Shalom, nakusalimu katika jina lipitalo majina yote la Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme YESU KRISTO, Mungu mkuu, Sifa na heshima, na utukufu ni vya kwake milele. Yeye ndiye mwokozi wetu, na huo ndio ukweli pekee uliodumu na utakaodumu duniani kwa wakati wote.
Tukisoma kile kitabu cha Matendo ya mitume 7:17 inasema..
“17 Basi wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu ulipokuwa unakaribia, wale watu wakazidi na kuongezeka sana huko Misri,
18 hata mfalme mwingine akainuka juu ya Misri, asiyemfahamu Yusufu.
19 Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi”.
Lipo jambo moja tunaweza kulitazama leo hii, biblia inatuambia wakati ile ahadi Mungu aliyomuahidia Ibrahimu kuwa siku moja uzao wake, utakwenda kuirithi nchi ya Kaanani aliyomuahidia, ulipokaribia, biblia inasema, kuna tukio lilifuata baada ya pale, na tukio lenyewe ni wana wa Israeli kuongezeka kwa kasi sana kule Misri.
Jambo ambalo liliwashtusha wamisri waseme ni nini kimewapata hawa watu mpaka wanazaliana kwa spidi kasi hivi, yaani pengine ndani ya miaka kumi tu , idadi imejizidisha mara 3 ukilishangisha na miaka mingine yote iliyopita huko nyuma, miaka mitatu tena mingine vivyo hivyo. Hilo liliwashtusha sana wamisri mpaka kuona tunazidiwa sasa tubuni njia mbadala..
Kutoka 1:7 “NA WANA WA ISRAELI WALIKUWA NA UZAZI SANA, NA KUONGEZEKA MNO, NA KUZIDI KUWA WENGI, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao. 8 Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.
9 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.
10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.
11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
12 LAKINI KWA KADIRI YA WALIVYOWATESA NDIVYO WALIVYOONGEZEKA NA KUZIDI KUENEA. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli”.
Umeona? Lakini biblia inatuambia kuongezeka kwao, hakukuwa bure tu bali kulikuwa na sababu, na sababu yenyewe ni kuwa ILE AHADI YA MUNGU ilikuwa inakaribia kwenda kutimizwa juu yao.
Nachotaka uone ni kuwa, sikuzote, ahadi ya Mungu inapokaribia kutimizwa, Mungu huwa anahimiza mambo fulani fulani yafanyike haraka sana ndani ya kipindi kifupi sana kisichoweza kudhaniwa. Wana wa Israeli pengine walikaa zaidi ya miaka 300, kule Misri na uongezekaji wao ulikuwa wa wastani tu, au wa kawaida sana, lakini walipokaribia karibia miaka 400 hapo, ndipo idadi ya watu ikaongezeka kwa ghafla sana.
Jambo hili linafunua nini kwa agano jipya?
Wengi wetu hatuijui vizuri historia ya ulimwengu, tunadhani mambo yalivyo sasahivi ndivyo yalivyokuwa miaka ya nyuma. Ndugu,fahamu karne ya 20 na ya 21, ndizo karne pekee ambazo zinawashangaza watu wengi sana ulimwenguni hususani wale wanaofuatilia habari za historia, tukisema karne ya 20 tunamanisha kuanzia mwaka wa 1901.
Mambo mengi sana yametimia yaliyokuwa yanazungumziwa na Bwana Yesu, pengine yalionekana kama ni uongo kwasababu hayakuwahi kutimia kwenye miaka yote ya huko nyuma. Lakini ilipotimia karne ya 20 yakaanza kuonekana, Jambo mojawapo ni kuchipuka tena kwa taifa la Israeli, ambalo linafananishwa na mtini. Pili, kutokea kwa vita vya dunia viwili, kulipuka kwa magonjwa yasiyohesabika, na yasiyotibika, hata mafua unayofahamu wewe, hayakuwepo miaka ya 1800, zote hizo zilizungumziwa katika Mathayo 24, Marko 13 na Luka 21
Na mbaya zaidi, kulipuka kwa wimbi la manabii wengi wa uongo duniani. Hili tumelishuhudia sana sana kwenye hii karne yetu ya 21, kote huko nyuma hakukuwahi kuwa hata na mtu aliyejiita nabii, lakini leo hii ni kitu cha kawaida sana..
Mambo mengine ni Kuongezeka kwa maasi, watu kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu, kuongezeka kwa teknolojia, smartphones, n..k ambapo kunatimiza ule unabii wa Danieli unaosema maarifa yataongezea(Danieli 12:4)…
Hayo yote ni kwasababu ile ahadi ya Mungu ya kulinyakuwa kanisa lake inakaribia kutokea hivi karibuni, kwahiyo Mungu anazidisha spidi ya mambo yote yatokee haraka haraka. Na mambo yote yakishatimia ghafla, atatokea Kristo na kulinyakua kanisa lake.
Ni kitendo cha kufumba na kufumbua, hutaona mtu. Tupo ukingoni mwa wakati, Mungu anahimiza mambo yake haraka haraka sasa hivi, Si wakati wa kuwa kama mke wa Lutu, mguu mmoja nje, mwingine ndani, ni wakati wa kumfuata Yesu wewe, kama wewe.
Luka 17:32 “Mkumbukeni mkewe Lutu.
33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.
34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.]”
Swali ni Je, umezaliwa mara ya pili, Je, wewe bado ni rafiki wa dunia? Je bado unaishi maisha ya kuwapendeza marafiki na wazazi? Mkumbuke mke wa Lutu.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Ni vitu vipi hivyo viwili visivyoweza kubadilika? (Ebr 6:18)
Wakati mwingine Mungu anatumia njia za dhahiri kabisa kufunua yale yanayoendelea rohoni. Kwamfano utaona wakati ule Yesu anakutana na yule kichaa, na kuyaamuru yale mapepo yamtoke, tukio lililofuata baada ya pale ni wale nguruwe kupelekwa moja kwa moja ziwani na yale mapepo na kuuliwa huko. Hiyo ni kufunua kuwa mapepo hayana malengo mengine zaidi ya kuua tu na kuangamiza, wala hakuna pepo zuri au jini zuri kama watu wa dini nyingine wanavyodhani, maadamu una pepo ndani yako, basi ujue lengo lao ni moja, kukuangamiza tu.
Na ndio maana utaona lile pepo ambalo wanafunzi wa Yesu walishindwa kulitoa, baba wa yule kijana alisema, mara nyingi linamtupa mwanangu kwenye maji..mara nyingine kwenye moto(Marko 9:22)..Fikiria wewe unadhani lengo lake lilikuwa ni nini kama sio kumwangamiza. Hivyo hata leo hii, ukiwa na pepo la uzinzi, ujue kuwa shabaha ni wewe ukutane na ukimwi, ufe kabla ya wakati wako, au hata ukumbane na mabalaa mengi mengi yasiyoeleweka,ili tu uondoke katika hali ya dhambi ujikute kuzimu.
Sasa, tukirudi katika habari ya mwanzo, tulisema Mungu huwa anaruhusu wakati mwingine mambo Fulani yaonekane kwa dhahiri ili kufunua hali halisi ya mtu ilivyo rohoni.
Sehemu nyingine tena utaona ni pale mtume Paulo, alipokutana na Yesu alipokuwa anaelekea Dameski kufanya kazi yake ya kuliharibu kanisa la Mungu, Na Bwana alipomtokea kama tunavyojua habari, ni kuwa nuru ya Yesu ilimwangazia pande zote, sasa kutokana na kuwa nuru ile ilikuwa kali, ilimfanya awe kipofu wa muda. Mpaka alipokwenda kuombewa na mtu mmoja aliyeitwa Anania baada ya siku tatu ndipo akaona tena.
Lakini baada ya kuombewa kwake, biblia inatuambia, vitu kama magamba vilidondoka machoni pake. Tusome.
Matendo 9:17 “Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
18 MARA VIKAANGUKA MACHONI PAKE VITU KAMA MAGAMBA, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.
haya magamba yalikuwa kwenye macho ya Paulo sikuzote lakini hakuwahi kuyajua, mpaka siku anaombewa na kudondoka ndipo anajua kitu hicho kilikuwa
Hiyo ilikuwa inafunua hali halisi ya Paulo ilivyokuwa rohoni. Alikuwa amepofushwa kikweli kweli na shetani, kwa kuwekewa haya magamba ya adui, bila hata ya yeye maskini kujijua.
Sasa haya magamba ya adui yapoje?
Haya, hayana malengo ya kuziba kila mahali katika maisha ya mtu hapana, haya yapo mahususi kukuziba lile eneo linalohusiana na kumjua Mungu. Unaweza ukawa na elimu yako nzuri, unaweza ukawa na hata na fedha nyingi, lakini unaweza ukashindwa kuiona njia Ya wokovu wa Mungu.
Pengine utakuwa mwepesi hata katika kufanya mambo mengine yote, utakuwa mwepesi kuelewa hata kanuni nyingine za maisha ya kila siku, lakini utakosa wepesi wa kuifahamu njia ya wokovu.
Ukihubiriwa habari za msalaba, kwako zinakuwa kama ni habari za kishamba vile, hata ukielezwa habari za kuzimu hazikushtui tena, haijalishi utatolewa na shuhuda nyingi kiasi gani, kwako ni kawaida tu, na ndio maana unaendelea na ulevi wako na uzinzi wako badi leo hii, sasa ukiona upo katika hali hiyo basi ufahamu magamba hayo ya rohoni yameshawekwa kwenye macho yako pasipo wewe kujijua. Pengine ulichobakiwa nacho ni kuisifia tu dini yako.
Na hali hiyo inaweza kuwa mbaya kiasi kwamba ukawa hata unaupinga wokovu, na kufanya vita nao kama ilivyokuwa kwa Paulo…Lakini jiulize unadhani Paulo alikuwa amekusudiwa kuwa mtu wa namna ile, ? Jibu ni hapana, ndio maana baada ya kuondolewa magamba hayo, akaupenda wokovu kwa namna isiyo ya kawaida, akawa mhubiri nambari moja wa njia ya wokovu.
Hii ni kazi ambayo shetani anaifanya kila kukicha, watu wanapofushwa macho yao ya rohoni, wasimjue Mungu, au wasione umuhimu wa wokovu, angali wakiwa bado hapa duniani.
2Wakorintho 4:3 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.
Magamba haya ukiyaendekeza ndani ya maisha yako, madhara yake utakuja kuyaona baada ya kifo. Kwasababu siku utakapokufa moja kwa moja utajikuta kule kuzimu, Na wewe huko utakuwa katika majuto yasiyokoma, kama ya yule tajiri wa Lazaro(Luka 16:19-31)… Mahali ambapo aliomba sana ndugu zake wasifike huko..
Ndugu yangu watu wanaoshuka kuzimu kila siku idadi yake haihesabiki, na wote huko laiti tungeonyeshwa hali zao zilivyo, jinsi wanavyojuta, jinsi wanavyosema tulipofushwa kiasi gani mpaka tukaudharau msalaba, na leo tupo hapa, tusingeuchukulia wokovu wetu juu juu tu. Hivyo tubu dhambi zako, mgeukie Kristo, na yeye atakuokoa. Epuka magamba haya ya ibilisi.
Kwasababu siku hizi ni za mwisho, na Kristo yupo mlangoni kurudi.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Paulo katika kazi yake ya utume, hakuwa tu na jukumu la kuwahubiriwa watu Kristo ili wamwamini, kisha wapokee ondoleo la dhambi halafu basi..Hapana, bali pia ni mtu ambaye alikuwa anatia bidii nyingi sana katika kuwajuza watu juu ya ukweli wote wa Mungu na siri nyingine zilizojificha katika maandiko tangu zamani.
Na ndio maana utaona alisema..
Waefeso 5:17 “KWA SABABU HIYO MSIWE WAJINGA, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.
Paulo alipiga vita ujinga ambao watu wanao kuhusu Mungu, kwasababu alijua ni jinsi gani unavyoweza kumgharimu mkristo kwa sehemu kubwa. Ujinga ni ile hali ya mtu kukosa maarifa ambayo kama angeyapata basi yangemsaidia kuishi au kutenda mambo fulani kwa ufanisi mahali alipo.. Kwamfano, mtu ukikosa kufahamu kuwa duniani kuna kitu kinachoitwa teknolojia, na kwamba ukitaka kuwasiliana na mtu aliye mbali utatumia kifaa kinachoitwa simu,
Sasa wewe hataki kusikia habari za simu, badala yake unataka tu kukaa maporini , kuwinda swala, kuna wakati utafika utahitaji kuwasiliana na ndugu zako wa mbali, hapo ndipo itakugharimu utumie miguu yako au punda kwenda kuwafuata na hiyo pengine itakuchukua mwezi mzima kwenda na kurudi, kiasi kwamba kama angepata maarifa ya simu, au vyombo vya moto basi kuwasiliana kwako au kusafiri kwako kungekuwa ni kurahisi sana na kwa haraka.
Vivyo hivyo na katika Ukristo, tunakosa maarifa mengi sana, na hiyo inapelekea pengine tunashindwa kuufurahia wokovu wetu , au kuona safari hii ni ngumu sana, au kushindwa kabisa kustahimili mengi. Siku zote Hatuwezi kumtumikia Mungu, juu ya kiwango cha ufunuo tulichonacho kuhusu yeye. Kiwango chako cha kumwelewa Mungu ndicho kitakachoeleza maisha ya wokovu unayoishi sasa.
Sasa Mtume Paulo ni mtu ambaye alikuwa anatamani kupata maarifa ya kutosha kuhusu ufalme wa mbinguni, na ndio maana siri nyingi zihusuzo kanisa, na Mungu tunazipata katika nyaraka zake.Na ndio maana sehemu nyingi utaona anasema Neno hili SITAKI MKOSE KUFAHAMU. Akiwa na maana hataki tuwe wajinga..
Embu tuangalie baadhi ya vitu ambavyo alitaka sisi tusikose kufahamu.
Anasema..
1Wathesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini”.
Ukiendelea kusoma pale utaona anaeleza jinsi siku ya unyakuo itakavyokuwa, kwamba utatangulia kwanza ufufuo wa wafu, hivyo wewe kama ni mkristo, ukiifahamu siri hiyo kwamba lipo tumaini la kufufuliwa na kuonana wa wapendwa wetu katika Imani waliotutoka, hatutakuwa na huzuni ya kupitiliza, kama watu wa kidunia walivyo, hatutakuwa wa kulalamika, na kulaumu laumu muda wote.
2) Kuhusu hukumu watakayokabidhiwa watakatifu.
1Wakorintho 6:2 “Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?”
Watakatifu watakaoshinda hawatahukumu tu ulimwengu, bali mpaka na malaika, Je ulishawahi kulifikiria hilo wewe utawahukumuje malaika? Fikiria tena hilo, uone ni mambo makubwa kiasi gani Mungu amewaandalia watu wake huko mbeleni.
3) Siri ya Yesu iliyojificha katika agano la Kale.
1Wakorintho 10:1 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo”.
Paulo anatufunulia siri nyingine kuwa hatupaswi kusoma agano la kale kama historia Fulani tu, tunapaswa tujue ndani ya historia zile Kristo amejificha, na Hivyo tunapaswa tusomapo tumwone Kristo, kwasababu vyote vile vilimfunua yeye. Hivyo Paulo anatuasa tusiwe wajinga pia katika hilo, tusome mawazo yetu tukiyaelekeza kwa Kristo.
4) Kuhubiri injili kuna dhiki.
2Wakorintho 1:8 “Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi”.
Wengi tunadhani katika kumtumikia Mungu ni mteremeko tu wakati wote, hapana, Bwana Yesu kiongozi wetu alipitia dhiki, mitume pia walipitia dhiki wakati mwingine, vivyo hivyo na wewe, unapaswa ulielewe hilo, ili kusudi kwamba litakapotokea, usije ukawa mjinga kwa kuacha kuifanya kazi ya Mungu, ukasema huyu ni shetani, kwani Mungu sikuzote haruhusu watu wake wapitie dhiki.
5) Miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu.
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
Anataka tufahamu kuwa hii miili tuliyopewa na dhamana, ni mali ya mwingine sio yetu, hivyo tuithamini kwasababu tukiiharibu kwa uzinzi, au pombe, au michoro, au chochote kile, tutaharibiwa na sisi. Hilo tusiwe wajinga, wengi wameuliwa na Mungu kwa njia hiyo.
6) Utumishi wa Madhabahuni.
1Wakorintho 9:13 “Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?”
Paulo hataki watu wawe wajinga pia kufahamu, watumishi wa Mungu wana haki ya kula vya madhabahuni, kwasababu ndivyo Mungu alivyoagiza na wala sio mwanadamu. Hivyo sio jambo la kujadiliana nalo au kushangaa utakapokutana nalo.
7) Karama za Rohoni.
1 Wakorintho 12:1 “Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu”.
Hapa yapo makundi mawili ya wakristo, lipo kundi ambalo haliamini kabisa, au haliruhusu karama za Mungu kutenda kazi katika kanisa la Kristo, wakisikia kuna mtu anakarama ya kuona maono wanasema ni shetani, wakiona kuna mtu ananena kwa lugha wanasema huyo sio Roho. Hivyo utakuta kanisa limebakiwa kuongozwa na wenyeviti na makatibu, na maaskofu- jina, na makasisi, basi, hakuna chochote cha Zaidi ya litrujia kufuatwa.
Kundi lingine, ni lile lisiloweza kumbanua karama za Roho, huduma za Roho, Utendaji kazi na Ujazo/Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Haya yote Mtume Paulo alitaka tusiwe wajinga, matokeo yake ni kuwa leo hii utakutana na watu wengi wenye karama huku wakiendelea na maisha yao ya kale wakidhani kuwa wana Roho Mtakatifu kumbe walishaachwa zamani, japokuwa karama zao zinaendelea kufanya kazi.
8) Mpango wa Mungu kwa mataifa.
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili”.
Hii ni siri kubwa ambayo tukiijua hatutaishi maisha ya patapotea kwenye ukristo wetu, siku tukifahamu kuwa Utimilifu wa mataifa utawasili, na kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea sisi hatutakuwa na neema tena ya kuupokea wokovu, bali itarudishwa tena Israeli kwa kipindi kifupi, ndipo tutakapoishi maisha ya umakini sana katika Ukristo wetu.
Wengi wetu tunadhani, tutaendelea tu hivi hivi mpaka Yesu atakaporudi, Ndugu, Wokovu utaishia kwa wayahudi sio sisi. Kwahiyo tukiwa wajinga tukidhani kuwa tutaendelea hivi hivi, tujue tupo katika hatari kubwa sana ya kuuokosa, Unyakuo. Bwana Yesu kuna wakati atasimama, na kuufunga mlango. Wakati huo utakuwa ni hapa hapa duniani, na sio mbinguni. Kwasababu Utimilifu wa mataifa utakuwa umewasili. Mungu atakuwa ameshamalizana na sisi, utakuwa ni wakati wa wayahudi tena.
Embu jiulize, Je, ikiwa neema hiyo inarudishwa kule Israeli, utampatia wapi tena Kristo, na wakati Roho Mtakatifu hayupo tena juu yako. Ikiwa leo hii, unamkataa unampinga, angali neema ipo, unadhani nafasi hiyo itakuwepo tena? Hivyo usiichezee hii neema ambayo ndio tunakaribia kumaliza nayo. Dalili zote zinaonyesha kuwa hatuna muda mrefu Unyakuo utapita. Wafu watafufuliwa, na sisi tutaungana nao kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni.
Hivyo tubu dhambi zako mgeukie Mungu.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
UTAWALA WA MIAKA 1000.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Marko 13:32 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
33 Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.
34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;
36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.
37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni”.
Nyumba ya Mungu inayozungumziwa hapo ni Kanisa lake, na kanisa sio jengo, bali ni mkusanyiko wa watu waliomwamini Kristo, (walioitwa kutoka katika ulimwengu wa dhambi, na kuingizwa katika neema ya kumjua yeye Wakolosai 1:13). Jengo ni mahali kanisa linapokutanika kumwabudu Mungu, kumshukuru, kumwimbia na kufarijiana, kuonyana pamoja na kukumbushana mambo ya msingi katika safari ya Imani.
Sasa katika mfano huo tunaona Bwana anaunganisha vitu viwili kwa pamoja; Anaunganisha shughuli za nyumba yake na ujio wake. Maana yake kuna vitu anategemea avikute vinaendelea kufanyika katika nyumba yake, na kila mtu ambaye ni amemwita na kumtoa katika ulimwengu wa dhambi, kwa ufupi ni kwamba anataka akute kila mtu yupo kwenye shughuli yake fulani, aliyompangia aifanye..
Kama ndani ya nyumba ulipangiwa kazi yake kuhakikisha usafi wa nyumba pamoja na choo, anataka akija akukute upo bize katika shughuli yake hiyo, na choo akikute kisafi muda wote, kadhalika kama mtu kazi yake ilikuwa ni ulinzi anataka akija amkute yupo macho muda wote, anazunguka huku na huko kuhakikisha usalama wa nyumba n.k.
Na katika kanisa la Kristo kuna kazi, hatujaitwa tukae tu…Bali tuifanye kazi yake, kwa karama alizotupa… Na vipawa alivyotupa sio vya maonyesho, mlinzi wa getini hajakabidhiwa ile bunduki na zile sare ili ajisifu yeye ana silaha, au ni shujaa, au atembee na hiyo silaha mtaani na kujionyesha, kwamba ni nani kama yeye, na kwamba yeye ni zaidi ya wote, ana uwezo wa kuua wote kwa dakika moja. Hapana, bali alipewa silaha hiyo kwaajili ya ulinzi wa pale alipowekwa,Sio kwa sifa.
Na karama za rohoni zote hatujapewa kwaajili ya sifa zetu, bali kwaajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, kama una karama ya kinabii, au kiinjilisti au nyingine yoyote hujapewa kwa lengo la kujisifu, bali ili uwatumikie wengine katika nyumba ya Mungu. Kama Mungu kakubariki sauti nzuri ya kumwimbia, hujapewa hiyo kwaajili ya sifa zako, wala Mungu hajakupa kwasababu anataka kukuinua kuliko wengine, bali amekupa ili kwa kuimba kwako watu watubu wamgeukie yeye, huku wewe mwenyewe ukiwa kielelezo. Hiyo ndio kazi uliyoitiwa uifanye.
Kwahiyo Kristo anataka akija akute kazi yake inafanyika ipasavyo, kila mtu katika eneo lake.
“Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe”.
Kwahiyo ni kama vile tupo katika jaribio, kila mtu anajaribiwa uaminifu wake kwa Mungu kulingana na kile Mungu alichokiweka ndani yake.
Na anasema anakuja haraka sana, na ujira wake (yaani mshahara wake) upo mkononi mwake..
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Kwahiyo huu sio wakati wa kuchezea karama au karama Mungu alizoziweka ndani yetu, ni wakati wa kuzifanyia kazi, kwasababu muda uliobaki ni mchache mpaka Kristo awasili, si wakati tena wa kulala, na kusema nitatubu kesho, nitamtumikia Mungu kesho, ni wakati wa kusema kila kitu kinachohusiana na ufalme wa mbinguni naanza kukifanya leo.
Na kama hujaokoka, huwezi kumtumikia Mungu..utafanyaje kazi katika kampuni ambalo hujaajiriwa??..Hivyo unapoamua kuokoka (yaani kumkabidhi Yesu maisha yako) unasajiliwa katika ufalme wa mbinguni, na hivyo Roho Mtakatifu anakupangia kazi kama anavyotaka yeye na si kama unavyotaka wewe au mtu mwingine yeyote. Kwahiyo kama hujampokea Yesu tubu leo kwa dhati huku ukiziacha kwa vitendo dhambi zote ulizokuwa unazifanya hapo awali. Kama utahitaji msaada zaidi katika hatua hii ya kumpokea Yesu, unaweza kutujuza inbox, au mtafute mtu yeyote aliye mtumishi wa Mungu karibu na wewe atakusaidia.
Na pia kama umeshaokoka, lakini unashindwa kuelewa karama/au huduma Mungu anayotaka umtumikie kwa hiyo, wasiliana na sisi tutakupa mwongozo wa jinsi ya kujua Neema ya Mungu iliyo juu yako.
Mwisho, kumbuka Bwana Yesu alisema katika Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake KILA SIKU, anifuate.”.
Kwahiyo katika kumfuata Yesu ni lazima tujikane kila siku, na si siku moja tu wala mara moja tu.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Mungu ni mmoja tu, lakini katika umoja wake amekuwa akijifunua katika majina mengi, kulingana na uweza wake alionao, au majira Fulani yaliyopita, au matukio ya namna tofauti tofauti yaliyotokea. Ni sawa, ni raisi Fulani aitwe JOHN, lakini huyo huyo anaweza akaitwa baba sehemu fulani, akaitwa mjomba sehemu nyingine , mhandisi kwa watu fulani, amiri jeshi mkuu eneo Fulani, babu sehemu nyingine n.k.
Unaona utaona vyeo vyote hivyo vimekuja aidha kulingana na wakati, au matukio, au nafasi aliyopo au ujuzi alionao n.k. Na vivyo hivyo Mungu wetu , alijifunua katika majina mengi, ambayo leo hii tutayatazama kwa ufupi.
ELOHIMU: Mungu mwenye uweza, muumbaji wa milele, mwenye nguvu (Mwanzo 1: 1, 17:7, Yeremia 31:33)
ADONAI: Mungu Mwenye enzi yote,kimbilio imara Mwa 15:2‐8, Kut 6:2‐3
EL-ELYONI: Mungu Aliye juu zaidi ‐Mwa14:18, Dan 4:34
YEHOVA-RAFA: Mungu-Atuponyaye. (Kutoka 15:26.).
YEHOVA EL – SHADAI: Mungu Ututoshelezaye (Mwanzo 17:1)
YEHOVA-NISI: Mungu ni Bendera yetu (Berani ya vita) (Kutoka 17:13-16).
YEHOVA-YIRE: Mungu atupaye (Mwanzo 22:14)..
YEHOVA-ROHI: Bwana ndiye mchungaji wangu (Zab 23)
YEHOVA-MEKADISHKEMU: Bwana atutakasaye (Kutoka 31:13)
YEHOVAH SABAOTHI: Bwana wa Majeshi (1 Samweli 1:3)
YEHOVA SHAMA: Bwana Yupo Hapa (Ezekiel 48:35).
YEHOVA EL-OHEENU: Bwana Mungu Wetu (Zaburi 99:5,8,9)
YEHOVA SHALOM: Bwana ni Amani Yangu (Waamuzi 6:24)
YEHOVA TSIDKEMU: Bwana ni Haki Yetu (Yeremia 23:6)
YEHOVA OLAMU: Mungu wa milele Zaburi 90:1-3
YEHOVA EL- GIBBORI: Mungu Mwenye Nguvu ( Isaya 9:6-9)
YE-SHUA (YESU): Mungu utuokoaye.(Mathayo 1:21 )
Jina Hili la YESU ndio jina tulilonalo mpaka sasa. Kwa kupitia hili ndio tunapata wokovu, kwa jina hili ndio tunamshinda adui, kwa jina hili ndilo tunapata Baraka, na kwa jina hili ndio tunaishi.
Lakini biblia inatuonyesha pia jina hili sio la kudumu, Upo wakati Kristo atakuja na jina jipya,(Ufunuo 19:12 ) jina hilo wakati huo litakuwa sio la Ukombozi tena, sio la kurehemu tena, bali litakuwa ni jina la kifalme. Na ndio maana wakati huu ambao angali bado neema ipo, usiruhusu, ikupite ikiwa wewe ni bado mwenye dhambi, Leo hii Kristo bado yupo kama kuhani mkuu akitupatanisha sisi na Mungu, ikiwa na maana kuwa mlango wa rehema bado upo wazi kwa kila mtu atakayetaka kuuingia, Lakini hautakuwa wazi sikuzote. Kwani dalili za kurudi kwa Yesu mara ya pili zimeshatimia zote, tunachongojea ni unyakuo tu.
Ikiwa upo tayari leo kumpa Yesu maisha yako leo ayaokoe basi huo utakuwa ni uamuzi wa busara sana kwako, Hivyo fungua hapa, kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Tarishi ni mtu aliyeajiriwa kwa kazi ya kusafirisha na kuwasilisha barua au nyaraka mahali pengine. Katika biblia watu ambao walikuwa wanatumwa kusambaza barua za wafalme kwa watu wa mji, au viongozi waliitwa Matarishi.
Kwa mfano katika habari hii, utaona enzi zile za wafalme kulikuwa na Mfalme aliyeitwa Hezekia ambaye alikusudia kurejesha tena sikukuu zilikuwa zimesahauliwa katika Israeli kwa miaka mingi, Hivyo ili adhma yake iweze kufanikiwa ilimbidi awaandae hawa wajumbe (matarishi) ili wamsaidie kulipeleka hili agizo lake kwa watu wote waliokuwa Israeli wapande Yerusalemu kwenda kumfanyia Mungu sikukuu ya pasaka..
2Nyakati 30:5 “Basi wakafanya amri kupiga mbiu kati ya Israeli yote, toka Beer-sheba mpaka Dani, ya kwamba watu waje wamfanyie pasaka Bwana, Mungu wa Israeli, huko Yerusalemu; maana tangu siku nyingi hawakuifanya kama vile ilivyoandikwa.
6 Wakaenda MATARISHI wenye nyaraka za mfalme na wakuu wake, kati ya Israeli yote na Yuda, na kwa amri ya mfalme, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia waliosalia wenu waliookoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru”.
Utaona tena, kipindi kile, cha Mfalme Ahasuero, Amri ilipotolewa na Mfalme kuwa wayahudi wote wanapaswa wauliwe ndani ya siku moja, utaona agizo hilo lilisambazwa katika miji yote kwa mikono ya hawa matarishi.
Esta 3:13 “BARUA ZIKAPELEKWA KWA MIKONO YA MATARISHI mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara”.
Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi..
Esta 8:10 “Akaandika kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutia muhuri kwa pete ya mfalme, akazipeleka barua kwa MATARISHI, wamepanda farasi, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, ndio waliozalishwa katika zizi la mfalme”.
Ayubu 9:25 “Basi siku zangu zina mbio kuliko TARISHI; Zakimbia, wala hazioni mema”.
Yeremia 51:31 “TARISHI mmoja atapiga mbio kumlaki mwingine, Na mjumbe mmoja atapiga mbio kumlaki mwenziwe, Ili kumpasha habari mfalme wa Babeli, Ya kuwa mji wake umetwaliwa kila upande”.
Soma pia 2Nyakati 30:10, Esta 8:14
Lakini swali la kujiuliza na sisi je ni matarishi wa habari gani? Je Ni habari za Kristo, au habari za watu mitaani?. Sote tunawajibu wa kuwa matarishi wa Kristo, tuwe wepesi kwenda kuwahubiria wengine habari njema za msalaba, ili waokolewe, kuliko habari nyingine zozote. Bwana anatazamia, vinywa vyetu, mikono yetu, maisha yetu, vyote vitumike katika kuutangaza ufalme.
Je, mimi na wewe tunafanya hivyo?. Majibu tunayo mioyoni mwetu,
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Buruji ni aina ya mnara ambao ulijengwa zamani mahususi kwa ajili ya kuvamia kambi za maadui zilizojengwa kwa kuta ndefu.
Kwa namna ya kawaida ilikuwa ni ngumu kuvamia ngome za namna hiyo..kwani askari walikaa juu ya kuta hizo ndefu wenye mishale ya moto na mawe mazito..kwahiyo kama nyinyi mtakwenda kushindana nao kwa njia za kawaida kwa pale chini. Kitakachokuwa kinaendelea ni kifo tu.
Hivyo iliwabidi wabuni njia nyingine za kuwashambulia maadui waliojizungushia boma juu ya kuta..ndipo hapo sasa yakagunduliwa haya maburuji..ambayo kwa chini yalikuwa na matairi manne..na urefu wake ulilingana na zile kuta za maadui zao au zaidi kidogo..hivyo askari walikuwa wanapanda mpaka juu kabisa mwa maburuji hayo…mahali ambapo watakuwa usawa mmoja na wale maadui zao..kisha wanaanza kuwashambulia..huku wanazidi kuusogelea ukuta wa mji kidogo kidogo.
Na wakishafanikiwa kufika kwenye ukuta wanashusha ngazi zao..kisha wanashuka kutokea huko huko juu na kuingia katika mji na kuanza kuwashambulia.
Tazama picha juu uone jinsi zilivyotengenezwa
Kwa kuwa buruji hizo zilikuwa zinajengwa kwa mbao..sasa ili kuzuia moto kutupwa kuziteketeza..walizizungushia chuma au ngozi za wanyama kiasi kwamba mishale ya moto hata ikitupwa haikuweza kuleta madhara.
Isaya 23:13
[13]Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; WAMESIMAMISHA BURUJI ZAO ZA VITA, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.
Pia kibiblia minara yote ya maficho iliyokuwa ndani ya ngome iliitwa kwa jina hili
Vifungu hivi vinaelezea neno hilo.
Waamuzi 9:46
[46]Kisha watu wote waliokaa katika ile buruji ya Shekemu waliposikia habari hiyo wakaingia ndani ya ngome ya nyumba ya El-berithi.
2 Mambo ya Nyakati 26:15
[15]Akafanya katika Yerusalemu mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu wastadi, iwekwe juu ya
na juu ya buruji, ili kutupa mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.
Soma pia Waamuzi 9:47,49 Yeremia 31:38, Sefania3:6 Wimbo 8:9 Nehemia 3:8
Halikadhalika pia kiroho zipo kuta nzito adui yetu ibilisi ameziweka mbele yetu.. lakini Tukimtumainia Bwana yeye mwenyewe ndio atakuwa buruji letu. Hatuhitaji nguvu za mwilini kupambana naye..bali zile za Rohoni..Wana wa Israeli walimwamini Mungu na wakafuata maagizo yake kwa ukamilifu..na walipokutana na zile kuta za Yeriko, sote tunafahamu ni nini kilitokea..ni kwamba zilizama chini zote..pakawa tambarare kama vile hakujawahi kuwa na kuta au ngome..
Halikadhalika na sisi tunahitaji kumwamini Mungu na kuishi sawasawa na njia zake. Na hayo mengine ya vita vya ibilisi yeye atayashughulikia mwenyewe kirahisi kabisa.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka?Je umepata uhakika kama ukifa leo utakwenda wapi?..una habari kuwa hili ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Na kwamba zile dalili zote za kuja kwa Yesu zimeshatimia tunachongojea sasa ni Unyakuo tu?
Unangojea nini? Tubu mrudie muumba wako katika hizi dakika za lala salama.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Nakusalimu katika jina la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tujikumbushe mambo ya msingi ambayo bila shaka moja ya hizi siku tutayaona yakitokea ulimwenguni.
Kwa kawaida ulimwengu umeundwa na makundi mengi ya watu, na kila kundi ni lazima utakuta kuna mtu Fulani linamtazamia, ambaye wanaamini ataulimwengu umeundwa na makundi mengi ya watu, na kila kundi ni lazima utakuta kuna mtu Fulani linamtazamia, ambaye wanaamini atakuwa aidha mkombozi wao wa kudumu au atakakuwa mkombozi wao atakayewaletea suluhisho la maisha yao kwa ujumla. Kwamfano Wanasayansi, kila siku wanatafiti, usiku na mchana, wakitumai siku moja watakutana na viumbe vinavyotoka sayari nyingine(Aliens), ambavyo wanaamini vitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kiteknolojia, hivyo siku watakapokutana navyo, na kuisoma sayansi yao basi matatizo mengi sana ya kijamii yaliyoshindikana yatatatuliwa. Hata pengine ikiwemo kifo au kuzeeka.
Vivyo hivyo, wanajamii,au wanasiasi nao hawapo tu hivi hivi, nao pia wanatazamia, atatokea kiongozi mmoja atakayeleta suluhu ya shida za watu, atakayeweza kuleta maendeleo ambayo yataigueza dunia na kuifanya kuwa sehemu ya amani, yenye furaha, na isiyokuwa na shida. Na ndio maana kila wanapomchagua kiongozi Fulani mpya, katika nchi wanampa muda ili waone kama ataweza kufanya hivyo, akishindwa watamtoa na kuleta mwingine, hivyo hivyo wataendelea mpaka wampate wanayemtafuta, lakini mpaka sasa bado hawajampata na ndio maana wanaendelea kuchagua na kurithisha, Jambo hilo lilikuwepo tangu zamani sana, na bado litaendelea kufanyika mpaka siku za mwisho.
Hali kadhalika na watu wa dini zote ulimwenguni, ikiwemo sisi wakristo kila dini inayo matarajio ya mtu fulani huko mbeleni atakayekuwa suluhisho la matatizo yao ya mwilini na rohoni, moja kwa moja.
Hivyo kiu hii ya kutafuta mtu fulani, au kitu fulani cha kuwatatulia matatizo yao, ni kiu ya asili ambayo Mungu aliiweka ndani ya mioyo wa mwanadamu Ili kusudi kwamba wamtafute yule ambaye anapaswa kutafutwa.
Ni pengo ambalo mwanadamu amejikuta analo tu ndani ya moyo wake maadamu anaishi duniani, na ndio maana kila siku anatafuta kwa bidii ni kwa namna gani ataweza kulijaza.
Hivyo kufanya habari kuwa fupi ni kuwa mtu sahihi ambaye alikuwa ameandaliwa kwa ajili yao hakuwa mwingine zaidi ya YESU KRISTO, huyu ndio jibu na suluhu ya tatizo na shida yoyote ya kiroho au ya kimwili, na huyu ndio wangepaswa wamtazamie, arudi kuja kuwakomboa na mateso ya ulimwenguni.
Sasa hakuna asiyejua kuwa hizi ni nyakati za majeruhi, kwamba Yesu yupo mlangoni kurudi kuleta suluhisho la matatizo yote ya ulimwenguni, lakini biblia inatuonyesha kabla kiongozi wa kweli hajarudi atatangulia kwanza yule wa uongo, na kwasababu watu hawapendi kuungozwa na Mungu, na huku ndani ya mioyo yao wana kiu ya kuongozwa, mtu huyu atakapokuja itakuwa ni rahisi sana dunia nzima kutekwa na yeye kwasababu atajifanya yeye kuwa kama Yesu,..Ndio maana Bwana Yesu alituonya akasema wakati wa mwisho watakuja wengi kwa jina lake wakisema wao ndio.. hivyo tusiwasikilize,
Ndivyo itakavyokuwa kwa kiongozi huyu atakuwa mashuhuri na amebobea katika Nyanja zote, atakuwa ni mwanasiasi, pia atakuwa ni mtu wa dini kweli kweli, ataushawishi ulimwengu kuwa ataleta Amani waliyokuwa wanaitafuta kwa muda mrefu, ataleta suluhu ya matatizo yao yote, na kwa jinsi atakavyokuwa na ushawishi mkubwa biblia inasema wale watu ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu watamwamini.
Ufunuo 13; 8 “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.
Hata iweje, ikiwa wewe wakati huo utakuwepo ulimwenguni, utamwamini tu, kama sio katika upande wa kisiasa, basi utamwamini tu katika upande wa kiimani/dini, kwasababu, mtu huyo atakuwa pia na uwezo mkubwa wa kufanya ishara kubwa na maajabu yasiyo ya kawaida.,
2Wathesalonike 2: 9 “yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo”;
Shetani anajua watu wanapenda ishara na hivyo atajaliwa kuzifanya tu, tena za wazi kwa wazi kwenye TV, watu wote wataziona, Kama vile alivyozifanya kipindi kile wazi wazi mbele ya farao pale Musa alipokwenda kuonyesha maajabu ya Mungu kwake, , watu watamwabudu kama Vile Mungu. Vilevile atakuwa Ni mtu ambaye atakuwa anaingia maagano mengi ya amani na watu wengi (Danieli 9:27) ….
Mtu huyo ndiye Mpinga Kristo, au kwa jina lingine asi, au mwana wa uharibifu.. kwa ufupi ni kuwa dunia nzima itamwelekea, na matokeo yake ni kuwa atafanikiwa kugeuza mfumo mzima wa dunia unavyokwenda, na wakati huo huo ndipo atakapoianzisha ile chapa ya mnyama kiasi kwamba hakuna mtu atakayeweza kununua au kuuza bila kuwa chapa hiyo, ikiwa na maana hata kuajiriwa.
Mpaka hapo Wanasayansi,watakapoliona hilo watakuwa wameshapata majibu yao, wananchi nao pia watakuwa wameshapata majibu yao, na viongozi wote vipofu wa dini watakuwa wameshampata masihi wao.
Wakati huo ukifika na kama wewe upo bado hapa duniani, ujue kuwa Dunia hii haitakuwa na zaidi ya miaka saba mpaka iishe. Kwasababu atapewa kutenda kazi yake ya kuua na kuchinja watu wote wasioipokea ile chapa yake kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Dhiki itakayokuwepo huko, biblia inasema haijawahi kutokea na wala haijatakaa itokee baada ya hapo. Kiasi kwamba mpaka mtu utoboe ,na hajashiriki kupokea chapa yake kwa namna yoyote ile, uwezekano wake ni sawa na asilimia sifuri. Ni jambo lisilowezekana kabisa.
Lakini mwishoni kabisa watu watakuja kugundua mbona hajaleta badiliko katika dunia, lakini hiyo itakuwa wameshachelewa, kwasababu mtu pekee ambaye anayeweza kuigeuza hii dunia na kuwa Paradiso ya Mungu ni MFALME YESU KRISTO PEKE YAKE.
Wakati huo ndipo Mungu ataanza kuiadhibu dunia kwa mpigo makali ya vitasa saba Ufu 16, ndipo watakapojua kuwa Kristo wa kweli anakuja. Hapo ndipo watakapojipanga wapigane na Kristo katika vita ile ya Har magedoni..lakini watauliwa wote ndani ya muda mfupi sana.
Mambo hayo hayana muda mrefu kuanza kutokea, kwasababu kama siri ya kuasi imeshaanza kutenda kazi unategemea vipi, tutakuwa na muda mrefu sana hapa duniani? Kila ishara ya siku za mwisho iliyozungumziwa kwenye biblia imeshatimia, tunachongojea hapa ni UNYAKUO tu, ambao hatujui ni lini, unaweza ukawa ni leo usiku, au kesho asubuhi, na ukishapita huo ndipo huyu mpinga Kristo ataanza kufanya kazi zake. Swali ni je! Upo ndani ya Kristo?. Je akirudi leo usiku unao uhakika wa kwenda kumlaki mawinguni? Kama huna uhakika fahamu kuwa dhiki kuu au ziwa la moto linakungoja, Na sijui utamjibu nini Yesu siku ile ya hukumu, kwa kusikia maneno yote hayo lakini hukutaka kuokoka.
Tubu mrudie muumba wako, hizi sio nyakati za kubembelezana tena.. Huu ni ule wakati wa NURU YA JIONI.
Maran Atha
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
UTAWALA WA MIAKA 1000.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.
ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.
Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?
INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.
Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe, karibu tujifunze biblia.
Je umewahi kujiuliza, mapepo yanapomtoka mtu yanakwenda wapi?..Je yanakufa au yanakwenda kuzimu?. Jibu ni kwamba idadi kubwa ya mapepo yanapomtoka mtu yanakwenda kutafuta kumwingia mtu mwingine, au yanarudi kutafuta kuingia pale yalipotoka kama mtu yule atakuwa hajajitakasa. Bwana wetu Yesu alitupa ufunuo huo..
Mathayo 12.43 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.
44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.
45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza….”.
Kwahiyo mapepo hayafi, bali yanapomtoka mtu yanarudi kwenye mzunguko. (Kama tu fedha inavyozunguka, inapotoka kwako haiendi kuchomwa wala kutupwa, bali inaenda kwa mwingine, na baadaye kurudia tena kwako kama umestahili kuipata).
Sasa ni muhimu kufahamu kuwa mapepo yapo kwenye mizunguko kila siku. Na ni muhimu pia kufahamu kuwa mapepo, pamoja na shetani wanaomba mbele za Mungu, (yaani wanapeleka hoja za maombi), na katika hayo mengine wanakubaliwa, na kufanyiwa kama walivyoomba. Ndio maana kuna umakini sana wa kuzidi kujitakasa, kwasababu biblia inasema shetani ni mshitaki wetu, maana yake anapeleka habari zetu mbele za Mungu, na katikati ya hizo habari anaingiza na maombi yake kututaka sisi.
Utaona alifanya hivyo kwa Ayubu, na alifanya hivyo kwa mfalme Ahabu..
1Wafalme 22: 19 “Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto.
20 Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi.
21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya.
22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo.
23 Basi angalia, Bwana ametia pepo wa uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako”.
Hivyo mapepo yanaomba kama sisi tunavyoomba, na kama yamestahili, yanapewa haki yao kama sisi tunavyopewa. Kwasababu Mungu ni mwenye haki, kila kiumbe alichokiumba anakipa kulingana na kinachostahili.. Kwamfano kama mtu ambaye hamtaki Mungu kabisa wala kumpenda ijapokuwa anajua yupo, lakini kamchagua shetani na kumwabudu, akiwa na akili zake timamu kabisa, mtu huyo ni milki halali ya shetani, ni haki ya shetani kuwa naye, hivyo ni haki ya shetani kumfanya lolote.
Sasa kwa mtu ambaye hajajitakasa, mapepo yanayozagaa huko na huko, yanaomba kwa Mungu kibali cha kumwingia, na zinapokosekana kabisa sababu za mtu huyo kuepushwa na mapepo hayo, ndipo mapepo hayo yanashinda hoja na hatimaye yanapewa ruhusa ya kumwingia .(Hivyo ndivyo watu wanavyoingiliwa na mapepo).
Kwamfano mtu ambaye ni mwasherati sana, tayari katika ulimwengu wa roho, idadi kubwa sana ya mapepo yameshatuma maombi ya kumwingia mtu huyo, lakini yanajaribu kuzuiliwa kwa muda, ili mtu Yule angalau atumiwe wahubiri wawili watatu watakaomwonya aache njia yake mbaya, lakini hasikii, siku zinasogea.. Bila kujua kuwa yupo kwenye hatari kubwa, lakini anaendelea hivyo hivyo, mwishowe yale mapepo yanashinda hoja na kupewa haki yao, ndio hapo yanaruhusiwa kumwingia huyo mtu.
Matokeo ya mapepo hayo kumwingia mtu ni aidha kumsababishia mauti ya ghafla ya mwilini na rohoni, na mikosi na magonjwa yasiyo na tiba mfano HIV, (na wengi hawafahamu kuwa wanaopata ugonjwa kama wa Ukimwi wala hawajaambukizwa na mtu mwenye ugonjwa huo. Wengi ni unaanzia tu kwao, kwasababu lile ni pepo, kama vile lilivyomwingia mtu wa kwanza kupata ugonjwa huo, ndivyo linavyomwingia mtu yeyote sasahivi, aliye mwasherati, sio lazima uambukizwe kutoka kwa mtu mwenye huo ugonjwa). Hiyo ni kutokana na mapepo hayo yameshinda hoja juu yako, kwasababu ya maisha anayoishi yasiyompendeza Mungu.
Unaweza kuuliza ni wapi tena maroho hayo yalionekana kumwomba Mungu…Tusome.
Mathayo 8.28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.
31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.
32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini”.
Hapo mapepo yanamwomba Bwana, na tena yanamsihi yasiende shimoni, bali yaende kwa nguruwe wale…Yalikuwa na sababu zote kwanini yaombe vile.
Na hata leo ni hivyo hivyo, wewe ni muasherati mapepo yanaomba ruhusa juu yako, na hata pengine yamesharuhusiwa bila wewe kujua, hayo yatakuongoza baharini kukuua kama yalivyofanya kwa wale nguruwe.
Umekuwa mtu wa vinyongo, na kutokusamehe, tayari umefungua mlango wa mapepo kukuvamia na kukuharibu..Umekuwa mwabudu sanamu na mchawi wewe tayari ni ngome ya adui.
Umekuwa mtu wa kuvaa kizinzi, na moyoni unajua kabisa mavazi kama hayo hata ukiitwa kwenye interview ya kazi huwezi kwenda nayo, lakini unaendelea kuyavaa na kukatisha nayo mtaani na hata kuingia nayo kanisani, fahamu kuwa wewe ni kituo cha mapepo.
Lakini leo umesikia neno hili, fungua moyo wako tubu, mwambie Bwana sitaki kuwa kituo cha mapepo, bali unataka kuwa kituo cha Roho Mtakatifu ndani yako. Na kama umedhamiria kutubu kabisa, unachopaswa kufanya baada ya toba hiyo ni kugeuka kikweli kweli, kama kulikuwa na watu hujawasamehe moyoni mwako kutokana na sababu Fulani Fulani, kuanzia dakika hii unawasamehe wote, haijalishi wamefanya kosa gani, kwasababu hata sisi Kristo alitusamehe.
Pia kama ulikuwa ni mzinzi na mwasherati, kuanzia dakika hii unakiri kuuacha kwa vitendo, maana yake Yule uliyekuwa unafanya naye uzinzi, unakata mawasiliano naye, na pia kama ulikuwa unavaa nguo za kizinzi unachoma, wala usiende kuzigawa, unazichoma zote usiache hata moja, na kama ulikuwa unatazama picha za pornograph na unasikiliza miziki ya kidunia katika simu yako unafuta yote kuanzia saa hii, wala usingoje kesho, kwasababu hujui yatakayozalika ndani ya siku moja, biblia inasema hivyo.
Na baada ya kufanya hayo na mengine yote yanayofanana na hayo, hapo toba yako itakuwa ni ya matendo, hivyo Roho Mtakatifu atashuka ndani yako kuhakikisha uyarudii matapishi na kuithibitisha imani yako, na hata kama kulikuwa ndani yako kuna mapepo, yataondoka yenyewe kwasababu Toba inayoambatana na matendo ina nguvu ya kufungua minyororo kuliko kitu kingine chochote, wala huhitaji kukemewa mapepo tena, (Toba ya namna hiyo hakuna pepo litakalosalia), ulichobakisha ni wewe kwenda kutafuta ubatizo sahihi wa maji tele (Yohana 3:23), na kwa Jina la Yesu Kristo kuukamilisha wokovu wako, kama bado hujabatizwa hivyo.
Na kuanzia hapo hakuna hoja yeyote ya shetani itakayoshinda juu yako, na mapepo yatawekwa mbali na wewe, na utaishi maisha yasiyo na usumbufu wowote kutoka kwa adui.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Bwana Yesu asifiwe. Karibu tujifunze neno la Mungu.
Paulo ni kielelezo kikubwa sana, kwa watu walio katika dhambi leo hii, ukiyatazama maisha Paulo, utajifunza mengi sana, Yeye mwenyewe anasema hapo zamani alikuwa ni mtukanaji, akiwa na maana alikuwa mtu asiyekuwa na maadili katika jamii, anasema tena alikuwa ni jeuri, kuonyesha kuwa alikuwa ni mtu mwenye kiburi kilichoshindikana,
Lakini ni heri angekuwa tu na tabia hizo ambazo ni za kawaida kuonekana kwa mwenye dhambi yeyote, kibaya zaidi alikuwa ni “mpinga-Kristo”, ile roho ya mpinga kristo ilikuwa tayari imeshamvaa, roho ya asi, mwana wa uharibifu, na kama tunavyojua kilele cha juu kabisa cha uasi wa dhambi ni kuwa adui wa Kristo, kama vile shetani alivyo, yaani kuwa mpinga-Kristo. Na ndio hatua ambayo mtume Paulo alikuwa ameshaifikia.
Yeye ndio alikuwa anaasisi mauaji yote ya watakatifu waliokuwa Yerusalemu kwa wakati ule, hata kifo cha Stefano yeye ndiye aliyetekeleza tukio lile zima, alikuwa ni katili wala alikuwa hana huruma na mtu yeyote aliyeitwa mkristo, Hiyo ikapelekea mpaka habari zake zikavuma kwenye makanisa yote ya wakristo, kiasi kwamba ilikuwa wakisikia tu Paulo yupo sehemu fulani, waliondoka na kwenda kujificha sehemu nyingine.
Hilo peke yake halikumtosha alianza kutanua mpaka na mipaka, akawa anaomba barua ili aende miji ya kando kando kwenda kuwakamata hao wayahudi wanaojifanya wanamwabudu Yesu, na kuwafunga. Hivyo kwa wakati ule alifanyika chombo kiteule cha ibilisi kupambana na uzao wa Mungu duniani. Unaweza tengeneza picha alikuwa ni mtu wa namna gani huyu. Huyu Unayemsoma kwenye nyaraka sio Yule Sauli wa zamani.
Lakini neema ya wokovu ilipomjia MARA MOJA TU. Na kutii, alipokea badiliko la ajabu sana. Badiliko ambalo lilimfanya awe Paulo na sio Sauli tena. Na kwa jinsi alivyoithamini ile neema, ndivyo Mungu alivyozidi kumwongezea neema juu ya neema mpaka, akawa zaidi hata ya wale mitume wengine ambao walionekana kama ni nguzo katika kanisa ambao mitume ambao walitembea na Yesu mwenyewe duniani.
1Timotheo 1:12 “Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu ALINIONA KUWA MWAMINIFU, akaniweka katika utumishi wake;
13 ingawa hapo kwanza nalikuwa MTUKANAJI, MWENYE KUUDHI WATU, MWENYE JEURI, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.
14 Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.
15 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.
16 Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE, wapate uzima wa milele.
17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina”.
Mtu ambaye hakuwahi kumwona Bwana Yesu akitembea duniani, mtu ambaye hakuwepo hata siku ile ya Pentekoste ya kwanza, mtu ambaye alikuwa ndio adui nambari moja wa msalaba, leo hii ndio tunasoma nyaraka zake akitufundisha sisi.
1Wakorintho 15:9 “Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.
10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja name”.
Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu, hatazami sana, ulimuudhi pakubwa kiasi gani huko nyuma, au uliiharibu kazi yake kiasi gani huko nyuma, anachoangalia ni jinsi gani umemaanisha leo hii kutubu, na kumgeukia, na kumtii yeye. Hapo hapo ndipo anapopatazama sana. Katika hali uliyopo anataka kuanzana na wewe hapo hapo
Na kwa jinsi utakavyoendelea kumaanisha ndivyo atakavyozidi kukupandisha viwango siku baada ya siku, mpaka unakuwa zaidi hata ya wale waliokutangulia katika imani zamani, hao ambao leo hii wanaonekana ni watu wa Mungu wakubwa. Hiyo ndiyo kanuni ya Mungu, hanaga, kwamba kisa huyu nilimtokea, au huyu nilizungumza naye kwa sauti, au huyu nilitembea naye kwa ishara, ndio maana ninampa neema..hilo hana.. ingekuwa ni hivyo asingemfanyia Mtume Paulo, angeendelea tu na wale wale mitume wake 12, kuwafanya wawe juu tu siku zote.
Pale pale unapotubu kwa kumaanisha kabisa kuacha maisha yako ya dhambi na kuanza maisha mapya naye.. Hapo hapo neema yake inaanza kumwagwa juu yako. Na viwango vyako vinapandishwa kuanzia dakika hiyo,.
Hivyo maanisha kumwamini Yesu, ishi maisha kama ya mtu aliyetubu. Onyesha bidii kwake, na wewe mwenyewe utakuwa shahidi kwa pale atakapokufikisha..
Paulo ni kielelezo tosha cha sisi, tunaomwamini Yesu leo, kwamba tutafanywa kama yeye au hata zaidi ikiwa tutakuwa waaminifu kama yeye.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo: