Sala ya Uponyaji/Maombi ya uponyaji
Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo.
Kusudi lingine kuu tukiachilia mbali lile la wokovu wa roho zetu ambalo lilimfanya Bwana Yesu aache enzi na mamlaka na ukuu kule mbinguni ashuke duniani, lilikuwa ni kutuponya na miili yetu pia.
Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa”,
Mathayo 8: 17 “Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu”.
Isaya 53:4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu;..”
Ni Yesu peke yake, ndiye mwenye uwezo wa kuyaondoa magonjwa yetu yote moja kwa moja, hakuna mwingine anayeweza kufanya hivyo, na ndio maana tunamtumaini yeye. Na ni mapenzi yake kuwa sisi tuponywe(Soma Mathayo 8:2-3). Inawezekana wewe unayeusoma ujumbe huu, upo katika hali mbaya wakati huu, inawezekana upo mahutihuti hospitalini,au umekuwa ukisumbuliwa na huo ugonjwa kwa muda mrefu, umejaribu kwenda huko na kule bila kupata mafanikio yoyote, umepoteza fedha nyingi kwa ajili ya matibabu lakini hakuna matumaini yoyote. Pengine hata ulishahudhuria katika nyumba za maombi lakini bado hali yako ipo palepale, nataka nikuambie usivunjike moyo, hilo bado halimfanyi Yesu asikuponye ugonjwa wako.
Inawezekana unao ugonjwa wa siri, na unaogopa hata kuwaeleza watu, inawezekana umepata ugonjwa usioponyeka, Umepata Ukimwi, au Kansa, au Kisukari, n.k. Nataka nikuambie hayo yote si kitu kwa Bwana Yesu.
Kama Yesu alifanya muujiza wa kuuponya mwili wa mtu ambaye alikuwa ameshakufa kwa ugonjwa mbaya sana(Lazaro) na mwili wake ulikuwa tayari umeshaanza kutoa mafunza kaburini, lakini akauridisha na ukiwa mzima bila shida yoyote.. Si zaidi wewe ambaye bado hata hujafa, bado hata mwili wako hujaanza kutoa mafunza? Atakuponya.
Anachotaka kwako ni kuamini tu! Basi.
Na imani inakuja kwa kusikia, hicho ndicho chanzo cha Imani, (Warumi 10:17) Unapolisoma Neno lake, imani inajengeka, unasoma shuhuda mbalimbali za jinsi Bwana alivyowaponya watu katika maandiko ndipo imani yako kwake inavyojengeka, na kuwa kubwa zaidi,
Unaweza kufungua masomo haya, na shuhuda hizi mbili tatu, zitakusaidia kuiimarisha imani yako;
Zaburi 107:19 “Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao”.
Sala ya Uponyaji/Maombi ya uponyaji
Lipo kusudi la Mungu kukufikisha katika ukurasa huu kwa wakati huu; Kwa baada ya maombi haya mafupi ambayo tutakwenda kuomba pamoja amini kuwa kuna tendo linakwenda kutendeka ndani yako kuanzia huu wakati;
Tunapokwenda kuomba pamoja nataka mahali ulipo, weka mkono wako katika eneo la ugonjwa lilipo. Kisha zungumza maneno haya:
Bwana Yesu, wewe ni mponyaji wangu. Ulisema unalituma Neno lako ili uniponye(Zab 107:20).. Na pia ulisema Neno lako li hai tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga wowote ukatao kuwili (Waebr 4:12). Hivyo Bwana Yesu mponyaji wangu, naomba sasa ulitume Neno lako ndani ya mwili wangu likafanye uponyaji. Likaondoe magonjwa yote haya yanayonisumbua (yataje). Likakate kate kazi zote za ibilisi zilizopangwa ndani ya mwili wangu. Nikawe mzima kabisa sawasawa na maneno yako uliyosema katika Yeremia 30:17 ..kwamba utanirejesha afya yangu na kuniponya jeraha zangu. Naiita afya yangu sasa sawasawa na ahadi zako kwa jina la Yesu Kristo, nauita uzima wangu kwa jina la Yesu Kristo.
Asante Mungu wangu kwa upendo wako, na kwa uponyaji wako. Amen.
Basi ikiwa umeomba sala hiyo fupi: Hapo hapo na mimi nitakwenda kukuombea.
Ee Mungu baba, nakushukuru kwa mwanao huyu ambaye ameona msaada pekee, unatoka kwako na si kwa mtu mwingine yeyote. Baba nakuomba ikiwa ametenda dhambi iliyomstahili ugonjwa huo nakuomba Mungu wangu umsamehe, ikiwa amepata ugonjwa huo kwa nguvu za giza basi leo natangaza mwisho wake, kwa Jina la Yesu Kristo. Naomba kama mtumishi wako, umpe afya yake, ili akajue kuwa hakuna mwingine awazaye kutuokoa sisi isipokuwa wewe YEHOVA, na kwa kupitia ushuhuda huo akapate kwenda kulitangaza jina lako kuu kwa mataifa. Asante kwa uponyaji huo ambao tayari umeshaanza kuingia katika mwili wake. Amen.
Sasa kama nilivyosema, zidi kuamini kuwa tayari Kristo amekuponya. Lakini pia ikiwa bado hujaokoka, (Yaani bado hujampa Yesu Kristo maisha yako) Ni vema ukafanya hivyo sasa. Kwasababu hali nyingine haziwezi kuondoka ndani ya mtu, kama mtu mwenyewe hajaamua kukubaliana na Yule anayekwenda kumponya.
Kumbuka wokovu wa roho yako ni bora zaidi kuliko huo wa mwili wako. Ukiponywa mwili, halafu roho ikaangamia faida yake ni nini? Lakini vikiponywa vyote ni faida jumla jumla. Tukizingatia kuwa hizi ni siku za mwisho na Yesu yupo mlangoni kurudi. Hatuna muda tena kwa kuvumiliana na shetani nyakati hizi za hatari, Hivyo bila kuchelewa, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba ya kupewa maelekezo mengine >>>> SALA YA TOBA
Bwana akubariki sana.
Kama utahitaji maombezi zaidi, basi wasiliana nasi kwa namba hizi bure, +255 693036618/ +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Neno hilo italisoma katika ile habari ya Stefano alipokuwa anatumiwa na Mungu kufanya ishara na maajabu yasiyokuwa ya kawaida katika kanisa lake.
Lakini baadhi ya wayahudi wa masinagogi mbali mbali walipoliona hilo wakamchukua kuja kujadiliana naye, na baada ya kuona kuwa wameshindwa waliingiwa wivu na kufanya mambo ambayo huwezi kudhani dhehebu la dini linaweza kufanya. Sasa moja ya sinagogi hilo lilikuwa ndio hilo lililoitwa Sinagogi la Mahuru; kulikuwa na mengine pia tusome.
Matendo 6:8 Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.
9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.
11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.
12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.
13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;
Sasa ni kwanini liitwe kwa jina hilo?
Biblia haijaeleza chochote kuhusu chimbuko la sinagogi hilo mpaka wakajiita hivyo, lakini inaaminiwa na baadhi ya wanazuoni kuwa kulikuwa na kundi la wayahudi ambao walikuwa ni watumwa wa dola ya Ki-Rumi, Na baadaye wakafanywa kuwa huru, na ndipo hapo wakawa na sinagogi lao, wakaliita Sinagogi la mahuru. Yaani sinagogi la watu waliofanywa kuwa huru.
Hivyo hata kama chimbuko la jina hilo lingekuwa ni tofauti na hiyo, lakini bado jina lake ni nzuri, “Mahuru”. Lakini shida inakuja ni pale ambapo mioyo yao haiakisi jina hilo. Ni wazi kuwa watu hawa hawakuwekwa huru moyoni, kwasababu kama wangewekwa huru wasingekuwa na wivu, na wasingemzushia Stefano habari za uongo. Hiyo ni kuonyesha kuwa walikuwa ni watu walio mbali na wokovu kuliko hata watu wasiomjua Mungu kabisa.
Tunajifunza nini?
Hatushangai hata sasa kuona yapo makanisa mengi, na mikusanyiko mingi, yenye majina mazuri ya rohoni, yenye misalaba mingi, yenye kila aina ya mapambo mazuri ya rohoni. Lakini ndani yake wanazipinga nguvu za Roho Mtakatifu kama walivyompinga Stefano.
Biblia ilishatabiri katika kitabu cha 1Timotheo 3 kuwa katika nyakati za mwisho watatokea watu wengi wa namna hiyo
2Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa……….
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao”.
Unaona watakuwa wenye mfano wa utauwa lakini wanazikana Mungu za Mungu.
Huu si wakati wa kujivunia dhehebu au dini ndugu, ni wakati wa kujivunia Kristo ndani yako. Unaweza ukawa na dhehebu zuri kweli, kubwa kweli, lakini Mungu amelikataa, wewe litakufaidia nini? Tunapaswa tuutafute utakatifu kwa bidii kwasababu hatuwezi kumwona Mungu tusipokuwa nao(Waebr 12:14).
Tunapaswa tujichunge tusifanane na hawa wa sinagogi la mahuru ambao wana jina zuri lakini ni wapinga-Kristo ndani yao.
Bwana atusaidie.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Jina la Bwana wetu libarikiwe daima. Nakukaribisha katika kujifunza Maneno ya Mungu. Leo kwa ufupi tutatazama sehemu ya maisha ya Bwana wetu Yesu jinsi yalivyokuwa hapa duniani. Kama tunavyojua maisha yake ni ufunuo tosha wa kanisa la Kristo jinsi linavyopaswa liwe.
Tukisoma maandiko tunaona Bwana Yesu alitabiriwa kuwa atatokea katika uzao wa Daudi, na pia katika mji wake ujulikanao kama Bethlehemu (kasome Mika 5:1, na Mathayo 2:6), na kama tunavyojua ni kweli yalitimia kama yalivyotabiriwa, alizaliwa Bethlehemu ya Uyahudi. Lakini Yesu hakuishi katika mji huo wa Daudi (Bethlehemu) au katikati ya wazao wa Daudi, bali alikwenda kuishi katika mji mwingine mmoja mdogo huko Galilaya ulioitwa Nazareti, ulio mbali kabisa na mji wa Bethlehemu. Nazarethi uli
Mji huu ulikuwa kaskazini mwa Israeli, na ndio wa mwisho kabisa kimaendeleo kuliko miji yote iliyokuwa Israeli wakati ule, ni mji ambao haukuandikiwa unabii wowote katika biblia nzima, japo Mungu tayari alikuwa ameshautolea unabii wake kupitia vinywa vya manabii wake (Mathayo 2:23). Ni mji ambao haukuwa na watu wengi, mji ambao haukuwa machachari, mji uliosahaulika kabisa, wala hakuna mtu aliyetazamia kuwa mtu yeyote mkuu angeweza kutokea huko?
Na ndio maana utaona hata Filipo alipokuwa anamwelezea Nathanieli habari za masihi, Nathanieli alimwambia Je! Inawezekana kweli jambo jema kutokea Nazareti, Mji kama ule ambao hauna sifa yoyote nzuri, iweje Masihi atokee huko, maandiko yanatuambia masihi atatokea mji mtakatifu kule Bethelemu, Yuda, iweje utuletee habari ya kijiji hichi ambacho hata hakina sifa yoyote nzuri,
Yohana 1:46 “Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone”.
Lakini hapo ndipo mahali sahihi ambapo Mungu alipachagua mwokozi wa ulimwengu aishi kwa miaka karibia 30. Karibia asilimia 90 ya maisha ya Bwana Yesu yalikuwa katika mji huu uliosahaulika, na ndio maana utaona kila mahali watu walikuwa wanamtambulisha kama Yesu wa Nazareti (Mathayo 26:11), Hiyo yote ni kwasababu maisha yake mengi aliyaishia huko. Na sio tu watu na mitume peke wao walimtambulisha kwa jina hilo, Pilato naye alimtambua kwa jina hilo, Mapepo nayo yalimtambua kwa jina hilo..
Marko 1:23 “Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti,
24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza”?
Hata yeye mwenyewe Bwana, alijitambulisha kwa jina la mji wake siku ile alipomtokea Sauli alipokuwa anakimbilia Dameski;
Matendo 22:6 “Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
27 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?
8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi”.
Inawezekana na sisi tunamtambua Bwana Yesu kwa jina hilo, lakini tumekuwa hatujui ni kwanini tunamwita wa Nazareti, tunapaswa tujue ni kwanini iwe Nazareti na sio Bethlehemu, au Korazini, au Kapernaumu?
Mungu anataka na sisi, tujue mazingira yetu, sio sababu ya yeye kutotimiza ahadi zake juu yetu. Kuna wengine wanasema ni kwasababu nipo kijijini, laiti ningekuwa mjini ningefanya hiki au kile kwa ajili ya Mungu, hiyo isiwe sababu ndugu, mkumbuke Yesu, Yule Yesu wa Nazareti na sio Yesu wa Bethlehemu..upate kujifunza!.
Pengine utasema kwasababu nimezaliwa Afrika, ningezaliwa ulaya ningemfanyia Mungu makubwa, ndugu mkumbuke Yesu wa Nazareti.
Tusiwe na sababu zozote zile, Bwana wetu alizaliwa katika hori la kulishia ng’ombe, alikuwa maskini biblia inatuambia hivyo, aliishi katika mji usiokuwa na maendeleo yoyote. Lakini kutoka katika mji huo dunia nzima imejua kuwa yeye ni mwokozi Yule Yule aliyetabiriwa na manabii.
Hivyo na sisi katika mazingira yoyote tuliyopo, haijalishi ni mazuri au mabaya, haijalishi ni ya kisasa au ya kale, tanaweza kulikamilisha kusudi la Mungu kikamilifu, kama Mungu alivyokusudia, endapo tukiwa waaminifu kwake kama Mwokozi wetu alivyokuwa mwaminifu kwa Baba.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Katika kitabu cha Zaburi na Mithali Neno mpumbavu linatajwa sana, naomba kufahamu mpumbavu ni mtu wa namna gani kibiblia?
Biblia haielezi moja kwa moja maana ya mpumbavu, bali inaeleza tabia zinazoambatana na mtu mpumbavu, embu tupitie baadhi ya vifungu vinavyolizungumzia neno hilo na mwisho kabisa hivyo ndivyo vitakavyotusaidia kujua mpumbavu ni mtu wa nanma gani;
Zaburi 14:1 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema”.
Mithali 10:8 “Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka”.
Mithali 9:13 “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu”.
Mithali 10:14 “Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu”.
Mithali 10:23 “Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo; Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima”.
Mithali 12:15 “Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri”.
Mithali 12:16 “Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu”.
Mithali 14:1 “Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe”.
Mithali 15:5 “Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara”.
Mithali 14:16 “Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai”.
Mithali 20:3 “Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana”.
Mithali 14:3 “Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi”.
Mithali 15:20 “Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye”.
Hivi ni baadhi ya vifungu tu, lakini unaweza kuona mpumbavu ni mtu anayetajwa kuwa ana dharau, asiye na heshima, anayeropoka ropoka, asimcha Mungu, asiamini hata kama kuna Mungu, asiyetaka kurekebishwa, anayependa ugomvi, anayesambaza habari za uzushi n.k.
Na tabia zote hizi huwa zinafanya na mtu mwenye dhambi, kwasasa ni mtu ambaye hajakombolewa na Yesu.
Hivyo tafsiri hasaa ya Neno mpumbavu, ni mtu ambaye hajazaliwa mara pili.
Kwahiyo ikiwa wewe upo nje ya Kristo, haijalishi utakuwa msomi kiasi gani, au utakuwa tajiri kiasi gani, a utakuwa na ushawishi mwingi kiasi gani, wewe ni mpumbavu kibiblia, kwasababu hutakosa tabia mojawapo ya wapumbavu zinayozungumziwa katika biblia.
Ni Yesu pekee ndio mwenye uwezo wa kumgeuza mtu moyo wake na kumfanya kuwa mtu mwingine kabisa. Yeye mwenyewe alisema.. Wote wanaompokea anawapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu. (Yohana 1:12). Hii ikiwa na maana ukimkaribisha Yesu katika maisha yako, ni uhakika kuwa UWEZO huo utakuja ndani yako, wa kuweza kuzishinda tabia zote za wapumbavu, yaani kushinda ulevi, kushinda uzinzi, kushinda anasa, kushinda usengenyaji n.k..
Hivyo kwanini usimpe leo YESU maisha yako ayaokoe, na utoke kuwa mojawapo ya wapumbavu mpaka kuwa mwana wa Mungu mteule, mbarikiwa aliyeandaliwa kwa ajili ya kuurithi uzima wa milele? Ikiwa upo tayari leo kuokoka, basi fungua hapa kwa ajli ya kuongozwa sala ya Toba na kupata maelekezo mengine ya kiroho >>>>> SALA YA TOBA
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Hivi ni vifupisho vya nyakati.
K.K – Maana yake ni Kabla ya kuzaliwa Kristo Yesu. Kwa kiingereza (B.C – Before Christ)
Na
B.K - Maana yake ni Baada ya kuzaliwa kwake Kristo Yesu. Kwa kiingereza (A.D– Anno Domino- Katika mwaka wa Bwana )
Lakini mahali pengine wanatumia kifupi cha K.W.K kumaanisha K.K. na WK kumaanisha B.K. Husasani kwa watu ambao sio wakristo, au hawaamini habari za Yesu Kristo, Lakini maana ni ile ile moja.
K.W.K maana yake ni Kabla ya wakati wa kawaida. Kwa kiingereza (B.C.E – Before the common Era)
Na,
W.K Maana yake ni Wakati wa kawaida. Kwa kiingereza (C.E– Common Era)
Kwamfano unaweza kukutana na habari fulani ya historia kwa mfano inasema kitabu cha Danieli kiliandikwa mwaka 600 KK, au 600 KWK, Hiyo inamaanisha kuwa kiliandikwa miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.
Au utakutana na habari inasema Hekalu la Yerusalemu lilibomolewa mwaka 70 BK, Au 70 WW. Maana yake ni hekalu lilibomolewa mwaka wa 70 baada ya Kristo kuzaliwa duniani.
Hivyo tunaposema huu ni mwaka fulani wa 2000 + haimaanishi tangu dunia iumbwe ni miaka elfu mbili imepita hapana, bali ni miaka 2000 baada ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kabla ya hapo kulikuwa na miaka mingine mingi iliyopita, zaidi ya 4000, ambayo ndiyo inahesabika kama miaka kabla ya Kristo.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka? Je! Unahabari kuwa hatuna muda mrefu sana, mpaka unyakuo upite? Yote yaliyotabiriwa yameshatimia, na kwamba pengine kizazi chetu kitashuhudia tukio zima la mwisho wa dunia? Swali la kujiuliza je na sisi tumejiwekaje.
Ikiwa upo nje ya Kristo na unataka leo ayageuze maisha yako. Basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako. Fungua hapa kwa ajili ya Sala ya Toba na maelekezo mengine >>> SALA YA TOBA
Na Bwana akubariki sana.
Pia Tazama maana ya maneno mengine ya kibiblia chini.
Kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Hosana ni neno la kiyahudi lenye maana ya “OKOA”. Neno hili limeonekana mara ya kwanza kwenye biblia kipindi wakati Bwana Yesu anaingia Yerusalemu, ambapo wenyeji walimpokea kwa furaha, wakimwimbia na kumtukuza Mungu kwa shangwe nyingi..
Yohana 12: 12 “Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;
13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, HOSANA! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!”
Habari hiyo hiyo unaweza kuisoma tena katika Mathayo 21:9, Mathayo 21:15, na Marko 11:9-10.
Sasa swali la kujiuliza ni kwanini, Hao watu watumie hilo Neno “Hosana” na si Neno lingine lolote…labda “karibu Ee Masihi..karibu ee Masihi”..badala yake wanamkaribisha kwa kumwambia “Hosana” yaani “okoa..okoa”.
Ikumbukwe kuwa Wayahudi (yaani Waisraeli), wakati Bwana Yesu yupo duniani walikuwa wapo chini ya utawala wa kirumi.. Wakati huo dola ya kirumi ndiyo iliyokuwa inatawala dunia nzima chini ya Mfalme Kaisari aliyeko Rumi.
Kwahivyo wakati Kristo yupo duniani, Israeli ilikuwa ni koloni la hawa warumi, Ndio maana utaona pia waliomsulubisha Bwana ni askari wa kirumi. Hivyo waisraeli wote walikuwa wanalazimishwa kumpa Kodi Kaisari, na walikuwa wanamtumikia. Na kwasababu walikuwa wanayajua maandiko kwamba ipo siku Masihi (yaani Kristo), atakuja na kuwaokoa na utumwa wote na maadui zote..kama maandiko yanavyosema…katika Zekaria
Zekaria 14: 3 “Hapo ndipo atakapotokea Bwana, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita”.
Hivyo Wayahudi wote walikuwa wanaitazamia hiyo siku ambayo Masihi atakuja kuwaokoa kwa mkono mkuu. Na baadhi waliokuwa wamemwamini Yesu kama ndiye Masihi huyo kafika, hivyo wakabeba matawi ya mitende na kumshangilia na kumfurahia alipoingia Yerusalemu, huku wakimwimbia..Hosana… hosana..au okokoa…okoa!
Na wanafunzi wake pia walitazamia wakati huo ndio ulikuwa umefika au umekaribia wa wakovu, wakati wa Masihi kuwapigania na kuwarudishia ufalme..wasiwe tena koloni la Taifa lingine. Ndio maana utaona kipindi kifupi tu baada ya kufufuka kwake, walimwuliza hilo swali..
Matendo 1:6 “Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?
7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao”.
Hivyo ule haukuwa wakati wa Masihi kuwaokoa Israeli, dhidi ya utawala unaowatumikisha. Iliwapasa kwanza wakahubiri injili kwa watu wa mataifa yote kwanza, na injili itakapokwisha kuhubiriwa na watu kuokolewa, Ndipo huo wokovu mkuu kwa Israeli uje.
Hivyo utafika wakati ambapo Kristo atashuka kutoka mbinguni kwa nguvu nyingi, naye atawapigania Israeli na kuwaokoa, wakati huo injili itakuwa imeshamalizika kuhubiriwa kwa mataifa yote na unyakuo utakuwa umeshapita, na ndio utakuwa mwanzo wa utawala wa Miaka 1000 ya Yesu Kristo hapa duniani, ambapo utakuwa utawala wa Amani, na atatawala akiwa pale Yerusalemu, Israeli Pamoja na watakatifu wake aliowanyakua.
Je! Wakati huo utakuwepo Pamoja na Kristo katika utawala huo, au utakuwa jehanamu?. Maisha yako ndio jibu lako.
Kama hujaokoka Mlango wa Neema upo wazi sasa, ila hautakuwa hivyo siku zote..Ukimpokea leo Kristo, utafanyika kiumbe kipya na utakuwa na uhakika wa kuzirithi ahadi za Mungu walizoandaliwa wote wampendao.
Kama umeamua leo kumpa Kristo Maisha yako basi fuatilisha sala hii ya toba hapa >> SALA YA TOBA.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Watu wa mataifa mengine yote ya ulimwengu tofauti na Taifa la Israeli, ndio wanaojulikana kama “watu wa Mataifa”.
Mungu alipoanza mpango wake wa kurejesha uhusiano wake na mwanadamu ambao ulipotea tangu pale Edeni, alianza na Taifa moja tu lijulikanalo kama “Israeli”, Na Taifa hili lilianza na mtu mmoja ajulikanaye kama Ibrahimu, ambaye huyu Ibrahimu akamzaa Isaka,.Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akazaa Watoto 12, na kwa kupitia majina ya Watoto hao ndipo yakazaliwa majina ya makabila 12 ya Israeli. Na hao Watoto wakazaa wana, na hatimaye likawa jeshi kubwa la watu wengi wa jamii ya Israeli, na kuwa Taifa.
Sasa watu wengine wote tofauti na uzao huo wa Ibrahimu, ndio watu wa mataifa. Kwasababu duniani kulikuwa na watu wengine wengi wa jamii nyingi, walikuwepo waMisri (ambao ndio sasa nchi ya Misri), walikuwepo waashuri (Ambao kwasasa ni maeneo ya Syria), walikuwepo wakushi (ambao sasa ni maeneo ya huku Afrika)..walikuwepo Wakaldayo (ambao sasa ni maeneo ya Iraq), walikuwepo watu wa bara la Hindi (ambao sasa ndio India), walikuwepo watu wa Uajemi na Umedi ambao ndio kwasasa maeneo ya (Kuwait,Qatar, UEA{Dubai} na sehemu za magharibi ya Saudi Arabia), walikuwepo Warumi (ambao sasa ndio Italy), walikuwepo Wayunani (kwasasa ni Ugiriki) na mataifa mengine mengi (Yote hayo yalijulikana kama Mataifa).
Sasa Mungu amekuwa akitembea na Taifa la Israeli pekee Kwa miaka Zaidi ya 1,500, wakati huo wote Mungu hakushughulika na hayo mataifa mengi yote (haijalishi yalikuwa yameendelea kiasi gani au yalikuwa yana watu wazuri kiasi gani). Taifa lake teule na pekee lilikuwa ni moja tu ambalo ni Israeli, ndio maana utaona Amri 10, walipewa Israeli na si watu wa Mataifa mengine, na agano lote la kale inahusu Habari za wana wa Israeli mwenendo wao na Mungu wao.
Sasa sio kwamba Mungu alikuwa hana mpango kabisa na watu wa Mataifa!. La! Alikuwa ana mpango nao mkubwa sana. Lakini siku zote hakiwezi kuzaliwa cha pili, kabla ya kuzaliwa cha kwanza, hawezi kunyonya mtoto wa pili kabla hajanyonya wa kwanza, hawezi kukumbatiwa mtoto wa pili kabla ya wa kwanza. Hata mama anayejifungua Watoto, ni lazima azaliwe mtoto wa kwanza, ndipo afuate wa pili… Na yule wa kwanza atapendwa na kutunza kabla ya yule wa pili.
Kwahiyo Taifa la Israeli ni mzaliwa wa kwanza kwa Mungu, na watu wa mataifa ni mzaliwa wa pili..
Kutoka 4: 22 “Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;
23 nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako”.
Hivyo ulipofika muda wa “mzaliwa wa pili kuzaliwa, (yaani wakati wa watu wa mataifa nao kukumbukwa na Mungu). Mungu alianza mpango wake huo kwa kumleta Mwanawe mpendwa Yesu Kristo, awe sababu ya wokovu kwa watu wote wa mataifa.
Kama kuku aliyeacha vifaranga vyake vya kwanza, kwa kuvidonoa na kuanza malezi mapya ya uzao wa pili, Ndicho alichokifanya Mungu kwa Israeli, Neema iliondoka kwao na kuhamia kwa watu wa mataifa (yaani mimi na wewe).
Warumi 11:25 “ Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili”.
Tangu wakati wa Bwana Yesu mpaka sasa, watu wa mataifa yote..tunaweza kumkaribia Mungu, na kuzirithi baraka zile zile za rohoni, kama walizokirimiwa Israeli.
Hiyo ndiyo SIRI YA MUNGU, ambayo ilifichwa kwa miaka mingi, ambayo hata wana wa Israeli wenyewe hawakujua kwamba ingefika siku moja, watu wa Mataifa nao watapata upendeleo kwa Mungu kama wao.
Paulo ambaye ni Muisraeli aliiandika siri hiyo kwa ufunuo wa Roho na kusema..
Waefeso 3:4 “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.
5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
6 YA KWAMBA MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI WA URITHI MMOJA, NA WA MWILI MMOJA, NA WASHIRIKI PAMOJA NASI WA AHADI YAKE ILIYO KATIKA KRISTO YESU KWA NJIA YA INJILI”.
Hivyo tangu Bwana Yesu aondoke duniani, imepita Zaidi ya miaka 2,000 kipindi kirefu Zaidi ya kile Mungu alichotembea na wana wa Israeli peke yao.. Maana yake ni kuwa kipindi cha Neema kwetu sisi watu wa mataifa nacho kinaenda kufikia ukomo. Na kitafikia ukomo kwa unyakuo.
Unyakuo ukishapita mlango wa Neema unakuwa umefungwa kwa watu wa Mataifa. Mungu atawarudia tena watu wake Israeli kwa kipindi kifupi sana cha juma moja ambalo ni sawa na Miaka 7, baada ya hapo, hukumu ya mataifa itaanza na Utawala wa amani wa Yesu Kristo wa miaka elfu.
Je umempokea Kristo?..Upo ndani ya neema?. Kama bado upo nje, basi jua umechelewa sana..hivyo usiendelee kupoteza muda, ingia ndani ya neema uisalimishe roho yako. Yesu anakupenda na alikufa kwa ajili yako.
kumbuka pia, watu wote ambao hawajaokoka, katika agano letu jipya huitwa watu wa mataifa,
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Nabii Elisha alikuwa ana maana gani kulia na kusema”Gari la Israeli na wapanda farasi wake”?
Kuota upo nchi nyingine.
Kama tunavyojua ukisafiri mahali ambapo ni tofuati na makazi yako ya asili, utakutana na mabadiliko mengi sana, hususani pale unapovuka mipaka na kuingia katika nchi nyingine, si ajabu kukutana na hali ya hewa ya aina nyingine, kukutana na watu wa jamii nyingine, kukutana na lugha gheni, n.k..
Na hiyo itakufanya usijione upo huru sana kama ulivyokuwa katika nchi yako mwenyewe.Na wakati mwingine inaweza kukufanya ujione haupo sehemu salama sana, kwasababu sio nchi yako, na haujaizoea.
Wana wa Israeli walipokuwa wanachukuliwa utumwani kupelekwa Babeli, wakiwa njiani walilia sana, hata wale wakaldayo,walipowashurutisha wawaimbie nyimbo za nchini mwao walikataa, wakasema tutaimbaje wimbo wa Bwana nchi ya ugenini?
Zaburi 137:1 “Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2 Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.
3 Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
4 Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni”?
Kwasababu walijua kabisa wanakwenda katika nchi ambayo sio ya kwao, katika mazingira ambayo hawajayazoea. Kwenye tamaduni mpya,
Hivyo unapojiona kwenye ndoto upo katika nchi ya ugenini, unaishi huko, au unatembea, Yapo mambo mawili hapo ambayo Mungu anakuonyesha.
Jambo la kwanza; Ikiwa wewe umeokoka, (yaani umeokolewa na Bwana Yesu), Hapo ni Mungu anakuonyesha wazi jinsi itakavyokuwa pale utakapotoka katika hifadhi yake. Utakuwa kama mtumwa, hivyo, jiangalie na jithibitishe, zidi kukaa katika mapenzi ya Mungu na kama ulikuwa umeshaanza kupoa, basi mgueukie Mungu wako kwa moyo wako wote. Ili ubakie katika nchi yako ya wokovu aliyokukusudia.
Lakini ikiwa hujaokoka, ni Mungu anakuonyesha hali yako ilivyo leo hii, upo katika nchi ya ugenini, japo hustahili kuwepo huko. Maisha yako yapo ugenini, hivyo huwezi kuwa huru, huwezi kuwa na amani, haijalishi pataonekana ni pazuri namna gani, Wana wa Israeli walilia, walipokuwa wanaenda ugenini. Hivyo na wewe pia uliye dhambini, upo ugenini, pengine kampani unazotembea nazo sio ambazo Mungu amekukusudia utembee nazo, Mungu anakuhitaji wewe ukae na watakatifu wenzako uyatafakari maisha ya mbinguni. Pengine ulevi, anasa, wizi n.k., sivyo ambavyo vinakupasa mtu kama wewe, na hilo unalijua kabisa, lakini bado unashikama nalo.
Embu yatafakari maisha yako, Je! Tangu ulipokuwa katika maisha ya dhambi ni raha gani umeipata au faida gani umepata?. Kwanini usizingatie kurudi nyumbani, kama yule mwana mpotevu aliyekwenda kuponda mali katika nchi ya mbali, lakini baadaye akazingatia kurudi kwa baba yake..Kwanini na wewe usizingatie kurudi kwa Baba yako wa mbinguni leo umwombe msamaha baada ya kupotea kwa muda mrefu.?
Ukisoma biblia utamwona Kaini yule aliyemuua ndugu yake ndiye aliyekuwa mtu asiye na kikao duniani, kama vile mapepo. Je na wewe unataka uwe mtu asiye na makao yake maalumu?
Leo hii ukikubali kutubu dhambi zako, Yesu atakupokea na kukusamehe, haijalishi wewe ni wa dini gani au dhehebu gani. Atakupokea, na kukukaribisha kwake, na atakupa raha nafsini mwako. Hivyo Kama upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya maelekezo ya sala ya Toba, na Bwana akubariki. >>> SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312/
Pia kwa ushauri/ratiba za ibada/ maombezi.
Jiunge kwenye magroup yetu ya Whatsapp kwa masomo ya kila siku ya Neno la Mungu.
Jiunge na channel yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Sodoma ipo nchi gani?
Sodoma na Gomora ni miji iliyokuwa katika nchi ya Kaanani (Ambayo ndio Israeli ya Sasa). Miji hii miwili ni moja kati ya miji mitano iliyokuwa katika bonde la Yordani..mingineyo ikiwemo, ni Adma, Seboimu, na Lasha.
Kama tunavyoijua habari, miji hii miwili (yaani Sodoma na Gomora) ndiyo iliyokuwa kiini cha maovu yote katika bonde hilo.
Mwanzo 19:24 “Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana.
25 Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile”.
Hata hiyo mingine nayo haikupona, nayo pia iliangamizwa;
Kumbukumbu 29:23 “ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua Bwana kwa ghadhabu yake na hasira zake”;
Lakini ni tahadhari gani tunapaswa tuchukue tunaposoma habari ya miji hii miovu?
Licha ya kuwa ilikuwa ni miovu lakini biblia inatuambia ilikuwa ni miji yenye kuvutia sana, mfano wa Edeni, Bustani ya Bwana soma (Mwanzo 13:10). Mfano tu wa dunia ya sasa. Ulimwengu wa sasa umejengeka na unavutia kuliko ule wa zamani,hilo lipo wazi, starehe za wakati ule haziweki kulinganishwa hata kidogo na starehe za wakati huu, lakini maovu yake ni zaidi ya yale ya Sodoma na Gomora.
Ushoga sio jambo la kushangaza tena, kiasi kwamba nchi zimefanikiwa kuhalalisha jambo hilo, na sehemu nyingine mpaka kwa yanayoyaita makanisa (ambayo kiuhalisia si makanisa), yamevuka mpaka huo na kuhalalisha ushoga bila hata kuogopa kumuhusianisha Mungu na matendo kama hayo maovu. Hiyo ni kuonyesha kuwa mwisho wa huu ulimwengu upo karibuni sana. Wapo watu wanajidanganya kuwa hii dunia haitaangamizwa, kwasababu Mungu alishasema hivyo wakati ule wa Gharika kuwa hatagharikisha.. Lakini hawajui kuwa ni kweli Mungu hatauangamiza huu ulimwengu kwa maji, lakini amesema ataugharikisha moto. Ambapo kila mtu mwovu, na kila kitu kitafumuliwa, biblia inasema hivyo soma.
2Petro 3:7 “Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu……..
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka”?
Unaona? Swali la kujiuliza ni je! Sisi tumejiwekaje? Katika kipindi hichi cha mwisho? Je na sisi tutapumbazwa na Ulimwengu huu kama Lutu na mke wake? Tukaacha kubaki mahali Mungu alipotuweka tukaenda kushikamana na mambo ya ulimwengu huu yanayodanganya?. Huu ni wakati wa kujiokoa nafsi yako, na si wakati wa kumwangalia ndugu, au rafiki, au mjomba anasemaje, kwasababu mwisho upo karibu.
Je umeokoka?
Kama bado na upo tayari kufanya hivyo leo, huo ni uamuzi wa busara sana kwako, kama upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba, na maelekezo mengine >>>> SALA YA TOBA
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Israeli ipo bara gani?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Shalom!. Karibu tuyatafakari pamoja maandiko.
Elimu yoyote ile ya kidunia ni hekima..hekima sio tu kujua Nahau, na misemo na methali. Mtu anayekwenda kusoma elimu fulani labda ya uchumi au udaktari, anaingiza hekima ndani yake ya namna ya kumtibu mtu au namna ya kufanya biashara. Kadhalika na Elimu nyingine zote mtu anazokwenda kuzisomea, anakuwa anajiongezea hekima katika nyanja hiyo anayokwenda kuisomea.
Sasa fomula ya kujiongezea maarifa katika mambo ya kidunia, haina tofauti sana na ile ya kujiongezea hekima katika mambo ya kiMungu. Tunapomwomba Mungu atupe hekima na maarifa katika kumjua yeye, haitakuja tu kwa kumwomba na kisha kukaa kusubiri, hapana!..Bali inakuja kwa kumwomba kwanza, na kisha kwenda kuitafuta.. Unapokwenda kuitafuta kwasababu ulishamwomba Mungu, anachokifanya yeye ni kuifanikisha njia yako katika kwenda kuitafuta…anakupa uwezo wa kuelewa kiwepesi zaidi kuliko kama ungekuwa hujamwomba.
Ni fomula ile ile tu ya mwanafunzi anayemwomba Mungu amfanikishe katika masomo yake, hawezi kuomba Mungu ampe uwezo wa kuelewa na kufanya vizuri katika mitihani na huku ameacha kusoma kabisa, hapo hatapata chochote, lakini kama amemwomba Mungu kwa Imani, na kwenda kusoma ndipo akili yake inaongezewa uwezo mara dufu zaidi ya kuelewa tofauti na yule mwanafunzi ambaye hajamwomba Mungu kabisa.
Na pia katika kuitafuta Hekima ya kiMungu ni hivyo hivyo, Tunapomwomba Mungu atupe hekima ya kiMungu sawasawa na Yakobo 1:5, hatupaswi kusubiri tu!..Ni wakati wa kuiweka imani katika matendo baada ya hapo..kwa kwenda kuanza kulisoma Neno lake kwa bidii na kumtafuta yeye kwa bidii zote, na kwa nguvu zote.
Mathayo 22:37 “Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza”
Ukianza kuweka bidii katika kumjua Mungu, kwa moyo wako wote kiasi kwamba moyo wako wote upo kwake, na unatumia akili zako zote ulizopewa na Mungu katika kumtafuta yeye, na kuifanya kazi yake, na pia unatumia nguvu zako zote Mungu alizokujali za kimwili na kiroho..Hekima ya kiMungu itazidi kuingia ndani yako, na utakuwa unazidi kumjua Mungu na kuwa na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kwa kadri siku zinavyozidi kwenda.. Bwana ataisafisha njia yako na utakuwa na hekima nyingi.
Utauliza vipi na Sulemani, na yeye aliipata hekima kwa njia hiyo hiyo?
Jibu ni ndio!..Sulemani baada ya kumwomba Mungu hekima, hakukaa tu na ghafla akaanza kujikuta anaelewa mambo…La! hakufanya hivyo, kinyume chake baada ya kumwomba Mungu hekima, alianza kutafuta huko na huko kwa kusoma mambo mengi ya kiMungu na kimaisha, ndipo hekima ikaingia ndani yake, Mungu akamsaidia kupata alichokiomba…Maandiko yanasema hivyo katika mstari ufuatao..
Mhubiri 12: 9 “Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi.
10 Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli”.
Huyo ni Sulemani, ambaye baada ya kuomba hekima, akajikita katika kwenda kuitafuta huko na huko, akajikita katika kutafakari sana..na alipopata uelewa wa mambo ndipo akazitunga mithali..Na alikuwa akitafuta kuelewa mambo KWA KUSOMA VİTABU VİNGİ, na kufanya utafiti mwingi, na alikuwa mpaka anachoka mwili kwaajili ya kusoma tu. Mpaka akasema “Kusoma sana kwa uchosha mwili”..
Mhubiri 12: 12 “….. hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; NA KUSOMA SANA HUUCHOSHA MWİLİ”
Je! Wewe ulishawahi kuzitafuta habari za Mungu kwa bidii namna hiyo mpaka Mwili ukachoka?..na uchovu anaouzungumzia hapo na Sulemani sio uchovu wa usingizi (maana kuna mtu atasoma Neno dakika 10 na kusikia usingizi, na mwisho akasema amechoka..Hapo! hujachoka! Bali umekuwa mvivu). Uchovu unaozungumziwa hapo na Sulemani ni kama ule mwanafunzi anaochoka wakati karibia na anapohitimu, baada ya kusoma miaka mingi. Pale ambapo kichwa chake kimejaa maarifa ya kutosha ya kuweza kukabiliana na mtihani wowote unaokuja mbele yake, lakini mwili wake umekuwa dhaifu kwa kuihangaikia hiyo elimu, alipokuwa akijitesa na kujizuia kwa mambo mengi ilimradi tu aipate hiyo elimu.
Bwana atusaidie nasi tuwe kama Sulemani, na tumpende Bwana Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, kwa akili zetu zote, na kwa nguvu zetu zote, ili tuweze kuipata hekima ya kiMungu ndani yetu…
Mithali 2:10 “Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako”.
Kama hujaokoka, Kristo yupo mlangoni, hizi ni siku za mwisho, na wokovu ndio mwanzo wa hekima..Hivyo mpokee Kristo leo kwa kumwamini na kutubu dhambi zako zote, na kubatizwa. Naye atakukubali, kama alivyosema katika Neno lake.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume, maana yake nini?