Monthly Archive Julai 2021

Nini maana ya Kuzumbua na kujitoja?

Nini maana ya kuzumbua na kujitoja? Katika biblia.(Walawi 6:3, Kumbukumbu 14:1, )

Jibu: Neno kuzumbua tunalisoma katika kitabu cha Mambo ya Walawi 6:3, na tafsiri ya neno hilo ni “kukipata kitu”, pengine ambacho kilikuwa kimepotea, au kimehamishwa mahali pake..

Walawi 6:1“ Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

2 Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya Bwana, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang’anya, au kumwonea mwenziwe;

3 AU KUZUMBUA kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo

4 ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang’anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea ALICHOKIZUMBUA yeye,”

Na hakuna mahali pengine katika biblia neno hili limeonekana tena.

Vile vile neno “kujitoja” tunalisoma katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 14:1, ambalo maana yake ni “kujikata”.. Mtu anayejikata kwa wembe au kisu katika mwili wake maana yake amejitoja kwa kitu hicho.

Kumbukumbu la Torati 14:1 “Ninyi mmekuwa wana wa Bwana, Mungu wenu; MSIJITOJE miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa”

Hakuna mahali pengine popote neno hili limeonekana katika biblia.

Katika maneno hayo mawili tunajifunza kuwa Mungu hapendezwi na dhuluma, maana yake kama ndugu yako kapoteza kitu na wewe ukakipata! (maana yake ukakizumbua), unapaswa umrudishie mwenyewe kitu hicho, hupaswi kubaki nacho wewe na kukificha kana kwamba ni chako na kumdanganya Yule aliyekipoteza.. jambo hilo halimpendezi Mungu kabisa.

Vile vile, biblia haijaturuhusu sisi kuitoja miili yetu, maana yake kuikata kata, kipagani… kama mfano wa wale manabii wa baali kipindi cha Nabii Eliya, walivyojikata..

1Wafalme 18: 28 “Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika”.

Hata leo, watu wanajikata katika matambiko yao ya kimila, na hata katika kuchanjwa chale, na wengine katika kujichora alama(tattoo). Namna zote hizi za kujikata ni machukizo mbele za Mungu, Kwasababu miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, maana yake Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu, hivyo hatupaswi hata siku moja kufikiri kuiharibu nyumba yake hii.. kwasababu tukiiharibu na yeye amesema atatuharibu sisi. (1Wakoritho 3:17)

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

CHUKIZO LA UHARIBIFU

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

PALE UNAPOKUWA NA SABABU ZA KUMLAUMU MTU, UFANYE NINI?

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

Rudi nyumbani

Print this post

SOMO no.02 (BINTI WA YEFTHA).

Karibu katika mwendelezo wa masomo yawahusuyo wanawake wa kwenye biblia,  Leo tutamtazama mwanamke mmoja/binti mmoja aliyekuwa mtoto wa pekee wa Mwamuzi wa Israeli.

Binti huyu alikuwa alikuwa ni mtoto wa pekee wa mtu aliyeitwa Yeftha, ambaye alikuwa ni Mwamuzi wa taifa la Israeli. Nafasi ya mwamuzi katika Israeli nyakati hizo, ilikuwa inakaribia sana kufanana na ile ya Mfalme, ingawa sio ya kifalme.  Hivyo mtu aliyekuwa mwamuzi katika Israeli katika nyakati hizo, alikuwa ni Mkuu sana, na mwenye kujilikana na kuheshimiwa katika nchi nzima.

Lakini tunasoma katika biblia alitokea Mwamuzi mmoja aliyeitwa Yeftha, ambaye huyu alikuwa ni shujaa sana..Na hakuwa na mwana wa kiume katika nyumba yake bali wa kike tu, tena mmoja. Lakini tunasoma wakati Fulani alipokwenda vitani, alimwekea Bwana nadhiri kubwa, kutokana na ukubwa wa vita iliyoko mbele yake, alitazama mbele yake akaona hiyo vita anayotaka kwenda kukumbana nayo, sio ndogo!, na endapo ikitokea kashinda basi ni muujiza wa Mungu tu umefanyika, na si kingine, kwasababu katika hali ya kawaida ni ngumu kushinda…kwasababu wanaokwenda kupigana nao ni wengi kuliko wao na wenye nguvu kuliko wao.

Kwahiyo ili kujihakikishia ushindi zaidi, alimwekea Mungu nadhiri, kwamba endapo Mungu atampa ushindi, basi kile cha kwanza, kitakachotoka kumlaki wakati anarudi vitani atakitoa kiwe sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana. Na katika mawazo  yake pengine alilenga mtumwa wake mmoja, au ndugu mmoja aliye katika nyumba yake, ndiye atakayekuja kumlaki (kwani nyumba yake ilikuwa na watu wengi, kwasababu yeye alikuwa ni Mkuu katika Israeli). Lakini cha kushtusha ni kwamba alitokea Binti yake wapekee kuja kumlaki, kinyume na matarajio yake. Na alipomwona akahuzunika sana, lakini akawa hana cha kufanya…(Hawezi kuitangua nadhiri yake)

Hebu tusome kidogo habari yenyewe kisha tusonge mbele..

Waamuzi 11:28 “Lakini mfalme wa wana wa Amoni hakuyasikiza hayo maneno ya Yeftha aliompelekea.

 29 Ndipo roho ya Bwana ikamjilia juu yake Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni.

30 NAYE YEFTHA AKAMWEKEA BWANA NADHIRI, AKASEMA, KWAMBA WEWE UTAWATIA WANA WA AMONI MKONONI MWANGU KWELI,

31 ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika milango ya nyumba yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na amani kutoka kwa hao wana wa Amoni, kitu hicho kitakuwa ni cha Bwana, nami nitakisongeza kiwe sadaka ya kuteketezwa.

 32 Basi Yeftha akavuka kuwaendea wana wa Amoni ili kupigana nao; naye Bwana akawaua mkononi mwake.

33 Akawapiga kutoka Aroeri hata kufikilia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa machinjo makuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli.

34 Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na machezo; naye alikuwa ni mwanawe pekee; hakuwa na mwingine, mwana wala binti, ila yeye.

35 Ikawa alipomwona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia Bwana kinywa changu, nami siwezi kurejea nyuma.

36 BINTI YAKE AKAMWAMBIA, BABA YANGU, WEWE UMEMFUNULIA BWANA KINYWA CHAKO; BASI UNIFANYIE SAWASAWA NA HAYO YALIYOTOKA KINYWANI MWAKO; KWA KUWA YEYE BWANA AMEKULIPIA KISASI JUU YA ADUI ZAKO, HAO WANA WA AMONI.

  37 Kisha akamwambia baba yake, Basi na nifanyiwe neno hili; niache peke yangu muda wa miezi miwili, ili nipate kwenenda milimani, na kuombolea uanawali wangu, mimi na wenzangu.

  38 Akamwambia, Haya, enda. Akampeleka mbali muda wa miezi miwili; naye akaenda zake, yeye na wenziwe, akauombolea uanawali wake huko milimani.

 39 Basi ikawa mwisho wa hiyo miezi miwili, akarudi kwa babaye, aliyemtenda sawasawa na ile nadhiri yake aliyokuwa ameiweka; naye alikuwa hajamjua mtu mume. Kisha ikawa desturi katika Israeli,

 40 kwamba binti za Israeli waende mwaka baada ya mwaka ili kumkumbuka huyo mwana wa Yeftha, Mgileadi, siku nne katika mwaka”

Leo nimetamani tujifunze kuhusu huyu binti, Kwasababu alikuwa ana roho ya Ushujaa ndani yake!..

Dada/Mama/ binti siku zote kumbuka hili: ni vizuri kwanza kujifunza kwa wanawake waliopo katika biblia kabla ya kuwatafuta wanaume.

Wanawake wengi wanapenda sana kujifunza kwa Isaka!.. Jinsi alivyonusurika kifo!, cha kuchinjwa na kutolewa sadaka ya kuteketezwa, lakini hawajui kuwa Isaka alinusurika tu!!, hakuchinjwa, wala hakutolewa sadaka… Yupo Shujaa mmoja katika biblia ambaye Alikubali mwenyewe kuchinjwa na nyama yake kukatwa katwa vipande na kisha kutolewa kama sadaka ya kuteketezwa!.. Ambaye pengine tutakapofika mbinguni tutamkuta ni mkuu kuliko ISAKA!..Na tutajilaumu sana kwanini hatukujifunza kutoka kwake!

Na huyo si mwingine zaidi ya huyu binti wa Yeftha!!. Binti huyu baba yake alimwambia dhahiri kabisa kwamba atakwenda kutolewa sadaka ya kuteketezwa!.. Jambo ambalo kiuhalisia ni gumu sana mtu kukubaliana nalo, lakini Binti huyu baada ya kupewa hizo taarifa!, wala hazikumwazisha.. wala hakuogopa kufa!, wala hakuogopa makali ya visu katika mwili wake, wala moto.. badala yake alisema maneno haya..

“36 BINTI YAKE AKAMWAMBIA, BABA YANGU, WEWE UMEMFUNULIA BWANA KINYWA CHAKO; BASI UNIFANYIE SAWASAWA NA HAYO YALIYOTOKA KINYWANI MWAKO; KWA KUWA YEYE BWANA AMEKULIPIA KISASI JUU YA ADUI ZAKO, HAO WANA WA AMONI”.

Bila shaka maneno kama haya, Isaka mwana wa Ibrahimu asingeweza kusema, pale alipokuwa anapelekwa mlimani kuchinjwa! Na Baba yake. Si ajabu, Ibrahimu hakumwambia Isaka chochote, kwamba anakwenda kumchinja na kumtoa sadaka!..pengine ingekuwa kitimtimu pale!, pangekuwa hapatoshi!, pangetokea vurugu kubwa sana!…Ndio maana Ibrahimu alimficha, kwasababu alimwona pengine hana huo utayari wa kujitoa kufa!!.

Mwanzo 22: 6 “Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.

 7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?

 8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja”.

Huyo ni Isaka anaulizia sadaka ya kuteketezwa ipo wapi!, maana yake yeye haimwingii akilini kujiweka katika hilo kundi!, kwamba yeye anaweza kuwa hiyo sadaka!.. Lakini alikuja kutokea Shujaa mmoja!, binti mdogo, ambaye taarifa za msiba si kitu kwake!, ambaye visu shingoni si kitu kwake, ambaye moto juu ya mwili wake si kitu kwake.. Zaidi ya yote alikuwa mtoto, tena ni binti, na tena ni BIKIRA!.. Lakini alikuwa na Imani kubwa kuliko ya Isaka!!. Huyu taarifa za kuchinjwa zilipomjia hakupepesuka wala hazikumshutua, alianza kuufikiria mambo mengine kabisa (Ubikira wake!!..na kwenda kuomboleza kwaajili ya huo, na alipomaliza kwa miezi miwili), kama vile kondoo apelekwavyo machinjoni, alikwenda mwenyewe na akachinjwa na kufa na kuteketezwa..

Labda inawezekana hujui vizuri!, sadaka ya kuteketezwa inakuwaje.

Sadaka ya kuteketezwa ambayo Mungu alimjaribu nayo Ibrahimu amtoe mwanawe , ilikuwa ni kwamba.. mtoto Yule anakamatwa, anafungwa kamba na kisha kisu kinapitishwa shingoni, anachinjwa kama ng’ombe, damu inachuruzika, na baada ya kuchinjwa, mwili wake unakatwa vipanda vipande, kisha vile vipande vinawekwa juu ya kuni, zilizopo juu ya mawe, na moto unawashwa na ile nyama inateketea kabisa mpaka inakuwa jivu!.. Hiyo ndiyo sadaka aliyokusudiwa Isaka!, ambayo Mungu alimwepusha nayo haikumpata, lakini ikatimia kwa shujaa huyu mmoja Binti wa Yeftha!, yeye alikubali mwenyewe kwenda kuchinjwa!.

Waebrania 11:35  “Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora”

Isaka aliibeba picha ya Yesu tu!, lakini huyu binti alilibeba tukio zima la Yesu!.. alionja kile Bwana alichokipitia pale Kalvari.. Na baada yake hatuoni mtu mwingine, awe mwanaume au mwanamke aliyefanya jambo la kishujaa kama hilo!, wengine wote kwenye biblia waliingia kwenye dhiki bila idhini zao, walishikwa wakakatwa vichwa na kuchinjwa, lakini si kujipeleka wenyewe kuchinjwa!…

Jambo hilo tunaliona kwa watu wawili tu! Kwenye biblia nzima, wa kwanza ni MKUU WA UZIMA MWENYEWE, MWAMBA-YESU KRISTO..Na mwingine ni huyu “Binti wa Yeftha”.

Dada/Binti /mama umeona ni jinsi gani una mashindano makubwa mbele yako??… Siku ile utajitetea vipi, kwamba umeshindwa kujitoa kwake!, na kumtumikia  kwasababu tu wewe si mwanaume??..Leo hii unaogopwa kuchekwa!, wenzako walikufa kabisa!..jambo ambalo hata mwanaume hawakuweza kulifanya!.. Bado huoni tu! Siku ya hukumu binti wa Yeftha atasimama kuhukumu mabinti wengi??..Bado huoni tu hilo!..fahamu kuwa!..hukumu ya wanawake itakuwa ni kali kuliko ya wanaume.. kwasababu katika biblia wapo wanawake waliofanya makubwa kuliko wanaume.  Eliya alimkimbia Yezebeli, ili ayanusuru maisha yake, lakini huyu binti wa Yeftha, yeye anakifuata kifo mwenyewe!..jiulize kati ya hao wawili ni yupi mwenye imani kubwa!..Wanawake kama hawa pamoja na mfano wa Yule Malkia wa Sheba Bwana Yesu aliyemtaja, watasimama kuhukumu vizazi vyetu..

Mathayo 12:42 “Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani”.

Hivyo, wewe kama Mwanamke, simama itambue nafasi yako!.. kama Dada simama!, kama binti simama!.. usiogope kufa!, badala yake uwe tayari kufa hata kwaajili ya imani, usiogope kupitia dhiki,badala yake uwe tayari kukumbana nazo kwaajili ya imani yako, usiogopwe kuonwa mshamba unapoacha mambo yote ya kidunia, na fashion zote!..Badala yake uwe tayari kuonekana umerukwa na Akili, Fahamu kuwa thawabu yako ni kubwa mbinguni.. Kuanzia leo anza kupiga mbio, ukijifunza kwa wanawake mashujaa katika biblia..

Vile vile usiutamanie  udunia, ukasema ngoja uule ujana, ndio utamtumikia Mungu, siku ile huyu binti wa Yeftha atasimama kukuhukumu, kwasababu yeye alikufa katika ubikira wake bila mume, angeweza kumwambia baba yake amruhusu akaolewe kwanza miezi miwili ndipo, amtoe sadaka!..lakini hakufanya hivyo, aliuthamini ubikira wake, akafa hivyo hivyo..

Vile vile hakuwa mtoto wa maskini, labda tuseme amechoka maisha ndio maana kakubali kujitoa afe!.. hapana!, alikuwa ni mtoto wa Mwamuzi wa Israeli..Ni tajiri sana!, kwasababu waamuzi walikuwa ni kama wafalme, lakini hakuutumainia utajiri wake, wala ubikira wake, wala uzuri wake.. Alikubali kuondoka!, kwasababu alijua, anao mji unao mngojea huko mbele. Yeru salem mpya. Alijua ufufuo unakuja na atakuwa mkuu katika ufalme wa mbinguni.

Kumbuka Mungu aliwachagua tu wanaume kwenye biblia wawe kama mwonekano tu!.. ndio maana utaona kila mahali wanatajwa wanaume..kama Isaka, Yakobo, Eliya n.k Lakini hiyo haimaanishi kuwa wao ndio wa kwanza katika ufalme wa Mbinguni.. Kwaufupi ni kwamba Mbinguni watakuwepo wanawake watakaopata thawabu kubwa hata kuliko hata wakina Ibrahimu, Isaka na akina Eliya na Musa. Kwasababu Mungu siku zote hana upendeleo.

Hivyo unaposoma biblia, anza kutafuta matendo ya wanawake mashujaa, ujifunze kwao, na vile vile, jifunze kwa wale waliojiharibia njia zao pia, ili uchukue tahadhari.

Mwisho wa muhtasari huu kumhusu “binti wa Yeftha” shujaa wa Bwana. Usikose mwendelezo wa wanawake wanaofuta!.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?

Rudi nyumbani

Print this post

SIKU YA HOFU YANGU NITAKUTUMAINI WEWE.

Daudi alisema..

Zaburi 56:3 “Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;

4 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini”?

Maadamu tupo hapa duniani, haijalishi tutakuwa ni watakatifu au mkamilifu kiasi gani, lakini maadamu tunaishi chini ya jua, zipo siku ngumu tutapishana nazo katika safari yetu ya imani. Hizo ni  nyakati zenye masumbufu sana, zenye kuvunjika moyo kusikokuwa kwa kawaida, zenye huzuni nyingi sana, zenye machozi na majonzi, Daudi alizitambua nyakati hizo na kuziita  “SIKU ZA HOFU YANGU”.

Na hizi zinatofautiana kati ya mtu na mtu, mwingine Siku ya hofu yake, ni vipindi cha Misiba.  Pengine amefiwa na mpendwa/wapendwa wake wa karibu sana kwa ghafla, labda kwa ajali mbaya, hichi kipindi huwa ni kigumu sana isivyoelezeka. Mfano wa watu kama hawa kwenye biblia alikuwa ni Ayubu, aliyefiwa na watoto wake wote 10 kwa mkupuo.

Mwingine,  siku ya hofu yake ni siku za kuwindwa na maadui ili auawe, mfano wa watu hawa ndiye kama Daudi mwenyewe aliyeandika habari hiyo. Yeye ilifikia wakati serikali nzima inamwinda, imwangamize. Embu jiweke wewe katika hiyo nafasi, maisha yako yote, unajificha mapangoni tu, kwasababu umesikia kuwa raisi na watumishi wake wote wa usalama wametumwa nchi nzima kukuwinda ili wakuue. Si jambo jepesi.

Mwingine siku ya hofu yake ni siku za  magonjwa. Amepatwa na ugonjwa wa ghafla ambao pengine hakuwahi kudhani kama ungemfikia mtu kama yeye, labda Ukimwi, au Kansa, au amepata ajali, na ikamletea ulemavu wa kudumu, kama vile kiharusi, au ukiwete, au kalazwa ICU, kwa kwa kipindi kirefu, huo wakati unakuwa ni mgumu sana kuchukulika,. Mfano wa mtu kama huyu ni Eprafodito ambaye alikuwa  ni mtume aliyetenda kazi pamoja na akina Paulo, yeye  ilifikia wakati hali yake ikawa mbaya sana karibu na kufa kwa kuugua.(Wafilipi 2:25-27)

Mwingine siku ya hofu yake ni siku ya kusalitiwa.  Aidha Kusalitiwa na ndugu yake katika imani, au kusalitiwa na wazazi kisa ameokoka, au kusalitiwa na mke/mume, au kusalitiwa na marafiki.  Kama vile Bwana Yesu alivyosalitiwa na Yuda. Huu pia si wakati mwepesi, hauchukuliki kirahisi. Jambo kama hili linaweza kumpelekea mtu mwingine hata kujinyonga, au kuleta madhara yoyote kwa wengine.

Mwingine siku ya hofu yake, ni siku za kukumbana na hasara. Kupoteza kila kitu, kupoteza mali zake alizozisumbukia, au fedha, au mashamba, au mifugo, kama vile Ayubu kiasi kwamba habakiwi na chochote. Madeni yamemsonga,  bado familia inamwangalia, akiangalia mikopo anapaswa arudishe,na asiporudisha nyumba inauzwa, jambo ambalo hakutegemea kabisa kama lingemtokea kwa haraka hivyo.  Hichi kipindi huwa ni kigumu pia, sio cha kuchukulika kiwepesi.

Na vipindi vingine vyote vya namna kama hiyo..

Sasa ukijikuta katika siku kama hizo, na wewe umekoka, usiwe na haraka kumkatia tamaa Mungu, usiwe mwepesi wa kukimbilia kwa wanadamu, vilevile usitoe maneno ya kukufuru, au kupeleka manung’uniko  yote kwa Mungu. Bali zidi kumtumaini yeye, kama Daudi alivyosema “Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe”.. Kuwa mtulivu kama Ayubu, utakumbuka hata wakati ambapo mke wake anamshauri amkufuru Mungu afe lakini yeye alimkemea  na kumwambia asiwaze kipumbavu kama wengine wafanyavyo,  Na wewe pia mtazame Mungu peke yake, usiwe na maneno mengi kwake katika siku kama hizo, na kuanza kusema kwanini hivi, kwanini vile, mtazame Mungu tu ndugu. Zipo sababu nyingine zilizo juu ya upeo wa ufahamu wako usizozijua.

Siku kama hizo , kifungu hichi kiwe faraja yako wakati wote..

Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho”.

Mtazame mtu kama Ayubu jinsi mwisho wake ulivyokuwa wa faraja, kwani yote aliyoyapoteza Mungu alikuja kumrudishia mara mbili, hata watoto nao Mungu alimpa wengine wazuri kushinda hata wale wa kwanza, na hata siku ile ya ufufuo bado Mungu atamkutanisha na wale watoto wake wa kwanza aliowapoteza.

Yakobo 5:11 “Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma”.

Daudi naye, japokuwa alilemewa na maadui zake (Sauli), lakini bado hakuacha kumtumainia Mungu, mwisho wa siku Mungu akamlinda, na kumuhifadhi hai, na kumstarehesha katika ufalme wake.

Nawe vivyo hivyo fahamu tu, mwisho wako utakuja kuwa mzuri endapo utaendelea tu hivyo hivyo kushikamana na Bwana. Kwasababu yeye ni mwingi wa rehema na huruma, kumbuka anajishughulisha sana na mambo yetu, Na zaidi ya yote alishayachukua masikitiko na fadhaa zetu zamani sana(Isaya 53:4).

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).

Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.

NAWE UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?

SWALI: Kwanini Bwana Yesu aliwalenga mbwa na nguruwe tu , na si wanyama wengine katika mfano wa Mathayo 7:6?

Mathayo 7:6 “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua”.


JIBU: Alitumia mfano wa wanyama hao wawili, kwasababu ya tabia zilizopitiliza za kutokujali walizo nazo, kwamfano Mbwa, ni mnyama wa kufugwa lakini bado ni mnyama asiyejali ni kitu gani anakula tofauti na wengine kama vile paka.. Na ndio maana anaridhika na vyakula vya majalalani au   makombo yaliyosalia ya majumbani, kama vile Bwana Yesu alivyosema katika…

Mathayo 15:26 “Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao”.

Vilevile ni heri ingekuwa anaishia kwenye makombo tu, lakini pia mbwa ni mnyama ambaye yupo tayari KUYALA MATAPISHI YAKE mwenyewe. Bila kujali kuwa ni uchafu ule. Sasa embu jiulize, kama hajali anachokula, atajali vipi, au atathamini vipi chakula kizuri unachompa?..Utadhani atakufurahia sana, kumbe mwenzako wala!!

Halikadhalika, na nguruwe naye. Ni mnyama wa kufugwa, lakini anapenda sana kukaa kwenye matope, jambo ambalo huwezi kuliona kwa kuku au mbuzi. Ni mnyama asiyethamini usafi hata kidogo. Sasa fikiria unaondoka, na kuchukua ile lulu yako ya thamani ambayo umeinunua kwa bei ghali, labda tuseme milioni 10, lulu ambayo unajua wanaovaa ni mamalkia tu au watu wenye uwezo, halafu unakwenda kumuogesha nguruwe wako vizuri na  kumvisha, lengo lako ni kutaka kumwona akipendeza.

Wewe unategemea nini kama sio kwenda kugaragara nayo kwenye matope,na kuikanyaga? Yaani ni heri hata ungemvisha punda, lakini sio nguruwe. Hivyo mbwa na nguruwe walitungiwa hata mithali yao tangu zamani, ambayo tunaisoma katika..

2Petro 2:22 “Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni”.

Ikifunua kuwa hata leo hii, wapo watu wenye tabia za wanyama hawa, ambao hawapaswi hata kidogo kupewa vitu vitakatifu (ikiwa na maana hawapaswi kupewa mambo ya ndani kabisa yamuhusuyo Mungu). Watu kama hawa hata ujaribuje kuwaeleza habari za Mungu, na uzuri wake, mambo ambayo pengine wewe uliyapata kwa mateso, na ulipoyapata ukayafurahia, ukadhani itakuwa sawa na kwao, ndugu utaishia tu kudharauliwa, kuchekwa, kukejeliwa, kutukanwa, na wakati mwingine kupigwa na kuudhiwa.

Hivyo wewe kama mkristo unapaswa uwe na hekima unapokutana na makundi ya watu wa namna hii. Ukishaona mtu anabishana na wewe kuhusiana na habari za Kristo, au anadhihaki dhihaki, tu wala usihangaike naye kumuhadithia maneno mengi, achana naye, kuwa kama mjinga kwake, nenda kwa Yule mwingine aliyetayari kusikia.. Kwasababu ukizidi kubishana na huyu mwishowe wewe ndio utakayeumia.

Hiyo ndio maana ya hiyo mithali, Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?

MTAWATUPIA MBWA NYAMA HIYO.

Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

UFUNUO: Mlango wa 18

Rudi nyumbani

Print this post

Tofauti kati ya kuhukumu na kulaumu ni ipi?

SWALI: Bwana Yesu asifiwe,.Naomba kufahamu tofauti kati ya kuhukumu na kulaumu, maana nashindwa kuelewa, imesema tusihukumu. Je kwa mtu anayetenda dhambi kwa makusudi unapomlaumu ni sawa na kumuhukumu?

Luka 6:37 “Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa”.


JIBU: Kuhukumu ni kitendo cha moja kwa moja kutoa/kuamua hatma ya mtu mwingine, Na hiyo inakuja pale mtu anapojiona yeye ni bora/mwema sana zaidi ya wale wengine, . Kwamfano mtu mmoja atamwona kahaba, au mlevi, au shoga barabarani na wakati huo huo atamwambia wewe ni ibilisi, mwana wa kuzimu, Au atakutana  na wapagani wanaabudu miungu yao mahali fulani, ataanza kuwanyooshea kidole na kuwaita makafiri wa motoni wale, bila hata kuwaambia kitu kingine chochote, kisa tu kawaona wanafanya matendo yasiyompendeza Mungu. Hapo tayari kashawahukumu.

Lakini Kulaumu ni kitendo cha kukosoa kila kitu, kwa lengo la kuonyesha kuwa  kitendo alichokifanya/anachokifanya Yule mwingine ni cha kupuuzi sikuzote, hakina maana. Na kwa kawaida watu wanaolaumu nao pia wanakuwa na fikra kwamba wao huwa hawakoseagi..Ingekuwa ni wamepewa fursa hiyo wangeitumia vizuri. (Wana tabia ya kujiona wao ni wakamilifu sikuzote)

Kwamfano lawama mara nyingi zinawakuta viongozi, Utakuta kiongozi, kafanya jambo fulani la kimaendeleo, lakini kwasababu mtu fulani anajiona yeye hawezi kukosea, ataanza kutoa kasoro, kwa kila kitu kilichofanywa hata kama ni kizuri, utasikia, kwanini zile pesa zisingetumiwa kwa hili au lile, kusingekuwa na matatizo haya na yale, hiyo ndio laumu. Kana kwamba yeye yupo sahihi wakati wote, hajawahi kufanya kitu akakosea.

Au mtu mwingine, labda mzazi wake ameshindwa kumtimizia haki yake ya msingi, pengine elimu, halafu amekuwa mtu mzima, akaona madhara ya kutopelekwa kwake shule. Sasa badala ajifunze “kuachilia” kama biblia inavyosema, achilieni, nanyi mtaachiliwa, yeye ataanza kuwalaumu wazazi  wake tangu ujana wake hadi uzee wake, kana kwamba walifanya makosa makubwa sana, Na kusahau kuwa yeye mwenyewe pia anayomakosa mengi, ambayo Mungu anayohaki ya kumlaumu kupitia hayo.

Vitendo vyote hivi Mungu havipendi. Kuhukumu pamoja na kulaumu, kwasababu na sisi Mungu atatufanyia hivyo hivyo siku ile ya hukumu, tusipobadilika, Na kwakweli Bwana atusaidie viondoke ndani yetu. Lakini pia tunapaswa tufahamu kuwa kuelezwa uhalisia wa mambo sio kuhukumiwa, jambo ambalo watu wengi wanatafsiri isivyosawa. Kwamfano mtu ni mlevi, halafu anaelezwa kuwa walevi wote biblia inasema wataenda jehanamu, akadhani hapo anahukumiwa.. Hapo haukumiwi, bali anaelezwa ukweli wa mambo. Kwamfano hata wewe ukimwona mtoto wako anacheza karibu na shimo, ukamwambia “watoto wanaocheza karibu na mashimo mwisho wao huwa ni kutumbukia na kufa”. Hapo hujahitimisha kuwa Yule mtoto ni wa kufa, lakini umemweleza uhalisia wa mambo. Hivyo na wewe unavyohubiriwa wazinzi wote watakwenda kuzimu, ujue kuwa hauhukumiwi, bali unaelezwa hatma ya maisha yako.

Unapoambiwa wanaojichubua miili yao wote na wanaovaa nguo za uchi uchi, hatma yao ni kwenye ziwa la moto. Hauhukumiwi wala haulaumiwi bali unahubiriwa hatma yako. Lengo la Yule mhubiri sio uende kwenye ziwa la moto bali utubu ili uikwepe hukumu.

Lakini mtu akikufuata na moja kwa moja akakwambia wewe ni ibilisi, au kafiri, au joka, au ajenti wa kuzimu, kana kwamba wewe huwezi kupokea neema yoyote kama ya kwake,. Huyo tayari ameshakuhukumu na biblia imekataza sana hilo, kwasababu anayejua hatma ya mtu ya mwisho ni Mungu na sio yeye. Lakini akikueleza matokeo ya ukafiri wako, hajakumukumu, zaidi kaonyesha upendo kwako.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA

Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?

Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni  ipi?

SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post

SOMO no. 01 (HAWA)

HAWA

Karibu katika mfululizo wa masomo yawahusuyo wanawake wa kwenye biblia, katika mfululizo huu, tutajifunza mengi yahusuyo majukumu ya wanawake kibiblia.

Katika biblia kulikuwepo na wanawake waliokuwa mfano mzuri wa kuigwa, na ambao hawakuwa mfano mzuri wa kuigwa, vile vile walikuwepo wanawake waliokuwa ni manabii wa kweli, na vile vile walikuwepo manabii wa uongo.

Kama mwanamke ni vizuri kujifunza kwa wote hawa, kabla ya kuanza kujifunza kwa Manabii na watumishi wa Mungu wa kiume katika maandiko.

Kwasababu mbio za wanaume ni tofauti na za wanawake. Katika tuzo na thawabu mbinguni hawatalingalishwa wanaume na wanawake.. bali wanaume kwa wanaume, na wanawake kwa wanawake..

Hata katika mbio za kidunia, wanawake wanapewa tuzo kulingana na mbio zao wao, na wanaume vivyo hivyo.. huwa hawachanganywi katika mbio, vinginevyo tuzo zote zingeenda kwa wanaume tu!, kwasababu ni ngumu wanawake kuwazidi mbio wanaume..

Hivyo ili kulitatua hilo, ndipo wanawatenga wanaume na wanawake.. Na Yule anayeibuka kidedea kwa wanawake anapewa tuzo sawa na yule aliyeibuka kidedea kwa wanaume..

1Wakorintho 9:24“ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.

25  Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.

26  Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; ”

Hivyo leo tutaanza kwa kujifunza kutoka kwa mwanamke wa kwanza, aliyeitwa Hawa. Kwa Hawa yapo mazuri ya kujifunza lakini pia yapo mabaya tusiyopaswa kujifunza kwayo..

Hawa ndiye mwanamke wa kwanza kuumbwa, na biblia inasema aliumbwa kama Msaidizi kwa Adamu (Mwanzo 2:20). Amsaidie katika majukumu yote ambayo Mungu alimpa Adamu. Hivyo HUDUMA ya kwanza ya Hawa aliyopewa na Mungu ilikuwa ni USAIDIZI!.. Na si “mke” Au “Mama”  Mungu hakumuumbia Adamu mke!, suala la mke lilikuja baadaye!.. Hakumuona Adamu na kumwona Yupo mwenyewe hivyo anahitaji mke wa kumliwaza!, au anahitaji mama wa kumlelea watoto wake!, ..Hapana!.. bali aliona anahitaji msaidizi wa kumsaidia shughuli alizompa..Hilo! ndilo la kwanza.. hayo mengine yalikuja baadaye.

Mwanzo 2:20 “Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; LAKINI HAKUONEKANA WA KUMSAIDIA ADAMU ALIYEFANANA NAYE”

Na usaidizi huo Hawa aliopewa si wa kutumia nguvu, ndio maana hakuumbwa na misuli, zaidi ya yote aliumbwa mwororo na mwenye umbo la wastani. Mungu angetaka awe msaidizi wa kutumia nguvu bila shaka angemuumba mwenye nguvu na mkubwa kuliko Adamu, lakini tunaona hakuwa hivyo.

Ikimaanisha kuwa usaidizi wake sio wa kutumia manguvu, bali hekima na akili. Wanyama kama ng’ombe, punda, farasi hao ndio waliumbwa kama wasaidizi wa Adamu kwa kutumia nguvu ndio maana waliumbwa wenye nguvu kuliko Adamu, ili ngamia amsaidie Adamu safari yake, hana budi awe mkubwa na mwenye nguvu kuliko Adamu. Lakini si Hawa!, usaidizi wa Hawa ulikuwa ni wa tofauti..

Hivyo USAIDIZI ndio huduma ya kwanza HAWA aliyopewa, Na hiyo hiyo huduma ya usaidizi Mungu alianza kuiweka kwa mwanamke wa kwanza anayeitwa Hawa, na wazao wote wa kike wanaofuata baada yake, wanayo hii HUDUMA ndani yao..Ndio maana wanaendelea kuzaliwa wakiwa kama Hawa, kimwonekano, wasio na misuli kama Hawa wa kwanza.

Hivyo hilo ni jambo la kwanza ambalo kila mwanamke anapaswa alijue, na shetani asilopenda walijue. Mungu anapomwangalia mwanamke yeyote duniani, anamwangalia kwanza kama MSAIDIZI kabla ya kumwangalia kama mke au Mama!. Hivyo kitu cha kwanza mwanamke anachopaswa kukifikiri na kukitafuta si Mume ili kumpendeza Mungu..bali Ile huduma ya usaidizi iliyopo ndani yake!, namna atakavyoivumbua na kuitumia ipasavyo.

Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”

Hivyo kama mwanamke ni lazima ujue!.. Usaidizi wako ni nini katika mahali ulipo!…Kibali ulichopewa unakitumiaje!.. ukienda mahali unapoona ni rahisi mwanamke kuaminika, na kukubalika kuliko mwanaume ni lazima ujiulize ..Ni kwanini iwe hivyo?..Ni lazima ujue kuwa kuna jambo la kusaidia pale, ambalo haliwezi kufanywa na wanaume!.. na jambo hilo si la kutumia nguvu bali akili, na hekima..Hivyo ni vyema uwe mshapu wa kulivumbua na kulitekeleza..

Labda tuchukue mfano pale katika Edeni.

Pengine wakati Adamu anawapa majina wale wanyama.. Hawa alipokuja akaweka mfumo bora wa kuwakumbuka, kwa kuwagawanya katika makundi au kwa kazi zao wanazozifanya!..ambao pengine kwa Adamu peke yake ingekuwa ni ngumu au asingeweka utaratibu mzuri..(Huo ni mfano tu).. Maana yake ni kwamba Hawa alipewa akili ya ziada, ambapo ikichanganyikana na ile ya Adamu, basi kazi ingefanyika vizuri zaidi!..

Vile vile katika kanisa, yapo mambo mengi hayapo sawa, ambayo yanahitaji usaidizi!.. Hayo yamefichwa kwenye macho ya wanaume, lakini yamewekwa wazi kwa wanawake werevu.

Katika kanisa ipo mifumo mingi ambayo kweli ni ya kiMungu, lakini endapo ikiendelea kwa namna hiyo hiyo, inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kutekelezeka, au hata kama ikitekelezeka basi isitekelezeke kwa ufasaha.. Ni wajibu wako wewe kama mwanamke wa kikristo kutafuta namna ya kulitatua hilo.

Umeona kuna jambo Fulani linakwenda kupotea, haraka sana unaingia kwenye maombi, au unakusanya wenzako wachache na kuingia kwenye maombi kuliombea,  au kuna jambo umeona halijafanyika vizuri chukua nafasi hiyo wewe kulifanya lifanyike vizuri zaidi ili mambo yasiharibike,  usisubiri mwingine afanye!, kila jambo unaloona ni tatizo au linaelekea kuwa gumu unatafuta namna ya kulitatua haraka sana, …Na hulitatui kwa kumuagiza mtu mwingine akalifanye! Bali kwa wewe mwenyewe kulifanya!… vinginevyo wewe hutakuwa tena msaidizi, bali ndiye unayesaidiwa kutekelezewa majukumu yako.

Kumbuka Sifa moja ya msaidizi sio yeye kusaidiwa!, bali ni yeye kusaidia. Kwahiyo kila kitu mwanamke anachokiona kinahitaji marekebisho na msaada, hana budi kukifanya yeye kabla ya kumwambia mwingine, ili akidhi vigezo vya kuwa msaidizi..

Na hekima ya kuona mambo ambayo yanahitaji msaada katika kanisa au katika maisha inatoka kwenye Neno la Mungu. Huwezi kukaa hulijui Neno la Mungu, halafu uwe na jicho la kuona marekebisho!.. Itakuwa ni ngumu sana, zaidi utaishia kudanganywa na Yule mwovu na kufanya uharibifu mkubwa kwasababu wewe ni lango!

Hawa alianza vizuri kazi ya usaidizi, lakini alipoanza kutoka nje ya mpango wa Mungu, na kwenda kutafuta maarifa kinyume na maagizo ya Mungu, akajikuta badala ya kumsaidia Adamu kuujenga ufalme, akajikuta anamsaidia kuubomoa!.. Na anguko lake likawa kubwa ambapo madhara yake mpaka leo hii yapo!!.

Vile vile mwanamke yeyote asipolijua Neno la Mungu na kudumu katika hilo, basi kazi yake au macho yake yatakuwa hayaoni kujenga bali kubomoa (Na hatajua kama amepofushwa macho). Na mwanamke ndiye shabaha ya kwanza ya adui kutafuta kupitishia uharibifu wake kabla hata ya mwanaume.

Hivyo kama mwanamke hauna budi kutafuta kujifunza Neno kwa bidii..usiku na mchana, ili hekima iingie ndani yako, ili macho yako yaone madhaifu sahihi, na uweze kuyarekebisha. Hilo ndio jukumu lako la kwanza ulilopewa, hayo mengine ya kuwa Mama, au mke hayana umuhimu sana zaidi ya hilo la USAIDIZI!.

Ukifanyika kuwa msaada mkubwa katika kazi ya Mungu na kuifanya ikue na kustawi, basi fahamu kuwa Mungu anakuheshimu sana na una thawabu kubwa sana mbinguni, kwasababu ndiyo huduma ya kwanza Mungu aliyompa mwanamke. (Unakuwa umetii agizo la Msingi na la awali)

Hata Bwana Mungu wetu, alipoona kutakuwa na kasoro nyingi baada ya Bwana wetu Yesu kuondoka duniani, alituachia msaidizi, ambaye ndiye Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu sio sisi kumsaidia yeye, bali ni yeye kutusaidia sisi..

Warumi 8:26  “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

27  Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”

Je na wewe unachunguza mambo?, na kuchukua udhaifu wa wengine, na hata wa kazi ya Mungu, na kuwa msaidizi bora?..kama bado!.. anza leo kwa bidii, na utaona jinsi Mungu atakavyotembea na wewe kwa viwango vingine!

Bwana akubariki.

Huu ni msingi wa kwanza tuliouweka,kuhusu huduma ya kwanza ya Mwanamke!..Tutazidi kusonga mbele kutazama, wanawake wengine, na mambo ya kujifunza kuhusu wao, hivyo usikose mwendelezo.

Bwana akubariki.

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)

SWALI: Nini maana ya “kuabudu malaika”, kama tunavyosoma, katika Wakolosai 2:18?


Wakolosai 2:18 “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili”;

JIBU: Watu wa mataifa walipoipokea injili kwa mara ya kwanza kutoka kwa mitume, utakumbuka kuwa walitoka moja kwa moja katika upagani, na kuingia katika ukristo, Hivyo walikuwa hawana misingi imara sana ya kufahamu utendaji kazi wa Mungu  hususani pale Mungu anapozungumza kupitia malaika zake. Na tatizo hilo lilionekana sana sana kwa  watakatifu waliokuwa  Kolosai kwa wakati ule.

Walikuwa hawajui, kuwa Mungu anafanya kazi na malaika zake kwa ukaribu sana, kama vile biblia inavyosema wale ni wajumbe wanaotumwa kutuhudumia sisi tutakaourithi wokovu(Waebrania 1:14)… Sasa baadhi ya wakolosai pale walipoona Mungu anazungumza nao mara nyingi kupitia sauti za malaika zake, au maono.  wakadhani, malaika nao wana uungu mmoja na Kristo. Hivyo wakaanza kuwaabudu kama vile wanavyomwabudu Yesu Kristo.

Kama jambo kama hilo pia lilitokea kwa mtume Yohana alipokuwa kule Patmo akionyeshwa yale maono na Mungu kwa mkono wa malaika, mpaka na yeye akataka kumwabudu Yule malaika aliyesema naye, sasa jiulize ikiwa yeye ambaye ni mkomavu katika imani alijaribu kufanya hivyo  itakuwaje kwa watu wa mataifa walioamini siku sio nyingi? Ni rahisi sana na wao kuanguka katika makosa hayo..

Soma..

Ufunuo 22:8 “Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo.

9 Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu”.

Soma pia Ufunuo 19:10, utaona tena jambo hilo hilo likijirudia tena.

Hivyo baadhi ya wakolosai waliingia katika makosa hayo, kama ilivyo sasa, kwa baadhi ya makanisa  kama Katoliki, ambao wanakuwa na maombi maalumu kwa ajili ya malaika walinzi waje kuwalinda. Jambo ambalo sio sawa, kwani maombi yetu yote na dua zetu zote, zinapaswa zielekezwe kwa Mungu tu peke yake, kupitia Kristo Yesu Bwana wetu na si mtu mwingine, aidha ni mtakatifu au malaika. Kufanya hivyo ni sawa na kuabudu sanamu.

Vilevile hii inatoa tahadhari, kwa kanisa hususani kwa manabii, ambao Bwana amewajalia neema ya kuona/kupokea ujumbe kwa Bwana kupitia malaika zake. Umakini wa hali ya juu unapaswa uwepo, wa kutowahusisha wajumbe hao na ibada yoyote. Bali wajue kuwa ni Kristo pekee ndiye anayestahili kuabudiwa, kwasababu hata malaika wenyewe wanamwabudu yeye. Tunachukulie tu kama wajumbe lakini sio kuwapa heshima kama ile ya Kristo mwenyewe.

Waebrania 1:6 “Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu”.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada?”

Nini maana ya “saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada?”

Nini maana ya kuabudu?

Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

Rudi nyumbani

Print this post

BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA

Huruma ni nguzo muhimu sana ambayo tunapaswa tuwe nayo sisi tuliompokea Kristo maishani mwetu.

Ni kwanini tuwe na huruma? Ni kwasababu Baba yetu naye ni mtu mwenye huruma.

Luka 6:36 “Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma”.

Lakini wengi wetu bado hatujafahamu vema huruma hasaa ni nini. Kuna tofauti kati ya huruma na Rehema(wafilipi 2:1). Rehema ni neno pana linalomaanisha kusamehe au kusaidia hata kama mtu huyo hastahili kupewa fadhili hizo, lakini huruma ni kitendo cha kuonyesha kusamehe/kusaidia/kujali kwa mtu ambaye anaonekana anahitaji msaada huo hata kama hatosema,au kuonyesha.

Kwa mfano mwanajeshi vitani anapomkamata adui yake (ambaye ni mwanajeshi kama yeye). Na ikatokea adui huyo akajisalimisha kwa magoti akiomba asiuliwe,..Na yule mwanajeshi akamsaheme, kwa kuomba kule, basi hapo kaonyesha kitendo cha huruma.

Lakini ikitokea, Yule adui amekamatwa lakini bado analeta ubishi, bado ni mkaidi, anataka kuleta madhara, na wakati huo huo  Yule mwanajeshi bado akayahifadhi tu maisha yake..Hiyo sio huruma bali ni rehema.

Mfano mwingine wa rehema  ni pale raisi anapowaachilia wafungwa, sio kwamba wale watu walimwomba watoke, au wamejirekebisha kwa tabia zao mbaya, au ni wema sana hapana bali ni pengine raisi anatimiza tu wajibu wake wa kisheria kama raisi, wa kusamehe wafungwa kila muhula kwake.

Mfano mwingine wa huruma ni pale Baba anapomtimizia mtoto wake mahitaji yake ya chakula au mavazi,huwezi kusema anaonyesha kitendo cha rehema, hapana, bali huruma, kwasababu anajua sikuzote mtoto ni dhaifu, hana uwezo wa kujiamulia mambo yake mwenyewe.

Hivyo rehemu na huruma vyote vinahitajika sana kwetu. Lakini leo tutajikita sana katika upande wa huruma, na tayari tumeshapata  msingi wa maana halisi ya huruma, kwamba huwa unaenda moja kwa moja kwenye kundi la watu wanaoonyesha kuhitaji msaada fulani.  Basi biblia inatufundisha sisi kama wakristo, tuonyeshe huruma zetu, kwa makundi kama hayo; kwasababu Baba yetu wa mbinguni naye anaonyesha huruma zake kwetu sisi tunapomlilia, usiku na mchana.

Kibiblia ni makundi gani tunapaswa tuyaonyeshee huruma zetu?

1) HURUMA KWA WENYE MAGONJWA.

Utaona katika maandiko Bwana Yesu aliwaponya wagonjwa wengi sana kwasababu aliwahurumia, hakuwaacha tu waende zao,bali alijitahidi kuchukuliana nao, na kuwaponya.

Marko 1:40 “Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.

41 NAYE AKAMHURUMIA, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.

42 Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.

Unaona? nasi vivyo hivyo, tunapoona wengine wanataseka na magonjwa, wanaumwa, hatupaswi kuwaacha hivi hivi, tuwe nao karibu tuwaombee, tujiweke na sisi katika nafasi zao, Jiulize je! Kama na wewe ungekuwa unaumwa kansa, au kisukari, au ukimwi kama Yule, halafu unaona  watu hawakujali hata kukuombea, utajisikiaje?.

Tazama tena kisa hiki kingine..

Luka 7:12 “Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.

13 Bwana alipomwona ALIMWONEA HURUMA, akamwambia, Usilie.

14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka”.

2) HURUMA KWA WENYE UHITAJI.

Kuna wakati jirani yako atakuwa amepungukiwa na kitu fulani aidha  mboga kidogo,  au sabuni, au pesa kidogo za matumizi, na pengine hilo lipo ndani ya uwezo wako, hupaswi kumuacha tu hivi hivi, bali uonyeshe huruma zako, kwasababu hivyo ndivyo Mungu anataka..

1Yohana 3:17 “Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia HURUMA ZAKE, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?

18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli”.

3) HURUMA KWA WALIOKUMBWA NA MATATIZO:

Kuna muda ambao, mtu fulani atahitaji msaada wa haraka kutoka kwako, labda mgonjwa wake kazidiwa anaomba msaada wako,wa kumfikisha hospitali, na wewe pekee ndio upo hapo wa kuweza kumsaidia, wakati kama huo, usijione kuwa upo buzy sana, au unawahi ibadani, zingatia kumsaidia kwanza, kwasababu biblia inatufundisha hivyo kwa ule mfano wa msamaria mwema;

Luka 10:30 “Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.

31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.

33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona ALIMHURUMIA,

34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza”.

4) HURUMA KWA WAKRISTO WALIORUDI NYUMA:

Hapa ni mahali pengine ambapo tunapaswa kupazingatia sana. Kuna wakati ndugu mwenzako katika imani anaweza kurudi nyuma, pengine akauacha wokovu kabisa, lakini akawa anatamani kurudi tena kwa Mungu, wewe kama mkristo, ni lazima uonyeshe huruma zako kwa mtu kama huyo kumsaidia, tutalisoma hilo katika ule mfano wa mwana mpotevu, utaona baada ya kuasi nyumbani na maisha kuwa magumu huko alipokwenda alizingatia kurudi nyumbani. Na aliporudi alimwambia baba yake maneno haya;  Lakini utasoma babaye hakumfukuza bali alimuhurumia.

Luka 15:19 “sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.

20 Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, AKAMWONEA HURUMA, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.

21 Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena.

22 Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;

23 mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi;

24 kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia”.

Vivyo hivyo na sisi tuwahurumie wale ambao wanarudi kwa moyo wa dhati kwa Mungu.

5) HURUMA KATIKATI YA WAAMINIO.

Vilevile sisi kama waaminio, tuliokoka, kanisa la Kristo, ni lazima tujue kuwa kila kiungo kinamuhitaji mwenzake, unapoona kiungo kimoja kimeumia, au kimefadhaika huna budi kukitibu, unapoona kimepungukiwa huna budi kukijali, kinapokukosea huna budi kikisamehe. Ndivyo Bwana anavyotaka.

Waefeso 4:32 “tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi”.

Bwana atusaidie tuyazingatie hayo, ili na sisi tufanane na Baba yetu wa mbinguni, ambaye anatuhurumia kila wakati.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UPENDO WA MUNGU.

JE! NI WAPI UTAPOKEA HISIA ZA KWELI ZA KI-MUNGU?

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

Je! Mfalme Abiya na Mfalme Asa walikuwa ni ndugu?

Rudi nyumbani

Print this post

FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo litukuzwe daima, karibu katika kuyatafakari maandiko.

Katika biblia tunasoma Kisa cha mabinti wa tano wa mtu mmoja, wa kabila la Manase, waliokuwa mashujaa katika Imani, hata kuibadilisha taratibu ambazo zilikuwepo.

Zamani wakati wana wa Israeli wanatoka Misri, kuelekea Kaanani. Mungu alimpa Musa maagizo ya kuigawanya hiyo nchi watakayoiendea.. Kwamba kila kabila, lipate sehemu ya ardhi katika hiyo nchi ya kaanani wanayoiendea. Lile kabila lenye watu wengi, basi litapewa sehemu kubwa ya ardhi, na lile lenye watu wachache basi litapewa sehemu ndogo ya ardhi.  Na kabila la Yuda ndio kabila lililokuwa na watu wengi kuliko kabila zote za Israeli, na kabila la Manase ndilo lililokuwa dogo kuliko yote (yaani lenye watu wachache).

Hivyo wakati wa kugawa urithi, walikuwa wanaangaliwa wale wazee wa ukoo ambao ndio vichwa vya ukoo, wanaomcha Mungu, hao ndio wanaopewa labda tuchukue mfano, hekari elfu moja, na hao ndipo wanagawa hizo ekari elfu kwa watoto wao wa kiume, kufuatia kila familia iliyopo chini yao. Hivyo mwisho wa siku kila familia ilikuwa inapata urithi wa ardhi katika hiyo nchi ya Kaanani waliyokuwa wanaiendea.

Lakini sasa katika hilo kabila lenye watu wachache kuliko kabila zote, yaani kabila la Manase, kulikuwepo na mtu mmoja ambaye alikuwa mashuhuri katika kumcha Bwana, ambaye naye pia alihesabiwa kama kichwa, ambaye aliandikiwa urithi katika hiyo nchi waliyokuwa wanaiendea.. Mtu huyo aliitwa SELOFEHADI.

Lakini kwa bahati mbaya mtu huyo alikufa kabla ya kuzaa mtoto wa kiume ambaye angerithi sehemu ya urithi huo, akawa anao mabinti tu!. Hivyo kutokana na jambo hilo, wana wa Israeli wakalitoa jina lake miongoni mwa watakaopata sehemu ya ardhi katika hiyo nchi ya ahadi wanayoiendea..Kwasababu wanawake hawawezi kupewa urithi!..

Lakini tunasoma jambo moja la kipekee lililotokea..kwa mabinti wa huyo Selofehadi, hatujui Baba yao aliwafundisha nini, lakini tunasoma kwamba walifanya jambo la kipekee kugeuza sheria na taratibu za Israeli kwa IMANI. Kwani walipoona tu! Baba yao amekufa na sehemu yake ya urithi imeondolewa, hawakuridhika, wakasema watamwendea Musa na kudai haki ya baba yao.. Kwamba sehemu ya urithi wa baba yao wapewe wao!.. jambo ambalo ni kinyume na utaratibu, kwani wanawake hawana ruhusa ya kurithi mali..Lakini wanawake hawa watano wa familia moja!, walishindana mpaka wakapata haki yao hiyo.

Hebu tusome kidogo..

Hesabu 27:1 “Wakati huo wakakaribia hao binti za Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa jamaa za Manase mwana wa Yusufu; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya; Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa.

 2 Nao wakasimama mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote, mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema,

 3 Babaetu alikufa nyikani, naye hakuwamo katika mkutano wa hao waliojikutanisha kinyume cha Bwana katika mkutano wa Kora; lakini akafa katika dhambi zake mwenyewe; naye alikuwa hana wana wa kiume.

 4 Kwa nini basi jina la babaetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake babaetu.

5 Basi Musa akaleta neno lao mbele ya Bwana

6 Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

 7 HAO BINTI ZA SELOFEHADI WANANENA LILILO HAKI; KWELI UTAWAPA MILKI YA URITHI PAMOJA NA NDUGU ZA BABA YAO; NAWE UTAWAPA URITHI WA BABA YAO.

8 Kisha utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, MTU AKIFA, NAYE HANA MWANA WA KIUME, NDIPO UTAMPA BINTI YAKE URITHI WAKE.

9 Tena ikiwa hana binti, mtawapa nduguze urithi wake.

 10 Na ikiwa hana ndugu, mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake.

  11 Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama Bwana alivyomwagiza Musa”.

Kabla ya hapo hakukuwa na sheria kwamba mtu akifa, kama hana mtoto wa kiume urithi wake uende kwa mabinti wake, lakini Mabinti hawa watano, WALILIFUNGUA HILO KWA IMANI. Laiti wangeendelea hivyo, labda mpaka leo Israeli, mabinti wasingekuwa wanapata urithi wowote. Lakini kwa Imani ya hawa mabinti watano wa mtu mmoja ambao majina yao yalitajwa kama MALA, NOA, HOGLA,  MILKA, na TIRSA, waliweza kubadili majira kwa Imani..na kuwafanya mabinti wengine wote wa Israeli wafurahi.

Mwanamke au binti, unayesoma haya…kabla ya kwenda kujifunza kwa akina Eliya, na Elisha, na Paulo walio wanaume, hebu jifunze kwanza kwa wanawake hawa!, jinsi gani walivyopata urithi wao!, hawakwenda kwa waganga!..wala hawakwenda kwenye vikundi vya kijamii, wala hawakuanzisha mgomo!, wala vurugu.. bali walikimbilia kwa Musa, aliye mtumishi wa Mungu pekee wakati huo, huku wakiwa na hoja zilizo shiba,  ambaye huyo Musa alilipeleka hoja zao kwa Baba wa mbinguni, na Baba wa mbinguni akatoa majibu..

Lakini sasa aliyesimama kama Musa, ni Bwana Yesu, huyo ndiye wa kukimbilia ili kudai urithi wako..Ukienda na hoja zenye nguvu mbele zake, utapata haki yako.. Na hoja zenye nguvu tunazipata katika Neno la Mungu..

Isaya 41:21 “Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo”.

Isaya 43: 26 “Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, UPATE KUPEWA HAKI YAKO”

Jambo linguine la kujifunza juu ya mabinti hawa watano ni UMOJA!. Hakutoka binti mmoja na kumfuata Musa.. hoja yake isingekuwa na nguvu.. Lakini walipojiunga mabinti wote watano na kuwa kitu kimoja..Ndipo hoja yao ilipokuwa na nguvu. Ni vile vile hata sasa, ili Hoja zetu ziwe na nguvu mbele za Mungu, ni lazima tuungane watu wa familia moja, ambao imani yetu ni moja, Baba yetu ni mmoja, na ndipo tukamsogelee.. Tukienda kwa umoja kama huo, basi nirahisi sana kupokea majibu kuliko kwenda mmoja mmoja..

Mathayo 18:19 “Tena nawaambia, ya kwamba WAWILI WENU WATAKAPOPATANA duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni”.

Umeona hapo, anasema “wawili wenu”.. maana yake ni zaidi ya mmoja.. watakapopatana… maana yake kinachotangulia ni kupatana na kukubaliana… na baada ya kupatana, wakiliomba hilo jambo watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.

Bwana atusaidie tuwe Umoja na imani kama ya mabinti wa Selofehadi pamoja na Umoja, ili tuweze kufungua milango iliyofungwa mbele yetu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

Je! Israeli wote wataokolewa siku ya mwisho kulingana na Warumi 11:26?

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

NGUVU YA MNADHIRI WA BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post

ANAKUJA KAMA “MWIVI” NA SI KAMA “ASKARI” FANYIKA CHOMBO CHA THAMANI.

Kikawaida tumezoea kujifunza mambo mema kutoka kwa maaskari, kwamfano pindi tunapoyaona majeshi ya polisi katika magwaride yao, jinsi yalivyo na utaratibu mzuri, huwa tunavutiwa nayo.. tunapoyaona yakiwa katika mafunzo ya kukamata wahalifu, tunavutiwa nayo.. na hata wakati mwingine kuitamani kazi ya uaskari..

Lakini kamwe huwa hatuvutiwi na tabia za mwizi!, na wala hatutamani kuwa wezi. Kwasababu mwizi, anakuja kwa lengo la kuchukia kitu ambacho ni cha mwingine, pasipo taarifa!..jambo ambalo linaudhi sana na lisilokubalika.

Lakini Neno la Mungu linasema “Bwana Yesu atakuja kama mwivi” na “si kama askari”

Na kama tunavyojua mwizi lengo lake ni kuiba vile vya thamani na si kingine!. Hivyo Bwana Yesu anakuja duniani kuiba vile vilivyo vya thamani na kuviacha vile visivyo vya thamani..

Ulimwengu huu unafananishwa na NYUMBA.. ambamo ndani yake kuna watu wema na waovu. Na mkuu wa huu ulimwengu ni shetani, na malaika zake..

 Kama vile mwizi ajavyo usiku, haji kuiba vitu vibaya bali vile vizuri vyenye thamani, ndivyo Bwana Yesu atakavyokuja kuiba watu wake  (wale walio watakatifu na wenye thamani machoni pake) na kwenda nao mbinguni.

Kufumba na kufumbua, ufalme wa giza utashangaa baadhi ya watu hawapo tena duniani,  wale ambao walidhani wapo chini yao, wale ambao walidhani siku moja watawatumia kwa shughuli zao za giza.. watashangaa wametoweka duniani, siku hiyo hata shetani haijui.. ghafla atashangaa tu watu baadhi hawapo!

Luka 17:34 “Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

35  Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

36  Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa”

Je! Hiyo sio tabia ya mwizi??.. hebu jiulize unakaa na mwanao ndani, mmelala asubuhi unakuta hayupo na milango imefungwa kwa ndani vile vile, umekaa na mume wako ghafla unashagaa katoweka..upo kazini na mtu Fulani ambaye unamjua ni mtu anayejishughulisha sana na masuala ya wokovu, ghafla unashangaa hayupo!!!

Ndugu yupo Mwivi anayeutazama sasa ulimwengu kutoka juu!.. Anatazama vile vilivyo vya thamani!.. anapanga mipango!.. na mipango imeshakamilika kitambo sana, atakuja saa tusiyodhani.. kufumba na kufumbua wale tuliokuwa tunawajua wanampendeza Mungu, watanyakuliwa.. na mkuu wa ulimwengu huu (atakasirika) kwasababu vile vilivyo vya thamani vimeondoka!, kama vile mtu anavyoamka asubuhi na kukuta vitu vyake vya thamani vimeibwa, atajikuta anavichukia hata vile vilivyoachwa na hata kuviharibu kwa hasira.

Ndicho kitakachotokea baada ya unyakuo, wakati watakatifu wapo mbinguni,  wale walioachwa watakutana na ghadhabu ya mpinga kristo, katika dhiki kuu.

Je wewe ni chombo cha thamani?..

Kumbuka vyombo vya thamani ni wale wote waliomwamini Yesu, na kutubu dhambi zao, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu na kupokea Roho Mtakatifu.. Hao ndio biblia inawaita watakatifu.

Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.

Na hao ndio waliopo sasa katika shabaha ya Bwana, (yaani kuja kuwatwaa na kwenda nao mbinguni). Lakini wengine watakaosalia wakati wa kurudi Bwana, biblia inasema watapitia dhiki kuu, pamoja na mapigo ya siku ya Bwana.

Je wewe ni chombo cha thamani ulimwengu?.. au kisicho cha thamani?

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

USINIE MAKUU.

Je ni wanyang’anyi wawili waliomtukana Bwana Yesu au mmoja?

KWA HIYO NDUGU, VUMILIENI, HATA KUJA KWAKE BWANA.

Rudi nyumbani

Print this post