JIBU: Hili ni swali watu wengi wanajiuliza ni Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, badala yake akamwacha Hawa ajaribiwe na yeye?.
Tunapaswa tufahamu wakati mwingine Mungu anaruhusu sisi wanadamu tujaribiwe kwa makusudi maalumu ili tuujue uweza wake na asili yake kwetu sisi na pia tumjue yeye zaidi, kwamfano jaribu kufikiria tungemjuaje kama yeye ni mwokozi kama tusingepotea katika dhambi?, tungejuaje yeye ni mponyaji kama tusingeumwa, tungejuaje yeye ni wa rehema kama tusingeanguka, tungejuaje yeye ni wa neema kama tusingekuwa hatuna haki, tungejuaje yeye ni mwenye msamaha kama tusingekuwa na makosa n.k…
Kumbuka pia sikuzote dhahabu ili ing’ae lazima ipitishwe kwenye moto mkali ijaribiwe na sisi kama watoto wa Mungu ni lazima tujaribiwe na ndio maana Mungu hakumuua shetani. Hata tulipokuwa shuleni, lengo la mwalimu kututungia mitihani migumu sio kutufunya sisi tufeli, hapana bali ni kutuimarisha zaidi ili tuweze kukabiliana na changamoto za mbeleni. Na ndivyo ilivyo kwa Baba yetu wa mbinguni. Mungu ana makusudi makubwa sana na sisi chini ya jua na ndio maana anatupitisha katika njia hiyo. Tunachopaswa kufahamu ni kuwa siku zote Mungu anatuwazia mawazo yaliyo mema
Yeremia 29:11 ” Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Yote haya Mungu kayaruhusu ili kutuwekea msingi mzuri wa maisha yajayo matamu ya umilele yasiyokuwa na mwisho. Hiyo ndio sababu kwanini Mungu hakumuua nyoka mwanzoni kabisa pale Edeni kabla hajaasi.
Zaburi 103:12 “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. 13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao. 14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. 15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo”.
Ubarikiwe sana.
Mada zinazoendana:
KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?
UZAO WA NYOKA.
NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?
CHANZO CHA MAMBO.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Swali linaendelea….na kutoa fungu la kumi kwa kupitia hiyo?,kwa mfano mimi nina rafiki yangu anafanya kazi kampuni ya TBL kazi ya kampuni hii ni kutengeneza na kuuza bia kama yalivyo makampuni mengine kama Serengeti nk. Huyu ndugu ni mkristo aliyeokoka na jumapili bila shaka hutoa fungu la kumi na sadaka zingine pia ana cheo kanisani ..je! ni kuna makosa yoyote kufanya hivyo?
JIBU: Kumiliki bar ni dhambi, vilevile kumiliki lodge lenye bar ni dhambi..biblia inasema wazi katika
Kumbukumbu 23:18 “usilete ujira wa kahaba wala mshahara wa mbwa katika nyumba ya Bwana, ni machukizo”
Kumbuka na sio tu kazi ya bar tu, bali hata na kazi nyingine yoyote isiyokuwa halali mfano biashara ya madawa ya kulevya, ufisadi, ulanguzi,uuzaji pombe,wizi, kamari, uuzaji sigara n.k kamwe usijaribu kufanya hivyo ukadhani kuwa Mungu ataziridhia sadaka zako, hata kama unatoa nyingi kiasi gani au kwa moyo kiasi gani, kwa kufanya hivyo utakuwa unajichukulia laana badala ya baraka, ni machukizo mbele za BWANA, kutii ni bora kuliko dhabihu(1 Samweli 15:22) Mungu ni mtakatifu na sio mtaka-vitu.
Kwahiyo unapokwenda mbele zake ni vema kufahamu kuwa yeye ni Mtakatifu na anaihitaji roho yako sana zaidi ya vitu vyako. Kwahiyo kuhusu hiyo kazi anapaswa aache,kwasababu biblia imeturuhusu kiungo chetu kimoja kikitukosesha tuking’oe. kumiliki bar ni dhambi..Hivyo amwombe tu Mungu awe mwaminifu atampa kazi nyingine tena nzuri zaidi ya hiyo.. Mungu Alisema kuwa anajua tunayahitaji hayo yote
Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”
Kwahiyo asiwe na wasiwasi hilo suala la baada ya kuiacha hiyo kazi atakula nini? hilo amwachie Mungu.Hivyo mshauri atafute kazi nyingine inayompa Mungu utukufu.
SADAKA ILIYOKUBALIKA.
TOFAUTI KATIKA YA ZAKA NA SADAKA NI IPI?
NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.
IMANI YENYE MATENDO;
JIBU: Kuzimu ipo, na ni sehemu iliyo halisi kabisa biblia inaelezea katika (Luka 16:19-31)… Mtu anapokufa katika dhambi (yaani haujaoshwa dhambi zake kwa damu ya YESU KRISTO)..mtu anaenda moja kwa moja kuzimu/jehanum, huko kuna mateso mengi sana, mtu huyo atakaa huko akingojea ufufuo wa wafu, ambao utakuja baada ya ule utawala wa YESU KRISTO wa miaka 1000 kuisha ambapo wafu wote watafufuliwa na kuhukumiwa mbele ya kile kiti cheupe cha Hukumu..
Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ukisoma pia Yohana 5:28 BWANA YESU aliyasema maneno hayo..
“Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”
Unaona wale wanaotenda mabaya wote watafufuliwa kwa ufufuo wa hukumu, hivyo baada ya kuhukumiwa kulingana na matendo yao ndipo watakapotupwa kwenye lile ZIWA LA MOTO atakapokuwepo shetani na malaika zake, lenye mateso mengi kuliko jehanum. ni kama tu vile mtu anapokamatwa na hatia anawekwa kwanza mahabusu kwa muda fulani akisubiria kupandishwa mahakamani, sasa akishahukumiwa mahakamani kulingana na makosa yake ndipo anapopelekwa magereza kutumikia makosa yake. na ndivyo itakavyokuwa kwa waovu wote walioikataa neema ya msalaba wa Bwana YESU KRISTO watakapokufa sasa hivi wataenda kuzimu kwenye vifungo na mateso, wakingojea hukumu ya mwanakondoo kisha baadaye watatupwa kwenye lile ziwa la moto.
Lakini wanaokufa sasa katika haki, wanapelekwa mahali panapoitwa “Paradiso” . Paradiso ni mahali panapofanana na mbinguni,lakini sio mbinguni, ni mahali pa raha, wanawekwa humo kwa muda fulani wakingojea ufufuo wa wenye haki, atakapokuja Bwana mawinguni, watafufuliwa na kuvaa miili ya utukufu na kuungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja kwenda na Bwana mbinguni kwenye karamu ya mwana kondoo. Paradiso kwa jina lingine ni Peponi.
1 Wathesalonike 4: 15 “Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.”
1 Wathesalonike 4: 15 “Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.”
Hivyo ndugu fahamu kuwa kuzimu ipo. Ni sehemu halisi kabisa.
NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?
JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?
MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
SWALI:Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa watakatifu, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?
JIBU
Kwa ufupi kulingana na kalenda ya Ki-Mungu, kwasasa tunasubiria unyakuo wa watakatifu ambao huo upo karibuni sana kutokea. Wakati wowote katika kizazi chetu hichi tunachoishi jambo hilo tunaweza tukalishuhudia kwa macho yetu, Hivyo huo ndio utakoanza kwanza… Sasa baada ya unyakuo wa watakatifu kupita ambao ni watu wachache sana watakaokwenda mbinguni . Kwasababu Bwana mwenyewe alishatuonya akasema “kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Lutu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake mwana wa Adamu, wakati ule watu wachache sana waliokoka (yaani nane kwa watatu kati ya mamilioni ya watu waliokuwepo duniani) ndivyo itakavyokuwa katika siku za unyakuo..Na sehemu nyingine alisema
Mathayo 22:14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.
Hivyo anazidi kusema…
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”.
Unaona hapo kwahiyo hili kundi litakalonyakuliwa ambalo lilishakwisha jiweka tayari tangu zamani kwenda na Bwana litakuwa dogo sana tofauti na wengi wanavyodhani kwamba watu watatoweka mabarabarani,na dunia nzima kutaharuki kwa tukio hilo n.k. Hilo jambo halipo. Kundi hili litakapoondoka hakuna mtu asiyemjua Mungu atakayejua, dunia nzima itaendelea na shughuli zake kama kawaida…watakuja kufahamu baadaye mambo ya mambo kubadilika ndipo watakapojua kuwa kumbe unyakuo wa watakatifu ulishapita.
Hivyo ukishapita unyakuo wa watakatifu, sasa ndio Dhiki kuu itaanza, hii itakuwa ndani ya kile kipindi cha miaka 7 ya mwisho, wakati huo mpinga-kristo atanyanyuka ili kuihimiza ile chapa ya mnyama ianze kutenda kazi haraka, kutakuwa na dhiki isiyokuwako kwa wale wote(wanawali wapumbavu) watakaokosa unyakuo.
Ndugu Wakati huo sio wa kutamani kuwepo, kwasababu mfano wa mateso yatakayokuwepo huko Bwana anasema hayakuwahi kutokea katika kipindi chochote katika historia na wala hayatakaa yatokee mengine mfano wa hayo baada ya hapo. Na pia kumbuka dhiki hiyo vile vile haitamuhusu kila mtu duniani, hapana bali nalo litakuwa ni kundi dogo tu, tena wale watakaogundua kuwa ule ni mfumo wa shetani, wakati huo dunia nzima itaifurahia mfumo wa mpinga-kristo. kwasababu wakati huo mpinga-kristo atakuwa mwerevu ili awapate wengi hivyo Utaonekana kama ni ustaharabu mzuri sana wa amani aliouleta, na utapendwa na wengi. Na wale wote watakaojaribu kuufichua uovu wake wao ndio wataonekana kama wenyewe ndio wapinga-kristo badala yake. Sasa baada ya hawa watu (bikiria wapumbavu) kuuliwa. Kitakachofuata kitakuwa ni ile siku kuu ya Bwana ya kutisha. Ambayo Bwana aliiweka mahususi kwa ajili ya watu wote waovu.
Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. ”
Sasa Hapo ndipo Bwana atajilipizia mwenyewe kisasi juu ya mataifa yote yaliyosalia ulimwenguni yaliyopokea ile chapa ya mnyama, na watu wote yasiyomcha Mungu, hii itaambatana na yale mapigo ya vitasa 7 (Ufunuo 16). Na ndio humo humo katikati vile vita vya Har-magedoni vitapangwa, pale mataifa yote duniani yatakusanyika ili kufanya vita na mwanakondoo, Hii haitakuwa kabisa vita kwasababu Mungu hapigani na wanadamu,.Bwana anasema ule upanga(Neno lake) utokao katika kinywa chake ndio utakaowaua.
(Ufunuo 19:11-21) Hao waliokusanyika. Hivyo Bwana atawaua wote, na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani. Hapa ndipo mataifa yote ulimwenguni yataomboleza wakitamani milima iwaangukie wajisitiri na ghadhabu ya Mungu mwenyezi, (Ufunuo 6:12).
Hivyo Mungu akishayahukumu mataifa kitakachofuata ni utawala wa amani wa Bwana wetu Yesu Kristo wa miaka1000. Huko dunia itarejezwa tena katika hali yake nzuri ya mwanzo kama Edeni au zaidi ya hapo, dhambi haitatawala tena (kwasababu shetani atakuwa amefungwa wakati huo),
japo waovu biblia inarekodi watakuwepo na ndio hao baada ya ule utawala kuisha, shetani atakapofunguliwa tena kwa kipindi kifupi akawadanganye ili walete madhara, Biblia inasema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza..Hiyo ndio hiyo vita ya Gogu na Magogu inayozungumziwa kwenye(Ufunuo 20:8),
Hivyo hiyo nayo hakutakuwa vita kabisa kwasababu pindi watakapotaka kujaribu kufanya hivyo moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote.
Kisha baada ya hapo YESU KRISTO Bwana wetu atakaa katika kiti chake cha enzi CHEUPE, na wafu wote watafufuliwa wale ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza pamoja na hao waliokuwa wanataka kufanya vita na watakatifu wa Mungu ndani ya ule utawala wa miaka 1000. Wote kwa pamoja watahukumiwa kulingana na matendo yao.
Kisha baada ya hapo watatupwa katika lile ziwa la moto alipo shetani na malaika zake. Na ndipo mbingu mpya na nchi mpya zitakapokuja…Kuanzia huo wakati na kuendelea muda utaondolewa, na umilele utaanza, mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha pita tazama yamekuwa mpya…
Haleluya..Huko tutazidi kumjua Mungu kwa namna isiyo ya kawaida.Tuombe tusikose kuwepo huko,.Biblia inasema mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia, wala kuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wampendao (1Wakorintho 2:9). Mungu wetu ni mwema. Libarikiwe jina lake. Milele na milele. Amina.
SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
DANIELI: Mlango wa 1
UFUNUO: Mlango wa 16.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
UDHAIFU WA SADAKA!
JIBU: Tukisoma Kumbukumbu 10:17 inasema…
“Kwa maana Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa”.
Hapa tunaona Mungu anajitambulisha yeye kama “Mungu wa miungu” sasa swali hawa miungu ni wakina nani?. Bwana Yesu alisema mahali fulani katika kitabu cha Yohana,..
Yohana 10:33 “Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. 34 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); 36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?”
Kwahiyo unaona hapo miungu inayozungumziwa hapo ni WATOTO WA MUNGU, (yaani sisi tuliomwamini yeye na kuoshwa kwa damu yake) inadhaniwa na wengi kuwa miungu iliyozungumziwa pale ni “SANAMU” LA! sivyo. Mungu hawezi akawa ni Mungu wa sanamu. Sanamu hata siku moja haziwezi zikampa Mungu utukufu, Na tunajua tabia za miungu ni lazima zifanane na Mungu, Hivyo basi kazi zile zile Mungu anazozifanya lazima na miungu izifanye, kwa mfano Mungu alitumia NENO lake kuumba na kufanya kila kitu na sisi vivyo hivyo kwa NENO lake tunaweza tukafanya kazi za Mungu vile vile kama yeye. Lakini tusipoweza kufanya hivyo inamaana sisi sio miungu kwasababu hatufanani na yeye. ni sawasawa tu na alivyojiita yeye ni MFALME wa wafalme, au BWANA wa mabwana.
Kwahiyo ili sisi tuwe miungu lazima tuwe ni WATOTO WA MUNGU wenye tabia kama za kwake nazo ni: Upendo, Imani, Haki, Utakatifu, utu wema, kiasi n.k Wagalatia 5:22 hivyo tuzidi kutia bidii katika kumjua yeye ili tustahili kuitwa miungu.
Maelezo haya unaweza kuyapata kwa njia ya video mwisho wa somo hili
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=Jqkm6O2IdUQ[/embedyt]
BWANA YESU ALIKUWA ANAONYESHA KUWA MUNGU NI MUNGU MWENYE AKILI TIMAMU.
JE! MUNGU ANAWEZA KULETA MAJIBU KUPITIA NGUVU ZA GIZA KAMA ALIVYOFANYA KWA MFALME SAULI?
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Rudi Nyumbani
JIBU: watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?..Ni swali ambalo halikuulizwa tu na watu wa kipindi cha Bwana Yesu pekee lakini hadi sasa swali hilo linaulizwa na wengi..
Tukisoma
Luka 13:23 ″Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 24 Jitahidini kuingia katika MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. ”
Luka 13:23 ″Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. ”
Ukisoma tena..Mathayo 7:13 -14 Inasema..
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Maandiko hayo yanaeleza wazi kabisa kwamba watakaokolewa ni WACHACHE, kwasababu njia imesongwa sana! lakini swali linakuja je hii njia imesongwa na nini? Ni wazi kabisa imesongwa na mambo mengi ya ulimwengu huu ambayo ni, anasa, upendaji fedha kupita kiasi, wivu, chuki,tamaa, uasherati uliokithiri ambao sasa upo mpaka kwenye mitandao mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo, mitindo ya wanawake kutembea nusu uchi, burudani na miziki ya kidunia,ufisadi n.k. na zaidi ya yote ni kuongezeka kwa wimbi kubwa la manabii wengi wa uongo na hivyo kuifanya ile njia ya kweli isitambulike kirahisi, kwasababu imechanganyikana na njia nyingine nyingi za uongo mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, na jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo ile njia ya ukweli inavyozidi kuwa nyembamba zaidi, imefikia hatua ya kwamba ukristo wa leo unapimwa na kiwango cha mafanikio ya kidunia aliyonayo mtu na sio mafanikio ya kiroho (yaani utakatifu), Neno la kweli limetupwa nje!.
Bwana Yesu Kristo aliweka wazi pale aliposema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu? je! katika siku za Nuhu waliokoka watu wangapi? tunaona waliokoka watu 8 tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwepo duniani wakati ule..na tena alisema kama ilivyokuwa katika siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adama..je! wakati wa Lutu walipona watu wangapi?..Jibu ni dhahiri kuwa ni walipon watu 3 tu kati ya mamilioni waliokuwa wanaishi Sodoma na Gomora wakati ule. Na kumbuka Bwana Yesu hawezi kusema uongo,kizazi cha Nuhu na Lutu kimefananishwa na kizazi chetu.
NA NI KWELI KABISA! watakaookolewa katika kizazi hiki cha mwisho tunachoishi ni WACHACHE MNO!!! Hivyo ndugu tujitahidi tuwe kati ya hao wachache watakaokolewa kwa kupita hiyo njia nyembamba iliyodharauliwa na kuchekwa na ulimwengu wote nayo ni UKRISTO ULE WA MTINDO WA KALE WA MITUME..ikiwa wewe ni mwanamke tupa nguo za kizinzi uvae kama mwanamke wa kikristo mwanamke wa kikristo havai vimini, suruali wala kaptula, hapaki wanja wala lipsticks, mwanamume wa kikristo hanywi pombe, sio mtukanaji, mkristo yoyote hapaswi kupenda mambo ya ulimwengu? Bwana Yesu alisema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako.? Ni wakati wa kutafuta vitu vya kimbinguni ile siku ile isitujie kama mwivi. Muda umeenda sana tunaishi katika kizazi kibaya kushinda vyote, tuwe macho Bwana yu mlangoni kuja. Amen.
UNYAKUO.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA
WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.
JIBU: Kwa ufahamu hakuna tatizo lolote kula nyama ya nguruwe au chakula chochote ambacho mtu anaweza kukipokea kwa shukrani mbele za Mungu…biblia inasema viumbe vyote vimetakaswa na Mungu, Tukisoma
1Timotheo 4:1-5 inasema..
“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. 4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”
“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”
Hivyo vyakula vyote ni halali lakini biblia inasema tule tu kwa IMANI, ila tukila kwa mashaka ni dhambi, na pia biblia inasema anayekula asimuhukumu yeye asiyekula, wala asiyekula asimuhukumu anayekula, kwasababu tumetofautiana ujuzi, haupaswi kumkwaza mwenzako(Ndugu yako) kwa ujuzi ulionao, ukimkosea mwenzako kisa hali nguruwe ni sawa na kumkosea Kristo mwenyewe
1wakorintho 8:13 inasema “Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.”…..8:8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.
1wakorintho 8:13 inasema “Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.”…..
8:8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.
Hivyo tunafundishwa tuwe na hekima tunapokuwa katikati ya jamii fulani ya watu, iwe ni wakristo au isiwe wakristo, sio tunapofika mahali na kukuta jamii fulani hawali chakula fulani (nguruwe), na sisi tunaanza kula mbele yao na kuwaudhi. Hivyo ni sawa na kumkosea Kristo, ndio maana Paulo anasema ni “heri nisile nyama kabisa kama itakuwa ni kikwazo kwa ndugu yangu.”
Na pia tukisoma.
Warumi 14:14 “Najua, TENA NIMEHAKIKISHWA SANA KATIKA BWANA YESU, YA KUWA HAKUNA KILICHO NAJISI KWA ASILI YAKE, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. 15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya. 17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. ”
Warumi 14:14 “Najua, TENA NIMEHAKIKISHWA SANA KATIKA BWANA YESU, YA KUWA HAKUNA KILICHO NAJISI KWA ASILI YAKE, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.
15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. ”
Hivyo katika agano la kale Mungu kukataza vyakula fulani visiliwe ni kwa ajili ya kutufundisha sisi wa agano jipya mambo kadha wa kadha, kwamfano, kama vile Bwana alivyotenga vyakula najisi na visafi, ilifunua rohoni kuwa kuna vyakula vilivyo visafi na najisi (mafundisho) hivyo wajitenge na vile vichafu, na kudumu katika vile vilivyo safi, kadhalika pia, ilifunua aina mbili za watu yaani waliowasafi(wayahudi), na walionajisi kwa wakati ule (mataifa) lakini Bwana alipokuja aliwatakasa wanadamu wote,(soma Matendo 10:9) kama aliwatakasa wanadamu je! si zaidi viumbe vyake vyote?..n.k.
2) Mkristo wa kweli haruhusiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara wala kuuharibu mwili wake kwa namna yoyote ikiwemo kuchora alama kwenye miili(Tatoo),uzinzi, mustarbation n.k. kwasababu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo hekalu la Mungu lazima liwe ni safi.
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
3) Kuhusu ubatizo, ubatizo sahihi kulingana na maandiko ni wa kuzamishwa katika maji mengi, na inapaswa iwe ni katika JINA LA YESU KRISTO, kulingana na maandiko na sio kwa jina la BABA na Mwana na Roho Mtakatifu, kama inafanyika kimakosa na makanisa mengi, kwa ufafanuzi mrefu kuhusu UBATIZO SAHIHI fuata link hii >> https://wingulamashahidi.org/2018/07/19/ubatizo-sahihi/
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
BWANA YESU ANAMAANISHA NINI KUSEMA MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?
UMEITIKIA WITO INAVYOPASWA?
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
SWALI: Je! Ni sahihi kwenda kumfuata kiongozi wa dini kwa mfano Padre na kumpigia magoti kumweleza dhambi zako?.kwasababu imeandikwa “Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa;(Yohana 20:23)”
JIBU: Kwa kuongezea hapo Bwana Yesu pia alisema..
Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.”
Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI, NA LOLOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI.”
Hapo tunaona Petro alipewa funguo za ufalme wa mbinguni za kufunga na kufungua,(ambazo ni sawasawa tu na kumwondolea na kumfungia mtu dhambi) na vivyo hivyo na mitume wengine wote waliosalia walipewa funguo hizo hizo, lakini haikuwa na maana kuwa “wanao uwezo wa kumwondolea mtu dhambi kwa kumtamkia tu basi” hapana! bali walipewa “FUNGUO” za kumfanya mtu kuondolewa dhambi zake(UELEWA),, na ndio maana Petro na mitume wengine walipowahubiria watu na kuamini moja kwa moja waliwaambia WATUBU na WAKABATIZWE KILA MMOJA WAO KWA JINA LA YESU KRISTO ili dhambi zao ziondolewe (Matendo 2:38) lakini hawakuwaambia..”Njooni sisi tumepewa uwezo wa kuwaondolea dhambi zenu hivyo pokeeni msamaha”….
Unaona hapo huo ufunguo ni UFUNUO/UELEWA wa jinsi ya kufanya dhambi za mtu ziondolewe, Na ndio huo wa kumuhubiria mtu atubu, kisha akishatubu akabatizwe, hapo ndipo dhambi zake zitakuwa zimeondolewa.
Lakini Papa na Mapadre, na baadhi ya viongozi wengine wa kidini hawafanyi kama mitume walivyofanya bali wao wanawatamkia tu watu kwamba wamesamehewa dhambi zao basi, bila kufuata mwongozo sahihi kwa kisingizio cha hayo maandiko ya kwamba wao wamepewa hayo mamlaka….(kutokana na kukosa UFUNUO wa Roho Mtakatifu ndani yao wanayatafsiri maandiko kwa akili zao ili kutimiza matakwa yao wenyewe.) Mungu atusaidie. Kwahiyo kiongozi yeyote wa kidini akikwambia umesamehewa dhambi zako, pasipo toba binafsi na ubatizo sahihi matamshi yake ni batili yakatae.
JE KUNA ANDIKO LINALOMRUHUSU MWANAMKE KUWA SISTER?
KATIKA MARKO 2:2-12, KWANINI BWANA YESU ALICHUKUA HATUA YA KUSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE KIWETE?
KWANINI MTUME PAULO HAKUMSAMEHE MARKO, PINDI WALIPOTAKA KWENDA WOTE KAZINI?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Biblia inaposema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika? ” Swali ni Je! sisi tutawahukumu vipi Malaika?.
1Wakorintho 6:2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
JIBU: Watakatifu wamefananishwa na BWANA wetu YESU KRISTO kwa sababu yeye aliitwaa asili ya mwanadamu na sio asili ya malaika wala kiumbe kingine chochote, maandiko yanamtaja yeye kama mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi (ambao ndio sisi),
Waebrania 2:16 ” Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake”.
Waebrania 2:16 ” Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake”.
Unaona hapo na kama vile Mungu alivyompa vitu vyote vya mbinguni, na vya duniani na vya kuzimu vivyo hivyo alimpa pamoja na hukumu yote (Yohana 5:22), na pia tukisoma:
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Kwahiyo kama Mungu amempa vyote ikiwemo na hukumu ya viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani, visafi na vichafu, vilivyopo na vitakavyokuja, hivyo ni dhahiri kuwa malaika wote watakatifu na walioasi wapo chini yake na watahukumiwa na yeye kulingana na njia zao, aidha ni nzuri au mbaya, kwa mfano ule ule atakavyowahukumu wanadamu wote watakatifu na waovu.Hivyo basi kama watakatifu watakuja kuketi pamoja na KRISTO (Ufunuo 3:21) ni wazi kuwa watahukumu pamoja na Kristo, maana wakati huo watasimama kama ndugu zake. Na ndio maana Mtume Paulo anaoujasiri wa kusema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika
Kwahiyo ndio ni kweli malaika wote watahukumiwa na watakatifu, wale malaika watakatifu watazidi kutukuzwa zaidi pamoja na Kristo katika umilele ujao, na wale waovu (shetani na malaika zake) watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto pamoja na wanadamu walioasi. kumbuka hizi hukumu zitafanywa na YESU pamoja na watakatifu wake tu!. Na ndio maana maandiko yanasema tutauhukumu ulimwengu na malaika wote.
Ufunuo 20:4 inasema…
” KISHA NIKAONA VITI VYA ENZI, WAKAKETI JUU YAKE, NAO WAKAPEWA HUKUMU; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”
Kwahiyo wale tu watakaoshinda na KUKETI PAMOJA NAYE KATIKA KITI CHAKE CHA ENZI hao ndio watakaohukumu ULIMWENGU na MALAIKA. Amina. Kumbuka watakaokuwa na mamlaka hayo ni wale watakaoshinda tu (watakaonyakuliwa).. Na mamlaka hayo tutayapata baada ya kumaliza maisha haya, lakini kwa sasa tumewekwa chini ya malaika, kama Bwana Yesu alivyowekwa chini yao kipindi yupo duniani (Waebrania 2:9 ) mpaka alipomaliza kazi na kutukuzwa..Kwahiyo tujitahidi tushinde maana biblia inasema..
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ” hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika ?
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ”
hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika ?
HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.
JE! KUNA MALAIKA WA AINA NGAPI?
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
JIBU: Hakuna ngozi yoyote iliyolaaniwa, watu wote kwa Mungu ni sawa, Mungu hana upendeleo kwa jamii fulani ya watu, Pia ni muhimu kufahamu utendaji kazi wa Mungu katikati ya wanadamu tangu kuumbwa kwao, Mungu alimchagua Ibrahimu na kumbariki yeye na uzao wake, kuanzia hapo Bwana Mungu aliliteua taifa moja pekee ambalo atashughulika nalo katika mpango wake wa wokovu kwa wanadamu (yaani taifa la Israeli), hilo pekee ndilo liliokuwa taifa la Mungu katikati ya mataifa yote ulimwenguni katika agano la kale.
Hivyo Wayahudi(au Waisraeli) kwa asili hawakuwa wazungu au watu wazuri nikiwa na maana kuwa “weupe sana” kuliko watu wa mataifa mengine duniani, walikuwa ni watu wa kawaida sana, na hata ngozi zao hazikuwa nyeupe kama za watu wa mataifa mengine mfano wa Ugiriki, Rumi, ambayo yalikuwa kando kando ya Israeli n.k ni jamii iliyokuwa inakaribia kufanana na Waarabu, na kama unavyojua Waarabu sio weupe kama wazungu au Wachina, hivyo Hao (waisraeli) ndio Mungu aliowateua sio kwa mwonekano wao bali kwa kusudi lake Mungu, ili baadaye aje kutimiza mpango wake wa wokovu alioukusudia kuja kuuleta kwa kupitia Bwana wetu Yesu Kristo kwa watu wa ulimwengu mzima na ndio maana utaona kuanzia mwanzo wa biblia hata mwisho huwezi kuona ngozi nyeusi au nyeupe ikitajwa, na sio tu ngozi nyeusi hutaweza pia kuona mzungu, au mchina yoyote, au mhindi yoyote akitajwa kama nabii halisi wa Bwana, kwasababu kwa wakati huo Mungu alikuwa anatenda kazi na wayahudi (waisraeli) tu. na sio na watu wa ulimwengu mzima,
Lakini ulipofika wakati wa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo kudhihirishwa ulimwenguni kote, watu wote mbele za Mungu tumekuwa sawa hakuna tena cha myahudi, au mtu wa mataifa au mweusi, au mwarabu, au mchina n.k Bwana Yesu Mungu wetu alikiondoa kile kiambaza cha kati kilichotutenga sisi na jamii ya waisraeli, na kutufanya mbele za Mungu kuwa wamoja, na ndio maana leo utaona kuna manabii, waalimu, wakizungu, wa ki-wakiafrika, wa-kichina, wa-kihindi, jambo ambalo hapo kwanza halikuwepo. Ilikuwa ni kwa wayahudi tu, na sio kwasababu eti wao ni weupe, hapana wakati huo wazungu walikuwepo wengi sana, wachina walikuwepo nao pia lakini hawakuruhusiwa hata mmoja kumkaribia Mungu wa Israeli katika shughuli zozote zinazohusiana na ibada..
Waefeso 2:11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; 12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. 13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. 15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. 16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”.
Waefeso 2:11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.
14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.
15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.
16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”.
Na Pia papa hatuwezi kumweka katika kundi la Mitume au Manabii, kwasababu mfumo wa anachokiamini ni kinyume na mfumo wa maandiko unavyoagiza..
JIRANI YAKO NI NANI?
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!