hivyo kuna hatari ya kupata hasara kubwa mbeleni kwa mtu kama huyo kupewa usimamizi.
Halikadhalika, Mungu kumuita mtu katika huduma, si jambo atakalolikurupukia, bali atakuandaa, kwa kipindi Fulani katika shule yake ya Roho Mtakatifu (hatulengi shule ya vyuo vya biblia). Na hivyo, mwishoni kabisa ndio atakuita ufanye jambo ili isiwe hasara kwa watu wake. Kwahiyo usiwe mwepesi wa kutaka kuanza jambo, kuwa mshuhudiaji, huku ukiwa chini ya uangalizi . Mtume Paulo japokuwa alikuwa anashuhudia habari za Kristo kwa ushujaa mwingi lakini alisubiri kwanza mpaka wakati wa Bwana.
Matendo 13:2 “Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. 3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao. 4 Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro”
2) Mifungo mirefu: Ipo mifungo ya kutokula na kunywa kwa kipindi kirefu kama wiki 2, mwezi, siku 40 n.k. Katika hali kama hizi, usijiamulie tu mwenyewe kwa akili yako kuiingia. Unawezi kupata matatizo au kifo kabisa. Kwasababu hiyo inahitaji ROHO wa Mungu kukuongoza. Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu.. aliongozwa na Roho, hakujiamulia tu kuanza mifungo hiyo.
Luka 4:1 “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, 2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa”
Hivyo zingatia haya, na Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
3) Unayefanya naye mapatano, au maagano: Maagano/mapatano yapo ya namna mbalimbali, yapo ya kipindi kifupi na mengine ya maisha, mfano, unapotaka kuingia katika ndoa, huna budi kumshirikisha Roho Mtakatifu, akupe mwongozo wake, ndio hapo inakugharimu utangulize maombi. Unapochagua viongozi wa kusimamia kundi, hupaswi kuwaza kwa akili zako, bali jipe muda wa Roho Mtakatifu kukufunulia. Ilimpasa Bwana afunge usiku kucha kuomba mwongozo wa wanafunzi wa kutembea nao. Unapotaka kutumika na mtu, usiyemjua chukua muda wa kumuuliza Roho Mtakatifu. kwasababu yapo makosa mengi ambayo hata katika maandiko yalitokea kwa kukosa kumshirikisha Mungu kwanza. Wakati fulani mfalme Yehoshafati alitaka kutumika na mfalme Ahabu, na ilikuwa nusu afe, kwasababu alifanya mapatano na mfalme mwovu.(2Nyakati 18:1-25)
Yoshua aliingia katika mapatano na maadui zake, ambao Bwana alimwambia awaangamize, na ndio hao wakaja kuwa mwiba kwa wayahudi baadaye. Hiyo yote ni kwasababu hawakuwa tayari kumsikiliza kwanza Roho Mtakatifu. Hivyo jambo lolote la kiroho, ambao unaona linahitaji umakini mkubwa, subiri kwanza uongozo wa Roho Mtakatifu. Usiangalie, zawadi, uzuri, utajiri, au chochote. (Yoshua 9:1-27)
Bwana akubariki.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.
Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.