Title 2020

MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.

Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. kwa link hii >> https://chat.whatsapp.com/GRri9BATojl2FNGbOJpjC6

Masomo mbalimbali ya Neno la Mungu.


Awali ya yote nakupa hongera kwa kupenda kutafuta kujifunza Neno la Mungu, lipo kusudi la Mungu kukufikisha hapa, biblia inatuambia..

1Timotheo 4:13 “…ufanye bidii katika kusoma…”

Ni wachache sana katika  wengi wanaozunguka mitandaoni kutafuta mambo ya msingi kama wewe.

Na unajua nini? bidii yako sio bure, Bwana Yesu alisema,

1Timotheo 4:13 “…ufanye bidii katika kusoma

Mathayo 7:8 “kwa maana kila..atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”.

Na pia alisema..

Mathayo 5:6 “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa’.

Kwahiyo unachokitafuta Bwana atakupatia, na pengine hata zaidi ya kile ulichokuwa unakitazamia,


Mahali hapa utakutana na masomo  mbalimbali ya Neno la Mungu, zaidi ya 1,000, na maswali mengi ya biblia yaliyojibiwa. Kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi kitabu cha ufunuo.

Ili kuingia katika horodha ya masomo ya mbalimbali ya Neno la Mungu, fungua hapa>>> MASOMO MAPYA

Ili kusoma maswali ya biblia yaliyoulizwa na kujibiwa fungua hapa >>> MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA

Ili kusoma shuhuda za Mashahidi wa Imani wa kale fungua hapa >>> WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

Je! ulishawahi kujiuliza Unyakuo ni nini, na utakuwaje? Na kwanini Bwana  Yesu alisema, Amin! Amin! Nawaambia kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatakapotokea, kusema kule kulimaanisha  nini? Tazama hapa >> AMIN, NAWAAMBIA, KIZAZI HIKI HAKITAPITA,

Je! Unafahamu kuwa kanisa tunaloishi mimi na wewe ndio kanisa la Mwisho lijulikanalo kama Laodikia? Tayari makanisa 6 yalishapita, na sasa tupo katika kanisa la mwisho? >>> AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

https://www.high-endrolex.com/16

Je unafahamu Historia ya nyimbo mbalimbali  za Tenzi>> TENZI ZA ROHONI

Je! Unajua Sadaka ni nini? Na umuhimu wake kwetu>> NGUVU YA SADAKA.

Je! Unajua aina za upendo, na upi tunapaswa tuwe nao?>> UPENDO NI NINI ?

Fahamu juu ya chukizo la uharibifu lililozungumziwa na Danieli na Bwana Yesu >> CHUKIZO LA UHARIBIFU

Ijue siku ya Bwana itakuwaje>> KIAMA KINATISHA.

Kwanini shetani aitwe nyoka wa zamani >> YULE JOKA WA ZAMANI.

Mbinguni ni wapi? Na je kuna aina ngapi za mbingu>> MBINGUNI NI WAPI?

Kuna siri gani katika kitabu cha Ruthu, kwanini kiandikwe na wakati yeye hakuwa mwanamke wa Kiyahudi, >>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:

Ni siri gani imelala katika kitabu cha Esta juu ya Kristo na kanisa lake? >>> ESTA: Mlango wa 1

Mfahamu Melkizedeki, Je! alikuwa ni nani? Na kwanini awe hana baba wala mama, wala mwanzo wa siku wala mwisho? >>HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?

Utawala wa miaka 1000 ni utawala gani? >>> UTAWALA WA MIAKA 1000.

Kitabu cha Danieli kina maudhui gani? Je naweza kupata uchambuzi wake tangu mwanzo hadi mwisho? >>> DANIELI: Mlango wa 1

Ubatizo sahihi ni upi? Kulingana na maandiko. >> UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?

Nahitaji kuokoka je nifanyaje?. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA


Kama utapenda masomo haya yawe yanakufikia kwa njia ya email/ whatsapp tutumie ujumbe katika namba hii :+255693036618 / +255 789001312

Print this post

USICHOKE KUNGOJEA, WALA USIKATISHWE TAMAA.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima, Nakukaribisha tena tuyatafakari maneno ya uzima.

Leo tutatazama kwa ufupi Habari ya watu wawili. Wakwanza ni mtu mmoja anayeitwa Yairo mkuu wa sinagogi, na wa pili ni mwanamke mmoja aliyekuwa anatokwa na damu kwa muda mrefu lakini baadaye alikuja kuponywa na Bwana Yesu kwa kulishika tu pindo la vazi lake.

Sasa lipo jambo moja la kusisimua nataka ulione kwa hawa watu wawili ambalo kila mmoja lilikuwa kichwani mwake. Embu tusome kidogo;

Luka 8:40 “Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote.

41 Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;

42 kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.

43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,

44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma”.

Sasa ukiangalia hapo, utaona huyu Yairo, alikuwa na binti yake aliyepatwa na matatizo katika umri wake wa miaka kumi na miwili (12), Na wakati huo huo alikuwepo yule mwanamke alitokwa na damu kwa muda wa miaka kumi na miwili (12). Ipo sababu kwanini biblia imeutaja umri wa mtoto na muda wa mwanamke kutokwa damu.

Kwamfano biblia inatuambia huyu Yairo hakuwa na mwana mwingine isipokuwa yule binti tu, pengine alimlea kwa taabu na shida, akiwa na matumaini kuwa huyu ndiye atakayekuja kuwa heshima yake ukubwani, pengine aliona mwelekeo mzuri wa binti yake, kama vile Yokebedi(mama yake Musa) alivyoona uzuri wa Musa tangu akiwa mdogo, akaamua kumficha ambapo kweli baadaye tunaona akaja kuwa nyota ya Israeli mwokozi wa Israeli,

Vivyo hivyo pengine huyu Yairo naye alimwona binti yake kuwa ni mzuri atakuja kuwa mcha Mungu kama Hana, au Sara, na kumletea fahari kwake, hivyo pengine akajitahidi kumlea katika maadili tangu anapozaliwa, mpaka anafikisha umri wa miaka 11, lakini alipofikisha umri wa miaka 12, ghafla akaanza kuona mabadiliko katika afya ya mtoto wake, miezi ya kwanza kwanza, hali inaanza kuwa mbaya mpaka inakaribia miezi ya katikati mtoto ndio yupo mauti uti kabisa,..katika hali kama hiyo anawaza afanyaje mtoto wake anakwenda kufa?

Je! Aruhusu maono yake yafe katika umri wa miaka 12,akizingatia kuwa ndio mwana pekee aliye naye? au afanye nini?. Lakini kama tunavyosoma habari, hakuruhusu jambo hilo litokee, hakuruhusu ndoto zake alizozihangaikia tangu zamani zizimwe na shetani katika mwaka wake wa 12 wa Maisha ya mwanawe, hapo ndipo akaanza safari ya kumtafuta Yesu.

Lakini huku nako upande wa pili, kulikuwa na mwanamke aliyetokwa na damu naye kwa muda mrefu, ambaye pia harakati zake za kutafuta uponyaji, zilianza tangu kipindi yule binti anazaliwa, tangu mwaka wa kwanza, akaendelea hivyo hivyo mpaka mwaka wa 2,..3…4, bila mafanikio mpaka mwaka wa 11, (Biblia inasema alikuwa ameshapoteza pesa zake nyingi kwa madaktari bila mafanikio) na ulipofika mwaka wa 12 bado hajapata alichokuwa anakitafuta, lakini naye siku moja akasikia Yesu yupo mjini..akasema sitakubali uponyaji wangu niliokuwa ninautafuta kwa miaka yote hii 12, leo hii ukatishwe na kukata tamaa, nitakwenda kukutana na Yesu.

Hivyo wote hawa wawili kila mmoja akaanza safari yake kivyake, na kama tunavyoisoma Habari Kristo aliwaponya wote, na wakapata walichokuwa wanakihangaikia, na kukiongojea.

Hata leo, tunapaswa tujifunze kuwa upo wakati wa kuyashindania yale maono ya kumtumikia Mungu ambayo tulikuwa tumeshaanza kuyafanya tangu zamani,haijalishi leo hii ni kipingamizi kikubwa kiasi gani kimesimama mbele yako, tunapaswa tuyashindanie…

Kwa kumkabidhisha Yesu hayo matatizo bila kuruhusu yaangamie kabisa..

Wapo watumishi ambao walishaanza kumtumikia Mungu,na walishapiga hatua fulani lakini pengine wakapitia vitisho Fulani vya ibilisi wakaacha kuhubiri, au kutumika. Ndugu usiruhusu taabu yako uliyoisumbukia iwe bure.

Kumbuka wapo wengine wamekuwa wakimwomba Mungu wapate kama tu hicho ulichonacho kwa muda mrefu, pengine tangu ulipoanza wewe kutumika, lakini bado hawajakipata, na hawakati tamaa kumwomba Yesu, na atawapa, kwanini wewe uruhusu kukata tamaa?

Mwaka wa 12 wa mtoto ya Yairo, Sio sawa na miaka 12 yule mwanamke aliyokuwa anangojea uponyaji wake..Hivyo na wewe, tatizo lako mpito lisikwamishe katika kazi yako ya utumishi Mungu aliyoiweka ndani yako.

Ili tushinde, ni lazima tushindane, Hivyo songa mbele.

Na sio tu kwenye kuifanya kazi ya Mungu, bali pia katika vitu vingine vyote unavyovitafuta vilivyo mapenzi ya Mungu, hupaswi kukata tamaa kabisa.

Bwana akubariki sana.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

KUOTA UMEFUNGA NDOA.

NENO LA MUNGU NI DAWA ILIYO TOFAUTI NA DAWA NYINGINE.

FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUOTA UNATOKA DAMU YA HEDHI.

kuota unatoka damu ya hedhi inamaanisha nini kibiblia?


Yapo mambo mawili;

Jambo la kwanza unapaswa ujue asilimia kubwa ya ndoto tunazoziota kila siku, si zote zina tafsiri ya rohoni kukusaidia, naweza kusema asilimia hata 90 ya unavyoviota kila siku vinatokana na ubongo wako wenyewe.

Ubongo wako Mungu kauumba kwa namna ambayo unaweza kuhifadhi kumbukumbu ya mambo unayofanya karibu kila siku, au mambo ambayo ulishawahi kuyapitia au mazingira ambayo ulishawahi kuyoana au kuwepo..

Kwahiyo katikati ya hayo yote, Ubongo wako utajiundia matukio na kuyachezesha akilini mwako wakati ukiwa umelala.

Biblia inasema hivi..

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;….”

Umeona? Kwamfano ikiwa wewe kazi yako ni uvuvi na mara nyingi huwa unakesha baharini kuvua, kuota ndoto unajiona unavua au unatengeneza nyavu, itakuwa ni kitu cha kawaida kwako kujirudia rudia mara kwa mara, halikadhalika kwa  mpishi, au mwalimu, au mjenzi, kuota anafanya mojawapo ya ujuzi wake, litakuwa ni jambo la kawaida sana.

Vilevile katika hizo zipo ndoto ambazo zinaotwa na jinsia husika tu, kwamfano kuota unajifungua, hizi ndoto huwezi sikia zikiotwa na mwanaume, vivyo hivyo na kuota unatoka damu ya hedhi ni ndoto zinazowahusu wanawake peke yao, mwanaume hawezi kuota hivyo kwasababu jambo kama hilo hajawahi kulipitia katika Maisha yake yote,

Kwahiyo ndoto kama hii ikikujia isikusumbue sana. Elewa ni ndoto itokanayo na mazingira unayopitia.

Lakini pia jambo la pili ni kuwa.. Mungu anaweza kuzungumza na sisi, pia kwa njia hizo hizo za ndoto za mazingira yetu ya kila siku.

Kwamfano katika biblia utaona kulikuwa na wafungwa wawili waliokuwa gerezani na Yusufu, mmoja alikuwa anafanya kazi ya kumnywesha mfalme, na wa pili alikuwa ni mpishi. Siku moja wote wawili wakaota ndoto, na ndoto walizoota zililandana na mazingira yao ya kazi.. Lakini zilikuwa zimebeba ujumbe mzito kutoka kwa Mungu.

Mwanzo 40:5 “Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. 

6 Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika. 

7 Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? 

8 Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie. 

9 Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu. 

10 Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva. 

11 Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake. 

12 Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. 

13 Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake……..

16 Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu. 

17 Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu. 

18 Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu..

Ukiendelea kusoma pale utaona ni kweli, mambo hayo yaliwakuta vilevile kama Yusufu alivyowatafsiria.

Unaona sasa “point” hapo ni kuwa walichoota kiliendana na kazi zao au mazingira yao ya kila siku, yule wa kwanza alikuwa ni mnyweshaji wa mfalme akajiona anaweka divai mezani pa mfalme, kutoka katika mzabibu, ..Yule mwingine ni mpishi, aliona mikate kichwani pake.

Vivyo hivyo na wewe kuota unatoka damu ya hedhi, mara mara,  na tena kama ndoto hiyo inakujia kwa uzito Fulani basi ujue upo ujumbe mzito Mungu wa Mungu nyuma yake.. Na ujumbe huo unatoka kwenye biblia.

Sasa ipo Habari moja ambayo pengine ulishawahi kuisikia, lakini leo hii nataka uifuatilie tena kwa ukaribu. Habari yenyewe ni kuhusu yule mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu kwa muda mrefu wa miaka 12. Tusome;

Luka 8:43  “Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,

44  alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.

45  Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.

46  Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.

47  Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.

48  Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani”.

Umeona mwanamke huyu, tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu, lilimgharimu pesa nyingi, kwa waganga, halikuweza kutatuliwa na mtu mwingine yeyote isipokuwa YESU TU PEKE YAKE.

Jiulize kwanini liwe ni kutokwa na damu, na si kingine?

Wewe unaota kutokwa na damu, jiweke katika nafasi ya huyo mwanamke, na ujue leo ni mahali gani sahihi pa kukimbilia.

Kama wewe hujaokoka, na unadhani dunia itakuwa ni jibu la Maisha yako, au utatuzi wa matatizo yako, leo hii ujue Mungu anasema na wewe kuwa  UMEMWACHA YESU APITE.

Mungu anakuonyesha YESU tu ndio jibu la Maisha yako, haijalishi wewe ni muislamu, au dini gani,..Ni Yesu tu pekee ndiyo kila kitu kwako. Na anachotaka tu ni ushike pindo la vazi lake, aiponye roho yako.

Maana ya Kushika pindo la vazi lake, ni kuonyesha kuwa unahitaji msaada, hivyo hapo ulipo kama Maisha yako yapo dhambini, basi tubu leo, mpe Bwana Yesu Maisha yako. Na atakupokea na ataiponya roho yako, na hata mwili wako ikiwa una matatizo.

Hivyo ikiwa upo tayari kutubu leo na kutaka akufanye kuwa kiumbe kipya, akuponye misiba yako, akupe tumaini jipya, hata kama wewe ni muislamu,  basi uamuzi huo ni wa busara sana. Hivyo fungua hapa  Kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Jiunge na kundi la whatsapp kwa kubofya chini;

Group la whatsapp  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tazama masomo mengine chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au kwa namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA?

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

MAANA YA MAJINA NA TAFSIRI ZAKE.

KUOTA NYOKA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUOTA UPO GEREZANI.

Kuota upo gerezani kunamaanisha nini?


Ndoto ya namna hii inaanguka katika makundi makuu matatu (3) ya watu.

  1. Mtu aliyeokoka
  2. Mtu aliye vuguvugu (Nusu kaokoka nusu dhambini)
  3. Mtu mwenye dhambi

Sasa ni vizuri ukajitathmini kwanza wewe mwenyewe na ukajijua upo katika kundi lipi kati ya hayo, ili upate tafsiri sahihi ya ndoto yako. Sasa tukianzana na kundi la kwanza.

1. Mtu aliyeokoka.(kuota upo gerezani)

Ikiwa wewe unajijua kabisa umeokoka, na umesimama katika Imani na hakuna chochote kinachokuyumbisha, Lakini cha kushangaza umejikuta katika ndoto upo gerezani, au kifungoni na hujui utatokaje. Nataka nikumbie hupaswi kuwa na hofu,.Shetani anaona Imani yako, na bidii yako kwa Mungu, na hivyo atafanya kila njia kukuzuia, au pengine ameshaanza kufanya hivyo katika Imani yako, wewe kusonga mbele, atajaribu kukusonga usifike mahali Fulani, lakini hawezi kufanikiwa.

Ipo mifano kadha wa kadha katika biblia, utaona magwiji wote wa Imani walipokuwa wanafanikiwa katika kumcha Mungu shetani hakutulia tu hivi hivi, badala yake alinyanyua vikwazo vya vifungo. Kwamfano utamwona Yusufu, wakati alipokataa kulala na mke wa Boss wake (Potifa), alisingiziwa na kutupwa gerezani na akakaa kule kwa muda wa karibu miaka 2..Lakini Yusufu hakuacha kumcha Mungu, kwasasababu, vifungo haviwezi kumshika mteule wa Mungu daima,  Na sote tunajua ni nini kilikuja kumpata Yusufu baada ya lile jaribu, ilikuwa ni kufanyika kuwa waziri mkuu wa Misri,

Vilevile utamwona Yeremia naye, alifungwa gerezani kwasababu alikuwa anawatabiria Israeli Habari za kweli za Mungu,(Soma vitabu vya Wafalme na Yeremia chote)

Utamwona tena Yohana Mbatizaji, yeye naye walimshika na kumtupa gerezani kisa tu, alimweleza mfalme Herode kosa lake la kuzini na mke wa ndugu yake, (Marko 6:17)

Halikadhalika utawaona mitume wa Kristo, akina Petro na Yohana vifungo viliwakuta, Paulo alipokuwa kuwa anasafiri katika ziara zake za kuhubiri injili Roho Mtakatifu alimshuhudia kabisa na kumwambia;

Matendo 20:23 “ isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.24  Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo”.

Wakati mwingine alipokuwa na Sila, walimkamata na kumtupa gerezani, lakini wakiwa kule gerezani, hawakufadhaika, bali walimwimbia Mungu na kumsifu,

Matendo 16:25  “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza”.

Vivyo hivyo na wewe, ikiwa ni mkristo ambaye unajijua umesimama kikamilifu katika Imani, unaweza ukawa unapitia sasahivi vipingamizi  vya kiimani, au vitakuja mbele yako kipindi sio kirefu, utakutana na shetani kutaka kukuzuia usisonge mbele na hicho unachomfanyia Mungu, basi usiogope, wewe fanya kama Paulo na Sila, zidi kumwimbia Mungu na kumsifu, na kuomba kwa bidii, kwasababu ipo hatua nzuri Zaidi Mungu anataka kukuvukisha.

Na ndio maana umeoteshwa ndoto kama hiyo upo gerezani, kifungoni. Usiogope, zidisha matendo yako kwa Mungu, wewe ni shujaa..

2. Mtu aliye vuguvugu.

Lakini kama wewe ni mkristo ambaye ni vuguvugu au ulishaanza kupoa, hapo mwanzo ulikuwa umesimama lakini sasahivi ni kama vile umerudi nyuma, na umeota ndoto kama hii upo gerezani, Hiyo ni tahadhari kubwa sana kwako.

Kumbuka shetani anakuwinda usiku na mchana,..Kwenye biblia alikuwepo mtu mmoja aliyeitwa Samsoni, yeye ni mfano wa wakristo vuguvugu wa leo, alilaghaiwa na uongo wa shetani mpaka akatoa siri ya nguvu zake. Na wote tunajua kilichomkuta baada ya pale ni nini?.

Alitobolewa macho, akatupwa gerezani na kufanyishwa kazi hata Zaidi ya punda..

Waamuzi 16:21 “Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza”

Ndivyo ilivyo hata na wewe, Mungu amekuotesha upo gerezani, ni kwamba upo karibuni kutekwa na ibilisi au pengine tayari ameshakuteka kabisa..Biblia inasema kurudi kwake nyuma mpumbavu kutamwangamiza.

Hivyo unachopaswa kufanya ni kutubu na kumgeukia Mungu haraka sana, kama unafanya mambo ambayo hayampendezi heri uache mara moja, Kwasababu Mungu hataki uangamie. Na ndio maana kakupa tahadhari hiyo.

3. Mtu mwenye dhambi.(kuota upo gerezani)

Lakini sasa kama wewe, upo dhambini tangu zamani, hujawahi kuwa na Habari na Mungu, kisha  umeota upo gerezani,..Ni Mungu anazungumza na wewe, na kukuonyesha hali yako ilivyo rohoni. Kwamba upo vifungoni, shetani amekunasa, shetani anaitesa roho yako.

Lakini habari njema ni kuwa lengo kuu mojawapo la Yesu kutumwa duniani ilikuwa ni kuwafungua na kuwaacha huru waliofungwa na ibilisi..

Hivyo ikiwa wewe ni mkristo jina tu, au mwislamu, au muhindu, au mpagani,.. Sikiliza unabii Mungu aliompa Yesu zamani..alisema.

Isaya 42:6 “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; 

7 kuyafunua macho ya vipofu, KUWATOA GEREZANI WALIOFUNGWA, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. 

8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu”

Na ndio maana Yesu alisema..

Zaburi 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, KUWATANGAZIA MATEKA UHURU WAO, NA HAO WALIOFUNGWA HABARI ZA KUFUNGULIWA KWAO”.

Hivyo leo umejiona upo vifungoni, pengine unateseka kutafuta njia ya kutoka huwezi, Yesu anakuita leo akuokoe,.

Zaburi 69:33 “Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake”.

Ukimpokea Yesu, atafanya mabadiliko makubwa katika Maisha yako, atakufungua katika laana nyingi ambazo hata wewe mwenyewe hukuwahi kuzijua, laana za ukoo, na laana za mapepo na majini, ikiwa utakuwa tu tayari leo kusema Bwana Yesu njoo niokoe yote hayo yatafanyika kwako.

Kwahiyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa  kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na ukimaliza kufanya hivyo basi Kristo anaanza sasa kuyafanya mabadiliko hayo moyoni mwako, na utaona jinsi anavyokufungua kifungo kimoja mpaka kingine. Kama alitufanyia sisi hivyo, atakufanyia na wewe, Hivyo amini tu na fungua moyo wako!

Bwana akubariki.

Pia tazama mafundisho mengine chini tayakusaidia kiroho sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au kwa namba hii +255 789001312

Group la whatsapp  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Mada Nyinginezo:

RABI, UNAKAA WAPI?

TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MTETEZI WAKO NI NANI?

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

KIAMA KINATISHA.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

UPONYAJI WA ASILI

Jina la Bwana libarikiwe.

Kuna kitu kimoja cha kipekee ambacho Mungu katuumbia sisi wanadamu “nacho ni uponyaji wa asili”

Huu uponyaji wa asili upo katika miili yetu na vile vile upo katika roho zetu. Na huo Uponyaji tumepewa bure wanadamu wote kama zawadi na Mungu wetu, na huo hauhitaji uwe mkristo au utumie jina la Yesu kuupata. Upo tu Mungu kauweka ndani ya kila mtu.

Kwamfano unapojikata na kisu mkononi kwa bahati mbaya, inaweza kukuchukua wiki kadhaa tu kupona na nyama yako ikarudi  vile vile, au unapoanguka na kuchubuka sehemu ya mwili wako, baada ya wiki kadhaa au mwezi Ngozi yako itakuwa imesharudia katika hali yake kama ilivyokuwa mwanzo, litabaki kovu tu lakini si jeraha!..

Kwahiyo ni kitendo cha muda tu..lakini mwisho wa siku utapona majeraha yako yote. Vinginevyo Mungu wetu asingeuweka huo uponyaji wa asili basi dunia ingekuwa ni jehanamu..pangekuwa si mahali pa kuishi.

Na katika roho ni hivyo hivyo, yapo majeraha ya rohoni ambayo mtu unaweza kuumizwa au kujiumiza mwenyewe. Majeraha hayo yanaweza kutokana na mambo Fulani Fulani ya kimaisha, na hayo pia Mungu kayawekea uponyaji wake wa asili…

Ndio maana unaweza ukakasirika sana sasahivi, ukapita muda kadhaa ile hasira inaanza kutulia na mwishowe inaisha kabisa… hapo ni uponyaji unafanya kazi yake.

Hivyo kama vile tunavyotumia njia za kuponya majeraha ya nje tutumie njia hiyo hiyo kuyatibu yale ya ndani.

Tukiumia kwa majeraha ya nje kama vidonda, huwa tunavisafisha vizuri, tunavipaka dawa na kisha tunavifunga..na kikubwa Zaidi tunahakikisha hatuvitoneshi, baada ya siku moja au mbili tunarudia tena hilo zoezi, mpaka mwishoni tunapona kabisa. Sasa zoezi hilo la kukisafisha na kukifunga na kuzuia kukitonesha ndilo litasaidia kidonda kile kipone haraka, lakini kisipofanyiwa matunzo hayo..basi hakitapona haraka, na matokeo yake kinaweza kuzidi kuwa kikubwa Zaidi na kutengeneza tatizo lingine likubwa zaidi.

Na majeraha ya ndani tunayaponya kwa njia hiyo hiyo. Pale tunapoumizwa na watu au mazingira Fulani kama wakristo, njia ni hiyo hiyo;

  1. Kwanza unaliosha jeraha lako: Maana yake unaondoa vitu vyote vya kando kando ambavyo vinaweza kukusababishia jeraha kuwa kubwa Zaidi. Hiyo ikiwapo kulikumbuka kumbuka lile tukio. Katika hatua hii bado maumivu utakuwa unayasikia.

  2. Unapaka dawa: Dawa ni Neno la Mungu; Hichi ni kipengele cha muhimu sana..Yapo maandiko mengi katika biblia yanayohusiana na hali unayopitia…Kama umeumizwa kwa kuaibishwa kwa kuzungumziwa maneno mabaya, vipo visa kama vyako katika biblia, kavisome hivyo ndio dawa ya majeraha unayopitia, kama umerushwa vipo visa vya waliorushwa katika biblia na Mungu akawaponya katika shida zao, kama ni tatizo kwa mume wako/mke wako, vipo visa vingi kama vyako katika biblia ambavyo Mungu aliwaponya watu n.k. Hiyo ndio dawa, n.k. Biblia inafariji, biblia inajengwa, biblia ina amanisha.

Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.

  1. Funga jeraha lako: Baada ya kupaka dawa (kwa maandiko), unalifunga jeraha lako,..Maana yake unasali (huu ni wakati wa wewe kufunga na kusali)…Neno la Mungu (ambalo ni dawa) linaambata na kufunga na kusali.. Unaposali unamzuia adui shetani, kukuletea majaribu ya kuzidi kuliongeza jeraha lako. Maombi ya kufunga yanaizuia sumu ya adui kuingia katika jeraha unalolipitia.(Mathayo 17:21)

  2. Usijitoneshe: Hii ni hatua ya mwisho..hakikisha hujitoneshi toneshi..hii ni ile hali ya kukumbuka kumbuka lile tukio na kulifikiri fikiri, jitahidi kwa kadri uwezavyo kutoliweka akilini.

Fanya hivyo siku ya kwanza, rudia tena siku zinazofuata, kila siku soma maandiko, funga, omba na usijikumbushe kumbushe…Kwa kufanya hivyo nakuambia ukweli..Haitapita kipindi kirefu utaona mabadiliko makubwa sana. Utapona majeraha yako ya muda mfupi sana. Kwasababu umeiwekea mazingira yanayofaa, ile nguvu ya uponyaji wa asili kufanya kazi ndani yako.

Lakini usipofanya hivyo..Utakuwa na majeraha ambayo hayaponyeki kila kukicha…Utaishi Maisha ya kuumia kila siku, na ya chuki, na ya vinyongo. Kila mtu utamwona ni adui yako, na kila Neno litakuwa linakuumiza. Utakuwa na majeraha ya miaka 20 iliyopita ambayo hayajapona bado! Utakuwa mtu wa kutokusamehe…Nakuambia ukweli sio mpango wa Mungu kuwa na majeraha ya rohoni kwa miaka 10..Ukiona una kinyongo, au bado unaumia kwa jambo lililotokea miaka 10 au 20 iliyopita..jaribu kutafuta suluhisho mapema..kwasababu kuna uwezekano nguvu ya msamaha haipo ndani yako, na jeraha unapozidi kuliacha huwa ndio linazidi kuwa kubwa kila siku na kuweza kuzaa tatizo kubwa Zaidi ya hilo.

Zaburi 38:5 “Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu”

Na sababu ya kutopona majeraha ndio hizo hapo juu kutofunga jeraha na kutoweka dawa!.. Unaweza kuwa unatatizo la kutopata mtoto, na ukasikia watu wanakusema vibaya..na hilo likawa ni jeraha kwako!..lakini kama Neno la Mungu halipo ndani yako; kama hujui Habari za akina Sara na wengineo ambao Mungu aliwafungua matumbo katika uzee wao, kama hujui Habari za Hana na Raheli ambao walisemwa kupita maelezo, basi hutaweza kupona haraka jeraha ulilonalo. Kwahiyo Neno la Mungu ndio dawa, inayoharakisha uponyaji wa ki-Mungu.

Zaburi 147:3 “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao”

Ndicho kinachowakuta watu wasiolijua Neno la Mungu (watu wa kidunia), wanahangaika na majeraha ya muda mrefu yasiyopona kwasababu hawana dawa, wala hawaijui dawa..Hivyo jeraha lolote lililo ndani yako, lisiwe kikwazo cha wewe kuikosa mbingu anza sasa kuusafisha moyo wako.

Bwana akubariki.

Mwisho kama hujaokoka, wakati umeenda sana, wakati wowote Kristo anarudi, biblia inasema..itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima halafu tupate hasara za nafsi zetu?. Mambo ya ulimwengu yanapita lakini Neno la Mungu lipo pale pale. Mgueukie leo Kristo, utubu dhambi zako, uoshwe kwa damu yake, ukabatizwe na kisha upokee Roho Mtakatifu, ambaye atakuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko.

Maran atha

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.

MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.

NAO WAKADHANI YA KUWA YUMO KATIKA MSAFARA;

UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.

JIRANI YANGU NI NANI?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

HASIRA YA MUNGU KUKUWAKIA, KWA KUTOMZUNGUZIA TU MUNGU IPASAVYO.

Shalom, karibu tena tujifunze maneno ya uzima ya Mungu wetu YEHOVA.

Kuna wakati Mungu anaweza kukaa kimya na kuruhusu mambo Fulani yatokee, ili aone watu wake watamzungumziaje kuhusu jambo hilo, Na hapo ndipo tunapopaswa tuwe makini, kwasababu mtu akikosa kujua makusudi ya Mungu ni nini, halafu akamzungumzia tu kutokana na mawazo yake au uonavyo yeye, anaweza kujisababishia hasira yake iwake juu yako.

Kuna jambo moja la namna hiyo ambalo lipo hasaa kwetu sisi watu wa kanisa la Laodikia, ambalo tunamzunguzia Mungu isivyopasa. Kosa hilo lilifanywa na watu wa kale na sisi bado tunataka kulirudia Na leo hii tutaliona katika biblia.

Kosa lenyewe lilifanywa na wale marafiki watatu Ayubu (yaani Elfazi, Sofari na Bildadi). Mawazo yao yalianzia pale, walipoona Mungu kamletea Ayubu majanga makubwa kama tunavyoyasoma katika biblia.. Walipoona ghafla mali za Ayubu zimepukutika, baadaye tena familia yake ikaondoka, na zaidi ya yote, magonjwa ya mauti yakawa yanamwandama…

Hivyo hawa marafiki zake watatu ambao walikuwa ni wenye hekima kweli kama yeye, na wakati mwingine wenye upendo, kiasi kwamba kufunga safari toka mbali kuja kumfariji Rafiki yao, na kulia naye, ni jambo la upendo mwingi..Lakini walikosa kujua kitu kimoja..Wao walidhani kigezo pekee cha mtu kukubaliwa na Mungu ni kuwa na mali, na utajiri, na mafanikio na Maisha mazuri basi…

Hivyo watu wote waliokuwa wanawaona barabarani kama matajiri, na wenye mali, walihitimisha kuwa ni marafiki wa Mungu wakubwa, Halikadhalika wale wanaopatwa na matatizo na shida, wanatumika chini ya laana kubwa ya Mungu..Hilo tu ndilo lilikuwa kikwazo kwao, lakini mengine yote hawakuwa na hatia..

Sasa ulipofika wakati wa Rafiki yao kipenzi Ayubu kukutwa na majanga kama yale, ndipo wakahitimisha kuwa Ayubu sasa kuna mahali alimkosea Mungu, tena mahali pakuwa sana, na hivyo ni lazima akiri, na atubu makosa yake, wakawa wanamshurutisha kwa nguvu, wakijaribu kushuhudia mabaya yake kwa kila namna..kwa kumwambia maneno kama haya:

Ayubu 4:7 “Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi?

8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.

9 Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika”.

Ayubu 8:3 “Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?

4 Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;

5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi;

6 Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.

7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.

Ayubu 15:34 “Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa”.

N.k n.k, hatuwezi kuorodhesha mistari yote hapa, lakini soma kitabu cha Ayubu kuanzia sura ya 4-25, utaona, msimamo wao hao watu jinsi ulivyokuwa mkali na ule ule, Kwamba Ayubu kupatwa na misiba ile ni matokeo ya uovu wake aliomtendea Mungu, Pamoja na familia yake..

Lakini kwasababu Ayubu alikuwa anamjua Mungu vizuri, hakuhitimisha kuwa kupitia shida, au mtu kuwa maskini au kupungukiwa ni kwamba Mungu amekukataa, badala yake alianza kuwaeleza siri ambayo walikuwa hawaijui akawaambia, wapo watu ambao wamemkataa Mungu, ambao hawaamini hata uweza wa Mungu, lakini Mungu huyo huyo anawapa, afya, amebariki kazi za mikono yao, amewafanikisha kwa kila kitu watakacho, na zaidi ya yote wamepewa Maisha marefu, lakini mwisho wa siku watakufa na watashuka kuzimu kwa ghafla…Hivyo kigezo cha kufanikiwa sio kigezo kuwa Mungu amekukubali..

Ayubu 21:7 “Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?

8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao.

9 Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.

10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.

11 Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza.

12 Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi.

13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula.

14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako.

15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?

16 Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mashauri ya waovu na yawe mbali nami.

17 Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimishwa? Na msiba wao kuwajilia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake?

18 Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba”?

Unaona? Hata baada ya kuelezwa maneno hayo, hilo halikuwafanya marafiki wa Ayubu wabadilishe mitazamo yao, msimamao wao bado ulikuwa ni ule ule, kwamba Ayubu kakosea mahali!, ndio maana yale yote yamempata…Mungu kamwe hawezi kuruhusu mabaya kama yale yamkute mja wake..hilo haliwezekani,

Lakini mwisho kabisa mwa kitabu cha Ayubu tunaona Mungu anasimama na kuanza kuzungumza sasa, akamwambia Ayubu maneno yafuatayo..

Ayubu 42:7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, HASIRA ZANGU ZINAWAKA JUU YAKO, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi HAMKUNENA YALIYO SAWA KATIKA HABARI ZANGU, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.

8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi HAMKUNENA MANENO YALIYONYOKA KATIKA HABARI ZANGU, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu”

Ni lipi tunafundishwa?

Kwa bahati mbaya, hata sasa mawazo kama haya mabovu yapo vichwani mwa baadhi yetu (Hususani wahubiri wa leo). Tunamwazia Mungu katika utajiri tu na mafanikio? Na mahubiri yetu kila siku ni hayo, na tunatumia mistari baadhi baadhi ya kusimami, kama walivyofanya wakina Bildadi, Sofari na Elfazi.

Ndugu unayosoma ujumbe huu, ikiwa na wewe unamnenea Mungu maneno kama hayo, ikiwa na wewe unamuhubiri Mungu kwa njia hiyo tu, ikiwa biblia unayoisoma unaona mistari tu kufanikiwa kimwili, na unawafundisha wengine hivyo..angalia sana..Hasira ya Mungu isije ikawa juu yako.

Kumbuka: (Sio kwamba tusihubiri mafanikio, la! Kwa Mungu yapo mafanikio, makubwa sana! lakini usihubiri kwamba wote ambao hawajafanikiwa na maskini wamepungukiwa na kitu kwa Mungu wao, hapo utakuwa hujamzungumzia Mungu vizuri). Hata ufanyaje huwezi elewa njia zote za Mungu, hivyo epuka kulazimisha kila jambo, na kutaka liwe kama wewe unavyotaka liwe. Sio kila mtu mwenye ulemavu ana laana!, sio wote wenye magonjwa ya muda mrefu yasiyopona kafungwa na nguvu za giza!..sio vipofu wote unaowaona au viziwi ni laana inawafuata… Wengine Mungu karuhusu wawe hivyo kwa makusudi yake yeye (kasome Yohana 9:1-3)

Yakobo 2:4 “ Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?”

1Wakoritho 10:11 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je Mungu anawapenda watu wote au ana chuki?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

Jehanamu ni nini?

JAWABU LA MAISHA YA MTU.

KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.

Rudi Nyumbani:

Print this post

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. kwa link hii >>> https://chat.whatsapp.com/FgA1HWRFZWH4IqqLunFGcs

Mistari ya biblia kuhusu ndoa  ni ipi?


Ndoa ni tendo ambalo Mungu aliliumba kwa makusudi kabisa, ili kumpa mwanadamu picha ya jinsi ndoa yake halisi itakavyokuwa kati ya yeye na watu wake, baada ya ulimwengu huu kuisha. 

Uhusiano walio nao mke na mume, ni mfano mdogo sana wa uhusiano atakaokuwa nao Mungu na watu wake watakaoshinda, katika mbingu mpya na nchi mpya.

Hivyo tutaitazama mistari michache ihusuyo ndoa za kibinadamu, na vilevile tutaitazama mistari michache ihusuyo ndoa ya ki-mbinguni(yaani Kristo na kanisa lake).

NDOA YA MKE NA MUME

Mwanzo 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”

Waefeso 5:25  “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake”;

Waefeso 5:33  “Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe”

Mithali 5:18 “…. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako”

Waefeso 4:2  “kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; 3  na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani”.

Marko 10:9  “Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe”

Wimbo 8:6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu. 

7 Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa”.

Waebrania 13:4  “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.

Mithali 30:18 “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu. 

19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana”.

Mithali 31:10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani”.

Mhubiri 4:9 “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. 

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! 

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto”?

Mathayo 19:6  “Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”

1Petro 3:7  “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe”

Malaki 2:16 “Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli…”

Ruthu 1:16 “Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; 

17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami”.

Yohana 13:34  “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo”.

1Wakorintho 13:4  “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5  haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya”;

Malaki 2:14 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. 

15 Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana”.

Mistari ya biblia kuhusu ndoa ya;

KRISTO NA KANISA LAKE.

Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.

Isaya 54:5 “Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote”.

2Wakorintho 11:2  “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi”.

Ufunuo 19:9  “Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.

Ufunuo 21:1  “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2  Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe”.

Luka 14:24  “Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.

Luka 5:34 “ Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao”?

Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo”.

Mathayo 25:1  “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.

2  Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.

3  Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;

4  bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

5  Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.

6  Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

7  Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.

8  Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.

9  Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.

10  Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

11  Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.

12  Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.

13  Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.

Ufunuo 22:17  “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

Hivyo ni wajibu wetu mimi na wewe kuhakikisha kwa gharama zozote hatuikosi hii karamu ya mwana-kondoo mbinguni, Kumbuka kama tunavyojua huwa kinaanza ndoa kisha baadaye karamu,.vivyo hivyo na kwa Mungu pia, inaanza kwanza ndoa, ambayo Kristo anafunga na watakatifu wake hapa hapa duniani, na baadaye atawanyakua kwenda nao kula naye karamu kule mbinguni.

Kwa mapana na marefu juu ya somo hili la karamu ya mwanakondoo, angalia somo lililoorodheshwa chini baada ya hili; Lakini kikubwa zaidi, ni kuwa tuhakikishe na sisi ni bibi-arusi ambao wapo tayari kumkojea Bwana wao aje waende karamuni.

Na tunakuwa bibi-arusi kwa kumwamini Yesu, na kubatizwa, na kuishi maisha yampendezayo.

Bwana akubariki.

Ikiwa utapenda tukuunge kwenye group la mafundisho ya biblia,Whatsapp: basi utatutumia ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

KARAMU YA MWANA-KONDOO.

MAFUNDISHO YA NDOA.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

MJI WENYE MISINGI.

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

MIHURI SABA

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.

Historia ya nyimbo KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili~ Tis So Sweet to Trust in Jesus.


Wimbo huu uliandikwa na mwanamke mkristo wa kiingereza aliyeitwa, Louisa M. Stead, Mnamo mwaka 1882, Ni wimbo unaoeleza furaha mtu anayoweza kuipata katika kumtegemea Kristo, Lakini nyuma ya uandishi wa wimbo huu, imelala historia nzito ya Maisha aliyopitia Louisa M stead,

Ilikiwa ni siku moja Louisa na mumewe Pamoja na mtoto wao wa kike aliyeitwa Lily, walipanga safari ya kwenda matembezi, wakiwa ufukweni mwa kisiwa kimoja ghafla walisikia  sauti kama ya mtu inapiga kilele za kuzama, kwenda kukimbia kuangalia wakamwona kijana mmoja, hilo lilimfanya mume wa Louisa, ajaribu kwenda kumwokoa, lakini katika jitihada zake za kufanya hivyo kwa bahati mbaya wote wawili wakazama, wakafa (kijana Pamoja na mume wake), mbele ya macho ya Louisa na binti yake.

Maisha yao baada ya hapo yalianza kuporomoka, Maisha yakawa magumu, Lakini wakagundua kuwa Mungu hakuwaacha katika hali zao, aliwatimizia mahitaji yao, hapo ndipo Louisa na binti yake walijifunza kumtegemea Mungu, na ndipo akauandika wimbo huu;

Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kukubali Neno lake,
Nina raha moyoni.
 
Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.
 
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kuamini damu yake,
Nimeoshwa kamili.
 
Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.
 
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kwake daima Napata,
Uzima na amani.
 
Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.
 
Nafurahi kwa sababu,
Nimekutegemea
Yesu,Mpendwa na Rafiki,
Uwe nami dawamu.
 
Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.

*****

Baadaye Louisa na binti yake wakasafiri kwenda Afrika kusini kwa kazi ya umishionari.

Lakini ni nini tunajifunza katika wimbo huu na uandishi wake?

Mimi na wewe tunaweza tukawa hatujapitia katika hali ngumu kama aliyopitia yeye, lakini yeye aliyeyapitia amemwona Mungu akimpigania, mpaka anaimba na kusema, “Nimemwona thabiti”..Hiyo ni kuonyesha kuwa hata wewe ukimwamini Yesu na kumtegemea, ..Utamwona thabiti/hakika akiwa na wewe katika maisha yako haijalishi leo unapitia mahali pagumu kiasi gani.

Imba wimbo huu ukikumbuka matendo yote makuu aliyokutendea nyuma. Na hakika utausikia uwepo wake nafsi mwako.

Bwana akubariki.

Tazama chini historia za nyimbo nyingine za Tenzi.

Tafadhali share na wengine.

Mada Nyinginezo:

NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics

MWAMBA WENYE IMARA

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya Shalom na Maran atha

Utauwa umewahi kusikia maneno haya mawili yakitamkwa miongoni mwa wakristo. (Shalomu na Maranatha) Lakini pengine huelewi maana yake!.

Nini maana ya Shalomu?

Shalomu au Shalom ni neno la kiebrania lenye maana ya “AMANI” Kwa kiingereza “PEACE”. Hivyo wayahudi pamoja na wakristo wa kanisa la kwanza walipokutana walisalimiana na kwa salamu ya neno hilo “Shalomu”.

Pia Mungu wetu jina lake ni YEHOVA-SHALOMU, maana yake “Mungu wa amani”

Waamuzi 6:22 “Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa Bwana; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso.

23 Bwana akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa.

24 Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri”.

Kasome pia Warumi 15:33, Warumi 16:20, Wafilipi 4:9, 1Wathesalonike 5:23, Waebrania 13:20

Na Bwana wetu Yesu anajulikana kama Mfalme wa Amani (kasome Isaya 9:6, Waebrania 7:2).

Hivyo kama Mungu wetu ni Mungu wa Amani na mwana wake wa pekee Yesu Kristo ni Bwana wa Amani, Basi na sisi pia tunapaswa tuwe watu wa Amani na watu wote ili tufanane na yeye, na sio Amani ya midomo tu! bali ya vitendo. Neno Shalom litokapo vinywani vyetu liwe ni udhihirisho wa kitu kinachoendelea katika maisha yetu kwamba tunayo Amani na watu wote. Na lisiwe linatoka tu vinywani na huku mioyoni mwetu kuna unafiki, shari na chuki. Ukitamka tu! na huku moyoni mwako kuna vinyongo na hasira, na shari basi utakuwa hujaelewa nini maana ya shalomu.

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”

1Petro 3:10 “Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.

11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana“.

Maana ya Maran atha

Ni neno la kiebrania hivyo hivyo lenye maana ya “Bwana wetu anakuja” ni neno la Faraja kwa wakristo wote wanaomgonja Bwana....1Wakorintho 16:23

Bwana atubariki.

Shalom.


Tafadhali washirikishe na wengine na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?

NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?

Je Mungu anawapenda watu wote au ana chuki?

MAMBO MENGINE HAYATOKI ISIPOKUWA KWA KUFUNGA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Maana ya watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.

SWALI: Nini maana ya hili Neno “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” (Hosea 4:6).


JIBU: Maarifa yanayozungumziwa hapo sio maarifa ya darasani.. ingawa hata hayo ya shuleni pia ni maarifa na yana nafasi yake katika maisha, lakini yaliyozungumziwa hapo sio hayo..

Maarifa yanayozungumziwa hapo ni maarifa ya kumjua Mungu.

Mithali 1:7 “Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu”

Hali kadhalika biblia inaposema “Mkamate sana Elimu, usimwache aende zake, maana yeye ndio uzima wako (Mithali 4:13)”.. Tafsiri ya kwanza ya mstari huo sio Elimu ya kidunia, bali ni elimu ya Ufalme wa Mbinguni.

Mathayo 13:51  “Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam.

52  Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale”

Kasome pia (Yohana 7:15-17, Marko 1:27,1Timotheo 6:3-5, Matendo 17:18-34), Na pia kuna somo tuliloliandikwa lenye kichwa “Fahamu majira tuliyopo na nini unapaswa uwe nacho”, upatapo nafasi lipitie utapata kuelewa Zaidi.

Kwahiyo mbele za Mungu mtu asiye na Elimu ni yule asiyezijua siri za ufalme wa Mbinguni ikiwemo uweza wa Mungu, na mtu asiye na maarifa ni yule asiyeyajua maarifa ya kimbinguni (maana yake hajui chochote kuhusu Mungu), haijalishi atakuwa na Elimu ya kidunia kubwa kiasi gani; awe profesa, awe dokta awe waziri au awe mtu yeyote yule mwenye elimu kubwa..kama hana Elimu na Maarifa ya ufalme wa mbinguni, basi mbingu inamwona ni hana Elimu wala maarifa yoyote…Na hivyo Ataangamizwa.

Ikiwa uko kwenye soko, swisswatch.is jukwaa letu ni chaguo lako bora! Duka kubwa zaidi la ununuzi!

Sasa tukirudi kwenye huo mstari wa Hosea kuna kitu cha kujifunza Zaidi..Hebu tuusome tena kwa makini..

Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”

Ukisoma kwa makini hapo inasema “watu wangu wanaangamizwa!” na sio “wanaangamia”..Maana yake ni kwamba mtu akikosa maarifa ya kimbinguni kuna kitu cha nje kitamwangamiza. Hataangamia tu peke yake..La! bali kuna kitu kitakuja kumwangamiza.

 Kwa lugha nyepesi ni kwamba maarifa ni kama “ULINZI”. Unapokuwa na maarifa mengi ya kumjua Mungu basi ni ngumu kushambuliwa na Adui yetu shetani na majeshi yake.

Mithali 1:26 “Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo; 

27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.

 28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.

  29 KWA KUWA WALICHUKIA MAARIFA, WALA HAWAKUCHAGUA KUMCHA BWANA. 

30 Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote. 

31 Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe.

 32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. 

33 Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya”.

Kwahiyo ni jukumu letu kila mmoja kuyatafuta Maarifa ya Mungu kwa bidii ili tusiangamizwe!..Ukikosa maarifa ya ki-Mungu, utawaogopa wachawi, ukikosa maarifa ya ki-Mungu hutajua tunaishi siku gani hizi, na hivyo utapotea katika hiki kizazi, na mwisho kwenda kuangamizwa katika moto wa milele.

Bwana atubariki.

Mada Nyinginezo:

HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

MSHIKE SANA ELIMU.

CHEMBE YA NGANO ISIPOANGUKA KATIKA NCHI, IKAFA,

Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?

USITOKE NJE YA HIFADHI YA MUNGU.

KUMCHA MUNGU NI NINI? NA MTU ANAMCHAJE MUNGU?

DAKIKA MOJA TU, INAKUFANYA UMWAMINI SHETANI?

Rudi Nyumbani:

Print this post