Mhubiri 10:16 “Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi!”
Mstari huu umegawanyika katika sehemu mbili;
Hapo mhubiri anajaribu kueleza uhusiano uliopo kati ya uongozi na ukomavu wa mtu. Akatumia mfano wa kijana, kwasababu mara nyingi ni ngumu sana kuipata busara kwa vijana, kutokana na kuwa hawana uzoefu mwingi wa maisha na pia hawajaandaliwa vya kutosha, kumudu nafasi za uongozi, kinyume chake kitakachowaongoza ni hisia tu za ujana na si vinginevyo. Na ndio maana mtu kama Sulemani alilitambua hilo alipotawadhwa tu mfalme akiwa bado kijana mdogo, alimwomba Mungu ampe hekima ya namna ya kuwaongoza watu wake. Na Bwana akamjalia.
1Wafalme 3:7 “Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
8 Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi.
9 Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? 10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili”
Walikuwepo pia wafalme wengine waliotawadhwa wakiwa wadogo kama Yoashi, lakini akasaidiwa na kuhani Yehoyada katika ufalme wake, na ukawa bora (2Wafalme 11-12)
Lakini tunakuja kuona kwa mwanawe Sulemani aliyeitwa Rehoboamu. Yeye naye alikuwa ni kijana lakini hakutaka mashauri kwa wazee waliomtangulia, kinyume chake, akasikiliza mashauri ya vijana wenzake Hivyo ikapelekea ufalme wake kugawanyika, na kupoteza makabila kumi kati ya kumi na mbili ya Israeli.(Soma 1Wafalme 12:1-16)
Maana yake kwamba kuwa na viongozi ambao wanatanguliza maslahi yao kabla ya kazi, nchi hiyo sikuzote huishia pabaya. Sikuzote watu wanakwenda kufanya kazi asubuhi, wakitarajia kile walichokihangaikia kutwa nzima ndio wakifaidi jioni, lakini hapa tunaona ni kinyume chake. Na jambo hili ni kweli, Tunaona katika baadhi ya mataifa yanayoendelea, wananchi wao wanapitia katika taabu, na umaskini wa hali ya juu, kutokana na kuwa viongozi wao, wanatazama maslahi yao binafsi wanapoingia madarakani na sio maslahi ya taifa.. Uchu wa madaraka na ukuu, ndio wanachokitazama lakini sio kujenga mataifa yao.
Hii inafunua nini rohoni?
Neno hili linawahusu, watumishi wote wa Mungu wanaosimama katika ngazi za uongozi. Ikiwa wewe bado ni kijana au mchanga katika huduma(hata kama una-mvi) na umepewa kundi ulichunge, Omba sana hekima kwa Mungu, pia kuwa tayari kujifunza kwa waliokutangulia, Sikuzote viongozi-wachanga, katika hatua za awali wanajiamini kuwa wanajua kila kitu, lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wanavyotambua kasoro zao nyingi. Hivyo ili kuepuka, kufanya makosa ya kiutumishi, tafuta sana msaada kwa Mungu katika hekima na mashauri.
Lakini pia, ikiwa wewe ni mchungaji, askofu, mtume, mwalimu, au unatumika katika huduma yoyote, epuka tamaa hususani ya mali. Si kila shilingi unayoipata uipeleke tumboni, au kujijengea majumba na biashara. Ni heri ukatazama kwanza hali ya kanisa la Kristo. Kama mchungaji mwema yakupasa kuipendezesha kwanza nyumba ya Bwana, kisha Baadaye Bwana mwenyewe ndio akupendezeshe wewe. Unatembelea gari ya Tsh milioni 40, halafu kanisa ni la makuti, Hapo ni nini unategemea kama sio ufukara wa kiroho hadi kimwili baadaye.
Kwahiyo hekima hizi zinatuonya, ili uongozi wetu usianguke mbeleni, hivyo tuzingatie sana maneno haya ya hekima. Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.
NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?
Swali: Tukisoma Marko 6:8, tunaona Bwana Yesu anawaruhusu wanafunzi wake “wabebe fimbo”, lakini tukirejea katika Mathayo 10:10 tunasoma habari tofauti, Bwana Yesu anawakataza wasibebe chochote hata fimbo..sasa mwandishi yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi? Je biblia inajichanganya yenyewe?.
Jibu: Biblia kamwe haijichanganya mahali popote, vinginevyo kitabu kizima kitakuwa ni cha uongo!. Lakini kama ni kitabu cha kweli kilichojaa maneno ya kweli ya uzima, na Roho Mtakatifu basi hakiwezi kuwa kitabu cha ushuhuda wa uongo!, au unaochanganya!..kinachochanganyikiwa ni fahamu zetu katika kukielewa kitabu hicho, lakini chenyewe kama chenyewe hakina kasoro yoyote.
Awali ya yote tuisome mistari hiyo…
Marko 6:7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
8 akawakataza wasichukue kitu cha NJIANI ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;
9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili”.
Hapa ni kweli tunaona Bwana anawaambia wasibebe chochote ila Fimbo tu!… Tusome tena habari hiyo katika kitabu cha Mathayo..
Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, WALA FIMBO; maana mtenda kazi astahili posho lake”.
Hapa tunaona Bwana anawakataza hata Fimbo wasibebe, na ilihali kule kwenye kitabu cha Marko tunaona anawaambia wasibebe kitu kingine chochote isipokuwa Fimbo tu!.. Sasa mwandishi yupi ni wa kweli na yupi ni wa uongo?.
Jibu ni kwamba waandishi wote ni wa kweli hakuna aliye mwongo!,
Katika Marko Bwana anawaambia wasibebe vitu vya njiani isipikuwa FIMBO TU!.. Sasa fimbo hakikuwa chakula bali ni kifaa kinachomwezesha mtu kutembea katika milima na mabonde! Ni kama tu kiatu kilivyo msaada kwa miguu katika safari ndefu za miiba na mavumbi.. Fimbo na yenyewe ilikuwa ni hivyo hivyo..
Kwahiyo fimbo ilikuwa ni sehemu ya kitu cha msingi mtu anachoweza kuwa nacho kwa safari kama tu vile mtu alivyo na kanzu au kiatu au nguo.
Lakini sasa Bwana alichowakataza ni wao kubeba fimbo ya pili au ya tatu, kana Kamba moja ikivunjika basi kutakuwepo na akiba. Hicho ndicho kitu Bwana alichowakataza akawaambia wabebe fimbo moja tu!. Wasihofie endapo hiyo waliyonayo itapata itilafu, kwani huko wanakokwenda Mungu wa mbinguni atawafungulia mlango watapata nyingine.
Lakini pia sio Fimbo tu!, bali hata kanzu!.. wasibebe na kujifungasha mizigo ya kanzu nyingi, waende na hiyo moja tu iliyopo mwilini kwasababu huko waendako Baba yao wa mbinguni anajua kuwa wana haja na nazo, hivyo wasitie wasiwasi kwasababu mtenda kazi amestahili posho yake (watapata huko waendako). Ndio maana akawakataza wasibebe kanzu mbili…
Marko 6:8 “akawakataza wasichukue kitu cha NJIANI ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;
9 lakini wajifungie viatu; akasema, MSIVAE KANZU MBILI”.
Hapo mwisho anasema “msivae kanzu mbili” maana yake ile moja waliyonayo mwilini inatosha.. vile vile wasibebe fimbo nyingine ya pili, hiyo moja watakayokuwa nayo inatosha!..sawasawa na hiyo Mathayo 10:10..
Kwahiyo biblia haijichanganyi, bali shetani ndiye anayetuchanganya….
Sasa kufahamu ni somo gani tunaloweza kujifunza nyuma ya hii habari fungua hapa>>> Bwana alimaanisha nini kusema“maana mtenda kazi astahili posho lake”
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je suruali ni vazi la kiume tu?
Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?
Gongo na Fimbo ni nini? Na vinawezaje kumfariji mtu? (Zaburi 23:4).
Je! habari ya muda aliotawala Mfalme Yekonia inajichanganya? (2Wafalme 24:8 na 2Nyakati 36:9).
Jibu: Biblia haijichanganyi mahali popote na haijawahi kujichanganya isipokuwa viwango vyetu vya kutafakari ndivyo vinavyotufanya tuone kuna utata mwingi kwenye biblia (na kumbuka tunapozungumzia biblia tunamaanisha ile yenye vitabu 66) na si zaidi ya hivyo!.
Vitabu 66 vya biblia ndivyo vilivyohakikiwa na Roho Mtakatifu kwa vizazi vyote kama Neno la Mungu lililo hai.
Sasa kabla ya kwenda kuitafakari mistari hiyo hebu tuisome kwanza..
Mwanzo 15:13 “Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa MIAKA MIA NNE.
14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi”
Tusome tena,..
Kutoka 12:40 “Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa NI MIAKA MIA NNE NA THELATHINI.
41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo MIA NNE NA THELATHINI, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri”.
Sasa swali ni hili, Mungu alimdanganya Abramu kuwa uzao wake utakaa miaka 400 na kumbe ni miaka 430?, je Mungu ni mwongo?
Jibu ni la! Hakudanganywa, kwasababu hiyo miaka 430 bado ipo katika namba mia nne, Mungu hakumwambia kuwa atakaa miaka mia nne kamili, bali alimwambia tu miaka mia nne, ikiwa na maana kuwa inaweza kuwa ni miaka mia nne kamili au miaka 410 au 430 au 470 au hata 490 lakini haitazidi hiyo miaka 400 na kuwa 500.
Ni sawa mtu na mtu akuulize wewe una miaka mingapi na umwambie una miaka 30 au 40, unaweza kumpa namba ya ujumla lakini kiuhalisia huenda unayo miaka 30 na miezi 6 au na miezi 7,au una miaka 40 na miezi 8 au 9.. Kwahiyo wewe kumwambia kuwa una miaka 30 au 40 unakuwa hujamdanganya.. Ni kweli ndio miaka yako, isipokuwa hujapenda kumwambia na miezi iliyo mbele ya hiyo miaka..Ungekuwa umemdaganya endapo kama ungemwambia unayo miaka 30 kamili au 40 kamili, hapo utakuwa umemdanganya!..
Vile vile Bwana Mungu hakumwambia Abramu kuwa Uzao wake utakaa utumwani miaka 400 kamili, bali alimwambia tu utakaa miaka 400.. Na ndivyo ilivyokuwa.
Kwahiyo biblia haijichanganyi.. Tazama pia miezi aliyotawala Yekonia je unajichanganya? >>> YEKONIA ALITAWALA MUDA GANI?
Je umeokoka?..kumbuka kuwa hizi ni siku za mwisho, na unyakuo wa kanisa ni muda wowote kuanzia sasa.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je! kuna mambo ambayo Mungu hawezi kuyafanya kulingana na Waamuzi 1:19?
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?
Je! habari ya muda aliyotawala Mfalme Yekonia inajichanganya? (2Wafalme 24:8 na 2Nyakati 36:9).
Je! biblia inajichanganya katika 1Petro 2:13 na Matendo 5:29.
Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?
Jibu: Kabla ya ufafanuzi tuisome mistari hiyo..
2Wafalme 24:8 “Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala MIEZI MITATU katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani wa Yerusalemu”.
Tusome tena,
2Nyakati 36:9 “Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu MIEZI MITATU NA SIKU KUMI; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana”.
Hapa tunaona mwandishi wa kitabu cha Wafalme anataja miezi aliyotawala Yekonia ni mitatu (3) lakini mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati ameongeza siku kadhaa mbele yake (miezi 3 na siku 10).
Swali, je! Ni yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi?.. au je biblia inajichanganya?. Au ina makosa katika uandishi?
Jibu ni la! Biblia haijichanganyi mahali popote na haijawahi kujichanganya, na wala haina makosa mahali popote kwasababu endapo ikijichanganya au ikikosewa, basi yote itakuwa ni uongo na sio Neno la Mungu, lakini tunaona maneno yaliyoandikwa kule ni nguvu ya Mungu, na ni uweza wa Mungu, na tena ni Roho, na hayana makosa…
Sasa tukirudi katika hiyo habari ya muda aliotawala Yekonia, je! Mwandishi yupi yupo sahihi?.
Jibu ni kwamba wote wapo sahihi, hakuna aliyekosea.
Mtu akikwambia nitakuja kukutembelea mwezi wa 3 halafu akaja mwezi huo wa 3 tarehe 10 je atakuwa amekudanganya?..bila shaka atakuwa hajakudanganya kwasababu hiyo tarehe ipo ndani ya huo mwezi wa tatu (haijatoka ndani ya huo mwezi wa 3).. hata kama atakuja tarehe 20 au 21 au 25 atakuwa bado hajakudanganya kwasababu bado tarehe hizo zipo ndani ya mwezi wa huo wa tatu.
Hali kadhalika Mwandishi wa kitabu cha Samweli kasema tu “Yekonia katawala miezi 3” ingawa alikuwa anajua na siku alizotawala lakini kapenda tu kufupisha, hajapenda kutaja na siku wala masaa wala dakika wala sekunde lakini kafupisha tu! Miezi 3.
Lakini mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati kapenda kutaja Miezi Mfalme Yekonia aliyotawala na Siku alizotawala, lakini hajapenda kutaja na masaa wala dakika wala sekunde… Huwenda angetokea na mwandishi mwingine angetaja Miezi aliyotawala, na siku na masaa na sekunde!.. na bado asingekuwa ametoa taarifa sahihi ambazo hazikinzani na za wale waliofupisha!.
Kwahiyo biblia haijajichanganya hapo!.wala haijichanganyi mahali popote. Tazama pia muda wana wa Israeli waliokaa Misri je ni miaka 400 au 430?..kujua hilo kwa urefu fungua hapa >>> Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?
Je unajua kuwa dhiki kuu itakuja baada ya unyakuo wa kanisa na unyakuo upo karibu?..tutumie ujumbe inbox kwa maelezo marefu juu ya hili.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
TUSIIFUATISHE KAWAIDA YA ULIMWENGU HUU.
Swali: Katika 1Nyakati 21:5 tunasona waliohesabiwa kwa Israeli na Yuda jumla ni askari 1,570,000 lakini tukirudi katika 2Samweli 24:9 tunaona jumla ya idadi ya askari waliohesabiwa walikuwa ni 1,300,000 kwa Yuda na Israeli, je biblia inajichanganya?.
Jibu: Turejee,
1Nyakati 21:5 “Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu mia nne na sabini elfu, wenye kufuta panga”.
Tusome tena…
2Samweli 24:8 “Nao walipokwisha kuzunguka nchi yote, wakaja Yerusalemu mwisho wa miezi kenda na siku ishirini.
9 Naye Yoabu akamtolea mfalme jumla ya hesabu ya watu; nao walikuwa wa Israeli mashujaa wenye kufuta panga mia nane elfu; nao wa Yuda walikuwa watu mia tano elfu”.
Ni kweli katika mistari hii miwili, panaonyesha tofauti ya Askari waliohesabiwa, tunaona kitabu kimoja kinataja idadi ya juu sana, na kingine kinataja idadi ya chini, sasa swali ni je biblia inajichanganya?
Jibu ni la! Biblia haijichanganyi kwasababu ni kitabu kilichovuviwa na Roho Mtakatifu. Fahamu zetu zinaweza kujichanganya katika kuielewa biblia lakini kamwe biblia haijawahi kujichanganya, hususani panapotokea habari moja kunukuliwa na waandishi wawili tofauti, kwasababu kama biblia itakuwa na makosa sehemu yoyote, basi kitabu kizima kitakuwa na mapungufu na hivyo hakiwezi kuwa kitabu kitakatifu.
Lakini mpaka Roho Mtakatifu aruhusu kidumu kwa nyakati zote na vizazi vyote ni wazi kuwa biblia yenye vitabu 66 ni maandishi matakatifu na ya kuaminiwa asilimia 100, kwaajili ya maarifa sahihi ya kiMungu, na haina makosa yoyote.
Sasa tukirudi katika hiyo habari tunayoisoma katika vitabu hivyo viwili (1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9) kila mwandishi alijaribu kunukuu aina ya askari waliohesabiwa..
Mwandishi wa kwanza wa kitabu cha 2Samweli 24:9 alinukuu idadi ya Askari ambao walikuwa ni MASHUJAA TU! Ambao idadi yao ilikuwa ni hiyo 1,300,000 Na Mwandishi wa pili wa kitabu cha 1Nyakati 21:5 alinukuu idadi ya Askari wote kwa ujumla (Waliokuwa mashujaa na wasio mashujaa)..ndio maana utaona idadi imeongezeka mpaka kufikia hiyo 1,570,000. Kwahiyo biblia haijichanganyi.
Ilikuwepo tofauti ya Askari wa kawaida na waliokuwa Mashujaa, waliokuwa mashujaa na wale waliokuwa wakongwe na wazoefu katika vita wenye uwezo mkubwa wa kupambana, kwamfano utaona Mfalme Uzia biblia inaonyesha alikuwa na Askari wa kawaida na waliokuwa mashujaa, waliozoea vita, wepesi na hodari wa vita.
2Nyakati 26:11 “Zaidi ya hayo Uzia alikuwa na jeshi la watu wa kupigana, waliokwenda vitani vikosi vikosi, sawasawa na hesabu walivyohesabiwa na Yeieli mwandishi, na Maaseya msimamizi, chini ya mkono wa Hanania, mmojawapo wa maakida wa mfalme.
12 Hesabu yote ya wakuu wa nyumba za mababa, WATU MASHUJAA, ILIKUWA ELFU MBILI NA MIA SITA.
13 Na chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la askari, mia tatu na saba elfu, na mia tano, ambao walipigana vita kwa nguvu nyingi, kumsaidia mfalme juu ya adui”.
Je unaliamini Neno la Mungu?
Je unajua Bwana Yesu alisema kuwa ”Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni (Mathayo 7:19 )??”
Je ni matunda gani unayozaa?..Mazuri au mabaya..
Mathayo 7:17 “Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni”
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE MASHUJAA 37 WA DAUDI.
Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.
Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?
USIZITEGEMEE NGUVU ZAKO KUKUSAIDIA!
Jibu: Turejee,
Mwanzo 9:20 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, BABA WA KANAANI, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema, NA ALAANIWE KAANANI; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake”.
Kumbuka hapo kwanza “Kaanani” halikuwa jina la Nchi, bali lilikuwa ni jina la ‘Mtu’. Na mtu huyo alikuwa ni mtoto wa nne (4) wa Hamu..
Mwanzo 10: 6 “Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani”.
Hatujui kwa undani mtoto huyu (Kanaani) alikuwa na tabia gani?..lakini ni wazi kuwa matendo yake yalikuwa kama ya baba yake Hamu, ndio maana akabeba laana ya moja kwa moja ya baba yake.
Sasa huyu Kanaani ndiye aliyelaaniwa na baadaye alikuja kuzaa watoto na uzao wake ukaitwa Uzao wa Kanaani, kufuatia jina la Baba yao, na walipotawanyika usoni pa nchi yote katika ule utawanyiko wa Babeli (Mwanzo 11:8-9) ndipo wakaenda kuishi mahali wana wa Israeli walipowakuta.
Kipindi wanaishi, ardhi ile ilijulikana kama nchi ya Wakanaani. Na kilichokuwa kimelaaniwa na Mungu si ile ardhi/nchi bali ni watu, (ambao ndio hao wakaanani)..ikiwa na maana kuwa hata kama wasingeishi katika ile ardhi na kwenda kuishi katika ardhi nyingine bado wangekuwa chini ya laana.
Kwahiyo wana wa Israeli wakati wanatoka Misri, Mungu aliwatoa Wakanaani kwenye ile ardhi na kuwaweka wana wa Israeli, kwasababu kilicholaaniwa katika Mwanzo 9:5 si ardhi bali ni watu, hivyo watu wanaweza kuondolewa na ardhi ikaendelea kutumika na wengine na ikawa nchi ya Baraka tu, ndio maana baada ya pale haikuitwa tena nchi ya wakanaani bali nchi ya Israeli.
Lakini swali ni je! Hawa Wana wa Hamu mpaka leo wamelaaniwa?.. Maana miongoni mwao kuna Kushi ambaye uzao wake ni watu weusi.
Jibu ni la! Kristo alikuja kuondoa laana zote pale Kalvari, na hivyo hakuna tofauti ya Myahudi na Mmisri, Mkushi na mwisraeli, mbele za Mungu… kama tumeokoka wote tunahesabiwa sawa mbele zake. Lakini kama hatutazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa roho wote mbele zake ni kama tuliolaaniwa.
Wakolosai 3:10 “mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.
11 Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote”.
Waefeso 2:16 “Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”
Je umezaliwa mara ya pili?..
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu”.
Bwana Yesu anarudi!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Wakaanani walikuwa ni watu gani?
TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA.
NI KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUMWELEWA MUNGU?
Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67).
SWALI: Bwana yesu apewe sifa, Naomba kufahamu, Kwanini Wana wa Israeli walimuhifadhi mwana-kondoo siku nne kabla ya kuchinjwa katika sikukuu ya pasaka.Je Kuna ufunuo gani tunaweza kupata katika Tendo hilo (Kutoka 12:6)
JIBU: Tusome..
Kutoka 12:3-7
[3]Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
[4]na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.
[5]Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.
[6]Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.
[7]Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.
Bwana aliwapa agizo la kuwatenga wana-kondoo Kutoka katika kundi siku ya 10, Kisha siku ya 14 kuchinja.
Maana yake ni kuwa sadaka/dhabihu Yao, ilipaswa itambilike mapema Kisha ikatengwa. Kama wangekaidi agizo hilo na kuchagua mwanakondoo siku Ile Ile ya kuchinja au hata siku moja kabla ilikuwa ni kosa mbele za Mungu.
Na sisi pia Bwana anapendezwa na dhahibu zenye maandalizi, ambazo zimetengwa mapema…Kwamfano unapokwenda ibadani jijengee desturi ya kumwandalia Mungu sadaka zako mapema..hata ikiwezekena siku kadhaa kabla..Kwa jinsi unavyoandaa mapema ndivyo inavyokuwa na utukufu mwingi zaidi..
Lakini pia Unahakikisha unaitenga kabisa na hesabu zako nyingine..(yaani haiguswi), mpaka siku ya kumtolea.
Hiyo itaifanya sadaka Yako ipokelewe Kwa furaha na Mungu, kuliko kufikiria kumtolea Mungu muda huo huo wakati ulikuwa na nafasi ya kufanya maandalizi. Ndio ufunuo ulio nyuma ya agizo hilo la Pasaka.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?
Kwanini Kristo aitwe Mwana-kondoo. (Yohana 1:29)
Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?
TUUTAFUTE USEMI MMOJA. TUUJENGE MNARA WA MUNGU
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.
Jibu: Turejee,
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye ‘ALIYE AMINA’, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu”
Neno Amina maana yake ni “Na iwe hivyo”.. Neno hili kwa lugha ya kiingereza ni “Amen” Hivyo Popote panapotajwa “Amina” au “Amen” maana yake ni “na iwe hivyo”.
Sasa kwanini Bwana Yesu ajitambulishe kwa neon hilo?..
Ni kuyatofautisha maneno yake na wengine! Kwamba maneno yake ni Thabiti.
Sasa ili tuelewe vizuri, turejee pale Bwana Yesu aliposema kuwa “Mimi ndimi Njia, na Kweli na Uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia yangu mimi (Yohana 14:6)”.
Tukiunyambua huo mstari vizuri, tunapata sentensi mbili 1. Yeye ndiye Njia, 2. Mtu haji kwa Baba ila kwa njia yake yeye.
Hapo Bwana anajiita kuwa yeye “Njia” anajifananisha yeye na kitu kisicho na uhai..lakini anazidi kufafanua ni kwa jinsi gani yeye ni njia kwa kuendelea kusema… “mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye” ikiwa na maana kuwa, kwa maneno ya Yesu na maisha yake, tukiyafuata hayo tutafika mbinguni (hayo ndio njia)… Njia zipo nyingi, lakini zote hizo hazimpeleki mtu mbinguni, isipokuwa njia ya Yesu tu! Ambayo ni Neno lake.
Sasa tukirejea tena hapo Bwana aliposema yeye ni “Amina” utaona mbele kidogo anaendelea kufafanua ni kwa namna gani yeye ni “Amina”.
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, SHAHIDI ALIYE MWAMINIFU NA WA KWELI, MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU”.
Anasema yeye ni Amina, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa kuumbwa kwa Mungu. Maana yake maneno yake ni hakika!, akisema amesema ni lazima iwe hivyo!.. Amina yake ni amina kweli.. wengine wanazo amina lakini zinaweza zisitimie kama walivyoseme. Lakini yeye (Yesu) maneno yake ni hakika!.. akisema basi ni lazima “ITAKUWA HIVYO KAMA ALIVYOSEMA” Ndio maana anaitwa Shahidi mwaminifu.. hajawahi kusema jambo halafu lisitimie..Ni mwaminifu kwa maneno yake siku zote.
Tusome,
Marko 13:31 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.
2Wakorintho 1:20 “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi”.
Je umemtumainia huyu ambaye Maneno yake hayapiti?. Alisema “Aaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16)” je unadhani kutakuwa na kanuni nyingine Zaidi ya hiyo?.. Alisema wadhalimu, na wachawi, na wazinzi, na walevi hawataurithi ufalme wa mbinguni, je unadhani anadanganya??..ni kweli itakuwa hivyo!, maneno yake kamwe hayapiti, Amina yake ni amina kweli..
Je umempokea Yesu?, je umebatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu?.. Kama bado basi tafuta kufanya hivyo mapema.
Maran atha?
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.
Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu
Je Henoko aliyeenda na Mungu alikuwa ni mwana wa Kaini? (Mwanzo 4:16)
Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.
Je! Moyo wako upo kweli kwake?
Kuna kauli Bwana Yesu alisema kuhusiana na watu kumwelewa Mungu na uweza wake kwetu, alisema..
Mathayo 13:14 “Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, WAKAELEWA KWA MIOYO YAO, WAKAONGOKA, NIKAWAPONYA”
Ametaja mambo makuu matatu,
Hatua ya mwisho ambayo Mungu anatarajia, pindi anapomfundisha mtu, au kusema naye ni KUELEWA. Hivyo ataanza kwanza kwa kumwonyesha mambo kadha wa kadha, yatapita mbele yake, ataanza kusema na yeye kwa njia nyingi, aidha kwa wahubiri wake, au ndoto, au maono, au vitu vya asili, au kwa Neno lake, au kwa maisha yake mwenyewe.. Lakini pamoja na njia zote hizo bado mtu huyo anaweza asimwelewe Mungu, kama Moyo wako haupo kwake.
Jambo ambalo watu wengi hatujui, ni kwamba Mungu anazungumza na kila mmoja, Na kila mmoja anaonyeshwa maono mengi na Mungu, kila mtu ameshakutana na Mungu, aidha uso kwa uso au katika roho, haijalishi ni mwema au mwenye dhambi, Lakini ni wachache sana walioweza kuielewa sauti yake iliposema nao.
Ni kwasababu gani hawaielewi? Ni kwasababu inahitaji MOYO ili kuielewa, Na sio macho au sikio. Kama moyo wako haupo kwake, sahau kumwelewa Mungu anaposema na wewe kwa njia yoyote ile. Hata kama itakuja kwa dhahiri, bado hutamwelewa. Sauti yake kwako itakuwa ni ngurumo tu, kama ilivyokuwa kipindi kile Bwana Yesu alipokuwa anazungumza na makutano kuhusiana na ufalme wa mbinguni.
Yohana 12:28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. 29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu”
Ni kwanini iwe hivyo kwao? Ni kwasababu kilichowapeleka kwa Yesu sio wokovu wa Roho zao, au upendo wao kwa Mungu, kilichowapeleka kwake, ni miujiza, uponyaji, uzuri, mwonekano, mazingira, basi, hakuna jipya. Wakishapata walichokuwa wanakitafuta hao wanaondoka zao kuendelea na mambo yao ya dhambi ya sikuzote.
Ndio maana hakukuwa na hata mmoja ambaye aliyeelewa mifano yote Yesu aliyokuwa anaisema mbele ya umati. Isipokuwa wanafunzi wake tu, pamoja na wachache waliomfuata baada ya pale kutaka kufafanuliwa.
Ndugu ikiwa leo unakwenda kanisani kutimiza tu ratiba, kutazama kwaya, kuangalia watu wamevaaje, hata ukiwepo humo unasinzia, unaangalia muda utatoka saa ngapi, ni kweli utakutana na Mungu, atasema na wewe, utamwona, utahisi uwepo wake, utanena hata kwa lugha, utasisimka moyo. Lakini kumwelewa, haitakaa iwezekane. Kwasababu Mungu hajifunui kwa watu ambao mioyo yao haipo kwake.Hana utaratibu huo.
Na sio tu kanisani, hata mahali popote pale, iwe ni shuleni, kazini, nyumbani, barabarani, Mungu huwa anazungumza, anasema kwa njia mbalimbali tena kirahisi sana, Lakini hutaelewa ikiwa huna moyo wa dhati kwa Mungu wako.
Alisema hivi;;
2Nyakati 16:9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, WALIOKAMILIKA MOYO KUELEKEA KWAKE…”
Alisema pia..
Mathayo 15:7 “Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, 8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami”.
Yatupasa sasa tuondoe unafiki wa ndani, kwa kumaanisha kweli kweli kumpenda Mungu kwa moyo, ili sasa aanze kutufunulia sauti yake na kazi zake. Tukimfuata Kristo tujue kinachotupeleka kule ni Utakatifu na haki, na sio kwasababu tunashida tutimiziwe mahitaji yetu, hapo ndipo atapendezwa na sisi, na hatimaye, tutamwona kila inapoitwa leo.
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?
NIFANYE NINI ILI NIKUBALIWE NA YESU?
Yohana 1:29 “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”.
Bwana Yesu sehemu nyingine anajulikana hivi kama Mwana-kondoo kufuatia tabia ya kondoo ilivyo.
Kondoo ni mnyama mpole sana na mnyenyekevu, tofauti na Mbuzi.. Kondoo Anapokatwa manyoya yake huwa hajigusi anatulia sana, na pia hawezi kujichunga mwenyewe huwa anamtegemea mchungaji asilimia mia. Tofauti na mbuzi au Ng’ombe.
Lakini pamoja na hayo kondoo aliyekomaa ambaye tayari kashaota pembe ijapokuwa ni mpole lakini kuna vipindi vichache vichache anakuwa na hasira hususani wakati wa mvua, na pia anapokutana na kondoo mwingine aliye wajinsia kama yake. Hivyo Bwana Yesu hajajifananisha na kondoo aliyekomaa, kwasababu anazo kasoro nyingi.. bali anajifananisha na kondoo mchanga, (mwana-kondoo) ambaye bado hata hajaota pembe, ambaye hawezi kupambana, aliye mnyenyekevu na mpole.
Bwana Yesu naye ni mpole mfano wa huyo.. Maandiko yanamshuhudia hivyo..
Mathayo 21:5 “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.
Na yeye mwenyewe anajishuhudia hivyo katika Mathayo 11:28.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; KWA KUWA MIMI NI MPOLE na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Je umemfuata Yesu aliye mpole?..yeye anayeongea nawe kwa sauti ya upole moyoni mwako, kwamba utubu dhambi?.
Kama bado unasubiri nini?
Okoka leo na ukabatizwe na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu nawe utapata ondoleo la dhambi…na jina lako litaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo na utakuwa na nafasi katika mji ule, mbingu mpya na nchi mpya.
Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.
Tutamshukuru Mungu kwa ajili yako, kwa mchango wako, ili kuifanya injili hii isonge mbele Tuma sadaka yako kwa namba hizi:
Airtel:+255789001312 -Devis Magembe
Mpesa: +255767992434-Denis Magembe