DON’T BE AFRAID WHEN YOU GO DOWN.

Mharabu ni nani katika biblia?

Kuna tofauti kati ya “Mwarabu” na “Mharabu”. Maneno haya mawili yameonekana sehemu kadhaa katika biblia na yana maana mbili tofauti.

Tukianza na “Mwarabu”.

Mwarabu au kwa wingi waarabu; ni jamii ya watu wanaoishi maeneno ya mashariki ya kati. Yaani maeneno ya  Syria,Jordani, Palestina, Saudi Arabia, Yordani, Yemen, Kuwait,  Iran, Iraq, na Uturuki. Wenyeji wa maeneo hayo ndio wanaojulikana kama waaramu.. akiwa mmoja ni mwarabu, wakiwa wengi ni waarabu.

Katika biblia watu hao wametajwa sehemu kadhaa..

Yeremia 3: 2 “Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pa wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, KAMA VILE MWARABU JANGWANI; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako”.

Na pia unaweza kusoma Isaya 13:20, utaona mwarabu akitajwa.

Lakini pia katika biblia kuna neno “MHARABU” , Neno hili au jina hili halihusiani na watu hao wenyeji wa mashariki ya kati, bali linamaanisha “Mharibuji”. Mtu anayetumwa kuharibu kwa kuua ni  Mharabu (Mithali 18:9), lakini pia Malaika wa Mungu anayetumwa kwa lengo la kuitimiza ghadhabu ya Mungu kwa kuua, naye pia anaitwa Mharabu.

Tunaweza kuona mfano mmoja katika biblia..

1Wakorintho 10:10 “Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu”.

Mharabu anayezungumziwa hapo, ni malaika yule aliyetumwa kuwaharibu na kuwaangamiza wana wa Israeli walipokuwa wananun’unikia Mungu jangwani..ambapo Bwana Mungu aliwaonya wana wa Israeli, waende katika njia zake ili wasiangamizwe na malaika huyo..

Kutoka 23: 20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.

21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake”.

Na hata leo, Mharabu wa Mungu yupo, kwaajili ya kutulinda katika safari ya wokovu, lakini tukienda kinyume na mapenzi ya Mungu, yupo mbele yetu kutupinga kama alivyowapinga wana wa Israeli na kuwaua wengi na kama alivyompinga Balaamu katika Hesabu 22.

Bwana atujalie neema yake na kutulinda.

Maran atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

USITAFUTE KUKANWA NA BWANA SIKU ILE.

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

VITA VYA IMANI NI VITA ENDELEVU.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

Rudi nyumbani

Print this post

FAHAMU UWIANO MUNGU ANAOHITAJI KUUONA KWETU.

Ipo kanuni moja ya Mungu, ambayo ni vema sisi sote tukaifahamu. Kanuni hiyo ni kuwa Mungu huwa hafanyi mambo yote peke yake, japo anaouwezo wa kutenda mambo yote yeye mwenyewe, lakini ni kanuni aliyojiwekea kwamba sehemu kubwa aitende yeye mwenyewe, na abakishe sehemu ndogo sana ambayo atashirikiana na viumbe vyake, au mwanadamu kuitenda.

Kwamfano Pale Edeni, Mungu alishaiumba kila kitu, angeweza kumwacha Adamu awe anakula tu, na kuisha maisha yake ya starehe kwa milele yote, lakini utaona alimpa Adamu jukumu dogo sana la kuilima na kuitunza bustani yake, jambo ambalo Mungu angeweza kulifanya yeye mwenyewe, kama aliweza kuimba dunia, angeweza pia kuilima na kuitunza bustani ile peke yake, mwanadamu aishi kwa raha siku zote.

Vivyo hivyo hata katika miili yetu hii aliyotupa, sote tunajua ni mali yake, lakini sio kila kitu anakifanya yeye peke yake, asilimia kuwa ni yeye ndio anayeitunza miili yetu, kwamfano ukitafakari, mapigo ya moyo yeye ndio anayeyashughulikia yaende katika mpangilio alioutaka, wewe hauhusiki na kitu chochote hapo,  kukuza nywele, au kucha, huelewi chochote, au kusukuma damu, jambo hilo halikuhusu hata kidogo, kana kwamba sio sehemu ya mwili wako n.k., Sasa fikiria mambo magumu kama hayo anaweza kuyafanya unadhani anashindwa kabisa kukuogesha kila siku, wewe ukiamka tu asubuhi tayari ni msafi? Au kukulisha chakula, wewe ukiamka tayari tumbo limejaa? Au kukutundikia dripu la maji ndani ya mwili wako kiasi kwamba ukipungukiwa na maji kidogo tu lenyewe tu linashusha, na hivyo hakuna haja ya kwenda kutafuta maji nje?..Kwanini aruhusu mpaka uanze kuteseka uandae chakula ule, na wakati mwingine kwenda kujisumbua kutafuta?

Hiyo yote ni kwasababu, Kanuni ya Mungu, ndivyo ilivyo kwetu sisi wanadamu, yeye mwenyewe kachagua afanye kwa sehemu kubwa, na ile sehemu ndogo sana ashirikiane na sisi kufanya.. Huo ndio uwiano wa Mungu. Na kama mtu akiipuuzia sehemu hiyo ndogo asiifanye, ajue kuwa matatizo makubwa sana atakumbana nayo, kama sio kifo kabisa.

Vivyo hivyo na mambo ya rohoni, tunajua kabisa Mungu ndio kila kitu kwetu, yeye ndio msaada wetu, yeye ndio tegemeo letu, yeye ndio kila kitu kwetu, pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya lolote, yeye ndiye anayejua kesho yetu, anayejua tutalalaje, tutaamkaje, Tunajua kabisa Mungu anatupigania na kutushindania kwa mambo mengi, mengine hata hatujui, lakini  pia katika hayo yote tupaswa kujua pia yapo mambo mengine anataka tushirikiane naye, ili vyote viende sawa sawa. Vinginevyo tukivipuuzia, tukasema tunamwachia Mungu kila kitu, tujue kuwa tutapata matatizo makubwa sana, hata vile vingine ambavyo Mungu anatutendea yeye mwenyewe bila kutushirikisha tunaweza tusivipate.

Ni sawa na kusema, Mungu ananikuza, anadundisha mapigo yangu ya moyo, anachuja damu yangu kwenye figo, pasipo kujishughulisha hivyo ngoja nisiende pia kujipikia chakula nile , kwani nitashiba tu mwenyewe.. Hapo utakufa ndugu yangu, haijalishi kuwa Mungu anakuhudumia kiuaminifu kwa hayo mengine usiyoyasumbukia. Huo utakuwa ni uvivu uliopindukia.

Ndio maana andiko hili linasema..

Mithali 26:15 “Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake”.

Sasa na rohoni nako vivyo hivyo, yapo mambo ambayo itakuhitaji wewe ufanye ili Mungu aende na wewe.. Na jambo mojawapo ni “MAOMBI” ikiwa  wewe sio mwombaji,  na umeokoka halafu unajidanganya kwa kusema Mungu anajua haja ya moyo wangu kabla hata sijaomba sawasawa na Mathayo 6:32, hivyo atanisaidia tu, mimi siombi, au naomba nikijisikia, kwani mimi ni mteule wake, siwezi potea..ukae ujue kuwa, Utapata hasara kubwa sana ya roho yako kipindi sio kirefu.

Bwana Yesu alivyosema, kesheni mwombe, alikuwa anamaanisha tuombe kweli kweli, kama yeye alikuwa ni mkamilifu, hana kosa lolote aliomba, inatupasaje sisi miti mikavu? Wakati mwingine Mungu anasimama kama jemedari wetu vitani, akitarajia tupigane pamoja naye, tushike panga pamoja naye, tukate pamoja naye,  sio tukae tukimtuzama akitupigania kila siku.

Kama utasubiria Mungu akulinde na washirikina, akutete kwenye mambo yako, akunyanyue katika huduma yako, akufanyie hiki, au kile,  na huku huombi, au hujibidiishi kwake, ukajidanganya kuwa umeokoka, hapo hesabu kuwa umepotea.

Vivyo hivyo katika kuifanya kazi ya Mungu, kuna wengine wanasema, Walio wake watakuja tu, wakisimamia andiko hili, 2Timotheo 2:19. Hivyo hawataki kujishughulisha na jambo lolote la ki-Mungu, hata kufagia uwanja wa kanisa. Ni kweli walio wake watakuja kwasababu Mungu anazo njia nyingi sana za kuwakomboa watu, wake. Lakini ipo asilimia ya huduma yake kaiweka ndani yetu sisi. Ambayo tunapaswa tuitimize. Ili tuweke ule uwiano anaouhitaji.

Lakini tusipoitimiza tukakaa tu hivi hivi,tujue kuwa tupo hatarini sana kufa kiroho. Hata kama tutaona leo hii Mungu anatushindania katika mambo yetu mengi, tujue tu kesho yetu itafika ukingoni. Tutarudi nyuma.

Kwahiyo tukae tukijua kuwa, ili ukristo wetu uende sawasawa, tutambue wajibu wetu na majukumu yetu kwa Bwana, kama vile Bwana anavyoyatambua majukumu yake, na wajibu wake kwetu, lakini kama upande wetu utasua sua, tufahamu kuwa, Mungu hataweza kutembea na sisi hata kidogo.

Hivyo Bwana atutie nguvu, tuwe waombaji, na pia tuone ni nini tunaweza kufanya kwenye kazi ya Mungu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

AINA TATU ZA WAKRISTO.

KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.

Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

ANGALIENI MWITO WENU.

TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.

KWANINI KRISTO AFE?

Rudi nyumbani

Print this post

KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.

Shalom karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu.(Zab 119:105)

Leo tuwatazame wanawake hawa wawili ambao tunaona Mtume Paulo,akiwataja kipekee zaidi katika biblia kutokana na bidii yao kwa Bwana. Mmoja aliitwa Euodia na mwingine Sintike. Mtume Paulo anasema wanawake hawa walishindania injili pamoja naye, hii ikiwa na maana bidii yao iliwazidi hata wanawake wengine wote, walikuwa tayari kutumika katika kanisa la Mungu, kama wanawake katika nafasi zao  kwa uaminifu pengine bila kuvutwa na mambo mengi, walikuwa tayari kuwatazama kwa bidii wanawake vijana na wazee, pengine sio tu kwenye kanisa hilo moja la Filipi, bali hata kwenye makanisa mengine  ya Makedonia, pengine walikuwa tayari kujitoa katika kuhimiza michango kwa ajili ya kazi za mitume, na injili kwa ujumla, walikuwa waombaji wazuri na wafungaji n.k.

Hivyo sifa zao zilivuma sana, mpaka tunaona hapa mtume Paulo akiwataja kwenye nyaraka zake. Lakini walikuwa na dosari moja, ambayo leo hii ni vizuri wanawake wote watakatifu wanaomcha Bwana wakaifahamu kwasababu ipo hata sasa katika kanisa.

Wafilipi 4:2 “Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, WAWE NA NIA MOJA KATIKA BWANA. 3 Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami,….”

Kama tunavyoweza kuona hapo pamoja na bidii yao, walikuwa wanatofautiana kwa mambo kadha wa kadha. Pengine, mmoja alimdharau mwingine, hivyo wakawa hawasikilizani, kila mmoja akawa anafanya kazi kivyake, hata mahali ambapo wangepaswa waunganishe nguvu kwa pamoja watumike, ili kumpiga shetani vizuri, walishindwa kutokana na tabia yao ya kudharauliana,  unaona, pengine mmoja alisikia maneno fulani kutoka kwa mwingine akizungumziwa vibaya, na hiyo ikawafanya wasusiane, unaona na mambo mengine kama hayo. Ikawafanya kila mmoja atumike kivyake. Lakini Mtume Paulo alikuja kuwasii kwa waraka wawe na Nia moja.

Wanawake hawa wanawakilisha makundi mbalimbali ya wanawake waliookoka kanisani, Sikuzote ni wanawake ndio wanakuwa wazito katika kushirikiana, utakuta ni kweli anayobidii kwa Mungu, wanamtumikia Mungu kwa moyo wake wote, lakini kuwatambua wanawake wenzake wenye bidii kama ya kwake, na kushirikiana nao, hilo ndio linakuwa tatizo kubwa.

Paulo alimuonya Eudia na Sintike, kwamba katika bidii yao wawe na Nia moja, waukamilishe wito wao. Hata leo hii Kristo anawataka wanawake wote kanisani wawe na Nia moja. Kwani Ibilisi anajua nguvu iliyopo ndani ya wanawake pale wanaposhirikiana kwa pamoja ajili ya kazi ya Mungu, anajua lile ni jeshi kubwa ambalo kwa muda mfupi sana, linaweza  kuvuruga mipango yake kama likimaanisha kuwa pamoja. (Zaburi  68:11 )

Anajua wanawake wanayobidii katika kuomba, analijua hilo, anajua wanawake ni wepesi katika imani, na ndio maana wapo kwa wingi kanisani, hivyo hataki jeshi la namna hii liwe na Nia moja, hataki washirikiane kwenye kazi, anataka kila mmoja atumike kivyake vyake ili nguvu iwe ndogo. Na anachofanya ni kupanda mbegu za kuchukiana, kusengenyana, wivu,kusemana, kijicho n.k. ili tu wachukiane.

Hivyo kama wewe ni mwanamke au Binti wa ki-Kristo, kataa hiyo roho kuanzia leo. Kataa hizo hila za shetani juu yako, jishushe kwa wenzako, na mwenzako naye ajishushe kwako, shirikianane, ili mpate  kupokea thawabu timilifu. Bidii yako ina thamani machoni pa Mungu, lakini umepungukiwa ushirikiano na wenzako,

Embu angalia wale wanawake walioizunguka huduma ya Yesu walivyokuwa. Walikuwepo waliokuwa ni  matajiri sana, wenye vyeo vikubwa katika jamii kwamfano Yoana, mke wa Kuza, wakili wa Herode,  lakini alikuwa tayari kushirikiana na Mariamu Magdalene aliyetolewa pepo saba. Angalia tena Mariamu ambaye alimzaa Yesu, hakujiona yeye ni zaidi ya wengine kisa kapewa neema ya kumzaa mwokozi wa ulimwengu, lakini alishirikiana na wenzake kwa nia moja. Na sio hao tu, biblia inasema na WENGINE WENGI, walikuwa ni nguzo muhimu sana kwenye huduma ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,

2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,

3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na WENGINE WENGI, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”.

Hata sasa wanawake wanaoshirikiana, wenye nia moja, watabakia kuwa  muhimili mkubwa sana katika kanisa. Lakini shetani atalipiga vita, Hivyo ikiwa wewe ni Euodia, leo hii  badilika, ikiwa wewe ni Sintike vilevile badilika, zitambue hila za shetani, kwa kuanza unyenyekevu.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

JE NI KWELI BWANA YESU SIKU YA KURUDI ATAFIKIA ISRAEL

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

Rudi nyumbani

Print this post

Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

Enzi zile za Bwana Yesu kulikuwa na makundi makubwa matatu yaliyokuwa na nguvu sana katika jamii, ambayo  yalikuwa yanampinga  sana vikali Bwana Yesu, tukiachalia mbali Mafarisayo na masadukayo ambao habari zao tunazijua sana, kulikuwa na kundi lingine la tatu lililoitwa Maherodi. Kama jina lao lilivyo ni watu ambao walikuwa wanamsapoti Herode, na kumtambua kama ndiye kiongozi na mtawala pekee anayepaswa kupewa heshima zote za kifalme, na hata utukufu. Kundi hili la watu lilikuwa lipo kisiasa zaidi kuliko kiroho.

Watu hawa hawakuwa na mapatano yoyote na mafarisayo na Masadukayo, kwasababu Masarisayo tangu zamani hawakuukubali utawala wa kirumi, bali walimtazamia Masihi ambaye atatoka katika uzao wa Daudi, atakayewakomboa dhidi ya watawala wao Warumi. Hivyo hawakuwahi kupatana kwa lolote, lakini kwasababu ya wivu ambao walikuwa nao kwa Yesu, walipatana na maherodi, ili tu wapate kuwa na nguvu ya kutosha ya kumwangamiza Bwana Yesu. Kama tu vile  Herode alivyopatana na Pilato wakati ule, watu ambao walikuwa ni maadui wa muda mrefu, lakini kwasababu ya kutanga kumwangamizi mwokozi wakapatana.

Marko 3:6 “Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake PAMOJA NA MAHERODI, jinsi ya kumwangamiza”.

Na ndio maana utaona, walikuwa wakituma watu kwao, na kumwandalia Yesu maswali ya mtego ambayo walijua majibu yake yatakinzana na sheria za Herode hivyo wapate sababu ya kumshitaki kwa majibu yake, lakini mipango yao wote ilishindikana mara nyingi. Utasoma habari hizo katika vifungu hivi;

Marko 12:13 “Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na MAHERODI, ili wamnase kwa maneno”.

Mathayo 22:16 “Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na MAHERODI, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu. 17 Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo”?

Marko 8:15 “Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode”.

Umeona, watu wa namna hii hata sasa wapo, kila taifa na kila nchi, tukiachilia mbali watu wa dini, ambao wanatumiwa na shetani, lakini wapo pia kundi lingine la watu ambao watakuwa tayari kupenda utukufu wa watawala kuliko utukufu wa Mungu. Kiasi kwamba wakiona jambo lolote hata la ki-Mungu linanyanyuka watataka tu kuliweka chini, hata kama halileti madhara yoyote au halisababishi vurugu yoyote katika  jamii, watataka kulishusha ili tu kuupendeza utawala.

Hawa pamoja na kiongozi wao Herode ndio waliohusika kumfunga na kumuua Yohana Mbatizaji, vilevile kumpeleka Bwana Yesu kwa Pilato.

 Watu kama hawa walikuwepo kipindi cha Bwana Yesu, na watakuwepo hata sasa. Na wakati wa dhiki kuu pia watakuwepo.

Biblia imetuonya tusipende kuwatumainia wanadamu zaidi ya Mungu.

Zaburi 118:8 “Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu”.

Kwasababu anayemtumainia mwanadamu kuliko Mungu, kibiblia watu kama hao wamelaaniwa (Yeremia 17:5).

Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Matuoni ni nini katika biblia?

IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.

KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?

Swali: Je Ni sahihi kwa Mkristo kupeleka kesi mahakamani?

Rudi nyumbani

Print this post

ENTER THROUGH THE NARROW DOOR.

Shalom. May the name of our Lord Jesus Christ.

Welcome, let us contemplate on the Word of God.

Luke 13:22-27 “

22 And he went through the cities and villages, teaching, and journeying toward Jerusalem.

23 Then said one unto him, Lord, are there few that be saved? And he said unto them,

24 Strive to enter in at the strait gate: for many, I say unto you, will seek to enter in, and shall not be able.

25 When once the master of the house is risen up, and hath shut to the door, and ye begin to stand without, and to knock at the door, saying, Lord, Lord, open unto us; and he shall answer and say unto you, I know you not whence ye are:

26 Then shall ye begin to say, We have eaten and drunk in thy presence, and thou hast taught in our streets.

27 But he shall say, I tell you, I know you not whence ye are; depart from me, all ye workers of iniquity.

The words of the Lord Jesus Christ in verse 24 above are one of the startling statements he spoke. Elsewhere in the Scriptures (Matthew 12:31 and 7:22),he also uttered terrifying statements. When carefully dismantled, they cause terror and fright. They cannot be taken so lightly but need to be given special care. whatever the Lord says will always come to pass. On that night, Jesus told Peter that before the cock could crow, he’d disown three times. As surely as he’d prophesied, a few moments later,Peter denied three times that he knew him. immediately, the cock crowed.

In Matthew 7:22, the Lord said that on the Day of Judgment, many people would say to him the very things he’d foretold beforehand. There will appear before him as many preachers on that day,telling him of how they had prophesied, cast out demons and performed many miracles in his name, but he will refuse them. Let us therefore strive and always prayerfully ask God to help us that we may not be among the lot which shall be turned away.

Today,we shall learn and meditate upon the words of Jesus in Luke 13:24.He told us to “make every effort to enter through the narrow door.” Let’s read another scripture to help us get a clear picture of his words.

14 Because strait is the gate, and narrow is the way, which leadeth unto life, and few there be that find it”.

In the scripture above, there are two things: door(gate) and road(way).We are told that the road is narrow which leads to life. Along this road, one cannot journey by any means such as a motorcycle or a vehicle. It is impossible for many people to pass while holding hands. Why? Because the road is narrow and only one person can walk along it

Salvation is exclusively personal. All that the Lord requires is that we personally place our trust in him. He/she must deny themselves and decide to follow him. Jesus is the narrow road. When you choose to follow him,you mustn’t come along with your religioun or denomination. You got to let go of it and go to him as you are.

The Lord said that “THE DOOR IS NARROW.” This means that where the narrow road ends is a door.This door is as narrow as the road itself. It’s impossible to to pass along the road while driving or riding on a bicycle, how about at the door? It would mean that one cuts off some of his body parts if they should get through the door; because the body could be too big to let them enter the door.The Lord said;

Matthew 5:30;”And if your right hand causes you to sin, cut it off. It is better for you to lose a part of your body than for your whole body to go to hell.”

Salvation is infinitely costly. it’s not easy. For this reason, Jesus told us to strive! We should try all means to enter through the narrow door.If we willingly commit to follow him, the Lord promises to help us in all things, (Matthew 19:26)

Is your wealth hindering you from seeking God? Lay them aside for a time. First seek the kingdom of God and all these  shall be added to you.Are your family members keeping you from turning to God and to do his will? Remember that the road is narrow and it’s impossible to pass along in groups. Lovingly tell your brothers that you are born again and have decided to follow Jesus at all costs.

We need to avoid the things which hinder us from entering into the heavenly kingdom, so we may attain the requirements for us to enter through the narrow door.We have to do quickly because a time will soon come when the door will be shut. Many will long to enter in but shall not be able. The Christian life is filled with struggles, but with the Lord on our side, nothing is impossible. If we let him have his way in our lives and rely on him,we shall be more than conquerors.

God bless you

Related articles:

WHATEVER YOU DO FOR CHRIST , COUNTS.

THERE’S POWER WHICH DRAWS US TO CHRIST, VALUE IT!

PRAY WITHOUT CEASING.

JONAH’S VINE.

Home

Print this post

Matuoni ni nini katika biblia?

Matuoni limetokana na neno “kituo”. Hivyo popote lilipoonekana katika biblia lilimaanisha kituo, au vituo au kambi. Na matuo hayo au kambi hizo zinaweza kuwa ni kambi za kazi, au za vita, au za makazi au za shughuli nyingine yoyote maalumu.

Kwamfano tunaweza kuona sehemu chache neno hilo lilipoonekana katika biblia..

2Wafalme 3: 24 “Hata walipokuja matuoni kwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata wakakimbia mbele yao; wakaendelea wakiwapiga-piga Wamoabi hata kwao”.

Hapo neno hilo limetumika kama “kambi ya vita”.. hivyo ni sawa na kusema “Hata walipokuja kambini mwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata wakakimbia mbele yao”

Pia tunaweza kulisoma katika..

2Nyakati 32:21 “Naye Bwana akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa wote, na majemadari, na maakida,MATUONI mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake mwenye haya ya uso. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, wale waliotoka viunoni mwake mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga”.

Mistari mingine yenye neno hilo ni Zaburi 106:16, 2 Nyakati 22:1, Amosi 4:10 na Zekaria 14:5.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

UFUNUO: Mlango wa 19

JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

Ni uthibitisho upi unaoonyesha kuwa kuna MBINGUNI na KUZIMU?

Rudi nyumbani

Print this post

ANGALIENI MWITO WENU.

1Wakorintho 1:26 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;”

Kwanini Mtume Paulo, alisisitiza kwamba tuangalie sana mwito wetu? Ni Kwasababu kwenye mwito ndipo watu wengi, tunapokosa shabaha, tukidhani Mungu anahitaji kwanza ujuzi fulani, au ukubwa fulani ndipo atuite tumtumikie, au tunadhani wale wenye vyeo vikubwa ndio hao Mungu anawatumia sana katika kazi yake.

Wito wa Mungu, ni tofauti na wito wa kibinadamu, Mungu akikuita, jambo la kwanza analolifanya kwako ni kukufagia kwanza, ikiwa wewe ni mtu mwenye ujuzi, au cheo fulani, au elimu fulani kubwa, ni anaondoa kwanza huo ujuzi wako kwake, anakufanya kuwa si kitu chochote, ndipo sasa akutumie, vinginevyo ukienda na cheo chako kwake, ukadhani hicho ndicho kitakachomshawishi yeye atembee na wewe, ujue kuwa umepotea.

Tumtazame, Musa, yeye alikuwa mrithi wa Farao, alikuwa anayo elimu kubwa ambayo hakuna asiyejua hilo , Biblia inatuambia Musa alifundishwa hekima yote ya ki-Misri na alikuwa pia ni mjuzi wa kipekee sana katika kuongea.

Warumi 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo”.

Na kumbuka kwa wakati ule taifa kama Misri ni sawa na Marekani ya leo, ni taifa lililokuwa linashikilia uchumi wa ulimwengu mzima.

Lakini tunaona Mungu alipoanza kumvuta kwake, alikimbilia kule jangwani, na huko akawa  anachunga mifugo ya mkwe wake Yethro, kwa muda mrefu sana wa miaka 40, wakati wote huo, Mungu hakujionyesha kwake, wala kujidhihirisha, unaweza ukajiuliza ni kwanini ichukue muda wote huo? hiyo yote ni Mungu alikuwa anamwondolea kwanza ule utashi wake aliokuwa anajiona anao, ule ujuzi wake, ambao hapo mwanzo alidhani pengine ndio angeutumia huo kuwaokoa wana wa Israeli, lakini ikawa ni kinyume na matazamio yake, aliendelea kukaa katika hali hiyo hiyo kwa muda wa miaka 40 mizima.

Na wakati ambapo hata ule ujuzi wake wa kuzungumza umekufa, hapo ndipo Mungu alipomwita, na ndio maana utaona alipoitwa na Mungu jambo la kwanza alimwambia  kuwa yeye sio Mnenaji, yaani hana uwezo tena kwa kuzungumza siasa majukwaani, kama alivyokuwa nao kule mwanzoni,

Kutoka 4:10 “Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.

11 Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana”?

Unaona? Musa huyu huyu, biblia inatuambia alikuja kuwa MPOLE kuliko watu wote waliokuwa duniani wakati ule. Kutoka kuwa muuaji, mpaka kuwa mtu mpole sana zaidi ya watu wote, si jambo jepesi inahitaji kujishusha kwa Mungu kweli kweli.

Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.”

Mtu kama huyo ndio Mungu alitembea naye. Na kanuni za Mungu huwa hazibadiliki, akisema hivi, ndivyo ilivyo, hata sasa, Mungu hatembei na watu wanaojiona kuwa ni bora kuliko wengine, hawatumii watu wanaojiona wana elimu kubwa au washupavu kuliko wenzao,  hawatumii kamwe watu wanaojiona ni vigogo kuliko wenzao, Na kama akitaka kukutumia basi jiandae kufanywa kama Musa,. Jiandae kushushwa kwanza. Vinginevyo sahau kutumiwa na Mungu.

Na ndio maana ukiendelea pale utaona anasema..

1Wakorintho 1:26 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;

27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;

29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu”.

Ndivyo ilivyo watu wasiokuwa na utashi wowote ni rahisi sana wao kutumiwa na Mungu kuliko watu wenye vyeo au wenye elimu kubwa za kidunia, kwasababu hao hawana cha kujisifia mbele za Mungu. Na watu wa namna hii ndio Mungu anaowafunulia siri zake nyingi.

Luka 10:21 “Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza”.

Halikadhalika, watu wasio na elimu kubwa za theolojia ndio wanaokuwa katika nafasi kubwa ya kutumiwa na Mungu kuliko hao wengine, kwasababu hawa hawana cha kutegemea isipokuwa uongozo wa Roho Mtakatifu, lakini hao wengine watategemea elimu zao za dini ndio ziwasapoti, au ziwalinde, au ziwape heshima.

Vivyo hivyo na sisi pia tunapaswa tuutafakari sana mwito wetu, tujiulize je Mungu tumempa nafasi ya ngapi katika maisha yetu, Je! Ni kweli tumeshusha viburi vyetu na kuvua ujuzi wetu, ili kumruhusu yeye atutumie? Au tumejikweza kwake na kujiona sisi ni wa kipekee sana kisa tuna elimu, au tuna vyeo, au tuna heshima kuliko wengine.

Tuutafakari mwito wetu, ili tujue ni wapi Mungu anataka tutembee naye, na tuanze kujishusha kuanzia sasa.. Kwasababu kiburi ni adui mkubwa wa utumishi wa Mungu. Tukitaka tutumiwe na Mungu tushushe kwanza viburi vyeo, na kujiona sisi ni sawa na watu wengine wote.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.

TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.

KUMTUMIKIA MUNGU, KUNAWEZA KUWE KINYUME NA MATARIJIO YAKO.

JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?

Je ni sahihi kuweka walinzi kulinda mali zetu?

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni sahihi kuweka walinzi kulinda mali zetu?

SWALI: Je ni sahihi kwa sisi tuliookoka na tunaomtegemea Mungu kuweka walinzi kulinda mali zetu  au mali za kanisa?. Kwasababu Biblia inasema Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure (Zab.127:1).

JIBU: Si dhambi kuweka walinzi au kuweka ulinzi katika mali zako, tena ni jambo la busara zaidi na la hekima. Unapokuwa na biashara yako au kazi yako ambayo ni halali inayompendeza Mungu, na ndani ya yake una mali nyingi, basi ni hekima kuweka ulinzi na pia kuifunga na kuhakikisha haitachukuliwa au kuibiwa kirahisi. Sio dhambi kabisa kufanya hivyo.

Kitu pekee ambacho si sawa na hakimpendezi Mungu, ni sisi kutegemea hao walinzi kama ndio msaada wetu na tegemeo letu la mwisho. Hapo ndipo linapokuja hilo neno..

Zaburi  127:1 “Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure”.

Kinyume chake ni kweli, Bwana akiijenga nyumba wajengao hawafanyi kazi bure, kadhalika Bwana akiulinda mji wakeshao hawakeshi bure. Vile vile Bwana akiwa upande wetu kwa chochote tukifanyacho, hicho tunachokifanya hakitakuwa bure.

Ipo mifano kadha wa kadha katika biblia ya kujifunza, lakini itoshe tu leo kujifunza juu ya Nehemia, mtumishi wa Mungu. Wakati alipopata maono ya kwenda kuukarabati mji mtakatifu Yerusalemu, alikutana na vizuizi vingi, vya watu kuyapinga hayo maono..Hivyo ikampelekea kuingia katika hatari kubwa hata kufikia kupoteza maisha yake, lakini yeye alikuwa anamcha Mungu, na kumtegemea..na alimtegemea kwa kila kitu, lakini ulipofika wakati wa kuijenga nyumba ile hakuwa na budi ya kumwomba Mungu na pia kuweka walinzi huku anaifanya kazi ile… Lengo ni ili wasirudishwe nyuma na maadui zao..

Nehemia 4:7 “Lakini ikawa, Sanbalati, na Tobia, na Waarabu, na Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno;

 8 wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo.

9 BALI SISI TULIMWOMBA DUA MUNGU WETU, TENA TUKAWEKA WALINZI, MCHANA NA USIKU, KWA SABABU YAO, ILI KUWAPINGA”.

Umeona, waliomba dua na pia wakaweka walinzi, lakini pamoja na kuweka walinzi, tumaini lao lote halikuwa kwa hao walinzi, bali walimtumainia Mungu, hivyo hawakukesha bure katika kuujenga huo mji na kuulinda, ndio maana mpaka leo kipande hicho cha ukuta kulichojengwa na Nehemia kipo Israeli, pale Yerusalemu maelfu ya miaka imepita bado sehemu ya ukuta ipo mpaka leo. (Tazama picha juu).

Hao waliweka walinzi na kukesha kuulinda na kuujenga mji, na mpaka leo sehemu ya ukuta ipo, kazi yao haikuwa bure..Lakini kama wangeweka walinzi na kuujenga huku wakizitumainia nguvu zao, hapo lingetimia hilo neno.. “Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye afanya kazi bure”..Ni wazi kuwa wangeshambuliwa na maadui zao na huo mji wanaoujenga wasingemaliza.

Kwahiyo tunajifunza, tuwapo na kitu chochote ambacho Mungu katubariki kwa hicho, basi hatuna budi kukutunza na kukulinda kwa kadiri tuwezavyo, Sio hekima wala akili kuacha milango wazi ya nyumba yako usiku, au kuacha wazi mlango wa sehemu ya biashara yako mpaka asubuhi ukiamini kuwa hakuna atakayeingia na kuzichukua mali zako. Nakuambia ukweli ukija asubuhi hutakuta chochote, kwasababu unamjaribu Mungu.

Itokee bahati mbaya umesahau kufunga mlango wa maingilio ya sehemu za mali zako, hapo Bwana ataingilia kati kuzilinda mali hizo utazikuta salama kimiujiza miujiza tu, haijalishi zipo mazingira gani… lakini kamwe usimjaribu Mungu kwa kuacha kukilinda kile ulicho nacho, huku ukisema Mungu atazilinda tu..hapo utakuwa unamjaribu Mungu na unatenda dhambi..

Na sio vitu vya mwilini tu ambavyo tunajukumu la kuvilinda, bali hata vitu vya rohoni, ambavyo ndio vya muhimu zaidi. Na cha kwanza kabisa cha kukilinda ni WOKOVU mtu alioupata..

Biblia inasema..

Ufunuo 3:11  “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.

Na pia inasema..

Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

 24 Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.

 25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa”

Umeona?..baada ya kumpokea Yesu sio wakati wa kujilegeza na kusema nipo salama!..bali ndio wakati wa kukilinda kile ulichokipokea..kwasababu WIZI wa rohoni upo!!…shetani anatafuta kwa hali na mali kuiba vile vya rohoni tulivyopewa na Mungu.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba ulinzi wa vitu vya rohoni na mwilini unapaswa uwe tabia ya kila mkristo, kama vile ilivyo tabia ya Mungu kutulinda sisi, yeye ijapokuwa ametupa tayari wokovu lakini bado anawatuma malaika wake kutuzunguka kutulinda pande zote usiku na mchana, hivyo na sisi hatuna budi kulinda vile tulivyopewa.

Bwana atubariki.

Kama hujampokea Yesu, nakushauri ufanye hivyo leo, hizi ni siku za Mwisho, na parapanda inakaribia kulia na Kristo kuchukua watu wake, kwenda nao mawinguni, Je! Utakuwa wapi siku hiyo?

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.

Swali: Je Ni sahihi kwa Mkristo kupeleka kesi mahakamani?

 Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?

Je ni sahihi kumtenga mtu anapofanya dhambi kanisani?

Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?

Rudi nyumbani

Print this post

IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.

Bwana YESU asifiwe sana, karibu tujifunze Neno la Mungu.

Awali ya yote ni vizuri tukaweka msingi kwanza wa kufahamu nini maana ya Sabato.

Sabato maana yake ni pumziko/kuacha kufanya kazi/ kustarehe/kuingia rahani mwako. Mungu alifanya kazi yake ya kuumba kwa muda wa siku sita mfululuzo kama tunavyosoma katika kitabu cha Mwanzo, na ilipofika siku ya saba kazi yote ilikuwa imeshamalizika, ndipo akastarehe/ akapumzika, hivyo akaibariki siku hiyo na kuifanya kuwa kama kumbukumbu la pumziko lake, na baadaye akawaagiza wana wa Israeli walipokuwa kule jangwani kwamba kila itakapofika siku hiyo waifanye kuwa ni sabato yao.

Lakini Sabato haikuwa ile siku yenyewe ya saba, bali sabato ilikuwa ni lile  pumziko lenyewe, Lakini “SABA” yenyewe inawakilisha pumziko la Mungu, kwasababu katika saba ndipo Mungu aliingia katika pumziko lake. Na ndio maana ukisoma kwenye biblia, Mungu hakuiwekea sabato yake mipaka kwamba iwe tu ni katika siku ya saba ,hapana.. Bali  utaona alikwenda mpaka kwenye mwaka wa Saba, ilikuwa kila mwaka wa saba, hakuna kupanda, wala kwenda kufanya kazi yoyote mashambani, bali waipumzishe ardhi, watulie majumbani kwao. Utalisoma hilo katika..

Walawi 25:1 “Kisha Bwana akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia,

2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana.

3 Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake;

4 lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.

Unaona, haikuishia hapo tu kwenye mwaka wa 7, bali pia miaka hiyo miaka 7, ikipita mara saba tena, kuna sabato nyingine itakayokwepo katika mwaka unaofuata..yaani 7×7 =49, ikiwa na maana, mwaka wa 50 ni sabato ya kumziko na maachilio, inayojulikana kama YUBILEE.

Walawi 25:11 “Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.

12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.

13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake”.

Haiishii hapo tu, tutakuja kuona mbele kidogo, sabato nyingine ambayo Mungu ameificha katika maandiko, ambapo ipo katika miaka 1000 kwa ajili ya wateule wake.

Sasa ikiwa tumeshafahamu, sabato ni PUMZIKO, na sio siku fulani, au mwezi fulani, au mwaka fulani, tutafahamu sasa kuwa hata wana wa Israeli kutolewa Misri na kupelekwa Nchi ya Kaanani, ni kwamba walikuwa wanaingizwa katika Sabato yao, (yaani rahani mwao,) ambayo Mungu alikuwa amewaandalia.

Lakini biblia inatuonyesha kuwa sio wote waliweza kuingia katika hiyo raha ya sabato yao, kutokana na kutokuamini kwao na matendo yao kuwa maovu. Si wote waliweza kuingia katika nchi ibubujikayo maziwa na asali isipokuwa wale wawili tu  lakini wengine wote waliosalia Mungu aliwaua kule jangwani.

Waebrania 3:8 “Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,

9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini.

10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;

11 KAMA NILIVYOAPA KWA HASIRA YANGU, HAWATAINGIA RAHANI MWANGU.

12 Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.

13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.

14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;

15 hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha.

16 Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?

17 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?

18 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale”.

Unaona? Wengi wao walishindwa kuingizwa katika pumziko lao, kutokana na kuasi kwao.. Lakini sasa bado biblia inatuambia, sabato yao ilikuwa ni kivuli tu cha sabato halisi inayokuja huko mbeleni ambayo Mungu aliwaandalia watu wake, waaminifu.  Mtume Paulo alisema kama ingekuwa Yoshua amewapa raha yenyewe, basi Daudi asingeandikaa tena mahali fulani huko mbeleni juu ya watu wa Mungu kuingia rahani mwa Mungu.

Waebrania 4:7 “aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu.

8 Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.

9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu”.

Umeona? Sisi kama watakatifu tunaomngojea Bwana bado hatujaingia kwenye raha yetu, au sabato yetu, ambayo Mungu alituandalia tangu zamani.. Sasa kumbuka Mungu huwa anapenda kutumia namba SABA, hasaa kuwakilisha sabato yake, kwa kustarehe kwake siku hiyo.

Na biblia inatuambia kwa Mungu miaka elfu moja ni sawa na siku moja. (2Petro 3:8). Sasa kama ulikuwa hujui ni kwamba tangu wanadamu tuumbwe, hadi sasa imeshapita miaka 6000, aidha inaongezeka kidogo sana, au inapungua kidogo sana. Lakini tupo katika mduara huo huo wa miaka elfu 6. Yaani Tangu Adamu mpaka Nuhu, inakadiriwa ni  miaka elfu 2 ilipita, na tangu Nuhu Mpaka kuzaliwa kwa Yesu vilevile inakadiriwa ni miaka elfu 2 ilipita, na tangu kuzaliwa kwa Yesu hadi sasa tunajua ni miaka elfu 2 tupo, kwahiyo jumla ni miaka elfu sita.

Na kama tunavyofahamu kwa Mungu miaka elfu ni sawa na siku moja, kwahiyo mpaka sasa ni kama siku 6 tu kwa Mungu zimepita, na siku ya saba ni sabato yake. Hivyo miaka elfu moja ijayo itakuwa ni sabato ya Mungu kwa watu wake.

Hapo ndipo lile Neno la UTAWALA WA MIAKA ELFU MOJA linakuja kutimia, ambalo Kristo atatawala na watakatifu wake hapa duniani, dunia ikiwa katika hali ya amani na furaha tele.. Kwa maelezo marefu juu ya utawala huu wa amani, tutumie ujumbe inbox tukupe somo lake.

Wakati huo dunia hii itakuwa kama paradiso, kwasababu hakutakuwa na shida wala taabu, wala mateso, tutamfurahia Mungu wetu kwa Muda mrefu sana wa miaka elfu moja, wakati huo sio wa kukosa ndugu yangu..lakini inasikitisha kuona kuwa wengi wetu hatutaingia katika raha hiyo kwa mfano tu wa kuasi kwa wana wa Israeli kule jangwani..

Hizi ni nyakati za za kumalizia hakutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili, yaani sisi ndio tutakaoshuhudia tendo zima la UNYAKUO, Jiulize wewe utakuwa wapi wakati huo utakapofika ndugu yangu, Na ndio maana mtume Paulo ametuonya na kutuambia..

Waebrania 3:12 “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.

13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi”.

Waebrania 4:11 “Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi”.

Huu sio wakati wa kutanga tanga na huu ulimwengu, Huu ni wakati wa kuelekeza macho yetu mbinguni, tuhakikishe kuwa hata tukifa tutakuwa katika ufufuo wa kwanza, na unyakuo ukipita basi tunaenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni, ambapo tutakula ile karamu ya mwana kondoo kisha tutarudi kutawala na Bwana hapa duniani.

Je! Umeokoka? Kama bado unasubiri nini? Tubu dhambi zako mfuate Yesu, akupe uzima wa milele.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

KAMA MKRISTO FAHAMU ZIPO HATUA UTAPIGISHWA NA MUNGU.

Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)

Rudi nyumbani

Print this post

TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.

Tafakari sana kabla hujafikia hitimisho Fulani ambalo ndio litakuwa la kudumu katika maisha yako.

Kuna watu wengi sana ambao shetani kawafumba macho, na kuwafanya wasifikiri vyema kabla ya kufikia hitimisho la maisha yao.

Kwamfano kuna watu wanatazama mwenendo wa watumishi wa uongo, au waliorudi nyuma, na kuhitimisha kwamba kamwe hawataokoka..kisa tu wameona hao watumishi wakifanya mambo ya ajabu yasiyopatana na wokovu kabisa.. Mtu wa namna hii tayari kafikia hitimisho la maisha yake bila kutenga muda wa kutafakari/ kufikiri sana.

Ndugu ni kweli umezunguka kila mahali hujaona mchungaji mkamilifu kama ulivyotaka wala ulivyotegemea…Lakini hiyo isikupe nafasi ya kusema hutamtafuta Mungu kamwe wala hutaokoka..Kwasababu ni kweli hujaona mchungaji mkamilifu lakini yupo aliye mkamilifu ambaye hakutenda dhambi kabisa hata moja, yaani YESU KRISTO, habari zake zimeelezwa kwa urefu katika maandiko, Umekataa kumsikiliza mchungaji wako kwasababu umeshuhudiwa kafumaniwa katika uzinzi, umekataa kumsikiliza muhubiri fulani maarufu kwasababu kakengeuka kawa kama watu wa kidunia n.k.. Lakini yupo mmoja aliye mkamilifu YESU KRISTO, mfuate huyo hao wengine waache.. Unafikiri utajitetea vipi siku ile ya hukumu?.

Utasema Bwana mimi nilikata tamaa ya kuendelea na wokovu kwasababu mchungaji wangu alinitaka kimapenzi, hakuwa mkamilifu,..ni kweli mchungaji wako anayo dhambi lakini alikuwepo YESU AMBAYE BADO NI MWAMINIFU, hana dhambi, mchungaji mkuu.. ungemfuata huyo Yesu, umwache mchungaji wako..Lakini wewe umewatapika wote…Utajitetea vipi siku ile???… kama vigezo vya utakatifu Bwana Yesu kavikidhi vyote, hana kosa wala hatia…Tafakari sana kabla ya kufanya maamuzi, usitafakari juu juu tu.

Bwana Yesu alisema maneno haya..

Yohana 8.46  “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?”

Mchungaji wako anayekuchunga anayo dhambi, pengine umemshuhudia akisema uongo, umemshuhudia akizini, lakini ni wapi Yesu umemshuhudia akisema uongo, ni wapi umemshuhudia akizini? …lakini wewe umemkataa Yesu aliye mkamilifu sawasawa na Mchungaji wako,..ni nani sasa utakayemkubali mwenye vigezo unavyovitaka wewe??…..Ndio maana anauliza swali hilo hapo juu “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?” … Yesu hana dhambi hata moja unamkataa…utamkubali nani kwamfano ukiulizwa hilo swali?….siku ile utajitetea vipi mbele ya Bwana?.

Utasema mimi ni kijana, siwezi kuishi maisha bila kufanya uasherati, kwasababu naishi mazingira ya vishawishi vingi…. Siku ile ataletwa kijana aliye mzuri kimwonekano kuliko wewe na aliyeishi katikati ya mazingira magumu kuliko wewe, lakini aliweza kuushinda uasherati kwa kishindo kikubwa…Hapo utazungumza nini cha kujitetea??.

Unajua ni kwanini biblia inasema watakatifu watauhukumu ulimwengu??

Ni kwa njia hiyo ya wanavyoishi…kama kuna dada ambaye mnaishi naye mtaani anavaa vizuri katikati ya dunia hii ya wanawake walioharibika akili, siku ya hukumu atawahukumu wanawake wote waliokuwa wanavaa vibaya…na atawahukumu si kwa maneno, bali maisha yake ndio yatawahukumu hao wengine…wakati hao wengine wanasema Bwana ilikuwa haiwezekani kila duka lilikuwa linauzwa nguo fupi, yeye atasimamishwa na kuulizwa alizipata wapi hizo ndefu..na hivyo maisha yake kuwa hukumu kwa wengine, (hiyo ndio maana ya watakatifu watauhukumu ulimwengu 1Wakorintho 6:2)

Kwahiyo usifikiri kwa vyovyote vile siku ile kuna kushinda hoja mbele ya kiti cha hukumu.. hakutakuwa na hoja yoyote ya kushinda, ndio maana leo hii..tunapata nafasi hii ya kukumbushwa kutafakari kwa makini kabla ya kufanya maamuzi.

Leo hii umeuacha wokovu kwasababu ya mchungaji wako, Rudi mgeukie Yesu Mchungaji mkuu asiye na dhambi, leo hii maneno ya muumini mwenzako yamekufanya usiupende wokovu au ukristo, ni wakati wa kumtazama Kristo na si mwanadamu.. Leo hii umevunjwa moyo na wakristo wenzako, au kiongozi wako katika imani, hata ikakufanya ukate tama kabisa ya kuendelea na wokovu…Ni wakati wa kuyaweka hayo mawazo pembeni kwasababu, shetani anataka ufikiri hivyo hivyo mpaka siku ya hukumu, ili ukose cha kujitetea siku ile.

Na kama hujampokea Yesu kwasababu nyingine yeyote, huu ni wakati wa kufanya hivyo, tunaishi siku za hatari sana, na adui yetu shetani ana wakati  mchache sana, amewekeza nguvu nyingi katika kuwafanya watu wasione mbele, badala yake wawe bize kutafuta mambo ya kidunia na kuwa na vijisababu vidogo vidogo vya kuhalalisha huo usingizi wa kiroho..Hiyo amka leo. Kristo anarudi, parapanda inakaribia kulia, na mwisho wa dunia kufika.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya K.K, na B.K?  (B.C na A.D).

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

UWE MWAMINIFU HATA KUFA.

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

Rudi nyumbani

Print this post