SWALI: Nimrodi ni nani? Na je! Alikuwa ni mtumishi wa Mungu?
Nimrodi ni kitukuu cha Nuhu kwa kupitia uzao wa Hamu,
Biblia inatuambia alianza kuwa mtu Hodari, na sio Hodari tu, bali alikuwa ni Hodari wa kuwinda mbele za Bwana, Mpaka enzi hizo ukatungwa msemo maarufu kwa jina lake (Soma Mwanzo 10:9),
Hivyo aliendelea na huo uhodari wake mpaka akafikia hatua ya kuwa na nguvu nyingi za kuanza kujenga miji mikubwa, ikiwemo Babeli na Ninawi.
Mwanzo 10:8 “Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa”
Lakini japokuwa alikuwa ni Hodari, alikuwa ni mwovu katika fikra zake na matendo yake, nakala nyingi za kale zinaonyesha, hata nia yake ya kutaka kuujenga mnara wa Babeli ilikuwa ni kumlipizia Mungu kisasi, kwamba kwanini aliwaua mababu zake, hivyo akaunyanyua mnara ule juu sana kuelekea mbinguni kiasi kwamba hata Mungu akileta tena mafurukio mengine asiweze kuwaangamiza.
Lakini jitihada zake hazikufika mbali, tunajua kilichotokea ni nini baada ya pale, ni kwamba walichafuliwa lugha zao na semi, ndoto zao zote zikayeyukia palepale, Kwasababu Mungu hadhihakiwi.
Lakini Pamoja na hayo bado tunakuja kuona Babeli iliendelea kuwepo kwa miaka mingi mbeleni, mpaka ikaja kuwa kitovu cha machafuko yote duniani, Na ndio hawa wababiloni baadaye wakaja kulichukua taifa la Israeli utumwani tena. Kama ulikuwa hujui ni kwamba chimbuko la ibada zote za sanamu na miungu, ilianzia huko, Hii miungu ya Rumi ya kuabudu mungu mke na katoto chake (ambayo kwa sasa wameipachika majina ya watakatifu kama Mariamu ) chimbuko lake lilikuwa ni huko,
Na ndio maana Babeli hiyo mpaka siku hizi za mwisho bado inaonekana kuishi, isipokuwa safari hii inatenda kazi rohoni. Katika kivuli cha dini.
Sasa muhasisi wa hayo yote alikuwa huyu Nimrodi.
Biblia inasema..
Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”
Usifurahie mafanikio ya kipumbavu hata kama utasifiwa na ulimwengu mzima, shetani naye alikuwa ni Hodari hivyo hivyo kabla ya kuasi, lakini ulikuwa ni uhodari unaokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.
Ezekieli 28:14 “Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele”.
Nasi pia tusiige mifano hiyo, tuwe wanyenyekevu kwa Mungu, tuishi kwa kuyafanya mapenzi yake, Hilo tu linatosha Sio kila jambo linalofanywa na watu Hodari wa mataifa yaliyoendelea na sisi tuigee, Ni heri tubakie na ushamba wetu kuliko tuige utukanaji, ushoga, au upagani, au uvaaji wa mavazi yasiyo na heshima mbele za Mungu na wanadamu.
Imemfaidia nini Nimrodi kuupata ulimwengu mzima, halafu amepata hasara ya roho yake?
Bwana atusaidie.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Je! Unazijua faida za kufunga na kuomba?
Embu isome Habari ifuatayo kwa makini;
Mathayo 17:18 “Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.
Mstari wa 21 unasema.. “Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”
Hii ikiwa na maana kuwa yapo mambo ambayo mtu atashindwa kuyafanya, haijalishi yeye ni mkristo au la, haijalishi yeye ni mtakatifu au la! kama hafungi na kuomba, basi atashindwa kufanya mambo mengi sana.
Embu tuzitazame faida za kufunga na kuomba..
1) Pale mtu unapofunga, ina maana kuwa hali chakula, au hanywi maji, kwa wakati Fulani, Na hiyo inampelekea mtu kuwa katika uhitaji mkubwa, Sasa uhitaji huo ndio unaoutesa mwili na kufanya mates ohayo yapenye mpaka kwenye nafsi ya mtu. Nafsi ya mtu ikishapokea mabadiliko hayo inaifanya roho ya mtu kuwa na mwitikio wa tofauti sana katika mambo ya rohoni. Tofauti na mtu ambaye hajafunga kabisa.
Kufungu kunakwenda sambamba na magonjwa, kwamfano mtu aliye katika hali nzito ya kuumwa au kuugua mwilini, mateso yale huwa yanashuka mpaka kwenye nafsi ya mtu, na ndio hapo utaona wagonjwa wengi wapo karibu na Mungu kuliko watu walio na afya zao,
Sasa turudi katika kufunga, pale unapofunga hata maombi yako yanakuwa na uzito wa tofauti ukilinganisha na siku nyingine ambazo ulikuwa hufungi, (jaribu hilo utalithibitisha) kama ulikuwa katika kuyatafakari maandiko, uelewa wako unakuwa wa ndani Zaidi tofauti na siku nyingine ambazo ulikuwa hufanyi hivyo .
Na kwa jinsi atakavyozidi kuenendelea kufunga kwa siku nyingi, ndivyo utakavyozidi kuwa mwepesi katika mambo ya rohoni.
Musa alifanikiwa kufunga siku 40 asiku na mchana bila kula, na sote tunajua ni nini alipata kule mlimani..Mungu alizungumza naye uso kwa uso, na kumpa zile Amri 10, Vivyo hivyo hata kwa Eliya naye alipofunga siku 40, Mungu alisema naye kwenye ule ule mlima wa Musa..
Halikadhalika na kwa Bwana wetu Yesu Kristo, yeye pia alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula chochote, mpaka ibilisi akatokea kumjaribu na kushindwa na aliposhuka kule mlimani alishuka na nguvu nyingi za Roho Mtakatifu ndipo akaanza kuhubiri injili na kuponya wangojwa katika Israeli yote.
Hivyo mifungo ya muda mrefu inafaa sana.
2) Faida nyingine ya kufunga inakusaidia kushusha chini matamanio ya mwili. Kwa kuwa chakula kinakuwa hakina sehemu kubwa katika mwili kwa wakati huo, hivyo hata kazi za uzalishaji wa homoni, zinapungua na hivyo inamfanya yule mfungaji awe katika hali ya utulivu Zaidi katika kumtafuta Mungu.
Biblia inatuambia pia, ukifunga, Mungu anakupa thawabu, Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu anathamini kujitesa kwetu kwa ajili yake.
Mathayo 6:16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Lakini pia unapaswa kujua kuwa kufunga kokote ni lazima kuambatane na kuomba..hivi ni vitu viwili vinavyokwenda sambamba, ni sawa na chai na sukari, unapobandika chai jikoni, inamaanisha kuwa sukari ni lazima iwepo chini pale inaongojea chai iepuliwe, vinginevyo haitaitwa chai.
Vivyo hivyo na Katika kufunga, hupaswi kufunga tu, unaamka asubuhi, unarudi jioni, halafu hufanyi lolote, unarudia tena hivyo kesho, na kesho kutwa,..hapo ni sawa na kufanya “diet” tu , Lakini unapofunga ni lazima uwe na malengo ya rohoni kwanini unafanya hivyo.
Hapo ndipo hapo sasa suala la kuomba lazima lijitokeze; Danieli alipofunga alikuwa mwombaji, vivyo hivyo na watu wote katika biblia..
Danieli 9:3 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako”;
Ukizingatia vigezo hivyo basi faida za kuomba ni kama zifuatazo;
Mathayo 26:40 “ Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”
Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Kama tulivyoona katika mistari ya mwanzoni juu, Bwana aliwaambia wanafunzi wake, pale waliposhindwa kutoa mapepo, kuwa namna ile haitoki isipokuwa kwa kufunga na kusali. Hata wewe unapojijengea ustaarabu wa kuwa mwombaji mzuri, basi unapokea mamlaka kubwa Zaidi ya kuamrisha nguvu za giza ziwatoke watu.
Siri nyingine ya maombi ni kuwa, kwa jinsi unavyodumu kwenye kuomba ndivyo unavyoukaribisha uwepo wa Mungu ndani yako..Na matokeo yake ni kuwa ile furaha ya wokovu inajengeka ndani yako.
Usipokuwa mwombaji, ni ngumu sana kuufurahia wokovu wako, utaona kama Mungu yupo mbali na wewe kila siku, utakosa ujasiri wa Imani yako, lakini ukiwa mwombaji amani Fulani utaipata na ujasiri.
Hivyo kama wewe, ulikuwa unalega lega, au ulikuwa hujua faida za kufunga, basi anza leo kufanya hivyo, pia hakikisha unajijengea utaratibu wa kuomba, saa moja kila siku, hicho ndio kiwango cha chini tulichopewa na Bwana Yesu.Kama ukifanya hivyo hakika utaona matokeo makubwa katika Maisha yako..
Utaona tofauti yako ya leo na jana.
Bwana akubariki.
Ikiwa utatamani kujua Zaidi juu ya faida za kufunga, basi tazama masomo mengine yaliyoorodheshwa chini hapa.
Lakini Kama hujaokoka, na unatamani kuokoka leo, Basi uamuzi huo ni mzuri sana, hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>>>
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
Namna ya kuomba
KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.
KIAMA KINATISHA.
NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.
SABATO TATU NI NINI?
Swali: Sabato tatu ni nini? Kama tunavyosoma katika Matendo 17:2
Jibu: Tusome,
Matendo 17:1 “Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko SABATO TATU,
3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo”.
Mstari huo haumaanishi kwamba kuna aina tatu za sabato au sabato zipo tatu. Hapana, bali unamaanisha Sabato tatu mfululizo.
Kwamfano tafakari hii sentensi.. “Yohana baada ya kuokoka alihudhurua kanisani JUMAPILI TATU mfululizo za mwezi uliopita”. Sasa hapo simaanishi jumapili zipo za aina tatu, bali namaanisha ni jumapili za majuma matatu. Ndivyo Paulo alichomaanisha hapo katika sabato tatu. Maana yake kwa sabato tatu mfululizo aliingia hekaluni kuhojiana nao kwa maneno ya maandiko.
Sasa unaweza kuuliza je! kwa mantiki hiyo na sisi tunapaswa tuishike sabato?
Jibu ni la! Sabato halisi katika agano jipya sio siku moja maalumu, bali ni kila siku ya maisha yetu tunayoishi, sasa kwanini hapo Paulo aingie kuhojiana nao wakati wa sabato?. Ni kwasababu kwa wakati huo wayahudi (yaani waisraeli), walikuwa bado wana desturi ya kuishika sabato. Hivyo siku pekee ya kuweza kukutana nao ni siku ya sabato katika masinagogi yao, siku nyingine zozote wasingeweza kupatikana ndio maana hapo Paulo alikwenda kukutana nao katika siku yao ya kuabudu.
Ni sawa leo utafute namna ya kuwapata watu wa dini Fulani kuhojiana nao kuhusu imani, huwezi kuwapata nje na ile siku yao wanayokutana kuabudu. Kama ni ijumaa, au jumamosi au jumapili, au siku nyingine yoyote ile, sasa kitendo cha wewe kuwafuata ili uwashuhudie katika siku yao ya Ibada haimaanishi kwamba na wewe umeihalalisha siku ile.
Kufahamu zaidi kuhusu Sabato halisi ni ipi, mwisho wa somo hili chini kabisa utaona orodha ya mada hizo zinazohusiana na sabato, zifungue uzisome.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
Karibu tujikumbushe mambo machache, ambayo yanaonekana ni madogo lakini ni ya umuhimu sana, katika mapambano ya Imani.
Kuna tofauti ya sadaka na msaada. Unapomsaidia maskini huo ni msaada, na una thawabu zake mbele za Mungu..lakini sadaka ina matokeo makubwa zaidi kuliko msaada.
Sadaka ni nini?
Sadaka ni matoleo yoyote yanayohusisha madhababu!.. Katika agano la kale, sadaka iliyokuwa inakubalika kwa Mungu ni ile iliyokuwa inapelekwa mbele ya madhabahu ya Mungu katika nyumba ya Mungu…iwe ni kafara ya kondoo, au sadaka ya mazao au chochote kile. Vigezo ni lazima ipelekwe katika hema ya kukutania au katika nyumba ya Mungu.
Usipeleke sadaka yako kwa maskini, ukifanya hivyo utakuwa hujatoa sadaka bali umetoa msaada, utabarikiwa kwa ulichotoa lakini si kama ungeitoa kama sadaka. Sadaka ni lazima ihusishe madhabahu ya ki-Mungu.
Hata watu wanaokwenda kwa waganga huwa wanapewa masharti ya kupeleka sadaka..Na ile sadaka wanapewa maagizo ya kuiacha pale kwenye madhabahu zao, ili ilete matokeo wanayoyataka, kama ni kuku ataambiwa ampeleke hapo wamchinjia hapo hapo na kumwacha pale pale…Huwezi kusikia wanapewa maagizo na waganga na kuambiwa wakachinje jogoo mweusi nyumbani halafu wakawape maskini, au wakaipeleke kwa mganga mwingine,! Huwezi kusikia hicho kitu!.watakuambia leta hapa (kwenye hii madhabahu) hiki au kile kama sadaka yako, kwasababu ili kitu kiwe sadaka ni lazima kihusishwe na madhabahu.
Kwahiyo hakuna sadaka pasipo madhabahu.
Bwana Yesu alisema maneno haya katika
Mathayo 23:18 “Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga”.
Maneno hayo yanaelezea uhusiano uliopo kati ya sadaka na madhababu.
Kwahiyo kama wewe ni mkristo, sadaka yako peleka kanisani na mahali unapokuzwa kiroho (kwamfano kwenye mikutano ya injili, semina n.k), ndipo utakapobarikiwa Zaidi… Bila kusahau kusaidia maskini na wenye uhitaji ambako pia kuna thawabu kubwa kutoka kwa Mungu. Lakini sadaka ina nguvu mara nyingi Zaidi ya hiyo, endapo utaelewa ufunuo wake!.. Ongeza bidii sana katika kutoa sadaka kuliko kupeleka michango yako sehemu nyingine.
Kuna fikra mbaya sana ambayo shetani kaisambaza kwenye akili za watu wengi, ambayo imewasababishia watu wengi kukosa baraka zao. Na hicho ni saikolojia ya kwamba ukiipeleka sadaka kanisani basi ni kuwatajirisha wale wachungaji na watumishi!, na hivyo ni afadhali kuipeleka kwa maskini, Hiyo ni saikolojia ya Adui, usikubali ikutawale.
Bwana Yesu alisema pia maneno haya..
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.
Mambo haya yanaonekana ni madogo machoni pa wengi, lakini yana umuhimu mkubwa sana. Hivyo ni muhimu sana kuyafahamu na kuyazingatia. Zaka yako ipeleke nyumbani kwa Bwana, Sadaka zako za shukrani vilevile ipeleke nyumbani kwa Bwana.
Mungu akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 693036618/ 0789001312
Mada Nyinginezo:
TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Ubatizo wa moto ni upi?
MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.
UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.
JE KUVAA PETE NI DHAMBI?
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
Kuota unalia kwa uchungu/Ukiota unalia maana yake ni nini kibiblia?.
Zipo ndoto zenye maana, na pia zipo ndoto zisizo na maana yoyote katika maisha ya mtu, hizi za pili ni ndoto ambazo zinatengenezwa na ubongo wako tu wenyewe, kwa kuchukua matukio ambayo aidha ulishawahi kuyafanya au kuyapitia huko nyuma, au mazingira unayoishi sasa, au mambo unayoyafanya mara kwa mara.
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…;”
Kwamfano kama wiki iliyopitia ulikuwa unahudhuria sana kwenye sherehe, tarajia moja ya ndoto unazoziota kila siku kuwa za namna hiyo.. Vivyo hivyo na ndoto hii ya kuota unalia/ukiota unalia kwa uchungu, inaweza kuja kutokana na mazingira yako ya nyuma, Wengine walifiwa na jamaa zao wa karibu kipindi sio kirefu, wengine walikuwa misibani.n.k..Hivyo ubongo unachukua matukio hayo na kuyarudia rudia kwenye ndoto zetu za kila siku.
Lakini pia ndoto ya namna hii inaweza kuja kwa namna ya kitofauti sana, pengine hujafiwa siku za hivi karibu, au hujapitia matatizo yoyote mazito ya kukufanya uwe katika huzuni kubwa..Lakini unashangaa usiku umeota unalia kwa uchungu mwingi, bila kujua sababu ya kulia kwako ni nini. Unalia tu, unalia tu,
Ukiona hivyo basi lipo jambo unapaswa ulijue rohoni..
Ndugu unayesoma ujumbe huu, fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho, na Yesu anakaribia kuja kulinyakua kanisa lake. Mwisho wa dunia upo karibu sana.
Kuota unalia kwa uchungu, Ni Mungu anakuonyesha kuwa jinsi hali itakavyokuja kuwa huko mbeleni ikiwa utaachwa katika unyakuo, na watu wote watakavyokuwa..Haijalishi wewe ni muislamu, ujumbe huu unakuhusu pia wewe, kiama kipo karibu, watu wataomboleza, kwa kilio na uchungu usioeleza, kwa hayo mambo ya kutisha ambayo Mungu atayaleta katika hii dunia,
Biblia inasema hivi;
Sefania 1:14 “Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; SHUJAA HULIA KWA UCHUNGU MWINGI HUKO!
15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,
16 Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.
17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.
18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha”.
Unaona, hali itakavyokuwa kwa watu hata wale wanaojiona mashujaa leo, watalia kwa uchungu mwingi..
Isaya 33:7 “ANGALIA, MASHUJAA WAO WANALIA NJE, WAJUMBE WA AMANI WANALIA KWA UCHUNGU.
8 Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.
9 Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani”.
Ni mambo ya kutisha sana, ikiwa leo Yesu amerudi, na umeachwa, kitakachokuwa kinaendelea kwako, ni zaidi ya ulichokiona katika ndoto..
Yeremia 4:8 “Kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha.
9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema Bwana, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa”.
Mathayo 13:41 “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, NDIKO KUTAKUWAKO KILIO NA KUSAGA MENO”.
Yapo maandiko mengi yanayoelezea maombolezo yatakayokuwa yanaendelea katika kipindi hicho lakini hatuwezi kuiorodhesha yote hapa, Kama utapenda kufahamu kwa marefu juu ya siku hiyo ya mwisho itakavyokuwa basi fungua hapa usome.>>> MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Hivyo Kama wewe hujaokoka, na unajijua kabisa unaishi katika maisha ya dhambi, basi ni vema ukamgeukia Kristo leo, ayaokoe maisha yako, Kukutana na ujumbe huu sio bure, Umeoteshwa ndoto hiyo ni kwasababu Mungu ana mpango na wewe. Hivyo usifanye moyo wako mgumu, mkabidhi Yesu maisha yako leo aanze kutembea na wewe na hakika utamwona kwa namna ambayo hukuwahi kumtazamia, na atahakikisha kuwa mabaya hayo yote hayatakukuta ikiwa atarudi leo..
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki sana.
Pia angalia vichwa vya masomo mengine chini, fungua upitie naamini vitakutoa sehemu moja kiroho hadi nyingine.
Ikiwa utapenda kupata mafundisho ya Neno la Mungu ya kila siku kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwa namna hii: +255 789001312
Au jiunge kwa kubofya hapa chini;
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.
SIKU ILE NA SAA ILE.
MAONO YA NABII AMOSI.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
FAHAMU MAJIRA ULIYOPO NA NINI UNAPASWA UWE NACHO.
NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.
Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. kwa link hii >>https://chat.whatsapp.com/LO2BncRILtiAlnRYfZWG2V
Masomo mbalimbali ya Neno la Mungu.
Awali ya yote nakupa hongera kwa kupenda kutafuta kujifunza Neno la Mungu, lipo kusudi la Mungu kukufikisha hapa, biblia inatuambia..
1Timotheo 4:13 “…ufanye bidii katika kusoma…”
Ni wachache sana katika wengi wanaozunguka mitandaoni kutafuta mambo ya msingi kama wewe.
Na unajua nini? bidii yako sio bure, Bwana Yesu alisema,
Mathayo 7:8 “kwa maana kila..atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”.
Na pia alisema..
Mathayo 5:6 “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa’.
Kwahiyo unachokitafuta Bwana atakupatia, na pengine hata zaidi ya kile ulichokuwa unakitazamia,
Mahali hapa utakutana na masomo mbalimbali ya Neno la Mungu, zaidi ya 1,000, na maswali mengi ya biblia yaliyojibiwa. Kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi kitabu cha ufunuo.
Ili kuingia katika horodha ya masomo ya mbalimbali ya Neno la Mungu, fungua hapa>>> MASOMO MAPYA
Ili kusoma maswali ya biblia yaliyoulizwa na kujibiwa fungua hapa >>> MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA
Ili kusoma shuhuda za Mashahidi wa Imani wa kale fungua hapa >>> WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
Je! ulishawahi kujiuliza Unyakuo ni nini, na utakuwaje? Na kwanini Bwana Yesu alisema, Amin! Amin! Nawaambia kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatakapotokea, kusema kule kulimaanisha nini? Tazama hapa >> AMIN, NAWAAMBIA, KIZAZI HIKI HAKITAPITA,
Je! Unafahamu kuwa kanisa tunaloishi mimi na wewe ndio kanisa la Mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Tayari makanisa 6 yalishapita, na sasa tupo katika kanisa la mwisho? >>> AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.
https://www.high-endrolex.com/16
Je unafahamu Historia ya nyimbo mbalimbali za Tenzi>> TENZI ZA ROHONI
Je! Unajua Sadaka ni nini? Na umuhimu wake kwetu>> NGUVU YA SADAKA.
Je! Unajua aina za upendo, na upi tunapaswa tuwe nao?>> UPENDO NI NINI ?
Fahamu juu ya chukizo la uharibifu lililozungumziwa na Danieli na Bwana Yesu >> CHUKIZO LA UHARIBIFU
Ijue siku ya Bwana itakuwaje>> KIAMA KINATISHA.
Kwanini shetani aitwe nyoka wa zamani >> YULE JOKA WA ZAMANI.
Mbinguni ni wapi? Na je kuna aina ngapi za mbingu>> MBINGUNI NI WAPI?
Kuna siri gani katika kitabu cha Ruthu, kwanini kiandikwe na wakati yeye hakuwa mwanamke wa Kiyahudi, >>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
Ni siri gani imelala katika kitabu cha Esta juu ya Kristo na kanisa lake? >>> ESTA: Mlango wa 1
Mfahamu Melkizedeki, Je! alikuwa ni nani? Na kwanini awe hana baba wala mama, wala mwanzo wa siku wala mwisho? >>HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?
Utawala wa miaka 1000 ni utawala gani? >>> UTAWALA WA MIAKA 1000.
Kitabu cha Danieli kina maudhui gani? Je naweza kupata uchambuzi wake tangu mwanzo hadi mwisho? >>> DANIELI: Mlango wa 1
Ubatizo sahihi ni upi? Kulingana na maandiko. >> UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?
Nahitaji kuokoka je nifanyaje?. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kwa njia ya email/ whatsapp tutumie ujumbe katika namba hii :+255693036618 / +255 789001312
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima, Nakukaribisha tena tuyatafakari maneno ya uzima.
Leo tutatazama kwa ufupi Habari ya watu wawili. Wakwanza ni mtu mmoja anayeitwa Yairo mkuu wa sinagogi, na wa pili ni mwanamke mmoja aliyekuwa anatokwa na damu kwa muda mrefu lakini baadaye alikuja kuponywa na Bwana Yesu kwa kulishika tu pindo la vazi lake.
Sasa lipo jambo moja la kusisimua nataka ulione kwa hawa watu wawili ambalo kila mmoja lilikuwa kichwani mwake. Embu tusome kidogo;
Luka 8:40 “Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote.
41 Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;
42 kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma”.
Sasa ukiangalia hapo, utaona huyu Yairo, alikuwa na binti yake aliyepatwa na matatizo katika umri wake wa miaka kumi na miwili (12), Na wakati huo huo alikuwepo yule mwanamke alitokwa na damu kwa muda wa miaka kumi na miwili (12). Ipo sababu kwanini biblia imeutaja umri wa mtoto na muda wa mwanamke kutokwa damu.
Kwamfano biblia inatuambia huyu Yairo hakuwa na mwana mwingine isipokuwa yule binti tu, pengine alimlea kwa taabu na shida, akiwa na matumaini kuwa huyu ndiye atakayekuja kuwa heshima yake ukubwani, pengine aliona mwelekeo mzuri wa binti yake, kama vile Yokebedi(mama yake Musa) alivyoona uzuri wa Musa tangu akiwa mdogo, akaamua kumficha ambapo kweli baadaye tunaona akaja kuwa nyota ya Israeli mwokozi wa Israeli,
Vivyo hivyo pengine huyu Yairo naye alimwona binti yake kuwa ni mzuri atakuja kuwa mcha Mungu kama Hana, au Sara, na kumletea fahari kwake, hivyo pengine akajitahidi kumlea katika maadili tangu anapozaliwa, mpaka anafikisha umri wa miaka 11, lakini alipofikisha umri wa miaka 12, ghafla akaanza kuona mabadiliko katika afya ya mtoto wake, miezi ya kwanza kwanza, hali inaanza kuwa mbaya mpaka inakaribia miezi ya katikati mtoto ndio yupo mauti uti kabisa,..katika hali kama hiyo anawaza afanyaje mtoto wake anakwenda kufa?
Je! Aruhusu maono yake yafe katika umri wa miaka 12,akizingatia kuwa ndio mwana pekee aliye naye? au afanye nini?. Lakini kama tunavyosoma habari, hakuruhusu jambo hilo litokee, hakuruhusu ndoto zake alizozihangaikia tangu zamani zizimwe na shetani katika mwaka wake wa 12 wa Maisha ya mwanawe, hapo ndipo akaanza safari ya kumtafuta Yesu.
Lakini huku nako upande wa pili, kulikuwa na mwanamke aliyetokwa na damu naye kwa muda mrefu, ambaye pia harakati zake za kutafuta uponyaji, zilianza tangu kipindi yule binti anazaliwa, tangu mwaka wa kwanza, akaendelea hivyo hivyo mpaka mwaka wa 2,..3…4, bila mafanikio mpaka mwaka wa 11, (Biblia inasema alikuwa ameshapoteza pesa zake nyingi kwa madaktari bila mafanikio) na ulipofika mwaka wa 12 bado hajapata alichokuwa anakitafuta, lakini naye siku moja akasikia Yesu yupo mjini..akasema sitakubali uponyaji wangu niliokuwa ninautafuta kwa miaka yote hii 12, leo hii ukatishwe na kukata tamaa, nitakwenda kukutana na Yesu.
Hivyo wote hawa wawili kila mmoja akaanza safari yake kivyake, na kama tunavyoisoma Habari Kristo aliwaponya wote, na wakapata walichokuwa wanakihangaikia, na kukiongojea.
Hata leo, tunapaswa tujifunze kuwa upo wakati wa kuyashindania yale maono ya kumtumikia Mungu ambayo tulikuwa tumeshaanza kuyafanya tangu zamani,haijalishi leo hii ni kipingamizi kikubwa kiasi gani kimesimama mbele yako, tunapaswa tuyashindanie…
Kwa kumkabidhisha Yesu hayo matatizo bila kuruhusu yaangamie kabisa..
Wapo watumishi ambao walishaanza kumtumikia Mungu,na walishapiga hatua fulani lakini pengine wakapitia vitisho Fulani vya ibilisi wakaacha kuhubiri, au kutumika. Ndugu usiruhusu taabu yako uliyoisumbukia iwe bure.
Kumbuka wapo wengine wamekuwa wakimwomba Mungu wapate kama tu hicho ulichonacho kwa muda mrefu, pengine tangu ulipoanza wewe kutumika, lakini bado hawajakipata, na hawakati tamaa kumwomba Yesu, na atawapa, kwanini wewe uruhusu kukata tamaa?
Mwaka wa 12 wa mtoto ya Yairo, Sio sawa na miaka 12 yule mwanamke aliyokuwa anangojea uponyaji wake..Hivyo na wewe, tatizo lako mpito lisikwamishe katika kazi yako ya utumishi Mungu aliyoiweka ndani yako.
Ili tushinde, ni lazima tushindane, Hivyo songa mbele.
Na sio tu kwenye kuifanya kazi ya Mungu, bali pia katika vitu vingine vyote unavyovitafuta vilivyo mapenzi ya Mungu, hupaswi kukata tamaa kabisa.
Bwana akubariki sana.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
kuota unatoka damu ya hedhi inamaanisha nini kibiblia?
Yapo mambo mawili;
Jambo la kwanza unapaswa ujue asilimia kubwa ya ndoto tunazoziota kila siku, si zote zina tafsiri ya rohoni kukusaidia, naweza kusema asilimia hata 90 ya unavyoviota kila siku vinatokana na ubongo wako wenyewe.
Ubongo wako Mungu kauumba kwa namna ambayo unaweza kuhifadhi kumbukumbu ya mambo unayofanya karibu kila siku, au mambo ambayo ulishawahi kuyapitia au mazingira ambayo ulishawahi kuyoana au kuwepo..
Kwahiyo katikati ya hayo yote, Ubongo wako utajiundia matukio na kuyachezesha akilini mwako wakati ukiwa umelala.
Biblia inasema hivi..
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;….”
Umeona? Kwamfano ikiwa wewe kazi yako ni uvuvi na mara nyingi huwa unakesha baharini kuvua, kuota ndoto unajiona unavua au unatengeneza nyavu, itakuwa ni kitu cha kawaida kwako kujirudia rudia mara kwa mara, halikadhalika kwa mpishi, au mwalimu, au mjenzi, kuota anafanya mojawapo ya ujuzi wake, litakuwa ni jambo la kawaida sana.
Vilevile katika hizo zipo ndoto ambazo zinaotwa na jinsia husika tu, kwamfano kuota unajifungua, hizi ndoto huwezi sikia zikiotwa na mwanaume, vivyo hivyo na kuota unatoka damu ya hedhi ni ndoto zinazowahusu wanawake peke yao, mwanaume hawezi kuota hivyo kwasababu jambo kama hilo hajawahi kulipitia katika Maisha yake yote,
Kwahiyo ndoto kama hii ikikujia isikusumbue sana. Elewa ni ndoto itokanayo na mazingira unayopitia.
Lakini pia jambo la pili ni kuwa.. Mungu anaweza kuzungumza na sisi, pia kwa njia hizo hizo za ndoto za mazingira yetu ya kila siku.
Kwamfano katika biblia utaona kulikuwa na wafungwa wawili waliokuwa gerezani na Yusufu, mmoja alikuwa anafanya kazi ya kumnywesha mfalme, na wa pili alikuwa ni mpishi. Siku moja wote wawili wakaota ndoto, na ndoto walizoota zililandana na mazingira yao ya kazi.. Lakini zilikuwa zimebeba ujumbe mzito kutoka kwa Mungu.
Mwanzo 40:5 “Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani.
6 Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.
7 Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?
8 Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.
9 Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu.
10 Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva.
11 Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.
12 Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu.
13 Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake……..
16 Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu.
17 Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.
18 Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu..
Ukiendelea kusoma pale utaona ni kweli, mambo hayo yaliwakuta vilevile kama Yusufu alivyowatafsiria.
Unaona sasa “point” hapo ni kuwa walichoota kiliendana na kazi zao au mazingira yao ya kila siku, yule wa kwanza alikuwa ni mnyweshaji wa mfalme akajiona anaweka divai mezani pa mfalme, kutoka katika mzabibu, ..Yule mwingine ni mpishi, aliona mikate kichwani pake.
Vivyo hivyo na wewe kuota unatoka damu ya hedhi, mara mara, na tena kama ndoto hiyo inakujia kwa uzito Fulani basi ujue upo ujumbe mzito Mungu wa Mungu nyuma yake.. Na ujumbe huo unatoka kwenye biblia.
Sasa ipo Habari moja ambayo pengine ulishawahi kuisikia, lakini leo hii nataka uifuatilie tena kwa ukaribu. Habari yenyewe ni kuhusu yule mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu kwa muda mrefu wa miaka 12. Tusome;
Luka 8:43 “Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.
46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.
47 Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.
48 Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani”.
Umeona mwanamke huyu, tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu, lilimgharimu pesa nyingi, kwa waganga, halikuweza kutatuliwa na mtu mwingine yeyote isipokuwa YESU TU PEKE YAKE.
Jiulize kwanini liwe ni kutokwa na damu, na si kingine?
Wewe unaota kutokwa na damu, jiweke katika nafasi ya huyo mwanamke, na ujue leo ni mahali gani sahihi pa kukimbilia.
Kama wewe hujaokoka, na unadhani dunia itakuwa ni jibu la Maisha yako, au utatuzi wa matatizo yako, leo hii ujue Mungu anasema na wewe kuwa UMEMWACHA YESU APITE.
Mungu anakuonyesha YESU tu ndio jibu la Maisha yako, haijalishi wewe ni muislamu, au dini gani,..Ni Yesu tu pekee ndiyo kila kitu kwako. Na anachotaka tu ni ushike pindo la vazi lake, aiponye roho yako.
Maana ya Kushika pindo la vazi lake, ni kuonyesha kuwa unahitaji msaada, hivyo hapo ulipo kama Maisha yako yapo dhambini, basi tubu leo, mpe Bwana Yesu Maisha yako. Na atakupokea na ataiponya roho yako, na hata mwili wako ikiwa una matatizo.
Hivyo ikiwa upo tayari kutubu leo na kutaka akufanye kuwa kiumbe kipya, akuponye misiba yako, akupe tumaini jipya, hata kama wewe ni muislamu, basi uamuzi huo ni wa busara sana. Hivyo fungua hapa Kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Jiunge na kundi la whatsapp kwa kubofya chini;
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tazama masomo mengine chini.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au kwa namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA?
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
Kuota upo gerezani kunamaanisha nini?
Ndoto ya namna hii inaanguka katika makundi makuu matatu (3) ya watu.
Sasa ni vizuri ukajitathmini kwanza wewe mwenyewe na ukajijua upo katika kundi lipi kati ya hayo, ili upate tafsiri sahihi ya ndoto yako. Sasa tukianzana na kundi la kwanza.
Ikiwa wewe unajijua kabisa umeokoka, na umesimama katika Imani na hakuna chochote kinachokuyumbisha, Lakini cha kushangaza umejikuta katika ndoto upo gerezani, au kifungoni na hujui utatokaje. Nataka nikumbie hupaswi kuwa na hofu,.Shetani anaona Imani yako, na bidii yako kwa Mungu, na hivyo atafanya kila njia kukuzuia, au pengine ameshaanza kufanya hivyo katika Imani yako, wewe kusonga mbele, atajaribu kukusonga usifike mahali Fulani, lakini hawezi kufanikiwa.
Ipo mifano kadha wa kadha katika biblia, utaona magwiji wote wa Imani walipokuwa wanafanikiwa katika kumcha Mungu shetani hakutulia tu hivi hivi, badala yake alinyanyua vikwazo vya vifungo. Kwamfano utamwona Yusufu, wakati alipokataa kulala na mke wa Boss wake (Potifa), alisingiziwa na kutupwa gerezani na akakaa kule kwa muda wa karibu miaka 2..Lakini Yusufu hakuacha kumcha Mungu, kwasasababu, vifungo haviwezi kumshika mteule wa Mungu daima, Na sote tunajua ni nini kilikuja kumpata Yusufu baada ya lile jaribu, ilikuwa ni kufanyika kuwa waziri mkuu wa Misri,
Vilevile utamwona Yeremia naye, alifungwa gerezani kwasababu alikuwa anawatabiria Israeli Habari za kweli za Mungu,(Soma vitabu vya Wafalme na Yeremia chote)
Utamwona tena Yohana Mbatizaji, yeye naye walimshika na kumtupa gerezani kisa tu, alimweleza mfalme Herode kosa lake la kuzini na mke wa ndugu yake, (Marko 6:17)
Halikadhalika utawaona mitume wa Kristo, akina Petro na Yohana vifungo viliwakuta, Paulo alipokuwa kuwa anasafiri katika ziara zake za kuhubiri injili Roho Mtakatifu alimshuhudia kabisa na kumwambia;
Matendo 20:23 “ isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo”.
Wakati mwingine alipokuwa na Sila, walimkamata na kumtupa gerezani, lakini wakiwa kule gerezani, hawakufadhaika, bali walimwimbia Mungu na kumsifu,
Matendo 16:25 “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza”.
Vivyo hivyo na wewe, ikiwa ni mkristo ambaye unajijua umesimama kikamilifu katika Imani, unaweza ukawa unapitia sasahivi vipingamizi vya kiimani, au vitakuja mbele yako kipindi sio kirefu, utakutana na shetani kutaka kukuzuia usisonge mbele na hicho unachomfanyia Mungu, basi usiogope, wewe fanya kama Paulo na Sila, zidi kumwimbia Mungu na kumsifu, na kuomba kwa bidii, kwasababu ipo hatua nzuri Zaidi Mungu anataka kukuvukisha.
Na ndio maana umeoteshwa ndoto kama hiyo upo gerezani, kifungoni. Usiogope, zidisha matendo yako kwa Mungu, wewe ni shujaa..
Lakini kama wewe ni mkristo ambaye ni vuguvugu au ulishaanza kupoa, hapo mwanzo ulikuwa umesimama lakini sasahivi ni kama vile umerudi nyuma, na umeota ndoto kama hii upo gerezani, Hiyo ni tahadhari kubwa sana kwako.
Kumbuka shetani anakuwinda usiku na mchana,..Kwenye biblia alikuwepo mtu mmoja aliyeitwa Samsoni, yeye ni mfano wa wakristo vuguvugu wa leo, alilaghaiwa na uongo wa shetani mpaka akatoa siri ya nguvu zake. Na wote tunajua kilichomkuta baada ya pale ni nini?.
Alitobolewa macho, akatupwa gerezani na kufanyishwa kazi hata Zaidi ya punda..
Waamuzi 16:21 “Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza”
Ndivyo ilivyo hata na wewe, Mungu amekuotesha upo gerezani, ni kwamba upo karibuni kutekwa na ibilisi au pengine tayari ameshakuteka kabisa..Biblia inasema kurudi kwake nyuma mpumbavu kutamwangamiza.
Hivyo unachopaswa kufanya ni kutubu na kumgeukia Mungu haraka sana, kama unafanya mambo ambayo hayampendezi heri uache mara moja, Kwasababu Mungu hataki uangamie. Na ndio maana kakupa tahadhari hiyo.
Lakini sasa kama wewe, upo dhambini tangu zamani, hujawahi kuwa na Habari na Mungu, kisha umeota upo gerezani,..Ni Mungu anazungumza na wewe, na kukuonyesha hali yako ilivyo rohoni. Kwamba upo vifungoni, shetani amekunasa, shetani anaitesa roho yako.
Lakini habari njema ni kuwa lengo kuu mojawapo la Yesu kutumwa duniani ilikuwa ni kuwafungua na kuwaacha huru waliofungwa na ibilisi..
Hivyo ikiwa wewe ni mkristo jina tu, au mwislamu, au muhindu, au mpagani,.. Sikiliza unabii Mungu aliompa Yesu zamani..alisema.
Isaya 42:6 “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa;
7 kuyafunua macho ya vipofu, KUWATOA GEREZANI WALIOFUNGWA, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu”
Na ndio maana Yesu alisema..
Zaburi 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, KUWATANGAZIA MATEKA UHURU WAO, NA HAO WALIOFUNGWA HABARI ZA KUFUNGULIWA KWAO”.
Hivyo leo umejiona upo vifungoni, pengine unateseka kutafuta njia ya kutoka huwezi, Yesu anakuita leo akuokoe,.
Zaburi 69:33 “Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake”.
Ukimpokea Yesu, atafanya mabadiliko makubwa katika Maisha yako, atakufungua katika laana nyingi ambazo hata wewe mwenyewe hukuwahi kuzijua, laana za ukoo, na laana za mapepo na majini, ikiwa utakuwa tu tayari leo kusema Bwana Yesu njoo niokoe yote hayo yatafanyika kwako.
Kwahiyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Na ukimaliza kufanya hivyo basi Kristo anaanza sasa kuyafanya mabadiliko hayo moyoni mwako, na utaona jinsi anavyokufungua kifungo kimoja mpaka kingine. Kama alitufanyia sisi hivyo, atakufanyia na wewe, Hivyo amini tu na fungua moyo wako!
Bwana akubariki.
Pia tazama mafundisho mengine chini tayakusaidia kiroho sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au kwa namba hii +255 789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
RABI, UNAKAA WAPI?
TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
MTETEZI WAKO NI NANI?
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
KIAMA KINATISHA.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Jina la Bwana libarikiwe.
Kuna kitu kimoja cha kipekee ambacho Mungu katuumbia sisi wanadamu “nacho ni uponyaji wa asili”
Huu uponyaji wa asili upo katika miili yetu na vile vile upo katika roho zetu. Na huo Uponyaji tumepewa bure wanadamu wote kama zawadi na Mungu wetu, na huo hauhitaji uwe mkristo au utumie jina la Yesu kuupata. Upo tu Mungu kauweka ndani ya kila mtu.
Kwamfano unapojikata na kisu mkononi kwa bahati mbaya, inaweza kukuchukua wiki kadhaa tu kupona na nyama yako ikarudi vile vile, au unapoanguka na kuchubuka sehemu ya mwili wako, baada ya wiki kadhaa au mwezi Ngozi yako itakuwa imesharudia katika hali yake kama ilivyokuwa mwanzo, litabaki kovu tu lakini si jeraha!..
Kwahiyo ni kitendo cha muda tu..lakini mwisho wa siku utapona majeraha yako yote. Vinginevyo Mungu wetu asingeuweka huo uponyaji wa asili basi dunia ingekuwa ni jehanamu..pangekuwa si mahali pa kuishi.
Na katika roho ni hivyo hivyo, yapo majeraha ya rohoni ambayo mtu unaweza kuumizwa au kujiumiza mwenyewe. Majeraha hayo yanaweza kutokana na mambo Fulani Fulani ya kimaisha, na hayo pia Mungu kayawekea uponyaji wake wa asili…
Ndio maana unaweza ukakasirika sana sasahivi, ukapita muda kadhaa ile hasira inaanza kutulia na mwishowe inaisha kabisa… hapo ni uponyaji unafanya kazi yake.
Hivyo kama vile tunavyotumia njia za kuponya majeraha ya nje tutumie njia hiyo hiyo kuyatibu yale ya ndani.
Tukiumia kwa majeraha ya nje kama vidonda, huwa tunavisafisha vizuri, tunavipaka dawa na kisha tunavifunga..na kikubwa Zaidi tunahakikisha hatuvitoneshi, baada ya siku moja au mbili tunarudia tena hilo zoezi, mpaka mwishoni tunapona kabisa. Sasa zoezi hilo la kukisafisha na kukifunga na kuzuia kukitonesha ndilo litasaidia kidonda kile kipone haraka, lakini kisipofanyiwa matunzo hayo..basi hakitapona haraka, na matokeo yake kinaweza kuzidi kuwa kikubwa Zaidi na kutengeneza tatizo lingine likubwa zaidi.
Na majeraha ya ndani tunayaponya kwa njia hiyo hiyo. Pale tunapoumizwa na watu au mazingira Fulani kama wakristo, njia ni hiyo hiyo;
Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.
Fanya hivyo siku ya kwanza, rudia tena siku zinazofuata, kila siku soma maandiko, funga, omba na usijikumbushe kumbushe…Kwa kufanya hivyo nakuambia ukweli..Haitapita kipindi kirefu utaona mabadiliko makubwa sana. Utapona majeraha yako ya muda mfupi sana. Kwasababu umeiwekea mazingira yanayofaa, ile nguvu ya uponyaji wa asili kufanya kazi ndani yako.
Lakini usipofanya hivyo..Utakuwa na majeraha ambayo hayaponyeki kila kukicha…Utaishi Maisha ya kuumia kila siku, na ya chuki, na ya vinyongo. Kila mtu utamwona ni adui yako, na kila Neno litakuwa linakuumiza. Utakuwa na majeraha ya miaka 20 iliyopita ambayo hayajapona bado! Utakuwa mtu wa kutokusamehe…Nakuambia ukweli sio mpango wa Mungu kuwa na majeraha ya rohoni kwa miaka 10..Ukiona una kinyongo, au bado unaumia kwa jambo lililotokea miaka 10 au 20 iliyopita..jaribu kutafuta suluhisho mapema..kwasababu kuna uwezekano nguvu ya msamaha haipo ndani yako, na jeraha unapozidi kuliacha huwa ndio linazidi kuwa kubwa kila siku na kuweza kuzaa tatizo kubwa Zaidi ya hilo.
Zaburi 38:5 “Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu”
Na sababu ya kutopona majeraha ndio hizo hapo juu kutofunga jeraha na kutoweka dawa!.. Unaweza kuwa unatatizo la kutopata mtoto, na ukasikia watu wanakusema vibaya..na hilo likawa ni jeraha kwako!..lakini kama Neno la Mungu halipo ndani yako; kama hujui Habari za akina Sara na wengineo ambao Mungu aliwafungua matumbo katika uzee wao, kama hujui Habari za Hana na Raheli ambao walisemwa kupita maelezo, basi hutaweza kupona haraka jeraha ulilonalo. Kwahiyo Neno la Mungu ndio dawa, inayoharakisha uponyaji wa ki-Mungu.
Zaburi 147:3 “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao”
Ndicho kinachowakuta watu wasiolijua Neno la Mungu (watu wa kidunia), wanahangaika na majeraha ya muda mrefu yasiyopona kwasababu hawana dawa, wala hawaijui dawa..Hivyo jeraha lolote lililo ndani yako, lisiwe kikwazo cha wewe kuikosa mbingu anza sasa kuusafisha moyo wako.
Bwana akubariki.
Mwisho kama hujaokoka, wakati umeenda sana, wakati wowote Kristo anarudi, biblia inasema..itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima halafu tupate hasara za nafsi zetu?. Mambo ya ulimwengu yanapita lakini Neno la Mungu lipo pale pale. Mgueukie leo Kristo, utubu dhambi zako, uoshwe kwa damu yake, ukabatizwe na kisha upokee Roho Mtakatifu, ambaye atakuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko.
Maran atha
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.
MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.
NAO WAKADHANI YA KUWA YUMO KATIKA MSAFARA;
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
JIRANI YANGU NI NANI?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.