Siku zote Mungu akitaka kumuokoa mtu neema yake huwa anaizidisha sana kwa kiwango cha juu kiasi kwamba kwa nje ni rahisi kuona kama anatumia nguvu, au analazimisha ndivyo ilivyokuwa kwa Lutu na mke wake na watoto wake… Wale malaika wawili walipoona wanachelewa chelewa, wanakawia kawia waliwashika mikono yao na kuwavuta mpaka nje ya mji kwa nguvu kwa jinsi Mungu alivyowahurumia…
Mwanzo 19: 15 “Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu.
16 Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.”
Lakini tendo hilo la kushikwa mikono halikuendelea milele walipofikishwa tu nje ya ule mji, wameshajua sasa yawapasayo kufanya jambo lililofuata waliambiwa..jiponyeni nafsi zetu msigeuke nyuma..Lakini Mke wa Lutu alijiharibia.
Mwanzo 19:17 “Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea”.
Ndugu, picha hii inatuonyesha kuwa wokovu ni tendo la neema kubwa sana, kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kujiokoa mwenyewe kwa nguvu zake…Na ndio maana Mungu aliona malaika hawatoshi kuja kutuokoa sisi na hukumu hiyo kubwa inayokuja huko mbele, badala yake akaamua kumtuma mwanawe kabisa , YESU KRISTO, ili aje kutuvuta sisi mbali na ile hukumu ya siku za mwisho na ziwa la moto…Yeye ndiye anayetushika mkono na kutuvusha kutoka katika ulee mji wa mauti na kutupeleka sehemu salama..
Lakini ikiwa ameshatuweka sehemu salama mbali na dunia, ni wajibu wa kila mmoja kuuthamini wokovu ule kwa kukimbia mbali zaidi na dhambi kama ilivyokuwa kwa Lutu na watoto wake..Ikiwa tulishaona mkono wa Mungu ulivyotuepua kutoka katika dhambi, hatupaswi kujilegeza tena, kusubiria tena neema itutoe kwenye dhambi tunazozitenda kwa uzembe wetu.. Tukishafikia hii hatua ni wakati wa kuziponya nafsi zetu…
Lakini embu tumtafakari mke wa Lutu ambaye ni mfano wa wale waliookolewa ambao mioyo yao bado ipo ulimwenguni, yeye alipogeuka nyuma alikuwa nguzo ya chumvi, unaweza kujiuliza ni kwanini awe nguzo ya chumvi na sio kitu kingine chochote labda tuseme nguzo ya mti, au ya chuma, au ya udongo?..Chumvi ni kiungo cha kipekee sana ambacho huwa kinadumu milele, yaani ukiihifadhi chumvi vizuri leo kwenye chupa mtu anatakaye kuja kuzaliwa miaka milioni moja mbele ataitumia na ikawa na ubora ule ule..
Na ndio maana Mungu sehemu nyingine alikuwa analifananisha Agano aliloingia na Daudi pamoja na wana wa Israeli kama agano la Chumvi, ikimaanisha kuwa ni agano la milele soma..
2Nyakati 13:5 “je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?”
Soma tena Hesabu 18:19..
Hivyo lile lilikuwa ni agano la kukataliwa milele kati yake na mke wa Lutu.. Hata sisi leo hii, ikiwa Bwana Yesu alishatuokoa, halafu tunauchezea wokovu wetu, leo tunaenda mbele, kesho tunarudi nyuma…hatuthamini ondoleo la dhambi tulilopewa siku ile tulipotubu bure, ..na wema wake wote Mungu aliotutenda, hatuoni kama kuokolewa kule ni jambo la bahati sana ambapo sio watu ulimwenguni wanaweza kupewa neema hiyo badala yake mguu mmoja kwa Kristo na mguu mwingine kwa shetani Tujue tu tupo hatarini kuwa MAWE YA CHUMVI katika roho..
Yaani Mungu kuingia na sisi agano la rohoni la milele kuwa hatukustahili kuokolewa na yeye, na matokeo yake ni kuwa safari yetu ya wokovu inakuwa imeishia pale pale, tunakuwa tumekufa,japo kwa nje tunaonekana tupo hai..Kumbuka hilo ni agano la milele, maana yake ni kuwa Mungu hatakaa akupokee wewe tena milele kwasababu ile nguvu ya kukuvuta kwake inakuwa haipo tena…utaendelea na ubaridi wako, mpaka siku unakufa ili uishie katika ziwa la moto..mifano hiyo ipo duniani leo hii, utakuta mtu alianza vizuri na Bwana, wengine hata walitokewa kabisa na malaika, wengine walisikia sauti ikizungumza nao, wengine wakaonyeshwa maono, wengine Mungu akawa anawapa chochote waombacho katika hatua za awali kabisa za wokovu wao, wengine wakaepushwa na hatari nyingi kimiujiza, wakajua kabisa sasa hapa safari imeanza..Lakini kwa tabia zao za kuyarudia rudia yale yale machafu ya nyuma kwa kipindi kirefu hiyo ikawafanya wageuke kuwa mawe ya chumvi..Ambao ndio hao leo hii huwezi kuamini hata kama walishawahi kumjua Kristo…
Wokovu sio jambo la kujaribu, na ndio maana biblia inatuambia..
Wafilipi 2:12 “………..utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
2 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
Ikiwa ni wewe mmojawapo ndugu yangu unayesoma haya, na ndani yako bado kuna kanuru kadogo ambacho kanakaribia kuzima… basi usikubali izime kabisa…ni vizuri ukatubu kwa kumaanisha kabisa mbele za Mungu sasahivi, na kuacha kwa moyo wako wote mambo maovu yote unayoyafanya kwa vitendo, na kumfuata Kristo, neema hii bado ipo juu yako na ndio maana unasikia ndani yako kuhukumiwa unaposoma haya,….huyo ni Roho Mtakatifu anakuvuta kwake tena, anza kugeuka na kupiga hatua mbele, usipoitii hiyo sauti itafika kipindi hutaisikia tena ndani yako, utakuwa ukipita mahali na kukutana na maneno kama haya utaishia kudhihaki na kukejeli, lakini sasa kuna hofu ndani yako kiasi kwamba unaogopa hata kusema neno lolote la kejeli, hiyo hofu ni ya thamani na ya muhimu sana, na ndio inayokuvuta utubu,
Hivyo Tubu leo acha kwenda disko, acha ulevi, mrudie mke/mume wako, acha wizi, acha rushwa, acha kila aina ya dhambi unayoifanya maishani mwako na wala usigeuke nyuma kama mke wa lutu..…hizi ni siku za mwisho..Siku yoyote unyakuo unapita, na hii dunia inakwenda kuwa jivu, Maisha yatasimama…kilichosalia kwako sasa ni nini kama sio kuyasalimika maisha yako kwa Bwana Yesu ayaokoe, naye atakupokea kwasababu anakupenda na kukuhurumia…dini yako ya kiislamu haitakupeleka popote, dini ya kikristo haitakupeleka popote, dhehebu lako mashuhuri halitakupeleka popote bali YESU KRISTO pekee ndiye atakayekupeleka sehemu salama..
Hivyo Ikiwa upo tayari leo hii kuanza tena upya na Bwana..
Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako.
Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Zingatia hayo na Bwana atakuwa pamoja na wewe daima. Ubarikiwe sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.
Yesu Kristo Bwana wetu…Amefufuka kweli kweli..
Kila tukio lililokuwa linatendeka wakati wa kusulubiwa kwa Bwana Yesu, wakati wa kuzikwa kwake na wakati wa kufufuka kwake lilikuwa na makusudi maalumu na lilikuwa lina ufunuo mkubwa sana..Hakuna tukio hata moja lililokuwa linatokea kwa bahati mbaya au nje ya mpango wa Mungu.
Mpaka tukio la Bwana Yesu kubeba msalaba wake kuelekea Goligotha huku akiwa na majeraha mwili mzima ni tukio ambalo lilikuwa tayari limeshatabiriwa… “lilifananishwa na kondoo anayepelekwa machinjoni”
Isaya 53:7 “Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake”.
Tukio la Bwana kuchomwa mkuki ubavuni lilishatabiriwa (katika Zekaria 12:10), na lilikuwa linamaana kubwa katika roho na katika mwili..Katika Roho lilifunua utakaso wa damu na maji,. Kwa damu yake tunatakaswa dhambi zetu na kupata msamaha kabisa kabisa..na katika maji tunatakasika kwa Neno la Mungu (Waefeso 5:26)..
Na Kusudio lingine la kimwili, Bwana kuchomwa mkuki ubavuni wakati akiwa pale Kalvari..Ni kuhakiki kifo cha Bwana Yesu..Asingechomwa mkuki ubavuni watu wangesema alishushwa pale msalabani akiwa bado hajafa vizuri, na alipokwenda kupelekwa kaburini alikuwa hajafa vizuri hivyo uzushi mkubwa wa uongo ungezushwa wakati wa kufufuka kwake..
Kwahiyo Mungu wa mbingu na nchi alilijua hilo ndio maana akaruhusu wamchome mkuki Ubavuni ili wahakiki wenyewe kwamba amekufa…kwasababu katika hali ya kawaida hakuna mtu atakayeweza kuchomwa mkuki wa ubavu ukaingia mpaka ndani ya moyo halafu akabakia kuwa hai. Warumi walikuwa wanatumia njia hiyo kummalizia mtu ambaye hajafa vizuri.
Vivyo hivyo tukio la Pilato kuandika anwani kwa lugha tatu juu ya msalaba wa Bwana Yesu, tukio hilo halikuwa la bahati mbaya bali lilikuwa na maana kubwa sana katika roho..Kwani lilikuwa ni unabii kwamba siku zijazo Kristo atahubiriwa na kutangazwa kwa mataifa yote na kwa lugha zote.
Yohana 19:19 “Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.
20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa KIEBRANIA, NA KIRUMI, NA KIYUNANI.
21 Basi wakuu wa makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi.
22 Pilato akajibu, Niliyoandika nimeyaandika”.
Baada ya siku chache, siku ile ya Pentekoste…wale walioshukiwa na Roho Mtakatifu..walisikika wakinena kwa lugha mpya za mataifa yote yaliyokuwa yanajulikana duniani. Ikimaanisha kuwa wakati umefika habari za kufa kwa Yesu na kufufuka kwake kuhubiriwa ulimwenguni kote kwa kila lugha, na kila jamii ya watu. Tangu huo wakati injili ilianza kusambaa ulimwenguni kote. Wakati huo zilikuwa tu hizo lugha tatu maarufu duniani, kiebrania, kirumi na kiyunani…Lakini leo tuna lugha Zaidi ya elfu 6 duniani…Na katika hizo zote Kristo kashatangazwa.
Kadhalika kwanini Bwana alipowekwa kaburini liliwekwa jiwe kubwa kulifunga kaburi na juu ya jiwe hilo pakawekwa muhuri? ambapo kazi ya muhuri huo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kaburi limefungwa lote kisawasawa hakuna nafasi ya kupenya mtu au kitu chochote kile kuingia ndani. Na jiwe lile lilikuwa ni la uzani mkubwa sana..halikuwa kama yale yanayoonekana kwenye tamthilia..lilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba ilihitajika kukodi wanaume kadhaa kulisogeza..Ndio maana wale wanawake pamoja na idadi yao kuwa kubwa siku ile ya kwanza ya juma walipokuwa wanakwenda kaburini bado walihitaji mtu/watu wa kuwasaidia kulisogeza lile jiwe..
Marko 16: 2 “Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;
3 wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?
4 Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno.”
Na malaika yule hakuliviringisha jiwe karibu na mlango kama filamu zinavyoonesha…bali liliviringishwa mbali na kaburi.
Luka 24:1 “Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
2 Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi”
Unaona ni mbali na kaburi..na si mbali na mlango …Ikiwa na maana kuwa lile jiwe lilihama kabisa kutoka katika yale mazingira ya makaburi.…jiwe walilikuta mbali kabisa, mahali ambapo hawakulitegemea…mahali ambapo si mazingira kabisa ya kusogezwa na mtu.
Kwahiyo Mungu aliruhusu liwe jiwe kubwa litumike, ili litakapoviringishwa mbali na kaburi..watu waamini kwamba hakika kuna kitu cha kimiujiza kimetendeka pale kaburini. Ni kweli Yesu kafufuka.
Na pia aliruhusu wale walinzi wawili wamwone yule malaika akishuka mbinguni kama umeme na waende kutoa habari za kufufuka kwake kwa wakuu wa makuhani (Mathayo 28:1-4)..maana pasingekuwepo mashuhuda upande wa makuhani pia, kungezuka uzushi mkubwa Zaidi ya ule uliozuka pale.
Sasa mambo hayo yote yalitokea ili sisi (mimi na wewe) tuamini kwamba ni kweli Yesu alisulubiwa, akafa na akafufuka kutoka katika wafu. Ukiamini hivyo leo hii basi utaokoka..Kama umeshawishika leo kuamini kwamba Kristo yupo hai leo, hayupo kaburini na kwamba anaweza kukuokoa maisha yako na wewe ukafufuka katika wafu… basi unachopaswa kufanya ni kutubu dhambi zako zote leo na kumwomba rehema..ulikuwa katika dhambi yeye anataka akusafishe na kukutakasa kwasababu anakupenda…
Upendo wake haupimiki wala haulinganishiki na kitu chochote..yupo tayari kukusamehe haijalishi umetenda dhambi ngapi kubwa..yeye atakusamehe zote na kusahau kabisa..na mbele zake utaonekana kama hujawahi kutenda dhambi kabisa….Sasa unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE,
NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithibitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, kama ulikuwa mwasherati usifanye tena uasherati, ulikuwa ni mtazamaji wa picha za ngono mitandaoni usifanye hivyo tena, ulikuwa mwizi, mtukanaji, mla rushwa, mtoaji mimba, muuaji, msagaji, mlawiti..usifanye hayo mambo tena…Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo namna hiyo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwabudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la BWANA YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Mungu akubariki, katika uamuzi wako wa busara unaoufanya..(huo ni uthibitisho wa kuamini kwamba Kristo amefufuka kweli kweli).
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Kwanini Mungu aliikubali sadaka ya Yeftha ya kumtoa binti yake kafara?
Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?
Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili, tunasoma pale Mungu alimlaani, na kumwambia.. “utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani”… Lakini tujiulize ni kwanini Mungu hakumrudishia Kaini mapigo ya uuwaji kama aliyoyafanya kwa ndugu yake badala yake akamwambia atakuwa mtu asiyekuwa na kikao duniani?.
Mwanzo 3:13 “Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua”.
Ndugu ni heri Mungu akuue, iishie hapo kuliko akuambie utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani..
Sasa unaweza kutafsiri kwa nje kwamba laana hiyo ilimaanisha kuwa Maisha yake yote Kaini yatakuwa ya umaskini, atakuwa mtu atakayekosa mahali pa kulala, atakuwa omba omba, atakuwa mtu wa mitaani tu, lala hoi asiyekuwa na kitu au uelekeo wowote wa maisha…
Lakini sivyo hivyo Mungu alivyomaanisha kwa Kaini, angalia vizuri utagundua kuwa baada ya kutoka tu pale Kaini ndiye aliyekuwa na mafanikio makubwa sana kuliko hata ule uzao wa Sethi uliochukua mahali pa Habili. Mwanzoni tu pale tunaona alijenga mji mkubwa akauita Henoko jina la mwanawe(Mwanzo 4:17). Na tunaona pia uzao wake baada ya hapo, ulikuwa Hodari, ndio uliokuwa na ugunduzi wa hali ya juu wa teknolojia, vitu kama chuma na shaba zilianzia kwao.. Hivyo kwa ufupi Kaini alikuwa na mafanikio makubwa kuliko hata uzao wa Sethi tukizingumzia kwa namna ya kimwili…
Lakini bado laana ile ya Bwana kuwa atakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani ilikuwa juu yake..?
Sasa kama sio hivyo basi Mungu alimaanisha nini?. Sikuzote tunajua mtu mtoro asiye na kikao(makao) ni mtu ambaye hajapata pumziko lolote maishani mwake la kudumu..na ndio maana wanasema moja ya mahitaji makuu matatu ya mtu ni pamoja na kuwa na malazi, au makazi, ukikosa mahali pa kutulia, unakuwa kama mkimbizi ambaye Maisha yake sikuzote hayana pumziko, leo hii upo hapa kesho upo kule, kila mahali kwako sio kwako, ni mgeni daima..
Hivyo Mungu alivyomwambia Kaini kuwa atakuwa mtoro na mtu asiyekuwa na makao, alikuwa anazungumzia hali yake ya rohoni jinsi itakavyokuwa, Maisha yake yote atakuwa ni mtu wa kutafuta lakini hatopata makazi ya kustarehe ya nafsi yake….hatapata pumziko la moyo wake daima..hatopata, hata atufuteje hatoona atakuwa ni huko na kule, wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo wa kila aina ya undanganyifu … jambo ambalo halikuonekana kwa Sethi na uzao wake, wao utaona tu muda mchache baada ya kumzaa mtoto wake Jina la Mungu lilianza kuitwa kwa nguvu.
Mwanzo 4:25 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.
26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana”.
Unaona? Muda mfupi tu uzao wa Sethi ulitambua ni wapi pumziko lipo, na haraka sana likayaendea makao ya kudumu ya roho zao.. Lakini uzao wa Kaini uliendelea kutangatanga na ulimwenguni na humo humo ndipo uchawi ukazaliwa, uovu ukazaliwa, uvuguvugu ukazaliwa, udunia ukazaliwa..n.k.
Hata leo hii, uzao wa Kaini na Sethi unajitambulisha kabisa kwa kazi zake..makundi yote mawili yapo duniani leo hii, lipo ambalo limeshatambua makao yao ya kudumu yapo wapi..Hawa ndio wale waliompokea Yesu Kristo na kupokea lile pumziko la kweli la nafsi zao.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Utawagundua kwa tabia zao, hata wakipitia dhiki, au shida, au misiba, au adha, hawapepesuki, kwasababu wanajua tayari yanayo makao yao ya kudumu milele mbinguni…hawana hofu ya Maisha kwasababu wanaye Kristo ndani yao….Amani ya Kristo inawatawala siku zote kwasababu walishampokea.
Lakini uzao ule mwingine wa Kaini kwasababu umeshalaaniwa ndio ule hautaki kumfuata Mungu japo unajijua kabisa unahitaji msaada wa nafsi zao..Huu upo buzy sikuzote kutafuta pumziko la nafsi zao katika kila wanachokiona, kama vile Kaini….Wana wa Kaini walioa wake wengi, na hawa wanatafuta pumziko kwa kuongeza idadi ya wake, (Mwanzo 4:19) na wakati mwingine kuacha wale walio nao na kuoa wengine. Roho zao zinazunguka zunguka kutafuta maana ya Maisha lakini haziwezi kuona kwasababu hazijui kuwa Maisha yapo katika Kristo tu peke yake..
Hawa tayari walishalaaniwa kama Kaini. Haijalishi wana mali au umaskini kiasi gani, bado wapo chini ya laana.
Swali ni je! Na wewe upo kundi lipi?. Ikiwa unasikia injili hutaki kuitii, ikiwa unahubiriwa habari za uhuru ulio katika YESU KRISTO halafu hutaki kuupokea basi fahamu kuwa Mungu hatakuua kama jinsi ambavyo hakumuua Kaini bali atakuacha uendelee na mambo yako ya kidunia ufanikiwe, uwe milionea, uwe mtu mashuhuri duniani, ujenge miji mikubwa kama ya Kaini uwe mgunduzi mpaka upokee tuzo za Nobeli lakini, rohoni uwe mtoro na mtu asiyekuwa na kikao duniani..
Utakuja kulithibitisha hilo siku ile umekufa, siku ile mwenzako wanatoka makubirini na unaowaona wanapewa miili mipya ya utukufu wanakwenda kuishi na Kristo milele katika majumba waliyoandaliwa kule mbinguni, wewe utakuwa huna kao lolote..bali mwisho wako utakuwa palepale kwenye lile ziwa la moto.
Hizi ni nyakati za mwisho mpendwa. Siku yoyote hapa paraparanda italia, mahubiri haya hatutayasikia tena, mavuno yataisha shambani, utakuwa ni wakati mwingine wa kuanza Maisha mapya ya umilele…Je utaimalizia umilele yako wapi? Jehanamu ya moto kwenye mauti ya milele au mbinguni?
Ni maombi yangu kuwa utatubu dhambi zako leo, ikiwa bado upo nje ya Kristo.. Umetanga tanga vya kutosha huu ni wakati wako sasa wa kutia nanga Kwa Kristo..kwasababu yeye ndio KAO LETU, na PUMZIKO LETU LA KWELI. Zingatia kurudi kwa Baba sawasawa na mfano ule wa mwana mpotevu Bwana alioutoa katika..(Luka 15:11-24)
Ubarikiwe sana.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Je! Ni wakina nani hao katika (Mathayo 16:28) ambao Bwana alisema hawataonja mauti mpaka atakapokuja?
JIBU: Tusome..
Mathayo 16:27 “Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
28 Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake”
Katika sentensi hiyo tunaona Bwana alikuwa anazungumza habari za kuja kwake jinsi kutakavyokuwa kwamba atakuja katika utukufu wa Baba yake na malaika zake na kufanya hukumu…Lakini wakati anazungumza maneno hayo akaongezea na sentensi moja ya kipekee sana kwamba “kuna watu ambao wamesimama naye pale wakati anaongea nao ambao hawataonja mauti hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake”.
Sasa ukianzia juu tena kidogo utaona kuwa Bwana Yesu hakuwa anazungumza maneno hayo mbele ya makutano..utagundua alikuwa anazungumza na wanafunzi wake 12 tu!..Kumbuka si mambo yote Bwana alikuwa anazungumza mbele ya makutano..kuna mambo alikuwa anazungumza mbele ya watu wote na kuna ambayo alikuwa anazungumza na wanafunzi wake tu!..Sasa mojawapo ya aliyokuwa anazungumza na wanafunzi wake tu ndilo hili kwamba “wapo ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona anakuja”…Maana yake ni kwamba miongoni mwa wale wanafunzi 12, kuna ambao hawataonja mauti kabisa.
Sasa swali la kujiuliza ni kweli Bwana alikuwa anamaanisha hivyo kwamba wapo ambao hawatakufa kabisa au alikuwa anamaanisha vingine?
Biblia inataja baadhi ya mitume walikufa..na historia pia inathibitisha vifo vya mitume wengine wote waliosalia…Hivyo hakuna mtume hata Mtume mmoja ambaye hakufa…Kwahiyo maana yake Bwana pale hakumaanisha kuwa hawatakufa kabisa kabla ya kushuhudia kuja kwake kwa mara ya pili(Ingawa huo uwezo wa kumfanya mtu asife kabisa hata atakapokuja anao lakini kwa pale hakumaanisha vile)..Bali alikuwa anamaanisha kuwa wapo ambao hawatakufa mpaka “watakapoonyeshwa jinsi atakavyokuja katika utukufu wake siku za mwisho”..Na kuonyeshwa huko si kwingine bali kwa njia ya maono ya wazi kabisa…Yapo maono yanayokuja kwa mfumo wa ndoto, na yapo yanayokuja kwa njia ya dhahiri kabisa…Haya ya Dhahiri mara nyingine yanajumuisha watu Zaidi ya mmoja wanaona kitu kinachofanana kwa wakati mmoja…lakini pia hayo mengine mara nyingi yanamtokea mtu mmoja mmoja na yanakuwa kwa mfumo kama wa ndoto.
Sasa ni lini walionyeshwa maono hayo ya kuja kwa Bwana kwa nguvu na utukufu?
Ukishuka kidogo sura inayofuata mstari wa kwanza biblia inasema…
Mathayo 17:1 “Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani;
2 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.
4 Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
5 Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
6 Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
7 Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope.
8 Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake.
9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu”
Umeona hapo mstari wa 2 unasema “AKAGEUKA SURA YAKE MBELE YAO; USO WAKE UKANG’AA KAMA JUA, MAVAZI YAKE YAKAWA MEUPE KAMA NURU.” Huo ndio utukufu ambao atakuja nao mwana wa Adamu siku za mwisho…ambapo kila jicho litamwona wakati huo uso wake utakuwa unang’aa kama jua, na mavazi yake yatakuwa meupi kama Nuru..Mataifa yote wataanguka chini na kuomboleza…naye atawahukumu waovu…
Kwahiyo hawa mitume watatu kati ya wale 12, ndio waliopata neema hiyo/bahati hiyo kuuona utukufu huo wa kuja kwa Yesu kabla hawajafa, na hivyo Neno la Yesu likatimia hapo kwamba wameuona utukufu wake kabla hawajafa. Na haikumaanisha kwamba wataendelea kuwa hai mpaka watakapomwona akija mara ya pili atakapotokea mawinguni hapana!….watakaomwona akitokea mawinguni kwa utukufu huo ni wale wote watakaokuwa wameachwa katika unyakuo, ambao wamebaki duniani na kuipokea chapa…lakini watakatifu wakati huo watakuwa wameshanyakuliwa na watakuja pamoja na Kristo siku hiyo ya utukufu wake…
Sasa tutazidi kujuaje kama hayo yote ni kweli?..Biblia inasema kwa vinywa vya mashahidi wawili, watatu kila neno lithibitike.
Tunaona tena Petro akilishuhudia jambo hilo…Jinsi alivyoona kuja kwake..
Tusome..
2Petro 1:16 “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na KUJA KWAKE; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.
17 Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
18 Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.”.
Uonaona hapo?..anasema hatukuhadithiwa na mtu kuhusu nguvu zake na KUJA KWAKE..(maana yake siku ile mlimani yeye pamoja na Yohana na Yakobo walionyeshwa KUJA KWAKE) na walishuhudia wenyewe.
Bwana akubariki sana.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Shetani anatolea wapi fedha, angali tunajua Fedha na dhahabu ni mali ya Bwana?.
Historia fupi ya Rozari kama inavyosomwa na kanisa katoliki.(kulingana na wakatoliki inajulikana kama Rozari takatifu)
Rozari asili yake ni neno la kiingereza “rosary” lenye maana ya “bustani ya maua ya waridi”…Maua ya Rose kwa kiingereza ndio yanaitwa “waridi”..Kwahiyo bustani yake ndio inayoitwa rosary.
Katika sehemu za Ulaya kuna utaratibu wa kupelekeana maua hayo ya waridi ni kama ishara ya kuonyeshana upendo (Ingawa upendo halisi hauwakilishwi kwa maua)…
Hivyo yapo maua hayo ya waridi yaliyo ya rangi ya nyekundu na Nyeupe. Hivyo wakatoliki wanaamini kuwa Maria ni mama mtakatifu kwao, hivyo anastahili kupelekewa mfano wa ua hilo la waridi..na Hivyo sala ya rozari ndio kama ishara ya kumpelekea mama huyo ua hilo jeupe la Waridi kama ishara ya upendo wao kwake.
Sasa Historia ya hiyo sala ya rozari takatifu kwa wakatoliki ilianzia wapi?
Ilianzia karne ya 3 ambapo kulikuwa na watu wanaojulikana kama wahermiti kulingana na Wakatoliki. Watu hawa waliamua kuwa wanasoma kitabu cha Zaburi kila siku SURA ZOTE 150. Lakini baadaye wakazipunguza na kukusudia kusoma sura zote 150 kwa muda wa wiki moja.
Kwa kuwa walikuwa ni watu wasio na elimu, walitumia mbegu ndogo za mimea kuwakilisha kila zaburi moja wanayoisoma..Hivyo wakawa na mbegu 150, kwa idadi ya zaburi zote 150, hivyo kila walipokuwa wanamaliza kusoma zaburi moja waliweka mbegu moja katika kapu ili iweze kuwasaidia kujua wapo zaburi ya ngapi..n.k
Baadaye kulingana na kanisa katoliki, wanasema watu hao majirani zao walivutiwa na sala hiyo ya zaburi, na wao pia wakaanza sala kama hiyo lakini wakawa wanasali sala ya “Baba yetu uliye mbinguni” mara 150, badala hiyo ya Zaburi.
Baadaye tena wakabadilika na kuanza kutumia shanga 150 zilizopitishwa kwenye kamba badala ya vimbegu vidogo vya mimea walivyokuwa wanavitumia hapo kabla.
Ilipofika karne ya 11 kadinali wa kikatoliki Mt. Peter Damiani, aliibadilisha sala hiyo kutoka katika kusali “Baba yetu uliye mbinguni” mara 150…Na kuwa “salamu Maria” mara 150.
Baadaye tena akatokea kiongozi mwingine wa kikatoliki akazigawanya hizo sala katika makundi 15..na kila baada ya salamu Maria 10 aliiweka Baba yetu uliye mbinguni…ikiwa vile vile kamba yenye vishanga 150.
Baada ya kipindi fulani tena wakavipunguza vile vishanga na kubakia vishanga 50 tu. Hivyo ndio mpaka leo wanasali rozari yenye vishanga hivyo 50.
Lakini Je jambo hilo ni la kimaandiko?
Jibu ni la! Si la kimaandiko kwasababu hakuna sehemu yoyote katika maandiko tumeagizwa tusali sala ya “Salamu Maria”. Kwasababu Maria si mtu anayetuombea..yeye alishakufa, wafu wote hawana habari na mambo ya maisha yetu haya…..Anayetuombea ni mmoja tu biblia imemtaja ambaye ni ROHO MTAKATIFU.
Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa”.
Umeona? ni Roho Mtakatifu na si Bikira Maria. Na Roho Mtakatifu hatumuombi atuombee na kusema “Salamu Roho Mtakatifu tunaomba utuombee”..hapana Roho Mtakatifu anatuombea pale na sisi tunapoomba..aidha kwa kunena kwa lugha au kwa maneno dhahiri..Yeye ni kama Mkalimani wetu mbele za Mungu. Mkalimani hawezi kuzungumza kama wewe huzungumzi.n.k
Hivyo sala yoyote inayohusisha kumwomba Mtakatifu fulani aliyekufa atuombee ni sala ya upotofu..inayowafumba watu macho na kuwafanya wawe wavivu wa kuomba wenyewe na kutamani kila wakati kuombewa tu! Na mtu anayesali sala hiyo anamwabudu shetani bila yeye kujijua.
Hali kadhalika sala halisi inatoka ndani ya Moyo, na si desturi au utaratibu fulani au fomula fulani ya kufuata. Unapotumia mfumo fulani wa kuhesabu shanga na kutimiza idadi fulani ya maneno..hapo utakuwa husali chochote zaidi ya kutimiza wajibu tu..Na hatuendi kumwomba Mungu ili kutimiza wajibu..Mungu anataka ibada halisi inayotoka ndani ya moyo wa mtu hata kama itamchukua mtu maneno machache lakini maadamu imetoka katika moyo uliomiminika mbele zake..hiyo inathamani kubwa sana mbele za Mungu kuliko maneno elfu yasiyo na maana.
Ukitumia mfumo fulani bila kuomba kwa Roho ni sawa na umemwekea Mungu baba, nyimbo zilizorekodiwa katika kaseti azisikilize afurahi..Umeona? ukifanya hivyo ni kumdharau Mungu..anachotaka kutoka kwetu ni nyimbo zinazotoka ndani ya vinywa vyetu zinazotoka moyoni..na sio nyimbo zilizorekodiwa…Kadhalika na sala anataka zinazotoka mioyoni mwetu na si zinazojirudia rudia kama kaseti.
Hivyo kwa hitimisho..sala ya Rozari si sala ya kimaandiko..Imebuniwa na Shetani, na lengo lake ni kuwaharibu watu kiroho. Hivyo kama upo huko ndugu..toka haraka sana!..Anza kumwabudu Mungu leo katika Roho na Kweli..Tupa hiyo rozari usiisali tena…umeshaujua ukweli, na pia washirikishe wengine wasiojua ukweli huu..
Hizi ni nyakati za mwisho shetani anatumia kila namna kuwazuia watu wasiijue kweli. Na anawatumia watumishi wake ambao kwa nje wanaonekana ni watakatifu, wanaonekana ni watumishi wa Mungu kumbe ndani ni Mmbwa mwitu wakali.
Bwana akubariki sana.
Ikiwa bado hujaokoka na unatamani kuokoka basi hujachelewa..kumbuka kuokoka sio dini mpya..bali ni kitendo cha kumpokea Yesu maishani mwako na kufanyika kiumbe kipya..kumkiri kwamba yeye pekee ndiye njia ya kweli na mpatanishiwa wa Mungu na wanadamu. Ukimkiri namna hiyo na kudhamiria kuacha dhambi kwa vitendo na kujikana nafsi yako na kumfuata yeye…ataingia moyoni mwako na kukubadilisha na kukufanya kuwa kiumbe kipya. Hivyo tubu na baada ya kutubu nenda katafute ubatizo sahihi wa kimaandiko wa kuzamishwa katika maji tele (Yohana 3:23) na kwa Jina la Yesu Kristo.
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
SWALI: Ndugu zangu Huyu Mariamu MAGDALENE ni nani?”..Je! Magdene ni jina la baba yake au ni Jina la ukoo wake?.
JIBU:
Mariamu Magdalene( wengine wanamwita Magdalena) ni yule mwanamke ambaye tunamwona kwenye biblia akitolewa pepo saba na Bwana Yesu..
Luka 8:2 “na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao. “
Ni mwanamke aliyefuata na Bwana Yesu tangu huo wakati hadi mwisho wa huduma yake ambaye yeye pamoja na wenzake, ndio waliokuwa wanamuhudumia Bwana kwa mali zao.
Mariam Magdalene tunamwona tena siku za mwisho mwisho kabisa kabla za Bwana Yesu kupaa yeye ndiye aliyeagizwa kwenda kuwaeleza wanafunzi wake juu ya kufufuka kwake.
Yohana 20:11 “Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 2
12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.
13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.
14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu.
15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.
16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).
17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo”.
Na kuhusu Hilo jina la Magdalene sio jina la baba yake, au la ukoo wake, Hapana aliitwa Mariamu Magdalene kuonyesha asili yake tu, ili kumtofautisha na Mariamu wengine kwenye biblia…Kumbuka hili jina Mariamu limetumika mara nyingi kwenye biblia..Hivyo ili kuwatofautisha hawa Mariam wote, huyu aliitwa mariamu Magdalene kuonyesha na Mariam aliyetokea huko mji wa MAGDALENE uliokuwa kando kando magharibi mwa bahari ya Galilaya huko Israeli. Lakini hilo sio jina la Baba yake au ukoo wake..Hapana ni jina la mji aliotokea.
Ni kama tu yule mwanamke Msamaria, hilo jina Msamaria sio jina la baba yake, hapana bali ni jina la mji anaotokea unaoitwa SAMARIA uliopo katikati ya Israeli.
Bwana akubariki.
Pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
RABONI!
JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?
Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
JINA LA MUNGU NI LIPI?
Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
Tuwaonapo nzige wa jangwani ni nini tunajifunza?
Shalom.. Karibu tuongeze jambo lingine kuhusu ufalme wa mbinguni..
Bwana Yesu alipotuambia utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake…Alimaanisha kweli ufalme huo ili kuupata inahitaji kuutafuta…Lakini jambo ambalo hatujui pia ni kuwa ufalme huo haujafichwa katika mambo magumu sana, kiasi kwamba itatuhitaji tuwe na shahada kubwa za elimu, au maarifa makubwa kuzijua, badala yake siri hizo zimefichwa katika mambo madogo sana, na hayo ndiyo yanayofanya ufalme huo usionekane kirahisi..Mambo mepesi sana ambayo huwezi kutazamia kama kweli hapo ndipo siri za Mungu zilipo.
Kwa mfano embu tafakari Bwana Yesu alivyosema..Watafakarini Kunguru (Luka 12:24),..hawapandi, wala hawavuni, wala hawana maghala lakini baba yenu wa mbinguni anawalisha hao wote, je ninyi si Zaidi kuliko hao wote?. Ikiwa wewe unaishi Dar es alaam au sehemu za pwani utakuwa umeshakutana na kunguru wengi sana, lakini kama Bwana Yesu asingelizunguza hili neno, ungekuwa unaona kama ni viumbe vyenye kero Fulani, vinaishi mjini tu kuuchafua mji, lakini kumbe siri moja ya ufalme wa mbinguni ipo hapo, kiasi kwamba mtoto wa Mungu akiitumia basi, atafanikiwa sana,
Kama hujui ni mmoja wa ndege wachache sana wanaoishi miaka mingi, kunguru anaishi mpaka miaka 80, anaishi mjini mahali wanaposema Maisha magumu(vyuma vimekaza), na kila siku anakula, anakunywa! Sasa ni rahisi kusema kunguru ndivyo walivyoumbwa staili hiyo ya maisha..Lakini Bwana Yesu anasema..Je! wale wanachokipi cha kuwapita nyie mpaka waishi Maisha ya kutokujisumbukia kama yale?..
Ndugu kama wewe umekosa Imani ya maneno kama hayo ya Kristo, nataka nikuambie wapo wenzako wanaishi kwa Neno hilo na Bwana anawahudumia kwa kila kitu Zaidi hata ya kunguru, mmojawapo ni mimi, hakuna siku inayopita bila kuwa na ushuhuda mpya maishani mwangu…mpaka nimeshazizolea naziona ni kawaida tu..Lakini zamani nalipoanza tu kuliamini hili Neno, nilijaribu kumweleza mchungaji mmoja kulitokea utata mkubwa.. Haijalishi Tutajaribu kuleta tafsiri nyingine tuzijuazo lakini Maneno ya Yesu ni imara, yatathibitika milele na milele..Hayo ndio mambo marahisi ambayo Mungu anajifunua ndani yake, lakini yanadharauliwa na wengi.
Leo hii tunasikia tena kuna jambo limezuka la wadudu wanaojulikana kama NZIGE WA JANGWANI, sana sana katika ukanda wa Afrika Mashariki. Tupaswa pia tujiulize maswali Je! Tupowatazama hawa wadudu tunaona tu maafa na majanga au tunaona pia kitu kingine ndani yake?..
Lakini biblia inawataja nzige kama moja ya kiumbe vinne vyenye AKILI nyingi sana..
Soma..
Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.
25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
27 NZIGE HAWANA MFALME; LAKINI HUENDA WOTE PAMOJA VIKOSI VIKOSI.
28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme”.
Kama hujawahi kufuatilia tabia ya nzige hawa, basi fahamu kuwa hawana tofuati sana na nzige hawa wa kawaida tunaowaona ambao kila mmoja anajitegemea kivyake, tofauti ipo tu pale ambapo wameshakuwa wengi huwa wote wanabadilika tabia, wanajikusanya pamoja..kisha wakishajikusanya wanaanza kuruka katika wingi wao, kama kimbunga, ukitazama kwa mbali unaweza ukaona kama ni vumbi tu linakuja jinsi walivyo wengi, unaambiwa katika kilometa moja ya mraba, wapo nzige Zaidi ya milioni 150, na katika kimbunga hicho wapo Zaidi ya nzige bilioni 100, na wote hawa wanaruka pamoja.
kwa siku wanaweza kusafiri zaidi ya kilimeta 150, sasa licha ya wao kuwa wengi hivyo unaambiwa katika kuruka kwao na kupishana kwao wakiwa bado hivyo mabilioni kwa mabilioni huko juu, hawagongani wakiwa angani, wala hawagusani, japokuwa wanaruka karibu karibu sana..Hawana kiongozi wa kuwaweza katika mstari, na kuwasimamia na kuwaambia wewe pita hapa, au wewe pita kule, lakini wanayo akili ya hali ya juu, ya kuwafanya waruke kwa ustaarabu, wakiwa na anza moja, ya kuelekea upande mmoja..
Na ndio hiyo inayowafanya wafanikiwe kufika mbali wote wakiwa pamoja, wahame kutoka taifa moja hadi lingine wakiwa na idadi hiyo hiyo ya majeshi..Na kusababisha maafa makubwa sana ya mazao isiyoelezeka..
Embu fikiria kikundi kimoja kinachojaza eneo la kilometa moja ya mraba, kwa siku moja kinauwezo wa kutafuna mazao, yanayoweza kuliwa na watu elfu thelathini na tano (35,000) ..Na wenyewe wakivamia basi wanamaliza mamilioni ya Hektari za mraba.. Na ndio maana wanakuwa tishio sana kwa mataifa..Hawa ndio mfano wa wale walitumwa kuitafuna nchi yote ya Misri.
Sasa, kwanini Biblia inatuambia wanaakili nyingi..Ni kwasababu Mungu anataka ni sisi tupate hekima ndani yake ili tufanikiwe katika kumshinda adui..
Si mpango wa Mungu tangu zamani tuwe na viongozi juu yetu sisi wa kutuongoza..Wana wa Israeli walimwomba Mungu awape mfalme juu yao..Mungu alikasirishwa sana na mawazo yao, kwasababu Mungu alitamani wamtumikie yeye wakiwa na nia moja kila mmoja bila kushurutishwa na mtu Fulani wa pembeni..(Soma 1Samweli 8:1-22)
Leo hii na sisi, tukitaka ulimwengu huu, tumshinde Shetani, hatuhitaji mpaka tuambiwe na watu Fulani majukumu ya kufanya..Bali sote kwa pamoja kila mmoja kwa nafasi yake, na kwa karama Mungu aliyopewa anyanyuke kwa nguvu zake aishambulie kambi ya Adui shetani kwa kuihubiri injili, tusisibirie mpaka Mchungaji wetu atuambie hivi au vile, tusisubiri mpaka viongozi watushurutishe tutoke tukaifanye kazi ya Mungu…Kwa jinsi shetani anavyoaharibu hakuna mtu asiyejua kuwa huu ni wakati wa mapambano..
Sisi ikiwa kila mmoja atasimama kwa nafasi yake, kama vile HAWA NZIGE WA JANGWANI.. Tukatoka tukiwa na lengo moja la kumuharibu ibilisi na kazi zake zote..Basi tujie kuwa kuzimu itabakia kuwa gofu..shetani atapata hasara isiyokuwa ya kawaida..Watu watamkimbilia Kristo kwa namna isiyoelezeka…Na tukitoka wote kama Jeshi kiongozi wetu akiwa ni Roho Mtakatifu na si mtu, kamwe hatutapishana kauli, kamwe hatutagongana katika njia zetu kama jinsi hawa nzige kwa wingi wao wasivyogongana wakiwa angani..
Lakini hiyo yote ni mpaka mimi na wewe, kutokuongejea mpaka tupangiwe majukumu ya kufanya na mtu Fulani, au mhubiri Fulani, au mpaka kanisa litupangie majukumu..
Naamini katika wakati huu wa kumalizia, tutalitafakari na hilo, katika kazi ya ujenzi wa ufalme wa mbinguni..Bwana azidi kutupa neema yake.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
UHURU WA ROHO.
KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.
KIFO CHA MTAKATIFU POLIKAPI (Policarp).
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?
SAA YA KUHARIBIWA IIJIAYO ULIMWENGU WOTE.
SIKU ILE NA SAA ILE.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.
Mwanamke wa Kikristo unapaswa ujue nini?
Karibu tujifunze Biblia, ambayo ndiyo mwanga wa njia zetu na Taa iongozayo miguu yetu.
Ujumbe huu unakuhusu wewe binti wa Mungu ambaye pengine una bidii ya kumtafuta Mungu, karibu leo tujifunze baadhi ya mambo ambayo yatakusaidia katika safari yako ya imani, na yatakayokuongezea maarifa ya kutosha ya namna ya kutembea na Mungu kwa jinsi anavyotaka wewe utembee naye.
Jambo la kwanza la kuzingatia binti wa Mungu usomapo biblia…usikimbilie kusoma habari za wanaume kama wakina Musa, Daudi, Ezekieli, Yohana au Paulo…Ni vizuri kusoma hayo yote!..lakini nataka nikuambie kwamba ukikimbilia kusoma habari za hao bila kusoma kwanza habari za wanawake wenzako kama wewe katika maandiko hakika nakuambia utakuwa umeukwepa msingi mkubwa sana na wa muhimu katika maisha yako.
Kabla ya kutaka kujifunza habari za Daudi na Ushujaa wake…Hebu ingia ndani kwanza kajifunze habari za bibi yake Daudi aliyeitwa RUTHU, ni jinsi gani alimpendeza Mungu..kayasome maisha yake na kajifunze habari zake kwa mapana na marefu jinsi alivyoishi na wakwe zake na jinsi alivyompendeza mumewe Boazi..Ikiwezekana kamata kalamu na karatasi zinakili zile points zote, zishike hizo na kuziishi ndizo zitakazokusaidia sana kuwa mwanamke unayeishi kwa kumpendeza Mungu kuliko kujifunza habari za ushujaa wa Daudi. Ushujaa wa Daudi kwako wewe mwanamke hauna manufaa sana kwako zaidi ya ushujaa wa Ruthu bibi yake Daudi, au ushujaa wa Abigaeli mkewe Daudi.
Kabla ya kujifunza kwa kina habari za Daudi jinsi alivyomwangusha Goliathi..hebu kajifunze kwanza habari za Abigaili mke wa Daudi jinsi alivyomzuia Daudi kwenda kumwaga damu, kajifunze kwanza jinsi Abigaili alivyomnyenyekea Daudi…ziige hizo tabia kwanza za mke wa Daudi, kabla ya kwenda kuziiga za Daudi.(1Samweli 25:2)
Hali kadhalika kabla ya kwenda kujifunza juu ya Imani ya Ibrahimu..Hebu kwanza jikite kumsoma kwa undani SARA!..Zitafute siri za mafanikio za Sara kabla ya kutamani kuzitafuta za Ibrahimu..za Ibrahimu hazitakusaidia sana wewe mwanamke zaidi ya za Sara..Ibrahimu aliambiwa akatahiriwe na asingefanya hivyo alikuwa anakwenda kinyume na maagizo ya Mungu sasa wewe Tohara inakusaidia nini, hayo maagizo yanakufundisha nini wewe?…Lakini ukijiingia ndani kujifunza Jinsi gani Sara alimpendeza Mungu..ukazijua siri zote za maisha ya Sara hakika hutabaki kama ulivyo, na shetani hatakaa akuweze kamwe kama alivyowashindwa wakina Sara.
Sara alifikia hatua ya kumweshimu mumewe mpaka akafikia hatua ya kumuita mumewe “Bwana” (kasome 1Petro 3:6)..Hebu na wewe iga kwanza hayo mazuri ya Sara kabla ya kukimbilia kutamani mazuri ya Ibrahimu.
Vivyo hivyo kabla ya kukimbilia kujifunza juu ya Petro, Yohana au Mathayo wanafunzi wa Bwana Yesu..hebu tenga muda kwanza kujifunza juu la kundi lingine la waliomfuata Yesu kwa bidii mfano wakina (Mariamu Magdalene, Susana, wakina Martha na Miriamu)…Ingia ndani kujifunza maisha ya hawa wanawake watakatifu ni jinsi gani walivyompendeza Mungu…usikimbilie kujifunza juu ya Mitume jinsi walivyokuwa hodari wa kwenda vijiji na vijiji kuhubiri…hayo hayatakusaidia sana zaidi ya kujifunza juu ya wanawake wakina Susana walivyomhudumia Bwana kwa mali zao..Hawakuwa miongoni mwa waliotumwa na Bwana kuzunguka huko na huko…. lakini sehemu kubwa ya Huduma ya Bwana michango ilitoka kwa hawa wanawake watakatifu.. Hilo ndio Jeshi kubwa linalomtumika Bwana!!
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, NA WENGINE WENGI, WALIOKUWA WAKIMHUDUMIA KWA MALI ZAO”.
Kabla ya kujifunza mazuri ya Tajiri Zakayo jinsi alivyomkaribisha Bwana nyumbani kwake na kutoa zaidi ya Nusu ya mali zake na kuwapa masikini(Luka 19:1-8)…Hebu kajifunze kwanza juu ya Martha jinsi alivyomkaribisha Bwana nyumbani kwake na akatoa Marhamu ya Nardo safi yenye thamani nyingi akampaka Yesu miguuni..na wala hakwenda kuiuza na kuwapa maskini kama ambavyo angefanya Zakayo…Na hiyo ikamsababisha kumpendeza Yesu zaidi ya alivyofanya Zakayo.(Yohana 12:1-7). Kajifunze ni kwanini alifanya vile Martha na wewe ukafanye vilevile…
Usitangulie kujifunza juu ya mazingira Bwana Yesu aliyowatokea Mitume wake 12..shughulika sana kujifunza juu ya mazingira aliyowatokea wale wanawake walio mashujaa wa Imani..Hata hivyo Pamoja na Utume waliokuwa nao wakina Petro lakini hawakuwa wa kwanza kujua kwamba Bwana amefufuka..badala yake ni wale wanawake watakatifu ndio walioifunua siri hiyo wa kwanza ya kufufuka kwa Bwana.. Mariamu ni mwanamke wa kikristo aliyekaa katika nafasi yake na ndiye aliyekuwa wa kwanza kujua kwamba mwokozi anazaliwa ulimwenguni na Zaidi ya yote yeye ndiye aliyempokea..ni wanawake hao hao ndio waliokuwa wa kwanza kujua Mwokozi hayupo kaburini yu hai!….Huoni kama kuna siri kubwa sana hapo?…hata kuja kwa pili kwa Kristo si ajabu baadhi ya wanawake watakatifu ndio watakaokuwa wakwaza kujua…sasa kwanini leo unaikimbia nafasi yako wewe mwanamke wa kikristo??…Unataka kuwa PETRO?
Na wanawake wengine wote katika biblia ambao walikuwa ni mashujaa wa Imani.. kajifunze kwao kabla ya kwenda kujifunza juu ya mashujaa wa Imani wa kiume..kajifunze jinsi walivyovaa, kajifunze jinsi walivyojisitiri…kajifunze juu ya akina Debora jinsi alivyokuwa mnyenyekevu kwa Baraka na Israeli yote, kajifunze juu ya akina Hana, Rahabu, Dorkasi, Esta na wengineo wengi.
Nenda pia kasome, Waraka ule wa pili wa Yohana ambao uliandikwa kwa mama yule mteule jinsi alivyowalea Watoto wake na kuwatunza, mpaka wakakaa katika hiyo kweli, na sifa zake zikavuma katikati ya mitume wa Kristo, na kuaswa kuwa asiyaache matendo yake, bali aipokee thawabu tilimlifu..
Halidhalika, kasome maandiko yanayowazungumzia wanawake wengi, tabia zao mbaya ujiepushe nazo..Na moja ya tabia ambayo imendikwa ni ile ya Udadisi (Au kwa lugha ya kisasa umbea/usengenyaji) soma 1Timotheo 5:13. Itakufaa Zaidi kuliko mambo mengi unayoyasoma katika biblia..
Vivyo hivyo katika makosa usikimbilie kujifunza makosa ya wanaume wa kwenye biblia…kwamfano kosa la Daudi kulala na mke wa Uria sehemu yako ipo wewe kama mwanamke?..au linakufundisha nini?…zaidi somo lile linawafaa wanaume…Wewe kajifunze jinsi wanawake kama YEZEBELI walivyomchukiza Mungu..kajifunze ni tabia gani alizokuwa nazo mwanamke Yezebeli zilizomfanya Mungu amchukue…Yezebeli alikuwa ni mchawi, muuaji na mwanamke anayejipamba uso….Ni mwanamke pekee aliyekuwa anapaka uwanja machoni ndani ya Biblia nzima hakuna aliyekuwa kama yeye..(kasome 2Wafalme 9:30), vivyo hivyo kajifunze kwa wanawake waliofanya makosa kama Mke wa Luthu, makosa yale na wewe usiyafanye, Mke wa Ayubu…kajifunze wanawake wengine waliofanya makosa kama Yule mke wa Ahasuero aliyeitwa Vashti, ambaye alikuwa na kiburi hamweshimu mume wake, kisa tu yeye ni mzuri mpaka kusababisha nafasi yake kuchukuliwa na mwanamke mwenye adabu kama Esta. Jifunze juu ya viburi vya hao vilipowafikisha kabla ya kujifunza juu ya kiburi cha mwanamume Kora aliyemdharau Musa mtumishi wa Mungu.
Bwana akubariki sana…Naamini kwa hayo machache pamoja na mengine mengi Bwana atakayokufunulia utapiga hatua moja katika kuyatenda mapenzi ya Mungu, Ewe mwanamke wa kikristo.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
EWE MKE! HESHIMA YAKO IPO KWA WAKWE ZAKO.
RABONI!
MARIAMU AKUTANA NA ELISABETI.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
Je! Mungu anaupendeleo kwa wanaume zaidi ya wanawake?
CHAPA YA MNYAMA
Heshima na Baraka za mwanamke uliyeolewa zipo kwa wakwe zako (hususani mama mkwe wako).
Vitabu viwili vikuu vilivyoitwa kwa majina ya wanawake ni Esta, na Ruthu. Vimeitwa hivyo sio kwasababu tu Mungu anataka kupitisha ujumbe wake wa wokovu kwa kanisa, lakini pia upo ujumbe mahususi unaowahusu wanawake.
Leo tutamtazama Ruthu kwa maneno machache sana. Wanawake wengi wanapitia mikwaruzo katika ndoa zao, na kikubwa ni saikolojia wanayojijengea kabla na baada ya kuolewa kwao, kuhusu wakwe zao, hususani mama-mkwe..Na hapo ndipo panapokuwa chanzo cha matatizo yote…Wanawake wengi wanaoniuliza juu ya matatizo ya ndoa zao, nimegundua kuwa asilimia kubwa hawana mahusiano mazuri na wakwe zao.
Nataka nikuambie ulipokuwa hujaolewa Baraka zako zilikuwa kwa wazazi wako waliokuzaa, lakini unapoolewa ujue kuwa Baraka za ndoa na za uzao wako zinahamia kwa wakwe zako haijalishi ni wabaya kiasi gani..
Kama tunavyofahamu habari ya Ruthu, na Orpa, wote hawa wawili waliolewa na watoto wa Naomi mkwe wao, lakini kwa bahati mbaya, Naomi akafiwa na mume wake na watoto wake wote wawili akabakia kuwa mjane, hivyo akawa hana mume wala mtoto wala mjukuu,..Lakini Naomi kwa ukarimu wake akawatangazia uhuru wakwe zake, warudi makwao kila mmoja akaolewe tena kwasababu bado walikuwa ni vijana na pia bado hawajazaa..Orpa akakubali kuondoa kurudi kwao, lakini Ruthu hakukubali kwasababu alijua Baraka zake zipo wapi…
Hivyo akaamua kurudi na mkwe wake nchi ya Israeli, akajitoa tu kama wakfu kuwa kama mjakazi wake, walipofika wakaishi pamoja,Na Ruthu akawa anamtumika mkwe wake kama mtoto wake kwa amani tu..Ruthu aliipoteza nafsi yake, ili tu amrudhishe mama mkwe wake, lakini alijua ndani yake haitakuwa bure kuwa vile.
Lakini kama tunavyojua, ni nini kilifuata baadaye..Licha tu ya Ruthu kuolewa na Yule tajiri Boazi ndugu yake Naomi, lakini watu wote walimwona kuwa anastahili kuliko watoto 7 wa Naomi..
Ruthu 4: 13 “Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na Bwana akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume.
14 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe Bwana, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.
15 Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, NAYE ANAKUFAA KULIKO WATOTO SABA, ndiye aliyemzaa.
16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake”.
Embu jiulize wewe mwanamke uliyeolewa, Je, mkwe wako alishawahi kukuona unastahili kuliko watoto wake wote alionao?.. Alishawahi kujivunia kwako kwa namna hiyo? Kama hakuna chochote alichowahi kujivunia kwako, lipo tatizo.
Na kama hiyo haitoshi, Ruthu ambaye alikuwa ni mwanamke wa kimataifa, akahesabiwa katika uzao wa Kiyahudi kama vile Rahabu alivyohesabiwa kwa tendo lake tu hilo , na huko huko baadaye ndipo alipokuja kutokea Mfalme Daudi.. Uzao wa kifalme na uzao wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Jaribu kufikiria tena jinsi uzao wake ulivyobarikiwa zaidi hata ya wanawake wengi wa kiebrania waliozaliwa na Ibrahimu…Na hiyo yote siri ilikuwa kwa MAMA MKWE WAKE na si penginepo. Ni yeye tu na Esta ndio waliopata nafasi ya vitabu vyao kuandikwa majina yao.
Hata wewe mwanamke uliyeolewa au unayekwenda kuolewa.. Timiza jukumu lako la kuwapenda wakwe zako kwasababu huko ndipo uzao wako utakapobarikiwa na ndipo ndoa yako itakapokuwa na amani..
Wewe kama siku zote huna habari na wakwe zako, unawasengenya, huwahudumii, huwaheshimu, unagombana nao, unawapenda kinafki tu, unafanya ili kutimiza wajibu tu, lakini hujitoi kwao, unaifikiria familia yako tu na ndugu zako…usitazamie kuwa Utabarikiwa uzao wako.
Biblia inakupa fundisho, litii ulifuate , watu wengi wenye matatizo ya ndoa huwa chimbuko ni hapo, pasipo hata wao kujua. Ikiwa humpendi mama wa mume wako, na usimpende na mume wako pia, lakini kama unampenda mume wako basi mpende na mama yake na ndugu zake ndipo utakapoishi kwa rah ana amani katika familia yako. Unaweza ukasema mimi ninaishi kwa raha, hao wakwe wananihusu nini..ni kweli utaishi leo kwa raha, lakini uzao wako unaweza usiishi kwa raha huko mbeleni..Na vile vile Maisha yako pia yanaweza yasiwe ya baraka.
Hiyo ni sheria ya Mungu ambayo ipo katika maandiko, ikiwa utataka kuwazaa akina YESE na Mfalme Daudi basi ambata na wakwe zako bega kwa bega, na kanuni hiyo itakulipa..Epuka mafundisho na injili za kwenda kupiga maadui zako, na kuwalenga wakwe zako..hapo utakuwa unazipiga baraka zako mwenyewe, utakuwa unajimaliza mwenyewe, ukidhani unajihami kumbe unajimaliza…Ukiona kuna kasoro Fulani ipeleke kwenye sala ukimwomba Mungu azidi kukupatanisha na wakwe zako sana, maana milango ya baraka zako ndio ipo huko.. siku zote zingatia hilo
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Usikimbilie tarshishi hakuna uzima
Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio mwanga wa njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu.
Kama ni msomaji wa biblia utakumbuka habari za Nabii Yona jinsi alivyoukimbia uso wa Bwana na kuelekea Tarshishi. Lakini umewahi kujiuliza TARSHISHI ulikuwa ni mji wa namna gani?…Ninawi tunaujua ndio uliokuwa mji mkuu wa Ashuru..lakini Tarshishi je!
Hebu kwa ufupi tujifunze juu ya huu mji na kisha tutapata jambo jipya ambalo linaweza kutusaidia katika nyakati hizi za hatari tunazoishi.
Mji wa Tarshishi ni mji ambao ulikuwa mahali panapoitwa Tiro..ambapo kwa sasa ni nchi ya Lebanoni…Nchi ya Lebanoni ni nchi iliyopo kaskazini mwa Israeli, kama vile Kenya ilivyo kaskazini mwa Tanzania (Na mpaka leo hiyo nchi inaitwa hivyo hivyo Lebanoni haijabadilika, inakaliwa na Waarabu sasahivi, lakini haina tena utajiri/ushupavu uliokuwa nao wakati ule)..
Sasa wakati wa vipindi vya wafalme wa Israeli nchi hii ya Tiro (Lebanoni) ambao mji wake mkuu ni Tarshishi ndio ulikuwa ni mji wa kibiashara mkubwa kuliko miji mingine yote. Ulikuwa unasifika kwa kuwa na MERIKEBU NYINGI ZA KIBIASHARA kuliko miji mingine yote. Na ulikuwa ni mji wenye uzoefu wa ki-biashara
Biblia inasema katika kitabu cha Ezekieli…
Ezekieli 27:12 “Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa”
Yeremia 10: 9 “Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi,….”.
Unaona? Vilevile Miti ya Mierezi ambayo ilitumika katika ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani, ilitoka huko Lebanoni, kulikuwa hakuna mahali pengine ambapo miti hiyo ilikuwa inapatikana, na njia ya usafirishaji iliyokuwa inatumika kusafirishia miti hiyo ni bahari (Njia ya Maji). Kwa ufupi sehemu kubwa ya malighafi za ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani zilitoka huko Tiro, ambao mji wake mkuu ni Tarshishi. Hata Dhahabu Sulemani alizozitumia kutengenezea vyombo vyake zilitoka huko Lebanoni..Sulemani alinunua dhahabu nyingi kutoka huko Lebanoni mpaka kufikia kiwango cha kuwa tajiri sana hata kuona kutumia madini ya fedha(silver) kutengenezea vito vyake ni kama kujishushia heshima..
1Wafalme 10: 21 “Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
22 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.
23 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima.”
Huko Tarshishi walikuwepo pia manahodha waliobobea sana, na pia kulikuwa na watu wenye elimu ya ujenzi kubwa sana..baadhi ya wajenzi wa hekalu lile la mfalme Sulemani aliwatolea huko huko Lebanoni.
Hivyo ipo mistari mingi sana katika biblia inayoelezea ushupavu wa Tarshishi…ipo mingi sana unaweza kuipitia kwa muda wako upatapo nafasi…Kasome (Ezekieli 27: 25-27, Ezekieli 38:13, 1Wafalme 22: 48, ).
Sasa kwa kuielewa sifa ya Huu mji wa wa Tarshishi tunaweza kujua ni kwanini Yona alikimbilia huko…Na kwanini alipanda merikebu…Kumbuka kutoka Israeli mpaka Tarshishi(huko Lebanoni) kulikuwepo na njia ya nchi kavu nzuri tu..lakini yeye alikwenda kupanda merikebu. Ni sawa leo mtu atake kwenda Tanga..aache kupanda basi achague kutumia ferry/meli pale bandarini Dar es salaam aende Tanga. Ni lazima anayo sababu ya kufanya hivyo..
Na ni wazi kuwa sababu yenyewe si nyingine Zaidi ya biashara…Yona pengine alikuwa na mizigo yake anakwenda kufanya biashara.. Tarshishi haukuwa mji wa kitalii..ulikuwa ni mji wa kibiashara..hivyo alipoisikia sauti ya Mungu ikimwambia aende Ninawi kuhubiri yeye akaona njia pekee ya kuipotezea hiyo sauti ni kuzama kwenye biashara zake…wala hakuchagua kukimbilia miji mingine kama Misri, au Moabu ambayo angepata pumziko..yeye alikuwa na sababu ya kwenda Tarshishi.. Angalau apate riziki kidogo.
Lakini kama tunavyojua ni nini kilimtokea njiani. Biashara iliishia pale pale, wakapata hasara merikebuni kwa kutupa bidhaa zao majini kupunguza uzito.. na mtaji wote ukaishia palepale.
Sasa kitu cha muhimu cha kujifunza hapo ni nini?..Usiikimbie sauti ya Mungu leo inayokuambia fanya jambo fulani au tii jambo fulani, usiidharau sauti hiyo na kukimbilia kufanya biashara zako. Ni kama bahati tu Yona alipata neema mipango yake ilikatishwa katikati haikukamilika…..angeweza kuachwa aende huko anakokwenda na Mungu akamtafuta mtu mwingine wa kwenda Ninawi kuhubiri na watu wa Ninawi wakaokoka lakini Yona huko alikokimbilia akafanikiwa na utajiri wake lakini akafa na huku hajalitimiza kusudi la Mungu aliloletewa duniani, na mwisho wa siku kupotea katika ziwa la moto milele.
Hivyo leo isikie sauti ya Mungu lipo kusudi la wewe kuwepo hapa duniani la kufanya mapenzi ya Mungu.. usilikimbie kusudi hilo kwa kisingizio cha kufanya biashara, Hizo biashara ni za muhimu sawa..lakini kulitimiza kusudi la Mungu ni muhimu Zaidi..Una safari 5-6 za kwenda China kila mwezi lakini huna siku ya kukaa kufunga na kusali na kulitafakari Neno. Mwaka unapita hujawahi kufunga useme angalau nautafuta uso wa Mungu. Hujawahi kusema angalau mwezi huu wote sitasafiri nitajikita katika kutafuta kujua mapenzi ya Mungu kwangu…Unatengeneza pesa lakini hutengenezi hazina yako mbinguni..Nchi zinakujua, Benki zinakujua, lakini mbinguni hujulikani.
Watu wengi wananiambia, mtumishi ninatamani kujifunza Neno, wengine wanasema ninatamani kwenda kanisani lakini kazi zinanisonga, shughuli zinanifanya kuwa buzy,..Nataka nikuambie unayo hatari kubwa sana ya kuiokosa mbingu.
Unakimbilia Tarshishi unaiacha Ninawi?..Unakimbilia kufanya uwekezaji unasahau kutangaza habari za ufalme wa mbinguni..Kumbuka Neema aliyoipata Yona sio atakayoipata kila mtu. Simama katika nafasi yako muda ni mchache, usiruhusu mbegu yako kusongwa na kitu chochote.
Bwana atusaidie.
Ikiwa hujampa Kristo Maisha yako..na unakazana kuifuata njia ya Ninawi!..nakushauri geuka leo..Bwana Yesu alisema “Baba yetu wa mbinguni anajua kuwa tuna haja na hayo yote, bali tuutafute kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo mengine yote tutazidishiwa”..Hivyo tubu leo kwa kukusudia kuacha dhambi, na kupunguza masumbufu ya Maisha haya ambayo yanakuvuta na kukusonga ukae mbali na Mungu wako.
Luka 21:34 “ Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, NA MASUMBUFU YA MAISHA HAYA; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”.
Chukua hatua leo, na Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo: