Upo umuhimu wa kufanya ushirika.
Ushirika unatokana na neno kushiriki. Na matokeo ya kushiriki ni kuambukizwa sifa au tabia ya kile kitu unachoshirikiana nacho.
Watu wengi hatujui hata Neno USHIRIKINA limetokana na neno kushiriki. Washirikina wanashiriki mambo ya kipepo, ili wapate sifa za kipepo, au waambukizwe tabia zao ndani yao na ndio maana wanaitwa washirikina. Ndio hapo utaona mtu anakwenda kwa mganga, kisha anapewa dawa Fulani anaambiwa anywe au aweke chini ya biashara yake, halafu itamfanya wateja wavutiwe na biashara yake. Mtu huyo analivuta pepo la mauti ndani yake, kwa ushirika anaoufanya kisa lile pepo linasimama pale na kushawishi watu waovu , kisha Yule mtu anapata anachokitafuta kwa muda, halafu mwisho wa siku pepo lile linageuka na kumuua,.kwasababu hatma ya shetani sikuzote ni kuchinja na kuiba. Lakini ikiwa mtu huyo hatofanya ushirikina wowote, hawezi kuwa na uwezo huo wa kipepo.
Sasa na katika Mungu ni vivyo hivyo. Unapokuwa nyumbani mwa Mungu Usiwe ni mtu wa kwenda na kutoka tu, kama mtembeleaji. Huna ushirika wowote na watakatifu wengine, huna ushirika wowote na Mungu,. Ukifanya hivyo hutakuwa na nguvu zozote au sifa au tabia zozote za ki-Mungu ndani yako.
Ushirika wa Kikristo Ni upi?
Kwamfano Unapohudumu, yaani unapojishughulisha na jambo Fulani ndani ya Kanisa labda kufundisha, kujitoa kwa ajili ya maendeleo ya kanisa kama kuchangia, kufagia, kujenga, kupiga deki, na vyovyote vile. Hapo ni sawa unafanya ushirika na watakatifu wengine katika kuujenga mwili wa Kristo. Na hivyo rohoni, unapokea uwezo au sifa nyingine ya ziada ambayo hapo kwanza ulikuwa huna. Na moja ya uwezo huo ni nguvu ya kuendelea mbele katika imani.
Na pia Meza ya Bwana. Huna budi kushiriki. Kwasababu hiyo inakuunganisha na Mungu moja kwa moja. Embu soma maandiko haya upate kuelewa vema;.
1Wakorintho 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. 16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, JE! SI USHIRIKA wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, SI USHIRIKA wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani”.
1Wakorintho 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.
16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, JE! SI USHIRIKA wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, SI USHIRIKA wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani”.
Umeona? Kumbe kikombe na mkate ule ni USHIRIKA.. ambao sisi tunafanya na Mungu. Na hivyo una matokeo yake makubwa rohoni. Yesu alisema mtu asipoula mwili wangu, na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake. (Yohana 6:53)
Vivyo hivyo na kutawadhana miguu watakatifu. Unapomwosha mwenzako miguu, maana yake ni kuwa unajishusha na kujinyenyekeza kwake, hivyo unapokea neema ya Upendano wa ndugu ndani yako.
Hivyo kwa ufupi ili utake kupokea tabia zote za Ki-Mungu ndani yako, kama Upendo, utu wema, furaha, amani, Uvumilivu, huna budi kuwa katika ushirika wake. Nje ya hapo, huwezi.
Matendo 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”
Usiukwepe ushirika wa Bwana.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
HUNA SHIRIKA NAMI.
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.
KANUNI RAHISI YA KUPOKEA BARAKA MARA DUFU.
HISTORIA YA BIBLIA YA KING JAMES, INA FUNZO GANI KWETU?
WANNE WALIO WAONGO.
Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?
Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
Rudi nyumbani
Print this post
Jibu: Katika biblia hakuna mahali popote panapoonyesha marehemu waliombewa..isipokuwa katika sehemu moja tu inaonyesha Marehemu mmoja aliyekuwepo katika mateso ya kuzimu aliomba ndugu zake walio hai wakahubiriwe injili ili wasifike katika dhambi na kwenda kule aliko, lakini tunaona maombi yake hayo hayakuwa na matokeo yoyote.Hebu tuisome hiyo habari..
Luka 16:27 “Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishiwa hata na mtu akifufuka katika wafu”
Umeona?..Huyu Tajiri alijaribu kuwaombea watu walio hai wasifike alipo lakini maombi yake yalizuiliwa, halikadhalika Sisi tulio hai hatuwezi kuwaombea watu waliokufa kwamba watolewe katika mateso ya kuzimu.
Kama kuna maombi ya kuwaombea wafu watoke katika mateso ya kuzimu na kuingia paradiso, basi vile vile yatakuwepo pia maombi au sala za kuwatoa watu peponi na kuwapeleka kuzimu.. Lakini kama hakuna maombi ya mtu kumtoa mtu peponi(yaani paradiso) na kumpeleka kuzimu…vile vile hakuna maombi yoyote ya kuweza kumtoa mtu kuzimu na kumpeleka peponi.
Utasema tunazidi kulithibitisha vipi hilo kimaandiko?
Hebu tuzidi kuisoma hiyo habari ya Tajiri na Lazaro…Tuangalie maombi mengine aliyoomba kuhusiana na yeye kutolewa kule.
Luka 16:23 “Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu.24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ILI WALE WATAKAO KUTOKA HUKU KWENDA KWENU WASIWEZE; WALA WATU WA KWENU WASIVUKE KUJA KWETU”.
Hapo mwisho anasema..kati Yao (hao walio kuzimu na walio peponi)..KUMEWEKWA SHIMO KUBWA kama mpaka, ili walio kuzimu wasiweze kuvuka kuingia peponi na walio peponi wasivuke kwenda kuzimu..Ikiwa na maana kuwa hakuna mwingiliano wowote wa walio kuzimu na walio peponi..Hilo shimo katikati yao lipo mpaka sasa.
Hivyo kwa hitimisho, maombi ya kuwaombea heri Marehemu au kuwaombea wapunguziwe adhabu ni maombi yasiyo ya kimaandiko na hayana matokeo yoyote… Vile vile sala za kuwaomba watakatifu waliofariki watuombee halipo kimaandiko.
Ni vizuri kutengeneza maisha yetu hapa duniani kabla ya kufa, kwa kumwamini Bwana Yesu na kutubu dhambi, kwasababu tukishakufa hakutakuwa na nafasi nyingine ya pili.
Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”.Bwana atusaidie.
Je sisi wakristo tunaruhusiwa kufanya 40 za marehemu?
MATESO YA KUZIMU.
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
USIRUHUSU INZI WATUE JUU YA ROHO YAKO.
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
Nakusalimu katika jina tukufu sana la mwokozi wetu Yesu Kristo, Nakualika katika kuyatafakari maneno ya uzima.
Leo tutajifunza siri mojawapo iliyokuwa nyuma ya watu wa zamani, ambayo tukiitumia na sisi italeta mageuzi makubwa sana katika ulimwengu huu tunaoishi. Wengi wetu tunadhani watu wa leo wanayoakili zaidi ya kuwashinda wale, lakini ukweli ni kwamba yapo mambo mengi yalifanywa na watu wa kale, ambayo mpaka leo hatuwezi kuyafanya. Mfano mmojawapo ni yale mapiramidi yaliyopo Misri (ambayo yapo katika maajabu saba ya dunia), teknolojia iliyotumika pale, hadi sasa hakuna ujenzi unaoweza kuwa kama ule, ijapokuwa tunazo teknolojia kubwa na za kisasa.
Tukisoma katika maandiko tunaona, Jinsi Babeli ilivyoanza kujengwa na kusitawi. Lakini hilo halikuwa jambo zito, kwasababu miji mingi pia ilikuwa inajengwa. Jambo lililoipelekea Babeli kuwa tofauti na miji mingine ni pale watu walipotaka kuunda Mnara, ndani ya mji ule, lengo lao likuwa ni kufika MBINGUNI, ili wajipatie jina. Sasa wengi wetu tunaona kama walikuwa ni wajinga kuunda hiyo Projekti yao. Tunadhani walikuwa wanafanya jambo la masiara au walikuwa hawaelewi kitu wanachokifanya. Ni sawa na leo mtu akumbie ninaunda ndege, ambayo itanifikisha mbinguni, ni rahisi kusema amerukwa na akili. Lakini maandiko yanatuonyesha watu hawa, walikuwa wanajua wanachokifanya mpango huo wangeweza kufanikiwa kama Mungu asingeingilia kati. Embu tusome habari hiyo tuombe jambo hilo;
Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. 3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. 5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, WALA SASA HAWATAZUILIWA NENO WANALOKUSUDIA KULIFANYA. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.
Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, WALA SASA HAWATAZUILIWA NENO WANALOKUSUDIA KULIFANYA.
7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.
Umeona hapo? Mungu hakusema hawa watu wamerukwa na akili, wanafanya kazi isiyokuwa na faida, bali alisema hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Maana yake ni kuwa watafanikiwa, Hivyo Mungu akaangalia NGUVU yao ya kufikia adhma yao ipo wapi? Akaona kuwa sio katika ile teknolojia, bali katika ule USEMI MMOJA waliokuwa nao.
Usemi maana yake ni NIA. Hawa watu waliingia maagano,wakapatana kwa moyo mmoja, kwamba kila mmoja atajitoa kwa akili, hali na mali, kuhakikisha Mnara huo unajengeka na kilele chake kinafika mbinguni, hata kama itawagharimu miaka 1000, lakini mwisho wa siku ni lazima wafike mbinguni. Lakini Mungu akaenda kuuchafua usemi wao wakawa hawaelewani baada ya pale, kwasababu walichokuwa wanakijenga ni kwa ajili ya JINA LAO na sio jina la MUNGU. Hivyo Usemi wao ukachafuliwa wakawa hawaelewani, mpaka na lugha zao zikageuzwa pia.
Ni nini Bwana anataka tuone hapo,
Ni nguvu ya USEMI MMOJA.
Na sisi kama kanisa la Kristo lililo hai. Nafasi yetu ya kuufikia utukufu WOTE wa Mungu ulio mbinguni tunao.
Kwasababu Tayari siku ile ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alirudisha USEMI HUU mmoja katikati yetu. Na ndio maana siku ile utaona watu walianza kunena kwa lugha za mataifa mengine magheni, kuonyesha kuwa Sasa Mungu anataka mataifa yote wakaribie waliunde taifa la Mungu haijalishi lugha zao, jinsia zao, rangi zao. Alikuwambusha tukio lile la Babeli, kwamba sasa lianze kufanyika tena kwa jina la Bwana.Watu wale wakatii na siku ile ile kanisa likaanza. Mnara wa Mungu ukaanza kujengwa duniani.
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. 7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia. 10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,.11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu. 12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia.
10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,.11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.
12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
Na ndio maana hatushangai kwanini Kanisa la kwanza lilikuwa na mapinduzi makubwa sana. Kwa kipindi kifupi sana injili ilinea duniani kote, na walikuwa hawana vyuo vya biblia. Ni kwasababu walikuwa na USEMI mmoja.
Lakini leo kanisa limevunjika vunjika, shetani kalisambaratisha, kachafua lugha yetu. Hata ndani ya kanisa moja kila mmoja anao usemi wake. Ijapokuwa wote mnaliamini Neno hilo hilo moja. Kwasababu gani, ni kwasababu tunatafuta utukufu wetu wenyewe na sio ule wa Mungu.
Ni kweli tutaunganishwa na Neno lakini tusipotaka kujishusha na kutii, ili tumwinue Kristo na sio sisi wenyewe, kamwe hatutaona utukufu wa Mungu kama vile inavyopaswa. Hatutaufikia moyo wa Mungu mbinguni, hatutaona udhihirisho wa wazi wa Miujiza mikubwa ya Mungu katika kanisa. Ni sharti tujikane nafsi zetu kila mmoja tumfuate Yesu , ili tuujenge mnara huu wa Bwana.
Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28 Maana ni nani katika ninyi, KAMA AKITAKA KUJENGA MNARA, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? 29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki”.
Tufahamu kuwa kanisa sio shirika la kijamii, sio huduma, wala sio chuo Fulani, bali ni udhihirisho wa Mungu duniani kupitia watu wake aliowakomboa. Hivyo ni lazima sisi kama viungo vya Kristo tujishikamanishe tuwe mwili mmoja Ili Kristo atende kazi zake duniani kama alivyokuwa anatenda zamani. Na hii inaanza na mtu mmoja mmoja, pale tunapodhamiria kuyatii maneno ya Kristo.
Bwana atujalie kuliona hilo.
Shalom.
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
Pentekoste ni nini?
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.
Kibiriti ni kitu gani? kama kinavyozungumziwa kwenye maandiko?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Jibu: Kushuhudia kunatokana na neno “Ushuhuda”. Mtu anayetoa taarifa ya jambo fulani alilolishuhudia au aliloshuhudiwa basi hapo anatoa ushuhuda.
Kwamfano mtu anaweza kuona ajali ya gari na akaenda kuwaelezea watu wengine tukio zima jinsi lilivyokuwa, hapo ni sawa na ametoa ushuhuda au amewashuhudia watu ajali ile.
Vile vile katika Ukristo, mtu anayewaelezea wengine mambo aliyoyaona au kuyasikia kumhusu Yesu…yani wema wake aliomtendea, au aliowatendea watu wengine, hapo ni sawa na kusema anawatolea ushuhuda au anawashuhudia wengine habari za Yesu.
Lakini tukija katika neno “Kuhubiri”…lenyewe ni neno pana linalojumuisha kushuhudia, kufundisha, kuonya, na kutoa maoni.
Kwamfano mtu aliyeshuhidia tukio la ajali ya gari na akaenda kulielezea/kulishuhudia kwa watu.. na baada ya hapo akaanza kutoa mafundisho na tahadhari kuhusiana na ajali kama hizo na jinsi ya kuziepuka..mtu huyo anakuwa ameihubiri ile habari za ajali.
Vile vile mtu anayeenda kutoa ushuhuda wa wema wa Yesu na habari za kufa na kufufuka kwake na mwishoni akaanza kuelezea faida za kumpokea Yesu, na hasara za kutompokea…ni nini Yesu anataka na nini hakitaki…Mtu huyo anakuwa amevuka kutoka hatua ya kushuhudia mpaka ya kuhubiri.Na sisi kama wakristo ni lazima tuzishuhudie habari za Yesu na pia tuzihubiri
2 Timotheo 4:5 “Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako”
Maran atha.
Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?
UTARATIBU WA KUTOA FUNGU LA 10 UPOJE?.
KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?
Je! Mungu anasababisha ajali au Majanga?
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?
Je! ni sahihi kwa mkristo kupokea fedha kutoka kwa mtu anayefanya kazi haramu kama za uuzaji wa dawa ya kulevya, wizi au bangi?
Jibu: Kama wewe ni mtu uliyeokoka, aidha mchungaji, au mwalimu, au muimbaji au mshirika wa kawaida, sio sahihi kupokea fedha zozote kutoka kwa mtu anayefanya kazi haramu kama za ujambazi au wizi, au uuzaji wa madawa ya kulevya, kwasababu kwa kufanya vile ni sawa na kushiriki zile kazi.
Kwasababu huwezi kupenda fedha za mtu mwovu, halafu ukachukia na kazi zake.. Huwezi kupenda boga halafu ukachukia ua lake.. Mpaka umekikibali kitu maana yake tayari umekikubali na chanzo chake..
Hivyo kama utapokea fedha kutoka kwa mtu anayeuza madawa ya kulevya, au jambazi, tayari moja kwa moja umehakikia chanzo chake na kukikubali!, lakini kama umekikataa chanzo chake pia huwezi kukubali matunda ya chanzo hicho, Kama Bwana Yesu alivyosema katika…
Luka 6:43 “Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; 44 kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu”
Luka 6:43 “Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri;
44 kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu”
Kwahiyo kibiblia sio sahihi kwa mtu aliyeokoka kupokea fedha kutoka kwa mtu anayefanya kazi haramu, aidha kwa lengo la kuendeleza huduma, au kwa lengo la kujiendeleza yeye mwenyewe. Ni sharti kwanza mtu huyo ageuzwe njia zake kwa kumpokea Yesu kikamilifu na kubadili kazi yake hiyo kwa kufanya kazi halali, ndipo fedha zake ziwe safi. (Hapo atakuwa ameufanya mti wake kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri)
Na sio tu kupokea, vilevile watu hao wafanyao kazi haramu kibiblia hawaruhusiwi kuzipeleka fedha zao kama sadaka au zaka katika nyumba ya Mungu, kwani ni machukizo makubwa sana..
Mithali 15:8 “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake”.
Soma pia Kumbukumbu 23:18 na Mithali 21:27.
Kwahiyo ni lazima kuvifanya vyanzo vyetu kuwa safi, ndipo na matunda ya vyanzo hivyo yawe safi, lakini kama vyanzo ni vichafu hata matunda yake yatakuwa machafu tu, kwa anayetoa na anayepokea. Ndio maana asilimia kubwa ya wanaopokea fedha kutoka kwa watu wanaofanya biashara haramu, zile fedha wanazozipokea ni lazima zitakuja kuwaletea madhara kwa namna moja au nyingine, kwasababu zinakuja na roho na maagizo ya ibilisi nyuma yake.
Bwana atusaidie.
Maran atha!
Mwana haramu ni nani kibiblia? (Kumbukumbu 23:2).
Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
Atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Maana yake nini?
SWALI: Nini maana ya haya maneno Mungu aliyomwambia Ayubu kuhusiana na tabia za Mbuni?
Ayubu 39:13 Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma? 14 Kwani yeye huyaacha mayai yake juu ya nchi, Na kuyatia moto mchangani, 15 Na kusahau kwamba yumkini mguu kuyavunja, Au mnyama wa mwitu kuyakanyaga. 16 yeye huyafanyia ukali makinda yake, kana kwamba si yake; Ijapokuwa taabu yake ni ya bure, hana hofu; 17 Kwa sababu Mungu amemnyima akili, Wala hakumpa fahamu. 18 Wakati anapojiinua juu aende, Humdharau farasi na mwenye kumpanda.
JIBU: Ukianzia kusoma mistari michache ya juu katika hiyo hiyo sura ya 39, Utaona Mungu anamweleza Ayubu baadhi ya wanyama ambao wanauwezo fulani mkubwa lakini hauwasidii kufanya mambo ya msingi, kwamfano mstari wa 5-8, anamtaja punda-milia, ni mnyama anayefanana na punda, ana nguvu na uwezo wa kukimbia zaidi hata ya punda, lakini je! Anamuuliza Ayubu unaweza kumkamata na kumfanya mtumwa wako akubebe mizigo? Au akulimie. Jibu ni la!
Mstari wa 9-12, anamtaja tena, Nyati, anamsifia nguvu zake, kwamba ni nyingi sana, lakini je utaweza kumfunga nira na kumwambia akulimie shamba lako kama ufanyavyo kwa ng’ombe? Jibu ni la kwasababu jambo hilo halipo ndani yake.
Na hapa kwenye mstari wa 13-18 Anamtaja tena Ndege mbuni na sifa zake. Anasema mabawa yake ni bora na mazuri, kiasi cha kuweza kuyatamia vema mayai ardhini zaidi ya ndege wengine wote duniani. Lakini kinyume chake ni kuwa mbuni ni ndege asiyejali mayai wala vifaranga vyake kuliko ndege wote unaowafahamu. Japokuwa anaouwezo mkubwa wa kuwashinda maadui zaidi ya ndege wote, lakini uwezo wake hautumii katika mambo yaliyo na faida. Mbuni anataga popote tu, hata kando ya njia,
hawezi kutafuta sehemu iliyo salama kama ndege wengine ambao huenda sehemu za maficho na kutaga huko ili watoto wao wawe salama pindi wazaliwapo lakini yeye hilo halijali, anataga popote apaonapo, matokeo yake ni aidha mayai yake kukanyagwa na wanyama wakubwa au kuibiwa na kenge au wanyama wengine wezi. Mbuni anaouwezo wa kutaga mpaka mayai 60 na kutamia yote yakatotolewa, lakini kwa tabia yake ya kutokujali anaweza kuambulia vifaranga viwili au vitatu tu. Anaweza kuyasahau mayai yake mchangani, jua au joto la mchangani likamsaidia kotolesha.
Na akishazaa, watoto wake awahudumii, kama wafanyavyo ndege wengine wadogo, ambao huakikisha wanazunguka huko na huko kutafuta vyakula vya watoto wao. Lakini bado maandiko haya yanaonyesha jinsi gani alivyomshapu kuliko hata farasi. Mwendo wa mbuni unauzidi mwendo wa farasi yoyote duniani. Kuonyesha jinsi alivyo mwepesi kujipigania lakini sio watoto wake.
Ni nini Mungu alikuwa anamwonyesha Ayubu ni kwamba, uwezo wa kufanya jambo Fulani sio tija ya mtu huyo kulitenda, kama Mungu hakumpa moyo huo. Wapo wenye mali nyingi, lakini hawana moyo wa kusaidia wanyonge, wapo wenye vipawa vizuri lakini hawezi kumwimbia Mungu. Nguvu zao ni bure hazina faida, wapo wenye uwezo wa kufundisha lakini hawewezi kujinyenyekeza chini ya makusudi ya Mungu watumiwe ili kuujenga ufalme wa Mungu, wanakuwa tu kama punda-milia wa nyikani.
Wapo wenye uwezo wa kulichunga kundi la Mungu lakini wanakuwa kama mbuni, nguvu zao, ukubwa wao hauwasaidii katika kujali kazi ya Mungu. Lakini Bwana akikupa moyo huo, basi utafanya hata kama utakuwa ni dhaifu, utafanya tu. Na hili ndio jambo ambalo tunapaswa tumwombe Bwana . ATUPE MOYO WA KUMTUMIKIA YEYE. Tusitazame kwamba mpaka tupate kitu Fulani ndio tuweze, mpaka tukasomee uchungaji ndio tuweze kuchunga, mpaka tupate pesa ndio tuweze kuisapoti kazi ya Mungu, Bwana atupe moyo huo tangu sasa wakati hatuna uwezo wowote. Kwani huo ndio utakaotusukuma kufanya makubwa.
Lakini pia yapo mambo matatu tunaweza kujifunza:
Jambo la kwanza ni sisi wenyewe, tusiwe kama mbuni ambao hatujali kuhudumia vinavyozalika ndani ya roho zetu. Kwa kutengeneza viota vyetu mahali salama,kinyume chake tunamwachia shetani azichukue mbegu zetu rohoni zinazopandwa, tunaziacha juu juu na matokeo yake ibilisi anakuja kuzila sawasawa tu na mfano wa mpanzi ambao Yesu aliutoa juu ya zile mbegu zilizoangukia njiani ndege wakazila. Ndivyo ilivyo maisha ya wengi, wanapolisikia Neno la Mungu badala walitunze na kulipalilia ndani yao ili liwazalie matunda wao wanazembea tu, wanaishi kama wanavyotaka. Hivyo tunakuwa wapumbavu kama mbuni, kwa kutokuzalisha chochote.
Jambo la pili: Linahusu familia: Wazazi wasiowajali watoto wao, Ni wajibu kwa mzazi kuwatunza wanawe, kwa kuwahudumia kimwili na kiroho. Imekuwa rahisi leo hii wazazi kujali sana Elimu za watoto wao jambo ambalo ni zuri, lakini kuhusiana na maisha yao ya kiroho wamewaweka nyuma . Hiyo ni hatari kubwa sana, usipompa Mungu watoto wako awalee, shetani atakusaidia kuwaelea. Na matokeo yake utayaona baadaye watakapokuwa watu wazima. Kama mzazi jali sana maisha ya kiroho ya watoto wako, wapeleke Sunday school, wapeleke katika semina za watoto kanisani, wahubirie, wafundishe kuomba, kufunga, kuimba nyimbo za wokovu n.k.
Jambo la tatu: Ni kuhusu watumishi wa Mungu. Bwana hataki tuwe kama Mbuni katika eneo la kulichunga kundi lake. Tunachowaza ni kujijali sisi tu, lakini kuwafuatilia na kuwachunga kondoo wa Bwana tunaona uvivu. Tunasahau kuwa shetani huko nje! Anafanya kazi usiku na mchana kuwarudisha tena ulimwenguni. Hivyo ni angalizo kwetu sisi watumishi wa Mungu. Popote ulipo hakikisha unalilisha na kulichunga kundi la Mungu dhidi ya Yule mwovu. Tuwe na hekima za ‘chungu’
Bwana akubariki sana.
Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?
NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?
“Humfukuza punda wake asiye baba”, nini maana ya mstari huu? (Ayubu 24:3)
HUDUMA YA (ELIFAZI, SOFARI, NA BILDADI).
Kuvyaza ni nini katika biblia? (Ayubu 21:10).
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
Swali: Katika Wagalatia 3:13 maandiko yanasema Bwana Yesu alisulubiwa juu ya mti, lakini tukirejea tena Yohana 19:19, tunaona biblia inasema Bwana alisulubishwa juu ya msalaba.. je maumbile ya huo msalaba au huo mti yalikuwaje?.. je ulikuwa ni mti uliosimama kama nguzo au miti miwili iliyokutana kama alama ya kujumlisha?
Jibu: Tuirejee mistari hiyo..
Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu AANGIKWAYE JUU YA MTI”.
Na tena..
Yohana 19:19 “Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”.
Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba ambao ulikuwa ni wa malighafi ya mti, na si wa malighafi ya chuma, au ya shaba, hiyo ndio maana ya “kuangikwa juu ya mti”,
Lakini tukirudi katika umbile la msalaba wa Bwana kama ulikuwa ni wa wima mfano wa nguzo au wa kukutana mfano wa alama ya kujumlisha, ili tujue maumbile yake yalikuwaje ni lazima turejee historia kidogo, kwasababu biblia haijatoa maelezo juu ya umbile la msalaba, maelezo iliyotoa ni malighafi ya msalaba tu!.. kuwa ni malighafi ya mti kama tulivyosoma hapo katika Wagalatia 3:13.
Tukirudi katika Historia sote tunajua kuwa wakati Bwana yupo duniani, utawala uliokuwa unatawala dunia nzima ulikuwa ni utawala wa Rumi, na ndio uliomsulubisha Bwana Yesu.
Sasa kulingana na historia, warumi walikuwa na adhabu nyingi walizowahukumu nazo wahalifu. Na mojawapo wa adhabu walizozitoa kwa wahalifu wakuu ilikuwa ni kumtundika mtu juu ya msalaba, na msalaba huo haukuwa nguzo moja ndefu, hapana bali ulikuwa ni nguzo mbili zilizokutana! (kafuatilie historia).
Hivyo mtu alining’inizwa mikono ikielekezwa katika nguzo mlalo na miguu na kichwa vikielekezwa katika nguzo wima, na mwili huo ukishikiliwa na misumari, na watu walisulubiwa uchi wa mnyama pasipo hata kuwa na kipande chochote cha kuzuia hata sehemu za siri.
Lengo la adhabu hiyo ilikuwa ni kumtesa mtu huyo kwa mateso na maumivu makali, na pia kumwua kwa kifo cha aibu, kutokana na kosa lake alilolifanya. Lakini si wahalifu wote waliokuwa wanahukumiwa adhabu hiyo, bali wale waliokutwa na kosa la kustahili kusulubiwa hivyo.
Kwahiyo Bwana Yesu aliangukia katika hukumu ya namna hii ya kusulubiwa juu ya msalaba, ingawa hakufanya kosa la kustahili kuuawa!, Lakini kwasababu ilikuwa ni kwa makusudi ya ukombozi wetu ilimbidi afe kifo cha aibu kama hicho ili sisi tupone!.
Lakini swali ni je! Wale wanaoamini kuwa Bwana Yesu alisulubiwa katika Nguzo ya wima, je hawataokolewa ikiwa wameshika na kuzitenda kanuni nyingine za imani?
Jibu ni la!.. Mtu akiamini kuwa Bwana Yesu alisulubiwa katika mti uliokuwa wima, au katika Miti miwili iliyokatana kwa mfano wa alama ya kujumlisha.. haimwongezei chochote wala haimpunguzii chochote katika vigezo vyake vya kuokolewa… Suala la msingi ni kuamini kuwa Yesu aliteswa na kusulubiwa kwaajili yetu, na akazikwa na kufufuka na akapaa mbinguni, na siku ya mwisho atarudi tena kutuchukua, hivyo tutubu na kuacha dhambi, lakini Mambo mengine hayana msingi sisi kuyajua…
Aina ya mti Bwana aliosulubiwa nao kama ni mshita, au mkoko hauna maana yoyote sisi kujua… vile vile na urefu wa mti au maumbile yake hivyo havitusaidii chochote wala havituongezei kitu katika vigezo vya kuokolewa, kama tu vile sura ya Bwana isivyoweza kutuongezea kitu kwa wakati huu (kwani hakuna anayeijua sura yake lakini bado wokovu tunapata) vivyo hivyo na maumbile ya msalaba hayatuongezei chochote, bali kuzaliwa mara ya pili.
Shekina ni nini? Na Je! Utukufu wa shekina unamaana gani?
UTHAMINI WITO WA PILI WA YESU ZAIDI YA ULE WA KWANZA.
BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
Wapelelezi wa uhuru wa wakristo ni watu gani (Wagalatia 2:4)?
Majukumu ya Mzazi ni kumlea mtoto katika njia inayompasa, kwasababu hekima ya Mungu inasema, hataiacha njia hiyo hata atakapokuwa mzee.
Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”
Lakini pamoja na kumlea mtoto katika njia impasayo ya kiMungu, mzazi pia hapaswi kumchokoza mwanae sawasawa na maandiko yafuatayo…
Waefeso 6:4 “Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana”.
Wakolosai 3:21 “Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa”
Sasa utauliza nini maana ya kuchokoza?
Kuchokoza kama ilivyotumika hapo, ni “kitendo cha kumfanya mtoto awake hasira, pasipo kuwa na sababu ya msingi”
Na baadhi ya sababu hizo ambazo zinaweza kumfanya mtoto awake hasira, hata kufikia hatua ya kukata tamaa au kufanya dhambi kama za kutoa maneno mabaya mdomoni au moyoni..ni kama zifuatazo.
1.Ukali wa mzazi uliopitiliza.
Mzazi anapokuwa mtu wa kufoka mara kwa mara, na kushutumu kwa ukali mambo yasiyo na mashiko ni rahisi kumfanya mtoto akate tamaa au awake hasira, na kitendo hicho kibiblia kinatafsirika kama “Mzazi kamchokoza mwanae”.
2. Kumwadhibu mtoto mara kwa mara bila kuwa na sababu ya msingi.
Wapo wazazi ambao mtoto akifanya kosa dogo tu, tayari wamekamata kiboko na kutoa adhabu kali. Ni lazima mzazi apime kosa, kama linastahili adhabu au linastahili kuonya tu!.. Lakini sio kila kosa hukumu yake iwe viboko!. Hilo linaweza kumfanya mtoto achukizwe sana badala ya kujengeka, na kibiblia ikahesabika kama umemchokoza mwanao na si kumjenga.
3. Kumdhalilisha mtoto
Wapo wazazi wasiowatia moyo watoto wao, badala yake wanawadhalilisha mbele ya watoto wenzao, au mbele ya jamii.. Jambo kama hili pia kibiblia linatafsirika kama mzazi kamchokoza mwanae.
Tunapaswa siku zote kuwathaminisha watoto wetu mbele ya watoto wengine, vile vile kuwatia moyo katika mambo mazuri wanayoyafanya.
Na wazazi wengi hawajui kama wanawachokoza watoto wao, na kuwaharibu utu wao wa ndani kwa ukali wao.
Hivyo kama mzazi, zingatia mambo hayo (Usiwachokoze watoto wako) na Bwana atakubariki na vile vile kuwabariki watoto wako.
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
Je! Wana wenu huwatoa kwa nani? maana yake ni nini?
KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?
Usiwe na Uchungu na Mke wako!.
(Masomo maalumu kwa Wanandoa)-UPANDE WA WANAUME/ MAJUKUMU YA WANAUME.
Neno la Mungu linasema..
Wakolosai 3:19 “Ninyi waume, wapendeni wake zenu MSIWE NA UCHUNGU NAO”
Hapo biblia imetoa maagizo mawili; 1)Kupenda na 2)Kutokuwa na uchungu.
1.Kupenda:
Kila mwanaume analo jukumu la kumpenda Mke wake kuanzia siku ile alipofunga naye ndoa mpaka siku ile kifo kitakapowatenganisha!. (Na hiyo ni Amri sio ombi). Tena anapaswa ampende kwa viwango vile vile vya kama Kristo alivyolipenda kanisa..
Waefeso 5:25 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake”
Kwahiyo kila Mwanaume ana wajibu wa kumpenda Mke wake siku zote za maisha yake… Ukiona upendo kwa mke wako unapungua, basi tafuta kuurejesha huo upendo kwa gharama zote!.(Jambo hilo linawezekana kabisa endapo ukimwomba Mungu, na wewe ukitia bidii katika kuurejesha upendo)
2. Kutokuwa na uchungu nao:
Amri ya pili waliyopewa wanaume juu ya wake zao, ni “KUTOKUWA NA UCHUNGU NAO” . Na mpaka biblia inasema “wanaume wasiwe na uchungu na wake zao” maana yake ni kwamba “wanawake wana mambo mengi ambayo wakati mwingine yanaleta machungu mengi”.
Kwamfano Matumizi mabaya ya Pesa… Hili ni moja ya jambo ambalo linaweza kumletea Mwanaume uchungu, hususani kama sehemu kubwa ya fedha anazitoa yeye, na pia tabia ya kuzungusha maneno ya siri ya familia kwa marafiki au kwa watu wasio na uhusiano wowote na familia, jambo hili pia linaweza kuleta uchungu kwa mwanaume. Na pia tabia ya kurudia makosa yale yale, na tabia ya kutokusikia au kukosa umakini wa baadhi ya mambo na hivyo kusababisha hasara Fulani, au kuwa wazito kufanya baadhi ya mambo, hizi zinaweza kuleta uchungu kwa mwanaume.
Lakini kwa sababu hizo au nyingine zozote, ni amri wanaume wote kutokubali uchungu ndani yao kwasababu ya kasoro hizo za wanawake.
Sasa Kwanini ipo hivyo?
Biblia imeweka wazi kuwa ni kwasababu “wanawake ni vyombo visivyo na nguvu”..
1Petr3:7 “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, KAMA CHOMBO KISICHO NA NGUVU; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe”
Kwahiyo kama mwanamke ni chombo dhaifu, ni lazima tu kitakuwa hivyo siku zote!.. hivyo ni lazima kuchukuliana nacho katika hali hiyo.. Lakini usipokichukulia kama ni vyombo dhaifu, na kukifanya kuwa ni chombo chenye nguvu, basi utakuwa ni mtu wa kuumia moyo kila wakati, na kujikuta unakuwa mtu uliyejaa uchungu na hasira na hata kufikia kuwa mtu wa ugomvi na makelele ndani ya nyumba. Jambo ambalo ni dhambi!!
Waefeso 4:31 “UCHUNGU WOTE NA GHADHABU NA HASIRA NA KELELE na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya”
Hivyo ni wajibu wa kila mwanaume aliyeoa kutokuwa na uchungu na Mke wake.
Neno “Uchungu wa mauti” lina maana gani kibiblia?
Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18
SHINA LA UCHUNGU, LISICHIPUKE NDANI YETU.
Nini maana ya msiwe waalimu wengi (Yakobo 1:3)?
MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.
SWALI: Naomba kufahamu maana ya hivi vifungu katika maandiko
Mhubiri 9:7-10
[7]Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako. [8]Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose marhamu. [9]Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua. [10]Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
[7]Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.
[8]Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose marhamu.
[9]Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.
[10]Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
JIBU: Kitabu Cha mhubiri ni kitabu kinachoelezea uhalisi wa maisha, mambo mazuri lakini pia mambo mabaya yaliyopo duniani mwanadamu anayoyasumbukia, yasiyokuwa na faida. Pamoja na siri nyingi mwanadamu asizoweza kuzivumbua, isipokuwa Mungu tu peke yake
Kwamfano anasema Dunia imejaa uchovu usioneneka, mambo yote ni ubatili kwasababu hakuna jipya chini ya jua mwisho wa siku tutayaacha yote hapa duniani.(Mhubiri 1:8)
Lakini pia pamoja na hayo hatupaswi kuyakinai maisha, kwani pia Yana mambo mazuri ambayo mwanadamu anaweza kuyafurahia endapo ataishi katika kumcha Mungu,
Ndipo hapo anasema.ule chakula chako, uvae mavazi meupe, uishi Kwa furaha pamoja na mke umpendaye siku zote za maisha Yako, ufurahie matunda ya kazi uliyoifanya maadamu tayari Mungu ameshakuridhia…yaani tayari upo ndani ya Kristo.
Hivyo Kama Mahali Mungu alipokuweka panastahili kufurahi basi furahi tu, kwasababu ni Mungu kakubariki, huku ukiwa ndani ya Bwana, kama ni mke Bwana kakupa mfurahie, kama ni mavazi mazuri vaa..Kwani mambo hayo ni ya hapa hapa tu duniani, Bwana ametukirimia,.Hatutakwenda nayo kule ng’ambo.
Sehemu nyingine anasema.
Mhubiri 8:15
[15]Kisha nikaisifu furaha, kwa sababu mwanadamu hana neno lo lote lililo jema chini ya jua, kuliko kula, na kunywa, na kucheka; na yakuwa hilo likae naye katika amali yake, siku zote za maisha yake alizompa Mungu chini ya jua.
Hivyo mhubiri anatuambia tuhakikishe kwanza Bwana ameziridhia njia zetu. Kisha furaha ya maisha ifuate baada ya hapo, Ndio kiini cha hivyo vifungu. lakini ikiwa tutafurahia maisha, lakini Mungu yupo nyuma, hiyo inageuka na kuwa anasa na tujue mwisho wetu utakuwa ni upotevu.
Zaidi sana sehemu nyingine anasema heri, “Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo” Mhubiri 4:6 Maana yake ni kwamba ikiwa umejaliwa kimoja, lakini upo katika amani ni bora kuliko kuwa na vingi lakini katika masumbufu.
Bwana atusaidie, tuishi kwa hekima katika dunia yake aliyotupa. Pastahilipo furaha tufurahi, pastahilipo kujizuia tujizuie kwelikweli. Mambo yote yawe katika uwiano ndani ya Kristo.
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
Furaha ni nini?
Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
Nini maana ya “mtakayoyafunga duniani, yatakuwa yamefungwa mbinguni”?
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?