Hakukuwa na mtu mmoja maalumu aliyefika mwezini, kulingana na Sayansi…Waliofika mwezini ilikuwa ni TEAM ya watu watatu (Neil A. Armstrong, Michael Collins na Edwin E. Aldrin Jr.) Hao ndio waliokuwa ndani ya chombo cha Kwanza kulichotua mwezini, na wote watatu walikuwa ni wa-Marekani na safari yao iliyojulikana kama Apollo 11. Safari yao ilichukua siku 8 na masaa 3..Kwenda na kurudi, Na hiyo ilikuwa ni Mwaka 1969.
Sasa kumbuka tukio lolote linaloendelea duniani, linafunua tukio fulani linaloendelea katika roho.
Kama wanadamu wamefikia hatua ya kutengeneza chombo ambacho kimewafanya wafike juu zaidi ya mawingu, na kutua Mwezini. Kadhalika kuna kitu pia kinaendelea kutengenezeka sasa katika roho, ambapo itafikia kipindi kitakamilika, na hicho kitalifanya kanisa kupaa juu sana zaidi ya mawingu na zaidi ya mwezi na kulifanya lifike mahali panapoitwa Mbinguni.
Na kama tunavyoona hiyo safari ya kwenda mwezini ilihusisha watu wachache sana, kadhalika, safari ya kwenda mbinguni itahusisha watu wachache sana, kwasababu biblia inasema mlango ni mwembamba na njia imesonga ielekeayo uzimani..
Hivyo ndugu, huu ni wakati wa kuingia ndani ya Kristo, kwani injili sasa inahubiriwa na teknolojia tunazoziona, Hizi ni zile siku za mwisho ambazo biblia imesema maarifa yataongezeka…Na tunaona jinsi yanavyoongezeka kwa Kasi, na katika roho pia yanaongezeka, watu wa Mungu hivi karibuni watafikia Imani ya kunyakuliwa na hivyo kuondoka kwenda mbinguni kwa Bwana..Je! na wewe utakuwa miongoni mwao?
Jibu unalo, tubu mpe Kristo maisha yako na uishi maisha yanayopatana na Toba yako.
Bwana akuabariki.
Mada Nyinginezo:
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA
NYOTA ZIPOTEAZO.
KUONGEZEKA KWA MAARIFA.
ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Upendo ni kitendo cha kuonyesha hisia za tofauti za ndani kwa mtu mwingine, Ni hisia zinazoonyesha pengine umeridhishwa na mtu huyo, au umemkubali, au umemuhurumia, au unataka kumkaribia uwe karibu naye n.k.
Kibiblia kuna upendo wa aina tatu:
UPENDO WA KWANZA NI UPENDO UNAOTOKANA NA HISIA:
Upendo huu unajulikana kama “EROS” Ni upendo unaozaliwa na hisia, Upendo huu ni maarufu sana kwa mke na mume, katika biblia Sulemani alijaribu kuuleza upendo ya namna hii:
Wimbo 1:13 “Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu. 14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi. 15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua. 16 Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani; 17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi”.
Wimbo 1:13 “Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu.
14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.
15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.
16 Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;
17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi”.
Huu ni Upendo ambao hauwezi kufananishwa na upendo kama wa mtu na ndugu yake au Rafiki yake.
AINA YA PILI YA UPENDO NI UPENDO UNAOZALIWA KWA VITU VINAVYOENDANA:
Unajulikana kama “PHILEO”. Upendo huu unazuka kutokana na mahusiano Fulani mtu mmoja alionao na mwenzake, anaweza akawa ni ndugu, au rafiki, au mchezaji mwenzake, au mfanyakazi mwenzake. Ni upendo ambao kusipokuwa na mahusiano Fulani ya karibu au faida Fulani ambayo mtu anaweza kuipata kwa mwenzake, hauwezi kuzaliwa.
Tunapaswa tupendane sisi kwa sisi, biblia inatuambia hivyo katika (1Yohana 2:9-10), vilevile inatuambia tupendane sisi tulio ndugu katika Bwana, lakini upendo wa namna hii haupo tu kwa waaminio bali hata kwa watu waovu pia wanao..Bwana Yesu alisema:
Mathayo 5:46 “Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo”?
Mathayo 5:46 “Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo”?
Unaona kwahiyo upendo huu bado hujafikia vile viwango vyenyewe.
AINA YA TATU YA UPENDO NI UPENDO USIO NA MASHARTI. UNAOJULIKANA KAMA “AGAPE” (UPENDO WA KI-MUNGU).
Huu ndio upendo Yesu Kristo aliokuwa anauzungumzia, ni upendo unaompenda mtu bila ya sababu yoyote, Ni upendo wa kiwango cha juu sana, unampenda mtu kwa kutokujali kama na yeye anakupenda au hakupendi, kama anakuchukia au hakuchukii, kama anakusema vibaya au hakusemi vibaya, kama anafaida yoyote kwako au hana faida yoyote kwako.
Upendo huu ndio YESU alikuwa nao kwetu, biblia pale inaposema “alitupenda Upeo”(Yohana 13:1), ilimaanisha kusema hivyo Alitupenda upeo kweli kweli, sio kwasababu tulikuwa ni watakatifu, au kwasababu tulikuwa waovu…au kwasababu alikuwa anatafuta ukubwa kwetu hapana, alitupenda tu, tena ile wa kutoka moyoni hadi kufikia hatua ya kuutoa uhai wake kwa ajili yetu.
Na upendo wa aina hii ndio Bwana anataka kila mmoja wetu awe nao, Ni ngumu kuufikia, hususani pale tunapoona mtu Fulani anayetuchukia au anatuzungumzia vibaya halafu huyo huyo ndio tunapaswa tumpende, kuna kama ugumu fulani..Lakini Huo ndio Mungu anataka kuuona kwetu haijalishi tutawapenda wake zetu na waume zetu kiasi gani, au ndugu zetu wengi kiasi gani au rafiki zetu wengi kiasi gani kama hatujaweza bado kuufikia huu upendo wa AGAPE, mbele za Mungu bado hatuna upendo..
Hizi ndizo tabia za upendo wa AGAPE.
1Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
1Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
Hivyo ili mimi na wewe tuweze kuufikia Upendo wa namna hii hatupaswi kuungojea kama hizo aina mbili juu, bali tunapaswa tuupapalilie kwa kuvumilia, kwa kutokurudisha baya kwa baya, kwa kutokusengenya, kwa kutokuhesabu mabaya ya mtu tu sikuzote, kuwaelewa watu ..n.k.
Tuombe Mungu atusaidie sote tufike hapo, kwasababu hapo ndipo Mungu mwenyewe alipo, na hiyo ndio inayojulikana kama karama iliyo kuu kuliko zote. Ukiwa nayo hiyo wewe ni zaidi ya nabii yoyote, au mwalimu yoyote, au mwinjilisti yoyote, au mtume yoyote duniani. Mungu anakuwa karibu sana na wewe.
Ubarikiwe sana.
Jiunge na Group letu ya whatsapp, la masomo ya kila siku kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
JIRANI YAKO NI NANI?
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
MPENDEZE MUNGU ZAIDI.
JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?
HERI, WALE MUNGU ASIOWAHESABIA MAKOSA YAO.
Shalom, mtu wa Mungu karibu tujifunze Biblia pamoja..
Wapo wanaodhani kuwa hakuna kuokoka duniani! lakini nataka nikuambie wokovu ni hapa hapa duniani..Mbinguni ni matokeo ya wokovu wetu.
Biblia inasema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu, Na kama ilivyokuwa katika siku za Lutu ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu..Hivyo tukijifunza ni vitu gani vilikuwa vinaendelea muda mchache kabla ya Matukio hayo mawili ya kuangamizwa dunia, tunaweza kuelewa ni mambo gani yatatokea katika siku za kuja kwa Kristo mara ya pili.
Tukio la kipekee tunaloweza kuliona kabla ya Moto kushuka sodoma na gomora ni namna watu walivyookoka…Yapo matukio mengi lakini leo tutalizungumzia hili moja.
Biblia inasema.
Mwanzo 19: 12 “Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; 13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu. 14 Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. LAKINI AKAWA KAMA ACHEZAYE MACHONI PA WAKWEZE. 15 Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu”.
Mwanzo 19: 12 “Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;
13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu.
14 Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. LAKINI AKAWA KAMA ACHEZAYE MACHONI PA WAKWEZE.
15 Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu”.
Tunasoma hapo, kabla ya gharika, kuna injili ya haraka haraka ilipita…Lutu aliambiwa akawaambie ndugu zake watoke mjini kwasababu mji unakwenda kuangamizwa, na laiti kama hao ndugu zake wangesikia, kila mmoja angeogopa na kwenda mbio kuwaambia ndugu zao wengine wa mahali pengine…na hao ndugu wengine wangewaambia wengine…Hivyo kwa kipindi kifupi watu wengi sana wangeokoka…laiti watu wangekuwa na masikio ya kusikia maonyo na kuwa hofu ya Mungu, hata baada ya hukumu ile kutamkwa bado kungekuwepo na nafasi ya KUOKOKA!..Lakini hata huo mlango mdogo wa Neema watu waliupuuzia na hivyo kusababisha kuangamizwa wote.
Na kama pia ukichunguza wakati wa Gharika, Nuhu hakuokoka peke yake, bali aliambiwa akawakusanye watu wa jamaa yake yote…Ni wazi kuwa naye pia alikwenda kuwaambia mambo yale yale…lakini inawezekana naye pia alionekana kama anacheza! Ndio maana akaishia kuingia safinani yeye na wanawe tu, kama Lutu alivyookoka yeye na wanawe!
Mwanzo 7:1 “Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki”. Mwanzo 7: 5 “Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru. 6 Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi. 7 Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika”
Mwanzo 7:1 “Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki”.
Mwanzo 7: 5 “Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru.
6 Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.
7 Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika”
Ndugu nafasi hii ndogo Mungu anayoitoa baada ya hukumu kutamkwa sio ya kwenda kutenda mema, hapana! ni nafasi ya kuokoka!! Hukumu imeshatamkwa..haiwezi kugeuzwa ni lazima ije tu kama ilivyotamkwa! Ni nafasi ya kuukimbia ulimwengu na kuingia safinani, hivyo hivyo kama ulivyo….Ni wakati wa kuikimbia sodoma na gomora ukiwa hivyo hivyo ulivyo…Usiende kumuaga mtu! Wala usiende kumwuliza baba yako au mama yako je! Natakiwa kuokoka? Ondoka sodoma kama ulivyo! Wewe kama wewe…wokovu unaanzia hapo hapo sodoma ulipo! kwasababu hukumu imeshatamkwa…Watoto wa Nuhu haikuhitaji utakatifu mwingi kupata nafasi ya kuingia safinani?..hawakuwa wakamilifu na ndio maana unaona baada ya kutoka safinani, Hamu aliuona uchi wa Baba yake…Lakini walitii injili ndio maana wakaokoka! tu Injili ya Nuhu ya mwisho ya kuokoka! Basi! Kulikuwa hakuna muda tena wa Mungu kusikiliza maombi ya watu…kulikuwa na mambo mawili tu! Aidha kuingia safinani uokoke au kubaki duniani uangamie.
Ukishaingia safinani tayari umeokoka! Hata kama mafuriko hayajaja!
Na siku za mwisho karibia na kuja kwa Yesu ndio injili ndio hiyo inahubiriwa na Roho Mtakatifu, hatuwezi kukaa na kumwomba Mungu kwamba asiiangamize dunia! Alishasema siku ya maangamizi itakuja ni kweli itakuja! Hakuna atakayeweza kubadilisha hilo… Na hivyo zipo chaguzi mbili tu mbele yetu! Kubaki ulimwenguni kuangamia au kuingia safinani kupona! Safina ni Bwana Yesu.
Kama unataka kuokoka na maangamizi..unamfuata Bwana Yesu ukiwa mwenye dhambi kama ulivyo wokovu ni hapa hapa duniani…haihitaji utakatifu kumwamini Yesu…Kwasababu kilichopo mbele ni kifo..Ukimwamini Yesu na kutubu moja kwa moja unapata nafasi ya kuingia safinani..na utakuwa umeokoka na maangamizi, kwasababu huwezi kuokoka mahali ambapo hakuna maangamizi!..Kisha baada ya hapo wewe mwenyewe atakuongoza katika utakatifu na ukamilifu wote,..wewe unachopaswa kufanya ni kuanzia huo wakati kutokuangalia nyuma tu,
Je! Upo safinani?…Umeitii Injili ya Roho Mtakatifu inayotuonya tujiepushe na ulimwengu?
Bwana akubariki
UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!
SAA YA KIAMA.
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
Ukiwasimamisha watu wawili mbele yako, mmoja daktari na mwingine mtu wa kawaida ambaye hajasoma, halafu ukawaonyesha wote wawili ndege ya kivita inayopaa hewani, kisha ukawauliza swali moja jepesi “ Je! Ile mnayoiona juu ni kazi ya nani”….moja kwa moja Yule mtu ambaye hajasoma atakuambia bila shaka ile ni kazi ya mtu,.. lakini Yule daktari si rahisi kwake kutoa jibu la kiwepesi wepesi hivyo, kulingana na kiwango chake cha elimu kumuhusu mwanadamu, atakuambia “mimi ninaona kazi ya ubongo wa mwanadamu”
Sasa ikiwa wewe ndio umeweka utoe alama hapo, ni nani kapata na nani kakosa, utatoa jibu gani?..Ni wazi kuwa Utagundua kuwa wote wawili wapo sahihi, isipokuwa tu Yule daktari kwa kuwa ameshamsoma sana mwanadamu katika fani yake ya utabibu aliyoipitia na kujua kuwa kilichondani ya mwanadamu ndicho kilichofanya kazi ile, hakuishia tu juu juu kumtaja mtu, bali aliingia ndani zaidi mahali huo uutu wake unaomfanya kuwa mtu unapotokea na hapo si pengine zaidi ya kwenye ubongo..hapo ndipo panapomtofauti kuwa huyu ni nyani na huyu ni mtu.
Vivyo hivyo, kwa mtu wa kawaida tu akiulizwa hii unayoiona duniani ni kazi ya nani, asilimia 99 watakuambia tunaona kazi ya Mungu, lakini ni wachache sana watakuambia tunaona kazi ya Neno la Mungu, ambapo huo ndio ubongo wa Mungu wenyewe. Kwa hilo ulimwengu mzima uliumbwa kwalo.
Webrania 11:3 “Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo Dhahiri”.
Lakini watu wengi wanachanganyikiwa wakidhani kuwa Neno la Mungu ni tofauti na Mungu..Kwamba ile ni nafsi nyingine ya tatu ya Mungu..Embu turudi pale kwenye ule mstari wa
Yohana 1:1 inaposema:
“1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika”.
“1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika”.
Sasa embu tumfananishe Yohana na Yule daktari mwenye elimu, ni wazi kuwa angesema maneno yake hivi “tangu zamani ubongo ulikuwepo, na huo ubongo ulikuwepo ndani ya mtu, na huo ubongo ndio mtu mwenyewe, vyote vimefanyika kwa huo, wala pasipo huo hakuna ndege yoyote ya kivita ingeweza kuumbwa au kitu chochote kile”..
Umeona hapo, Ndivyo ilivyo kwa hata katika habari za Neno la Mungu ndio Ubongo wa Mungu, huwezi kulitenga Neno lake na yeye, kwasababu yeye ndio Neno lenyewe..
Tunajua kabisa taarifa zote zimuhusuzo mwanadamu, na ufahamu wake wote upo kwenye ubongo kibaolojia, kwamba ukitaka kujua siri zake basi cheza na ubongo wake, ukitaka kujua uwezo wake wa kufikiri au kufanya mambo, au kuamua, basi cheza na ubongo wake, lakini kama ukijifanya unaweza kumfahamu Mtu kwa kumwangalia tu sura yake au urefu wake, au uzuri wake, au kazi zake, utapotea na usiambulie chochote ..
Vivyo hivyo na leo hii, ili umwelewe Mungu, huna budi kuusoma ubongo wake, na ubongo wake ni Neno lake, hutakaa umjue Mungu kwa vitu alivyoviumba, hutakaa umjue Mungu kwa maajabu anayoyafanya, utamjua Mungu kwa Neno lake tu..basi..
Kama ni hivyo basi? Je hili Neno lake likoje likoje na tutalipata wapi?.
Mungu alijua shida itakuja hapo kwa wanadamu, hivyo akatugawia ofa kubwa sana, ambayo hakuna mtu angeweza kufiki kama Mungu angekaa afanye kitu kama hicho, na ofa hiyo si nyingine zaidi ya kuliundia Neno lake mwili kama ule ule wa binadamu, na kulifanya liishi na wanadamu, liongee, lizungumze nao, liulizwe maswali, litufundishe sisi namna ya kumjua Mungu, na kumfikia yeye..na huo mwili ndio ule ulioitwa YESU KRISTO, mwana wa Mungu aliye hai, Haleluya!! (1Timotheo 3:16)
1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);”
1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);”
Sasa unaweza kuona kazi imerahisishwa, tunaweza kujua siri zote na ufahamu wote wa Mungu kama tutaweza kumfahamu vizuri YESU KRISTO na kuyafuata maagizo yake yote aliyotuagiza. Yeye ndio huo Ubongo wa Mungu unaozungumza na sisi kila siku..Tukiyashika maneno yake basi hakuna kitu chochote kitakachoshindikana kwetu.
Hivyo, ikiwa unahitaji kumjua Mungu au kumkaribia na kuzungumza naye, au kuzijua siri zake zote, hatua ya awali kabisa ya kuanzana nayo ni kumwamini YESU KRISTO, na kumpa maisha yako ayaongoze..Na hiyo inakuja kwa kutubu kwanza dhambi zako zote mbele zake kwa kumaanisha kabisa kuziacha, na kutokuzifanya tena, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38 kama hukuwahi kubatizwa, nawe utakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu. Na kuanzia huo wakati na kuendelea ataanza kukupa uelewa wa kumjua Mungu, kwa namna ambayo hukuwahi kuijua.
Lakini ukitafuta kumjua Mungu kwa nje nyingine mbali na YESU KRISTO,..Hesabu kuwa umepotea. Kwasababu maandiko yanasema katika
Yohana 14:6 “ Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”
Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” ujumbe huu Na kwa wengine.
Na Bwana atakubariki.
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
SADAKA ILIYOKUBALIKA.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
Freemason ni nini? nini historia ya freemason?, nani mwanzilishi wa freemason na Je! Freemasons ni wa kuogopwa? Masharti ya freemason ni yapi?
Shalom! Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tuongeze maarifa ya Neno la Mungu.
Leo tutajifunza juu ya kikundi kinachoitwa “Freemasons” na jinsi gani ya kutoka au kuwasaidia ambao tayari wameshaingia humo.
Kwa kuanzia tujifunze kidogo historia ya kikundi hicho: Freemasons tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni “wajenzi huru” ingawa hawatambuliki kwa jina hilo, lakini kwa asili ni kikundi cha wajenzi. Kikundi hichi kilianzishwa miaka mingi kinadai tangu wakati wa ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani, japo umaarufu wake umekuja kuwa mwingi katika karne za hivi karibuni.
Kikundi hichi kinaamini “kulikuwa kuna siri zimefichika ambazo ndizo zilitumika katika ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani”…Na kama vile wakristo wanavyoamini kuwa Yesu Kristo ndiye Masihi na kiini cha siri zote za Mungu. Vivyo hivyo Na Freemasons wenyewe wanamwamini mtu mmoja anayeitwa HURAMU, Kama Masihi wao, huyu anapatikana katika kitabu cha 1Wafalme 7, ambaye ndiye aliyekuwa mtu wa mji wa Tiro ambao kwa sasa ni maeneo ya nchi ya Lebanoni. Huyu ndio kama Masihi wao, Na Mwanzilishi wa freemasons kulingana na wao.
JE FREEMASONS NI KIKUNDI CHA SIRI?
Sasa kikundi hichi ni cha Siri, tukisema ni cha siri haimaanishi watu wake hawaonekani, au majengo yao hayajulikani..Hapana! Vikundi vya Freemasons vyote vimesajiliwa na serikali zote duniani, na vinalipa kodi, kwahiyo ni watu waliowazi..Kitu pekee ambacho ni siri ni “IBADA ZAO”. Na sheria za dunia zinawalinda kufanya ibada zao kwa siri. Kama vile sheria zinavyolilinda shirika la COCACOLA kuficha formula ya utengenezaji wa vinywaji vyao.Ni watu wachache sana wanafahamu, Na hiyo yote ni kuzuia unakiliji wa bidhaa zao.(www.wingulamashahidi.org)
Freemasons ina wanachama zaidi ya milioni 6 duniani kote, miongoni mwao wakiwa, maraisi, wanasiasa, wana uchumi, wanasayansi, madaktari, waalimu, viongozi wa dini, wakulima, n.k…Idadi kubwa ya wanachama hao ipo nchini Uingereza na Wales.
Mshirika kabla ya kujiunga ni lazima awe ana imani ya kuwa kuna “nguvu ya Kiungu”….Hiyo ikifunua kwamba tayari hicho ni “kikundi cha rohoni” kama huamini huwezi kuwa mshirika …Wanaojiunga huko ni watu kutoka dini zote duniani, waislamu, wahindu, wakristo-jina, wabudha n.k..Baada ya mshirika mpya kujiunga anatakiwa kukusanyika na wenzake mara kwa mara katika majengo yao maalumu ya ibada yanayoitwa “Grand Lodges”..Na wanawake hawaruhusiwi kujiunga katika kikundi hicho.
Ndani ya Ibada hizo kwenye majengo yao wanatumia ishara ya vitu vingi, katika vidole, mikono, miguu, na pia wana ishara za picha na vito kama pete, mikufu, stika, ribbons, na ishara za vifaa vya ujenzi kama bikari, rula, pembe tatu.n.k na Kila ishara ina maana yake. Kama vile sisi wakristo tunavyokuwa na ishara ya misalaba kanisani mwetu, Inafunua kitu kilichotendeka Kalvari.
Sasa Ibada hizo zinabadilika kulingana na vyeo, wenye vyeo vya chini hawafanyi ibada zinazofanana na wenye vyeo vya juu, na pia wenye vyeo vya chini hawafahamu siri nyingi kama wanazofahamu wenye vyeo vya juu. Hapa ndipo watu wengi wasipojua!…tutakuja kupaelewa vizuri mbele kidogo mwa somo hili…
Sasa vyeo hivyo vimegawanyika katika ngazi kuu 33 wanazoziita “shahada” au “degrees”
Mshirika mpya anayejiunga, kuna viapo anaambiwa aape, moja ya viapo hivyo ni kukiri kuwa mwaminifu, na kutokufichua siri yoyote ya chama hicho, na pia ataambiwa akiri kwamba endapo atafichua basi atakufa, na pia anaambiwa aape kwamba atakuwa mwaminifu, na pia atakuwa tayari kushirikiana na wenzake, na kusaidiana na wenzake kwa hali na mali…(www.wingulamashahidi.org)
Na katika hatua za awali, ataambiwa tu hicho ni kikundi cha kijamii!, kinachoamini katika ujenzi, na cha kusaidiana, na wala hataambiwa siri nyingi za kikundi hicho,..Na wala hawatamkataza kurudi kusali katika kanisa lake kama ni mkristo. Ila kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda na anayozidi kupanda vyeo, ndipo ataanza kugundua kuwa sio sehemu ambayo aliambiwa pindi alipokuwa anajiunga.
Wengi waliojiunga na kutoka wanasimulia…”kuwa pindi walipojiunga, hawakujua chochote na pia walikuwa wanauhuru wa kuendelea kurudi kwenye makanisa yao kuabudu” na tena walikuwa wanapingana vikali na wale waliokuwa wanakishutumu chama hicho kuwa ni chama cha kishetani” na kinachoamini mauaji.
Wengine wanasema “Nilikuwa mshirika wa chama hicho kwa miaka mingi lakini sikuwahi kujua kuwa ni chama kinachomuabudu shetani” kwasababu wote tuliokuwa ndani ya chama hicho wenye degree ndogo, tulikuwa na upendo, na tulikuwa tunasaidiana, na kupeana fursa..Mpaka nilipofika ngazi za juu ndipo nilipoelewa kuwa sio sehemu salama”..mmoja aliyekuwa na degree ya 2 aliyetolewa huko na Bwana Yesu alihojiwa… je! ulishawahi kumuona shetani ndani ya ibada zenu?…akasema la! hata siku moja, wala sijawahi kuona vitu vya kiroho kama mapepo ndani ya logde! nilikuwa naingia na kutoka tu kama ninavyoingia kanisani…Na wala nilikuwa siamini kwamba ni kikundi kibaya kwa miaka kadhaa…na wala sikuwahi kutoa kafara yeyote ya mtu! mpaka baadaye sana nilipokuja kugundua kuwa hayo yanafanyika na wenye shahada za juu na hawatuambii sisi.
Kuanzia shahada ya 30 na kuendelea ndio wanaotokewa na mapepo na kuzungumza na shetani mwenyewe, na hao ndio wanaojua siri nyingi za chama hicho kuwa ni chama cha kumwabudu shetani moja kwa moja! na agenda kubwa ya chama hicho ni “kuikimbiza dunia katika ustaarabu mpya wa ulimwengu” ambao utakuja kuhasisiwa na Mpinga-kristo, chini ya utawala wa kirumi” katika siku za mwisho, lakini wengine wa shahada za chini hawaelewi sana.(www.wingulamashahidi.org)
Freemasons pamoja na vikundi vingine vya kichawi kama Iluminati, Brotherhood, ku-klax-klan,sisterhood, vinafanya kazi zinazofanana..Vyote ni vikundi vya kumwabudu shetani. Kwahiyo sio wote waliojiunga na freemasons wanaoelewa wapo sehemu gani.
Dhana iliyopo sasa hivi, ambayo hiyo inatokana na kukosa maarifa ni kwamba mtu aliyejiunga na freemasons tayari huyo ni pepo! hapana! hiyo si kweli kama tulivyotangulia kusema wapo wengine hawajui chochote wamedanganyika tu wakidhani kuwa ni kikundi cha kijamii cha kusaidiana kama vikundi vingine, hawaelewi vizuri freemason ni nini..Sasa hao wanahitaji msaada! Kumbuka ni watu kama wewe na mimi, wanapumua, wanasikia maumivu, wana hofu kama wewe na mimi, hivyo ni wa kusaidiwa kutoka huko kabla hawajazama kikabisa kabisa humo…sio wa kuwakimbia…Wanahitaji injili ya Yesu Kristo ya msamaha wa dhambi..wengine hawaelewi wamepelekwa tu na marafiki zao, ni kama tu makahaba waliojiingiza kwenye madanguro sio wote wanaelewa madhara ya kuwa kule, wanahitaji wokovu kama wewe ulioupata.
Ukienda pasipo maarifa kwa mtu ambaye ni freemason na kumwambia wewe ni shetani! unaabudu shetani na unatokewa na shetani kila siku na kuzungumza naye na kuua watu na kuwatoa kafara! na unakunywa damu…kwasababu tu umemwona kavaa pete yenye alama zao…
Ni rahisi sana kumkosa kwasababu hivyo unavyovisema unaweza kuta havifanyi katika levo aliyopo huko…kwasababu wote wanaojiunga huko kwa mara ya kwanza ni lazima wadanganywe… Hivyo huyo ni kumweleza kwa maarifa mwanzo wa chama hicho na mwisho wake.. Na kumweleza Injili ya Yesu Kristo ya msalaba…Lakini ukikutana naye na kuanza tu! kukemea hapo hapo! na kumwogopa!…na kumhakikishia kwamba yeye ni mchawi..atakushangaa sana na hatakuelewa, na pengine atakuchukia na itamfanya azidi kuamini kuwa yupo sehemu salama zaidi. Wengi waliojiunga huko ni kwasababu wamekosa maarifa..Hivyo wanatakiwa waokolewa kwa kupewa maarifa ya Neno la Mungu. Hivyo usikose maarifa ya namna ya kuvua roho za watu!.
Biblia inasema katika
Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;..”
Na pia jambo lingine watu wasilolijua ni kwamba Freemasons watu hawajiungi kwa kupitia Facebook, wala hawajiungi kwa kupitia vipeperushi huko barabarani, wala vinakala juu ya nguzo za umeme…Huo wote ni utapeli tu ambao watu wanadanganywa…Ni watu wa kawaida ambao wanatafuta kupata pesa za kitapeli. Na pia freemasons ni kitu kidogo sana kwa mtu aliyeokoka haipaswi kukuzwa kiasi hicho mpaka kutengeneza hofu ya kupita pembezoni mwa barabara yenye jengo la freemasons, wala kumsalimia mtu aliyejiunga huko..Hakuna chochote kitakachokupata ukiwa ndani ya Kristo kwasababu shetani ni yule yule, unayeshindana naye kanisani ndio huyo huyo huko freemason! Sasa unachoogopa ni nini? (www.wingulamashahidi.org)
Na pia usikose maarifa kuwa freemasons ni mahali watu wanakwenda kupewa pesa!! hawaendi kupewa pesa, waliotoka huko na kumpa Bwana Maisha yao, wanasema “watu wote wanaojiunga huko ni wafanya kazi” na kule hawapewi pesa kana kwamba kuna ATM inayomwaga pesa…hapana! isipokuwa waliopo kule wanapeana fursa wao kwa wao, na ndio moja ya viapo vyao… freemasons wenzao waliopo ngazi za juu katika shughuli za ulimwengu kila mmoja ana jukumu la kumwangalia mwenzake aliye chini..
Kama mmoja yupo ngazi ya juu katika serikali anamnyanyua freemasons mwenzake aliye chini, kama mmoja ni mkurugenzi basi ikitokea nafasi ya kazi anamtafuta freemason mwenzake anamchomeka hapo n.k hiyo ndio maana unaona mtu aliyejiunga anaweza kupata maendeleo ya ghafla, na endapo akijitoa wananyanganya ile nafasi, ndio maana unaona mtu anaporomoka ghafla. Lakini sio kwamba wanapewa hela za kimajini ambazo zinatokea tu kichawi! Huko ni kukosa maarifa!
Hivyo kama umejiunga huko! Kumbuka kujiunga kunakozungumziwa sio kwa kupitia facebook! Au mtandaoni….Kuna watu nimekutana nao, wanakuja kuomba msaada, wamedanganywa na matapeli facebook na kuambiwa wasipotuma kiasi fulani watakufa! Na hivyo wanaogopa na kutuma pesa! Hao ni matapeli..kujiunga kunakozungumziwa ni kule kuwasili kwenye hayo maukumbi yao, na kupewa viapo na kukutana na washirika wengine. Kama umejiunga kwa namna hiyo, mlango wa kutoka upo wazi.(www.wingulamashahidi.org)
Huko ulipo upo kwenye elimu ya shetani kamili, na nguvu za giza zimekufunika..Unamwabudu shetani sasa bila kujua, lakini ipo siku utamwabudu waziwazi, hivyo unayo nafasi ya kutoka…haijalishi uliapa kiasi gani! Kuwa utakitumikia chama hicho na endapo ukitaka kutoka utakufa! Nataka nikuambie hutakufa! Zaidi ya yote ukiendelea kukaa huko ndio utakufa.
Hapo ulipo fanya jambo moja la kiimani! Tubu! Na uwaambie mimi sio mmoja wenu tena! Watakutishia lakini hakuna kitakachokupata! Kwasababu aliye upande wako ni mkuu kuliko aliye upande wao. Na usiende tena huko, wala usifanye ibada zao, wala ishara zao, choma vito vyao, uniform zao, pamoja na mihamala yao..futa na namba za washirika wenzako. Tafuta kanisa la kiroho linaloamini injili kamili ya YESU KRISTO, dumu huko, Na ukae katika mafundisho ya Kweli ya Kristo Yesu. Au wasiliana nasi inbox, au kwa namba hizi 0789001312/.
Kumbuka washirika wote wa Freemasons watakwenda kuzimu kwasababu wanamwabudu shetani kama wasipotubu! Hivyo kama hutatubu utakwenda kuzimu….Hivyo kwa hitimisho freemason ni nini?…jibu ni kikundi cha kishetani kinachomwabudu shetani.
Bwana akubariki.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
USIPIGE MATEKE MCHOKOO!
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
VITA DHIDI YA MAADUI.
UNYAKUO.
JEHANAMU NI NINI?
Biblia haijaweka bayana safina ilijengwa kwa muda gani, Wapo wanaosema ilijengwa kwa muda wa miaka 120 kufuatia mstari wa kitabu cha Mwanzo 6:3 ” Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.”
Lakini bado hiyo haileti maana kamili..Lakini pia biblia inasema Nuhu aliwazaa watoto wake akiwa na miaka 500,(Mwanzo 5:32) Na inasema aliingia katika safina akiwa na miaka 600, hivyo kufanya tofauti ya miaka 100 hapo, ambayo ndani ya hiyo pengine ndiyo aliyotumia kuijenga safina, lakini pia hoja hiyo ina mapungufu kidogo.
Kwa ufupi ni kwamba biblia haijaeleza ilijengwa kwa muda gani, hivyo pengine ni jambo ambalo halina umuhimu sana kwetu kulijua.
Jambo la Muhimu kujua ni kwamba, Kama dunia ya kwanza iligharikishwa na maji kwa ajili ya maovu ya watu, basi na dunia hii ya pili tunayoishi mimi na wewe nayo pia itagharikishwa vile vile kutokana na maovu ya wanadamu.. Na Biblia inasema haitagharikishwa kwa maji tena bali kwa moto.
Biblia inasema hivyo katika
2Petro 3:6 ” kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. 7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.”
2Petro 3:6 ” kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.”
Dhambi kama uzinzi, rushwa, chuki, fitina, kutokusamehe, ulevi, ushoga, ulawiti, usagaji, utukanaji, tamaa mbaya, utoaji mimba, wizi na nyingine zote ndio iliyoizamisha dunia ya kwanza kwenye maji. Na ndizo zitakazoizamisha dunia hii tunayoishi sasa katika moto. Kama Mungu alipozungumza alitenda kwa Nuhu, kadhalika alivyozungumza sasa katika Neno lake atatenda.
Je! na wewe bado upo ulimwenguni? bado hujampa Kristo maisha yako, na kuacha dhambi? Unyakuo upo karibu sana kutokea.
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya kila siku, kwa njia ya email, au whatsapp, basi tutumie ujumbe kwenye namba hii : +255789001312
NUHU ALIKUWA NA WATOTO WANGAPI?
NUHU ALIISHI MIAKA MINGAPI?
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
NUHU WA SASA NI YUPI?.
Nuhu aliishi jumla ya miaka 950, hiyo ndio jumla ya miaka yake…Aliishi miaka 600 kabla ya Gharika, na aliishi miaka mingine 350 baada ya gharika.
Mwanzo 9:28 “Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini. 29 Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa”.
Mwanzo 9:28 “Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.
29 Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa”.
Nuhu na wanawe ndio walikuwa watu wamwisho kuishi umri mrefu, kwani baada ya gharika Bwana Mungu alisema miaka ya Mwanadamu itakuwa 120 tu!
Tunajifunza kuwa si lishe bora ndiyo inayompa mtu maisha marefu, wala si kuzingatia mazoezi la hapana! Kinachompa mtu maisha marefu ni KUMCHA BWANA, Laiti kama wanadamu wa wakati ule wasingefanya maovu kiasi kile cha kuleta gharika juu ya nchi…mpaka leo wanadamu tungekuwa tunaishi mamia ya miaka, lakini kutokana na maovu yetu miaka yetu imeshusha namna hii.
Hivyo tukitaka tuishi maisha marefu katika haya maisha tuliyopewa hatuna budi kumcha Mungu, lakini tukivunja amri zake na kuishi maisha ya dhambi ndio tunakivuta kifo chetu karibu nasi.
Bwana atusaidie sana kwa hilo.
NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?
DOWNLOAD PDF
WhatsApp
Biblia inasema Nuhu alikuwa na watoto watatu tu! SHEMU, HAMU na YAFETI, ambao wote walikuwa wakiume.
Mwanzo 5:32 “Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi” Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika”.
Mwanzo 5:32 “Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi”
Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika”.
Na Hao ndio walioingia kwenye safina pamoja na wake zao.
Mwanzo 7:7 “Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika”.
Hivyo ndani ya safina kulikuwa na watu 8 tu!
Inasikitisha kiasi gani? watu 8 tu ndio waliopona kati ya mabilioni waliokuwa wanaishi duniani?..Mlango wa safina ulipofungwa watu walitamani kuingia lakini wakashindwa.
Na sisi je tutapataje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii? (Waebrania 2:3). Na dunia hii ya mwisho biblia inasema watakaopona ni wachache sana, watakaonyakuliwa ni wachache sana..Ni wale tu watakaojitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba
Luka 13.24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu”.
Luka 13.24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu”.
Tujitahidi tuwe mimi na wewe
Maran atha!
Kuzimu ni mahali, ambapo roho za watu waliokufa zinakwenda..Ni sehemu ya rohoni ambayo haionekani kwa macho ya kibinadamu..
JE! WANAOENDA KUZIMU NI WATU GANI?
Wanaoenda kuzimu ni watu ambao wameasi Neema ya Yesu Kristo, wale wote ambao waliikataa Neema ya Msalaba iliyoletwa na Mwana wa Mungu Yesu Kristo, watahesabika kuwa na hatia ya kuingia kuzimu…Kwasababu biblia inasema tunahesabiwa haki kwa Neema, ambayo hiyo inatokana na Imani ya kumwamini Yesu Kristo.
Kwahiyo mtu anapokufa, katika dhambi (Yaani nje ya Neema ya Yesu Kristo) anashuka moja kwa moja kuzimu, ambako huko kuna mateso makali, na roho yake inakuwa imefungwa. Atakaa huko mpaka wakati wa mwisho wa KITI CHEUPE CHA HUKUMU, Ambapo biblia inasema wafu wote watafufuliwa na kisha kuhukumiwa kulingana na matendo yao, hivyo mtu aliyekufa katika dhambi atasimama siku ile mbele ya kiti kile cheupe cha Hukumu na kisha kuhukumiwa sawasawa na matendo yake. Na baada ya kuhukumiwa atahamishwa kutoka kuzimu alipokuwepo na kuhamishiwa katika ZIWA LA MOTO, Ambako kuna matezo mengi zaidi..
Kinyume chake wanaokufa katika haki sasa, wanakwenda mahali panapoitwa Paradiso, mahali pa raha, wakingojea ufufuo wa Unyakuo ambapo watafufuliwa na kuvaa miili ya Utukufu na kisha kwenda Mbinguni kwa Bwana.
Je Umempa Bwana Yesu maisha yako? Upo ndani ya Neema ya Yesu Kristo, au unasubiria ufe na kwenda kuzimu? Kumbuka hakuna nafasi ya Pili ya kutubu baada ya kushuka kuzimu..Kila atakayeingia kuzimu atasubiria adhabu ya ziwa la moto.
Bwana akubariki!
KUMWAMBIA MTU MWENYE DHAMBI KUWA ATAKWENDA KUZIMU ASIPOTUBU JE! NI KUHUKUMU?
NITAAMINI VIPI KAMA KUNA MBINGU AU KUZIMU?
JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.
UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.
Rudi Nyumbani
Jambo ambalo watu wengi hawafahamu ni kuwa ndani ya mtu kuna kitu kinachoitwa DHAMIRI.. Hichi ndicho kinachomshuhudia mtu kuwa alichokifanya ni sahihi au sio sahihi hata kama jambo hilo litaonekana mbele za watu ni jema, ikiwa ni baya, basi ndani ya moyo wake mtu huyo dhamira yake yenyewe tu itamshuhudia kuwa alichofanya sio sahihi, au kama kitendo alichokifanya ni sahihi, basi dhamira yake vilevile itamshuhudia hivyo hata kama ulimwengu mzima utasema alichokifanya ni kibaya.
Sasa mtu anapofanya kosa, labda tuseme labda kamtukana ndugu yake, au katoka nje ya ndoa kisirisiri, au kaiba, au kamsengenya mwenzake, au kamsababishia mwenzake jambo baya pengine kamwambukiza ugonjwa wa ukimwi kwa makusudi, moja kwa moja ndani ya moyo wake mtu huyo, Dhamiri yake inamshuhudia kafanya kitendo baya…
Hivyo siku ile ya mwisho Mungu ataihukumu dhamira yake.
1Timotheo4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, WAKICHOMWA MOTO DHAMIRI ZAO WENYEWE;”
1Timotheo4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, WAKICHOMWA MOTO DHAMIRI ZAO WENYEWE;”
Dhamiri yako inakushuhudia kabisa umefanya makosa.
Wengi wetu tunaogopa tuomba msamaha, bali tunatafuta njia mbadala ya kujisafisha..
Mimi sio mfuatiliaji wa mambo ya siasa lakini linikutana na jambo moja nikajifunza, kama wewe ni mfuatiliaji wa Siasa utakumbuka kuna kipindi baadhi ya wabunge na mawaziri walimzungumzia vibaya Mheshimiwa Raisi, na sauti zao zikarekodiwa na kusikiwa karibu kila mahali nchi nzima..
Lakini baadhi yao, walipoona kuwa walichokifanya sio sahihi, walijisalimisha wenyewe na kwenda kumfuata Raisi ikulu kumwomba msamaha..Na mmojawapo akakiri mwenyewe na kusema tangu ule wakati mambo hayo yalipojulikana hakuwa na Amani kabisa, hata usiku usingizi alikuwa hapati, lakini sasa anasema baada ya kumwona Raisi na kumwomba msamaha, ile amani yake yote imemrudia tena..
Unaona hapo? Kilichokuwa kinamtesa ndani ya nafsi yake ndio hiyo dhamiri ambayo pengine hata wewe inakusumbua leo hii, Dhamiri yake ilikuwa inamshuhudia kuwa alichokifanya kweli sio sahihi, hivyo moja kwa moja hakwenda kutafuta njia mbadala ya kujisafisha, kwa namna yoyote ile, kama angefanya vile basi ile hali ya kuhukumiwa bado ingeendelea kubaki ndani yake, haijalishi watu nchi nzima itamwona ameonewa..Hivyo njia pekee ilikuwa ni kwenda kuomba msamaha.
Vivyo hivyo na wewe pengine umefanya jambo unajua kabisa sio sahihi,..na dhamiri yako inakushuhudia, nataka nikuambie usikawie kuomba msamaha, ikiwa ulimkosea mzazi wako basi mfuate na kumwomba msamaha, ikiwa ulimkosea rafiki,au bosi, au jirani, mke wako, mume wako au Mungu mwenyewe kwa kufanya dhambi za makusudi mbele zake basi usikawie kuomba msamaha,..
Kwasababu faida ya kwanza utakayoipata kwa kuomba msamahani ni kuwa utakuwa HURU na kujihisi AMANI nyingi. Ipo sauti inaweza kukwambia ndani yako Aaah! Yule hatakusamehe, au aah! Yule atakuona wewe ni mnyonge!!..Nataka nikuambie hakuna mtu ambaye akiona mtu amejishusha mbele zake na kumwomba masamaha asimuhurumie Yule mtu, hakuna…Hata kama ni wewe ukiona mtu ambaye siku moja alikusema vibaya akaja kwa upole na kukiri kuwa alikukosea, akaomba msamaha kwa dhati kabisa, ukamchukia mtu huyo haiwezekani..Kwanza ndivyo utakavyompenda zaidi..Sasa na wewe usiogope kwenda kuomba msamaha..fanya haraka kabla hujafa katika hali hiyo.
Pia Mungu anataka kitendo cha kuomba msamaha kiwe sehemu ya maisha yetu mbele zake,..Na ndio maana hata katika ile sala ya Baba yetu..utaona tunasema Utusamehe dhambi zetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, 10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupe leo riziki yetu. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]”
Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]”
Hivyo usiogope kuomba msamaha.
Ubarikiwe.
Mada nyinginezo:
RACA.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
FAIDA ZA MAOMBI.
EPUKA KUTOA UDHURU.