Tukisoma 2Samweli 24:13, tunaona biblia imesema ni miaka 7 imewekwa mbele ya Dauidi, Lakini tukienda kusoma tena habari hiyo hiyo katika kitabu cha 1Nyakati 21:12, tunaona biblia inataja miaka 3 ya njaa na si 7 tena. Je! Ipi ni ipi?
Labda tuanze kusoma habari hiyo katika kitabu cha 2 Samweli..
2Samweli 24:11 “Na Daudi alipoondoka asubuhi, neno la Bwana likamjia nabii Gadi, mwonaji wake Daudi, kusema,
12 Nenda, ukanene na Daudi, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo.
13 Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, MIAKA SABA YA NJAA ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma”.
Hapo tunaona kweli ni miaka 7, Lakini tusome tena habari hiyo katika Mambo ya Nyakati.
1Nyakati 21:11 “Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo;
12 MIAKA MITATU YA NJAA; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma”.
Kwa mistari hiyo ni rahisi kusema biblia inajichanganya.. Lakini kiuhalisia, biblia haijichanganyi mahali popote, wala haijakosewa mahali popote.
Katika habari hiyo, waandishi wote wawili wa vitabu hivyo, walikuwa wapo sahihi.. hakuna ambaye hakuwa sahihi, kwasababu wote walikuwa wanaongozwa na Roho Mtakatifu katika kuandika. Isipokuwa kila mmoja aliandika katika mazingira tofauti na mwenzake, na hawakunakiliana hivyo, ushuhuda wa mmoja hauwezi kufanana asilimia mia na wa mwingine.
Hebu chukua mfano, umefungua taarifa ya habari katika vyombo viwili tofauti, ni wazi kuwa unaweza kusikia habari moja lakini imefafanuliwa tofauti katika vyombo vyote viwili lakini habari ni ile ile moja.
Habari hizo haziwezi kufanana asilimia mia, vinginevyo kimoja kitakuwa kimenakili habari ya mwingine kama ilivyo.
Kadhalika kitabu cha Samweli sio nakala ya kitabu cha Mambo ya Nyakati, kadhalika kitabu cha Luka sio nakala ya kitabu cha Mathayo..ingawa vyote vinaweza kuwa vinaelezea matukio yanayofanana, lakini haviwezi kufanana asilimia mia, kwasababu ni mashahidi wawili tofauti. Ndio maana unaona Ushuhuda wa Luka haifananini asilimia mia na wa Mathayo au Marko.
Sasa labda turudi katika habari hiyo ya Daudi..
Tukianza na kitabu hicho cha 2Samweli 24, labda turudi sura mbili nyuma, tuone ni tukio gani lilitokea.. kisha tutaanza kuelewa ni kwasababu gani Mwandishi hapa kataja miaka 7 badala ya 3..
Tusome,
2Samweli 21:1 “Kulikuwa na njaa siku za Daudi MUDA WA MIAKA MITATU, MWAKA KWA MWAKA; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni”.
Umeona hapo? Kabla Daudi kutaka kwenda kuwahesabu watu, kulitangulia njaa miaka 3, ambapo njaa hiyo ilisababishwa na Sauli kuwaua wagibeoni.
Sasa baada ya Daudi kutafuta utatuzi wa njaa hiyo, maandiko yanatuambia alifanya kosa lingine la kwenda kuwahesabu Israeli, jambo ambalo lingeiingiza tena Israeli katika baa la njaa kwa miaka mingine 3 mbele. Na kama ukisoma pale, Sensa ya kuwahesabu Israeli ilichukua miezi kama 9 na siku 20 (2Samweli 24:8).
Kwahiyo ukichukua Miaka 3 ya njaa iliyosababishwa na Sauli, ukijumlisha na hiyo miezi 9.. utaona ni kipindi cha takribani Miaka 4. Na maandiko yanasema baada ya Daudi kuwahesabu Israeli ndipo Neno la Bwana likamjia..kwahiyo inawezekana ikawa siku ile ile alipomaliza kuwahesabu au wiki moja baadaye au mwezi mmoja baadaye ndipo Neno la Bwana likamjia.. Lakini yote katika yote miaka 4 iliisha ambayo ilikuwa ya njaa..kabla ya kuja mingine 3 kwaajili ya kosa hilo la kwenda kuwahesabu.
Kwahiyo ukichukua hiyo miaka 3 ya Sauli, ukajumlisha KIPINDI CHA MWAKA MZIMA cha SENSA, Pamoja na Neno la Bwana kumjia Daudi, Ukajumlisha na MIAKA HIYO 3 Daudi aliyoambiwa achague, Jumla yake utapata ni miaka 7.
Kwahiyo Mwandishi wa katika kitabu hicho cha Samweli alichokuwa anakimaanisha ni kwamba Endapo Daudi atachagua janga la miaka 3 ya njaa.. atakuwa amefanya JUMLA ya miaka ya njaa katika Israeli kuwa SABA.
Lakini tukirudi kwa mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati, yeye alikwenda moja kwa moja kwenye hiyo miaka 3 ya mwisho, pasipo kuhesabu ile 3 ya kwanza iliyotangulia, pamoja na ule mmoja wa Sensa. Na ndio maana utaona katika kitabu hicho cha Mambo ya Nyakati hajaeleza popote kuhusu Njaa hiyo ya kwanza iliyosababishwa na Sauli…kama alivyoeleza mwandishi wa kitabu cha Samweli.
Kwahiyo hakuna utata wowote katika hiyo mistari.
Sasa ilikuwepo sababu kwanini Mungu achukizwe na Daudi katika kwenda kuwahesabu Israeli..Sababu hiyo kwa urefu unaweza kuisoma hapa>> USIZITEGEMEE NGUVU ZAKO KUKUSAIDIA
Mwisho, tukumbuke kuwa Kristo yupo mlangoni kurudi kulinyakua kanisa lake.. na atakuja kama mwivi, Je! umejiandaa?. Kama bado mwamini Yesu leo, na kubatizwa, upate ondoleo la dhambi.
Bwana atubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Hii ni sehemu ya tatu ya mfululizo wa masomo kwa wanawake, katika sehemu ya kwanza na ya pili tumeona, ni kwanini Bwana aliwatambua baadhi ya wanawake, kwa jinsia zao, na sio kwa majina yao, kwa kuwaita “wanawake”, na sehemu nyingine kuwatambua kwa mionekano yao kwa kuwaita “Binti” na sio labda kwa majina yao..ipo sababu, ikiwa hujapata bado, chambuzi zake, basi tutumie msg inbox tukutumie..
Lakini leo tutasonga mbele tena, kuona ni kwanini baadhi ya wanawake, aliwatambua kwa majina ya “MAMA”.
Mama ni cheo cha ukomavu, kwasababu mpaka uitwe mama ni wazi kuwa lazima utakuwa na watoto uliowazaa au unaowalea chini yako. Sasa tukirudi kwa Bwana Yesu, kuna wanawake aliwaona ni “Wamama rohoni”, sio mwilini, kwasababu kulikuwa na wanawake wengi, lakini si wote aliwaita “Mama” kama tu vile si wote aliwaita “Binti yangu”, bali baadhi tu.
Sasa embu twende tukasome baadhi ya Habari katika biblia kisha tuone, ni nini Bwana anatufundisha katika Habari husika. Mwanamke wa kwanza tutakayemtazama ni yule mkananayo. Tusome;
Mathayo 15:21 “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.
22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, MAMA, IMANI YAKO NI KUBWA; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.
Angalia asili ya huyu mwanamke, hakumtafuta Bwana kwa shida zake mwenyewe, au kwa matatizo yake mwenyewe, bali alimtafuta Bwana Yesu kwa shida za mwanawe.. Japokuwa mwanzoni hakujibiwa chochote, hata baada ya pale alipewa na maneno ya kukatishwa tamaa ya kuitwa mbwa, lakini bado hakuacha kuomba kwa shida ya mtu mwingine, kwasababu uzito wa mwanae ulikuwa kama wakwake.
Hiyo ni kuonyesha ni jinsi gani asivyojali vya kwake tu, bali hata vya wengine…
Mwanamke mwingine ni Mama yake Yesu mwenyewe, ambaye tunamsoma katika Yohana 2:1-4 siku ile alipoalikwa katika Harusi..
Yohana 2:1 “Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
3 Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu akamwambia, MAMA, TUNA NINI MIMI NAWE? Saa yangu haijawadia”.
Angalia tabia yake alijali shida za wengine, aibu za wengine, akazifanya kama ni za kwake. Na kumpelekea Kristo, na muda huo huo akamwita “mama”
Mwingine ni Mariamu Magdalena, asubuhi ile ya kufufuka kwa Bwana, alikuwa akilia pale makaburini ndipo Yesu akamtokea na kumwambia “Mama unalilia nini?” Saa hiyo hiyo Yesu akamtuma kwa ndugu zake kwenda kuwatangazia injili. Akawa mtu wa kwanza kupewa neema ya kuwahubiria watu wengine Habari za kufufuka kwa Bwana Yesu. (Yohana 20:11-18)..
Neema hiyo si kila mwanamke atapewa, bali ni wale “wamama rohoni tu” Wanawake waliokomaa kiroho,ambao wanajua wajibu wao kwa Bwana, wanajua kuwaongoza wengine katika njia za Mungu, haijalishi umri wao Rohoni watu kama hawa, wanawekwa kundi moja na akina Sara, na Rebeka, na Mariamu, na Elizabeti na wengineo. Kwasababu wamevuka viwango cha utoto, hadi kufikia hatua ya utu uzima ya kuzaa na kulea.
Swali ni je! Wewe, dada upo katika kundi gani? Bwana anapokuona anakutambuaje? msichana? Au Mtu? Mtoto? Au Mama?. Kabla hujafikiria kuyatazama Maisha ya mitume wa Yesu mfano wakina Petro waliishije, embu tafakari kwanza, Maisha ya wanawake wacha Mungu katika biblia waliishije. Hiyo itakusaidia sana mwanamke.
Tamani sana, Kristo akutambue kama “Mama” Ni heshima ya juu sana, Kristo anaweza kumpa mwanamke, iliyosawa na ya “Kitume”. Kua kiroho timiza wajibu wako wa kuitangaza injili na pia kuwasaidia wengine kumjua Mungu rohoni.
Bwana akubariki.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
SWALI: Je! Siku ya unyakuo watoto wachanga watanyakuliwa? Na vipi kuhusu walio bado tumboni, na wenyewe watanyakuliwa au wataachwa?
JIBU: Hili ni moja ya swali gumu kwasababu biblia haijaeleza moja kwa moja ni nini kitawatokea watoto siku ile ya Unyakuo, Hivyo tutajaribu kueleza kwa kadiri ya tunavyoona katika baadhi ya vifungu kwenye maandiko.
Ukitazama katika biblia, utaona, wapo watoto walipata neema kutokana na haki za wazazi wao, mfano wa hawa ni watoto wa Nuhu, na Lutu, vilevile wapo watoto walioadhibiwa kutokana na makosa ya wazazi wao. Utaliona hilo pia katika vile vizazi vyote vya Sodoma na Gomora, pamoja na gharika vyote viliteketezwa, hadi watoto walipata adhabu kwa dhambi za wengine. Lakini hiyo haimaanishi kuwa wataadhibiwa tena baada ya kifo.
Pia tukumbuke kuwa hata katikati ya kipindi cha dhiki kuu, bado watu wataendelea kutungishwa mimba na kuzaliwa, hivyo litakuwepo kundi la vichanga ambavyo vitazaliwa katikati ya dhiki kuu na vitakufa katika maangamizi yao..Hilo tunalithibitisha katika andiko hili;
Mathayo 24:19 “Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!
20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.
Unaona? Kwahiyo siku ile ikifika, kuna uwezekano wa watoto wengine kunyakuliwa (hata wale walio tumboni), na vilevile wengine kubaki, japo hatuwezi kusema hivyo ndivyo ilivyo, Yote tunamwachia Mungu. Ikiwa ni wote watanyakuliwa, au ni baadhi, Tunachopaswa kufahamu ni kuwa Mungu ni wa haki, atayaleta yote katika mizani, na yote yatakuwa sawa tu mwisho wa siku, na tutaona kabisa hukumu zake ni za haki. Kama vile Malaika mbinguni wanavyokiri hivyo..
Ufunuo 16:7 “Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako”.
Cha muhimu tunachopaswa kujua ni kuwa sisi ambao tayari tumeshafikia kimo cha kuyajua mema na mabaya, Kama hatutayatengeneza mambo yetu sasa, kwa kumpokea Bwana Yesu Kristo kwa kumaanisha kabisa, na kujitwika misalaba yetu na kumfuata, tujue kuwa unyakuo ukipita tutaachwa. Na matokeo yake, yatakuwa ni kuingia katika mateso makali ya dhiki kuu pamoja na Jehanamu ya moto.
Je! Umeokoka? Je! Umebatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako? Kumbuka Unyakuo ni wakati wowote, tubu umruidie muumba wako. Parapanda ni siku yoyote inalia, hakuna dalili iliyosalia..
Bwana Yesu akubariki.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Mwerezi ni aina ya mti uliokuwa unapatikana maeneno ya nchi ya Lebanoni, Ulikuwa unastawi pia sehemu mbalimbali za dunia, lakini ulistawi zaidi katika nchi ya Lebanoni, iliyopo kaskazini mwa nchi ya Israeli.
Aina hii ya mti ilitumika kwa matumizi mengi, kutokakana ubora wake na uimara wake ukulinganisha na aina nyingine ya miti. Mti huu wa Mwerezi ulikuwa ni mgumu na usiooza kirahisi.
Nchi ya Lebanoni, ilijipatia utajiri kutokana na biashara ya miti hii, ambapo Mataifa mengi duniani kama Misri, Ashuru, Babeli na Israeli ilinunua miti hii kutoka huko Lebanoni, kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi.
Mfalme Daudi alitumia miti hii ya Mierezi kutoka Lebanoni kuijenga nyumba yake.
2Samweli 5:11 “Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, AKAMPELEKEA NA MIEREZI, NA MASEREMALA, NA WAASHI; NAO WAKAMJENGEA DAUDI NYUMBA”.
2Samweli 7:2 “mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika NYUMBA YA MIEREZI, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.”
Lakini pia Nyumba ya Mungu ambayo ilikuja kujengwa na Sulemani, Mwana wa Daudi, ilitengenezwa pia kwa Mierezi mingi kutoka Lebanoni.
1Wafalme 5:5 “Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu.
6 BASI UAMURU WANIKATIE MIEREZI YA LEBANONI; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni”.
Na hata baada ya Mfalme Nebukadneza kuliharibu hekalu hilo la Sulemani, hekalu la pili lilipokuja kujengwa na wakina Zerubabeli, lilijengwa sehemu kwa miti hiyo ya Mierezi.
Ezra 3:6 “Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa bado.
7 Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete MIEREZI KUTOKA LEBANONI mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi”.
Hivyo Mwerezi katika biblia imetumika kama ishara ya UTAJIRI. Kama vile DHAHABU.
Tunaona vitu vikuu viwili vilivyotajwa sana katika ujenzi wa nyumba ya Mungu ni MWEREZI pamoja na DHAHABU. Kutokana na uthamani wa vitu hivyo.
Na kama Mti wa Mwerezi ulivyojipatia sifa hivyo, Bwana Mungu anasema walio Haki wote watasitawi kama Mwerezi.
Zaburi 92:12 “Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama MWEREZI WA LEBANONI.
13 Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
15 Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu”.
Je! Wewe ni mwenye HAKI?
Kumbuka mwenye haki sio mtu anayesema anafanya mema huku yupo nje ya Kristo, hiyo sio tafsiri ya mwenye haki. Bali tafsiri ya mwenye haki ni mtu Yule, aliyempokea Yesu, na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, huyo ndiye anayehesabiwa haki kwa IMANI HIYO ya kumwamini Yesu. Mwingine yeyote ambaye hamwamini Bwana Yesu, na kujitumainia katika mambo yake anayoyafanya anayoamini kuwa ni mema, anakuwa bado si mwenye haki mbele za Mungu.
Lakini wote waliompokea Yesu, watasitawi na kuwa na heshima kama miti ya Mierezi.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Biblia inamaanisha nini inaposema “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake”?
Shilo ni nini?
Katika biblia Shilo ulikuwa mji mtakatifu, ambapo Kabla ya Mungu kupachagua Yerusalemu kama mji atakaoweka jina lake milele, hapo kabla wana wa Israeli walikuwa wanakusanyiko huko Shilo, kama sehemu takatifu ya kufanyia ibada na kutolea dhabihu.
Na hata sanduku la agano mara tu baada ya wana wa Israeli kuingia nchi ya ahadi, mji uliotueuliwa kwaajili ya kuliweka sanduku hilo la agano la Mungu..ulikuwa ndio huo wa mji wa Shilo, ambapo sanduku hilo lilikaa mjini huko bila kutoka kwa miaka mingi mpaka Wafilisti walipokuja kulichukua kutoka huko sababu ya makosa ya wana wa Israeli (1Samweli 10-11).
Huko Shilo pia ndiko Nabii Samweli alikolelewa maisha yake yote (1Samweli 1:24 )
Mji huu wa Shilo ulikuwa unapatikana kaskazini mji mwa mji wa Betheli, karibu na Samaria.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu mji huo kupitia mistari ifuatayo > Yoshua 18:8-10, Yoshua 19:51, Yoshua 21:2, Waamuzi 18:31, Waamuzi 21:19, 1Samweli 1:9, Zaburi 78:60.
Lakini swali ni je! Hii Shilo mpaka leo ni sehemu takatifu?.
Jibu ni la!
Shilo ya Leo sio tena huko Israeli, bali ni katika Neno la Mungu.
Katika Kweli ya Neno la Mungu na katika Roho Mtakatifu..tunamwabudu Baba..kama Bwana Yesu alivyosema..
Yohana 4:21
“Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.
22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”
Je umempokea Roho Mtakatifu, je unaliishi Neno?.
Bwana akubariki.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Jibu: Tusome,
Matendo 12:20 “Naye Herode ALIKUWA AMEWAKASIRIKIA SANA WATU WA TIRO NA SIDONI; wakamwendea kwa nia moja, na wakiisha kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana nchi yao ilipata riziki kwa nchi ya mfalme.
21 Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao.
22 Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu.
23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho”.
Tiro na Sidoni ni miji iliyokuwepo kaskazini mwa mji wa Galilaya, miji hiyo kwasasa ni sehemu za Lebanoni.
Zamani za biblia Herodi ndiye alikuwa anatawala Yudea, na watu wa miji ya Tiro na Sidoni, walikuwa wanaitegemea Yudea kwa chakula. Lakini ulifika wakati Herode alichukizwa nao (biblia haijataja sababu ni nini), lakini alichukizwa nao, na akakatisha kuwauzia chakula hao watu wa Sidoni na Tiro.
Watu wa Tiro na Sidoni, walipokaa muda mrefu bila chakula, ikawabidi wakatafute amani na Herode huko Yudea, lakini njia waliyoitumia ni kumtafuta mtu aliyeitwa Blasto, ili amshawishi Herode waweze kuwa na mdahalo wa wazi na Hao watu wa Sidoni, kwasababu haikuwa rahisi Herode, kumfikia.
Huyu Blasto ambaye alikuwa anafanya kazi katika nyumba ya Mfalme Herode, na ambaye ndiye aliyekuwa mtu wake karibu kuliko wengine wote, alifanikiwa kumshawishi Herode azungumze na watu wa Tiro na Sidoni kwa wazi.
Hivyo siku ilipofika Herode alijitokeza kuzungumza na watu hao. Lakini kama inavyojulikana Herode alikuwa ni mtu wa kupenda utukufu, alikuwa anajitukuza yeye kama Mungu hapo Yudea. Alikuwa anapenda kuabudiwa kama Mungu. Alimuua Yakobo ndugu yake Yohana kwa upanga, na mwisho alimfunga Petro ili amuue kama alivyomuua Yakobo, lakini Malaika wa Bwana alimwokoa na mauti yake. Na hapa anasimama ili ajitukuze, awaonyeshe watu wa Sidoni na Tiro kwamba yeye ndiye anayetoa chakula!, pasipo yeye wao hawawezi kuishi.
Na watu wa Sidoni kwasababu ni watu wa kipagani waliozoea kuabudu miungu, na kumtukuza mtu yeyote ambaye wanamwona ni wa tofauti, kama wale watu wa Athene waliotaka kumtukuza Paulo na Barnaba..
Matendo 14:11 “Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.
12 Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji”.
Kadhalika na hawa watu wa Tiro na Sidoni walipomwona tu Herode kasimama anahutubia kimajivuno na kimajigambo kiasi kile, wote kwa pamoja wakaanza kupaza sauti zao na kusema “Hii ni sauti ya Mungu na si mtu..hii ni sauti ya Mungu na si mtu”
Tofauti na akina Paulo na Barnaba ambao wao walipoona watu wanawageuza miungu-watu walizirarua nguo zao na kuwaeleza kuwa wao ni watu tu kama wao, na sio Mungu. Kinyume chake Herode yeye hakufanya hivyo, bali moja kwa moja alizidi kujitukuza na kutaka kuchukua utukufu zaidi.
Na kwasababu Mungu hashiriki utukufu wake na wanadamu, pale pale Malaika wa Bwana alishuka akampiga Herode kwa change, Chango ni ugonjwa mbaya wa kuliwa na minyoo.. kwa maelezo marefu juu ya ugonjwa huu fungua hapa >>>>>> CHANGO KIBIBLIA
Lakini ni nini tunajifunza katika habari hiyo?
Tunachoweza kujifunza kikubwa ni kuwa Mungu hashirikiani utukufu na mwanadamu yeyote…Na ni jambo la hatari sana kutafuta ufukufu, jambo lililombadilisha shetani kutoka kuwa Kerubi na kuwa Ibilisi ni hilo hilo, la kutafuta kuabudiwa.
Na jambo lingine pia linalomhuzunisha Mungu sio sisi tu kutafuta kuabudiwa bali hata sisi tunapotafuta kuabudu watu au kitu kingine chochote.
Tunapoabudu sanamu, au watu, au fedha au kingine chotechote kile kuna hatari kubwa sana ya kuadhibiwa na Mungu.
Bwana atusaidie na kutubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Jibu: Labda tuanze kusoma kuanzia juu kidogo..
Waefeso 5:31 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
32 SIRI HIYO NI KUBWA; ILA MIMI NANENA HABARI YA KRISTO NA KANISA.
33 Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe”
Siri Paulo aliyoimaanisha hapo, sio nyingine Zaidi ya hiyo aliyoitaja hapo kwamba “WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA”. Hiyo ndiyo SIRI yenyewe.. Na kwanini iwe siri?, ni kwasababu ni jambo gumu kueleweka au kufafanulika kwamba watu wawili tofauti wenye miili miwili tofauti wamekutana halafu wanakuwa mwili mmoja, na ilihali ni watu wawili tofauti wenye miili miwili tofauti.. afadhali angesema “watakuwa nafsi moja au watakuwa wamoja”.. kidogo ingeweza kuwa rahisi kueleweka, lakini kuwa mwili mmoja? Hapo ni lazima kuna siri katikati yake.
Tunaona pia Bwana Yesu alilisisitiza tena jambo hilo hilo katika injili ya Marko.
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”
Kwahiyo hiyo ni SIRI kubwa sana.
Lakini biblia imetupa uvumbuzi wa siri hiyo, ni kwa jinsi gani, wawili wanakuwa mwili mmoja na si roho moja.
Na uvumbuzi huo tunaupata pale Mwanzo, Mungu alipowaumba Adamu na Hawa.. Biblia inasema
Mwanzo 2:21 “Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, SASA HUYU NI MFUPA KATIKA MIFUPA YANGU, na NYAMA KATIKA NYAMA YANGU, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”.
Hapo katika mstari wa 23, tunaona Adamu hakusema huyu ni “roho katika roho yangu” wala “nafsi katika nafsi yangu”..bali alisema huyu “ni nyama katika nyama yake”.. akimaanisha mwili wa mwanamke yule ni mwili wake…kwasababu katwaliwa kutoka kwake.
Kwahiyo mtu yeyote anayekwenda kuoa au kuolewa, yule aliyejiungamanisha naye, tayari wanakuwa mwili mmoja, kwasababu wote asili yetu ni Adamu. Na kama wanakuwa mwili mmoja maana yake, Baraka zote wanashiriki pamoja, na vile vile laana zote wanashiriki pamoja na mambo yote mazuri au mabaya, ya mwilini au rohoni wanakuwa wanashiriki pamoja.
Ndio maana kuna hatari kubwa sana ya kutoka nje ya ndoa na kuzini, au kufanya uasherati.. kwasababu yule unayezini naye, au unayefanya naye uasherati, kiroho unajiunganisha naye na kuwa mwili mmoja bila wewe kujijua, maandiko yanasema hivyo..
1Wakorintho 6:13 “…………….Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili………………….
15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16 Au hamjui ya kuwa YEYE ALIYEUNGWA NA KAHABA NI MWILI MMOJA NAYE? MAANA ASEMA, WALE WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA”
Hivyo kahaba au mtu yeyote unayefanya naye uasherati, kama kuna Laana amezibeba katika maisha yake, wewe unayeshiriki naye, nawe pia unazibeba, kama ana roho na mapepo unaposhiriki naye uzinzi huo, yale mapepo nawe pia yanapata hifadhi ndani yako, (mnayashiriki pamoja) kwasababu tayari mmekuwa mwili mmoja.
Ndio maana moja ya amri za Mungu ni USIZINI! Kwasababu uzinzi una madhara makubwa sana kiroho na kimwili.
Wagalatia 5:19 “ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Bwana azidi atubariki.
Marna tha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
SWALI: Musa alikuwa na mawasiliano ya ana kwa ana na Mungu, hata kuuona uso wake lakini katika Yohana 1:18, inaonekana Yohana anakanusha kuwa hakuna mtu aliyewahi kumwona Mungu isipokuwa Kristo pekee.
Jibu: Kumwona Mungu kunakozungumziwa hapo sio KUMTAZAMA USONI, kwamba anaonekanaje, mwonekano wake ukoje, uso wake unafananaje fananaje n.k. La! Sio kwa namna hiyo. Bali kumwona kunakozungumziwa hapo ni kwa ufahamu.
Kwamfano tunaposema TUMEUONA MKONO WA BWANA, haimaanishi tumeenda mbinguni tukauona mkono wake jinsi ulivyo, au umeshuka chini tukauona jinsi ulivyo, rangi yake na idadi ya vidole alivyo navyo! N.k. La! Bali tunamaanisha tumeona uweza wake mkuu!. Vile vile tunaposema tumemwona Bwana katika maisha yetu, haimaanishi ameshuka mbele yetu na tukamwona sura yake, bali tunamaanisha tumeona uwepo wake na kuutambua.
Kadhalika maandiko hapo yanaposema hakuna aliyemwona Mungu haimaanishi “aliyemwona Uso wake jinsi ulivyo” bali inamaanisha “hakuna aliyemjua Mungu na kumfahamu, kiuweza na kimamlaka kikamilifu” isipokuwa Kristo peke yake. Wengine wamemwona na kumwelewa lakini si kwa kiwango ambacho Mungu mwenyewe, alikuwa anataka watu wamwelewe.. Hivyo ni sawa na hawakumwona kabisa! Au kumwelewa. Ni Bwana Yesu pekee ndiye aliyemwelewa na kumfunua Baba, kikamilifu…
Luka 10:22 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia”.
Umeona? Kristo pekee ndiye aliyemjua Mungu, jinsi inavyopaswa kumjua.. Musa hakumjua Mungu, ndio maana torati ya Musa havikuweza kumkamilisha mwanadamu!.. Kristo ndiye aliyekuja kumfunua Mungu kwetu jinsi inavyopaswa, na kutuonyesha mapenzi yake kamili..
Yohana 1:17 “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo”.
Kwamfano Wanafunzi wa Yesu walikuwa wanamwona Bwana Yesu kila siku, lakini walikuwa hawamjui, macho ya mioyo yao yalikuwa yamefumbwa. Ndio maana alipowauliza Yeye ni nani, wakawa wanakosa jibu sahihi, mpaka Petro ambaye alifunuliwa na Baba, aliposema yeye ni Mwana wa Mungu, ili litimie hilo neno “WALA HAKUNA AMJUAYE MWANA ILA BABA”; WALA HAKUNA AMJUAYE BABA ILA MWANA, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia”.
Hivyo Bwana Yesu(Mwana wa Mungu).. ndio kila kitu katika haya maisha. Hakuna mtu mwingine yeyote, au nabii mwingine yeyote ambaye tunaweza kumfuata au kumtegemea maneno yake tukafika mbinguni. Injili ya Musa haikumhaidia mtu kufika kule Baba aliko, wala ya Nabii mwingine yeyote.. Ni Yesu pekee ndiye aliyetoa njia ya Watu kumfikia Baba Mbinguni!!..kwasababu yeye ndiye anayemjua.. Na njia hiyo ya kumfikia Baba ni YEYE MWENYEWE, yaani maisha yake na Neno lake.
Yohana 14:5 “Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”
Je! Unataka kwenda mbinguni kwa Baba?
Kama ni ndio!, basi tambua NJIA NI YESU. Hakuna elimu nyingine yeyote, wala dini nyingine yeyote, wala maarifa mengine yeyote, ambayo yataweza kukufikisha mbinguni.. isipokuwa ni YESU TU!. Huyo ndiye aliyemwona Baba na Baba mwenyewe akamthibitisha.. hivyo hakuna njia ya mkato ya kufika mbinguni.
Hivyo kama hujampokea, mpokee leo na utubu na kubatizwa, ili aingia maishani mwako na kukuongoza katika njia ya uzima wa milele.
Maran atha!
[embedyt] https://www.youtube.com/embed?listType=playlist&list=PLIIhnDzXkeEcXSNPlq09Q5yonU3MOLI0h&v=kuCSAZcnM80&layout=gallery[/embedyt]
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?
Kama Mungu ndiye kaumba kila kitu, je ni yeye huyo huyo ndiye aliyeumba dhambi pia?
Hosea 12:9 Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za KARAMU YA IDI.
JIBU: Tofauti na inavyodhaniwa hapo, na watu wa dini tofauti, kwamba Biblia inazitambua sherehe za kiislamu!. Jambo ambalo si kweli.
Ni vizuri kufahamu kuwa lugha yetu ya Kiswahili imetohoa maneno mengi sana kutoka katika lugha ya kiharabu, hata wakati ambapo biblia inatafsiriwa katika Kiswahili ilifuata mkondo huo huo. Kwamfano Sehemu nyingine utaona neno “shehe” likitajwa (1Samweli 5:8), na hapa unaona pia Neno “Idi” .
Kulingana na lugha ya kiharabu neno IDI, linamaanisha “Sherehe”. Haijalishi ni sherehe ya aina gani, inaweza ikawa ni ya kidini au ya kitaifa, au ya kitamaduni, au ya kimuungano..
Hivyo imezoeleka na watu wengi wasioilewa lugha ya kiharabu kudhani kuwa Idi ni neno la sikukuu ya kiislamu, kumbe sio.
Katika biblia ya kiharabu, mahali popote, kulipotajwa sherehe ya kiyahudi, Neno Idi liliandikwa pale. Mfano, palipoandikwa sikukuu ya pasaka, iliandikwa “idi ya pasaka” n.k..
Hivyo, hatushangai na Neno hilo kuonekana katika baadhi ya vifungu kwenye biblia. Hiyo yote ni kwasababu lugha yetu ya Kiswahili, imeundwa kutoka katika lugha nyingi mbalimbali. Kwahiyo inayozungumziwa hapo sio sikukuu ya kiislamu, bali ni sikukuu ya vibanda, ambayo wana wa Israeli walikuwa wakiisheherekea kwa katika vibanda pindi walipokuwa jangwani.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Hii ni sehemu ya pili ya mfululizo wa masomo kwa wanawake, katika sehemu ya kwanza tumeona, ni kwanini Bwana alipokutana na yule mwanamke mwenye dhambi, alimtambua kwa jinsia yake (Yaani “mwanamke”) na sio kwa mwonekano wake wa kike pengine wa kiumri au wa kimaumbile. Hiyo ni kufunua kuwa ujumbe alioubeba yule mwanamke ulikuwa ni wa kijinsia.. yaani maalumu kwa wanawake. Hivyo kama hukupata maelezo yake, unaweza kunitumia ujumbe inbox nikakutumia.
Leo tutaenda katika sehemu ya pili: ya BINTI.
Mahali pengine, Bwana Yesu, aliwatambua wanawake wengine kama, binti zake.. Na cha ajabu ni kuwa, wengine walikuwa pengine wana umri mkubwa kuliko yeye, lakini bado aliwaita BINTI zake, akifunua kuwa kutazama kwake hakukuwa katika jicho la kimwili bali la rohoni. Embu tusome, kisa hiki kimoja..kisha tuone ni ujumbe gani Bwana alitaka kuupitisha kwa ulimwengu kupitia mwanamke huyu.
Mathayo 9:20 “Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake.
21 Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.
22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, BINTI YANGU; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.”.
Swali la kujiuliza ni kwanini alimtambua mwanamke huyu kama binti na sio pengine kama Mama, au bibi?
Ni kwasababu ya Imani yake ya kipekee aliyokuwa nayo kwake..Ambayo hakuiona kwa watu wengine wote waliomfuata, ijapokuwa alihangaika kwa miaka 12 kutafuta suluhu la matatizo yake asipate, lakini alipofika kwa Yesu kwa mara ya kwanza tu hakumuhesabia kama mmojawapo wa wale matapeli aliokutana nao, huko nyuma, waliomchukulia fedha zake.
Bali alimwamini moja kwa moja kwa asilimia 100, akasema, nitakapoligusa tu pindo la vazi lake, muda huo huo nitakuwa mzima, kumbuka hakusema sio “naamini nitapona, au pengine nitapona” hapana, bali alisema “NITAPONA” kuonyesha kuwa alikuwa na uhakika wa yule aliyekutana naye sio mbabaishaji au tapeli…. Na ndio maana akaona hata hakuna sababu ya kwenda kumsumbua kuzungumza naye, au kumwomba aje kumtembelea, Bali aliona pindo la vazi lake, tu linatosha yeye kuwa mzima..
Na Yesu alipoiona Imani yake saa ile ile akamgeukia na kumwita “Binti yangu”.. Akampa nafasi ya kipekee sana Kama Mtoto wa kike aliyemzaa yeye mwenyewe, ambaye ana haki zote za kupokea mema yote ya Baba yake.
Tujiulize ni wanawake wangapi leo Bwana anaweza kuwaita binti zangu? Usidhani Kristo kukuita binti yake, kwasababu ya umri wako mdogo, au mrembo wako, au utanashati wako, hilo halipo, yeye hana jicho la mwilini, kama sisi tulilonalo, haangalii umri wala umbile.
Kama wewe ni mwanamke lakini unafika kwa Kristo ili kujaribu jaribu tu, uone kama Bwana atakujibu au la!,atakusaidia au la! unamlinganisha na wale waganga wa kienyeji uliowahi kuwatembelea huko nyuma.. uone kama atajibu au la!. Ujue kuwa wewe sio binti wa Yesu.
Mabinti wa Yesu, tangu walipokutana na Yesu utawakuta wametulia kwa Bwana hadi sasa, wanaouhakika na waliyemwendea, hawahitaji kusaidiwa na mtu, kuelewa kuwa Yesu ni muweza, wanafanya mambo yao wakiwa wame-relax, huwezi kuwakuta leo kanisani Kesho, disco, leo wamevaa magauni, Kesho wanakatiza barabarani na visuruali na vikaptura, leo kwa nabii huyu Kesho kwa yule..huwezi kuwakuta wapo namna hiyo.
Hao ndio binti za Mungu. Na faida yao ni kuwa kwasababu wameshaitwa binti za Mungu, tayari wanaourithi kutoka mbinguni. Jambo ambalo wengi hawajui wakidhani kila mtu atakuwa mrithi wa kila baraka ya Mungu mbinguni.
Dada/mama/bibi tambua ni nini Kristo anatamani kuona kwako, acha kutangatanga na huu ulimwengu, Acha kujaribu jaribu, maanisha kumfuata Kristo.. Yeye mwenyewe anasema.
2Wakorintho 6:17 “Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu WANANGU WA KIUME NA WA KIKE”,
Kumbuka hizi ni siku za mwisho, Kristo anarudi siku yoyote. Bado tu hujatulia kwa Bwana? Injili tuliyobakiwa nayo sasa hivi sio ya kubembelezewa tena wokovu, ni wewe mwenyewe aumke usingizini, umtafute Mungu wako. Kwasababu muda umeshaisha.
Maran atha..
Usikose sehemu ya tatu na ya mwisho ya Makala hii, ambayo, tutaona pia ni kwanini Bwana Yesu aliwatambua wanawake wengine kama MAMA.
Bwana akubariki..
Maran atha
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo: