Category Archive Maana ya maneno

Hadaa ni nini kibiblia? (2Petro 2:14)

Kuhadaa ni kudanganya, au kulaghai, kutumia njia isiyosahihi/ ya mkato kufanikisha au kupata jambo.

Neno hilo utalipata katika vifungu hivi baadhi;

Mwanzo 31:20 “Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia”

Mithali 12:5 “Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa”

Warumi 1:28  Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 1.29  Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na HADAA; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya

2Petro 2:14  wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;

2Petro 2:18  Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;

Mifano halisi ya kuhadaa ni hii;

> Kama mume, unapotoka na kwenda kwenye kumbi za starehe kucheza miziki na kuzini na kulala huko na makahaba, kisha unamwambia mke wako umesafiri, huko ni kuhadaa.

>Kama mfanyabiashara, unapopunguza uzito jiwe la mizani, ili umpimie mteja kipimo kidogo kwa bei ileile, au unapozidisha bei ya bidhaa juu zaidi ya ile iliyo elekezi, huko ni kuhadaa.

> Kutumia ujuzi wako, au utumishi wako, kusema uongo, ili kupata maslahi Fulani kutoka kwa huyo mtu. Kwamfano wewe ni mchungaji, halafu unasema Bwana ameniagiza mtoe kiwango Fulani cha fedha kila mmoja ili kupokea uponyaji kutoka kwangu, . Hapo umewahadaa watu wa Mungu, kwasababu unajua kabisa tumeambiwa tutoe bure, kwasababu tulipokea bure.

Tabia ya kuhadaa ni tabia ya shetani, kwani ndio silaha ya kwanza aliyoitumia kumwangusha mwanadamu pale Edeni, alipokwenda kumuhadaa Hawa, kwa kumwaminisha kuwa akila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya hatokufa. Lakini ilikuwa kinyume chake.

Bwana Yesu anasema, shetani ni baba wa uongo. Hivyo na sisi tunapodhihirisha tabia hii ya kutumia udanganyifu na hila, ni wazi kuwa tunadhihirisha tabia za wazi na za asili za shetani.  Kumbuka Hadaa ni zao la wivu na kutokupenda maendeleo kwa wengine.

Tukiwa na upendo. Tabia hii itakufa ndani yetu. Tuutafute upendo wa Mungu

Je! Unasumbuliwa na dhambi hii au dhambi nyingine yoyote? Yesu pekee ndio tiba, atakusaidia kuishinda. Ikiwa upo tayari leo kumfanya kuwa Bwana na kuupokea msamaha wake bure. Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

WENYE KUHADAA ROHO ZISIZO IMARA.

Sukothi ni nini? (Mwanzo 33:17).

Kuba ni nini (Ayubu 22:14)?

Ipi tofauti kati ya matoleo na sadaka?

Maana ya Mithali 19:15 ‘Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito;

Fahamu Maana ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.

Rudi nyumbani

Print this post

Kujikinai/kukinai ni nini?

Neno hilo kama linavyotumika kwenye biblia..linamaanisha aidha mojawapo ya mambo haya matatu:

  1. Kushiba Hadi kufikia hatua ya kutokipenda Tena kile ulichokipokea Mwanzo.
  2. Kuwadharau wengine Kwa kufanya mambo ambayo huruhusiwi kuyafanya
  3. Kujigamba/kujiona wewe unajitosheleza Kwa HAKI yako.

1. Kwamfano katika vifungu hivi limetumika kwa tafsiri ya kushiba,..

Mithali 27:7

[7]Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali;  Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.

Mithali 25:17

[17]Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi;  Asije akakukinai na kukuchukia.

Mhubiri 1:8

[8]Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.

2). Lakini pia vifungu hivi, vinaeleza kukinai kama kuonyesha kudharau wengine, kwa kukaidi maagizo kwa makusudi.

Kumbukumbu la Torati 17:12

[12]Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli.

Soma pia.. Kutoka 21:14

3) Halikadhalika mahali ambapo kunaonesha kujikinai kama kujihesabia haki mwenyewe ni hapa

Luka 18:9-14

[9]Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.

[10]Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.

[11]Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.

[12]Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.

[13]Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.

[14]Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Soma pia 2Petro 2:11, 

Hivyo na sisi hatupaswi kuwa na sifa hizo mioyoni mwetu. Uendapo mbele za Bwana, Acha kujihesabia haki, Bali jinyenyekeze penda kuomba rehema Kwa Bwana, zaidi ya kueleza sifa zako..na hatimaye Mungu atakuridhia, kwasababu Mungu anawapinga wenye kiburi na kuwapa neema.wanyenyekevu.

Amen

Je! Umeokoka? Ikiwa bado na unapenda Kristo akusamehe dhambi zako zote, na akupe uzima wa milele. Basi fungua hapa ili uweze kupata mwongozo sala ya toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Baradhuli/Mabaradhuli ni nini au ni nani kwenye biblia?

Mawaa ni nini? Kama tunavyosoma katika biblia?

SI KWA MATENDO BALI NEEMA.

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

UUNGU NI NINI? (1Petro 1:3-4)

Tofauti ya deni na dhambi ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

Mawaa ni nini? Kama tunavyosoma katika biblia?

Mawaa ni nini? Mawaa ni dosari au kasoro iliyo katika kitu, ambayo inapelekea kukifanya kitu hicho kisifae tena, au kikose vigezo.

Kwamfano mtu ambaye ana sifa ya kuwa na uso mzuri halafu, kukatokea jipu shavuni. hapo ni sawa na kusema ana-mawaa. Jipu lile limeuharibu uzuri wake.

Au ukinunua bati la kuwekeza kwenye nyumba yako, halafu ukaona tobo katikati ya bati hilo, tayari lina mawaa, halifai kwa ujenzi. Au shati jeupe halafu likawa na doa dogo jeusi, huo ni mfano wa mawaa, halifai kwa kuvalika.

Vilevile rohoni na sisi pia hatupaswi kuonekana na mawaa ya aina yoyote,  Kwamfano katika vifungu hivi; Mungu anatarajia kanisa lake alilolikomboa kutoka katika dhambi lisionekane na mawaa (dosari yoyote) ndani yake

Wakolosai 1:21  “Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22  katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama”

Hivyo wewe kama mkristo uliyeokoka, ni lazima ujue kuwa una wajibu wa kuishi maisha ya utakatifu na ukamilifu, usiseme nimeokolewa kwa neema Yesu alishayamaliza yote, Hivyo unaenda kama utakakavyo, anaitenda kazi ya Mungu huku unaishi na mke/mume ambaye si wako. Wewe una mawaa, na hivyo mbingu huwezi kuiona.

Au unatoa zaka, unaimba kwaya, ni kiongozi wa vijana, na huku unatazama picha za ngono mtandaoni, hapo una-mawaa, Unafunga na kusali, unadumu hekaluni usiku na mchana na huku unakula rushwa kazini kwako. Hapo ndugu una-mawaa.

Hivyo hatuna budi kuwa kanisa la Kristo kwelikweli Bwana analolitazamia lisilo na mawaa wala lawama, wala kunyanzi. Ndivyo tutakavyopokewa kuingia katika uzima wa milele.

Neno hilo utalipata katika vifungu hivi

1Timotheo 6:13  “Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14  kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.

Yohana 1:27  “Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa”.

Soma pia

Waebrania 9:14, 2Petro 2:13

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka, kama la! Ni nini unachosubiria mpaka sasa, una habari kuwa  parapanda inakaribia kulia, Yesu anarudi? Dalili zote zimeshatimia? Fikiri akikukuta katika hali hiyo utamweleza nini? Angali ukweli umeshaujua? Embu tubu leo dhambi zako, mgeukie Kristo, azioshe, akupe uzima wa milele bure.

Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo akupe uzima wa milele bure, basi fungua hapa ili uweze kupata mwongozo wa sala hiyo. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

Mikono iliyotakata ni mikono ya namna gani? (1Timotheo 2:8).

TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

Mtakatifu ni Nani?

ISHARA YA KANISA LA LAODIKIA

USIPOWATAMBUA YANE NA YAMBRE, KATIKA KANISA LA KRISTO, UJUE UMEPOTEA.

Rudi nyumbani

Print this post

Kuba ni nini (Ayubu 22:14)?

Jibu: Tusome,

Ayubu 22:12 “Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!

13 Nawe wasema, Mungu anajua nini? Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?

14 Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU. 

15 Je! Utaiandama njia ya zamani Waliyoikanyaga watu waovu?”

Kuba ni mzunguko wa Anga, Ukitazama juu utaona ncha za mbingu ni kama duara, ndio maana jua wakati wa asuhuhi ni kama “linachomoza kutoka chini upande wa mashariki” na wakati wa mchana linaonekana lipo juu kabisa (utosini) lakini inapofika  jioni “linazama tena chini upande wa magharibi”..

Sasa huo mduara wa anga ndio unaoitwa “KUBA” na maandiko yanasema Bwana anatembea juu ya mduara huo, kuonyesha utukufu wake.

Ayubu 22:14 “Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya KUBA YA MBINGU”. 

Hivyo andiko hili linaonyesha utukufu na ukuu wa Mungu, kuwa yuko juu sana na mwingi wa uweza.

Je umemrudia yeye aliyezifanya Nyota na Mwezi, na anga na viumbe vyote?..

Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.

 2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua”

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

MKUU WA ANGA.

NYOTA ZIPOTEAZO.

Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?

Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.

Mbinguni ni sehemu gani?

Rudi nyumbani

Print this post

Alani ni nini?(1Samweli 17:51)

Alani ni kifuko cha kuhifadhia upanga ambacho huvaliwa kiunoni na askari hususani wakati wa vita. Tazama picha juu.

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;

1Samweli 17: 51 “Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia”

1Nyakati 21:27 “Bwana naye akamwamuru malaika; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena”.

Yohana 18:11  “Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?”

Soma pia,  Ezekieli 21:3, 5

Je! Chombo hichi kinafunua nini rohoni?

Kama tujuavyo upanga na alani, ni kama pochi na pesa, havitengani. Na upanga, kibiblia ni Neno la Mungu (Waefeso 6:17, Waebrania 4:12). Hivyo Neno la Mungu halihifadhiwi penginepo zaidi ya kwenye moyo. Pale linapohitajika kutumika hutolewa moyoni na sio penginepo. Kwahiyo chombo hichi kijulikanacho kama Alani, kinauwakilisha moyo wa Mtu.

Na kama tunavyojua upanga hutumiwa na mtu yoyote, unaweza hata kumwangamiza  mwenye nao, ukitumiwa na adui. Ndivyo alivyojaribu kufanya shetani alipomjaribu Bwana na kumwambia ‘imeandikwa’, Lakini kwasababu Yesu alikuwa amejaa ‘Kweli yote’. Aliweza kumpokonya upanga huo huo na kummaliza nao.

Hivyo ni muhimu pia kujaa ‘Kweli yote’ sio Neno tu peke yake, yaani kuufahamu ukweli wa Neno la Mungu. Kwasababu ibilisi anaweza kulitumia kukuangusha ikiwa hutakamilishwa katika hilo, kwamfano anaweza kuja kukwambia kuoa wake wengi si dhambi, kwani Yakobo, alioa wake wengi, Daudi alioa wake wengi, Sulemani alioa wake wengi, na wote hawa walikubaliwa vizuri na Mungu, vivyo hivyo na wewe ukifanya hivyo utakubaliwa tu, hamna shida,. Lakini je! Hiyo ni kweli yote? Kweli yote inasema Mungu alimuumba mtu mke na mume, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.(Mathayo 19:4-9), hakuumba Adamu mmoja, Hawa wengi. Hivyo usipojua kuligawanya vema Neno la Mungu kwa msaada wa Roho ni rahisi shetani kukupiga.

Na ndio maana maandiko yanatusihi tuivae ‘kweli’ kiunoni.

Waefeso 6:13  “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?

Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi

Kwanini Bwana Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakanunue upanga?

Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?

Kwanini Mungu aseme “Alaaniwe azuiaye upanga wake usimwage damu” (Yeremia 48:10).

NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.

Rudi nyumbani

Print this post

Tirshatha ni nini? (Ezra 2:63)

Neno hili utalipata katika vifungu hivi kwenye biblia.

Ezra 2:63 Na huyo Tirshatha akawaambia wasile katika vitu vitakatifu sana ,hata atakaposimama kuhani mwenye urimu na Thumimu.

Nehemia 8:9 Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa Bwana, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati

Nehemia 10: 1 Basi hawa ndio waliotia muhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;

Soma pia Nehemia 7:65

Tirshatha ni neno la kiajemi, ambalo linamaanisha mtawala aliyeteuliwa kuongoza uyahudi chini ya ufalme wa uajemi. Kwa jina lingine ni gavana/ liwali, Katika vifungu hivyo vinamwonyesha Nehemia alikuwa kama Tirshatha/Mtawala. Soma pia (Nehemia 5:18).

Lakini pia Zerubabeli, alipewa nafasi hii kama tunavyosoma hapo kwenye Ezra 2:63, Hivyo wote hawa walisimama kama wakuu wa majimbo hayo wayaangalie, na kusimamia kazi zote walizoagizwa na mfalme.

Bwana akubariki.

Tazama pia maana ya maneno mengine ya kibiblia chini.

Je! Umeokoka? Je, unatambua kuwa Kristo anakaribia kurudi? Umejiandaaje? Tubu dhambi zako ukabatizwe upokee Roho Mtakatifu uwe salama zizini mwa Bwana. Muda ni mfupi sana tuliobakiwa nao, huu si wakati wa kubembelezewa wokovu, ni wewe mwenyewe kuona na kugeuka upesi. Ikiwa upo tayari kuyakabidhi maisha yako kwa Bwana basi fungua hapa ili upate mwongozo wa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Ayari ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)

HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.

NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?

FUMBO ZA SHETANI.

Rudi nyumbani

Print this post