Jibu: Tusome mstari huo kuanzia juu kidogo.
Warumi 14:21 “Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.
22 Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.
23 Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. NA KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI”
Tukirudi juu Zaidi katika Mstari wa 14, Neno la Mungu linasema..
Warumi 14:14 “Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi”
Katika mistari hii, biblia ilikuwa inazungumzia juu ya vyakula..Na katika agano jipya, biblia imesema hakuna chakula chochote kilicho najisi.. Kwasababu kinachomwingia mtu mdomoni hakimtii unajisi, bali kile kimtokacho moyoni mwake ndicho kinachomtia mtu unajisi..Ni Bwana wetu Yesu ndiye aliyetupa ufunuo huo, ambao ni kweli kabisa..kasome Mathayo 15:16-20.
Kwahiyo katika agano jipya, nguruwe sio najisi, Kambale sio najisi, hata wanaokula nyoka hawapati unajisi wowote.
Lakini kwasababu ufunuo huo umekuwa mgumu kueleweka kwa wengi, kwamba vyakula vyote vimetakaswa.. Hivyo bado wanabaki kuamini kuwa vipo baadhi vilivyo najisi, kama nguruwe, Kambale, na vingine baadhi…. Sasa hawa ndio biblia inawataja kuwa “DHAIFU WA IMANI” (Warumi 14:1), haijalishi wao watajiona wana Imani kiasi gani, lakini biblia imewataja kuwa ni dhaifu wa Imani. Na miongoni mwao wapo Wakristo na wasio wa Kristo.
Sasa kwasababu biblia ni kitabu cha Hekima, imetufundisha jinsi ya kuenenda na hawa watu,
Kwanza: hatupaswi kuyahukumu mawazo yao (Maana yake kuwalazimisha waamini tunachoamini sisi, ikiwemo pia kushindana nao hatupaswi kushindana nao).
Pili: hatupaswi kuutumia ujuzi huo tulionao sisi kuwafanya wamkosee Mungu, au wamwache Kristo au kumchukia.
Maana yake ni kwamba labda umemhubiria Muislamu, akamwamini na kumpokea Kristo, lakini bado akawa anaamini kuwa nguruwe ni najisi. Na wewe kwasababu una UJUZI wa kujua kuwa hakuna kilicho najisi, hupaswi kwenda kula nguruwe mbele yake..au kumlazimisha ale nguruwe, ukifanya hivyo mwisho wa siku utamhuzunisha na kumfanya arudi nyuma au auchukie ukristo moja kwa moja..Na tukimkosesha mtu mmoja kwaajili ya chakula biblia inasema tunamtenda Kristo dhambi (Ndio hapo biblia inasema ni heri nisilie nyama kabisa kama itamkosesha ndugu yangu)..
1Wakoritho 8:11 “Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa ujuzi wako, naye ni ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
12 Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo.
13 Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu”
kwasababu hata asipokula hivyo vyakula tunavyokula sisi haviwafanyi wao wasiende mbinguni. Wasipokula nguruwe Maisha yao yote au Kambale, na wakawa wamempokea Kristo, watafika mbinguni tu.. Hivyo hatupaswi kutumia UJUZI wetu kuiharibu kazi ya Mungu ya wokovu.
Ndivyo biblia inavyosema katika..
Warumi 14: 1 “Yeye aliye DHAIFU WA IMANI, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.
2 Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
3 Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali.
4 Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha”
Sasa kwa huyu mtu ambaye ni DHAIFU WA IMANI, ambaye moyoni mwake “anaamini kabisa kwamba kula nguruwe ni dhambi, au kula chakula Fulani ni dhambi”.. mtu huyu akaacha kufanya hicho kitu anachokiamini na kwenda kula nguruwe au chakula kingine chochote ambacho anajua sio sawa kulingana na anachokiamini moyoni mwake. Huyo mtu ni wazi kuwa baada ya kula, moyoni mwake ATASIKIA HALI YA KUHUKUMIWA. Sasa hiyo hali ya kuhukumiwa anayoisikia maana yake ni kwamba, amefanya kitu kinyume na anachokiamini, Hapo tayari kafanya tendo ambalo halijatokana na kile anachokiamini, na hivyo ANATENDA DHAMBI!!…Hiyo ndio maana ya “KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI”,
Lakini kama macho yake yalifumbuka na kupata ufunuo kuwa “ni kweli hakuna kilicho najisi” na kwa ufunuo huo akaenda kula chakula ambacho hapo kwanza alikuwa anakiona ni najisi..Ni wazi kuwa mtu huyo baada ya kula hatasikia kuhukumiwa moyoni mwake, kwasababu amefanya kitu akiwa na uhakika kwamba hamtendi Mungu dhambi, na hivyo atakuwa kafanya jambo lile kwa Imani, na kwake hiyo haitahesabika kuwa ni dhambi.
Hivyo ndugu unayesoma ujumbe huu, ambaye ni mkristo, kama unaamini kuwa bado kuna vyakula najisi, na hivyo dhamiri yako inakushuhudia kwamba hupaswi kula, basi usivile lakini hakikisha unaushikilia utakatifu wote na kukaa katika maagizo ya Mungu.
Na kama wewe haupo katika Imani ya kikristo (maana yake ni Muislamu au mtu wa Imani nyingine), fahamu kuwa Yesu anakupenda na alikufa kwaajili yako..Njoo kwa Yesu na heshima yako hiyo hiyo uliyonayo, yeye atakuongezea nyingine juu ya hiyo itakayodumu milele, …njoo kwa Yesu na ustaarabu wako huo huo, hatakupokonya, badala yake atakuongezea na mwingine mwingi udumuo milele…njoo kwa Yesu na maadili yako hayo hayo, na kujisitiri kwako huko huko, atakuongezea na mwingine mwingi…Njoo kwa Yesu ukiwa huli nguruwe hivyo hivyo, wala hatakuambia uanze kuzila nguruwe..anachokihitaji ni roho yako na si tumbo lako, akuokoe akupe uzima wa milele bure!..Kwasababu yeye ndiye aliyetumwa kuukomboa ulimwengu, wala hakuna mwingine.
Hivyo kama umeamua leo kumpokea hatua inayofuata ni rahisi sana, hapo ulipo piga magoti, kisha fuatilisha sala hii kwa kufungua hapa >>> SALA YA TOBA
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Luka 23:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze biblia.
Kama tunavyojua wengi wetu, kwamba Kristo hakusulubiwa peke yake pale Kalvari, bali alisulubiwa pamoja na wanyang’anyi wengine wawili. Na wote walikuwa wametundikwa msalabani kama Bwana, kufunua kuwa na wao pia wapo katika mateso na uchungu. Lakini kilichowashangaza zaidi ni kuona anayejiita ni mkombozi naye pia yupo katika mateso kama wao. Katika hali ya kawaida ni jambo linalochanganya kidogo. Hivyo kila mmoja akawa na neno la kumwambia Bwana Yesu.
Wa kwanza akatangulia kumwambia Bwana,……
“Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini YESU HAKUMJIBU NENO. (Luka 23.39 )”
Kitendo tu cha kuanza kwa kumwambia Bwana…wewe si Kristo?..hicho tayari ni kitendo cha kukosa heshima!..na hakujua kama tayari kamtukana Mungu, kwa kusema tu hivyo..
Mfano kamili wa watu wengi wa siku hizi za Mwisho, Wapo katika dimbwi kubwa la matatizo, na shida lakini watasimama mbele za Mungu, na kusema “kama wewe Mungu upo na una nguvu, mbona huniokoi na shida hizi” na pia “mbona baadhi ya watu wako wana shida nyingi, waokoe watu wako kwanza na shida zao na ndio utusaidie sisi”.
Hawajui kwamba tayari wanamtukana Mungu kwa hayo maneno. Sasa watu wa namna hii, kamwe wasitazamie kupokea majibu yoyote kutoka kwa Mungu, kwasababu wamekosa unyenyekevu…
Ndio maana unaona huyo mnyang’anyi alitazamia atajibiwa na Bwana kwa kejeli zake, lakini Kristo hakutoa neno lolote hata la kumwambia atubu!
Lakini tukiendelea na Mtu wa pili, ambaye naye pia alikuwa anaswali kama hilo hilo kichwani?, isipokuwa huyu alituliza akili yake na kufikiri mara mbili, na kujua kuwa yaliyompata amestahili kupokea malipo yake, na kwamba Kristo yaliyompata hakustahili, maana yake ni kwamba amejitoa kusulubiwa kwaajili ya makosa ya watu wengine, na si kwa makosa yake….kwa kutafakari sana..roho ya unyenyekevu ikamwingia, na ya kuomba msaada..
Luka 23:40 “Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.
42 Kisha akasema, EE YESU, NİKUMBUKE UTAKAPOİNGİA KATİKA UFALME WAKO.
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”
Hebu mtafakari huyu mtu wa pili, Hata hakuomba kushushwa msalabani aendelee na maisha yake, hakumwomba Yesu amshushe arudi akaione familia yake, hakuomba Yesu amwokoe pale msalabani arudi kwenye biashara yake, hakuomba Yesu amwokoe pale msalabani ili asiendelee kuteseka na maumuvi ya misumari…lakini alimwomba Yesu UZIMA BAADA YA KIFO. Alikikubali kifo, lakini aliomba tu uzima baada ya hicho kifo. Alisema nitastahimili shida ninayoipata sasa, nikipata msamaha wa kushushwa hapa msalabani sawa, nisipopata pia ni sawa, nitavumilia mateso, lakini tu, niupate huo UZIMA WA MILELE, baada ya kufa kwangu. Huyo pekee yake ndiye Kristo aliyemjibu!.
Lakini yule wa Kwanza hakujibiwa Neno hata moja. Na matokeo yake alikufa katika mateso yake na akakosa vyote, akakosa maisha ya dunia aliyokuwa bado anayatamani, na vile vile akakosa uzima baada ya kifo.
Ndugu yangu, huu sio wakati wa kumfuata Kristo ili upate MALI, na huku huna uzima wa milele moyoni mwako..Kristo hatakujibu chochote!..Unapitia shida sasa za kidunia, sio wakati wa kulia uondolewe kwenye hizo shida huku shida ya roho yako bado ipo, huku hutaki kusikia hata habari za Neno lake, Ukisikia habari za Yesu kwako ni habari za kupoteza muda tu, comedy zinazolikebehi Neno lake ndizo zinazokuchekesha… hapo usitazamie kujibiwa chochote.
Tafuta uhakika kwanza wa uzima wa maisha baada ya haya kuisha, Ndio kitu cha muhimu kwa sasa. Ukikimbilia kuomba msaada wa mambo ya kidunia, kuna uwezekano mkubwa usikipate hicho unachokitafuta na ukafa katika shida zako, na ukakosa vyote (ukakosa Uzima wa Milele pamoja na Mali unazozitafuta).
Mathayo 6: 33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”.
Leo umesikia ujumbe huu, pengine ulikuwa unamtukana na kumdhihaki Mungu pasipo kujua..Upo kwenye shida kweli lakini umekuwa mtu wa kulalamika mpaka kufikia kumdhihaki Mungu… ndio maana leo umekutana na ujumbe kama huu ni kwasababu Kristo bado anakupenda, ndio maana bado hujafa..Upo hapo msalabani umening’inia na shida zako, zinakutesa kweli, unatamani kutoka hapo…Usikimbilie kutafuta msaada wa kutoka hapo kwanza, kwasababu kwa dhambi zako umestahili kuwepo hapo ulipo…Unachopaswa kufanya sasa, ni kuanguka chini, kwa unyenyekevu na kutubu na kumwomba Bwana Yesu msamaha kwa dhambi zako, na kumwambia kuanzia leo nakufuata naomba unipe uzima wa milele…Hata kama usiponitoa katika haya mateso ninayopitia sasa, naomba unipe UZİMA WA MİLELE, hata kama nikifa leo pasipo kupata chochote katika haya maisha naomba Uzima wa milele baada ya kifo..hicho ndio cha kwanza tunachokihitaji sisi.
Ukiomba maombi ya namna hiyo Roho Mtakatifu atashuka ndani yako kukupa jibu la maombi yako, amani ya ajabu itashuka ndani yako, na utaona akili yako imebadilika na kuwa kama ya Bwana Yesu, kiasi kwamba hizo shida zitakuwa sio kitu kwako, kwajinsi hiyo furaha itakavyokuwa kubwa ndani yako.
Lakini kwanza mpokee Kristo katika maisha yako, na tubu…Na pia kama umetubu hakikisha unatafuta ubatizo sahihi, ambao ni wa maji tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38) kukamilisha wokovu wako.
Na pia kama utapenda kushare ujumbe huu na wengine, tunaomba usiondoe chochote, ikiwemo anwani ya www wingulamashahidi org pamoja na namba zetu hizi 0789001312.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Je! Biblia ina vitabu vingapi?
Biblia takatifu ina jumla ya vitabu 66, kati ya hivyo 39 ni vya agano la kale, na 27 ni vya agano jipya.
Ifuatayo ni orodha ya vitabu vya agano jipya:
Zipo zinazosemekanakuwa ni biblia, ambazo zina vitabu 72 na nyingine zaidi. Na zinatumiwa na baadhi ya madhehebu ya kikristo kama vile Katoliki na Othrodoksi. Vitabu hivyo vilivyoongezwa havijathibitishwa kuwa vimevuviwa na Roho Mtakatifu hivyo hatupaswi kuviamini.
Biblia tunayopaswa kuiamini ni ile yenye vitabu hivyo 66 vilivyoorodheshwa hapo juu.
Shalom.
Je! utapenda uwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp? kama ndivyo basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Wakaldayo ni wenyeji wakongwe wa Mji wa Babeli. Mji wa Babeli ulikuwepo maeneo ya nchi ya Iraq kwasasa.
Hawa wakaldayo ndio waliowachukua mateka wana wa Israeli na kuwapeleka utumwani Babeli..
Yeremia 21:8 “Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.
9 Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.
10 Maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu niuletee mabaya, wala nisiuletee mema, asema Bwana; utatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza”.
Ezra 5:12 “Lakini hapo baba zetu walipomkasirisha Mungu wa mbingu na nchi, hata akaghadhibika, akawatia katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Mkaldayo, naye ndiye aliyeiharibu nyumba hii, akawachukua watu mateka mpaka Babeli”
Pia Ibrahimu kabla ya kuhamia nchi ya Kaanani, alikuwa anaishi huko Uru ya Wakaldayo. Kwasababu Babeli tayari ilikuwepo miaka mingi kabla hata ya Taifa la Israeli kuwepo, ndipo ule Mnara wa Babeli ulipotengenezewa.
Mwanzo 11:31 “Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko”.
Hivyo popote biblia inapowataya Wakaldayo ina maanisha Wenyeji wa Babeli.
Je una habari kuwa Babeli iliyowachukua wana wa Israeli mateko kwa namna ya kimwili, ipo leo kwa namna ya kiroho?..Kama ulikuwa hujui basi kasome kitabu cha ufunuo mlango wa 17 na kuendelea.
Na Babeli hiyo ya rohoni inawachukua utumwa watu wengi leo pasipo wao kujua, na mwisho wa siku inawaua kiroho na kuwapeleka kuzimu. Na Babeli hii sasa inafanya kazi kwa nguvu katika dini na madhehebu, na Bwana ataihukumu katika siku za mwisho.
Ufunuo 14:8 “Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake”.
Kwa urefu kuhusu Babeli hii ya rohoni fungua hapa >> BABELI YA ROHONI
Je umeokoka?. Kumbuka Kristo anarudi saa na wakati usiodhani?..Wakati unafikiri bado sana ndio wakati anaokuja..
Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.
Kama hujampokea ni vizuri ikampokea sasa hivi, wala usisubiri hata dakika 5 mbele, kwasababu hujua yatakayojitokeza dakika mbili mbele. Hivyo hapo ulipo piga magoti, kisha tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na Bwana wa huruma na Neema atakusamehe bure, na kukutakasa. Na baada ya hapo tafuta ubatizo sahihi, wa maji mengi na kwa jina la Yesu, na tafuta kanisa la Kristo la kiroho, lililo karibu nawe, jiunge hapo na wakristo wenzako ili ujengeke kiroho, na Roho Mtakatifu atakuongoza kufanya yaliyosalia.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
SWALI: Wibari ni nani? Na kwanini wanatajwa kama moja wa viumbe wanne wenye akili nyingi?(Mithali 30:26)
JIBU: Wibari ni wanyama wadogo wanaokaribia kufanana na sungura, kwa jina lingine wanajulikana kama pimbi, au kwanga, au perere, tazama kwenye picha.
Wanyama hawa utawaona wakitajwa kwenye vifungu hivi katika biblia;
Walawi 11:4 “Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu”.
Zaburi 104:18 “Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari”.
Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.
25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba”.
Lakini ni kwanini wametajwa kama moja ya viumbe vinne vyenye akili nyingi duniani?
Ni kwasababu ya tabia yao, wanyama hawa ni waoga, hawali nyama, wala hawapo machachari sana ukilinganisha na wanyama wengine, hawawezi kukimbia sana, kwa ufupi ni viumbe dhaifu ambavyo ni rahisi kukamatwa na maadui zao, lakini katika udhaifu wao, wanajua ni wapi pa kujihifadhi nafsi zao, na si hapo pengine zaidi ya kwenye miamba.
Wibari wanatengeneza nyumba zao kwenye mapango ya miamba, mirefu, na migumu, kiasi kwamba adui zao ni ngumu kuwaona au kuwakamata, tofauti na wanyama wengine kama ngiri au sungura n.k ambao wao wanachimba mashimo ambayo hata adui zao wanaweza kuwafuatilia na kuyafukua na kuwakamata, au mvua ikija ikajaza mashimbo yao wakafa, au upepo mkubwa ukivuma unaweza kufukia mashimo yao kwa udongo utakaoporomoka au kuingia, hivyo hiyo inawafanya maisha yao kuwa hatarini sana japokuwa ni machachari au wana uwezo mkubwa wa kukimbia.
Lakini wibari kweli sio kama wanyama wengine, ni wadhaifu sana lakini wanafahamu ni wapi wanaweza kuwa salama.
Je na sisi, tutashindwa akili na wibari?
Usalama wetu upo wapi? Je tumeyajenga maisha yetu wetu wapi? Je, ni mashimoni au kwenye vichuguu, au kwenye miti au kwenye mwamba?. Tujue tu kuwa mwamba ni mmoja tu, naye ni YESU KRISTO peke yake. Ukiwa nje ya Kristo, fahamu kuwa maisha yako yapo katika hatari zote, haijalishi utajiona wewe ni mjanja kiasi gani, haijalishi utajiona ni hodari kiasi gani, haijalishi ni tajiri kiasi gani, shetani atakumaliza tu..Huna safari ndefu..
Sikiliza maneno ya Yesu..
Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa”.
Kweli itakuwa ni ajabu sana tukishindwa akili na mnyama pimbi.
Shalom.
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=mJ0AkfAcM4I[/embedyt]
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Fungua hapa >> MAFUNDISHO
Bustani ya Edeni ipo nchi gani kwa sasa duniani?
Mungu alipoiumba dunia, alichagua eneo moja, na kulifanya kuwa la kipekee na la kitofauti na maeneo mengine yote aliyoyaumba duniani. Eneo hilo akaliita Edeni. Edeni maana yake ni eneo la furaha kuu, utulivu,paradiso ya Mungu.
Lakini hakuishia hapo tu bali ndani ya hiyo Edeni upande wa mashariki alitengeneza bustani nzuri sana, ambayo inajulikana na wengi kama bustani ya Edeni. Bustani hii ndiyo Mungu aliyomweka mwanadamu wa kwanza hapo aishi (yaani Adamu na uzao wake.)
Lakini kama tunavyosoma biblia, wazazi wetu wa kwanza walipoasi, walifukuzwa kutoka katika bustani ile, na kuanzia hapo, hakuna aliyejua makao halisi ya bustani ya Edeni yalikuwa wapi, vifunguu pekee vinavyotupa taswira ya eneo la bustani ya Edeni ni hivi;
Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.
11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;
12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.
13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.
14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati”.
Kama tunavyoona hapo, kulikuwa na mto uliokuwa unatoa maji kutoka bustanini na baadaye ukagawanyika katika vichwa vinne, na viwili kati ya hivyo (yaani Hidekeli na Frati) vinajulikana mpaka sasa na vipo maeneo ya nchi ya Iraq, ili kusoma na kufahamu zaidi historia yao fungua hapa >>>> Mto frati na Hidekeli Na hiyo imewafanya masomi wengi wa biblia kudhania kuwa Edeni ilikuwa maeneo ya nchi ya Iraq au kando kando yake.
Lakini vile vingine viwili (yaani Pishoni na Gihoni) havijajulikana bado. Na iyo imewafanya wengine kudhani bustani ya Edeni ilikuwa nchi ya Uturuki ya sasa n.k.
Hivyo, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kudhania kuwa Edeni ilikuwa Iraq, au Uturuki au sehemu nyingine yoyote. Na hiyo ni kwasababu ya mabadiliko makubwa ya nchi yaliyokuwa yanatokea wakati wa gharika na ule wakati wa kugawanyika kwa nchi (Mwanzo 10:25). Historia inaonyesha kuwa dunia ilibadilika mwonekano wake kwa sehemu kubwa sana.
Lakini ni wazi kuwa Edeni haikuwa pengine zaidi ya mashariki ya kati, na sio Afrika kama wanasayansi wanavyoamini, nami naamini ilikuwa katika nchi Kaanani (Yaani Israeli ya sasa).
Lakini ikiwa biblia haikutupa maelezo ya kutosha kuhusu jeografia ya bustani ya Edeni baada ya wazazi wetu wa kwanza kuasi, ni wazi kuwa hakuna umuhimu sana wa kujua bustani hiyo iko wapi kwasasa, kwasababu hayo yalishapita. Bali sasa Mungu ametutilia mkazo hasaa kutufahamisha juu ya Edeni yetu ya mbinguni inayokuja.
Yaani ile Yerusalemu mpya, mji mtakatifu ushukayo kutoka mbinguni kwa Mungu. Na Yerusalemu hiyo itashuka juu ya mbingu mpya na nchi mpya zitakazoumbwa kwa wakati huo baada ya utawala wa miaka elfu moja kuisha. Kama vile tu ilivyokuwa Edeni ilivyoumbwa juu ya dunia ya wakati ule. Kufahamu zaidi juu ya utawala wa miaka 1000 fungua hapa >>> UTAWALA WA MIAKA 1000.
Lakini kisichojulikana na wengi ni kuwa, si kila mtu atakayeruhusiwa kuingia ndani ya mji huo. Bali wale watakatifu tu watakaoshinda ulimwengu huu.
Tujiulize, Je! Mimi wewe tutakuwa miongoni mwa hao watakaouingia huo mji mpya wa dhahabu yaani Yerusalemu ya Mbinguni, Edeni halisi ya Mungu? Je! Mambo ya ulimwengu huu bado yanatusonga, mpaka siku ile itukute ghafla tukaachwa?. Je! Unajua kuwa unyakuo upo karibu sana, na dalili zote za kurudi Kristo duniani zimeshatimia?
Ikiwa wewe bado hujaokoka na leo hii utapenda kumkabidhi Kristo maisha yako ayaokoe na akupe uweza wa kufanyika mtoto wake, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako ambao hautaujutia milele. Hivyo kama upo tayari, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Masheki ni watu wenye hadhi ya juu sana, wenye jina kubwa na heshima katika jamii au taifa,
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi katika biblia;
Ayubu 29:9 “Wakuu wakanyamaa wasinene, Na kuweka mikono yao vinywani mwao;
10 Sauti yao masheki ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao”.
Zaburi 68:31 “Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara”.
Zaburi 83:11 “Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna”.
Zaburi 105:22 “Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima”.
Hata Kristo atakaporudi mara ya pili hapa duniani na kutawala kama BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME, Atakuwa na masheki wake chini yake. Watu ambao atawapa heshima kubwa kuwa makuhani wake na wafalme katika enzi yake yote duniani kote.
Na watu hao watakuwa si wengine zaidi ya watakatifu walioshinda zamani, na watakaoshinda sasa ulimwengu huu mbovu.
Hizi ni baadhi ya ahadi alizowaahidia watakaoshinda.
Ufunuo 2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu”.
Ufunuo 3:12 “Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya”.
Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
Je! Mimi na wewe tupo miongoni mwa watakaoshinda? Kama bado, Je! Upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo? Ikiwa jibu ni ndio basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> SALA YA TOBA
Bwana atutie nguvu.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.
Na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 06930366018
Mada Nyinginezo:
Mhubiri 7:20 “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.
21 Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.
Kitabu cha Mithali na Mhubiri ni vitabu vilivyojaa mafunzo mengi ya maisha ya kawaida, tukiachilia mbali yale ya rohoni. Vitabu hivi vimeandikwa na mtu mmoja ambaye ni Sulemani. Hivyo leo tutaangalia jambo moja la kujifunza kwenye maisha yetu ya kawaida sisi kama wakristo.
Kama tunavyosoma hapo katika mstari wa 21 na 22 inasema “usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa”… Sasa ni jambo la kawaida kwa kadiri tunavyoishi hapa duniani, kupitia katika hali tofauti tofauti, kuna wakati utapitia hali ya kuzungumziwa vibaya, kusengenywa, haijalishi utakuwa ni mwema, au umefanya mazuri kiasi gani, hilo haliepukiki, hata kama wewe ni mtakatifu vipi?.
Sasa biblia inatuambia, tunapokuwa katika mazingira kama hayo, tusitie moyoni kila kitu tunachokisikia, au kwa namna nyingine tuvipuuzie, haijalishi tulichoambiwa kinachoma kiasi gani, hiyo ni kwa faida yetu wenyewe..
Lakini tatizo linakuja kwetu pale ambapo tunakisikia kidogo tu tumezungumziwa vibaya, na sisi hapo hapo tunaanza kutafuta, ni nani huyo kasema, ni nani kamwambia, na kama hiyo haitoshi tunaendelea kutafiti na yule aliyemwambia ni nani kamweleza, na yule aliyeelezwa katolea wapi taarifa hizo, na kwanini wamefanya hivyo, hivyo tunaendelea, mpaka unazalika mlolongo mrefu ambao hauna mwisho.
Sasa ukisoma mstari wa 22 utaona unatupa madhara ya kufanya hivyo na kutuambia ikiwa mtu ataendelea kutafuta tafuta hivyo, kuchunguza chunguza hivyo.., kutafuta mchawi ni nani,.mwisho wa siku atashangaa kusikia mambo ambayo asingetazamia kusikia kutoka kwa watu wake ambao hawategemei kabisa.. Ukisoma hapo anatumia mfano wa “mtumwa”, mtu ambaye ni mjakazi wake anayekuheshimu atasikia anamtukana..
“21 Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana”.
Hivyo kabla hujaanza kuyafikiria mambo ya wanadamu, utakapoona habari fulani inakujia ya kusemwa vibaya, ikwepe, au ipuuzie kabisa kwa usalama wa moyo wako, kisha endelea na shughuli zako za kawaida, Watu wengi (hususani wakristo) wanaohangaika huku na huko kutafuta ni nani aliyewasengenya au Yule anazungumzia nini kuhusu mimi, mwisho wa siku wanakuwa na vinyongo na watu wote, wanakuwa na chuki zisizokuwa na sababu, wanapoteza hata imani na Mungu na kuanza kuishi maisha ya visasi, maisha ya kutokusamehe, na Maisha ya uchungu, hata maombi yao yanakuwa ni ya kuwalenga tu maadui zao, mawazo yao ni kukomoa tu, nipate hiki nimfundishe yule adabu n.k. kisa tu alimsikia Fulani akimcheka.. Na pia kamwe hawawezi kuwa na maombi ya unyenyekevu mbele za Mungu, bali ya kunung’unika tu na kulalamika.
Na kumbe hajui yule mtu aliyemsengenya pengine hata hakuwa na chuki na yeye kwa kiwango hicho anachokifikiri yeye, alizungumza tu kama mwanadamu ambaye hawezi kuuzuia ulimi wake, na pengine alishatubu na akawa anamuombea, lakini yeye kwa kuwa alishasikia fulani alimzungumzia vibaya, hilo jambo ataendelea nalo moyoni mwake kwa miaka na miaka..Atasema kwanza yule nilishawahi kumsikia akinisema hivi au vile.
Hivyo kabla hatujamkasirikia fulani kwasababu ya kutuzungumzia vibaya, tunapaswa tujiulize je na sisi hapo nyuma hatujawahi kumsengenya mtu yeyote katika maisha yetu?. Kwasababu Ule mstari wa 22 unasema;
“21 Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.
Unaona? Imetumia neno “mara nyingi”. Pengine hata wewe ulishawahi kuzungumza maneno ambayo usingeweza kuyasema mbele ya huyo jirani yako, Lakini akija mbele yako humwekei vinyongo.
Hivyo na sisi pia tunapaswa tuachilie, tusiwe wapelelezi sana kwa yale tunayoyasikia kuhusu sisi, ukisikia mtu anakuambia fulani kakuzunguzia hivi au vile, usitake kujua zaidi ya hapo.. Kwasababu utajikuta una chuki na kila mtu, pengine hata mke wako, au dada yako, au mwanao, kwa sababu hiyo tu ya udadisi.
Tunapaswa tufahamu tu, kuzungumziwa vibaya au kusengenywa ni sehemu ya maisha yetu maadamu tupo hapa duniani. Hivyo hakuna haja ya kufuatilia fuatilia. Hiyo kazi tumwachie shetani, Sisi tutafute mambo msingi ya imani yetu. Na kamwe hutapata mtu mkamilifu asilimia mia moja hapa duniani, kama unayemtaka wewe, tukilielewa hilo tutaishi Maisha ya upendo na furaha sana.
Bwana atusaidie katika hilo kwenye safari yetu ya wokovu.
Je! Umeokoka? Je! Unajua kuwa hizi ni nyakati za mwisho? Na kwamba hatutakuwa na muda mrefu sana Unyakuo utapita, na mwisho wa dunia utafika? umejiandaaje? Je! Bado upo vuguvugu? Ikiwa hujamkabidhi Yesu maisha yako ni heri ufanye hivyo sasa. Na wokovu unakuja kwa kutubu dhambi zako na kwa kubatizwa ipasavyo hivyo, zingatia hayo na uyakamilishe. Kwani hizi ni dakika za majeruhi. Bwana yupo mlangoni kurudi.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Kicho ni hali ya hofu. Kwamfano pale biblia inaposema kicho cha Bwana, inamaanisha hofu ya Bwana.
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja neno hilo katika biblia;
Matendo 9:31 “Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu”.
Waefeso 5:20 “na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo”.
Waebrania 12:28 “Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho”;
Kumbukumbu 7:21 “Usiingiwe na kicho kwa sababu yao; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu katikati yako, Mungu mkuu, mwenye utisho”.
Kumbukumbu 28:67, 2Samweli 23:3, Ayubu 15:4
Hivyo nasi pia tunapaswa tuwe na kicho cha Mungu ndani yetu, hicho ndicho kitakachotufanya tuishi maisha yampendazayo yeye hapa duniani, tukikosa hofu ya Mungu, hatutaona hata shida kuua, au kuiba, au kuzini, kwasababu hatumwogopi Mungu. Lakini ikiwa kicho chake kinakaa ndani yetu,tutaogopa kufanya mambo yasiyompendeza kwasababu tunajua Mungu wetu ni mkuu sana, anaweza kutenda lolote juu ya maisha yetu.
Yeremia 5:22 “Je! Hamniogopi mimi? Asema Bwana; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
23 Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao.
24 Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche Bwana, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa”.
Bwana atusaidie kicho chake kiumbike ndani yetu.
Shalom.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Angalia maana ya maneno mengine ya biblia chini.
Na ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618
Mada Nyinginezo: