DON’T BE AFRAID WHEN YOU GO DOWN.

Hapa ana maana gani kusema hivi? ” Usiseme moyoni mwako,Ni nani atakayepanda kwenda Mbinguni? (yaani ni kumleta Kristo chini), “au,Ni nani Atakayeshuka kwenda Kuzimu? (yaani, ni kumleta Kristo juu,kutoka kwa wafu.). {Warumi10:6-7.}

JIBU: Ukisoma kuanzia hiyo mistari wa kwanza wa kitabu cha Warumi Mlango wa 10, Utaona kuwa Mtume Paulo alikuwa anazungumza habari za juu ya Wayahudi ambao wanaamini katika kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria na wala sio kwa Imani.   Sasa Mtume Paulo alichokuwa anataka kuonyesha ni kwamba..Torati Musa aliyopewa na Mungu, imezungumza habari zote mbili yaani habari ya kuishi kwa sheria kwamba Mtu akiitenda sheria zilizoandikwa katika mbao zile ataishi katika hizo..Yaani Mtu akifanya maagizo yote ya torati basi atafanikiwa katika maisha yake.. Na pia torati hiyo hiyo mahali pengine pia imezungumzia kuhusu haki ipatikanayo kwa njia ya Imani kwamba..

Sheria za Mungu zikiandikwa ndani ya moyo wa mtu basi naye pia atabarikiwa zaidi..Kwasababu maana halisi ya agano jipya ni kuwa zile zile sheria za Mungu zinakuwa zinaandikwa ndani ya Moyo wa Mtu.   Sasa ukisoma Kitabu cha kumbukumbu utaona Mungu anaizungumzia hiyo Mtume Paulo aliyoinukuu.

Kumbukumbu 30: 11 “Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali.

12 Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya?

13 Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya?

14 Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.

15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya”

Unaona Haki ipatikanayo kwa njia ya Imani kwamba sheria za Mungu zitakuwa karibu sana na mtu mahali alipo, hazipo mbinguni kwamba Bwana Yesu aende akatuchukulie atuletee katika gari la moto, au hazipo kuzimu kwamba Bwana Yesu azifuate atuletee katika mbao kama Musa alivyozileta katika mbao kwa wana wa Israeli ili wazishike.. Hapana sheria zake ataziandika ndani yetu (ndani ya mioyo yetu)..zipo karibu sana na sisi, hakuna haja ya kwenda milimani kuzitafuta kama alivyofanya Musa, wala hakuna haja ya kusubiria mtu atoke mbinguni au kuzimu kutufundisha…yeye Bwana ataziandika mioyoni mwetu kutufundisha mwenyewe..

Hiyo ndiyo maana ya huo mstari.. “Usiseme moyoni mwako,Ni nani atakayepanda kwenda Mbinguni? (yaani ni kumleta Kristo chini), “au,Ni nani Atakayeshuka kwenda Kuzimu? (yaani, ni kumleta Kristo juu,kutoka kwa wafu.) Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo”   Mtume Paulo alielezea vizuri zaidi juu ya agano hilo jipya katika kitabu cha 

Waebrania 8:8 “…Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba a Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; NITAWAPA SHERIA ZANGU KATIKA NIA ZAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAZIANDIKA; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena”

Ubarikiwe!


Mada Nyinginezo:

NOTI YA UFALME WA MBINGUNI

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

KIFAA BORA CHA MATUMIZI.


Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, maandiko yanasema,

Mhubiri 10:10 “Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa”.

Katika tafsiri nyingine hilo Neno Chuma limetafsiriwa kama shoka, ikiwa na maana kuwa kama shoka ni butu au halinolewi mara kwa mara basi itampasa mtu kutumia nguvu zaidi katika kukata vitu au kuchonga, au kuchanja kama anakata nyama itampasa atumie nguvu zaidi kuikata nyama ile, kama anakata mti basi itampasa atumie jitihada ya ziada yenye kuchosha kuudondosha mti kwasababu Shoka ni butu haliwezi kupenya kwa haraka ndani ya shina..Tofauti na kama kifaa hicho kingekuwa ni kikali, angetumia nguvu chache tu na matokeo kuwa makubwa ndani ya muda mfupi…

Ni kama tu kisu au kiwembe kikiwa ni kakali basi ukipitisha hata kwenye karatasi ni mara moja tu limegawanyika, lakini kama ni butu basi utakipeleka mbele na nyuma, na utachukua muda, na bado halitachanika vizuri kama lile lililochanwa na kiwembe kikali..

Lakini Mhubiri anaendelea kwa kusema, “walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa”,.. Ikiwa na maana usipoweza kutumia hekima, kuamua maisha yako kwa kukifanya kisu chako kuwa kikali basi mambo yako, licha tu ya kuwa magumu lakini pia utatumia nguvu nyingi kuyafikia…

Duniani Vipo visu vingi tofauti tofauti na mashoka tofuati tofauti na kila mtu analo lake, ambalo kwa namna moja au nyingine linamsaidia kufanya mambo yake kuwa mepesi, wengine ni elimu, wengine ni ujuzi, wengine ni fedha n.k..Lakini hasara moja ya vifaa hivyo vyote sio vya kudumu, huwa vinakuwa butu kwa jinsi muda unavyokwenda na kwa jinsi vinavyotumika…. Mtu akiviacha vinachakaa na pia isitoshe havitumiki kila mahali…huwezi kutumia elimu kutibu kifo, vile vile huwezi tumia pesa kununua furaha, au upendo au amani..

Ni kifaa kimoja tu ambacho Mtu mwenye akili na Hekima anaweza kukitumia kwa matumizi yote na kukata kila kitu pasipo kutumia nguvu, na bado kutokupungua ubora wake na makali yake…Nacho ni Neno la Mungu..

Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”

Mtu akiwa na Neno la Mungu peke yake, hiyo ni salaha tosha, ya kurahisisha mambo yako..hili haliwi butu kama vile mengine, linao uwezo sio tu wa kukata kwa ukali zaidi ya upanga wowote, bali pia linaweza kuchoma hata kuzigawanya nafsi na roho, yaani linaingia ndani ya moyo wa mwanadamu na kugawanyisha kila kitu na kutambua mawazo yake, kitu ambacho pesa haiwezi kufanyi, elimu ya dunia hii haiwezi kufanya, ujuzi wowote ule wa mwanadamu hauwezi kufanya..

Ndio maana mtu yeyote aliyejaa Neno la Mungu ndani yake, hakuna jambo lolote linaloweza kumlemea hata liwe gumu kiasi gani kwasababu anafahamu vizuri silaha aliyonayo inaubora kiasi gani..

Mhubiri anatushauri NI HERI KUTUMIA HEKIMA NA KUFANIKIWA, tunapaswa tujue ni kifaa gani kitakachotufaa katika maisha yetu, katika mapori yanayotuzunguza mbele yetu ambayo yanapaswa yafyekwe kweli kweli, kifaa ambacho tunaweza kukabiliana na adui yetu ibilisi na kummaliza haraka sana bila kutumia nguvu nyingi… silaha hiyo si nyingine zaidi ya Neno la Mungu. 

Waefeso 6: 17 “Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;”

Tunapoliishi Neno la Mungu, maisha yetu hatutayaona ni magumu, hatutasumbuka kama ulimwengu unavyosumbuka, Kwani ni Mungu mwenyewe ndiye atakayekuwa anatupigania,,Lakini tunapoliweka Neno la Mungu kando, tunapolidharau na kuchagua mambo mengine, au kuyaona mambo mengine ni ya muhimu zaidi ya Neno lake, tuwe na uhakika kuwa safari yetu itaishia ukingoni…Ni kutumia kifaa butu, kuufyeka msitu…Mambo yatakuwa magumu tu, huo ndio ukweli, Nira iliyo nyepesi ipo kwa Bwana Yesu tu, pengine kote ni Nzito na mateso yasiyoelezeka..(Mathayo 11:28)

Ndugu/Kaka Ikiwa hujayakabidhi maisha yako kwa BWANA Mlango wa Neema upo wazi, usisubiri baadaye au kesho, muda umekwenda sana kama unyakuo hautakukuta moja ya hizi siku, hujui baadaye yako itakuwa vipi, waliokufa leo asubuhi sio kwamba walikuwa waovu zaidi yako wewe, au walikuwa wameshajiandaa kwa safari ya kwenda huko ng’ambo, hapana lakini kifo kiliwakuta kwa ghafla tu, na ndivyo kitakavyotukuta wote walio haki na wasio haki…Hivyo fanya uamuzi wa busara wakati huu kwa kutubu dhambi zako kama hujatubu na kumgeukia Bwana sasa hivi.. kumgeukia Bwana Yesu sio kuwa vuguvugu, ni kitendo cha kumaanisha kabisa….Kisha utafute mahali wanapobatiza ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa Jina la YESU KRISTO, kama pia bado hujafanya hivyo..Upate ondoleo la dhambi zako, kulingana na (Matendo 2:38) ili Bwana akupe kipawa cha Roho wake Mtakatifu ambaye ndio muhuri wetu, Mungu anaotutia mpaka ile siku wa ukombozi wetu (Waefeso 4:30).

Bwana azidi kukubariki.

Maran atha!

HOME

Print this post

SEHEMU ISIYO NA MAJI.


Maji yanawakilisha uhai, mahali ambapo hapana maji hapana uhai hiyo inajulikana na watu wote….Sayari zilizopo huko juu hazina maji, na ndio moja wapo ya sababu inazozifanya zisiwe na uhai…Hivyo hata hii dunia tunayoishi iliumbwa kutoka katika maji.

2 Petro 3: 5 “Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;

6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia”.

Mwanzo 1: 1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji”.

Kwahiyo sehemu yoyote isiyo na maji ni makazi ya kifo…Kadhalika katika roho, yapo maji ya rohoni, ambayo hayo mtu yeyote asiyekuwa nayo, moyo wake unakuwa ni nchi kavu, au nchi kame, makao ya kifo… Na hivyo Roho Mtakatifu hawezi kushuka mahali palipo pakame, yeye anashuka mahali penye maji, kama alivyotua wakati wa kuitengeneza upya dunia ya kwanza, alitua juu ya uso wa vilindi vya maji, ndipo akaanza uumbaji….Maji na Roho vinakwenda pamoja, (1 Yohana 5:9

“Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja.) ndio maana kuna umuhimu sana wa kubatizwa ubatizo wa maji mengi na si wa kunyunyiziwa ndipo Roho aingie ndani ya mtu, kwasababu dunia ya kwanza biblia inasema Roho Mtakatifu hakutua juu ya chemchemi, au juu ya unyevunyevu bali juu ya uso wa vilindi, ikiwa namaana kuwa ni dunia yote ilikuwa imejaa maji sio sehemu baadhi tu! hapana Bali yote..ndipo uumbaji ukaanza.

Mtu aliyempa Kristo Maisha yake kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi, na kwa jina la Yesu Kristo, hapo mtu huyo ni sawa na anaujaza moyo wake na maji ya uzima..Moyo wake unakuwa umejaa maji mpaka juu kabisa, vilindi vya maji ya uhai vinakuwa juu yake, na hivyo tayari Roho Mtakatifu kushuka juu yake na kuanza uumbaji, anakuwa amezaliwa mara ya pili na kuwa kiumbe kipya. Roho Mtakatifu anaanza kusema na iwe Nuru juu yake, na inakuwa hivyo, Roho Mtakatifu anaanza kutenga maji na maji,na kutengeneza ndani yake mito, chemichemi, na vipindi vya mvua, na kuchipusha kile ki-kijani ndani yake n.k

Bwana Yesu alisema katika 

Yohana 7: 38 “Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”.

Sasa tumeshaona ni namna gani Roho ya mtu aliyezaliwa mara ya pili mbele za Mungu inaonekana kama ni mahali penye maji, penye uhai na mahali ambapo ni makazi ya Roho Mtakatifu, na tumeshaona kuwa Ili Roho Mtakatifu akae ndani ya mtu ni lazima ubatizo sahihi wa kimaandiko wa maji mengi uhusike..Kama Ilivyokuwa katika uumbaji.

Vivyo hivyo mtu yeyote ambaye hajamwamini Yesu Kristo, wala hajabatizwa inavyopaswa wala hajapokea Roho Mtakatifu, moyoni mwake ni nchi kavu..Na hakuna namna yoyote ile ambayo Roho Mtakatifu atatua juu yake…Na kama Roho Mtakatifu hatatua juu yake basi ni Dhahiri kuna roho nyingine zitatua juu yake…Na hizo si zaidi ya roho chafu za Mapepo…Roho za Mapepo ndizo zinazotafuta sehemu kavu isiyo na maji na kushuka juu yake..Tusome..

Mathayo 12:43 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”.

Unaona hapo?..Biblia inasema anapitia sehemu isiyo na maji, na hiyo si nyingine Zaidi ya mtu ambaye hajamwamini Kristo, na hajabatizwa na kupokea Roho Mtakatifu.Kitu kimoja watu wengi wasichokijua ni kwamba shetani sasa hayupo kuzimu…wala haungui moto sasahivi…shetani yupo hapa hapa duniani na baadhi ya mapepo yake, yapo mapepo baadhi biblia imesema kuwa ndio yapo kuzimu sasa kwenye vifungo, lakini sio yote! (2 Petro 2:4) Idadi kubwa ya mapepo yapo huru ulimwenguni, yakisubiri siku ya mwisho ifike yakusanywe yote pamoja na shetani yakatupwe katika lile ziwa la moto.

Haya yaliyopo huru sasa hayatamani kwa namna yoyote kwenda huko kuzimu(au kwa lugha nyingine shimoni), kwasababu yanajua mateso yaliyopo kule, ndio maana yalimsihi sana Bwana wakati ule yasipelekwe shimoni (soma Luka 8:30-32).

Na kitu kingine kisichojulikana na wengi ni kuwa, mtu yeyote ambaye hajampa Kristo Maisha yake, anayo mapepo ndani yake, anaweza akawa anayo machache au mengi, na yanatofautiana ubaya, yapo yaliyo mabaya sana na yapo ya wastani, yapo ambayo madhara yake ni ngumu kuonekana kwa wazi na yapo ambayo madhara yake yanaonekana waziwazi, lakini yote katika yote mtu ambaye hajampa Kristo Maisha yake, mwili wake ni makao ya roho chafu…aidha anajua au hajui..Na wengi wenye mapepo hawajijui kama wanayo, Mpaka siku watakapobadilika ndio watakapojijua kuwa hawakuwa sawa hapo kwanza.

Sasa mtu anayempa Kristo Maisha yake leo na kukusudia kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu mapepo yanamtoka, na kumbuka mapepo yakimtoka mtu sio lazima yalipuke! Hapana! Kufikiri hivyo ni kufikiri kichanga! Mapepo mengi yanawatoka watu pasipo hata kulipuka wala kuonesha mabadiliko yoyote ya mwili, baada ya kipindi Fulani tu mtu ndio atajiona amekuwa tofuati kuliko alivyokuwa hapo kwanza. Kwahiyo baada ya mapepo haya kutoka ndani ya mtu hayaendi kuzimu wala hayaendi jangwani, yanakwenda kutafuta mahali ambapo hapana maji, na huko si kwingine Zaidi ya mtu ambaye hajampa Kristo Maisha yake au kwa Wanyama, kwasababu Wanyama hawana Roho Mtakatifu, kipawa hicho hawajaahidiwa wao…Lakini yanapendelea Zaidi watu kuliko ya Wanyama…Kwahiyo mtu huyo kila siku anakuwa anaongeza mapepo juu ya mapepo ndani yake pasipo kujijua, ndio maana mtu ambaye hajampa Kristo Maisha yake, hali yake ya kiroho kila siku inazidi kuwa mbaya…Kwanini? Kwasababu kila siku anaongoza idadi ya mapepo ndani yake?

Unaweza kutengeneza picha yule mtu Bwana Yesu aliyemwombea alikuwa ana mapepo wangapi? Biblia inasema ni jeshi! Sasa hebu fikiri nguruwe pale walikuwa 2,000 na kila nguruwe tuseme kaingiwa na mapepo mawili tu! Kwa hesabu hizo jumla ya mapepo yaliyokuwa ndani ni wazi kuwa ni Zaidi ya mapepo 4,000 ndani ya mtu mmoja!.. na kila pepo linatabia yake..

Hivyo ndugu ambaye hujampa Kristo Maisha yako au ambaye mguu mmoja leo huko mwingine kule…hayo ndio madhara yatakayokupata endapo hutaamua kufanya maamuzi thabiti sasa…Kama hali yako itazidi kuwa mbaya kila kukicha, shetani yupo na anafanya kazi sasa…Mkabidhi Yesu Kristo Maisha yako ukabatizwe kama hujafanya hivyo, ili akupe na Roho wake Mtakatifu ili vijito vya maji ya uzima vianze kububujika ndani yako. Na ufanikiwe katika roho yako, na mwili wako usiwe makazi ya roho chafu za shetani. Nguvu za shetani sasa zinafanya kazi sana, kuliko kipindi cha nyuma, na hiyo yote biblia inatumbia ni kwasababu anajua kuwa muda wake umebakia mchache, na ndio maana utaona leo hii matendo mengi maovu ya ajabu ajabu yanatokea ulimwenguni, vitu ambavyo huwezi ukadhani kama mwanadamu anaweza kuvifanya..Hivyo fanya bidii uingie katika ulinzi wa Damu ya Yesu Kristo kwa kutubu na kumwamini Yeye.

Bwana akubariki sana.


Mada Zinazoendana:

MAJI YA UZIMA

UBATIZO SAHIHI

JE! NI SAHIHI MTU KUBATIZWA KWENYE MAJI YA KISIMANI?

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

MKUU WA GIZA.


Rudi Nyumbani

Print this post

Je!, Inakubalika kumtolea mtu mwengine damu?(blood transfusion).

JIBU: Ikiwa Bwana alituagiza tupendane sisi kwa sisi hata tufikie hatua ya kuweza kutoa uhai wetu kwa ajili ya wengine wapone kama yeye alivyofanya kwetu sisi, Sasa! damu itakuwa ni kitu gani kwetu?. Tumeambiwa tusipende kwa neno au kwa ulimi tu bali kwa tendo.   Biblia inatuambia

1Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.

17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?

18 Watoto wadogo, TUSIPENDE KWA NENO, wala kwa ulimi, BALI KWA TENDO NA KWELI.”  

Ni sawa na kumwona ndugu yako amepungukiwa damu na, hivyo asiposaidiwa atakwenda kufa muda si mrefu, na wewe angali unao uwezo huo wa kumsaidia na hautaki unasema sitoi damu yangu ni dhambi, hivyo nakuombea tu,kisha Mungu akupumzishe salama, je! hapo utakuwa umeonyesha upendo gani kwa ndugu yako huyo?. Huoni kama utakuwa umependa kwa Neno na wala si kwa tendo?.   Lakini wapo watu wanafanya hivyo kama biashara kwa kisingizio cha kuwa wanasaidia watu, wanatoa damu zao, wanatoa figo zao, si kwa lengo la kumsaidia ndugu yake, bali kwa lengo la kufanya biashara. Hiyo ni dhambi mbele za Mungu na wanaofanya hivyo siku zinakuja watuvuna walichokipanda.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

NI RAHISI KWA NGAMIA KUPENYA KATIKA TUNDU LA SINDANO, JE! NI SINDANO IPI HIYO INAYOZUNGUMZIWA?

JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOANA?

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA

SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!

RABONI!


Rudi Nyumbani:

Print this post

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

Tukisoma kitabu cha Mithali sura ya 30 tunamwona mtu mmoja aliyeitwa Aguri bin Yake akiandika mithali ambazo ni mahusia aliyompa mtu mmoja anayeitwa Ithieli. Kati ya mambo mengi aliyokutana nayo katika maisha yake kuna manne yaliyomshangaza sana nayo ni haya tunayoyasoma katika mstari wa 18,


Mithali 30:18 “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.

19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.


Ukiisoma hii mistari kwa juu juu utaona unaweza usione jambo lolote la kushangaza, lakini ukiitafakari kwa undani utagundua kweli alivyoviona vinamshangao mkubwa sana katika mienendo yao. Hapo amevitaja vitu vine, Kwanza ni TAI, pili NYOKA, tatu MERIKEBU, na nne MTU pamoja na Mwanamke..


Aguri alitafakari kutembea kwao kukamshangaza sana, kwa mfano alimtazama Tai jinsi anavyoweza kwenda kwa kasi hewani, akaona japokuwa amepewa miguu lakini haitegemei miguu yake katika mwendo wake, leo hii hakuna mnyama yoyote wala ndege yeyote mwenye mwendo wa kasi kama Tai,Vile vile akamtazama Mnyama nyoka, ambaye nawe pia unamfahamu jinsi alivyo hana miguu, lakini nyoka kama koboko anakimbia karibia mara 2 zaidi ya mwendo ya wanadamu wengi..Hivyo Aguri akaona kumbe hata miguu sio nyenzo pekee ya kuamua mwendo wa kiumbe hai, kwamba bila hicho mambo hayawezi kwenda..


Akachunguza tena, Merikebu bahari akaona haina magurudumu kama vifaa vingine vya usafiri mfano ma gari, baiskeli, treni au pikipiki lakini inauwezo wa tembea tena kwa kasi tu..hata ingepewa matairi bado yasingeweza kumsaidia katika mwendo kasi wake, kama tu vile miguu isivyomsaidia Tai kutembea kwa kasi, na kama vile miguu isivyotumika kwa nyoka kukimbia kwa kasi, jongoo anayefanana na nyoka mwenye miguu mingi kuliko nyoka na kuliko Wanyama wengi lakini bado hawezi kukimbia..


Hivyo Aguri akamalizia kuchunguza na mwendo wa mwingine ambao ulimshangaza naamini zaidi ya yote nayo ni ni mwendo wa Mtu pamoja na msichana, hapo ukisoma katika tafsiri nyingi inaeleza kwa undani zaidi inasema jinsi mtu na msichana wanavyopendana, au mwenendo wao katika upendo.


Mara nyingi nimekutana na watu wakikosoa ndoa za wengine, labda utaona mmoja anasema mbona kulikuwa na wanawake wazuri kuliko Yule kwanini amemwoa yule bibi-kizee?, mwengine atasema kwanza alishakuwa na watoto huko nyuma ni kitu gani kilichomfanya ampendee, mwingine anatasema alikuwa ni kahaba maarufu anayejulikana mtaa mzima, imekuwaje huyu jamaa kampenda?, mwingine atasema Yule mwanaume hana mwelekeo, hana pesa Yule mwanamke kampendea nini?..Mwingine atakuwa kweli anayopesa lakini mwanamke /mwanamume Yule hakumpenda kwa ajili ya mali zake, Hayo ni maswali ambayo yapo kila mahali, Uliyempenda wewe mwingine atajiuliza ulimpendea nini?


Hilo ndio jambo linaloshangaza, kati ya wawili wapendanao. Kile kinachodhaniwa kuwa kingekuwa chanzo cha wao kuwa pamoja kinagundulika kuwa sio.


Na ndivyo ilivyo Kristo na kanisa lake..Kristo ndio Mume wa kanisa, ametuoa sisi tulio kanisa lake..


2 Wakoritho 11:2 “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.”


Yeye hakutazama kuwa sisi tulikuwa ni wachafu kiasi gani, au tulikuwa hatustahili kiasi gani?, Aliacha enzi yake na utajiri wake wote, na mamlaka yake, kuja duniani kutukomboa sisi, mambo ambayo hata malaika hawana majibu nayo, kwanini alitupenda… akatoa uhai wake kwa ajili yetu sisi tusiostahili..Ukatazama ni kitu gani kizuri alichokiona kwetu, huwezi kukiona, ukitazama ni faida gani basi ataipata kutoka kwetu huwezi kuiona, ametupenda tu kwasababu ametupenda…Huo ni mwendo wa ajabu sana.


Vivyo hivyo na Kanisa lake halisi linarudisha upendo wa namna hiyo hiyo kwake. Japo sasa hatumwoni kwa macho lakini tunampenda, wengi watajiuliza mbona huyo Yesu mnayemtumika hamumwoni? Jibu ni kwamba Upendo tulio nao kwake hautegemei macho kujidhihirisha, ni zaidi ya macho, na hata kama tutamwona kwa macho bado hatutategemea macho yetu kumpenda yeye..Kuna kitu ndani yetu kinachotufanya tutamani kuwa naye siku zote, hakielezeki kwa namna ya kibinadamu.


1Petro 1:8 “Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,”


Vile vile hatumpendi Bwana Yesu kwasababu ya utajiri wake,.Upendo wetu kwake ni zaidi ya hapo..


Hivyo wewe ndugu ambaye bado upo nje ya Kristo umeshajua ni kwasababu gani unaona ni ngumu kumtumikia Mungu usiyemwona au usiyetembea naye? ni kwasababu hujaingizwa bado kwenye pendo lake., Siku ukiingizwa hutahitaji macho ili kutembea naye, hutahitaji akupe kwanza kitu Fulani ndipo umpende..Kwani atajidhihirisha kwako kwa namna ya ajabu ambayo hata macho hayafikii hicho kilele.


Unasubiri nini? Yeye anasema “Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.(Zaburi 34:8)”


Mkaribishe sasa maishani mwako aanze kutembea na wewe mwendo ambao hata watu wa nje watashangaa unawezaje kuwa naye katika hali zote, utafanyika kuwa Bibiarusi na utaingia kwenye pendo ambalo litakusangaza hata wewe ambalo hutatamani hata utoke.


Warumi 8: 38 “ Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,

39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.


Ufunuo 22: 17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.”


Ubarikiwe.Tafadhali “Share” na kwa wengine..


Mada Nyinginezo:

JAWABU LA MAISHA YA MTU.

AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

MSTARI HUU UNA MAANA GANI? “YUKO MWENYE HAKI APOTEAYE KATIKA HAKI YAKE”?

DHAMBI ISIYO NA MSAMAHA.

MATUMIZI YA DIVAI.

WALIOITWA NI WENGI, ILA WATEULE NI WACHACHE.


Rudi Nyumbani:


Print this post

Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?

JIBU: Kwanza tunapaswa kufahamu kuwa si mapenzi ya Mungu sisi tupitie shida yeyote ile.Lakini zipo shida na dhiki ambazo Mungu huwa anaziruhusu ziwapate wale wateule wake kwa kutimiza kusudi Fulani, aidha kwa kuwafundisha, au kwa kuonyesha utukufu wake, au kwa kuwaonya, lakini mwisho wa siku shida hizi huwa zinaishia na mwisho mwema, na ndio maana mtume Paulo alisema mahali fulani katika 

2Wakorintho 12:9 “ Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

Kadhalika zipo shida ambazo zinatokana wanadamu wenyewe, au tunaweza kusema zinasababishwa na wanadamu wenyewe na hizo hazipo ndani ya uwezo wa Mungu kuzizua bali kwa mwanadamu mwenyewe unajua ni kwasababu gani? Jaribu kuwazia mfano huu. Kama vile sisi wanadamu wenyewe kwa wenyewe hatupendi kuchaguliwa baadhi ya mambo kwamfano kijana anapofikia hatua ya kuoa au kuolewa, mzazi mwenye busara hatoweza kwenda kumlazimisha mtoto wake aoe mke amtakaye yeye hata kama msichana huyo atakuwa ni mzuri kiasi gani, au atakuwa na maadili kiasi gani, suala la maamuzi ni la mtu binafsi. Hivyo kitu pekee atakachoweza kufanya kama mzazi mwenye busara ni kumshauri tu, na kumpa mapendekezo mema lakini si kumlazimisha, hata kama anajua huyo mke mtoto wake aliyekwenda kumchagua atakuja kumletea madhara makubwa kiasi gani mbeleni, bado hana uwezo wa kumlazimisha asimwoe. 

Na ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, mara zote anaona madhara yanayokuja mbele yetu, na ni kweli anatamani kuyazuia, lakini jambo analoweza kulifanya yeye kama Mungu wetu, ni kututahadharisha, au kutuonyesha jinsi mwisho wake utakavyokuwa, ili tusipotee au tusidondoke kwenye madhara. Sasa suala la kuamua kuendea au kutokuiendea njia hiyo ni la mtu binafsi. Ikiwa mtu atakubali mashauri ya Mungu basi, Mungu atamwepushia mabaya yale lakini ikiwa hatakubali basi Mungu atamwacha aangamie, hata kama Mungu atakuwa na uwezo mkubwa kiasi gani wa kumwepusha, bado hatoweza kufanya hicho kitu.

Kwasababu Mungu katuumbia sisi ndani yetu uwezo wa kuchagua.Ikiwa mtu ni mzinzi, na huku Mungu alishamwonya kuwa wazinzi hawataurithi ufalme wa mbinguni, na mtu huyo bado anaendelea katika njia zake mbovu, Hapo Mungu hawezi kumzuia japo anajua kabisa njia yake mwisho wa siku ataishia kifo, halafu aende kwenye ziwa la moto. Alimwonya shetani, hata kabla hajawa shetani, lakini hakumlazimisha asihasi, japo alijua kuwa ataasi na mwisho wa siku kuishia motoni,Mungu alimwonya lakini hakutaka kusimama katika kweli kama malaika wengine watakatifu walivyokuwa. Na ndivyo ilivyo hata kwetu,Mungu katuwekea maamuzi yetu binafsi. Kukubali au kukataa. Hakuna kulazimishwa.

Ubarikiwe


 

Mada zinazoendana:

JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI, KWAMFANO AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE KUZAMA?

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

MVUTO WA TATU!


Rudi Nyumbani:

Print this post

Katika Warumi 8:18-25. Je! Viumbe vinatazamiaje kwa shauku kufunuliwa kwa Mwana wa MUNGU?

JIBU: Jambo lisilofahamika na wengi ni kwamba, viumbe navyo vitakuwepo katika ulimwengu ujao (Mbingu Mpya na nchi Mpya)..Mungu alipoiumba dunia hakuwaumba wanadamu peke yao, bali aliwaumba pamoja na wanyama na ndege, Na Mwanadamu alipoasi, laana aliyolaaniwa haikumpata Mwanadamu peke yake bali hata na wanyama, mwanadamu alipoambiwa atakufa, na wanyama pia walikufa, Mwanadamu alipoambiwa atazaa kwa uchungu wanyama nao pia walizaa kwa uchungu.  

Mungu alipoiangamiza dunia kwa gharika, wanyama nao waliangamizwa..na kadhalika Mungu alipowaokoa baadhi ya wanadamu wachache katika safina (Nuhu na wanawe) pia kulikuwepo na baadhi ya wanyama waliookoka na gharika. Hivyo mahali popote mwanadamu alipo wanyama nao wapo, kwasababu waliumbwa kwa ajili ya mwanadamu.   Kwahiyo kama vile sisi wanadamu tunavyotamani siku ya kufunuliwa kwetu, yaani siku tutakayoiingia Mbingu Mpya na Nchi Mpya, siku ambayo hatutakiona tena kifo, wala uchungu, wala shida na wanyama na viumbe vyote vivyo hivyo vinatamani kama sisi. Navyo vinatamani kutoka katika laana hii ya dhambi, na kuingia uhuru wa Umilele.

  Biblia inasema katika ulimwengu ujao ulimwengu utakuwa na Amani, kutakuwa hakuna dhiki kwa wanyama, wala tabu. Wanyama hawatakulana tena, simba atakula majani kama ng’ombe, na mbwa mwitu atakaa pamoja na mwanakondoo.

  Isaya 11: 6 “Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.

7 Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe.

8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.

9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari”.

Kwahiyo wanyama na viumbe vyote vinatamani siku ya kuwekwa kwao huru kufike, kama sisi tunavyotamani siku hiyo ifike.

  Mungu akubariki.


Mada Nyinginezo:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

NUHU ALIWALETAJE WANYAMA WOTE KWENYE SAFINA

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

SEHEMU ISIYO NA MAJI.

KISASI NI JUU YA BWANA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Akawaambia Enendeni ulimwenguni mwote,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE.(Marko16:15.) Yesu Anamaanisha nini kusema MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?

JIBU: Wakati ule Mtume Petro alipokuwa kule Yafa katika nyumba ya Yule mtu mtengenezaji ngozi, siku moja aliumwa na njaa sana, na alipotaka kwenda kuandaa chakula biblia inasema alizimia na kuona maono, na ndani ya maono yale aliona kitu kama nguo kubwa ikishuka kutoka juu na ndani yake imebeba viumbe vya aina zote duniani, wanyama wa kila namna. Na Bwana akamwambia Petro aende kuwachinja ale. Lakini kama tunavyosoma Petro alimjibu Mungu na kumwambia tangu azaliwe hajawahi kula vitu vilivyo najisi. Na ndipo hapo Mungu akamwambia nilivyovitakasa mimi usiviite wewe najisi.(Matendo 10). 

Sasa pale ni jambo gani BWANA alikuwa anataka kumwonyesha Petro, Tukisoma ile habari, kuanzia mwanzo utaona kuwa kulikuwa na mtu mmoja mcha Mungu aliyeitwa Kornelio, Ni mtu ambaye hakuwa myahudi, wala hakujua sheria zozote za kiyahudi, Ni Mtu wa mataifa, lakini kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu alipewa neema ya kuwa mmojawapo wa wateule wa Mungu. Sasa kumbuka kabla ya hapo watu wa mataifa kule Israeli walijulikana kama najisi, hivyo hawakuruhusiwa kuchangamana na wayahudi kwa namna yoyote ile ya ibada. Lakini Mungu alimwambia Petro nilivyovitakasa mimi usiviite wewe najisi najisi, Ondoke uende katika nyumba ya Kornelio akawahubirie injili, akawabatize na wao pia wapokee habari njema za Yesu Kristo waokoke. Hivyo vile viumbe vya aina tofauti tofauti alivyoviona Petro, najisi, na visivyo najisi, vitambaavyo, virukavyo, vyenye miguu minne, nguruwe, bundi, popo, mbuzi, pweza,karungu-yeye, kivunja-chungu n.k.

Vilikuwa vinawakilisha jamii tofauti tofauti za watu waliopo duniani. Na ndio maana baada ya Petro kupata ufunuo huo ndio utaona kuanzia huo wakati nao pia wakaanza kuhubiri injili kwa watu wa mataifa pia, jambo ambalo hapo kabla walikuwa hawafanyi, walikuwa wakihubiri wa wayahudi tu peke yao. Japo YESU alishatangulia kuwapa maagizo hayo kabla lakini hawakumwelewa. Sasa ndio tukirudi kwenye huo mstari ambao Bwana aliwaambia mitume wake siku ile aliyokuwa anapaa kwenda mbinguni akisema “Enendeni ulimwenguni mwote,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE.” Alimaanisha waende wakahubiri injili kwa kila jamii ya watu waliopo ulimwenguni bila kuchagua hawa ni wayahudi, hawa si wayahudi, bila kujali rangi, dini zao, utamaduni wao, taifa lao, lugha zao n.k. Ilimradi ni mwanadamu basi injili ni lazima imfikie. Lakini Bwana hakumaanisha tukawahubirie kuku, na panya, na mijusi, na konokono injili.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

AGIZO LA UTUME.

INARUHUSIWA KULA NYAMA YA NGURUWE KWA MKRISTO WA KWELI?

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU

MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.

MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Wala msimwite mtu baba duniani; Bwana anamaanisha nini kusema hivyo?

JIBU: Neno hilo halimaanishi kuwa hatupaswi kabisa kumwita mtu yeyote baba duniani hata wazazi wetu, hapana kama ni hivyo basi Mungu angekuwa anapingana na Neno lake pale aliposema “Waheshimu baba yako na mama yako (Kutoka 20:12)”

unaona?. Lakini tunapaswa kufahamu maneno hayo Bwana aliwalenga watu wa namna gani, ukisoma mistari hiyo kuanzia juu utaona kuwa aliwalenga wale mafarisayo na masadukayo ambao wao, walipenda kuchukua nafasi ya Mungu duniani kwa kila kitu, walitaka watu wawaone kama pasipo uwepo wao, hawawezi kumjua Mungu, pasipo watu kuongozwa na wao hawawezi kumfikia Mungu, yaani kwa ufupi walikuwa wanachukua nafasi ya Kristo duniani. Na ndio maana tukisoma tangu juu tunaona Bwana akiwaambia maneno haya..

Mathayo 23:1Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema,

2 Waandishi na Mafarisayo WAMEKETI KATIKA KITI CHA MUSA;

3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.

4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.

5 Tena matendo yao yote huyatenda ILI KUTAZAMWA NA WATU; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;

6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,

7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.

8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.

9 WALA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI; MAANA BABA YENU NI MMOJA, ALIYE WA MBINGUNI.

10 WALA MSIITWE VIONGOZI; MAANA KIONGOZI WENU NI MMOJA, NAYE NDIYE KRISTO”.

Mambo hayo hayo ndio tunayoweza kuyaona leo hii katika Kanisa la kirumi (Katoliki), ofisi ya kiPapa inajulikana kama “ofisi ya baba mtakatifu” na watu humweshimu yeye kama mpatanishi wa dhambi zao, na anaonekana kama ni mtu aliye na kibali cha karibu zaidi kwa Mungu zaidi ya watu wengine wote, hivyo amepewa heshima ya kipekee, anaketi mbele katika masinagogi (Katika umoja wa makanisa) ili atazamwe na ulimwengu wote kuwa yeye ni baba mtakatifu. Sasa Heshima kama hizo ambazo zinazohusianishwa na uhusiano na vyeo mbele za Mungu kwamba mtu Fulani ni mwenye cheo Fulani cha kipekee mbele za Mungu zaidi na wengine, ndizo Kristo alizokuwa anazikemea, kwamba tusimwite mtu yeyote Baba kwa namna hiyo, au kiongozi, au Rabi. Kwasababu sisi sote ni ndugu na hakuna aliye juu ya mwenziwe.  

Pale Mtume Paulo alipomwita Timotheo na Tito wanae, alikuwa anaonyesha uhusiano aliokuwa nao kama mtumishi wa Mungu aliyewazaa katika injili, na kuwalea, kwa mfano wa Baba kwa mwanawe, lakini hakuwa na maana kuwa yeye yupo juu ya mwenzake, wala hakutanua hirizi zake wala kuongeza matamvua yeye, kiasi cha kukaa masokoni kupewa heshima na watu, kwamba ni sharti aanze yeye mbele za Mungu kisha wao, na kwamba pasipo yeye hawawezi kumfikia Mungu, Hapana na hakuna mahali popote Paulo alisisitiza yeye aitwa aitwe Baba.

Utaona nyaraka zake zote Mtume Paulo, alianza na “Mimi Paulo, mfungwa na Mtumwa wa Yesu, sehemu nyingine anasema mimi Paulo mtume wa Yesu Kristo”..Lakini hutaona sehemu yoyote anaanza kwa kusema “Mimi Paulo, Baba Mtakatifu wa kanisa takatifu korintho”..hapana hutaona hicho kitu.  

Lakini inasikitisha zaidi kusikia leo hii watu wanagombania kuitwa baba, na wengine kwa nguvu, hata kama huyo mtu hana mahusiano yeyote ya kiiamani na yeye anayetaka amwite, bado atataka aitwe tu baba, hayo ndiyo Kristo aliyoyakataa, hiyo ni roho ya mpinga-kristo.

Lakini ikiwa ubaba wowote hautahusianishwa na kuchukua nafasi yoyote ya Kristo, huo hauna shida yoyote, ni kama tu vile unavyomwita mzazi wako baba au mama, hiyo haikuchukui nafasi yeyote linapokuja suala la kumwabudu Mungu, kwasababu unajua Baba yako aliye mbinguni ndiye anayestahili kupewa heshima zote za ibada na za kiungu.

Vivyo hivyo ikiwa utatoa heshima yako kwa kiongozi wako yeyote, au mwalimu wako, kanisani, hakikisha kuwa hilo halichukui nafasi ya Kristo, mnapokuja kwenye suala la kumwabudu Mungu basi sisi wote ni ndugu na tunapaswa kupeleka heshima zote, shukrani zote, na maombi yote kwa Mungu na sio kwa mwanadamu yeyote kama kanisa katoliki lifanyavyo kwa mapadre wao na Papa, na baadhi ya makanisa ya kiroho ambayo yanamfanya mtu mmoja kama ndio kila kitu kwao, huku wakimwita baba na pasipo yeye wanajihisi hawawezi kumwabudu Mungu. Hizo ni ibada za sanamu.

  Ubarikiwe sana.

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ni kwa nini tunasema tunamwabudu MUNGU aliye hai ,Je! wale wanaomwabudu shetani sio mungu wao aliye hai?

JIBU: Embu tutafakari mfano huu, utatusaidia kupata majibu ya maswali yetu. Tunajua kuwa Dunia tunayoishi sasa hivi ni dunia ya utandawazi na kugunduliwa kwa Kompyuta kumefanikisha kurahisisha mambo mengi sana, Komputa sasa inAaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu pekee angeweza kufanya, unaweza ukaiuliza swali lolote na ikakusaidia kupata sehemu kubwa ya majibu yako, inaweza kukusaidia kufanya mahesabu yako, inaweza ikakusaidia kuwasiliana na mtu mwingine aliye mbali, inaweza ikakuonyesha picha, inaweza ikakuhifadhia kumbukumbuku zako, inaweza ikakusaidia kutafiti, na hata kufanya kazi n.k. Kwa ufupi komputa sasa tunaweza kusema ni chombo ambacho kina ufanisi mkubwa karibia na mwanadamu, tunaweza kusema kina uhai fulani, Na uhai huo ni wazi kabisa hakijapewa na mwingine zaidi ya mwanadamu. 

Lakini pamoja na hayo tunajua hata kiwe na ufanisi mkubwa kiasi gani, bado tu uhai wake hauwezi kuwa halisi kama wa mwanadamu mwenyewe, vipo vitu vingi kitashindwa kufanya ambavyo mwanadamu angeweza kufanya, kwamfano Komputa haiwezi kufariji, haiwezi kupima hisia za mtu, komputa haiwezi kuonyesha fadhili, komputa ukiiomba chakula haiwezi kukupa, komputa haiwezi kuona mambo ya mbeleni ili kuchukua tahadhari n.k..yenyewe inaongozwa na kwa yale tu mwanadamu aliyoyapachika ndani yake, nje ya hapo haiwezi kujichagulia mambo yake yenyewe. Vivyo hivyo tukirudi kwa Mungu wetu.

Tunajua sisi sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, na kama vile alivyo hai, na sisi basi tutakuwa hai, lakini uhai tulionao si kama ule wa kwake, sisi ni mfano wa Komputa zilizotengenezwa na Mungu, tunaouwezo wa kuonyesha tabia zote za Mungu lakini haimaanishi tutakuwa na ule uhai halisi kabisa kama wa Mungu mwenyewe, wa kufikia hatua ya kuweza hata kuumba, kufanya kila kitu, kuona mambo yote ya mbeleni yanayokuja, kuchipusha chakula ardhini, hatuwezi pia kujihakikishia uzima wetu wa milele kama sio kutoka kwake. Hivyo tunavyosema Tunamwabudu Mungu aliye HAI, tunamaanisha Mungu awezaye kufanya mambo yote, Mungu anayetoa uhai katika mambo yote, Mungu ambaye hashindwi na lolote,Shetani hawezi kuumba chochote,japo anaishi, hajui hata kesho yake itakuwaje sasa ataitwaje mungu aliye hai? Yeye kapewa tu sehemu ya uhai kama sisi tulivyopewa, hawezi kusema sasa nataka jua lizime, au leo mimea yote duniani ikauke,hana uwezo huo hivyo hawezi kuitwa Mungu aliye hai.. Neno zuri labda linaweza kumstahili yeye kuitwa nao hao wanaomwabudu ni “mungu aliyepewa pumzi”, lakini sio Mungu aliye hai aliye hai ni mmoja tu! anayekaa mbingu za mbingu.

Isaya 46:9 “kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; 10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote. 11 Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.”

 Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

JINA LA MUNGU NI LIPI?

USILITAJE BURE JINA LA BWANA!

NINI MAANA YA ELOHIMU?

SIKU ZA MAPATILIZO.

UPENDO


Rudi Nyumbani:

Print this post