Category Archive Mafundisho ya msingi

USILIPIZE KISASI.

Kwanini hatupaswi kujilipiza kisasi?… Kwasababu maandiko yanatufundisha kuwa kisasi ni juu yake yeye atalipa.

Warumi 12:19 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, KISASI NI JUU YANGU MIMI; MIMI NITALIPA, ANENA BWANA.

20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake”.

Tabia ya kujilipiza kisasa Bwana Mungu aliikataa tangu Mwanzo na Bwana Yesu akaja kuithibitisha tena katika Mathayo 5.

Tunaona baada ya Kaini kumwua ndugu yake Habili kwasababu ya wivu, Mungu alimlaani Kaini kwa kosa lile..

Lakini Mungu hakumwua Kaini bali alimlaani juu ya ardhi kwamba ataendelea kuishi lakini ardhi itamkataa… Kila kilimo atakachokifanya juu ya ardhi hakitafanikiwa, ndio maana baada ya pale hatuoni Kaini na uzao wake wakiendelea na kazi yake ya ukulima badala yake tunasoma wanaanza kutengeneza vyuma, na wapiga filimbi (Mwanzo 4:17-22).

Sasa baada ya Bwana Mungu kumlaani Kaini alijua kabisa kuna watu watakuja kusikia habari zake kwamba ni mwuaji, na pia kalaaniwa na Mungu, hivyo watataka wajichukulie hukumu aidha ya kumwua au kumnyanyasa…

Sasa Mungu kwa kulijua hilo, akamwekea Kaini alama, ili kila mtu atakayemwona asimguse…

Na alama hiyo ikaendelea kuwepo juu ya Kaini na uzao wake, iliyowatofautisha uzao wa Kaini na uzao mwingine.

Na Bwana akasema mtu atakayemwua Kaini, basi atalipwa kisasi mara 7,

Mwanzo 4:13 “Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.

14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

15 BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga”

Hivyo watu walivyosikia hivyo wakaogopa kumnyooshea mikono yao Kaini, kwasababu walijua kuna adhabu kubwa sana katika kufanya hayo…

Umeona?..Kumbe kisasi na hasira ndani ya maisha ya mtu ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu..
Ndivyo maandiko yanasema…

Mithali 24:17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;

18 BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.

Ikiwa na maana kuwa kama adui yako amekutenda mabaya na wewe usimrudishie yale mabaya, mwombee Bwana ambadilishe, itakuwa heri kwako…na utasikia ule mzigo umeondoka ndani yako…

Lakini kama ukifikiri kwamba njia ya kuondoa mzigo (uchungu) ndani yako ni wewe kujilipiza kisasi, nataka nikuambie kuwa ndio utauongeza badala ya kuupunguza, kwasababu utakayemlipa kisasi utakuwa umeweka uadui naye hivyo shetani anaweza kumtumia tena kufanya jambo lingine kwa wakati mwingine kwa njia nyingine…lakini lililo baya zaidi ni kwamba utakuwa umekosana na Mungu pia.

Sasa nini kifanyike ili kuishinda nguvu ya kisasi ndani yako?

1. Wokovu.

Wokovu ndio mlango wa Imani. Ni lazima kumwamini Yesu na kumkiri.


2. Maombi (yanayoambatana na mifungo).

Baada ya kuokoka ni lazima uwe mtu wa maombi. Maombi yatakufanya uwe na nguvu za kiroho ambazo zitakusaidia wewe kushinda dhambi.

3 .Kusoma Neno.

Neno la Mungu (biblia) litakusaidia kukujenga utu wako wa ndani. Kwamfano Neno lifuatalo ukilijua litakusaidia wewe kutolipiza kisasi.

Mhubiri 7:21 “Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.

22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.

Mambo haya matatu ukiyazingatia sana basi Nguvu ya kisasi haiwezi kufanya kazi ndani yako, utakuwa mtu wa kusamehe na kuombea wanaokuudhi, na mengine kumwachia Bwana, na hivyo utu wako wa ndani utajengeka sana.

Maran atha!.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?

KISASI NI JUU YA BWANA.

Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?

SADAKA INAKOMESHA LAANA!

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

Rudi nyumbani

Print this post

JE NI KIKOMBE KIPI UTAKINYWEA SIKU ILE?

Rohoni vipo vikombe viwili ambavyo Mungu ameviandaa kwa wanadamu.

  1. Kikombe Cha kwanza kinajulikana kama kikombe Cha ghadhabu ya Mungu.
  2. Na kikombe Cha pili kama kikombe Cha baraka/ wokovu.

KIKOMBE CHA GHADHABU

Kama hufahamu, Mungu Huwa anajiwekea “akiba” ya hasira yake. Ikiwa na maana si mwepesi kutimiliza hasira yake Kwa haraka, Huwa anaikusanya na siku ikifika kipimo chake Kisha akaimimina hapo huwa hapana Rehema Tena. Ni kilio na kusaga meno!.

Soma

Nahumu 1:2-3

[2]BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.

[3]BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.

Mifano halisi ya hasira ya Mungu tunaiona kipindi Cha gharika, kipindi Cha sodoma na Gomora. Na ameahidi pia katika siku za mwisho ataleta hukumu hiyo Kwa ulimwengu mzima, na itatimilika yote katika lile ziwa la moto.(2Petro 3:7-5)

Utapata majibu Kwanini Leo,  Mungu anaonekana kama vile yupo kimya Kwanini uovu unaendelea hachukui hatua stahiki duniani, fahamu ni kwamba anangoja kipimo chake kijae, kikombe kijae ili waovu wanywe ghadhabu yake yote. Ndivyo alivyowaambia Ibrahimu kuhusu kuangamia Kwa wakaanani, alikuwa anasubiria uovu wao utumie (Mwanzo 15:16), na siku ilipofika Yoshua aliwaangamiza wote.

Hivyo mtu unapokuwa mwovu unakijaza kikombe Cha ghadhabu ya Mungu, Na kama dhiki kuu itakupita basi utakatana na kikombe hicho siku Ile ya hukumu, utakinywa Kwa kutupwa kwenye lile ziwa la moto.

Ufunuo wa Yohana 14:10

[10]yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.

KIKOMBE CHA BARAKA.

Lakini pia watakatifu nao Bwana anawawekea akiba ya Baraka na mema. Kwa maisha ya haki wanayoishi sasa hapa duniani, usidhani kuwa hayo mema unayotendewa ndio malipo stahiki Kutoka Kwa Mungu wako,hapana..Bwana anakijaliza kikombe Cha watakatifu na siku Ile tutakinywea na Yesu Kristo kule mbinguni kwenye Karamu ya Mwana kondoo. Haleluya.

Mathayo 26:27-29

[27]Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;

[28]kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

[29]Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

Hapo ndipo tutakapoona wema wote wa Mungu maishani mwetu. Tutakinywea kikombe hicho, tutamiminiwa thawabu na Raha isiyo na kifani. Hapo ndipo tutakapojua ni jinsi gani Mungu anavyotujali. Usikose mbingu ndugu, kosa vyote lakini Unyakuo usikupite.

Ndugu ukiona unamtumikia Mungu Leo huoni faida yoyote, kama vile huoni malipo yoyote, ,tambua kuwa Bwana anaona..anaweka tu akiba, utaipokea Raha siku Ile itakapofika.

Unapojitesa kuishi maisha ya haki, halafu unaona kama vile Mungu hakujali..usijidanganye kikombe unakijazilisha tu. Wakati wa kukinywea utafika.

Soma haya maneno ya faraja Mungu aliyoyatamka Kwa watu wake..

Malaki 3:13-18

[13]Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?

[14]Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za BWANA wa majeshi?

[15]Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.

[16]Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.

[17]Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.

[18]Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.

Bwana atupe macho ya kumwelewa yeye. Kijazilishe kikombe Cha wokovu wako. Ili siku Ile ushiriki mema yote.

Ubarikiwe.

Je umeokoka? Kama bado unasubiri Nini Leo usifanye hivyo. Ikiwa upo tayari kumgeukia Yesu na kumfanya mwokozi wa maisha Yako, akusamehe dhambi zako. Basi ni wewe tu kufungua moyo wako na kuikubali msamaha huo.Ikiwa upo tayari kufanya.hivyo basi fungua hapa Kwa mwongozo huo.

Bwana akubariki..

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

SIKU YA MAONYESHO MAKUU YA BWANA YESU, IPO KARIBU.

NIMEAZIMIA KUWAKUSANYA MATAIFA. NIPATE KUWAMWAGIA GHADHABU YANGU

UUNGU NI NINI? (1Petro 1:3-4)

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.

Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?

IEPUKE GHADHABU YA MUNGU.

USIIHARIBU TABIA YAKO KWA MAZUNGUMZO YAKO.

Rudi nyumbani

Print this post

NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

“Romans road to salvation”

Njia ya wokovu ndani ya kitabu Cha Warumi ni Nini? 

Ni mpango wa wokovu wa mwanadamu, ambao umeainishwa vyema kutoka katika kitabu Cha Warumi.

Kitabu hichi kinaeleza jinsi mtu anavyoweza kuupokea wokovu kutoka Kwa Mungu.

Hivyo ikiwa wewe bado hujaufahamu mpango wa Mungu kwako, wa namna ya kuupokea wokovu basi kitabu hichi kimeanisha vifungu ambavyo vinakuonesha ni jinsi gani utaweza kuupokea.

Lakini pia ikiwa wewe hujui ni wapi pa kuanzia unapokwenda kuwashuhudia watu habari za wokovu, basi kitabu hichi kinakupa mwongozo wa namna ya kuwahubiria wengine habari njema. Na vifungu muhimu vya kusimamia..

Hivi ni vifungu “mama”

Cha kwanza: Warumi 3:23

Warumi 3:23

[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

Tuendapo Kwa Mungu, lazima tujue hakuna mwenye haki hata mmoja sote Tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Tumetenda dhambi, Vilevile ikiwa wewe ni mhubiri/mshuhudiaji, huna budi kumuhubiria mtu jambo hilo, kwamba hakujawahi kutokea mwema hapa duniani. Hivyo wote tunauhitaji mpango wa Mungu wa wokovu katika maisha yetu.

Kifungu Cha pili: Warumi 6:23

[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Hapa, Mungu anatuonesha, matokeo ya kudumu katika dhambi zetu, ambazo wote tulikuwa nazo, kuwa ikiwa tutaendelea kubaki katika Hali hiyo hiyo basi tutakutana na mauti ya milele, lakini tukipokea zawadi ya Mungu basi tutapata uzima wa milele.

Kifungu Cha Tatu:  Warumi 5:8

[8]Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Kwamba sasa hiyo zawadi ya Mungu ambayo itapelekea uzima wa milele ni Yesu Kristo, yeye ndiye aliyetolewa na Mungu kuzichukua dhambi zetu zote, kwa kifo cha pale msalabani. Pale tuliposhindwa sisi wenyewe basi Yesu alikuja kutusaidia kuchukua makosa yetu.

Kifungu Cha nne: Warumi 10:9-10.

Hiki sasa kinaeleza Namna ya kuupokea wokovu;

Warumi 10:9-10

[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

[10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Kwa kuamini kwetu kuwa Yesu Yu hai, na kwamba anakomboa wanadamu, na vilevile kumkiri Kwa kinywa kuwa ndiye Bwana na mwokozi wetu. Basi tunaupokea msamaha huo wa dhambi Bure, bila gharama yoyote. Na deni letu la dhambi linakuwa limefutwa tangu huo wakati

Hivyo ni sharti ujue kuwa msamaha wa dhambi hauji Kwa matendo Yako mema, Bali unakuja Kwa kuikubali kazi ya Yesu msalabani iliyofanyika Kwa ajili ya ukombozi wako.

Halikadhalika Wewe kama mshuhudiaji vifungu hivi viwepo kichwani mwako.

Kifungu Cha tano cha mwisho: Warumi 5:1

[1]Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

Maana yake ni kuwa baada ya mtu kumkiri Kristo, na kumkubali kama Bwana na mwokozi wake. Basi anapaswa awe na AMANI na Mungu kwasababu hakuna mashtaka yoyote ya adhabu juu yako. Hakuna hukumu yoyote ya mauti ipo juu yake.

Huo ndipo mpango wa awali wa wokovu wa Mungu Kwa mwanadamu. Ambapo tunapaswa kufahamu kama ulivyoanishwa katika  kitabu hichi Cha Warumi.

Kisha baada ya hapo tunawafundisha watu kuitimiza haki yote au kusudi lote la Mungu juu yetu, Ikiwemo ubatizo wa maji, na ule wa Roho Mtakatifu.

Ikiwa bado hujaokoka, na utapenda kuupokea msamaha wa Yesu Bure maishani mwako, basi Unaweza kuwasiliana na sisi Kwa namba uzionazo chini ya chapisho hili kwa ajili ya mwongozo huo Bure. Vilevile na Ule wa ubatizo.

Bwana akubariki.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.

Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?

Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?

USIISHIE TU KUPATA HAKI, BALI PATA NA WOKOVU.

Rudi nyumbani

Print this post

NI KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUMWELEWA MUNGU?

Je! Moyo wako upo kweli kwake?

Kuna kauli Bwana Yesu alisema kuhusiana na watu kumwelewa Mungu na uweza wake kwetu, alisema..

Mathayo 13:14  “Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15  Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, WAKAELEWA KWA MIOYO YAO, WAKAONGOKA, NIKAWAPONYA”

Ametaja mambo makuu matatu,

  1. Kuona – Kwa macho
  2. Kusikia –kwa masikio
  3. Kuelewa – Kwa moyo

Hatua ya mwisho ambayo Mungu anatarajia, pindi anapomfundisha mtu, au kusema naye ni KUELEWA. Hivyo ataanza kwanza kwa kumwonyesha mambo kadha wa kadha, yatapita mbele yake, ataanza kusema na yeye kwa njia nyingi, aidha kwa wahubiri wake, au ndoto, au maono, au vitu vya asili, au kwa Neno lake, au kwa maisha yake mwenyewe.. Lakini  pamoja na njia zote hizo  bado mtu huyo anaweza asimwelewe Mungu, kama Moyo wako haupo kwake.

Jambo ambalo watu wengi hatujui, ni kwamba Mungu anazungumza na kila mmoja, Na kila mmoja anaonyeshwa maono mengi na Mungu, kila mtu ameshakutana na Mungu, aidha uso kwa uso au katika roho, haijalishi ni mwema au mwenye dhambi, Lakini ni wachache sana walioweza kuielewa sauti yake iliposema nao.

Ni kwasababu gani hawaielewi? Ni kwasababu inahitaji MOYO ili kuielewa, Na sio macho au sikio. Kama moyo wako haupo kwake, sahau kumwelewa Mungu anaposema na wewe kwa njia yoyote ile. Hata kama itakuja kwa dhahiri, bado hutamwelewa. Sauti yake kwako itakuwa ni ngurumo tu, kama ilivyokuwa kipindi kile Bwana Yesu alipokuwa anazungumza na makutano kuhusiana na ufalme wa mbinguni.

Yohana 12:28  “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. 29  Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.30  Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu”

Ni kwanini iwe hivyo kwao? Ni kwasababu kilichowapeleka kwa Yesu sio wokovu wa Roho zao, au upendo wao kwa Mungu, kilichowapeleka kwake, ni miujiza, uponyaji, uzuri, mwonekano, mazingira, basi, hakuna jipya. Wakishapata walichokuwa wanakitafuta hao wanaondoka zao kuendelea na mambo yao ya dhambi ya sikuzote.

Ndio maana hakukuwa na hata mmoja ambaye aliyeelewa mifano yote Yesu aliyokuwa anaisema mbele ya umati. Isipokuwa wanafunzi wake tu, pamoja na wachache waliomfuata baada ya pale kutaka kufafanuliwa.

Ndugu ikiwa leo unakwenda kanisani kutimiza tu ratiba, kutazama kwaya, kuangalia watu wamevaaje, hata ukiwepo humo unasinzia, unaangalia muda utatoka saa ngapi, ni kweli utakutana na Mungu, atasema na wewe, utamwona, utahisi uwepo wake, utanena hata kwa lugha, utasisimka moyo. Lakini kumwelewa, haitakaa iwezekane. Kwasababu Mungu hajifunui kwa watu ambao  mioyo yao haipo kwake.Hana utaratibu huo.

Na sio tu kanisani, hata mahali popote pale, iwe ni shuleni, kazini, nyumbani, barabarani, Mungu huwa anazungumza, anasema kwa njia mbalimbali tena kirahisi sana, Lakini hutaelewa ikiwa huna moyo wa dhati kwa Mungu wako.

Alisema hivi;;

2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, WALIOKAMILIKA MOYO KUELEKEA KWAKE…”

Alisema pia..

Mathayo 15:7  “Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, 8  Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami”.

Yatupasa sasa tuondoe unafiki wa ndani, kwa kumaanisha kweli kweli kumpenda Mungu kwa moyo, ili sasa aanze kutufunulia sauti yake na kazi zake. Tukimfuata Kristo tujue kinachotupeleka kule ni Utakatifu na haki, na sio kwasababu tunashida tutimiziwe mahitaji yetu, hapo ndipo atapendezwa na sisi, na hatimaye, tutamwona kila inapoitwa leo.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.

MWANANGU, NIPE MOYO WAKO;

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?

NIFANYE NINI ILI NIKUBALIWE NA YESU?

Je! Mwendo wa Sabato ulikuwaje kibiblia?(Matendo 1:12)

Rudi nyumbani

Print this post

Mtiririko wa vitabu vya biblia kwanini upo vile?

SWALI: Kwanini vitabu vya biblia vipo katika mtiririko ule, na sio kinyume chake?

Ni vema kufahamu kuwa mtiririko wa kibiblia wa agano la kale na agano jipya, haukuwekwa na Mungu, kwamba kianze kitabu hiki kifuate hiki, kianze cha Mwanzo kisha kifuate cha Kutoka. Hapana bali ni utaratibu uliowekwa na wanadamu, ambao kimsingi unamaudhui mazuri, na uligawanya hivyo ili kumsaidia msomaji kufahamu vizuri, kuliko vingeorodheshwa  tu kila kimoja eneo lake, ingewia ngumu kwa msomaji anayependa kujifunza Biblia kuelewa kiwepesi.

Mtiririko ambao sisi tunaoutumia ni tofauti na mtiririko ambao Wayahudi wanautumia kwa vitabu vya agano la kale.

Kwa mfano mtiririko wetu (Ambao unajulikana kama mtiririko wa kiprotestanti), una vitabu 39 vya Agano la kale. Lakini mtitiriko wa Kiyahudi, una vitabu 24 kwa agano hilo hilo la kale,.

Vitabu vyetu ni kama vifuatavyo

Vitabu vya Sheria

  1. Mwanzo
  2. Kutoka
  3. Mambo ya Walawi
  4. Hesabu
  5. Kumbukumbu la Torati

Vitabu vya Historia

  • Yoshua
  • Waamuzi
  • Ruthu
  • 1Samweli
  • 2Samweli
  • 1Wafalme
  • 2Wafalme
  • 1Mambo ya Nyakati
  • 2Mambo ya Nyakati
  • Ezra
  • Nehemia
  • Esta

Vitabu vya Mashairi

  1. Ayubu
  2. Zaburi
  3. Mithali
  4. Mhubiri
  5. Wimbo ulio bora

Vitabu vya Manabii (Wakubwa)

  • Isaya
  • Yeremia
  • Maombolezi
  • Ezekieli
  • Danieli

Vitabu vya manabii (Wadogo)

  • Hosea
  • Yoeli
  • Amosi
  • Obadia
  • Yona
  • Mika
  • Nahumu
  • Habakuki
  • Sefania
  • Hagai
  • Zekaria
  • Malaki                                                     

Lakini utajiuliza kwanini biblia ya kiyahudi iwe na vitabu 24 na sio 39? Je vingine vimeondolewa? Jibu ni hapana, bali baadhi yao vilijumuishwa kama ni kitabu kimoja kwamfano.

> Vitabu viwili vya wafalme kwao ni kitabu kimoja.

> Vitabu viwili vya Mambo ya Nyakati kwao ni kitabu kimoja.

> Vitabu viwili vya Samweli kwao ni kitabu kimoja.

> Ezra na Nehemia vimeweka kama kitabu kimoja.

> Vitabu 12 vya Manabii wadogo kwao ni  kitabu kimoja.

Jumla yake ni vitabu 24 Badala ya 39.

Hivyo tukirudi katika biblia yetu, yenye vitabu 39 kwa agano la kale, Orodha ile haijawekwa kulingana na vipindi vilipoandikwa, bali kulingana na ‘asili ya vitabu’. Ndio hapo utaona hiyo migawanyo mikuu mitano (Yaani vitabu vya Sheria, vya historia, vya mashairi, vya Manabii wakubwa na wale wadogo).

Kutaja manabii wakubwa haimaanishi kuwa walikuwa na vyeo vya juu au walikuwa na nguvu zaidi ya wale wengine hapana, bali ni kutokana na wingi wa uandishi wao, yaani waliokuwa na uandishi mwingi waliwekwa katika kundi hilo la manabii wakubwa.

Tukirudi katika agano jipya.

Vipo vitabu 27, na vyenyewe pia havijaandikwa kulingana na wakati wa uandishi, japo havipishani sana na wakati wa uandishi.

Huu ndio mgawanyo wake.

Vitabu vya Injili

  1. Mathayo
  2. Marko
  3. Luka
  4. Yohana

Kitabu cha Historia

  • Matendo

Nyaraka za Paulo

  • Warumi
  • 1Wakorintho
  • 2Wakorintho
  • Wagalatia
  • Waefeso
  • Wafilipi
  • Wakolosai
  • 1Wathesalonike
  • 2Wathesalonike
  • 1Timotheo
  • 2Timotheo
  • Tito
  • Filemoni

Nyaraka kwa wote

  1. Waebrania
  2. Yakobo
  3. 1Petro
  4. 2Petro
  5. 1Yohana
  6. 2Yohana
  7. 3Yohana
  8. Yuda

Unabii

  • Ufunuo

Halikadhalika Nyaraka za Mtume Paulo ziliorodheshwa katika mpangilio ule kutoka na  urefu wa uandishi na sio umuhimu wa nyaraka Fulani zaidi ya nyingine, kwamfano utaona kitabu cha kwanza kwa urefu cha Mtume Paulo ni Warumi na ndio kilichowekwa cha kwanza. Vilevile kirefu zaidi ya vyote alivyoviandika kwa Watu, ni cha Timotheo ndicho kilichopangiliwa cha kwanza.

Lakini pamoja na kwamba havikuweka katika mpangalio wa nyakati za uandishi bado zinamtiririko mzuri unaelekeana na historia, kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka ufunuo.  Japo pia katika usomaji haimaanishi ufuate mtiririko huo, bali unaweza kuanza vyovyote upendavyo kwa jinsi Roho Mtakatifu atakavyokuongoza.Kwasababu hakuna sehemu yoyote katika maandiko tumewekewa mtiririko huo.

Pia zipo biblia nyingine mfano ile ya Kikatoliki yenye vitabu 73, ambayo kimsingi haijavuviwa na Roho wa Mungu kwani kuna baadhi ya vitabu vimeongezwa ambavyo hukinzana na mafundisho ya msingi ya imani, na hivyo hatupaswi kuifuata. Biblia yetu ina vitabu 66 tu. Kama vilivyoorodheshwa hapo juu. Zaidi ya hivyo hutoka kwa Yule mwovu.

Bwana akubariki sana.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Tofauti kati ya maandiko na Neno ni ipi?

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

HISTORIA YA BIBLIA YA KING JAMES, INA FUNZO GANI KWETU?

Vitabu vya Deuterokanoni ni vya kiMungu?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

ISHARA YA KANISA LA LAODIKIA

Karibu katika mafunzo ya biblia.

Kwanini tunasema kuwa hili ni kanisa la Mwisho la Laodikia?, Je ni viashiria gani vinavyotutambulisha kuwa hali ya kanisa la Laodikia lile la saba ambalo Mtume Yohana alionyeshwa kwenye Maono  katika kitabu cha Ufunuo ndio hali halisi ya kanisa letu la siku za mwisho?.

Awali ya yote hebu tujikumbushe historia ya yale makanisa saba, tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo Mlango wa 2 na wa 3.

Makanisa saba tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo ni makanisa ambayo yalikuwa katika miji 7 tofauti tofauti. (Efeso, Smirna, Pergano, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia, Ufunuo 1:11).

Hivyo  na makanisa hayo yalijulikana kwa majina ya miji hiyo,  na Yote ilikuwa inapatikana katika eneo lijulikanalo kama “Asia Ndogo” ambapo kwasasa ni nchi ya “Uturuki”.

Sasa kila kanisa lilikuwa na tabia yake, kulingana na huo mji (unaweza kusoma tabia hizo katika Ufunuo 2-3). Na kanisa la Mwisho kabisa kutajwa ambalo ndio la saba lililoitwa Laodikia lilikuwa na tabia nyingine ya kipekee ambayo kwa hiyo ndiyo tutajua kuwa kanisa letu la sasa linafanana na kanisa la huo mji au la!.

Sasa kabla ya kwenda kusoma tabia za kanisa hilo katika kitabu cha Ufunuo, hebu kwanza tuweke msingi mwingine wa kuelewa jambo lingine, ambalo litatusaidia kuelewa hili vizuri.

Katika biblia maandiko yanatabiri kuwa dalili za siku za mwisho ni Maasi kuongezeka katika kiwango cha miji ya Sodoma na Gomora, au miji ya Nyakati za Nuhu (Soma Luka 17:26-28).

Maana yake ni kuwa kama hali ya maovu haijafikia kile kiwango cha maasi ya Sodoma na Gomora, basi bado ule mwisho utakuwa upo mbali, lakini kama hali ya mji itafikia kile kiwango cha maasi ya Sodoma na Gomora basi ni wazi kuwa ule mwisho umefika.

Kwahiyo ni sahihi kusema kuwa  Miji ya Sodoma na Gomora ni ishara au alama ya miji ya siku za mwisho, Hivyo tukitaka kujua kuwa tupo siku za mwisho basi tujilinganishe na miji ya Sodoma na Gomora. (2Petro 2:6 na Yuda 1:7).

Na sasa tunaona kabisa kuwa kizazi chetu ni kama kile cha Sodoma na Gomora na hata huenda kimepita, kwasababu katika miji ya Sodoma na Gomora kulikuwa na mwingiliano wa ndoa za jinsia moja..vile vile na sasa hali ni hiyo hiyo, ushoga upo kila mahali, mauaji, dhuluma n.k kwahiyo tupo siku za mwisho.

Vile vile na kanisa la Mji wa Laodikia, ambao ulikuwepo katika enzi  za kanisa la Kwanza,  lilikuwa ni Ishara ya kanisa la siku za mwisho. Maana yake ni kuwa tukitaka kujua kuwa tunaishi katika kanisa la mwisho, basi tunapaswa tujilinganishe kanisa letu na lile la Laodikia. Tukiona yanafanana kitabia basi tujue kuwa hili ndio kanisa la mwisho na unyakuo umekaribia.. lakini tukiona kuwa bado hatujafikia viwango vya kanisa lile basi tujue kuwa ule mwisho huenda bado sana.

Sasa hebu tusome tabia za kanisa la Laodikia katika biblia.

Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15  NAYAJUA MATENDO YAKO, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; INGEKUWA HERI KAMA UNGEKUWA BARIDI AU MOTO.

16  Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17  Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.

Umeona tabia za kanisa la Laodikia?..Biblia inasema ni kanisa ambalo lilikuwa vuguvugu, si moto wala si bariki.. mfano kamili wa kanisa la wakati huu. (Kumbuka hapa tunazungumzia kanisa na si watu wa ulimwengu, watu wa ulimwengu ishara yao ni miji ya Sodoma na Gomora na sisi kanisa ishara yetu ni kanisa la mji wa Laodikia).

Kanisa la wakati huu utaona mtu mguu mmoja nje mguu mmoja ndani, leo yupo kanisani kesho disco, leo anamwabudu Bwana kesho anasikiliza miziki ya kidunia, simu yake nusu ina nyimbo za injili nusu nyimbo za kidunia, kabati lake nusu lina nguo za kujisitiri nusu lina nguo za nusu uchi, maneno yake nusu ya heshima nusu ya kihuni, biashara yake nusu ni halali nusu ni haramu, duka lake nusu lina bidhaa njema nusu lina bidhaa haramu (pombe, na sigara), leo atatoa sadaka kesho anaonga/ anaogwa.n.k

Hiyo ndiyo ilikuwa hali ya kanisa la Laodikia na ndio hali ya kanisa la Sasa tulilopo.

Hiyo ndiyo alama pekee inayotutambulisha siku si nyingi unyakuo wa kanisa utatokea. Kwasababu hakutakuwa na kanisa lingine litakalotokea lenye tabia nyingine, hili la Laodikia biblia imetabiri ndio kanisa la Mwisho baada ya hapo ni unyakuo ndio maana utaona pale, baada ya ujumbe wake kumalizika kilichofuata ni Yohana kuchukuliwa juu mbinguni.

Ufunuo 4:1 “Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo”.

Wakati kanisa hili la Laodikia limechafuka hivi, Bwana analiandaa kundi lake dogo, na kuliambia litoke huko, kama vile alivyowaokoa Nuhu na Luthu..Vile vile kanisa la Laodikia litaingia katika dhiki kuu kwasababu ni kanisa vuguvugu lakini kundi dogo ambalo litakuwa safi na litakuwa Moto na si Vuguvugu hilo litaenda na Bwana katika unyakuo.

Ndugu unyakuo umekaribia sana, Yesu yupo Mlangoni kurudi, ondoka katika uvuguvugu, wa kidunia, kuwa Moto.. Ukiamua kumfuata Kristo basi mfuate kwelikweli, usiige desturi za kidunia, ukiamua kuwa mtu wa kujisitiri fanya hivyo kikweli kweli usiwe nusu nusu, ukiamua kumfuata Yesu basi jikane kweli kweli.

Uvuguvu Kristo anauchukia kuliko hata Yule mtu aliye baridi kabisa.. kwasababu yeye mwenyewe anasema ni heri mtu awe moto au baridi kuliko vuguvugu..

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.

Babewatoto ni nani katika biblia?(Isaya 34:14).

Babeli ni nchi gani kwasasa?

JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?

Rudi nyumbani

Print this post

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu.

Kama wengi wetu tunavyojua kuwa hakuna wokovu nje ya Yesu Kristo, wala hakuna Maisha nje ya Yesu Kristo. Kama Mtume Paulo alivyoandika kwa uweza wa Roho kwamba ‘Mauti ilikuja kwa njia ya mtu mmoja(Adamu)…kadhalika uzima utaletwa kwa njia hiyo hiyo ya mtu mmoja (ambaye ni Kristo)’.

Kwahiyo yeye peke yake ndio njia iliyo sahihi na iliyothibitishwa ya kumfikia Mungu..njia nyingine zote tofauti na yeye ni za upotevu, haijalishi zina wafuasi wengi kiasi gani.

Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani, alizungumza kwa mifano mingi, yote ni kwa lengo la kumfanya mwanadamu aelewe mpango wa Mungu juu ya Maisha yake…Alitumia mifano ya miti, mashamba, wafanyabiashara, wakulima,familia, wageni, wafalme na mingine mingi ambayo hata haijaandikwa kwenye biblia, kwasababu kama yangeandikwa mambo yote aliyoyafanya moja moja…biblia inasema hata dunia isingetosha kwa jinsi vitabu vingekuwa ni vingi (Yohana 21:25)..

Lakini tunaona baada ya kuondoka alikuja tena kuzungumza na Mtume Yohana katika maono , alipokuwa katika kisiwa kile cha Patmo na kumpa mfano namna ambayo huwa anavyowajilia watu wake alimwambia…

Ufunuo 3: 20 ‘’Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami’’.

Mfano huo Bwana Yesu aliutoa kuonyesha ujio wake kwa mtu ni kama wa mgeni…Ujio huu sio wa kulichukua kanisa…kwasababu ujio wa kuja kulichukua kanisa alisema utakuwa kama ujio wa mwizi…hata kuja kwa kugonga na kusihi, bali atakuja usiku watu wakiwa wamelala na atachukua walio wake na kuondoka….ndio maana unyakuo ukipita sio watu wote watajua…Kwahiyo kuna kipindi Bwana Yesu atakuja kama mgeni na kuna kipindi atakuja kama mwivi.

Sasa katika mfano huu..anasema tazama nasimama mlangoni nabisha! Kubisha maana yake ni kugonga mlango huku unatoa sauti Fulani kama hodii hodii!! Hiyo ndiyo maana ya kubisha!..Kwahiyo hapa Bwana anasema nasimama nabisha, halafu anasema mtu akiisikia sauti yake na kuufungua mlango ataingia…hii ikiwa na maana kuwa mtu anaweza akaisikia sauti yake na asifungue…au mtu anaweza asiisikie kabisa sauti yake…labda kutokana na kwamba amelala au kutokana na usumbufu uliopo ndani ya nyumba kuwa mkubwa (labda kelele za miziki au watu).

Na baada ya kuingia utaona anasema…’nitakula pamoja naye na yeye pamoja nami’…sasa tafakari hapo kwa makini, hasemi tutakula pamoja hapana!…bali anasema nitakula pamoja naye…na yeye pamoja nami…ikiwa na maana kuwa alipokuwa anangonga alikuja na chakula chake, hakuja mikono mitupu…kadhalika na yule mtu aliyemfungulia atamkuta na chakula chake…na hivyo kila mmoja atashiriki na mwenzake kile alichokiandaa.

Sasa ukiingia ndani Zaidi kuutafakari mfano huu utaona kuwa unahusu wakati wa jioni…lugha yetu ya Kiswahili haijajitosheleza katika maneno mengi…lakini kama ukisoma tafsiri nyingine kama zile za kiingereza au kigiriki utaelewa vizuri kuwa ni wakati wa jioni ndio Bwana alikwenda kugonga mlango.. ni wakati wa chakula cha jioni (evening supper).

Kwahiyo katika mfano huo Bwana anakuja kugonga mlango wakati wa jioni…akiwa na chakula chake, hajaja kudoea wala kula vya watu bure!…Inaashiria kuwa Kristo anapotaka kuja kuingia katika Maisha yetu sio kwa lengo la kutaka vya kwetu, au kutuharibia Maisha hapana! Bali ni kwa lengo la kutupa sisi faida. Na atakuja jioni, hizi ni nyakati za jioni, wakati wa kumalizia wa mwisho wa dunia ndugu.

Na kama tunavyojua tabia ya mgeni anapogonga, huwa hagongi mfululizo kama vile analazimisha mlango ufunguliwe…bali utaona anagonga kidogo kwa utaratibu kisha anatulia kidogo, akiona hasikiwi atarudia tena kwa sauti kidogo baada ya muda Fulani kupita..atafanya vile kwa kipindi Fulani, akiona hakuna kabisa majibu labda yule mtu amelala usingizi mzito hawezi kusikia hatavunja mlango ataondoka arudi tena baadaye au arudi wakati mwingine…Lakini akigundua yule mtu kule ndani anamsikia lakini hataki kumfungulia makusudi tu! Basi ataondoka asirudi tena…kwasababu anajua hahitajiki mahali pale.

Na Ndivyo hivyo Kristo anavyogonga mioyoni mwetu leo hii, atakutumia wahubiri pale mahali ulipo, kwa kukusihi umfungulie moyoni mwako aingie…akiona bado humsikii ataongeza watumishi kila mahali utakapokwenda hata kwenye mitandao utakutana na Neno lake, sauti yake utaisikia kila mahali ikikuita, utakapoitii ataingia, na vitu alivyokuja navyo kukuletea hutaamini macho yako kuvioona..Lakini endapo unajua kabisa huyu ni Kristo ananiita kupitia mahubiri, na kuwa hii ni sauti yake kabisa na unafanya makusudi kutokumfungulia…basi ataondoka na Neema hiyo itakwenda kwa wengine..

Ndugu usidanganyike kuwa utatubu uzeeni, Sauti ya Mungu itarudia kuita kwa wale watu ambao wakati Bwana amegonga wapo usingizini…wale watu ambao nguvu za giza zimewafunga kiasi kwamba hawawezi kuisikia injili…hao ndio Bwana ataendelea kuwaita kila wanapokwenda, mpaka watakapoamka usingizini, na kundi hili mara nyingi ni lile kundi ambalo halijawahi kabisa kupata nafasi ya kuujua msingi wa Imani ya kikristo, wale watu ambao wamezaliwa katika familia za kipagani, au familia za watu wasio wa dini, na hawamjui Kabisa Kristo…hawa ni sawa wapo usingizini au wapo kwenye makelele ya ulimwengu kiasi kwamba hawawezi kuisikia sauti ya Bwana Yesu..Hivyo Bwana ataiongeza sauti yake mpaka wasikie.Watapata Neema kubwa Zaidi.

Lakini kwa wengine ambao wamezaliwa katika Ukristo tangu udogoni, wamehubiriwa vya kutosha kuhusu msalaba, na wanaielewa kabisa sauti ya Yesu inapoita, na wengine mpaka wamemwona Bwana katika maono, na wamepewa ishara kadha wa kadha, Bwana akiwaita na hawataki kusikia…Kristo ataondoka kwao na asirudi tena kamwe. Wengi hawapendi kusikia hivi lakini huu ndio ukweli maandiko yanasema hivyo..Wana wa Israeli Taifa la Mungu yaliwatokea hayo, si Zaidi watu wa mataifa.. Bwana Yesu aliwaambia waisraeli maneno haya, baada ya kuwaonya mara nyingi na kushupaza shingo zao haya ndio aliyowaambia:

Mathayo 23:37 ‘’Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.

39 Kwa maana nawaambia, HAMTANIONA KAMWE TANGU SASA, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana’’.

Aliwaambia ‘’hamtaniona kamwe tangu sasa’’..Hili Neno ni kali sana na linaumiza…’’kutengwa na Mungu milele’’..Si ni afadhali tutengwe na wanadamu kuliko Mungu…Ni heri wanadamu wote wanichukie na kunitenga lakini sio Mungu, ni heri nichokwe na wanadamu wote lakini sio Mungu.

Hebu tafakari leo hii Kristo anakwambia haya maneno ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’!!!…Yaani wewe na Kristo ndio Basii!!…

Leo hii usikiapo maneno haya kwenye mtandao, na bado hutaki kuacha dhambi na ulimwengu, kumbuka haukuwa mpango wa Mungu usikie injili yake kwa njia hii ya mitandao..Mpango wake ulikuwa siku ile ile ulipoisikia injili kwa mara ya kwanza ulipohubiriwa na mtu aliyeshika biblia mkononi ungeamini, kulikuwa hakuna sababu ya wewe kuja kusikia tena injili hapa……lakini kwasababu Moyo wako ulikuwa mgumu, ndio maana amekufuata kwa njia nyingine hii ya mtandao..ili awe na uhakika kabisa unaisikia sauti yake. Lakini unaidharau..pengine hii ndio sauti yake ya mwisho kwako, isikie ufungue, asije akakwambia kama alivyowaambia wayahudi ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’….Maneno haya yalizungumzwa na Kristo yule yule aliyesema ‘njooni kwangu nyinyi nyote’….hapa anasema ‘hamtaniona tena kamwe’…sehemu nyingine anasema ‘tokeni kwangu’.

Pale ulipo mwambie Bwana natubu dhambi zangu zote, na kukusudia kutokuzifanya tena, tubu kabisa kwa kudhamiria kabisa kuacha kuzifanya.Mfungulie mlango na yeye ataingia ndani yako haraka kukugeuza, hataanza kukulaumu kwanini nimegonga muda wote huo ukufungua, yeye si kama sisi, moja kwa moja atazungumza na wewe na muda wa kula ukifika atakufungulia hazina zake alizokuletea mshiriki pamoja, atakupa baraka zote za mwilini na rohoni, na kukufundisha maneno yake ya uzima. Utakuwa na tumaini la uzima wa sasa na ule wa baadaye.

Lakini usipotaka ataondoka, na siku moja atakuja kama mwivi, siku hiyo hatokuja kwako tu bali atakuja kwa ulimwengu mzima, atavunja atavunja mlango na kuwaiba waliowake ndani, na kwenda nao mbinguni, huku nyuma moto utawaka. Usitamani uwepo hicho kipindi cha dhiki kuu. FIKIA TOBA LEO!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Ni maombi yangu kuwa utakitendea kazi ulichokisikia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 


Mada Zinazoendana:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Moja ya maagizo muhimu sana ambayo Bwana YESU KRISTO aliyatoa kwa kanisa ni ubatizo.

Mengine yakiwemo kushiriki,kutawadhana miguu kwa wakristo,wanawake kufunika vichwa vyao wakati wa ibada.Kati ya hayo ubatizo ni muhimu sana kwa mwamini yeyote kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake.Lakini ubatizo huu shetani ameuharibu usifanyike ipasavyo kwa sababu anajua una madhara makubwa katika kumbadilisha mkristo.na hiyo ndiyo imekuwa kazi ya shetani tangu awali kuyapindisha maneno ya Mungu na kuzuia watu wasimfikie Mungu katika utimilifu wote.

Makanisa mengi leo hii yanabatiza watu au watoto wachanga kwa kuwanyunyuzia maji. Wakibatiza kwa jina la BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kulingana na mathayo 28:19. “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu”..swali ni je! hili jina linatumiwa ipasavyo kubatizia?

Kwa kukosa Roho ya ufunuo na uelewa wa maandiko viongozi wengi wa dini wameacha kweli. Na kugeukia mafundisho ya kipagani na kibaya zaidi wengi wao wanaujua ukweli lakini wanawaficha watu wasiujue ukweli kwa kuogopa kufukuzwa kwenye mashirika yao ya dini. Watu kama hawa ni adui wa msalaba

 Bwana aliowazungumzia akisema 

Mathayo 23:13″ ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamuingii wala wanaoingia hamwaachi waingie.”

 Tukirejea tena kwenye maandiko

Yohana 5:42-43 “walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.Mimi nimekuja kwa JINA LA BABA YANGU, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.”

hapa tunaona dhahiri kabisa jina alilonalo Yesu ni jina la BABA yake. Kwa namna hiyo basi jina la baba yake ni Yesu.

Tukirudi tena kwenye maandiko yohana 14:26 Yesu Kristo alisema “lakini huyo msaidizi,huyo Roho mtakatifu ambaye baba atampeleka  KWA JINA LANGU, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”na  hapa tunaona Roho Mtakatifu alitolewa kwetu kwa jina la Bwana Yesu. kwahiyo hapa biblia inatufundisha dhahiri kabisa kuwa jina la Roho Mtakatifu ni Yesu.

Na tena kwenye maandiko tunaona kuwa Roho Mtakatifu ndiye Baba mathayo 1:20 “…Yusufu, mwana wa Daudi usihofu kumchukua Mariamu mkeo maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu” kwahiyo Baba ndiye yule yule Roho na ndiye yule yule aliyechukua mwili na kuishi pamoja nasi kwahiyo hapa hatuoni ‘utatu’ wa aina yeyote ambao unahubiriwa leo hii na makanisa mengi.  Mungu ni mmoja tu!.

Kwahiyo jina la Baba ni Yesu na jina la Mwana ni Yesu na jina la Roho Mtakatifu ni Yesu; baba,mwana na roho ni vyeo na sio majina kwa mfano mtu anaweza akawa baba kwa mtoto wake,mume kwa mke wake,babu kwa mjukuu wake lakini jina lake anaweza akawa anaitwa Yohana na sio ‘baba,mume au mjukuu’ vivyo hivyo kwa Mungu.aliposema mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu alikuwa anazungumzia Jina la YESU KRISTO ambalo ndilo jina la baba na mwana na Roho Mtakatifu.

Katika biblia Wakristo na mitume wote walibatizwa na kubatiza kwa JINA LA YESU KRISTO na sio kwa JINA LA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU. ubatizo huu wa uwongo ulikuja kuingizwa na kanisa katoliki katika baraza la Nikea mwaka 325 AD pale ukristo ulipochanganywa na upagani na ibada ya miungu mingi ya Roma.

Tukisoma matendo ya mitume 2:37-38 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao. wakamwambia Petro na mitume wengine , tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwa kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

Tukisoma tena  katika maandiko Filipo alipoenda Samaria na wale watu wa ule mji walipoiamini injili walibatizwa wote kwa jina lake Yesu Kristo matendo 8:12 ” lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habati njema za ufalme wa Mungu na  JINA LAKE YESU KRISTO  wakabatizwa wanaume na wanawake”

Na pia matendo 8:14-17  inasema ” Na mitume walipokuwa Yerusalemu, waliposika ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu.wakawapelekea Petro na Yohana ambao waliposhuka wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila WAMEBATIZWA TU KWA JINA  LAKE BWANA YESU”

Tukirejea tena.

Matendo 10:48  Petro alipokuwa nyumbani mwa Kornelio alisema maneno haya “Ni nani awezaye kuzuia maji,hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vilevile kama sisi? akaamuru WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO”

Tukisoma tena katika matendo 19:2-6  hapa Paulo akiwa Efeso alikutana na watu kadha wa kadha akawauliza.” je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?, wakamjibu, la, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema, kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu. Waliposikia haya WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU”

Mitume wote hawa kuanzia Petro,Yohana,Filipo na mtume Paulo wote hawa walibatiza kwa jina la Yesu Kristo je? tuwaulize hawa viongozi wa dini wanaobatiza kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu wameutolea wapi??? na biblia inasema katika

Wakolosai 3:17 ” na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote  katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu baba kwa yeye”..

hii ina maana tukiomba tunaomba kwa jina la Yesu,tukitoa pepo tunatoa kwa Jina la Yesu, tukiponya watu tunaponya kwa jina la Yesu,tukifufua wafu tunafufua kwa jina la Yesu na tukibatizwa tunabatizwa kwa jina la YESU biblia inasema kwenye

Matendo 4:12 “…kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”

na hakuna mahali popote katika biblia mtu alibatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu

na maana ya neno ubatizo ni “kuzamishwa” na sio kunyunyuziwa, kwahiyo ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kwenye maji sawasawa na maandiko na hakuna mahali popote katika maandiko watoto wachanga wanabatizwa. Ubatizo ni pale mtu anapoona sababu ya yeye kutubu na kuoshwa dhambi zake ndipo anapoenda kubatizwa kwa jina la Yesu kwa ondoleo la dhambi zake.

Ewe ndugu Mkristo epuka mapokeo ambayo Yesu aliyaita “chachu ya mafarisayo” penda kuujua ukweli ndugu mpendwa na ubadilike na umuombe Roho wa Mungu akuongoze katika kweli yote usipende mtu yeyote achezee hatima yako ya maisha ya milele, uuchunge wokovu wako kuliko kitu chochote kile,Mpende Mungu, upende kuujua ukweli,ipende biblia..Mwulize mchungaji wako kwa upendo kabisa kwanini anayafanya hayo huku anaujua ukweli na kama haujui mwambie abadilike aendane na kweli ya Mungu inavyosema kulingana na maandiko.

Kama hujabatizwa au umebatizwa katika ubatizo usio sahihi ni vema ukabatizwa tena kwa jina la YESU KRISTO kwa ondoleo la dhambi zako kwani ubatizo sahihi ni muhimu sana..ukitaka kubatizwa tafuta kanisa lolote wanaoamini katika ubatizo sahihi tulioutaja hapo  juu au unaweza ukawasiliana nasi tutakusaidia namna ya kupata huduma ya ubatizo sahihi, karibu na mahali ulipo 0789001312

 Mungu akubariki 

  jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP             

  (ubatizo sahihi wa kuzamishwa na KWA JINA LA YESU KRISTO)

Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=kuCSAZcnM80[/embedyt]

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:


Mada Nyinginezo:

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:

SAUTI AU NGURUMO

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

JE! NI HATUA ZIPI MUHIMU ZA KUFUATA BAADA YA UBATIZO?

UBATIZO WA MOTO NI UPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

Kuna tofauti kati ya UBATIZO wa Roho Mtakatifu na UPAKO wa Roho Mtakatifu.

Watu wanachanganyikiwa wakidhani kuwa na upako, au nguvu za Roho Mtakatifu, ndio Umebatizwa na Roho Mtakatifu. Lakini hii sio kweli, mtu anaweza kuwa na upako wa Roho Mtakatifu, akaponya magonjwa, akafufua wafu, akanena kwa lugha, akaona maono, akatabiri au kuota ndoto na ikaja kutokea, na bado asiwe amebatizwa na Roho Mtakatifu. Tunaona kabla ya Pentekoste wanafunzi wa Yesu ikiwemo Yuda aliyemsaliti Bwana walikuwa wanafanya ishara zote hizi na bado walikuwa hawajabatizwa na Roho wa Mungu..

Biblia inasema Mathayo 5:45

“…..maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.”

Hii ni SIRI kubwa sana inayozungumzwa hapo, Bwana anaachia nguvu zake kwa waovu na wema, anaachilia nguvu zake za uponyaji,miujiza, kwa wote waovu na wema n.k. Hivyo kigezo cha mtu kufanya ishara na miujiza si tiketi ya yeye kuwa mwana wa Mungu, Bwana aliwaambia wanafunzi wake..

Luka 10:20″ Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”

Unaona alituambia tusifurahi kwa sababu miujiza inatendeka na sisi bali kwasababu majina Yetu yameandikwa mbinguni hii ikiwa na maana,tunapaswa tufarahi tunapokuwa na mahusiano na Mungu na uhakika wa kwenda mbinguni na sio tunapokuwa na uwezo wa kutoa pepo au kufanya miujiza.

Katika kipindi hichi cha mwisho shetani amefanikiwa kuwadanganya wengi kwa njia hii, kwa kushindwa kutofautisha ubatizo halisi wa Roho Mtakatifu na Upako wa Roho Mtakatifu, si jambo la kushangaza kuona mtu anatoka kuvuta sigara na akaenda kunena kwa lugha, nabii katoka kuzini na bado akaenda kutoa unabii na huo unabii ukatimia kama ulivyo, mtu katoka kwenye ufisadi na akaenda kumwombea mtu akafufuka na bado anaota ndoto, ishara na miujiza vikifuatana naye, mtu katoka kutukana na bado akaenda kufundisha,na kutoa mapepo na bado nguvu za Mungu zikashuka na watu wakafunguliwa katika vifungo vyao..

lakini hiyo sio uthibitisho ya kwamba mtu huyo amepokea Roho Mtakatifu usidanganyike. Mungu anaweza kutumia chombo chochote kutenda kazi yake kama chombo cha kuazima tu, kazi ya hicho chombo ikiisha Mungu anaondoka. Kwa mfano tunaona katika biblia Mungu alimtumia Punda kuzungumza na Balaamu, lakini baada ya kuupeleka ujumbe yule punda akarudia katika hali yake ya mwanzo ya upunda.

Hivi ndivyo watu wanavyotumiwa na Mungu kama vyombo vya kuazima lakini wasiwe watu halisi wa Mungu, wamenyeshewa tu ile mvua ya upako ambayo inawanyeshea wote waovu na wema. Hii ni SIRI kubwa watu wanapaswa waijue.

Bwana Yesu alisema

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

Mstari huu unajieleza wazi kabisa juu ya watu wanaojidhani kuwa wanafanya miujiza na ishara ndio uthibitisho kuwa wao ni wana wa Mungu.

LAKINI UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NI UPI?

Uthibitisho wa Roho Mtakatifu pale anaposhuka juu yako anakufanya uwe kiumbe kipya (uzaliwe mara ya pili), anasafisha ile hali ya kutamani dhambi na kukufanya uwe mtakatifu na pia atakuongoza katika kuijua kweli yote tusome..

 Yohana 16:12 “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari”.

Jambo la kwanza Mkristo yeyote aliyepokea Roho Mtakatifu lazima Roho amuongoze katika kuijua ukweli, ikiwemo uelewa wa maandiko,kiu na shauku ya kumjua Mungu siku baada ya siku.na kufanywa ufanane na Yesu Kristo. Roho ya mafunuo itakuja juu yake, Hatafungwa na mambo ya dini bali na NENO la Mungu tu, na Roho atamweka mbali na ulimwengu, yaani kiu ya kuupenda mambo ya ulimwengu itaanza kufa ndani yake.

Jambo lingine ni Roho atashuhudia ndani yake kuwa yeye ni Mwana wa Mungu ( atakushuhudia katika maisha unayoishi)

Warumi 8:15 “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu”;

Mtu huyo ataondokewa na hofu ya maisha kwa kuwa anajua anaye baba mbinguni, na Baba anamshuhudia ya kuwa yeye ni mtoto wake ndani yake. 

Kuna watu angali wakijidanganya kuwa wana Roho Mtakatifu lakini wamekosa haya mambo, ndani yao tamaa ya mambo ya ulimwengu imewavaa, Hawana uhusiano wowote  wao na Baba yao wa mbinguni, hofu na masumbufu ya maisha haya yamewasonga kana kwamba hawana Baba mbinguni, Wanalipinga siku zote NENO la Mungu, kuthibitisha dini zao na madhehebu yao(mfano wa mafarisayo na masadukayo), Hawapendi kuijua kweli halisi ya injili inayowapeleka watu mbinguni bali injili za pesa na mafanikio ya ulimwengu huu tu.

Sasa watu kama hao ni dhahiri kuwa hawajashukiwa na Roho wa Mungu bado, haijalishi wanafanya miujiza kiasi gani. Sio kwamba kuwa na hizo ishara ni mbaya, tofauti ni hii hawa wanakuwa wamenyeshewa mvua tu lakini hawana Roho, na wale waliobatizwa kweli kweli wanakuwa na vyote, 

Hivyo basi Roho wa Mungu anaposhuka juu ya mtu kwa mara ya kwanza huyo mtu anaweza akaanza kunena kwa lugha, au kuona maono, au kutabiri au akapata msisimko, au kushukiwa na nguvu za Mungu nyingi ndani yake,au akapata hisia ya tofauti ambayo hakuwahi kuisikia hapo kabla, wengine wakati Roho akishuka juu yao amani ya kipekee inawashukia,wengine hawasikii chochote lakini watafahamu kwa jinsi Roho wa Mungu anavyougua ndani yao, haya yote ni udhihirisho wa nje ambao hata wale wengine(magugu) wanaweza kuupata.

Lakini uthibitisho halisi ni jinsi maisha yako yatakavyokuwa yanaanza kubadilishwa na kufanywa kiumbe kipya siku baada ya siku kwa kutakaswa kwa Neno. na ubatizo wa Roho Mtakatifu unaambatana na karama za Mungu lakini kama tulivyosema mtu anaweza kuonyesha zile karama za Roho na asiwe amebatizwa na Roho Mtakatifu.

Na kuna mtazamo pia ya kuwa “kunena kwa lugha” kuwa ndio uthibitisho wa mtu kupokea Roho Mtakatifu, mtazamo huu si kweli mtu anaweza kunena kwa Lugha na asiwe amepokea Roho Mtakatifu kwasababu hichi ni kipawa cha Roho na kinamshukia yeyote kwa jinsi Roho alivyomjalia mtu, kumbuka hata mashetani wananena kwa lugha, Na kipawa hichi sio lazima kila mtu awe nacho,

kwasababu biblia inasema 

1wakoritho12:28 “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
29 Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza?
30 Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri”?

Si unaona hapo sio wote wenye hicho kipawa cha kunena kwa Lugha. Kwahiyo mtu anaweza akabatizwa na Roho Mtakatifu na asinene kwa lugha, bali akaonyesha karama nyingine tofauti na hiyo, aidha unabii, au karama ya uponyaji, au neno la maarifa, au miujiza n.k. kwa jinsi Roho atakavyokujalia.. Mafundisho ya kwamba kila mtu lazima anene kwa lugha sio sahihi mwisho wa siku kama mtu hajapewa hicho kipawa anaishia kunena kwa akili zake tu, na kutakuwa hakuna kufasiri 1wakoritho 14.

Kwahiyo mpendwa kama haujabatizwa na Roho Mtakatifu mwombe Bwana naye atakupa Luka 11:9-13..”Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” 

Kumbuka kutoa zaka, kusaidia yatima, kuhudhuria ibada kila jumapili, hayo hayatoshi hata watu wasioamini wanafanya hayo na zaidi ya hayo(mfano mzuri ni waislamu)

soma….

Mathayo 5:20″ Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. “

Hii haki inakuja kwa kuzaliwa mara ya pili, hauwezi kuingia katika ufalme wa mbinguni pasipo hiyo, na ukishabatizwa na Roho Mtakatifu ndio kuzaliwa mara ya pili.

Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

Kumbuka Roho mtakatifu ndiye MUHURI wa Mungu, (maana ya neno MUHURI ni kwamba “KAZI IMEKAMILIKA JUU YAKO”).waefeso 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi”. Pasipo huyo hauwezi kwenda mbinguni, kwa sababu biblia inasema warumi 8:9 “……….Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”. 

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

JE! KARAMA NI UTHIBITISHO WA KUWA NA MUNGU?

JIPE MOYO.

BWANA ALIPOSEMA “SIKUJA KUTANGUA TORATI BALI KUITIMILIZA” ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?

rejeabiblia.com


Rudi Nyumbani

Print this post