DON’T BE AFRAID WHEN YOU GO DOWN.

HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM

 Katika Biblia, Mungu daima aliuleta Ujumbe Wake kwa watu wa ulimwengu kupitia kwa nabii wa kizazi hicho. Yeye alisema na Musa kupitia kichaka kilichowaka moto na akampa agizo la kuwaongoza Waebrania kutoka Misri. Nguzo ya Moto iliyo dhahiri pamoja na ishara zingine zilitolewa kuthibitisha huduma yake. Yohana Mbatizaji alileta Ujumbe kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya kule kuja kwa Masihi. Wakati akimbatiza Bwana Yesu katika Mto Yordani, Sauti kutoka Mbinguni ililithibitisha agizo la Yohana la kumtambulisha Mwana-Kondoo wa Mungu, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa kukaa ndani Yake.” Miaka kadhaa baadaye, Sauti ya Bwana ilisikika tena ikizungumza na nabii wakati Yeye aliponena na Paulo kwa Nuru ya kupofusha, na baadaye akampa agizo la kuyaweka makanisa katika utaratibu. Kote katika Agano Jipya na la Kale, Mungu kamwe hajapata kuzungumza na watu Wake kupitia mfumo wa kimadhehebu ama shirika la kidini. Yeye daima amesema na watu kupitia mtu mmoja: nabii Wake. Naye aliwathibitisha manabii hawa kwa ishara za kimbinguni.

LAKINI JE! NI VIPI SIKU HIZI? JE! MUNGU ANGALI ANALIFUNUA NENO LAKE KWA MANABII? JE! KUNGALI KUNA ISHARA ZA KIMBINGUNI? JE! MUNGU ANGEMTUMA NABII WA SIKU HIZI ULIMWENGUNI? JIBU LILILODHAHIRI KABISA NI, “NDIO!”

Manabii wa kale walikuwa ni watu jasiri wa Mungu, wala hawakuhofu kukabiliana na mashirika ya kimadhehebu. Kusema kweli, karibu kila wakati walishutumiwa na makasisi. Eliya aliyapa changamoto mashirika ya kidini ya siku zake, akiwauliza kama Mungu angeiheshimu sadaka yao, ama yake. Walipiga makelele. Walitabiri. Wakaruka-ruka juu ya madhabahu hayo. Wakajikata-kata kwa visu. Bali Mungu hakuwasikia. Eliya aliangalia juu Mbinguni na kusema, “Na ijulikane leo ya kuwa Wewe Ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi Wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.” Ndipo basi akaagiza moto ushuke kutoka Mbinguni na kuiteketeza ile sadaka. Nabii Mikaya alishindana na Mfalme wa Israeli, na ukuhani wote, wakati alipomkemea Kuhani Mkuu Zedekia kwa kutabiri uongo. Huyo kuhani Mkuu alimchapa kofi usoni naye Mfalme akamfunga gerezani kwa kusema kweli. Hata Bwana Yesu alichukiwa sana na mashirika ya kidini ya siku Zake hata wakamsulibisha pamoja na wahalifu wabaya sana. Kama historia ikishikilia kuwa ni ya kweli, nabii angechukiwa na mfumo wa sasa wa kimadhehebu, naye angebandikwa jina la mzushi, nabii wa uongo, ama jina baya zaidi. Ila Mungu angemtetea mtumishi Wake.

KAMA KULIKUWAKO NA NABII KATIKA SIKU HIZI ZA KISASA, ANGEKUBALIKANAJE NA KANISA KATOLIKI? KANISA LA KIBAPTISTI? KANISA LA KILUTHERI, AU NA DHEHEBU LINGINE LOLOTE?

Bwana Yesu aliwaagiza wote wanaomwamini Yeye: “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; Watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.” (Marko 16:17-18). Je! Andiko hili ni la kweli leo? Ikiwa si la kweli, je! Maneno ya Bwana yalikoma kutumika lini? Kote katika Biblia, manabii waliweza kuwaponya wagonjwa, kutoa pepo, na kufanya miujiza. Musa alimweka yule nyoka wa shaba mbele za watu wa Israeli kuwaponya wakiumwa na nyoka wa sumu (Hesabu 21:9). Naamani, Mshami hodari, alimjia Elisha apate kuponywa ukoma (II Wafalme 5:9). Wakati kijana mwanamume mmoja alipoanguka kutoka kwenye dirisha la juu akafa, mtume Paulo alimkumbatia na kuurejesha uhai kwenye mwili uliokufa (Matendo 20:10). Tuna taarifa ya kama miaka 3½ pekee ya maisha ya Bwana wetu Yesu, bali katika miaka hiyo michache, Yeye aliendelea kuwaponya wagonjwa. Vipofu walifanywa kuona. Wenye ukoma waliponywa. Viziwi walipokea kusikia kwao. Viwete walitembea. Kila namna ya ugonjwa iliponywa (Mat. 4:23).

Mungu pia aliwathibitisha manabii wake kwa njia zingine mbali na uponyaji. Hata siri zilizofichwa sana za moyo zilijulishwa watu hawa wa Mungu. Mfalme Nebukadreza alikuwa na ndoto iliyomsumbua, lakini asingeweza kukumbuka ilikuwa inahusu nini. Nabii Danieli alimfumbulia mfalme huyo ndoto hiyo pamoja na unabii uliofuata (Dan 2:28). Hakuna kitu alichofichwa Sulemani wakati Malkia wa Sheba alipokuja mbele zake. Yeye alikuwa amejazwa sana na Roho hata yeye alimpambanulia maswali ya moyoni mwake kabla hajayauliza (I Wafalme 10:3). Elisha alimfichulia Mfalme wa Israeli mipango yote ya Mfalme wa Shamu, hata maneno ya binafsi aliyonena katika chumba chake cha kulala (II Wafalme 6:12).

Kupitia matendo Yake mwenyewe, Bwana Yesu mara nyingi alionyesha ya kwamba Roho huyu wa utambuzi ni Roho wa Kristo. Yeye aliitambua tabia ya Nathanaeli wakati aliposema, “Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake!” Ndipo Yesu akaendelea kumwambia Nathanaeli mahali alipokuwa wakati Filipo alipomwambia kuhusu Masihi (Yohana 1:48). Wakati Nathanaeli alipoona ya kwamba Yesu aliujua moyo wake, papo hapo alimtambua kuwa Ndiye Kristo. Mara ya kwanza Yesu alipomwona Petro, alimwambia jina la baba yake, Yona (Yohana 1:42). Ndipo Petro alipoacha mambo yote na kumfuata Yesu maishani mwake mwote. Yesu alikutana na yule mwanamke Msamaria kisimani na kumwambia dhambi zake za wakati uliopita. Maneno yake ya kwanza yalikuwa, “Bwana, naona kwamba wewe u nabii” (Yohana 4:19). Watu wote hawa watatu walikuwa wametoka katika tabaka mbali mbali za maisha, hata hivyo walimtambua Yesu mara moja wakati alipoonyesha karama ya utambuzi.

Je! karama hii ilitoweka wakati ukurasa wa mwisho wa Biblia ulipoandikwa? Iwapo miujiza hii imeandikwa dhahiri jinsi hii katika Biblia, iko wapi siku hizi? Nabii wa siku hizi hakika angethibitishwa kwa miujiza.

Je! Mungu amewasahau watu Wake? Je! angali anaweza kuponya wagonjwa? Je! angali ananena nasi kupitia manabii Wake? Je! yeyote wa manabii hao alitangulia kuiona siku hii?

JE! KUNA NABII AMBAZO HAZIJATIMIZWA BADO?


1) AHADI YA NABII KATIKA SIKU ZA MWISHO 

Maneno ya mwisho kabisa yaliyoandikwa katika Agano la Kale yanatoa ahadi hii: “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.” (Mal 4:5-6)

Siku ya Bwana iliyo kuu na ya kuogofya haijakuja bado, kwa hiyo inatupasa kumtazamia nabii Eliya kwa moyo. Katika Biblia, manabii hawakuyajilia madhehebu makubwa ya kidini. Waliwajilia wachache waliochaguliwa. Wazia kama yule nabii wa Malaki 4 angelikuja, asitambulikane. Vipi kama yeye ni kama wale manabii wa kale, na ni watu wachache tu wanaomtambua? Kama nabii huyu atarudi katika siku za mwisho, tutamjuaje? Jibu lake linaonekana dhahiri katika Maandiko. Yeye atakuwa na tabia ya nabii. Atazijua siri za moyo. Atafanya miujiza. Madhehebu ya kidini yatajaribu kumkosoa. Bali kutakuwako na wachache waliochaguliwa ambao watamtambua kama mjumbe aliyeahidiwa kwa ajili ya siku hizi.

TUTAJUAJE WAKATI ELIYA ATAKAPORUDI? YEYE ATAONYESHA TABIA ZIPI KUSUDI TUWEZE KUMTAMBUA?

Eliya alikuwa ni mtu wa nyikani. Ishara kuu na maajabu yaliifuata huduma yake. Alihubiri dhidi ya maovu ya siku zake. Zaidi sana alihubiri dhidi ya utovu wa uadilifu wa Malkia Yezebeli. Wakati Eliya alipotwaliwa juu Mbinguni katika gari la moto, roho yake ilishuka juu ya Elisha. Ndipo ishara kuu na maajabu yakaifuata huduma ya Elisha, naye pia alihubiri dhidi ya dhambi za ulimwengu. Manabii hao wote wawili walisimama peke yao dhidi ya mashirika ya kidini ya siku hizo. Mamia ya miaka baadaye, roho yule yule alirudi duniani katika Yohana Mbatizaji. Nabii Malaki alibashiri ya kwamba Eliya angerudi kumtambulisha Bwana: “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu…” (Malaki 3:1). Yohana Mbatizaji alitimiza hayo wakati akihubiri toba miongoni mwa watoto wa Mungu. Kama vile Eliya, yeye alihubiri dhidi ya mfalme na madhehebu ya kidini ya siku hizo. Bwana Yesu alithibitisha ya kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye nabii wa Malaki 3 katika Kitabu cha Mathayo (11:10): “Huyu ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakayeitengeneza njia yako mbele yako.” Luka 1:17 inasema ya kwamba roho ya Eliya (Elias) ilikuwa iwe katika Yohana Mbatizaji, “Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto.” Lakini angalia kwamba sehemu ya pili ya Malaki 4 ilikuwa bado haijatimizwa: “…na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.” Sehemu hiyo ya Maandiko itatimia kabla ya kuja kwa Kristo Mara ya Pili.


MIAKA ELFU MBILI BAADA YA YOHANA MBATIZAJE, WAKATI UMEWADIA TENA KWA ROHO YA ELIYA KURUDI DUNIANI.

Siku hiyo imewadia! Katika wakati huu, tumeiona roho ya Eliya ikirudi. Yeye aliupinga mfumo wa madhehebu ya kisasa. Alizikemea dhambi za ulimwengu. Alionyesha ishara na maajabu yasiyohesabika. Aliihubiri Biblia neno-kwa-neno kutoka Mwanzo hadi Ufunuo. Nabii wa Malaki 4 alikuja kama ilivyoahidiwa, naye akaleta Ujumbe kutoka kwenye Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu. Jina la nabii huyo ni William Marrion Branham. Sisi tunamwita “Ndugu Branham.”

  •     Oral Roberts, mwinjilisti anayejulikana sana ulimwenguni na mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Oral Roberts.

    “William Branham, niliyempenda na kuamini yeye ni nabii wa Mungu.”

  •     Dr. T.L. Osborn, mwinjilisti wa Kipentekoste na mwandishi hodari.

“William Branham alikuja kwetu kama nabii wa Mungu na akatuonyesha katika karne ya ishirini vitu vile vile dhahiri ambavyo vilionyeshwa katika Injili…Mungu amewatembelea watu Wake, kwa kuwa nabii mkuu ameinuka miongoni mwetu.”

  •     Ern Baxter, mwinjilisti, meneja wa Miamsho ya Branham kwa muda wa miaka saba, pia mmoja wa viongozi wa mwanzoni wa Huduma Mpya ya Kanisa la Kiingereza.   

    “Kabla ya kumwombea mtu, angetoa utondoti sahihi kuhusu maradhi ya mtu huyo, na pia utondoti wa maisha yao – mji wanamoishi, kazi, matendo-hata huko nyuma kabisa utotoni mwao. Branham kamwe hakufanya makosa hata mara moja akiwa na neno la maarifa katika miaka yote niliyokuwa pamoja naye. Hiyo inajumuisha, kwangu mimi, maelfu ya visa.”

Hakuna mtu ambaye ameugusa ulimwengu kwa undani hivyo tangu Bwana Yesu Kristo alipotembea duniani. Kutoka kwenye asili duni katika kibanda cha chumba kimoja kwenye milima ya Kentucky, hadi Amarillo Texas ambako Bwana alimchukua Nyumbani, maisha yake daima yalijaa matukio ya mambo ya kimbinguni. Kwa kuongozwa na Malaika wa Bwana katika mwaka wa 1946, huduma ya Ndugu Branham ilitoa cheche iliyowasha kipindi cha ufufuo mkuu wa uponyaji ulioenea Marekani upesi na kote ulimwenguni. Hata siku ya leo, yeye anatambuliwa na wanahistoria Wakristo kama “baba” na “kiongozi” wa ufufuo wa uponyaji wa miaka ya 1950 ambao ulilibadilisha Kanisa la Kipentekoste na hatimaye ukaizaa huduma ya Karisma, ambayo siku hizi inashawishi karibu kila dhehebu la Kiprotestanti. Hata hivyo, kama ilivyo kawaida yao, madhehebu yanayapuuza mafundisho yake na kulikana agizo lake.

Popote alipoenda, Mungu alithibitisha ya kwamba Ndugu Branham ndiye nabii wa kizazi hiki. Kama vile Ayubu, Bwana alisema naye katika upepo wa kisulisuli. Kama vile Musa, Nguzo ya Moto ilionekana ikimwongoza. Kama vile Mikaya, alishutumiwa na makasisi. Kama vile Eliya, yeye alikuwa ni mtu wa nyikani. Kama Yeremia, aliagizwa na Malaika. Kama Danieli, yeye aliona maono ya usoni. Kama Bwana Yesu, alijua siri za moyo. Na kama vile Paulo, yeye aliwaponya wagonjwa.

Bwana amewatembelea watu Wake tena kupitia nabii. Katika wakati wenye giza sana wa historia, ambapo uadilifu umezama kwenye viwango ambavyo kamwe havijaonekana katika siku za nyuma na silaha za maangamizi ya hadhara zikitishia kwenye upeo wa macho, mtu mnyenyekevu alitumwa kutoka kwenye uwepo wa Mungu kuialika jamii inayokufa ipate kutubu.

Mwanafunzi mpendwa Yohana aliandika kuhusu Bwana Yesu:

Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa. Amina. (Yohana 21:25).

Jambo lilo hilo linaweza kusemwa kuhusu maisha ya Ndugu Branham. Kuna zaidi ya jumbe 1,200 zilizorekodiwa pamoja na maelfu ya hadithi zinazohusu maisha ya mtu huyu hodari. Hata sasa tunaendelea kusikia shuhuda mpya za ushawishi wake juu ya maisha ya mamilioni ya watu. Kijitabu hiki kisingeweza kubabia ushawishi ambao mtu huyu wa Mungu alikuwa nao juu ya ulimwengu.

2) MWANZO WA MAISHA YANGU (WILLIAM BRANHAM)


 

“Nilipozaliwa katika kibanda kidogo cha Kentucky kule juu, Malaika wa Bwana aliingilia dirishani na kusimama pale. Kulikuwako na Nguzo ya Moto.”

Mapambazuko yalikuwa tu ndiyo kwanza yaanze kupenya giza la mbingu baridi za Aprili. Lile dirisha moja la mbao lilifunguliwa lipate kuiachilia nuru ya asubuhi iingie kwenye chumba hicho kidogo sana cha kibanda. Robini aliyesimama karibu na hilo dirisha alionekana amechangamka sana asubuhi hii na alikuwa akiimba kwa mapafu yake yote. Ndani ya kibanda hicho, kijana Charles Branham aliitia mikono yake kwenye ovaroli yake mpya kabisa na kuinama akimwangalia mke wake mwenye umri wa miaka 15. “Tutamwita jina lake William,” akasema baba yake.

Ndani ya hilo dirisha ikaja Nuru ya kimbinguni. Hiyo nuru ilijongea humo chumbani na kuning’inia juu ya kitanda ambapo huyo mtoto ndiyo kwanza azaliwe. Hii ilikuwa ni Nuru ile ile iliyowaleta wana wa Kiebrania kutoka Misri. Ilikuwa ni Nuru ile ile iliyokutana na Paulo akienda zake Dameski. Nayo itaenda kumwongoza mtoto huyu mdogo apate kumwita Bibi-arusi wa Kristo kutoka ulimwenguni. Hiyo Nuru haikuwa ni mwingine ila ni huyo Malaika wa Bwana, ile Nguzo ya Moto; na kwa mara nyingine tena ilikuwa imemtokea mwanadamu.

Na mle ndani, katika kibanda hiki kidogo cha mbao, asubuhi hiyo tarehe 6 Aprili, mkunga alifungua dirisha kusudi nuru iweze kuangazia ndani ili Mama na Baba waione sura yangu. Ndipo Nuru ya karibu ukubwa wa mto iliingia ikizungukazunguka upesi kupitia dirishani. Ilizungukazunguka mahali nilipokuwa, kisha ikashuka kitandani. Watu kadhaa wa mlimani walikuwa wamesimama pale. Walikuwa wakilia.

Makazi hayo duni yalikuwa katika milima ya Kentucky kusini, karibu na mji mdogo wa Burkesville. Ilikuwa ni tarehe 6 Aprili, 1909. Mtoto huyo mchanga alikuwa ndiye wa kwanza kati ya watoto kumi ambao wangezaliwa na Charles na Ella Branham.

Haikuchukua muda mrefu kabla ya Malaika wa Bwana kumtembelea mtoto William Branham tena.

Wakati alipokuwa mtoto mchanga, Malaika wa Bwana kwanza alisema naye, akisema ya kwamba angeyaishi maisha yake karibu na mji unaoitwa New Albany. Aliingia nyumbani na kumwambia mama yake yaliyokuwa yametukia tu. Kama mama yeyote, hakuitilia maanani hadithi hiyo naye akamweka kitandani apate kutuliza neva zake changa. Miaka miwili baadaye, familia yake ilihamia Jeffersonville Indiana, maili chache tu kutoka mji wa New Albany ulio kusini mwa Indiana.

Malaika alisema tena na huyo nabii kijana miaka michache baadaye. Ilikuwa ni siku tulivu ya Septemba huku jua lenye joto likiwaka kupitia kwenye matawi ya majira ya kupukutika. Mtoto huyo alikuwa akichechemea huku amebeba ndoo mbili za maji kupitia kwenye ujia. Gunzi la hindi lilikuwa limefungiwa chini ya kidole chake cha mguu kilichojeruhiwa kisije kikaingia uchafu. Aliketi chini ya mti mrefu wa mpopla apate kupumzika. Machozi yalikuwa yakitiririka kutoka machoni mwake huku akilia juu ya msiba wake: marafiki zake walikuwa wakijifurahisha kwenye shimo la mahali hapo la kuvulia samaki, naye alikuwa amekwama akimchotea baba yake maji. Mara, upepo ukaanza kuzungukazunguka juu yake mtini. Akapangusa macho yake na kusimama kwa miguu yake. Akasikia sauti ya majani yakichakarisha katika upepo…bali hakukuwa na upepo. Akaangalia juu, na yapata nusu ya urefu wa kwenda juu wa huo mpopla, kitu fulani kilikuwa kikizungushazungusha hayo majani yaliyokauka.

Mara Sauti ikanena, “Usinywe pombe wala kuvuta sigara wala kuuchafua mwili wako kwa njia yoyote, kutakuwako na kazi utakayofanya utakapokuwa mtu mzima.” Mvulana huyo aliyeingiwa na hofu mwenye umri wa miaka saba aliangusha ndoo zake akakimbilia kwa mamaye.

Majuma machache baadaye, alikuwa akicheza gololi na ndugu yake mdogo. Hisi ya ajabu ilimjia. Akaangalia huko kwenye Mto Ohio na kuona daraja zuri. Watu kumi na sita walianguka wakafa wakati hilo daraja lilipokuwa likivuka mto. Nabii kijana alikuwa ameona ono lake la kwanza. Alimwambia mama yake, naye akaandika simulizi lake. Miaka kadhaa baadaye, watu 16 walianguka wakafa wakati daraja la Mtaa wa Pili huko Louisville, Kentucky lilipokuwa likijengwa juu ya Mto Ohio.

Bwana alikuwa akimwonyesha maono ya usoni. Na kama vile manabii waliomtangulia, maono hayo hayakukosea kamwe.

3) MIAKA YA UJANA

 

Kote katika maisha yake, Ndugu Branham alitamani kuwa nyikani. Kwenye umri wa miaka 18, aliondoka Indiana kwenda kwenye milima ya magengemagenge ya magharibi. Kukaa kwake Arizona hakukuchukua muda mrefu kabla ya kulazimika kurudi.

Siku moja niliamua ya kwamba nilikuwa nimepata njia ya kuondolea mbali wito huo. Nilikuwa ninakwenda magharibi kufanya kazi kwenye ranchi. Ewe rafiki, Mungu ni mkuu tu huko nje kama alivyo mahali popote. Naomba ufaidike na uzoefu wa maisha yangu. Anapokuita, mjibu.

Asubuhi moja ya Septemba katika mwaka wa 1927, nilimwambia mama yangu ya kwamba nilikuwa ninaenda kwenye ziara ya kupiga kambi huko Tunnel Mill, ambako ni kama maili kumi na nne kutoka Jeffersonville tulikoishi wakati huo. Nilikuwa tayari nimepanga safari ya Arizona pamoja na marafiki fulani. Wakati mama aliposikia kutoka kwangu tena, sikuwa Tunnel Mill bali Phoenix, Arizona, nikimkimbia Mungu wa Upendo. Maisha ya ranchi yalikuwa ni mazuri sana kwa muda, lakini mara yalichujuka, kama ilivyo kwa anasa nyingine yoyote ya ulimwenguni. Ila hebu niseme hapa, Mungu Asifiwe, ya kwamba uhusiano wa maisha na Yesu unazidi kuwa mtamu na mtamu wakati wote wala hauchujuki. Yesu huleta amani kamilifu na faraja siku zote.

Mara nyingi nimesikia upepo ukivuma katika misonobari mirefu. Ilionekana kana kwamba ningeweza kusikia sauti Yake ikiita huko mwituni, ikisema, “Adamu, uko wapi?” Nyota zilionekana zikiwa karibu sana mtu ungaliweza kuzichuma kwa mikono yako. Mungu alionekana kuwa yuko karibu sana.

Jambo moja kuhusu nchi hiyo ni zile barabara jangwani. Mtu ukitoka kwenye barabara, unapotea kwa urahisi. Mara nyingi sana watalii wanaona maua madogo ya jangwani na wanaondoka kwenye barabara kuu kwenda kuyachuma. Wanazurura jangwani na wanapotea na mara nyingine wanakufa kwa kiu. Ndivyo ilivyo katika njia ya Mkristo — Mungu ana njia kuu. Anazungumza juu yake katika Isaya, mlango wa 35. Inaitwa “Njia Kuu ya Utakatifu.” Mara nyingi anasa ndogo za ulimwengu zinakuvuta kukutoa kwenye njia kuu. Ndipo umepoteza mawasiliano yako na Mungu. Jangwani wakati mtu umepotea, mara nyingine kunatokea mazigazi. Kwa wale watu wanaokufa kwa kiu, mazigazi hayo yatakuwa ni mto ama ziwa. Mara nyingi watu huyakimbilia na kutumbukia ndani yao ndipo tu wanakuta kwamba wanaogelea tu kwenye mchanga wenye joto. Wakati mwingine ibilisi anakuonyesha jambo fulani ambalo anasema ni wakati wa kujifurahisha. Hayo ni mazigazi tu, ni kitu ambacho si halisi. Ukisikiliza utajikuta tu ukijilundikia huzuni nyingi kichwani mwako. Usimsikilize, mpendwa msomaji. Mwamini Yesu awapaye maji yaliyo hai hao wenye njaa na kiu.

Siku moja nilipata barua kutoka nyumbani ikisema ya kwamba mmoja wa ndugu zangu alikuwa ni mgonjwa sana. Ilikuwa ni Edward, aliyenifuata kwa umri. Hakika nilifikiri haukuwa mbaya sana, kwa hiyo niliamini atapona. Walakini, jioni moja siku chache baadaye nilipokuwa nikirudi kutoka mjini kupitia kwenye bwalo la chakula kwenye ranchi, niliona karatasi mezani. Nikaichukua. Ilisema, “Bill, njoo huku kwenye malisho ya kaskazini. Muhimu sana.” Baada ya kuisoma mimi pamoja na rafiki yangu tulienda kwenye malisho hayo. Mtu wa kwanza niliyekutana naye alikuwa ni maskini Mteksasi aliyefanya kazi kwenye ranchi hiyo. Jina lake lilikuwa ni Durfy, bali tulimwita “Pop.” Alikuwa na uso wenye huzuni aliposema, “Billy, jamani, nina habari za kuhuzunisha kwako.” Wakati uo huo mnyapara akaja akitembea. Wakaniambia ya kwamba barua ya simu ilikuwa ndiyo kwanza ifike, ikiniambia kuhusu kifo cha ndugu yangu.

Rafiki mpendwa, kwa muda kidogo nisingeweza kusogea. Yalikuwa ndiyo mauti ya kwanza nyumbani mwetu. Ila ninataka kusema ya kwamba jambo la kwanza nililowazia lilikuwa kama alikuwa tayari kufa. Nilipogeuka na kuangalia mbuga hiyo pana ya majani ya manjano, machozi yalitiririka mashavuni mwangu. Jinsi nilikumbuka vile tulivyopambana kwa pamoja tulipokuwa watoto wadogo na jinsi tulivyopata shida nyingi.

Tulienda shuleni bila chakula cha kutosha. Vidole vya miguu vilikuwa vimetokeza kwenye viatu vyetu na ilitulazimu kuvaa makoti yaliyochakaa yaliyofungwa shingoni kwa pini kwa kuwa hatukuwa na mashati. Jinsi nilivyokumbuka pia ya kwamba siku moja mama alikuwa ameweka bisi kidogo katika ndoo ndogo kwa ajili ya chakula chetu cha mchana. Hatukula pamoja na watoto wengine. Tusingeweza kupata chakula kama walichokuwa nacho. Daima tungechurupukia kilimani tupate kula. Ninakumbuka hiyo siku tulipokuwa na bisi, tulifikiri ilikuwa ni tafrija hasa. Kwa hiyo ili kuhakikisha nilipata fungu langu la hizo, nilitoka kabla ya adhuhuri na kuchota konzi nzima kabla ndugu yangu hajapata fungu lake.

Basi nikisimama hapo nikiangalia mbuga pana iliyokaushwa na jua niliwazia juu ya mambo hayo yote na kujiuliza iwapo Mungu alikuwa amempeleka mahali bora zaidi. Ndipo tena Mungu aliniita, lakini kama kawaida, nilijaribu kuupiga vita.

Nilijiandaa kuja nyumbani kwa ajili ya mazishi. Wakati Kasisi McKinney wa Kanisa la Port Fulton, mtu ambaye ni kama tu baba kwangu mimi, alipohubiri mazishi yake, alitamka ya kwamba “Huenda ikawa kuna wengine hapa wasiomjua Mungu, kama wapo, mkubalini sasa.” Loo, jinsi nilivyoshikilia kiti changu. Mungu alikuwa akinishughulikia tena. Msomaji mpendwa, Yeye anapoita, mwitikie.

Sitasahau kamwe jinsi ambavyo maskini Baba yangu na Mama walivyolia baada ya yale mazishi. Nilitaka kurudi Magharibi bali Mama alinisihi sana nikae hata hatimaye nikakubali kukaa kama ningaliweza kupata ajira. Mara nikapata ajira kwenye Kampuni ya Utumishi wa Umma ya Indiana.

Yapata miaka miwili baadaye nilipokuwa nikipima mita katika duka la mita kwenye Mtambo wa Gesi huko New Albany, nililemewa na gesi na kwa majuma kadhaa niliteseka kutokana nayo. Niliwaendea madaktari wote niliowajua. Sikuweza kupata nafuu. Niliumwa na tumbo lenye asidi, iliyosababishwa na athari ya gesi. Hali ilizidi kuwa mbaya wakati wote. Nilipelekwa kwa wataalamu huko Louisville, Kentucky. Hatimaye walisema ni kidole tumbo changu na wakasema ilibidi nifanyiwe upasuaji. Sikuweza kuamini jambo hilo kwa kuwa kamwe sikuwa na maumivu ndani ya ubavu wangu. Madaktari walisema wasingeweza kunifanyia jambo lingine lolote mpaka nifanyiwe upasuaji. Hatimaye nilikubali ufanywe bali nilisisitiza ya kwamba watumie nusukaputi ya kawaida ili kwamba niweze kuufuatilia huo upasuaji.

Loo, nilitaka mtu fulani asimame kando yangu ambaye alimjua Mungu. Niliamini katika maombi bali sikuweza kuomba. Kwa hiyo mhudumu kutoka kwenye Kanisa la Kwanza la Kibaptisti aliambatana nami kwenye chumba cha kufanyiwa upasuaji.

Waliponichukua kutoka mezani wakanipeleka kwenye kitanda changu, nilijisikia nikiendelea kuwa dhaifu zaidi na zaidi wakati wote. Moyo wangu ulikuwa ukidunda kwa shida. Nilihisi kifo kikiwa juu yangu. Kupumua kwangu kulikuwa kukipungua wakati wote. Nilijua nilikuwa nimefikia mwisho wa safari yangu. Ewe rafiki, ngoja mpaka utakapofika hapo wakati mmoja, ndipo utakapofikiria juu ya mambo mengi uliyofanya. Nilijua kamwe sikuwahi kuvuta sigara, kunywa pombe, wala kuwa na tabia zozote chafu bali nilijua sikuwa tayari kukutana na Mungu wangu.

Ewe rafiki yangu, kama wewe ni mfuasi baridi na wa kawaida tu wa kanisa, utajua wakati utakapofika mwisho ya kwamba huko tayari. Kwa hiyo kama hayo tu ndiyo unayojua kumhusu Mungu wangu, ninakuomba papa hapa upige magoti na kumwomba Yesu akupe tukio lile la kuzaliwa mara ya pili, kama vile alivyomwambia Nikodemo katika Yohana mlango wa 3, na loo, jinsi ambavyo kengele za furaha zitakavyolia. Jina Lake na lisifiwe.

4) MIAKA YA UJANA – INAENDELEA

Kulianza kuingia giza zaidi kwenye chumba hicho cha hospitali, kana kwamba kilikuwa ni kwenye msitu mkubwa. Niliweza kusikia upepo ukivuma kupitia kwenye majani, hata hivyo ilionekana ni huko mbali sana mwituni. Huenda umesikia kishindo cha upepo ukivuma kwenye majani, ukizidi kukukaribia. Niliwaza, “Vema, hiki ni kifo kikija kunichukua.” Loo! nafsi yangu ilikuwa ikutane na Mungu, nilijaribu kuomba bali sikuweza.

Kadiri upepo ulivyosogea karibu, ndivyo ulivyozidi kutoa sauti kubwa. Majani yakatatarika na kwa ghafla, nikazimia.

IIlionekana basi kana kwamba nilirudia tena kuwa mvulana mdogo pekupeku, nimesimama kwenye ule ujia chini ya mti ule ule. Nikasikia sauti ile ile iliyosema, “Usinywe pombe kamwe wala kuvuta sigara.” Na majani niliyosikia yalikuwa ni yale yale yaliyovuma katika ule mti siku ile.

Lakini wakati huu ile Sauti ilisema, “Nilikuita nawe hukukubali kwenda.” Ikarudia kwa mara ya tatu.

Ndipo nikasema, “Bwana, kama huyo ni Wewe, nijalie nirudi tena duniani nami nitaihubiri Injili Yako hadharani na pembeni mwa barabara. Nitamwambia kila mtu habari zake!”

Wakati ono hili lilipopita, nilikuta ya kwamba sikuwa nimepata kujisikia vizuri zaidi. Daktari wangu mpasuaji alikuwa angali yumo humo jengoni. Alikuja na akaniangalia na akashangaa. Alionekana kana kwamba alifikiri ningekuwa nimekufa, ndipo akasema, “Mimi si mtu anayeenda kanisani, kazi yangu ni kubwa mno, bali ninajua Mungu amemzuru mvulana huyu.” Kwamba ni kwa nini yeye alisema hivyo, sijui mimi. Hakuna mtu aliyekuwa amesema jambo lolote kuhusu jambo hilo. Kama ningalikuwa nimejua wakati huo ninachojua sasa, ningalitoka kwenye kitanda hicho nikipaza sauti Sifa kwa Jina Lake.

Baada ya siku chache niliruhusiwa kurudi nyumbani, bali nilikuwa ningali mgonjwa na nililazimika kuvaa miwani machoni mwangu kwa sababu ya dosari katika jicho. Kichwa changu kilitikisika nilipoangalia kitu chochote kwa kitambo kidogo.

Nilianza kumwomba na kumtafuta Mungu. Nilienda toka kanisa moja hadi lingine, nikijaribu kupata mahali fulani ambapo palikuwa na wito wa madhabahuni wa mtindo wa kale. Jambo la kuhuzunisha lilikuwa kwamba sikuweza kupata popote.

Nilisema ya kwamba kama ningejaliwa kuwa Mkristo, kweli ningekuwa Mkristo hasa. Mhudumu aliyenisikia nikitoa tamshi hilo alisema, “Sasa Billy jamani, unaelekea kwenye ulokole.” Nikasema ya kwamba kama kamwe nikipata dini, nilitaka kuisikia wakati ikija, kama tu vile wanafunzi walivyofanya.

Loo Jina Lake lisifiwe. Nilipata dini baadaye kidogo na ningali ninayo, na kwa msaada Wake, nitaidumisha daima.

Usiku mmoja nilimwonea Mungu njaa sana na kuonea njaa tukio halisi hata nilitoka nikaenda nje nyuma ya nyumba kwenye kibanda cha zamani na kujaribu kuomba. Sikujua jinsi ya kuomba wakati huo kwa hiyo nilianza tu kuongea Naye kama vile ambavyo ningeongea na mtu yeyote yule. Mara kukatokea Nuru huko bandani na ikafanya msalaba na Sauti iliyotoka msalabani ikasema nami katika lugha ambayo sikuweza kuifahamu. Kisha ikaondoka ikaenda zake. Nilipigwa na bumbuazi. Nilipojirudia tena niliomba, “Bwana, kama huyo ni Wewe, naomba uje uzungumze nami tena.” Nilikuwa nikisoma Biblia yangu tangu niliporudi nyumbani toka hospitalini na nilikuwa nimesoma katika I Yohana 4, “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu.”

Nilijua ya kwamba roho fulani alikuwa amenitokea, na nilipoomba alitokea tena. Ndipo ilionekana kana kwamba kulikuwako na ratili elfu moja zilizonyanyuliwa toka kwenye nafsi yangu. Niliruka juu na kukimbilia nyumbani na ilionekana kana kwamba nilikuwa nikikimbia hewani.

Mama akauliza, “Bill, umepatwa na kitu gani?” Nikajibu, “Sijui bali kwa kweli ninajisikia vizuri na mwepesi.” Singeweza kukaa hapo nyumbani tena. Ilibidi nitoke nje na kutimua mbio.

Nilijua basi ya kwamba kama Mungu alinitaka nihubiri, angeniponya. Kwa hiyo nilienda kwenye kanisa lililoamini katika kupaka mafuta, nami nikaponywa papo hapo. Niliona basi ya kwamba wale wanafunzi walikuwa na kitu fulani ambacho wahudumu wengi sana siku hizi hawanacho. Wanafunzi walibatizwa na Roho Mtakatifu na kwa hiyo waliweza kuponya wagonjwa na kufanya miujiza mikuu katika Jina Lake. Kwa hiyo nikaanza kuomba kwa ajili ya ubatizo wa Roho Mtakatifu na nikaupata.

Siku moja yapata miezi sita baadaye, Mungu alinipa shauku ya moyo wangu. Alisema nami katika Nuru kuu, akiniambia niende nikahubiri na kuwaombea wagonjwa Naye angewaponya haidhuru walikuwa na ugonjwa wa namna gani. Nikaanza kuhubiri na kufanya yale ambayo aliniambia nifanye. Ee rafiki, siwezi kuanza kukwambia yale yote yaliyotendeka: Macho mapofu yalifumbuliwa. Viwete walitembea. Kansa zimeponywa, na kila namna ya miujiza imetendwa.

Siku moja mwishoni mwa Barabara ya Spring, Jeffersonville, Indiana, baada ya uamsho wa majuma mawili, nilikuwa nikibatiza watu 130. Ilikuwa ni siku yenye joto ya Agosti na kulikuwako na watu kama 3,000. Nilikuwa karibu na kumbatiza mtu wa 17 wakati mara moja niliisikia ile Sauti ndogo, tulivu tena na ikasema, “Angalia juu.” Mbingu zilikuwa kama shaba kwenye siku hiyo yenye joto ya Agosti. Hatukuwa na mvua kwa yapata majuma matatu. Niliisikia Sauti hiyo tena, na halafu tena mara ya tatu ikasema, “Angalia juu.”

Nikaangalia juu na nyota kubwa inayoangaza ikashuka kutoka mbinguni, ambayo nilikuwa nimeiona mara nyingi hapo kabla bali sikuwa nimewaambia habari zake. Mara nyingi nimewaambia watu juu ya kuonekana kwake nao wangecheka tu na kusema, “Bill, unawazia tu hayo. Ama labda ulikuwa unaota.” Lakini Mungu asifiwe, wakati huu alikuwa amejionyesha wazi kwa wote, kwa sababu ilikuja karibu sana nami hata sikuweza kuzungumza. Baada ya sekunde chache kupita nilipaza sauti na watu wengi wakaangalia juu na kuiona hiyo nyota juu yangu kabisa. Wengine walizimia wakati wengine wakipiga makelele na wengine wakakimbia. Ndipo hiyo nyota ikarudi mbinguni na mahali ilipokuwa imeondoka palikuwa ni futi kumi na tano mraba na mahali hapa pakaendelea kusogea na kuvurugika ama kana kwamba mawimbi yalikuwa yakifingirika. Mahali hapa palikuwa pamefanya wingu dogo jeupe na hiyo nyota ilitwaliwa juu katika wingu hili dogo.

Kama vile Yohana Mbatizaji, nabii huyu alithibitishwa kwenye maji ya Ubatizo.

5) KUZURIWA NA MALAIKA

 

Maono yaliendelea. Aliambiwa na makasisi wenzake ya kwamba maono yake hayakutoka kwa Mungu. Aliambiwa alikuwa amepagawa na roho mchafu. Hili lilimsumbua sana. Mzigo huo ukawa mzito sana asingeweza kuubeba, kwa hiyo akaenda nyikani akayatafute Mapenzi ya Mungu. Alikuwa amejitolea sana hivi kwamba aliapa kutorudi bila jibu. Ilikuwa ni kule, kwenye kibanda cha kale cha kutega wanyama, ndipo Malaika wa Bwana alipompa agizo lake. Miongoni mwa mambo mengine, Malaika huyo alimwambia hivi: “Ukiwafanya watu wakuamini wewe, na uwe mwaminifu unapoomba, hakuna kitakachosimama mbele ya maombi yako, si hata kansa.”

Tashwishi zote ziliondoka. Sasa alikuwa na agizo na kwa ujasiri akajitokeza. Uamsho wa uponyaji ulikuwa umeanza.

Mamia ya maelfu walihudhuria miamsho ya Branham. Maelfu waliponywa katika Jina la Bwana Yesu Kristo. Wainjilisti wengine kama vile Oral Roberts, T.L. Osborn, na A.A. Allen mara wakamfuata Ndugu Branham na kuanzisha miamsho yao wenyewe ya uponyaji. Bwana alizimimina baraka Zake kuliko hapo awali. Mkono wa uponyaji wa Yesu Kristo mara nyingine tena ulikuwa umewagusa watu Wake.

  • Kasisi F.F. Bosworth, mwinjilisti anayejulikana ulimwenguni kote na mmoja wa wazee waanzilishi wa dhehebu la Assemblies of God pamoja na mfumo wa siku hizi wa Upentekoste.


“Mara nyingi nimelia kwa furaha kuhusu karama ya hivi karibuni ya Mungu kwa kanisa la ndugu yetu mpendwa, William Branham, pamoja na karama yake ya ajabu sana ya uponyaji. Hili ni jambo la Mungu kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo (Efe. 3:20), kwa maana kamwe sijapata kuona wala kusoma juu ya chochote kinachofanana na huduma ya uponyaji ya William Branham.”

  •    Kasisi Gordon Lindsay, mwandishi hodari, mhudumu, na mwanzilishi wa Chuo cha Kristo kwa Mataifa Yote.

 “Katika tukio moja, tuliangalia wakati akizungumza na mtu fulani aliyelala kwenye machela. Mwanzoni hakukuwako na ishara yoyote ya jibu la kueleweka kutoka kwa mtu huyo. Baadaye maelezo yalitoka kwa mkewe aliyekuwa amesimama hapo karibu, ya kwamba mtu huyo hakuwa tu akifa kwa kansa, bali alikuwa ni kiziwi wala asingeweza kusikia yaliyokuwa yakisemwa.

Ndugu Branham basi akasema ya kwamba ingefaa mtu huyo kupokea kusikia kwake ili kwamba aweze kumwelezea kuhusu kuponywa kwa kansa yake. Kulikuwa na muda mfupi wa maombi. Mara moja mtu huyo aliweza kusikia! Machozi makubwa makubwa yalitiririka mashavuni mwa mtu huyo ambaye uso wake jioni nzima ulikuwa haushiriki kitu kabisa na haukuonyesha hisia yoyote. Alisikiliza kwa shauku kuu alipokuwa akiambiwa juu ya ukombozi wake kutokana na kansa.”

  •     William D. Upshaw, Mbunge wa Marekani (1919-1927), alipigania Urais wa Marekani katika mwaka wa 1932. Alikuwa ni kiwete tangu alipoanguka akavunja mgongo wake akiwa mtoto. Alikuwa na umri wa miaka 84 wakati alipoponywa kabisa kutokana na maombi ya Ndugu Branham, baada ya kuwa kiwete kwa muda wa miaka 66. Kamwe hakuhitaji tena kiti cha magurudumu ama mikongojo hata mwisho wa maisha yake.

“Ndugu Branham akasema, ‘Huyo Mbunge ameponywa.’ Moyo wangu ukaruka. Nikapiga hatua nikatoka na kumkubali Bwana kama Mponyaji wangu. Nikaweka kando mikongojo yangu…ndipo upande wa chini wa Mbinguni ukaanguka!”

  • Georgia Carter, Milltown Indiana, aliponywa ugonjwa wa kufisha wa T.B. mwaka wa 1940 wala kamwe hakuugua ugonjwa huo hata wakati mmoja tena maishani mwake. Anawakilisha makumi elfu ya watu ambao wameponywa kupitia kwa huduma yake na wangali wanaponywa leo.

    “Nilikuwa nimelala chali kwa muda wa miaka minane na miezi tisa nikiwa na T.B. na madaktari walikwishanikatia tamaa. Hata sikuwa nimefikisha uzito wa ratili 50 na ilionekana kana kwamba matumaini yote yalikuwa yamekwisha. Ndipo kutoka Jeffersonville, Indiana, alikuja Kasisi WM Branham katika ono alilokuwa ameona la mwana-kondoo akiwa ameshikwa kichakani na alikuwa akilia ‘Milltown’, ambako ndiko ninakoishi. Ndugu Branham hakuwa amewahi kuja huku wala kujua mtu yeyote aliyetoka huku. Akiingia, aliweka mikono juu yangu na akaomba, akiliitia juu yangu Jina la Bwana wetu mpenzi Yesu. Kitu fulani kilionekana kunishika na kwa ghafla nilikuwa nimeamka na kumshukuru Mungu kwa nguvu Zake za kuponya. Sasa mimi ni mpiga piano kwenye kanisa la Kibaptisti hapa.”

6) ILE NGUZO YA MOTO

 

Mara nyingi Ndugu Branham hutoa sifa za Nguzo ya Moto iliyoithibitisha huduma yake. Ilikuwako alipozaliwa, ilionekana na maelfu ukingoni mwa Mto Ohio, na ilionekana kumfuata kokote alikoenda. Ilikuwa ni mwaka wa 1950 ambapo Bwana aliwapa waaminio na wasioamini vile vile thibitisho lisilokanushika ya kwamba Nguzo hii ya Moto ilikuwa pamoja na nabii huyu.

Usiku huo ulikuwa umegubikwa na ubishi kwenye Jumba Kubwa la Mikutano la Sam Houston. Ndugu Branham alikuwa akiongoza uamsho wa uponyaji uliokuwa ukienea nchini. Baraka za Bwana Yesu zilikuwa zikimiminika kama mvua kwenye mashamba ya ngano ya kiroho. Bali hizo ishara kuu na maajabu hazikutokea bila upinzani. Kama ilivyo kawaida siku zote, adui alimwinua mshindani. Vikosi hivyo viwili vilikutana Houston, Texas, Naye Malaika wa Bwana Mwenyewe akashuka kupiga vita.

Maelfu tayari walikuwako kushuhudia miujiza isiyohesabika iliyomfuata mtu huyu wa Mungu. Siku moja kabla, kundi la wahudumu walimpa changamoto nabii kufanya mjadala juu ya uponyaji wa Kiungu, bali changamoto hiyo ilimwangukia rafiki mzee mwaminifu wa nabii, Kasisi F.F. Bosworth. Hao wenye kushuku wengi waliongozwa na mhudumu wa mahali hapo wa Kibaptisti na ambaye ni mnenaji mkosoaji wa uponyaji wa kiungu. Mjadala huo uliokuwa unakuja ulifichuliwa kwa magazeti, ambayo upesi yalichapisha vichwa vya habari, “Manyoya ya Kitheolojia Yatapeperushwa Saa 1 usiku Wa Leo Katika Jumba Kubwa la Mikutano La Sam Houston.”

Mpinzani alimkodisha mpiga picha mweledi, Ted Kipperman wa Studio za Douglas, apate kunakili mjadala huo kwa picha. Jioni hiyo, picha zilipigwa za Ndugu Bosworth akiwa amesimama kwa ustaha huku huyo mwenye kushuku akiwa katika mikao ya kumtishia; wakati mmoja kidole chake kimekitwa kwenye uso wa mzee huyo mnyenyekevu.

Mjadala huo ulipoanza, Kasisi Bosworth upesi alithibitisha uhakika wa uponyaji wa Kiungu kwa ushuhuda wa Maandiko na halafu, kusudi asiliache swali lo lote, akawaomba wote waliokuwa wameponywa maradhi yao kusimama. Maelfu wakasimama kwa miguu yao. Baada ya hao walioponywa kuketi chini, aliwaomba wale wote waliokuwa wameponywa kwa uponyaji wa Kiungu waliokuwa ni wafuasi wenye sifa njema wa dhehebu la mtu huyu wangesimama. Wafuasi mia tatu wa kanisa hilo wakasimama na kwa fahari wakaonyesha rehema ambayo Bwana Yesu alikuwa amewaonyesha.

Changamoto basi ikatokea kwa huyo mwenye kushuku. “Hebu huyo mponyaji wa Kiungu ajitokeze. Hebu atende kazi.” Ndugu Bosworth akasema wazi ya kwamba Yesu alikuwa Ndiye Mponyaji pekee wa Kiungu, bali kelele za majigambo ya mkosoaji yakaendelea. Hatimaye, Ndugu Bosworth akamwalika Ndugu Branham jukwaani. Akakubali mwaliko huo huku kukiwako na makelele ya shangwe ya kumuunga mkono.

Nabii, huku amejazwa na Roho Mtakatifu, alitoa jibu hili:

    Siwezi kumponya mtu yeyote. Nasema jambo hili. Wakati nilipokuwa mtoto mchanga aliyezaliwa katika Mkoa wa Kentucky, kulingana na mama yangu mpendwa, na jambo ambalo limethibitishwa maishani mwangu mwote, kuna Nuru iliyoingia kwenye chumba cha kibanda maskini kile kilichosongamana vitu kule, mahali kilipokuwa, hakijasakafiwa, hata hakikuwa na dirisha, walikuwa tu na maskini kitu fulani cha kale kama dirisha pale, kama kijilango, nao wakakisukuma wakakifungua yapata saa kumi na moja alfajiri, na Nuru hii ikazunguka ikaingia kama wakati tu kukipambazuka. Tangu wakati huo, imekuwa pamoja nami. Ni Malaika wa Mungu. Alikutana nami uso kwa uso miaka michache iliyopita. Kote katika maisha yangu, Yeye aliniambia mambo ambayo yametukia, nami nimeyasimulia tu kama vile alivyoniambia. Nami ninampa changamoto mtu yeyote mahali popote, aende kwenye mji niliolelewa, ama popote pale, ambapo tamshi limepata kutolewa katika Jina la Bwana, ila lile lililotimia vile vile hasa jinsi lilivyosemwa lingekuwa.

Baada ya kusema maneno hayo, Roho Mtakatifu alishuka hapo jukwaani, naye mpiga picha mwenye kusisimkwa akapiga picha. Ndugu Branham aliondoka jukwaani kwa tamshi rahisi, hata hivyo la kinabii: “Mungu atashuhudia. Sitasema zaidi.”

Mwenziwe Bw. Kipperman upesi alienda kuzisafisha picha hizo kwa ajili ya taarifa za habari za kesho yake asubuhi. Aliona kitu cha ajabu alipokuwa akiitoa picha ya kwanza kutoka kwenye mmumunyo wa kusafishia. Hiyo, kama picha zingine tano zilizofuata, ilikuwa ni tupu. Aliushika moyo wake akaanguka kufudifudi wakati alipotoa picha ya mwisho kutoka kwenye mmumunyo huo. Hapo, kwenye picha hiyo ya mwisho, kulikuwako na ile Nguzo ya Moto katika umbo linaloonekana imetulia juu ya kichwa cha nabii wa Mungu, William Marrion Branham.

Wana wa Israeli waliishuhudia ile Nguzo ya Moto ikimwongoza Musa, nao watu wa siku hizi wameishuhudia Nguzo ile ile ya Moto ikimwongoza nabii mwingine.

Picha hiyo upesi ilipelekewa George J. Lacy, Mchunguzi Mweledi wa Hati Zinazoshukiwa wa F.B.I. ya Marekani, ambaye aliihakiki picha hiyo kwa maoni yake ya kitaalamu. Hati rasmi iliyotolewa na Bw. Lacy iko kwenye ukurasa unaofuata.

Hii ilikuwa ni mapema zaidi kabla ya makompyuta na kamera za tarakimu, wala haingeweza kuelezewa kwa njia zozote zinazojulikana na sayansi, mbali na kwamba kulikuwa na Nuru halisi juu ya kichwa cha William Branham. Leo hii picha hiyo hiyo inaweza kuonekana kwenye Maktaba ya Bunge la Marekani, katika makao makuu ya taifa, Washington DC.

7) SIRI ZIMEFUNULIWA

 

Mapema katika huduma ya Ndugu Branham ilikuwa wazi kwamba mfumo wa kimadhehebu uliundwa kuyaendeleza madhehebu ya kidini, wala si Injili ya kweli. Ndugu Branham aliiamini Biblia Neno kwa Neno, wala asingepatana, hata kama ilimaanisha kutengwa na wenzake, marafiki, ama familia.

Wakati angali akiwa ni mfuasi wa Kanisa la Kimishenari la Baptisti, aliombwa kuwaweka wakfu wahudumu wanawake. Hata hivyo, yeye alijua Maandiko vizuri sana. I Timotheo 2:12 inasema dhahiri, “Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume; bali awe katika utulivu,” na I Wakorintho 14:34 inasema, “Wanawake na wanyamaze katika makanisa, maana hawana ruhusa kunena…” Hii haikuwa ni kuwapinga wanawake, bali Biblia ilikuwa imeliandika dhahiri jambo hilo. Wakati mkataa ulipotolewa, yeye asingepatana kwa hiyo akaliacha kanisa hilo.

Hilo halikuwa ndilo Andiko la pekee lililopuuzwa na madhehebu. Bwana alimfunulia Ndugu Branham ukweli juu ya ubatizo. Yesu angewezaje kuagiza, “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu,” hata hivyo kila ubatizo uliorekodiwa katika Biblia ulikuwa ni katika Jina la Yesu? Mtume Petro aliagiza katika Matendo 2:38 kutubu na kubatizwa katika Jina la Yesu Kristo. Maandiko hutenda kazi katika umoja mkamilifu, bali ilihitaji nabii kuifunua siri hii: “Baba” si jina, “Mwana” si jina, na “Roho Mtakatifu” si jina. Ni kama tu vile mtu mmoja ni baba kwa watoto wake, mwana wa wazazi wake, na ndugu wa ndugu zake, hata hivyo jina lake si “baba,” “mwana,” wala “ndugu.” Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni sifa za Jina Lake Yesu Kristo. Mathayo 28:19 na Matendo 2:38 yamekuja kulingana kikamilifu.

 Hata ile dhambi ya asili katika Bustani ya Edeni ilifunuliwa, sio kama kula tunda, bali ni jambo ovu zaidi. Je! kula kipande cha tunda kungewezaje kuwafunulia Adamu na Hawa mara moja kwamba walikuwa uchi? Kwa kweli haileti maana. Tofaa lina uhusiano gani na uchi? Nabii wa Mungu aliifunua siri hii wazi wazi.

 Malaika walionenwa habari zao katika Ufunuo mlango wa 2 na wa 3 ni akina nani? Huenda majina yao yakasikika yanafahamika.

 Wale wapanda farasi wa kisiri wa Ufunuo mlango wa 6 ni akina nani? Wana jambo moja shirika lililo muhimu sana.

 Je! Marekani imetajwa katika Kitabu cha Ufunuo?

 Wale 144,000 waliookolewa katika mlango wa 7 ni akina nani?

 Yule kahaba mkuu wa mlango wa 17 ni nani? Utambulisho wake na siri hizi zote zilifunuliwa katika Ujumbe wa nabii huyu mkuu aliyetumwa kutoka kwa Mungu.

 Si kwamba tu miujiza isiyohesabika ilimfuata mtu huyu, bali siri zilizofichwa katika Biblia katika nyakati zote pia zilifunuliwa katika huduma yake. Ilionekana wazi kwamba nabii huyu alitimiza Maandiko mengi zaidi mbali na Malaki 4.

Ufunuo 10:7: Isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.

Sauti inawalilia walimwengu watoke kwenye madhehebu na walirudie Neno asili la Mungu. Kila mmoja wetu ana nafasi ile ile waliyokuwa nayo Petro, Yakobo, na Yohana. Tuna nafasi ya kuhesabiwa pamoja na wachache wa Mungu walioteuliwa ambao wasingeyasujudia madhehebu ya kidini ya siku hizi.

Maandiko matakatifu yamenakili maisha na matendo ya watu waliotembea pamoja na Mungu na walikuwa wametiwa mafuta sana na Roho hata walitangaza BWANA ASEMA HIVI, nayo maneno yao yakathibitishwa kwa ishara na maajabu yasiyoweza kukosea. Walikuwa ni manabii wa Mungu, na Sauti ya Mungu kwa kizazi chao.

Je! nyakati ziko tofauti sasa na vile zilivyokuwa wakati Yesu alipokuwa hapa? Viongozi wa dini ndio waliomsulibisha. Wanafunzi walikuwa wachache mno miongoni mwa mfumo mkubwa sana wa kidini. Walitengwa, wakadhihakiwa, na hatimaye wakauawa kwa kuchukua msimamo dhidi ya mfumo wa madhehebu makubwa. Huenda tusiuawe kwa ajili ya imani zetu siku hizi, bali hakika tunateswa. Kama vile Mafarisayo na Masadukayo, wao hawawezi kuikana miujiza iliyoifuata huduma ya Ndugu Branham kwa hiyo wanakimbilia kufanya mashambulizi ya namna nyingine. Huenda ukasikia ya kwamba yeye alikuwa ni nabii wa uongo, kiongozi wa kundi lililojitenga, ama mabaya zaidi. Kwa kweli, yeye alikuwa ni mtu mnyenyekevu wa Mungu ambaye alisimama imara dhidi ya utawala wa kimabavu ambao madhehebu na vikundi vya dini yanao juu ya watu wa Mungu. Walimshambulia Yesu jinsi hiyo hiyo wakati Yeye alipopinga mafundisho yao ya sharti na mapokeo.

Mungu aliuheshimu msimamo wa Ndugu Branham wa kuamini kila Neno katika Biblia, Naye anaitumia huduma yake kuwaongoza mamilioni ya watu kwa Yesu Kristo. Leo hii, Sauti ya Malaika wa Saba inapiga baragumu kwa nguvu vile vile ilivyopata kuipiga. Kadiri ya watu milioni mbili ulimwenguni kote wanauamini Ujumbe wa Ndugu Branham. Huenda hii ikawa ni uchache mdogo sana wa watu bilioni mbili wanaokiri Ukristo, lakini je! ni wakati gani ambapo watu wa Mungu hawakuwa katika uchache?

Tuna zaidi ya jumbe 1,200 zilizorekodiwa zilizo na Sauti ambayo ilitabiriwa ingekuja katika Ufunuo 10:7. Kila moja ya jumbe hizi inafungua siri zaidi za Mungu. Sauti hiyo inapatikana kwa ajili yako kama unapenda kuisikia.


CHAGUO NI LAKO

Rev. William Marrion Branham;

“Kamwe siwaletei watu ujumbe kusudi wanifuate, ama wajiunge na kanisa langu, ama waanzishe shirika na dhehebu fulani. Sijafanya hivyo kamwe wala sitafanya hivyo sasa. Sina haja ya mambo hayo, bali nina haja ya mambo ya Mungu pamoja na watu, na kama naweza kulitimiza jambo moja tu nitaridhika. Jambo hilo moja ni kuona uhusiano wa kweli wa kiroho baina ya Mungu na watu umeimarishwa, ambapo watu wanakuwa viumbe vipya katika Kristo, wamejazwa na Roho Wake na wanaishi kulingana na Neno Lake. Ningewaalika, ningewasihi na kuwaonya watu wote waisikie sauti Yake wakati huu, na kuyatoa maisha yenu kabisa Kwake, hata kama vile ninavyoamini moyoni mwangu kwamba nimeyatoa yangu yote Kwake. Mungu awabariki, na hebu kuja Kwake na kuifurahishe mioyo yenu.”

(CHANZO)

http://themessage.com/sw/home

THEMESSAGE.COM
P.O. Box 950
Jeffersonville, IN 47131, USA
812-256-1177

Print this post

DHAMBI YA MAUTI

Dhambi ya mauti, ni ipi katika maandiko?


1Yohana 5:16 “Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti.

IKO DHAMBI ILIYO YA MAUTI. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.

17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.

Biblia inaeleza wazi kuwa kuna DHAMBI ZA MAUTI na DHAMBI ZISIZO ZA MAUTI:

DHAMBI ISIYO YA MAUTI:

Hii ni dhambi ambayo mtu akiifanya anaweza akatubu na kusamehewa, na dhambi hii ni ile inayotokana na aidha kutenda pasipo kukusudia, au inatendeka kutokana na uchanga wa kiroho, au kwa kukosa maarifa  au jambo lingine lolote linaloweza kutendeka ambalo halijavuka mipaka ya neema.

Dhambi  ya namna hii biblia inasema mtu anaweza akatubu au akamuungamania mwenzake na akasamehewa, akaendelea kuishi na asife. Lakini kuna dhambi mtu akiitenda hiyo hata huyo mtu aombeje, anaweza akasamehewa kosa tu lakini adhabu ya mauti ipo pale pale, je! hii dhambi inasababishwa na nini?

DHAMBI YA MAUTI:
Dhambi hii ipo kwa namna mbili, ya kwanza kwa wale watoto wa Mungu (watumishi wake) na ya pili ni kwa watu wengine ambao neema ya Mungu inalilia masikioni mwao lakini wanaichezea.

Namna hizi mbili tunaweza tukaona zimefananishwa  na Musa na wana wa Israeli kule jangwani, Musa akiwa mfano wa “watumishi wa Mungu”, pamoja na kwamba Mungu alitembea nae kwa namna ya tofauti hata kuliko manabii wote, lakini alitenda dhambi kwa kosa kutokutii maagizo ya Mungu na kuchukua utukufu wa Mungu, alifanya vile akijua kabisa kuwa ni kosa ikampelekea kutenda DHAMBI YA MAUTI, 

Musa kwa kweli alisamehewa lile kosa lakini adhabu ya mauti ilikuwa pale pale iliyomsababishia apoteze hata zile ahadi zote Mungu alizomuahidia za kuiona nchi ya Ahadi. Hata leo hii wapo watumishi wanatenda hii dhambi, wanachukua utukufu wa Mungu na kutokutii maagizo yake, inapelekea Mungu kuwaadhibu huduma zao zinakatishwa kama ilivyotokea kwa Anania na Safira walipomdanganya Roho Mtakatifu na kupokea adhabu ya kifo pale pale japo walikuwa ni watoto wa Mungu. Hizo zote ni DHAMBI ZA MAUTI.

Vivyo hivyo na wana wa israeli ni mfano kamili wa “wakristo vuguvugu” wa leo kumbuka wana wa israeli ijapokuwa waliuona utukufu wote wa Mungu, na maajabu yote na miujiza yote lakini mioyo yao haikuwa mikamilifu  ijapokuwa Mungu aliwavumilia kwa muda mrefu watubu lakini hawakutaka wakaanza kuabudu sanamu, wakafanya uasherati, wakawa wakimnung’unikia Mungu na kumjaribu ikafika wakati neema ya Mungu juu yao ikakoma Mungu akaapa kwamba wote wangekufa nyikani ijapokuwa walitubu kwa kulia na kuomboleza hata hivyo hakuna hata mmoja wao aliyeiona nchi ya ahadi isipokuwa wale wana wao tu!, unaona hiyo ndiyo DHAMBI YA MAUTI.

Unajisikiaje pale ambapo unaona ungestahili kupata baraka fulani halafu unazikosa, hautakaa uzipate tena milele? fikiri juu ya hilo, na ndio maana maandiko yafuatayo yanatuonya yakisema

1 Wakorintho 10:1

Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;

3 wote wakala chakula kile kile cha roho;

4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.

6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.

8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.

10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.

11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. 

Mfano kamili wa kanisa la leo lililo vuguvugu kupita kiasi” linaona utukufu wa Mungu karibu kila mtu anafahamu kabisa kuwa KRISTO ni mwokozi, mponyaji, na wengi wao wamebatizwa wanaenda kanisani, wanaujua ukweli wote lakini utakuta bado mtu ni mwasherati, mlevi, mtukanaji, anaenda disco, msengenyaji, anatazama pornography, anavuta sigara, anavaa mavazi ya kiasherati n.k. angali akifahamu Mungu hapendezwi na watu wa namna hiyo. Anaiona neema ya Mungu lakini bado anaidharau mfano ule ule wa wana wa Israeli, Lakini watu kama hawa hawajui kuwa wapo hatarini kutenda DHAMBI YA MAUTI.

kama tu Mungu hakuweza kumwachilia mtumishi wake Musa kwa kosa dogo tu la kutokutii wewe unadhani utaponea wapi ikiendelea na maisha yako ya dhambi?..Ni kweli Musa alisamehema lakini adhabu ya kutokuiona nchi ya ahadi kwa njia ya Mauti ilikuwa pale pale.

Kwa namna hiyo hiyo unahubiriwa injili leo umgeukie Mungu, uache dhambi utubu usamehewe unasema hapana ngoja nile maisha nitakuja kutubu baadaye unaweza usiseme kwa mdomo lakini moyo wako unasema unaendelea kuwa mwasherati pale unapopata ugonjwa usiokuwa na matumaini mfano ukimwi unaona ndio sababu ya kumgeukia Mungu angali wakati ulipokuwa mzima hukufanya hivyo? Ni kweli ukitubu unaweza ukasemehewa lakini adhabu ya mauti ipo pale pale ndio maana utaona watu wa namna hiyo hata waombeweje hawaponi, sababu ni kwamba wameshatenda DHAMBI YA MAUTI.

Sisemi hili kwa kukutisha lakini ndio ukweli, hatuna budi  kuyachunguza maisha yetu kila siku.

Mara nyingine sauti ya Mungu inakulilia uache dhambi ya ulevi na uvutaji sigara ili usafishwe maisha yako lakini unaziba masikio yako hutaki kusikia. Mungu anaruhusu pepo la Kansa linakuingia unapata kansa ya koo au mapafu au ini hapo ndipo unapoona sababu ya kumrudia Mungu ni kweli ukitubu Mungu anaweza kukusamehe lakini adhabu ya kifo ipo pale pale Kwasababu apandacho mtu ndicho atakachovuna. Mungu sio wa kumtegea kwamba niache nifanye mambo yangu kisha nikishafika mzee au wakati fulani ndipo nimgeukie, Mungu hadhihakiwi.

MADHARA YA DHAMBI YA MAUTI:

Madhara yake makubwa ni kwamba utapoteza thawabu yako katika ule ulimwengu ujao kwasababu umelikatisha kusudi la Mungu juu yako, ndio hapo kama Mungu alikupa huduma au anataka uwe na huduma haiwezekani tena kuendelea nayo kwasababu ulishatenda DHAMBI YA MAUTI, huna budi kuondoka nafasi yako anapewa mtu mwingine kama ilivyomtokea Yuda nafasi yake ilichukuliwa na mtu mwingine. wakati wengine wakipewa mataji yao mbinguni siku ile kwa kazi nzuri walizotaabika nazo duniani wewe utakuwa huna lolote, utabaki mtu wa kawaida milele. Hivyo ndugu, biblia inasema

 1Petro 1:10 ” KWAHIYO NDUGU, JITAHIDINI ZAIDI KUFANYA IMARA KUITWA KWENU NA UTEULE WENU; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. ” .

Itikia wito wa Mungu ulio ndani yako sasa kabla hazijaja siku zilizo mbaya utakazosema ee! Mungu wangu nisamehe nataka kuishi lakini usiweze kusikilizwa dua zako kwa upumbavu wako mwenyewe. Ndugu Tukisikia hili tuogope kwasababu imeandikwa..

Wafilipi 2:12 “Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA.KWA MAANA NDIYE MUNGU ATENDAYE KAZI NDANI YENU, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. “

AMEN!

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

DHAMBI ISIYO NA MSAMAHA.

MIISHO YA ZAMANI.

KUMWAMBIA MTU MWENYE DHAMBI KUWA ATAKWENDA KUZIMU ASIPOTUBU JE! NI KUHUKUMU?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “NA KONDOO WENGINE NINAO AMBAO SI WA ZIZI HILI” HAO KONDOO WENGINE NI AKINA NANI?


Rudi Nyumbani

Print this post

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

Kuna tofauti kati ya MAMLAKA(CHEO) na UTAJIRI. Unaweza ukawa tajiri lakini usiwe na mamlaka au cheo na pia unaweza ukawa na CHEO na usiwe tajiri au unaweza ukawa na vyote viwili kwa pamoja. Kwamfano viongozi wenye vyeo kama wakuu wa mikoa, madiwani, mawaziri na mameya, wana nguvu na usemi juu ya watu wote pamoja na matajiri huko huko, haijalishi matajiri wana fedha kiasi gani, hiyo haiwapi wao mamlaka ya kuiamrisha nchi. Kiongozi akisema ndiyo ni ndiyo na hapana ni hapana japokuwa hao viongozi wanaweza wasiwe na mali na utajiri wowote wa kuwazidi hao matajiri wa nchi lakini wamepewa mamlaka makuu juu ya wote yaani matajiri na wasio matajiri. Lakini matajiri hawawezi wakawa na mamlaka juu ya wakuu wa nchi (Viongozi).

Vivyo hivyo katika ukristo, kuna UKUU na UTAJIRI. tutazame utajiri ni upi na ukuu ni upi;

UTAJIRI KATIKA UFALME WA MBINGUNI: 

Kama tunavyofahamu utajiri unakuja kwa bidii na juhudi za mtu, kwa jinsi unavyofanya kazi sana, na kujiwekea hazina ndivyo utajiri wake unavyokuja. Na ndivyo ilivyo hata kwa Mungu utajiri katika Kristo unakuja unapokuwa mwaminifu katika kazi ya Mungu. bidii yako kuitumia karama uliyopewa katika kuhubiri, kuwavuta watu kwa Kristo, kutumika katika kanisa, kutenda wema na ukarimu, kutoa sadaka, kusaidia yatima na wajane pamoja na maskini n.k, kiufupi kazi zote njema zinazotokana na Mungu. Yote haya ni HAZINA unayojiwekea mbinguni ambao ndio huo UTAJIRI wako, 

Luka 12:33 “Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.Kwa kuwa HAZINA YENU ILIPO, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu. “

 Unaona jinsi utoavyo sadaka ndivyo utajiri wako unavyoongezeka mbinguni.

Marko 12:41 “Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.

42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.

43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini AMETIA ZAIDI kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;

44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake AMETIA VYOTE ALIVYOKUWA NAVYO, ndiyo riziki yake yote pia. ” 

Unaona tena hapo kitu cha pekee alichokuwa nacho yule mwanamke ni pale alipotoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya BWANA, ikamfanya aonekane mbinguni kuwa mwenye utajiri mkubwa kuliko wote, nasi pia tunafundishwa tufanye hivyo sio tu pale tunapozidiwa na mali tumtolee Mungu, bali hata katika hali ya upungufu tuliyopo tumtolee Mungu vyote ili UTAJIRI wetu mbinguni uwe mkubwa.

UKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI:

Tukisoma..

Mathayo 18:1 “Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,
2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa KAMA VITOTO, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
4 Basi, YE YOTE AJINYENYEKESHAYE  MWENYEWE KAMA MTOTO HUYU, huyo ndiye aliye MKUU katika ufalme wa mbinguni.”

Wengi wanadhani unapohubiri injili, au unapotoa sadaka sana, au unapotumika kanisani sana kunakufanya wewe kuwa MKUU mbinguni hapana huko kote ni kukuongezea utajiri(HAZINA) yako mbinguni lakini sio kukupa wewe UKUU au MAMLAKA, Kama tulivyotangulia kusema mtu anaweza akawa na mamlaka na asiwe tajiri, au anaweza akawa na vyote kwa pamoja na ndivyo ilivyo hata kwa Mungu, UKUU au UKUBWA, au MAMLAKA unakuja kwa njia moja tu. Biblia inaiita “KUJINYENYEKEZA NA KUWA MDOGO KULIKO WOTE KATIKA KRISTO” Kwa mfano wa mtoto mdogo Hilo tu!.

Na kujinyenyekeza huku kunakuja kwa namna mbili..

1.Unyenyekevu kwa MUNGU. 
Bwana Yesu alituambia tuwatazame watoto wadogo, kwasababu watoto wadogo siku zote wanaweka tegemeo lao lote kwa Baba zao kwa kila kitu kwa chakula,afya,malazi,mavazi n.k., wao ni kama kondoo pasipo wazazi wao hawawezi kufanya lolote, wanapoadhibiwa ni wepesi kubadilika na hawana kinyongo, kichwa cha mtoto mdogo ni chepesi kujifunza kuliko cha mtu mzima kwasababu yupo tayari siku zote kukubali kusikia, mtoto mdogo ni mtii, na anaamini lolote atakaloambiwa na wakubwa zake bila kushukushuku, Na ndivyo Bwana Yesu alivyokuwa kwa BABA yake tunasoma kila mahali alikuwa anamtaja BABA, BABA, BABA,ikiashiria pasipo BABA yake hawezi kufanya lolote soma Yohana 5:19″Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. “..Unaona hapo jinsi YESU alivyojinyenyekesha chini ya mapenzi ya baba yake na kuwa mtii hata MUNGU akamfanya kuwa mkubwa kuliko vitu vyote vya mbinguni na duniani. 

Wafilipi 2:8 “tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, ALIJINYENYEKEZA AKAWA MTII HATA MAUTI, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. “

Na sisi vivyo hivyo tunapaswa tujinyenyekeze chini ya BABA yetu wa mbinguni mfano wa MTOTO-na-BABA yake. mapenzi yetu yafe lakini ya Mungu yatimizwe maishani mwetu.Hii ndiyo sadaka ya kwanza mtu anaweza akamtolea Mungu yenye kumpendeza. Kumbuka BWANA YESU alishuhudiwa na BABA kwanza kuwa AMEMPENDEZA kabla hata hajaanza kuhubiri injili au kufanya kazi ya Mungu.(mathayo 4). Hii ni namna ya kwanza na ya pili ni;

2.Kujinyenyekeza chini ya ndugu (wakristo).

Bwana Yesu aliwaeleza wanafunzi wake,atakayetaka kuwa mkubwa kati yenu na awe mdogo kuliko wote, kama yeye alivyokuwa mdogo kuliko wote. YESU alimnyenyekea BABA pamoja na wanadamu Vivyo hivyo na sisi pia sio tu kumtii Mungu halafi tunawadharau ndugu zetu, na kujifanya sisi ni KITU fulani cha kipekee zaidi ya wao. tunapaswa tujishushe tuwatumikie wenzetu mfano ule ule wa YESU KRISTO hata kufikia kiwango cha kuona nafsi ya ndugu yako ni bora kuliko ya kwako. Tusome..

Marko 10:42 “Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; BALI MTU ATAKAYETAKA KUWA MKUBWA KWENU, ATAKUWA MTUMISHI WENU,
44 NA MTU ANAYETAKA KUWA WA KWANZA WENU, ATAKUWA MTUMWA WA WOTE.

45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, NA KUTOA NAFSI YAKE IWE FIDIA YA WENGI.” 

Mahali pengine Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake.

Mathayo 11:11 ” Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini ALIYE MDOGO KATIKA UFALME WA MBINGUNI ni MKUU kuliko yeye. “

Hii ikiwa na maana kuwa yule ANAYEJINYENYEKEZA (KWA MUNGU na KWA WANADAMU) na KUWA MDOGO, Huyo ndiye aliye MKUU kuliko Yohana mbatizaji,.Unaweza ukaona ni faida gani aliyonayo mtu yule ajishushaye kama mtoto mdogo halafu anakuwa mkubwa kuliko hata manabii mfano wa Yohana Mbatizaji na wote waliomtangulia kabla yake.

Katika utawala unaokuja huko mbele wa milele, Kristo akiwa kama MFALME WA WAFALME, atatwaa wafalme wengine hao ndio watakaoitawala dunia wakati huo milele, sasa hizi nafasi za wafalme hawatapewa wale MATAJIRI WA ROHO bali wale WAKUU WA ROHO. Hawa wakuu watakuwa na amri, na usemi kwa kila kitu na kila kiumbe duniani kitakuwa chini yao kwasababu watakuwa wamepewa hayo na MKUU WA WAKUU (YESU KRISTO), Biblia inasema wataichunga dunia kwa fimbo ya chuma,(Ufunuo 2:26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. )… watakuwa wenye mataji mengi kama leo hii tu huwezi kuwakaribia hawa wafalme wa dunia ambao sio kitu itakuwaje kwa wale?? watakuwa ni miale ya moto kama BWANA MWENYEWE.

Vivyo hivyo na MATAJIRI watapewa heshima yao, watamiliki hazina nyingi, watakuwa na HESHIMA katika ulimwengu kama tu vile matajiri wa ulimwengu huu wanavyoheshimika sasa, chochote watakachotaka watapata, kwasababu walijiwekea HAZINA nyingi mbinguni, kuna viwango vya umiliki watafikia wewe usiye na kitu hutaweza kufika. 

Bwana mwenye haki atamlipa kila mtu kwa kadri ya alichokipanda ulimwenguni. Kumbuka wapo pia watakaokuwa MATAJIRI NA WAKUU kwa pamoja. Hao ndio wale waliojinyenyekeza na kumtumikia Mungu kwa bidii na kwa moyo, waliitangaza injili, walikuwa watumishi kati ya ndugu, watakatifu, waaminifu katika karama walizopewa, walikuwa kama vitoto vidogo mbele za MUNGU, walikuwa na mapenzi yao wenyewe lakini wakayakataa na kuyakubali mapenzi ya MUNGU maishani mwao, katika mapito yao yote hawakumnung’unikia, walitii na kumwamini pasipo majadiliano kama tu mtoto na baba yake mfano wa BWANA WETU YESU KRISTO.

Kwahiyo ndugu tuutafute UKUU na UTAJIRI WA MBINGUNI. lakini zaidi UKUU ambao kwa huo tu ndio utakaokuleta karibu na Mungu.

Ufunuo 3:19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. “

Mungu akubariki.


Mada Nyinginezo:

JIWE LA KUSAGIA

HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

SIKU ZA MAPATILIZO

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE? NA TENA WANA WA ISRAEL WALIMFUKIZIA UVUMBA MALKIA WA MBINGUNI, NDIO YUPI HUYO?


Rudi Nyumbani

Print this post

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

Neno la Mungu linasema pale tulipo dhaifu ndipo tulipo na nguvu, ikiwa na maana pale tunapokuwa si kitu ndipo tunapoonekana kuwa kitu mbele za Mungu, Bwana Yesu alisema yeye ajishushaye atakwezwa na ajikwezaye atashushwa, pale tunapokataa akili zetu kututawala na kumwachia Mungu azitawale ndipo tutakapofungua mlango na wigo mpana wa kuuona UWEZA wa Mungu zaidi katika maisha yetu.

Na ndio maana mtume Paulo alisema

2Wakoritho 12:9-10″ Naye akaniambia neema yangu yakutosha; maana UWEZA WANGU HUTIMILIKA KATIKA UDHAIFU. Basi najisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili UWEZA WA KRISTO ukae juu yangu.Kwahiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida kwa ajili ya Kristo. MAANA NIWAPO DHAIFU NDIPO NILIPO NA NGUVU.”

uweza wa mungu

Mungu hawezi akawa ni mponyaji kwetu kama hatujawa na madhaifu (mwenye afya haitaji tabibu),mafarisayo na masadukayo YESU alikuwa hana maana kwao kwasababu wao walijiona kuwa wana afya hivyo hawakufaidiwa chochote na uweza wa Mungu katika Yesu Kristo. Kwa kawaida huwa tunashukuru pale tunapotendewa mahitaji yetu, huwezi ukashukuru au ukaomba kama unayo mahitaji yako yote.

Na pia hauwezi kutegemea kama unao uwezo wa kujitegemea. vivyo hivyo na kwa Mungu wetu ili tuweze kuuona UWEZA WAKE, yatupasa tuwe dhaifu mbele zake kwa namna zote, kiasi cha kwamba tujione pasipo yeye sisi hatuwezi lolote. Kwa jinsi tutakavyojiachia kwake kwa kila kitu ndipo tutakapofungua wigo wa yeye kutuhudumia sisi na kuuona uweza wake,

Watoto wa Mungu wamefananishwa na kondoo na sio mbuzi kwasababu kondoo hawezi akajiongoza mwenyewe huwa anamtegemea mchungaji wake kwa kila kitu tofauti na mbuzi wao wana uwezo wa kwenda kujichunga wenyewe hivyo hawahitaji msaada mkubwa sana kutoka kwa mchungaji. Vivyo hivyo Na mtoto mdogo anahudumiwa kwa kila kitu na wazazi wake ikiwemo malazi, chakula, afya, n.k. kwasababu anaonekana dhaifu kwa wazazi wake pasipo wao hawezi kufanya lolote hivyo uweza mkubwa wa wazazi wake unaonekana juu yake,

Kwa jinsi hiyo hiyo na sisi pia tunapaswa tuwe hivyo kwa Baba yetu wa mbinguni, sisi ni watoto kwake tunapaswa tujinyenyekeze kama vitoto vichanga ili tuone uweza wake katika maisha yetu, kumbuka yule mtoto anapojifanya amekua na kutaka kujiamulia mambo yake mwenyewe ndipo kidogo kidogo anapojiachilia kutoka katika mikono ya wazazi wake na uweza wao unavyozidi kupungua juu yake, mpaka inafikia wakati mzazi hana sehemu yoyote kwa mtoto.

Biblia inasema “Mkaribieni Mungu naye atawakaribia”(Yakobo 4:8). hii ikiwa na maana kwa kiwango kile kile tutakachompa Mungu katika maisha yetu, ndicho atakachokitumia kufanya kazi katika maisha yetu. Kama unampa Mungu Jumapili kwa jumapili na yeye atajifunua kwako hiyo hiyo jumapili kwa jumapili, kama ni mwezi kwa mwezi na ndivyo hivyo atakavyojifunua kwako mwezi kwa mwezi, lakini kama ni siku kwa siku ndivyo utakavyomwona siku kwa siku, kwa kiwango kile kile utakachopima ndicho utakachopimiwa biblia imesema.

Kama umempa Mungu asilimia 20 ya maisha yako ayatawale ataonekana kwako katika hiyo asilimia 20 usitegemee zaidi ya hapo, kama umempa 70% ataonekana katika hiyo 70, kama umempa 100% ataonekana katika hiyo 100% kama Bwana YESU alivyompa Baba yake. Maana uweza wa Mungu unatimilika katika udhaifu na udhaifu huu ni pale unapokataa kuzitegemea akili zako na kuwa kama mtoto mchanga mbele zake.

Nakumbuka kipindi cha nyuma zamani kidogo tulikuwa tumepanga chumba sehemu fulani na kila mwisho wa mwezi tulikuwa na desturi ya kulipia bill ya umeme lakini ilifika wakati fulani hatukupata pesa ya kulipia na hatukuwa na chochote mfukoni lakini tulimwamini Mungu na kumwachia yote, tukasema kama Mungu wetu yupo atatupigania, maana hao wadai pesa za umeme ni watu wakorofi ukipitisha tu siku moja haujalipia ni balaa umelianzisha, lakini ulipofika mwisho wa mwezi hatukuwa na chochote mfukoni,

cha ajabu wale wadai-umeme hawakuja siku hiyo kudai pesa ya umeme na sio desturi yao, vyumba vingine vyote walienda kulipa kilikuwa kimebaki chumba chetu tu! lakini ni kama walipigwa upofu hivi hawakuja, ukaingia mwezi mwingine, tarehe 1,2,3……mpaka tarehe 24 tulikuwa bado hatujalipa deni la mwezi uliopita na kweli hela hatukuwa nayo na umeme tunaendelea kutumia lakini tulimwachia Mungu yote tulisema liwalo na liwe hatutamkopa mtu,

nakumbuka siku hiyo hiyo pia gesi ya kupikia iliisha kwahiyo matatizo yakaongezeka, lakini ilipofika tarehe 25 mida ya jioni huku tukiwa na mawazo tulifungua simu tukakuta sh.48,000 kwenye mpesa hatukujua imetoka wapi, haijatumwa na mtu yoyote, wala hakuna jina wala message ya kuonyesha mtu katuma pesa, ni kama vile iliongezeka katika account ya m-pesa. tukaenda kuitoa jioni ile ile cha ajabu saa hiyo hiyo baada ya kuitoa hiyo pesa wale wadai-umeme wakafika na ghadhabu wanataka pesa yao ya umeme ya mwezi uliopita, tukawapa saa ile ile, sh.15,000 kiasi kilichobaki tulinunua gesi na matumizi mengine.. Bwana amekuwa akituonekania sisi watoto wake kwa namna hii mara nyingi tu na kwa njia nyingi.

Lakini tungesema tujiongeze tukakope pesa hakika uweza wa Mungu tusingeuona maana yeye anasema zaburi 46:1″ Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, MSAADA UTAKAOONEKANA TELE WAKATI WA MATESO.” pale tutapokuwa dhaifu na kumwachia yeye ndipo tutakapouona uweza wa Mungu, wana waisraeli wasiongeweza kuona bahari inagawanyika kama wasingekutana na kizuizi cha bahari, wasingekula mana kama wasingepita jangwani, wasingepasuliwa maji miambani kama wasingekuwa na kiu, Hivyo pale unapomkabidhi Mungu mambo yote atawale katika misukosuko pasipo kutafuta njia mbadala ya akili zako, ndipo uweza wa Mungu utakapoonekana.

Vivyo hivyo unapopitia shida fulani, au unapoumwa, au tatizo fulani haraka haraka usikimbilie kutafuta njia mbadala, usianze kutangatanga jua hiyo ndio fursa ya wewe kuuona uweza wa Mungu na ndio yeye anataka iwe hivyo, ndio ni vizuri kwenda hospitali na sio dhambi kwenda hospitali lakini sio kila ugonjwa kukimbilia hospitali ukifanya hivyo uweza wa Mungu utauonaje?,

Naweza nikakupa mfano ulifikia wakati nilikuwa nikipata ugonjwa kidogo nakimbilia dawa lakini ilifika wakati nikasema nataka nimuone Mungu katika maisha yangu, yeye aniponye pasipo kumtegemea mwanadamu wala dawa, nikasema sitameza kidonge cha aina yoyote wala kwenda hospitali, tangu niseme hivyo hadi sasa ni miaka mingi imepita sijawahi kumeza kidonge wala kwenda hospitali, kila ninaposikia hali ya udhaifu ndani yangu, nasema Bwana ndiye daktari wangu ataniponya na kweli ile hali haidumu baada ya muda mfupi narudia hali yangu ya kawaida, kwa kufanya hivyo uweza wa Mungu nauona ndani ya maisha yangu kila siku.

Na kwako wewe ndugu unaweza ukasema mbona sijawahi kumwona Mungu akinifanyia miujiza katika maisha yangu? ni kwasababu wewe mwenyewe hujaruhusu atende kazi ndani yako. haujataka kuwa dhaifu mbele zake kwa kujishusha kuwa kama mtoto,.jambo fulani limetokea chukua iwe ndio fursa ya wewe kumwona Mungu wako usitegemee akili zako, wala mwanadamu wala kitu chochote,mwachie yeye na utauona utukufu wake kila siku.

Hiyo ndio njia pekee itakayokufanya uone UWEZA WA MUNGU maishani mwako na ndio njia Paulo aliyoinena na kuiishi iliyomfanya amwone Mungu siku baada ya siku katika huduma yake. kwa mfano shedraki, Meshaki na Abednego walipohukumiwa kutupwa katika tanuru la moto hawakusita walimwachia Mungu yote na kwa kufanya hivyo waliweza kukutana na Mungu kule na kupelekea Mungu wao kutukuzwa babeli yote, vivyo hivyo na Danieli pia alipotupwa katika tundu la simba aliuona uweza wa Mungu kule, tukiwaangalia pia akina Paulo na Sila walipotupwa gerezani ndipo walipouona uweza wa Mungu pale malaika wa Mungu alipoitetemesha ardhi na kufungua malango ya gereza. Hawa wote ni kwasababu walikubali kuwa wadhaifu kwa ajili ya Bwana hivyo ikawafanya wauone utukufu mkubwa wa Mungu.

Mithali 3:5-6 ” Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zake mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye naye atanyosha mapito yako.”

Amen!

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

UPUMBAVU WA MUNGU.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI

KWANINI MUNGU AWACHOME WATU KWENYE ZIWA LA MOTO NA HALI YEYE NDIYE ALIYEWAUMBA?


Rudi Nyumbani

Print this post

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Karibu tuongeze maarifa katika Neno la Mungu,

Tukisoma kwenye biblia kitabu cha warumi 4 tunaona mtume Paulo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kwa matendo yake bali kwa Imani, lakini tukisoma tena katika kitabu cha Yakobo 2, Yakobo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki kwa Imani tu, bali pia na kwa matendo. Tunaona sentensi hizi mbili zinaonekana kama kupingana, Lakini je! Biblia kweli inajipinga au ni sisi uelewa wetu ndio unaojipinga??..tuichambue mistari hii miwili kwa undani kidogo..

1) Warumi 4:1-6

“1 Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili?
2 KWA MAANA IKIWA IBRAHIMU ALIHESABIWA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE, ANALO LA KUJISIFIA, LAKINI SI MBELE ZA MUNGU.

3 Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.

5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

6 Kama vile Daudi anenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,.

Ni dhahiri kuwa hapa mtume Paulo alipokuwa anazungumzia MATENDO, alikuwa analenga matendo yatokanayo na sheria  ya kwamba hakuna mwanadamu yoyote anaweza akasimama mbele za Mungu kwa matendo yake kuwa ni mema au amestahili kumkaribia Mungu.

Kwa mfano mtu kusema nimestahili kwenda mbinguni kwa matendo yangu mazuri, mimi sio mwasherati, sio mwizi, sio mtukanaji, sio mlevi, sio mwongo, sio mwuuaji n.k. kwa kusimamia vigezo kama hivyo hakuonekana hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu isipokuwa mmoja tu naye ni BWANA wetu YESU KRISTO! wengine wote kama biblia inavyotaja kuanzia Adamu mpaka mwanadamu wa mwisho atakayekuja duniani Mungu alishawaona wote tangu mwanzo kuwa wamepungukiwa na utukufu wake,

Warumi 3:23″ kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; “

 na ukisoma pia Zaburi 14:2-3 inasema

 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.” 

Hivyo hii inadhihirisha kabisa hakuna hata mmoja atapata kibali mbele za Mungu kwa matendo yake mazuri.

 Lakini swali ni je! kama sio kwa matendo, basi mtu atapata kibali mbele za Mungu kwa njia gani tena??..

Ukiendelea kusoma mbele tunasoma mtume Paulo anasema ni kwa njia moja tu tunaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu nayo ni njia ya kumwamini BWANA YESU KRISTO tu!. Ndio njia pekee inayotupa sisi kupata kibali mbele za Mungu, kwa namna hiyo basi tunayo haki ya kuwa na uzima wa milele, kwenda mbinguni, kubarikiwa kwasababu tumemwamini mwana wa Mungu YESU KRISTO na sio kwa matendo mema tuyatendayo.

Kumbuka zipo dini nyingi zenye watu ambao wanatenda matendo mema lakini je! wanao uzima wa milele ndani yao? utakuta ni wema kweli wanatoa zaka, wanasaidia maskini, sio waasherati, sio  walevi n.k. lakini bado Mungu hawatambui hao. Lakini sababu ni moja tu, hawajamwamini mwana wa Mungu ili aziondoe dhambi zao.

Kwahiyo tunaona hapo jambo kuu Mungu analolitazama ni wewe kumwamini mwana wa Mungu, na ukishamwamini (yaani kumpa maisha yako) ndipo ROHO wake MTAKATIFU anakutakasa na kukufanya uishi maisha matakatifu ya kumpendeza.

2). Lakini tukirudi kusoma kitabu cha Yakobo 2:21-26 

“21 JE! BABA YETU IBRAHIMU HAKUHESABIWA KUWA ANA HAKI KWA MATENDO, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?

22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.

23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.

25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?

26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Katika kifungu kile cha kwanza ukiangalia kwa undani utaona kuwa mtume Paulo alikuwa anazungumzia juu ya MATENDO YATOKANAYO NA SHERIA. Lakini hapa Yakobo hazungumzii habari ya matendo yatokanayo na sheria bali ni MATENDO YATOKANAYO NA IMANI.. hivyo ni vitu viwili tofauti. 

MFANO WA MATENDO YATOKANAYO NA IMANI:  

Kwamfano: Mtu amepimwa na daktari na kuambiwa kuwa anaugonjwa wa kisukari, na hatakiwi kula vyakula vyenye asili ya sukari na wanga. lakini mtu yule akilishikilia lile Neno kwenye biblia Mathayo 8:17 linalosema ” ….Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. ”

Na kuliamini na kuamua kuchukua hatua na kusema mimi ni mzima na sio mgonjwa kwasababu yeye alishayatwaa madhaifu yetu, na kusimama na kutembea kama mtu mzima asiyeumwa na kula vyakula vyote hata vya sukari na wanga ingawa daktari alimkataza, akiamini kuwa amepona kwa NENO lile atapokea uponyaji wake. sasa  kitendo cha yeye kuchukua hatua ya kuishi kama mtu mzima ambaye haumwi japo ni mgonjwa na kula vile vyakula alivyoambiwa asile hicho ndicho kinachoitwa MATENDO YA IMANI Yakobo aliyoyazungumzia..

Unaona hapo haki ya huyo mtu kuponywa haikutokana na matendo ya sheria (yaani utakatifu, kutokuwa mwasherati, au mlevi au mwizi n.k.). bali ni matendo yaliyotakana na kumwamini YESU KRISTO katika NENO lake ndio yaliyomponya. Na ndio jambo hilo hilo lililomtokea Ibrahimu pale alipomwamini Mungu na kumtoa mwanae kuwa dhabihu, kwahiyo kile kitendo cha yeye kumtoa mwanawe hayo ndiyo MATENDO yanayozungumziwa na Yakobo YA IMANI kwasababu hiyo basi ikampelekea yeye kupata haki mbele za Mungu.

Unaona hapo haikuwa sababu ya yeye kutokuwa mwongo, au mlevi, au muuaji n.k. ndio kulimpa haki yeye ya kubarikiwa hapana bali ni kumwamini Mungu na kuiweka ile imani katika matendo. Kwasababu kama ingekuwa kwa usafi wake Mtume Paulo asingesema Ibrahimu hana la kujisifu mbele za Mungu.

Vivyo hivyo kwa mambo mengine yote kwamfano haki ya kuzungumza na Mungu, haki ya kuponywa magonjwa,  haki ya kubarikiwa, haki  ya kwenda mbinguni, haki ya karama za rohoni, haki ya kuwa mrithi, n.k. havitokani na MATENDO YA SHERIA bali MATENDO YA IMANI. Kwa sisi kumwamini YESU KRISTO katika Neno lake ndipo tunapopata vyote.

Kwahiyo matendo yote mema ya sheria yanakuja baada ya kuwa ndani ya Kristo na hayo ndiyo yanayokupa uhakika kama upo ndani ya Kristo, ni kweli huwezi ukawa ni mkristo halafu bado ni mlevi, mwasherati, mwongo, mwizi n.k.. lakini jua katika hayo mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kama tukitaka tuhesabiwe katika hayo hakuna mtu atakayesimama mbele za Mungu.

Kumbuka Ibilisi anawinda IMANI yetu kwa Bwana pale tunapoiweka katika matendo na sio kingine, tunasamehewa dhambi kwa imani, tunaponywa kwa imani, maombi yetu yanajibiwa kwa imani, kila jambo tunapokea kwa Mungu kwa IMANI IPATIKANAYO KATIKA NENO LAKE.

Lakini shetani anaenda kinyume kukufanya udhani utasamehewa dhambi kwasababu unashika amri kumi, au  kwa kufunga na kuomba sana ndio utapata haki ya kuponywa, n.k. Bwana amesema Waebrania 10:38 ” Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. “

Wagalatia 2:16 ” hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki. “

Waefeso 2:8-9 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. “

Bwana akubariki.

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?


Rudi Nyumbani

Print this post

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA.

Kumbukumbu 22:5″ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.

Kumbukumbu 22:5" Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako".

Na bado Isitoshe  BWANA anawapelekea watu wake kuwaonya lakini bado wanadhihaki na kuziba masikio yako wasisikie

Warumi 1:18-28″ Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.

 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.

 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.

Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;…….Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo,………………

Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Tunahitaji uthibitisho gani tena kuwa tunaishi katika siku za mwisho nyakati za hatari kama hizi?? JE! umeokolewa,..umempa KRISTO maisha yako? umeoupokea ujumbe wa wakati huu aliouleta Mungu kupitia mjumbe wake ndugu William Marrion Branham wa kanisa la saba na la mwisho ?.

Kama hujafanya hivyo ndugu ni vema ukamgeukia BWANA kabla mlango haujafungwa…

Mungu akubariki.

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group


Mada Nyinginezo:

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

SIRI YA MUNGU.

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani

Print this post

EDENI YA SHETANI:

Pale Edeni Mungu alimweka Adamu na Hawa, Na kwa muda wote waliokuwepo bustanini Biblia inatuambia walikuwa UCHI na hawakujitambua kuwa wako vile, lakini baada ya dhambi kuingia ndipo walipojijua kuwa wapo uchi. Hii ina maana gani?.

Hapo mwanzo Mungu alipowaumba Mungu aliwawekea “UTAJI MTAKATIFU” katika macho yao ambao ungewafanya wasijue dhambi na ule utaji ulikuwa si kingine bali ni ROHO MTAKATIFU. Lakini tunajua walipoasi ule utaji ukaondoka hivyo Mungu akaamua kuwafanyia mavazi ya ngozi ili kuwasitiri.

Lakini Shetani naye tangu ule wakati alianza kutengeneza EDENI yake kidogo kidogo, awarudishe watu katika kuwa UCHI tena na kuwavua mavazi ambayo Mungu aliwavisha.

Takribani Miaka elfu sita sasa tangu Adamu kuumbwa imepita na shetani amekuwa akiimarisha hii edeni yake kwa kuwatia watu “UTAJI WAKE MCHAFU” wa kuwafanya watu waishi na wasijione kuwa wako uchi na wenye dhambi. Hii  ni hatari sana.

Miaka ya zamani kwa kweli mwanamke kutembea amevaa suruali barabarani alikuwa anajulikana kama KAHABA, Lakini sasa hivi zimekuwa ni nguo rasmi kuendea kila mahali mpaka kwenye nyumba za ibada, na sasa imevuka zaidi ya hapo vimini na nguo zinazoonyesha maungo yote wazi ni jambo la kawaida kuliona na  hata haliwashangazi watu tena..Huoni kama ni “UTAJI” wa shetani huo umewavaa watu hata pasipo wao kujua??. na wanaume pia wanaonyesha maumbile yao wakiwa na nguo za ndani tu!. Leo hii wanaume na wanawake wanatembea uchi wa mnyama barabarani pasipo aibu yoyote.

Edeni hii ya shetani inaanzia katika roho. Tunaona kanisa la kwanza lililoanza na Mitume lilikuwa na ule UTAJI wa ROHO MTAKATIFU, Ikiwa na maana kazi zake zote zilitendeka katika uvuvio wa Roho wa Mungu na usafi lakini sasa hivi katika kanisa hili la mwisho tunaloishi  ule utaji wote umeondoka kilichobakia ni utaji wa shetani unaomfanya mtu awe VUGUVUGU na asijijue,

Utakuta mwanamke anaingia kanisani nusu uchi na asijione kuwa yupo uchi, mwanamume ni mzinzi lakini anajiona yeye yupo sawa tu mbele za Mungu, mtu ni mlevi na anajiona yeye ni mkristo aliyesafi, mwanaume anafuga rasta na kujiona hana hatia, utakuta mkristo anaabudu sanamu na asione shida yoyote angali biblia inasema usijifanyie sanamu ya kuchonga usiisujudie wala kuiabudu, mtu kaokoka ni msengenyaji na hata hasikii kuhukumiwa nafsini mwake juu ya hilo analolifanya.n.k.

Ni dhahiri kabisa tunaishi katika kanisa la mwisho linaloitwa, LAODIKIA na ujumbe wetu tuliopewa na BWANA ni huu..

Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 KWA KUWA WASEMA, MIMI NI TAJIRI, NIMEJITAJIRISHA, WALA SINA HAJA YA KITU; NAWE HUJUI YA KUWA WEWE U MNYONGE, MWENYE MASHAKA, NA MASKINI, NA KIPOFU NA UCHI.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “

Kama unavyoona sisi tunaambiwa  tunajiona kuwa ni matajiri kumbe ni maskini na tu “UCHI”

Ni uthibitisho kabisa kuwa huu ni UTAJI WA SHETANI umelifunika kanisa hili la mwisho. Tunaishi nyakati za hatari tubu. mpokee ROHO MTAKATIFU  huo ndio muhuri wa Mungu utakaotuokoa sisi katika kizazi hichi cha mwisho. kumbuka pasipo Roho Mtakatifu hakuna unyakuo, Umeamua kumfuata Bwana mfuate kweli kweli na kama umeamua kumfuata shetani mfuate kweli kweli usiwe vuguvugu.

Tazama video chini, ujionee mwenyewe ulimwengu tunaoishi ulipofikia na jinsi Edeni hi ya shetani ilipofikia ili ujue tunaishi katika nyakati za hatari watu kutembea uchi barabarani si ajabu tena..Na kama vile shetani alivyoiharibu Edeni ya Mungu vivyo hivyo na ya kwake imeandaliwa kwa ajili ya uharibifu ambao upo karibu kutokea.

Mungu akubariki.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU

BWANA YESU ALIMAANISHA NINI PALE ALIPOSEMA “MKONO WAKO UKIKUKOSESHA UKATE?


Rudi Nyumbani

Print this post

MAJI YA UZIMA.

Una kiu? Kunywa MAJI YA UZIMA.Siku zote roho ya mwanadamu imejawa na KIU ya mambo mengi yahusuyo mema, kwa mfano KIU ya kupata FURAHA, kiu ya kuwa na AMANI, kiu ya UZIMA USIOKOMA,kiu ya kuwa na UPENDO kiu ya KUTENDA MEMA, kiu ya kutaka UTAKATIFU,  kiu ya kuwa MNYENYEKEVU na MVUMILIVU, kiu ya KUWA NA RAHA, kiu ya KUWA KARIBU NA MUNGU ..n.k..

Lakini wengi wanatafuta njia za kuzikata kiu hizi kwa njia nyingi tofauti tofauti za kibinadamu. wengine wanatafuta RAHA kwa kufanya anasa, wengine wanatafuta AMANI kwa kunywa pombe, wengine wanatafuta FURAHA kwa kupata mali, wengine wanatafuta UZIMA WA MILELE kwa waganga na wapiga ramli, wengine wanatafuta UPENDO kwa kulaghai, wengine wanatafuta UHURU kwa kuua n.k..

Lakini ni dhahiri kuwa njia zote hizo ni batili, yaani aidha hazikati kabisa au zinakata kiu kwa muda tu! baada ya hapo tatizo linarudi  palepale..Lakini kuna habari njema, ya mmoja tu anayeweza kuikata kiu yako moja kwa moja isikuwepo tena naye si mwingine zaidi ya BWANA YESU. 

Kwa yeye utapata Raha nafsini mwako, furaha isiyokoma, amani, upendo, unyenyekevu, upole, utakatifu, kujua kumcha Mungu, na uzima wa milele n.k..Hivyo nakushauri Mkaribishe moyoni mwako na hakika ataikata KIU yako, usiipuuzie sauti yake ikuitapo . kwa maana maandiko yanasema:

Yohana 7:37-38 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, YESU akasimama, akapaza sauti yake akisema, MTU AKIONA KIU, NA AJE KWANGU ANYWE. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake”. 

Yohana 4:13-14 “Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 

Mungu akubariki.

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

SEHEMU ISIYO NA MAJI.

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?

NI RAHISI KWA NGAMIA KUPENYA KATIKA TUNDU LA SINDANO, JE! NI SINDANO IPI HIYO INAYOZUNGUMZIWA?

JE! MABALASI BWANA ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA TU KWA KAZI HIYO?


Rudi Nyumbani

Print this post

ZIFAHAMU NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE SABA.

Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..

Ufunuo 1:12-20″ Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni  kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri. Tafadhali pitia taratibu mpaka mwisho ili uelewe.

  • vile vinara saba vinavyozungumziwa ni makanisa saba tofauti tofauti ambayo yamepita tangu wakati wa Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani hadi wakati tunaoishi sasa.
  •  Na zile nyota saba ni malaika saba/wajumbe wa duniani(wanadamu 7 ambao Mungu aliwatia mafuta ) kupeleka ujumbe kwa hayo makanisa saba. Kila mjumbe kwa kanisa lake.

NYAKATI YA KWANZA:

Kanisa: Efeso

Malaika/Mjumbe: MTUME PAULO

kipindi cha kanisa: 53AD -170AD

Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7

onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.

Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.


NYAKATI YA PILI;

Kanisa; Smirna

Malaika/Mjumbe;IRENIUS

kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD

Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe’s book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo). Japo wakristo walikuwa maskini sana  Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni  Matajiri. ufunuo 2:8-11

Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

NYAKATI YA TATU;

Kanisa ; Pergamo

Malaika/Mjumbe; MARTIN

Kipindi; 312AD -606AD

Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17

Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo

Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.

NYAKATI YA NNE:

Kanisa; Thiatira

Malaika/Mjumbe;COLUMBA

Kipindi; 606AD -1520AD

Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.

Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29

Thawabu;Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

NYAKATI YA TANO:

Kanisa; Sardi

Malaika/Mjumbe; MARTIN LUTHER

kipindi; 1520AD -1750AD

Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6

Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.

Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.

NYAKATI YA SITA;

Kanisa;Filadelfia

Malaika/Mjumbe; JOHN WESLEY

Kipindi; 1750AD -1906AD

Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ”tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda”.ufunuo 3:7-13

Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.

NYAKATI YA SABA;

Kanisa; Laodikia

Mjumbe;WILLIAM BRANHAM

Kipindi;1906- Unyakuo

Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua, watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa.

Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?. Mungu alimtuma mjumbe wake ndugu William Branham kulionya kanisa letu lirudi katika NENO na imani iliyohubiriwa na mitume pamoja na utakatifu.

Onyo; Kristo anasema kanisa liwe na bidii likatubu na kumgeukia Mungu.

Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22       

Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.

Mungu akubariki

MARAN ATHA!

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:

+255693036618/ +255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo

VIPINDI VINNE VYA MAISHA VILIVYO VIGUMU MTU KUMKUMBUKA MUUMBA WAKE.

WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

UFUNUO: Mlango wa 1

DANIELI: Mlango wa 1

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA?

Jibu ni ndio kwasababu biblia inasema pasipo kumwagika damu ya Yesu hakuna ondoleo, ukisoma waebrania 9:22 “Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. ”

Hii ndio njia pekee ambayo Mungu aliichagua tangu awali kwamba, ili tendo lolote la rohoni lifanyike na kufanikiwa ni lazima damu ihusishwe, na ndio maana tunaona katika agano la kale ilikuwa kwamba ili mtu apate kibali mbele za Mungu ni lazima aende na sadaka, ambapo mnyama alisiyekuwa na mawaa anachinjwa ili kufanya upatanisho, na mambo yote yanaliyohusishwa na dhambi yalikuwa yanatakaswa kwa damu, hiyo ilikuwa ni kanuni.

Kwahiyo tunaona damu ina mahusiano makubwa kuwa  kama kiunganishi kati ya ulimwengu wa mwilini na wa rohoni, na ndio maana hata shetani kwa kulijua hilo anapenda kutumia damu ili kufanikisha mambo yake maovu katika ulimwengu huu,

Kwamfano mara nyingi wachawi wanawaambia watu wapeleke damu za mnyama fulani ili kufanikisha mambo yao ya kishirikina pamoja na  haja za hao watu, na ukitazama kwa makini utaona kuwa wanapendelea zaidi damu za wanadamu kuliko za wanyama kwasababu wanajua hizo zina mlango mkubwa zaidi wa kuunganisha mambo ya rohoni na ya mwilini kiurahisi. Na ndio maana hao wanaotoa damu za watu utakuta matokeo yao ya kiroho(kichawi) yanakuwa ni makubwa zaidi kuliko wale wanaotoa za wanyama.

Kuna kitu kikubwa sana ndani ya DAMU ambacho mkristo akikitambua hakuna chochote kitakachomsumbua na hakika ataweza kufanya mambo yote, ataweza kufanya yote ya mwilini na ya rohoni, na kama tunavyojua  hiyo damu ili iwe na nguvu ni lazima iwe ya mwanadamu na sio mnyama, tena inatakiwa ipatikane ya mwanadamu asiyekuwa na hila wala mawaa, hakika ikipatikana hiyo ni zaidi ya tambiko lolote ambalo lilishawahi kufanyika duniani!!!

Kumbuka mambo yote yanatoka rohoni, ni ngumu kushindana na watumishi wa shetani ambao wamepata nguvu nyingi za kumkaribia shetani kwa sadaka zao za damu za watu wasio na hatia,halafu  na wewe unataka kwenda kushindana nao pasipo damu yoyote, hapo ni lazima ushindwe tu! ni lazima ujue mbinu za kumshinda adui yako, mambo ya rohoni yana kanuni zake.

Lakini habari njema ni kwamba hii damu yenye nguvu ipitayo damu zote isiyoharibika ambayo inaweza ikashinda mambo yote ipo na inajulikana, na hii si nyingine zaidi ya DAMU YA YESU ambayo haikuwa na hila wala mawaa yoyote. lakini wengi wanashindwa kuielewa matumizi yake, na ndio maana shetani anaendelea kupata nguvu juu yao, 

Jambo shetani analotaka ni waifahamu tu lakini wasiielewe matumizi yake, kila mtu anaifahamu damu ya mwanakondoo lakini ni wachache wanayoielewa, siku utakapoielewa kisawasawa utamshinda shetani kwa kila nyanja.

ukisoma;

Ufunuo 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

11 NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANAKONDOO, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. “

Unaona hapo? ni Damu tu ya mwana-kondoo inayoweza kumshinda yule joka ( shetani ) na hakuna kingine chochote. Lakini wengi wanadhani utamshinda kwa  kutamka tu  “nakukemea kwa damu ya Yesu”……akidhani hapo amempata shetani, kumbe hajui hapo hajafanya lolote kama hajaingia ndani ya hilo Agano kwanza. Ni lazima uingie kwanza.

JINSI YA KUINGIA KATIKA HILI AGANO LA DAMU YA YESU.

Kumbuka katika agano la kale kuhani mkuu alipokuwa akienda kila mwaka kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa njia ya damu za wanyama, hakuwa anafanya kwa watu wote wa ulimwengu mzima bali tu kwa wale waliokuwa katika hilo agano yaani wana wa Israeli pekee. Na ndio waliokuwa wanafunikwa dhambi zao na kushiriki baraka zote za rohoni na sio watu  wa ulimwengu mzima.

Vivyo hivyo katika Agano jipya ili maombi yako yasikiwe, ili sadaka zako zikubaliwe, ili dhambi zako zisamehewe, ili uweze kumshinda shetani na magonjwa yake yote na laana ni lazima uingie katika hili Agano jipya la DAMU YA YESU KRISTO. na hauingiii kwa kuzaliwa katika familia ya kikristo, wala hauingii kwa kujiunga na dhehebu fulani, wala hauingii kwa njia nyingine yoyote isipokuwa KWA KUTUBU kwanza, NA KUMWAMINI YESU KRISTO, NA KUBATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kisha upokee ROHO MTAKATIFU hapo ndipo umezaliwa mara ya pili na umeingia katika hili AGANO HILI KUU.

Sasa kuanzia hapo na kuendelea ile damu inaanza kunena kwa ajili yako mbele za Mungu, shetani hana la kukushinda kwa lolote, wala la kukushitaki, kwasababu damu isiyoharibika tayari ipo kunena kwa ajili yako, hauhitaji kupigana na wachawi, wala waganga, wala kuogopa magonjwa au shida, ipo hiyo damu tayari inafanya kazi kuliko tambiko lolote lililowahi kufanyika tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.

Kumbuka shetani anapotaka kuleta laana juu yako jambo la kwanza analoangalia ni je! upo chini ya damu? shetani hawezi kulaani kilichobarikiwa kama vile Balaamu alivyoshindwa kuwalaani wana wa Israeli.

Kwahiyo ndugu hakuna njia nyingine yoyote katika hii dunia unaweza ukamshinda shetani isipokuwa kwanza kutubu, na kumruhusu Yesu Kristo ayasafishe maisha yako kwa damu yake, uchukua uamuzi wa kubatizwa leo kwa ubatizo ulio sahihi wa kuzamishwa na sio wa kunyunyuziwa na iwe ni  kwa jina la YESU KRISTO kulingana na maandiko ( matendo 2:38.), kisha Bwana atakupa Roho Mtakatifu hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuingia katika lile AGANO KUU LA DAMU YA YESU, kwa uhakika wa maisha yako ya sasa na ya baadae, kumbuka hakuna ubatizo wa watoto wachanga, kama ulifanyiwa hivyo hapo hujabatizwa unapaswa ukabatizwe tena.

Nakukumbusha tena ndugu yangu hauwezi ukamshinda shetani kwa njia nyingine yoyote ile, sio kwa matendo, wala kwa juhudi yako bali kwa damu ya mwana-kondoo pekee. 

Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. “. tubu, kabatizwe na upokee Roho Mtakatifu.

Mungu akubariki!


Mada Nyinginezo:

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

MKATAE SHETANI NA MAWAZO YAKE YA KIBINADAMU.

JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?

UBATIZO WA MOTO NI UPI?

JINSI DHAMBI INAVYOMGHARIMU MTU SANA.


Rudi Nyumbani

Print this post