SWALI: Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa? Kwani kunaendelea mabishano baina ya wakristo baadhi, wengine wanasema kwasasa huduma hizo hazitendi kazi tena kufuatana na andiko la Paulo katika
Waefeso 2:20 linalosema;
[20]Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
…Lakini wengine wanasema huduma hizo hadi sasa zipo katika kanisa. Je ukweli ni upi?
JIBU: Kabla hatujafahamu kwanza kama huduma za mitume na manabii zinaendelea hadi sasa au la!…tutazame kwanza aina za manabii wa mwanzo, na mitume wa mwanzo walikuwaje..
1)Manabii wa kutia msingi wa wakati wote
2)Manabii wa kuthibitisha misingi.
1 ) Hawa manabii wa kutia misingi; Ndio wote waliotiwa mafuta na Mungu kaandika biblia takatifu…mfano wa hawa ndio kama Yeremia, Isaya, Nahumu, Malaki, Yoeli, Yona, Habakuki..n.k. Kwamba nabii zao zisimame kama msingi na mwongozo wa daima wa kuliongoza kanisa la Mungu wakati wote..
2 ) Manabii wa kuthibitisha: Hawa Mungu aliwanyanyua kutoa mwongozo wa wakati fulani tu mahususi.. Walikuwa wanasema Neno la Mungu lakini la wakati fulani tu ambapo ukishapita basi, unabii huo hauna umuhimu tena kwa vizazi vijavyo.
Mfano wa hawa utawasoma wengi sana..wakina Mikaya, Aguri, Odedi, Azuri, Ahiya, pia katika agano jipya walikuwepo wakina sila, agabo..n.k
Vivyo hivyo tukirudi na katika Mitume wa Kristo.
Wapo ambao waliotiwa mafuta kwa lengo la kuweka misingi ya daima. Hawa ndio wote tunaosoma nyaraka zao katika maandiko..mfano Paulo, Petro, Yakobo, Yohana, Yuda, Mathayo, Luka.
Na wapo waliowekwa kwa ajili ya kutihibitisha / kutia misingi midogo.midogo. Mfano wa hawa ni Epafrodito Wafilipi 2:25..
Sasa tukishafahamu…hilo…tunaporudi katika lile andiko linalosema..mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii tunaweza kuelewa
Tusome;
Waefeso 2:20
Maana yake ni kuwa sisi kama kanisa tumejengwa juu ya mafunuo ya manabii watangulizi na mitume watangulizi wale waliochaguliwa kuweka misingi ya daima..(Yaani kwa lugha rahisi tumejengwa juu ya BIBLIA TAKATIFU)…
Hakuna namna tutajengwa juu ya misingi mingine mipya zaidi ya hiyo yao.. Hivyo kwasasa hatuna manabii na mitume kama wale watangulizi, ambao walipokea mafunuo ya moja kwa moja ya namna ya kulijenga kanisa la Kristo..ni sawa na kusema hatuna mitume mfano wa Paulo au Petro au manabii mfano wa Yeremia au Isaya, kwasasa.
Lakini wapo mitume na manabii wa nyakati ndogo ndogo, ambao wanafanya kazi za kuthibitisha misingi ambayo tayari ipo lakini sio wa kuleta jambo jipya duniani..
Kwamfano kazi mojawapo ya mitume ilikuwa ni kwenda kupanda makanisani mapya maeneo mapya..hivyo, mtu yeyote mwenye huduma.hii ndani yake, ni mtume lakini kazi yake itakuwa ni kutembea katika mstari ule ule wa mitume wa kwanza..hapaswi kuja na jambo lake jipya..anapaswa ahubiri kilekile mitume walichokifundisha, hapo atakuwa amekidhi kuitwa mtume.
Ni sawa na mtu anayejenga nyumba ya gorofa..msingi mkuu ni mmoja..ule uliopo chini…lakini akitaka aweke nyumba juu yake ni sharti afuata ramani ya msingi wa chini….
Ndivyo ilivyo kwa huduma hizi za kitume na kinabii.. Ni lazima zirejee katika biblia takatifu chochote kitolewacho lazima kionekane katika biblia sio katika maono yao wenyewe wanayojitungia.
Paulo aliandika maneno haya;
1 Wakorintho 3:10-15
[10]Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.[11]Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.[12]Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.[13]Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.[14]Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.[15]Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.
[10]Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
[11]Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
[12]Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.
[13]Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.
[14]Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.
[15]Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.
Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa tofauti ya wale na hawa ni kwamba wote kazi yao ni moja ya upandaji wa kanisa la Kristo,mahali na mahali, isipokuwa wasasa hawaleti fundisho jipya, au maono mapya isipokuwa yale ambayo tayari yameshaanzishwa na mitume.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nitamjuaje nabii wa Uongo?
JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
Hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.
JINSI MTUME PAULO ALIVYOUTHAMINI WITO WAKE, JUU YA WENYE VYEO.
VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Huu mstari una maana gani?
Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”.
JIBU: Mstari huo unatupa picha kuwa, kumbe vipo vitu vya kurithishwa, lakini pia kuna vitu ambavyo hatuvipati kwa kurithishwa..
Kwamfano, hapo anasema mali; kama nyumba, magari, kazi, hivi vitu mtu anaweza kuvipata kutoka kwa wazazi wake,..Lakini linapokuja suala la MKE MWENYE BUSARA. Sio jambo la kurithishwa, au kutafutiwa na wazazi, au kupatwa kwa njia ya mali, au kwa uzuri, au kwa cheo, au kwa nguvu..Hapana, bali mke mwenye busara anatoka kwa Mungu tu! Na si sehemu nyingine.
Kumbuka hapo anasema ‘mke mwenye busara’..Sio ‘mke’…ikiwa na maana, ‘mke’ anaweza kupatikana popote tu pale, hata bar, kazini, barabarani, disco, vyuoni, mtaani, n.k. utampata.. Lakini mwenye busara, hatoki pengine isipokuwa kwa Bwana tu.
Ndio kama huyu aliyezungumziwa katika Mithali 31:10-31..Ambaye sifa zake ni; Kumcha Bwana siku zote, kuwahurumia maskini na wahitaji, Kuishi vyema na watumwa wake, kuwa msaidizi kwa mumewe, asiye mvivu n.k. Biblia pia inasema katika 1Petro 3:1-6 mke mwenye busara ni Ni mtiifu kwa mumewe, mpole, mtulivu, ajisitiriye, aitunzaye nyumba yake.
Hivyo kumpata huyu, wala usijichoshe kwa njia za vitu au mali. Bali nenda mbele za Bwana, mwombe, mshirikishe, mpango wako, kisha yeye mwenyewe atamsogeza kwako, na utamfurahia.
Kumbuka: Kinyume chake pia ni kweli. Mume mwenye busara, hapatikani pengine popote isipokuwa kwa Bwana tu. Mume mwenye busara, ni Yule amchaye Bwana, ampendaye mke wake, kama nafsi yake mwenyewe, ailindaye familia yake, aihudumiaye nyumba yake.(Waefeso 5:25). Hivyo yakupasa umwombe Bwana, kabla ya kuchukua maamuzi ya kutafuta mke/mume.
Shalom.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.
WANA-NDOA: Baba Mkwe, Na mama Mkwe.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Je! taratibu za kufunga ndoa [yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?
MAFUNDISHO YA NDOA.
Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?
MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.
KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.
Katika maisha bila shaka kuna siku ambazo uliwahi kuamka asubuhi na kuona siku yako inakwenda vizuri sana, una furaha, unafanikiwa, au unautulivu, au unapokea taarifa nzuri mahali Fulani, kazini kwako, kwenye familia n,k. Lakini kuna siku ambazo unaamka huoni uzuri wowote, aidha unaumwa, unaudhiwa na watu, unapata hasara kazini, unapokea taarifa za msiba, unaibiwa, unapigwa, unapata ajali Fulani, n.k.
Ukiwa kama mwanadamu, nyakati hizi za raha na masumbufu ni lazima ukumbukane nazo, haijalishi utakuwa ni mkamilifu kiasi gani.. Na Mungu ameruhusu iwe hivyo, ili kutaka sisi tukue vema katika hali anayoitaka yeye..
Embu tafakari maandiko haya;
Mhubiri 7:14 “Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”.
Mungu ameyaweka hayo yaende sambamba, kwamba hili lisimuache Yule, wala Yule lisimwache huyu..Haiwezekani kila siku utakayoamka asubuhi tu iwe ya furaha,..au iwe ya huzuni tu..hapana,
Sasa kwanini afanye hivyo?
Sababu zipo tatu (3)
Mungu anapenda kutupa furaha, hivyo zipo nyakati utaburudishwa tu na Mungu, hata kama sio sasa wakati huo utafika tu katika maisha yako. Atakufajiri tu kwa njia zake mwenyewe anazozijua. Atakatiza furaha katika siku Fulani Fulani, au katika kipindi Fulani cha maisha, Hivyo Jifunze kumfurahia Mungu wako wakati unafanikiwa, kwa kumshukuru sana..(Yakobo 5:13)
Sikuzote mtu huwa anafikiri vizuri anapokuwa katika shida au mateso Fulani, anapopitia kuumwa kidogo, analazwa, hapo ndipo anapojitambua kuwa yeye sio kitu, hawezi kutenda jambo lolote kwa nguvu zake, au kwa mafanikio yake, hivyo hiyo inamfanya sikuzote tumaini lake alielekeze kwa Mungu. Kwahiyo basi ujifunze kufikiri sana unapokuwa katika matatizo au masumbufu fulani, kwasababu ndicho Mungu anachokitaka hapo, zidi kuwa mwombaji, jifunze Biblia, kaa uweponi, ukishindwa kulielewa hilo utakuwa ni mtu wa kulaumu laumu, kunung’unika nung’unika ovyo sikuzote uingiapo katika vipindi hivi.(Wakorintho 8:1-10 )
Mungu anataka uhai wetu wote, tuumimine mikononi mwake, anataka kila jambo tunalolifanya tuseme BWANA akipenda, (Yakobo 4:13-16 ), anataka tukiamka asubuhi tumwombe kibali cha siku mpya, tunapomaliza siku tumshukuru..Tunapoanza mwezi mpya tumwombe, tunapomaliza tumshukuru, tunapoongeza umri mwingine wa maisha tupeleke shukrani zetu kwake.
Ndivyo Mungu alivyokusudia tuishi. Ni vizuri tuyatambue haya mapema ili tusiwe watu wa kutokuzielewa njia za Mungu wakati mwingine. Tuendelee kumcha Mungu katika majira tuyapitiayo kwa wakati huo,
Anasema pale mema au mabaya yanapokuja tu ghafla, kwa kutokujua mwenyewe..Hiyo inakupa sababu ya kujinyenyekeza, mbele za Mungu, na kumkabidhi Mungu mambo yako yote. Kwasababu hujui kama kesho utakufa au utaendelea kuishi..Ndio maana pale anasema “ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”
Kwa kumalizia tafakari tena maandiko haya;
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani”.
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani”.
Bwana atusaidie.
Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.
Nyakati za kuburudishwa ni zipi? (Matendo 3:19).
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)
Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.
Mego ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Mithali 17:1)
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia..
Vipo vipindi viwili vya Bwana Yesu kutuita katika maisha yetu.
Hebu tujifunze namna alivyowaita wanafunzi wake mara ya kwanza na mara ya pili, ili itusaidie na sisi kujua jinsi wito wa Mungu ulivyo..
Mara ya kwanza Bwana Yesu aliwaita wanafunzi wake kipindi wapo katika shughuli zao, ndio hapo utaona anamfuata Petro na Adrea kuwaambia wamfuate (Mathayo 4:19), baadaye tena anamfuata Mathayo katika shughuli yake ya utoza ushuru na kumwambia nifuate (Mathayo 9:9). Lakini katika wito wote wake huo, hakuwapa masharti yoyote magumu wanafunzi wake.. wengi wao aliwapa maneno ya faraja tu kuwa “watakuwa wavuvi wa watu badala ya samaki”.. wengine waliambiwa wataona mbingu zikifunguka na malaika wakishuka na kupanda juu ya Mwana wa Adamu (Yohana 1:51).
Kwahiyo wito wa kwanza kwa ufupi ulikuwa ni wito wa faraja na wa matumaini, haukuwa wito wa Masharti..
Lakini tunapokuja katika wito wa pili, tunaona Bwana Yesu akizungumza maneno mengine ambayo ni magumu kidogo… Tunaona anawaita tena kwa mara ya pili: Na wakati huu hawabagui tena kama alivyofanya hapo kwanza.. kwamba anakwenda mahali Fulani na kumtafuta Petro na Adrea peke yao!, na kuacha watu wengine, au anakwenda Forodhani na kumchagua Mathayo peke yake !, na kuacha watoza ushuru wengine..
Bali tunaona wakati huu wa pili, anawaita watu wote kwa pamoja, bila kubagua yule ni wanafunzi wake au sio wanafunzi wake, na kuwaambia maneno mengine mapya.. Na maneno hayo tunayasoma katika mstari ufuatao…
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate”
Mara ya kwanza Bwana Yesu hakutoa uhuru wa mtu yeyote kumfuata, yeye ndio alikwenda kuwatafuta akina Petro, na kuwachagua watembee naye.. Lakini mara hii ya pili, ANATOA NAFASI KWA WOTE! (wakike au wa kiume, awe mdogo au mkubwa, awe mlemavu au mzima).. na anawaambia wote (Mitume pamoja na Makutano). Kuwa mtu yeyote akitaka kumfuata, “AJIKANE MWENYEWE, AJITWIKE MSALABA WAKE AMFUATE”.
Wito huu wa pili ni kama unaufanya ule wito wa kwanza usiwe na nguvu tena!!.. Kwasababu hapa Bwana Yesu anawaita wote(wanafunzi wake pamoja na watu wa mataifa).. Pengine wakina Petro walingetemea maneno hayo waambiwe wakutano tu!, lakini wanashangaa na wao wanajumuishwa huko huko..
Wote wanapewa agizo moja! Bila upendeleo.. Maana yake ni kwamba pia alitoa mlango wa mtu yeyote kuondoka kama anataka kuondoka, haijalishi tayari alikuwa ameshaitwa hapo kwanza, haijalishi kama alikuwa tayari ameshapewa ahadi na Bwana…
Tunaweza kulithibitisha hilo katika…
Yohana 6:66 “Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.67 Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, JE! NINYI NANYI MWATAKA KUONDOKA?68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.69 Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu”
Yohana 6:66 “Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.
67 Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, JE! NINYI NANYI MWATAKA KUONDOKA?
68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
69 Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu”
Umeona hapo?.. Yule Petro ambaye aliitwa hapo kwanza kwa wito wa faraja, safari hii Bwana anamwuliza “JE UNATAKA NA WEWE UNATAKA KUONDOKA??”, anamwuliza pia na Nadhanieli ambaye aliambiwa ataona malaika wakipanda na kushuka juu ya mwana wa Adamu, “JE UNATAKA NA WEWE UNATAKA KUONDOKA??”, maana yake ni kwamba kama wangetaka kuondoka, basi mlango upo wazi Bwana angewaruhusu wala asingembembeleza… Na ahadi zile alizowaahidiwa Bwana angewapa wale waliokuwa tayari. (Hii inaogopesha sana!!).
Ndugu inawezekana kipindi unasikia wito wa Mungu kukuita ulikuwa unapokea maneno ya faraja kutoka kwa Bwana Yesu, na kujiona wewe ni wa kipekee sana…huenda Bwana Yesu alikwambia wazi kabisa kuwa utakuwa mtumishi wake na utawavuta wengi kwake na utakuwa Baraka kwa maelfu ya watu..
lakini nataka nikuambia kuwa “usibweteke na wito huo wa kwanza wa faraja”…”utendee kazi wito wa pili” Kwasababu hata Petro na Yohana waliambiwa hivyo hivyo, hata Nadhanieli mara ya kwanza aliambia maneno ya faraja kama yako!..lakini baadaye Bwana Yesu aliwageukia na kuwaambia kuwa “Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate”…Na Bwana Yesu aliwaweka kundi moja na makutano kana kwamba hakuwahi kuwaita huko nyuma.. Kana kwamba siku hiyo ndio aliyokuwa anawaita kwa mara ya kwanza.
Ndugu yangu, huenda ulishausikia wito wa Kwanza, na sasa upo katika wito wa pili, Amua leo kumfuata YESU upya kwa kujikana nafsi!!.. Wakina Petro, baada ya kusikia hayo maneno ndipo walipojijua kuwa wanapaswa wahakiki wito wao upya!.. Ndipo wakaamua kujikana nafsi kweli kweli na kumfuata Yesu.
Na wewe leo, achana na ukristo vuguvugu wa kujisifia maono au karama, anza kujikana nafsi na kubeba msalaba wako, kaa mbali na dhambi na ulimwengu, kwa kadiri uwezavyo, weka chini fasheni za kidunia ambazo hazimpi Mungu utukufu, acha kuvaa kikahaba, acha kuweka wigi kichwani, acha kuweka hereni na mikufu, na kuvaa nguo za kubana..ni machukizo kwa Mungu (1Timotheo 2:9), acha kuabudu sanamu, acha kufanana na watu wa ulimwengu huu….hata kama dunia nzima itakuona umerukwa na akili, hata kama ndugu na wanadamu watakwona umechanganyikiwa.. wewe mfuate Yesu, na udunia uweke nyuma, na siku ile utapokea Taji ya uzima.
Kumbuka siku zote kuwa “waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache”(Mathayo 22:14).
Tujitahidi tuwe wateule wa Bwana Yesu.
Maran atha!
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.
Swali: Pale Forodhani, Mathayo alipokuwa ameketi ndio mahali gani? (Mathayo 9:9).
Jibu: Tusome,
Mathayo 9:9 “Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona MTU AMEKETI FORODHANI, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata”
“Forodha” ni “Nyumba au kijumba kidogo” kinachotumika kukusanyia mapato.. Kwamfano watu wanaofanya kazi benki, huwa wanaketi ndani ya madirisha Fulani maalumu ya kupokea au kutoa fedha, sasa vyumba vile walivyopo ndivyo vinavyoitwa “forodha” ( kwa lugha nyingine).
Hali kadhalika watu wanaofanya kazi katika mashirika ya kukusanya mapato, huwa wanaketi katika chumba maalumu chenye dirisha ambapo wanapokea fedha na kutoa risiti. Vyumba hivyo ambavyo vimetengenezwa mahususi kwaajili ya kupokea wateja na kodi zao, au ada zao, au ushuru wao ndivyo vinavyoitwa Forodha.
Katika siku hizi Forodha pia zinatengenezwa na wafanya biashara, kutokana na kutanuka kwa wigo wa kibiashara, kwamfano watu wanaofanya kazi za uwakala wa mitandao ya simu mf. Mpesa n.k huwa wanatengeneza Viforodha vidogo, kwaajili ya shughuli zao hizo za kutoa na kupokea fedha.
Lakini ni funzo gani tunalipata kwa Mathayo aliyeketi Forodhani?..
Mathayo alipoitwa na Bwana Yesu, muda ule ule aliitikia wito!, hakungoja kesho, wala baadaye, badala yake muda ule ule alimfuata Bwana YESU.. Ijapokuwa alikuwa yupo katika mazingira magumu ya kumfuata Bwana Yesu, lakini ilimgharimu kuacha vyote na kumfuata Yesu!. Na faida ya kumfuata Yesu, Mathayo pamoja na wenzake waliyoipata, ni kwamba walikuja kupata mara mia kwa vile vyote walivyovipoteza, na zaidi sana walipata ahadi ya uzima wa milele.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”.
Je ni kazi yako ndio kikwazo cha wewe kumfuata Yesu?, je ni watoto wako au mke wako au wazazi wako ndio kikwazo cha wewe kumfuata Yesu kwa moyo wako wote na nguvu zako zote?.. kama kazi yako ndio kikwazo, basi nataka leo umkumbuke Mathayo, yeye kazi yake aliona si kitu zaidi ya wito wa Mungu!. Na mwishowe leo hii tunasoma waraka wake huu.
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.
Nakusalimu katika jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima.
Nehemia ni mtu aliyekusudia kutoka katika moyo wake, kwenda kuukarabati ukuta wa Yerusalemu uliokuwa umebomoka, mtu huyu hakuwa nabii, wala kuhani, wala hakujulikana popote, lakini kwa kuguswa kwake moyoni kwa habari alizozisikia kuhusiana na uharibifu ule, aliumia sana, ndipo akajitia nguvu, kumwomba Mungu kibali na baadaye akapewa, na kuweza kwenda Yerusalemu kwa ajili ya kazi hiyo ya kuukarabati. Sasa hatuna muda wa kueleza historia yote, kwa muda wako waweza kusoma habari yake tangu mwanzo hadi mwisho katika kitabu hicho.
Hivyo naamini kwa kuyatazama mapito yake, utapata funzo, hata na wewe ambaye, anataka kuingia katika kazi ya kusimama “mahali palipobomoka” ili upakarabati.
Sasa wakati Nehemia anafika Yerusalemu, ili kuanza operasheni yake ya kuujenga tena ukuta ule, ilimbidi kwanza, atembee, katika malango yote, na sehemu zote za ukuta huo ili atathimini, uharibifu uliotokea, pamoja na nguvu na gharama zitakazotumika kuukarabati tena..
Biblia inatuambia, aliondoka, usiku wakati ambapo watu wamelala, akaanza kuuzunguka ukuta ule wa mji ambao ulikuwa ni mrefu sana, Kuonyesha kuwa mpango bora wa kukarabati kusudi la Mungu, huwa hashirikishwi kila mtu, bali watu wachache sana tena, waaminifu, ambao wanaweza kuchukua mzigo wako..Tusome
Nehemia 2:11 “Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu.12 Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe”.
Nehemia 2:11 “Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu.
12 Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe”.
Anaendelea kusema…
13 Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto. 14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; LAKINI HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.15 Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo.16 Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo. 17 Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena.
13 Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto. 14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; LAKINI HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.
15 Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo.
16 Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo. 17 Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena.
Hapo mwanzo alipoanza safari,alikuwa na mnyama wake, Ambaye ni farasi/punda.. Mnyama Yule alimsaidia sehemu baadhi tu kufika,na kuona uharibifu uliotokea katika kuta, lakini alifika mahali, ambapo mnyama asingeweza kupita katika penyo zile, bali ni mtu tu! Hapo ndipo ikabidi amwache mnyama Yule, atembee yeye kama yeye, mguu kwa mguu, kutazama sehemu za ukuta, ndogo ndogo, za mafichoni, zilizokuwa zimeharibiwa vibaya sana na maadui zao. Asingefanya hivyo, ukarabati wake ungeishia pale pale punda alipoishia, asingekarabati kote.
Ndipo alipomaliza ziara hiyo, akarejea mjini, na kuwaambia makuhani na wahusika wote, hali ilivyokuwa.
Bwana anasema..
Ezekieli 22:30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu”.
Sikuzote kusimama mahali palipomoboka si rahisi, Mungu anatafuta watu hao mfano wa Nehemia hawaoni,,ni lazima tufahamu kuwa zipo gharama kubwa sana, za kukarabati, waweza kudhani, utakwenda na taasisi, au utakwenda na ushirika, au utakwenda na kiwango Fulani cha pesa kwenye akaunti yako.. Hapana vyote hivyo vinaweza kukusaidia kwa muda tu, bali utafika wakati hivyo vyote havitakusaidia, bali itakubidi usimame wewe kama wewe, kama ni kuomba, kama ni kuhubiri, kama ni kukemea dhambi, kama ni kuanzisha jambo..
Mnyama aliye chini yako, hataweza kuvuka nawe, ndugu zako hawataweza kutembea na wewe,katika maono hayo Mungu aliyokupa juu ya kusudi lake, .. Bali ni wewe kama wewe.
Ilimpasa Nehemia afanye hivi, japokuwa alipitia changamoto nyingi, mpaka mbeleni wakawa wanamdhihaki na kumwambia, ukuta unaoujenga jinsi ulivyo dhaifu, hata mbweha wakipita juu yake utaanguka.(Nehemia 4:3), Lakini hakuvunjika moyo, yeye aliendelea kusimama mpaka mwisho ..
Walipokuwa wanaujenga, mkono mmoja ulishika silaha, na mwingine tofali, waliujenga katika hofu, usiku kucha, Lakini mwishoni ulikamilika, katika utukufu mwingi. Na faida yake ni kwamba hadi sasa tunaisoma habari ya Mtu huyu Nehemia, na kumbukumbu lake lipo hadi leo.(Nehemia 4: 17-23)
Ndugu zipo kuta nyingi sana zilizobomolewa na ibilisi, hadi sasa Bwana anatafuta watu watakaosimama, makanisani kujenga nyumba yake, watakaosimama kwa vijana, kuwaweka kwenye misingi ya imani, watakaosimama kwa familia na watoto kuwafundisha kumcha Bwana. Watakaosimama katika Neno la Mungu, kufundisha injili ya kweli isiyoghoshiwa, na kukemea mafundisho potofu..
Swali ni Je! Sisi tutaweza kusimama na kujenga upya?
Kama ni hivyo basi tuwe tayari hata wakati mwingine kusimama peke yetu, kama Nehemia, pale ambapo hatuona sapoti, uwe ndio wakati wa kusonga mbele, na kuitenda kazi ya Mungu, pale ambapo tunaona vita, na dhihaka, tusife moyo bali uwe ndio tuifanye kazi, usivunjike moyo wala usikate tamaa..Kwasababu Kujenga kuna gharama. Lakini faida zake ni kubwa sana mwishoni.
Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)
Wana wa Asafu ni akina nani katika biblia?
Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?
TIMAZI NI NINI
UFUNUO: Mlango wa 17
Pango la Makpela ni lipi, je lina umuhimu wowote kwetu?
Neno Buruji lina maana gani katika biblia?
SWALI: Naomba kufahamu mstari huu unamaana gani?
Mhubiri 4:4 “Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.
JIBU: Sulemani ni mtu ambaye alipewa na Mungu uwezo wa kutambua hekima ya mambo yote yanayotendeka huku duniani.. Na moja ya jambo ambalo aliliona na kutolea habari zake ni kuhusiana na chanzo cha mafanikio mengi ya watu ni nini?.. Na ndio hapo anasema..
“Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake”.
Kwamba kila utajiri, au kazi za ustadi, yaani nyumba nzuri, magari mazuri, mavazi mazuri, hatua zote za mafanikio, asilimia kubwa hutokana na mtu kupingana na mwenzake, kwa tafsiri iliyo nzuri ni kwamba hutokea mtu kushindana na mwingine..ambacho chanzo chake ni wivu.
Kwamfano, mtu atasema mbona Fulani amenunua gari, mimi sijanunua, ngoja nikakope pesa nifanye kazi juu chini na mimi mwaka huu ninunue la kwangu zuri kuliko lile.. Sasa mtu kama huyu atapata gari kweli, lakini chanzo cha gari lake sio malengo yake, bali ni kwasababu wenzake wanayo magari yeye hana.
Hata mashirika makubwa, kufanikiwa kwao ni kwa mashindano, utaona kampuni moja la simu limetoa ofa hii, kesho lingine linaiga ofa ile ile na zaidi, ili lisipoteze wateja.. Hivyo yamefanikiwa kwa njia hizo hizo, za mashindano.
Tajiri mmoja atashindana na tajiri mwenzake ili awe namba moja, hivyo atafanya kazi kwa bidii usiku kucha, ili asishindwe na mwenzake, watashindana kibidhaa n.k.. Mchungaji mmoja atashindana na mchungaji mwingine kwa wingi wa washirika, au kwa ukubwa wa kanisa,
Sasa hayo yote Sulemani ameyaona na kusema ni ubatili, ni sawa na kujilisha(kuufuata) Upepo. Maana yake ni kuwa mafanikio yanayokuja kutoka katika wivu, au mashindano, hayana afya yoyote kiroho.
Hii inatufundisha nini?
Wafilipi 2:14-15 inasema..
“14 Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,
15 mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu”
Kama watakatifu, hatupaswi kutafuta kitu chochote kwa kushindana, utasema mwenzangu ana neema kubwa kama ile, ngoja na mimi nikafunge na kuomba nimpite,. Hapana, bali tunapaswa tuishi kwa kumtazama Mungu,kila mmoja katika nafasi yake aliyopewa na Mungu, na kuitendea bidii hiyo, kwasababu kwa kupitia hiyo ndio Mungu atatufanikisha, na sio kwa neema za wengine..
Bwana atubariki.
Tafadhali share na wengine ujumbe huu;
Nini maana ya “Amali” na “Ijara” katika biblia?
Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.
Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?
Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
Biblia inatufundisha kuomba bila kukoma…
Wathesalonike 5:17 “ombeni bila kukoma”
Leo tutatazama ishara chache ambazo zitatutambulisha kuwa kiwango cha maombi yetu kimejitosheleza au kimemfikia Baba yetu.
1.MZIGO KUPUNGUA NDANI YAKO.
Hii ni ishara ya kwanza itakayokutambulisha kuwa maombi yako yamefika kwa Bwana.
Unapoomba na kuona mzigo wa kile unachokiombea umepungua ndani yako, basi hiyo ni ishara kuwa kiwango chako cha maombi kimefikia kilele kwa muda huo.
Sasa swali utauliza utajuaje kuwa mzigo umepungua ndani yako?. Tuchukue mfano rahisi, Ulikuwa una jambo la muhimu au la siri ambalo ulikuwa umepanga kumweleza mtu Fulani (labda rafiki yako), na hujapata nafasi, ila unaitafuta kwa bidii, kiasi kwamba huwezi kutulia mpaka umemweleza jambo hilo, au umpe taarifa hiyo, sasa kipindi utakapokutana naye na kumweleza yote ya moyoni mwako, kuna hali Fulani unajiona mwepesi baada ya hapo, (unajiona kama huna deni tena, umeutua mzigo), unaona amani inarudi, na unakuwa huru.. Sasa hiyo hali unayoisikia baada ya kufikisha ujumbe kwa uliyemtarajia ndio kwa lugha nyingine ya (Mzigo kupungua ndani yako).
Kwahiyo hata sisi tunapoomba, yaani tunapopeleka hoja zetu mbele za Mungu, kabla ya kuzipeleka tunakuwa na mzigo mzito ndani yetu, lakini tunapokaa katika hali ya utulivu na kusema na Mungu kwa unyenyekevu mambo yetu na hoja zetu, basi kuna hali/hisia fulani ambayo Bwana Yesu anaiachia ndani yetu, inayotupa wepesi katika roho zetu, na kupunguza ule mzigo, kiasi kwamba, kama ulikuwa unamwombea Mtu, kuna hali Fulani inakuja ndani yako kuwa maombi yako yamemfikia Mungu, na hivyo amani ya kipekee inashuka ndani yako, na unajikuta ile hamu ya kuendelea kuombea hilo jambo inaisha, badala yake inakuja hali nyingine ya kumshukuru Mungu na kumshangilia na kumfurahia.
2. ANDIKO KUKUJIA au KUMBUKUMBU YA JAMBO FULANI.
Hii ni ishara ya pili ya maombi yetu kumfikia Baba..
Unapokuwa katika maombi, halafu ghafla likaja andiko katika ufahamu wako, na andiko hilo linauhusiano mkubwa na kile ulichokuwa unakiombea.. basi fahamu kuwa maombi yako yamefika, na hivyo Bwana anakuthibitishia kwa kukupa hilo andiko. Au unaweza kuwa unaomba halafu ghafla ukaletewa kumbukumbu Fulani ya kisa Fulani katika biblia, ambapo kupitia kisa hiko imani yako ikanyanyuka na kujikuta unapata amani au furaha kubwa.. basi hiyo ni ishara kuwa maombi yako yamefika, na hivyo katika hiyo hatua na kuendelea ni wakati wa kumshukuru Mungu na kuutafakari ukuu wake, kwasababu Bwana kashajibu na kusikia.
Vile vile unapokuwa katika maombi na moyoni una mzigo mkubwa kwa kile unachokiombea, halafu ghafla ikaja kumbukumbu Fulani ya kipindi Fulani cha maisha ambacho Mungu alikupigania ukauona mkono wake, au ukaja ushuhuda Fulani kichwani mwako wa mtu mwingine, na ghafla ukajiona umepata nguvu nyingine basi hiyo ni ishara kuwa hoja zako zimefika mbele zake na hivyo Bwana amekuthibitishia kwa kukukumbusha uweza wake na mkono wake.
3. NGUVU MPYA.
Unaweza usisikie chochote unapokuwa katika maombi, (yaani usisikie mzigo kupungua ndani yako) au usiletewe andiko lolote, lakini ukajikuta unapata nguvu ya kuendelea mbele zaidi….
Maana yake kabla ya maombi ulikuwa umekata tamaa, hata nguvu ya kuendelea mbele ulikuwa huna, lakini baada ya maombi..unaona kuna ujasiri umeongezeka ndani yako, kuna nguvu ya kuendelea mbele imekuja ndani yako, ingawa moyoni mzigo bado hujapungua..
Sasa hiyo hali ya kutiwa nguvu kabla ya kupokea majibu ya maombi yako ni ishara kuwa Maombi yako YAMEMFIKIA BWANA, ila wakati wa kupokea majibu yako bado!…Hivyo Bwana anakutia nguvu ili usije ukazimia kabisa, au ukaanguka kabisa…wakati huo zidi kujisogeza mbele zake kwa maombi ya shukrani…
Kwamfano unaweza kuwa unasumbuliwa na ugonjwa ambao ni mbaya sana, na umemwomba Mungu kwa muda mrefu, akuponye na hapo ulipo upo katika hali ya mauti uti, lakini ukajikuta unapata unafuu mkubwa sana, na hata kuendelea na shughuli zako kana kwamba huumwi kabisa.. lakini ule ugonjwa bado haujaondoka!.. sasa hiyo hali ya kupata unafuu baada ya maombi, ni ishara kuwa Bwana alishasikia maombi yako, ila siku kamili ya muujiza mkuu bado!, (na itafika tu)..lakini amekutia nguvu ili kukuonyesha kuwa yupo pamoja na wewe na ili usije ukazimia kabisa..
Vile vile unaweza kumwomba Bwana akupe kazi fulani nzuri ambayo kupitia hiyo utayafanya mapenzi yake, lakini badala ya kukupa hiyo shughuli unayoiomba muda ule uliomwomba, yeye anakupa riziki za kukutosha tu wakati huo.. (ulitegemea upewe kazi lakini yeye anakupa riziki tu)…Ukiona hivyo jua ni ishara ya kuwa maombi yako yameshamfikia yeye, Ndio maana anakutia nguvu…ni suala la muda tu!, mambo yote yatakaa sawa..
Isaya 40:27 “Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? 28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. 29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”.
Isaya 40:27 “Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie?
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;
31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”.
Zipo ishara za kutambulisha kuwa maombi yetu yamemfikia Baba yetu, lakini kwa hizi chache itoshe kusema kuwa Bwana Mungu wetu anatupenda na anatujali na anasikia maombi yetu. Lakini kumbuka kuwa kama bado hujampokea Yesu, (yaani hujaokoka), basi fahamu kuwa Mungu hasikilizi maombi yako wala hajibu. (Yohana 9:31)
Sasa ni kwanini hajibu, wala hasikilizi maombi ya watu ambao hawajampokea?.. Ni kwasababu mtu wa namna hiyo hawezi kuomba sawasawa na mapenzi yake, (kwasababu yeye mwenyewe alisema kuwa mafanikio ya mpumbavu yatamwangamiza, Mithali 1:32) na Mungu hapendi mtu yeyote aangamie wala apotee, bali wote wafikie toba na wafanikiwe..Hivyo atahakikisha kwanza unapata wokovu ndipo mengine yafuate..
Kwahiyo suala la kwanza ni wokovu kabla ya mambo mengine yote.. Kama hujampokea Yesu, kwa kutubu dhambi zako, na kubatizwa katika ubatizo sahihi, basi ni vizuri ukafanya hivyo mapema iwezekanavyo, ili uwe mshirika wa Baraka za Mungu.
Lakini kama tayari umeshampokea Yesu na umesimama vizuri katika imani, basi fahamu kuwa yote unayomwomba Mungu atakupatia sawasawa na ahadi zake, hivyo zidi kumwamini na wala usiishiwe nguvu.
Bwana akubariki
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
SAUTI NYUMA YA ISHARA.
MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu, Karibu tuzidi kuyachambua maandiko;
Mwanadamu anasongwa na mambo mawili pale linapokuja suala la kuamua hatma ya maisha yake ya milele. Je! Atii au apate maarifa kwanza?. Pale Mungu anapomwambia Usizini? Je, asifanye hivyo? Au achunguze kwanza ni nini kipo nyuma ya tendo hilo, ndipo awe huru sasa kuchagua kuzini au kutokuzini?
Ukweli ni kwamba asili ya mwanadamu ni kutaka maarifa kwanza, ya kitu ndipo baadaye atii, Lakini Je! Biblia inatufundisha nini kuhusiana na maamuzi sahihi na Salama ambayo Mungu aliyaweka kwa mwanadamu.
Tukisoma ile habari ya pale bustanini biblia inatuambia,.. Mungu alipanda miti yake, kisha alipomaliza akatoa maagizo kuhusiana nayo akasema..
Mwanzo 2:16 “Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika”.
Lakini mwanadamu akaona, hayo maelezo ya Bwana Mungu hayajitoshelezi, kwanini atuzuie tusile, hajui kuwa sisi tunataka tupate sababu kwanza, (tupate maarifa), kujua ni nini kwanza kipo nyuma ya mti huo, ndipo tuwe sasa huru kuchagua kuula, au kutoula. Ndipo wao wakauendea na kuula.
Mwanzo 3:4 “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni MTI WA KUTAMANIKA KWA MAARIFA, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala”.
Lakini walipofanya vile, hawakuvuna chochote, matokeo yake wakajikuta tayari wameshaingia kwenye matatizo ambayo mpaka sasa tunayashiriki, yale maarifa waliyoyategemea kuwafanya wawe bora, yakawa mauti kwao.
Asili yetu sisi wanadamu hatukuumbwa kwenye kupata maarifa kwanza, ndio tuishi, bali kwenye kutii kwanza.. Ndivyo tulivyotengenezwa na Mungu.. Kwamba tukitembea katika kutii tutakuwa salama sikuzote,..hayo mengine yatakuja baadaye. Ndicho alichokifanya Ibrahimu alipoambiwa akamtoe mwanawe sadaka ya kuteketezwa alitii kwanza, hakudadisi na kusema kwanini huyu Mungu atoe maagizo ya kishetani kama haya ya kuua watu, yeye alitii, ndipo akaja kujua sababu baadaye.
Hii ikiwa na maana kuwa,..Kama Yesu katuambia wazinzi wote, na waongo wote, hawataurithi uzima wa milele, bali sehemu yao ni katika lile ziwa la moto. Tunahitaji nini tena, kutafuta uzuri uliopo nyuma ya uzinzi, mpaka tukaujaribu.au kutafuta eneo la kijeografia la jehanamu, tulione ndio tuamini?
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Bwana Yesu anasema.. Yeye ndio njia, na kweli na uzima, mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye (Yohana 14:6), FULL STOP!..Sasa kwanini tutafiti njia zetu wenyewe za kutupa wokovu? Kwanini uishi kwa mitazamo yako, au ya wanadamu, wanaokuambia hakuna mwisho wa dunia, au hakuna maisha baada ya kifo
Katika nyakati hizi za hatari ambazo biblia inazitaja (2Timotheo 3:1), ni lazima “tuongeze maarifa ya kulijua Neno la Mungu, na sio maarifa ya kuyadadisi maneno ya Mungu, kama Adamu na Hawa”..Tutapotea haraka sana, tukiwa watu wa namna hii, kutilia mashaka maneno ya Mungu, kila andiko tunalolisoma, tunasema kwanini iwe hivi, au iwe vile?, kwani kuna shida gani, nikinywa bia yangu na simdhuru mtu? Acha kabisa hayo mawazo ya ibilisi..Utapotea…Wewe tii sasa, sababu utakuja kuzijua mbeleni. Sayansi itakuambia haipo hivyo, ukweli ni huu, mwanadamu wa kwanza alikuwa ni sokwe, uthibitisho umepatikana, hakuna Mungu..Ndugu hapo ndio umepotea kabisa, Kumbatia Neno la Mungu.
Tunapohubiriwa tuache anasa, jambo la kwanza ni kutii, hilo Neno, haijalishi itatugharimu kiasi gani..Tunapohubiriwa tuvae mavazi ya kujisitiri, tuache vimini, tuache rushwa. Tusiulize ulize kwanini..Ni kuweka kando kwanza..Sababu tutakuja kujua huko mbeleni.
Tunusuru roho zetu…Tulipokee Neno la Mungu kama lilivyo.
Bwana atusaidie sana.
Maran Atha.
Tofauti kati ya Hekima, ufahamu na maarifa, ni ipi?
Maana ya watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
AINA SABA (7) ZA UNAFIKI, AMBAZO UNAPASWA UJIEPUSHE NAZO.
Bilauri ni nini kibiblia?(Ufunuo 21:11,22:1)
TUYATENDE MAMBO YOTE KWA UZURI NA UTARATIBU.
Je mke wa Musa alikuwa ni Mweusi?
Shalom, karibu tuyatafakari maandiko.
Bwana Yesu ameruhusu miujiza itokee kwenye maisha yetu kwa malengo makuu mawili (2), Lengo la Kwanza ni ili SISI TUPATE FAIDA (TUNUFAIKE) na lengo la pili; ni ili TUTUBU.
Wengi wetu tunalijua hili lengo la Kwanza, na ndilo tunalolitafuta kwa bidii, pasipo kujua kuwa Lengo la pili ndio kuu kuliko la Kwanza, na ndilo Mungu analoliangalia kuliko yote.
Ndugu unaweza kumwomba Bwana Yesu akuponye kansa, na kwa huruma zake akakuponya, unaweza kumwomba Bwana Yesu akupandishe cheo kazini na kwa huruma zake akakufungulia mlango huo, ukapata fursa kazini, unaweza kumwomba Bwana Yesu akufungulie mlango wa riziki au kazi, au akupe uzao na kweli akakufanyia muujiza huo mkubwa ukapata uliyoyahitaji, unaweza kumwomba akufanikishe katika ndoa au masomo, na ikatokea kama ulivyomwomba..
Sasa fahamu kuwa Bwana Yesu kakufanyia muujiza huo au miujiza hiyo, lengo lake ni ili wewe uwe na furaha, na uishi maisha mazuri sawasawa na maneno yake haya..
Yohana 6: 23 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu”
Yohana 6: 23 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu”
Hilo ni lengo la kwanza la Bwana kuruhusu miujiza maishani mwako, lakini sio lengo kuu. Kwasababu unaweza kuponywa Kansa, au Ukimwi lakini bado ukaenda kwenye ziwa la Moto, unaweza kupata kazi nzuri, na kufunguliwa tumbo na kuzaa watoto wengi, lakini bado siku ile akakukana. Kwahiyo lengo kuu la miujiza ya Bwana si kutimiza furaha zetu, au mapenzi yetu. Bali lengo lake kuu ni ili sisi TUTUBU TUNAPOIONA MIUJIZA HIYO!!.
Je unakumbuka Mtume Petro kilichomtokea baada ya Bwana kumfanyia muujiza ule mkubwa wa kupata samaki wengi?..Petro hakufurahia tu kupata riziki, hakufurahia kupata fedha za kwenda kununua kiwanja cha kujenga, kwasababu ya ule wingi wa samaki, hakufurahia mikopo atakayokwenda kukopesha hapo baadaye kwasababu ya wingi wa wale samaki.. bali utaona alikimbilia toba..
Luka 5:4 “Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, ONDOKA KWANGU, KWA KUWA MIMI NI MTU MWENYE DHAMBI, BWANA.9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata”
Luka 5:4 “Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;
7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.
8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, ONDOKA KWANGU, KWA KUWA MIMI NI MTU MWENYE DHAMBI, BWANA.
9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata”
Umeona?.. Simoni hakusema hapo “ondoka kwangu Bwana kwa kuwa mimi ni mtu maskini” au kwakuwa mimi ni mtu mwenye matatizo mengi ya kiuchumi au kibiashara.. bali alisema “kwakuwa mimi ni mtu mwenye dhambi” (maana yake alitubu).. Na ndipo Bwana akamwambia tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba katika miji ile ile ambayo Petro alikutana na Bwana mara ya kwanza, yaani miji mitatu ya (Bethsaida, Kapernaumu na Korazini), Miji hii yote ilikuwa kando ya bahari ya Galilaya..Bwana Yesu alikuwa akitembea huku na huko katika miji hiyo, na kufanya miujiza kama hiyo hiyo, aliyoifanya kwa Petro.
Lakini tofauti ya Petro na watu wengine wa miji hiyo, ni kwamba Petro alitubu kwa miujiza ya Bwana, lakini wengine wengi wa miji hiyo, waliifurahia tu miujiza ya Bwana lakini hawakutubu.
Walifurahia tu watoto wao kuona wanatokwa na mapepo, lakini hawakufikiri kuacha dhambi zao, ingawa Bwana alikuwa anawahubiria toba, walifurahia kubarikiwa kazi zao na biashara zao lakini hawakufikiria kutubu, hawakufurahia kuacha ulevi wao, wala kuacha uzinzi wao, wala kuacha rushwa zao wala kuacha mambo mengine mabaya, ingawa waliifurahia miujiza ya Bwana.
Na hatimaye Bwana Yesu akawaambia maneno yafuatayo…
Mathayo 11:20 “Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo NDANI YAKE ILIFANYIKA MIUJIZA YAKE ILIYO MINGI, KWA SABABU HAIKUTUBU.21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”
Mathayo 11:20 “Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo NDANI YAKE ILIFANYIKA MIUJIZA YAKE ILIYO MINGI, KWA SABABU HAIKUTUBU.
21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.
22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.
23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”
Hapo anasema alianza kuikemea kwasababu haikutubu “si kwasababu haikushukuru baada ya kufanyiwa miujiza”, au si kwasababu waliitumia vibaya ile miujiza, kwamba baada ya kubarikiwa katika shughuli zao walitumia vibaya fedha!.. La!!.. lakini iliikemea kwasababu moja tu kwamba HAIKUTUBU!!
Na tena anasema itakuwa ni rahisi kwa Sodoma kustahimili adhabu yake siku ile ya hukumu kuliko miji hiyo, maana yake ni kwamba kumbe pamoja na kwamba watu wa Sodoma na Gomora waliadhibiwa kwa moto katika mwili, lakini kumbe kuna bado kuna adhabu nyingine inawangojea huko!! Hii inaogopesha sana..
Lakini Bwana Yesu anazidi kusema, itakuwa ni rahisi watu wa Sodoma kustahimili adhabu kuliko watu wa miji hiyo ya Korazini, na Bethsaida na Kapernaumu. Maana yake adhabu ya watu wa Kapernaumu na Korazini na Bethsaida itakuwa ni kubwa sana, katika ziwa la moto.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, Tumwogope Mungu!.. Miujiza anayotufanyia kila siku ambayo tunaiona kwa macho yetu sio kwa lengo la kutuburudisha bali ni kwa lengo la sisi Kuamini kwamba yupo na kwamba yeye hapendi UCHAFU, hivyo tutubu!, tuyatakase maisha yetu, ili tusipate hasara siku ya mwisho ya hukumu.
Ukiaona Bwana kakujibu maombi yako, ni kwasababu anataka uache usengenyaji wako, ukiona Bwana kakujibu maombi yako kimuujiza ni ujumbe kwako kwamba anataka uache kuvaa unavyovaa nguo za kubana na zisizo na heshima, anataka uache ulevi wako, na si kwamba anakusapoti na ulevi wako au uzinzi wako, au uuaji wako, amekuonyesha miujiza hiyo ili wewe ujue kwamba yeye yupo na anakutazama.
Lakini ukidharau sauti ya Mungu hiyo, ambayo inakutaka utubu, na kuifurahia miujiza tu na ishara, basi fahamu kuwa unajiwekea akiba ya hasira ya Mungu..
Warumi 2:4 “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa WEMA WA MUNGU WAKUVUTA UPATE KUTUBU?5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu”
Warumi 2:4 “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa WEMA WA MUNGU WAKUVUTA UPATE KUTUBU?
5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu”
Mpokee Yesu leo na tubu kwa kudhamiria kuacha dhambi na kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu, na Bwana atakukubali na kukupatia kipawa cha Roho wake mtakatifu.
NAYE ALIKUWA HANA BUDI KUPITA KATIKATI YA SAMARIA.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
MIUJIZA YA KRISTO, HAITEGEMEI KANUNI ZA KIBINADAMU.
Furaha ni nini?