Bwana YESU asifiwe sana, karibu tujifunze Neno la Mungu.
Awali ya yote ni vizuri tukaweka msingi kwanza wa kufahamu nini maana ya Sabato.
Sabato maana yake ni pumziko/kuacha kufanya kazi/ kustarehe/kuingia rahani mwako. Mungu alifanya kazi yake ya kuumba kwa muda wa siku sita mfululuzo kama tunavyosoma katika kitabu cha Mwanzo, na ilipofika siku ya saba kazi yote ilikuwa imeshamalizika, ndipo akastarehe/ akapumzika, hivyo akaibariki siku hiyo na kuifanya kuwa kama kumbukumbu la pumziko lake, na baadaye akawaagiza wana wa Israeli walipokuwa kule jangwani kwamba kila itakapofika siku hiyo waifanye kuwa ni sabato yao.
Lakini Sabato haikuwa ile siku yenyewe ya saba, bali sabato ilikuwa ni lile pumziko lenyewe, Lakini “SABA” yenyewe inawakilisha pumziko la Mungu, kwasababu katika saba ndipo Mungu aliingia katika pumziko lake. Na ndio maana ukisoma kwenye biblia, Mungu hakuiwekea sabato yake mipaka kwamba iwe tu ni katika siku ya saba ,hapana.. Bali utaona alikwenda mpaka kwenye mwaka wa Saba, ilikuwa kila mwaka wa saba, hakuna kupanda, wala kwenda kufanya kazi yoyote mashambani, bali waipumzishe ardhi, watulie majumbani kwao. Utalisoma hilo katika..
Walawi 25:1 “Kisha Bwana akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia,
2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana.
3 Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake;
4 lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
Unaona, haikuishia hapo tu kwenye mwaka wa 7, bali pia miaka hiyo miaka 7, ikipita mara saba tena, kuna sabato nyingine itakayokwepo katika mwaka unaofuata..yaani 7×7 =49, ikiwa na maana, mwaka wa 50 ni sabato ya pumziko na maachilio, inayojulikana kama YUBILEE.
Walawi 25:11 “Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.
13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake”.
Haiishii hapo tu, tutakuja kuona mbele kidogo, sabato nyingine ambayo Mungu ameificha katika maandiko, ambapo ipo katika miaka 1000 kwa ajili ya wateule wake.
Sasa ikiwa tumeshafahamu, sabato ni PUMZIKO, na sio siku fulani, au mwezi fulani, au mwaka fulani, tutafahamu sasa kuwa hata wana wa Israeli kutolewa Misri na kupelekwa Nchi ya Kaanani, ni kwamba walikuwa wanaingizwa katika Sabato yao, (yaani rahani mwao,) ambayo Mungu alikuwa amewaandalia.
Lakini biblia inatuonyesha kuwa sio wote waliweza kuingia katika hiyo raha ya sabato yao, kutokana na kutokuamini kwao na matendo yao kuwa maovu. Si wote waliweza kuingia katika nchi ibubujikayo maziwa na asali isipokuwa wale wawili tu lakini wengine wote waliosalia Mungu aliwaua kule jangwani.
Waebrania 3:8 “Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
11 KAMA NILIVYOAPA KWA HASIRA YANGU, HAWATAINGIA RAHANI MWANGU.
12 Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
15 hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha.
16 Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?
17 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
18 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale”.
Unaona? Wengi wao walishindwa kuingizwa katika pumziko lao, kutokana na kuasi kwao.. Lakini sasa bado biblia inatuambia, sabato yao ilikuwa ni kivuli tu sabato halisi inayokuja huko mbeleni ambayo Mungu aliwaandalia watu wake, waaminifu. Mtume Paulo alisema kama ingekuwa Yoshua amewapa raha yenyewe, basi Daudi asingeandika tena mahali fulani huko mbeleni juu ya watu wa Mungu kuingia rahani mwa Mungu.
Waebrania 4:7 “aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu.
8 Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.
9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu”.
Umeona? Sisi kama watakatifu tunaomngojea Bwana bado hatujaingia kwenye raha yetu, au sabato yetu, ambayo Mungu alituandalia tangu zamani.. Sasa kumbuka Mungu huwa anapenda kutumia namba SABA, hasaa kuwakilisha sabato yake, kwa kustarehe kwake siku hiyo.
Na biblia inatuambia kwa Mungu miaka elfu moja ni sawa na siku moja. (2Petro 3:8). Sasa kama ulikuwa hujui ni kwamba tangu wanadamu tuumbwe, hadi sasa imeshapita miaka 6000, aidha inaongezeka kidogo sana, au inapungua kidogo sana. Lakini tupo katika mduara huo huo wa miaka elfu 6. Yaani Tangu Adamu mpaka Nuhu, inakadiriwa ni miaka elfu 2 ilipita, na tangu Nuhu Mpaka kuzaliwa kwa Yesu vilevile inakadiriwa ni miaka elfu 2 ilipita, na tangu kuzaliwa kwa Yesu hadi sasa tunajua ni miaka elfu 2 tupo, kwahiyo jumla ni miaka elfu sita.
Na kama tunavyofahamu kwa Mungu miaka elfu ni sawa na siku moja, kwahiyo mpaka sasa ni kama siku 6 tu kwa Mungu zimepita, na siku ya saba ni sabato yake. Hivyo miaka elfu moja ijayo itakuwa ni sabato ya Mungu kwa watu wake.
Hapo ndipo lile Neno la UTAWALA WA MIAKA ELFU MOJA linakuja kutimia, ambalo Kristo atatawala na watakatifu wake hapa duniani, dunia ikiwa katika hali ya amani na furaha tele.. Kwa maelezo marefu juu ya utawala huu wa amani, tutumie ujumbe inbox tukupe somo lake.
Wakati huo dunia hii itakuwa kama paradiso, kwasababu hakutakuwa na shida wala taabu, wala mateso, tutamfurahia Mungu wetu kwa Muda mrefu sana wa miaka elfu moja, wakati huo sio wa kukosa ndugu yangu..lakini inasikitisha kuona kuwa wengi wetu hatutaingia katika raha hiyo kwa mfano tu wa kuasi kwa wana wa Israeli kule jangwani..
Hizi ni nyakati za za kumalizia hakutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili, yaani sisi ndio tutakaoshuhudia tendo zima la UNYAKUO, Jiulize wewe utakuwa wapi wakati huo utakapofika ndugu yangu, Na ndio maana mtume Paulo ametuonya na kutuambia..
Waebrania 3:12 “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi”.
Waebrania 4:11 “Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi”.
Huu sio wakati wa kutanga tanga na huu ulimwengu, Huu ni wakati wa kuelekeza macho yetu mbinguni, tuhakikishe kuwa hata tukifa tutakuwa katika ufufuo wa kwanza, na unyakuo ukipita basi tunaenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni, ambapo tutakula ile karamu ya mwana kondoo kisha tutarudi kutawala na Bwana hapa duniani.
Je! Umeokoka? Kama bado unasubiri nini? Tubu dhambi zako mfuate Yesu, akupe uzima wa milele.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Tafakari sana kabla hujafikia hitimisho Fulani ambalo ndio litakuwa la kudumu katika maisha yako.
Kuna watu wengi sana ambao shetani kawafumba macho, na kuwafanya wasifikiri vyema kabla ya kufikia hitimisho la maisha yao.
Kwamfano kuna watu wanatazama mwenendo wa watumishi wa uongo, au waliorudi nyuma, na kuhitimisha kwamba kamwe hawataokoka..kisa tu wameona hao watumishi wakifanya mambo ya ajabu yasiyopatana na wokovu kabisa.. Mtu wa namna hii tayari kafikia hitimisho la maisha yake bila kutenga muda wa kutafakari/ kufikiri sana.
Ndugu ni kweli umezunguka kila mahali hujaona mchungaji mkamilifu kama ulivyotaka wala ulivyotegemea…Lakini hiyo isikupe nafasi ya kusema hutamtafuta Mungu kamwe wala hutaokoka..Kwasababu ni kweli hujaona mchungaji mkamilifu lakini yupo aliye mkamilifu ambaye hakutenda dhambi kabisa hata moja, yaani YESU KRISTO, habari zake zimeelezwa kwa urefu katika maandiko, Umekataa kumsikiliza mchungaji wako kwasababu umeshuhudiwa kafumaniwa katika uzinzi, umekataa kumsikiliza muhubiri fulani maarufu kwasababu kakengeuka kawa kama watu wa kidunia n.k.. Lakini yupo mmoja aliye mkamilifu YESU KRISTO, mfuate huyo hao wengine waache.. Unafikiri utajitetea vipi siku ile ya hukumu?.
Utasema Bwana mimi nilikata tamaa ya kuendelea na wokovu kwasababu mchungaji wangu alinitaka kimapenzi, hakuwa mkamilifu,..ni kweli mchungaji wako anayo dhambi lakini alikuwepo YESU AMBAYE BADO NI MWAMINIFU, hana dhambi, mchungaji mkuu.. ungemfuata huyo Yesu, umwache mchungaji wako..Lakini wewe umewatapika wote…Utajitetea vipi siku ile???… kama vigezo vya utakatifu Bwana Yesu kavikidhi vyote, hana kosa wala hatia…Tafakari sana kabla ya kufanya maamuzi, usitafakari juu juu tu.
Bwana Yesu alisema maneno haya..
Yohana 8.46 “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?”
Mchungaji wako anayekuchunga anayo dhambi, pengine umemshuhudia akisema uongo, umemshuhudia akizini, lakini ni wapi Yesu umemshuhudia akisema uongo, ni wapi umemshuhudia akizini? …lakini wewe umemkataa Yesu aliye mkamilifu sawasawa na Mchungaji wako,..ni nani sasa utakayemkubali mwenye vigezo unavyovitaka wewe??…..Ndio maana anauliza swali hilo hapo juu “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?” … Yesu hana dhambi hata moja unamkataa…utamkubali nani kwamfano ukiulizwa hilo swali?….siku ile utajitetea vipi mbele ya Bwana?.
Utasema mimi ni kijana, siwezi kuishi maisha bila kufanya uasherati, kwasababu naishi mazingira ya vishawishi vingi…. Siku ile ataletwa kijana aliye mzuri kimwonekano kuliko wewe na aliyeishi katikati ya mazingira magumu kuliko wewe, lakini aliweza kuushinda uasherati kwa kishindo kikubwa…Hapo utazungumza nini cha kujitetea??.
Unajua ni kwanini biblia inasema watakatifu watauhukumu ulimwengu??
Ni kwa njia hiyo ya wanavyoishi…kama kuna dada ambaye mnaishi naye mtaani anavaa vizuri katikati ya dunia hii ya wanawake walioharibika akili, siku ya hukumu atawahukumu wanawake wote waliokuwa wanavaa vibaya…na atawahukumu si kwa maneno, bali maisha yake ndio yatawahukumu hao wengine…wakati hao wengine wanasema Bwana ilikuwa haiwezekani kila duka lilikuwa linauzwa nguo fupi, yeye atasimamishwa na kuulizwa alizipata wapi hizo ndefu..na hivyo maisha yake kuwa hukumu kwa wengine, (hiyo ndio maana ya watakatifu watauhukumu ulimwengu 1Wakorintho 6:2)
Kwahiyo usifikiri kwa vyovyote vile siku ile kuna kushinda hoja mbele ya kiti cha hukumu.. hakutakuwa na hoja yoyote ya kushinda, ndio maana leo hii..tunapata nafasi hii ya kukumbushwa kutafakari kwa makini kabla ya kufanya maamuzi.
Leo hii umeuacha wokovu kwasababu ya mchungaji wako, Rudi mgeukie Yesu Mchungaji mkuu asiye na dhambi, leo hii maneno ya muumini mwenzako yamekufanya usiupende wokovu au ukristo, ni wakati wa kumtazama Kristo na si mwanadamu.. Leo hii umevunjwa moyo na wakristo wenzako, au kiongozi wako katika imani, hata ikakufanya ukate tama kabisa ya kuendelea na wokovu…Ni wakati wa kuyaweka hayo mawazo pembeni kwasababu, shetani anataka ufikiri hivyo hivyo mpaka siku ya hukumu, ili ukose cha kujitetea siku ile.
Na kama hujampokea Yesu kwasababu nyingine yeyote, huu ni wakati wa kufanya hivyo, tunaishi siku za hatari sana, na adui yetu shetani ana wakati mchache sana, amewekeza nguvu nyingi katika kuwafanya watu wasione mbele, badala yake wawe bize kutafuta mambo ya kidunia na kuwa na vijisababu vidogo vidogo vya kuhalalisha huo usingizi wa kiroho..Hiyo amka leo. Kristo anarudi, parapanda inakaribia kulia, na mwisho wa dunia kufika.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Jina kuu la Bwana wetu Yesu libarikiwe.
Ni siku nyingine tena Bwana ametupa pumzi yake kuiona, leo tutajifunza somo linalohusiana na utakaso kwa mtakatifu. Lakini kabla hatujafika kwenye utakaso, ni vizuri tufahamu kwanza mtakatifu ni mtu wa namna gani kibiblia..
Wengi tunafahamu labda mtu mpaka aitwe mtakatifu ni lazima awe ameshakaa kwenye wokovu miaka mingi,, lakini kibiblia sio hivyo. Bali pale mtu anapoamua kuokoka, pale anapoamua kuacha maisha yake ya dhambi, na kumgeukia Bwana Yesu, na kusafishwa na damu yake, na kubatizwa, wakati huo huo anakuwa tayari kashafanyika kuwa mtakatifu, haijalishi mambo mengine yatakuwa hayajaondoka vizuri ndani yake,..Kile kitendo tu cha kumpokea Yesu maishani mwake, mtu huyo mbinguni ni mtakatifu kwasababu hana deni la dhambi, anakuwa sawasawa tu na mkristo mwingine aliyekaa katika wokovu kwa miaka 50.
Lakini tatizo linakuja ni pale ambapo mtu huyo anadhani akishampokea Yesu, ndio basi inatosha, Nataka nikuambie hilo halipo katika safari ya ukristo. Utarudi nyuma tu siku sio nyingi, na utakatifu wako utakufa na utakuwa kama vile mtu ambaye hajaokolewa.
Fahamu baada ya kuwa mtakatifu, hatua inayofuata kwako ni lazima iwe Kujitakasa.. Ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..
Ufunuo 22:11 “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA”.
Unaona inasema mtakatifu azidi kutakaswa, ikiwa na maana ukiwa mtakatifu hupaswi kubakia pale pale sikuzote, ni jukumu lako kujitakasa siku baada ya siku. MTAKATIFU ni kama BETRI ya simu. Pale inaponunuliwa ndani yake huwa imeshaumbiwa nguvu ya kutosha ya kuifanya simu iwake kwa muda wa miaka mingi sana hata 10 na zaidi. Lakini Betri hiyo haitegemei tu ile nguvu iliyowekwa ndani yake kuipa uhai simu siku zote, hapana, bali inatarajia pia iwe inachajiwa mara kwa mara, hata kila siku, ili kuzisisimua nguvu zilizoko ndani yake iendelee kuifanya simu iwake kwa muda wote huo.
Lakini kama isipochajiwa, ni wazi kuwa hautaweza kuwasha simu, na matokeo yake ni kuwa itakuwa kama jiwe tu lisilokuwa na maana yoyote, haijalishi kuwa ndani yake kuna nguvu nyingi kiasi gani.Vivyo hivyo na utakatifu nao.. utakatifu bila utakaso Umekufa.
Unapookoka leo hii, unapoamua kumpa Yesu maisha yako, hiyo peke yake haitoshi zipo hatua za kuanza kupiga, ili kuufanya ule utakatifu kuwa hai ndani yako siku baada ya siku. Yapo maisha unapaswa uanze kujizosha kuishi ili Mungu aweze kukutakasa (kukutia nguvu ) ya kuendelea kuishi maisha ya utakatifu siku baada ya siku .
Warumi 6:22 “Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, MNAYO FAIDA YENU, NDIYO KUTAKASWA, na mwisho wake ni uzima wa milele”.
SASA MTU ANAJITAKASAJE?
Kwanza ni kwa kukujifunza Neno la Mungu kwa bidii: Unapookoka, ni jukumu lako kusoma Neno na kusikiliza Neno, hususani mafundisho yanayolenga utakatifu. hiyo itakusaidia kujua biblia inasema nini katika kila jambo unalotaka kulifanya. Hivyo kuwa rahisi kujiepusha na mambo ambayo hayampendezi Mungu.
1Petro 1:22 “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo”.
Pili ni kwa kuwa mwombaji na kufunga: Maombi ni nguzo nyingine inayomtia mtu nguvu ya kuendelea kudumu katika utakatifu Mungu anaouhitaji ndani ya mtu. Usipokuwa mwombaji huwezi kudumu katika wokovu, huwezi kuyashinda majaribu kwa namna yoyote ile. Vilevile na katika kufunga, kunakusaidia kufikiria zaidi mambo ya rohoni kuliko ya mwilini na matokeo yake kuzishinda tama zake.
Tatu ni kwa kujizoeza kuishi maisha yampendezayo Mungu: Kujizoesha ni jambo lingine la msingi sana, kwamfano mtu aliyejizoesha kuamka alfajiri sana, huwa inafikia wakati kuamka kwake asubuhi kunakuwa ni kwepesi sana tofauti na Yule ambaye hajajizoesha kuamka mapema.. Vivyo hivyo na katika Utakatifu, tukijizoesha kuishi maisha ya haki, baadaye yanakuja kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku yenyewe bila hata kutumia bidii nyingi.
1Timotheo 4:8 “Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”.
Nne, Ni kwa kuifanya kazi ya Mungu: Kuitenda kazi ya Mungu ikiwemo kuwahubiria wengine ni chaji nzuri sana ya utakatifu. Kwasababu inakufanya ukae katika uwepo wa ki-Mungu muda mrefu, kwasababu unamlazimisha Roho Mtakatifu aje kufanya kazi na wewe, na sikuzote alipo Roho Mtakatifu, lazima uwepo utakatifu.
Hivyo kwa kuhitimisha, ni jukumu la kila mmoja wetu KUJITAKASA kila siku, ili aendelee kudumu, hakunaga Utakatifu wa kusema mimi nimeokoka, halafu huonyeshi bidii yoyote, hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe, utasema tu kwa mdomo lakini kwa matendo utakuwa mbali nao. Ni lazima tujichaji (tujitakase) ili tuweze kudumu kwenye huo utakatifu. Siku hizi za mwisho Bwana Yesu alitusisitiza sana kufanya hivyo, kwasababu maovu yameongezeka, na yeye yupo mlangoni kurudi.
2Petro 1:8 “Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, AMESAHAU KULE KUTAKASWA DHAMBI ZAKE ZA ZAMANI.
Mimi na wewe tusisahau utakaso wa kila siku.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
SWALI: Naomba kufahamu maana ya mstari huu ; Mithali 16:1 “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”.
JIBU: Mstari huu unatukumbusha kuwa si kila jambo tunalolipanga katika maisha tunaweza kulitolea maamuzi yake asilimia mia. Ni kweli Mungu anaturuhusu tupange mipango yetu mingi kwa jinsi tupendavyo, lakini tunapaswa tukumbuke pia sio kila mpango tulioupanga ni lazima uje kama tulivyotarajia.
Kwamfano utaona Balaamu alipomwendea Mungu ili kuwalaani Israeli, jibu la Mungu lilikuwa ni kuwabariki badala ya kuwalaani. (Hesabu 22-24). Utaona alikwenda kweli na mipango yake kwa Mungu ili kumridhisha Balaki, akidhani utakuwa ni vema pia kwa Mungu, lakini badala yake aliambiwa aibariki Israeli badala ya kuilaani.
“Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”
Hivyo tunapopanga mipango yetu, tunapaswa tujinyenyekeze kwa kusema Bwana akipenda kama biblia inavyotuasa hapa,
Yakobo 4:13 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;
14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.
15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya”.
Unaweza kweli ukawa umepanga uje kuwa daktari ukubwani, lakini mipango yako au ndoto zako ghafla zimevuruguka kuona kwamba unalazimika kwenda kusomea kitu ambacho hujakipenda, sasa unapokuwa katika hali kama hiyo na wewe ni mkristo kumbuka huu mstari.. “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”
Unaweza ukawa umepanga, ufanikishe jambo fulani, mwaka uliopita lakini haujafanikisha kutoka na vikwazo fulani, pengine ukaanza kulaumu kwanini haikuwezekana, sasa ukijikuta katika hali kama hiyo na wewe ni mkristo ambaye unaouhakika umeokolewa na Kristo, hupaswi kuwa na huzuni, ujue ipo mipango mingine mzuri zaidi ambayo Mungu kaiweka mbele yako, pengine unaweza usiione sasa hivi, lakini baadaye ukaiona na kumshukuru Mungu, na kusema asante Mungu kwa kunipitisha njia hii leo.
Hivyo kila jambo ulifanyalo, usilipe asilimia mia kwamba ni lazima liwe kama ulivyolipanga, kumbuka wewe sio Mungu, anayejua kesho kwa asilimia yote ni Mungu peke yake..Kwahiyo wewe amka asubuhi, panga mipango yako, kisha mshirikishe Mungu na umalizie na Neno IKIWA ITAKUPENDEZA MUNGU..
Ikiwa imempendeza basi litafanikiwa kama ulivyopanga lakini ikiwa halikumpendeza basi atakuandalia njia nyingine iliyo bora zaidi.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
JIBU: Tusome mstari wenyewe.
Mhubiri 1:15 “Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki”.
Hapo utaona vipengele viwili, cha kwanza ni: Yaliyopotoka hayawzi kunyoshwa. Na cha pili ni yasiyokuwapo hayahesabiki.
Tukianza na hicho cha kwanza cha Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,..Tukumbuke kuwa kitabu cha Mhubiri ni kitabu kinachoeleza juhudi za mwanadamu za kutafuta suluhu ya mambo yote yaliyopo duniani kwa nguvu zake mwenyewe pasipo kumuhusisha Mungu. Na ndio maana utaona mhubiri ambaye ndiye aliyejibidisha katika kufanya hivyo, mwisho wa siku anaishia kusema ni UBATILI Mtupu, mambo yote na hekima yote ya mwanadamu ni ubatili tu, ni sawa na kuufuata upepo ambao mwanzoni unaweza kukupa matumaini kuwa utakufikisha mahali, lakini mwishowe unapotea tu ghafla njiani, hujui ulipoelekea umekuacha tu hewani. Ndivyo alivyo mwanadamu anayehangaika kukimbizana na ulimwengu huu.
Sasa aliposema “Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa” Ni kuwa aliona, kuna mambo ambayo yalikatazwa na Mungu, au kwa namna nyingine tuseme hayapo katika uhalisia wake, na pengine anaweza kuyaweka sawa na kuyafanya yaonekane yanafaa katika jamii, Umeona? Ndipo kwa hekima yake akajaribu kufanya hivyo aone kama yatakuwa kweli ni sawasawa, lakini mwisho wa siku akagundua hata ufanyaje kile kilichokataliwa na Mungu (yaani kupotoshwa) hakiwezi kufanywa kiwe sawasawa. Ni kujitafutia tu matatizo na shida zisizokuwa na sababu.
Mbeleni kidogo utaona anasema..
Mhubiri 7:13 “Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
Ni kama leo tu, watu wanatafuta namna ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja..wanajaribu kufanya kila mbinu, ionekane kuwa ile ni ndoa iliyokubaliwa na Mungu, lakini bado haiwezi kuwa ndoa, na hilo wanalijua, wengine mpaka wanajibadilisha jinsia waonekane kama wanaume, au wanawake, lakini bado zile jinsia zao zinaendelea kubakia nao ndani yao.. Na matokeo yake wanaishia kupata matatizo mabaya ya kiafanya na kuishia kufa.
Ndivyo walivyo hata na mashoga, wanapojaribu kuwa kama wanawake, maumbile yao yanaharibika wanashindwa kukaa hata katika jamii na watu wengine wakihofia aibu. Kwasababu yaliyopotoshwa hayawezi kunyoshwa, Unaona? Si hilo tu Wapo wengine wanajichubua ngozi zao ili wabadili rangi ya miili yao wawe weupe, sote tunajua mwisho wao watu wa namna hiyo ni nini, ni kuishia kupata kansa ya ngozi na kufa.
Inastaajabisha leo hii, kuona wanawake nao wanasema suruali ni mavazi ya jinsia zote. Haijalishi wataihalalisha vipi wataitengeneza kwa muundo gani unaoonekana wa kike, lakini bado vazi la suruali litabakia kuwa vazi la kiume tu, wewe unayejaribu kukinyosha kitu ambacho Mungu kakipotosha kwako unajitafutia matatizo na hukumu.
Unaweka mawigi, kucha za bandia, ili uonekane wa tofauti na Yule wa kwanza ambaye Mungu alikuumba..Embu Itafakari vema kazi ya Mungu, na uache kukinyosha kile ambacho Mungu kakipotosha. Hiyo ndio maana ya kifungu hicho.
> Sasa tukirudi kwenye kile kipengele cha pili ambacho kinasema “Wala yasiyokuwapo hayahesabiki”.
Hii dunia imejawa na mambo mengi ya Mungu, ambayo bado mwanadamu anazidi kuyavumbua kila siku, lakini mpaka sasa takwimu zinaonyesha, bado asilimia 86 ya viumbe havijajulikana duniani, japokuwa ameishi duniani kwa muda mrefu sasa
Mambo yasiyojulikana ni mengi kuliko yanayojulikana, wanasayansi wanalijua hilo, kila siku wanavumbua mambo mapya, wanashangaa kumbe na hili lipo na lile lipo..Hiyo inawafanya wawe buzy usiku na mchana kutafuta na kutafiti tu, siku zinakuja siku zinakwenda, wanaendelea tu hivyo hivyo, wanasahau mpaka na mambo ya msingi ya roho zao.. Wanadhani katika kuvumbua huko ndio siku moja watapata jawabu la maisha ya mwanadamu hapa duniani.
Mhubiri anasema hayo yote ameshayafanya, lakini amegundua ni ubatili mtupu, kwamba yasiyokuwepo hayahesabiki, hata kama nitakuwa buzy miaka yangu yote kutafiti, kamwe sitavumbua yote. Ni sawa na kuufuata upepo. Huoni leo hii wanadamu walivyo buzy na mambo ya duniani wanasahau mambo ya mbinguni ambayo ni ya kudumu milele? Kiasi kwamba huwezi kuwaeleza chochote, nje ya sayansi wanayojitumainisha nayo.
Lakini Mhubiri mwishoni anatoa jumla ya mambo yote, anasema, linalompasa mwanadamu kufanya ni KUMCHA MUNGU, NA KUZISHIKA AMRI ZAKE (Mhubiri 12:13) basi. Na wewe pia hakuna mahali popote utakapoweza kupata jawabu la maisha isipokuwa kwa Kristo tu peke yake. Hii dunia itakutesa sana, lakini Ukimpa leo maisha yako,ayaongoze, ukaanza naye upya ameahidi kukupa pumziko la roho, hiyo ni ahadi yake.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Hivyo kama upo tayari leo kutubu na kuanza naye upya, basi fungua hapa kwa maelekezo ya sala ya Toba..>>. SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Kuhuluku ni Neno lingine linalomaanisha KUUMBA.
Kwamfano tukisema Mungu kahuluku jua na mwezi, tunamaanisha kuwa Mungu ameumba jua na mwezi.
Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo vinalielezea Neno hilo;
Isaya 43:1 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu”.
Isaya 45: 12 “Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru”.
Isaya 45: 7 “Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na KUHULUKU UBAYA; Mimi ni Bwana, niyatendaye hayo yote”.
Katika huu mstari wa mwisho utaona anasema sio tu ameumba vitu vya asili na wanadamu au mambo mema tu peke yake, hapana, bali anasema yeye pia ni Mungu anayehuluku UBAYA, Yaani anaumba ubaya. Jambo ambalo wengi hatulijui.
Ndio Mungu anaumba ubaya ndugu yangu,. Alipoleta gharika ule ulikuwa ni ubaya, lengo lilikuwa ni kuwagharikisha watu wote waovu waliokuwa duniani wakati ule. Embu Soma maneno haya anavyosema;
Ayubu 38:22 “Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe,
23 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita”?
Unaona?
> Aliposhusha pia ule moto na kibiriti, wakati wa Sodoma na Gomora ule ni uovu aliouumba yeye mwenyewe mahususi kwa ajili ya watenda dhambi.
> Alipoleta tena Tauni mara kadha wa kadha kwa taifa la Israeli pale walipomwasi na kumkasirisha kule jangwani na sehemu nyinginezo, ule ulikuwa ni ubaya aliohuluku, kwa watu waasi.
> Vilevile alivyoleta CORONA ulimwengu ni Ubaya uliotoka kwake yeye mwenyewe kutuadhibu sisi wanadamu tunaoishi duniani leo hii kwa matendo yetu maovu. Hakuna mwanasayansi yoyote aliyeuunda ugonjwa huo, Huo ni ugonjwa uliotoka kwa Mungu mwenyewe kama pigo.
> Lakini hayo yote ni mwanzo tu ubaya wenyewe ambao Mungu alishaundaa tangu zamani kwa watenda dhambi wote ikiwemo ibilisi pamoja na mapepo yake yote. Na ubaya wenyewe ndio lile ZIWA LA MOTO.
Hivyo Mungu ni wa kumuogopa sana.. Ni kweli yeye ni Mungu wa rehemu na neema nyingi, kwa wale wamtiio, lakini pia ni wa ghadhabu na hasira nyingi, kwa waovu wote. Na ndio maana leo hii anakupa Muda wa kutosha wa kutubu ili umgeukie yeye akusemehe dhambi zako. Usifurahie unatenda dhambi halafu hakuna chochote kinachokutokea, usifurahie unaua, unafanya ushirikina, unazini, lakini Mungu hakufanyi chochote ukadhani utaendelea kuwa hivyo milele. Upo ubaya mbele yako. Na ni jukumu lako kufahamu hilo ili siku ile usije ukasema sikuambiwa.
Hivyo tubu dhambi zako umgeukie Mungu, akuoshe, ili ushiriki wema wa Mungu na sio ubaya wake.
Kama upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya SALA YA TOBA, na Maelekezo mengine >> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Pia Tazama tafsiri ya maneno mengine ya kibiblia chini.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?
Kiango ni kifaa maalumu cha kushikilia au kuning’inzia taa, tazama picha, kwa jina lingine kinaitwa kinara. Na nilazima kinyanyuke au kiwe sehemu ya juu kidogo, ili kuruhusu mwanga wa hicho kilicho juu yake (yaani taa) kuangaza mahali pote.
Na Pishi ni bakuli dogo, au kapu ndogo. Tazama picha,
Hivi ni vifungu ambavyo utaweza kukutana na maneno hayo;
Mathayo 5:15 “Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani”.
Marko 4:21 “Akawaambia, Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au mvunguni? Si kuwekwa juu ya kiango”?
Luka 11:33 “Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga”.
Soma pia Luka 8:16
Hivyo mpaka hapo tunaweza kupata picha sasa Bwana Yesu alimaanisha nini kutoa mfano huo, kuwa tunapoamua kuokoka hatupaswi kuuficha wokovu wetu, kuuweka chini ya bakuli bali ni sharti tuungaze kwa watu wote, kwanza kwa matendo yetu na pia kwa kuwahubiria ili kusudi kwamba wavutwe na wao katika wokovu tulionao.
Na ndio maana pale kwenye Mathayo 5:15 akamalizia na kusema..
16 “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Shalom.
Tazama maana nyingine ya maneno ya biblia chini.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Bwana Yesu alimaanisha nini aliposema; Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao?
Shalom, jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe milele.
Karibu tujifunze Neno lake.
Ukisoma kitabu cha Ufunuo sura ya 12, utaona habari kuu inayouzungumziwa pale ni kuhusu mapambano ambayo aliyafanya tangu akiwa mbinguni, na anayoendelea kufanya hadi sasa.
Utaona mapambano hayo yamegawanyika katika vipengele vikuu vitatu. Cha kwanza vita ile aliyoifanya mbinguni akiwa na malaika zake, ambayo alishindwa, na matokeo yake akatupwa chini,
Kipengele cha pili utaona ni ile vita aliyoifanya na yule mwanamke aliyemzaa mtoto mwanaume, ambaye nchi ilimsaidia. Na mwanamke yule analiwakilisha Kanisa la Israeli kwa ujumla. Wakati Bwana Yesu anazaliwa, utaona shetani kwa kupitia Herode alikuwa ameshaanza kuleta maafa Israeli, kwa kuwaaua wale watoto wote waliozaliwa wakati mmoja na Yesu, lengo likiwa ni kumwinda Yesu, afe, Lakini Mungu akamuhamisha Kristo akilimbilie Misri kwa muda, na hiyo ilikuwa ni kulinusuru taifa zima.
Na kipengele cha tatu na cha mwisho ambayo ndio kiini cha somo letu la leo Ni vita ambayo shetani aliita kwa uzao wake wote wa huyo mwanamke uliosalia. Yaani wote watakaofanana na Kristo, waisraeli wa rohoni, hao ndio anamalizia kufanya nao vita , na vita hiyo ni endelevu, ilianza tangu kipindi kile Kristo anaondoka duniani, mpaka leo hii, na itaisha na unyakuo.
Lakini kuna jambo moja la kuona pale, shetani alipoanza kufanya vita na kanisa la Kristo, hakusimama mbinguni tena au nyuma yetu kuleta mafuriko, kama alivyofanya kwa yule mwanamke, hapana, bali biblia inatuambia alikwenda kusimama JUU YA MCHANGA WA BAHARI.
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake AFANYE VITA JUU YA WAZAO WAKE WALIOSALIA, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI”.
Sasa mchanga wa bahari unawakilisha nini?
Hapo inaposema kwenye mchanga wa habari inamaanisha kwenye ufukwe, yaani alikwenda kusimama ufukweni, mpakani, kati ya habari na nchi kavu. Hii ikiwa na maana vita vyake hasa vipo pale mpakani, kuhakikisha kinachotoka habarini hakiji nchi kavu. Na hata kama kikitokea kimevuka nchi kavu, basi hakitapita hivi hivi tu.
Sasa kibiblia habari au palipo na maji mengi inawakilisha ulimwengu,(Ufunuo 17:15) ..Na nchi kavu ni wokovuni..Bwana Yesu alimwambia Petro njo nami nitakufanya kuwa mvuvi wa watu. Yaani kuwatoa watu kutoka kwenye ulimwengu na kuwaleta katika Nuru ya wokovu,
Hii ikiwa na maana mtu yeyote ambaye hajaokoka, kwamba yupo baharini, hivyo akishaokoka, ni anakuwa anahamishwa kutoka kwenye maji na kuletwa nchi kavu.
Hivyo sasa tunamwona hapa shetani kasimama ufukweni, lengo lake likiwa ni kukipinga kile kinachotoka kule kuja nchi kavu. Kumpinga mtu Yule ambaye anataka kutoka kwenye dunia na kuja katika wokovu. Mtu yule nayetaka kuacha kuishi maisha yake machafu na kuja katika maisha mapya ya utakatifu. Hapo ndipo vita vya ibilisi vilipo haswaa.
Hapo ndipo utakapokutana na shetani, hakuna mahali pengine utamwona ibilisi kwa uwazi wote kama hapo. Ndio vita vyake vilipo. Hatahangaika na wewe ambaye sikuzote upo dhambini, wala hutamwona akikugasi, lakini siku ambapo unafanya uamuzi ndipo utakapomwona akitaka kukusumbua, kama vile alivyotaka kumwangamiza Kristo tu alipozaliwa duniani.
Lakini ni wajibu wetu kumshinda, na tunamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa Neno la ushuhuda wetu sawasawa na
Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Hivyo kaa ukijua kuwa pale unapotaka kufanya badiliko la kweli la maisha hapo ndipo pa muhimu sana, na shetani analijua hilo na ndio maana anasimamia hapo, kwahiyo ni wajibu wako kumshinda, haijalishi ataleta vita vya aina gani, Kumbuka hizi ni siku za mwisho, na Bwana Yesu alisema, ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu ndio watakaouteka. Mathayo 11:12
Kwahiyo huna sababu ya kuanza kuogopa kudharauliwa, au kuchekwa, au kutengwa au kudhihakiwa kisa tu umeamua kuokoka au kuishi maisha ya wokovu. Jitwike msalaba wako umfuate Yesu, ili upokee taji la ushindi ufikapo kule.
Bwana akubariki
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Wakati mwingine kuna mambo unasoma kwenye biblia unaishia kuogopa sana, hususani pale unapoona mtu Mungu anafanya mambo ambayo hata mwenye dhambi si rahisi ayafanye. Kwamfano embu tuwaangalie hawa watu wawili, [Daudi na Yuda]. Hawa wote tunajua walikuwa ni watiwa mafuta wa Mungu, tukianzana na Daudi, tunajua alikuwa ni shujaa sana, na katika ushujaa wake, aliweza kuchagua mashujaa wake wengine 37 waaminifu ili kumsaidia katika vita, na kuipigania Israeli.
Lakini katikati ya mashujaa hao kulikuwa na mwingine ambaye alikuwa mwaminifu sana pengine hata Zaidi ya mashujaa wengine wote, na huyo aliitwa Uria. Uaminifu wake tunausoma jinsi ulivyokuwa.. hakuwa tayari kwenda kujiburudisha nafsi yake wakati kazi ya vita haijamalizika, na wenzake wapo bado mapambanoni, haijalishi kuwa ni mfalme ndiye aliyempa ruhusu ya kuondoka, hakuwa tayari kuondoka.
2Samweli 11:8 “Daudi akamwambia Uria, Haya, shuka nyumbani kwako, ukanawe miguu yako. Basi Uria akatoka katika nyumba ya mfalme, na tunu ya vyakula ikamfuata, iliyotoka kwa mfalme.
9 Lakini Uria akalala mlangoni pa nyumba ya mfalme, pamoja na watumishi wote wa bwana wake, wala hakushuka nyumbani kwake.
10 Watu walipomwambia Daudi ya kwamba, Uria hakushuka nyumbani kwake, Daudi akamwambia Uria, Je! Hukutoka safarini? Mbona hukushuka nyumbani kwako?
11 Naye Uria akamwambia Daudi, Sanduku, na Israeli, na Yuda, wanakaa vibandani; na bwana wangu Yoabu, na watumishi wa bwana wangu, wamepiga kambi waziwazi uwandani; nami niende nyumbani kwangu, kula na kunywa, na kulala na mke wangu? Uishivyo, na kama roho yako iishivyo, mimi sitafanya jambo hili. 12 Basi Daudi akamwambia Uria, Ngoja hapa leo tena, na kesho nitakuacha kwenda zako. Basi Uria akakaa Yerusalemu siku ile, na siku ya pili yake.
13 Naye Daudi akamwalika, akala, akanywa mbele yake; naye akamlevya; hata wakati wa jioni akatoka kwenda kulala kitandani mwake pamoja na watumishi wa bwana wake, lakini hakushuka nyumbani kwake.”
Unaweza ukajiuliza, mtu kama huyu, labda ndio angependwa kipekee na Daudi, na kupewa zawadi nyingi kwa moyo wake huo wa uaminifu na Upendo, lakini kinyume chake Daudi ndio akampangia njama za kumwangamiza. Tena kumwangamiza katika huo huo uaminifu wake.. Na akafanikiwa, akamuua kwenye vita, pale alipowaambia mashujaa wake wamwache mwenyewe auawe.
Huyo ndio Daudi mtiwa mafuta wa Bwana, Lakini ni nini kilichompelekea afanye vile, hakufanya vile kwasababu alipenda, bali kwasababu ya shinikizo la dhambi lililokuwa nyuma yake. Na dhambi yenyewe ilianzia pale, alimuona mke wa Uria, akamtamani, kisha akamchukua alale naye, akadhani itaishia pale pale tu, hakujua kuwa madhara Zaidi yanaweza kuja, matokeo yake akapata mimba yule mwanamke, Na Daudi alipoona hivyo akataka kumbambikizia Uria mimba ambayo si yake , ili tu kusitiri aibu, ndio maana akampa likizo ya ghafla, ili akalale na mkewe, lakini Uria alikuwa mwaminifu hakukwenda kulala na mke wake, alibaki kambini, ndipo Daudi ikambidi abuni mbinu nyingine ya kusitiri uovu wake, ndipo akaamua kukiua kiungo chake kiteule, kisichokuwa na hatia yoyote. Hilo ndio shinikizo la dhambi.
Mwingine ni Yuda, huyu naye alianza dhambi kidogo kidogo tu, ya wizi, hakujua tamaa hiyo itampelekea kuisaliti damu isiyokuwa na hatia, akadhani ni mambo rahisi rahisi tu, akaendelea kuwa mwizi, mpaka ikafikia hatua ile dhambi iliyokuwa ndani yake ikamshinikiza, kupata hela nyingi Zaidi na njia pekee ambayo ingempelekea kuipata ni kwa kumsaliti Bwana wake, Mtakatifu ili wale wakuu wa makuhani wampe Hela.
Sasa usidhani kwamba kumsaliti Bwana wake ambaye alijua anampenda upeo, na kumweshimu ilikuwa ni jambo analolifurahia sana, hapana, bali lile shinikizo la dhambi ndio lililompelekea kuchukua maamuzi ambayo yalimletea majuto ya milele.
Yuda alimsaliti Bwana wake, alimsaliti jemedari wake, alimsaliti mwokozi wake aliyependa, kwa dhambi ndogo tu ya kupenda fedha na wizi.
Huoni leo hii watu wanawatoa ndugu zao kafara kwa waganga wa kienyeji, unadhani hawawapendi ndugu zao, wanawapenda lakini lile shinikizo la dhambi ambalo lilianza zamani kama tamaa tu ya mali ndilo lililowafikisha mahali ambapo inawagharimu wafanye hivyo, wasipofanya ndio wamekwisha.
Huoni leo hii mabinti wengi, wanatoa mimba ovyo, kama vile si kitendo cha uuaji wanachokifanya. Usidhani hawawapendi watoto wao, lakini lile shinikizo la dhambi pengine la kukwepa aibu, kukwepa kutengwa, kukwepa kufukuzwa shule, kukwepa majukumu, linawafanya watende vitendo hivyo vya kinyama kila kukicha.
Hata wewe leo hii usidhani huwezi kumuua mtu kwa kumpiga risasi, usidhani huwezi kufanya mambo ya ajabu kupindukia, usiseme hivyo kama ni mtendaji wa dhambi hizo ambazo unaziona za kawaida tu, unaweza kutenda tena na ukawa ni mnyama kuliko hata magaidi wenyewe, kama utaivumilia dhambi ndani yako, Haijalishi utajiita ni mtumishi wa Mungu.
Dhambi ni ya kuiogopa sana, usiseme yule ni mke wa mtu ngoja nikazini naye leo tu basi, hakutakuwa na shida yoyote, usijaribu kufanya hivyo ndugu, usiseme ngoja niibe kile kidogo kwenye kampuni, hakitaniletea madhara yoyote, usifanye hivyo.. Dhambi inashinikizo kubwa sana, inakupeleka mahali ambapo huwezi kuchomoka mpaka ufanye kufuru mbaya sana. Laiti Daudi au Yuda angelijua tangu mwanzo kuwa watasababisha damu zisizo na hatia kumwagika wasingedhubutu kufanya mambo kama yale.
Lolote unaloliona ni dogo maadamu ni dhambi jiepushe nalo tu, kwa usalama wa maisha yako ya rohoni.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Je mtu anayeua anabeba dhambi zote za yule aliyemuua?
USIINGIE MKATABA NA DHAMBI.
ROHO ANENA WAZIWAZI
Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
Shalom..Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Neno la Mungu linasema katika…
1 Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”
Maana ya kunena waziwazi ni kwamba…“ananena pasipo maficho yoyote wala pasipo siri yoyote”..yapo mambo ambayo Roho Mtakatifu akiyanena yanahitaji ufunuo mpana kutoka kwake..kwamfano utaona katika kitabu cha ufunuo sehemu kadha wa kadha, anasema “yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”. Au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema “yeye mwenye akili na aweze kuyajua haya yanayozungumzwa maana yake ni nini”..kwamaana inahitajika ufunuo kuyajua.
Kwamfano tunaweza kujifunza mfano mmoja, ambapo Roho hajanena waziwazi.
Ufunuo 2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.
28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”
Hapo Roho kanena..lakini si wazi..kwasababu atakayesoma hajaambiwa nyota ya asubuhi hapo ni nini, wala hajaambiwa hao mataifa atakaowachunga ni wakina nani…maana yake mambo hayo yote yanahitaji ufunuo wa Roho kuyaelewa…hayajanenwa waziwazi..
Lakini katika hiyo 1Timotheo 4 biblia inasema Roho anena waziwazi..kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na Imani, wakisikiliza roho zidanganyazo….na mafundisho ya mashetani..
Hapo anasema wakizisikiliza roho zidanganyazo…na si wakizitazama au wakiziabudu..bali wakizisikiliza..maana yake hizo roho zinazungumza na zipo nyingi.
Sasa hizo zinazungumzaje?
Roho hizi zinazungumza kwa njia kuu mbili.
1. Katika nafsi ya mtu
2. Kupitia watumishi wa shetani, ambao wamevaa mavazi ya kondoo.
1. Katika nafsi ya mtu ni pale mtu anaposikia sauti au msukumo wa kwenda kufanya jambo lililo kinyume na mapenzi ya Mungu.. Kwamfano kama mtu atasikia sauti ikimwambia akatoe mimba, au akaue, au akaibe, akaabudu sanamu au akafanye uasherat, ukavae nguo za nusu uchi, ukapake lipatick, ukavae suruali kwa mwanamke, ukaende kwa waganga, ukaachane na mke wako/mume wako wa ndoa..n.k.kama akiisikiliza hiyo sauti na kwenda kufanya mojawapo ya hayo tayari atakuwa kasikiliza roho hiyo idanganyayo.
2. Vile vile kama atamsikia mtu au mhubiri akimshawishi kufanya mojawapo ya mambo hayo hapo juu tayari, na kwenda kufanya kama alivyosikia kutoka kwa huyo mtu au mhubiri, tayari atakuwa ameisikiliza roho hiyo na imeshamdanganya, aidha kwa kujua au kwa kutokujua..kupitia huyo mhubiri.
Hivyo Roho anatuambia waziwazi kuwa nyakati za mwisho ambazo ndizo hizi watu wengi sana watakuwa wanazisikiliza hizi roho..na si wachache bali ni wengi..Hivyo ni wajibu wetu kuwa macho,na kuwa makini sana ili tusiwe miongoni mwa hao “wengi”…ndio maana ametuambia waziwazi ili tujue hali halisi, na tuweze kujilinda.
Huu ni wakati wa kuzichunguza sana roho..niliwahi kukutana na mtu akaniambia ameokoka na anaamini sana sauti yoyote inayomjia ndani yake ni ya roho mtakatifu..Nikamuuliza anatumia nini kuipima hiyo sauti.. akasema anatumia hisia tu…hivyo hawezikudanganyika.
Ndugu hata uwe mhubiri mkubwa kiasi gani, hata uwe unanena kwa lugha, hata uwe unatabiri, au unaona maono, hata uwe kila siku unatembelewa na malaika..roho za yule adui yetu shetani hazichunguzwi kwa ujuzi au utaalamu au uzoefu fulani au kwa hisia..hapana!! bali zinachunguzwa kwa Neno la Mungu tu..
Maana yake ni kwamba hata kama nimeokoka sio kila sauti inayokuja ndani yangu ni ya kuiamini, bali ni lazima ipimwe na neno la Mungu..kama inakubaliana na Neno hiyo ni sauti kutoka kwa Mungu..lakini kama inapingana na Neno, haijalishi imekuja kwa nguvu kiasi gani, au umekuja na amani kiasi gani, au imekuja na hisia nzuri kiasi gani…hiyo si ya kuifuata ni sauti kutoka kwa yule adui. Biblia inasema..
2 Wakorintho 11:14 “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru”.
Na neno la Mungu tunalijua kwa kusoma biblia kwa bidii sana…hiyo ndiyo silaha.
Kumbuka tena usisahau neno hili… Roho anena waziwazi, kuwa nyakati za mwisho wengi watajitenga na Imani, na kusikiliza roho zidanganyazo… ni maombi yangu kuwa mimi na wewe hatutakuwa miongoni mwa hao “wengi”.
Kama hujampokea Yesu mpaka sasa, kwasababu fulani fulani, unazozijua wewe, fahamu kuwa umeshasikiliza roho hizo na zimekudanganya…Hivyo fungua leo macho yako na mgeukie Kristo uanze upya, naye atakupokea na kukusaidia kwasababu anatamani wewe uwe na uzima kuliko wewe unavyotamani.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo: