DON’T BE AFRAID WHEN YOU GO DOWN.

Je! Kushiriki au kujihusisha kwenye michezo ni dhambi?..

SWALI: Kama vile kutazama mpira (simba na yanga), au kucheza mipira ya kikapu n.k?

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa vimtokavyo mtu ndani ya moyo ndivyo vinavyomfanya kuwa najisi..Chochote mtu anachokifanya, au anachojihusisha nacho kinachomsababishia moyoni mwake kutoke ugomvi, ubishi, mashindano, hasira,matusi kitu hicho tayari ni najisi kwake…Biblia inasema.

Wafilipi 2: 3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake’’.

Swali je! Kuna mchezo wowote ambao ukiufuatilia haukupeleki kwenye mashindano(malumbano)?…kushindana mpaka wakati mwingine kutukana na kufanyiana mizaha. Kama upo basi huo sio najisi kwako. Biblia pia inasema… 

Wafilipi 2: 14 ‘’Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, 

15 mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu’’. 

Jiulize kuna mchezo wowote ambao ukishaisha haukupeleki kwenye manung’uniko?..yaani kuwanung’unikia wahusika wa huo mchezo, au kumnung’unikia mwenzako? Neno linasema hapo, ‘’ambao kati yao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu’’…sasa ni mwanga gani utakaoonesha endapo ukiwa ni mshabiki, au mtu wa manung’uniko, au mtu wa mizaha, au mbishi, na mtu wa mashindano? Ni kitu gani hapo kitakachomfanya mtu asiyeamini avutiwe na Imani yako?…

Jiulize tangu uanze kuwa mshabiki wa mpira kuna mtu yeyote alishawahi kuokoka alipokutazama wewe wakati unaangalia mpira, au wakati wa wewe kumaliza kuangalia mpira? Au wakati magoli yanapofungwa?..kama ulishawahi kumbadilisha mtu kwa njia hiyo, basi kwako michezo sio najisi…Lakini kama bado ujue kuwa ni dhambi kujihusisha nayo. Hebu fikiria endapo Bwana Yesu yupo duniani angekuwa ni mshabiki wa mchezo Fulani, akishamaliza kuhubiria makutano anakwenda viwanjani kutazama michezo na akitoka hapo anashindana na wanafunzi wake kuhusu ule mchezo, tungewezaje kumwelewa?..angekuwa anatuchanganya…

Na sisi hatupaswi kuwachanganya watu walio nje ya Imani yetu. Wanapaswa wavutiwe na mienendo yetu ili watoke huko na kuja huku tuliko (2 Timotheo 2:24). Swali la mwisho kabisa la kujiuliza, ni juu ya muda unaotumia katika kushabikia au kuangalia hiyo michezo, jitathimini muda unaotumia kutazama hiyo michezo, ulinganishe na muda unaotumia kusali au kuomba au kusoma Neno. Kama unatumia dakika 10 kuangalia michezo na unatumia masaa matano au Zaidi kusoma Neno, basi ni wazi kuwa Michezo sio kitu kilichochukua nafasi moyoni mwako, na kinaweza kisiwe na madhara kwako, lakini kama unatumia masaa mawili kutazama michezo na Neno la Mungu au sala unatumia dakika tano au husali kabisa Hiyo ni Ashera ndani ya moyo wako, hivyo unaishi Maisha ya dhambi.

Kama kwenye ibada unasinzia halafu kwenye michezo unachangamka hilo Ashera kwako, Kama kwenye michezo unaouwezo wa kupiga kelele kwa nguvu kwa ujasiri wote, mpaka mtaa wa pili wanasikia halafu, ibadani kumsifu Mungu unaona aibu unanong’ona kwa sauti ya chini, ni machukizo mbele za Mungu. Kwahiyo kwa ujumbla michezo yote inayozaa magomvi, chuki, matusi, hasira, uchungu,mizaha,mafarakano, utani mbaya, vinyongo, manung’uniko, mashindano,visasi, vita, makwazo, tamaa, ulevi,wizi n.k..Yote ni kutoka kwa yule Adui kwahiyo ni dhambi kujihusisha nayo.

 Ubarikiwe.

Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye
namba hizi: +255789001312/ +255693036618


Mada Nyinginezo:

KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?

JE! UMEYABATILISHA MAMBO YA KITOTO?

INJILI YA MILELE.

KITABU CHA UKUMBUSHO

KWANINI USIICHAGUE TUZO ISIYOHARIBIKA?

KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Adamu aliwasaliana na Mungu kwa lugha ipi pale bustanini?

JIBU: Biblia haijataja lugha gani ilikuwa inatumika pale Edeni, Lakini ni wazi kuwa kulikuwa na lugha Fulani iliyotumika, kwasababu Mungu ametuumba sisi wanadamu tuwe tunawasiliana kwa njia ya kuzungumza, na hatuwezi kuzungumza bila lugha.   Sasa Mwanadamu wa kwanza Adamu alivyoumbwa ni tofauti na wengine tuliofuata..sisi wengine safari yetu ilianzia katika matumbo ya mama zetu lakini sio Adamu. Adamu Mungu alimwumba mkamilifu, maana ya mkamilifu ni kwamba hajazaliwa wala hajarithi, wala hajafundishwa, yaani ameumbwa tayari ana maarifa kichwani mwake. Tofauti na sisi, tunapozaliwa itatuchukua muda mrefu sana maarifa yaingie kichwani mwetu, mpaka tuweze kuelewa hichi na kile…inachukua miaka mingi….

Ndio maana Mungu alipomtengeneza Adamu alimletea wanyama aangalie atawaitaje..Adamu akawapa majina wote pale pale…hakuhitaji kujifunza kwanza herufi na matamshi..pale pale alianza kuzungumza…Huo ni uwezo wa kipekee sana.   Kwahiyo Adamu aliumbwa na lugha tayari kichwani ambayo kwa kupitia hiyo angeweza kuwasiliana na mkewe, wanawe pamoja na Mungu..(Ingawa Mungu ana uwezo wa kuzungumza na sisi pasipo lugha na tukamwelewa).   Na lugha hiyo Adamu aliyoumbwa nayo ni wazi kuwa iliendelea kutumika kwa vizazi na vizazi mpaka wakati wa Babeli..ambapo lugha nyingi ndipo zilipozaliwa..(Mwanzo 11). Kwahiyo kuitambua lugha yenyewe hasaa ni ipi, ni ngumu inawezekana ni moja ya lugha tunazotumia sasahivi, au ilishamezwa ndani ya lugha nyingine na kupotea kabisa..  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.

MTU MWENYE KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

DHAMBI YA MAUTI

BEI YA UFALME WA MBINGUNI:

FUVU LA KICHWA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Ni dhambi kwa kijana aliyeokoka kuvaa suruali za kubana (model), kunyoa mitindo (mfano kiduku), ?

JIBU: Kumbuka mavazi tangu zamani licha tu ya kuwa na matumizi ya kujisitiri yalitumika pia kueleza hali ya mtu rohoni jinsi ilivyo. Kwamfano kwenye biblia utaona kulikuwa na mavazi ya kifalme (2Nyakati 18:9, Esta 6:8), Ni mavazi yaliyoweza kumtofautisha mfalme na watu wengine wa kawaida.Kulikuwa na nguo za magunia, tunalithibitisha hilo sehemu nyingi katika biblia, mtu akionekana amevaa mavazi ya magunia iliashiria kuwa yupo katika majonzi na maombolezo makubwa ya rohoni, pengine kwa kufiwa au kuomba toba mbele za Mungu…

Pia biblia inataja kuwa kuna mavazi ya kikahaba, (Mwanzo 38:14 ) ukisoma Mithali 7:10 inasema “Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;…mtu yeyote aliyekuwa ameonekana ameyavaa hayo” Kulikuwa na mavazi ya kikuhani pia ambayo yakivaliwa, yanamjulisha Yule ni Kuhani nk. yote hayo mtu alipokuwa akivaa yalikuwa yaashiria kitu Fulani rohoni.

Vivyo hivyo hata sasa, mavazi yanabeba tafsiri Fulani ya mtu rohoni. Kama binti wa kike anatembea barabarani kava kimini, au suruali, au top, au nguo nyepesi inayoonyesha maungo yake ya ndani, huyo tayari ni kahaba, kwasababu mavazi hayo yanavaliwa na wale makahaba wa KASINO na DISCO, ndio kitambulisho chao kule., mfano leo hii ukikutana na gari linye kibao juu kimeandikwa TAXI, huhitaji mpaka lisimame na kuliuliza kama kweli ni TAXI, moja kwa moja tokea likuwa kule mbali utalipunga mkono, lisimame kisha utapanda, kwani kibao chenyewe kinajieleza juu kwa gari lile ni la umma,

halidhadhalika ukimwona binti anatembea na nguo hizo hauhitaji kumthibitisha kama yeye ni kahaba tayari mbinguni na duniani anaonekana kama ni kahaba. Sasa kwa kijana wa kiume, suruali za milegezo, suruali za kubana (zinazojulikana kama utumbo wa kuku), hizo zinajulikana ni za wasanii wa kidunia na wanamtindo wa ulimwengu huu ambao hata habari na Mungu hawana…Lengo lao kubwa ni kuitangaza miili yao na mitindo yao.. Sasa Jiulize wewe kijana wa kikristo unayesema umeokoka unavaa milegezo,na suruali za kubana n.k. mbinguni na ulimwenguniunadhani unaonekanaje?, wewe na wanamuziki wa ulimwengu huu ni kitu kimoja hata kama utakana, ndivyo ulivyo..

Halidhadhalika unanyoa viduku, na kusuka, na kufuga rasta mtu akipita barabarani akakuita kama mmoja wapo wa wasanii wa ulimwengu wanaofanya hivyo au akikuita Bob Marley mvuta bangi utakwazika?.

Biblia inasema.

Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

2 Wala msiifuatishe NAMNA YA DUNIA HII; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.

Hilo neno hapo juu NAMNA YA DUNIA HII, linamana ya FASHION. Kabla haujafikiria kuvaa suruali ya kubana, embu mvishe kwanza Yesu, kabla hujafikiria kunyoa kiduku mnyoe kwanza Yesu, ukiona hizo nguo hawezi hata kuzitazama mara mbili , inakupasaje wewe kama hayo mambo hayamstahili Mungu, wewe unayavaa ya nini?. Hivyo ni DHAMBI kwako..

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

FASHION! NI DHAMBI KWA BINTI ZA MUNGU.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.

JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! kuchora tattoo ni dhambi?

JIBU: Biblia inasema katika kitabu cha Mambo ya

Walawi 19: 28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala MSIANDIKE ALAMA MIILINI MWENU; mimi ndimi Bwana”.

Bwana alikataza watu kuchanjwa chale kwasababu chale zote zinahusiana na ibada za wafu, au ushirikina, Bwana hajawahi kuwaagiza wana wa Israeli wanapopatwa na matatizo fulani au wanapohitaji kinga ya jambo Fulani wachanjwe chale..Hizo zilikuwa ni ibada za kipagani ambazo tunaona hapa Bwana anawaagiza wana wa Israeli wasizifuate hizo desturi…Bwana aliwaagiza kuwa tiba ya magonjwa yao ni kuzishika sheria zake basi na sio kwenda kujichanja mwilini.  

Lakini pia aliwaagiza wasiandike alama zozote katika miili yao (tattoo). Sasa wengi hawajui asili ya tattoo…watu wa zamani walikuwa hawachori tattoo kwa lengo la urembo kama sasahivi, watu wa zamani walikuwa wanachora tattoo kwenye miili yao kwa lengo hilo hilo kama la kuchanja chale, (kwa lengo la ibada) ilikuwa ni ibada za miungu, na walikuwa wanafanya hivyo kufuata maagizo ya miungu yao kuwa wanapotaka wapate jambo Fulani, au wajikinge na hatari Fulani, ni lazima wachore alama hizo katika miili yao..  

Hivyo zinaweza kuwa ni michoro ya aina Fulani ya wanyama kama vile nyoka, ndege, au wakati mwingine majina Fulani ya lugha zisizoeleweka, au alama za jua, au mwezi n.k. Na kwasababu shetani ndiye aliyekuwa nyuma ya mambo hayo basi kila aliyefanya hivyo alikuwa ananufaika kwa sehemu Fulani kwa masuala ya kishetani..ni kama tu mtu aliyechanjwa chale au anayetembea na hirizi leo, anakuwa anatembea na pepo Fulani linalomkinga dhidi ya mambo Fulani yanayohusiana na anachokiamini.   Lakini miaka ilipokwenda mbele watu waliwaona watu wanaojichora tattoo kuwa wanapendeza, hivyo pasipo kuchunguza asili la lile jambo ni ipi nao pia wakaenda kuiga mioyoni mwao wakidhani kuwa wanaweka urembo tu kwenye miili yao kumbe wanaweka uchawi na mapepo kwenye miili yao pasipo wao kujijua..wanajiongezea roho Fulani za yule adui katika maisha yao.   Kwahiyo mwili wowote wenye tattoo tayari una pepo fulani ndani yake, kwasababu asili ya tattoo au chale sio urembo bali kinga Fulani za kichawi..

Na Biblia imetuonya kuwa miili yetu inapaswa iwe hekalu la Roho Mtakatifu.  

1Wakorintho 6: 19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.  

Kumbuka hapo biblia haijasema miili yetu sisi tuliomwamini Bwana YESU kuwa ni NYUMBA YA KAWAIDA, bali ni HEKALU, hekalu ni tofauti na nyumba za kawaida, kuna nyumba za aina nyingi, zipo za kulala wageni(guest house), nyumba za kuhifandhia mizigo, nyumba za kiofisi nk lakini HEKALU ni nyumba maalumu kwa ajili ya Ibada tu!!..sasa nyumba yenye chale au yenye tattoo itakuwaje hekalu la Mungu,?..Unaona?

kwahiyo kuchora tattoo ya aina yoyote ile sio sahihi.   Kama ulijichora tattoo huko zamani, au ulichanjwa chale udogoni na sasa umempa Bwana maisha yako hiyo ni vizuri sana, ile roho nyuma ya hiyo tattoo imeondoka lakini shetani bado atakuwa na visababu vichache vichache vya kukushitaki mbele za Mungu, hivyo chukua uamuzi wa kwenda kuvifuta hivyo vitu ili shetani asipate sababu yoyote ya kukushitaki..na pia mwili wako usitumike kuitangaza kazi za shetani, kwasababu usipofuta ni sawa na kampuni fulani la matangazo..   Hivyo futa tattoo zote mwilini mwako, uuwekwe mwili wako wakfu kwa Mungu sasa ili autumie..  

Ubarikiwe.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

JE! KUBET NI DHAMBI?

JE! KUSHIRIKI AU KUJIHUSISHA KWENYE MICHEZO NI DHAMBI?

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?

AMPOKEAYE NABII KWA KUWA NI NABII, ATAPATA THAWABU YA NABII; MSTARI HUU UNAMAANA GANI?

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Mbinguni Kutakuwa na kula na kunywa?.

JIBU: Biblia haijaeleza kwa mapana na marefu mambo yatakayokuwa yanaendelea mbinguni baada ya unyakuo kupita, na ndio maana mtume Paulo anasema katika 1Wakorintho 13:9 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;..”

Hivyo kuhusu kama watakatifu watakula au hawatakula na kunywa biblia haijatoa jibu la moja kwa moja lakini tunaweza kutazama baadhi ya mistari inaweza kutusaidia kupata picha fulani. Tukisoma:

Marko 14.23 “Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote.

24 Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.

25 Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.

26 Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni”. 

Tunaona katika habari hiyo hapo, Yesu akiwaagiza mitume wake kwa habari ya kunywa katika ufalme wa mbinguni, Lakini pia tukimtazama Bwana baada ya kufufuka kwake alikuwa na mwili wa umilele wa utukufu usioweza kufa tena, wala kuugua, mwili ambao uliweza kufanya mambo makubwa zaidi yasiyoweza kufanywa na mwili wowote wa asili, ule mwili uliweza kupotea na kutokea mahali popote, uliweza kuchukua sura tofauti tofauti, uliweza kupaa, na mpaka sasa unaishi n.k. Na kumbuka pia biblia inatuambia “siku atakapodhihirishwa tutafanana naye (1Yohana 3:2)”..Sasa jambo ambalo utaliona pale alipowatokea mitume wake baada ya kufufuka kwake aliwaambia wampe chakula chochote ale.

Luka 24.41 “Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?

42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.43 Akakitwaa, akala mbele yao”. 

Hiyo inatupa picha kwa sehemu jinsi miili hii ya utukufu itakavyokuwa, haitakuwa na mipaka Fulani kwamba kwasababu ni ya umilele haitaweza kula wala kunywa. Ni kweli kabisa uzima wa hiyo miili hautakuwa tena katika vyakula, inaweza kuendelea kuishi bila ya njaa wala chakula wala kutegemea chochote kile,kwasababu asili yake ni ya kimbinguni lakini hiyo haimaanishi kuwa haitaweza kunywa wala kula. Pia kumbuka Adamu kwa asili kabla ya kuasi alikuwa mtu wa umilele, asiyeweza kufa, wala kuugua, wala kuzeeka, lakini pamoja na ukamilifu wake Mungu bado alimuumbia ndani yake kula na kunywa katika ile bustani ya Edeni. Hivyo tusubiri tuone, tukifika huko tutajua zaidi, kikubwa tu tunachopaswa kufanya sasahivi ni kujitahidi kuishi maisha ya ushindi yampendezayo Mungu ili siku ile itakapofika tusikose kuyaonja hayo mambo mazuri Mungu aliyotuandalia ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?

CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.

JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.

UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.

MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?

SWALI: Maana unanipa utata je! Ni kwamba Nisiwabariki watu asubuhi?.


JIBU: Kumbuka Neno kubariki katika biblia ni Neno pana, licha tu ya kuwa na maana ya kutoa Baraka kwa mtu lakini pia linaweza kumaanisha kushukuru, kutukuza, kusifia, kusujudia, au kuhimidi..inategemea na mahali lilipotumika.   Kwamfano mstari kama huu

Zaburi 96:2 “Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku”

Haimaanishi tu tulibariki (kwa kulitakia mema jina lake), hapana bali pia linamaanisha litukuzeni, lihimidini jina lake takatifu.   Sasa tukirudi kwenye huo mstari hapo juu, Tunaweza kuona kuna mambo mawili ambayo yamesababisha Baraka za huyu mtu zibadilishwa na kuwa laana. Jambo la kwanza ni kitendo cha yeye kumbariki mwenzake kwa SAUTI KUU. Na jambo la pili ni kufanya hilo tukio ASUBUHI NA MAPEMA.

  Mpaka mtu amsifie mwenzake kwa sauti kuu, kumbuka sio sauti tu ya kawaida hapana bali kwa sauti KUU ni wazi kuwa mtu huyo lengo lake ni asikiwe au aonekane na watu kitu anachokifanya na siku zote sifa za namna hiyo huwa zinakuwa si za kweli bali ni za kinafki. Na ndio hapo zinageuzwa na kuwa laana, mfano wake ndio ule Bwana Yesu alioutoa katika..  

Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.”

Unaona mtu huyu, kama angekuwa na nia kweli ya kubariki angemwombea yeye mwenyewe kwa siri au kwenda kuzungumza naye kawaida tu, na sio mpaka apige panda mbele.  

Pili kitendo cha mtu huyu kufanya hivyo asubuhi na mpema katika roho kuna maana kubwa sana. Sikuzote asubuhi na mapema ni wakati mtulivu ndio mwanzo wa siku, ambao mtu analazima kukatiza usingizi wake kwa ajili ya mambo ya muhimu sana. Na jambo la kwanza kabisa mtu akiamka asubuhi anachopaswa kufanya ni Kumbariki Mungu wake (kwa kumshukuru, kumwimbia na kumsifu). Ndege wakiamka asubuhi jambo la kwanza wanalolifanya ni kumsifu Mungu kwa sauti kuu ya shangwe, utawasikia kila mahali kwenye viota vyao kabla hata hawajaenda popote huko ndani wanamsifu Mungu.   Daudi aliamka ALFAJIRI na kumbariki Mungu kwa vinanda na vinubi kwa sauti Kuu sana.  

Zaburi 57:7 “Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti. Nitaimba, nitaimba zaburi, 8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, NITAAMKA ALFAJIRI. 9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa. 10 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni. 11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako”.  

Halikadhalika Mungu aliwaamsha Manabii wake, asubuhi na mapema wawpeleke habari njema za wokovu kwa watu wake(Yeremia 44:4)

Unaona Alfajiri siku zote ni ya Mungu..Ukiamka na Bwana, basi siku yako yote itakuwa ni ya Baraka.   Lakini huyu anaamka asubuhi na mpema jambo la kwanza ni kumpa mwanadamu utukufu, tena kwa sauti kubwa kana kwamba yeye ndio aliyemfanya aamke asubuhi. Hivyo mbele za Mungu kwake inakuwa ni laana. Mambo kama hayo yanajirudia hata sasa hivi ikiwa utamka asubuhi jambo la kwanza ni kukimbila SMARTPHONE yako uangalie message zote jana zilizotumwa whatsapp na facebook. Jambo la kwanza ni kuchati na kupiga simu za biashara zako, jambo la kwanza ni kuamka na kuwatukuza wanadamu badala ya muumba wake, Jambo la kwanza ni kuongea na mpenzi wako ambaye hata si mke wako/mume wako.Basi fahamu kuwa hata siku yako nzima umeiharibu mwenyewe.

Mika 1: 1 “Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, kwa sababu ya katika uwezo wa mikono yao”.  

Isaya 5:11 “Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!”.

Hivyo Ujumbe mkuu hapo tuopaswa kuufahamu ni kuwa kitendo cha kusumbukia kitu kingine asubuhi na mapema tena kwa sauti kubwa kabisa, basi hicho kitu ni wazi kabisa kimekuwa ni KINGA yako, na biblia imeweka wazi kuwa amelaaniwa mtu Yule amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake. (Yeremia 17:5).   Alfajiri ikiwa ni ya Bwana, basi yaliyosalia nayo yatabarikiwa.

Warumi 11:16 “Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika”

Ubarikiwe.

Print this post

Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?

SWALI: 2 Samweli1:17-18. Inasema: Daudi akamwomboleza Sauli,na Yonathani, mwanawe,…”(Kama ilivyoandikwa katika KITABU CHA YASHARI’).Hicho kitabu cha Yashari ni kipi?


JIBU: Kumbuka Biblia sio kitabu cha kinabii tu kutabiri mambo yajayo peke yake, hapana bali pia ni kitabu kilichorekodi historia ya mambo yaliyopita, Na hiyo yote ni ili kutufundisha na kutuonya sisi kwa mifano iliyo hai ambayo ilishawahi kutokea huko nyuma,tuamini na kugeuka,

Hivyo sikuzote ili historia iweze kukubalika kuwa ni kweli ipo wazi kuwa ni lazima iwe imetibitishwa kwa ushahidi zaidi ya mmoja,   Kwa mfano haiwezekani historia ya vita vya Kagera ijulikane na watanzania tu peke yao watu wengine duniani wasiifahamu, yaani tujitangaze duniani kote sisi tulipigana vita na Uganda, lakini hakuna taifa hata moja lililoona hilo na kuthibitisha habari hiyo, kwa namna moja au nyingine zinaweza zikawa ni habari za kuzusha tu, lakini kama jirani zetu wakenya walishuhudia ni kweli, waganda walishuhudia ni kweli tulipigana nao, na Waafrika wote waliokuwepo kipindi kile watashuhudia jinsi walivyoshirikiana na sisi katika vita vile, basi hiyo vita kwa asilimia zote itakuwa ni ya ukweli na ilishawahi kupiganwa na hata kwa vizazi 100 vijavyo havitaweza kukana kwa ushahidi huo.  

Vivyo hivyo biblia nayo, ilivyoandika habari, kwa kuwathibitishia watu kuwa hayo yote ni kweli ikiwa kama mtu atatokea hatoamini kilichoandikwa, basi vipo vitabu vingine ambavyo vimerekodi habari za matukio hayo hayo biblia iliyoyarekodi, na mojawapo ndio hichi kitabu cha YASHARI ambacho tunaona kimeandika maombolezo ya mashujaa na sehemu nyingine matendo makuu yaliyofanywa na mashujaa wa Israeli.   Sasa tafsiri ya hilo Neno Yashari “NI MTU MWEMA AU MTU MTU WA HAKI”, hili ni Neno la Kiyahudi, hivyo kitabu cha Yashari ni kitabu cha mtu mwema, au mtu wa haki, na kitabu hichi katika biblia hakijazungumziwa hapa tu tunakisoma pia katika kitabu cha Yoshua :

Yoshua 10:12 “Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.

13 Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. Hayo, Je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha YASHARI? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima”.


Unaona, vipo pia vitabu vingine vinatajwa mbali na hii biblia yetu, ukisoma Hesabu 21:14, utaona kimoja kinaitwa kitabu cha VITA VYA BWANA. Ukisoma pia (1Nyakati 29:29), Utaona kulikuwa na kitabu kinachojulikana kama KITABU CHA TAREHE CHA SAMWELI MWONAJI, kulikuwa na kitabu cha tarehe ya Nathani nabii, na pia kulikuwa na kitabu cha tarehe ya Gadi mwonaji; Pia kulikuwa na kitabu cha tarehe cha wafalme wa Yuda, ukisoma (1Wafalme 14:29), utaliona hilo:..

1Wafalme 14:29 “Na mambo yake Rehoboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?”

Unaona vyote hivyo vilinakili matukio ambayo biblia ilirekodi pia. Lakini sasa hiyo haimaanishi kuwa ni vitabu vilivyovuviwa na Roho Mtakatifu kwamba vitumike kuwa mbadala wa Biblia hapana, Hivyo vipo kuithitisha kuwa Biblia ni kweli na sio biblia kuthibitisha kuwa vitabu hivyo ni kweli.   Halikadhalika leo hii, utasema mimi siiamini kuwa biblia ina habari za ukweli, wala siamini kama YESU alizaliwa na bikiria kwa uweza wa Roho Mtakatifu, wala siamini kama alipaa, hizo ni hadithi za kutunga tu, zilibuniwa tu na watu Fulani Rumi, lakini nataka nikuambie vipo vitabu vingi vya historia na vya kidini mbali na hiyo biblia unayoitilia mashaka na vyote vinathibitisha ujio wa kwanza wa Yesu Kristo kuwa ni yeye pekee ndiye aliyezaliwa na bikiria kadhalika vinathibitisha ujio wake wa pili duniani kuwa atakuja kuuhukumu ulimwengu wote. na mojawapo wa vitabu hivyo ni QURAN!..

Sasa sio kwamba Qurani ni kitabu cha kweli cha Mungu hapana, kina mambo mengi sana yasiyo ya ukweli, lakini ndani yake kibebea chembechembe ndogo za ukweli kwamba ni kweli alishawahi kutokea Mtu wa kipekee aliyezaliwa bila dhambi na kuishi duniani anayeitwa YESU, na huyo atarudi tena mara ya Pili.   JE! Mambo yote Yesu aliyoyafanya tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake, na kurudi kwake hayakuandikwa katika kitabu cha waislamu Quran?. Ni uthitisho gani tena unahitaji?   Utakwenda wapi uukimbie uso wa Mungu, na ukweli uliopo katika Kristo Yesu?. Tubu leo YESU ndiye Njia kweli na uzima, NA YUPO MLANGONI KURUDI TENA, Hakuna tumaini nje ya yeye. Wala siku ile hakutakuwa na cha kujitetea.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

JE! VITABU VYA BIBLIA VILIWEZAJE KUKUSANYWA PAMOJA?

VITABU VYA BIBLIA: SEHEMU YA 1

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)

SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?

WITO WA MUNGU

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! tunaruhusiwa kumuombea mtu ambaye haweki bayana kile anachohitaji kuombewa?

SWALI: Je! Kwetu SISI WATAKATIFU mtu akikuambia umuombee anaTATIZO halafu ukimuuliza ni tatizo gani asikuambie tatizo(Anasema hilo ni siri yake moyoni)-Huyo Tumuombee hilo tatizo lake la siri yake moyoni au?? Karibuni wapendwa..


JIBU: Kuna maombi ya kuombeana sisi kwa sisi ambayo hayahitaji mtu kumuhadithia mwingine ili amwombee, kwamfano kumwombea ndugu yako, Mungu amlinde na Yule mwovu, Mungu asimsahau katika ufalme wake, Mungu ampe kuokoa, Mungu ampe afya njema, Mungu amsaidie asimame katika imani asitetereke, Mungu ampe Amani na Upendo, mafanikio n.k..hayo ni maombi ambayo kila siku tunatakiwa tuyatamke kwa ndugu zetu wote wa mwilini na rohoni, Ndio jambo ambalo Mtume Paulo pia alikuwa analifanya:

Wakolosai 1:9 “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, HATUACHI KUFANYA MAOMBI NA DUA KWA AJILI YENU, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;

10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;’’ 

Lakini yapo mahitaji mengine ambayo ni LAZIMA mtu AYANENE kwa faida yake mwenyewe, kama amedhamiria kuhitaji msaada kutoka kwa wengine. Kama mtu anayehitaji kuombewa tatizo Fulani linalomsumbua halafu haweki bayana hitaji hilo, nguvu ya kuombewa itatoka wapi, ni wazi kuwa anajizuilia Baraka zake yeye mwenyewe.

Biblia inaposema tuchukuliane mizigo, inamaanisha kuwa tusaidiane kwa kuitambua mizigo ya wenzetu, ukubwa wake, na uzito wake, ili mtu ajue ni jinsi gani kwa sehemu ya neema aliyopewa atamsaidia kuubeba, lakini kama mzigo kauficha mwenyewe ndani yake, wale wengine hata wakimwombea hawataomba ipasavyo, kwasababu hawatajua ukubwa au uzito wa tatizo lenyewe. 

Jaribu kufikiria labda mtu ana ugonjwa ambao unamsumbua kwa muda mrefu, halafu hataki kuwaambia watu wanaomwombea kuwa anaumwa yeye anasema niombeeni tu..wale watu kweli wataomba pamoja naye lakini hiyo itaishia pale pale, lakini kama mfano kama angeweka bayana kuwa anasumbuliwa na ugonjwa Fulani (akautaja jina) na ameshahangaika muda mrefu bila matumaini yoyote, sasa kwa kuzungumza tu vile tayari katika roho anauchukua ule mzigo wake na kuwapa wengine, ndio hapo inatokea wale wenzake wanaguswa sana na shida yake, huruma zinawajaa ndani, wanaamua hata kutenga muda wao kufunga na kuomba kwa ajili ya shida yake, wengine wanampa maneno ya faraja ya kimaandiko, wanakuwa karibu naye kila siku, wengine wanaguswa wanamsaidia katika mahitaji machache ya mwilini kama kuna ulazima, na mwisho wa siku Yule mtu uponyaji wake unamfikia kwa haraka zaidi kwasababu walikuwepo wengine kuuchukua mzigo pamoja naye..

 Hivyo ni lazima tujue kuwa kuna aina ya mahitaji ambayo mtu anaweza kukuombea bila hata ya kueleza siri ya moyo wako, lakini kuna mahitaji mengine kwa faida yako mwenyewe, unapaswa uwaambie ndugu wengine waaminifu, kumbuka pia sisemi kuwa kila jambo umweleze mtu, hapana, yapo mengine hayapaswi kuwekwa hadharani bali kwa watu uliowathibitisha kuwa ni waaminifu kwa Mungu. Kuna vitu vitu kama ukimwi, kesi za mauaji, n.k. hizo tafuta tu watumishi waaminifu wa Mungu, lakini vitu vingine kama magonjwa ya kawaida, ndoa, migongano, uzinzi n.k. Zungumza kwa ndugu wengine.

Lakini usikae na tatizo lako moyoni ikiwa unahitaji kweli kuombewa na wengine. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

KWANINI KUNA WATU WANAFANYIWA DELIVERANCE LAKINI BAADA YA MUDA WANARUDIWA TENA NA HALI ILE ILE?

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Samweli aliruhusuiwa kuhudumu hekaluni kama vile Walawi wakati yeye ni mu-Efraimu?

SWALI: Katika Biblia tunaona, ni Makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kuhudumu katika Hema ya Mungu, na ndio walioruhusiwa kuingia ndani ya nyumba ya Mungu,ambao walikuwa ni wa kabila la LAWI mwingine yeyote akiingia kule anakufa, lakini katika biblia hiyo hiyo tunamwona mtoto Samweli ambaye hakuwa Mlawi aliwekwa ndani ya ile hema mbele ya lile sanduku la agano, na hakufa na tunasoma Baba yake aliyeitwa ELKANA alikuwa anatokea katika kabila la EFRAIMU, ukisoma 1 Samweli 1 utaona jambo hilo. Hapo nahitaji ufafanuzi kidogo.


JIBU: Tukisoma

1Samweli 1:1 inasema

“ Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, MWEFRAIMU”.  

Ni kweli kabisa kwa sentensi hiyo inaonyesha dhahiri kuwa Baba yake Samweli alikuwa ni Mwefraimu, lakini ukijifunza maandiko kwa undani! Utagundua kuwa Elkana Baba yake Samweli hakuwa Mwefraimu bali alikuwa Mlawi. Kumbuka wakati wa agano la kale, Kipindi ambacho Yoshua anaigawanya nchi ya Kaanani kwa makabila yote ya Israeli, Kabila la LAWI halikuwa na urithi wowote, Mungu aliwaweka wawe wakfu kwake kwa ajili ya shughuli ya madhabahuni tu, hivyo walipovuka Yordani walitawanywa na kukaa katikati ya makabila yote kuwahudumia watu katika masuala ya Torati na Ibada,..

Hivyo walawi waliokuwa wanakaa Dani, waliitwa wanadani, walawi waliokuwa Rubeni waliitwa warubeni, vivyo hivyo walawi waliokuwa wanakaa Efraimu waliitwa waefraimu.

Kumbukumbu 18:1 “Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake.

2 Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia”  

Sasa kuthibitisha jambo hilo kuwa Samweli alikuwa ni mlawi, turudi katika kitabu cha Mambo ya Nyakati..Tusome.

1 Nyakati 6:33 “Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, MWANA WA SAMWELI;

34 MWANA WA ELKANA, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;

35 mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;

36 mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli;

37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora;

38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.

39 Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;

40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya;

41 mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido;

42 mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei;

43 mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

44 Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;

45 mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia;

46 mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri;

47 mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, MWANA WA LAWI.

48 Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu”.  

Unaona hapo? Ukiufuatilia huo uzao wa Elkana baba yake Samweli utaona unakuja kuishia kwa LAWI. Kwahiyo ni wazi kuwa Baba yake Samweli, Elkana hakuwa Mwefraimu bali Mlawi..Mungu asingeweza kuruhusu mtu yeyote asiyekuwa mlawi kuhudumu katika nyumba yake au hema yake.   Kwahiyo Samweli alikuwa ni Mlawi, Mlawi mwenye asili ya Efraimu   Ni sawa na leo Mchaga aliyezaliwa Kenya aje kuishi Tanzania, moja kwa moja atajulikana kama ni Mkenya..kwasababu amezaliwa Kenya na si Tanzania, ingawa asili yake na kabila lake ni Tanzania.   Kwahiyo hiyo ndio sababu Elkana baba yake Samweli aliitwa Mwefraimu, ni kutokana na mahali alipotokea na sio kutokana na kabila lake.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

YONA: MLANGO 1

JE! ADAMU ALIWASALIANA NA MUNGU KWA LUGHA IPI PALE BUSTANINI?

CHAPA YA MNYAMA

NITAMJUAJE NABII WA UONGO?

PENTEKOSTE NI NINI?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia ituambia tusalimiane kwa busu takatifu. Hili busu ndio lipi?

SWALI: 1 Petro 5:14 Biblia inasema …“Salimianeni kwa BUSU LA UPENDO. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. ”….Hapo ana maana gani? Mfano Binti mtakatifu akikutana nami anibusu shavuni kisha anisalimu au Mimi nikionana na Mke wako barabarani kwa kuwa ni mtakatifu kama mimi nimbusu kisha nimsalimu SHALOM?..


JIBU: Ukisoma mstari huo kwa makini utaona biblia inasema ‘BUSU LA UPENDO’ Sehemu nyingine biblia inataja kama BUSU TAKATIFU..Unaweza kusoma hiyo katika Warumi..Warumi 16: 16 “Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.”.. Na Pia katika 1Wakorintho16:20 inasema: “Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.”…Na mistari mingine utakayoweza kukutana na hilo neno ni 2 Wakorintho 13:11, na 1 Wathesalonike 5: 24…Mistari yote hiyo inathibitisha kuwa kuna kitu kinaitwa Busu Takatifu. Sasa zamani kipindi cha Bwana wetu Yesu Kristo, na hata kabla ya hapo, kulikuwa na utaratibu wa kubusiana kama ishara ya salamu ya heshima kidogo, salamu ya kubusiana ndio ilikuwa salamu ya msingi kabisa kwa wakati huo, kama sasahivi ilivyo salamu ya kupeana mkono…kwahiyo watu walikuwa wakikutana walikuwa wanabusiana kwa nia ya kuonyesha upendo,shukrani, uthamani wa mtu n.k…Na kumbuka haikuwa busu la mdomo kwa mdomo hapana! Bali busu la mdomo kwa shavu au ubavu wa shavu. Na sasa tukirudi kwenye biblia inasema kuwa tusalimiane kwa BUSU TAKATIFU, ikiwa na maana kuwa sio Busu la mapenzi, wala sio busu la ubaya kama lile Yuda alilomsaliti nalo Bwana katika.. 

Mathayo 26: 48 “Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.

49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu”. 

Bali busu linalotajwa hapo ni BUSU LA HERI, NA BARAKA na UPENDO..Yaani mtu anambusu ndugu yake katika Kristo kwa nia ya kumtakia heri na Baraka kutoka kwa Mungu, kama mwamini. Lakini huo ulikuwa ni utamaduni wa zamani za wakati huo, ambapo Busu lilikuwa halina tafsiri nyingi tofauti tofauti kama ilivyo leo…Lakini leo hatuna utaratibu huo wa kubusiana..tuna utaratibu wa kupeana mikono…ambao huo unaweza kubeba maana kubwa zaidi au pengine hata sawa na kubusiana…Leo hii mwanamume akikutana na mwanamume mwenzake na kumbusu mbele za jamii haileti hiyo tafsiri Mtume Paulo aliyokuwa anaizungumzia hapo ya BUSU TAKATIFU, bali inaleta tafsiri nyingine…

Ingekuwa ni kwa kipindi cha wakati wake ingeweza kueleweka..Kwa wakati huu Busu takatifu linalokubalika katikati ya kanisa ni Busu kati ya dada na dada, au kati ya mzazi na mtoto na si kati ya kaka na dada ambao si ndugu, au kaka na kaka…Busu kati ya kaka na kaka inaleta tafsiri nyingine na maswali mengi,… 

Kwahiyo hapo ni muhimu kutofautisha tu salamu zinazotumika kulingana na nyakati..Mtume Paulo hakusema kuwa hilo ni agizo toka kwa Mungu, kwamba ni lazima kila tukutanapo tusalimiane kwa kubusiana..hapana! kwasababu salamu zinabadilika kulingana na nyakati…angekuwepo katika wakati huu ambao tunapeana mikono au kukumbatiana kama salamu badala ya kubusia, angeshauri tusalimiane kwa kupeana mikono ya Utakatifu, nk. Kwahiyo ukikutana na mwamini mwanamke, msalimie tu kwa kumpa mkono hiyo ni sawa na kumsalimia kwa busu takatifu haileti tofauti yoyote. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

NINI MAANA YA MSTARI HUU: (MTU AMBARIKIYE MWENZAKE KWA SAUTI KUU ASUBUHI NA MAPEMA; ITAHESABIWA KUWA NI LAANA KWAKE.MITHALI 27:14 )?

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

UZAO WA NYOKA.

FASHION! NI DHAMBI KWA BINTI ZA MUNGU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post