Jibu: Tusome,
Waefeso 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni”
Hapo maandiko yanasema tumejengwa juu ya “Msingi wa Mitume na Manabii “na si juu ya “Mitume na Manabii” .. Na pia inasema tumejengwa juu ya “Msingi” na si juu ya Misingi ya mitume na manabii. Ikiwa na maana kuwa Msingi ni mmoja tu, ambao tumejegwa juu yake, (mbele kidogo tutakuja kuuona huo msingi ni nini).
Sasa yapo maswali mawili hapo ya kujiuliza; 1) Hawa Mitume na Manabii ni akina nani na 2) Huo msingi ni nini?
1) Mitume na Manabii:
Mitume na Manabii wanaozungumziwa hapa katika Waefeso 2:20 sio hawa waliopo sasa, Bali ni wale walioandika biblia, kama Musa, Yeremia, Hosea, Ezekieli na Malaki vile vile mitume wale 12 wa Bwana pamoja na wengine kama akina Paulo, ambao waliandika biblia.
Mtu yeyote aliyepo sasa, au atakayekuja kutokea na kujiita mtume au nabii, basi afahamu kuwa andiko hilo la Waefeso 2:20 halimhusu hata kidogo. Na shetani amewapandikiza watu wengi kiburi (watu wanaojulikana kama mitume na manabii wa leo), na kuanza kujivuna kuwa wao ndio Msingi wa kanisa.. Jambo ambalo si la kweli hata kidogo.
2) Msingi
Msingi ambao sisi tumejengwa juu yake ni ule waliokuwa nao Mitume, ikiwa na maana kuwa kile Mitume walichokifanya msingi, ndicho hicho hicho sisi (kanisa la Mungu) tunajengwa juu yake. Sasa ni kitu gani Mitume na Manabii wa kwenye biblia walikifanya msingi?… Hicho si kingine zaidi ya YESU KRISTO MWENYEWE!!!. Huyu ndiye Msingi wa kanisa na ndiye aliyekuwa msingi wa mitume, na ndio msingi wetu sisi na bado ataendelea kuwa msingi siku zote.
1Wakorintho 3:11 “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, YESU KRISTO”.
YESU KRISTO ndio Mwamba ule ambao yeye mwenyewe alisema kuwa kanisa lake litajengwa juu yake.
Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”.
Umeona? Mwamba unaonenewa hapo sio Petro bali ni yeye YESU MWENYEWE!.. yaani huo Ufunuo Petro alioupata wa YESU KUWA MWANA WA MUNGU Ndio MSINGI, na NDIO MWAMBA ambao kanisa litajengwa juu yake.
Kanisa lolote leo ambao YESU sio kiini cha Imani hiyo, hilo sio kanisa la kweli, vile vile imani yoyote ile isiyomweka YESU kama msingi badala yake inawemweka mwanadamu mwingine au mnyama au sanamu basi imani hiyo ni imani ya Uongo n.k
Mahubiri yoyote yasiyomweka YESU msingi, hayo ni mahubiri kutoka kwa Yule adui.Mtumishi yoyote Yule, awe mchungaji, mwalimu, mtume, nabii au mwinjilisti asiyemweka YESU kama kiini na kitovu cha Mafundisho huyo si wa kweli, kwa mujibu wa maandiko.Vile vile mtu yeyote ajiitaye Mkristo na Yesu si msingi wa maisha yake, huyo ni mkristo jina tu wa uongo.Bwana atusaidie tumweke Yesu msingi wa maisha yetu.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa?
Nitamjuaje nabii wa Uongo?
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
Rudi nyumbani
Print this post
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Neno la Mungu linasema..
Warumi 5:1 “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo”.
Je! ni haki gani hiyo tunayohesabiwa, ambayo tukiisha ipata basi tutapata amani?
Jibu ni kwamba si haki moja!, bali ni haki ZOTE Njema!… Mfano wa hizo ni kama zifuatazo…
1.HAKI YA KUISHI MILELE.
Tunapomwamini Bwana Yesu tunapata haki ya kupata UZIMA WA MILELE.. ambayo tuliupoteza pale Wazazi wetu wa kwanza walipoasi.
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?”
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?”
Pia Yohana 3:36, Bwana Yesu anasema maneno kama hayo hayo…
2. HAKI YA KUWA NA UZIMA, NA AFYA.
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”
Hivyo magonjwa hayatatutawala, bali uzima na afya, kama tukiwa ndani ya Yesu, maana yake AFYA ni haki yetu!.. tunapopitia maradhi ya muda mrefu maana yake hapo ni shetani katudhulumu haki yetu, hivyo hatuna budi kuishindania haki yetu mpaka tuipate katika mahakama ya kimbinguni, huku tukitumia katiba yetu biblia. Na tunapong’ang’ania kwa bidii bila kuchoka, wala kukata tamaa basi tunaipata haki yetu ya kuwa wazima siku zote.
3. HAKI YA KUMWONA MUNGU.
Unapomwamini Yesu ni haki yako kumwona Mungu katika maisha haya na katika yale yajayo.. Kumwona Mungu si lazima tumwone kwa macho, bali utamwona katika maisha.. Maana yake utapitia vipindi vingi vya maisha ambavyo vitakujulisha kuwa Mungu yupo nawe, pia utaona miujiza mingi ya kiMungu ambayo itakujulisha kuwa Mungu yupo nawe, na zaidi sana kila utakapomwita Mungu utamwona..
Mathayo 28:20 “……….na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”.
4. HAKI YA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU.
Zamani Roho Mtakatifu alikuwa anashuka juu ya baadhi ya watu tu (ambao ni manabii) tena kwa kitambo kidogo, lengo ni kuwapa ujumbe kutoka kwa Mungu, na baada ya hapo anaondoka.. Kwasababu ROHO TAKATIFU ya Mungu haiwezi kukaa ndani ya Mwanadamu aliye mchafu.
Lakini baada ya Bwana YESU kuja, kaja kutuletea Haki ya sisi kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu, jambo ambalo si la kawaida..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
Hivyo yale matunda ya Roho tunayoyasoma katika Wagalatia 5:22, ambayo ni upendo, amani, furaha n.k Hayo yote ni haki yetu sisi kuyapata.. Kuwa amani ni haki yako wewe uliye ndani ya Kristo, kuwa na furaha ni haki yako.
5. HAKI YA KUFANIKIWA KIMWILI NA KIROHO.
Tunapomwamini Bwana Yesu na kukaa ndani yake, hatupati tu haki ya vitu vya kiroho, bali pia tunapata haki ya vitu vingine vya kimwili ikiwemo mafanikio.
3 Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”
Pia Neno la Mungu linasema..
2Wakorintho 8:9 “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake”.
Na haki nyingine zote zilizosalia, ni Ahadi yetu. Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana kuingia ndani ya Kristo.. Ukiwa nje ya Kristo, shetani atakudhulumu haki zako zote hizo na hakuna popote utakapokwenda kushitaki.
Bwana akubariki.
Maran atha.
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
UMEITIMIZA HAKI YOTE?
Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?
Pale unapotubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha maovu, na maisha ya kale ya dhambi, wakati huo huo Mungu anakusamehe dhambi zako kabisa kabisa. Lakini hutasikia, hisia Fulani, au badiliko Fulani la wakati huo huo, kwani fikra zako za dhambi za zale bado zitaendelea kuzunguka kwenye akili yako. Hivyo wengi wakishaona hivi wanadhani kuwa Mungu hawajawasamehe, na hivyo wanaendelea kubaki katika mashaka, au kurudia rudia kumlilia Mungu awasamehe.
Na hapa hapa shetani ndipo anapata nafasi ya kuwatesa, na kuwakandamiza, wengine wanajikuta kila siku wanaomba Toba Mungu nisikie unisamehe!, Mungu nisikie unisamehe!, kumbe tayari Mungu alishawasamehe tangu siku ile ya kwanza walipomaanisha kweli kweli kugeuka na kukataa kurudia dhambi zao.
Ndugu, fahamu hata kama wewe utakuwa na kumbukumbu la nyuma la dhambi zako, lakini kwa Mungu ni tofauti, yeye akisamehe anasahau kabisa.
Waebrania 8:12 “Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena”.
Unapokwenda mbele za Mungu, lazima uamini kwa moyo wako wote umeshasamehewa, vita vya kimawazo vinavyoanza kuja tangu huo wakati, huna budi kuvishinda, kwa kuvipinga, ukisikia moyoni mwako unaambiwa, aah! Wewe dhambi zako ni nyingi, ile dhambi ulishamkufuru Roho Mtakatifu, pinga, kataa sema mimi nimeshasamehewa kwa damu ya Yesu Kristo.
Kisha unavyozidi kufanya hivyo baada ya kipindi Fulani utaona amani ya Mungu imekuvaa.
Lakini pia ni lazima ukumbuke kuwa yapo mambo yanayochangia pia kusamehewa dhambi zetu, na yenyewe ni sisi kuwasamehe waliotukosea kama wapo.
Bwana Yesu alisema..
Mathayo 6:14 “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”.Hivyo uombapo msamaha zingatia kuwa moyo wako ni mweupe kwa wengine.
Bwana akubariki
Shalom.
NINI MAANA YA KUTUBU
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!
KIFAHAMU KIGEZO CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).
Jibu: Tusome..
Wafilipi 3:2 “Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao”
Hapa kuna makundi matatu yaliyotajwa ambayo tunapaswa tujihadhari nayo, kundi la Kwanza ni “MBWA” kundi la Pili ni “WATU WAJIKATAO” na kundi la tatu ni “WATU WATENDAO MABAYA”.
Sasa kabla ya kwenda kuangalia Mbwa ni watu wa namna gani, kwanza tuyatazame haya makundi mawili ya mwisho, ambayo ni watu wajikatao na watenda mabaya..
Watu “watendao mabaya” wanaozungumziwa hapo, ni watu walio ndani ya imani lakini wanatenda mabaya.. watu hawa biblia imetuonya tujihadhari nao, yaani tusichangamane.. Mtume Paulo alizidi kuliweka hili vizuri katika kitabu cha 1Wakorintho 5:9-11.
1Wakorintho 5:9 “Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. 10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye”.
1Wakorintho 5:9 “Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.
10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye”.
Lengo la kutochangamana na makundi haya ya watu walio ndani ya kanisa lakini ni watenda mabaya, ni ili wajisikie aibu kwa wanayoyafanya na hatimaye wageuke na kutubu.
Kundi la Pili: Ni “Watu Wajikatao”.. kumbuka hapa anasema “watu wajikatao” na sio “watu wajikataao” kuna tofauti ya kujikata na kujikataa.. hapa wanazungumziwa watu wanaojikata!.. Sasa ni watu gani hao wanaojikata?.. si wengine bali walikuwa ni wayahudi ambao walikuwa wanashinikiza tohara, kuwa ndio dalili ya kukubaliwa na Mungu..
Lilikuwepo kundi la walioamini, ambao hata sasa lipo lililokuwa linasisitiza tohara kuwa ni jambo la lazima, na kwamba mtu asipotahiriwa hawezi kukubaliwa na Mungu. Watu hawa walikuwa kweli wamemwamini Yesu lakini sheria za torati bado zilikuwa zinawaendesha, ambazo kimsingi hizo haziwezi kumkamilisha mtu, bali Neema ya Yesu pekee… kushika mwezi, mwaka, siku, sabato haya yote hayafai katika kumkamilisha mtu.
1Wakorintho 7:19 “Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu. 20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa”
1Wakorintho 7:19 “Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.
20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa”
Kwa maelezo mengine marefu kuhusiana na watu wajikatao unaweza kufungua hapa >>> WATU WAJIKATAO
Na kundi la Tatu na la Mwisho, ambalo biblia imetaja tujihadhari nalo ni kundi la “MBWA”.
Sasa utajiuliza hawa “Mbwa” ni akina nani?
Bwana Yesu aliwataja wazi kabisa hawa Mbwa ni wakina nani.. Tusome..
Mathayo 7:15 “Jihadharini na MANABII WA UONGO, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni MBWA-MWITU WAKALI. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti”
Mathayo 7:15 “Jihadharini na MANABII WA UONGO, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni MBWA-MWITU WAKALI.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti”
Umeona?… Kumbe Mbwa wanaozungumziwa hapo ni “Manabii wa Uongo” na tena hawajatwi kama Mbwa tu!, bali kama “Mbwa-Mwitu” tena wakali!.. maana yake wasiohurumia kundi.. Na hatutawatambua kwa mionekano yao, kwasababu kwa nje wamevaa mavazi ya kondoo, (wanafanana na watumishi wa kweli wa Mungu) lakini tutawatambua kwa matunda yao, maana yake kwa yale wanayoyafundisha na wanayoyaishi.
Na manabii wa uongo ni mjumuisho wa Mitume wa Uongo, wachungaji wa uongo, waalimu wa Uongo, pamoja na waimbaji wa Uongo. Kwaufupi watu wote wanaosimama kutangaza injili kwa wengine! Lakini maisha yao ya ndani si wakristo, ila kwa nje wanasifika kama watumishi wa Mungu.
Ikiwa mtu atasimama na kuhubiri injili nyingine tofauti na ile iliyoandikwa katika biblia, basi huyo kibiblia ni “Mbwa”, ikiwa mtu atahubiri injili isiyo ya wokovu, badala yake ya kumpoteza mtu au kumfanya afurahie dhambi..mtu huyo kibiblia ni Mbwa, na tumetahadharishwa kukaa mbali naye.
Nabii wa Kweli wa Mungu atakuwa kama Musa!, Mpole kuliko wote, na mwenye kuwaelekeza watu kwa Mungu na si kwake wala kwa shetani.
Kumbukumbu 13: 1 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye”
Kumbukumbu 13: 1 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye”
Je! Unaongozwa na nani?.. Manabii wa Uongo, Miujiza na Ishara au NENO LA MUNGU?.
Kumbukumbu 6:4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote”.
Kumbukumbu 6:4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote”.
Maran atha!
Watu wajikatao ni watu wa namna gani? (Wafilipi3:1).
Mstari huu una maana gani? “Tupa chakula chako usoni pa maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi”. (Mhubiri 11:1)Kutekewa maana yake nini?(Mathayo 22:12)
Mungu anatufundisha kusamehe mara saba sabini, ila Kwanini yeye hakumsamehe Adamu alipoasi?.
HAKUONA MAHALI PA KUTUA KWA WAYO WA MGUU WAKE.
VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI
Jibu: Tusome kuanzia mstari wa 8 ili tuweze kuelewa vizuri..
Mathayo 22:8 “Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili.9 Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini.10 Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? NAYE AKATEKEWA”.
“Kutekewa” kunakozungumziwa hapo si Kutekewa maji au kinywaji fulani, hapana!…Bali maana yake Ni “KUKOSA MANENO”…
Mtu anayekosa Neno la kujibu pale anapoulizwa, mtu huyo Ndio katekewa..Katika habari hiyo Bwana Yesu anatoa mfano wa mtu aliyeishiwa maneno baada ya kukutwa hana vazi la harusi.
Hali itakayokuwa kwa wengi katika Ile siku ya mwisho. Maandiko yanaonyesha kuwa katika siku ya mwisho, Bwana atawakataa watu wengi, ambao hawakuwa na vazi la Harusi walipokuwa duniani.Na vazi la harusi maandiko yameweka wazi kuwa Ni “Matendo ya haki ya watakatifu”.
Ufunuo 19:8 “Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu”
Katika siku ile wengi watadhani Ni dini zao zintakazowapa kibali Cha kuingia uzimani, wengine watadhani Ni Imani zao n.k. pasipo kujua kuwa bila utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”
Na Utakatifu hatuupati kwa nguvu zetu, Bali kwa msaada wa Bwana.
Tunapotubu kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi zetu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi Kama bado hatujabatizwa Basi Bwana anatupa Roho wake mtakatifu ambaye huyo ndiye atakayetusaidia sisi kuweza kuwa wakamilifu na watakatifu.
Hivyo tukiupata utakatifu katika maisha yetu, Basi katika Roho tutaonekana mbele zake tumevaa vazi la harusi na hivyo siku Ile hatutatekewa mbele zake, hatutaishiwa maneno.
Lakini tukiyakosa hayo, huku tukitumainia dini zetu, na madhehebu yetu, na theologia zetu… basi tujue kuwa tutakosa cha kujibu mbele zake siku Ile..
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
BALI WANA WA UFALME WATATUPWA NJE!.
TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.
MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU
Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
JIBU: Wapo wanaofikiri kwamba shetani amefungwa, atakuja kufunguliwa kipindi Fulani huko mbele, lakini pia wapo wanaodhani, shetani anaishi mahali Fulani kuzimu( aidha chini ya bahari, au kwenye sayari fulani), ambapo huko kuna amesimika utawala wake unaofanana na huu wa duniani.
Lakini ukweli ni kwamba shetani hajafungwa, wala hayupo katika eneo Fulani rasmi la mwilini, ambalo unaweza kwenda ukakutana naye.
Ikumbukwe kuwa ibilisi anafanya kazi katika ulimwengu wa roho, alipoasi mbinguni, alitupwa chini duniani, akaanza kazi yake ya kuudanganya ulimwengu mpaka akafanikiwa kuuteka ukawa chini ya milki yake, Tunalithibitisha hilo katika maneno aliyomwambia Bwana Yesu.
Luka 4:5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke
Luka 4:5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.
7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke
Hivyo shetani yupo anazunguka zunguka duniani hana makao rasmi, Alimwambia hivyo Mungu.
Ayubu 1:6 “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. 7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo”.
Atakuja kufungwa kipindi ambacho utawala wa miaka 1000 wa amani wa Yesu Kristo kuanza, na baadaye atafunguliwa kidogo, lakini kwasasa hajafungwa yupo duniani ndio chanzo cha maovu yote, wala hana eneo Fulani rasmi kwamba amejijengea anaishi huko na mapepo yake, hapana bali wanafanya kazi katika ulimwengu wa roho, wakijigawanya tu katika vitengo mbalimbali, wengine katika anga, wengine, katika mataifa, wengine katika familia moja moja, na wengine katika kila huduma/au kanisa la Kristo lilipo, wengine katika uchawi n.k.
Hivyo, sisi tutamshinda na kumpinga tu kwa kulishika Neno la Mungu, na kudumu katika maombi daima.
MBINGUNI YUPO NANI SASA?
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
POPOBAWA NI KWELI YUPO?
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
MATESO YA KUZIMU.
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
1Timotheo 5:23 “Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara”
Haya ni maneno ya mtume Paulo kwa mtoto wake wa kiroho Timotheo, Ni rahisi kuyachukulia juu juu, lakini ukitazama kwa undani utaona jinsi watu wa kale walivyojitoa kwa Bwana,bila kuruhusu hali zao za mwilini kuwakwamisha.
Kama tunavyosoma, Timotheo alikuwa ni kijana mwenye bidii sana, aliyetumika na Mtume Paulo katika kuineza injili sehemu kubwa ya dunia, lakini kijana huyu hakuwa vizuri sana kiafya kama tunavyodhani, alikuwa anasumbuliwa na tumbo, lakini kama hilo halitoshi, alikuwa pia anapatwa na magonjwa ya MARA KWA MARA, tena katika ujana na sio uzee. Ni heri magonjwa hayo yangekuwa ni ya siku moja, bali ya mara kwa mara. Paulo aliishi naye kwa muda mrefu hivyo alikuwa anamwelewa sana, anashangaa leo yupo sawa, kesho, ni mgonjwa, wiki hii yupo sawa, wiki ijayo tumbo linamsumbua sana.
Lakini katika yote hayo, hakuwa kama Dema ambaye alimwacha Paulo, akaurudia ulimwengu, yeye aliendelea kuitenda kazi ya Bwana katika madhaifu yake ya mwili, Ni mtu tu pekee ambaye Paulo alijiona amani kumwachia hata huduma yake aiendeleza duniani. Alikuwa kama Elisha kwa Eliya.
Hivyo mwishoni kabisa mwa huduma, tunaona hapa Paulo anamwandikia waraka huu na kumsisitiza, asinywe maji tu peke yake, bali na mvinyo kidogo kwa ajili ya magonjwa hayo ya mara kwa mara, Paulo hapa anampa ushauri wa kitabibu, zaidi ya ule wa kiroho, kwani zamani mvinyo , ulitumika kwa ajili ya baadhi ya magonjwa, lakini sasa kwa wakati wetu tunazo dawa za hospitalini. Unaweza kujiuliza Paulo ambaye Mungu alimtumia kwa ishara na miujiza ya kupita kawaida, angepaswa amweke, mikono, na kukemea magonjwa hayo ya mara kwa mara yamwachie, lakini alitambua kuwa si kila wakati hali itakuwa hivyo, mambo mengine Mungu anayaruhusu yatokee kwa sababu zake.
Ni kama Elisha, ambaye, alisumbuliwa na ugonjwa ambao ulikuja kumuua, lakini hakumwacha Bwana, na kusema Mungu gani huyu hanioni, aliendelea kuwa nabii wa Mungu,
2Wafalme 13:14 “Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!”
Ni nini Bwana anataka tujifunze?
Katika madhaifu yetu, kamwe tusipunguze spidi ya kumtumikia Mungu, kwasababu mambo tunayoyapitia sisi walishayapitia watakatifu wengine waliotutangulia. Kijana Timotheo, alikuwa ni mdhaifu sana kimwili, lakini aliichapa injili ya Kristo, bila kujali yamsibuyo. Alisafiri huko na huko.
Yawezekana na wewe, ni mhubiri au mtumishi wa Bwana, lakini vidonda vya tumbo, haviishi ndani yako ijapokuwa umemwomba sana Bwana aviondoe lakini bado huoni matokeo yoyote, endelea hivyo hivyo kutumika usisubiri upone, una magonjwa Fulani ya kichwa ambayo yanakuja na kuondoka, yanakuja na kuondoka, yasikukwamishe, mkumbuke Timotheo, kunywa dawa za hospitalini, songa mbele, unasumbuliwa na saratani, unasumbuliwa na sukari, inapanda, inashuka, kila siku ni kuchoma sindani, Usingoje kwanza Bwana akuponye, endelea, kwani huzijui njia za Bwana, hujui ni kwanini leo upo hivyo, huwenda amekusudia, uishi maisha marefu kuliko zaidi ya wengine katika hali hiyo hiyo ili jina lake litukuzwe, na uwaponye wengi wanaosumbuliwa na maradhi kama hayo, Elisha baada ya kufa katika ule ugonjwa wake, tunaona bado mifupa yake ilifufua wafu, Hivyo kuugua si kikwazo cha Mungu kutokututumia sisi.
Tujipe moyo tusonge mbele, Bwana anatupenda, kwani yeye mwenyewe alisema, pale tuwapo dhaifu ndipo tulipo na nguvu.
2Wakorintho12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 12.10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.
UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
Nini maana ya..“wakiwazuia watu wasioe” (1Timotheo 4:1)
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
MAUMIVU NYUMA-YA-HUDUMA.
NINI TOFAUTI KATI YA KARAMA, UTENDAJI KAZI NA HUDUMA.
KANSA/SARATANI INATIBIKA.
Jibu: Adhabu iliyompata Adamu na Hawa, haikutokana na hasira ya Mungu!.. bali ilikuwa ni matokeo ya walichokifanya.
Hebu tafakari mfano huu…. “unamwonya mtu asile kitu Fulani kwasababu unajua madhara ya hicho kitu kwamba endapo akikila basi kitamsababishia apofuke macho na hata kufa huko baadaye, kwasababu kina sumu mbaya ndani yake”.
Lakini huyo mtu ambaye ulimtahadharisha asifanye hivyo, hakukusikiliza wewe badala yake akaenda kula hicho kitu ambacho madhara yake ni kupofuka macho na hata kufa. Na siku alipokula wewe ukajua na kwa huzuni ukaenda kumwuliza kwanini ulikula?..yeye akatoa sababu zake anazozijua yeye, kisha wewe ukamwambia kwamba.. “kwasababu umekula hicho kitu basi macho yako yatapofuka siku si nyingi na pia utakufa!.
Sasa swali ni je!, kwa wewe kumwambia hivyo kwamba “atapofuka macho na kufa” je umemhukumu, au umemwambia tu mambo yatakayompata kutokana na kitu alichokifanya?.. Au je kwa wewe kumwambia hivyo, kuna uhusiano wowote wa wewe kumsamehe au kutomsamehe?.. Jibu ni la!, wewe umemwambia tu madhara ya alichokifanya na kuanzia pale utaanza kumhurumia na kumtafutia suluhisho ili ile sumu iliyoingia ndani yake iweze kutoka….
Ndicho kilichotokea pale Edeni, adhabu aliyoipata Adamu na Hawa ni kwasababu ya matokeo ya walichokifanya na si kwasababu ya hasira ya Mungu!!. Na Mungu kwa huruma zake, kuanzia pale ndio akaanza mpango wa kumponya mwanadamu kwa madhara aliyoyaingiza katika maisha yake.
Na ndipo akapata mpango bora, ambao huo utaondoa moja kwa moja madhara yaliyoingia ndani ya Mwanadamu, na mpango huo si mwingine zaidi ya ule wa kumtoa Mwanawe wa pekee YESU KRISTO, aje kufa kwa ajili ya dhambi zetu, na kutukomboa, kuanzia hapo Mungu akamtoa Adamu pale Edeni ili amweke katika mpango mpya na ulio kamili, utakaomkamilisha.
Yesu Kristo pekee ndiye tiba ya KIFO ambacho kilikuwa kimeingia katika maisha yetu tangu siku ile wazazi wetu, Adamu na Hawa walipoasi.
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi”
Yesu Kristo ndiye tiba ya mambo yote, ndiye suluhisho la matatizo yote ya maisha, na pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya lolote.
Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”.
Na nje ya Yesu Kristo hapana wokovu..
Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
Je! Umempokea Yesu katika maisha yako?.. je umebatizwa katika ubatizo sahihi? Je umepokea Roho Mtakatifu wa kweli?. Kama bado unasubiri nini?
JUMA LA SABINI (70) LA DANIELI
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
JINA LAKO NI LA NANI?
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
KWANINI TUNAPASWA KWENDA KUIHUBIRI INJILI KWA UJASIRI WOTE?
Kuna wakati Bwana Yesu alianza safari ya kuchosha ya kutembea kutoka Yerusalemu kuelekea Galilaya..lakini maandiko yanatuonyesha katika safari yake yote hiyo hakuona mahali popote pa kupumzika, japo alikatiza katika vijiji na miji midogo midogo.
Lakini alipofika Samaria mahali ambapo hapakai wayahudi, aliingia katika eneo ambalo, huwenda alihisi amani nyingi ya Mungu ikibubujika ndani yake, na hapo hapo akaona kisima cha maji akatulia apumzike kidogo.
Lakini maandiko yanatupa uelewa eneo hilo lilikuwa ni la namna gani mpaka likamfanya Yesu avutiwe nalo…yanasema..mahali pale palikuwa ni karibu na Shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe..
Yohana 4:3-8
[3]aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.
[4]Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria.
[5]Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.
[6]Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
[7]Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.
[8]Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula.
Yesu aliiiona ardhi ile katika roho, aliona mbaraka ule wa Yakobo kwa mwanawe Yusufu unavyomkaribisha pale, hivyo hakuweza kupita hivi hivi bila kutenda jambo…aliiona haki ya Yusufu inamlilia shambani kwake.. Kumbuka Israeli yote ilikuwa ni Milki ya wana wote wa 12 wa Yakobo, lakini si kila shamba la mwana wa Yakobo Yesu alipumzika.
Hivyo kitendo cha Yesu tu kutulia pale, kama tunavyojua habari watu wengi wa Samaria wakapokea wokovu akawaokoa watu ambao hawakustahili wokovu kabisa (yaani wasamaria).
Unaweza kujiuliza ni wakati gani Yakobo alimpa Yusufu shamba hilo? Waweza kusoma habari hiyo katika..Mwanzo 48:21-22
Utaona akipewa sehemu mara dufu ya wenzake.. Na hiyo yote ni kwasababu Yakobo alimpenda Yusufu kwa tabia zake njema.
Ile Tabia ya Yusufu ya kumcha Bwana alipokea thawabu sio tu za wakati ule alipofanyika kuwa waziri mkuu wa Misri.. Lakini tunaona pia hadi kipindi cha Bwana Yesu baraka zake bado zilitembea.
Leo hii ukimcha Mungu wewe kama kijana, utawasababishia wengine kupokea neema ya wokovu hata wakati ambapo haupo hapa duniani.. Kumcha Mungu ni uwekezaji mkubwa sana zaidi ya mali.
Bwana akikubariki uzao, basi huwenda vitukuu vyako vikawa majeshi hodari ya Kristo, kwasababu Yesu anapita kuangalia ni wapi mbaraka wa Yusufu upo ili apumzike?akakuona wewe.
Akikubariki mashamba au mali, siku za mbeleni aidha uwapo hai au ufapo, Kristo atapita hapo na patakuwa kitovu cha madhabahu nyingi za Mungu.
Chochote kile ukiachacho duniani, kama sio mali, kama sio shamba, kama sio vitu..basi Mungu atatumia hata mifupa yako kuwaponya wengine.. Ndivyo Mungu alivyovyafanya kwa Elisha baada ya kufa na miaka mingi kupita ameshasahaulika, amebakia tu mifupa,kaburini, lakini maiti ilipoangukia mifupa yake, ile maiti ikafufuka.
Je ni tabia gani unaionyesha kwa Mungu sasa, hadi akupe shamba lake spesheli ambalo Kristo atakuja kupumzikia hapo siku za mbeleni? Watoto wako, vijukuu vyako, vitabrikiwaje kama wewe hutamcha Mungu sasa?
Tafakari maisha ya Yusufu, kisha fananisha na yako utapata majibu. Yatupasa tuichukie dhambi, tuchukie uasherati, tuchukie wizi, tuwe waaminifu, tuishi maisha yanayompendeza Mungu sikuzote.
Na hatimaye na sisi tutakuwa wokovu kwa vizazi vyijavyo.
Bwana atuponye..Bwana atusaidie.
Shalom
WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE
Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
UVUMILIVU NA MIKAKATI YA ABSALOMU, INA FUNZA NYUMA YAKE.
Kuiaua Nchi ni kufanya nini? (Waamuzi 18:2).
Injili iliyopo kwa Samaki aina ya Eeli.
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze biblia, Neno La Mungu wetu.
Mwanzo 8:6 “Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; 7 akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. 8 Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; 9 bali YULE NJIWA HAKUONA MAHALI PA KUTUA KWA WAYO WA MGUU WAKE, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani”
Mwanzo 8:6 “Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya;
7 akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.
8 Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;
9 bali YULE NJIWA HAKUONA MAHALI PA KUTUA KWA WAYO WA MGUU WAKE, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani”
Tunaona wakati wa Nuhu kutoka safinani… Aliwaachia ndege wawili ili kupima hali ya mazingira ya nje. Na ndege wa kwanza ambaye ni “KUNGURU” aliondoka lakini hakumrudia Nuhu.. lakini ndege wa pili ambaye ni “NJIWA” Alipoondoka na kukuta nje maji yamejaa kila mahali, alirudi safinani..
Sasa ni kwanini Njiwa arudi na kunguru asirudi?.
Siri ipo katika ile sura ya Saba, kuhusiana na wanyama Najisi na wasio Najisi.
Mwanzo 7:1 “Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. 2 Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. 3 Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote”
Mwanzo 7:1 “Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
2 Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke.
3 Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote”
Sasa Kunguru yupo katika kundi la Ndege Najisi,
Walawi 11:13 “Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; 14 na mwewe, na kozi kwa aina zake, 15 na kila kunguru kwa aina zake”
Walawi 11:13 “Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu;
14 na mwewe, na kozi kwa aina zake,
15 na kila kunguru kwa aina zake”
Na njiwa yupo katika kundi la ndege Safi (yaani wasio najisi) ndio maana alikuwa anatumika katika matoleo.
Sasa tabia ya ndege/wanyama najisi ni za tofauti na zile za wasio najisi. Wanyama najisi wanakula chochote na wanaweza kuishi popote.. lakini Wanyama/ndege wasio najisi wanachagua vitu vya kula, vile vile wanachagua mazingira ya kuishi, si kila mahali wanaweza kuishi.
Ndio maana tunaona huyu kunguru alipoachiwa, alienda kuzunguka zunguka huko nje, lakini njiwa aliona mazingira ya nje si salama, bado wakati wake, na hatimaye akarudi safinani.
Sasa wanyama najisi kiroho wanafananishwa na watu wa ulimwengu huu, walio mbali na MUNGU, na wanyama Safi (yaani wasio najisi) wanafananishwa na watu wa Mungu, waliookolewa kwa damu ya thamani ya YESU KRISTO, ambao hawajitii unajisi na mambo ya dunia.
Kama vile njiwa alivyozunguka huko na huko na kuona safinani ni mahali salama katika dunia iliyoharibika.. vile vile watu wa Mungu, kamwe hawawezi kuona hii dunia ipo salama, au ni mahali pa kustarehe kuliko safinani. Na safina ni BWANA YESU!.
Ukiona unaifurahia dunia iliyochafuka, dunia iliyojaa anasa, dunia iliyo mabaya basi katika roho wewe ni najisi.. Ukiona unaufurahia uasherati, ulevi, wizi unaoendelea duniani, na hata wewe mwenyewe kuwa mshirika wa hayo, basi fahamu kuwa unafanana na Yule kunguru! Na hivyo ni najisi mbele za Mungu kulingana na biblia.
Mathayo 15:18 “….vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; 20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi…”
Mathayo 15:18 “….vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi…”
Je! wewe ni miongoni mwa walio najisi au safi? Kama bado dhambi inatawala maisha yako basi upo hatarini hivyo suluhisho ni kumgeukia Yesu kwa kutubu na kumaanisha kuacha dhambi, na Yesu atakupokea na kukupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, ambaye kupitia huyo atakutakasa kwa kukupa uwezo wa kufanya yale mema ambayo ulikuwa unashindwa kuyafanya kwa nguvu zako.
Kataa ukunguru!
maran atha!
Kwanini Mungu aliwaita Adamu na Hawa jina moja?
JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.
Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?
Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO