Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu Yesu Kristo, utukufu na heshima vina yeye milele na milele.AMEN. Nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya Mungu, na leo tutaona vile uaminifu unavyomshawishi Mungu, kukupa neema Zaidi ya unachokiomba.
Tumekuwa na maombi mengi sana mbele za Mungu, wakati mwingine tunatamani Mungu atutumie kama Fulani katika biblia, Lakini tusipojua kanuni za Ki-Mungu, kamwe hatutakaa tuvipate, haijalishi tutakuwa ni waombaji au wafungaji wazuri namna gani mbele za Mungu.
Mungu kumfanya Musa, kuwa Mchungaji wa taifa la Israeli, haikuwa ni kwasababu ni mwisraeli tu au anaomba sana. Hapana, ni kwasababu ya maamuzi aliyoyafanya zamani, ambayo yalimponza hata kuwa vile kama alivyokuwa kwa miaka 40. Musa aliona kustarehe katika jumba la kifalme, si kitu, moyo wake ukaanza kuugua juu ya ndugu zake waebrania aliokuwa anaona wanateswa, hivyo siku moja alipoona mmojawapo anaonewa na Mmisri, alikuwa radhi kumtetea ndugu yake, mpaka kumuua yule mmisri, kuonyesha kuwa aliwapenda waebrania kwelikweli, Hata siku ya pili yake, alipoona hao hao waebrania wanagombana, hakuwaacha hivi hivi tu, bali alikwenda kutafuta namna ya kuwapatanisha ili wawe na umoja. Lakini yule aliyemtapeli mwenzake, akamwambia unataka kuniua kama ulivyomuua yule mmisri jana.
Musa angeweza kukana hayo mashtaka hata kwa rushwa kwasababu alikuwa na uwezo huo.. Lakini kinyume chake, akawa tayari, kukubali mashutumu, kwamba yeye ndiye aliyefanya vile, akakimbia akaenda zake jangwani, huku moyo wake ukiugua tu kwa ajili ya ndugu zake. Utaona japokuwa hakujua njia sahihi ya kuwaokoa ndugu zake, lakini alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake, kufanya awezacho.(Matendo 7:22-40)
Huyo ndio mtu ambaye baada ya miaka 40, Mungu anamtokea katika kijiti cha moto, akimwambia, nakutuma uenda Misri ukawaokoe watu wangu kwa mkono mkuu. Ndipo Mungu akamtumia kwa uwezo mkubwa namna ile, kwasababu aliona uaminifu wake, katika kile alichokitamani.
Matendo 7:35 “Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti. 36 Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini”.
Matendo 7:35 “Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti.
36 Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini”.
Ukitamani kuwa mchungaji, onyesha tabia hizo tangu sasa kabla hujawa mchungaji wa kanisa la Kristo, ili Bwana ashawishwe, kukupa huduma hiyo, je, unalipenda kundi la Mungu, je unalithamini? , je upo tayari kuwalisha watu chakula cha kiroho, na kusimama nao katika shida zao, bila kuruhusu ibilisi awameze?
Hilo ni jambo la muhimu sana, kulifanya sasa ndugu..
Daudi kabla hajafanywa na Mungu kuwa mchungaji wa Israeli, aliwahi kuwa mchungaji wa kondoo na mbuzi, lakini alipoona adui wanataka kuja kulishambulia kundi, hakuliacha na kukimbia, bali aliweza kupambana na simba, Pamoja na dubu na kuwashinda, akiwa na fimbo tu. Mungu akamuona kuwa huyu anafaa hata kwa watu wangu Israeli kwasababu anathamini, kundi analoliongoza, hata kuwa tayari kuyahatarisha Maisha yake, kwa ajili ya hili..(1Samweli 17:34-36)
Umeona, Bwana Yesu alisema..
Luka 16:10 “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia”.
Je ni sisi tuitwao wachungaji/Waalimu, wainjilisti, tunazo tabia hizi?
Wapo watu wengine wanasema, Bwana naomba unipe mali nyingi kama Sulemani, ili nizitumie kuisogeza injili yako mbele. Kumbuka, kabla Mungu hajakupa, atahitaji kwanza, aone ulichonacho unakitoaje? Umebarikiwa laki moja, Je!, ulishawahi kuwa radhi kutoa vyote, au sehemu kubwa ya mali zako kwa Mungu mara nyingi, hata kuwa tayari kulala njaa, au kukosa mahitaji yako, kwa Mungu?
Ikiwa hivyo hufanyi, unaishia tu kuomba, jua kuwa utajiri huo unaouhitaji, kamwe hutaweza kuupata.
Mtume Paulo, alilijua hilo, ndio maana akawa mwaminifu sana katika kumtumikia Mungu, katika udogo, ndipo Mungu akamfanya kuwa mtume na Mwalimu wa mataifa.
1Timotheo 1:12 “Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;”
Hivyo ndugu, chochote, ukitamanicho kwa Mungu, waweza kukupata, lakini, anza sasa, kujitoa kwa hicho, kuwa tayari kuiponza roho yako, hata wakati mwingine kupoteza kila kitu, kwa ajili ya utumishi huo, na hakika yake utakipata kwa Mungu.
Uaminifu wako sasa ni mtaji wa ukitakacho kesho.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
JE UNATAMANI KUMJUA MUNGU, NA HUJUI PA KUANZIA?
THAWABU YA UAMINIFU.
Gongo na Fimbo ni nini?
Unyenyekevu ni nini?
NIFANYE NINI ILI NIPENDWE NA MUNGU?
Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?
Rudi nyumbani
Print this post
Jibu: Tusome,
Isaya 45:3 “nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli”.
Hazina za gizani ni baraka zote zilizoshikiliwa na adui shetani ambazo zingepaswa ziwe zetu.
Hazina hizi zinakuwa zinashikiliwa na adui kwa kitambo tu, na pale tunapotia bidii basi tunaweza kuzitwaa na kuzirejesha kwetu.
Mfano wa hazina za gizani ni zile wana wa Israeli walizozipata kutoka katika jeshi la Washami.
Wakati ule ambao Israeli walikuwa wana njaa kali, hata kufikia hatua watu kula mavi ya njiwa, na kichwa cha punda…na wakati huo huo mji wote ulikuwa umezungukwa na jeshi la Washami pande zote.
na Mungu akayasikilizisha majeshi ya washami mishindo ya farasi, na kwa hofu kubwa wakaacha vyakula vyao vyote na kukimbia kutoka katika zile kambi zao walizokuwepo, na wana wa Israeli wakaenda kuzitwaa zile Nyara na vile vyakula.. Hivyo wakawa wamepewa na Bwana hazina zilizikuwepo gizani.
2 Wafalme 7:5 “Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. 7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. 8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. 9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. 10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. 11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme. 12 Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini. 13 Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone. 14 Basi wakatwaa magari mawili na farasi zake; mfalme akawatuma kuwafuata Washami, akasema, Enendeni, mkaangalie. 15 Wakawafuata mpaka Yordani; na kumbe! Njia yote ilikuwa imejaa mavazi na vyombo, walivyovitupa Washami, wapate kukimbia upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi, wakamwambia mfalme. 16 Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la BWANA”.
2 Wafalme 7:5 “Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu.
6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.
7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao.
8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme.
10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.
12 Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini.
13 Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone.
14 Basi wakatwaa magari mawili na farasi zake; mfalme akawatuma kuwafuata Washami, akasema, Enendeni, mkaangalie.
15 Wakawafuata mpaka Yordani; na kumbe! Njia yote ilikuwa imejaa mavazi na vyombo, walivyovitupa Washami, wapate kukimbia upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi, wakamwambia mfalme.
16 Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la BWANA”.
Sasa huo ni mfano wa hazina ambazo zilikuwa gizani (yaani zimeshikiliwa na adui), lakini baadaye zikaondolewa kutoka kwa adui na kupewa watu wa Mungu. Na hata sasa zipo hazina nyingi ambazo zipo gizani, ambazo zinapaswa ziwe za kwetu..Adui kazishikilia, na sisi tusipopiga hatua kwenye kuteka nyara basi adui ataendelelea kuzimiliki na sisi tutaendelea kutateseka.
Na hazina zenyewe zinaweza kuwa ni WATU au VITU. Kuna watu wetu wengi leo ambao wameshikwa na adui vile vile kuna vitu vyetu vingi ambavyo vimeshikwa na adui, ambavyo tukiwa imara katika Imani tunaweza kuvitwaa na kuviteka. Maandiko yanasema..
2 Wakorintho 10:4 “maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; NA TUKITEKA NYARA KILA FIKRA IPATE KUMTII KRISTO”.
2 Wakorintho 10:4 “maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; NA TUKITEKA NYARA KILA FIKRA IPATE KUMTII KRISTO”.
Maana yake tukivaa silaha hizo za Mungu, basi tutakuwa na uwezo wa kuziteka hazina zote za gizani…kama ni watu wetu wapo gizani, basi tunaweza kuwatoa huko, kama ni vitu vyetu vipo gizani, basi tunaweza kuvirejesha endapo tukivaa silaha hizo na kuingia vitani.
Sasa swali ni je!. Hizo silaha za kwenda kuteka nyara hazina za gizani ni zipi? Si nyingine zaidi ya zile silaha 7 tunazozisoma katika kitabu cha Waefeso 6:10-18, ambazo ni WOKOVU, KWELI, HAKI, IMANI, UTAYARI,NENO, na MAOMBI.
Ni kupitia silaha hizo tu, ndio tunaweza kuzipata hazina za gizani na mali zilizofichwa sawasawa na hiyo Isaya 45:3.
Maran atha!
Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi
TUZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA.
Je Mkristo kutembea na walinzi (Bodyguards),ni sawa?
Kwanini Mungu aseme, Alaaniwe azuiaye upanga wake usimwage damu (Yeremia 48:10).
Deraya ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 59:17
DOWNLOAD PDF
WhatsApp
Kikawaida ulafi ni tabia ya kupenda kula kuliko pitiliza, Sio vibaya kula, na pia sio dhambi kula na kushiba..
Lakini tabia hii inapovuka mipaka kiasi kwamba kila kitu kinachokuja mbele ya macho yetu ni kutamani kukila kama vile wanyama..(huo ni ulafi).
Biblia imetaja tabia hii kuwa haitokani na Roho Mtakatifu Kwasaababu matunda ya tabia hiyo ni mabaya.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ULAFI, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ULAFI, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Mtu mlafi atatoa chochote ili ale au anywe, hata kama ameshiba, atatafuta kila njia ili aliridhishe tumbo lake kwa chochote atakachokitamani, anaweza hata kuiba, au kudhulumu, au kufanya jambo lolote lisilo la kiMungu ilimradi tu, apate chakula anachokihitaji.
Anaweza kuhudhuria karamu yoyote atakayoalikwa hata kama hiyo karamu ni ya mashetani..lengo lake ni ili ale na kunywa tu!.
Mtu mlafi ni rahisi kuingia katika mtego wowote wa ibilisi, Esau aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa chakula,
Waebrania 12:16 “Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya CHAKUKA KIMOJA”.
Hebu tuangalie hekima moja ya Sulemani aliyoiandika kuhusiana na ulafi na madhara yake.
Mithali 23:1 “Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako. 2 Tena ujitie kisu kooni, KAMA UKIWA MLAFI. 3 Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila…… 6 Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa; 7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. ATAKUAMBIA HAYA, KULA, KUNYWA; LAKINI MOYO WAKE HAUWI PAMOJA NAWE. 8 Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.”
Mithali 23:1 “Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.
2 Tena ujitie kisu kooni, KAMA UKIWA MLAFI.
3 Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila……
6 Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;
7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. ATAKUAMBIA HAYA, KULA, KUNYWA; LAKINI MOYO WAKE HAUWI PAMOJA NAWE.
8 Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.”
Umeona?..wanawake wengi na mabinti wanaingia katika mtego wa dhambi ya uasherati kutokana na ulafi (wanatamani kila aina ya chakula wanachokiona), na shetani anakitumia hicho kuwakamata.
Wengine wanaingia katika mitego ya kula rushwa kwasababu ya Ulafi, wengine wanaingia katika mitego ya kuua, au kudhulumu kwasababu ya Ulafi.
Na hata wengine wanaingia katika umaskini kwasababu ya ulafi (biblia inasema hivyo katika Mithali 23:20-21), Kwasababu muda wote mtu huyo anakuwa anafikiria kula tu, na hafikiri vitu vingine.
Na mojawapo ya dalili za siku za mwisho, biblia imetabiri ni watu kuwa WALAFI (watu watakuwa wakila na kunywa).
Luka 17:26 “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. 27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote”.
Luka 17:26 “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.
27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote”.
Hivyo hatuna budi kuwa na kiasi na kujihadhari na ulafi.
Luka 21:34 “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ULAFI, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
Luka 21:34 “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ULAFI, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
Na pia tabia ya ULAFI, siku zote inaenda kinyume na MFUNGO.
Mtu aliye mlafi, huwa hapendi wala hawezi kufunga na hivyo anakuwa pia anakosa baraka nyingi za kiroho kwasababu maandiko yanasema “mambo mengine hayatoki isipokuwa kwa kufunga na kuomba(Mathayo 17:21)”.
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba tunapookoka hatuna budi kuacha na ULAFI pia!, Kwasababu tabia hiyo haitokani na Roho Mtakatifu.
1 Petro 4:3 “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na KARAMU ZA ULAFI, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali.
Bwana atubariki.
Je! Mbinguni Kutakuwa na kula na kunywa?.
Je tunaruhusiwa kutumia vidonge wakati wa kufunga?
Nini maana ya “chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu”?
Katika Mathayo 15:21-28, Yesu alikuwa na maana gani alipomwambia huyu Mama kwamba chakula cha watoto hawapewi mbwa?
CHAKULA CHA ROHONI.
SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya huu mstari,
Mithali 16:2 “Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu”.
JIBU: Kama vile Biblia inavyosema moyo huwa mdanganyifu kuliko kitu kingine chochote, (Yeremia 17:9), ikiwa na maana ni kawaida ya mwanadamu, kuziona njia zake zote alizozichagua ni sawa mbele zake, ni mara chache sana, kusikia mtu anakiri kuwa uamuzi anaoufanya ni wa kishetani,
Nimekutana na waganga wa kienyeji wanasema kitu tunachokifanya ni sawa, hakina madhara yoyote, ukienda kwa waabudu sanamu, watakuambia vivyo hivyo hizi ni ishara tu, tunaabudu Mungu yuleyule, Ukienda kwa wauza pombe watakuambia nao maneno hayo hayo n.k… Kwasababu biblia inasema njia “ZOTE” (sio moja) za mtu ni safi machoni pake mwenyewe.
Lakini Bwana huzipima roho za watu. Ikiwa na maana, Mungu anazichunguza nia zetu. Yeye hashawishwi na kile tunachokiona ni sawa, kwa macho yetu, au kwa mitazamo yetu, bali anatazama ndani Zaidi ya mwanadamu, anaweka kwenye mizani, anatazama nia, ya mtu ilikuwa ni nini, na matokeo yake yatakuwa ni nini mwishoni..
Kwamfano Mafarisayo na Masadukayo, walijihesabia haki, kwa mapokeo yao, wakijiona kuwa ni watakatifu, na bora kuliko wengine, lakini Bwana Yesu aliwaita wanafki. Kwasababu, kazi yao ilikuwa ni kusafisha kikombe kwa nje tu, lakini ndani ni kuchafu, wanafunga ili waonekane na watu, wanaomba ili waonekane ni wazuri katika mambo hayo. Walikuwa wanajifanya kumwita Yesu Rabi, lakini ndani wamejaa wivu. (Mathayo 23:1-39)
Hivyo nasi twapasa tulijue hilo, ili tusidanganyike.
Kitabu cha 1Wakorintho 13, inasema nijaposema kwa lugha za wanadamu na Malaika, nijapoutoa mwili wangu uungue moto, nijapotoa mali zangu zote niwape maskini, nijapokuwa na unabii, na Imani timilifu ya kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo mimi si kitu, ni sawa na bure tu.
Waweza kuwa mhubiri mzuri, mkubwa, unaokoa roho za watu, nawe ukaona njia hiyo ndiyo inayompendeza Mungu zaidi, lakini ndani yako unahubiri kwasababu ya fitina, kama inavyosema Wafilipi 1:15, au upate umaarufu, au upate fedha,.ujue unachokifanya ni bure.
Hivyo, katika lolote tulifanyalo, ili liwe na faida njema nyuma yake, lazima tujue nia yetu ya dhati kufanya hivyo ni nini, Ndicho Bwana anachokitazama sana, kuliko, hichi cha nje tukionyeshacho.
Kulikuwapo na wale watu, waliokataa, kwenda harusini walipoalikwa, na ukitazama kibinadamu sababu za wao kutokwenda zina mashiko kabisa, mwingine anasema ninaoa, hivyo ni sharti niwe na mke wangu kwa kipindi hiki, lakini Bwana Yesu aliona kama ni UDHURU wanatoa wote, kwasababu yeye ndio anayechunguza mioyo, akaona kutoa kwao udhuru ni kwasababu hawakuthamini wito wake tangu mwanzo.
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, 17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. 18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. 19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. 21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. 22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. 23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. 24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,
17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.
20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.
23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.
24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.
Hivyo na sisi tusitoe udhuru katika mambo ya ki-Mungu, unapoitwa uokoke, hata kama unazo sababu elfu za kutokuacha hicho unachokifanya ikiwa Mungu anataka ukiache, tii tu. Kwasababu hatuwezi kumshawishi Mungu kwa mitazamo yetu tu, kwa vile tuonavyo sisi kuwa ni bora, au vafaa Zaidi kwasasa, naye akashawishika, bali anaelewa kila kitu, na matokeo ya vyote mwishoni utakuwaje..
Hatuna budi, kumtii Mungu.
Bwana akubariki.
UTAYAFIKIAJE MANENO SAFI YA MUNGU?
Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?
KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,
AKETIYE MAHALI PA SIRI PAKE ALIYE JUU.
NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.
VIACHENI VYOTE VIKUE HATA WAKATI WA MAVUNO.
MWENGE WAKO WA UHURU UPO WAPI?
Biblia inasema..
1 Wakorintho 2:10-12
[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. [11]Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. [12]LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA, BALI ROHO ATOKAYE KWA MUNGU,makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
[11]Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
[12]LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA, BALI ROHO ATOKAYE KWA MUNGU,makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
Zipo Roho mbili tu huku duniani.
Roho wa Mungu, na roho ya dunia. Kama mtu usipoipokea Roho ya Mungu, basi utaipokea roho ya dunia.
Hakuna mwanadamu anayejiongoza yeye mwenyewe hapa duniani kwa roho yake tu. Hilo halipo.
Sasa kama jinsi hayo maandiko yanavyotuambia Roho wa Mungu huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu.. Maana yake ni kuwa yeye ndiye anayetufunulia siri za ufalme wa mbinguni, pamoja mambo ambayo Mungu anataka sisi tuyafanye tukiwa hapa duniani..ukisoma Yohana 16:13 inasema
[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Umeona hiyo ndio kazi ya Roho wa Mungu..ndio maana mtu aliyepokea kweli Roho Mtakatifu hawezi ishi kidunia kwasababu ni roho nyingine kutoka mbinguni kwa baba ipo yake ikimfundisha kuishi kulingana na misingi ya Mungu.
Lakini kinyume chake ni kweli. Watu wote ambao hawana Roho wa Mungu, wanayo roho ya dunia
Na yenyewe inachunguza mambo ya ulimwengu huu na kuwafundisha watu kuishi kiulimwengu. Ndio maana hushangai kuona tabia nyingi mbaya kila siku zikivumbiliwa lengo tu ni kuwafanya kuwa wakidunia.
Ukiona mwanamke unapenda fashion, vimini, kujichubua, unavaa suruali, unaweka mak-eups, kijana unavaa milegezo, unanyoa viduku, unakunywa pombe, unacheza kamari, unasikiliza nyimbo za kidunia, unakwenda disco, unafanya ushirikina, unazini, unakula rushwa, unaiba, unapenda fedha, unadanganya ni uthibitisho kuwa roho ya dunia imekuvaa ndio maana inakuhimiza na kukufundisha kufanya hayo mambo kwa bidii.
Na mwenye roho hii ni shetani mwenyewe..Na kama ikitokea Bwana Yesu amerudi leo..basi ujue utabaki hapa duniani. Kwasababu roho yako ni ya hapa hapa na ka ikitokea umekufa basi utaenda moja kwa moja kuzimu kwasababu huko ndiko hatma ya roho hiyo itakapoishia..
Biblia ipo wazi kabisa inasema..
Warumi 8:9
[9]Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. LAKINI MTU AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA ROHO WA KRISTO, HUYO SI WAKE.
Ukikosa Roho wa Mungu, mbinguni huendi. Huu si wakati wa kumvumilia zaidi shetani, au kuwa rafiki wa dunia. Tunapojichanganya na mambo yake ndipo tunapovaliwa na roho hii chafu. Jiponye nafsi yako, ndugu, hizi ni siku za mwisho.
1 Yohana 2:15
[15]Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Hivyo ndugu, njia pekee ya kuipokea Roho ya Mungu ambayo itakusaidia na kukufundisha kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Ni kutubu kwa kumaanisha kabisa kugeuka na kuuacha ulimwengu..kisha ukishafanya hivyo unakuwa tayari kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo ikiwa kama haukubatizwa hapo mwanzo.
Baada ya huo wakati ni kuanza kuonyesha bidii ya kujifunza biblia, kuomba, kuzingatia fellowship zitakazokusaidia kukua kiroho. Na Roho wa Mungu akishaona umemaanisha hivyo, atashuka juu yako na kukutia Muhuri, na kukusaidia kuishi maisha ya wokovu.
Huku ukingojea siku yako ifike uende mbinguni, Roho hiyo ilipo.
Ikiwa utahitaji msaada ya kupokea wokovu, àu ubatizo sahihi.Basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi
+255693036618/ +255789001312
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizo
MFALME ANAKUJA
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.
Kusubu ni nini? Miungu ya kusubu ni ipi?
Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?
TUKIO LA MUSA NA ELIYA KUMTOKEA BWANA, LIMEBEBA UJUMBE GANI?
Nyakati za kuburudishwa ni kile kipindi cha utawala wa miaka elfu moja.
Kipindi hicho ni kipindi ambacho dunia itarejeshwa na kuwa kuwa nzuri zaidi hata ya Edeni, ni kipindi ambacho tutatawala na Kristo kama wafalme baada ya kuonekana wadhaifu nyakati nyingi, ni kipindi ambacho tutaishi kama malaika wasioumwa wala wasiozeeka wala kufa.
Hicho kitakuwa ni kipindi cha kufutwa machozi kwa wateule, na kipindi cha kutawala pamoja na Kristo (kwa ufupi kitakuwa ni kipindi cha kuburudika).
Matendo 3:18 “Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo. 19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, ZIPATE KUJA NYAKATI ZA KUBURUDISHWA; 20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; 21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu”.
Matendo 3:18 “Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.
19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, ZIPATE KUJA NYAKATI ZA KUBURUDISHWA;
20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani;
21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu”.
Umeona?..Kristo sasahivi yupo juu mbinguni, lakini atakuja tena kutoka huko aje aifanye dunia kuwa kama Edeni na hata zaidi ya pale, na kuwaburudisha wato wote waliojikana nafsi sasa, wanaochekwa sasa kwaajili ya jina lake, walioua kuacha uzinzi, ulevi, uvaaji mbaya, utukanaji n.k kwaajili ya jina lake.
Na nyakati hizo zimekaribia sana, kinachosubiriwa ni kondoo wa mwisho kuingia ndani ya zizi, ili majira hayo yaanze.
Lakini swali jepesi ni je!.. Umempokea Yesu leo?..je utakuwepo katika hiyo miaka ya kuburudishwa au utakuwepo katikamahali pa mateso majira hayo yatakapoanza?.
Ni heri ukatubu leo, na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu kama bado hujatubu wala kubatizwa ubatizo sahihi wala kupokea Roho.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Nini maana ya Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu;?
Nini maana ya Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu&?
NJIA MOJAWAPO YA KUPATA MSAADA KUTOKA KWA BWANA.
Rudi nyumbani:
Kusubu kibiblia ni kitendo cha kuyeyusha dhahabu au fedha au ‘kito’ chochote kwa lengo la kuunda kitu kingine kipya.
Neno hilo utalisoma sehemu nyingi katika biblia kwa mfano hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana nalo;
Mambo ya Walawi 19:4
[4]Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Maana yake msaifanye sanamu za kuyeyusha,
Kumbukumbu la Torati 27:15
[15]Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.
Soma pia..
2Nyakati 24:4, 28:2, Waamuzi 17:3, Hesabu 33:52, 1Wafalme 7:23.
Maana yake ni ipi kiroho?
Hata sasa watu wengi, wanajiundia sanamu zao za kusubu rohoni bila wao kujijua…kwa kugeuza maumbile ya vitu vyema na kuvitumia isivyopasa..mpaka kuviabudu.
Kwa mfano fedha si mbaya lakini leo hii watu wameigeuza fedha kuwa mungu wao..kiasi kwamba kwao Mungu si kitu zaidi ya fedha, maisha yao yote ni kuhangaikia mali, kana kwamba hiyo ndio itakayowafikisha mbinguni, kaacha kumtumikia Mungu, hata muda na ibada hana, dai lake ni “Natafuta pesa’’ Sasa hizo ndio sanamu za kusubu..
Wengine biashara kwao zimeshageuka na kuwa sanamu za kusubu, wengine wanadamu., wengine muvi, wengine magemu, wengine mipira.
Tunapaswa tujilinde sana kwasababu sanamu za namna hii zinamtia Mungu WIVU, na wivu ni mbaya kuliko ghadhabu..
Ni heri Mungu akukasirikie kwa makosa mengine kuliko kwa kukuonea wivu.
kwasababu adhabu ya wivu ni mbaya sana kuliko ya hasira..
Mithali 27:4
[4]Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika;
Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
Tujilinde mioyo yetu na ibada za sanamu. Mungu hakuwahurumia wana wa Israeli walipotengeneza ndama ya kusubu na kuiabudu kule jangwani. Japokuwa yeye ndiye aliyewaokoa kwa mkono hodari.
Vivyo hivyo na wewe ukisema umeokoka, epuka kugeuza kitu chochote kuwa Mungu wako. Usiruhusu kamwe chochote kuchukua sehemu ya Mungu yako.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)
Shetri ni nini kama tunavyosoma katika Marko 3:38?
Kuvyaza ni nini katika biblia? (Ayubu 21:10).
Zeri ya Gileadi ni nini?
Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
Haya ni maswali 8 maarufu yahusuyo Zaka.
1. Ni nani anayepaswa kutoa fungu la 10?,
2. Je fungu la 10 tunatoa katika faida au mtaji?
3. Je tunapopewa zawadi tunazitolea fungu la 10?,
4. Je fedha ya mkopo inatolewa fungu la 10?.
5. Je Kama mshahara wangu ni milioni moja lakini kutokana na makato ya serikali kama kodi, na pspf, najikuta napokea sh.laki 7 tu, je zaka natoa kutoka katika hiyo laki 7 au kutoka katika ile milioni.?
6. Je kama nimepokea mshahara ambao haupo katika mfumo wa kifedha, mfano napewa ng’ombe au kuku, namtoleaje zaka huyo?
7. Je!. Tunaweza kuweka deni la fungu la 10? Yaani badala ya kutoa.kila.siku, tukakusanya na hatimaye tukaja kulipa mwisho wa mwezi au mwaka?
8. Je! Fungu la 10 linapaswa lipelekwe wapi kimaandiko?.Na je kuna ulazima wowote wa kulipa zaka?
Tukianza na swali la kwanza.
1. Ni nani anayepaswa kutoa fungu la 10?(Zaka).
Jibu: Kila mtu aliyeokoka ana wajibu wa kutoa fungu la 10. Haijalishi umri wake, jinsia yake?, au hali yake ya kiuchumi.
Maana yake kama unafanya kazi ya mikono au haufanyi, ni lazima kutoa fungu la 10 (yaani kulipa zaka).
2. Fungu la 10 tunatoa katika faida au mtaji?
Fungu la 10 linatolewa katika faida na si mtaji. Mfano una mtaji wa laki moja, na kazi unayoifanya imakupa faida kwa siku sh. Elfu kumi. Hapo zaka utatoa kutoka katika hiyo faida uliyoipata na si. Kutoka katika mtaji ulionao (maana yake kiasi cha zaka unachopaswa utoe hapo kwa siku ni sh. Elfu moja).
3. Je tunapopewa zawadi tunazitolea fungu la 10?
Kama zawadi hiyo uliyopewa utaifanya kuwa mtaji, basi hutaitolea zaka, lakini utatoa katika faida huo mtaji utakayoizalisha. Lakini kama zawadi hiyo matumizi yake ni kama ya mshahara wa kawaida..yaani katika kujihudumia kwa chakula, makazi au malazi, basi utaitolea zaka.
Na vile vile kama hufanyi kazi yoyote, au bado hujapata kazi, chochote kitakachofika mkononi mwako kwaajili ya mahitaji yako, hicho utakitolea zaka.
4. Je fedha ya mkopo, tunaitolea zaka?
Kama mkopo uliochukua ni kwa lengo la mtaji wa biashara, hupaswi kuutolea zaka, bali utatoa zaka katika faida utakayoipata kutoka katika mkopo huo.
Lakini kama mkopo ulioupokea ni kwa lengo la kujihudumia kimaisha kama chakula, mavazi au malazi (Huo ni kama mshahara, hivyo unapaswa uutolee zaka).
5. Kama mshahara wangu ni milioni moja lakini kutokana na makato ya serikali kama kodi, na pspf, najikuta napokea sh.laki 7 tu, je zaka natoa kutoka katika hiyo laki 7 au kutoka katika ile milioni moja.?
Jibu: Zaka utatoa kutoka katika hiyo milioni moja na si kutoka katika hiyo laki 7, maana yake kiasi cha zaka hapo kitakuwa ni sh. Laki moja kila mwezi.
6. Je kama nimepokea mshahara/Zawadi ambayo haupo katika mfumo wa kifedha, mfano napewa ng’ombe au kuku, namtoleaje zaka huyo?
Jibu: Kama ng’ombe huyo utamfanya kuwa mtaji, hautamtolea zaka, isipokuwa faida utakazozipata kutoka katika shughuli hiyo, utaitolea zaka (maana yake kama utafanya biashara ya kuuza maziwa, faida utakayoipa kupitia maziwa hayo, utalipa zaka).
Lakini kama utamtumia kwaajili ya kitoweo, hapo huna budi kutafuta thamani ya ngombe huyo na kutoa sehemu ya 10, maana yake kama ng’ombe ana thamani ya milioni moja basi utatoa laki moja kama zaka, au kama hutaweza kupata thamani hiyo, basi utaitoa sehemu ya 10 ya nyama kama zaka.
7. Je!. Tunaweza kuweka deni la fungu la 10? Yaani badala ya kutoa kila siku, tukakusanya na hatimaye tukaja kulipa mwisho wa mwezi au mwaka mwaka?
Jibu: Ndio! Lakini kama kuna ulazima wa kufanya hivyo. Mfano unaweza ukawa unapata faida ndogo, ambayo mahesabu ya zaka yake yanakuwa ni chini ya sh.50, sasa huwezi kutoa sh 40 au 20 au 10 kama zaka kila siku, kwasababu hata matumizi ya hizo sarafu hayapo!.Kwahiyo suluhisho ni kufanya mahesabu ya kiasi kinachopatikana kwa wiki au mwezi, na kulipa kwa pamoja.
Vile vile hakuna ratiba maalumu ya kimaandiko ya wakati wa kulipa zaka..maana yake kama mtu atachagua kulipa kila mwisho wa wiki, hafanyi dhambi, mwingine kila mwisho wa mwezi hakosei, mwingine kila mwisho wa miezi mitatu pia afanyi makosa, ilimradi analipa kiasi chote kwa uaminifu. (Lakini ni vizuri zaidi kulipa mapema, ili kuzuia mlundikano wa madeni..lakini kila mtu anao ustaarabu wake, ambao yeye anauwezo wa kuumudu).
8. Je fungu la 10 linapaswa lipelekwe wapi?..kwa mayatima, kanisani, kwa mtumishi wa Mungu au wapi?.
Ili kupata kupata jibu la swali hili kwa urefu unaweza kufungua hapa >>>> NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
JE! KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KULIPA ZAKA?
Kwanini Mungu anajifanya kama hajui mambo?
KITABU CHA UKUMBUSHO
Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.
ZIKUMBUKE FADHILI ZA MUNGU
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
Je! Ni thawabu gani inayozungumziwa hapo?.
Jibu: Ili tuelewe vizuri, labda tuanzie kusoma kuanzia mstari wa 40
Mathayo 10:40 “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. 41 Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki”
Mathayo 10:40 “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.
41 Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki”
Sasa swali, ni thawabu gani inayozungumziwa hapo?..Jibu la swali hili tutalipata katika mstari unaofuata wa 42
Mathayo 10:42 “Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, HAITAMPOTEA KAMWE THAWABU YAKE”.
Kumbe thawabu inayozungumziwa hapo ni THAWABU KUTOKA KWA MUNGU kwa jinsi sisi tunavyowakaribisha watumishi wake!. Yaani kiwango utakachompimia Mtu wa Mungu,(yaani kumbariki) na jinsi utakavyomchukulia, ndicho na Mungu pia atakachokupimia wewe!..
Kama umempokea Mtumishi wa Mungu, kama mtu wa heshima sana, na ukambariki sana.. Ndivyo Mungu na yeye atakavyokuchukulia wewe kama mtu wa Heshima sana, na mwenye kustahili thawabu nyingi.
Lakini kama umempokea kama mtu wa kawaida, kwamba ni mtu mzuri tu!..basi na Mungu naye atakuchukulia wewe kama mtu mzuri tu, na kukupa thawabu kama hiyo hiyo uliyompimia huyo mtu wa Mungu.. Na kama umemlaani mtumishi wa Mungu, na Mungu naye atakulaani.
Bwana Yesu sehemu nyingine alisema maneno haya..
Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, NDICHO WATU WATAKACHOWAPA VIFUANI MWENU. KWA KUWA KIPIMO KILE KILE MPIMACHO NDICHO MTAKACHOPIMIWA”.
Unaona hapo?..anamalizia hapo kwa kusema, KIPIMO MPIMACHO NDICHO MTAKACHOPIMIWA!!..
Mfano wa Mwanamke aliyepata thawabu ya Nabii ni yule mwanamke wa Sarepta aliyemkaribisha Nabii Eliya na kumpikia chakula, ale..kwakuwa alimpokea yule kama Nabii na kumpa chakula, kama mtu wa heshima sana, Mungu naye akampa heshima kwa kulizidisha pipa lake la unga siku zote wakati Israeli yote ina njaa. (1Wafalme 17:9-16)
Kwahiyo na sisi tujitahidi siku zote kupima kipimo kizuri kwa watu wote, hususani walio watumishi wa Mungu, ili na sisi tupimiwe kipimo kilicho kikubwa na Mungu
Bwana atajalie tuwe miongoni mwa watu wa kubariki, ili na sisi tubarikiwe.
Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”
Nitamjuaje nabii wa Uongo?
Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
Kuna majira yakupasa uisikie sauti ya Mungu, kuliko hasara utakayoingia, ili kuiponya nafsi yako.
Kuna mfalme mmoja wa Yuda anaitwa Amazia, Huyu mfalme siku moja alijikuta anaingia katika vita na maadui zake (Waedomi), Hivyo alichokifanya ni kupanga vikosi vya wanajeshi yake, ili kwenda kushindana nao. Lakini bado aliona majeshi yake hayatoshi, hivyo akaenda kwa ndugu zake, waliokuwa upande wa Israeli, ili awaajiri wanajeshi wao kwa fedha nyingi sana..
Hivyo akawaajiri wanajeshi takribani Laki moja (100,000).
Lakini tunaona alipokuwa anakaribia kwenda vitani, nabii wa Mungu alimfuata, akamwambia, achana na hao askari uliowaajiri, kwasababu mimi sipo nao..Nenda mwenyewe na jeshi lako vitani.
Likawa ni jambo gumu kwake, kwasababu tayari anapunguza nguvu, na kama hiyo haitoshi, tayari alishalipa fedha nyingi sana kwa ajili ya majeshi hayo..Amewekeza fedha zake nyingi katika vita na haziwezi kurudishwa.
Lakini kwasababu Amazia alikuwa anamcha Mungu, alitii sauti ya Mungu, akawa tayari kuipokea hasara, hiyo. Akaenda vitani na jeshi lake dhaifu, na Bwana akamsaidia kushinda, tena kwa ushindi mnono.
2Nyakati 25:6 “Akaajiri pia watu mashujaa mia elfu wa Israeli kwa talanta mia za fedha. 7 Lakini mtu wa Mungu akamjia, akasema, Ee mfalme, usiwaache jeshi la Israeli waende nawe; kwa kuwa Bwana hayupo pamoja na Israeli, yaani, wana wote wa Efraimu. 8 Lakini ukitaka kwenda, haya, jitie nguvu upigane; Mungu atakuangusha mbele ya adui; maana MUNGU ANAZO NGUVU ZA KUSAIDIA, NA KUANGUSHA. 9 Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia nilizowapa jeshi la Israeli? MTU WA MUNGU AKAJIBU, BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO”.
2Nyakati 25:6 “Akaajiri pia watu mashujaa mia elfu wa Israeli kwa talanta mia za fedha.
7 Lakini mtu wa Mungu akamjia, akasema, Ee mfalme, usiwaache jeshi la Israeli waende nawe; kwa kuwa Bwana hayupo pamoja na Israeli, yaani, wana wote wa Efraimu.
8 Lakini ukitaka kwenda, haya, jitie nguvu upigane; Mungu atakuangusha mbele ya adui; maana MUNGU ANAZO NGUVU ZA KUSAIDIA, NA KUANGUSHA.
9 Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia nilizowapa jeshi la Israeli? MTU WA MUNGU AKAJIBU, BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO”.
Ni mara ngapi, watu wengi wanashindwa kumfuata Yesu, kisa hasara watakazoingia kwa uamuzi huo?
Niliwahi kuzungumza na mtu mmoja, anasema anampenda Mungu kweli, lakini anamiliki bar tena sio moja bali kadha wa kadha, na anasema ndipo anapopatia rizki. Nikamwambia hana budi kuacha biashara hiyo, kwasababu Mungu anaouwezo wa kumpa kitu kingine bora kuliko hicho, ikiwa tu atamtii Kristo. Lakini jambo hilo likawa bado ni gumu kwake kulipokea, akaendelea na biashara yake.
Mwingine pia tulimshuhudia akawa yupo tayari kuokoka, lakini madai yake ni kuwa hana kazi, anatumia njia ya kujiuza ili apate pesa za kulipa kodi, na bili za maji na umeme.. Anasema kabisa nikiokoa najua hii kazi nitaacha, na sitakuwa na chanzo chochote cha mapato, nitaishije mjini?
Ndugu ikiwa na wewe ni mmojawapo wa watu wanaoshindwa kuacha kazi za ibilisi, kisa tu, umewekeza pesa nyingi katika hizo, au unahofia utakuwa maskini, au ukifanya kazi nyingine utapata kipato kidogo.. Nataka ukumbuke hilo andiko hapo juu kuwa “Bwana anazo nguvu za kusaidia, na kuangusha”.. Na “tena, Anaweza kukupa Zaidi sana kuliko hizo”
Anaweza kukupa mara dufu ya hivyo. Na hata kama hatokupa basi anaweza kukufanya uishi kwa raha na amani kuliko hata hapo ulipokuwepo. Bwana Yesu anasema,..Itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima, kisha upate hasara ya nafsi yako?. Amazia, alikubali kuingia hasara akijua kabisa Mungu kweli atampa Zaidi ya vyote alivyovipoteza.
Ni heri ukampa Yesu Maisha yako ayaokoe, kipindi hichi cha kumalizia, watu wengi wamenaswa kwenye vitanzi hivi…Wakiangalia mitaji yao yote imelalia kwenye michezo ya kamari, imelalia kwenye madawa ya kulevya, imelalia kwenye biashara za pombe na sigara, imelalia kwenye mavazi ya kikahaba na kidunia.
Achana nayo, mwamini Mungu anayekuita. Utakuwa salama, na atakusaidi kumudu Maisha yako..
SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?
Kwanini wakristo wengi ni maskini?
ORODHA YA WAFALME WA ISRAELI.
JAWABU LA MAISHA YA MTU.
APENDAYE FEDHA HASHIBI FEDHA.
NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.
ENZI NA MAMLAKA AMEZIFANYA KUWA MKOGO
Uru wa Ukaldayo ni nini?