DON’T BE AFRAID WHEN YOU GO DOWN.

MWANA WA MUNGU.

Biblia inasema katika

Waefeso 4: 13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.

15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, KRISTO.”

Hapo anasema NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, ikiwa na maana kuwa, kuna uwezekano tukamfahamu kidogo, hivyo inahitajika kumfahamu sana MWANA WA MUNGU (YESU KRISTO) Na kusudi lenyewe la kumfahamu sana Yesu Kristo, sababu zimeshatolewa hapo mbele nazo ni “ili tusiwe tena watoto wachanga tukichukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja,na kuzifuata njia za udanganyifu”.

Moja ya jukumu la muhimu sana kwa mkristo yoyote aliyezaliwa mara ya pili ni KUJIFUNZA KUMJUA YESU KRISTO NI NANI??…Kwa maana neno lenyewe Mkristo, limetokana na neno KRISTO yaani yeye aliyetiwa mafuta na Mungu, kwa hiyo kama Yesu ndiye Kristo moja kwa moja wafuasi wake wataitwa Wakristo. Taifa la Tanzania lina watu wake wanaoitwa watanzania, kadhalika na taifa la Marekani, watu wake wanajulikana kama wamarekani, vivyo hivyo Taifa la Yesu Kristo, watu wake wataitwa Wakristo..

Kwahiyo ni wajibu wetu na haki yetu kumjua Yesu Kristo kwa undani kuwa yeye ni nani? Katoka wapi? Je! Ni Mungu au ni mwanadamu wa kawaida tu? Anaokoaje okoaje watu!, alikuwa wapi kabla ya ulimwengu kuumbwa, yupo wapi sasahivi, na atakuwa wapi baadaye,? Na kama yupo ana mamlaka gani sasa na anafanya nini sasahivi, na atakuwa na mamlaka gani baadaye?, je! kuna umuhimu wowote kumfuata na kumwamini? Je! kuna sababu yoyote ya kujitumainisha kwake au la!? Kwanini afe? Na kisha azikwe na kisha afufuke? Je! kulikuwa na umuhimu wowote wa yeye kufanya hivyo? Na kwanini aondoke na asingeendelea kubaki duniani? Na kwanini apae kurudi alikotoka sababu kuu ya kufanya hivyo ni nini?..Kwanini alikuwa anajiita mwana wa Adamu, hilo neno mwana wa Adamu maana yake ni nini? na lina mahusiano gani kati yake na sisi? Kwanini anajiita yeye ni mwana wa Daudi? Ana uhusiano gani na Daudi? Na kwanini sehemu nyingine anasema yeye ndiye aliye na ufunguo wa Daudi? Huo ufunguo wa Daudi ndio upi? Na unafungua nini (Ufu 3:7)?

Na kwanini sehemu nyingine anajiita mwana wa Mungu,.. kwanini wanamwita simba wa Yuda kwanini sio simba wa mwituni?,… na kwanini anajiita yeye ni Jiwe kuu la pembeni?, hilo jiwe kuu la pembeni ndio kitu gani? Kwanini anajiita yeye ni mwana kondoo? na wala si ng’ombe?… Kwanini anajiita yeye ndiye ile nyota ya asubuhi,… Kwanini anasema yeye ndio njia na kweli na uzima? Mtu anawezaje kuwa njia?…. Kwanini anajiita shahidi mwaminifu? ….Kwanini anasema yeye ni mzaliwa wa kwanza wa waliokufa? Je! wafu wana wazaliwa wa kwanza na wa mwisho? Nk..nk…nk

Sasa kama huna majibu ya maswali hayo kwa angalau asilimia themanini (80%) na bado unasema wewe ni mkristo, unahudhuria kanisani na kuwa mshirika mwema…Basi jua kuwa HUMFAHAMU YESU KRISTO NI NANI. Na kwasababu hiyo basi utabakia kuwa mtoto mchanga na utachukuliwa na kila aina ya upepo wa Elimu unaokuja mbele yako, mtu Fulani akitokea akikwambia Yesu yuko hivi, utafuata tu! mwingine akitokea akikuambia yuko vile…utafuata tu! hata mganga wa kienyeji akivua hirizi zake na kuvaa suti na kuanza kukuhubiria habari za Yesu kwa jinsi anavyojua yeye, UTAMWAMINI TU! kwa kwasababu HUMJUI YESU KRISTO, Kwasababu wewe ni kama mshabiki wake tu YESU! sio mtu wa Taifa lake, hustahili kuitwa Mkristo, ni Mkristo jina tu!…

Swali maarufu na la kipekee Bwana Yesu alilowahi kuwauliza mitume wake ni hili “Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?”… Unaona swali hilo? Mitume hawakuwa na bahati mbaya sana kuulizwa hilo swali na Bwana Yesu, hata leo Roho Mtakatifu anakuuliza wewe unayesoma ujumbe huu moyoni mwako “Nawe wasema kuwa mwana wa Adamu ni nani?”…je! ni Bwana na mwokozi tu? au ni nani zaidi?..

Nataka nikwambie tu ndugu wa thamani? Unayesoma ujumbe huu…Tafuta sana kumjua Yesu Kristo kuliko kitu kingine chochote! Kuliko hata hizo mali unazozihangaikia, kwasababu uzima, mauti, tumaini, hatima, na mambo yote yanatoka kwake…Dunia yote sasahivi imewekwa chini yake, hakuna chochote kinachotokea kiwe kibaya au kizuri ambacho hajakiruhusu yeye?… Hakuna mtu yeyote ambayo anaweza kutenda jambo lolote liwe baya au zuri kabla yeye hajalipitisha..

Maombolezo 3: 37 “Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza?

38 Je! Katika kinywa chake Aliye juu Hayatoki maovu na mema?”

Unaona hapo? Bwana ndiye muhasisi wa kila kitu! Kwaufupi tu hatuwezi kumwelezea hapa jinsi alivyo lakini yeye ndiye aliyetiwa mafuta na Mungu mwenyewe, nyota iliyosahihi kabisa ya kufuata! Isiyoelekeza upotevuni.

Matokeo ya watu kuzombwa na mafundisho mengi ya uongo yaliyopo duniani sasa ni kutokana na kwamba watu hawamjui Yesu waliyempokea, kwasababu biblia inasema yupo yesu mwingine anayehubiriwa duniani.

(2Wakoritho 11.4 Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!).

Tukiyajua hayo, tutakuwa makini na tutatia bidii kutaka kumjua YESU KRISTO mwokozi wetu kwa undani kila iitwapo leo ili tusimame upande ulio salama, vinginevyo hatuwezi kwepa kuchukuliwa na wimbi hili la upotevu lilipo duniani pasipo hata sisi kujua. Maana biblia inasema watawadanganya yamkini hata walio wateule.

Ni maombi yangu kuwa kuanzia leo,utamtafuta kumjua Huyu Yesu Kristo kwa undani wake?, uweza wake Kumbuka Biblia pia inamtaja yeye kuwa ni SIRI YA MUNGU, hivyo kama ni siri inahitajika bidii kuijua, hivyo basi tumepewa jukumu la kuzidi kumjua Yesu Kristo kwa undani kwa kadri siku zinavyozidi kwenda hata tutakapoufikia umoja wa Imani unaozungumziwa hapo..

Print this post

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

Bwana Yesu alitufundisha SALA iliyo ya kipekee sana, ambayo tunaweza kusema ni sala mama iliyobeba vipengele vyote muhimu vitakavyotuongoza sisi katika kumwomba Mungu daima. Na katika sala hiyo kuna mahali tukifika tunasema UFALME WAKO UJE.

Ulishawahi kujiuliza au kutafakari kwa karibu kidogo ni kwanini ufalme wake uje?. Hiyo inatupa picha kuwa Upo ufalme ambao bado hujafika, nao si mwingine zaidi ya ule wa mbinguni. Mambo yanayoonekana mwilini siku zote yanafunua mambo ya rohoni, katika mwili tunaona falme nyingi tofauti tofauti na kila falme inatafuta kuwa kubwa na yenye nguvu zaidi ya nyingine ili imiliki.. Lakini pia unapaswa kujiuliza ikiwa wanadamu wote ni sawa, ikiwa wanadamu wote walitoka kwa mtu mmoja Adamu, ni kwanini basi wasingekuwa na ufalme mmoja imara, unaomiliki dunia yote?. Ni kwanini basi tunaona falme nyingi tofauti tofauti duniani na kila moja inataka kuwa zaidi ya nyingine?. Ipo sababu inayoifanya dunia kuwa hivyo,

Tunafahamu siku zote ili familia isimame haiwezi kuwa na mababa wawili, ni lazima awepo mmoja tu atakayetawala na kuongoza kila kitu kwenye nyumba vinginevyo kama ingekuwa hivyo basi migongano lazima ingejitokeza na hivyo familia isingeweza kusimama, kadhalika na hii dunia ili isimame haiwezi ikawa na FALME zaidi ya moja inayotawala kote. Vinginevyo siku zote kutaendelea kutokea uharibifu kama tunaouna leo hii duniani.

Sasa ili tufahamu hatma ya falme hizi zote za dunia zilizopo sasa ni vizuri kujifunza kwanza hatma ya falme zilizotutangulia huko nyuma hata kabla ulimwengu kuumbwa, zilitokeaje tokeaje na kusimamaje mpaka leo hii Tunaona kuna ufalme mmoja tu usioasika wa MUNGU ambao ndio huo tunautazamia uje hivi karibuni Kwasababu biblia inasema,

Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani(1Wakorintho 10:11)”.

Embu sasa tujifunze jinsi ule ufalme wa mbinguni ulivyoweza kusimama, Kama tunavyosoma biblia inatuambia hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi..Ikiwa na maana ya MBINGU makao ya malaika na NCHI makao ya wanadamu. Lakini haituambii kuwa mbingu ilikuwa ukiwa, bali nchi ndio iliyokuwa ukiwa na ukiwa huo uliendelea kwa kipindi Fulani biblia isichokitaja mpaka hapo Mungu aliposhuka tena kuiunda dunia na kumuumba mwanadamu ndani yake na baadaye kuja kumpa ufalme.

Sasa tukirudi kule mbinguni baada ya malaika kuumbwa aliunda mfumo wa ufalme, utakaoweza kutawala mambo yote ya kule. Na kama tunavyofahamu ni kawaida ya Mungu kuvitawaza viumbe vyake ili visimamie kazi zake zote za umiliki. Na ndio hapo tunakuja kuwaona malaika wa juu kabisa wakina Michaeli, Gabrieli, na Lusifa,(ambaye ndio shetani) wanatokea ili waongoze vyote katika upana wa mbingu ile, waongoze jamii kubwa sana ya malaika watakatifu waliokuwa mbinguni, wasimamie kazi zote za Mungu zilizokuwa zinaendelea mbinguni. Wauendeshe ule ufalme Mungu aliouweka chini yao katika kanuni zote na utaratibu wote ambao Mungu alikusudia ufanyike. Waende sawasawa na mapenzi ya Mungu.

Ni ufalme uliokuwa wa amani kwa muda mrefu,Mungu aliufurahia akiona jinsi malaika zake wanavyokwenda kwa hekima zake lakini ilifika wakati mambo yakabadilika, Shetani kwa kuona ujuzi uliokuwa ndani yake kuwa ni mwingi, kwa kuona uzuri na hekima aliyokuwa nayo katika bustani ya Mungu ya mbinguni akatamani kuwa kama Mungu, akatamani ule ufalme ungekuwa wake ajitawale mwenyewe, sasa ameshajua kila kitu hana haja tena ya kutembea chini ya kanuni za Mungu, anataka na yeye akawe na ufalme wake ajitegemee, na mawazo yake yalikuwa siku moja amwangushe muumba wake chini ili amiliki vyote(Isaya 14). Hivyo alianza kidogo kidogo kubudi njia zake mwenyewe za udanganyifu huku akisapotiwa na baadhi ya malaika wengine waliokuwepo mbinguni ambao nao pia hawakutaka kutawaliwa. Ikaendelea hivyo hivyo mpaka mapambano yalipozuka mbinguni.

Lakini shetani kwa akili zake chache alifahamu kuwa utaleta upinzani mkubwa sana kwenye ufalme ule kiasi cha kutetemesha mbingu. Alijua hata kama vita itatokea na akashinda basi ufalme ule utagawanyika na kuwa falme mbili. Yeye ataondoka na vyake, na wale kubakiwa na vyao, Hakujua kuwa kama kuna yeyote mbinguni anaouwezo wa kumshusha chini kiasi ambacho tunamwona sasahivi..

Embu jaribu kufikiria mpaka shetani anafikia hatua hiyo ya kuonyesha kiburi kikubwa namna hiyo, Mungu alikuwepo wapi asimpoteze kabisa?. Hii inatuonyesha kuwa Mungu ni Mungu wa uhuru, ikiwa mtu utauchagua uovu uwe sehemu ya maisha yako, Mungu hatakuja kukuondolea kama apendavyo japo anao uwezo huo, bali atamshauri lakini akikataa atamwacha uende kumwangamiza, kwasababu sisi hakutuumba kama maroboti tusiokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi.

Hivyo kiburi cha shetani kilivyozidi kunyanyuka, alivyojiona kuwa ndio anazidi kupata nguvu mbinguni, anaamua sasa atakalo.. Biblia inatuambia ALIANGUKA GHAFLA KAMA UMEME KUTOKA MBINGUNI.

Siku yalipomtokea hayo hakuamini kama ingekuwa ni kiwepesi namna hiyo jinsi alivyoanguka kwa ghafla dizaini ile…Yaani kitendo cha kufumba na kufumbua yeye na malaika zake walijikuta wametupwa chini kwenye dunia ambayo hapo mwanzo ilikuwa haijakawaliwa na wanadamu.

Na ndio maana Bwana Yesu anasema Luka 10:8 “..NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI KAMA UMEME.”

Unaona hapo?. Hakuna kitu kinachosafiri haraka hapa duniani kama Umeme, Hivyo Bwana Yesu kusema hivyo alitaka kuonyesha ni jinsi gani kuanguka kwa shetani kulivyokuwa kwepesi kushinda alivyoweza kufikiria na kwa haraka, yaani wakati alipoanza kujiundia ufalme wake bandia ambao ulionekana kama ni mkubwa kule mbinguni, ulivunjwa mara moja, na kujikuta yeye pamoja na malaika zake hawapo tena mbinguni. Ni tendo la haraka sana kama vile UMEME.

Embu tusome kidogo baadhi ya unabii uliomuhusu Shetani na ufalme wake aliokuwa amejiundia.:

Ezekieli 28: 12 “Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.

13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.

14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.

15 ULIKUWA MKAMILIFU KATIKA NJIA ZAKO TANGU SIKU ILE ULIPOUMBWA, HATA UOVU ULIPOONEKANA NDANI YAKO.

16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.

17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.

19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele”.

Isaya 4: 11 “Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.

12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!

13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.

14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.

15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.

16 Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;

17 Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?

18 Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe;

19 Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu.

20 Hutaungamanishwa pamoja nao katika mazishi, Kwa maana umeiharibu nchi yako, Umewaua watu wako; Kizazi chao watendao uovu hakitatajwa milele”.

Hivyo ndivyo Shetani na ufalme wake ulivyo sasa. 

SASA MAMBO HAYO YANATUFUNDISHA NINI?.

Kama Mungu aliziumba Mbingu na nchi, na kule mbinguni aliweka ufalme, kadhalika na katika nchi aliweka ufalme wake. Na ufalme huo Ulianzia Edeni katika bustani ya Mungu. Akamweka mwanadamu wa kwanza katika bustani hiyo, naye ndiye Adamu kama tu vile Mungu Mungu alivyomweka shetani katika Edeni ya mbinguni bustani ya Mungu (kama tulivyosoma hapo juu kwenye Ezekieli 28:13). Lakini mwanadamu hakutaka kutawaliwa na Mungu ndipo naye akausikiliza ule uongo wa shetani akaasi, na kuanzia hapo ndipo ukawa mwanzo wa ufalme mbovu huko huko zikatokea na nyingine nyingi duniani na kila moja ya hizo falme zipo chini ya malaika wa shetani sasa. Na shetani akiwa kama mfalme wa wafalme wa ulimwengu huu sasa.

Kumbuka shetani alishashindwa mbinguni akijua kuwa lile anguko lake lilikuwa kuu sana. Hivyo alipotupwa huku duniani anawavaa wanadamu wawe na tabia kama za kwake ili nao siku ya uharibifu wao ufike kwa ghafla na haraka sana kama UMEME. Ili wote kwa pamoja wajikute katika lile ziwa la Moto.

Na ndio maana biblia ilishasema katika..

1Wathesalonike 5: 2 “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, NDIPO UHARIBIFU UWAJIAPO KWA GHAFULA, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.”

Ndugu, anguko la ufalme huu mbovu wa shetani unaoendelea sasa duniani utakuja kwa ghafla sana na haraka, mahali ambapo wanadamu wanasema sasa sayansi yetu imetufikisha mbali, ustaarabu wetu wa umoja wa mataifa na haki za kibinadamu sasa zinazuia uvunjifu wa amani duniani, hivyo dunia inaweza kuendelea kuwepo kwa muda wa mabilioni ya miaka, Kumbuka hapo hapo ndipo shetani alipofikia kabla hajaanguka aliwaza kule mbinguni. lakini siku yalipompata ndipo alipojua kuwa aliye juu ndiye anayetawala. Kadhalika ndivyo itakavyokuwa kwa dunia hii ambayo ipo karibuni kutoweshwa, Ni lazima iwe hivyo ili kuupisha ufalme wa Mungu kuchukua nafasi yake kwa kupitia YESU KRISTO BWANA WETU.

Mji wa Babeli, uliotukuka sana duniani zamani hizo na uliohusika kuwachukua wana wa Israeli mateka, ulikuwa ni ufalme ambao hakuna mtu angeweza kutegemea kama ungeanguka, kwa jinsi ulivyokuwa na ulinzi mkubwa, na kuta imara, na ustaarabu mkubwa..lakini ulipofika siku yake ya maangamizi, Viganja vilitokea ukutani mwa mfalme wa ufalme huo na kuandika MENE MENE, TEKELI na PERESI..Usiku huo huo ndio ulikuwa mwisho wa mji unaoitwa Babeli. Ndivyo itakavyokuwa kwa falme zote za duniani zilizopo leo, uharibifu utakuja gafla na UFALME WA YESU KRISTO, UTAKUJA.

Ufunuo 11:15  “Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, UFALME WA DUNIA umekwisha kuwa UFALME WA BWANA WETU NA WA KRISTO WAKE, naye atamiliki hata milele na milele”.

Hivyo ndugu, usifuate upepo wa huu ulimwengu unavyoelekea, ukapumbazika kwa jinsi unavyozidi kunawiri ukadhani kuwa bado muda mrefu Kristo kurudi mara ya pili na kuangusha huu ufalme wa giza uliopo sasa. Jua tu uharibifu wake utakuja saa watu wasioweza kuutazama. Utaanguka kama umeme. Ni maombi yangu kuanzia sasa utajiweka tayari na kuanza kutazama mambo ya ufalme wa mbinguni unaokuja usiohasika zaidi ya mambo ya ulimwengu huu ambayo ni kitambo tu.

Bwana akubariki sana.

Print this post

JIWE LA KUSAGIA

Marko 9.41 “Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
42 Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. “Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini”.

Bwana Yesu alisema Ishara hizi zitafuatana na hao waaminio? kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya (Luka 1:17-18).

Lakini pamoja na ishara hizo, zipo ishara nyingine zinazofuatana na hao waaminio..Na ishara hizo ni thawabu zinazoambatana nao, kadhalika na laana zitakazoambana nao kama wasipotii.

Mtu aliyemwamini Kristo, akatubu na kuacha dhambi zake kabisa, na kupokea Roho Mtakatifu, Bwana huwa anampa thawabu mkononi mwake katika ulimwengu wa roho na huwa hiyo thawabu inatembea naye…Inapotokea kafika mahali kakaribishwa na watu na kuhudumiwa vizuri hata nafsi yake ikafurahi na kuburudika, wale watu waliomhudumia mtu huyo kwakuwa ni mtu wa Kristo, huwa biblia inasema haimpiti kamwe thawabu yake. Kumbuka kumtendea wema Mkristo ni tofauti na kumtendea mema maskini ambaye sio Mkristo.

Ukimtendea mema Mkristo ni sawa umemtendea mema Kristo mwenyewe kwasababu ndani ya yule mtu, yupo Kristo mwenyewe. Ukimkaribisha umemkaribisha Kristo mwenyewe, ukimbariki ni sawa umembariki Kristo mwenyewe..Hivyo thawabu yake ni kubwa zaidi kuliko thawabu ya kumsaidia mtu mwingine yoyote ambaye sio mkristo.

Lakini pamoja na kwamba kuna Baraka zinazoambatana na watoto wa Kristo, wote waliozaliwa mara ya pili, zipo pia Laana zinazofuatana na hawa watoto wa Mungu. Biblia inasema “amlaaniye Israeli atalaaniwa na ambarikiye Israeli atabarikiwa…Sasa licha ya wale wa Israeli tunaowaona kule mashariki ya kati, wapo pia waisraeli ambao ni waisraeli hasa,.. na hawa sio wengine zaidi ya watoto wote wa Mungu,waliompokea Bwana Yesu Kristo na kumwamini na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake. Hawa ndio waisraeli hasa biblia inayowataja.

Hivyo kumlaani mtu yoyote ambaye ni milki ya Bwana Yesu, mtu aliyeamua kuyasalimisha maisha yake kwake ni sawa na kumlaani Kristo mwenyewe na ni sawa na kujilaani wewe mwenyewe… Kwahiyo ni muhimu sana kuchunga midomo yetu, mbele za watoto wa Mungu. Usimwone ni Mpole ukamdharau wala usimwone ni wa huruma ukamtamkia maneno yasiyofaa utajitafutia matatizo ambayo chanzo chake hutakijua.

Sasa laana nyingine iliyo mbaya, ambayo inatembea na hili kundi la watoto wa Mungu, ni ile itokanayo na KUWAKOSESHA.

Ni heri umlaani mtu aliyempa Kristo maisha yake, kwasababu mtu huyo anaweza kukusamehe na pengine Mungu akaepusha ghadhabu yake juu yako, lakini kosa lolote mtu atakalofanya litakalomfanya yule mtoto wa Mungu aliyekuwa amesimama kiimani KUANGUKA…Hilo ni kosa ambalo halina msamaha ni baya kuliko kosa la kumlaani.
Sasa nini maana ya KUKOSESHA.

Kukosesha ni jambo lolote ambalo mtu anaweza kumfanyia mtoto wa Mungu kwa makusudi aliyesimama kiimani kuanguka na kurudi nyuma au kutenda dhambi, au kosa lolote litakalomfanya mtoto wa Mungu amkosee Mungu wake.

Kwamfano imetokea Binti kampa Kristo maisha yake kweli na kakusudia kuacha dhambi kabisa, na kabatizwa, Na akaanza kuishi maisha ya ukristo kulingana na maandiko, lakini kijana mmoja pale pale kanisani anayejua kabisa maandiko anatokea na kuanza kumsumbua na kumtaka, na hatimaye kumdanganya, na kwasababu ya ule uchanga wa kiroho wa yule binti akanaswa na mtego wa Shetani na kuanguka katika dhambi ya uasherati na kumkosea Bwana Mungu wake, sasa yule binti Bwana atamwadhibu … Lakini yule kijana aliyemkosesha ana adhabu kubwa zaidi kuliko ya yule binti.. Au binti anayejua kabisa kijana Fulani kaokoka na anamtumikia Bwana kwa moyo,lakini kwa tama yake ya macho anaanza kumtafuta kijana yule na kumshawishi, kwa kujipendekeza hata akamwangusha yule kijana kwenye dhambi ya uasherati wake hapo Ndio biblia inasema… “Ingemfaa zaidi mtu huyo JIWE LA KUSAGIA LIFUNGWE SHINGONI MWAKE, akatupwe baharini, KULIKO KUMKOSESHA MMOJAWAPO WA WADOGO HAWA.”

JIWE LA KUSAGIA NI NINI BASI?.

Zamani watu walikuwa hawasagi nafaka kwa mashine kama tulizonazo sasa, walikuwa wanasaga kwa kutumia mawe mawili, lile kubwa linakaa chini na lile dogo linakuwa juu ndio linalotumika kusagia…mawe haya yanakuwa ni mazito sana ili kusudi kusaidia nafaka ile iweze kusagika na kuwa unga…Sehemu chache sana katika nyakati hizi ndio bado zinatumia huo ustaarabu wa usagaji wa nafaka. Lakini zamani ilikuwa ni lazima kila nyumba iwe na hilo jiwe, hata kama hiyo nyumba ni maskini vipi, ilikuwa ni kitu cha muhimu sana, ni kama tu kinu kwa sasa..usipokuwa na jiwe hilo ilikuwa huwezi kula kwasababu ndio kifaa cha msingi kabisa cha riziki kilichokuwa kinahitajika katika nyumba kwa wakati huo.

Sasa Bwana Yesu alitumia mfano wa jiwe la kusagia, kufunua kwamba mtu yoyote atakayemkosesha “mmojawapo wa wadogo wamwaminio yeye” ingelimfaa zaidi mtu huyo jiwe hilo la kusagia lifungwe shingoni mwake na kwenda kutupwa baharini…Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba INGEMFAA ZAIDI MTU HUYO RIZIKI YAKE YOTE ANAYOIPATA IONDOLEWE, NA IWE KITANZI KWAKE CHA KUMWUA KATIKA MAANGAMIZI AMBAYO YANATOKANA NA HIYO RIZIKI. na pale anaposema akatupwe katika bahari alimaanisha mtu huyo, ATUPWE KATIKA ZIWA LA MOTO”

Unaona hiyo laana jinsi ilivyo mbaya?? Ina maana kuwa katika mahali popote unapopatia riziki, hiyo sehemu inakuwa kitanzi kwako cha kukufanya wewe uangamie kwa kuzama kama mtu anavyozama katika maji akiwa na jiwe shingoni, na hatimaye hiyo sehemu yako ya kujipatia riziki (kazi yako) inakuua na kuwa sababu ya kukupeleka katika ziwa la Moto.

Ulikuwa unafanya kazi nzuri, na kupata kipato kizuri, hiyo kazi inageuka kuwa kitanzi kwako inaanza kukushusha chini, inakuzamisha kwenye matatizo ambayo hayajawahi kutokea, inakutafuna na mwisho wa siku inakuua, na baada ya kifo inakupeleka katika ziwa la moto. Hata kama bado hujafikia hatua ya kujitafutia mwenyewe lakini ikiwa unafanya dhambi hizo za makusudi, itafika tu wakati utatatufa kitu kwa ajili ya maisha yako. Na ndiko huko huko utakapokwenda kujimalizia mpaka kuzimu.

Ndugu yangu unayesoma haya, jiepushe na watoto wa Mungu, wewe binti kaa mbali na walioamua kumfuata Bwana Yesu, usijaribu kuwashawishi wawe kama wewe ulivyo, usijaribu kuwashawishi watoke katika mstari ili kumkosea Bwana wao wawe kama wewe. Kama wewe umeamua kuwa vuguvugu basi kuwa kwa nafsi yako mwenyewe, usiwafanye watoto wengine wa Mungu wajikwae kwasababu yako, ni kujitafutia matatizo yasiyokuwa na utatuzi.

Usiwashawishi wengine, kuvaa vimini, kuvaa suruali, kupaka wanja, kwenda disco, na ndani ya dhamira yako unajua kabisa, mambo hayo ni makosa kuyafanya kwa watumishi wa Mungu…Usijaribu kuyafanya hayo, kwasababu ni sawa na unamfanyia Kristo mwenyewe.

1Wakoritho 8: 12 “Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo”.

Kwa nje utamwona katika hali ya udhaifu, lakini ndani yake yupo Kristo, Siku ile ya Mwisho Bwana Yesu alisema atawatenga kondoo na mbuzi, mbuzi ni wale wote waliolikwaza na kulihuzunisha na kulikosesha kundi hili la watoto wa Mungu, wale wote ambao waliwalaani, na kuwatesa na kuwakosesha watoto wa Mungu hao wote watakaa mkono wa kushoto wa YESU Kristo siku ile, watahukumiwa na kisha watatupa katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti.

Mathayo 25: 41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.

Kama ulikuwa unafanya hayo pasipo kujua, Bwana ni mwenye Rehema, anachotaka kwako ni ukiri tu ulifanya hayo pasipo kujua na kwamba unahitaji kugeuka na kuwa kiumbe kipya, kwa kudhamiria kabisa kumuishia Mungu, na kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza yeye.. Na kuwa katika kundi lake lililobarikiwa la kondoo na sio mbuzi. Baada ya kutubu Bwana alitupa maagizo ya kwenda kubatizwa, hivyo katafute haraka mahali panapobatiza ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa JINA LA YESU KRISTO na baada ya kufanya hivyo Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kweli yote. Baada ya hapo utakuwa na uhakika wa uzima wa milele, na umekamilisha hatua za muhimu za wokovu.

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

JINA LAKO NI LA NANI?

TUNAYE MWOMBEZI.

MJUE SANA YESU KRISTO.

DALILI ZIPI ZITAMTAMBULISHA MTU KUWA AMEFANYIKA KIUMBE KIPYA?


Rudi Nyumbani

Print this post

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

Biblia inatuambia kuwa malaika ni roho watumikao, kuwahudumia wale watakaourithi wokovu. (Waebrania 1:14). Biblia inatuambia pia shetani naye ni mshitaki wetu, yeye na jeshi lake la mapepo wakitushita sisi mbele za Mungu wetu mchana na usiku tunaona kama walivyofanya kwa Ayubu (Ufunuo 12:7), vivyo hivyo malaika watakatifu wa Mungu ambao hao Mungu aliwaweka kwa lengo la kutuhudumia sisi (yaani wakristo), wanasimama mbele za Mungu wetu usiku na mchana wakipeleka habari zetu njema mbele zake.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO MBINGUNI SIKU ZOTE HUUTAZAMA USO WA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI.” (Mathayo 18.10).

Hii ni huduma kuu ya malaika walio nayo sasa.

Lakini japo malaika hawa wamepewa uwezo mkubwa zaidi yetu sisi, japo ni watakatifu sana kuliko sisi, japo ni wakamilifu kuliko sisi lakini tunasoma wanaposimama mbele za Mungu ili kupeleka habari zetu mbaya wanatetemeka na kuogopa, Embu fikiria leo hii unajiita mkisto, na siku ile ulipofanyika kuwa mwana Mungu, ulifahamu kuwa Kristo alilituma jeshi lake la malaika kukulinda pamoja na kuhusukia kuchukua dua zako na matendo yako mema mbele za MUNGU. Lakini jaribu kifikira wewe unayejiita mkristo halafu leo hii unakwenda kuzini, na huku unajua kabisa wapo malaika watakatifu walitumwa kutembea na wewe, halafu wanakuona unafanya kitendo hicho cha aibu na cha kichafu ambacho mtu anayejiita Mkristo hastahili kukifanya. Wewe unadhani malaika watakatifu watapeleka repoti gani nzuri ya kwako mbele za Mungu.?

Kwasababu kumbuka unapoomba maombi yako yanachukuliwa na malaika na kufikishwa mbele ya kiti cha enzi, unapofanya wema, wema wako unachukuliwa na malaika moja kwa moja na kuwasilishwa mbele ya kiti cha enzi, anapofanya tendo lolote jema linachukuliwa na kupelekwa katika kumbukumbu za kimbinguni zikingojea kusomwa mbele ya kiti cha enzi mbinguni, kadhalika yule malaika husika naye huwa anajisikia fahari kupeleka habari njema kama hizo mbele za Mungu. Hata akifika pale atakusifia kwa maneno mazuri na kumkumbusha Mungu na mambo mengine ya kwako mazuri unayoyafanya hata kama hujawahi kumwomba Mungu. Malaika wanakuwaanapanda j na kushuka juu yako kupeleka mema yako na kukuhudumia sawasawa na maono aliyoyaona Yakobo (aliona malaika wakipanda juu na kushuka) Mwanzo 28:12 “Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake”.

Lakini unapokuwa ni mwovu halafu unasema umeokoka, umebatizwa, umepokea Roho Mtakatifu, hataweza kupeleka habari yoyote njema mbele za Mungu kwa ajili yako?. Kumbuka yeye ni mtakatifu lakini matendo yako yanamfanya ajione mchafu na asiyestahili kupeleka habari zako mbaya mbele zake. Na hii ni mbaya sana kwasababu wakati Mungu atakapopokea ripoti za wana wake wengine duniani, za kwako zitakuwa hazifiki, na hapo atakapomuuliza malaika husika aliyepewa jukumu la kutembea na wewe, vipi habari za huyu mtu kwanini hazinifikii, lakini kwa kuwa malaika wa Bwana ni wenye hekima nyingi, watajaribu kuzungumza tu yale mema ya nyuma uliyokuwa anayafanya na kusitiri ubaya wako. Lakini jicho la Mungu linaloona mbali, litatazama lenyewe. Na yeye na kuuangalia mwenendo wako yeye mwenyewe. Hapo ndugu usitamani ufikie hatua hiyo kwasababu hakuna msamaha tena ghadhabu ya Mungu ni kali, hatua hiyo ukishafikia ni nani atakayekutetea?.

2Petro 2:10 “Na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.

11 Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; IJAPOKUWA MALAIKA AMBAO NI WAKUU ZAIDI KWA UWEZO NA NGUVU, HAWALETI MASHITAKA MABAYA JUU YAO MBELE ZA BWANA.

12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;

14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;

15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;”.

Unaona hapo biblia inasema “; IJAPOKUWA MALAIKA AMBAO NI WAKUU ZAIDI KWA UWEZO NA NGUVU, HAWALETI MASHITAKA MABAYA JUU YAO MBELE ZA BWANA”.

.. Unasema wewe ni mkristo lakini unapojisikia tu kutenda dhambi unakwenda kufanya bila kuogopa kuwa Mungu juu anakutazama. Unakuwa mlevi wa chini chini, hutaki ujulikane kwa wakristo wenzako, hujui kuwa malaika wa Bwana wanaona mambo unayoyafanya, wanakosa jambo jema la kwenda kuzungumza juu yake mbele ya kile kiti kitakatifu cha Enzi mbinguni. Unakula rushwa, unakuwa mwizi, unaabudu sanamu, unatazama pornography na unafanya mustarbation kisirisiri ni kweli mwanadamu hakuona lakini wapo wengine wanaokuona, na hao si wengine zaidi ya malaika wa Bwana na mashetani.

Ikiwa sifa zako njema hazipelekwi na malaika basi uwe na uhakika kuwa mambo yako maovu yanachukuliwa na mapepo na kuimbwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu usiku na mchana.

Sasa baada ya Mungu mwenyewe kushuka na kuangalia matendo yako, kwa dua za hayo mashetani ambazo ziliwasilishwa mbele zake, akiona jinsi uliyoonywa mara nyingi ugeuke hutaki ndipo hapo Bwana anatoa tamko. HUYU SI WANGU TENA!. Unakabidhiwa shetani, kuanzia huo wakati unakuwa milki halali ya shetani, hali yako inakuwa mbaya kuliko ulivyokuwa mwanzoni wale malaika waliotumwa kukulinda wanaondoka, habari zako zinasitishwa kutajwa mbinguni wema wako wote unasahauliwa.

Tafsiri ya jina shetani au Ibilisi ni MCHONGEZI au MSHITAKI. Kazi ya shetani kubwa ni kutushitaki mbele za Mungu usiku na mchana…Malaika wao wanapeleka habari zetu njema mbele za Mungu lakini shetani na majeshi yake wao wanapeleka habari mbaya mbele za Mungu. Hiyo ndiyo vita kubwa inayoendelea katika ulimwengu wa Roho, kati ya malaika na mapepo.

Hawapigani kwa kukatana na mapanga, hapana bali wanashindana kwa hoja.

Tuchukue mfano mwepesi..mkristo mmoja anayeitwa Rodgers anayesema ameokoka leo kafunga na kusali lisaa limoja, katoa zaka kanisani, na kamsaidia ndugu mmoja aliyekuwa na uhitaji mtaani kwake, sasa kinachotokea katika ulimwengu wa Roho yule malaika wake anayetembea naye anapeleka habari za wema wake huo mbele za Mungu, na kumwambia Mungu kuwa Mtumishi wako Rodgers kafanya hichi na kile leo, hivyo anastahili thawabu Fulani kulingana na Neno lako hili na lile, Lakini bahati mbaya wakati malaika hao wanamsifia Rodgers mbele za Baba, Rodgers pasipo kulijua hilo kesho yake anakwenda kuzini..kinachotokea sasa ni shetani na malaika zake wanakwenda kumchongea Rodgers mbele za Mungu, kwamba yule mtu mnayesema ameokoka na anastahili kupata hichi na kile leo hii tumemwona anazini hivyo kulingana na Neno hastahili kuitwa mtoto wa Mungu kwasababu maandiko yanasema aziniye na mwanamke hana akili kabisa(Mithali 6:32) na zaidi ya yote maandiko “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu 1Yohana 3:9 ” …na kumbuka haya mapepo yanatoa kabisa mistari mbele za Mungu kumshtaki Rodgers na kwasababu yametoa hoja za nguvu mbele za Mungu, wanakuwa wamewashinda wale malaika wanaomsifia Rodgers na hivyo Rodgers anakabidhiwa shetani. Hivyo ndivyo shetani anavyowashitaki watu.

Unakumbuka maandiko yanasema wana wa Mungu (Malaika) siku moja walipokwenda kujihudhurisha mbele za Mungu shetani naye alikwenda katikati yao kumshitaki Ayubu? (Hiyo inapatikana katika kitabu cha Ayubu 1:6-12).

Kwahiyo Mtu anayeishi maisha ya uvuguvugu na bado anasema ni Mkristo, anafanyika kuwa chombo cha shetani kikamilifu, kama ulikuwa mzinzi kidogo hapo ndipo unajikuta nguvu mbaya ya uasherati unakuvaa unakuwa unakuwa zaidi ya hapo, pombe ulikuwa unakunywa kidogo, unafikia hatua ya kumaliza hata kreti, tabia yako inabadilika ghafla na kibaya zaidi hata kumrudia Mungu hutaweza tena kwasababu Bwana Yesu alishasema hakuna mtu anayeweza kuja kwangu, isipokuwa kwanza kavutwa na Baba yangu aliye mbinguni. Sasa kama ni Mungu mwenyewe kakukataa unadhani ile nguvu ya kutubu wakati huo utaitolea wapi?. Haiwezekani.Na mwisho wake ni Mauti, kwasababu biblia inasema mshahara wa dhambi ni MAUTI, Na ndio maana malaika watakatifu wanaogopa kupeleka mashitaka yako mabaya juu mbele za Mungu, kwasababu wanafahamu madhara yatakayomkuta mtu huyo mara baada ya kukataliwa.

Ni jambo la kuogopesha sana. Leo hii Bwana anapotuambia tuwe moto, anaamisha kweli kweli, maana tukiwa vuguvugu ndio huko kutapikwa kunafuata. Inasikitisha kuona kwamba mtu anasema ameokolewa na Bwana lakini mambo ya kidunia hajayaacha,.bado anavaa kidunia, anavaa vimini, anavaa suruali, anakwenda Disko, anasikiliza nyimbo za kidunia, anaipenda dunia kuliko kumpenda Mungu, anatazama pornography, anakwenda kwa waganga,ni mtukanaji. Biblia inasema ni heri mtu huyo asingookoka kabisa, kwasababu hata wale malaika watakatifu wasingeletwa kumtazama, Lakini kuwa vile halafu unaishia kuwatia visirani, na kuwafedhehesha unadhani mwisho wake utakuwa ni nini?.

Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri Bwana aliwaagizia malaika wake aende mbele yao, na akawaonya wasimtie kisirani kwa mienendo yao mibovu kwa kuwa hatawasamehe,(kutoka 23:20) Unaona tunasema tumekuwa wakristo tujue kuwa hatupo wenyewe. Bali Roho wa Kristo yupo pamoja nasi kadhalika na jeshi la kifalme la malaika wa mbinguni lipo pembeni yetu kutuhudumia. Hivyo tunapaswa tuwe makini sana na mienendo yetu.

Ni maombi yangu, leo hii utaulinda wokovu wako, kila wakati. Ikiwa malaika tu wenyewe wanaogopa kupeleka habari zetu mbaya, japo wao ni watakatifu, unadhani sisi tunapaswa tuishije. Malaika japo wokovu hauwahusu wao lakini wanasita kuizungumza mienendo yetu mibaya mbele za Mungu, si zaidi sisi ambao tupo duniani ambao wokovu unatuhusu? Tunapaswa tujilinde sana mienendo yetu ya kikisto.

Ikiwa bado hujampokea Kristo katika maisha yako huu ndio muda, unachopaswa kufanya ni kutubu mwenyewe kwa kumaanisha kuacha dhambi zako na maisha yako ya kale, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo upate ondoleo la dhambi zako, (Matendo 2:37-38)na baada ya hapo utafanyika mwana wa Mungu kwa Roho wa Kristo atakayekuja ndani yako.. Nawe pia jeshi hili la kimbinguni la malaika watakatifu litatumwa kwako kukulinda, kukutetea na kupelekea habari zako njema mbele za kiti cha Enzi usiku na mchana.

Print this post

SIKU ZA MAPATILIZO.

Zamani ilikuwa watu wakihadithiwa habari za siku za mwisho, walikuwa wanatetemeka na machozi yakiwatoka, lakini sasahivi Watu wanapuuzia, watu hawana hofu tena wakidhani kuwa yale mapigo yaliyoandikwa katika kitabu cha ufunuo ni kama hadithi ambazo hazitakuja kutokea duniani siku za hivi karibuni, wanaona kama mambo yale hayatauhusu sisi kabisa,ni ya watu wa vizazi vingine vya mbeleni sana vitakavyokuja, hivyo hawana haja ya kuyafuatilia sana, wengine wanayachukulia kiwepesi wepesi, wengine wanafanyia mizaha pale biblia inaposema siku hiyo watu wote, wakiwemo wafalme, majemedari, wakuu wa nchi, matajiri, watumwa, watu wa kila namna watakapojificha chini ya mapango na miamba na kuiomba iwaangukie ili tu wajisitiri na hiyo hasira kali ya mwana-kondoo ambayo inakwenda kumwaga juu yao (Ufunuo 6:12).

Hicho sio kipindi cha kukitamani kabisa, na ndio maana Bwana anatupa tahadhari mapema, akituonya tangu zamani tusitamani kuwepo huko, kwasababu pindi utakapojikuta tu umeingia katika hasira kali ya mwana-kondoo, huko ujue neema ya Kristo ilishaondoka siku nyingi. Mungu ni Mungu wa kisasi, biblia inasema kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Sasa siku hizo ndizo Bwana alizozitenga KUPATILIZA maovu ya ulimwengu wote. Ni kipindi maalumu ambacho Bwana amekiandaa kwa wale ambao wanaukataa wokovu sasa hivi na wanaoipinga kweli. Kwa watu wote wanaofanya maovu sasa hivi kwa siri, wakidhani kuwa Mungu hawaoni. Wakati wa Nuhu Mungu aliwapatiliza watu wa kipindi kile kwa adhabu moja yaani gharika, watu wa Sodoma kwa adhabu moja yaani moto, lakini watu tunaoisha sasahivi ambao tumeshaona mifano yote hiyo lakini hatutaki kutubu biblia inasema, kizazi hiki kimeandaliwa, dhiki, mapigo, pamoja na moto.

Hii ikiwa na maana kabla ya watu kuteketezwa kabisa ni lazima Bwana kwanza APATILIZE maovu yao yote waliyoyatenda, siku zote za maisha yao walizoishi hapa duniani, kwa dhiki na kwa mapigo ya vile vitasa 7 kisha waangamizwe halafu baada ya hapo kitakachofuata ni kutupwa katika lile ziwa la moto.

Ni lazima kwanza Bwana alipe kisasi kwa maovu yote yanayoendelea duniani sasa hivi. Siku hizo za kutisha Bwana Yesu aliziita siku za mapatilizo, alipokuwa pale katika milima ya Mizeituni akiwaleza wanafunzi wake mambo yatakayotokea katika siku za mwisho.

Luka 21:22 “Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.”.

Unaona? Yote yaliyoandikwa ni lazima yatimie, kisasi Bwana alichosema atalipa ni lazima kije tu, maovu yanayoendelea sasa hivi duniani, mauaji, ubakaji, uabuduji sanamu, uchawi, uzinzi, n.k. yote Bwana ni lazima ayapatilize kabla ule mwisho haujafika.

Ezekieli 7: 5 “Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, JAMBO BAYA LA NAMNA YA PEKE YAKE; ANGALIA, LINAKUJA.

6 Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.

7 Ajali yako imekujia, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.

8 BASI HIVI KARIBU NITAMWAGA GHADHABU YANGU JUU YAKO, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; NAMI NITAKUPATILIZA MACHUKIZO YAKO YOTE.

9 Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga”.

Siku hizo Bwana anasema hakutakuwa na huruma, watu watalia na kujutia na kutubu lakini hakuna atakayesikia, mpaka ghadhabu ya Mungu ya mwisho itakapomalizwa kumwagwa duniani. Na Bwana anasema ni HIVI KARIBUNI. Wapo watu wanadhani mwisho bado siku nyingi. Ni jambo la kutisha sana kujikuta umebaki siku ile, kwasababu ni lazima Mungu apatilize uovu wote, kwa watu wote wanaokufuru leo, na kuutukana msalaba.

Waebrania 10:28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

30 Maana twamjua yeye aliyesema, KUPATILIZA KISASI NI JUU YANGU, MIMI NITALIPA. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.

31 NI JAMBO LA KUTISHA KUANGUKA KATIKA MIKONO YA MUNGU ALIYE HAI.”

Ndugu kanisa tulilopo ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama LAODIKIA (Ufunuo 3 ). Na makanisa mengine 6 yalishapita, na hili tulilopo ndilo la 7 na la mwisho, kama hujui hilo basi jaribu kufuatilia utalifahamu hilo. Kanisa lile la sita lijulikanalo kama FILADELFIA, kutokana na kumpendeza Mungu kwao, Mungu aliliahidia kuliepusha na ILE SAA YA KUJARIBIWA iliyokuwa imewekwa tayari kuujilia ulimwengu mzima (Ufunuo 3:10). Hivyo hiyo saa ni lazima ije katika kanisa letu hili, la Laodikia. Ni siku za mapatilizo ya ouvu wote. Siku ambayo dunia itajaribiwa.

Siku hizo za hatari, hata manabii wote wa uongo, pamoja na yule mpinga-kristo, ambaye atatokea Taifa la RUMI, Kanisa Katoliki, kulingana na unabii wa kibiblia, na wachungaji wote wa uongo, na waalimu wote wa uongo, na wote wanaojiita watumishi wa Mungu ila wa uongo, Hukumu zao zote zitapatilizwa pia katika hicho kipindi.

Yeremia 23: 1 “Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema Bwana.

2 Kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; ANGALIENI, NITAWAPATILIZA UOVU WA MATENDO YENU, ASEMA BWANA”.

Ezekieli 13:6-11 “ Wameona ubatili, na uganga wa uongo, hao wasemao, Bwana asema; lakini Bwana hakuwatuma; nao wamewatumainisha watu ya kuwa neno lile litatimizwa.

7 Je! Hamkuona maono ya bure, hamkunena mabashiri ya uongo? Nanyi mwasema, Bwana asema; ila mimi sikusema neno.

8 Basi tazama, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu mmenena ubatili, na kuona uongo, basi, kwa sababu hiyo, mimi ni juu yenu, asema Bwana MUNGU.

9 Na mkono wangu utakuwa juu ya MANABII WANAOONA UBATILI, na KUTABIRI UONGO; hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.

10 Kwa sababu hiyo, KWA SABABU WAMESHAWISHI WATU WANGU, WAKISEMA, AMANI; WALA HAPANA AMANI; na mtu mmoja ajengapo ukuta, tazama, waupaka chokaa isiyokorogwa vema;

11 basi waambie hao wanaoupaka ukuta chokaa isiyokorogwa vema, ya kwamba utaanguka; kutakuwa mvua ya kufurika;”

Unaona hapo! Biblia inasema manabii hawa wa Uongo wanawashawishi watu wakiwaambia AMANI,kuna amani na wakati hakuna amani, ndugu yangu epuka injili za faraja, injili ambazo huambiwi madhara ya dhambi zako, wala madhara ya hukumu ya milele, wewe ni kutiwa moyo tu na maisha yako unayoishi hata kama ni machafu kiasi gani..

Siku hizo utawala mbovu wa Roma chini ya kanisa Katoliki lililohusika kuua watakatifu wa Mungu zaidi ya milioni 68, katika kipindi cha Giza, na kumwaga damu zisizo na hatia katika vipindi vyote vya kanisa, Bwana atalihukumu nalo pia, biblia inasema hivyo. Ndio yule Babeli mkuu, mama wa makahaba na machukizo ya nchi,anayezungumziwa katika kitabu cha ufunuo

sura ya 17. Mungu atapatiliza damu za watakatifu wake juu yao.

Ufunuo 19:1 “Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu.

2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na KUIPATILIZA damu ya watumwa wake mkononi mwake.

Hivyo huu sio wakati wa kuzisubiria siku hizo, neema bado ipo

Yeremia 5: 7 “Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba.

8 Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake.

9 Je! Nisiwapatilize kwa sababu ya mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juuya taifa la namna hii?”

Biblia inasema “Tokeni kwake enyi watu wangu Ufunuo 18:4”..tutoke katika mambo ya ulimwengu huu, tujiepushe na kizazi kilichomkataa Bwana, tujiokoe nafsi zetu, maana siku ya Bwana inayowaka kama moto inakuja.

Mtume Petro baada ya kuwahubiria watu maneno ya uzima ya Yesu Kristo, walimwuliza wakisema

Matendo 2: 37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, JIOKOENI NA KIZAZI HIKI CHENYE UKAIDI.

41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”.

Na wewe leo unayesikia maneno haya, Roho anakuonya vile vile, tubu leo ukabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo, kama hujafanya hivyo, upokee kipawa cha Roho Mtakatifu na ujiepushe na KIZAZI HIKI CHENYE UKAIDI.

Print this post

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

Mwili wa mwanadamu au mnyama yoyote ni makazi ya roho, hakuna mtu asiyekuwa na roho ndani yake wala hakuna mnyama asiyekuwa na roho ndani yake. Kwahiyo mwili ni kama mavazi ya roho. 

Kwahiyo mtu aliyempa Yesu Kristo maisha yake, aliyetubu kabisa dhambi zake, na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, ndani yake kunakuwa na roho mbili, {Roho yake binafsi na Roho wa Mungu(Roho Mtakatifu)}. Roho Mtakatifu kazi yake anapoingia ndani ya mtu, kazi yake ni kuwa msaidizi, anaisaidia roho ya mtu aliyempa Bwana maisha yake ili itende mapenzi ya Mungu aliye mbinguni. Anaingia katika vyumba vya ndani kabisa vya moyo na anafanya kazi kwa namna ya kipekee ambayo haiwezi kuchunguzika kirahisi.
biblia imesema katika:

1Wakorintho 6: 19 “ Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Sasa kumbuka hapo inasema kuwa mwili wenu ni HEKALU LA ROHO MTAKATIFU, haijasema miili yenu ni NYUMBA YA ROHO MTAKATIFU. Na kama unavyojua hekalu ni tofauti na nyumba ya kawaida, nyumba ya kawaida inaweza ikawa na matumizi mengi, inaweza ikageuzwa ikawa ya kupangishwa, inaweza ukauzwa, inaweza kutumika leo kama nyumba ya familia kesho ikawa nyumba ya kulala wageni, inaweza ukageuzwa ikawa sehemu ya biashara n.k Lakini tunapozungumzia hekalu, haliwezi likawa kwa jinsi mtu anavyotaka…Hekalu kazi yake ni moja tu “NI MAHALI PA KUFANYIA SALA NA IBADA BASI!”

Kwahiyo Unaweza ukaona hekalu ni sehemu nzito kidogo, na ina sheria kali kidogo kuliko nyumba ya kawaida. Hivyo mtu anapopokea kipawa cha Roho Mtakatifu mwili wake siku ile ile unageuka, na kuwa HEKALU LA ROHO MTAKATIFU. Kuanzia huo wakati na kuendelea shughuli zinazofanyika ndani yake ni shughuli za Ibada na sala tu!.

Ndio maana Roho Mtakatifu anazidi kusisitiza jambo hilo hilo kwa kinywa cha Mtume Paulo na kusema…

1Wakorintho 3: 16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa HEKALU LA MUNGU, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Kama pia ni mfuatiliaji wa maandiko utagundua kuwa Hekalu ni tofauti na Sinagogi, Sinagogi ni mahali palipokuwa pameandaliwa na wayahudi wa zamani kwa ajili ya kujifunza sheria na torati, kwasasa tunaweza tukasema ni mahali kama kanisani. Na haya masinagogi yalikuwepo mengi, sehemu kadha wa kadha katika Israeli, Lakini Hekalu lilikuwa ni moja tu! duniani, na hekalu Lilikuwa na sehemu na sehemu kuu tatu 1) UA WA NDANI, 2) PATAKATIFU na 3) PATAKATIFU PA PATAKATIFU.

Kwa lugha nyepesi UA wa ndani ni UANI, Tengeneza picha nyumba yenye uzio wa ukuta, NA Ina sebule na chumba kimoja,sasa kule uani, ndipo palipoitwa UA WA NDANI katika Hekalu la Mungu, na sehemu ya pili paliitwa PATAKATIFU…Sehemu hii kwa sasa tunaweza tukapaita SEBULENI, na sehemu ya tatu na ya mwisho paliitwa PATAKATIFU PA PATAKATIFU..kwasasa tunaweza kusema ni kile chumba cha ndani cha MASTER.

Sasa Bwana aliagiza sehemu zote hizi zinapaswa ziwe safi. Kusiwepo mtu yoyote wa kulitia unajisi HEKALU LA MUNGU. Na sio kila mtu aliyekuwa na ruhusa ya kuingia ndani ya hekalu la Mungu, isipokuwa makuhani peke yao wana wa Lawi.. Lakini sehemu nyingine kama kwenye masinagogi watu wote walikuwa wanaruhusiwa kuingia kusali na kujifunza torati.

Sasa kama biblia inasema sisi ni Hekalu la Roho Mtakatifu basi ni wazi kuwa ndani yetu kuna sehemu kuu tatu ambazo zinapaswa ziwe takatifu sana.

Sehemu ya kwanza ni Miili yetu kwa nje(ambayo inafananishwa na ule UA WA NDANI), Sehemu ya pili ni ndani ya miili yetu ambapo kuna Nafsi (panapofananishwa na PATAKATIFU) Na sehemu ya tatu ni ndani kabisa mwa vyumbwa vya roho zetu (ambapo ndipo PATAKATIFU PA PATAKATIFU). Sehemu zote hizi tatu zinapaswa ziwe takatifu. 

Bwana Yesu alipofika Yerusalemu, alikuta watu wanauza njiwa, na kufanya biashara kwenye Hekalu la Mungu, na ndipo Hasira ya kimungu ikawaka ndani yake.. na kuanza kuangusha kila kitu ndani ya Hekalu na kusema maneno haya… “Imeandikwa, NYUMBA YANGU ITAITWA NYUMBA YA SALA; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.Mathayo 21:13”

Unaona hapo, sio kwamba hakukutana na watu katika masinagogi mengine mbali mbali waliokuwa wanafanya biashara, alikutana nao wengi hata alipokuwa Nazareti lakini hakuchukizwa nao sana kama alivyochukizwa na wale waliokuwa wanafanya biashara katika HEKALU TEULE MOJA TU LA MUNGU MWENYEZI lililokuwa Yerusalemu…

Kumbuka hawa wafanya biashara hawakuwa wanafanya biashara ndani kule PATAKATIFU PA PATAKATIFU. Hapana! Walikuwa wanafanya biashara zao maeneo ya UA WA NJE, ndani wasingeweza kufika kwasababu ni kuhani mkuu tu! peke yake ndiye aliyekuwa anaingia kule.

Sasa hayo yana maana gani? Tunapokuwa tumeokoka, na Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu, moja kwa moja, miili yetu inabadilishwa na kuwa Hekalu la Mungu, kumbuka sio kila mtu ni hekalu la Mungu, hapana! Bali ni wale tu waliompa Bwana Yesu maisha yao, hao ndio miili yao inafanyika Hekalu la Roho Mtakatifu. Wengine ambao hawajampa, miili yao sio hekalu la Mungu kwasababu ndani yao hawana Roho Mtakatifu, wana roho nyingine…Hivyo miili yao ni mahekalu ya hizo roho nyingine ambazo ni za mashetani.

Kwasababu hiyo basi, tunaweza kufahamu kuwa MIILI YETU, na NAFSI ZETU na ROHO ZETU zinapaswa ziwe katika hali ya USAFI kila wakati kwasababu, NDIVYO VIUNGO VITATU vinavyounda Hekalu la Roho Mtakatifu. 

1Wathesalonike 5: 23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.

Unaona hapo, usafi unaanza Nje ya Mwili, kisha kwenye Nafsi ya mtu, na mwisho unaishia ndani katika roho ya Mtu.

Sasa hebu tujifunze kidogo usafi wa nje wa mwili unaohitajika ni upi? 

Inaaminika na wengi kuwa “Mungu huwa haangalii mwili na badala yake anaangalia roho tu” Nataka nikuambie kwa upendo kabisa ndugu yangu unayesoma haya, Mungu haangalii mwili, au nafsi yako, wala roho yako, Mungu anaangalia Hekalu lake kwa ujumla. Na hekalu lake ndio limeundwa na hivyo vitu vitatu mwili, nafsi na roho.

Kumbuka tena waliokuwa wanafanya biashara katika Hekalu la Mungu, ambao Bwana Yesu aliwafukuza walikuwa hawafanyi biashara hizo ndani ya patakatifu, au patakatifu pa patakatifu, hapana! Walikuwa wanafanya karibu na UA WA NDANI. Na jambo hilo bado lilimchukiza sana Bwana.. 

Na kadhalika leo, jambo lile lile Biashara inapofanyika katika UA WA NDANI (juu ya mwili), jambo hilo ni baya sana na linamchukiza Mungu, kuliko mambo mengine yote!! Na jambo hilo linaweza kumsababishia mtu hata mauti ya kimwili. Yafuatayo makuu mawili yasiyotakiwa kabisa kufanyika juu ya Hekalu la Mungu.

1 ) UASHERATI

Uasherati ndio jambo la kwanza kabisa linaloweza kumwangamiza mtu anayesema amempa Bwana maisha yake, Na uasherati/uzinzi ndio dhambi ya kwanza inayoliharibu Hekalu la Roho Mtakatifu..Mtu mzinifu na bado anasema ameokoka..anafanya dhambi mbaya kuliko hata mtu mwuaji ambaye hajampa Bwana maisha yake.

* 1 Wakorintho 6:17 “Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
18 IKIMBIENI ZINAA. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.

* Mithali 6: 32 “Mtu aziniye na mwanamke HANA AKILI KABISA; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”.

Nangependa nikukumbushe kitu kimoja mwana wa Mungu, Hasira ya Mungu haiji kwanza kutokana na maovu ya watu wasiomwamini, hapana! Ghadhabu ya Mungu duniani inaletwa kwanza kutokana na maovu ya watu wanaomwamini…Kumbuka gharika ya kwanza ilikuja kwasababu gani? “Ni kwasababu wana wa Mungu waliwatamani binti za Binadamu” yaani Watoto wa Mungu waliwatamani binti wa ulimwengu huu, ndipo ghadhabu ya Mungu ilipopanda.

Na kadhalika katika siku hizi za mwisho, watu wengi wanaosema wameokoka lakini ni vuguvugu ndio watakaochangia pakubwa kuivuta ghadhabu ya Mungu duniani…Ukisoma pia biblia agano la kale utaona, Bwana Mungu alikuwa akichukizwa na maovu ya wana wa Israeli, sio kwamba wana wa Israeli ndio waliokuwa watu waovu kuliko wote duniani, hapana ni kwasababu wao ndio waliokuwa wana wa Mungu. Hivyo maovu wanayoyafanya wao yanaonekana sana machoni pa Mungu, kuliko watu wa mataifa.

Shetani anachofanya katika siku hizi za mwisho, ni kuwadanganya watu wanaosema wamempa Bwana maisha yao, wakike na kiume kujiingiza katika mahusiano..kwa kisingizio kwamba watakuja kuoana wakati Fulani mbeleni, hivyo wanaingia katika dhambi ya uasherati, pasipo kujua njama za shetani.

Kaka/Dada..usidanganyike, uashetari kabla ya ndoa, ni sawa na kujiwekea kitanzi mwenyewe shingoni na kwenda kujiua. Ni sawa na ndege anayeenda mtegoni peke yake biblia inasema hivyo katika (Mithali 7:23-27). 

Biblia inasema pia “unafanya jambo litakalokuangamiza nafsi yako”. Bwana hawezi kuridhia huo uovu juu ya Hekalu lake, ambalo lingepaswa kuwa Takatifu, na sehemu ya sala. Ni heri uwe umeamua kuwa mtu wa ulimwengu kuliko kusema umeokolewa na YESU KRISTO halafu unafanya uasherati. Ni hatari sana.

2 ) Jambo la Pili ni MAPAMBO

Mapambo yoyote ambayo yanaweza kuning’inizwa juu ya mwili wa mtu, ni machukizo mbele makubwa mbele za Mungu, Wengi hawapendi kusikia haya lakini ni afadhali usikie leo hii ubadilike, ili siku ile usije ukasema “mbona sikupata mtu aliyeniambia ukweli”.

Nataka nikuambie UKWELI ndugu/Dada yoyote unayevaa wigi, au unayevaa herein au unayevaa nguo fupi (yaani vimini, pamoja na suruali kwa wadada)..au unayevaa mambo yoyote ambayo hujui maana yake, na bado umesema umempa Bwana maisha yako..kama unafanya hayo pasipo kujua, leo hii nakuambia ukweli yaache mambo hayo yanapeleka mamilioni kuzimu. Mwili wako tangu ulipompa Bwana maisha yako ulifanyika Hekalu lake, sio nyumba yake…zingatia hilo Neno HEKALU!!

Utauliza kuvaa herein kuna shida gani? Historia ya kutobolewa masikio ipo kwenye biblia..Katika agano la kale kitabu cha kutoka Mlango wa 21 tunasoma..

“1 Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi

2 Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.

3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye.

4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.

5 Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru;

6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake ATALITOBOA SIKIO LAKE KWA UMA; NDIPO ATAMTUMIKIA SIKUZOTE.”

Unaona hapo? Mtumwa aliyekataa uhuru ndiye aliyetoboliwa sikio? Ishara kwamba amekataa kupewa uhuru..kwahiyo leo hii mtu yoyote awe mwanaume au mwanamke anayetobolewa masikio katika roho ni “mtumwa aliyekataa uhuru” na uhuru tunaopewa leo ni uhuru wa dhambi, kwahiyo mtu anayetoboa masikio na kuweka hereni ni ishara ya mtumwa aliyekataa kuwekwa huru mbali na dhambi na Bwana wake.

Ndugu au dada unayetoboa masikio na kuvaa hereni, jiepushe na hayo mambo…pengine ulifanya pasipo kujua, tubu tu na ujirekebishe kwasababu ulikuwa hujui..huwezi kuziba lile tundu kwenye sikio lakini acha kuvaa hizo hereni kwasababu ukifanya hivyo unakuwa unatilia muhuri lile agano la kukataa uhuru.

Kadhalika pia uvaaji wa WIGI na upakaji wa UWANJA pia upo katika biblia.. Ukisoma kitabu cha 2 Wafalme 9: 30 “Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; AKATIA UWANJA MACHONI MWAKE, AKAPAMBA KICHWA CHAKE, akachungulia dirishani”.

Huyu mwanamke Yezebeli ndiye mwanamke pekee katika maandiko aliyekuwa anapaka uwanja, hakukuwa na mwanamke yoyote aliyekuwa anapaka wanja katika Israeli, sasa huyu Yezebeli alikuwa ni mke wa Mfalme Ahabu, asili yake hakuwa mwisraeli bali alikuwa ni mwenyeji wa nchi inayojulikana leo kama Lebanoni. Huyu mwanamke hakuwa anamwabudu Mungu wa Israeli, bali alikuwa anamwabudu Baali miungu ya kipagani.

Mfalme Ahabu alipomtoa katika hiyo nchi ya Lebanoni, alikuja Israeli na manabii wake wa kipagani (manabii wa Baali) kumsaidia kufanya shughuli zake za kuabudu miungu, mwanamke huyu Biblia inasema alikuwa ni MCHAWI !!! Na hivyo uchawi wake ulizidi mpaka kwenye mwili wake, alikuwa anapaka UWANJA kama desturi ya miungu yao, kuongeza nguvu zake za kiroho.

Mwanamke huyu ndiye aliyewakosesha sana Israeli na kuwafundisha baadhi ya waisraeli kushiriki ibada za sanamu, ndiye aliyemsumbua sana nabii ELIYA, Na alikuwa mkatili sana,kwa ufupi alileta machafuko makubwa sana Israeli. Na roho yake utakuja kuona inatajwa tena katika kitabu cha ufunuo. 

Ufunuo 2: 20 “Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia YULE MWANAMKE YEZEBELI, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake”.

Kwahiyo nataka uone dada roho iliyopo ndani ya hayo mapambo(wanja,wigi na hereni)..wanawake wachawi wa kimataifa ndio waliokuwa wanafanya hivyo ili kuchochea nguvu za giza ndani yao, ni sawa sasahivi wachawi wanavyovaa hirizi viunoni, kujichanja chale,na kujichora na machaki usoni na kutembea uchi miaka Fulani mbeleni ije kuwa fashioni watu wote wafanye hivyo…hicho ndicho kilichotokea kwa wigi na uwanja, na uchoraji wa tatoo zamani wachawi ndio waliokuwa wanafanya lakini nyakati hizi ni watu wanaojiita watu wa Mungu…Uchoraji wa Tatoo zilikuwa zinafanyika kwenye ibada za wafu na zilikuwa ni desturi za kipagani..

Walawi 19: 28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, WALA MSIANDIKE ALAMA MIILINI MWENU; mimi ndimi Bwana”.

Kwahiyo dada au kaka unayesoma ujumbe huu, fahamu kuwa tangu siku ulipompa Bwana maisha yake, Roho Mtakatifu alikugeuza wewe kuwa Hekalu lake takatifu, usiliharibu ili naye asikuharibu. Kama ulikuwa unafanya hayo pasipo kujua, Mungu ni mwenye huruma, leo hii umeujua ukweli ukitubu kwa kusudia kutokufanya hayo tena yeye ni mwamini atakusamehe kulingana na Neno lake, tupa leo hizo suruali ulizokuwa unavaa, tupa leo hizo wigi, na hereni ulizokuwa unavaa, acha kupaka uwanjua na lipstick…weka nywele zako katika uhalisia wake, zitunze tu, na la muhimu kabisa Acha uasherati. Usitamkwe kabisa! Litakase Hekalu la Mungu.

Bwana akubariki, na kama hujampa Bwana maisha yako, ni vyema ukafanya hivyo leo, angali mlango wa Neema haujafungwa, mgeukie yeye kwamaana biblia inasema “mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijakaribia siku zilizo mbaya”.

Bwana akusaidie katika hilo na aikamilishe safari njema aliyoianza moyoni mwako.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki.


Mada Nyinginezo:

YEZEBELI

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?

JE! UNAMPENDA BWANA?

KITENDAWILI CHA SAMSONI

SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.


Rudi Nyumbani

Print this post

MARIAMU

Inaaminiwa na wengi wetu kuwa Mariamu, mama, aliyemzaa Bwana wetu Yesu Kristo, alikuwa ni mwanamke wa kipekee sana, na aliyebarikiwa zaidi ya wanawake wengine wote, na kabla hajapata Neema ya kumzaa Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa ni mtu mkuu sana, na anayependwa sana na aliyeheshimika sana…Lakini je! ni kweli maandiko yanasema hivyo?

Tukisoma maandiko kitabu cha Luka 1: 1.42 inasema  “akapaza sauti kwa nguvu akasema, UMEBARIKIWA WEWE KATIKA WANAWAKE, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa”.

Maneno hayo yalizungumzwa na Elizabeth, mama yake Yohana Mbatizaji baada ya kukutana na Mariamu, Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu akambariki na kumwambia UMEBARIKIWA WEWE KATIKA WANAWAKE.

Sasa jambo la muhimu la kuzingatia hapo ni hilo neno “KATIKA” Hakusema “kuliko wanawake wote” hapana bali “katika

Ikiwa na maana kuwa katika wanawake waliobarikiwa na yeye (Mariamu) ni mmoja wapo..na sio kwamba yeye kabarikiwa kuliko wote..

Wakati Fulani mwanamke mmoja alimtaja Mariamu kuwa kabarikiwa sana, mbele ya umati mkubwa wa watu na mbele ya Bwana Yesu, lakini Bwana alimrekebisha pale pale na kumwambia HERI walisikiao Neno la Mungu na kulishika..

Sasa maana ya neno heri ni  amebarikiwa yeye

Luka 11:27 “Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri {limebarikiwa} tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema, Afadhali, heri{wamebarikiwa} walisikiao neno la Mungu na kulishika”.

Kwa lugha nyepesi katika mstari huo tunaweza kusema “…Mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake akamwambia; amebarikiwa mwanamke Mariamu aliyekuzaa, lakini Bwana akasema amebarikiwa zaidi mwanamke Yule alisikiaye Neno la Mungu na kulishika”

Kwahiyo unaweza ukaona hapo ingekuwa Mariamu amebarikiwa kuliko wanawake wote, Bwana Yesu asingemkosoa huyu mwanamke aliyekuja Kumtangaza Mariamu hadharani kuwa ni mbarikiwa.

Na pia kumbuka Bwana  Yesu hakutabiriwa kutokea katika ukoo wa Mariamu, bali ukoo wa Yusufu Mumewe Mariamu..ndio maana ukisoma pale mwanzo wa kitabu cha Mathayo utaona ukoo wa Bwana Yesu Ulianzia kwa Ibrahimu na ukaishia kwa Yusufu mumewe Mariamu, na haukuanzia kwa Ibrahimu na kuishia kwa wazazi wake Mariamu. Hivyo unaweza ukaona ni neema tu Mariamu kumzaa Bwana.

Kwahiyo ni muhimu kufahamu hilo ili tusije tukamwona Mtu Fulani ni wa kipekee sana katika maandiko zaidi ya mwingine, Imefikia wakati watu wanamaabudu Marimu, bila hata hofu ya Mungu, mwanamuhisisha katika ibada zao na kumtolea shukrani kana kwamba yeye ni Kristo. Hata Nabii Eliya biblia inatuambia alikuwa ni mtu mwenye tabia moja na sisi (Yakobo 5:17). Mfano kama  biblia isingeandika vile leo hii si ajabu tungewaona watu wamemfanya leo kuwa ni mtu wa nne katika uungu wa  Mungu.

Ni YESU KRISTO,  peke yake aliye Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana ndiye aliyekuwa wa kipekee zaidi ya wengine wote duniani…

Sasa tukirudi kwenye kiini cha somo ambacho tutaona  ni jambo gani lililomfanya Mariamu, apate neema ya kumzaa Mwokozi wa Ulimwengu Yesu Kristo.

Awali ya yote Biblia takatifu haijaelezea maisha ya nyuma ya Mariamu kabla ya kumzaa  Bwana wetu Yesu Kristo..Lakini tukiyachunguza maandiko  kwa undani tunaweza tukapata dondoo chache za maisha yake ya nyuma jinsi yalivyokuwa..

Sasa kabla ya kumsoma Mariamu hebu tuwasome kidogo Wanawake wachache kwenye maandiko waliopewa neema ya kuzaa baadhi ya MASHUJAA..

Tukianza na mwanamke wa Kwanza wakati wa kipindi cha Waamuzi, aliyekuwa (Mke wa mtu mmoja aliyeitwa Manoa) Tunasoma hivi..

Waamuzi 13: 2 “Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; NA MKEWE ALIKUWA TASA, hakuzaa watoto.

3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini UTACHUKUA MIMBA, NAWE UTAMZAA MTOTO MWANAMUME.

4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;

5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti”.

Mwanamke huyu ndiye aliyemzaa shujaa Samsoni…Sasa ukiyachunguza kwa makini maisha yake utagundua alikuwa ni Mwanamke aliyekuwa MNYONGE kwa sababu alikuwa tasa..wakati  wanawake wengine wana watoto yeye hakuwa na mtoto hata mmoja na umri wake umeshakwenda…Na inaelekea alikuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu akimwomba Mungu usiku na mchana, na pengine alimwekea nadhiri Bwana kwamba endapo atapata mtoto wa kiume atampatia Bwana kama sadaka.  Hivyo aliendelea kubakia katika hali hiyo hiyo paka siku malaika wa Bwana alipomtokea na kumwambia atazaa mtoto wa kiume (Samsoni) ambaye atawaokoa watu wake Israeli na maadui zao. Huyu Samsoni biblia inasema alikuwa ni Mnadhiri wa Bwana tangu tumboni mwa mama yake.

Tukirudi tena kwenye maandiko tunamwona mwanamke mwingine aliyezaa Shujaa..Na huyu si mwingine zaidi ya Hana mke wa Helkana. Huyu naye hakuwa na mtoto kwa muda mrefu na zaidi ya yote, mke mwenza alikuwa akimtesa na kumchokoza mara kwa mara kutokana na hali yake ya utasa..Hivyo kwasababu ni mcha Mungu na alikuwa mwenye haki alimwekea Bwana nadhiri kwamba endapo atapata Mtoto wa kiume atamweka wakfu kwa Bwana maisha yake yote…na Bwana alimkumbuka akampa Neema ya kumzaa Nabii Samweli, aliyekuja kuwa nabii mkubwa sana Israeli na Mwamuzi. Na hivyo Bwana akautoa UNYONGE wake akampatia Faraja yake dhidi ya dhiki na mateso aliyokuwa anayapitia kwa muda mrefu.

Hivyo Hana alifurahi sana mpaka akazungumza maneno haya..

1 Samweli 2: 1 “Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;

2 Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.

2 Samwli 2:3 “Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.

4 Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.

5 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.

6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.

7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.

8 HUMWINUA MNYONGE KUTOKA MAVUMBINI, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake”.

Ukisoma mstari wa 8 unasema “HUMWINUA MNYONGE KUTOKA MAVUMBINI Ikifunua kuwa hapo kwanza Hana alikuwa mnyonge lakini Bwana alimwinua kutoka mavumbini, alikuwa chini na sasa  Bwana kamwinua juu sana..alikuwa hana mtoto lakini sasa kamzaa shujaa Samweli n.k

Tukimtazama mwanamke wa Mwisho katika maandiko ambaye naye pia alizaa Shujaa…alikuwa ni Elizabethi aliyekuwa ndugu yake Mariamu. Huyu Elizabeth naye alikuwa ni Tasa, hakuwa na Mtoto mpaka alipokuwa mzee, yeye pamoja na Mume wake Zakaria walikuwa ni wacha Mungu.. Na zaidi ya yote mume wake alikuwa ni Kuhani hivyo walikuwa wakiomba dua usiku na mchana kuhusu hali yao..Siku moja malaika alimtoke Zakaria na kumwambia mkewe aliye Tasa atachukua Mimba, na atazaa mtoto ambaye atawarejesha wengi kwa Bwana.. Na huyu mtoto tunakuja kumwona si mwingine zaidi ya YOHANA MBATIZAJI, ambaye alitabiriwa kuja kwa roho ya Eliya..Shujaa wa Bwana aliyetabiriwa kuitengeneza njia ya Bwana. Habari yake inapatikana katika (Luka mlango wa kwanza wote).

Sasa tabia za wanawake wote hawa watatu,: Yaani Mke wa Manoa, Hana, pamoja na Elizabethi utaona kuwa walikuwa ni wanawake wanyonge na wacha Mungu, na watulivu, na waliodharaulika… Hakuna hata mmoja aliyekuwa na heshima katika jamii ya watu wake wanaowazunguka, walikuwa ni wanawake wasio na uzao, kwa mfano Hana, hakuwa na watoto lakini bado alikuwa anamcha Mungu, alikuwa hakosi zamu za kwenda kuabudu Yerusalemu…Hivyo kwa mienendo yao inayompendeza Bwana na ya utulivu, na ya kusubiri kwa muda mrefu, Bwana akawapa neema ya Kuzaa MASHUJAA..

Na sio hao tu, tazama maisha ya Sara ambaye alikuwa mgumba kwa miaka mingi, mwanamke aliyemcha Mungu na mume wake mpaka kufikia hatua ya kumwita mumewe bwana. Mwanamke aliyedharauliwa na wanawake wengine wote lakini yeye ndiye alikuyekuja kumzaa Isaka. Vivyo hivyo tunaowaona akina Rebeka mambo yale yale, Raheli ambaye alikuja kumzaa Yusufu, mambo yale yale n.k.

Sasa mpaka hapo tumeshaanza kupata picha ya MWANAMKE MARIAMU jinsi alivyokuwa naye alikuwa ni mwanamke wa dizaini gani?? Kwa kuwasoma maisha ya hao wanawake watatu waliotangulia unaweza ukapata picha kuwa Mariamu naye sio kwamba alikuwa ni mwanamke aliyekuwa na kila kitu, au aliyekuwa na heshima…Hapana! Utaona tabia yake na maisha yake ni lazima itakuwa yanafanana na hao wanawake watatu waliomtangulia… Inawezekana yeye hakuwa Tasa kwasababu alikuwa ni Bikira lakini alikuwa ni mjonge mahali Fulani.. alikuwa ni mwanamke aliyedharaulika…pengine familia yao ilikuwa inajulikana ni duni tu, na pengine ilikuwa haina jina…Pengine wabinti wenzake walikuwa wanafanikiwa na kuzaa watoto wenye sifa, yeye alijitunza tu! Alikuwa anachekwa kama Hana, alikuwa ni mdhaifu, na alikuwa hana umaarufu wowote, pengine alikuwa hana uzuri sana wa kuvutia kama mmojawapo ya wanawake wa kidunia waliokuwepo kipindi kile, lakini alikuwa mcha Mungu…

Lakini ulipofika wakati. Bwana akautazama unyonge wake..akamkirimia kumzaa SHUJAA WA MASHUJAA, na MFALME WA WAFALME haleluya!! Malaika wa Bwana akatumwa kama alivyotumwa kwa mke wa Manoa, akatumwa kama alivyotumwa kwa Zekaria Mume wa Elizabethi, akaambiwa atachukua mimba kwa uwezo wa Roho na kumzaa Bwana Yesu. Hivyo Bwana akawa amemwondolea unyonge wake, na yeye akajihisi ni mwanamke kati ya wanawake waliobarikiwa..ndio maana utakuja kuona akisema…

Luka 1: 46 “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;

48 Kwa kuwa ameutazama UNYONGE WA MJAKAZI WAKE. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;

49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu.

50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.

51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

52 Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; NA WANYONGE AMEWAKWEZA.

53 WENYE NJAA AMEWASHIBISHA MEMA, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu”.

Unaona anasema hapo “wanyonge amewakweza” ikiwa na maana kuwa hapo kwanza naye pia alikuwa mnyonge.

Ni jambo gani la kujifunza kwa Mariamu na wanawake hawa wengine?

Katika hali zao za Unyonge walimngojea Bwana na kumtumainia kwa saburi, na pili walijua Bwana ndiye anayeshusha na ndiye anayepandisha…Walipoona tabu nje! Bwana ndiye aliyekuwa kimbilio lao, Hana hakuzunguka kwa wapunga pepo kupata utatuzi wa tatizo lake, wala Elizabethi hakuwatafuta waganga wamtatulie tatizo lake la kukosa mtoto, walijua ni Bwana ndiye aliyewafunga matumbo yao na ipo siku yatafunguka..hivyo waliendelea kukaa katika njia zake..

Hakuna hata mmoja unaona akimlaumu Mungu katika hali yake ya unyonge aliyokuwa anapitia, wote walikuwa katika hali ya utulivu mpaka ulipofikia wakati wa Ahadi zao kutimia wote walizaa mashujaa..Ukimsoma pia Sara na Rebeka na Raheli na Ruthu aliyekuwa bibi yake Daudi..utaona jambo hilo hilo, wote walikuwa ni wanawake wavumilvu na hawakuiacha njia yao ya haki na mwisho wakazaa mashujaa.

Hivyo Dada/Kaka unayesoma ujumbe huu, ukitaka kuzaa Shujaa katika maisha yako epuka manunguniko, epuka njia za mkato, kubali kudharauliwa na kuwa mnyonge, kubali kuonekana sasa wewe ni mshamba katika Kristo,kubali kuonekana tasa usiyeweza kufanya chochote maadamu unamcha Mungu usiogope. kwasababu utafika wakati Bwana atalikumbuka teso la kijakazi wake kama Mariamu alivyosema.

Unapokosa kitu sasa usiwalaani waliokuwa nacho, wabariki,ukikosa mtoto sasa usiwalaani wanaokulaani, usizunguke kwa waganga, wala usiuache UTAKATIFU wako, ishi maisha yanayompendeza Mungu kila siku,ukijiepusha na mambo yote mabaya ya ulimwengu, kwasababu Mungu anao wakati wake na majira yake, na ukifika wakati Bwana atakufurahisha kama alivyomfurahisha Mariamu , atautoa unyonge wako kama alivyoutoa wa Mariamu na wengine.

Isaya 54: 1 “Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana”.

Bwana akubariki.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.


Mada Nyinginezo:

MIRIAMU NI NANI

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.


Rudi Nyumbani

Print this post

UHURU WA ROHO.

Kama tunavyosoma biblia baada ya wana wa Israeli kuingia katika nchi ya Ahadi, hawakuwa na Mfalme, kila mtu alifanya jambo aliloliona ni jema machoni pake, ndivyo Biblia inavyosema katika…

Waamuzi 17: 6 “Siku hizo hapakuwa na mfalme katika israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe”.

Lakini tunasoma pamoja na kuwa hawakuwa na Mfalme wala serikali yoyote inayotawala juu yao, waliishi kwa amani na Furaha, hakukuwa na mtu aliyemtawala mwenzake, wala aliyekuwa juu ya mwenzake, wote walikuwa sawa. Na walikaa katika hali hiyo kwa mamia ya miaka kwasababu ndivyo Bwana Mungu alivyopenda waishi katika hali hiyo, kwamba asiwepo aliye mkuu zaidi ya mwingine, yeye Bwana ndiye atakayekuwa Mkuu kwao na Mfalme wao.

Unaweza ukajiuliza leo hii mfano Taifa lisiwe na Raisi, wala mawaziri, wala serikali ya uongozi, litakuwaje!! kwamba kila mtu anafanya kile akionacho kuwa ni chema machoni pake, Ni wazi kuwa Taifa la namna haliwezi kusimama, ni taifa litakalo jaa vurugu, mauaji, dhuluma, uonevu, ubeberu, na mambo mengine mabaya yataonekana tu, kwasababu hakuna viongozi juu yao..

Lakini haikuwa hivyo kwa Wana wa Israeli, baada ya kutoka Misri, hawakuwa na Mfalme wala Raisi, wala mawaziri, lakini walikaa kwa utulivu na kwa utaratibu.. Kwasababu Mungu mwenyewe alikuwa katikati yao kama Roho Mtakatifu (Mfalme wao asiyeonekana kwa Macho). Akiwaamua na kuwaongoza katika utulivu na uhuru..kwa namna isiyoweza kuelezeka na kuchunguzika Ndio maana biblia inasema katika…

2 Wakoritho 3:17 Basi “BWANA” ndiye Roho; walakini ALIPO ROHO WA BWANA, hapo ndipo PENYE UHURU.”

Nataka uone hapo maandiko yanaposema kuwa “BWANA NDIYE ROHO”…Ikimaanisha kuwa Roho Mtakatifu ndiye Bwana Yule Yule, sio nafsi nyingine ya tatu hapana ni Yule Yule Bwana..Hata katika hali ya kawaida huwezi kumtenganisha mtu na Roho yake, wewe na Roho yako ni kitu kimoja, Roho yako sio nafsi yako ya tatu hapana! Roho yako ni wewe mwenyewe! Ndio maana na hapa maandiko yanasema “BWANA NDIYE ROHO” Na hakuna mahali popote katika maandiko matakatifu yamemtaja kuwa Mungu ana nafsi tatu. Hapana Mungu ni mmoja ana nafsi moja na Roho yake ni moja..Ndio maana na sisi wanadamu hatuna nafsi tatu, bali tuna nafsi moja, na Roho moja na mwili mmoja kwasababu katuumba kwa mfano wake na sura yeke yeye mwenyewe mwenye nafsi moja na Roho moja na mwili mmoja.

Sasa Kumbuka “BWANA NDIYE ROHO”… Roho Mtakatifu ndiye Yule Yule Yesu Kristo akifanya kazi katika Roho,..alipokuwa hapa duniani alikuwa anafanya kazi katika mwili, lakini ili kwamba ajiletee faida kubwa zaidi ilimpasa aondoke ili aje tena katika roho..ndio maana utaona alisema “bado kitambo kidogo hamnioni na tena bado kitambo kidogo mtaniona”, akimaanisha kuwa atakuja tena kwetu kwa njia nyingine bora zaidi itakayomfanya aingie ndani yetu, na ndio hiyo njia ya Roho, ambayo ndio ukamilifu wake kwetu sisi .

Na tukisoma pia kitabu cha Ufunuo mlango wa pili na wa tatu, tunaona Bwana Yesu Kristo akitoa ujumbe kwa Yale makanisa saba, Lakini mwanzo wa kila kanisa utaona anajitambulisha kuwa ni Bwana Yesu ndiye anayezungumza maneno yale lakini mwisho wa ujumbe utaona anasema “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”.. Hebu tuchukue mfano wa kanisa moja la Thiatira.

Mwanzoni mwa ujumbe anasema Ufunuo 2:18-19 “Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu,[YESU KRISTO] yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.”..

Sasa huyu ni Bwana Yesu ndiye anayeyazungumza maneno hayo, lakini mwishoni mwa Barua hatuoni akimalizia kama alivyoanza, kwamba badala ya kusema “mwenye masikio na asikie neno hili ambalo Mwana wa Mungu anayaambia makanisa” badala yake anasema “mwenye masikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.. Kwahiyo ni dhahiri kuwa “BWANA NDIYE ROHO” kama MTUME PAULO alivyosema.Hivyo ni muhimu kufahamu haya, ili kujiwekea vizuri msingi wa kumwelewa Bwana wetu Yesu Kristo na uweza wake, na utendaji kazi wake sasa katikati ya kanisa.

Lakini tukiendelea kwenye kile kipengele cha pili cha ule mstari kinachosema ““BWANA” ndiye Roho; walakini ALIPO ROHO WA BWANA, hapo ndipo PENYE UHURU.”

Nataka tukiangalie hicho kipengele kinachosema “ALIPO ROHO WA BWANA HAPO NDIPO PENYE UHURU”

Kwa kulinganisha na habari ile ya wana wa Israeli baada ya kutoka Misri, tunaona Bwana hakuwaweka chini ya Utumwa mwingine walipoingia kaanani, hakuwaweka tena chini ya wafalme kama farao, wala chini ya majemedari, wala hakuruhusu tena warudie maisha ya kiutumwa katika nchi ya Ahadi waliyokuwa wanaiendea. Bwana alikuwa Mfalme wao wa Amani, alikuwa katikati yao kama Roho. Akiwaweka katika utulivu, na uhuru wa hali ya juu. Bwana aliwalinda na roho mbaya za ugomvi, mateso, chuki, visasi, ubeberu, na maadui wote, fitina, dhiki, mashindano, ubinafsi…waliishi wote kama ndugu wa familia moja, na mataifa yote duniani yaliwaogopa kwa umoja huo uliokuwa katikati yao,..

Bwana aliwalinda kwa ile Hekima ya NZIGE, kama Mfalme Sulemani alivyoizungumza katika Mithali zake..Akisema nzige ni wadudu walio na akili nyingi sana.

Mithali 30: 27 “NZIGE HAWANA MFALME; Lakini huenda wote pamoja VIKOSI VIKOSI”.

Bwana aliwapa uhuru wa hali ya juu, kiasi kwamba kila mtu aliweza kufanya alilolitaka. Kulikuwa hakuna Taifa lingine duniani lililojiendesha bila mfalme, mataifa yote ya ulimwengu yalilishangaa Taifa la Israeli lenye mamilioni ya watu kipindi hicho linajiendesha pasipo mfalme na bado linafanikiwa kuliko mataifa yote, linapigana na maadui zake na kuwashinda.

Lakini tunaona maandiko yanasema baada ya miaka mingi kupita, kikainuka kizazi kingine ambacho hakikuutaka uhuru ule Bwana aliowapa na badala yake wakataka kuwa na Mfalme kama mataifa mengine, Na kwasababu walilisisitiza hilo jambo kwa nguvu Bwana akawapa haja ya mioyo yao, lakini hawakujua kuwa wamemkataa Bwana mwenyewe ambaye alikuwa katikati yao kama Roho awapaye uhuru, amani, furaha,upendo, raha na heri katika ile nchi ya Ahadi, wao wakataka uongozi wa kibinadamu…Japo Bwana aliwaonya kuwa mfalme watakayemchagua atatwaa binti zao na kuwafanya wajakazi wake, atatwaa mali zao na kuzifanya zake, atawalipisha kodi na atawashurutisha waishi kama wanavyotaka wao, lakini wao bado walimkataa Roho mtakatifu na kutaka uongozo wa wanadamu.

1Samweli 8:1-22

“1 Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.

2 Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.

3 Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.

4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;

5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.

6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.

7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.

8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.

9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.

10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana.

11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.

12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.

13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.

14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.

15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.

16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe”.

17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake.

18 NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE.

19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;

20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu.

21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana.

22 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake”.

Mstari wa 18 unasema ..“NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE.

Unaona hapo?. Baada ya Israeli kujitwalia mfalme ndio ulikuwa mwanzo wa matatizo kwa taifa lile, tunakuja kusoma baadaye hao hao wafalme ndio waliokuwa wakwanza kuweka vinyago tena Israeli kama walivyokuwa kule Misri. Israeli ikaanza kudhoofika kidogo kidogo mpaka kufikia hatua ya Mungu kuchukizwa nao kwa sanamu zao na kutawanywa katika mataifa yote ulimwenguni.

Mambo hayo ni kivuli cha mambo yanayoendelea sasa, Mfalme wetu ni YESU KRISTO, ambaye hapo kwanza alikuja katika mwili, akatufundisha katika mwili, lakini sasa yupo katikati yetu katika ROHO anatuonya katika roho, anatuita kutoka katika utumwa wa dhambi na kutuingiza katika Uhuru wa Roho. Kwasababu BWANA NDIYE ROHO, na alipo Roho hapo ndipo penye uhuru.

Na kanisa leo limetoka katika kutawaliwa na ROHO MTAKATIFU na kuzama katika utawala wa kibinadamu, Sio Roho tena anaamua bali ni mitazamo ya wanadamu, sio tena karama za Roho zinazoongoza kanisa bali ni vyeo vinavyoongoza kanisa, kiasi kwamba ukiwa mchungaji mkuu, au kasisi, au padre, papa au shemasi, au askofu basi wewe unaweza ukasimama badala ya YESU KRISTO DUNIANI, Unaweza ukasamehe dhambi, unaweza ukawabariki watu katika dhambi zao, n.k..ndio maana hakuna, uhuru, umoja,wala amani, wala usafi,wala utakatifu ndani ya kanisa, kwasababu Kristo katupwa nje! Haiwezekani kupaa kama nzige, wakati kuna uongozi mwingine zaidi ya ROHO MTAKATIFU, Wana wa Israeli baada ya kumkataa Bwana kama Mfalme wao, ndio vyanzo vya matatizo yote ndani ya Taifa la Israeli vilipoanzia, wakaanza kujiweka watumwa wao kwa wao.

Kwahiyo Biblia inatuonya tutuoke huko, kwenye kamba za dini na udhehebu, zilizoacha uongozi wa Roho Mtakatifu (Yesu Kristo) na kuingiza uongozi wa wanadamu, Tumgeukie Mfalme wetu Yesu Kristo ambaye leo hii katika mwisho wa nyakati anatuonya “yeye aliye na sikio alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”..Toka katika dhambi, rudi katika Neno, toka katika uvuguvugu ambao Bwana kasema atakutapika, toka katika ulevi, toka katika anasa za ulimwengu huu, rushwa, uasherati, usengenyaji, utukanaji, uuaji, ushirikina na mambo mengine yote yanayofanana na hayo..

2 Wakorintho 6 : 14 “…kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”

Rudi katika kamba za kimadhehebu kwasababu hayo yote yameshahukumiwa. Tafuta Roho Mtakatifu kwasababu huo ndio MUHURI WA MUNGU. Biblia inasema hivyo katika waefeso 4:30, ikiwa na maana kuwa ukipokea Roho Mtakatifu ndani yako, basi wewe tayari ni kazi iliyokamilika. Mungu kashakutia alamu kuwa wewe ni wa kwake. Na pasipo Roho Mtakatifu hakuna uhuru wala hakuna unyakuo. Dini wala udhehebu havikuhakikishii hilo isipokuwa Yesu Kristo peke yake. Tubu leo uoshwe dhambi zako na Bwana atakupa Roho wake.

Print this post

HUIJUI KAZI YA MUNGU, AFANYAYE MAMBO YOTE.

Ni kweli sisi kama wakristo tunaomngojea Bwana ni wajibu wetu kila siku kuelekeza macho yetu mbinguni, tukichunguza katika maandiko yale yatupasayo kufahamu juu ya siku hizi za mwisho na kuangalia dalili zote zinazoeleza kuja kwa pili kwa Kristo, Na kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa maandiko utagundua kuwa hichi kizazi tunachoishi ndio kile kizazi kilichotabiriwa na Bwana kushuhudia kuja kwa pili kwa Kristo. Kwasababu kuu mbili kwanza ni kizazi kilichoshuhudia kuchipuka tena kwa “mtini” (yaani Taifa la Israeli), Pili: Tunaishi katika kanisa la 7, na la mwisho, ambalo ni moja ya yale makanisa 7 tunayasoma katika kitabu cha (Ufunuo 2&3), litaisha na unyakuo. Na hakutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hilo. Na kanisa hili lilianza mwanzoni mwa karne ya 20, (yaani mwaka 1900) na litaisha na kunyakuliwa kwa kanisa.

Kadhalika biblia inatabiri pia katika wakati wa mwisho, kabla ya kuondoka kwa bibi-arusi wa Kristo na kwenda mbinguni kwenye karamu ya mwanakondoo, ni sharti kwanza IMANI ionekane ndani ya huyu bibi-arusi (Luka 18:8). Ni imani itakayomfanya anyakuliwe, vinginevyo kanisa halitaweza kuenda mahali popote kama halitafikia viwango hivyo vya ukamilifu Mungu analotaka liwe nalo. Hivyo ili hayo yote yatokee ni sharti kuwepo na uamsho na uvuvio mkubwa sana wa Roho Mtakatifu kabla ya huo wakati kufika ili wateule wawezi kufikia kiwango hicho cha ukamilifu Bwana anachotaka kukiona katika kanisa.

Na ndio ukija kusoma katika kitabu cha Yoeli 2: 23 utaona Inasema hivi;

“Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi MVUA YA MASIKA, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na MVUA YA VULI, kama kwanza.”

Unaona hapo? Biblia inazungumzia juu ya MVUA YA MASIKA na MVUA YA VULI au kwa tafsiri nyingine mvua hizi zinajulikana kama MVUA ZA KWANZA, na MVUA ZA PILI. Au mvua za sasahivi na mvua za baadaye..Sasa mvua ya kwanza Bwana aliiachilia katika ile siku ya Pentekoste, mwanzo kabisa wa kanisa na mwanzo wa ukristo, (Matendo 2), lakini ipo mvua ya mwisho ambayo Bwana ataiachilia tena katika dunia nayo itakuwa ni kwa ajili ya kulitimiliza kanisa, kwa ajili ya kuondoka hapa duniani. Na utukufu wake ni sharti uwe mkubwa kuliko ule utukufu wa lile kanisa la kwanza. Biblia imetabiri hivyo. Katika Hagai 2:9 

“Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi…”

Hivyo mambo yatakayoambatana na uamsho huo mkubwa ambao upo mbio kutokea ni mambo ambayo hayajazoeleka kuyaona katika wakati wowote wa kanisa tangu lianze siku ile ya Pentekoste hadi sasa. “Zile nguvu za zamani zijazo” za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ndio zitaonekana hicho kipindi, Sehemu ya pili ya ule unabii wa Yoeli aliotabiri juu ya siku za mwisho zitakavyokuwa ndio zitakwenda kuonekana katika kipindi cha majira hayo kama tunavyosoma:

Matendo 2:16-21.

“16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,

17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.

18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.

19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi.

20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.

21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.”

Ukisoma katika maandiko hayo sehemu moja ya unabii huo utaona umetimizwa, kwamfano sehemu ya ndoto, maono, kutabiri, lakini sehemu nyingine bado yaani sehemu ya ishara za juu mbinguni, na nchi, damu, moto,jua kuwa giza n.k.. Sasa hicho kipengele kilichobakia, kitatimizwa katika kipindi hicho cha uamsho huo wa mwisho wa kanisa. Kadhalika ukisoma kitabu cha Ufunuo 10, utaona pia zipo ngurumo 7 ambazo sauti zake hazijiandikwa mahali popote katika biblia nazo hizi zitafunuliwa katika hicho kipindi karibu na ukamilifu wa kanisa takatifu la Mungu. Ujumbe utakaotolewa na hizo ngurumo 7, utakuwa ni ujumbe wa kumkamilisha bibi-arusi wa Kristo tu peke yake, na si mtu mwingine aliye nje ya mpango wa wokovu. Kwao jumbe hizo zitasikika kama ngurumo tu, hawatuaelewa chochote.

Hivyo tukiyafahamu hayo, tunajua kabisa huu ni wakati wa kujiweka tayari na kwamba mambo hayo siku yoyote yanatokea. Lakini Sasa embu turudi katika kiini cha somo letu la leo.

Kuna wakati wanafunzi wa Bwana baada ya kuona kuwa Kristo sasa ameshashinda na kupewa mamlaka juu ya vitu vyote baada ya kufufuka kwake kutoka katika wafu, wanafunzi wake wakatanuka vichwa vyao wakidhani kuwa ule ndio wakati Mungu aliokuwa anauzungumzia tangu zamani wa Bwana kuwapigania Israeli na kuwarudishia ufalme wao ambao ulikuwa umetwaliwa na wapagani kuwa muda mrefu ndio wakati sasa umefika Israeli watapata raha, na kwamba Bwana atakwenda kuwaangamiza watu wote na mataifa yote yasiyomcha Mungu.

Hivyo hiyo ikawafanya wale wanafunzi wahamishe mawazo yao yote katika kutafuta kufanya mapenzi ya Mungu kwa wakati waliokuwepo na kuwafanya wafikirie mambo ya mwisho wa dunia. Walitaka mambo yaishe haraka haraka, hawakutaka kusikia kitu kingine chochote kinachohusu wokovu, hawakuwa na muda wa kufikiria kuokoa nafsi za watu ili zisiangamie huo muda utakapofika, wao walifikiria juu ya jamii ya watu wao tu, hawakujali na watu wengine ambao hawakuwahi kuisikia kweli, watu wa mataifa ambao laiti na wao wangeijua kweli ya wao wasinge abudu sanamu.

Kumbuka Mitume waliyajua maandiko na kuelewa kuwa siku masihi wao atakapokuja kuuchukua ufalme basi atawaokoa na maadui zao wote waliokuwa waliowatesa kwa miaka mingi. Ni kweli kabisa hilo jambo lilitabiriwa na ni lazima lije kutokea, katika siku hizi za mwisho lakini lile lilikuwa sio jukumu lao kuliharakisha.

Matendo 1:6-8 “6 Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?”

Unaona walijua kabisa hilo. Lakini jibu lake lilikuwa ni hili..

7 Akawaambia, SI KAZI YENU kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

8 LAKINI MTAPOKEA NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI WANGU katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Ndugu tukiyaelewa hayo maneno vizuri yatatusaidia sisi tunaoishi katika kipindi hichi ambacho tunaona kweli wakati wa mavuno upo karibu, na siku yoyote Bwana anarudi kama walivyoona mitume kwa kipindi chao. Je! na sisi kwa kulijua hilo tutahamisha mawazo yetu ya kumtumika Mungu, mawazo yetu ya kumzalia Mungu matunda ya kazi, na kustarehe na kusema tunangojea huo uamsho wa mwisho ufike sisi tuondoke?. Tuna relax tukingojea hizo sauti za ngurumo 7 zifunuliwe?. Tunangojea mpaka Mvua ya pili ishuke ndio tuanze kumtumika Mungu? Na huku hatutaki kutazama hali za watu waliokatika dhambi huu wakati, hatutaki kuyajua mapenzi ya Mungu kwetu sisi sasa hivi ni nini?..Sisi muda wote Ngurumo 7 zitafunuliwa,..ngurumo 7 zitafunuliwa.

Lakini Bwana Yesu vivyo hivyo anatuambia na sisi watu wa leo

“Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

8 LAKINI MTAPOKEA NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Ndugu, njia za Mungu HAZITAFUTIKANI, hujui leo na kesho Mungu kaipanga vipi, au kaamua kipi kianze au kipi kiishe, Mfalme Sulemani alijaribu kufanya hivyo kuzichunguza njia za Mungu ajue mwanzo wake na mwisho wa njia zake, lakini alishindwa na mwisho wa siku alimalizia na kusema:

Mhubiri 9: 17 basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.

Pia Mtume Paulo anasema:

Warumi 11:33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala NJIA ZAKE HAZITAFUTIKANI!.

Mwisho kabisa ikiwa Bwana ametupa na sisi nguvu ya kuwa mashahidi wake, hatuna budi sasa kufiria kumzalia Mungu matunda kwa wingi iwezekanavyo, na kuacha kupoteza muda mrefu kungojea mambo ambayo huna uhakika ni muda gani yatatokea. Kumbuka watu wengi wanaokaa katika hali hiyo ya kusubiria kipindi Fulani cha uvuvio kifike na huku hawana muda na shamba la Mungu sasa huwa hawafiki mbali. Kwasababu wanaishi kama watu waoteaji tu, na si kama watu wa Imani. Soma.

Mhubiri 11: 4 “Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.

5 Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.

6 Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa,kama ni hii au hii,au kama zote zitafaa sawasawa.”

Tenda kazi ya Mungu bila kuangalia msimu, au wakati unaofaa Bwana huwa analaani miti ile inayosubiria msimu ndio izae, kumbuka ule mtini Bwana Yesu alioulaani ambao alitarajia akute matunda juu yake na akakosa hivyo akaulani. Biblia inasema haukuwa umezaa kwasababu ulikuwa sio msimu wake wa kuzaa, kama Bwana angeenda katika kipindi cha msimu wake ni wazi kuwa angekuta matunda, lakini njaa ilimshika kabla ya msimu kufika. Hivyo usitegemee msimu, mwisho wa siku utajikuta huzai chochote. Anza kutafuta kufanya mapenzi ya Mungu sasa angali LEO IPO, KWASABABU KESHO SI YAKO.

Print this post

NYOTA YA ASUBUHI.

Ulishawahi kuitazama kwa ukaribu ile nyota ya asubuhi? Kama ulishawahi kuifuatilia na ukaona tabia yake utagundua ni ya kipekee sana, kwasababu ndio nyota pekee inayochelewa kupotea asubuhi na ndio nyota pekee inayotangulia kuonekana wakati wa jioni kabla ya nyingine… Ukiifuatilia kwa makini utagundua kuwa hii nyota ya asubuhi ndio ile ile nyota ya jioni na iko moja tu!.

Sasa jambo la kipekee sana kuhusu hii nyota ni kwamba licha tu ya kuwa inachelewa kupotea asubuhi na kuwahi kuchomoza jioni…lakini pia HUWA INAONEKANA MCHANA. Mchana kweupe wakati kukiwa hakuna mawingu nyota hii inaonekana, Mimi binafsi nikiwa na watu kadhaa tuliwahi kulithibitisha hilo..Wakati juu kukiwa hakuna mawingu, anga la Blue tumewahi kuiona hii nyota zaidi ya mara moja.

Kwa kawaida unaweza ukadhani ni jambo lisilowezekana lakini lipo!..kwasababu hata mimi mwanzo sikuwahi kutegemea kuona nyota yoyote mchana saa saba…lakini ilitokea nikaiona siku hiyo, na sikuwa mwenyewe tulikuwa wengi nao pia waliiona, na siku inayofuata iliendelea kuonekana. Sasa hii nyota kulingana na dunia inavyosogea na yenyewe huwa inasogea…asubuhi inaweza ikaonekana mashariki, mchana ikaonekana juu ya utosi jioni ikaonekana magharibi..inabadili eneo kulingana na mzunguko wa dunia. Ukipata muda ifuatilie nyota hii, utagundua haya yote na mengine zaidi ya haya.

Sasa katika maandiko Bwana amefananishwa na hii NYOTA YA ASUBUHI. Kutokana na tabia ya nyota hiyo ilivyo…Kama tu vile sehemu nyingine Bwana Yesu alivyofananishwa na SIMBA WA YUDA, alifananishwa na simba kutokana na tabia ya samba ilivyo, kwanza Simba ni mnyama aliye na nguvu kuliko wanyama wengi, na mwenye ujasiri kuliko wanyama wote, na sehemu nyingine anajulikana kama Mfalme wa mwituni..kadhalika na Bwana wetu Yesu Kristo, aliposhinda mauti pale Kalvari, alipewa nguvu, na heshima na uweza na ufalme wa dunia yote na mbingu zote, kama vile Simba alivyo mfalme wa mwituni, kadhalika na Bwana wetu Yesu Kristo alifanyika Mfalme wa ulimwengu wote.

Sasa tukirudi katika ILE NYOTA YA ASUBUHI, utaona kuwa licha tu ya kung’aa asubuhi na jioni, lakini pia inang’aa mchana, hivyo inang’aa katika vipindi vyote vya siku, yaani asubuhi, mchana na jioni na usiku. Biblia inasema:

Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ILE NYOTA YENYE KUNG’AA YA ASUBUHI.

Ikimfunua BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye yeye ameshinda na kukaa katika NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA, aling’aa milele iliyopita, anang’aa nyakati hizi na atang’aa milele…

1 Timotheo 6: 14 “..hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;

15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;

16 ambaye yeye PEKE YAKE HAPATIKANI NA MAUTI, AMEKAA KATIKA NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele”.

Amina. 

Wakati nyota nyingine zote zinang’aa jioni na asubuhi kufifia, Nyota ya Yesu Kristo haififii kamwe, NURU YAKE HAIHARIBIKI, (Haifunikwi) wakati wanadamu mashuhuri, watu maarufu, watu wakuu, na wafalme wa dunia wanakuja na kuondoka, lakini Yesu Kristo Mfalme wa Wafalme na Bwana wa mabwana anadumu milele, vizazi na vizazi hapungui nguvu, wala uweza, wala mamlaka..ANANG’AA HATA MCHANA KWEUPE..anatoa NURU isiyoweza kufunikwa na nuru nyingine, Je! Unajua kuwa mtu pekee anayeshikilia namba moja kwa umaarufu duniani kwa wakati wote ni YESU KRISTO??…Kama hujui hilo nenda kasome kwenye vitabu vya rekodi ya dunia,.. (hata mambo ya ulimwengu huu tu yanamtangaza) Ndio maana Bwana Yesu alisema yeye ndiye NURU YA ULIMWENGU. Ikiwa na maana kuwa hakuna Nuru nyingine zaidi yake. Mbingu na nchi zitapita lakini Yesu ni yeye yule jana na leo na hata milele. Haleluya!

Yohana 1: 9 “Kulikuwako NURU HALISI, amtiaye NURU KILA MTU, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua”.

Umeona hapo? Anasema kulikuwako na NURU halisi, ikiwa na maana kuwa zilikuwepo nuru nyingine lakini hazikuwa halisi, na Nuru hii halisi, ina uwezo wa kumtia Nuru kila mtu , ikiwa na maana kuwa ina uwezo wa kumfanya kila mtu kuwa kama yeye alivyo.

Ndugu yangu, Yesu Kristo Mkuu wa Uzima anataka watu wote, tuwe kama yeye, anataka wote tung’ae kama yeye, anataka tuangaze hata mchana kweupe, kusiwepo na chochote kinachoweza kutuzima, milele na milele, na ndio maana maandiko pia yanasema katika..

Mithali 4:18 “Bali njia ya wenye haki ni kama NURU ING’AAYO, Ikizidi kung’aa HATA MCHANA MKAMILIFU”.

Unaona hapo wenye haki, yaani wote waliyoikubali NURU HALISI (YESU KRISTO), biblia inasema watang’aa hata mchana Mkamilifu. Siku ile watakapomaliza kazi yao hapa ulimwenguni, ndio watadhihirika mng’ao wa utukufu wao ulivyo. Watakuwa kama miale ya Moto, watang’aa kuliko jua. Bwana hataki maisha yako leo yawe hivi kesho yanyauke, anataka uishe milele. 

Danieli 12:3 “Na walio na hekima WATANG’AA KAMA MWANGAZA WA ANGA; na hao waongozao wengi kutenda haki WATANG’AA KAMA NYOTA MILELE NA MILELE”.

Mathayo 13: 40 “Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.

41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,

42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

43 Ndipo wenye HAKI WATAKAPONG’AA KAMA JUA katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie”.

Je! Na wewe leo umetiwa nuru na ile Nuru halisi (Yesu Kristo)? Je! Umemkabidhisha maisha yako leo? Siku tunazoishi ni za hatari, Kristo anakaribia kurudi kulichukua kanisa lake, na kukusanya ngano ghalani na makapi kuyakusanya kwenda kuchomwa moto. Yesu Kristo ndiye Nuru ya ulimwengu, na ukombozi kwa mwingine yoyote isipokuwa yeye..Tubu leo, ukabatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, naye Bwana atakutia Muhuri wa Roho wake Mtakatifu.

Ubarikiwe!


Mada Nyinginezo:

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

UMEFUNULIWA AKILI?

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.


Rudi Nyumbani

Print this post