Title Devis

Masuke ni nini? (Luka 6:1, Marko 4:28)

Masuke ni nini  katika biblia?

Masuke ni ile sehemu ya nafaka inayotoa ua na mbegu ndani yake, Kwamfano Ngano suke lake linachipuka kwa pale juu, tazama picha, na nafaka kama mahindi suke lake ndio lile linalochipukia hindi lenyewe. Lakini nafaka yote sio suke, wala hindi lote sio suke, bali ile sehemu inayotoa mbegu au ua au tunda ndio inaitwa suke.

suke la ngano

suke la hindi

Hivyo  zamani, kama mtu akitaka kula ngano iliyo mbichi, ambayo kiafya ilikuwa haina shida, kwani jamii za watu wa mashariki ya kati kama vile wapalestina na waarab,  zamani na hata sasa, wanaoutarabu huo wa kula, nafaka mbichi, hususani ngano ambayo haijapikwa..

Na katika kula kule, ni sharti, uipukuse pukuse au uipure pure kwanza ili kuondoa yale makapi yake, ibakie tu ngano, kisha ndio uile.

Sasa zamani Mungu alishatoa maagizo, kuwa kama mtu ukisikia njaa, na akakutana na shamba la jirani pembeni yake, unayoruhusu ya kwenda na kula kile kilicho katika shamba lile, lakini sio kuvuna na kuondoka navyo.

Kumbukumbu 23:25 “Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako”.

Sasa utaona tukio lingine kuna wakati Bwana Yesu alikuwa anapita na wanafunzi wake, na wanafunzi wake walikuwa na njaa, na kwa bahati nzuri wakakutana na shamba la nafaka njiani, kama tunavyoijua habari wakaingia na kuanza kupura yale masuke ili wale ngano, na siku hiyo ilikuwa ni siku ya sabato.

Luka 6:1 “Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao”.

Na  mafarisayo walipoona  wakaanza kuwashutumu kuwa wanaihalifu sabato kwa wanachokifanya, ndipo Bwana Yesu akawaeleza habari ya alichofanya Daudi alipokuwa na njaa jinsi alivyokula ile mikate ya wonyesho ambayo sio sahihi yeye kuila bali makuhani tu peke yao.

Na mwisho kabisa  akawaambia mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.

Nasi pia Je ni sahihi kuingia katika shamba la mtu yeyote na kula matunda  ya mashamba yake, kwa mfano miwa yake, au machungwa yake bila ya kupewa ruhusu kwa kigezo cha mstari huo?

Tunapaswa tujue Israeli walipewa agizo hilo kama taifa, kwahiyo sheria hiyo ilijulikana kwa watu wote. Lakini sisi tuliokatika mataifa, tunaishi katikati ya makundi ya watu wengi, na asilimia kubwa sio wacha Mungu. Hivyo tunapaswa tutumie hekima, ya kwenda kuomba kwanza, vinginevyo ukikutana na mtu asiyekuwa na huruma ya kibinadamu anaweza kukuletea matatizo.

Bwana akubariki.

Hivi ni baadhi ya vifungu vingine vinavyolizungumzia Neno hilo  “Masuke”

Marko 4:28 “Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.

29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika”.

 

Mwanzo 41:5 “Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema.

6 Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.

7 Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.”

Walawi 23:14 “Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote”.

Soma pia Mathayo 12:1  na Marko 2:23

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.

HERODE NA PILATO, MAADUI WAWILI WAPATANA.

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya “heri mtu asiyekaa barazani pa wenye mizaha?”

 SWALI: Zaburi 1:1 inasema ..“heri mtu asiyekaa barazani pa wenye mizaha”. Je, ni mizaha gani inaongelewa hapo na kuna tofauti gani kati ya Utani na mizaha, na Kama hamna tofauti je hata kutaniana na mtu ni dhambi pia?


JIBU: Kuna mambo ya msingi tunatakiwa tujifunze katika vifungu hivyo, Embu tuvisome tena vizuri..Anasema;

Zaburi 1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha”.

Ukitazama hapo utaona vitu vitatu; KWENDA, KUSIMAMA, na KUKETI.

Vyote hivyo tumezuiwa tusivifanya. Hapo inaposema ‘kwenda’ maana yake ni ‘kutembea’. Hivyo kwa namna ya kawaida, tukizungumzia katika Nyanja ya dhambi, Kutembea kuna heri kidogo kuliko kusimama kwenye dhambi, na kusimama kuna heri pia kidogo kuliko kuketi chini. Kwasababu mpaka unaketi ni wazi kuwa unaonyesha ndio umefika, yaani umetia nanga, hapo ndio panakuvutia. Lakini vyote hivyo biblia imetukataza tusivifanye kwa makundi hayo matatu ya watu.

Kundi la kwanza ni la watu wasio haki

Watu wasio haki ni watu ambao hawana habari na Mungu, watu ambao hawana hofu ya Mungu hata kidogo, wapo tayari kutenda mambo maovu bila kujali kuwa ni machukizo mbele za Mungu au la. Hawa tumeonywa tusitembee katika mashauri yao.

Kundi la pili ni wakosaji.

Hawa ni watu wanaovunja amri za Mungu kwa makusudi, wanaweza wakasema wao ni wakristo, au wana hofu ya Mungu, lakini matendo yao, yanawathibitisha wao ni wakosaji utakuta (ni wazinzi, wafiraji, washirikina, wezi, warushi, n.k.) hao nao tumeambiwa tusisimame karibu nao.

Kundi la tatu ni Watu wenye MIZAHA.

Hawa ndio wabaya zaidi kwani sio tu ni waovu, na wakosaji, bali wamevuka hiyo mipaka hadi kufikia hatua ya kuleta mizaha mpaka kwenye mambo matukufu ya Mungu, kudhihaki, kukejeli, kukashfu Neno la Mungu, na wokovu kwa ujumla kwao ni jambo la kawaida.. Biblia inasema..

2Petro 3:3 “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,

4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa”.

Hawa tumeonywa tusiketi nao kabisa, kwasababu wapo mabarazani (maana yake kwenye majukwaa, au sehemu yenye mkusanyiko wa watu).

Ni mara ngapi utaona  watu wanaifanyia biblia comedy kwenye majukwaa na watu wamelipa kiingilio, wameketi pale chini wanacheka na kufurahia, huku wakimtaja Bwana Yesu, au mmojawapo wa manabii wa kwenye biblia, na kuwatolea mifano kana kwamba Yule biblia ni kitabu cha story za vichekesho? Ni mara ngapi umewaona kwenye tv au umewatazama youtube?. Hao tumeambiwa tujitenge nao. Hata tusisikilize vichekesho vyao, kwasababu ni machukizo makubwa mbele za Mungu.

Hivyo tukirudi kwenye swali? Je kuna tofauti gani kati ya utani na mzaha,?

Mzaha ndio unaopelekea utani, hivyo ni vitu vinavyoshadidiana. Na pia sisi kama wakristo, hatupaswi kuwa na mizaha kwenye mambo yanayohusiana na imani zetu, au yanayovuka mipaka ya maadili yetu. Vinginevyo tutakuwa tunatenda dhambi. Biblia inasema hivi;

1Wakorintho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”

Kitu kimoja kinachoharibu tabia ya Mkristo, ni mizaha… Mtu anayejizoeza mizaha, ndivyo anavyopalilia tabia nyingine mbaya ndani yake kama uzinzi, na uongo..Siku zote uzinzi unaanzia kwenye mizaha na utani uliopitiliza, vile vile tabia ya uongo inafunikwa na kivuli cha utani..

Mithali 26:19 “Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, JE! SIKUFANYA MZAHA TU?”

Hivyo tunapaswa tuwe na kiasi kama Mtume Paulo alivyomwonya  Timotheo

2Timotheo 4:5 “Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote,….”

Bali tufurahishwe na sheria za Bwana.

Mithali 19:29 “Hukumu zimewekwa tayari KWA WENYE MZAHA; Na mapigo kwa mgongo wa wapumbavu”

Tukifanya hivyo. Shetani hatatuweza.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI

UVUMILIVU WA MUNGU ULIPOKUWA UKINGOJA.

CHEMBE YA NGANO ISIPOANGUKA KATIKA NCHI, IKAFA,

KUNA UMUHIMU WA KUWA MTU WA KURIDHIKA.

Je! ile habari ya watu wawili wenye pepo inajichanganya?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

Tusome..

Matendo 3:1  “Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.

2  Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika MLANGO WA HEKALU UİTWAO MZURİ, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu”.

Biblia inasema Hekalu lilijengwa vizuri sana, na kwa vitu vya thamani. (1Wafalme 6, imeelezea mwonekano wa hekalu la Mungu). Hivyo Hekalu lilikuwa limejengwa kwa vitu vya thamani, na lilikuwa linamwonekano mzuri..

Tunalithibitisha hilo tena katika kitabu cha Luka..

Luka 21:5  “Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, JİNSİ LİLİVYOPAMBWA KWA MAWE MAZURİ na sadaka za watu, alisema,

6  Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa”.

Umeona?. Kwahiyo Hekalu lilikuwa zuri, na kama tunavyojua..Mlango wa kuingilia mahali popote siku zote unatengenezwa kuwa mzuri kuliko, milango mingine ya ndani midogo midogo, Mlango wa mapokezi unakuwa unapambwa sana. Mageti ya kuingilia mijini yalikuwa yanapambwa sana kuliko mageti madogo madogo ya ndani ya hiyo miji, hali kadhalika hata leo mageti ya kuingilia kwenye maonyesho fulani huwa yanapambwa sana ili kuvutia wanaokuja, na kuyapandisha hadhi maonyesho hayo.

Na ndio hivyo hivyo, Mlango wa kuingilia hekaluni ulikuwa umepambwa sana na wenye mwonekano mzuri, hivyo Wayahudi wakauita Mlango MZURI kwasababu kwanza, ndio ulikuwa mzuri kwa mwonekano kuliko milango yote, na ndio mlango wa kuingilia Nyumbani kwa Mungu wa mbingu na nchi. Hivyo wakauita MLANGO MZURI.

Matendo 3:9 “Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu.

10  Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye MLANGO MZURİ WA HEKALU; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata”.

Lakini pamoja na uzuri wake wote, Bwana Yesu alisema hapo kwenye (Luka 21:6)..halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa, na kweli miaka michache tu baadaye hekalu hilo lilipotea, na hakukuwa tena na kitu kinachoitwa MLANGO MZURI, Israeli. Hata waliokimbilia kuingia katika huo mlango walikufa kwa upanga.

Lakini biblia imetaja mlango mwingine MZURI ambao huo unadumu milele..

Tuusome..

Yohana 10: 9 “ MİMİ NDİMİ MLANGO; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

10  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; MİMİ NALİKUJA İLİ WAWE NA UZİMA, KİSHA WAWE NAO TELE.

11  Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.

Yesu ndiye MLANGO MZURI unaodumu milele. Na alikuja ili tuwe na Uzima, kisha tuwe nao tele, je umempokea?. Kama bado basi maisha yako yapo hatarini, hivyo mpokee leo akupe uzima wa milele.

Kama hujampokea na unatamani kufanya hivyo sasa, basi uamuzi unaofanya ni wa thamani, kwa msaada wa namna wa kuongozwa sala ya Toba, basi fungua hapa >> KUONGOZWA SALA YA TOBA.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

YAKINI NA BOAZI.

Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

Kwanini Samweli aliruhusuiwa kuhudumu hekaluni kama vile Walawi wakati yeye ni mu-Efraimu?

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

USINIE MAKUU.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Karibu tujifunze biblia.

Neno la Mungu linasema katika..

Warumi 12:3 “Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu ASINIE MAKUU KUPITA ILIVYOMPASA KUNIA; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha Imani”.

Sasa kunia makuu kunakozungumziwa hapo ni kupi?

Tukiendelea mbele kidogo katika mistari hiyo inayofuata tutapata jibu kamili…

“4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;

5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.

6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.”

Umeona?. Maana yake ni kwamba…Usiwaze moyoni mwako, na kujiona kuwa… “unaweza kuwa na karama zote au nyingi”.

Kwamfano mtu mmoja, atataka yeye ndio awe mchungaji, yeye ndio awe Nabii, yeye ndio mwalimu, yeye ndio Mtume, yeye ndio Muinjilisti n.k… Kwaufupi karama zote za rohoni yeye ni zake. Anajiona yeye hawezi kuwa na karama moja tu”..yeye hawezi kuwa mwinjilisti tu peke yake ni lazima atakuwa ni Nabii pia..hawezi kuwa Mwalimu peke yake ni lazima atakuwa Mwalimu na Nabii mkuu, hawezi kuwa Mtume tu peke yake, ni lazima atakuwa ni Mtume na Nabii mkuu.. N.k Sasa hiyo ni mifano tu, ambayo ndio biblia inatuonya kwamba Tusinie Makuu kuliko tunavyopaswa kunia.

Roho ya kunia Makuu, inaua roho ya unyenyekevu ndani ya mtu, na hatimaye kuundoa kabisa uwepo wa Mungu ndani ya mtu.

1Petro 5: 5 “…Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema”

Na karama tulizopewa sio za mashindano wala za kujionyesha yupi bora Zaidi, au yupi mwenye neema kubwa zaidi. Karama yeyote inayotumika kwa matumizi hayo, tayari imeshavamiwa na shetani. Karama tulizopewa ni za kuhudumiana ili kuwakamilisha watakatifu na kazi ya huduma itendeke ili mwili wa Kristo ujengwe. na sio kuringishiana wala kuzitumia hizo kujinyanyua juu ya wengine.

Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;

12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”;

Bwana atusaidie.

Kama bado hujampokea Kristo, mlango wa Neema upo wazi sasa, ila hautakuwa hivyo siku zote. Hivyo geuka leo, na kumkabidhi Maisha yako, kwasababu muda tuliobakiwa nao hapa duniani sio mwingi, wakati wowote parapanda ya mwisho inalia na Kristo atalinyakua kanisa lake, kitakachosalia huku duniani ni hukumu. Hivyo mimi na wewe tusiwe miongoni mwa watakaoangukia kwenye hukumu ya Mungu.

Kumbuka kuzimu ipo na mbingu vile vile ipo. Na Uzima au Mauti, tunachagua tukiwa hapa hapa duniani, baada ya kifo hakuna nafasi ya kufanya uchaguzi. Hivyo fanya uamuzi uliobora sasa kabla siku zako za kuishi hapa duniani hazijaisha.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.

KARAMA YA MUNGU NI UZIMA WA MILELE.

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

BONDE LA KUKATA MANENO.

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neema ni nini?

Neema ni nini kibiblia?


Neema ni “upendeleo usio na sababu” au kukubaliwa kusikostahili. Upo upendeleo wenye sababu na usio na sababu. Mfano wa upendeleo wenye sababu ni huu tulionao sisi wanadamu, sisi tunapendelea walio wetu, yaani watu tunaowajua au wenye manufaa katika Maisha yetu kama vile ndugu zetu, marafiki zetu n.k.

Hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kumpendelea adui yake..Hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kumpendelea yule mtu anayemuudhi. Hakuna mwanadamu yeyote mwenye uwezo wa kutoa huo upendeleo, isipokuwa Mungu peke yake. Ni Mungu tu ndio mwenye uwezo wa kufanya hivyo, Mungu ana uwezo wa kumpendelea yule mtu ambaye hastahili kabisa mbele zake.

Sasa ili tuielewe neema vizuri hebu soma hichi kisa..

Mathayo 20:9  “Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.

10  Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.

11  Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba,

12  wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.

13  Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?

14  Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.

15  Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?

16  Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho”.

Umeona hapo, hao waliofanya kazi lisaa limoja tu wamelipwa sawa na wale waliotaabika mchana kutwa. Ni kama vile wamependelewa, lakini hakukuwa na  sababu yeyote iliyowafanya wao walipwe sawa na wale wengine waliotaabika mchana kutwa, basi tu ni kama wamependelewa, wangepaswa walipwe kiwango kidogo Zaidi ya wenzao, na Zaidi ya yote hao ndio wangepaswa walipwe wamwisho, lakini chaajabu ndio wametangulia kulipwa…Sasa huo ndio mfano wa NEEMA.

Lakini ipo NEEMA moja kubwa sana ambayo sisi wanadamu tumepewa na Mungu. Nayo hiyo si nyingine Zaidi ya UZIMA WA MILELE. Baada ya anguko pale Edeni, hatukustahili tena tupate nafasi ya kuishi milele, Habari yetu ndio ilikuwa imeishia pale. Hatujui labda angeamua kuumba viumbe wengine, hilo hatulijui..lakini shughuli yetu ndio ilikuwa imeishia pale..

Lakini Mungu akatazama, na pasipo sababu yoyote (kama bahati tu!) ikatokea akapenda tu kutupa UZIMA WA MILELE, Wala usidhani ni kwasababu tulikuwa tunatilisha huruma sana mbele zake, ndio sababu akatuhurumia akatupa uzima wa milele..la!, wala sio sababu tulimwomba. Ni neema tu!..Ni neema tu…

Hakukuwa na sababu yoyote ya sisi kuupata tena uzima wa milele. Wala Mungu kutupoteza daima isingekuwa ni kitu kikubwa sana kwake, kwasababu kabla ya kutuumba sisi alikuwepo milele huko mamilioni na mamilioni ya miaka, alikuwepo huko peke yake pasipo sisi..Kwahiyo kamwe tusifikiri kwamba tulikuwa ni lulu sana mbele zake, ndio maana akatupa tena nafasi ya kuupata uzima wa milele.. Ni Neema tu!..Ni neema tu!..tumependelewa pasipo sababu yeyote. Angeweza kufuta na kuumba wengine na angetusahau sisi moja kwa moja…

Na alianza mpango huo wa wokovu kwa kumtuma Mwanawe mpendwa Yesu Kristo, ambaye kila amwamini huyo ATAPATA UZIMA HUO WA MILELE.

Yohana 1:14  “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; AMEJAA NEEMA NA KWELI”.

Kwahiyo hebu tutafakari kama tumeokolewa kwa neema, (maana yake tumepata upendeleo ambao hatukustahili)..tunawezaje leo kuudharau Msalaba wa Yesu?.

Biblia inasema katika…

Waebrania 2:3  “sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia”.

Neema ya Msalaba sio kitu cha kuchezea hata kidogo. Kwasababu ndio kitu pekee kilichoificha ghadhabu ya Mungu juu yetu sasa, ikiondoka Neema hapo ndio tutajua kuwa hatukuwa watu maalumu (special) sana mbele za Mungu. Hapo ndipo tutakapojua kuwa kumbe Mungu anaweza kuishi bila sisi.

Waebrania 10:28  “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29  Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?”.

Ndugu tuko ukingoni kabisa mwa hii Neema kuisha, Hii nafasi tuliyopewa ya kuokoka haitakuwepo milele. Siku parapanda ya mwisho itakapolia ndio utakuwa ukomo wa hii neema. Na kwa wale watakaoukosa unyakuo ndio watahakiki nini maana ya neema maana, watakapoona kilio cha maumivu yao hayasikiwi na Mungu, wakiwa katika ziwa la moto, watakapokuwa wanaungua na kulia kwa machozi, ndipo wakiwa huko watajua kuwa hisia zao si kitu mbele za Mungu, wataona kumbe hatukuwa watu maalumu sana, mbele za Mungu kama tulivyokuwa tulikuwa tunadhani au tunahubiriwa, ndipo watajua kuwa waliichezea neema..

Ndugu mimi na wewe tusiwe miongoni mwa watakaotengwa na Mungu milele. Leo hii mpokee Kristo kama hujampokea kwa kutubu dhambi zako zote ulizokuwa unazifanya na kuziacha kabisa, Kristo yupo mlangoni mwa moyo wako sasa, anatamani aingie ili ayaokoe Maisha yako..Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa na wala si kesho basi fungua hapa >> SALA YA TOBA

Neema ya Kristo ikae nasi sote.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

KUZIMU NI WAPI

ITAFAKARI SIKU YA HUKUMU.

KITABU CHA UZIMA

Ni kweli mtu anaweza akafa lakini roho yake ikawa inatumika kama msukule (kumilikiwa na mtu fulani kwa wakati) mahali pengine?

Rudi Nyumbani:

Print this post

VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.

Hivi ni baadhi ya vipimo mbalimbali vilivyotumika kupima vitu katika biblia, Vikikaridiwa kwa vipimo vya kisasa.

Vipimo vya Urefu.

  • Mwanzi = 2.7 Mita
  • Pima 1= Mita 1.8 (Futi 6)
  • Shubiri = sm 22.2
  • Dhiraa = 0.5 Mita
  • Mkono 1= SM 44.7

Vipimo vya vitu vikavu.

  • Pishi =Lita 2
  • Efa = Lita 22
  • Kabi = Lita 1

Vipimo vya vimiminika (maji maji)

  • Logi 1= 0.31
  • Hini 1= Lita 3.67
  • Bathi 1= Lita 22
  • Kori 1= Lita 220
  • Homeri 1 = lita 208

Vipimo vya uzito

  • Shekeli [Shekeli 1 = Gramu 11.42]
  • Mina [Mina 1 = Gramu 570]
  • Talanta [Talanta 1= kg 34.2]
  • Dinari [Dinari 1= Gramu 3.85]
  • Beka 71g………………….Kutoka 38:26
  • Gera 57g……………….Kutoka 30:13

Je!  utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp? Kama jibu ni ndio, basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312  tukuunge.

Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?

SWALI: Ni nini alichokifanya Yakobo kwa ile mifugo ya Labani mpaka ikaongezeka kwake kwa wingi kuliko ya mjomba yake?


Tukisoma biblia tunaona baada ya Yakobo kumtumkia mjomba yake Labani kwa miaka 14, ilifika wakati akataka sasa kwenda kujitegemea na kuilea  familia yake mwenyewe. Ndipo Labani akamwuliza amlipe nini?

Sasa kwasababu Yakobo alikuwa anachunga mifugo yake, na kwa njia hiyo Mungu alibariki Labani kuwa na mifugo, basi Yakobo akamwomba  sehemu ya mifugo yake akaichunge ili ile itakayozaliwa baadaye iwe ni mshahara wake. Ndipo Labani akakubali akaingia naye mapatano kuwa Yakobo ataichukua tu ile mifugo yenye madoa na marakaraka, na myeusi, lakini ile mingine atamwachie yeye. Na kwamba kile kitakachozaliwa kikiwa ni cha marakaraka basi kitaendelea kuwa ni cha Yakobo lakini kikiwa ni kingine basi mali hiyo ni ya Labani.

Hivyo, Labani alivyoona hivyo, akakubali kwa moyo mkunjufu, kwasababu alijua kabisa hilo haliwezekani, na hata likiwezekana basi litakuwa ni kwa uchache sana. Ndipo wakakubaliana kwa moyo mmoja,Yakobo akawachukua wale wenye madoadoa na marakaraka wakatenganana kwa umbali wa mwendo wa siku tatu.

Ndipo Yakobo akabuni njia yake. Tusome..

Mwanzo 30:35 “Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe.

36 Akajitenga na Yakobo mwendo wa siku tatu; naye Yakobo akachunga wanyama wa Labani waliosalia.

37 Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito.

38 Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa.

39 Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka.

40 Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani.

41 Ikawa kila walipopata mimba wanyama wenye nguvu, Yakobo akaziweka zile fito mbele ya macho ya hao wanyama katika mabirika ili kwamba wachukue mimba kati ya zile fito,

42 lakini wanyama walipodhoofika hakuziweka zile fito. Basi wale dhaifu walikuwa wa Labani, na wenye nguvu walikuwa wa Yakobo.

43 Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda”.

Kama tunavyosoma hapo, Yakobo, alikwenda kusimamisha fito za miti, mahali ambapo mifugo inanywea maji, kwa kawaida mifugo inakutanika mingi sehemu moja mahali pa kunywea maji na hivyo ni rahisi kukutana kwa ajili ya kuzaliana., Lakini biblia haituelezi chochote, ni nini lengo la Yakobo kufanya vile, alikuwa analengo gani pale watakapozitazama zile fito, pengine labda alidhani zitasisimua homoni vina saba vyao na kusababisha wazae wanyama wenye maraka raka, au zile fito ziliwasaidia katika kuzaliana kulingana na jamii yao kwa haraka, hatujui imani ya Yakobo ilikuwa ni nini, pengine alikuwa anajaribu kutumia njia za kisayansi aliyoingundua mwenyewe au kusimuliwa, vilevile hatujui  biblia haijatueleza..

Lakini tunachojua ni kuwa alichokifanya kwa mitazamo yake sicho ambacho kiliwapelekea wale kondoo zake na mbuzi zake kuzaliwa wenye marakaraka au madoa doa.. Utakuja kuliona hilo katika mistari inayofuata, alipokuwa akimwambia Raheli juu ya ndoto aliyoiota.

Mwanzo 31:7 “Na baba yenu amenidanganya, akabadili mshahara wangu mara kumi; lakini Mungu hakumwacha kunidhuru.

 8 Aliposema, Walio na madoadoa watakuwa mshahara wako, wanyama wote wakazaa madoadoa. Aliposema, Walio na milia watakuwa mshahara wako, ndipo wanyama wote wakazaa wenye milia.

 9 Hivi Mungu akamnyang’anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi.

10 IKAWA, WAKATI WALE WANYAMA WALIPOCHUKUA MIMBA, NALIINUA MACHO YANGU NIKAONA KATIKA NDOTO, NA TAZAMA, MABEBERU WALIOWAPANDA HAO WANYAMA WALIKUWA NA MILIA, NA MADOADOA, NA MARAKARAKA.

11 Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa.

Unaona? Hivyo si fito zilizowafanya wale kondoo na mbuzi wazae wanyama wenye marakaraka bali ni nguvu za Mungu rohoni,.

Hata sasa, hiyo ni kutuonyesha kuwa Mungu akitaka kukubariki, haijalishi bidii zako nyingi kiasi gani, au uvumbuzi wako unaoudhani utakusaidia, Ukiwa mcha Mungu, ni Mungu ndiye atakaye kupa uwezo huo wa kuvipata. Japokuwa inaweza kuonekana kwa nje kama ni wewe ndio uliyefanya kwa ushapu wako. Bali kiuhalisia si wewe, ni Mungu ndiye aliyekutia nguvu.  Kama Yakobo asingekuwa mcha Mungu, unadhani ni nini angeambulia pale kama sio majani ya fito tu.

Kumbukumbu 8:12 “Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake;

13 na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;

14 basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa……………….

17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo

18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo”.

Bwana atusaidie tulishike agano lake.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.

Ni udhaifu gani ulikuwa katika macho ya Lea mke wa Yakobo?

Yakobo alikuwa na watoto wangapi?

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kikoto ni nini?(Yohana 2:15)

Kikoto ni nini?


Kikoto ni aina ya kiboko mfano wa mjeledi. Tazama picha juu.

Tunaweza kuona wakati ule Yesu alipokwenda Hekaluni na kukuta watu wameigeuza nyumba yake kuwa pango la wanyang’anyi, tendo alilolifanya ni kuunda aina hii ya mjeledi, kwa kuusokota kwa kamba mbeleni. Ili awaadhibu vizuri wale watu waliokuwa wanasitiri maovu yao kule, waliokuwa wanafanya biashara zao mule ndani , pamoja na mifugo yao.

Yohana 2:13 “Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara”.

Ili kujua Bwana Yesu alimaanisha nini kusema msiigeuze nyumba ya Baba yangu kuwa pango la wanyang’anyi fungua hapa>> USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

Hiyo ni kutuonyesha kuwa wivu wa Mungu sikuzote unaleta adhabu.

Na adhabu hii ipo kwenye makundi mawili;

Kundi la kwanza: Ni kwa wale watu wanaolinajisi hekalu lake leo hii (yaani Kanisa), kwa kufanya mambo ambayo hayana misingi ya kiimani. Mfano kuigeuza kazi ya Mungu kama biashara, kuabudu masanamu, kwenda nusu uchi kanisani, n.k.

Na kundi la pili: Ni lile la watu wanaolinajisi hekalu lake (yaani Miili yao) kwa kufanya mambo ambayo hayampendezi. Kama vile uzinzi, uuaji, ulevi, n.k. Kwani biblia inasema;

1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

19 Au hamjui ya kuwa MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Na inasema tena;

1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Unaona? Na kikoto hichi tayari kipo mkononi mwa Bwana. Hivyo tujichunguze na sisi tumelitunzaje hekalu lake?  Kama tumekuwa tukiliharibu, ni heri tumgeukie kwa Bwana sasa, kabla ya wakati wa kuharibiwa haujafika. Kwasababu ukishafika na tukakutwa katika hali kama hizo, tujue kuwa hakuna neema tena.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya uvuvio?.

Nini maana ya kuabudu?

MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

MADHARA YA KUPUUZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

Mataifa ni nini katika Biblia?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya uvuvio?.

Uvuvio ni Nini?

Neno uvuvio maana yake ni “kupuliza hewa kwa nguvu”..unapopuliza makaa ya moto maana yake unayavuvia makaa. Unaweza kuuvuvia makaa ya moto kwa mdomo au pepeo.

Ayubu 20: 26 “…..Moto ambao HAUKUVUVİWA na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake”.

Maana ya mstari huo ni kwamba, moto ambao umezuka tu wenyewe ambao haujapulizwa na mtu utaiteketeza nyumba yake.. Jambo ambalo ni kweli, kwani nyumba zote zinazoungua, ni kutokana na moto, uliojivuvia wenyewe wakati mtu huyo hayupo..kwasababu kama mwenye nyumba angekuwa ni yeye kauvuvia huo moto asingeruhusu, auvuvie mpaka uwe mwingi kiasi cha kuunguza hema yake, anguvuvia kiasi cha kutosha kupikia au kufanyia shughuli zake ndogo, na kuuzima atakapomaliza. Pia unaweza kusoma Isaya 57: 13, inazungumzia habari hiyo hiyo ya Uvuvio.

Sasa tukirudi katika Agano jipya, tunaona biblia imelifananisha tendo la kupokea Roho Mtakatifu, na uvuvio.

Yohana 20: 22  “Naye akiisha kusema hayo, AKAWAVUVİA, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu”.

Maneno hayo aliyazungumza Bwana, kama ahadi ya kitu kitakachokuja kuwatokea wanafunzi wake siku chache mbele…Na tarehe ilipofika, iliyopangwa na Mbingu ya wao kumpokea Roho Mtakatifu (yaani siku ile ya Pentekoste)..Roho aliwafikia kama UVUVİO WA UPEPO.

Maana yake ni kwamba Roho Mtakatifu alikuja juu yao kama UPEPO ULİOPULİZWA.. Na kama unajua kazi ya upepo ni kuchochea moto. Kikawaida upepo unavyozidi kuwa mkali ndipo moto na wenyewe unavyozidi kuwaka na kusambaa kwa kasi na kusababisha madhara makubwa..

Matendo 2: 1  “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2  Kukaja ghafula toka mbinguni UVUMİ KAMA UVUMİ WA UPEPO WA NGUVU UKİENDA KASİ, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3  Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4  Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”.

Ule upepo ulianza kuchochea, cheche ndogo iliyokuwepo ndani yao, na kufanya Moto mkubwa kuwaka ndani yao, Moto ule ulianza kukaa kwanza kwenye ndimi zao, kila mmoja akaanza kuzungumza kwa lugha mpya, na maneno yenye moto, unaounguza kila kazi za ibilisi na unaoteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo, na baadaye ukasambaa katika mwili wao wote, na kuwafanya waweze kufanya miujiza na ishara zisizo za kawaida.

Hivyo Roho Mtakatifu hata sasa yupo, Ahadi ile hawakupewa mitume pekee yao..Biblia inasema hivi..

Matendo 2:37  “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  KWA KUWA AHADİ Hİİ Nİ KWA AJİLİ YENU, NA KWA WATOTO WENU, NA KWA WATU WOTE WALİO MBALİ, NA KWA WOTE WATAKAOİTWA NA BWANA MUNGU WETU WAMJİE.

40  Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi”.

Biblia inasema hapo katika mstari wa 39, kwamba ahadi hiyo ya Roho Mtakatifu ni kwa watu wote, watakaomjia Bwana. Yaani mimi na wewe, na mtu mwingine yeyote, Sasa tunamiaje Bwana?..Biblia imetupa jibu katika huo mstari wa 38 kwamba….. “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Ndugu, inawezekana kuna kipawa Mungu kaweka ndani yako na haujijui, inawezekana kuna huduma ameweka ndani yako kwaajili ya kuujenga ufalme wake, na haujui au nguvu yako ni ndogo (ipo kama cheche tu).. Hiyo ni kwasababu UVUVIO haujapita juu yako.. moto uliopo ndani yako bado haujachochewa, lakini siku utakapochochewa ndipo utakapoona tofauti yako ya siku hizo na siku za nyuma. Kama unatamani uvuvio huo, fomula ni hiyo hapo juu.. “tubu dhambi zako, kwa kumaanisha kuziacha kabisa, kisha katafute ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu sawasawa na Matendo 2:38, na Bwana ataleta uvuvio wa Roho Juu yako.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Nini tofauti kati ya Roho Mtakatifu na Roho Takatifu?

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

6# SWALI : Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe, Kama umeamka salama ni jambo la kumshukuru Mungu sana, hivyo nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya Uzima ya Bwana wetu, ambayo ndio chakula cha roho zetu.

Neno la Mungu linasema..

Yeremia 7: 9 “Je! Mtaiba, na kuua, na kuzini, na kuapa kwa uongo, na kumfukizia Baali uvumba, na kuifuata miungu mingine ambayo hamkuijua;

10 KISHA MTAKUJA NA KUSIMAMA MBELE ZANGU KATIKA NYUMBA HII, iitwayo kwa jina langu, na kusema, Tumepona; ILI MPATE KUFANYA MACHUKIZO HAYO YOTE?

11 Je! Nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, imekuwa PANGO LA WANYANG’ANYI MACHONI PENU? Angalieni, mimi, naam, mimi, nimeliona jambo hili, asema Bwana”.

Tusome tena…

Mathayo 21: 13  “akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYI

Umewahi kujiuliza kwanini, kwanini Bwana alitumia huo usemi…. “bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYİ”. Umewahi kutafakari pango la wanyang’anyi ni kitu gani?.

Siku zote wezi/vibaka wanakuwaga na maskani yao wanayojifichia, ambayo kwao ndio sehemu salama, na inakuwa ni sehemu ya maficho kwa muda, mara  nyingi inaweza kuwa kwenye kipori fulani, au kwenye jengo fulani ambalo halijakamilika, au kwenye mapango ambayo ndani yana giza, Lengo ni kwamba wakishamwibia mtu, wanakimbilia huko, kujificha kwa muda, na baadaye kurudia tena kufanya uhalifu wao…hivyo inakuwa ni ngumu kuwakamata.. Na mara nyingi kwenye hayo maficho yao, ndio sehemu zao za kuchezea kamari, au kuvuta sigara, au kufanyia biashara zao haramu kama za kuuziana mihadarati n.k

Mfano kamili wa leo, mtu atatoka kufanya uasherati, lakini mtu huyo huyo jumapili atakwenda kanisani…jumatatu atarudia kufanya kile kile kitu na kurudi tena kanisani, jumapili inayofuata…Mtu huyo ameigeuza nyumba ya Mungu kuwa pango la wazinzi, kanisa ni sehemu yake ya kujisitiri kwa muda, ili aonekane kwamba na yeye ni mkristo, au ili ajifariji moyoni kwamba bado anampenda na kumjali Mungu, na ili ajifariji kwamba jamii inamwona msafi..Lakini kiuhalisia hana mpango wa kuacha uasherati wake, wala hana mpango wa kumwacha yule mtu anayeishi naye ambaye wanayefanya naye uasherati.

Mwingine ni fisadi, au tapeli lakini atahudhuria kanisani kama ilivyo ada, na wala haendi kwa lengo la kubadilika, bali anakwenda pale kama sehemu yake ya kusitiri maouvu yake..

Ndugu yakumbuke maneno ya Bwana.. “Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa PANGO LA WANYANG’ANYİ”.

Usiigeuze nyumba ya Mungu kuwa ni sehemu yako ya maficho ya dhambi zako…bali pageuze kuwa mahali pa sala, mahali patakatifu pa kukujenga roho yako. Kadhalika nyumbani kwa Mungu sio mahali pa kwenda umevaa nusu uchi, umevaa vimini, au umepaka wanja na lipstick, au umenyoa kiduku, kwa ufupi sio mahali pa kutangaza mwili wako au biashara yako…pale ni mahali pa kumheshimu Mungu.

Kama Bwana alizipindua zile meza za wafanya biashara kwenye nyumba yake, hatashindwa kuipindua biashara ya kuuza mwili wako huo usio na staha uliokuja kuuza pale kwenye nyumba yake. Kama umeamua kutangaza biashara ya mwili wako, yapo mapango mengi huko mitaani, lakini usijaribu kuiguza nyumba ya Mungu kuwa kama mojawapo ya mapango hayo.

Kama hujampa Kristo maisha yako, wakati ni sasa. Tubu leo naye atakusamehe bure kabisa. Kumbuka Kristo anarudi, siku moja hutasikia maneno kama haya ambayo unaona sasa ni upuuzi na kelele..wakati huo unyakuo utakuwa umepita, na hutasumbuliwa sumbuliwa na mahubiri tena. Lakini akiamua kutubu leo, Kristo atakupokea kama neno lake linavyosema..katika Yohana, na atakupa Roho Mtakatifu atakayekuongoza katika kuijua kweli yote.

Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”.

Maran atha

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

LIVUNJENI HEKALU HILI, NAMI KATIKA SIKU TATU NITALISIMAMISHA.

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

Bawabu ni nani/nini?

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

Rudi Nyumbani:

Print this post