Shalom, karibu tujifunze biblia…Kuna madhara makubwa sana ya kutombana mwanao..na kumruhusu tu kufanya lolote analojiamulia, kwa kuogopa kuwa atakuchukua…
Mtoto kamwe hawezi kukuchuku! unapomwonya au kumbana.…Hebu jiulize wewe wakati ukiwa mdogo, mzazi wako alipokuzuia au alipokubana ufifanye jambo Fulani je ulimchukia?…ni wazi kuwa hukumchukia zaidi uliona tu ni kama mzazi hakipendi kile kitu na si kwamba hakupendi wewe.
Vivyo hivyo na wewe unapombana mwanao asifanye vitu Fulani Fulani ambavyo unaona vina muelekeo mbaya wa kumletea madhara mwanao huko mbeleni, hufanyi dhambi…unapoona kuna tabia inaanza kukithiri ya kupenda kutazama Tv kwa muda mrefu, usiache kuithibiti hiyo tabia..Unapoona kuna tabia ya kuanza kuzurura zurura…mbane, si kila siku ni ya kwenda kucheza cheza na kutazama Tv, ni lazima ziwepo siku za kujifunza Neno nyumbani, watoto wana vichwa vizuri sana vya kushika mambo/kukariri…Kwahiyo katika hali walizopo ni lazima uwape mistari ya kuishika kichwani, hata kama hawaielewi sasa, lakini itakaa ndani yao kama akiba, watakapokuwa watu wazima itakuwa tayari ipo kichwani, hivyo watakapoanza kuitafakari watakuwa hawana kazi ya pili ya kuikariri tena…
Na pia ni lazima ziwepo siku za kujisomea masomo ya shuleni wawapo nyumbani, ni lazima yawepo masaa ya kumfundisha mwanao kusaidia vijishuhuli vidogo vidogo..Hata kama hakuna shughuli yoyote ya kusaidia (labda nyumbani wapo wafanya kazi wa kutosha)…usikubali mwanao abweteke, mtengenezee kazi ya kufagia, kupika, kuosha vyombo, kupasi, kufua nguo, kufanya usafi n.k..Pia mtume mahali kama dukani n.k..Na pia unapoona kuna vijitabia vya kiburi na utundu vinaanza basi tumia kiboko kidogo kuvidhibiti…
Mithali 23:13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. 14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.
Mithali 23:13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.
sio dhambi na wala hatakuchukia….Usiusikilize uongo wa shetani moyoni mwako kwamba ukimrudi mwanao atakuchukia…Kamwe watoto hawana chuki, wala vinyongo…
Ukiona mtu anakinyongo na mtu Fulani kwa kitu alichofanyiwa utotoni…kiuhalisia kinyongo hicho kilimwingia baada ya yeye kuwa mkubwa na kukitafakari kile kitu kibaya alichofanyiwa…Lakini katika hali ile ya utoto aliyokuwepo hakuwa na ufahamu huo…Hivyo hata mtoto leo hii ukimwadhibu kwa kosa lolote lile hawezi kukuchukia badala yake atajifunza kutokukifanya kile kitu….na siku atakapokuwa mkubwa ndipo atakumbuka zile adhabu na atakapotafakari kwamba ulikuwa unamwadhibu au ulikuwa unambana kwa kwa faida yake mwenyewe ndipo atakapokupenda zaidi…atasema moyoni mwake kama mama/baba asingenizuia na ile tabia yangu sijui leo ningekuwa wapi..na hivyo atakupenda zaidi kuliko kukuchukia lakini tabia ya kutombana mwanao kwa kuogopwa kuchukiwa…nakuambia ukweli siku mtoto Yule atakapokuwa mtu mzima na kutafakari ni jinsi gani ulivyokuwa unamwangalia tu anapotukana, au anapofanya mambo yasiyofaa pasipo kumwambia chochote atakuchukia na kusema hukuwa unamjali.
Kumbuka Uzao wa Tumbo lako ni thawabu yako mwenyewe…Mtoto uliyepewa ukimtunza vyema ni kwa thawabu yako mwenyewe katika siku za baadaye…
Zaburi 127:3 “Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, UZAO WA TUMBO NI THAWABU”.
Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”.
Pia kama bado hujapata mtoto na umeolewa/umeoa….usiwe na hofu, mwamini Mungu, usijiangalie umri uliopo, hata kama ni miaka 50..wapo waliozaa wakiwa na miaka 90 sembuse wewe mwenye miaka 60?..Kwahiyo wakati wa Mungu ni bora kuliko wa wanadamu..zidi kujitenga na ulimwengu na kuishi maisha ya utakatifu na kumcha Mungu kama kawaida…hayo mengine mwachie Baba, huwa anafanya njia mahali pasipo kuwa na njia, na mahali pasipoonekana dalili….na huwa anarudishaga miaka iliyoliwa na parare kwa watoto wake..Hivyo muamini Mungu na mngojee. Na upatapo mtoto kumbuka siku zote kwamba kutombana kufanya mambo yasiyofaa ni kwa hasara yako mwenyewe na yake pia.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.
USIPUNGUZE MAOMBI.
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Shalom,
Nakukaribisha tutafakari pamoja vifungu vifuatavyo vya maandiko, naamini lipo jambo utajifunza mwishoni mwa somo..
Matendo 16:6 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. 7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, 8 wakapita Misia wakatelemkia Troa. 9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie”.
Matendo 16:6 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.
7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,
8 wakapita Misia wakatelemkia Troa.
9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie”.
Wengi wetu tunafahamu vipingamizi pekee mtume Paulo alivyokuwa anapitia vya kuhubiri injili vilitoka kwa shetani, lakini hatujui kuwa kuna wakati mwingine Mungu mwenyewe alikuwa anamzuia Paulo asihubiri injili japokuwa alitamani kufanya hivyo,.
Mungu anafanya hivyo sio kwamba hataki watu wahubiriwe injili kama ilivyo kwa shetani, hapana, bali ni kawaida yake kuwapa vipaumbele vya kwanza wale ambao wanaonyesha kiu ya kutaka kumjua yeye.
Ili kutimiza haya maandiko.
Mathayo 5:6 “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa”.
Na haya..
Mathayo 5:3 “Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao”.
Kama ukichunguza hiyo mistari utaona, Mungu hakumkataza Paulo kufika kabisa katika hiyo miji iliyotajwa hapo juu, lakini aliifikia na kuipita, kuonyesha kuwa kama kungekuwa na utayari wa wenyeji wa pale kutamani kumjua Mungu basi wangeanzwa kwanza wao, kisha ndio wafuate wale wengine..
Jaribu kufikiria anafika pale Frigia, anataka tu kuanza kuhubiri Mungu anamzuia, anaondoka anaenda mji unaofuata Galatia huko nako Mungu anamzuia anaondoka tena anafikiria labda ashuke kwenye miji mingine ya Asia (ambayo ndio kama Efeso, Smirna, Pergamo, Laodikia n.k. ) lakini huko nako Mungu anamwambia asihubiri chochote aondoke…
Haishii hapo anaondoka tena Asia anafika mji ulioitwa Misia ili aanze kuhubiri bado Mungu anamkataza, anafika Troa bado Mungu hampi kibali, wakati sasa akiwa hapo Troa ukingoni kabisa mwa mji ndipo Mungu anamwonyesha maono ambayo yalikuwa yanaonyesha jinsi watu wa kule Ng’ambo ya bahari Makedonia walivyokuwa wanahitaji msaada mkubwa sana wa kiroho..
Ndipo hapo utaona inamgharimu Paulo kuvuka bahari sasa asafiri, mpaka kwenye hiyo miji ya Makedonia ambayo, ilikuwa ni Filipi, Thesalonike, na Beroya.. Ili kuihubiri injili.. Si jambo rahisi
Ili kuelewa vizuri jaribu kutengeneza picha labda mtumishi wa Mungu anatoka nchi ya mbali Afrika Magharibi labda tuseme Ghana, anafika nchi za Afrika ya kati kama vile Congo n.k., Mungu anamwambia pita usihubiri, anafika mpaka nchi zetu za Afrika mashariki, Anaanzia Uganda anaambiwa pita, anafika Kenya anaambiwa pita, anafika hapa Tanzania, bado Mungu anamwambia usihubiri hapo, sasa akiwa ameshavuka kote toka kigoma, akiwa pale Daresalaam, Mungu anamwambia panda Meli nenda taifa la India wapo watu wangu kule wanahitaji msaada wa kunijua mimi..
Ndivyo ilivyokuwa kwa Mtume Paulo na wenzake, walienda Makedonia na kweli kule walikutana na watu ambao kwanza walikuwa ni maskini, lakini walikuwa tayari kumtolea Mungu kwa moyo wao wote..na zaidi ya yote walikuwa tayari kulipokea Neno la Mungu, mfano watu wa Beroya ndio wale ambao walikuwa wapo tayari kuchunguza maandiko ya kujua ufasaha wa yote,
2Wakorintho 8:1 “Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; 2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na UMASKINI WAO uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. 3 Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;
2Wakorintho 8:1 “Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;
2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na UMASKINI WAO uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.
3 Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;
Hivyo mimi na wewe tunajifunza nini?
Mungu ni yeye ule jana na leo na hata milele, kama mengi ya makanisa ya Asia hayakustahili kupewa neema ya wokovu kwanza, atafanya na kwetu vivyo hivyo kama hatutakuwa tayari kuipokea.
Tupaswa tujiulize je! mioyo yetu ni kweli ina kiu ya kumjua Mungu, kiasi kwamba mpaka rohoni Mungu anatufananisha na watu wa Makedonia?.. Vuka, uje Makedonia utusaidie?. Je! ni kweli tunaonyesha tunahitaji msaada kutoka kwa Mungu? Je tunastahili msaada?.. Kama ni kweli tunaonyesha tunahitaji msaada, basi hapo ndipo Mungu atakapofungua njia ya kutusaidia, kwa namna ya ajabu.
Na tunaonyesha tunahitaji msaada kwa namna gani?.. Tunaonyesha kwa bidii yetu sisi ya kutafuta yeye kwa nguvu zetu zote, kwa akili zetu zote, kwa mioyo yetu yote na kwa Roho zetu zote.
SAYUNI ni nini?
Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?
USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
Shalom mtu wa Mungu, karibu tuyatafakari maandiko…leo ni siku nzuri Bwana aliyotupa..hivyo ni vyema tukachukua nafasi hii kulitafakari Neno lake kwa ufupi..
Kumbuka siku zote kuwa baada ya kumpokea Kristo, kila mmoja wetu anawajibu wa kuifanya kazi ya Mungu kupitia karama Mungu aliyoiweka ndani yake. Kuna hatari kubwa sana ya kutoitumia karama Mungu aliyoiweka ndani yako kabisa….Na madhara makubwa yapo baada ya maisha haya…wakati ule ambapo watakatifu watapewa thawabu zao wewe hutakuwa na chochote…
Katika siku ile waliokuwa waaminifu kwa karama zao watapewa thawabu kubwa zaidi..na wale waliokuwa walegevu na kuleta faida ndogo katika ufalme wa mbinguni watalipwa kidogo, na wale ambao hawajafanya kitu kabisa hawatapewa chochote…
Lakini ni heri kufanya hata kama ni KIDOGO sana ukapata kitu kule kuliko kutofanya kabisa…
Hebu naomba usome mfano huu Bwana alioutoa…inawezekana ulishawahi kuusoma hapo kabla mara nyingi, na kuurudia rudia…. lakini hebu chukua muda tena sasa hivi kuusoma hadi mwisho taratibu, pasipo kuruka kipengele hata kimoja, kuna kitu cha kipekee sana nataka tujifunze leo.
Luka 19:11 “Waliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara. 12 Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. 13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, FANYENI BIASHARA HATA NITAKAPOKUJA. 14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale. 15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi. 17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida. 19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano. 20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. 21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 23 BASI, MBONA HUKUIWEKA FEDHA YANGU KWA WATOAO RIBA, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. 25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. 26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho”.
Luka 19:11 “Waliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara.
12 Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, FANYENI BIASHARA HATA NITAKAPOKUJA.
14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.
15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.
16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.
17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.
19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.
20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
23 BASI, MBONA HUKUIWEKA FEDHA YANGU KWA WATOAO RIBA, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.
26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho”.
Mfano huo unamhusu Bwana Yesu mwenyewe, yeye ndio mfano wa huyo mtu kabaila..ambaye aliondoka na kwenda nchi ya mbali(mbinguni) kutuandalia ufalme…na alipoondoka alitupatia vipawa (karama) akatuambia tukawafanye watu wote kuwa wanafunzi (maana yake kuwahubiria na kuwageuza wamwamini yeye kila mmoja kwa kipawa alichopewa)…Na siku moja atarudi kutoka huko nchi ya mbali(mbinguni)…alipokwenda kututengenezea ufalme…atarudi duniani kwaajili ya utawala wa miaka 1,000 (Ufunuo 20).. Na siku atakaporudi atawaangamiza wale wote ambao hawakumkubali (yaani watu waovu)..Na baada ya kuwaangamiza waovu wote ndipo atakapowakusanya watumishi wake waliompokea…na hapo kila mmoja ataketi na kutoa hesabu ya faida aliyoileta katika ufalme wa mbinguni..
Watasimama wachungaji, watasimama waimbaji, watasimama mitume, watasimama mashemasi, waalimu, manabii, maaskofu, wazee wa kanisa, waumini wote na kila mmoja atatoa hesabu jinsi alivyoitumia karama yake…waliofanya vizuri watapewa mamlaka makubwa na waliokuwa wavivu watakosa vyote…
Sasa katika kisa hicho tunasoma kuna mmoja alifukia talanta yake chini…kwa uvivu akijitumainisha kwamba Bwana huwa hasaidiwagi kazi…yeye anang’oa pando asilolipanda, kazi ambayo hajaifanya yeye anaiharibu!…kwahiyo akajifariji kwamba Mungu huwa hasaidiwi kazi…hatutegemei hata tusipokwenda kuhubiri walio wake watakuja tu!.. kwanza unaweza kwenda kuhubiri ukakosea kosea maneno ndio ukawa umemuudhi badala ya kumfurahisha……pia sio lazima sana kumtolea kwani hata tusipochangia chochote kwenye kazi yake yeye ni tajiri na sisi ni mavumbi hivyo atafanya njia tu kwa vyovyote vile(hasaidiwi kazi)……pia yeye hahitaji sana sifa zetu, tayari anao malaika wengi wanaomwimbia….. n.k
Kwahiyo kwa kujitumainisha huko na visingizio hivyo… mtu wa namna hii akawa hafanyi kazi ya Mungu akafananishwa na mtu aliyefukia fedha yak echini ya shimo…siku ile ikafika na Bwana akamhukumu kwa kinywa chake…
Ndugu mpendwa baada ya kuokoka…usikae ufikiri kwasababu Mungu ni mkuu basi hatutegemei sisi….Ni kweli hatutegemei anaweza kufanya asilimia mia pasipo sisi…lakini hataki tuwe wajinga!…Sio kwasababu kasema maneno haya…
Matendo 7:49 “Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani mtakayonijengea? Asema Bwana, 50 Au ni mahali gani nitakapostarehe? Si mkono wangu uliofanya haya yote?”
Matendo 7:49 “Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani mtakayonijengea? Asema Bwana,
50 Au ni mahali gani nitakapostarehe? Si mkono wangu uliofanya haya yote?”
Basi na sisi ndio tubweteke tusimjengee nyumba…kwasababu amesema yeye hakai kwenye nyumba zilizofanywa na mikono yetu…Ndugu Usikae ufikiri hivyo kamwe!.. Daudi aliujua vizuri huo mstari pamoja na Sulemani mwanawe lakini walimjengewa Bwana nyumba hivyo hivyo…na Mungu akapendezwa nao..Sikia maneno Sulemani aliyoyasema..
1Wafalme 8: 26 “Sasa, Ee Mungu wa Israeli, nakusihi, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako, Daudi, baba yangu. 27 LAKINI MUNGU JE? ATAKAA KWELI KWELI JUU YA NCHI? TAZAMA, MBINGU HAZIKUTOSHI, WALA MBINGU ZA MBINGU; SEMBUSE NYUMBA HII NILIYOIJENGA! 28 Walakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee Bwana, Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo. 29 Macho yako yafumbuke na kuielekea NYUMBA HII usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa”.
1Wafalme 8: 26 “Sasa, Ee Mungu wa Israeli, nakusihi, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako, Daudi, baba yangu.
27 LAKINI MUNGU JE? ATAKAA KWELI KWELI JUU YA NCHI? TAZAMA, MBINGU HAZIKUTOSHI, WALA MBINGU ZA MBINGU; SEMBUSE NYUMBA HII NILIYOIJENGA!
28 Walakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee Bwana, Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo.
29 Macho yako yafumbuke na kuielekea NYUMBA HII usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa”.
Walijua Mungu mbingu hazimtoshi na huku duniani ni mahali pa kuwekea miguu yake..lakini walilazimisha kumjengea Mungu duniani japokuwa waliyajua hayo maandiko…na mpaka leo Hekalu la Sulemani linajulikana.
Vivyo hivyo na wewe..usiseme Bwana ana malaika wengi…usiseme Bwana hahitaji fedha yangu kwani dhahabu zote na fedha zote ni za kwake… Usiseme sio lazima kujisumbua kuhubiri kwani Bwana anao watumishi wengi…usiseme sio lazima kujisumbua kuimarisha kazi ya Mungu kwasababu Mungu hahitaji msaada kutoka kwetu..ukifanya hivyo utakuwa umefukia talanta yako chini uliyopewa…
Na Mwisho kabisa Bwana alimwambia Yule mtu aliyefukia ile fedha chini maneno haya…” BASI, MBONA HUKUIWEKA FEDHA YANGU KWA WATOAO RIBA”… Mtu anayeweka fedha kwa watoa riba…maana yake haendi kuifanyia shughuli yoyote ile hela..ni kuiweka tu baada ya wakati Fulani inajizalisha…ni kama vile umemkopesha mtu hela…Sasa kazi ya kukopesha haitumii jasho lolote…ni kuwekeza tu hela na kusubiria faida basi!….Hata hiyo kazi nyepesi ambayo haihitaji jasho! Bwana angetegemea aione kwa huyu mtu lakini hakuiona..
Kadhalika na wewe…inawezekana huwezi kabisa kusimama mimbarani, au kwenda mitaani kuhubiri… basi angalau wekeza kwenye kazi ya Mungu kwa fedha zako au mali zako kwa uaminifu, nunua kinanda, nunua mifuko kadhaa ya cement, au nunua chochote kile uwezacho kipeleke nyumbani kwa Mungu…kwasababu unapomtolea Mungu, fedha au mali zile zinakwenda kutumika katika kuifanya kazi ya Mungu na hivyo unaleta faida katika ufalme wa Mbinguni… ukifanya hivyo angalau Bwana atakuheshimu siku ile utakuwa umeiweka talanta yako kwa watoa riba…
Bwana atusaidie sana katika hayo..
Kama bado hujampa Yesu maisha yako…tunaishi katika siku za mwisho, Kristo yupo mlangoni kurudi…hivyo tubu leo kwa kumaanisha kuacha dhambi zote unazozifanya kama ulevi, rushwa, anasa, uasherati, uuaji, ufiraji, ulawiti,ushoga, usagaji, utazamaji wa picha za ngono, kujichua na nyingine zinazofanana na hizo…Tubu leo kwa dhati na amua kuziacha…na baada ya kuomba rehema Bwana atukusamehe kama alivyoahidi…Na amini kashakusamehe kama umetubu kwa dhati!..Na baada ya hapo tafuta ubatizo sahihi ambao ni wa maji tele na kwa jina la Yesu ambalo ndio jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu…na baada ya hapo Roho Mtakatifu ambaye tayari atakuwa ameshafika karibu yako atakupa uwezo wa kuzishinda hizo dhambi ulizoziacha..ili usizirudie tena…na mengine yaliyosalia atakuongoza kuyafanya.
Maran atha
USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.
Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano.
MAOMBI YA VITA
FAIDA ZA MAOMBI.
Shalom..
Asubuhi ile Mariamu Magdalene alipokwenda kaburini na kukuta jiwe limeondolewa na mwili wa Yesu haupo, aliondoka ghafla na kwenda kuwapa taarifa wanafunzi wa Yesu, na kuwaambia Bwana hayupo kaburini wamemwiba na hatujui ni wapi walipompeleka..
Taarifa hiyo ya kushtusha iliwafanya watu wawili waondoke mahali pale kwa kasi sana, mmoja alikuwa ni Yohana na mwingine alikuwa ni Petro ili kwenda kuthibitisha kama waliyoelezwa ni kweli au La..
Yohana 20:2 “Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka. 3 Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini. 4 Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini. 5 Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. 6 Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala, 7 na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake. 8 Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini. 9 Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka”.
Yohana 20:2 “Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.
3 Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini.
4 Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini.
5 Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia.
6 Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala,
7 na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake.
8 Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini.
9 Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka”.
Sasa ukiangalia hapo, utagundua Yohana alipofika pale kaburini na kuchungulia kwa mbali, aliona kweli Bwana hayupo na vitambaa vya sanda vimelala pale chini, pengine hilo lilimpa uhakika kuwa kweli mwili wa Bwana uliibiwa usiku na kuhamishwa pale na kupelekwa mafichoni sawasawa na maneno ya Mariam Magdalene..
Lakini tunaona Petro alipokuja baadaye kidogo, yeye kuishia pale mlangoni tu, bali alipitiliza moja kwa moja mpaka ndani kabisa mwa kaburi pale Bwana alipokuwa amelazwa ili kuthibitisha jambo hilo, Lakini alipofika karibu aliona jambo lingine la kushangaza kidogo, ambalo ndio lililowapa uhakika kuwa Bwana hakuibiwa bali ni kweli alifufuka..
Jambo hilo pengine hata wewe hukuwahi kulifahamu, ukisoma huo mstari wa 7 utaona vitambaa vya sanda vilikuwepo kweli pale chini sawasawa na Yohana alivyoona kule nje, lakini ile LESO ya kichwani biblia inasema haikuwa Pamoja na vitambaa bali ilizongwa zongwa mbali kabisa mahali pake yenyewe.. Sasa hilo neno kuzongwa zongwa biblia inamaanisha KUKUNJWA VIZURI, yaani hiyo leso ya kichwani ilikunjwa vizuri kwa utashi na Bwana mwenyewe kisha akaenda kuiweka kwa mbali kidogo na vile vitambaa vilivyokuwa vimefungwa mwilini mwake, pengine kwenye mwamba wa juu kidogo, mbali na pale alipokuwa amelala..
Hilo ni jambo la kufikirisha sana… Kama kweli wezi walikuja kumuiba wasingekuwa na muda wa kuikunja leso na kuiweka sehemu yake yenyewe mfano wa mtu anayekunja shati lake na kuliweka kabatini.. mwizi hawezi kufanya kazi kama hiyo..
Hilo ni tendo linaloonyesha kuwa Bwana hakuibiwa, bali alifufuka, na alipofufuka alianza kujifungua yeye mwenye taratibu, alipoliza, akaichukua ile leso ya kichwa akaanza kuikunja bila haraka yoyote akaenda kuiweka ndipo akaondoka..
Hilo ndilo lililowafanya Petro na Yohana biblia iseme katika mstari wa nane, wakaamini..
Habari hiyo inatufundisha nini?
Hatuwezi tukaufahamu ukweli wa Kristo kwa kuambiwa ambiwa tu, vilevile bado hatuwezi kuelewa siri ya kufufuka kwake kwa kusimama mlangoni mwa kaburi lake, Tutaelewa siri za Kufufuka kwa Kristo kwa kuzama kabisa mule kaburini alipokuwepo kama Petro, yaani kuwa tayari kufa na Kristo na kufufuka Pamoja naye kwa Habari ya dhambi, ndipo tutakapoelewa siri za kufufuka kwake kwa mapana na marefu..
Tukubali tu tusipotaka kuzama ndani katika wokovu, kamwe hatutakaa tuelewe maana ya ufufuo maishani mwetu, tukiwa wakristo vuguvugu, au wakristo jina, au wakristo wa kusita sita, wakristo wa kuvutwa vutwa tujue kuwa wapo tuliowaacha nyuma mfano wa Petro watatutangulia siku moja kuzijua siri za Kristo kuliko sisi ambao tunajiona tumeshajua kila kitu, na huku bado tupo mguu mmoja nje mwingine ndani.
Naamini hatutakuwa wasikiaji tu wa hadithi, bali tutayatendea kazi, tutazama kaburini kuuthibitisha ufufuo,…hicho ndicho Bwana anachokitaka maishani mwetu.
Bwana atubariki sote.
SHETANI ANAITHAMINI HATA MAITI YAKO.
JE! PAKA KULIA USIKU NI ISHARA YA UCHAWI?
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.
Nitaitofautishaje sauti ya Malaika na ya Roho Mtakatifu?
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Shalom, mtu wa Mungu..karibu tuyatafakari maandiko pamoja,
Biblia inasema…
2Wakorintho 10:3 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”
2Wakorintho 10:3 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”
Kazi ya kwenda kuvua watu inafananishwa na shughuli za wanajeshi vitani…Wanajeshi wanapotaka kushambulia mahali huwa hawampi adui taarifa…na wanafanya hivyo, wanashtukiza tu…na wakisha angamiza wote wanateka mateka na kuchukua nyara vitu vyao..
Na katika kazi ya uvuvi wa watu ni hivyo hivyo…Hatupaswi kuingia mkataba na adui, wala kushauriana naye…tunachopaswa kufanya ni kila mara kuvamia kambi ya adui na kuteka mateka..
Unaposikia msukumo wa kuhubiri, sio suala la kusema hapa panafaa au hapafai..unachopaswa kufanya ni unavamia!…kwasababu katikati ya kambi ya Adui kuna mateka…na mateka unawaweka huru kwa kuwavamia..Ingawa vita utakutana navyo hiyo ni kawaida hata kambi ya adui akivamiwa ghafla ni lazima ijibu mashambulizi kidogo hata kama inajua itakwenda kushindwa..
Ukiwa shuleni, hata mwanya mdogo unaoupata, usipoteze muda…hubiri Habari njema, ukiona mgonjwa mahali mwanya huo ulioupata mnyang’anye shetani hilo teka…Mwombee apone na mhubirie, Ukikutana na mtu mwenye mapepo..itumie hiyo fursa vizuri, ya kuyakemea hayo mapepo yamwondoke na kumweka huru huyo mtu, na kisha Mweleze Habari za Yesu…
Usitazame huyu ni mkubwa kuliko mimi hawezi kunisikiliza, huyu ana elimu kuliko mimi, huyu ana heshima kuliko mimi, anavaa vizuri kuliko mimi, ni mwalimu wangu, ni kiongozi wangu, au nimekutana naye tu siku ya kwanza usiyaangalie hayo hata kidogo.. Kwasababu silaha ulizo nazo zina NGUVU! Kuifanya kila Fikra imtii Kristo. Wapo maprofesa waliobadilishwa fikra zao wakamtii Kristo na watu ambao hawajasoma hata darasa moja..Wapo maraisi waliowekwa huru na injili ya watu ambao hawajasoma hata darasa moja. Wapo waliokuwepo sugu lakini leo hii ni watumishi wa Mungu. Kwahiyo vaa silaha na ingia kazini..
Nguvu ile ile iliyokubadilisha wewe ndiyo hiyo hiyo itakayowabadilisha na wengine..wewe mpaka umemtii Kristo ni kwasababu Kristo alimtumia Mtumishi wake kuja kumnyang’anya shetani wewe ambaye ulikuwa mtumwa wake…Na baada ya kumpokonya shetani ndipo akakufanya wewe kuwa TEKA lake. Na hakuishia hapo akakupa na wewe Kipawa (yaani karama)..ambayo ni silaha na kazi yake mojawapo ni kwenda na wewe kuteka mateka mengine na kuyaleta kwa Kristo.
Waefeso 4:7 “Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. 8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa”.
Waefeso 4:7 “Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.
8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa”.
Hivyo kama umempa Kristo Maisha yako…ni jukumu lako kwenda kuteka mateka…kwasababu tayari silaha unayo…kama ni mtaani ingia anza kuhubiri, na utaona matokeo, kama ni shuleni ni hivyo hivyo, kama ni kusafiri huko na huko fanya hivyo kwa nguvu zote kwa karama Mungu aliyoiweka ndani yako, kama ni katika mahospitali na magereza..usikawie kawie..Nenda kwasababu Mungu atakuwa Pamoja nawe siku zote kukuongoza… yakumbuke haya maneno ya Yesu mwenyewe Bwana wetu aliyoyasema..
Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; NA TAZAMA, MIMI NIPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE, HATA UKAMILIFU WA DAHARI”
Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; NA TAZAMA, MIMI NIPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE, HATA UKAMILIFU WA DAHARI”
Atakuwa Pamoja na wewe hata ukamilifu wa dahari!…dahari maana yake ni nyakati/wakati….Hivyo hapo maana yake ni kwamba ameahidi kuwa “Pamoja nasi mpaka mwisho wa nyakati”…Lakini hiyo ni kama tutaondoka na kwenda kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi…na kuwafanya kuwa mateka wa Kristo.
Bwana atusaidie kumuamini..
Kumbuka pia katika kwenda kuhubiri kuwa mwaminifu na kuwa na nia ya Kristo, sio nia ya kuwa maarufu au kutafuta fedha, bali ya kutafuta roho za watu…huku ukijua kuwa una thawabu yako mbinguni na Kristo anakuja upesi..
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
Kuungama ni nini?
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
Katika biblia Neno “Mshenzi” linatajwa.Kwanini liwekwe?
KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI, NJAA NA TAUNI.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Upotevu una malipo. Pale mtu anapoufahamu ukweli, lakini hataki kuufuata, pale mtu anaposikia kila kukicha acha dhambi, mpe Yesu Maisha yako, dunia hii inakwenda kuisha, dalili zote zinaonyesha, magonjwa ya Tauni Bwana Yesu aliyoyazungumzia kuwa yatatokea nyakati za Mwisho yanaonekana sasa, watu kupenda pesa, watu kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu yanaonekana sasa ulimwenguni kote, tetesi za vita, manabii wa uongo kuzuka, Injili kuhubiriwa ulimwenguni kote, Israeli kama mtini kuchipuka tena, yote hayo yameshatimia lakini ni kama kelele kwake..
Mpaka sasa hakuna mtu anayejiita mkristo ajiyejua kuwa tunaishi katika siku za kumalizia, dakika za majeruhi, majira ya parapara kulia, na lakini mtu huyo huyo anayeyafahamu hayo yote hataki kuchukua hatua yoyote rohoni mwake, anaposikia injili anaona ni kama ya watu fulani hivi waliokata tamaa ya Maisha wajulikanao kama walokole, kila siku anasema moyoni “nita”….“nita” nitaacha siku moja, nitatubu siku moja, na huku bado anatazama picha za ngono mitandaoni, anazini, anajijua kabisa yupo upotevuni, lakini bado anaendelea kufanya hivyo, na kusahau kuwa Upotevu huo ulio ndani yake unao malipo yake..
Na malipo yenyewe, sio yale ya kwenda motoni hapana, kabla hujafika huko, Mungu anachofanya kwanza katika Maisha haya ni kukuacha..Ni heri ukaachwa na ulimwengu mzima lakini sio kuachwa na Mungu..ukishaachwa tu wakati huo huo maroho mengine mabaya ya kuzimu yanakuingia, na ndio hapo unajikuta kiwango chako cha kufanya maasi kinaongezeka mara mbili Zaidi, kama ulikuwa ni mwasherati hutaishia kufanya na jinsia tofauti tu, utafika kutamani hata jinsia ya aina yako, au viumbe vingine, au vitu vingine,..hayo ndio malipo ya uovu wako..
Warumi 1:26 “Hivyo Mungu ALIWAACHA wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU wao yaliyo haki yao”.
Warumi 1:26 “Hivyo Mungu ALIWAACHA wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU wao yaliyo haki yao”.
Hapo mstari wa 27 unasema.. wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao..Unadhani walioishia kuwa mashoga walianzia wapi? Walianzia kwenye dhambi ya uzinzi na uasherati lakini wakakataa kumtii Mungu alipokuwa anaugua ndani ya mioyo yao, wakapata malipo ya upotevu wao..Vivyo hivyo na dhambi nyingine zote, huwa zinakwenda hatua nyingine iliyo ovu Zaidi, kama mtu huyo hatataka kumtii Mungu na kubadilika..
Biblia pale inaendelea kusema..
“28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, 30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, 31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; 32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”.
“28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”.
Ndugu tumtii Yesu Kristo ambaye alituokoa bure kwa damu yake. Anatuwazia mawazo yaliyo mema, ikiwa tutamwamini na kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha yeye mwenyewe atatusafisha na kutusamehe kabisa na kutufanya kuwa wapya tena haijalishi tulimkosea namna gani..
Hivyo Ikiwa leo hii utahitaji kumpa Yesu Maisha yako, basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu katika roho na kweli, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Fanya hayo yaliyo ya msingi na yaliyosalia Bwana atashughulika nayo maishani mwako.
Ubarikiwe sana
NDUGU,TUOMBEENI.
MTANGO WA YONA.
HAKI HAIMWACHI KUISHI.
Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?
MAOMBI YA YABESI.
DOWNLOAD PDF
WhatsApp
Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”.
Hebu tujifunze kitu kuhusu milango mitano ya ufahamu tunayoijua…ambayo ni Pua, ngozi, ulimi, macho na masikio…milango hii kazi yake ni kukupa uhakika au kukujulisha mambo yanayoendelea katika mazingira yanayokuzunguka hata kabla hujayakufikia..
Hebu tuchukue mfano unatembea barabarani kwa miguu na mbele yako umbali wa kama mita 100 kuna moto mkubwa umewashwa….Sasa kwa kutumia macho yako mawili unaweza kuuona ule moto na kuepukana nao kabla hata hujaufikia…maana yake ni kwamba macho yamekupa uhakika ya hatari itarajiwayo kabla hujaifikia..
Hali kadhalika unaweza ukafumbwa macho lakini kwa kutumia masikio yako ukasikia sauti ya moto ukiteketeza kitu kwa mbali na hivyo ukachukua tahadhari katika hiyo njia unayoiendea kabla hata hujafika eneo la tukio…hapo napo masikio yamekupa uhakika wa hatari uliyopo mbele yako kabla hata hujaifikia.
Sio hilo tu!..unaweza kufumbwa macho na ukazibwa masikio lakini kwa kutumia pua yako unaweza kuunusa moto mita kadhaa mbele kabla hata hujaufikia…ukasikia harufu ya moshi na vitu vinavyoteketea na hata ukajua ni nini kinaungua kama ni takataka au miti au vitu vya plastiki n.k…Lakini ukajua kabisa kuwa kuna moto mkubwa mbele na hivyo ukajihadhari kabla hata hujafika eneo la tukio..
Na pia sio hilo tu peke yake…unaweza ukafumbwa macho, ukazibwa masikio na pua zako zisifanye kazi lakini kwa kutumia ngozi ukapata majibu yale yale ambayo pua, macho na masikio yaliyapata..kwa kutumia ngozi unaweza ukahisi joto linaongezeka kila unapozidi kukaribia tukio na hivyo ukachukua tahadhari aidha ya kusimama au kubadili njia au kuahirisha safari…Na hivyo ukapata uhakika wa hatari inayokuja…
Sasa huo ni mfano tu mmoja mwepesi ambao umetumia hisia nne..ipo inayotumia hisia zote tano..sasa mfano huo ni unaonyesha ni namna gani inawezekana kabisa kulitambua jambo hata kabla halijafikiwa…ni utashi wa mwili ambao Mungu kamwekea kila mwanadamu kwamba kabla mabaya hayajamfikia kwa ghafla achukue tahadhari…na kama umechunguza Mungu hajamzuia mtu kuifuata hatari..alichofanya ni kumpa hisia za kuihisi kabla haijamfikia au hajaifikia…kujamzuia mtu kuingia kwenye moto unaowaka mbele yake…huo ni uchaguzi wa mtu binafsi…(ukikuta moto unawaka mbele yako na wewe ukajitupa juu yake, huo ni uchaguzi wako). Ukikaa kwenye reli na unaiona Treni inakuja kwa kasi na honi inapiga tangu mbali lakini hutaki kutoka pale, ni uchaguzi wako.
Hali kadhalika biblia imeyafananisha maisha yetu na safari…katika safari yetu ya maisha…Ni roho zetu ndizo zinazosafiri…Miili yetu ipo hapa hapa duniani, inazunguka katika shughuli za kila siku za maisha, lakini roho zetu zinasafiri…Na mbele ya safari yetu (yaani huko tunakoelekea) kuna mambo makubwa mawili 1) MOTO na 2) MBINGU.
Kama vile mwili ulivyo na hisia na Mungu kaziwekea roho zetu hisia vivyo hivyo…Na hisia hizo naamini pia zipo nyingi kama vile hisia za mwili zilivyo nyingi….Hizi hisia za roho ni kutusaidia tujue hatari au baraka zilizopo mbele yetu…na kuchukua uamuzi wa kuziendea au kuzikwepa.
Ndugu mbeleni kuna ziwa la moto…kama hujapewa macho ya kuiona kuzimu katika maono/ndoto, basi Mungu atakujulisha kwa masikio ya rohoni..katika maisha yako utasikia tu habari za kuzimu na ukali wake na zitakupa uhakika kabisa kwamba kuzimu ipo…Hiyo sauti ni lazima utaisikia katika maisha yako….Hali kadhalika kama hutaisikia sauti inayokupa uhakika ya kwamba unalisogelea ziwa la moto…basi utaisiki harufu ya kulikaribia ziwa la moto…na ndio maana katika Maisha yako ya ulevi, ya wizi, ya uasherati, ya kutomcha Mungu, kuna alamu fulani ndani inakuambia kabisa ukiendelea kuishi hivyo utaishia pabaya, hapo ni hisia ya harufu inafanya kazi yake katika roho yako..n.k N.K.
Lakini ukizipuuzia hizo hisia ndugu yangu..na kusema mimi siamini kama kuna kuzimu kwasababu sijawahi kuiona kwa macho…nakuambia ukweli hujawahi kuiona kweli kwa macho yako lakini umeisikia na kuihisi…macho yako yamefumbwa kweli lakini bado hisia nyingine zinakupa uhakika kwamba unaliendea ziwa la moto!…kwasababu huwezi kuuhisi moto mbele yako na kusikia harufu yake na kisha kuzama huko..na kujitetea kwamba hukuuona kwa macho!…ulipaswa uchukue tahadhari kwa kutumia hisia nyingine..ambazo zilikuwa zinakutahadharisha kwamba huko unakoelekea sio!
Ndugu KUZIMU IPO!..Na MBINGU pia IPO!..Ukisubiri uone ndipo uamini utapotea…
Nakushauri kama hujampa Kristo maisha yako au kama bado ni VUGUVUGU hebu chukua muda kasome mistari hii (Ufunuo 3:15-17)...na usiseme nitampa Kristo maisha yangu kesho au nitafanya mabadiliko kesho!…biblia inasema hujui yatakayozaliwa ndani ya siku moja…(Mithali 27:1)..maana yake ni kwamba hata leo unaweza ukafa ghafla au parapanda ya mwisho ikalia..Je utakuwa wapi??..Macho yako hayajaiona mbingu bado…lakini hisia nyingine zilikuambia mbingu ipo….Jiulize Unaposoma ujumbe huu hisia nyingine inakuambia nini?..Je utamlaumu nani siku ile utakapojikuta kwenye ziwa la moto milele?..
Dhambi inavutia sana..na shimo la kuzimu ni kama mtego…hata kabla hujaufikia vizuri ukisema utajikuta limekuvuta ghafla na kuzimu haishibi watu biblia inasema hivyo…Shetani hakupendi hata kidogo..anachokifanya ni kupeleka wengi kuzimu kwasababu anajua yeye hawezi kuokolewa tena!..hivyo anaona wivu kukuona wewe binti/kijana uliyezaliwa tu juzi kukuona utaishi milele..Hivyo geuka leo kwa dhati kama hujageuka, na ukatubu na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu kabla wakati wa hatari haujafika. Mbinguni tumeandaliwa mambo mazuri sana, hata hisia zetu zimeshaanza kuzihisi.
Kumbuka aliyekabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani (yaani Yesu Kristo) anakuja upesi…na anasema maneno haya…
Ufunuo 22.12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. 15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. 16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi. 17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye”
Ufunuo 22.12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye”
Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?
Tunapaswa tufe kwa habari ya dhambi kwasababu kitendo hicho ni kitendo kinacholazimisha UHAI wetu kuhamishwa toka pale ulipokuwa kwanza na kwenda sehemu nyingine..
Kama vile tunavyojua siku zote kitu pekee kinachoweza kuuhamisha uhai wa mtu ni Kifo. Ukifa leo hii Moja kwa moja uhai wako unatoka na kwenda kwingine.., Na hiyo inapelekea watu kutokutujua mahali ulipoelekea, haijalishi watakutafuta vipi kamwe hawatakaa wajue mahali ulipo isipokuwa Mungu peke yake.
Na ndivyo ilivyo pale mtu anapokufa kwa habari ya dhambi, kwa kuzaliwa mara ya pili, Uhai wake unahamishwa na kwenda kuficha na Mungu mwenyewe, mbali na shetani au kitu kingine chochote, kiasi kwamba hata ibilisi akutafuteje rohoni hawezi kukupata kamwe…
Biblia inasema..
Wakolosai 3:3 “Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu”.
Unaona, pale tunapokufa ndipo uhai wetu unapofichwa. Ikiwa tutasema tumeokoka, lakini bado tunaendelea kuyaishi maisha yale yale ya kale, tuwe na uhakika kuwa Mungu hata hana shughuli na uhai wetu..Ikiwa hatutakuwa tayari kuacha uzinzi wetu, uasherati, disko, fashion, matusi, ulevi, ambayo tunafanya mara kwa mara n.k. basi tujue bado shetani anayo mamlaka makubwa sana juu ya uhai wetu..
Anao uwezo wa kututumia vyovyote apendavyo, anao uwezo wa kuyashinda maamuzi yetu, anao uwezo wa kutuletea majaribu ya ajabu ajabu, ikiwemo vifo visivyo vya wakati, anao uwezo wa kuyazuia maombi yetu, anauwezo wa kutufanya tusiyaelewe maandiko. Na zaidi ya yote anakuwa na uwezo wa kuyaingilia maisha yetu kwa viwango kikubwa sana kwa kwa kutumia majeshi ya mapepo yake.
Na ndio hapo utaona, mtu anasema siwezi kushinda dhambi Fulani, siwezi kuacha kuishi maisha Fulani ya dhambi, siwezi kuacha kujichua , Ni kwasababu hakukubali kufa kwanza ili uhai wake uchukuliwe na kwenda kufichwa kwenye moyo wa Mungu.
Mtu aliyefichwa uhai wake, shetani anakuwa haelewi chochote Mungu alichokipanga juu yake, shetani anachofanya ni ku-kisia kisia tu, pengine kesho yake itakuwa hivi au itakuwa vile, lakini haelewi chochote uhai wake unaendelea kuwa moyoni mwa Mungu mbinguni daima, umefichwa huko, ukisubiria wakati maalumu wa kufichuliwa tena.. Kwasababu kitu kinachofichwa ni sharti siku moja kifichuliwe/kifunuliwe.
Na utafunuliwa lini? Biblia inaendelea kusema..
Wakolosai 3:3 “Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu”.
Wakolosai 3:3 “Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu”.
Ipo siku ambayo, watu wote wa Mungu watafahamu kusudi halisi la Mungu kuwaumba ni nini?.. siku watakapoona mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, siku ambayo watakavikwa miili mipya isiyoharibika na kutawala na Kristo kama wafalme na makuhani milele.. Ni siku isiyokuwa na mfano, Hatupaswi kuikosa hata mmoja wetu.
Na ndio maana biblia inazidi kutuambia..katika
Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”.
Lakini kama utausoma tu ujumbe huu au mwingine wowote mfano wa huu, kwa desturi na mazoea ya kila siku, kujitimizia tu ratiba yako, na huku hutaki kufanya badiliko lolote ndani yako, uhai wako bado hauuthamini upo mikononi mwa ibilisi, ufahamu kuwa kila unalolisikia shetani naye analihesabu na kuliandika, ili siku ile utakapojikuta katika mitego yake ya hatari ya kukumaliza, awe na hoja za kutosha za kumwambia Mungu ni kwanini hupaswi kupewa msaada.
Je! shetani anaweza kuyajua Mawazo ya mtu ,hata kama mtu huyo hatayatamka?
JIWE LA KUKWAZA
KABLA YA MAANGAMIZI, KRISTO HUWA ANAONYESHA KWANZA NJIA YA KUTOROKEA.
CHEMBE YA NGANO ISIPOANGUKA KATIKA NCHI, IKAFA,
Bwana Yesu ndiye Mkuu wa Uzima (Matendo 3:15) Kwasababu alitabiriwa kuwa atakuwa Mkuu Zaidi ya wote..(Luka 1:15)..Na kwasababu hiyo basi Mungu alimpaka Mafuta ya Ukuu kuliko wote (Waebrania 1:9)..na uweza wa ajabu aliuweka juu yake….”Uweza wa kuwaweka huru waliofungwa na uteka wa shetani.(Luka 4:18).. Na kwa jina lake ametupa sisi wote tulio mwamini, mamlaka ya kuzitenda kazi zake zote…na utukufu ule aliokuwa nao ametupa sisi (Yohana 17:22)..Hivyo tuna nguvu kama za Simba zisizokuwa na mwisho, za kufanya makubwa kama aliyoyafanya Mkuu wa Uzima Yesu.
Kwasababu alisema..
Marko 16:17 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”.
Marko 16:17 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”.
Kwasababu hiyo basi mimi kama mmoja wa waliomwamini yeye, na kupewa mamlaka hayo…
Amini kuwa Ameyafanya hayo yote…Na yatakuwa kama ulivyoamini.
ZABURI 18: 1 “WEWE, BWANA, NGUVU ZANGU, NAKUPENDA SANA; BWANA NI JABALI LANGU, NA BOMA LANGU, NA MWOKOZI WANGU, MUNGU WANGU, MWAMBA WANGU NINAYEMKIMBILIA, NGAO YANGU, NA PEMBE YA WOKOVU WANGU, NA NGOME YANGU”
Maran atha!
YESU MPONYAJI.
KISIMA CHA MAJI YA UZIMA NI KILE KILE CHA ZAMANI.
USITOKE NJE YA HIFADHI YA MUNGU.
WAZAZI WA YOHANA NA YAKOBO.
Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?
VITA VYA IMANI NI VITA ENDELEVU.
Je! Mtume Paulo alikuwa ni Mrumi, myahudi au raia wa Tarso? Nachanganyikiwa kusoma pale Paulo anajitaja kama raia wa Rumi tena wa kuzaliwa wakati yeye ni myahudi?…
JIBU: Tukisoma katika matendo tunaona Mtume Paulo akijitambulisha kama yeye ni mwenyeji wa Tarso mji wa Kilkia..
Matendo 21:39 “Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa.
Kama tunavyoweza kusoma hapo ni wazi kuwa mtume Paulo hakuzaliwa Israeli wala Rumi(Italia) Bali alizaliwa mji wa Tarso sehemu ijulikanayo kama Kilikia ambao kwasasa ungekuwepo maeneo ya kusini kidogo mwa Uturuki”.
Hivyo uraia wake wa Rumi aliutolea wapi?
Ifahamike kuwa enzi zile Mtu kuwa Mrumi ulikuwa ni mtu wa daraja la juu sana kuliko raia mwingine wowote chini ya jua, na pia ulikuwa na haki kuliko watu wengine. Kwasababu enzi hizo Ngome ya Rumi ndio iliyokuwa inatawala dunia, hivyo ukiwa raia wa Rumi ulikuwa na raia wa daraja la juu sana.
Kwanza ilikuwa hauruhusiwi kupigwa au kufungwa bila kushtakiwa, tofauti na raia wa mataifa mengine..Kitendo cha kumpiga tu raia waki-Rumi bila kumshitaki adhabu yake ilikuwa kali sana iadha kifungo au kifo wakati mwingine.
Pili raia wa Rumi alikuwa na uwezo wa kukata rufaa, ikiwa hajaridhika na mashtaka aliyohukumiwa nayo, anao uwezo wa kukata rufaa. Tofauti na raia wengine hukumu ikitolewa imetolewa, kama ni kufa utakufa tu, kama adhabu basi utaadhibiwa tu! hakuna cha rufaa. Na hiyo ndio iliyokuwa inawafanya mitume wengi, na watakatifu wengi wauawe wakati wa kanisa la kwanza kwasababu hawakuwa warumi.
Vilevile kwa Rufaa hiyo anao uwezo wa kufikisha mashitaka yake hata kwa kaisari mtawala mkuu mwenyewe kule makao makuu Rumi, ana akasikilizwa na kupewa haki yake.
Na katika nyaraka zao za historia ya Rumi inayonyesha kuwa raia wa Rumi alikuwa anapewa vipaumbele vya kwanza kuingia mikataba mingi ya kisheria pasipo kuwa na vizuizi vingi tofauti na wale wengine..
Hivyo enzi zile kuwa raia wa Rumi ilikuwa ni bahati sana,ni Zaidi ya sasahivi labda mtu kupata uraia wa mataifa makubwa yaliyo endelea.
Vilevile uraia huo ulikuwa unapatikana aidha kwa kuzaliwa au kwa fedha nyingi..Soma.
Matendo 22:27 “Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. 28 Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa”.
Matendo 22:27 “Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo.
28 Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa”.
Sasa tukirudi katika swali Paulo alitolea wapi Uraia wa Rumi wa kuzaliwa angali yeye hakuwa Mrumi wala hakuzaliwa katika taifa la Rumi(Italia) wakati ule?
Biblia inatupa mwanga juu ya mji wa Tarso Paulo aliozaliwa kwamba ulikuwa ni mji USIOKUWA MNYONGE..
Matendo 21:39 “Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa”.
Unaona mji huo wa Taso ambao ulikuwa Upo Kilkia ni mji ambao haukuwa kama miji mingine iliyokuwa chini ya ngome ya kirumi, bali huu ulifanywa kuwa Huru, japo biblia haielezi ni kwasababu gani uliachwa huru, lakini ni mji ambao raia wao waliachwa huru kuchagua uraia wao wenyewe (Ndio maana ya kutokuwa mnyonge)…Na ndipo huko huko Paulo alijipatia uraia wa Rumi wa kuzaliwa.
Jambo lingile la kujifunza ni kuwa japo mtume Paulo alikuwa na uraia wa Rumi na kwamba alikuwa na haki zote za kukataa mashtaka yoyote ya mapigo na vifungo yaliyomkuta, lakini aliruhusu wakati mwingine kupigwa hadi kutoka damu na kutupwa gerezani.. Na mwishoni ndio anajitambulisha kwa waliomshitaki, kuwa yeye ni Mrumi, nao wanaogopa sana.. (Soma Matendo 16:16-40)
Lakini kwa kufanya vile utaona alipata faida mara mbili, kwanza alijiongezea thawabu kwa Mungu kwasababu alipigwa kwa ajili ya ushuhuda wa Kristo, na pili, alimwokoa yule askari wa magereza na familia yake yote.
Hivyo na sisi wakati mwingine tunaweza tukawa na nguvu za kuzuia mashtaka yetu aidha kwa vyeo vyetu au kwa ukubwa wetu, au kwa mamlaka yetu, au kwa kujua kwetu sheria lakini hatupaswi kufanya hivyo kila wakati, isipokuwa tu pale inapopasa tukiwa na sababu maalumu kama ilivyokuwa kwa Paulo wakati walipotaka kumshtaki wampige tena wamuue alipokwenda Yerusalemu, lakini alikataa na kusema mimi ni Mrumi, na akakata rufaa ya kwenda Rumi, si kwa lengo la kwenda kujitetea bali kwa lengo la kwenda kuwafikishia injili watu wa Rumi.(Soma Matendo 22-26 )
Bwana atubariki.
Je! Mtume Paulo alimwabudu malaika aliyetembea naye?
Mtume Paulo alioa?
Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema katika 1Wakorintho 15:31″…NIKAKUFA KILA SIKU?
SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.
Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?