Ni muhimu kufahamu kuwa kila kitu kilichopo sasa au kitakachokuja tayari kilishatabiriwa. Watu wanaomtafuta Mungu walishatabiriwa na vile vile watu watakaomkataa Mungu tayari wameshatabiriwa.
Kadhalika upo unabii wa watakaokolewa siku za mwisho, na upo unabii wa watakaotupwa katika lile ziwa la moto.
Unabii wa watakaokolewa siku ya mwisho, ni kama huu ufuatao…
Mathayo 8:11 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;”
Na unabii wa watakaopotea siku za mwisho ni kama huu ufuatao…
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Sasa nabii hizo nabii mbili ni lazima zitimie kama zilivyotabiriwa, maana yake watakuwepo watu watakaokolewa na watakaopotea, hakuna namna yeyote jambo hilo litaepukika, wala kubadilishwa, hata tufunge na kuomba Nabii hizo mbili lazima zitimie.. watakuwepo watakaokwenda jehanamu!..na watakuwepo watakaoenda mbinguni.
Sasa kitu cha kipekee katika Nabii zote Mungu anazozitoa huwa HATAJAGI MAJINA, Kwamba Fulani na Fulani ndio wataokolewa, na Fulani na Fulani ndio watakaopotea. Hapana! Kamwe hatoi majina, ikiwa na maana kuwa nafasi ya kwenda mbinguni ipo kwa kila mtu, vile vile nafasi ya kwenda motoni ipo kwa kila mtu. Hivyo nijukumu la kila mtu kuhakikisha anapambana kuwepo miongoni mwa watakaokolewa, na si miongoni mwa wanaopotea. Na kama akishinda maana yake atakuwa katika lile kundi la waliotabiriwa uzima wa milele. Lakini akishindwa atakuwa miongoni mwa waliotabiriwa kuingia kwenye adhabu ya milele.
Hivyo hata utabiri wa Yuda kumsaliti Bwana Yesu haukumtaja jina kwamba atatokea Mtu Fulani anayeitwa Yuda, huyo atamsaliti Bwana. Hapana! Hakuna utabiri wowote unaosema hivyo.. bali ulitaja tu tabia.
Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”
Maana yake ni kwamba miongoni mwa wale mitume 12, kila mmoja alikuwa anayo nafasi ya kumsaliti Bwana na kutimiza unabii huo!, na vile vile kila mmoja alikuwa na nafasi ya kutomsaliti Bwana. Sasa inapotokea mmoja anayeendekeza hiyo tabia ya kutokujali, zaidi ya wengine wote, pamoja na kwamba anaonywa na anaujua ukweli, lakini hataki kubadilika na kuufuata ukweli, basi huyo ndio anachukua nafasi ya kutimiza huo unabii. Na miongoni mwa wanafunzi wa Bwana wote, ni Yuda pekee ndiye aliyekuwa anaonyesha tabia za kutokujali, alikuwa ni mtu wa kupenda fedha, hata alikuwa anafikia hatua ya kuiba katika mfuko wa Bwana. Ingawa Bwana alishawambia mapema kwamba mmoja wao atamsaliti, lakini Yuda kwa kulijua hilo wala hakujali, wakati wengine walitilia maanani, na kujizuia kwa hali zote ili wasimsaliti Bwana, lakini Yuda hakujali, na mwishowe..akawa yeye ndiye aliyetimiza huo unabii… “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, Yuda alikuwa na hatia kuisaliti damu ya Bwana Yesu, na alifanya dhambi.
Lakini ya Yuda yamepita, Na unabii wake kashautimiza, tumebaki sisi, tunaoishi sasa…je na sisi unabii wetu ni upi?
Tusome 2Timotheo 3….
2Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 4 WASALITI, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; 5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao”.
2Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
4 WASALITI, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao”.
Hapo Mstari wa 4 hapo unasema, watatokea watu WASALITI, na sio wasaliti tu!, bali pia watakuwa wakaidi, wenye kujivuna, wakali, wasiopenda mema n.k.. Yuda alikuwa ni MSALITI tu!, lakini hakuwa na hizo tabia nyingine. Lakini hawa wa siku za mwisho wametabiriwa kuwa na usaliti pamoja na tabia nyingine mbaya nyingi juu yake.
Jiulizae kama wewe ni miongoni mwa hao?.. kama una tabia moja wapo ya hizo au baadhi ya hizo, basi fahamu kuwa unautimiza huo unabii bila ya wewe kujua, hivyo huna sababu ya kumshangaa, wala kumlaumu Yuda kwa kumsaliti Bwana, kwasababu wewe ni zaidi ya Yuda.
Bwana atusaidie, tusiwe miongoni mwa watakaotimiza unabii wa watu waovu wa siku za mwisho, bali tutimize unabii wa watu wema watakaotokea siku za mwisho,ambao wataurithi uzima wa milele.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
Tofauti kati ya ufunuo, unabii na maono ni ipi?
Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
Rudi nyumbani
Print this post
Moja ya mambo muhimu kuyafahamu pia ni kuhusu Roho Mtakatifu. Kwasababu Roho Mtakatifu ndio ukamilifu wa sauti ya Mungu kwetu..
Sasa kabla ya kwenda kuzitazama kazi kuu tatu za Roho Mtakatifu, hebu tuweke msingi kidogo wa kuufahamu utendaji kazi wa Mungu, katika ofisi zake tatu.
Wakati wa agano la kale, Mungu alizungumza na watu kutoka mbinguni, mwanzo wa agano hili jipya Mungu akazungumza na sisi ndani ya mwili wa Bwana Yesu.(Waebrania 1:2), na baadaye akazungumza na sisi kupitia Roho Mtakatifu. Ni sawa na kusema.. Mungu alizungumza nasi akiwa juu yetu(Kama Baba), kisha akazungumza nasi akiwa pamoja nasi katika mwili wa kibinadamu (Imanueli) na mwisho Mungu anazungumza ndani yetu kama(Roho Mtakatifu).
Katika hatua hizi tatu, hatua hiyo ya mwisho ndio hatua kamilifu kuliko nyingine zote, kwasababu Ni sauti ya Mungu iliyo karibu sana na sisi kuliko ilivyokuwa juu yetu (kama Baba), au ilivyokuwa pamoja nasi (kama mwana).
Ni sawa mtu azungumze na wewe kwa sauti kuu akiwa juu kabisa kwenye gorofa, kiasi kwamba humuoni ila unachoweza kusikia ni sauti yake tu na wewe upo chini ya hilo ghorofa, bila shaka kuna maneno ambayo unaweza usiyasikie vizuri kwasababu yupo mbali, hivyo maneno mengine unaweza kuyaelewa kinyume na alivyosema.. Lakini huyo mtu atakapotoka huko aliko na kushuka chini ukamwona, akawa kama mita 5 kutoka mahali ulipo, akizungumza na wewe ni rahisi kumsikia vizuri kuliko alivyokuwa kule juu, ambapo ulikuwa unasikia sauti tu na sasa unamsikia na kumwona, lakini pia bila shaka wakati anazungumza kuna maneno unaweza usiyasikie vizuri, hata wewe unapozungumza na mtu aliye karibu na wewe ni lazima utapitia vipindi vichache vichache vya kuomba arudie alichosema…
Lakini hebu tafakari tena endapo huyo huyo mtu akikukaribia sana kiasi kwamba mdomo wake unafika katika sikio lako, bila shaka hapo utakuwa unamsikia vizuri zaidi kuliko alivyokuwa mita mbili mbele yako..hapo huwezi kumwambia arudie rudie yale anayoyasema.. Hivyo utamsikia vizuri kuliko kawaida, na utamwelewa, kwasababu amesogea karibu sana na wewe.
Na utendaji kazi wa Mungu ni hivyo hivyo, Roho Mtakatifu ni sauti ya Mungu iliyo karibu sana na sisi, haijaishia kusikika masikioni tu, bali inasikika hadi mioyoni mwetu. Ni sauti isiyo na chenga chenga. Sauti ya Bwana Yesu ilikuwa ni kamilifu, lakini ilikuwa na chenga chenga kwetu, hatukuweza kumwelewa vizuri kwasababu alikuwa anazungumza nje ya miili yetu. Ndio maana ilimpasa Bwana aondoke ili Yule Roho aje juu yetu.
Yohana 16:7 “ Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu”.
Umeona hapo? Bwana hana budi kuondoka ili Roho Mtakatifu aje…(Na kumbuka Roho Mtakatifu ndiye Yule Yule Bwana Yesu mwenyewe, isipokuwa anakuja katika roho (soma 2Wakorintho 3:17),
Sasa baada ya kuelewa hayo, twende kwa pamoja tukazitazame kazi kuu tatu za Roho Mtakatifu kwa ulimwengu.
1) Kazi ya kwanza ni kuuhakikisha ulimwengu kwa habari ya DHAMBI 2) Atauhakikisha kwa habari ya HAKI 3) Atauhakikisha kwa habari ya HUKUMU.
Hizi ndio kazi kuu tatu za Roho Mtakatifu kwa Ulimwengu, tutaziangalia moja baada ya nyingine.
1. Kwa habari ya dhambi:
Yohana 16:8 “Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi”
Yohana 16:8 “Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi”
Kuhakikisha maana yake ni “kuweka sawa jambo”. Kitu ambacho hakikukaa vizuri sasa kimewekwa vizuri maana yake kitu hicho“kimehakikiwa”. Kadhalika Hapo Bwana Yesu anasema huyo Roho atakapokuja atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, maana yake hapo kwanza yeye alizungumza kuhusu dhambi lakini hakueleweka vizuri, lakini atakapokuja huyo Roho ataizungumzia vizuri dhambi kwa sauti ya ukaribu zaidi, na atafanya wengi kuelewa dhambi ni nini, kuliko jinsi wangemwelewa Bwana.
Ndio maana Bwana Yesu anasema hapo… “Kwa habari ya dhambi, KWA SABABU HAWANIAMINI MIMI ”… maana yake yeye aliihubiri sana kuhusu dhambi, lakini watu hawakumwamini. Hivyo Roho Mtakatifu atakuja kuielezea vizuri na wengi wataamini. Na kumbuka dhambi ni “kutomwamini Mwana wa Mungu, kwamba yeye ndiye mkombozi wa ulimwengu”. Hiyo ndiyo dhambi…hayo mengine kama uasherati, wizi, uchawi, uuaji n.k ni matokeo ya dhambi. Kwahiyo Bwana Yesu alihubiri sana kwamba “kila amwaminiye atapata uzima wa milele lakini Yule asiyemwamini atahukumiwa, maana yake atakuwa na dhambi”. Lakini pamoja na kuyasema hayo sana kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu, si wengi waliomwamini, ndio maana injili haikufika duniani kote, kipindi Bwana Yesu yupo duniani anahubiri. Ni wachache tu ndio waliokuwa wanaisikia sauti yake, wengine walikuwa hawamwelewi.
Lakini baada ya Roho Mtakatifu kushuka siku ile ya Pentekoste, Petro alivyosimama siku ile kuhubiri habari ya dhambi, biblia inasema watu zaidi ya elfu tatu waliokoka ndani ya siku moja.(Matendo 2:41). Na wakati miezi miwili tu nyuma, Bwana Yesu alizungumza maneno hayo hayo, tena mji ule ule Yerusalemu, lakini waliishia kumsulubisha, kwasababu hawakumwelewa.
Yohana 12:37 “Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini; 38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”
Yohana 12:37 “Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;
38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”
Lakini miezi miwili tu baadaye kama tunavyosoma katika kitabu cha Matendo 2, Roho Mtakatifu alipozungumza kwa kinywa cha Petro, wale ambao hawakumwamini Bwana Yesu Yerusalemu, walianza kumwamini kwa kasi sana.
2. Kwa habari ya HAKI.
Yohana 16:10 “kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena”
Katika kipengele ambacho Bwana hakukigusia kabisa wakati yupo hapa duniani, ni kipengele cha HAKI. Na haki inayozungumziwa hapo, ni haki ile ipatikanayo kwa njia ya IMANI. Hii Bwana hakuigusia kabisa, na lengo la kutoielezea hii ni kwasababu ya ugumu wa mioyo ya watu, Ndio maana aliwaambia “yapo mambo ya kuwaambia lakini kwa wakati huo wasingeweza kustahimili,mpaka huyo Roho atakapokuja”
Yohana 16:12 “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, LAKINI HAMWEZI KUYASTAHIMILI HIVI SASA. 13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”.
Yohana 16:12 “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, LAKINI HAMWEZI KUYASTAHIMILI HIVI SASA.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”.
Umeona jambo mojawapo ambalo wasingeweza kustahimili endapo wangeambiwa ni hilo la “HAKI”. Laiti Bwana angewafunulia siri Mitume kwamba, sisi watu wa mataifa nasi ni warithi wa ahadi za Mungu, kwamba kwa NEEMA tunahesabiwa HAKI kwa Kumwamini Yesu, kwamba na sisi ni warithi wa ahadi za Mungu, ni dhahiri kuwa wangerudi nyuma. Wangesema Bwana Yesu kachanganyikiwa. Yule aliyemwita Yule mwanamke wa kimataifa “Mbwa” halafu leo anamwita “mrithi”?.. Yule ambaye aliwatuma na kuwaambia “msifike miji ya mataifa kuhubiri (Mathayo 10:5)” ghafla anawaita tena mataifa ni warithi!!… Yule aliyesema “sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Mathayo 15:24)”. Leo hii yeye ndio atutume sisi huko kwao kuhubiri??.. Hakika amechanganyikiwa.
Hivyo Bwana aliliacha hilo hakuwaambia mitume, pamoja na mengine mengi ili yaje kufunuliwa na Roho Mtakatifu baada ya kuondoka kwake. Kwasababu kwa uchanga waliokuwa nao Mitume, wangeambiwa hizo siri, wangemwacha Bwana na kurudi nyuma (wasingeweza kustahimili)
Na siku ya kuifunua hiyo siri ya HAKI YA MUNGU ilipofika, Roho Mtakatifu alimfunulia kwanza Mtume Petro, kipindi kile cha lile ono la Kornelio, na baada ya hapo alikuja kumfunulia tena Mtume Paulo hiyo siri..
Hebu soma hichi kisa taratibu..
Matendo 11:1 “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa Mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. 2 Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, 3 wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. 4 Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema, 5 Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia. 6 Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani. 7 Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule. 8 Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu. 9 Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi. 10 Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni. 11 Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria. 12 Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule; 13 akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro, 14 atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote. 15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo. 16 Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu. 17 BASI IKIWA MWENYEZI MUNGU AMEWAPA WAO KARAMA ILE ILE ALIYOTUPA SISI TULIOMWAMINI BWANA YESU KRISTO, MIMI NI NANI NIWEZE KUMPINGA MUNGU?”
Matendo 11:1 “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa Mataifa nao wamelipokea neno la Mungu.
2 Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye,
3 wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.
4 Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema,
5 Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.
6 Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.
7 Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule.
8 Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu.
9 Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi.
10 Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni.
11 Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.
12 Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;
13 akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro,
14 atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote.
15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.
16 Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.
17 BASI IKIWA MWENYEZI MUNGU AMEWAPA WAO KARAMA ILE ILE ALIYOTUPA SISI TULIOMWAMINI BWANA YESU KRISTO, MIMI NI NANI NIWEZE KUMPINGA MUNGU?”
Umeona hapo? Kornelio ambaye ni mtu wa Mataifa anapokea Roho Mtakatifu baada ya kuamini, tena Roho Yule Yule waliyepokea wakina Petro walio waisraeli, bila shaka Petro alijua ni kwanini Bwana Yesu hakuwaambia hiyo siri wakati wapo duniani, alijua ingekuwa ni ngumu wao kumeza!… Maana unaona hapo juu tu kama tulivyosoma, mitume wengine walipopata habari ya kwamba Petro kaingia kwa watu wa mataifa, walishindana naye vikali..Mpaka Petro alipowaelezea kwa utaratibu..
Hiyo ndiyo siri ya Mungu ambayo ilisitirika tangu zamani, kwamba sisi watu wa MATAIFA, ni warithi wa ahadi za Mungu, kwamba tunahesabiwa HAKI YA KUURITHI UZIMA WA MILELE bure kwa njia ya IMANI YA KUMWAMINI YESU, Mitume hapo kabla walidhani wokovu ni kwaajili yao tu! (Wayahudi), lakini kumbe sivyo!.. hata watu wa mataifa pia..
Mtume Paulo naye aliielezea siri hii katika Wakolosai 1:26-27, na katika Waefeso 3:6, unaweza kuisoma mistari hiyo binafsi.
Hiyo ndio maana Bwana Yesu akasema kwamba…. “kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena”…..Maana yake alipaswa aelezee hiyo Haki, lakini anaondoka anakwenda kwa Baba na wala hawatamwona tena, na wala hataielezea hiyo siri, lakini Roho atakuja kuliweka hilo sawa!..maana yake atalifunulia kanisa.
3. Kwa habari ya HUKUMU.
Yohana 16:11 “kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa”.
Hapo mkuu wa Ulimwengu anayezungumziwa ni “shetani”. Na Bwana Yesu anasema…Mfalme wa ulimwengu amekwishahukumiwa.. Sasa hukumu inayozungumziwa hapo si ile ya ziwa la moto, (Hiyo ni kweli ilishapitishwa kitambo), lakini hukumu inayozungumziwa hapa si hiyo, bali ni hukumu ya kunywang’anywa mamlaka ya ulimwengu!!. Na kwamba mamlaka yote ya Duniani amekabidhiwa Yesu.
Na mamlaka hayo shetani aliyapoteza wakati Bwana Yesu akiwa hapa duniani!. Kwajinsi alivyoutoa uhai wake kwaajili ya wengi, akakabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani.
Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, NIMEPEWA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI”.
Sasa atakapokuja Roho Mtakatifu, ataliweka hilo sawa katika mioyo ya watu wengi, Watu wataelewa kwa undani ni kwa jinsi gani sasa hivi YESU NDIYE ANAYETAWALA MBINGUNI NA DUNIANI, NA HAKUNA MFALME MWINGINE KAMA YEYE. Mitume hawakumwelewa Bwana Yesu vizuri wakati wakiwa naye!!. Walikuja kumwelewa vizuri baada ya kuondoka kwake!. Kwamba alikuwa ni nani?.. Yule Yohana ambaye alikuwa anaegemea kifuani pa Yesu, ambaye alikuwa anamwona Bwana Yesu kama kaka yake tu! (Yohana 13:23)… Huyo huyo anakuja kumwona Bwana Yesu katika kisiwa cha Patmo kama miale ya moto, na anaanguka chini ya miguu yake kama mtu aliyekufa!! (Kasome Ufunuo 1). Roho Mtakatifu anamfunulia Yule Yule Yesu kama Mfalme wa wafalme, ambaye enzi na mamlaka yote ni zake.
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 AKAVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKE, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote”
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 AKAVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKE, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote”
Hivyo Roho Mtakatifu, atakapokuja atauonyesha ulimwengu kuwa YULE mkuu wa ulimwengu, shetani…hata kitu! Mbele za Bwana, kashashindwa…
Yohana 14:30 “ Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu”
Hana mamlaka yoyote juu ya wote waliomwamini Yesu..kashahukumiwa na kunyang’anywa mamlaka ya duniani na kuzimu. Wafu wote wanamilikiwa na Bwana Yesu (Warumi 14:9), maana yake ni kwamba mfano wa jambo lililotokea kwa Samweli, kuletwa juu na yule mchawi, kwasasa haliwezekani tena, kwasababu mkuu wa ulimwengu kashahukumiwa (kashanyang’anywa hayo mamlaka), anayewamiliki wafu wote kwasasa ni Mkuu wa Uzima, YESU!. Huyo pekee yake ndiye mwenye mamlaka ya kuileta roho ya mtu juu na kuishusha chini, yeye peke yake ndiye mwenye mamlaka na uwezo wa kufufua au kuua!.
Kwahiyo kwa kazi hizo tatu ambazo Bwana Yesu alizozitaja, ndizo zinazokamilisha ushuhuda kamili wa Roho Mtakatifu kwa ulimwengu!!..
Na Roho huyo ndiye anayeshuhudia hata sasa…Na anashuhudia kwa vinywa vya watumishi wake waliojazwa na Roho Mtakatifu, Kwamba Kristo ni kweli!, na Watu wote kutoka mataifa yote na makabila yote anawapokea na kuwakubali na kuwahesabia Haki ya kupata uzima wa milele endapo watamjia, Kadhalika Bwana YESU ndiye mmiliki wa mbingu na nchi na shetani hana kitu mbele zake. Hivyo yeye ndio tumaini pekee la kulikimbilia na kulitegemea.
Je umezitii ushuhuda hizo za Roho Mtakatifu???.. kwa Kumpokea Yesu maishani mwako na kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha kabisa???, kumbuka yeye anapokea watu wote haijalishi ni kutoka Taifa gani, wala kabila gani.
Kama bado hujamwamini, basi fahamu kuwa umeukataa ushuhuda wa Roho Mtakatifu maishani mwako.. Na hivyo utakuwa na HATIA kubwa, kwasababu Roho Mtakatifu amezungumza na wewe kwa sauti ya kueleweka kabisa, hivyo umeukataa ushuhuda ulio mkamilifu kabisa.
Hivyo mpokee leo Yesu maishani mwako, Ukubali ushuhuda wa Roho Mtakatifu, ili ufanikiwe katika roho yako, biblia inasema yeye Roho Mtakatifu anatutamani kiasi cha kutuonea wivu, anatamani aingie ndani yako kuliko wewe unavyotamani aingie ndani yako, hivyo ulichobakisha tu ni kutii!.. kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa ubatizo sahihi, kama bado hujabatizwa. Kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38).
Na baada ya hapo, Neema ya kipekee ya Bwana itakuwa nawe daima.
Bwana atubariki.
UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU.
KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Jibu: Tusome.
Marko 6.7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; 8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni; 9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili. 10 Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale”
Marko 6.7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;
9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili.
10 Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale”
Hapo Bwana aliwakataza wasichukue chochote katika safari yao, maana yake huko wanakokwenda watavipata vyote, wasitie wasiwasi, kwamaana endapo wakianza kutia wasiwasi na kuvisumbukia vitu hivyo kwamba huko wanakokwenda watakula nini, watalala wapi, watavaa nini..itawasababisha kupoteza umakini wa hiyo kazi wanayoiendea, itawagharimu kuanza kwanza kutafuta fedha za kutosha, itakayowawezesha kwenda kukaa siku hizo zote na kurudi.. Hivyo Bwana kwa kulijua hilo akawaambia wasibebe chochote hata chakula kwasababu Mungu atawapatia huko waendako.
Lakini pamoja na kwamba aliwaambia wasibebe chochote, mwisho aliwaambia “isipokuwa fimbo tu”
Sasa kwanini fimbo?
Fimbo si chakula, wala si fedha..bali ni kifaa ambacho kilikuwa kinawasaidia watu katika kutembea.. Kwa nyakati zetu hizi, mara nyingi ni wazee ndio wanaotumia fimbo, lakini zamani marika yote walikuwa wanatembea na fimbo, kwasababu kuna nyakati za kutembea umbali mrefu, na kupanda milima na kushuka, hivyo fimbo ilikuwa ni kifaa cha msaada sana, katika hayo mazingira..hususani katika kupandia milima.
Hivyo wanafunzi katika kwenda kuhubiri kwao, hapana shaka watapanda milima mingi na mabonde mengi ili kuwafikia kondoo wa Mungu waliotapakaa huko na kule, hivyo kifaa hicho ni cha muhimu kwao, ndio maana Bwana akawaambia wakibebe.
Hata sasa, agizo la Bwana ni hilo hilo, popote tuendapo, atuagizapo kwenda kuhubiri, tusiangalie hali tulizonazo…kwasababu huko tuendapo atatufungulia mlango wa kupata riziki, sisi tufikiri tu kusudi lake, mengine tumuachie yeye..Ndio maana baadaye tunaona wanafunzi waliporudi walitoa ushuhuda kuwa hawakupungukiwa..
Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? WAKASEMA, LA!”
Bwana ni Yule Yule, hajabadilika kama aliwatuma wanafunzi wake bila chochote lakini hawakupungukiwa katika safari zao, hata sisi atakapotutuma hatutapungukiwa. Tunachopaswa kufanya ni kumwamini tu na kujinyenyekeza chini yake na kuukubali utumishi wake kwa moyo wote. Hayo mengine tumwachie yeye, atahakikisha anatuhudumia.
Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)
KUNA WAKATI YESU ATAPITA NA WATU HAWATAJUA.
Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?
TOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA YESU, NA YA WAANDISHI.
Shalom! karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu, taa iongozayo miguu yetu na Mwanga wa njia yetu, iendayo mbinguni.
Katika biblia tunaona yapo maagizo mengi ambayo Mungu wetu ametupatia Moja kwa moja, Kwamfano agizo la Upendo!. Hili ni agizo ya kwamba ni lazima tupendane!
1Yohana 3:10 “Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. 11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, KWAMBA TUPENDANE SISI KWA SISI”
1Yohana 3:10 “Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, KWAMBA TUPENDANE SISI KWA SISI”
Maana yake tusipokuwa na upendo! Hata tufanye nini hatuwezi kuiona mbingu, haijalishi tutanena kwa lugha kiasi gani, haijalishi tutatoa unabii, na kufanya miujiza mikubwa kiasi gani…
1Wakorintho 13: 1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2 TENA NIJAPOKUWA NA UNABII, NA KUJUA SIRI ZOTE NA MAARIFA YOTE, NIJAPOKUWA NA IMANI TIMILIFU KIASI CHA KUWEZA KUHAMISHA MILIMA, KAMA SINA UPENDO, SI KITU MIMI. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.
1Wakorintho 13: 1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 TENA NIJAPOKUWA NA UNABII, NA KUJUA SIRI ZOTE NA MAARIFA YOTE, NIJAPOKUWA NA IMANI TIMILIFU KIASI CHA KUWEZA KUHAMISHA MILIMA, KAMA SINA UPENDO, SI KITU MIMI.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.
Hayo ni maagizo ya moja kwa moja ambayo tumepewa. Lakini pia yapo maagizo ambayo hatujapewa moja kwa moja, lakini tusipoyafanya tutahukumiwa kwayo.
Leo tutajifunza Agizo moja la msingi, ambalo hatujaagizwa, lakini ni wajibu wetu kulitenda….(Tafadhali naomba usome kwa makini huku ufahamu wako ukiupeleka katika kupata kitu kipya na si kutafuta kasoro, akili yako ukiipeleka katika kutafuta kasoro, shetani atakusaidia kuipata, lakini ukiipeleka katika kujifunza basi utapata kitu kipya).
Sasa agizo hilo si linguine zaidi ya “UTOAJI”.
Suala la utoaji limekuwa lango la watu wengi kuingia katika wokovu na kutokea. Wapo ambao wakisikia kuhusu utoaji wanalipokea Neno hilo kwa furaha na kuwasogeza zaidi kwa Mungu na wapo ambao wakilisikia, ndio linawatoa zaidi kwa Mungu..Na ndio linakuwa tiketi/sababu ya kuuacha wokovu kabisa kabisa, kwasababu ndani ya fahamu zao shetani kashawapandikizia mbegu ya kwamba wanataka kunyonywa vya kwao. Hivyo shetani analichukua wazo hilo na kuwahubiria waiache njia ya wokovu au waidharau. Lakini leo nataka tupate akili mpya kuhusu Utoaji, ili itusaidie tusije tukakosa kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Kabla ya kuendelea mbele hebu tusome mistari michache, tuilinganishe na mingine kisha tutapata kuelewa kiini cha somo letu la leo. (Katika mistari hiyo zingatia vipengele vilivyoanishwa kwa herufi kubwa)
Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu; 10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE. 11 Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka. 12 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. 13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 14 NA MTU ASIPOWAKARIBISHA wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu. 15 Amin, NAWAAMBIA, ITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMU, KULIKO MJI ULE”.
Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE.
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE.
11 Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka.
12 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni.
13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 14 NA MTU ASIPOWAKARIBISHA wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu.
15 Amin, NAWAAMBIA, ITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMU, KULIKO MJI ULE”.
Maagizo hayo ni Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake, wakati anawatuma kwenda kuhubiri, akawaambia wanapotoka wasibebe chochote, (fedha au chakula) kwasababu huko wanakokwenda, Mungu atawafungulia mlango wa kuvipata hivyo, maana yake wapo watu watakaoguswa moyo na kuwakaribisha na kuwapa mahitaji yao,kama chakula, fedha, nguo n.k kwasababu sio wote watakuwa na moyo mgumu wa kutoa. Lakini Mwisho wa maagizo hayo anawaambia.. “mtu yeyote asiyewakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu”. Halafu anamalizia kwa kusema… “Amin, NAWAAMBIA, ITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMU, KULIKO MJI ULE”.
Maana yake ni kwamba kitendo cha wale watu kutowakaribisha (maana yake wasipowafadhili) wala kusikia maneno yao, watapata adhabu kubwa kuliko watu wa Sodoma.
Sasa hebu twende pamoja tena katika Mathayo 25
Mathayo 25:31 “ Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto…. 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, ONDOKENI KWANGU, MLIOLAANIWA, MWENDE KATIKA MOTO WA MILELE, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 KWA MAANA NALIKUWA NA NJAA, MSINIPE CHAKULA; NALIKUWA NA KIU, MSININYWESHE; 43 NALIKUWA MGENI, MSINIKARIBISHE; NALIKUWA UCHI, MSINIVIKE; NALIKUWA MGONJWA, NA KIFUNGONI, MSIJE KUNITAZAMA. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Mathayo 25:31 “ Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto….
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, ONDOKENI KWANGU, MLIOLAANIWA, MWENDE KATIKA MOTO WA MILELE, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 KWA MAANA NALIKUWA NA NJAA, MSINIPE CHAKULA; NALIKUWA NA KIU, MSININYWESHE;
43 NALIKUWA MGENI, MSINIKARIBISHE; NALIKUWA UCHI, MSINIVIKE; NALIKUWA MGONJWA, NA KIFUNGONI, MSIJE KUNITAZAMA.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Umeona hapo?. Bwana alipowatuma wakina Petro bila kubeba chakula cha safari, lengo lake ni wale wapate riziki kupitia wale watakaowahubiria, ndio maana akamalizia pale juu kwa kusema “MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE.” Wakina Petro ni watenda kazi, (yaani wanafanya kazi ya kuhubiri), hivyo wanastahili posho zao, yaani riziki zao huko wanakokwenda kuhubiri, ndio maana akawaambia hata wasihangaike kutoka na akiba ya chakula, wala mavazi, kwasababu watavipata huko wanakokwenda.
Lakini chaajabu ni kwamba Bwana Yesu, hajatoa sheria wala hajatoa Agizo kwa wale watakaohubiriwa kwamba ni lazima watoe!!.. Kwamba ni lazima au ni amri kuwafadhili wakina Petro na Mitume wanapohubiri,.. Angeweza kuwaambia wakina Petro kwamba wawaambie watu wanaowahubiria kwamba “Kila mkutano wanaofanya wachangie, au kila mtaa wanaofika, Bwana kasema wapewe chochote”.. Lakini Bwana aliwaambia wasiseme lolote..wao kazi yao ni kutoa bure!, wasipopewa chochote wasonge mbele, wala wasionyeshe kama ni wahitaji!, wala wasiombe ombe!… Lakini mwisho tunaona Bwana anatangaza hukumu kwa wale wote ambao hawakuwakaribisha watumishi hao wa Mungu. Kwamba atawabagua kama mbuzi!
Ni nini tunajifunza hapo?
Yapo maagizo ambayo hayajaagizwa. Unaweza leo ukakwepa kumtolea Mungu, ni kweli hajakulazimisha, wala hajakuwekea kiasi, wala hajakuagiza kwamba ni lazima umtolee, amekaa kimya kuhusu hilo eneo, lakini huna budi kufahamu na kuwa na hekima kwamba ni wajibu wako kumtolea Mungu. Kama huamini kuwa kitendo cha kutomtolea Mungu ni dhambi soma tena hiyo Mathayo 25:31-43. Jiulize ni kwanini Bwana hajawafananisha wale mbuzi na watu wanaomkufuru, au wanaomtukana, au manabii wa uongo, lakini badala yake kawafananisha na watu ambao walikuwa hawamjali kimatoleo.
Ndio siku hiyo utasema.. “Bwana hukusema watumishi wako watoe bure?”… ni kweli alisema hivyo “lakini na wewe hukupaswa kukaa tu bila kuwa na hekima”. Hata mgeni anapokuja nyumbani kwako hatakuja kama anauhitaji, atakuja kama kashiba, au kama hana kiu..Lakini pengine ana njaa, na kiu..na anaweza kuondoka hivyo hivyo, kama wewe hutatumia hekima, angalau kumletea hata glasi ya maji… sio lazima akuambie naomba chakula!..kamwe hutasikia hilo likitoka kinywani mwake kama huyo mgeni ni mstaarabu.. Na Bwana Yesu ni hivyo hivyo, yeye ni mstaarabu wa wastaarabu, na watumishi wake wa kweli ni hivyo hivyo…kamwe hatakuja kwako na kukwambia nina haja na hichi au kile. Ni wajibu wako wewe kulijua hilo. Na kama hutakuwa na hekima ya kutosha ya kuweza kupambanua mambo, basi ni rahisi kuangukia katika hukumu siku ile ya mwisho.
Hilo ni jambo ambalo leo ningependa tulitafakari, leo ndugu. Popote pale ulipo mjali Bwana, pasipo kuambiwa, yapo maagizo ambayo Bwana atatuambia moja kwa moja bila kupinda panda, lakini yapo maagizo ambayo Bwana katuachia sisi wenyewe tuyapambanue, na tuyatekeleze…
Hebu tafakari hapo kanisani kwako, ni nini umefanya tangu umefika!.. kumbuka matendo yako yanatangulia hukumuni. Lakini usipokuwa na hekima kwa kudhani kuwa hakuna haja ya kumjali Bwana kwa matoleo yako, basi siku ile atakuweka katika kundi la mbuzi. Ni heri tukalijua hili mapema, ili siku ile ya mwisho tusije tukazuiliwa.
Hegai 1:4 “Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika”
Bwana atubariki na kutusaidia.
LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
Nini maana ya siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja? (2Petro 3:8)
Makao ambayo Yesu alikwenda kutuandalia ni yapi?
MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.
Yeremia 48:11 “MOABU AMESTAREHE TANGU UJANA WAKE, NAYE AMETULIA JUU YA SIRA ZAKE, WALA HAKUMIMINWA KUTOKA CHOMBO KIMOJA KUTIWA CHOMBO KINGINE, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika. 12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Yeremia 48:11 “MOABU AMESTAREHE TANGU UJANA WAKE, NAYE AMETULIA JUU YA SIRA ZAKE, WALA HAKUMIMINWA KUTOKA CHOMBO KIMOJA KUTIWA CHOMBO KINGINE, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Unajua sira ni nini?
Sira ni yale makapi yanayosalia baada ya pombe kuchachushwa, ni mchanganyiko wa maganda ya mbegu na wadudu waliokuwa wanaichachusha pombe hiyo. Kwa kawaida pombe kama divai inapomalizika kuchachushwa, wanachofanya ni kuimimina kwenye vyombo vingine kwa ajili ya matumizi na kuiacha Sira chini.. kwasababu yenyewe inakuwa kama topetope au urojo urojo fulani hivi.
Lakini makapi haya huwa yanathamani kubwa sana kwa wachachushaji, kwasababu pombe inayokaa muda mrefu juu ya Sira, huwa inaubora tofauti na ile ambayo, imekaa kwa muda mfupi. Kwa jinsi itakavyokaa sana juu ya sira basi ladha ya divai ndivyo inavyokuwa nzuri sana, vilevile mwonekano wake na harufu yake inakuja Zaidi, Lakini ile ambayo imechachushwa tu na saa hiyo hiyo au baada ya kipindi kifupi ikaondolewa na kupelekwa katika vyombo vingine huwa haina uzuri saa kama ile iliyodumu muda mrefu juu ya sira.
Wanaotengeneza divai, za ghali kama vile zinazoitwa champagne, huwa zinaachwa muda mrefu juu ya sira, hata miezi 4 na Zaidi, hivyo ubora wake unakuwa wa juu Zaidi kulinganisha na divai nyingine za kawaida. (Soma pia Isaya 25:6)
Sasa tukirudi katika mstari huo tuliousoma hapo juu, biblia inasema..
“Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine…”
Moabu katika historia ni taifa ambalo, tangu lilipozaliwa halikupitia migogoro kabisa, au kama lilipitia basi ni midogo midogo sana ambayo haikulisababishia taifa hilo madhara makubwa, ukilinganisha na mataifa mengine, Moabu haikuwa na majanga, wala vita, wala njaa wala shida shida, lakini pamoja na kwamba ilijaliwa hivyo haikujua ni kwanini Mungu aliwaacha wawe vile, kinyume chake yenyewe iliendelea tu kufanya maovu na matendo yasiyompendeza Mungu kwa muda mrefu.
Na ndio maana hapo inafananishwa na divai ambayo imekaa juu ya sira yake kwa muda mrefu, divai ambayo haikuharakishwa kumiminwa miminwa kwenye vyombo vingine, ikiwa na maana kuwa haikuchukuliwa utumwani, haikupitishwa katika matatizo, iliendelea kubakia katika ustawi wake kwa muda mrefu..
Ikawa inadhani kuwa kamwe haitakaa ukumbane na mabaya, yenyewe imebarikiwa tu, ikafikiria hao wengine wanaoadhibiwa kama Israeli wana laaana na mikosi kutoka kwa Mungu.
Lakini tukisoma mistari inayofuata inasema hivi..
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika. 12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
Umeona, kuna wakati ulifika, wakaldayo walikuja na kuwaangamiza na kuwachukua utumwani na kuwaharibu kabisa, na uzuri wao ukapotea ghafla, jambo ambalo hawakutazamia kama lingekaa liwapate, kama wengine.
Ndugu yangu, leo hii unatenda dhambi lakini huoni chochote, unazini Bwana hakuadhibu kwa lolote, unafanya mambo yako machafu kwa muda mrefu sasa, unakwenda kwa waganga, hauumwi, kinyume chake unazidi kustawi, unaendelea kufanya anasa na ulevu, unasema mbona hakuna dhara lolote linalonipata, hujiulizi ni kwa nini? Unachodhani ni kuwa wewe ni spesheli sana kwake sio? embu soma mstari huu tena ujifunze jambo..
Sefania 1:12 “Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami NITAWAADHIBU WATU WALIOGANDA JUU YA SIRA ZAO; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya”.
Umeona, Mungu utafika wakati atakuchunguza kwa taa, wewe ambaye umetulia juu ya Sira yako, huangaishwi angaishwi, unafanikiwa angali upo katika dhambi, unayesema, Mungu hawezi fanya jambo lolote hata nikiwa mwovu kiasi gani.
Jiangalie, hukumu ipo, utakufa ghafla, na moja kwa moja utajikuta upo jehanamu kama yule Tajiri wa Lazaro, ambaye hapa duniani alikuwa akijitumaisha katika Maisha yake ya anasa tu, hajali kama kuna kuzimu, au hukumu, hajali kama kuna kiama chake mbeleni.. Na wewe ndipo utakapojikuta huko kama hutatubu, ukilia na kuomboleza, ukisema laiti ningelijua, laiti ningelijua..
Wakati huo utakuwa umeshachelewa ndugu. Leo hii ukiona Mungu hafanyi chochote juu ya dhambi zako, sio kwamba anayafurahia hayo Maisha unayoishi, anakutazama tu, yamkini siku moja utatubu, lakini ikifikia wakati haoni badiliko lolote la wewe kumgeukia yeye, atakujia na kukuondoa duniani kama alivyofanya kwa Wamoabu.
Biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubali ni leo, usingojee siku Fulani ukasema hiyo ndio itakuwa siku yako ya wokovu, haitakaa ije kamwe. Mpe Yesu Kristo Maisha yako leo ayaokoe, Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha tafuta mahali ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO ili upate ondoleo la dhambi zako, na Kisha mwenyewe Mungu atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu ili akae na wewe siku zote za Maisha yako.
Hata kama ikitokea Maisha yako yamefikia ukingo leo, basi unaouhakika wa kuurithi uzima wa milele.
Ikiwa utapenda kuokoka, na unahitaji msaada huo basi unaweza, kutafuta kanisa la kiroho lililokaribu na wewe, wakusaidie au ukawasiliana na sisi kwa namba zetu hizi +255693036618 /+255789001312 kwa ajili ya Sala ya Toba na maagizo mengine.
Bwana akubariki sana.
JE! ULEVI NI DHAMBI?.
“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?
Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?
UFUNUO: Mlango wa 15
Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu. Biblia inatuambia..
“Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; (Mithali 25:4)
Tunapoiona dhahabu au madini mengine yote, yanang’aa sana, mpaka kufikia kiwango cha kuuzwa kwa thamani kubwa sana, hatupaswi kudhani, huko chini yanapochimbwa yanatoka kama yalivyo. Hapana, mengi ya hayo yanakuwa yamechanganyikana na mawe mengine au uchafu mwingi tofauti tofauti, kiasi kwamba unaweza kukutana na mwamba mkubwa sana, na ndani yake kukawa na kiwango kidogo sana cha dhahabu au fedha.
Hivyo, ili kuitapata dhahabu yenyewe safi, inawagharimu wafuaji wafanye kazi ya ziada, na kazi yenyewe ndio hiyo ya kutenganisha madini hayo kutoka katika hizo takataka nyingine, Zipo takataka ambazo unaweza kuziondoka kwa kuzichuja tu au kupepeta, lakini zipo ambazo itakuhijitaji utumie moto ili kuzitenganisha, kwasababu inakuwa zzimechanganyikana na dini lenyewe hadi ndani.
Hivyo wanachokifanya ni kwenda kuyachoma mawe hayo, kwa joto kali sana mpaka yayeyuke, na yakishayeyuka na kuwa kama uji uji, ndipo sasa uchafu unajitenga na dhahabu yenyewe. Kwa kupanda juu, hapo ndipo yule mfuaji anapoondoa uchafu ule, na atarudia tena hizo hizo hatua kwa jinsi atakavyoweza, na kwa jinsi anatakavyozidi kuondoa takatakata hizo zote hata zile ndogo, ndivyo, mnga’o wa fedha hiyo unavyozidi kuja.. hatimaye, inatokea ikiwa nzuri sana yenye kunapendeza, tayari kwa matumizi yenye thamani.
Mithali 25:4 “Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;”.
Hivyo na sisi pia kama wakristo, tunapookoka tunakuwa hatuna tofauti na fedha/dhahabu iliyochimbwa katikati ya miamba, tumetolewa huko tukiwa na mambo mengi ya kidunia ambayo yameshikamana sana na sisi,
Sasa tunapookoka, kanuni ni ile ile inatugharimu tuingizwe katika moto, ili tuwe safi kabisa, Na moto huo anayetuingiza Mungu, na pia tunajiingiza sisi wenyewe.
Hapo ndipo utaona pale tunapokuwa wakristo tu, Mungu anaruhusu tupitishwe katika majaribu mbali mbali ya moto ili tuwekwe safi. Ndio maana biblia inasema;
1Petro 1:6 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo”.
1Petro 1:6 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo”.
Yakobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”.
Yakobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”.
Unaona, ni jambo la kawaida Mungu, kuwapitisha watoto wake katika majaribu ya namna mbalimbali, lengo sio kuwaangamiza, bali kuwaimarisha Zaidi.
Pia Neno la Mungu linatuambia na sisi wenyewe, tunapaswa tuondoe takataka katikati ya kila kitu tunachokifanya katika maisha yetu ya ukristo ili Mungu aweze kutufanya kama vile anavyotaka, iwe ni katika huduma zetu, au shughuli zetu n.k..
Tukitaka tumwone Mungu katikati ya Maisha yetu, tuondoe mambo ambayo hayampendezi, tuondoke uzinzi, tuondoe usengenyaji, tuondoke kuchat chati kusikokuwa na maana mitandaoni, na kutazama muvi muvi zisizotujenga, tuondoe mizaha, tuondoe unafki, tuondoe rushwa, tuondoe uvaaji mbovu, n.k. Mambo kama haya tukiyazingatia basi Mungu, atatuletea ule mng’ao tunaostahili kuwa nao sisi kama wakristo, na tutakuwa wa thamani nyingi mbele zake na mbele za ulimwengu.
2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.
Kumbuka mambo kama haya kuyaondoa, haihitaji kuwa mlegevu legevu, inahitaji kujiingiza wewe mwenyewe katika moto wako, (kujinyima, kukataa na kuepuka) kila kitu ambacho unaona hakimpendezi Mungu. Hata kama nafsi yako inakitamani vipi, unakipinga. Unakubali kuonekana wa ajabu, lakini moyo wako uwe salama, na faida yake utaiona baadaye.
Vilevile hata katika Maisha yetu ya huduma, ili Kristo atende kazi vema, na ukuu wake uthibitike tunapaswa tuondoe mambo yote maovu katikati ya kanisa, tusiwe radhi na wazinzi na wapotoshaji katikati yetu, na Mungu atajifunua miongoni mwetu.
Mithali 25:4 “Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; 5 Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki”.
Mithali 25:4 “Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;
5 Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki”.
Bwana atusaidie sote, Na atubariki.
Shalom.
KUNA UMUHIMU WA KUWA MTU WA KURIDHIKA.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Fuawe ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 41:7
NYAYO TUNAZOPASWA KUZIFUATA.
Jibu: Hakuna mstari wowote katika biblia takatifu unaosema kwamba dunia siku moja itakunjwa kama karatasi na kutupwa motoni. Mstari ambao unawachanganya wengi ni ule wa Isaya 34:4 unaosema..
Isaya 34:4 “Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, NA MBINGU ZITAKUNJWA KAMA KARATASI, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.”
Ukiisoma hiyo Isaya 34, utaona ni unabii wa Siku ya mwisho. Na katika huo mstari wa 4, unabii unasema kuwa siku hiyo “mbingu zitakunjwa kama karatasi”. Hapo anasema “mbingu” na si “nchi” au “ardhi” au “dunia” bali mbingu!!. Hizo ndizo zitakazokunjwa kama karatasi… Na mbingu inayozungumziwa hapo sio ile Malaika watakatifu waliyopo, La!.. bali ni hii tunayoiona yenye nyota, mwezi na jua, na sayari.
Na hazitakunjwa kama karatasi na kisha kutupwa motoni!.. La! Maandiko hayajasema hivyo, yameishia tu hapo kusema kuwa zitakunjwa kama karatasi. Na kukunjwa kunakozungumziwa hapo sio kukunjwa kwa kusokotwa sokotwa kama uchafu, hapana! Bali kukunjwa kama vile mtu anayekunja ngozi.
Sasa ili tuelewe vizuri zitakunjwaje kunjwaje siku hiyo kama karatasi, twende pamoja kwenye kitabu cha Ufunuo.
Ufunuo 6: 12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13 NA NYOTA ZIKAANGUKA JUU YA NCHI KAMA VILE MTINI UPUKUTISHAVYO MAPOOZA YAKE, UTIKISWAPO NA UPEPO MWINGI. 14 MBINGU ZIKAONDOLEWA KAMA UKURASA ULIVYOKUNJWA, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Ufunuo 6: 12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 NA NYOTA ZIKAANGUKA JUU YA NCHI KAMA VILE MTINI UPUKUTISHAVYO MAPOOZA YAKE, UTIKISWAPO NA UPEPO MWINGI.
14 MBINGU ZIKAONDOLEWA KAMA UKURASA ULIVYOKUNJWA, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Umeona hapo?.. Katika siku ile ya mwisho, muhuri wa 7 utakapofunguliwa, wakati Yesu atakaporudi na watakatifu wake aliowanyakua. Siku hiyo, nyota zitaanguka, (maana yake zitaondolewa). Ghafla tu, watu watashangaa jua limezama wakati wa adhuhuri, na mwezi umekuwa mwekundu kama damu.. na juu nyota zinaanza kujikusanya pamoja na kuanguka..kama vile ukurasa (Yaani karatasi) linavyofunguliwa..
Tunaweza kulisoma tena jambo hilo vizuri katika kitabu cha Mathayo..
Mathayo 24:27 “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”
Mathayo 24:27 “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”
Unaweza kusoma pia unabii huo katika Isaya 13:9-11.
Kwahiyo dunia haitakunjwa kunjwa na kutupwa motoni, bali ni mbingu, na mbingu hizo hazitakunjwa na kutupwa motoni, bali zitaanguka (maana yake zitaondolewa!!). Na tendo hilo litatokea baada ya unyakuo wa kanisa kupita na dhiki kuu kupita, wakati ambapo Kristo atarudi kwa mara nyingine pamoja na watakatifu wake wale walionyakuliwa, sasa wale ambao watakuwa wamesalia duniani, waliopokea chapa, na kunusurika katika mapigo ya vitasa saba, watalishuhudia hilo tendo la mbingu kuondolewa kama ukurasa, siku hiyo jua litazima ghafla na mwezi utakuwa kama damu, na wataona nyota zinashuka kama vile vimondo vinavyoonekana usiku… Na kutokana na hilo tendo, itasababisha dunia iwe katika giza nene sana, kwasababu hakuna jua, mwezi unaoangaza wala nyota..
Na wakiwa katikati ya hilo giza nene watamshuhudia Kristo akitokea mawinguni kwa utukufu mwingi kama umeme, pamoja na wale watakatifu wake aliowanyakua, na chini ya ardhi visiwa vitahama, na kutatokea na tetemeko ambalo halijawahi kutokea mfano wake, watu wote watakufa, isipokuwa kundi dogo, ambalo lilihifadhiwa kuingia katika ule utawala wa miaka elfu, Kristo atakapotawala na bibi arusi wake hapa duniani.
Bwana atusaidie tusiukose unyakuo, ili siku moja tutawale naye tukiwa kama makuhani na wafalme. Ni heri tukose kila kitu katika huu ulimwengu lakini tusiikose mbingu.
Nini maana ya ‘kuhuluku’ kama tunavyosoma katika biblia?
“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?
UPUMBAVU WA MUNGU.
MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?
KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?
SWALI: Je! Mwandishi wa kitabu cha Warumi alikuwa ni Paulo au Tertio? kulingana na mstari huu;
Warumi 16:22 “Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana”.
JIBU: Paulo katika maneno yake ya utangulizi alishatupa mwangaza kuwa yeye ndiye aliyekiandikia kitabu hicho, kiwaelekee watakatifu wote waliokuwa Rumi. Tusome;
Warumi 1:1 “PAULO, MTUMWA WA KRISTO YESU, ALIYEITWA KUWA MTUME, NA KUTENGWA AIHUBIRI INJILI YA MUNGU; 2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu; 3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, 4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu; 5 ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; 6 ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo; 7 KWA WOTE WALIOKO RUMI, WAPENDWAO NA MUNGU, WALIOITWA KUWA WATAKATIFU. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo”.
Warumi 1:1 “PAULO, MTUMWA WA KRISTO YESU, ALIYEITWA KUWA MTUME, NA KUTENGWA AIHUBIRI INJILI YA MUNGU;
2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu;
3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,
4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu;
5 ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;
6 ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo;
7 KWA WOTE WALIOKO RUMI, WAPENDWAO NA MUNGU, WALIOITWA KUWA WATAKATIFU. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo”.
Lakini baadaye karibia na mwishoni mwa waraka huu tunakuja kumwona mtu mwingine aliyeitwa Tertio akijitokeza na kusema ameuandika waraka ule. Sio kwamba mtume Paulo hakuhusika hapana, Jibu ni kwamba Tertio alikuwa ni mwandishi wa mtume Paulo, aliyekuwa anamwandikia nyaraka zake. Aidha kwa kuandika kile alichokuwa anaambiwa au kwa kunakili kile alichoandikiwa na Paulo, japo hakuna sehemu nyingine katika biblia Tertio anaonekana akitajwa.
Na kulikuwa na sababu ya mtume Paulo kutokutumia mkono wake mwenyewe kuandikia waraka huu, pengine Tertio alikuwa ni mwandishi mwaminifu anayejulikana sana na watakatifu waliokuwa Rumi kwa umahiri na ufanisi wa kazi zake zilizothibitishwa. Hivyo mtu akiona waraka ulionakiliwa na yeye, basi ilikuwa ni rahisi kuamini uhalisia wa yule mwandishi husika. Kwasababu wakati huo walikuwepo pia watu waliojifanya ni mitume, na kutoa kopi zao wakidai kuwa ni za mitume, ili tu kuwachanganganya watu.
Na ndio maana mtume Paulo ili kuthibitisha nyaraka zake, sehemu nyingine alikuwa anatia sahihi yake mwishoni, soma(2Wathesalonike 3:17), na pia na hapa aliona ni vema amtumie huyu Tertio kuuandika kwa warumi, iwe kama sahihi yake.
Hivyo waraka huu uliandikwa na Paulo, lakini aliyeunakili ni Tertio.
Hii ni kutufundisha kuwa, si kila kazi ya Mungu, hata kama tutaiona ni nyepesi kiasi gani, tuifanye sisi mwenyewe, wakati mwingine tutahitaji tushirikiane na viungo vingine vya Kristo, ili kuleta ufanisi Zaidi wa kazi hiyo kwa watu wake.
Bwana akubariki.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6
Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.
Kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe.
Kumbuka Mungu yupo katika masumbufu, Na pia Mungu yupo katika utulivu. Katika majira yote na wakati wote jifunze kuzungumza na kuisikia sauti ya Mungu.
Unaweza ukajiuliza ni kwanini Mungu alimtokea Ayubu katika upepo wa kisulisuli na kuzungumza naye, (Ayubu 38:1), lakini Eliya alimtokea katika mazingira ya utulivu mkuu?.(1Wafalme 19:11-13)
Jibu ni kuwa sio kwamba alikuwa anataka kumtisha Ayubu hapana bali alikuwa anataka kumuonyesha kuwa katikati ya misukosuko, katikati ya tufani za Maisha, katikati ya dhiki, katikati ya shida, katikati ya magonjwa, na umaskini yeye yupo hapo kuzungumza naye na kumsaidia. Biblia inasema..
Nahumu 1:3b “..Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani,…”
Vilevile alipojifunua kwa Eliya katika sauti ya upole na utulivu, alikuwa hamwonyeshi kuwa yeye anajua kuongea kwa utulivu sana, na upole hapana, lakini alikuwa anamwonyesha kuwa katikati utulivu na amani yeye pia yupo kuzungumza na watu wake.
Mwanzoni Ayubu alidhani Mungu amemwacha kwa dhiki alizokuwa anazipitia ,alidhani hastahili tena mbele za Mungu, hata Mungu alipokuwa anasema naye kwa kinywa cha Elihu mwana wa Barakeli, hakutambua, alidhani Mungu kakaa mbali naye, mpaka akadhubutu kusema laiti kama Mungu angekuja nihojiane naye (Ayubu 13:3) akidhania kuwa Mungu yupo mbali naye.
Kumbe hakujua Mungu alikuwa karibu naye kuliko alivyokuwa anadhani. Leo hii lipo kundi kubwa la wakristo, linadhani pale palipo na amani tu, pale palipo na mafanikio tu ndio Mungu yupo hapo katikati yao, pale wanapopitia raha, wanapokuwa katika afya na mafanikio katika biashara zao, pale wanapopata heshima hapo ndipo wanaweza kukaa chini na kuzungumza na Mungu.
Lakini pale mambo yanapoharibika kwa ghafla, tufani na upepo kidogo wa kusulisuli unapovuma juu yao wanamtupa Mungu nyuma yao, wanasema Mungu hawezi kuwepo hapa ameniacha, wanapopitia dhiki kidogo utaona ni rahisi kupoa kama sio kuuacha wokovu kabisa, wanapougua, hawategi sikio tena kusikia chochote kuhusu Mungu. Wanachofanya ni kukimbilia kutafuta njia mbadala kwa ajili ya suluhu za shida zao.
Kumbuka biblia inasema.. Nahumu 1:3b “..Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani,…”
Unaona, sio tu katika mahali pa utulivu, lakini pia katikati ya Tufani na kisulisuli. Wakati mwingine Mungu atakujilia kwa njia hii. Hivyo uonapo hayo ikiwa wewe ni mkristo, usiogope.
Kuna wakati mtume Paulo alipitia njaa mara nyingi lakini hakumwacha Bwana. Kuna wakati alipitia kutajirika sana lakini bado aliendelea na Bwana.. mpaka akadhubutu kusema ninayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Wafilipi 4:12 “Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. 13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.
Wafilipi 4:12 “Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.
Je na sisi tunaweza kusimama kwa ujasiri na kuzungumza na Mungu katika tufani ? Bwana atusaidie tuyatambue na hayo ili tusiiache Imani, kwasababu maadamu tupo duniani, Mambo ya ghafla yanaweza kututokea, lakini hatupaswi kumtupa Mungu nyuma.
Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?
USIISHI KWA NDOTO!
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
Maswali na Majibu
Tusome,
Yohana 5:45 “Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi. 46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. 47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?”
Yohana 5:45 “Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.
47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?”
Mstari huo haumzungumzii Musa kama Musa, kwamba yupo mahali Fulani mbinguni, anawashitaki watu..hapana!! bali unazungumzia maneno ya Musa (yaani mahubiri yake). Hayo ndiyo yayowashitaki watu sasa, na yatakayowashitaki watu siku ya hukumu, ndio maana hapo katika mstari wa 47 unamalizia kwa kusema.. “Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?”.
Sasa Ni kwa namna gani maneno ya Musa yanawashitaki watu sasa?, tutakuja kuona mbele kidogo, lakini sasa tuangalie kwa ufupi ni jinsi gani yatawashitaki watu siku ya hukumu…
Bwana Yesu alisema mahali Fulani maneno haya..
Yohana 12:47 “Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu 48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, ANAYE AMHUKUMUYE; NENO HILO NILILOLINENA NDILO LITAKALOMHUKUMU SIKU YA MWISHO. 49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.”
Yohana 12:47 “Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu
48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, ANAYE AMHUKUMUYE; NENO HILO NILILOLINENA NDILO LITAKALOMHUKUMU SIKU YA MWISHO.
49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.”
Umeona? hapo Bwana Yesu anasema..”Neno analolihubiri ndilo litakalohumu siku ya mwisho”.
Hivyo hata Musa naye, hasimami kumhukumu mtu, bali injili yake ndiyo itakayohukumu watu siku ya mwisho..Kama Musa alitabiri kwamba “Atakuja Masihi”, na Masihi alipokuja kweli kulingana na huo unabii, watu wakamkataa Masihi huyo, basi siku ile ya hukumu, Unabii ule alioutoa kwa uwezo wa Roho utawahukumu wale watu, waliomkataa Masihi. Kwasababu Musa alisema kitu alichoonyeshwa na Mungu, na wala si kwa nafsi yake.
Na si maneno ya Musa tu peke yake, bali na ya Mitume wote wa Mungu na Manabii katika biblia takatifu.
Kwamfano utaona mahali Fulani Mtume Paulo alisema maneno yafuatayo kwa uwezo wa Roho…
1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? MSIDANGANYIKE; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”
Na mtu akausikia mstari huo aliouzungumza Paulo kwa ufunuo wa Roho, lakini akaudharau, na kuona kama kasema hayo kwa akili zake, siku ile ya hukumu, Maneno hayo ya Mtume Paulo yatamhukumu. Ndio maana Mtume Paulo mwenyewe alisema tena maneno yafuatayo..
Warumi 2: 16 “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, SAWASAWA NA INJILI YANGU, kwa Kristo Yesu”.
Hapo anasema “sawasawa na Injili yangu”.. maana yake tutahukumiwa kulingana na Injili ya Paulo, na mitume wengine kwenye biblia, ndio maana nyaraka za Mitume, Roho Mtakatifu kazifanya leo kuwa ni Neno lake. Chochote kilichozungumzwa na Mtume Paulo katika biblia, au Mtume Petro, au Yohana, au Mathayo kimekuwa ni NENO LA MUNGU KAMILI, na wala si la huyo mtume, na ndicho siku ile ya hukumu, kitakacho hukumu watu.
Mtume Paulo alisema kwa ufunuo wa Roho…“ Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika kama sina upendo mimi si kitu”. Maana yake kama hatutatafuta upendo kwa bidii, na kujitumainisha kwa karama tulizo nazo, kama lugha au unabii, siku ile hatutaurithi uzima wa milele, kwasababu Neno hili litasimama kutuhukumu, kwamba tulipaswa tuwe na upendo na si karama tu peke yake.
Lakini pamoja na hayo, Maneno yote ya Watumishi wa Mungu waliopo katika Biblia, yanasimama pia kutuhukumu leo, Maana yake ni kwamba Injili ya Musa, Paulo, Petro, Yohana, na wengine wengi katika biblia, yapo yanatuhukumu wakati huu.
Sasa yanatuhukumu kwa namna gani?
Jibu ni rahisi, kwa njia ya MASHITAKA!.
Mtu anayejiita ameokoka, na huku anajua kabisa katika biblia Mtume Paulo aliandika kwa uwezo wa Roho katika..
1Wakorintho 6:16 “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja”
Na kwa kulijua hili neno, akakaidi na kwenda kufanya uasherati makusudi, moja kwa moja Shetani analichukua hili andiko na kwenda nalo mbele za Mungu, kumshitaki mtu huyo, atakachosema ni hichi>> “Bwana Mungu Yule mtu, anayesema amekupokea wewe, tazama anafanya uzinzi na kahaba makusudi na ilihali anajua kabisa katika maandiko yako umesema, yeye ajiunganishaye na kahaba ni mwili mmoja naye,”.
Kwa mashitaka kama hayo, shetani anashinda hoja juu yako, na hivyo unahesabika kuwa na hatia juu ya hilo andiko… Ni heri ungekuwa hujaokoka halafu unafanya hayo, shetani asingekuwa na hoja nyingi juu yako, lakini unasema umempokea Yesu lakini unafanya uasherati, hapo ndipo unakabidhiwa shetani na Adui yako shetani anaweza kukufanya lolote kuhakikisha kuwa unakuwa mwili mmoja na Yule unayezini naye… Maana yake matatizo yake yote na laana anazobeba huyo unayezini naye, zinakuja kwako (kwasababu mmeshakuwa mwili mmoja), hata kama anamapepo basi na wewe ni rahisi kuyashiriki. Ndio maana kuna hatari kubwa sana ya kulipuuzia Neno la Mungu, hata tukiwa hapa duniani, kabla hata ya kufika siku ya hukumu.
Hivyo ni muhimu sana kulifuata na kulishika Neno la Mungu, na wala si la kulidharau, kwasababu ndilo tutakalohukumiwa nalo siku za Mwisho na ndilo linalotushitaki sasa kupitia adui yetu shetani. Na neno la Mungu linapatikana katika kitabu kimoja tu! Kinachoitwa Biblia yenye vitabu 66, na si kwenye kitabu kingine chochote.
Kama hujampokea Yesu leo, huu ndio wakati wako, shetani hakupendi kama unavyodhani, anachokitaka kwako ni ufe katika dhambi zako, siku ile ukahukumiwe na kutupwa katika lile ziwa la Moto. Huko tumwache aende peke yake, lakini sisi tujiokoe roho zetu kwa kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo, na kutubu dhambi zetu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu, na kupokea Roho Mtakatifu, ili tujiweka salama na tuwe na uhakika wa uzima wa milele.
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?
MMESIKIA KWAMBA IMENENWA?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?