Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
USIRUDI NYUMA KWA KUITUMAINIA HAKI YAKO.
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
NI LAZIMA KUISHIKILIA IMANI MPAKA MWISHO.
Mwandishi na Uchambuzi wa kitabu cha wafilipi
Kama pale mwanzo kinavyojitambulisha “Waraka wa Paulo mtume kwa wafilipi”.
Paulo ndiye mwandishi wa kitabu hiki. Ni moja ya nyaraka ambazo Paulo aliziandika akiwa kama mfungwa, aidha kule Rumi.
Maudhui makuu ya waraka huu mfupi wenye sura nne(4) yalikuwa ni kuwatia moyo watakatifu na kuwahimiza waiendeleze furaha ya Mungu ndani yao,bila kukwamishwa na dhiki za aina yoyote, lakini pia sehemu ya pili ni kuwataka wapige hatua katika mwenendo wao ndani ya injili waliyoipokea.
Tukianza na hiyo sehemu ya kwanza:
Paulo anahimiza watakatifu kufurahi katika dhiki zote, ikizingatiwa kuwa Kanisa hili lilishuhudia vifungo na mapigo mengi ya Paulo. Kama tunavyosoma kwenye Matendo 16:16-40, Kule ambapo Paulo na Sila walipigwa sana na kutupwa gerezani, biblia inatuambia kulikuwa ni huku Filipi. Lakini hata katika waraka huu bado anashuhudia kuwa dhiki zake, zimekuwa wazi kwa maaskari, na watu wote wa huko (1:12-13).
Hivyo Paulo alijua watu wa Filipi huwenda wakawa na huzuni nyingi juu yake, au juu ya injili, kutokana na dhiki nyingi walizoziona kupitia yeye.
Lakini hapa anawaeleza kuwa yeye anafuraha sikuzote katika Kristo.
> Anaendelea kueleza furaha yake haiathiriwi na watu wanaomzushia fitna ili apitie mateso, maadamu anayeathirika ni yeye si Kristo. Basi bado anafurahi..(1:17-18)
> Anasema hata akihukumiwa kifo kwa ajili ya watakatifu, bado furaha yake itazidi zaidi wala haiwezi kuathiriwa..
Wafilipi 2:17-18
[17]Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
[18]Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.
Hivyo anawahimiza pia na wafilipi wafurahi kama yeye, wala wasione huzuni kwasababu ya dhiki hizi, kwasababu tumewekewa kuwa sehemu yetu katika ushuhuda wa injili.
Wafilipi 1:29
[29]Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;
Hizi ni sehemu nyingine kadha wa kadha Paulo akihimiza jambo hilo hilo,
Wafilipi 3:1
[1]Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana.
Wafilipi 4:4
[4]Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
Sehemu ya Pili:
Katika sehemu ya pili Paulo anahimiza watakatifu kuwa na mwenendo unaipasa injili waliyopokea. Na hiyo ni ili wasiwe na ila na lawama,na udanganyifu. Kuonyesha kuwa injili, inayo na taratibu zake..Sio kuamini tu na kusema nimeokoka…bali pia kutii agizo lake.
Wafilipi 1:27
[27]Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;
Anaendelea kusema watakatifu wana wajibu wa kunia mamoja, kutenda mambo yote bila majivuno,wala manung’uniko, wala mashindano, wanapaswa kutenda yote bila ubinafsi bali na ya wengine..
Anasisitiza watakatifu wanapaswa wawe wanyenyekevu, wenye nia ya Kristo..ambaye yeye hapo mwanzo alikuwa kama Mungu lakini alijishusha kwa kukubali kuachia nafasi yake, akawa kama mtumwa, akajinyenyekeza mpaka mauti ya msalaba,lakini Mungu akamkweza zaidi ya vitu vyote..Na sisi tulioipokea injili tunapaswa tuwe na nia hiyo hiyo ya unyenyekevu.(2:1-16)
Anasisitiza zaidi Wakristo wanapaswa wawe wapole, pia wawe waombaji na wenye shukrani.(4:5)
Halikadhalika ni wajibu wetu sote kuutumiza wokovu tulioupokea kwa kuogopa na kutetemeka, kwasababu ndiye Mungu atendaye kazi ndani yetu.(2:12-13)
Pamoja na hayo Watakatifu wana wajibu pia wa kuyahakiki mambo yote yaliyo mazuri na kuyaiga, (2:1-2)
Wafilipi 4:8
[8]Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Lakini pia anawatahadharisha kujiepusha na wahubiri wa uongo akianzana na wayahudi (watu wa tohara), ambao wanahubiri wokovu kwa njia ya torati zaidi ya ile tuipatayo ndani ya Kristo Yesu kwa njia ya imani. (3:1–16,)
Pamoja watumishi ambao fundisho lao ni la mambo ya duniani tu, na sio yale ya kumwelekeza mtu mbinguni (3:17-21).
Mwisho, Paulo anatoa salamu zake, na shukrani kwa huduma ya utoaji kanisa hilo lililomfanyia, na linaloendelea kumfanyia.
Hivyo kwa hitimisho, waraka huu maudhui kuu ni kuwafariji watakatifu wafurahi katika mambo yote, tukizingatia tunda la Roho ni furaha. Yesu alisema tufurahi na kushangalia pale tunapoudhiwa, kwa ajili ya jina lake. Hivyo, hakuna eneo lolote furaha ya Mungu ndani yetu ,inastahili kukatishwa. Tupitiapo magonjwa kama Epafrodito(2:25-30), shida, njaa, tumefundishwa kuyaweza yote ndani ya Kristo(4:12-3). Hivyo furaha yetu haiwezi kuathiriwa..Ilinde furaha yako.
Lakini anahimiza mwenendo upasao injili. Kwamba huo utaweza kufanikiwa pale tunapokubali kuwa na nia kama ile ya Kristo, ya unyenyekevu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Kama kinavyoanza kwa utambulisho wake, ‘Waraka wa Paulo mtume kwa Wakolosai’.
Paulo ndiye mwandishi wa waraka huu.
Madhumuni makuu ya waraka huu ulikuwa ni kuwasisitiza Wakolosai jinsi Yesu alivyo UTOSHELEVU WOTE, ambaye kwa kupitia yeye Uumbaji wote umekamilishwa ndani yake, lakini si hilo tu bali na utimilifu wote wa ki-Mungu unapatikana ndani yake, pamoja na hazina zote za hekima na maarifa.
Akiwa na maana kuwa mtu akimpata Kristo, hahitaji kitu kingine cha pembeni kumkamilisha yeye, Utoshelevu wote upo kwake.
Hivi ni vifungu mama,
1:15-17
“15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye”.
2:3
ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.
2:9
“Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili”.
Anaeleza kwa undani katika sura ile ya pili, kwamba ni kutokana na uwepo wa watu waliolivamia kanisa na kuwadanganya kwa maneno ya ushawishi, nia zao ni kuwafanya mateka kwa elimu isiyo na matunda, ya mapokeo ya kibinadamu, yasiyo ya Kristo (2:8). Kwamba mtu akishika hayo, ndio utimilifu wote unapatikana.
Vilevile kuonekana kwa baadhi ya desturi za kiyahudi ndani ya kanisa, kama vile kushika sikukuu, tohara, sabato, na mwandamo wa mwezi. Vikidhaniwa kuwa vitu hivyo vinaweza kuleta ukamilifu wote pamoja na Kristo (2:11-23)
Na pia kuzuka kwa ibada bandia za kuabudu viumbe vya rohoni (malaika), kwa mawazo kuwa mtu ataupokea ukamilifu.(2:18)
Paulo anaeleza yote hayo hayana wokovu, isipokuwa kwa njia ya haki tuliyoipokea kwa msalaba wake uliofuta hati ya mashtaka yetu, kwa mateso yake pale msalabani ambayo kwa kupitia njia hiyo tumepokea msamaha wa dhambi, pale tu tunapoamini na kubatizwa (2:12-17)
Sehemu ya tatu Paulo anaeleza kwamba kuamini ni pamoja na kuuvaa utu upya wa Kristo. Hivyo huyu mtu hatarajiwi kuendelea kuishi hivi hivi tu, kisa Kristo amemkamilisha kwa kila kitu, bali anapaswa aenende kwa Kristo mwenyewe, ayafikiri yaliyo juu, (3:1-17),
Kwa namna gani?
Kwa kuzifisha tabia za mwilini, kama uasherati, uchafu, kutamani, mawazo mabaya, ghadhabu, matusi. Lakini pia kujivika utu wema, moyo wa rehema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, kusameheana, upendo, ibada. Vilevile si tu katika mambo ya rohoni , bali mpaka kwenye ngazi za kifamilia, kwamba wake kuwatii waume zao, na waume kuwapenda wake zao, na watoto kuwatii wazazi. Hizo ndio tabia za utu mpya.
Katika sura ya 4.
Bado Paulo aendelea kueleza huo mwenendo ndani ya Kristo, unapaswa uonekane mpaka kwa mabwana, kwa watumwa wao. Kwamba mabwana wawape watumwa haki zao, Lakini pia watakatifu wote, wanapaswa kudumu katika maombi, na kuenenda kwa hekima kwa watu wasioamini, katika usemi bora, na kujifunza kuukomboa wakati.
Na mwisho.
Paulo anawasilisha salamu za washirika wenzake wa injili, kwa Wakolosai ikiwemo, Epafra, Luka, Dema, marko, Aristarko, Yusto.
Hitimisho.
Kwa ufupi waraka huu, hueleza kwamba utoshelevu wote upo ndani ya Kristo tu na sio zaidi ya hapo, hatuhitaji kitu kingine cha pembeni kutukamilisha sisi, Lakini ni wajibu wa huyu mkristo kutembea katika maisha mapya ndani yake. Kwasababu mambo yote mawili yanakwenda sambamba hayatengani. Kristo huokoa na kutakasa wakati huo huo. Unapookolewa, saa hiyo hiyo umevikwa utu upya. Huwezi kuendelea katika dhambi.
Ni kipi cha ziada tunachoweza kujifunza katika waraka huu?.
Maombi ya Paulo na Eprafa yasiyokoma kwa kanisa hili(1:3, 9, 4:12):
Hatuna budi kujijengea desturi ya sikuzote kuliombea kanisa la Bwana, hususani mahali tulipo, pamoja na watakatifu wengine tuwajuao. Kwasababu kusimama kwa kanisa hutegemea sana maombi yasiyokoma.
Bwana akubariki. ||kiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii. Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,
Rudi Nyumbani
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE MASHUJAA 37 WA DAUDI.
Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu (Zekaria 13:7-9)
Kitabu hichi kama kinavyojitambulisha, “Waraka wa Paulo kwa Warumi” mwandishi wake ni Mtume Paulo.
Kitabu hiki alikiandika akiwa Korintho mahali palipoitwa Kenkrea (Warumi 16:1)
Tofauti na nyaraka nyingine ambazo Paulo aliziandika kwa makanisa ambayo alikuwa tayari ameshayatembelea/ameyapanda hapo nyuma. Waraka huu tunaonyeshwa Paulo hakuwahi kufika Rumi. Lakini alisikia mwitikio wao wa injili, hivyo likawa ni tamanio lake pia awafikie na wao, lengo likiwa sio kupanda juu ya msingi wa watu wengine bali wajengane kiimani.(1-18),
Na kweli tamanio lake tunaona lilikuja kutimia baadaye, kama tunavyosoma kwenye kitabu cha matendo ya mitume, katika ile ziara yake ya mwisho kama mfungwa, alifika Rumi, na huko akafanikiwa kuhubiri injili sawasawa na tamanio lake (Matendo 27-28).
Hichi ni kitabu kinachoeleza misingi ya imani ki-mpangilio . Kuanzia asili ya wokovu wetu, haki ya Mungu, na mwenendo wa kikristo. Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana kwa mkristo yoyote kukielewa vema kitabu hichi.
Baada ya Paulo, kueleza tamanio lake la kuwafikia katika utangulizi wake, tunaona katika mistari hiyo anasisitiza kwanini afanye hivyo? Ni kwasababu ya ‘Nguvu ya Injili yenyewe’, Akisema Injili ni uweza wa Mungu uuletao wokovu. Na hivyo haionei haya kuihubiri kwa watu wote..kwa wayahudi na watu wa mataifa pia.
Sehemu ya pili Paulo anaeleza jinsi wanadamu wote walivyopungikiwa na utukufu wa Mungu kuanzia watu wa mataifa ambao wameshindwa kuitii kweli ya Mungu iliyofunuliwa kwao kwa mambo yake yaliyo dhahiri kabisa yanayotambulika hata pasipo sheria, kwamba mambo ya asili yanafundisha haki ya Mungu, lakini walikataa kutii. Vilevile na wayahudi pia ambao walikuwa na sheria lakini walishindwa kuyatenda yote kulingana na yaliyoandikwa. Hivyo hakuna hata mmoja mwenye haki, wote wamewekwa chini ya hukumu ya ghadhabu ya Mungu, kwa kushindwa kutenda haki yote.
Kwa kuwa wanadamu wameshindwa kuwa wakamilifu, Paulo anaeleza njia ambayo Mungu ameitoa kwa mwanadamu kuweza kuhesabiwa haki. Ni njia ambayo inadhihirishwa bila matendo ya sheria, tunayoipata kwa kumwamini tu Yesu Kristo. Yaani pale mtu anapomwamini Bwana Yesu kwamba kifo chake kimeleta ukombozi wa roho yake, basi mtu huyo anakuwa amehesabiwa haki kuwa ni Mtakatifu mbele za Mungu.
Kulithibitisha hilo Paulo akaendelea kueleza kwa mfano wa Ibrahimu jinsi Mungu alivyomhesabia haki bila sheria yoyote, na kwamba sisi pia tutahesabiwa kwa njia hiyo hiyo.
Katika sehemu hii Paulo anaeleza maisha baada ya kuhesabiwa haki, kwamba mkristo anapaswa aendelee kutakaswa na kuwa kama Kristo. Lakini kutokana na mashindano kati ya mwili na roho. Ili aweze kuushinda mwili anapaswa ajifunze kuishi kwa Roho, kwa kuruhusu utendaji kazi wake ndani yake. Maneno hayo ameyarudia pia katika waraka wake kwa Wagalatia (Wagatia 5:16). Kwamba mtu anayeenenda kwa Roho kamwe hawezi kuzitimiza tamaa za mwili.
Lakini mbele kidogo anaendelea kuhimiza upendo wa milele wa Mungu, uliodhihirishwa kwetu kupitia Yesu Kristo, ambao hauwezi kutenganishwa na kitu chochote tukijuacho duniani au mbinguni.
Kwenye sura hizi, Paulo anaeleza uhuru wa Mungu wa kuchagua, na siri iliyokuwa nyuma ya Israeli kukataa injili. Anaeleza mpango wake wa wokovu kwa mataifa na waisraeli, kwamba iliwapasa wao wakatae injili ili sisi watu wa mataifa tuipokee injili. Na hivyo anaeleza sisi pia tunapaswa tuupokee wokovu kwa unyenyekevu wote kwasababu tusipokaa katika kuamini tutakatwa, kama wao walivyokatwa.
Paulo anaeleza jinsi tunavyopaswa kuitoa miili yetu kama dhabihu iliyo hai takatifu yenye kumpendeza Mungu, tunawajibu wa kupendana sisi kwa sisi, tusiwe watu wa kulipa kisasi, tuishi kwa heshima, tuhudumiane katika karama mbalimbali tulizokirimiwa na Mungu, tutii mamlaka zilizowekwa, vinywa vyetu vitoe baraka, tumtumikie Mungu kwa bidii, tudumu katika sala, tuishi kwa amani sisi kwa sisi, pia tuweze kuchukiliana katika viwango mbalimbali vya imani bila kuhukumiana.
Kwa ufupi sura hizi zinaeleza tabia zetu zinapaswa ziweje baada ya wokovu.
Paulo anaeleza mpango wake wa kuwafikia Warumi pindi atakapokuwa anasafiri kwenda Spania kuhubiri injili. Akiomba akumbukwe katika maombi dhidi ya watu wabaya, na mwisho anatoa salamu kwa watakatifu wote walio Rumi, pamoja na angalizo kwa watu waletao fitna katika injili waliyoipokea wajiepushe nao
Kitabu hichi kinaeleza
Haki ya Mungu ikoje, ambapo hapo mwanzo ilidhaniwa inapatikana kwa sheria au matendo ya mwanadamu, kumbe sio, hayo yalishindwa bali kwa njia ya Yesu Kristo, lakini pia kinaeleza namna ambavyo tunaupokea wokovu huo kwa neema kwa njia ya Imani, na pia jinsi Mkristo anavyopaswa aishi kulingana na wokovu alioupokea. Kwamba sio kwasababu amehesabiwa haki bure bila matendo, basi aishi maisha kama atakayo, hapana vinginevyo atakufa.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.
Rudi Nyumbani
Silaha ya Mwisho mwisho kabisa ya adui kumshambulia Mtu ni “ULIMI WA UOVU”.. Ukiona Maneno ya uongo kuhusu wewe, au ya vitisho au ya uchonganishi yanatembea huku na huko basi fahamu kuwa adui ndio yupo katika hatua za mwisho mwisho, kukuacha!..(Ni wakati wa kumaliza jaribu).
Na kama ukiweza kusimama katika hiko kipindi bila hofu, wala kutetereka wala kurudi nyuma, basi shetani unaweza usimwone tena baada ya hapo, kwa kipindi kirefu sana.
Mfano katika biblia tunamwona Nabii Yeremia,
Adui alimtafuta mara nyingi kwa njia mbalimbali ili amnyamazishe asitoe unabii, lakini kila alichojaribu ili kumzuia Yeremia asitoe unabii, kilishindikana, na ndipo akatumia silaha yake ya mwisho ya NDIMI ZA UOVU, ili yamkini amtishe Yeremia, lakini pia haikusaidia,
Yeremia 18:18 “Hapo ndipo waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njoni, na TUMPIGE KWA NDIMI ZETU, wala tusiyaangalie maneno yake yo yote.
19 Niangalie, Ee Bwana, ukasikilize sauti ya wanaoshindana nami”.
Wakati huo kilitokea kikundi kiovu na kuanza kumtisha Yeremia kwa maneno mengi, na pia kumzushia mambo mengi na zaidi ya yote, ya uchonganishi na kumchafua mbele ya Mfalme, ili tu Yeremia akamatwe asiendelee kutoa unabii.
Yeremia 38: 4 “Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari.
5 Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lo lote kinyume chenu”.
Mtu mwingine aliyepigwa kwa NDIMI OVU ni nabii Danieli, soma Danieli 6..
Sasa kwanini Adui, aiweke hii silaha ya ulimi kama chaguo lake la mwisho?… Ni kwasababu anajua ulimi wa mtu unaweza kuwasha moto mkubwa, na kama mtu hatakuwa na Imani ya kutosha basi anaweza kuanguka kabisa…
Yakobo 3:6 “Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”
Hivyo shetani anaweza kukuwashia tu moto kupitia ulimi wa mtu au ndimi za watu, na moto huo ukawa mkubwa sana, kiasi kwamba kama huna imani na ujasiri wa kutosha, unaweza kurudi nyuma kabisa.
Shedraka, Meshaki na Abednego walijikuta wapo katika tanuru la Moto, kwasababu tu ya baadhi ya watu waliotumia ndimi zao kupeleka mashitaka kwa mfalme kuwa hawataki kuisujudia ile sanamu.(Danieli 3:8-12).
Danieli naye alijikuta katika tundu la simba kwasababu tu ya vinywa vya watu, na Yeremia naye alijikuta katika lile shimo refu lenye giza lililojaa matope kwasababu ya maneno ya watu(Yeremia 38:6)..
Lakini wote hao walishinda, kwani moto ule uliokusudiwa juu yao uliwala maadui zao, na mashimo yale na matundu yale yaliyokusudiwa juu yao yaliwaharibu maadui zao, lakini kama wangetetemeka na kuogopa na kurudi nyuma bila shaka wangepotea kwa kuharibiwa na ibilisi!.
Na sisi hatuna budi kusimama Imara bila hofu, kwa ujasiri mwingi pale ambapo adui anatumia NDIMI za watu kama silaha yake…
Hiko ni kipindi cha kuwa na imani na ujasiri….mipango inapopangwa ya vitisho au uchonganishi, havitasimama endapo wewe utasimama.
Ni wakati kusimama na kuamini huku tukiomba, na silaha za ndimi zao zitaanguka, na Bwana atatukuzwa.
Ifuatayo ni mistari inayozungumzia hatari ya NDIMI ZA UOVU…
Zaburi 57:4 “Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.”
Zaburi 64: 2 “Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona”
Zaburi 140:1 “Ee Bwana, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri.
2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita.
3 Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao”.
Lakini pamoja na kwamba adui anatumia ndimi kutushambulia, vile vile na sisi tunaweza kutumia ndimi hizo hizo, kumharibu.
Mithali 18:21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake”
Tunampiga shetani kwa ndimi zetu, kwa njia ya KUOMBA, na hususani maombi yanayohusisha mfungo.
Bwana atubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Swali: Kughafilika maana yake nini?
Jibu: Turejee…
Wagalatia 6:1 “Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo”
Kughafilika maana yake ni “Kuchukuliwa na jambo fulani baya”.. Mtu aliyeghafilika anakuwa amezama katika Uovu na anakuwa haoni tena kama ni kosa kufanya uovu ule (kiasi kwamba ufahamu wake unakuwa kama umefungwa)..
Kwamfano mtu aliyezama katika anasa ambao hapo kwanza alikuwa anaukataa, mtu huyo anakuwa “Ameghafilika katika anasa za dunia” n.k
Biblia inatufundisha kuwa watu kama hawa ni kuwarejesha kwa roho ya upole, Maana yake kwa kuwafundisha taratibu na kuwaombea mpaka watakaporudi katika mstari, na hiyo ndiyo tafsiri ya kuchukua mzigo wa mwingine, (yaani ni kumrejesha katika kweli, mtu aliyekengeuka, na si kumwombea baada ya kufa!)
Mtu aliyekufa hakuna mtu anayeweza kuuchukua mzigo wake wa dhambi, bali atasimama nao mbele ya kile kiti cha hukumu..
Wagalatia 6:5 “Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe”
Na sio tu mtu, bali hata Bwana mwenyewe hatamchukulia mtu mzigo wa dhambi, baada ya kifo….
Yohana 8:21 “Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; NANYI MTAKUFA KATIKA DHAMBI YENU; mimi niendako ninyi hamwezi kuja…….
24 Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba MTAKUFA KATIKA DHAMBI ZENU; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, MTAKUFA KATIKA DHAMBI ZENU”.
Je umeokoka?.. una uhakika Bwana YESU akirudi leo utakwenda naye?.
Maran atha..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Uchambuzi na Mwandishi wa kitabu cha Wagalatia
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
Je, kama hauna ubatizo sahihi hauwezi kuwa na Roho Mtakatifu?
Ni uchafu gani unaozungumziwa katika Wagalatia 5:19?
Kila mahali pana mamlaka yake, na mamlaka hizo huwa ni wajibu kwa walio chini yake kuzitii. Kwamfano katika familia Mungu ameweka mamlaka, Baba awe kichwa, na mama msaidizi wake, hivyo ni wajibu wa watoto kuwatii wazazi wao . Familia haiwezi kusimama,.kama mtoto atataka nafasi ya baba, kwamba yeye ndio atoe maamuzi ya mwisho, au ajiamulie la kufanya, awapangie wazazi wake majukumu ya ndani. hilo haliwezekani.
Vilevile katika ngazi ya utawala wa kidunia, Mungu kaziweka mamlaka na anataka watu wote wazitii, kwasababu hazijaamuriwa na mwanadamu bali yeye Mungu mwenyewe..
Warumi 13:1-2
[1]Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
[2]Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.
Tito 3:1-2
[1]Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; [2]wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.
Sasa hizi ni mamlaka za kidunia. Zipi kuhusu Mungu, unadhani hana mamlaka?
Mungu pia ameweka mamlaka yake duniani, ambayo ni kuu kupita hizo zote, na kupitia hiyo huwahudumia watu wake. Na anataka tuitii na kuitetemekea kwasababu ni yeye mwenyewe atendaye kazi kupitia hiyo.
Je mamlaka hiyo kaiweka kupitia nani?
Bila shaka kupitia wachungaji wetu/waangalizi wetu, ndani ya kanisa
Ni vema kufahamu kuwa kiongozi yoyote wa kiroho (anayeisimamia kweli). Hakujiteua mwenyewe kwenye nafasi hiyo. Mitume wa Yesu hawakujichagua wao. Bali walichaguliwa na Mungu mwenyewe.
Mtu yeyote aliyepewa maono ya kuanza kanisa, na ukajikuta upo chini yake, au kateuliwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani ya kanisa (Matendo 14:23), Huyo ni wa kumtii sana. Kama vile unavyowatii watawala au mazazi wako kwenye familia, haijalishi atakuwa na mapungufu kiasi gani, au umri wake ni mdogo au mkubwa kiasi gani, awe mwenye uwezo au asiye na uwezo kiasi gani.
Kwanini uwaheshimu.
Hivyo wajibu ni wako kurudisha moyo wa upendo, na kuwasikiliza.
1 Wathesalonike 5:12-13
[12]Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; [13]mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.
Hivyo ni wajibu kuonyesha moyo wa kunyenyekea kwao.
Waebrania 13:17
[17]Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
Hapo kwenye Waebrania 13:17b anasema..
..ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi
Na matokeo yake utendaji kazi ndani ya kanisani utakuwa hafifu. Ukishaanza kuonyesha tabia ya kutosikiliza unachoelekezwa, unapewa jukumu hutekelezi, hurudishi mrejesho, unafanya tofauti na wengine, yeye anataka uende kulia wewe unaenda kushoto, , yeye anafundisha hiki wewe unafundisha kile. Fahamu kuwa jambo hilo litamhuzunisha kiongozi wako. Na hivyo kupelekea hamasa ya kuhudumu kupungua. Na madhara yake ni kuwa Mungu kukata utendaji kazi wake mahali hapo,
Wakati ule Haruni na Miriamu dada yake. walimnenea Musa maneno mabaya kwasababu na mke wake ambaye hakuwa myahudi. Mungu aliwaadhibu kwa kumpiga ukoma Miriamu kwasababu tu hiyo ya kutoonyesha adabu kwa mtumishi wake.
Hesabu 12:7-8
[7]Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
[8]Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Ni kosa kumnenea vibaya mchungaji wako. Epuka masengenyo na uasi na matabaka ndani ya kanisa. Uonapo kosa mwombee, au mfuate mweleze uwapo naye peke yake. Hilo litamjenga zaidi ya kutoa malaumu na manung’uniko. Adui hutumia sana njia hii kuleta mafarakano na magomvi, na mapigo kanisani.
Mheshimu mchungaji wako, zaidi ya raisi wa nchi kwasababu yeye ni balozi wa mbinguni na Mungu atakuinua (1Petro 5:1-6)
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
Ipi tofauti kati ya KUHANI na MCHUNGAJI.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Rudi Nyumbani
Wazia jambo hili, raisi amepewa taarifa na wataalamu wake wa hali ya hewa kwamba kuna kimbunga kikubwa kinatokea bahari.
Hivyo akachukua hatua ya kuwatahadharisha wananchi wake wasifike maeneo yote ya pwani. akawaelekeza na namna ya kujilinda, na mazingira yote hatarishi, akawajuza na madhara ambayo tayari kimbunga hicho kimeshaleta, akawaonya sana wakae ndani mpaka hicho kipindi chote cha hatari kitakapokwisha.
Lakini cha kushangaza kesho yake wakaonekana watumishi wa raisi na mawaziri , pamoja na watumishi wote wa serikalini wakiwa ufukweni wakiogolea na kufurahi na kustareheka..kana kwamba hakuna hatari yoyote mbeleni.
Unadhani ni wazo gani litajengeka kwa wananchi juu ya raisi wao?
Watasema raisi ni mwongo. Ametulaghai, mbona mamlaka yake haichukui hatua ya janga lililotangazwa?
Lakini heri na hapo, unadhani raisi naye atajisikiaje moyoni, kwa wale watu waliomtendea hivyo?
Sasa hilo ndilo watu wanalolifanya kwa Mungu sasa mpaka anaonekana ni mwongo.
Neno la Mungu linasema…
1 Yohana 5:10-12
[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
[11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
[12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
Mungu alimtuma Yesu duniani, kuushuhudia ulimwengu kuwa una dhambi, Na mwana wake kuja duniani ni kwa lengo hilo kuu la kuwaokoa watu dhambini.
Hivyo Mungu akamshuhudia kwa sauti kutoka mbinguni, kwa ishara na miujiza mingi,.kwa Roho Mtakatifu aliyetuachia, lakini bado watu wakapuuzia, wakaendelea na mambo yao. Sasa huko ndiko kumfanya Mungu mwongo. Yaani kufikiri kuwa sisi hatukutenda dhambi, tunamfanya yeye kuwa mwongo.
1 Yohana 1:10
[10]Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
Hivyo mtu yeyote anayekataa injili, ni kwamba anamfanya yeye aonekane mwongo. Ushuhuda wake ni uongo, kazi aliyoifanya ni bure, ni kuthibitisha mtu anaweza kuishi tu mwenyewe apendavyo na akawa na maisha ya milele?
Je! umempokea Yesu, kama Bwana na mwokozi wa maisha yako. Kama ni La! ndugu Kamwe usimfanye Mungu mwongo.
Amini ushuhuda wake kupitia mwana wake kwasababu ni kweli usipookolewa na yeye. Uzima wa milele haupo ndani yako. Dhambi ipo, na bado itaendelea kuwepo juu yako, hata kama utakuwa na matendo mazuri kiasi gani.
Fanya uamuzi sasa ya kuokoka. Hukumu ipo mbele na inatisha.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JINSI YA KUUHARIBU UJANA WAKO.
NI NJIA GANI MTU AITUMIE AWEZE KUSHINDA TAMAA NA VISHAWISHI?
NINYI AKINA BABA MSIWACHOKOZE WATOTO WENU
Rudi Nyumbani
SWALI: Je! Paulo, alikuwa na injili yake, tofauti na wengine? sawasawa na (Warumi 2:16)
Warumi 2:16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
JIBU: Katika habari hiyo mtume Paulo hakumaanisha kwamba anayo injili nyingine ya kipekee tofauti na mitume wengine wa Kristo, na kwamba ya kwake tu ndiyo Mungu atakayoitumia kuzihukumu siri za wanadamu.
Hapana mitume wote walikabidhiwa “injili moja”. Nayo ni kushuhudia wokovu ulioletwa duniani na mtu mmoja tu, ambaye ni YESU KRISTO, kwa lile tendo la kufa na kukufuka kwake kama fidia ya dhambi za ulimwengu, ambapo mtu akiamini basi amepokea ondoleo la dhambi na uzima wa milele. Na mtu yeyote ambaye hatamwamini huyu basi hukumu ya Mungu inakuwa juu yake.
Kwahiyo Paulo kama mmoja wa hao waliokabidhiwa injili hiyo, alikuwa na ujasiri kuwaeleza watu wale wa Rumi, kwamba kupitia injili yake hiyo sahihi, Mungu atawahukumu wanadamu, kwasababu anayehubiriwa ni Yesu Kristo. Ni sawa tu na Petro, au Yohana, au Yakobo, wangesema maneno kama hayo, wasingewezeka kupingana na Paulo kwasababu wanachokishuhudia wote ni kitu kimoja. Ndio maana tunaona maneno ya mitume wote, yameunganishwa katika kitabu kimoja kinachoitwa BIBLIA.
Lakini kwa nini Paulo aliongeze Neno hilo “sawasawa na injili yangu” Na asingeishia kwenye injili tu?.
Ni kwasababu wakati ule kulikuwa na watu waliomhubiri Yesu mwingine na injili nyingine, tofauti na ile waliyoihubiri mitume wa kweli. Na hawa watu, wengi wao walikuwa ni wayahudi wa tohara, Hivyo ilimbidi aliweke wazi hilo ili watu wabakie kwenye injili sahihi ya kweli.
Injili hizo Paulo aliziona kwenye makanisa kadha wa kadha kama tunavyosoma katika vifungu hivi;
2Wakorintho 11:4 Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!
Na..
Wagalatia 1:6 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na
kugeukia injili ya namna nyingine. 7 Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.
Umeona, hiyo ndio sababu ya Paulo na kule Rumi kuitamka kauli hiyo, “sawasawa na injili yangu”. Ili kuwapa ufahamu kuwa hizo nyingine wanazozisikia huko nje, hazina uhai wowote wa kumwokoa mtu, au kumtetea siku ile ya hukumu.
Hata sasa, mambo ni yale yale, kumekuwa na madhehebu mengi, imani nyingi, ambazo zote zinadai ni za kikristo, lakini ukiangalia uhalisia wake humwoni Kristo ndani yake, wala injili ya Kristo. Fundisho lililo mule ndani sio fundisho la mitume. Watu hawahubiriwi tena toba ya kweli na kumwangalia Kristo kama kiini cha wokovu wao. Wanafundishwa mambo mengine kabisa wengine mafanikio, wengine uchawi, wengine miujiza n.k kama ndio utimilifu wa ukristo. Sasa mambo kama hayo, hayaweza kumtetea mtu siku ya hukumu.
Bali injili ya Yesu Kristo, kupitia mitume wake. Ambayo ni hii biblia tuliyonayo, ndio tunayopaswa tuiegemee, kwasababu katika hiyo ndio tutakayohukumiwa.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
je! Paulo aliwalaani Wagalatia na Wakorintho?
Maana ya ‘Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake’
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Rudi Nyumbani